Simulizi: Harakati za Jason Sizya

Simulizi: Harakati za Jason Sizya

ufukweni mombasa.JPG

270

Niliamua kupiga moyo konde na kujaribu kuupoteza mshtuko mkubwa usoni mwangu kisha nikageuka na kumtazama yule mtu mwenye mavazi yaliyobana huku nikifahamu fika kuwa tayari usalama wangu ulikuwa mashakani na hivyo nilipaswa kuwa makini sana na watu wale.

“Nilidhani sisi ni wamoja, kwani ninyi ni akina nani na mna shida gani na mimi?” niliuliza kwa kujiamini ingawa niligundua kuwa sauti yangu ilikuwa imepwaya. “Au basi, ngoja niondoke.”

“Usijidanganye huendi popote. Tumekuwa tukiisubiri hii bahati kwa muda mrefu na hatuwezi kuichezea tena,” yule mtu mwenye mavazi yaliyobana aliongea huku akiivua miwani yake na hapo nikayaona macho yake na kumtambua. Alikuwa ni yule mwanamume aliyenifuata na gari aina ya Nissan Patrol jeusi asubuhi wakati naelekea Red Brick Restaurant kuonana na Leyla. Nilipoyatazama vizuri macho yake nikagundua kuwa hayakuwa na huruma hata kidogo.

“Tummalize kabla mambo hayajawa mengi,” mmoja wa wale watu alisema huku akiikoki bastola yake kuondoa usalama.

“No! huyu anahitajika akiwa hai, mkuu ana hamu ya kuonana naye akiwa hai,” yule mtu mwenye mavazi yaliyobana alisema. “Hebu mpekue.”

Kisha mmoja wa wale watu akanisogelea ili anifanyie upekuzi. Sikutaka kuendelea kuzubaa kwani nilifahamu fika nini ambacho kingefuatia baada ya pale. Nikaamua kufanya shambulio la ghafla, nikageuka kwa pigo makini nikiruka juu na kuzipiga teke bastola za wale watu wawili waliokuwa nyuma yangu.

Nilipotua chini nikamchota mtama yule mtu mwenye nguo za kubana na kumbwaga chini kama gunia. Alianguka huku akinitukana tusi zito na kunilaani kwa shambulizi lile makini la kushtukiza.

Wakati nakaa sawa mmoja wao hakunipa nafasi ya kujipanga badala yake akawahi kunichapa teke zito la kifuani lililonitupa ukutani na kunisababishia maumivu makali mno. Niliwahi kusimama haraka na kuchomoa bastola yangu kwani sikutaka kupoteza muda. Risasi moja niliyoiruhusu kufanya safari ikasafiri kwa shabaha makini na kukisambaratisha kichwa chake.

Kuona vile mtu mwenye mavazi yaliyobana akaruka juu huku akiachia teke kali, hata hivyo lilikuwa pigo dhaifu kwani niliwahi kulidaka kisha nikamchota mtama mwingine maridadi kupitia mguu wake mmoja uliosalia chini. Pigo lile likamfanya yule mtu atue chini kwa matako na kupiga yowe kali la maumivu huku akiponyokwa tena na tusi zito mdomoni. Alipotaka kuinuka akajikuta akitazamana na mdomo wa bastola yangu mkononi. Hofu iliyomwingia ikamrudisha chini taratibu.

Muda huo huo mlango wa kile chumba ukapigwa kumbo, wote tukashtuka na nilipotazama mlangoni nikawaona Leyla na Dennis Njoroge wakiingia kwa mtindo wa kininja, kwani waliruka juu na kutua katikati ya chumba kama paka huku bastola zao zikiwa mikononi tayari kwa lolote. Ujio wao ukanipa nguvu na hatimaye tukafanikiwa kuwadhibiti wale jamaa wawili. Kisha Leyla akawasiliana na kiongozi wa kikosi kazi Joram Kamau (E01).

Sikuwa na muda wa kupoteza kwani bado sikujua ni wapi alipokuwa Abshir. Rahma wa Singida tayari alikwisha dhibitiwa na Leyla na kukabidhiwa kunakostahili. Nikatoka na kuelekea ukumbini huku nikipishana na Joram Kamau akiwa na makachero wawili. Macho yetu yalipogongana tu nikanyanyua mkono wangu wa kushoto na kugusa upande wa kulia wa ncha ya kola ya shati niliyokuwa nimeivaa kumwashiria kuwa mambo hayakuwa shwari.

Bila kusita naye akanijibu kwa kugusa sikio lake la kushoto kuashiria kuwa hata yeye anaona hivyo. Nikaongeza mwendo na kuwapita nikielekea ukumbi wa mikutano kumtafuta Abshir. Nikakumbuka kutazama saa yangu ya mkononi na kugundua kuwa ilishatimia saa tisa na dakika hamsini na tisa. Ilisalia dakika moja tu mkutano ufunguliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya ambaye alifika kumwakilisha Naibu Rais.

Wakati nikishuka haraka toka kule juu nikamwona mwanamume mmoja aliyevaa suti ya gharama kama za wanausalama akiwa makini sana kutazama huku na kule kama aliyekuwa akitafuta kitu muhimu sana alichokipoteza, uso wake ulijawa na wasiwasi. Nikahisi mwili wangu ukisisimka na vinyweleo vikisimama, haraka nikavaa miwani yangu ili nimpige picha. Muda huo huo yule mwanamume aligeuka kutazama upande wangu na hapo nikawa nimempiga picha vizuri na ile miwani maalumu na kuzisafirisha mpaka kwenye tarakilishi ili kuoanisha sura yake na sura zilizokuwepo, kifaa kile kikambaini kuwa ni Abshir.

Nikamwona Abshir akinitazama kwa hofu katika namna ambayo nilifahamu kabisa kuwa alitaka kuzimia, kwani hakuamini kama nilikuwa hai, tena nikiwa kamili gado.

“Abshir yupo hapa, kila mmoja akae kwa tahadhari sasa!” nilisema kwenye kifaa maalumu kuwapa taarifa watu wangu wa kikosi kazi cha CSSG.

Copy!” nikajibiwa mara moja.

Haraka nikatoka kasi kuelekea kule alikokuwepo Abshir, wakati huo Abshir alikuwa anapeleka mkono wake kwenye mfuko wa koti na kuchomoa bastola kubwa aina ya Kimber 1911, kisha akaielekeza kwangu akiwa tayari kwa lolote.

Sikujali, nilikusanya nguvu za kutosha nikaruka juu na kujiviringisha kwa kasi kuelekea alipokuwa amesimama na wakati huo huo nikisikia mvumo wa risasi zilizopita karibu yangu. Nikamkumba kwa nguvu. Sote tukapiga mweleka chini kama mizigo huku bastola ikimtoka Abshir na kuangukia kando. Hesabu zangu zikiwa zimeenda vizuri, nilichupa kuiokota ile bastola yake huku Abshir akiendelea kugaagaa pale sakafuni bila ya mafanikio.

“Gaidi! Msaada gaidi!” nilipiga kelele kutoa tahadhari kwa watu mle ukumbini. Nilikuwa nimefanya uamuzi wa kijasiri na wa hatari sana kwa kujitosa kumkabili yule gaidi. Na hapo nikamwona mwenyekiti wa kamati ya uratibu wa mkutano huo, Abdoulkader Omar akitoa amri kwa wanausalama fulani akiwataja kwa majina ili wanikamate. Nikatambua kuwa wao pia walikuwa miongoni mwa mamluki.

Kauli yake ilinitia hasira hasa nilipowashuhudia wanausalama wawili mamluki wakizielekeza bastola zao kwangu, macho yao yaliashiria mauaji. Sikusubiri, nikaruka na kutua kwa kupiga goti moja chini na kufyatua risasi mbili mfululizo zilizowapata wale mamluki kabla hawajafanya chochote. Mmoja risasi ilimpata kwenye kiganja chake cha mkono ulioshika bastola na kukisambaratisha na mwingine risasi ilimpata kwenye bega lake na kumtupa chini kama mzigo huku akipiga kelele za maumivu.

Kisha nikawaruka walinzi waliojaribu kunizuia huku bastola yangu ikiwa mkononi. Wakati nikiwa hewani mmoja wa walinzi akajaribu kunishika mguu na kunikosa, nikaanguka na kubiringika kama tairi, wakati huo huo nikasikia sauti ya Joram Kamau ikiwaamuru wale walinzi waniache nifanye kazi yangu. Nikaweka bastola yangu sawa kumwelekea Abshir kwani muda huo ni mimi tu niliyemwona wapi kasimama.

Abshir aling’amua hatari iliyomkabili, bila shaka alijua kuwa mimi ni bingwa wa shabaha, akajirusha kwenye dirisha la kioo na kukitawanya kioo kile vipande vipande na kuangukia nje. Sikumwacha, nami nikapita hapo hapo na kujikuta nipo nje chini. Nikamwona akikimbilia kwenye maegesho ya magari, nikaachia risasi moja iliyompata kwa nyuma upande wa kushoto wa kifua chake na kutokea mbele. Akaanguka chini akiwa hana uhai.

Nilimfuata na kusimama nikiutazama mwili wake kwa hasira, mara nikasikia sauti ya risasi kutoka ndani ya ule ukumbi wa mikutano. Nikashtuka na kurudi haraka kule ukumbini. Kumbe Joram Kamau na timu yake walikwenda kumweka chini ya ulinzi Abdoulkader Omar. Yeye alishatambua nini kingetokea na hivyo kabla hawajamfikia akachomoa bastola yake na kujipiga risasi kinywani kwa risasi moja tu iliyoufumua ubongo wake, akaanguka chini akiwa maiti.

Huu ni mwisho wa Msimu wa Tano kwenye mfululizo wa Harakati za Jason Sizya. Usikose Msimu wa Sita katika mkasa uitwao “Taharuki”.
 
Kazi nzuri kabisa kiongozi.
Ila leo umeruka namba 263 na 268
 
View attachment 2346108
262

Saa 7:15 usiku…



Saa saba na robo usiku ilinikuta nikishushwa na teksi katika barabara ya Old Malindi usawa wa ACK St. Mary’s Parish Church – Utange, kisha nilianza kutembea kwa utulivu kando ya ile barabara ya Old Malindi huku mara kwa mara nikigeuka na kutazama nyuma yangu kama kungekuwa na pikipiki, gari au mtu yeyote akinifuatilia. Sikumwona mtu yeyote, pikipiki wala gari hivyo nikaamini kuwa hali bado ilikuwa shwari. Nilikuwa nimechoka sana, mwili na akili kutokana na misukosuko ya siku nzima.

Teksi iliyonileta hadi pale ACK St. Mary’s Parish Church – Utange ni ile ile iliyokuwa imenipeleka nyumbani kwa Miriam Mutua kutokea Bamburi Beach Villa. Nilipotoka nyumbani kwa Miriam nilikuwa na wasiwasi wa kupata usafiri usiku huo lakini nikashangaa kumkuta dereva wa teksi akiwa bado ananisubiria pale pale tulipokubaliana japokuwa nilimweleza kuwa angeondoka endapo asingeniona baada ya nusu saa. Kumbe ni Leyla aliyempa maelekezo ya kutoondoka!

Sasa nikiwa natembea, utulivu katika barabara ile ulinipa hadhari ya namna yake hadi nilipokaribia kwenye Kanisa la Agape Fellowship Center – Shanzu, nikasimama kidogo kando ya ile barabara nikiyatembeza macho yangu kwa makini kuyapeleleza mandhari yale na niliporidhika na tathmini yangu nikaanza tena kutembea taratibu huku mkono wangu mmoja ukiwa ndani ya mfuko wa koti langu umeikamata bastola.

Nilinyanyua mkono wangu uliovaa saa na kutazama saa, ilishatimia saa saba na nusu za usiku. Muda ulikuwa umesonga sana hivyo matumaini ya kumkuta Merina akiwa macho kwa tafsiri nyingine yalikuwa madogo sana.

Mara kumbukumbu juu ya jinsi nilivyoonana na Merina kwa mara ya kwanza kule Serena Beach Resort ikaanza kujengeka taratibu kichwani mwangu. Merina alikuwa msichana mrembo ambaye mwanamume yeyote angejisikia fahari kuwa naye. Japokuwa safari yangu kuja pale Mombasa ilikuwa kwa ajili ya Leyla lakini sasa nilijikuta nikiwa mateka wa nafsi mbele ya Merina.

Baada ya kulivuka Kanisa la Agape Fellowship Center nikageuza shingo yangu na kuyatembeza tena macho yangu kwa makini kisha nikachepuka haraka upande wa kushoto na kuanza kukatiza vichochoro huku nikijihisi mpweke kwani giza lilikuwa zito japokuwa baadhi ya nyumba zilikuwa zikiwaka taa lakini mwanga wa taa zile haukuwa na msaada wowote katikati ya lile giza.

Mara moja nikageuka tena nyuma kuangalia kama kungekuwa na mtu yeyote akinifuatilia. Bado sikumwona mtu yeyote na hivyo nikaamini kuwa hali ilikuwa bado shwari. Nilipoifikia nyumba aliyokuwa akiishi Merina nikasimama tena nikiupima utulivu wa eneo lile. Bado hali ilikuwa shwari na hapakuwa na kiashiria chochote cha uwepo wa kiumbe hai eneo lile. Niliporidhika kuwa mambo yalikuwa shwari nikausogelea mlango na kugonga taratibu.

“Nani?” sauti ya Merina ilisikika toka ndani mara tu nilipogonga, ikiuliza kwa wasiwasi. Nikashangaa kuona kuwa hadi muda huo alikuwa bado hajalala.

“Ni mimi, J,” nilijibu kwa sauti ya chini na mara mlango ukafunguliwa taratibu na Merina akachungulia nje, aliponiona akashusha pumzi na kuufungua mlango huku akinipisha niingie.

Usiku huo alikuwa amevaa nguo nyepesi ya kulalia ambayo ilishindwa kuyaficha maungo yake na kunifanya nizione chuchu zake laini zilivyosimama kwa utulivu kama zilizokuwa zikinidhihaki. Kiuno chake chembamba chenye shanga kilikuwa kimefinyangwa vizuri kuushikilia mzingo wa makalio yake ya wastani usiokinaisha kuutazama. Tumbo lake lilikuwa dogo lenye kitovu laini chenye kishimo na mapaja yake yalikuwa laini na mang’avu yenye misuli imara.

Mwili wangu ulishikwa na ganzi na akili yangu ilianza kuyumba na
kupoteza uelekeo kama bondia niliyetaka kukumbwa na tatizo la kizunguzungu.

“Mbona umesimama, tafadhali pita ndani,” sauti ya Merina ilinizindua toka kwenye mduwao ule. Nikaachia tabasamu la aibu na kushusha pumzi za ndani kwa ndani.

Wakati naingia ndani Merina alikuwa bado amesimama pale kando ya mlango na alinitazama kwa tuo kama mtu ambaye hakuamini kuniona tena. Kisha tabasamu jepesi likajitokeza usoni kwake.

“Ndiyo nini kuniweka roho juu kiasi hiki!” Merina aliniuliza kwa sauti ya kulalama huku akiendelea kunitazama usoni.

Nilitabasamu na kumwambia, “Pole sana kwa kunisubiri, hata hivyo sikukusudia.”

Merina hakusema kitu, alifunga mlango vizuri kisha akanikabili. “Mbona hujalala hadi saa hizi?” nilimuuliza huku nami nikimkabili. Tukatazamana.

“Ningewezaje kulala wakati sijui uko katika hali gani? Nimeshindwa kabisa kupata usingizi tangu nilipofika hapa nyumbani,” Merina alinijibu huku akinitazama kama mama amtazamavyo mwanawe mpendwa.

“Ungelala tu!” nilimwambia. “Nilikuwa na uhakika ningerejea tu!”

Merina hakunijibu kitu zaidi ya kutabasamu na hapo nikamkaribia zaidi na kumshika kiunoni bila ruhusa yake, hata hivyo sikukutana na upinzani wowote. Merina alinitazama machoni kisha akaachia tabasamu la aibu. Nikaichukua mikono yake na kuipitisha nyuma ya shingo yangu, nikamwona akinikumbatia na kisha akaniletea mdomo wake na hapo ndimi zetu zikakutana.

Muda mfupi uliofuata tulikuwa kama tuliopagawa, kisha tukachukuana hadi chumbani kwenye kitanda kikubwa cha futi tano kwa sita cha samadari huku kila mmoja akiwa amepandwa na wazimu wa mapenzi. Na kilichoendelea humo chumbani kilituhamisha kutoka dunia hii na kutupeleka kwenye ulimwengu mwingine wa huba, sayari ya raha kwa ajili yetu. Merina alijua namna ya kuzitendea vyema hisia zangu.

* * *

Inaendelea...
hivi kwanini mademu wote jason anaowakulaga hawapati mimba
 
hivi kwanini mademu wote jason anaowakulaga hawapati mimba
Haha! Belinda alipata Jason akamkataa akajiua. Zakia alipata ikaleta shida kwenye ndoa yake akanywa sumu ikatoka. Jamila alipata akaua mtu kwa risasi na yeye akajiua. Zainabu na Rehema wana watoto...
 
Haha! Belinda alipata Jason akamkataa akajiua. Zakia alipata ikaleta shida kwenye ndoa yake akanywa sumu ikatoka. Jamila alipata akaua mtu kwa risasi na yeye akajiua. Zainabu na Rehema wana watoto...
Nawakumbuka hao,ila jamaa hajui kuvaa malboro jaman 😁😁😁😁
 
Asante sana Bishop Hiluka, ni kama vile umesomea ujasusi. Nikiwa nasoma nilijiona kama mimi ndio Jason Sizya. Umetufikisha upeo wa juu siye wasomaji wako. Maswali yote niliyokuwa nayo kichwani umeyajibu kwenye sehemu hii ya mwisho.
 
Asante sana Bishop Hiluka, ni kama vile umesomea ujasusi. Nikiwa nasoma nilijiona kama mimi ndio Jason Sizya. Umetufikisha upeo wa juu siye wasomaji wako. Maswali yote niliyokuwa nayo kichwani umeyajibu kwenye sehemu hii ya mwisho.
[emoji120][emoji120] sasa jiandaeni na msimu wa sita wa Harakati za Jason Sizya katika 'TAHARUKI' ni full ujasusi...
 
taharuki..jpg

271

Ground zero…




Saa 10:20 jioni…

KWA dakika kadhaa nilitulia pale dirishani katika ofisi yangu binafsi iliyokuwa kwenye ghorofa ya kwanza ndani ya jengo la Makumbusho Plaza kwenye Kituo cha Daladala cha Makumbusho huku nikiendelea kutazama mandhari ya eneo lile kana kwamba nilikuwa nikiyaona kwa mara ya kwanza katika maisha yangu. Nilikuwa nikiyachunguza mandhari yale na nisijue nilikuwa natafuta nini! Hata hivyo hisia zangu ziliniambia kuwa niendelee kuyachunguza tu na baada ya muda ningekiona nilichokuwa nikikitafuta.

Kwa utulivu kabisa huku nikiwa nimeweka mkono wangu wa kushoto mfukoni na mkono wa kulia nikiwa nimeuegemeza pale dirishani nilivutiwa kuwaangalia watu wengi waliokuwa wakikimbia na kusukumana na wengine walisimama kando ya barabara ambayo daladala zilitumia kuingilia katika kituo cha daladala wakiwa wamekata tamaa huku wakisubiri daladala zilizokuwa zikiingia na kutoka katika kituo kile cha daladala cha Makumbusho kilichopo Manispaa ya Kinondoni, Jijini Dar es Salaam.

Ilikuwa ni jambo la kawaida abiria wa daladala kugombea kupanda magari katika nyakati hizo za jioni, hasa abiria wa magari yaliyokuwa yakifanya safari zake kutoka pale Makumbusho na kuelekea maeneo ya Tegeta, Kunduchi, Mbagala na Gongo la Mboto. Katika kituo hicho cha daladala cha Makumbusho abiria wa maeneo hayo na hata maeneo mengine ya jiji waligeuka kuwa na hulka ya aina moja. Pindi daladala likifika basi abiria wote waligeuka kuwa wanariadha! Na walipoufikia mlango wa daladala wote waligeuka kuwa mabondia kwa jinsi walivyokuwa wakiugombea mlango mmoja wa gari.

Nikiwa pale juu dirishani niliwatazama watu wale kwa umakini sana kama niliyepewa mtihani wa kuchunguza jambo fulani ili baadaye nijibu maswali, na uwepo wangu hapo ukanifanya nijikute nikivutiwa sana na kile kilichokuwa kikiendelea pale kituoni, ilikuwa ni kama mchezo fulani wa kugombea magari ambao haukuchagua jinsia wala umri, na hata kadhia ya urembo haikutazamwa kabisa.

Walikuwepo wasichana warembo sana ambao walikuwa na hadhi ya kuwa warembo wa taji la urembo wa taifa na hata dunia lakini walikuwa wameipakata vyema mikoba yako makwapani, macho mbelembele tayari kwa kugombea daladala ambalo lingeingia katika kituo hicho cha daladala cha Makumbusho.

Abiria wengine walikuwa wamejiweka sawa kabisa kuvamia gari lolote ambalo lingeonekana lina maandishi ya kule walikokuwa wakielekea hata kama kondakta wa gari hilo angewaambia kuwa gari hilo lilikuwa halifiki huko. Kwa jinsi walivyoonekana ni kama wanariadha wa mbio fupi waliokuwa wakisubiri amri tu ili waanze kutimua mbio. Ilipendeza sana kuwatazama, iwapo tu wewe si mmoja kati ya wale waliokuwa wanawania usafiri huo.

Kwa kweli nilivutiwa mno na kile kilichokuwa kikiendelea pale kituoni hasa zile purukshani za watu ambazo zilikuwa zikiwavutia pia vibaka kufanya yao. Kwangu kila kitu kinaweza kuwa habari, inategemea muktadha au unakitazama kitu hicho kwa jicho gani. Hivyo nilikuwa nimepata wazo la kupiga picha za video na kuandaa kipindi maalumu juu ya adha ya usafiri wa daladala jijini Dar es Salaam hususan nyakati za asubuhi na jioni.

Nikaona kuwa ili kipindi kipendeze zaidi ilibidi nizipige picha hizo kwa kificho kwenye vituo mbalimbali vya daladala na maeneo tofauti.

Usishangae kwa nini nilikuwa nafanya hivi… nilikuwa bado ni Jason Sizya yule yule, jasusi mwenye macho ya udadisi na moyo ya utafiti lakini niliyependa kujifunza mambo mapya hata yale yasiyohusiana na taaluma yangu. Nilipenda kuyaweka wazi macho yangu ili nione kila kitu, na sikio langu kumsikiliza kila mtu, iwe anazungumza upuuzi ama anajenga hoja chanya na madhubuti! Nilifanya hivi nikiweka maanani kitu kimoja tu; nakuruhusu unieleze lolote unaloweza, unishauri lolote unaloona linafaa kunishauri lakini kuchukua ushauri wako na kuufanyia kazi ilibaki kuwa juu yangu mimi na akili zangu!

Si kila nililoliona au lililosemwa ningelifanyia kazi… Hakuna gharama yoyote katika kuona na kusikiliza ila kuna gharama katika kufanyia kazi hayo uliyoyaona au kuyasikiliza.

Bado nilikuwa nafanya kazi katika Taasisi ya SPACE kwenye kitengo maalumu cha kufuatilia jumbe mbalimbali zilizotumwa kwenye mitandao ili kujua kama ujumbe fulani ni ‘serious and sensitive’ ama sivyo, na kisha kuzichunguza kwa umakini kabla ya kuamua nini cha kufanya.

Hivyo majukumu yangu yalibaki kuwa yale yale, kwenye taasisi ile ile, na kwa lengo lile lile ingawa watu wengine wasingeweza kubaini kwa kuwa sasa nilifanya kazi kama mwandishi wa habari za uchunguzi nikipiga picha na kuandaa vipindi mbalimbali vya kiuchunguzi na kuvirusha kwenye runinga au kupeleka kwenye vyombo vya habari.

Kwa kifupi, tangu niliporejea nchini kutoka jijini Mombasa, Kenya baada ya kufanikiwa kuzuia shambulizi la kigaidi lililokuwa lifanywe na kundi la Alshabab katika hoteli ya Bamburi Beach Resort, kama ilivyoandikwa katika mkasa unaoitwa ‘Ufukweni Mombasa’, niliwekwa kufanya kazi kama Ofisa Kificho wa Idara ya Usalama wa Taifa na hapo ndipo nilipoamua kufungua kampuni ya Capital Media Inc.

Kampuni hii ilikuwa inachapisha gazeti la kila wiki la mtandaoni la Mambomoto na ilimiliki kituo cha runinga cha mtandaoni (Online TV) cha Mambomoto TV.

Ndiyo, kwa kila hali umakini wangu kwa kila kitu nilichokiona na kukisikia ulizidi mara dufu. Ule ‘u-Jason Sizya’ katika fikra zangu uliendelea kuwepo. Kwani wahenga walisema kuwa tabia haina dawa! Ni tabia hiyo, au ‘u-Jason Sizya’ huo ndiyo ulionifanya nisimame pale dirishani na kwa kupitia katika kioo cha dirisha lile nianze kufuatilia kwa umakini sana na kumsoma (kama scanner) kila mtu aliyekuwepo mahali hapo na kila kilichokuwa kikiendelea pale kwenye kituo cha daladala cha Makumbusho.

Baada ya kukumbuka hayo nikaachia tabasamu na kuchukua kamera yangu kubwa na ya kisasa ya ki-uandishi wa habari aina ya Lumix SFX-20 yenye lenzi kubwa ya kuona mbali na kisha nikaanza kupiga picha za video za matukio yale ya abiria kugombea daladala katika kituo cha daladala cha Makumbusho.

Wakati nikiendelea kupiga picha mara macho yangu yakahama kutoka kwa wale watu waliokuwa wakigombea kupanda kwenye magari na sasa yaliuvuka moja kwa moja ule mtaa uliokuwa ukikatisha mbele ya lile jengo la Makumbusho Plaza ambamo ofisi zangu za Capital Media Inc. zilikuwemo na kuangalia upande wa pili kulikokuwa na jengo refu zaidi lenye ghorofa zaidi ya kumi. Jengo lile lilijulikana kama Alpha Mall, na lilikuwa limejengwa kando ya Barabara ya Bagamoyo.

Na hapo macho yangu yakatulia kulitazama gari moja aina ya Toyota Prado TX la rangi ya fedha lililokuwa na namba za binafsi kutokana na utambulisho wa namba zake, likiwa limeegeshwa kando ya jengo katika maegesho maalumu ya magari chini ya lile jengo la Alpha Mall. Kamera yangu ya ki-uandishi wa habari pia ilihama sambamba na macho yangu na kuanza kupiga picha katika jengo lile.

Endelea...
 
Back
Top Bottom