Simulizi: Harakati za Jason Sizya

Simulizi: Harakati za Jason Sizya

taharuki..jpg

290

“Je, kuna lolote ambalo umeliona si la kawaida katika miezi ya karibuni kuhusu dada yako?” nilimuuliza huku nikiyatuliza macho yangu kwenye uso wake.

Dk. Uledi alisita kidogo na kushusha pumzi kama aliyekuwa anafikiria jibu, pengine alikuwa akijaribu kuvuta picha. Akatingisha kichwa chake kukataa.

“Lakini nahisi hapa kuna tatizo moja. Nimesikia mahali kuwa dada yako alikuwa ametengana na mumewe. Unaweza kuniambia ni kitu gani kilichowatenganisha?”

“Siwezi, kwa sababu sijui chochote. Dada yangu hakupenda kuweka mambo ya familia yake wazi ndiyo maana wengi wamekuja kufahamu kuwa yeye na mumewe wametengana baada ya kifo chake. Lakini hata kama ningejua sidhani kama ningeweza kukwambia ili ukaitangazie dunia,” Dk. Uledi alisema na kushusha pumzi.

“Nafahamu kuwa Waziri Ummi alikuwa mtu mwadilifu sana asiyeweza kumvumilia mtu asiye mwadilifu… je, unadhani labda mumewe alikuwa na makandokando jambo lililosababisha hata wakatengana?”

Kwa mara ya kwanza Dk. Uledi aliachia tabasamu. “Ni kweli Ummi hakuwa mwanamke wa kumvumilia mtu mwenye makandokando lakini sidhani kama mumewe alikuwa hivyo.”

“Zipo tetesi kuwa Rashid Mrutu ni mmoja wa wafanyabiashara wakubwa wa mihadarati, kuna ukweli wowote juu ya hilo?” nilimuuliza Dk. Uledi huku nikimtazama kwa umakini.

Dk. Uledi alisita kidogo kabla hajasema, “Hizo ni tetesi na zitabaki kuwa tetesi.”

“Na inaonekana kuwa lile bomu lililolipuka pale Alpha Mall lilikuwa limekusudiwa kumuua Waziri Ummi, hili unalisemaje?” nilimuuliza tena Dk. Uledi, na hapo nikamwona akishtuka kidogo.

“Kwa vipi?” Dk. Uledi aliniuliza huku akinikazia macho.

“Mazingira yanatia shaka. Kifo cha waziri kimetokea wiki tatu tu tangu kijana wake Fikiri Mrutu afe kifo cha kutatanisha, halafu bomu lenyewe lililipuka muda mfupi tu tangu afike pale Alpha Mall hali inayoashiria kuwa wauaji walimfuatilia au kukusudia yeye. Wewe unasemaje?”

“Dah, nahisi kuwa maswali yako yalipaswa kuulizwa na polisi na si mwandishi wa habari kama wewe,” lilikuwa jibu la Dk. Uledi.

“Ni kweli lakini mwandishi mzuri ni yule anayewatangulia polisi kubaini mambo, si kusubiri taarifa ambazo mara nyingi huwa zimechujwa sana na kukosa ukweli,” nilimwambia Dk. Uledi. Hata hivyo hakuwa tayari kunieleza hisia zake…

_____

Sasa nilikuwa nimetulia ofisini kwangu nikiwa na magazeti yale nikizipitia habari kuhusu shambulio la bomu lililosababisha kifo cha Waziri Ummi Mrutu. Katika yote niliyoyasoma au kuyasikia kitu kimoja kilikuwa dhahiri, kama alivyoandika mwandishi wa gazeti la Rindima kuwa; Waziri Ummi hakustahili kufa kifo hiki.

Dhana hii ilinipa kitendawili kigumu sana kukitegua hasa nikizingatia ukweli kuwa muuaji au wauaji wake wangeweza kutumia njia nyingine kumuua lakini badala yake wakaamua kutumia njia ya bomu ambalo liliua pia watu wengine wasiokusudiwa.

Wakati wanahabari waking’ang’ana na tukio ambalo kwa mujibu wa kazi yao lilikuwa la kusisimua, wanausalama tulikuwa katika wakati mgumu kuliko wakati mwingine wowote ule. Tulihangaika kimwili na kiakili, jasho likitutoka, hasa kwa kutokujua wapi pa kuanzia na wapi pa kuishia.

‘Waliolipua bomu hilo walikusudia kutoa ujumbe gani?’ Ni swali la kwanza kabisa ambalo lilivisumbua vichwa vya wanausalama. Tuliteseka zaidi kwa kutokuwa na jibu rahisi kwa swali hilo. Hivyo, maswali yaliyofuatia yalikuwa; ‘Ni nani, au kundi gani lililofanya ugaidi huu?’; ‘Sababu na malengo yao ni ipi?’; ‘Na wangenufaika vipi na kitendo chao?’ Yote haya yalipita katika kila kichwa cha mwanausalama na kutuchanganya zaidi.

Bila ya jibu lolote kwa maswali hayo liliibuka lile kubwa zaidi ambalo si kwamba lilivisumbua tu vyombo vya ulinzi na usalama bali pia lilivitisha sana; ‘Je, tukio hili ni mwanzo au mwisho wa makusudio ya magaidi hao?’

Hadi wakati huo nikiwa nimeketi ofisini kwangu tayari vyombo vya ulinzi na usalama vilikuwa katika hali ya hadhari. Hakukuwa na ndege iliyoruka toka nje au ndani ya nchi bila kupitiwa na macho ya rada za vyombo hivi. Mipaka yote pia ilidhibitiwa huku ikihakikishwa kuwa hakuna shambulio lolote toka nje ambalo lisingedhibitiwa kwa nguvu zote.

Nilikuwa nimemsikia msemaji wa polisi akisema kuwa taarifa ambazo ziliwafikia toka nchi adui na rafiki zilionesha kutokuwepo kwa fununu yoyote ya nchi yoyote, au kundi lolote la kigaidi kujihusisha na tukio hili. hali hii ilizidi kuwachanganya wakuu wa vyombo vya usalama kama ambavyo kila mtu alivyochanganywa!

Nilishusha pumzi na taratibu niliachana na magazeti yale na kukizungusha kiti changu cha ofisini nilichokikalia kwenda upande wa kushoto sehemu kulipokuwa na rafu yenye vitabu, majarida mbalimbali na mafaili, na hapo nikaweka kituo nikiyatembeza macho yangu kudadisi kama kungekuwa na chochote ambacho kingenisaidia katika kufanyia kazi zangu. Wakati nikitafakari simu yangu ya mkononi ikaanza kuita.

Niliitazama vizuri na kuliona jina la Tunu Michael kwenye kioo cha simu, nikashusha pumzi na kuminya midomo. “Hallo, mkuu!” nilizungumza kwa sauti tulivu mara tu nilipoipokea ile simu na kuiweka kwenye sikio langu.

“Vipi umefikia wapi?” Tunu aliniuliza

“Bado nachakata taarifa, baadaye nitaziwasilisha kwako,” nilimjibu.

“Jitahidi maana wakuu wananiuliza tumefikia wapi. tunazo siku tatu tu za kufanikisha jukumu letu. Pia kuna jambo nimelipata nadhani linaweza kuwa msaada mkubwa katika kuwafikia adui zetu,” Tunu alisema. “Naomba tuonane saa kumi na mbili na nusu jioni. Nitakueleza baadaye wapi tukutane.”

“Sawa, mkuu,” nilisema na hapo Tunu akakata simu.

Baada ya simu ya Tunu kukatwa mara ile simu ya mezani mle ndani ofisini nayo ikaanza kuita. Nikaunyanyua ule mkonga wa simu na kuuweka sikioni huku macho yangu yakiutazama mlango wa kuingilia mle ndani.

Sauti laini ya kike kutoka upande wa pili wa ile simu ilinitanabaisha kuwa mzungumzaji alikuwa Radhia Jumanne, mfanyakazi wa mapokezi.

“Hallo, Radhia!” niliongea kabla Radhia hajaniambia dhumuni la simu ile baada ya kuisikia sauti yake.

“Bosi, kuna mtu anahitaji kukuona,” sauti nyepesi ya Radhia ilipenya kwenye ngoma ya sikio langu.

“Ana shida gani?” nilimuuliza Radhia kwa wasiwasi.

Endelea...
 
taharuki..jpg

291

“Sijui, amesisitiza kuwa anahitaji kukuona wewe,” Radhia alisema.

“Ni mwanaume au mwanamke?” nilimuuliza tena Radhia.

“Ni mwanamke, ni mama wa makamo…” Radhia alisema na hapo hapo nikamwambia, “Basi mruhusu aje!”

“Sawa bosi,” Radhia alisema na kukata simu.

Nilibaki nikiwa nimeushika ule mkonga wa simu nikiutazama kwa makini kana kwamba ulikuwa na majibu yote kuhusu kile kilichokuwa kikipita kichwani kwangu muda huo. Mawazo yangu yalikuwa yakisafiri na kufikiri aina ya mgeni aliyetaka kuniona.

Baada ya sekunde chache kupita nikasikia sauti ya mtu akigonga mlango wa ofisi yangu na kisha akaufungua na kuingia. Machoni mwangu ilijengeka taswira ya mama mwenye umri wa takriban miaka hamsini. Alikuwa mrefu na mnene akiwa katika mwonekano wa kupendeza wa gauni zuri la kitenge. Uso wake ulikuwa umesawajika.

“Karibu sana, mama,” nilimkaribisha mama yule huku nikimtathmini.

“Nashukuru sana, baba,” yule mama aliniitikia huku akiyatembeza macho yake mle ndani kama aliyekuwa akiipeleleza ofisi yangu kisha akapiga hatua zake taratibu kuisogelea ile meza yangu ya ofisini na alipoifikia akavuta kiti na kuketi.

Muda wote macho yangu yalikuwa yameweka kituo kumtazama yule mama kwa umakini hadi alipoketi kwenye kiti, kisha nilishusha pumzi za ndani kwa ndani.

“Naitwa Mama Rutabingwa… Anastazia Rutabingwa,” yule mama alijitambulisha kwangu na kuvunja ukimya.

Okay, karibu sana,” nilimkaribisha tena.

“Sijui wewe ndiwe Jason Sizya?” yule mama aliniuliza huku akinitazama kwa wasiwasi.

“Kwani unataka kuonana na Jason Sizya au unahitaji huduma inayotolewa na ofisi hii?” nilimuuliza yule mama kwa udadisi zaidi.

“Vyote!” yule mama alinijibu kwa utulivu huku akiumba tabasamu hafifu usoni mwake.

“Basi mimi ndiye Jason Sizya,” nilimwambia kumtoa wasiwasi.

“Ofisi yako inashughulika na nini?” yule mama aliniuliza, na hapo nikamtazama kwa mshangao kidogo.

“Kwani wewe ni kipi kilichokuleta hapa?” nilimuuliza huku sauti yangu ikishindwa kuuficha mshangao wangu.

Yule mama alishusha pumzi ndefu kisha akazamisha mkono wake wa kuume ndani ya mkoba wake aliokuwa amebeba, kisha akaongea kwa huzuni, “Kijana wangu amekufa wiki mbili zilizopita akiwa mikononi mwa Polisi…”

Mkono wake ulipotoka ulikuwa umeshika picha fulani ya ukubwa wa 5X7 ambayo aliisogeza karibu yangu pale juu ya meza. “Jina lake anaitwa Magnus Rutabingwa…”

Niliichukua ile picha pale juu ya meza na kuitazama kwa umakini. Ilikuwa ni picha ya kijana wa kiume mwenye umri kama wangu, alikuwa mwembamba mrefu na alivaa suti ya bluu ya dengrizi, yaani suruali na koti vyote vya kitambaa cha dengrizi. Alikuwa na nywele nyingi kichwani alizozinyoa mtindo wa kileo na ndevu alizozichonga mtindo wa ‘O’. Uso wake ulikuwa na furaha.

Niliitazama vizuri sura yake lakini sikuweza kumtambua. Ilikuwa sura ngeni kabisa machoni mwangu.

“Magnus Rutabingwa!” nilirudia kulitamka jina lile huku nikimtazama yule mama.

Kisha yule mama alitoa picha nyingine na kuiweka juu ya meza. Nikaichukua na kuitazama, ilimwonesha kijana yule yule akiwa katika mavazi yale yale ila safari hii alikuwa ameketi na msichana mmoja wakiwa katika hali ya mahaba. Nikagundua kuwa picha hizo zilipigwa siku moja na eneo moja.

Msichana huyo alikuwa mrefu mwenye rangi ya ngozi ya maji ya kunde na alivalia blauzi ya rangi ya kijivu pamoja na suruali nyeupe ya dengrizi iliyobana vyema umbo lake zuri. Miguuni alivalia raba nyeupe. Nywele na masikio yake alikuwa ameyaziba kwa kofia ya kijivu aina ya mzula. Uso wake ulikuwa mrefu na mpole, wenye macho ya wastani ila makali. Mdomo wake mdogo alikuwa ameupaka rangi ya kahawia na ulichanua kwa tabasamu. Yeye pia sura yake ilikuwa ngeni kabisa machoni kwangu.

“Huyo ni mkewe… Nataka unisaidie kupata haki yangu juu ya mwanangu maana naona wanataka kunidhulumu,” yule mama aliniambia huku akiyazuia machozi yaliyoanza kumtoka.

“Haki ipi, mama? Na nikusaidieje kuipata hiyo haki wakati mimi si mwanasheria?” nilimuuliza yule mama huku macho yangu yakielea juu ya zile picha.

“Magnus ni mwanangu wa kwanza kati ya watoto watatu niliowazaa, alikamatwa na polisi kwa kesi ya kubambikwa baada ya kuwa kwenye mgogoro na mkewe ambaye alifunga naye ndoa miaka miwili iliyopita ila hawakubahatika kupata mtoto…” yule mama alisema kwa huzuni. “Inasemekana aliteswa sana akiwa chini ya ulinzi wa polisi na kufikwa na umauti huo. Kama mama nilikataa kuuchukua mwili nikitaka uchunguzi ufanyike kwanza lakini huyo mwanamke akanizunguka na kuuchukua mwili akidai kuwa yeye ndiye mke na mwenye haki ya kumzika Magnus…”

“Dah! Kama mke halali huenda ni kweli ana haki ya kumzika mumewe lakini ilikuwaje aka…” nilitaka kumuuliza yule mama lakini akanikata kauli.

“Walikuwa wametengana kwa miezi sita sasa kwa kuwa huyu binti hakuwa mwaminifu kwenye ndoa yake. Nimeshangazwa sana kuona akiibuka baada ya Magnus kufa na kutoa madai ya ajabu, tena akisaidiwa na kigogo mmoja ambaye ni mjomba wake ili wadhulumu mali za mwanangu,” yule mama alisema kwa huzuni.

“Mwanao alikuwa na mali zipi?” niliuliza kwa utulivu.

“Alimiliki maduka mawili makubwa ya nguo moja likiwa Kariakoo na lingine Kijitonyama, nyumba moja ya kisasa iliyopo Kijitonyama, kiwanja kikubwa huko Bunju na magari mawili. Vyote hivi huyu mwanamke kwa kushirikiana na jamaa zake wanataka kudhulumu.”

“Sasa kwa nini usiende kufungua shauri mahakamani kama unadhani mwanao anapokwa haki yake?” nilimuuliza kwa mshangao yule mama.

“Hata nikifungua kesi najua sitatendewa haki kwa kuwa mjomba wa huyu binti ni Waziri wa Katiba na Sheria,” yule mama alisema kwa huzuni.

“Sasa ulitaka nikusaidie kivipi, labda…!” nilimsaili huku nikimtazama kwa umakini.

“Najua wewe ni mwandishi mahiri wa habari za uchunguzi usiyeogopa chochote, kalamu yako ni silaha kubwa sana katika mapambano ya kudai haki… kwa hivyo nimekuja kwako kutaka msaada, ufuatilie jambo hili na kuandika habari hizi ili dunia ijue kuwa mimi mwanamke mjane nadhulumiwa mali ambazo Magnus amezirithi toka kwa marehemu baba yake, hakuzichuma na mkewe,” yule mama alisema na kufuta machozi yaliyoanza kumtoka na kuchuruzika mashavuni.

Nilimtazama yule mama kwa muda kisha nikamuuliza ni wapi yule binti, mke wa kijana wake alikokuwa anaishi! Akanieleza jina la eneo, mtaa na namba ya nyumba.

Nilimwita Evans Mwinuka nikamkabidhi kwa yule mama nikimtaka akamsikilize kwa umakini na kuona namna ya kumsaidia kulishughulikia suala lake kwa kuwa mimi nilikuwa na mambo mazito zaidi ya kufuatilia. Evans alikuwa mmoja wa waandishi wachache wa habari wafukunyuku waliokuwa tayari kufanya kazi za hatari hata kwenye mazingira magumu na ya hatari.

Evans alishaandika habari za matukio kadhaa yaliyoitikisa nchi, matukio ambayo kwa wengine zilikuwa habari mpya (exclusive news) za kutisha. Jambo hili lilimfanya kupewa jina la ‘Sauti ya Jamii’, jina alilopewa hata kabla sijakutana naye na kumwajiri kwenye kampuni yangu.

Endelea...
 
taharuki..jpg

292

Alikuwa mrefu kiasi mwenye mwili mkubwa na rangi ya ngozi yake ilikuwa ni maji ya kunde. Alikuwa mcheshi sana ingawa kwa mtazamo wa haraka haraka ungeweza kudhani kuwa hakuwa mzungumzaji. Sura yake ilikuwa ya tabasamu muda wote na macho yake yalikuwa makali kama macho ya kachero mbobezi. Urefu, mwili wake na utanashati wake vilikuwa vitu vilivyowavutia wasichana wengi aliokutana nao.

Evans alikuwa mcheshi sana na mchapakazi aliyeitambua kazi yake vizuri. Hakuna mwandishi yeyote, hata mmoja, aliyepata bahati ya kufanya naye kazi, aliyemchukia wala kutofurahishwa naye bali walifarijika sana kufanya kazi pamoja.

Kama ilivyokuwa kwangu, Evans hakusita kufichua uovu popote ulipofanyika na wakati wowote pasipo kujali ulifanywa na nani au kikundi gani cha watu, ilimradi tu maslahi ya taifa yalionekana kuchezewa, na alijitoa maisha yake kwa ajili ya jamii kwa hali na mali bila kujali kama kazi hiyo ingeyagharimu maisha yangu au la! Ilikuwa kawaida yake kutoacha mambo juu juu kama ilivyo kwa waandishi wengi.

Alifanya kazi zake kwa uangalifu mkubwa pasipo kubahatisha, na pale alipohisi kulikuwa na utata hakuacha kufanya uchunguzi wa kina au kutafuta uhakika kwangu na kwa watu alioamini kuwa wangekuwa na majibu au walilifahamu jambo hilo zaidi yake.

Wakati yule mama akiondoka na Evans ilikuwa ikielekea kutimia saa tisa na robo za mchana. Nikatamani kujua vyombo vya habari vilikuwa vimebaini nini hadi muda huo, nikawasha runinga na kufuatilia matangazo yaliyokuwa yakiendelea kwenye runinga. Nilimsikiliza mtangazaji wa kituo kimoja cha runinga cha nyumbani aliyekuwa akifanya mahojiano na baadhi ya jamaa na majirani wa Waziri Ummi, nyumbani kwa marehemu Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Na hapo nikatamani kucheka. Yalikuwa ni mahojiano ya kawaida sana, na mwandishi hakuwa mbunifu katika kuuliza maswali bali alifanya kazi ki-mazoea, Waingereza wanasema “business as usual”.

Mmoja wa wanafamilia aliyejitambulisha kuwa ni mama mdogo wa Waziri Ummi, alikuwa anahojiwa na kueleza namna alivyoguswa na msiba huo. Hata hivyo, mwanafamilia huyo hakuweza kueleza kwa muda mrefu akakabwa na kilio cha kwikwi, alionekana kusononeka sana, na mara kikohozi kidogo kilimtoka, na nyuma yake wimbi la machozi lilikuja mbio, na mahojiano yakakatishwa. Kisha mtangazaji alianza kumhoji kaka wa marehemu, Dk. Uledi ambaye pia alikuwa na majonzi makubwa.

Mtangazaji alimuuliza Dk. Uledi ameupokeaje msiba huo! Nikashangaa sana! Iweje mwandishi mkongwe kama yule kuuliza swali jepesi kiasi kile ‘eti umeupokeaje msiba?’ kana kwamba yeye hajawahi kufiwa na ndugu au mtu wa karibu! Nikabadilisha kituo, na hapo nikakutana na mahojiano mengine kuhusiana na hali halisi ya usalama nchini. Hapo nilimwona Katibu Mkuu wa chama kimoja cha upinzani akieleza kuwa wamepokea taarifa zile za ugaidi kwa mshtuko mkubwa sana hasa kifo cha waziri aliyekuwa tegemeo la taifa.

“Chama kinalaani tukio hilo la kigaidi na tunavitaka vyombo vya usalama kuharakisha uchunguzi wa tukio hili na kuchukua hatua kali kwa magaidi wote waliohusika,” alisema.

Nikabadilisha tena na hapo nikakutana na taarifa toka Jeshi la Polisi. Nilimwona msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Selemani Bwera, akivieleza vyombo vya habari kuwa bomu lililolipua jengo la Alpha Mall lililetwa hapo na pikipiki ya magurumu matatu na kwamba tayari wameshaanza uchunguzi wa kujua nani mmiliki wa pikipiki hiyo na nani aliyekuwa akiiendesha.

Kisha alieleza kwamba, timu iliyojumuisha wataalamu wa milipuko (Bomb Squad) na wataalamu wa uchunguzi wa eneo la tukio (Forensic Experts) walikuwa wamefanya uchunguzi kwenye eneo la tukio na kutambua aina ya bomu lililotumika, vifaa na aina ya vilipuzi vilivyotumika kutengeneza bomu, nguvu na uzito wa mlipuko husika, na madhara yaliyosababishwa na bomu hilo.

Ripoti ya awali ilisema kuwa mlipuko uliotokea pale Alpha Mall ulikuwa na uzito wa kilogramu 600 ambapo madini aina ya TNT yalikuwa yameunganishwa na gesi aina ya methane upande mmoja na mwingine liquefied petroleum gas (LPG), vyote vilikuwa vimeshindiliwa kwa mgandamizo mkubwa sana ndani ya tanki dogo na kuzungukwa na mifuko kadhaa ya amonium nitrate, kiasi kwamba zikidaka moto basi hilo tanki lazima ligeuke kombora mfano wa kombora la Rocket Propelled Grenade (RPG).

Hiyo kwangu ndiyo ilikuwa taarifa muhimu niliyoihitaji, nilichukua notebook yangu nikaandika taarifa hiyo: TNT + LPG + Amonium Nitrate = RPG.

Baada ya hapo yaliendelea matangazo mengine ambayo hayakuwa muhimu sana kwangu. Sikutaka kuendelea kusikiliza matangazo yale, niliizima runinga kisha niliyahamishia mawazo yangu kwenye tarakilishi yangu. Macho yangu niliyaelekeza kwenye kioo cha ile tarakilishi lakini sikuwa naona chochote, fikra zangu wakati huo zilikuwa nje kabisa ya jengo lile. TNT + LPG + Amonium Nitrate = RPG.

Sasa nilitaka kujua iwapo kuliwahi kutokea shambulio la kigaidi ambalo bomu la aina hiyo kama ilivyoelezwa na SACP Selemani Bwera lilitumika toka miaka kumi iliyokuwa imepita. Majibu niliyopata yalikuwa ya kusisimua.

Nikiwa mfuatiliaji mzuri wa maswala ya aina hii nilitumia programu yangu ya TracerMark kutafuta taarifa hizo. Matukio yapatayo kumi na mbili yalikuwa yameripotiwa kwa uwazi, majina au aina ya watuhumiwa wakitajwa na waathirika wa matukio hayo waliopoteza maisha yao kwa bomu la aina hiyo.

Mehmet Aghi, mtuhumiwa maarufu wa Uturuki aliyekuwa akitumikia kifungo cha miaka ishirini na tano jela, alitajwa mara tatu kuhusika na matukio matatu ya kigaidi kwa kutumia aina hii ya bomu.

Katika tukio moja, mwanasiasa mmoja mkubwa wa Nigeria aliyekuwa akipinga sera ya kampuni za kibeberu za mafuta, alijeruhiwa sana na kuponea chupu chupu huku baadhi ya wafamilia na jamaa zake wakiuawa, wakati wakiwa kwenye sherehe ya kifamilia. Tukio la pili lilitokea nchini Venezuela, ambapo Waziri wa Viwanda wa nchi hiyo aliuawa pamoja na watu wengine.

Tukio la tatu lililomhusisha Mehmet Aghi lilitokea katika nchi ya Siria dhidi ya kiongozi mmoja mpinzani wa Rais wa nchi hiyo ambaye alionekana kuwa kibaraka wa Marekani na Israeli. Huyu alifia hospitalini, lakini ilikuwa baada ya kueleza jinsi Mehmet alivyomtumia ujumbe wa vitisho mara tatu kabla ya jaribio hilo.

Hadi hapo sikuona kama Mehmet alikuwa mtu wangu, kwani tayari alikuwa gerezani akitumikia kifungo cha miaka ishirini na tano, pia mara nyingi alitoa onyo kabla ya kutekeleza kusudio lake.

Niliendelea kuchimbua zaidi taarifa zile na kukutana na watuhumiwa wengine wawili, akiwemo raia wa India kutoka Jimbo la Kashmir, Rajesh Khan, ambaye alikuwa mtu maarufu sana duniani, na pia alikuwa akihusishwa na undumilakuwili (double agent) kati ya India na Pakistani. Hata hivyo baada ya kusoma habari zao hawakunivutia kabisa.

Endelea...
 
taharuki..jpg

293

Hadi hapo bado sikuona kama matukio yao ya kigaidi yalionesha kuwa na uwiano wala malengo maalumu isipokuwa walionesha kutumiwa kwa sababu ya uroho wa fedha tu.

Niliendelea kufuatilia kwa umakini nikichimbua taarifa lakini sikuona taarifa ambazo zingenivutia na ilibaki kidogo tu niachane na taarifa hizo na kuzima tarakilishi ili niende msibani mara nikakutana na tukio moja lililonifanya nisite kidogo.

Lilikuwa tukio la lililodhaniwa kuwa na chembechembe za ugaidi lililotokea miaka mitano iliyokuwa imepita katika Viwanja vya Uhurumaarufu kama Uhuru Park, jijini Nairoibi nchini Kenya. Tukio hili lilihusu mlipuko mdogo wa bomu uliotokea katika mkutano wa kampeni ya ‘Uzalendo Kwanza’ ambao Naibu Rais ndiye aliyetarajiwa kuwa mgeni na badala yake akawakilishwa na Gavana wa Nairobi, Paul Chege. Katika tukio lile watu 13 walipoteza maisha, 26 walijeruhiwa akiwemo Paul Chege huku watatu kati yao wakiwa katika hali mahututi.

Ilikuwa taarifa ya mauaji ambayo yaliyowahi kutikisha jiji la Nairobi na kuwasisimua sana wanahabari na wachunguzi wa maswala ya ugaidi Afrika Mashariki kwani japokuwa nchi ya Kenya ilikuwa ikiandamwa na matukio ya kigaidi toka kikundi cha kigaidi cha Alshabab lakini tukio hili lilikuwa la aina yake lililokuwa tofauti na matukio mengine yaliyokihusisha kikundi hiki.

Lilikuwa tukio ambalo gaidi aliyehisiwa kulifanya alijulikana kwa jina la Bosco Gahizi ingawa hakupata kuonekana wala kutuhumiwa kwa vigezo vya dhati na mpelelezi yeyote yule wa Afrika Mashariki. Bosco Gahizi alikuwa akiua kwa bomu la mchanganyo wa TNT + LPG + Amonium Nitrate, na mwaka uliofuatia baada ya tukio lile la Nairobi aliibuka tena katika nchi tofauti, kwa kazi tofauti.

Kama mtu mwingine yeyote yule aliyevutwa na habari yoyote iliyohusishwa na muuaji huyu, nilizisoma habari zake kwa umakini mkubwa na tafakuri. Katika miaka mitano iliyokuwa imepita matukio manne yalihusishwa na gaidi huyu. Mtindo wa mauaji ulikuwa ni ule ule wa kutumia bomu la mchanganyiko wa TNT + LPG + Amonium Nitrate na kila alipotimiza ugaidi wake alitoweka bila kuacha chembechembe yoyote ya kasoro ambayo ingeweza kumfanya apatikane.

Hata hivyo, tukio la nne alilolifanya nchini Ivory Coast lilitibuliwa toka mikononi mwa Gahizi baada ya watuhumiwa kadhaa kupatikana na ushahidi kudhihirisha kuwa waliyafanya au kushiriki.

Gahizi alikuwa Mnyarwanda wa kabila la Kihutu aliyekimbia machafuko nchini Rwanda kufuatia mauaji ya kimbali yaliyoikumba nchi hiyo baada ya mauaji ya Rais Habyarimana. Mengi yaliandikwa kuhusu historia yake kuwa alikuwa jasusi hatari sana, mbobezi wa ujasusi wa kimtandao ambaye alikuwa akikodiwa kupanga matukio ya kigaidi kwenye nchi tofauti za Kiafrika.

Wazazi wake na ndugu zake wote walikufa kwenye machafuko hayo na yeye kuchukuliwa hadi kambi moja nchini Uganda ambako haikuchukua muda wasimamizi fulani wa kambi ile kugundua kuwa alikuwa kijana jasiri sana mwenye upeo mkubwa wa fikra na mstahimilivu, na huo ukawa mwanzo wa safari yake mpya ya kimaisha.

Baada ya hapo alihamishwa toka kambi ile na kupelekwa katika nchi nyingine ambayo iliendelea kubaki kuwa siri kubwa na huko alipewa mafunzo ya nguvu. Alifundishwa kutumia silaha mbalimbali, kutengeneza mabomu, kutega na kuyategua n.k. huko ndiko alikofundishwa namna ya kutengeneza bomu la mchanganyiko wa TNT + LPG + Amonium Nitrate ambalo lingeweza kubomoa jumba la ghorofa zaidi ya kumi.

Alikuwa amefuzu kutumia silaha mbalimbali na mafunzo ya kujihami hasa karate na judo na kufanikiwa kupata mkanda mweusi, kiwango cha third degree kabla hata hajajiunga rasmi na chuo chochote. Pia alijifunza lugha mbalimbali kama Kiswahili, Kiingereza, Kifaransa, Kichina, Kiarabu, Kispaniola, Kijerumani na lugha zingine nyingi. Lugha zote hizi alizisoma kwa bidi na alifanya vizuri katika kila lugha aliyofundishwa.

Alikuwa msomi wemye Shaha ya Uhandisi wa Umeme aliyohitimu kutoka katika Chuo Kikuu cha Birzeit nchini Israeli na kisha aliajiriwa kama mkufunzi wa uhandisi umeme katika taasisi ya Electrical Maintenance Bengazi Ltd iliyopo nchini Libya, alikofanya kazi kwa miaka miwili tu akaacha na kujiunga na chuo cha Technion – Israel Institute of Technology ambako pia alijiunga tena na programu maalumu ya kijasusi…

Gahizi ndiye aliyeratibu tukio la kigaidi katika mkutano wa Bulawayo nchini Zimbabwe ambao Rais wa Zimbabwe alinusurika kuuawa na bomu katika Uwanja wa michezo wa White City. Pia alihusishwa kupanga tukio la mlipuko wa bomu katika mkutano wa Waziri Mkuu wa Ethiopia kwenye bustani kuu ya Meskel jijini Addis Ababa, ambapo watu 83 walijeruhiwa huku 6 wakiwa katika hali mahututi. Yapo matukio mengine mawili aliyohusishwa nayo katika nchi za Rwanda na Ivory Coast.

Gahizi alikuwa akipanga mambo yake kwa ustadi mkubwa huku akihakikisha washirika wenzake hawajuani na wala hawamjui bosi wa uhalifu na alikuwa haachi alama, na moja ya vitu vilivyomsaidia sana kufanya matukio ya ugaidi kwa mafanikio bila kuhusishwa ni uwezo wake wa kupanga mikakati ya utekelezaji! Alikuwa mwanamkakati mzuri wa kiufundi wa matukio!

Kwanza alipenda kuzuru eneo alilotaka kufanyia uhalifu kazi ambayo aliifanya kwa umakini mno, kisha alitafiti juu ya tukio lenyewe aambavyo angelitekeleza kwa kusoma mandhari yanayozunguka eneo husika na akijiridhisha alitafuta washirika aliodhani wangemfanyia kazi, akiwalenga watu wenye makandokando kwa kuwatishia kutoa siri zao nje endapo wasingempa ushirikiano…

Gahizi alikuwa anatafutwa sana na wanausalama wa nchi mbalimbali kwa kupanga matukio ya uhalifu.

Kwa habari hizi niliamini kuwa hata tukio la bomu pale Alpha Mall lilifanyika kwa mkono wa Gahizi hasa ikizingatiwa kuwa bomu lililotumika lilikuwa na mchanganyiko ule ule wa TNT + LPG + Amonium Nitrate.

Endelea...
 
taharuki..jpg

294

Hivyo, niliposoma tena habari hizi zilizokusanywa na wanausalama wa mashirika ya kijasusi ya Mossad la Israeli na CIA la Marekani kumhusu Bosco Gahizi akili yangu ilizinduka ghafla nilipoyalinganisha na tukio la bomu katika jengo la Alpha lililosababisha kifo cha Waziri Ummi Mrutu. Sasa sikuwa na shaka kabisa kuwa mkono uliotumika kuandaa bomu hili ulikuwa wa Gahizi.

Kwa namna fulani, nilijisikia faraja kwa kulibaini hilo. Niliamini kuwa nilikuwa nimepiga hatua kubwa sana. Hata hivyo, haikuchukua muda kugundua kuwa ilikuwa hatua fupi kwani bado ilizua maswali mengi zaidi ya majibu. Je, ni akina nani waliomkodi Gahizi kufanya ugaidi? Kwa uzoefu wangu nilishuku kuwa Gahizi hakuwa mwendawazimu bali lilikuwepo kusudi maalumu, lilikuwepo kundi la watu hususan vigogo au wafanyabiashara wakubwa kuliko mmoja mmoja kwani ndani ya kundi hilo kungetokea mmoja wao ambaye siku moja angeutapika ukweli, ama katika ulevi ama kwa matumizi ya fujo ama hata usaliti tu.

Gaidi mmoja mmoja ni yeye Gahizi na roho yake. Asingetoa siri zake kwa gharama zozote hata kwa kumwuza mama yake mzazi. Sasa niliamini kuwa pamoja na kwamba nilikuwa na ile video iliyomwonesha yule mtu (ambaye bado sikufahamu kama ndiye Gahizi mwenyewe au la) aliyetega lile bomu lililomuua Waziri wa Mambo ya Ndani pamoja na watu wengine, lakini kazi iliyokuwa mbele yangu haikuwa lele mama. Nilihitaji kujuani nani waliomtuma Gahizi na sababu ipi iliyowafanya wamuue waziri huyo?

Mara nikakumbuka jambo. Naam… Kulikuwa na jambo lingine muhimu sana la kulifuatilia! Mojawapo ya kanuni ya upelelezi ni kwamba kila kitu mbele yako ni mtuhumiwa katika namna yake. Hutakiwi kupuuza chochote kile, wala kukidharau. Kwani yeyote anaweza kufanya lolote kwa sababu yoyote.

Nikazama kwenye mtandao wa ‘Youtube’, kisha nikaandika maneno “Hotuba za Waziri Ummi Mrutu” kwenye kiboksi cha mtandao huo na hapo hapo zikaja video nyingi za waziri huyo za michango yake bungeni na kwenye shughuli zake mbalimbali, video zilizokuwa 'hot issues' mtaani.

Licha ya kusifika kwa ukali lakini Waziri Ummi Mrutu alikuwa mwanamke mpole sana kwa wananchi wanyonge. Picha za video zilifichua uso wake mzuri uliojaa ucheshi, huku macho yake yakionesha ung’aavu na hekima. Kiwiliwili chake chenye urefu wa kadiri, kilijaa uhai na matumaini yote katika maisha. Hata sauti yake, pale video moja ilipomwonesha wakati akitoa hotuba enzi za uhai wake, ilithibitisha jambo moja; hakustahili kufa kabisa kufa kifo kile.

Katika video ile Waziri Ummi alionekana akiongea kwa uchungu kuhusu ufisadi ulivyokuwa umetamalaki nchini Tanzania na alidai kuwa kulikuwa na viongozi wenye akaunti za mabilioni ya shilingi katika benki nje ya nchi hasa Uswisi na alikuwa tayari kuwashughulikia bila kujali nafasi zao kwenye jamii au uhusiano wake na wao na kwamba akikuwa akiiandaa orodha yao na pindi akikamilisha angeyaweka majina yao hadharani bila woga.

“Ni viongozi wasio na uzalendo, wanaodhoofisha uchumi wa nchi yetu, viongozi waliojawa na uchu wa madaraka na kufuja fedha za wavuja jasho. Ni viongozi ambao nashangaa ninaposikia mnawapamba kwa msamiati uliojengwa kitafsida zaidi, eti mafisadi! Ukweli unabaki kuwa hawa ni wezi, matapeli na majambazi kama walivyo majambazi wengine… na walipaswa kuwa gerezani saa hizi…” video hiyo ilimwonesha Waziri Ummi akieleza kwa uchungu.

Katika video nyingine Waziri Ummi alikuwa akiwasema viongozi wa Jeshi la Polisi kuwa walikuwa wanawaogopa wafanyabiashara wa mihadarati na wengine walikuwa wanashirikiana nao, akasema kuwa yupo tayari kwa vita dhidi yao na kuwa aliwafahamu na orodha yao alikuwa nayo.

Kisha niliiona video ambayo ilisemwa kuwa ndiyo ilikuwa hotuba ya mwisho ya Waziri Ummi Mrutu kabla hajauawa, hotuba hiyo alikuwa ameitoa bungeni siku mbili tu kabla ya tukio lile la kigaidi lililokatisha maisha yake. Katika video hiyo Waziri Ummi alieleza nia yake ya kuwasilisha muswada wa sheria ya kuweka mipaka kwa bidhaa za nje kwenye kikao kijacho cha Bunge.

Waziri Ummi alisema kwamba soko la bidhaa za Tanzania lilikuwa limefurika bidhaa bandia na hafifu kutoka nje hasa China zilizokuwa zikiingizwa na wafanyabiashara wasio wazalendo kwa kushirikiana na maofisa wa forodha na vigogo fulani, na kwamba watu hao walikuwa wanadhoofisha uchumi wa ndani, kwa bidhaa za wazawa kukosa soko.

Katika hotuba hiyo Waziri Ummi alisema kuwa, kwa asilimia kubwa bidhaa za nje hasa China zilikuwa zinawaharibu wanawake wa Kiafrika, walikuwa wanabadilika rangi ya ngozi kama kinyonga na hata shepu zao zilianza kuharibika. “Kwa nini tusiruhusu bidhaa halisi za Kiafrika zichukue nafasi ya soko badala ya hizi takataka za Kichina?” Waziri Ummi alisema kwa uchungu.

Kisha alibainisha kuwa kulikuwa na wafanyabiashara wakishirikiana na baadhi ya vigogo walikuwa wanamshutumu na kumtumia jumbe za vitisho lakini yeye hakuogopa na wala asingeacha kuwapigania Watanzania na wana Afrika Mashariki hata kama ingembidi kufa. Baada ya hapo ndipo akaahidi kuwa alikuwa mbioni kulishauri Baraza la Mawaziri aruhusiwe kuwasilisha muswada bungeni ili Bunge litunge sheria ya kuweka mipaka ya bidhaa za nje ambazo zilitakiwa ziongezewe kodi ili biashara za wazawa na wafanyabiashara toka nchi za Afrika Mashariki wapate ahueni.

Kufika hapo kengele ya hatari ikalia kichwani mwangu na mlango wa sita wa fahamu ukafunguka. Nilihisi kuwa hapo ndipo kulikuwa na harufu ya jambo nililopaswa kulichunguza. Sikutaka kuzipuuza hisia zangu, niliona kuwa nimepata mahali pa kuanzia kuwatafuta maadui wa waziri huyo ambao ndio waliomkodi Bosco Gahizi kufanya kile alichokifanya.

Hata hivyo upepo ulikuwa haueleweki! Baharia yeyote mzoefu hawezi kujitoma baharini bila uhakika wa safari yake. Hivyo, nilifikia uamuzi wa kulifikisha suala hili kwa mkuu wangu ili niingie kizani kwa ajili ya kuusoma mwenendo wa mambo kabla ya kuja na mkakati kabambe wa kuwatia nguvuni watu hao.

Nilishusha pumzi za ndani kwa ndani nikionesha kuridhika na hatua niliyoifikia kisha niliinuka kutoka kwenye kiti changu huku nikiwa natabasamu, nikaitia mikono yangu mifukoni kwa utulivu na kugeuka kuelekea dirishani. Nilisimama pale dirishani na kwa kupitia ukuta msafi wa kioo cha dirisha hilo niliweza kuona vizuri mandhari ya nje ya mitaa ile ya Makumbusho. Chini ya lile jengo letu pilika pilika za watu zilikuwa zimerejea.

Nikaiegemeza mikono yangu pale dirishani na huku nikitazama pilika pilika katika Barabara ya Bagamoyo ambazo zilikwisha rudi kama kawaida, kulikuwa na foleni ya magari kwenye barabara na ongezeko la watembea kwa miguu, kelele za watu na honi za magari na pikipiki.

Kwa dakika kadhaa nilitulia pale dirishani huku nikiendelea kutazama mandhari ya eneo lile kana kwamba nilikuwa nikiyaona kwa mara ya kwanza katika maisha yangu. Kisha nilianza kuyachunguza mandhari yale na nisijue nilikuwa nikitafuta nini!

Endelea...
 
taharuki..jpg

295

Kwa utulivu huku nikiwa bado nimeiegemeza mikono yangu pale dirishani nilivutiwa kuwaangalia watoto watatu waliokuwa wakipita chini ya lile jengo letu katika mtaa wa Wakatibado. Watoto wale walikadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 10 na 12, walikuwa wamevalia mavazi chakavu huku wakiwa wanatumia vileo aina ya gundi zilizokuwa kwenye chupa, na mmoja kati yao alikuwa na kipande cha sigara.

Kwa mwonekano wa haraka tu niliweza kuwatambua watoto hao kuwa walikuwa watoto walioishi katika mazingira magumu, wengine huwaita atoto wa mitaani au chokoraa. Niliwatazma kwa umakini na kuhisi donge la huzuni likinikaba kooni, huzuni ilichukua nafasi na kuiondoa furaha yote niliyokuwa nayo muda mfupi kabla sijawaona watoto wale.

This world is not fair! Not fair at all!” (Hii dunia haina usawa! Haina usawa kabisa!) niliwaza kwa huzuni huku nikiwakodolea macho atoto wale.

Nilishusha pumzi ndefu na kuwatazama tena wale atoto lakini sikuwaona. Niliangaza macho yangu huku na kule lakini sikuwaona. Tayari walikwisha potelea mtaani! Nilirejea kwenye kiti changu huku nikihisi moyo wangu kutawaliwa na huzuni kubwa. Mara nikakumbuka jambo…

Nilipanga kuziingiza tena picha za yule mwanamume aliyefika katika jengo la Alpha Mall na ile pikipiki ya magurudumu matatu iliyobeba bomu ili kujiridhisha kuwa hakuwa Bosco Gahizi, jasusi wa kukodiwa aliyejihusisha na kazi za matukio yenye utata kama lile la Alpha Mall. Nikiwa katika kutaka kuziingiza picha zake kwenye programu ya TracerMark mlango wa ofisini kwangu ukafunguliwa ghafla na kunishtua.

Niligeuza shingo yangu kutazama kule mlangoni na kumwona Winnie aliyeingia mle ofisini na kuurudishia mlango, kisha alipiga hatua za madaha kusogelea pale kwenye meza yangu na kisha alisimama huku akinitazama kwa umakini.

Sikupendezwa na ujio wake ofisini kwangu muda huo, hata hivyo nilitengeneza tabasamu la kirafiki la makaribisho huku macho yangu yakiganda kumtazama usoni. Kwa sekunde kadhaa macho yangu yakajikuta yakipumbazwa na uzuri wa binti huyo. Hata hivyo bado nilijishangaa kwa kuendelea kushindana na nafsi yangu kila nilipomwona binti huyu.

Ukweli nilikuwa nikimpenda sana na hata yeye alijua hivyo, na alijitahidi kunionesha kuwa alinipenda sana na muda wote alinisubiri nitamke neno, lakini haikuwa hivyo. Mara nikajishtukia na kushusha pumzi ndefu huku nikilamba midomo yangu iliyokauka.

Winnie alikuwa amesimama akinitazama kwa umakini, alikuwa amebeba kikombe cha kahawa ya Kiitaliano (cappuccino) na sahani iliyokuwa na keki mbili. Ndiyo kwanza nikakumbuka kuwa nilikuwa sijatia chochote tumboni tangu asubuhi. Hata hivyo sikuwa tayari kuipokea kahawa yake, si kwamba sikutaka kunywa kahawa bali nafsi yangu ilisita.

Niliitazama saa yangu, ilikuwa saa kumi kasoro robo jioni! Dah… muda ulikuwa unakimbia kweli kweli! Nilishtuka sana kwa kuwa nilipaswa kwenda kwenye msiba nyumbani kwa Waziri Ummi kabla sijakutana na Tunu saa kumi na mbili na nusu jioni.

Nilimshukuru Winnie kwa kahawa na kuizima tarakilishi yangu kisha niliinuka toka kwenye kiti changu ili niondoke. Muda wote Winnie alikuwa akinitazama usoni kwa umakini kama aliyekuwa akijaribu kuyasoma mawazo yangu. Uso wake uliokuwa umepambwa na tabasamu sasa ulionesha mchanganyiko wa mshangao na hasira. Kisha alivuta pumzi ndefu halafu akazishusha taratibu.

Nilimtazama usoni kwa udadisi na hapo akaachia tabasamu ambalo niliona kabisa lilikuwa la kulazimisha.

“Samahani, Winnie, natakiwa kuwahi sehemu hivyo sitaweza kunywa kahawa,” nilimwambia Winnie huku nikimtulizia macho usoni.

“Mh!” Winnie aliguna kisha alichukua kikombe na sahani yenye keki na kuanza kuondoka pasipo kusubiri neno lolote kutoka kwangu. Alionekana kukasirishw na kitendo changu cha kuikataa kahawa aliyoniandalia.

“Winnie!” nilimwita kwa sauti kavu. Winnie akageuza shingo yake kunitazama, sura bado kaikunja. Nikaongea kwa sauti tulivu huku nikijitahidi kutabasamu, “Naomba usijisikie vibaya, ni kwa kuwa…”

“Wala usijali,” Winnie alinikata kauli. “Si lazima uniamini kama unadhani hisia zako hazitaki kuniamini!”

“Kwa nini unasema hivyo?” nilisema kwa sauti tulivu. “Nakuamini, na zaidi ya yote nakupenda!” nilisema katika namna ya kumtoa shaka.

“Jason, nadhani unapaswa kuwa mkweli tu wa moyo wako badala ya kuniambia maneno ya kunifariji. Najua hakuna kitu kama hicho ndani yako. Suala la kumwamini mtu au kumpenda linatoka moyoni ila kama moyo wako haujaamua, ni sawa tu! Wala usiulazimishe,” Winnie alisema kwa huzuni huku akilengwalengwa na machozi.

“Unajua kabisa kuwa hakuna mtu hapa kazini aliye karibu mno na mimi zaidi yako, jiulize kwa nini!” nilimwambia.

“Tuwe wakweli tu, Jason… nadhani tunapaswa kuangalia roho zetu kama zipo sahihi kwa tukifanyacho. Ni roho pekee ndiyo itakufanya ujue kuwa hili ndilo ama hapana. Najua wajua kuwa huwezi kumtambua mtu kwa kumwangalia lakini kuna muda roho ndiyo inakuongoza kumtambua mtu huyo. Kama huhisi chochote kuhusu mimi ni vyema ukajali sana maamuzi yako kutoka nafsini kuliko kushinikizwa…” Winnie alisema kwa hisia kali. Kisha akaendelea.

“Najua huwezi kusema ukweli kwa kuogopa kuwa labda utaniudhi. Binafsi sina kinyongo kwa sababu najua unapaswa kuangalia roho na nafsi yako inataka nini au kumpenda nani. Kama unaye unayedhani anafaa kuaminiwa, mpe nafasi hiyo lakini uwe macho katika matendo yako. Kamwe usijejutia maamuzi ya nafsi na roho.”

Nilibaki kimya nikimtazama Winnie kwa mshangao wakati akifunguka yaliyokuwemo katika moyo wake.

“Unajua moyo wa mwanadamu ni msitu wenye kiza kinene ambacho kinasababisha usione ya mbele. Moyo wa mwanadamu umegubikwa na weusi ambao ni Mungu pekee ndiye ajuaye nini kilichomo humo. Hakuna kuaminiana katika dunia hii. Wa kumwamini ni moyo wako tu…” Winnie alihitimisha na kufungua mlango kisha alinitazama kwa namna ambayo ilidhihirisha kuwa alikuwa ameumizwa sana moyoni mwake, halafu akatoka na kuufunga mlango nyuma yake.

Kwa sekunde chache zilizofuata nilibaki kimya nikiutazama ule mlango wa ofisi yangu kwa utulivu huku akili yangu ikiwa mbali kabisa na eneo lile. Tangu nilipogundua kuwa Winnie alikuwa ofisa kificho wa usalama wa taifa na huenda alikuwa amepenyezwa kwenye kampuni yangu kwa misheni maalumu, nilianza kuwa makini mno. Nilikuwa na uhakika kuwa hakufahamu kama nilikwisha jua kuhusu jambo hilo.

Hata hivyo jambo ambalo yeye hakulifahamu kabisa ni kwamba mimi nilikuwa jasusi mbobevu. Mtu hatari kuliko hatari yenyewe, na hivyo alipaswa kuniogopa.

* * *

Mambo yanazidi kunoga, endelea kufuatilia Harakati za Jason Sizya...
 
Tuombe Mungu maana sasa hivi naanza kuipitia upya na kubadilisha baadhi ya vitu halafu ndo naposti, kwani nahisi nilivuka mipaka kwa kuongelea mambo yasiyopaswa kuongelewa hadharani...

Tusameheane wakuu...
Kaunda Suit walikuja pm nini? Only in Tz.
 
Tuombe Mungu maana sasa hivi naanza kuipitia upya na kubadilisha baadhi ya vitu halafu ndo naposti, kwani nahisi nilivuka mipaka kwa kuongelea mambo yasiyopaswa kuongelewa hadharani...

Tusameheane wakuu...
Shukrani sana mkuu., tupo hapa tunaendelea kusubiri mwendelezo
 
Haya wapendwa tatizo lishajulikana yani hapa hata asipopost mwaka tatizo limeletwa kwetu natamani tufanye mawili matatu ili tupate kitu roho inapenda. Bishop kama uko radhi weka namba wapenzi wasomaji tujisachi trabu na trati tufanye lolote jambo
 
Haya wapendwa tatizo lishajulikana yani hapa hata asipopost mwaka tatizo limeletwa kwetu natamani tufanye mawili matatu ili tupate kitu roho inapenda. Bishop kama uko radhi weka namba wapenzi wasomaji tujisachi trabu na trati tufanye lolote jambo
No zake ni hizi 0685-666964 thibitisha mkuu@Bishop Hiluka
 
Haya wapendwa tatizo lishajulikana yani hapa hata asipopost mwaka tatizo limeletwa kwetu natamani tufanye mawili matatu ili tupate kitu roho inapenda. Bishop kama uko radhi weka namba wapenzi wasomaji tujisachi trabu na trati tufanye lolote jambo
Dah! Sikuwaza kabisa jambo hili, ahsante sana 🙏 mpendwa kwa kujali..
No zake ni hizi 0685-666964 thibitisha mkuu@Bishop Hiluka
Thanks, man🙏 Boogman nimeipata na ndo maana nimekuja kutupia...
Mkuu Bishop Hiluka thibitisha kama hii ni namba yako please
Ndiyo, namba yangu ni hiyo aliyoibandika Boogman hapo juu...
 
taharuki..jpg

296

Kundi la Buibui…




Saa 12:50 jioni…

MPAKA kufikia muda wa saa moja kasoro robo ya jioni hakukuwa na mtu yeyote aliyekuwa amefikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa kuhusika na tukio la ugaidi katika jengo la Alpha Mall. Maofisa wa Usalama wa Taifa walikuwa wakiendelea kufuatilia taarifa za mtu mmoja aliyeonesha dalili za kutia mashaka. Mtu huyo aliyetambuliwa kwa jina la Saleh Khalid alikuwa amefika katika hospitali moja ya binafsi jijini Tanga akiwa na majeraha miguuni na sehemu za nyuma ya mwili wake.

Hali hiyo ilimpa shaka daktari mmoja aliyemtibu mtu huyo hospitalini hapo, kwamba huenda alikuwa amejeruhiwa wakati akikimbia kutoka katika eneo la tukio. Daktari huyo, aliyekuwa ameajiriwa kama mmoja wa watoa taarifa (informers) wa Idara ya Usalama wa Taifa, aliwapigia simu polisi wa jijini Tanga ambao walimfuatilia mtu huyo na kumweka chini ya ulinzi. Taratibu za kumfanyia mahojiano zilikuwa zikiendelea.

Pia mtuhumiwa mwingine alikuwa amekamatwa katika Kiwanja cha Ndege cha Abeid Aman Karume mjini Zanzibar, wakati akijaribu kuondoka nchini akielekea Kenya. Mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya maofisa wa uhamiaji kugundua kuwa hati yake ya kusafiria ilikuwa bandia yenye jina la Patrick Kinyanjui. Baada ya kupekuliwa mtuhumiwa huyo alikutwa akiwa na begi la nguo, kadi ya benki ya KCB, simu ya mkononi aina ya Iphone 12 Pro Max na fedha mchanganyiko; Shilingi za Tanzania 1,800,000 na Dola za Marekani 3,600.

Maofisa wa Usalama wa Taifa walikuwa wakiendelea kumhoji mtu huyo, wakati mipango ya kumrudisha jijini Dar es Salaam ikiendelea.

Hizi zilikuwa ni taarifa za kiintelijensia zilizokuwa zimewasilishwa kwenye Idara ya Usalama wa Taifa, taarifa ambazo Tunu Michael, mkuu wangu wa kazi, alizipata na kunidokeza wakati tukiwa tumeketi nyumbani kwake Oysterbay, kwa kikao cha kupashana taarifa muhimu za kazi.

Tunu alikuwa amenieleza hayo kutokana na furaha aliyokuwa nayo kufuatia taarifa nzuri niliyomkabidhi kuhusiana na upelelezi wangu wa tukio la kigaidi katika jengo la Alpha Mall. Taarifa yangu ilikuwa imeandaliwa vizuri na ilikusanya kila aina ya ushahidi.

Yapo ambayo Tunu aliyafahamu kama ile video iliyomwonesha yule mtu akifika na pikipiki ya magurudumu matatu pale kwenye jengo la Alpha Mall, lakini kilichomkosha zaidi ni ule uchunguzi nilioufanya baada ya kupokea taarifa za Msemaji wa Jeshi la Polisi, SACP Selemani Bwera kuwa bomu lililolipuka lilikuwa na mchanganyiko wa TNT + LPG + Amonium Nitrate.

Ilikuwa taarifa ya kina iliyokuwa na viambatanisho vyote muhimu, ambavyo vingine nilivipata kwa msaada wa mashirika ya kijasusi ya Mossad na CIA na kuongezea mtazamo wangu kisha nikabaini kuwa gaidi aliyelipua bomu kwenye jengo la Alpha Mall aliitwa Bosco Gahizi.

Tunu aliisoma taarifa ile kwa umakini sana na baada ya kumaliza alinitazama kwa muda kama aliyepigwa na butwaa, na bila kujitambua alinikumbatia halafu akanipiga mabusu mfululizo. “Excellent!” alimaka kwa furaha huku akinitazama usoni kama asiyeamini.

Mara, kama aliyegutuka kuwa hakupaswa kufanya vile aliniachia na kuniomba msamaha kabla hajashusha pumzi za ndani kwa ndani. Tuache masikhara, Tunu alikuwa mwanamke mrembo sana na alinisisimua pindi aliponikumbatia, na ukizingatia kuwa nilikuwa nimemzidi umri, lakini nilishindwa nifanye nini kwa kuwa nilimheshimu kama bosi wangu.

“Taarifa yako ni nzuri sana, ina details za kutosha na inatia moyo mno. In fact, hakuna ofisa yeyote au kundi lolote ambalo limefikia hatua hii hadi sasa…” Tunu alisema akionesha furaha yake. “Kesho nina kikao na DGIS, nitampatia taarifa hii, na pia nitamshauri tumjulishe Rais. Kwa vile ni wewe uliyeiandaa basi upo uwezekano mkubwa mkurugenzi mkuu wa Idara akataka kukuuliza maswali au kupata maelezo ya ziada, hivyo uwe standby.”

“Sawa, Mkuu,” nilisema kwa unyenyekevu.

Kisha nilimwonesha video ya hotuba ya mwisho ya Waziri Ummi Mrutu niliyoipakua kutoka kwenye mtandao wa Youtube na kumweleza shaka yangu kuwa huenda ndiyo iliyosababisha kifo chake. Tunu aliichukua pia hotuba hiyo na kuiunganisha na taarifa yangu, kama kielelezo kingine ambacho kingesaidia kuwapata waliohusika na tukio lile la kigaidi.

Baada ya hapo ndipo Tunu alipoamua kunieleza kuhusu taarifa ile ya kiintelijensia. Halafu aliniambia kuwa pia kulikuwepo na taarifa nyingine ambayo yeye binafsi aliitilia shaka.

Taarifa iliyoeleza kuwa, saa chache zilizokuwa zimepita mtu mmoja aliyejitambulisha kuwa msemaji wa kikundi kiitwacho Tanzanian Islamic Resistance Movement, kilichokuwa kikiendesha harakati zake Kaskazini mwa nchi ya Msumbiji katika Jimbo la Cabo Delgado, alipiga simu katika ofisi za kituo cha runinga ya taifa (Televisão dê Moçambique) jijini Maputo, Msumbiji, akidai kuwa kundi lake ndilo lililohusika na mashambulizi hayo.

Mtu huyo aliyekuwa akizungumza kwa ufasaha lugha za Kireno, Kiswahili na Kiarabu, hakueleza sababu za shambulio hilo, hakutaja uraia wake na wala hakueleza kwa kina shabaha ya kundi alilokuwa analiwakilisha.

“Kwa nini unadhani kuwa taarifa hii ina walakini?” nilimuuliza Tunu kwa shauku huku nikimtazama kwa umakini usoni.

“Ni hisia zangu za kijasusi zinazoniongoza kuitilia shaka taarifa hii. Naona kabisa kuwa imetengenezwa makusudi ili kutupoteza lengo kwa kutufanya tuelekeze macho yetu nje ya nchi badala ya kumtafuta adui ndani,” Tunu aliniambia. Kisha akaongeza, “Kutokana na kile tulichojadili asubuhi, aliyekusudiwa kuuawa hapo ni Waziri Ummi, na wa kumuua ni maadui zake ambao hawawezi kuwa kundi hili! sioni kabisa link yoyote kati yake na hili kundi.”

Nilijikuta nikikubaliana moja kwa moja na hoja ya Tunu.

Kisha Tunu alinionesha taarifa kutoka vyanzo vya kiintelijensia iliyoonesha uwepo wa vikundi vidogo vidogo vya kigaidi vilivyokuwa vinafanya kazi chini ya kundi la Islamic State (IS) huko Kaskazini mwa nchi ya Msumbiji katika Jimbo la Cabo Delgado. Japokuwa vikundi hivyo vilitofautiana kiitikadi na mikakati lakini vyote vilikuwa vinaunga mkono vita dhidi ya ukombozi wa Dola la Kiislamu.

Kundi la Tanzanian Islamic Resistance Movement lilikuwa limeanzishwa miezi michache tu iliyokuwa imepita kwa lengo la kuja kuiondoa madarakani Serikali ya Tanzania. Baada ya miaka mingi ya mikakati isiyofanikiwa ya kundi la Islamic State, kundi hili liligawanyika katika makundi madogo madogo yanayojitegemea ikiwemo kundi hili la Tanzanian Islamic Resistance Movement.

Ilisemekana kuwa baadhi ya wanachama wa kundi hili walishiriki kwenye mauaji ya raia katika maeneo ya Mkuranga, Kibiti na Rufiji mkoani Pwani nchini Tanzania. Jambo ambalo lilifanya kundi hili kuwa kivutio kwa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), ni fatwa iliyotolewa na kiongozi wake, kuhamasisha mapambano dhidi ya raia wa Tanzania walioishi Msumbiji.

Jambo kuu lililoisukuma TISS kuanza kulifuatilia kwa ukaribu kundi hili ni kitendo cha wanachama wa kundi hili kuwanyanyasa Watanzania waliokuwa wakiishi katika Wilaya za Mueda na Palma nchini Msumbiji, kuwapora mali zao na kuwachania hati zao za kusafiria kwa makusudi ili kuhalalisha kuwa walikuwa wameingia nchi Msumbiji kinyume cha sheria.

Taarifa hizo za kiintelijensia zilieleza kuwa ni kweli walikuwepo Watanzania waliokuwa wakiishi kinyume na sheria za Msumbiji kwa maana ya kuwa wahamiaji haramu lakini hilo halikuhalalisha vitendo walivyokuwa wakifanyiwa kwani vilikiuka sheria na haki za binadamu za umoja wa mataifa. Na hivyo ilionesha dhahiri kuwa Serikali ya Msumbiji ilikuwa imeshindwa kuwalinda raia wa Tanzania.

Endelea...
 
Back
Top Bottom