Simulizi: Harakati za Jason Sizya

Simulizi: Harakati za Jason Sizya

taharuki..jpg

313

Sajenti Mambo!




Saa 10:10 alasiri…

MIMI na Pamela tulishuka taratibu kwenye ngazi za jengo lile la Alpha Commercial Bank tukitokea juu kwenye ofisi ya meneja wa benki ile zikiwa zimebakia dakika ishirini kabla ya shughuli katika benki ile kufungwa mnamo saa kumi na nusu. Wakati tukishuka tulipishana na makachero watatu wa Polisi kutoka Kituo Kikuu cha Polisi (Central Police) kilichokuwa na dhamana ya kusimamia usalama wa eneo lile.

Miongoni mwa makachero wale wa polisi nilimtambua Inspekta Thomas Dilunga aliyekuwa ameambatana na askari wengine wawili. Walikuwa wamefika pale benki mara baada ya kupewa taarifa za kifo cha meneja wa benki ile, Andrew Adonis, aliyejiua mwenyewe ili kujiweka huru kama ambavyo mwenyewe alidai.

Inspekta Tom, kama alivyofahamika kwa wengi, alikuwa akitembea haraka na kwa kujiamini, na wakati tukipishana alikuwa amekunja sura yake, macho yakiwa mbele pasipo kunitazama kana kwamba hakuwa akinifahamu, na mara tu tulipopishana nikageuka haraka na kumtazama. Ni wakati huo huo na yeye alikuwa na lengo kama langu la kugeuka na kunitazama, hivyo macho yetu yakakutana. Hakuna aliyeongea neno kati yetu ila macho yetu yaliongea mengi.

Kisha nikamwona Inspekta Tom akitingisha kichwa chake na kuachia tabasamu huku akiniangalia kwa macho yaliyosomeka, “wewe mwandishi kiboko aisee, umewahi hata huku!” Inspekta Tom alinifahamu kama mwandishi wa habari za uchunguzi niliyekuwa mwepesi kunusa matukio ya hatari popote yalipokuwa.

Ni Luteni Lister aliyekuwa ametoa taarifa kwa mkurugenzi mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa na kituo cha polisi mara baada tu ya kifo cha meneja huyo kutokea, na baada ya dakika kama ishirini na tano hivi ndipo polisi wale walifika hapo benki, kwa maelekezo ya Luteni Lister. Kisha Luteni Lister alitushauri mimi na Pamela tumwachie jukumu la kutoa maelezo kwa wale polisi na twende tukamsubiri kwenye gari letu.

Wakati tukishuka Pamela alikuwa amebeba mkoba ambao ndani yake kulikuwa na ile bahasha yenye vielelezo vyote muhimu kama barua ya maelekezo kwa meneja, hundi ya benki yenye jina la SSP Kambi, bank statement, cash flow na orodha ya majina ya watu wote waliopaswa kupokea mgawo wa fedha.

Wakati tukimaliza kushuka zile ngazi na kufika eneo la chini la benki, tulikuta wafanyakazi wa benki ile na wateja wachache wakiwa wametahayari sana, walikuwa wamejikusanya katika vikundi vidogo vidogo na nyuso zao zilionesha wazi jinsi walivyokuwa wametaharuki kusikia meneja wa benki amejiua kwa risasi wakati akihojiwa.

Ilinishangaza sana baada kugundua kuwa taarifa za kifo cha meneja huyo wa benki zilikuwa zimeshasambaa haraka kwenye mitandao ya kijamii kama ubuyu.

Wakati tukiwa tumefika pale eneo la chini huku macho yangu yakitembea haraka kuzitazama sura za watu waliokuwepo eneo lile, nilivutiwa kumtazama msichana mmoja mweupe mwenye umbo la kuvutia miongoni mwa watu waliokuwepo eneo lile. Sura yake ilikuwa ndefu na macho yake alikuwa ameyafunika kwa vioo vyeusi vya miwani yake. Pua yake ilikuwa ndefu na mdomo wake ulikuwa na kingo pana.

Sikupata nafasi ya kumtathmini vizuri msichana yule usoni ingawa niliweza kuukadiria umri wake kuwa ulikuwa ni kati ya miaka ishirini na tano hadi ishirini na nane. Alikuwa amevaa fulana nyepesi nyeupe iliyoyahifadhi matiti yake yenye ukubwa wa wastani na juu yake alivaa shati zito jeusi la kitambaa cha dengrizi.

Kiuno chake kilikuwa chembamba kiasi kilichoizuia suruali yake ya rangi nyeusi ya kitambaa cha dengrizi na miguuni alikuwa amevaa viatu virefu vya ngozi aina ya Travolta. Kichwani alikuwa amevaa kofia nyeusi aina ya mzula iliyozifunika nywele zake ndefu na mgongoni alikuwa amebeba begi dogo jeusi la ngozi.

Nilihisi kuuona mshtuko kwenye uso wa yule msichana baada ya kukutanisha macho yetu japokuwa alijitahidi kuumeza mshtuko wake, na kisha nikamwona akianza kupiga hatua za haraka kuelekea kwenye mlango wa kutokea. Ingawa alionesha kujiamini sana wakati akitembea huku mjongeo wake ukitengeneza starehe ya kipekee iliyotokana na mtikisiko wa umbo lake la kike lakini lililokuwa kakamavu, nilitambua kuwa alikuwa na hofu.

Wakati akifika pale kwenye mlango wa kutokea na kabla hajatoka kabisa aligeuka na kunitazama na hapo macho yetu yakakutana tena. Nikamtambua.

Alikuwa ni yule msichana niliyemwona kwa mara ya kwanza usiku wa siku ya tukio la mlipuko wa bomu, wakati nikimshusha Winnie eneo la Mwananyamala A. Msichana huyu alikuwa pamoja na yule ofisa usalama wa taifa, Deogratius Rutashobya, kisha wakaingia ndani ya gari la kifahari aina ya Range Rover Velar la rangi nyeupe lenye vioo vyeusi na kuondoka.

Mara ya pili nikamwona kwenye msiba Mikocheni B, nyumbani kwa Waziri Ummi Mrutu, kabla hajaondoka akiwa na SSP Yusuf Kambi kwa gari la kifahari aina ya BMW X6 la rangi nyeusi lililokuwa na vioo vyeusi, na nikafanikiwa kuwafuata hadi Mbezi Beach, kwenye nyumba ya SSP Kambi.

Safari hii tulipotazamana nikaona katika uso wa msichana yule kitu kilichonishtua sana. Kitu hicho kilikuwa ni chuki mbaya iliyoshindwa kujificha.

Hisia zilikuwa jambo muhimu sana katika kazi yangu ya ushushushu na kamwe sikutaka kuzipuuza. Macho ya yule msichana yaliyojificha nyuma ya miwani myeusi yalipokutana na macho yangu yule dada aligeuka na kutoka haraka. Mara moja moyo wangu ukapoteza utulivu, damu ikanichemka mwilini, nywele zikanicheza na jasho jepesi likaanza kunitoka.

Hey!” nilijitahidi kumwita yule msichana kabla hajapotea huku nikimfuata haraka.

Pamela ambaye muda huo alikuwa akiongea na yule msichana wa dawati la huduma kwa wateja aliushtukia mchezo, hivyo aliachana na yule msichana na kuanza kutoka haraka kumfukuzia yule msichana.

Hallo!” nilimwita tena yule msichana lakini ilikuwa kazi bure kwani si tu kwamba hakuniitikia bali pia hakugeuka wala kusimama, na badala yake alizidisha mwendo na kupenya katikati ya watu akaelekea kwenye viunga vya maegesho ya magari.

Wakati namfuata kule kwenye maegesho ya magari nikasita kidogo baada ya kusikia muungurumo wa injini ya gari likiyaacha maegesho yale ya magari, nikashtuka baada ya kugundua kuwa nilikuwa nimechelewa. Hata hivyo sikuwa na uhakika kama ni yule msichana aliyekuwa anaondoka au mtu mwingine. Pamela naye alisita na kusimama huku macho yake yakiwa makini kutazama kule ambako muungurumo wa gari ulisikika.

Mara tukaliona gari moja la kifahari la rangi nyeusi aina ya Nissan V8 lenye vioo vyeusi visivyoonesha waliomo ndani likiyaacha maegesho yale na kuingia kwenye ile barabara ya mtaa wa India iliyokuwa ikikatisha mbele ya lile jengo la Alpha Commercial Bank na kushika uelekeo wa upande wa kushoto kama lililokuwa likielekea Posta.

Endelea...
 
taharuki..jpg

314

Macho yangu yalikuwa makini sana kulitazama lile gari aina ya Nissan V8 wakati likinipita huku nikijaribu kutafakari iwapo ni yule msichana aalikuwa anaondoka au la, huku nikiwaza hatua za kufanya, na hapo nikakiona kioo cha upande wa kushoto cha gari lile kikishushwa kidogo. Nikawa makini sana, nikamwona yule msichana akiniangalia huku akiachia tabasamu la dharau.

Lilikuwa tukio la kushtukiza ambalo sikuwa nimelitarajia kwani yule msichana alikuwa anaondoka eneo lile na kuelekea kusikojulikana. Moyo wangu ukapiga kite kwa nguvu baada ya kuhisi kuwa nilikuwa nimezidiwa ujanja na yule dada, jambo ambalo liliusononesha sana moyo wangu.

Hata hivyo sikutaka kukata tamaa, hivyo nikaanza kutimua mbio nikilifukuza lile gari huku mkono wangu nikiupeleka kiunoni ilipokuwa bastola yangu, lakini sikufanikiwa kwani ilionekana wazi kuwa kila kitu kilikuwa kimepangwa. Lile gari aina ya Nissan V8 lilikunja kuingia Mtaa wa Zanaki kwa mwendo wa kasi wakati mimi nikiwa umbali usiopungua mita hamsini kutoka lilipokuwa gari hilo.

Niliendelea kutimua mbio nikilifukuza lile gari lakini nilijikuta nikifanya kazi bure kwani gari lile lilikuwa katika mwendo wa kasi ya ajabu. Nilipofika kwenye ile kona ya kuingia Mtaa wa Zanaki nilisimama nikilitazama gari lile namna lilivyokuwa likitokomea mbele yangu huku donge la hasira likiwa limenikaba kooni. Kwani kwa maana nyingine ni kama niliyekuwa nimepoteza pointi zote muhimu za ushindi katika pambano langu.

Nilikata tamaa kabisa na kuanza kutembea kivivu vivu nikirudi kule kwenye eneo la maegesho ya magari katika jengo la Alpha Commercial Bank huku mawazo mengi yakipita kichwani mwangu. Pamela alikuwa amesimama katikati ya barabara akinitazama kwa namna ya kukata tamaa, mikono yake ikiwa kiunoni.

Wakati nikirudi huku kijasho chepesi kikiwa kinanitoka kwenye sehemu mbalimbali za mwili wangu na mapigo ya moyo wangu yakienda mbio sana kila nilipokuwa nikitafakari kitu ambacho kingefuatia baada ya pale, mara nikamwona mwanamume mmoja miongoni mwa watu waliojikusanya eneo lile wakishangaa, alikuwa akinikazia macho katika namna ya kuvuta umakini wangu ili nimwone.

Nilimtazama yule mtu kwa umakini, alikuwa amesimama kwenye kona ya jengo lile la Alpha Commercial Bank, jirani kabisa na eneo la maegesho ya magari, akiwa katika mavazi ya kiraia miongoni mwa raia wengine waliokusanyika eneo lile wakishangaa. Mara moja nikamtambua. Alikuwa kachero wa polisi, Sajenti Albert Mambo, kutoka Kituo cha Polisi cha Oysterbay.

Nilimfahamu Sajenti Mambo kwa kuwa mara kwa mara tulikutana kwenye majukumu ya kikazi wakati nikiwa katika harakati zangu za uandishi wa habari za uchunguzi, nikashtuka sana kumwona pale kwani yeye alikuwa mmoja wa watu ambao majina yao yalikuwemo kwenye orodha ya watu waliostahili kupata mgawo wa fedha toka kwenye benki ile.

Tulipotazamana nikaona akiachia tabasamu. Hata hivyo nilipomtazama vizuri usoni haraka nikagundua kuwa kulikuwa na kitu hatari kilichokuwa kimejificha nyuma ya tabasamu lake. Tabasamu lake lilikuwa limeficha kitu mfano wa huzuni kubwa machoni mwake ingawa alikuwa akijitahidi kuficha hisia zake zisitambulike kwa watu wengine. Moyo wangu ukapiga mshindo kwa nguvu.

Hata hivyo nilijizuia kufanya chochote kwa kuchelea kuyavuta macho ya watu ambao hawakupaswa kabisa kujua kazi yangu halisi ya ushushushu. Walitakiwa waendelee kutambua kuwa nilikuwa mwandishi wa habari za uchunguzi. Pia sikupenda kugeuka kivutio kwa kutazamwa tazamwa na watu, hivyo nikaongoza kuelekea kwenye gari letu.

Moyoni nilihisi kuwa kulikuwa na hila fulani iliyokuwa ikitaka kuchezwa eneo lile lakini nikajifanya sijagundua lolote kwenye uso wa Sajenti Mambo na kuzidi kupiga hatua nikiliendea gari letu aina ya Nissan Patrol la rangi ya jeshi lenye vioo vya giza visivyoruhusu mtu kuona waliomo ndani, mali ya Idara ya Usalama wa Taifa lililokuwa limesajiliwa kwa namba za binafsi.

Pamela alikuwa ananifuata taratibu kwa nyuma huku macho yake yakifanya kazi kubwa na makini ya kuzikagua nyuso za watu waliokuwepo eneo lile. Wakati nikilifikia gari letu, ambalo lilikuwa limejitenga kidogo na magari mengine kwenye yale maegesho ya magari, nikaingiza ufunguo kwenye kitasa cha mlango na kuufungua mlango wa gari ili niingie lakini hisia zangu zikanitahadharisha kuwa kabla ya kuingia ndani ya gari nilipaswa kugeuka nimtazame kwanza Sajenti Mambo.

Hivyo kabla sijaingia nikayapeleka macho yangu haraka kumtazama Sajenti Mambo, alikuwa bado kasimama pale pale na muda wote alikuwa akinitazama, na kwa kufanya vile macho yangu yakakutana na macho yake, akakunja sura yake na kutingisha kichwa chake katika namna ya kunizuia nisiingie ndani ya lile gari huku akinikazia macho. Nikagundua kuwa alikuwa akifanya vile kwa tahadhari akiwa hataki mtu mwingine aone kama alinizuia. Kisha nikakiona kilichokuwa kimefichika ndani ya macho yake. Jambo la hatari!

Mlango wa hisia ya sita katika ubongo wangu ukafunguka, ilikuwa ni hisia iliyonifahamisha kuwa nilipaswa kuchukua hatua za haraka kwani kulikuwa na hatari kwenye lile gari na jambo baya lingeweza kutokea wakati wowote. Nilikumbuka wakati wa mafunzo ya ushushushu nchini Misri maendeleo ya hisia ya sita yalikuwa yanapewa uzito mkubwa kwa wanafunzi wa ujasusi, na kadri yalivyosisitizwa ndivyo ambavyo yalinijenga kutambua umuhimu wa nyenzo hiyo muhimu.

Sasa akili yangu ilifanya kazi haraka. Hivyo kufumba na kufumbua, kwa nguvu zangu zote nilirudi nyuma haraka huku nikimpitia Pamela aliyekuwa akija taratibu, nikampiga kumbo kama mwanamieleka huku nikijirusha na kudondoka chini, mbali na lile gari. Pamela alijirusha akaanguka chini mbali na mimi huku akinitazama kwa mshangao. Muda ule ule sauti ya kishindo kikubwa cha mlipuko ikazizima eneo lile.

Moto mkubwa uliruka hewani na nilipotazama upande ule nikaliona lile gari letu aina ya Nissan Patrol likinyanyuliwa juu zima zima kutoka pale lilipokuwa limeegeshwa na kurushwa hewani kama kiberiti huku likisambaratika vipande vipande. Vipande vya vioo vilirushwa huku na huko na kurudi ardhini kama matone ya mvua, vikijeruhi watu waliokuwa wamezagaa eneo lile kushangaa.

Vipande vile vilitawanyika angani na kwa kuwa madhara yake nilikuwa nikiyafahamu vizuri hivyo nikawahi kujiviringisha na kupotelea chini ya gari moja aina ya Town Hiace lililokuwa jirani na pale nilipoangukia. Na bila kupoteza muda niliinua mkono wangu wa kushoto kuitazama saa yangu ya mkononi niliyokuwa nimeivaa. Mishale ya saa hiyo ilinionesha kuwa ilikuwa imetimia saa kumi na dakika ishirini (juu ya alama) jioni.

Sikusahau kuwa, mojawapo ya mambo muhimu anayopaswa kufanya Ofisa Usalama wa Taifa anapokuwa kazini, ni kujua na kutunza muda sahihi wa kila tukio linalotokea. Kufanya hivyo husaidia sana katika uchunguzi utakaofanywa baadaye hususan katika kuunganisha nukta, kujumlisha moja na moja ili kupata mbili, kupunguza idadi ya watuhumiwa, na hata kutambua sababu na lengo lililofanya tukio husika kutokea au kufanywa katika muda huo.

Endelea...
 
taharuki..jpg

315

Kisha niligeuza shingo yangu kumtazama Pamela nikamwona akiwa amejificha kwenye gari lingine aina ya Toyota Prado TX lililokuwa limeegeshwa jirani na pale alipoangukia. Yote haya niliyashuhudia yakifanyika ndani ya sekunde tano tu. Nilichokisikia baada ya pale ni kelele za hofu zikihanikiza kutoka kwa umati wa watu waliokuwa eneo lile kushuhudia.

Kisha mabaki ya lile gari letu aina ya Nissan Patrol yalirudi chini na kujibwaga tena ardhini katikati ya barabara ile ya India na lile gari likalalia ubavu huku likiendelea kuteketea kwa moto. Nilijiinua haraka kutoka pale chini huku nikiangaza macho yangu kuangaza huku na kule, nilikuwa nikimtafuta Sajenti Mambo, ambaye hata hivyo alikuwa ameshayeyuka kama upepo mara baada ya tukio lile la bomu kutokea. Kwa hakika alikuwa ametuokoa kutokana na kifo kibaya sana cha bomu.

Kisha niligeuka kumtazama Pamela kule alikokuwa amejificha, naye sikumwona! Hata hivyo sikuwa na wasiwasi na Pamela, nilijua yupo sehemu salama. Nilijitahidi kumtafuta kwenye umati ule wa watu na mara nikamwona akiishia kwenye kona fulani katika mtaa ule.

Haraka sana nikatambua kuwa alikuwa akielekea kwenye ‘Kituo’ yaani mahali tulipokubaliana kukutana kama ikitokea dharura. Utaratibu huu ni wa kawaida kwa maofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa na husaidia sana kujipanga upya kama mkipotezana au yakitokea mashambulizi msiyoyatarajia na kutawanyika, kama ilivyotokea sasa.

Muda huo huo niliwaona baadhi ya watu waliokuwa na ujasiri wakilikimbilia lile gari letu lililokuwa likiteketea kwa moto pale barabarani na kulizunguka huku wengine wakija nilipokuwa nimesimama kwa nia ya kunisaidia. Nikaondoka nikitembea haraka haraka kumfuata Pamela upande ule nilioamini alielekea nikiupita mkusanyiko wa watu walioanza kunishangaa. Hata hivyo sikuwajali.

Ingawa umati wa watu ulianza kuwa mkubwa mno lakini sikuwa na shaka yoyote ya kutomwona Pamela kwani nilijua angekuwa ameshafika kwenye ‘Kituo’, Mtaa wa Kaluta, kwenye jengo la Hospitali ya Burhani. Wakati nikikaribia kwenye kituo, kwa mbali nikamwona Pamela akiwa ameshafika. Alikuwa amesimama huku akiwa katika tahadhari kubwa, hata hivyo uso wake ulionekana kutulia na kutokuwa na woga hata kidogo.

“Oh, Jason! Dah, tungekufa leo!” Pamela aliniambia kwa sauti ya chini mara tu nilipomfikia kisha akashusha pumzi za ndani kwa ndani. Tukakumbatiana kwa nguvu kana kwamba tulikuwa mapacha tuliokutana ghafla baada ya kupotezana kwa miaka mingi.

“Hawa watu ni hatari mno, Pamela. Ni zaidi ya vile tufikiriavyo! Yaani walipanga kutumaliza kwa bomu ili wapoteze kabisa ushahidi, hata hivyo tumshukuru Mungu bado tunapumua…” nilisema huku macho yangu yakiangaza huku na kule katika namna ya kulikagua eneo lile.

Muda huo huo nikamwona Luteni Lister akija haraka kuelekea pale tulipokuwa tumesimama huku macho yakiwa yamemtoka pima. Alikuwa anaongea na simu. Macho yetu yalipogongana tu nikanyanyua mkono wangu wa kushoto na kugusa upande wa kulia wa ncha ya kola ya shati nililokuwa nimeivaa kumwashiria kuwa mambo hayakuwa shwari. Bila kusita naye alinijibu kwa kugusa sikio lake la kushoto kuashiria kuwa hata yeye alifahamu hivyo. Kisha aliongeza mwendo ili aweze kutufikia haraka zaidi.

Wakati huo sauti za ving’ora vya magari ya Polisi na yale ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji zikaanza kusikika tokea upande fulani wakati magari hayo yakija katika mtaa ule wa India kwenye eneo la tukio kwa mwendo wa kasi, na muda mfupi baadaye nikayaona magari matatu yakipita katika Mtaa wa Zanaki na kukunja kuingia mtaa ule wa India kwa makeke; mawili yakiwa ya polisi na moja la zimamoto.

“Imekuaje jamani, maana nimesikia mshindo tu?” Luteni Lister alituuliza kwa sauti kavu kidogo mara tu alipotufikia.

Nikamsimulia kwa kifupi jinsi ilivyokuwa tangu nilipomshtukia yule msichana wakati tunatoka ndani ya ofisi ya meneja, na yeye akiwa miongoni mwa mashuhuda waliokuwepo pale benki na jinsi alivyotoroka na gari aina ya Nissan V8 jeusi lenye vioo vyeusi visivyoonesha waliomo ndani, kisha nilivyogonganisha macho yangu na ya Sajenti Mambo ambaye alionekana kufahamu jambo na kunizuia kwa macho nisiingie ndani ya gari letu, na sekunde chache baadaye mlipuko wa bomu ukatokea.

Luteni Lister alitweta kisha akashauri tuondoke haraka eneo lile na kutafuta usafiri wa kutufikisha makao makuu ya Idara ya Usalama wa Taifa eneo la Oysterbay, kwani alikwisha wasiliana na mkurugenzi mkuu, mzee Rajabu Kaunda, kuhusiana na kadhia ile. Tukaondoka haraka eneo lile huku tukipishana na wanausalama walioelekea eneo lile, tukatafuta teksi na kuikodi tukimtaka dereva atupeleke kwenye Kanisa Katoliki la St. Peter, Oysterbay.

Wote tulikuwa kimya kabisa kila mmoja wetu akitafakari kivyake, nikiwa nimeketi kiti cha nyuma kando ya Pamela, hisia juu ya Sajenti Mambo zikaanza kuziteka taratibu fikra zangu. Nikajiuliza tena kwa nini Sajenti Mambo aliamua kutuokoa kutoka katika ule mlipuko ya bomu la kutegwa kwenye gari letu. Kisha nikaukumbuka ule mlipuko wa bomu huku nikiulinganisha na thamani ya maisha yetu na hali ile ikanifanya nizidi kuhisi kuwa kulikuwa na mambo mengi makubwa na ya siri sana yaliyokuwa yamefichika katika mkasa huu.

Kwa mara ya kwanza nikaanza kuhisi kuwa kama genge hilo hatari lilikwisha fahamu kuwa nilikuwa na ushahidi dhidi yao wangeweza hata kuidhuru familia yangu na hivyo kulikuwa na hatari kuwa nilikuwa nimeitumbukiza familia yangu kwenye hatari baada ya kujitosa kwenye harakati za upelelezi juu ya mkasa huu hatari zaidi wenye siri nzito iliyofichika ndani yake. Siri ambayo gharama ya kuitunza ililingana na thamani ya uhai wa familia yangu.

Kitendo cha kuwaona wanausalama na makachero wa polisi, tena wengine wakiwa wa ngazi ya juu wakiwa wamejiingiza katika mtandao huu hatari si tu kwamba kitendo kile kilikuwa kimenishtua sana bali pia kilikuwa kikielekea kuninyima raha na usingizi kwani nilifahamu ugumu ulipo katika kupambana na mtandao huu.

Hivyo nikapanga kumpigia simu Rehema ili kumwambia aahirishe safari yake ya kuja jijini Dar es Salaam hadi suala hili lipite maana nilikuwa na uhakika tungewatia mbaroni watu waliohusika na milipuko ile ya kigaidi ndani ya muda mfupi, na pia Rehema alipaswa kuchukua tahadhari huko huko alikokuwa.

Nilipaswa kuchukua hatua ya kumpigia simu haraka iwezekanavyo mara tu nikishafika makao makuu ya Idara ya Usalama wa taifa kwani Rehema alikuwa amewasiliana nami asubuhi ya siku ile na kuniambia kuwa alipanga kurejea jijini Dar es Salaam siku ya Ijumaa, na siku hii ilikuwa ni Jumanne. Wakati nikiwaza hayo mara simu yangu ikaanza kuita na kunishtua. Niliitazama ile simu kwa umakini na kuliona jina la Rehema!

Dah! Moyo wangu ukapiga kite kwa nguvu na hisia za hofu, kitu ambacho kwa kawaida kilitokea kwa sababu maalumu, zikaanza kuninyemelea pasipo sababu ya msingi. Niliikodolea macho ile simu kana kwamba nilikuwa nimeshika guruneti la kutupa kwa mkono, akili yangu taratibu ikaanza kuzama kwenye kuwaza kuwa huenda kulikuwa na tatizo huko Tabora.

Endelea...
 
taharuki..jpg

316

Kilichonitia hofu ni kwamba sikuwa tayari kuona familia yangu ikiingia kwenye matatizo ya aina yoyote. Niliendelea kuitazama ile simu kwa wasiwasi na kuwafanya akina Luteni Lister na Pamela wageuke kunitazama kwa mshangao, kwa macho yaliyouliza ‘kulikoni!’

Hata hivyo, sikutaka kuiacha ile simu iendelee kuita zaidi kwani ilikuwa mbioni kukatika baada ya kuita kwa muda mrefu. Haraka nikaipokea na kukiweka sikioni huku nikiipa akili yangu utulivu wa hali ya juu.

“Hallo!” nilisema kwa sauti tulivu mara tu nilipoiweka ile simu sikioni huku nikishusha pumzi za ndani kwa ndani.

“Hallo, habari za saa hizi, Baba Edwin?” badala ya sauti ya Rehema nilijikuta nikiisikia sauti ya Zainabu, alikuwa anaongea kwa furaha.

Nilishtuka kidogo, nikaitoa simu toka kwenye sikio langu na kuitazama ile namba kwa umakini. Ilikuwa ni namba ya Rehema lakini sauti ilikuwa ya Zainabu! Nikashangaa sana! Hata hivyo kitendo cha kuisikia sauti ya Zainabu kikanifanya nimkumbuke mwanangu, Edwin Sizya, mtoto niliyempata kwa Zainabu, aliyekuwa amepewa jina la Edwin, la mjomba wangu Mchungaji Edwin Ngelela.

“Hallo…! Hallo!” Zainabu aliita kwa sauti iliyobeba wasiwasi baada ya kuona nipo kimya.

“Ndiyo, Zai, nakusikia!” nilijibu kwa sauti tulivu. “Nimeshangaa kidogo maana namba ni ya Rehema lakini sauti ni ya Zainabu!” niliongea huku nikiachia kicheko hafifu. Nilipenda kuwaita wanawake wale kwa majina yao badala ya kutumia majina ya watoto wao, yaani Mama Junior na Mama Edwin.

Zainabu naye akacheka kidogo. “Nilijua tu lazima ushangae. Tumefanya makusudi,” Alisema huku akiendelea kucheka. Kisha akaongeza, “Vipi unaendeleaje huko?”

“Huku kwema kabisa. Sijui ninyi huko?” nilimjibu huku nikijiuliza wanawake hao walikutana wapi! Je, ni Rehema aliyekwenda Kilosa au Zainabu ndiye alikwenda Tabora?

“Huku tunamshukuru Mungu, bado anatulinda…” Zainabu alisema na kuongeza, “Nimeona kimya nikataka kukujulia hali.”

“Dah, nisamehe tu maana huku mambo ni mengi mno na muda hautoshi. Kwani Rehema hajakwambia?” nilimuuliza Zainabu kwa sauti tulivu.

“Kaniambia. Halafu pole sana na mikasa ya mabomu maana nasikia bomu lililipuka jirani kabisa na ofisi yako,” Zainabu alisema.

“Ndo hivyo, hadi sasa hali bado ni ya taharuki maana waliofanya ugaidi huo bado hawajapatikana…” nilijibu, kisha nikashindwa kuvumilia na kuuliza, “Kwani mpo Tabora au Kilosa?”

Zainabu hakunijibu na badala yake aliangua kicheko. Alipenda sana kucheka. Kisha aliniambia. “Hebu ongea na Mama Junior, huyu hapa!”

“Hello!” niliisikia sauti ya Rehema toka upande wa pili wa simu.

“Nambie, mamaa,” nilisema huku nikuma midomo yangu. “Mko wapi?”

“Tupo Kilosa, tumeingia jioni hii,” Rehema alisema. Nikashangaa sana maana tulipoongea asubuhi hakuwa ameniambia kama angekwenda Kilosa. Na ijapokuwa Rehema na Zainabu hawakuwahi kuwa na ugomvi lakini pia hawakuwa na ukaribu wa kiasi cha kutembeleana, jambo lililonishangaza! Nikajiuliza Rehema alikuwa amefuata nini kilosa? Kwa nini hakuniambia kama angekwenda Kilosa? Na urafiki wao ulianza lini kiasi cha kutembeleana?

“Mbona hukuniambia kama mngekwenda Kilosa?” nilimuuliza Rehema kwa mshangao.

Rehema akacheka. “Ndo nakwambia sasa kuwa tupo Kilosa. Tutakuwepo hapa kwa siku mbili halafu sote tutakuja Dar es Salaam Ijumaa maana Zainabu anataka kuongea na wewe.”

Maneno ya Rehema yakanishtua kidogo. Nikamuuliza kwa wasiwasi kidogo. “Kuongea na mimi kuhusu nini?”

“Unajua…” Rehema alianza kusema. “Kuna kitu Zainabu anatamani kukwambia lakini anashindwa.”

Sasa nilishtuka zaidi na akili yangu ikaenda mbali zaidi. Nilianza kujiuliza iwapo Zainabu alikuwa mjamzito maana nilikumbuka ile wiki niliporudi toka Mombasa baada ya ule mkasa uliopewa jina la ‘Ufukweni Mombasa’, nilikwenda Kilosa nikipanga kukaa siku moja tu kisha nielekee Tabora kwa wazee, lakini nikajikuta nikikaa pale kwa siku tano, Zainabu akiwa ndo kampani yangu.

Basi katika siku zile tano mimi na Zainabu tulikuwa na muda mzuri sana wa kufurahia maisha na kupeana malavidavi ya nguvu, na ukweli ni kwamba sikuwahi kujutia kitendo hicho kwa kuwa Zainabu alikuwa ni zaidi ya vile nilivyomdhania. She was so sweet! Ule utamu ambao unasema mbona leo tamu zaidi ya jana? Na kesho unasema vile vile, dah!

Nikakumbuka jinsi mechi tuliyoicheza siku ya kwanza tu nilipofika Kilosa, hakika ilikuwa mechi kali sana, mechi ya kuombana msamaha kwa yote yaliyotokea, mechi ya kupeana adhabu kwa sababu ya kufarakana, mechi ya kuambiana jinsi tulivyokuwa tumepoteana na jinsi kila mmoja wetu alivyokuwa na hamu na mwenziwe, mechi ya kuambiana namna tulivyotamaniana. Kwa kweli ilikuwa ni mechi iliyojaa mihemuko, sex that was full of emotions!

Siku hiyo Zainabu alishindwa kujizuia, alilia mno! Mpaka sasa nikiwa ndani ya teksi nikielekea makao makuu ya TISS nilikuwa bado nashindwa kuelewa kilichomliza namna ile kilikuwa nini! Labda ni ile hisia kuwa asingeweza kuwa na uhuru na mimi kwa kuwa nilikuwa mume wa mwanamke mwingine! Lakini yote kwa yote, muda wote alinikumbatia kwa nguvu kama aliyekuwa anaogopa kuniachia kwa kuhofia ningemkimbia.

Siku hiyo niliishuhudia michirizi ya machozi kwenye mashavu yake na mara zote Zainabu alikuwa haniangalii machoni japo kwa kawaida alikuwa msichana jasiri ambaye haoni haya kukuangalia moja kwa moja machoni, siku hii hakuwa na huo ujasiri!

Siku naondoka kwenda Tabora kwa wazee tuliamua twende wote. Ilikuwa safari ya kukumbukwa. Tuliingia Tabora usiku sana baada ya kujikuta tukibanjuka safarini. Tatizo la Zainabu lilikuwa moja, ukipitisha tu mkono katikati ya mapaja yake anakwambia analoana, duh!

Ilikuwa inanibidi nitafute sehemu kisha niegeshe gari letu pembeni, haha! Kuna wakati nilimalizia mle mle ndani ya gari na kuna mahali kulikuwa na vichaka fulani, nikampeleka nyuma ya kichaka kimoja kisha nikamwinamisha. Dah! Hadi tunafika Tabora tulikuwa tumechoka mno!

“Umenisikia?” sauti ya Rehema ilinizindua toka kwenye mawazo yangu ya kuwaza ngono. Nikatabasamu na kushusha pumzi.

“Kitu gani?” nilimuuliza Rehema huku moyo wangu ukidunda kwa nguvu.

“Zainabu ameniambia kuna mtu anataka amuoe hata kesho akikubali, ila yeye anasita kwa kuogopa kuwa Edwin bado mdogo sana. Ila mi najua hataki kuolewa kwa kuwa bado anakupenda sana,” Rehema alisema. Hata sikumjibu.

Nikatafuta namna ya kuyakwepa mazungumzo hayo. Kwa kumwambia kuwa muda huo nilikuwa na wenzangu ndani ya gari tukielekea sehemu na kwamba tungeongea baadaye. Pia nilimwomba aahirishe kwanza safari ya kuja Dar es Salaam kwa kuwa kiota kilikuwa kinateketea kwa moto mkali ambao ungeunguza makinda. Bahati nzuri Rehema alikuwa mtu wa kitengo, akanielewa.

* * *


Tukutane tena wakati mwingine hapa hapa kuzifuatilia Harakati za Jason Sizya...
 
Rehema kirangaaaaa kichokupeleka kilosa nini?! Unajiamini nini wewe, ukiwekewa sumu ufe je mume mwenyewe sasaa mchafu muhuni fox simpendi
 
NAKUBALI SANA BAHARIA JASON UJAWAHI NIANGUSHA KWENYE MASWALA YA KUCHAKATA MBUSUSU AKA KIPOCHI MONYOYA
 
Lete mambo tunakufutilia kwa ukaribu sana hongera mnoooo hadithi tamu sana.Twende kazi sasa angusha epsode nyingine
 
Back
Top Bottom