316
Kilichonitia hofu ni kwamba sikuwa tayari kuona familia yangu ikiingia kwenye matatizo ya aina yoyote. Niliendelea kuitazama ile simu kwa wasiwasi na kuwafanya akina Luteni Lister na Pamela wageuke kunitazama kwa mshangao, kwa macho yaliyouliza ‘kulikoni!’
Hata hivyo, sikutaka kuiacha ile simu iendelee kuita zaidi kwani ilikuwa mbioni kukatika baada ya kuita kwa muda mrefu. Haraka nikaipokea na kukiweka sikioni huku nikiipa akili yangu utulivu wa hali ya juu.
“Hallo!” nilisema kwa sauti tulivu mara tu nilipoiweka ile simu sikioni huku nikishusha pumzi za ndani kwa ndani.
“Hallo, habari za saa hizi, Baba Edwin?” badala ya sauti ya Rehema nilijikuta nikiisikia sauti ya Zainabu, alikuwa anaongea kwa furaha.
Nilishtuka kidogo, nikaitoa simu toka kwenye sikio langu na kuitazama ile namba kwa umakini. Ilikuwa ni namba ya Rehema lakini sauti ilikuwa ya Zainabu! Nikashangaa sana! Hata hivyo kitendo cha kuisikia sauti ya Zainabu kikanifanya nimkumbuke mwanangu, Edwin Sizya, mtoto niliyempata kwa Zainabu, aliyekuwa amepewa jina la Edwin, la mjomba wangu Mchungaji Edwin Ngelela.
“Hallo…! Hallo!” Zainabu aliita kwa sauti iliyobeba wasiwasi baada ya kuona nipo kimya.
“Ndiyo, Zai, nakusikia!” nilijibu kwa sauti tulivu. “Nimeshangaa kidogo maana namba ni ya Rehema lakini sauti ni ya Zainabu!” niliongea huku nikiachia kicheko hafifu. Nilipenda kuwaita wanawake wale kwa majina yao badala ya kutumia majina ya watoto wao, yaani Mama Junior na Mama Edwin.
Zainabu naye akacheka kidogo. “Nilijua tu lazima ushangae. Tumefanya makusudi,” Alisema huku akiendelea kucheka. Kisha akaongeza, “Vipi unaendeleaje huko?”
“Huku kwema kabisa. Sijui ninyi huko?” nilimjibu huku nikijiuliza wanawake hao walikutana wapi! Je, ni Rehema aliyekwenda Kilosa au Zainabu ndiye alikwenda Tabora?
“Huku tunamshukuru Mungu, bado anatulinda…” Zainabu alisema na kuongeza, “Nimeona kimya nikataka kukujulia hali.”
“Dah, nisamehe tu maana huku mambo ni mengi mno na muda hautoshi. Kwani Rehema hajakwambia?” nilimuuliza Zainabu kwa sauti tulivu.
“Kaniambia. Halafu pole sana na mikasa ya mabomu maana nasikia bomu lililipuka jirani kabisa na ofisi yako,” Zainabu alisema.
“Ndo hivyo, hadi sasa hali bado ni ya taharuki maana waliofanya ugaidi huo bado hawajapatikana…” nilijibu, kisha nikashindwa kuvumilia na kuuliza, “Kwani mpo Tabora au Kilosa?”
Zainabu hakunijibu na badala yake aliangua kicheko. Alipenda sana kucheka. Kisha aliniambia. “Hebu ongea na Mama Junior, huyu hapa!”
“Hello!” niliisikia sauti ya Rehema toka upande wa pili wa simu.
“Nambie, mamaa,” nilisema huku nikuma midomo yangu. “Mko wapi?”
“Tupo Kilosa, tumeingia jioni hii,” Rehema alisema. Nikashangaa sana maana tulipoongea asubuhi hakuwa ameniambia kama angekwenda Kilosa. Na ijapokuwa Rehema na Zainabu hawakuwahi kuwa na ugomvi lakini pia hawakuwa na ukaribu wa kiasi cha kutembeleana, jambo lililonishangaza! Nikajiuliza Rehema alikuwa amefuata nini kilosa? Kwa nini hakuniambia kama angekwenda Kilosa? Na urafiki wao ulianza lini kiasi cha kutembeleana?
“Mbona hukuniambia kama mngekwenda Kilosa?” nilimuuliza Rehema kwa mshangao.
Rehema akacheka. “Ndo nakwambia sasa kuwa tupo Kilosa. Tutakuwepo hapa kwa siku mbili halafu sote tutakuja Dar es Salaam Ijumaa maana Zainabu anataka kuongea na wewe.”
Maneno ya Rehema yakanishtua kidogo. Nikamuuliza kwa wasiwasi kidogo. “Kuongea na mimi kuhusu nini?”
“Unajua…” Rehema alianza kusema. “Kuna kitu Zainabu anatamani kukwambia lakini anashindwa.”
Sasa nilishtuka zaidi na akili yangu ikaenda mbali zaidi. Nilianza kujiuliza iwapo Zainabu alikuwa mjamzito maana nilikumbuka ile wiki niliporudi toka Mombasa baada ya ule mkasa uliopewa jina la ‘Ufukweni Mombasa’, nilikwenda Kilosa nikipanga kukaa siku moja tu kisha nielekee Tabora kwa wazee, lakini nikajikuta nikikaa pale kwa siku tano, Zainabu akiwa ndo kampani yangu.
Basi katika siku zile tano mimi na Zainabu tulikuwa na muda mzuri sana wa kufurahia maisha na kupeana malavidavi ya nguvu, na ukweli ni kwamba sikuwahi kujutia kitendo hicho kwa kuwa Zainabu alikuwa ni zaidi ya vile nilivyomdhania.
She was so sweet! Ule utamu ambao unasema mbona leo tamu zaidi ya jana? Na kesho unasema vile vile, dah!
Nikakumbuka jinsi mechi tuliyoicheza siku ya kwanza tu nilipofika Kilosa, hakika ilikuwa mechi kali sana, mechi ya kuombana msamaha kwa yote yaliyotokea, mechi ya kupeana adhabu kwa sababu ya kufarakana, mechi ya kuambiana jinsi tulivyokuwa tumepoteana na jinsi kila mmoja wetu alivyokuwa na hamu na mwenziwe, mechi ya kuambiana namna tulivyotamaniana. Kwa kweli ilikuwa ni mechi iliyojaa mihemuko,
sex that was full of emotions!
Siku hiyo Zainabu alishindwa kujizuia, alilia mno! Mpaka sasa nikiwa ndani ya teksi nikielekea makao makuu ya TISS nilikuwa bado nashindwa kuelewa kilichomliza namna ile kilikuwa nini! Labda ni ile hisia kuwa asingeweza kuwa na uhuru na mimi kwa kuwa nilikuwa mume wa mwanamke mwingine! Lakini yote kwa yote, muda wote alinikumbatia kwa nguvu kama aliyekuwa anaogopa kuniachia kwa kuhofia ningemkimbia.
Siku hiyo niliishuhudia michirizi ya machozi kwenye mashavu yake na mara zote Zainabu alikuwa haniangalii machoni japo kwa kawaida alikuwa msichana jasiri ambaye haoni haya kukuangalia moja kwa moja machoni, siku hii hakuwa na huo ujasiri!
Siku naondoka kwenda Tabora kwa wazee tuliamua twende wote. Ilikuwa safari ya kukumbukwa. Tuliingia Tabora usiku sana baada ya kujikuta tukibanjuka safarini. Tatizo la Zainabu lilikuwa moja, ukipitisha tu mkono katikati ya mapaja yake anakwambia analoana, duh!
Ilikuwa inanibidi nitafute sehemu kisha niegeshe gari letu pembeni, haha! Kuna wakati nilimalizia mle mle ndani ya gari na kuna mahali kulikuwa na vichaka fulani, nikampeleka nyuma ya kichaka kimoja kisha nikamwinamisha. Dah! Hadi tunafika Tabora tulikuwa tumechoka mno!
“Umenisikia?” sauti ya Rehema ilinizindua toka kwenye mawazo yangu ya kuwaza ngono. Nikatabasamu na kushusha pumzi.
“Kitu gani?” nilimuuliza Rehema huku moyo wangu ukidunda kwa nguvu.
“Zainabu ameniambia kuna mtu anataka amuoe hata kesho akikubali, ila yeye anasita kwa kuogopa kuwa Edwin bado mdogo sana. Ila mi najua hataki kuolewa kwa kuwa bado anakupenda sana,” Rehema alisema. Hata sikumjibu.
Nikatafuta namna ya kuyakwepa mazungumzo hayo. Kwa kumwambia kuwa muda huo nilikuwa na wenzangu ndani ya gari tukielekea sehemu na kwamba tungeongea baadaye. Pia nilimwomba aahirishe kwanza safari ya kuja Dar es Salaam kwa kuwa kiota kilikuwa kinateketea kwa moto mkali ambao ungeunguza makinda. Bahati nzuri Rehema alikuwa mtu wa kitengo, akanielewa.
* * *
Tukutane tena wakati mwingine hapa hapa kuzifuatilia Harakati za Jason Sizya...