Simulizi : Nguvu ya Mapenzi

Simulizi : Nguvu ya Mapenzi

SEHEMU YA 37

Erick aliona ni vyema yeye ndio aende kuwachukua dada zake shuleni na kwavile alijifunza kuendesha gari hakuona tatizo, basi akawasha gari na kwenda hadi shuleni kwao, kwakweli Erica alifurahi sana kuona kaka yao ndio amewafata pale shuleni. Basi Erick alimuuliza Erica,
“Angel yuko wapi?”
“Sijui, labda darasani kwao”
Basi wakamsubiria kwa muda ila walipoona haendi wakaamua kwenda darasani kumuangalia dada yao.
Ni kweli leo Angel alichelewa kutoka kutokana na adhabu ambayo alipewa na mwalimu ila alipoona muda umeenda na wengine wote wameondoka akaona ni vyema nae aondoke tu ukizingatia mule darasani walibaki wawili tu yani yeye na Samir basi Angel akainuka ili atoke ila Samir alimvuta mkono hadi nyuma ya darasa na kuanza kumbusu mdomoni, Erica aliingia na kushangaa huku akisema,
“Dada”
Angel alishtuka na kuogopa maana alijua kila kitu kitafika kwa mama yao ukizingatia mdogo wake ni mbea sana.


Ni kweli leo Angel alichelewa kutoka kutokana na adhabu ambayo alipewa na mwalimu ila alipoona muda umeenda na wengine wote wameondoka akaona ni vyema nae aondoke tu ukizingatia mule darasani walibaki wawili tu yani yeye na Samir basi Angel akainuka ili atoke ila Samir alimvuta mkono hadi nyuma ya darasa na kuanza kumbusu mdomoni, Erica aliingia na kushangaa huku akisema,
“Dada”
Angel alishtuka na kuogopa maana alijua kila kitu kitafika kwa mama yao ukizingatia mdogo wake ni mbea sana.
Basi Angel alijiengua toka kwa Samir na kuanza kutoka nje ila bado Samir alimvuta na kumwambia,
“Nakupenda sana Angel”
Kisha akamuachia aende, kwakweli Angel alihisi kama mapigo ya moyo wake yakienda kwa kasi na kuwakimbilia wadogo zake kisha, akaona gari ya nyumbani kwao akaogopa sana ila hofu ikapungua alipomuona Erick akimuita kuwa akapande na waende nyumbani, basi Angel alipanda huku akiona aibu hata kuwatazama wadogo zake na safari ya kwenda nyumbani ikaanza.
Walipofika nyumbani basi Erick alimuuliza kwanza dada yake,
“Angel, utanisemea kwa mama kuwa sijaenda shule leo?”
Angel Akaka kimya tu na kushuka huku akielekea ndani, basi Erica nae akashuka ila Erick alivyoshuka akamvuta Erica kwa nyuma na kumwambia,
“Kilichotokea kwa dada leo ndio kitu kinachofanya nihofie pia kuhusu wewe Erica, kiukweli nakupenda na sipendi upotee jamani”
Erica alimuangalia tu kaka yake na kuingia ndani bila ya kusema chochote kile kwani taswira ya alivyomkuta dada yake ilikuwa ikimjia kwenye kichwa chake.
 
SEHEMU YA 38

Angel alienda kujilaza tu kitandani hata sare za shule hakuvua wala nini kwani kile alichofanyiwa na Samir kilikuwa kikitembea katika akili yake, na lile neno la mwisho aliloambiwa na Samir kuwa anapendwa sana lilikuwa linatembea vizuri sana katika akili yake yani hadi akimfikiria anajikuta akisisimka tu mwili mzima na kujisemea,
“Oooh Samir, kwanini najihisi hivi? Yani ndio nakupenda? Sitaki Samir, niache nisome. Oooh hata masomo yenyewe hayapandi tena maana kichwa change kimezungukwa na Samir”
Yani hakuwa na amani kwani muda wote alikuwa akimuwaza Samir, hata dada yao alipowaita kwaajili ya chakula alilihisi hilo sema hakuwa na uhakika kama Angel anaweza kumwambia ukweli.
Basi Vaileth alimuita Erica ili kumdadisi tu kama anafahamu kinachoendelea kwa Angel,
“Dadako anaonekana kuwa na mawazo sana, nini kinamsumbua”
“Labda sababu nimemfuma leo anahisi nitamwambia mama”
“Umemfuma kivipi?”
“Nimemkuta ananyonyana midomo na mwanaume darasani kwao”
Mama yao nae alikuwa akiingia kwahiyo alisikia hilo vizuri sana na kushindwa kuanza hata na salamu zaidi ya kumuuliza Erica vizuri,
“Erica unaongelea nini?”
Erica nae alishtuka kwani hakujua kama mama yao angerudi kwa muda huo kutokana na jinsi alivyoongea nao jana yake, basi mama yake akamuuliza tena,
“Hebu nieleze Erica, ni kitu gani kimetokea kwa Angel?”
“Mama, kiukweli leo dada Angel alichelewa kutoka darasani basi nikaamua kwenda kumuangalia ndio tukamkuta akifanya kama wazungu wanavyofanyaga kwenye video”
“Alikuwa na nani?”
“Simjui ila ni mkaka wa kwenye darasa lao”
Basi mama yao akamuacha pale sebleni na kisha kuondoka zake ambapo moja kwa moja Erica alijua tu mama yao anaenda kumuhoji Angel. Basi alimuhurumia dada yake na kumwambia Vaileth,
“Dada, eti mama atampiga Angel eeeh!”
“Sijui ila mama yenu amechukia sana”
Basi nae Erica akainuka na kuondoka pale sebleni.
 
SEHEMU YA 39

Moja kwa moja mama Angel alienda chumbani kwa Angel na kumkuta kajilaza tu, yani alikula na sare zake na alienda tena kujilaza na sare zake, hakujishughulisha kuzivua kabisa, basi mama Angel akamshtua Angel na kumuuliza,
“Hivi Angel mara ya mwisho kukupiga ulikuwa na umri gani?”
Angel alikaa kimya tu, kisha mama yake akaongea,
“Ni mvulana gani uliyekuwa ukifanya nae tabia mbaya shuleni?”
“Mama, haikuwa dhamira yangu”
“Haikuwa dhamira yako nini, hivi unayajua madhara ya mapenzi wewe? Unajua mapenzi yanaweza kukutenda kitu gani? Unaelewa mapenzi ni shetani gani? Unajua mapenzi wewe?”
Angel alikaa kimya tu, na mama yake akamuuliza tena,
“Niambie, ni Samir eeeh!”
Angel aliitikia kwa kichwa, kwakweli mama Angel alisikitika sana na kujikuta akimnasa vibao vitatu Angel halafu akatoka chumbani kwa Angel na kwenda chumbani kwake ambapo alikaa na kujikuta akilia tu huku akisema,
“Ni wapi nimekosea kwenye malezi ya huyu mtoto jamani! Mbona nimejitahidi kila kitu kama mama bora, kwanini mwanangu anaharibikiwa? Kitu gani Angel sijampatia, nimempa maisha mazuri, nimempeleka shule nzuri, kila kitu nawapa humu ndani, kila hitaji lao wanapata na kwanini inakuwa hivi jamani. Huyu Angel anataka kunitenda nini mimi?”
Muda huo huo mumewe nae aliingia ndani na kumkuta akilia basi alimbembeleza na kumuuliza kinachomliza,
“Sikia nikwambie, nimejitahidi kwa kila hali ila Angel asipitie maisha ambvayo mimi nimeyapitia, sitaki Angel azae nje ya ndoa kwani naelewa maumivu ya kuzaa nje ya ndoa, mtu unadharaulika, thamani yako inapungua na utu wako unapungua, kila mtu anakuona kuwa mkosaji, kwa hakika mimi bila wewe nadhani ningechanganyikiwa maana kila siku akili yangu ilikuwa haisongi, sasa kwanini Angel anataka kurudia maishayale niliyopitia mimi jamani!”
“Kwani kafanyaje?”
Basi akamuelezea kile ambacho ameelezewa kuhusu Angel, mumewe alimpooza pale na kumwambia,
“Usilie mke wangu, wewe ni mama bora, haya mambo mengine ni kawaida tu hata yasikuumize kichwa. Jumatatu nitaenda shuleni kwakina Angel, na nitaonana na huyo kijana, kwa hakika nitamuonya kwani sitaki masikhara na binti yangu kabisa.”
Mama Angel alifarijika kusikia vile na kumkumbatia mumewe, ila kiukweli alihisi kupatwa na mawazo sana juu ya mtoto wake.
 
SEHEMU YA 40

Usiku wa siku hiyo, Angel alijihisi kujiwa na ndoto juu ya Samir tu na alijihisi kumpenda Samir haswaaa hadi alikuwa akishtuka na kumtaja,
“Samir”
Alikaa kitandani na kulaumu sana kichwa chake kuwa na mawazo ya Samir kiasi kile yani hata kibao alichopigwa na mama yake hakikumuingia kwenye akili yake kabisa.
Kulipokucha, mama yake akaenda chumbani kwake na kuongea nae,
“Mwanangu Angel naomba niambie mwanangu huyo Samir kakupa nini?”
“Kwanini mama?”
“Unajua hadi usiku unaita Samir jamani, kwanini lakini jamani! Angel mwanangu naomba usome, nahitaji uwe mtu unayejitambua kwenye maisha, soma mwanangu jamani”
Angel alimuangalia tu mama yake kisha mama yake alimtaka ajiandae ili atoke nae kwani aliona ni vyema kufanya hivyo ili kuichangamsha akili ya mwanae kidogo.
Basi Angel alijiandaa na kutoka na mama yake.

Nyumbani wakina Erick na Erica nao waliamua kutulia na kuangalia Tv, kwenye luninga ile kulikuwa na tamthilia inaendelea ambayo ilihusu mapenzi na kufanya waiangalie kwa makini sana, basi vaileth nae alienda na kuongea nao kuwa ile tamthilia ni muendelezo,
“Yani kila siku huwa inaonyeshwa sema mnakuwa shule”
“Inahusu nini dada?”
“Yani humu kuna mdada na mkaka wanapendana ila wanashindwa kuambiana basi wanavyofanyiana hadi raha kuwaangalia”
“Mmm jamani kwanini wanashindwa?”
“Kutongoza kipaji Erica, yani sio wote wanaweza kusema ni kiasi gani wanapenda, utakuta mtu anaumia tu moyoni mwake lakini kusema ukweli anaogopa”
Mara Erick aliinuka na kuondoka, ambapo vaileth alimuuliza,
“Erick rafiki yangu hujaipenda au?”
“Aaaah basi tu kichwa change hakipo sawa”
“Basi tutaongea vizuri rafiki yangu”
Basi Erick akaondoka na Erica alimuuliza Vaileth,
“Kwahiyo dada Erick pekee ndio rafiki yako eeeh!”
“Hamna wote nyie ni marafiki zangu ila huwa napenda sana kuongea na Erick, kwanza sio muongo, sio muigizaji, yani akikwambia kitu basi lazima anyooshe maelezo yake na kama kitu hakipendi lazima utajua tu kuwa hakipendi”
“Mmmh dada, nani muongo sasa humu ndani?”
“Sijasema kuwa nyie ni waongo hapana ila namaanisha kuwa Erick yupo tofauti sana”
Basi Erica alimuangalia tu huyu dada yake kisha akaendelea kuangalia ile tamthilia.

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 41

Angel na mama yake wakati wanarudi nyumbani, basi mama yake akaguswa bega, kugeuka nyuma alifurahi sana kwani alimuona mtu ambaye walifahamiana ila ni muda mrefu umepita tangu kuonana kwao,
“Khee jamani Dora upo!!”
“Nipo, za siku. Yani tumepotezana kabisa”
“Ni kweli tumepotezana ten asana tu, nipe habari. Mumeo hajambo!”
Dora aliinama chini kidogo na kumfanya mama Angel amuulize kwa makini kuwa imekuwaje,
“Vipi Dora jamani?”
“Mume wangu alifariki”
“Jamani, pole sana ndugu yangu jamani. Kwahiyo sasa hivi unaishi wapi?”
“Nilikuwa naishi nae mkoani na ndiko alikofia, yani nimerudi siku sio nyingi ila kuna nyumba tulijenga na ndio ninayoishi, kaniachia mtoto mmoja, kwahiyo kwasasa naitwa mama Jesca”
“Oooh hongera kwa kupata mtoto, hivi kumbe James alikufa! Hata nyumbani hatujapata taarifa”
“Ndugu yangu ndugu yangu mngepatia wapi taarifa? Mume wangu kafa kifo cha aibu, nitakusimulia vizuri ila nina mengi sana ya kuzungumza na wewe rafiki yangu, halafu kwenu nimepasahau nilitaka hata kwenda kumsalimia mama yako, halafu dada yako nina ujumbe wake ambao niliachiwa na mume wangu, kwakweli nina mengi sana”
“Karibu nyumbani basi”
Ilibidi mama Angel amshawishi ili rafiki yake huyo afike kwake mara moja na aweze kupafahamu ili siku nyingine aweze kufika, basi alikubali na kuondoka nae huku wakiongea mambo mbalimbali ambapo walianza kucheka na kukumbushana mambo ya usichana wao.
Mama Angel alikuwa akiendesha gari huku rafiki yake akiwa amekaa pembeni basi akamwambia,
“Ila Erica una bahati sana wewe, yani una bahati sijapata kuona jamani, kwahiyo hadi leo unaishi vizuri tu na Erick?”
“Ndio, tumezoeana mno kwasasa, tofauti na kipindi kile cha uoga uoga”
Wakacheka na akamkumbushia tena,
“Hivi na wale waliokuwa wanakufukuzia kipindi kile waliacha? Kwanza vipi Bahati jamani natamani nijue kaishiaje”
Mama Angel alicheka na kumwambia rafiki yake,
“Kuna mtoto kumbuka”
“Halafu hujanitambulisha, ndio Angel huyu”
“Eeeeh ndio mwenyewe”
“Kheee kakuwa huyo, halafu saivi kidogo anafanana fanana na wewe, hizo nywele za Rahim hizo”
“Mmmmh naomba acha hizo stori rafiki yangu”
Mama Angel hakutaka kuongea chochote kuhusu mambo ya zamani ya Angel kwani hakutaka Angel amjue baba yake halisia ni nani kwani hakuwa yule ambaye Angel alizoea kumuita baba, basi waliondoka hadi kufika nyumbani kwa mama Angel na kushuka huku akimkaribisha sana pale nyumbani kwake.
Dora aliingia na kusifia uzuri wa ile nyumba,
“Jamani hongera shoga yangu, kwakweli maisha umeyapatia jamani”
Mama Angel alicheka tu na kuingia ndani ambapo alimkuta Erica na kumtambulisha kwa yule mgeni, ambaye alishangaa,
“Kheee anaitwa Erica? Si jina lako hili?”
“Ndio jina langu ila nimeona nimpe mwanangu, unajua nilizaa mapacha, basi kuna huyu Erica na kaka yake Erick, wewe Erica hebu kamuite Erick”
“Kumbe ile mimba ndio ulizaa mapacha, nakumbuka nilikuacha na mimba”
“Basi ndio hao watoto”
Basi Erica alinyanyuka na kwenda kumuita kaka yake ndani, na muda kidogo tu Erick alifika na kumsalimia yule mgeni kisha mama yake alimtambulisha ila mgeni yule aliguna sana baada ya kumuona Erick mpaka mama Angel alimuuliza,
“Mbona umeguna hivyo?”
“Hamna kitu, nimefurahi tu kuwafahamu watoto wako, nami nitakuletea mwanangu umfahamu. Ila kwasasa naondoka kwani natakiwa kuna mahali niwahi halafu nitakuja tena tuongee vizuri”
Wakabadilishana namba pale na mama Angel alitoka kumsindikiza ila bado alimuuliza kwanini aliguna baada ya kumuona Erick,
“Mbona umeguna sana dora, tatizo ni nini?”
“Hakuna tatizo ila kwanini mmewapa watoto majina yenu?”
“Kani kuna ubaya? Nataka watoto hawa wapendane kama ambavyo wazazi wao tulipendana”
“Hebu acha masikhara yak ohayo, nyie mlipendana ila mlikuwa wapenzi, ila watoto hawa ni ndugu halafu unataka wapendane kama nyie, una maana gani?”
“Hapana sio hivyo unavyomaanisha wewe, nataka wanangu wawe na upendo tu, halafu sababu mimi na baba yao wengi walituhisi ni mapacha”
“Mmmh hata kama, unajua unavyotoa majina uwe unaangalia na nyuma ikoje”
“Kivipi jamani, kwani watoto huwa hawachukui majina ya mama zao? Huwa hawachukui majina ya baba zao?”
“Ni wengi tu huchukua hivyo ila na nyie mna historia gani? Sina ubaya kusema hivi ila nimewapenda wanao wana heshima hadi raha, vipi Angel hujampeleka kwa babake nini?”
“Ni historia ndefu, ila kwa kifupi babake Angel yani Rahim alikuwa na lengo baya la kunivunjia ndoa yangu, niliruhusu awe anakuja kumuona mtoto ila akawa anafanya mambo ya ajabu sana, tukipata muda nitakueleza vizuri zaidi, kwahiyo mimi na mume wangu tuliamua kuhama tulipojenga na kujenga pale na kuanzisha maisha mapya yap eke yetu yani sisi na watoto wetu, basi tokea hapo Angel hajui kama alishawahi kuwa na baba wa kuitwa Rahim”
“Oooh haya, akija Erick msalimie sana”
Kisha mama Jesca akaondoka zake.
 
SEHEMU YA 42

Angel aliingia chumbani kwake na kukumbuka maneno ya yule mama kuwa huyu mtoto nywele zake kama Rahim, basi akaanza kujiuliza,
“Rahim ni nani? Kwanini mimi nywele zangu ni kama za Rahim?”
Alikosa jibu na kuvizia mama yake akiingia ndani basi alimfata chumbani na kumuuliza,
“Mama, kwani Rahim ni nani?”
“Mwanangu kuna siku nitakaa na wewe na nitakueleza vizuri juu ya huyo mtu na utaelewa tu”
“Unajua mama sielewi, kwani baba sio baba yangu?”
“Nyamaza wewe mtoto, funga mdomo wako huo, asingekuwa babako angekupenda kiasi hiki? Angekusomesha, angekulisha na kukujali?”
“Ndiomana nikawa nashangaa mama, sijauliza kwa maana mbaya kwani mimi najua baba ndio baba yangu na ananipenda sana”
Na muda huo baba yao nae alirudi kwahiyo alimsalimia na kumpisha mule chumbani kwa mama yake, kisha baba Angel alimuuliza mama Angel maana alisikia kidogo,
“Kuna nini kwani? Umemwambia ukweli Angel?”
“Hapana mume wangu siwezi kufanya hivyo, tutamuharibu Angel kisaikolojia maana siku zote anakufahamu wewe kama baba yake halafu leo uje umwambie kuna mjinga mmoja ndio baba yake, kwakweli tutamuharibu kisaikolijia”
“Aaaah nikajua umemwambia ukweli, ila mazungumzo hayo yalianzia wapi?”
Basi mkewe alimueleza jinsi walivyoenda mjini na kukutana na rafiki yake ambaye alifika nae nyumbani kwake,
“Kheee bado tu una urafiki na yule mtu na umemleta hadi nyumbani, ila mke wangu yule ni mropokaji sana, yani usishangae siku akiropoka kwa Angel”
“Hapana bhana, saivi amekuwa, ni mama ujue, ana mtoto mmoja wa kike”
“Hata kama, ile ni tabia yake ya kuropoka na hawezi kuiacha, ila sijui labda kabadilika siku hizi. Haya nilikoenda yote nimeyafanikisha na jumatatu nitaenda shuleni kwakina Angel halafu Erick nitamuhamisha shule tayari nafasi nimeshapata”
“Kheee Erick unamuhamisha shule?”
“Ndio, kaniomba sana kuwa ile shule haitaki na mimi nimemsikiliza, nataka watoto wangu wasome na sio waishie kati kama mimi baba yao, kwahiyo kama kasema mahali Fulani hapataki na ana sababu zake nikaona ya nini kumlazimisha? Basi nimemtafutia sehemu nyingine na Jumatatu nitaenda kumchukulia baraua shuleni kwao”
“Ila ungefanya jambo la muhimu zaidi kumuhamisha Angel shule maana yule ndio yupo kwenye wakati mbaya.”
“Mke wangu, Angel kabakiza mwaka tena sio mwaka ni miezi tu kumaliza kidato cha nne kwanini tuanze kumsumbua hivyo?”
“Mbona kuna wengine wanahamisha watoto wao”
“Naweza sema kuwa hawajielewi, yani ni muda mchache tu umebaki, tutaichanganya akili ya mtoto.”
Mama Angel alitulia tu kwani kwenye kundi la wasiojielewa inamaana hadi dada yake yupo humo kuwa nae hajielewi kwani kahamisha mwanae wa kidato cha nne.
 
SEHEMU YA 43

Jumapili ya leo walijiandaa vizuri kwenda kanisani ila Angel alidai kuwa anaumwa kwahiyo hakwenda na kubaki nyumbani tu, hakuwa akiumwa ila alikuwa na mawazo sana kuhusu Samir.
Basi walipoondoka wote, Vaileth alimuita na kuongea nae,
“Angel, hebu niambie mdogo wangu tatizo ni nini? Eti wakati huyo mwanaume anakubusu ulijihisi vipi”
Angel alimuangalia huyu dada na kumwambia,
“Yani sijui nielezaje jamani, ila siku ile hata sijui nilijihisi vipi”
“Ila Angel mdogo wangu, masomo ni muhimu zaidi, usichanganye mapenzi na shule utakuja kujutia, mapenzi yapo na daima yataendelea kuwepo yani hayaishi wala hayatoisha kwahiyo muda muafaka ukifika utayapata tu mapenzi na utakuwa nayo hadi utayachoka”
“Mmmh!”
“Usigune Angel, sikia nikwambie ni kweli wewe ni binti mrembo sana una kila sifa ya kufanya kila mwanaume avutiwe na wewe ila sio kila mwanaume atakupenda kweli, maana wengine watakutamani tu kuwa nawe kwa muda mfupi na kisha kuachana na wewe, kwakweli unatakiwa kuwa makini sana mdogo wangu, mapenzi yapo na yataendelea kuwepo kwahiyo shule kwanza, soma mdogo wangu kwani elimu ni ya muhimu sana”
“Ila kwanini mimi najihisi hivi sasa?”
“Hiyo ni kawaida tu wala usione ni tofauti sema cha kufanya jiweke mbali na huyo mtu na umuone kuwa ni mbaya na anataka kuharibu maisha yako, hebu fikiria ukipata mimba sasa utaendelea na shule? Unadhani ataendelea kukupenda na kukujali? Nione hivi mimi, nilipata mimba nikiwa kidato cha pili, kwakweli niliacha shule na ndoto ya kusoma ilikatika pale, mwanaume alinikimbia na maisha yakawa magumu sana kwa upande wangu”
“Kwahiyo mwanao yuko wapi kwasasa?”
“Yupo kwa wazazi wangu na mimi nimeamua kuja kufanya kazi za ndani, kwakweli huwa najutia sana, nilijitoa ufahamu na kujiingiza katika mapenzi wakati nikiwa bado mwanafunzi na sasa najutia mdogo wangu tena najutia sana”
“Pole dada Vai”
“Hiyo pole yako itatenda kazi kwangu vizuri endapo utaamua kuendelea na masomo yako na kuachana na mambo ya mapenzi kabisa, fikiria masomo Angel’
Basi Angel alimsikiliza Vaileth na kiasi Fulani kuwa kama mtu aliyeelewa alichokuwa akiambiwa, kisha akamuuliza tena,
“Ila nitafanyaje sasa ili nisimuwaze sana”
“Unatakiwa ufanye kwa makini unachofanya, yani kuwa makini sana. Fikiria maisha yako ya mbeleni, panga maisha yako sasa, ukiona unamuwaza sana basi njoo unisaidie kazi za hapa na pale maana ukijishughulisha utashangaa tu huna mawazo nae wala nini”
“Sawa dada nimekuelewa”
“Kuwa makini sana Angel, dunia ina mambo sana hii, zingatia masomo”
Basi Angel akiendelea kuongea na Vaileth pale alishangaa kuona Hanifa akifa pale kwao ilibidi amkaribishe vizuri tu.
“Mmmh shoga yangu za tangu Ijumaa? Nimeona bora leo nikufate”
“Ila kitu chenyewe mpaka niende kwenu jamani hanifa?”
“Ndio, ni muhimu sana tena sana shoga yangu”
“Ila hatuchukui muda mrefu?”
“Yani wala hakuna kuchukua muda wala nini, muda huu huu tunarudi”
“Basi twende haraka haraka maana mama na baba wameenda kanisani na leo sidhani kama watawahi kurudi, twende muda huu”
Basi Angel alienda kujiandaa haraka haraka na kutoka ila vaileth akamwambia,
“Angel unaenda vipi mahali bila kumuaga mama yako?”
“Sikia dada, yani hata hatuchukui muda mrefu, ni jambo la muhimu halafu ni siku nyingi acha leo nikaone mara moja”
Basi yeye na Hanifa wakaondoka zao hapo nyumbani.
 
SEHEMU YA 44

Vaileth alibaki na muda ulienda ila Angel hakurejea nyumbani wala nini, akawaza mama yao wale watoto akirudi itakuwaje yani lazima atamfokea tu, na kweli muda kidogo walirudi kutoka kanisani na kama kawaida mama Angel aliamua kwenda kumuangalia Angel chumbani ili kujua anaendeleaje maana alisema kuwa anaumwa asubuhi, alishangaa kwenda chumbani kutokumkuta mtoto wake, basi akarudi kwa Vaileth na kumuuliza,
“Angel yuko wapi?”
“Alikuja rafiki yake mmoja hapa wa kuitwa Hanifa ndio kaondoka nae”
“Kheee jamani huyu mtoto loh! Sijui huyo Hanifa anakaa wapi jamani”
Kwakweli alihisi hata chakula kichungu kwa muda huo kwani alikuwa akimuwaza mtoto wake tu, basi akawaita Erick na Erica na kuwauliza kama wanapafahamu kwakina Hanifa,
“Eti jamani kuna anaepafahamu kwakina Hanifa?”
Wote waligoma ila Erick alikumbuka jambo na kusema,
“Nadhani huyo nafahamu dukani kwao, maana kuna siku za nyuma niliwahi kwenda na dada mara moja”
“Oooh naomba nipeleke mwanangu, jamani huyu Angel ataniua kwa presha dah!”
Basi Erick alitoka nje na mama yake na kuingia kwenye gari na kuanza safari ya kumpeleka dukani kwakina Hanifa.

Angel na Hanifa waliongozana hadi dukani ila wakamkuta James ambapo hanifa alimuuliza,
“Mjomba kaenda wapi?”
“Mmm katoka kidogo ila kasema mumsubirie”
“Aaaah tuna haraka jamani, ngoja nikamuangalie nyumbani”
Basi Hanifa akaondoka na kumuacha James pale akiwa na Angel ambapo James alianza kuongea na Angel,
“Katika maisha yangu sijawahi kuona msichana mrembo kama wewe, hakika nakupenda sana Angel”
Basi Angel alikaa kimya tu, ambapo James aliendelea kumuelezea jinsi alivyo mrembo,
“Kwakweli nakupenda sana, na nikikupata hakika utajihisi unamiliki dunia maana nitakupenda, nitakujali, nitakuthamini na kukuheshimu”
Halafu James akasogea ili ambusu Angel, ila Angel alimsukuma pembeni na kusema,
“Sitaki, sijafata hayo mimi”
“Ila umefata nini?”
Angel akakaa kimya ambapo James aliendelea kumwambia,
“Ni heri unipe mimi mtoto mwenzio kuliko huyo mtu mzima unayetaka kumpa”
“Kumpa nini?”
“Tunda”
“Tunda lipi?”
“Kumbe hujui kama una tunda? Twende ndani nikakuonyeshe”
Angel alichukia na kumsonya james, yani katika vitu ambavyo James hakuvipenda ni kusonywa na mwanamke, basi akamwambia
“Angel umenisonya, ila ungejua nilivyo hata usingethubutu kunisonya”
Muda huo huo alifika Hanifa na mjomba wake ambapo Hanifa alimtambulisha Angel pale na Angel alimsalimia kwa heshima zote yule mjomba,
“Shikamoo mjomba”
Ila huyu mjomba hakuitikia wala nini na akatangulia ndani ya chumba ambacho kilikuwepo dukani, halafu Hanifa nae alimshika Angel mkono na kuingia nae kwenye chumba hiko halafu alimuacha humo kisha yeye alitoka na wala hakuongea chochote na James zaidi ya kuondoka tu.
 
SEHEMU YA 45


Erick alifika na mama yake kwenye lile duka na wakashuka kwenye gari ambapo nje ya lile duka walimkuta James, yani huyu mama alichukia sana ukizingatia ashawahi kumuona huyo James akimnyemelea mtoto wake, basi alimfata na kumkukunja huku akimwambia,
“Wewe mjinga, nionyeshe mtoto wangu alipo”
James akawa anajiuma uma basi mama Angel akamnasa kibao na kumwambia,
“Nitakufunga wewe mtoto ujue, yuko wapi mwanangu Angel?”
James hakuongea neno zaidi ya kuongozana na yule mama hadi kwenye chumba cha lile duka. Basi walipofika akaanza kugonga ila mama Angel alimsukuma pembeni na kufungua ule mlango, alishtuka sana kumkuta mwanae akiwa chini hana fahamu halafu yule mwanaume ndio anataka kumuingilia kimwili, yani mama Angel alipatwa na hasira sana na kwenda kumsukuma yule mwanaume pembeni ambapo alianguka chini kwani kilikuwa ni kitendo cha gafla sana kutokea.
Yule mwanaume alipoanguka ndipo alipotazamana vizuri na mamake Angel, yule mama alisikia akisema kwa jazba,
“Kumbe ni wewe!!”
Yule mjomba alitazama macho chini kwa aibu maana alikuwa akifahamiana na huyu mama.



James hakuongea neno zaidi ya kuongozana na yule mama hadi kwenye chumba cha lile duka. Basi walipofika akaanza kugonga ila mama Angel alimsukuma pembeni na kufungua ule mlango, alishtuka sana kumkuta mwanae akiwa chini hana fahamu halafu yule mwanaume ndio anataka kumuingilia kimwili, yani mama Angel alipatwa na hasira sana na kwenda kumsukuma yule mwanaume pembeni ambapo alianguka chini kwani kilikuwa ni kitendo cha gafla sana kutokea.
Yule mwanaume alipoanguka ndipo alipotazamana vizuri na mamake Angel, yule mama alisikia akisema kwa jazba,
“Kumbe ni wewe!!”
Yule mjomba alitazama macho chini kwa aibu maana alikuwa akifahamiana na huyu mama.
Kwakweli mama Angel alikuwa na hasira sana na kwenda kumuinua mwanae ambaye alikuwa hajitambui kwa wakati huo kisha akambeba na kutoka nae nje ambapo walimpandisha kwenye gari na kumtaka Erick awahishe hospitali ili akamuangalie Angel kazimia na nini ila walipofika karibu na hospitali Angel alizinduka huku akishangaa shangaa kwakweli mama yake alifurahi kumuona mwanae kazinduka yani akajikuta akishindwa hata kumfokea kabisa.
Basi alitaka waende hivyo hivyo kwa daktari ila Angel akagoma ikabidi warudi nyumbani tu yani kwakweli huyu mama hata hakujua aanzie wapi kumsema Angel kwani akikumbuka ni machozi yalimtoka tu.
Walifika nyumbani na kumtaka Angel aende chumbani halafu yeye hakuongea kitu zaidi ya kwenda chumbani kwake na kuanza kulia kama ambavyo alilia siku aliyoambiwa mwanae amefumwa akiwa na Samir,
“Jamani kwanini lakini? Kwanini Angel ananifanyia hivi? Huyu mtoto ananitaka kitu gani jamani!”
Alilia sana mpaka pale Erica alipoenda chumbani na kumgongea maana kuna mgeni alikuwa amekuja,
“Mama, mamkubwa kaja”
Basi mama Angel akajifuta machozi na kutoka kwenda kuongea na dada yake.
 
SEHEMU YA 46

Alifika sebleni na kumkuta dada yake nae akionyesha sura ya hasira ila alimpokea na kumkaribisha vizuri, sema dada yake nae aligundua kuwa mdogo wake ana matatizo basi aliomba kuongea nae kwanza ili kujua kakumbwa na matatizo gani, ikabidi watoke pale ndani ya nyumba na kuelekea kwenye bustani ili kuweza kuongea maana hata yeye aliona vyema akimwambia dada yake atapumua,
“Nini kinakusumbua mdogo wangu? Una maisha mazuri, mumeo anakupenda sana, huna mawazo kama hela ipo, tatizo ni kitu gani yani nini kinakusumbua?”
“Ni Angel dada”
“Kafanyaje Angel/ niambie mdogo wangu, usikae na kitu moyoni maana kitakuumiza zaidi natumai unaelewa nikisema hivyo”
“Naelewa dada”
“Haya, niambie”
Basi akamsimulia kwa kifupi jinsi ambavyo amemkuta Angel,
“Kheeee hatari, kwahiyo kambaka?”
“hapana hajambaka ila ningechelewa kidogo tu basi angembaka jamani mwanangu”
“Pole sana mdogo wangu, huyu Angel nae kwanini amekuwa hasikii kiasi hiko jamani? Huyo mwanaume nae amekuchanganya kwanini?”
“Nadhani dada sijawahi kukwambia kuhusu hili, kuna mwanaume alikuwa akiitwa George, nilikutana nae kipindi nasoma chuo, mwanzoni niliamini ananipenda kumbe anahitaji msichana bikra, yani alipotembea na mimi na kukuta si bikra aliniacha peke yangu nikiwa sina hata nauli, nakumbuka siku hiyo nililia sana na kulaumu kwanini nilimuamini kiasi kile nilichomuamini. Nikaja kujua ukweli kuwa huyo mwanaume ni muhuni balaa, na pale alipo ameathirika yani kaathirika kitambo sana, yule rafiki yangu Dora alitembea pia na huyu George, halafu leo nimemkuta anataka kunibakia mwanangu kwakweli nimeumia sana, kwanini mimi jamani? Kwanini mimi nafanyiwa hivi!! Yani watu wananifatilia na utu uzima huu jamani, sio wakati wangu wa kulia kwasasa, ila kwanini Angel ananitesa kiasi hiki, kwanini huyu mtoto ananieleleza sana mimi!”
“Nadhani ni vyema sasa ukamwambia Angel asili yake, anatakiwa amfahamu babake wa ukweli”
“Mmmh si ndio itakuwa balaa”
“Hapana, unatakiwa kumueleza Angel kuhusu ukweli wa maisha yake, mueleze jinsi ulivyohangaika nae, mueleze jinsi babake alivyokutenda, ili kama akiamua kuyafanya maisha yake hovyo ajue ukweli kabisa kuwa anakuumiza kwa kiasi gani, mwambie Angel ukweli”
“Nasubiri hata afike chuo ndio nimwambie ukweli maana kwasasa nitaichanganya akili yake, unajua siku zote Angel anajua huyu ndio baba yake mzazi! Kwakweli nimepata mume mwenye upendo sana, yani anampenda mwanangu hadi nafurahia kwakweli, sijui ningefanyeje mimi kama huyu asingekuwa mume wangu ila kwanini Angel ananifanyia hivi jamani!”
“Mwambie ukweli, nakwambia mdogo wangu ukweli utakuweka huru, mwambie ukweli. Si unaona kama Junior anaelewa fika kama baba yake alikuwaje”
“Eeeeh tena bora umenikumbusha dada, nilikutana na Dora, nasikia James amekufa”
“Ndio amekufa”
“Kumbe unajua dada?”
“Najua vizuri ila sikuwaambia wala nini, kwanza ni kujichoresha, kwa yule mwanaume niliondoka mwenyewe, sasa niseme kitu gani? Alikufa ndio”
“Eeeeh aliumwa nini?”
“Na wewe nawe, aliumwa nini kivipi? Si alikuwa na ukimwi yule? Ila hapa mwishoni nasikia alianza tena uhuni yani uhuni ndio ulipamba moto na amefia guest akiwa na mwanamke, sasa sijui kitu gani ila kafia guest”
“Kheee shemeji nae, hakuacha uhuni jamani loh!”
“Basi ndio naimba wimbo mmoja na Junior kila siku, baba yake kafia guest sijui nay eye anataka hivyo jamani! Katoto kale kanahitaji maombi kwakweli, peke yangu siwezi, nishamkanya hadi nimechoka jamani ila mtoto hasikii hahambiliki jamani”
“Kheee pole dada”
“Ila sio kilichonileta huku, bali kilichonileta ni watoto wa wifi yako jamani mimi nimechoka, huyu tumaini anaweza fanya tuharibu undugu kwakweli”
“Eeeeh wamefanyaje tena dada”
“Watoto ni wavivu wale sijapata kuona, ila ni malezi ambayo mama yao kawalea yani tumaini kawaendekeza sana watoto wake jamani, yule mdogo yupo darasa la pili ila hawezi kufua hata nguo yake ya ndani jamani! Malezi gani haya sasa? Kwakweli Tumaini anakera, yani watoto wake wananikera jamani, nilijua nitamkuta mumeo nilitaka niongee nae ili aongee na dada yake, mimi nimechoka jamani”
“Pole, tulipotoka kanisani kuna mahali alipitia”
“Ila jamani Mungu huyu kweli mkali, hadi mumeo nae anaenda Kanisani mmmh! Yani kabadilika kabisa kama sio yeye, ila wanaume hawaaminikagi ujue”
“Kivipi dada? Unamaanisha atakuwa ananisaliti?”
“Sina maana hiyo”
Mara simu ya mama Junior ikaita na kumfanya aipokee ila alipata habari ya kumshtua kidogo na kumuaga mdogo wake,
“Vipi tena dada?”
“Nasikia Junior huko kapiga mtu, sasa kashikiliwa polisi. Ngoja niende”
“Kheee watoto hawa jamani, tuzaage tu kutoa machango tumboni, hawa wangebaki kwenye viuno vyetu basi tungetolewa uvimbe kama kichwa cha mtu. Pole dada, utaniambia yatakayojiri”
Basi mama Junior akaondoka na mama Angel alirudi ndani.
 
SEHEMU YA 47

Muda huu mama Angel alienda tena chumbani kwa Angel na kuongea nae kwa ukaribu zaidi,
“Mwanangu unajua hatujaongea kabisa, hebu niambie imekuwaje kwanza?”
“Mama, kwakweli sikujua kabisa, siku zote Hanifa kaniambia kuna kitu anataka kunionyesha na sikujua ni kitu gani kwakweli”
Basi Angel akaanza kumueleza mama yake toka siku ile alipoenda pale dukani kwakina Hanifa na jinsi walivyotaka kutoroka shule na kupewa adhabu na vile alivyoondoka nae siku hiyo,
“Sasa tumefika pale, kumbe ndio kaenda kumuita mjomba wake, tumeingia pamoja kwenye kile chumba na mwenzangu akaondoka mara yule mjomba wake akasogea na kusema kuwa ananipenda sana, pale pale niliinuka na kutaka kuondoka ila yule mjomba alinivuta na kunipulizia sijui nini usoni basi nikapata usingizi na kuanguka chini”
“Kheee mwanangu, ila kila siku naongea kuhusu marafiki jamani, kuna wengine katika maisha sio marafiki wazuri, wapo kwa lengo la kukuharibia maisha tu, sasa Hanifa kwako sio rafiki mwema kabisa, ona alichotaka kukutenda sasa jamani! Yani mjomba wake angekubaka, halafu unajua kama ameathirika!”
“Ameathirika!!”
“Ndio, ana ukimwi yule alitaka kukuambukiza mwanangu, jamani Angel hebu tulia basi, hutaki uwe kama mama yako? Muda muafaka utapata mume sahihi katika maisha yako na atakujali na kukuheshimu ila sio hawa wa kutaka kukuharibia masomo yako, kuwa makini mwangu. Nadhani unanielewa”
“Nakuelewa mama”
“Leo sitakupiga kabisa, maana hata nikikupiga ni kazi bure tu ila nakwambia kuwa jipende mwanangu, maisha yako ni ya thamani sana kuliko kitu chochote kile”
Angel alimuitikia mama yake pale na kumuomba msamaha kwani alijua wazi kuwa ameshamkosea mama yake, basi mama yake akainuka na kuondoka.
Alibaki Angel mwenyewe akijisemea,
“Kwakweli nimemkosea mama, ila kaacha mambo yake yote na kuja kuniokoa mimi, hivi kwanini sisiskii jamani!! Kwani Angel una matatizo gani??”
Akawa akijiuliza mwenyewe tu kwani alijishangaa pia kwa kutokusikia anachoambiwa.
 
SEHEMU YA 48

Baba yao aliporudi, mama yao alienda kuongea nae na kumwambia jambo lililotokea siku hiyo,
“Unajua huyo mwanaume aliyetaka kumbaka Angel ni nani?”
“Nani?”
“Ni George, yule mwenye undugu na mamako”
“Khaaa yule jamaa kakumbwa na nini lakini, mbona anatenda mambo ya ajabu sana? Yani nashangaa jamani, maukoo mengine yana watu wa ajabu hatari, utanipeleka huko nikazungumze nae, kwakweli sijapenda kabisa hilo jambo jamani”
“Ndio hivyo mume wangu”
Basi wakongea na mwishowe wakalala ila kulipokucha mapema kabisa baba Angel alijiandaa na watoto wake ili aende nao shuleni kama alivyoamuahidi mke wake kwani alitaka pia kuonana na huyo Samir.
Basi alipanda nao kwenye gari yake na kuondoka pale nyumbani wakielekea shuleni, walifika na alishughulikia maswala ya uhamisho wa Erick kisha akamuulizia Samir ili apate kumuona na kuzungumza nae,
“Samahani mwalimu, namuhitaji huyu kijana wa kuitwa Samir, yupo kidato cha nne. Nahitaji kuzungumza nae”
Basi mwalimu alienda kumuangalia na kurudi na jibu,
“Oooh kumbe hajaja shule leo”
Mwalimu mwingine akasikia na kusema,
“Huyu Samir, mama yake amepiga simu na kusema mwanae anaumwa”
Basi baba Angel alishindwa kuonana na Samir, zaidi ya kumalizia uhamisho wa Erick na kuondoka nae ili waelekee kwenye shule ambayo alipata nafasi.

Leo Angel anaangalia darasani kwa makini sana na anatamani kumuona Samir ila hakumuona maana Samir hakwenda shule siku hiyo, basi Yusra alisogea karibu na kumuuliza,
“Angel muda wote unaangaza macho kwani unamtafuta nani?”
“Nilikuwa namuangalia Samir naona leo hayupo”
“Hata Hanifa pia hayupo”
“Dah usiniambie habari za Hanifa, yani yule sio rafiki bali ni nyoka”
“Umeona eeeh! Nilikwambia mimi ukawa unakataa kuhusu Hanifa, ila hata kaka yako Junior pia hayupo”
“Ooooh, jamani watu kidato cha nne halafu hawaji shule”
“Inategemea na mapenzi yao na shule, watu wengine hawapendi shule kabisa, yani wanakuja shule tu kwasababu ila shule hawaipendi, wa kwanza wao ni Hanifa”
Kwakweli leo Angel hata hakutaka kuzungumzia habari za Hanifa kwani alihisi kumchefua kila akikumbuka ambacho alitaka kufanyiwa na mjomba wa Hanifa, basi Yusra akamwambia tena,
“Ila nahisi Samir yupo na Hanifa leo ndiomana wote hawajaja shule”
Angel aliinama chini, na Yusra alielewa kuwa ile mada imemuumiza Angel basi aliamua kumbadilishia mada na kuzungumza nae kuhusu vitu vingine.
 
SEHEMU YA 49


Leo Erica akiwa darasani kuna mgeni aliletwa pia, na yule mgeni alitambulishwa kwa jina la Elly, yani alivyoingia darasani tu moja kwa moja alienda kukaa kwenye dawati moja alilokaa Erica na wote darasani wakacheka na kupiga makofi, alivyofika pale alimwambia Erica,
“Naitwa Elly, na wewe je?”
“Naitwa Erica”
“Nafurahi kukufahamu”
“Asante”
Basi wakaendelea na masomo yao ila Elly alionekana kumuangalia sana Erica kiasi cha kumfanya Erica amuangalie kwa macho ya wizi, yani hadi wanamaliza masomo na kuondoka nyumbani bado Elly alimfata Erica na kumuaga,
“Kwaheri Erica, leo nitaenda kumwambia mama yangu kuwa kuna rafiki nimempata na nimependa sana kuwa nae karibu, najua mama yangu atafurahi sana. Yani mama yangu ana upendo sana, akikuona atakufurahia na atakuzawadia. Kwaheri Erica”
Bado Erica alimuangalia sana Elly aliyeonekana kumzoea ndani ya siku moja tu, basi Angel alifika kumchukua mdogo wake ambapo nae alimkuta bado Elly yupo, yani alimuaga Erica ila alikuwepo tu yani hata hakujishughulisha kuondoka, na alipomuona Angel alimsalimia vizuri sana,
“Kumbe Erica una dada yako, ooh dada wewe ni mzuri sana nimefurahi kukufahamu, mimi naitwa Elly”
“Na mimi naitwa Angel, ila mbona unaongea sana?”
“Ni kweli naongea sana ila mimi ni mstaarabu sana, mama huwa ananiambia kuwa nimerithi ustaarabu toka kwa baba yangu, ila mimi sijawahi kumuona baba maana alimkimbia mama kitambo sana. Nataka kupambana na maisha nije kumsaidia mama yangu, na niwe baba bora sio kama baba yangu”
“Ila si umesema baba yako ni mstaarabu sana?”
“Ndio baba yangu ni mstaarabu sana na amenirithisha mimi ustaarabu wake”
“Kheee wewe Elly unaachwa na basi la shule shauri yako, wenzio tukiachwa kuna dereva huwa anatufata”
“Mimi sipandi basi la shule, ila naenda kwetu kwa mguu tu hata sio mbali wala nini, karibuni sana nyumbani kwetu”
Basi Angel na Erica wakaondoka na kumuacha Elly ambaye aliondoka pia kurudi nyumbani kwao.
 
SEHEMU YA 50

Walivyofika nyumbani, Erick nae alikuwa amefika nyumbani basi walianza kuongea habari za Elly,
“Kwani Erica umemtoa wapi yule?”
“Dada, yule ni mgeni yani kaja leo ujue, ila namshangaa kanizoea vile”
Erick aliwapita pale kama hawaoni vile na kuelekea ndani basi Angel alicheka sana na kusema,
“Jamani mtu fidenge kahama shule lakini bado roho inamuuma loh!”
Erica hakuchangia neno kabisa, kwani alipoingia tu ndani moja kwa moja alienda chumbani kwa Erick na kuanza kuongea nae,
“Eeeeh niambie shule mpya ikoje Erick”
“Ni nzuri tu”
“Kwahiyo umeona ni vyema kuwa mbali nami jamani Erick!”
“Sijapenda kuwa mbali nawe, hujui jinsi gani naumia kukuona unaongea na wale vichaa wakina Abdi, kwakweli roho inaniuma sana”
“Kwani huwa unafikiria ni nini kaka yangu jamani!”
“Nahisi lazima watakutaka tu”
“Hapana kaka yangu, nipo makini sana”
“Una uhakika Erica hakuna atakayekuwa anakurubuni huko shuleni? Unajua mimi sipendi kuona nakukataza jambo halafu bado unalifanya, ila hivi tunacyokuwa mbali mbali inajenga kitu katika mioyo yetu yani lazima utakuwa unanikumbuka tu uwepo wangu kwako nami nitakuwa nakumbuka uwepo wako, hivyo kufanya kila mmoja wetu kujua thamani ya mwenzake”
“Ila sio vizuri kwakweli, wewe ndio ulikuwa mtetezi wangu”
“Mimi bado ni mtetezi wako, nitakuwa nakuja kukuona Erica hata usijali ila nisingeweza kwakweli kusoma shule moja na wewe na kuendelea kuona ule upuuzi wako na Abdi maana ipo siku ningepigana nae zaidi na kutoana hata ngeu. Ila kwasasa naomba uwe mkweli kwangu,chochote kitakachotokea shuleni naomba uniambie. Upo tayari kwa hilo?”
“Nipo tayari”
“Haya, nieleze leo huyo Elly ni nani na alikuwa akisema nini?”
Basi Erica alimueleza kuhusu Elly, jinsi alivyofika kwenye shule yao na jinsi alivyokuwa akiongea nae, ilionyesha kidogo Erick karidhika nay ale maelezo kwani alitabasamu na kuendelea kuwa na furaha kama siku zingine, basi Erica akaamua kwenda kuendelea na mambo mengine maana kiukweli hakupenda kumkera Erick kabisa.
Itaendelea
 
SEHEMU YA 51


Mama Angel siku ya leo aliwasiliana na mumewe na kwenda nae pamoja kwenye duka la wakina Hanifa ambapo ndio Angel alitaka kubakwa kwenye duka hilo, basi walifika ila walikuta lile duka limefungwa inaonyesha kuwa aliogopa kuwa huenda anafunguliwa kesi na ndiomana akafunga duka.
Basi wakasikitika pale kisha baba Angel akasema,
“Ngoja nimpigie mama yangu ili nijue huyu George ni kitu gani kimemsibu”
Basi akapiga simu na muda huo huo mama yake alipokea ile simu kisha akamsalimia na kuanza kuongea nae,
“Naona leo umenikumbuka”
“Mbona mimi huwa nakukumbuka kila siku mama jamani!”
“Unikumbuke wapi? Simu mpaka nipige mimi ndio kunikumbuka huko na leo sijui umelala ubavu gani hadi kuamua kunipigia”
“Aaah mama jamani, achana na hizo habari ila nilikuwa nakuuliza kuhusu George, yuko wapi siku hizi nan i kitu gani kimempata?”
“George sijui ana matatizo gani ila siku hizi ana hela si haba, halafu kuna watoto wawili na ndugu zake anawalea, ila nasikia siku hizi kawa mshirikina”
“Kheee mshirikina? Kivipi mama jamani?”
“Ndio hivyo hivyo usishangae wala nini, George ni mshirikina na anafanya vitu vya ajabu balaa halafu nasikia hataki kuoa kabisa, kwakweli simuelewi jamani”
Basi baba Angel akaagana tu na mama yake na kumtaka mkewe kuwa waondoke mahali hapa,
“Nitakuja mwenyewe ipo siku, sina hofu na ushirikina wake wala nini”
Basi wakaongozana na kurudi nyumbani tu.

Leo wakina Angel walijiandaa na kwenda shuleni kama kawaida ila baba yaao hakwenda tena bali alienda kwenye shughuli zake tu.
Walivyofika shule yani Angel kabla hajaingia darasani alishangaa Samir kumsogelea na kumkumbatia kwa nguvu, Angel akabaki kusema tu,
“Samir niachie, watu wanatuangalia”
Samir akamuachia na kucheka kisha akwambia,
“Kwani watu kitu gani wakati nakupenda sana, natamani dunia yote ijue ni jinsi gani nakupenda Angel”
Kwakweli Angel alibaki kimya tu kwani hakutegemea kwa muda huo kama angesikia maneno hayo toka kwa Samir, kisha Samir akaongea tena,
“Nimeumwa jana tu ila nimeona kama mwaka jamani, nakuwaza sana Angel, natamani muda wote nikuangalie kisura wangu”
Angel aliamua kukimbilia darasani kwani yale maneno ya Samir yalikuwa yanasisimua moyo wake na mwili wake.
Angel alikaa darasani ila aliwaza sana kuhusu Samir kwa muda huo, kiasi kwamba akisikia Samir anaitwa basi anashtuka yeye, naye Samir alikuwa akimuangalia sana Angel basi aliposhtuka kila aliposikia jina la Samir ilikuwa ni furaha sana kwa Samir kwani aliona ni jinsi Angel nae anampenda yeye.
Muda wa mapumziko, Samir alimfata Angel karibu na kumwambia,
“Angel, najua unanipenda pia usivunge”
“Samir tafadhali niache”
“Kwani nimekufanyaje Angel jamani? Unajua bado nakumbuka siku ile tulivyokiss”
Angel akainuka na kutoka kabisa mule darasani kwani alihisi kuingiwa na ushawishi.
 
SEHEMU YA 52

Muda wa kutoka darasani ulivyofika basi Angel alitoka ila nyuma alifuatwa na Samir ila hakujua kama Samir anamfata kwa nyuma, alipofika nje alimkuta mdogo wake anamsubiria ila Samir alisogea pia pale pale mbeleya mdogo wake Angel akambusu Angel na kumwambia,
“Nakupenda sana Angel”
Kwakweli Angel alijihisi kusisimka sana, hadi mdogo wake akamvuta mkono kuwa waondoke ndipo Angel aliondoka pale shuleni kwao.
Walifika nyumbani ila kuna muda Erica alikuwa akimuona dada yake anatabasamu mwenyewe, na alipofika kwao ni moja kwa moja akaenda chumbani kwake, basi Erica nae akaenda chumbani kwa mama yao kwani hakupenda kabisa kumuona yule Samir akimbusu tena Angel mbele ya macho yake.
Alimkuta mama yake akiwa amejilaza maana siku hiyo hakutoka kwenda popote, basi alimuamsha na kumsalimia kisha alianza kuongea nae,
“Mama, kuna jambo limetokea shuleni kwakweli sijalipenda hata kidogo”
“Jambo gani mwanangu?”
“Mama, yule mkaka leo kambusu tena dada halafu mbele ya macho yangu”
Mama Angel alikurupuka kutoka kitandani utafikiri kapewa habari gani maana alihisi kuchanganyikiwa baada ya kuisikia ile habari, alimuuliza tena Erica,
“Hebu nieleze vizuri mwanangu”
“Yani tulikuwa tunatoka shule, dada akaja nilipo ili tuondoke,na nyuma yake alikuja yule mkaka na kumsogelea dada halafu akambusu na kumwambia kuwa anampenda sana”
Mama Angel alipumua kwanza kwani aliona mwanae Erica anajionea mengi sana ambayo asingepaswa kuyaona kutokana na kuwa bado mdogo, akajiuliza cha kufanya ila alimshukuru mwanae kwanza na kukaa chini maana hata jibu la kufanya na Angel dhidi ya yule kijana hakuwa nalo wala nini, alijihisi kuumwa na tumbo kwakweli maana kila alipomfikiria huyo kijana alikosa jibu kabisa ila hata akashindwa kwenda kumuuliza Angel kwani alihisi kupata mawazo ya hali ya juu.
Muda huo Erica alitoka na kwenda chumbani kwa Erick ambaye naye alikuwa amerudi kutoka shule basi alimueleza jinsi dadake alivyokuwa akipewa busu na Samir,
“Eeeeh Erica, hebu nionyeshe alimbusu vipi?”
“Alimbusu mdomoni”
“Kama vipi?”
Basi Erica alimsogelea kaka yake kumuonyesha mfano wa Angel alivyofanywa na Samir, ila alijishtukia baada ya kufanya vile na haraka haraka akatoka chumbani kwa kaka yake, alimuacha Erick akiwa anacheka tu.

Angel alikaa akiwa na mawazo sana juu ya Samir, muda wote alikuwa akiwaza jinsi Samir anavyomwambiaga na jinsi alivyofanya siku hiyo, akaanza kujiambia,
“Huyu Samir itakuwa kweli ananipenda jamani, wengine wote walikuwa wakinidanganya ila huyu Samir atakuwa anamaanisha kweli”
Mara mama yake aliingia chumbani kwa Angel maana baada ya kujishauri sana aliamua kufanya hivyo, alimkuta Angel akiwa kajiinamia tu basi akamwambia,
“Mawazo juu ya Samir hayo mwanangu eeeh!”
Angel alimuangalia mama yake kwa aibu na kumsalimia pale, kisha mama yake akamwambia,
“Angel mwanangu, katika dunia hii ni mimi na baba yako ndio tunakupenda kweli na tupo tayari kwa chochote kwaajili yako ila sio huyo Samir mwanangu, atakuharibia masomo yako. Mbona umekuwa huelewi kiasi hiko lakini jamani! Unataka niongee kwa lugha gani labda ndio utaelewa? Niweke tarumbeka ndio uelewe mwanangu! Huyo Samir hakufai, kwakweli ukiendelea hivi itabidi tu nikuhamishe shule, sijali upo kidato cha ngapi ila nitakuhamisha shule”
Kisha mama Angel alitoka mule chumbani kwa Angel ila maneno yake hayakumzuia Angel kuendelea kumuwaza Samir.
 
Back
Top Bottom