Simulizi : Nguvu ya Mapenzi

Simulizi : Nguvu ya Mapenzi

SEHEMU YA 71

Mama Angel akiwa katulia alipigiwa simu na wifi yake na kuanza kuongea nae,
“Kwakweli wifi asante sana, yani jana wale wageni wmaekula na kusifia balaa yani nimepata sifa hizo mke wangu hadi balaa”
Muda huu mumewe nae alirudi kwahiyo aliongozana nae chumbani huku akiongea na ile simu,
“Kwakweli kaka muache tu achanganyikiwe juu yako”
Basi mama Angel alikuwa akicheka hadi mumewe kutaka kujua akizungumza na nani, basi mama Angel alimpa mumewe ile simu kuwa nay eye aongee nae, basi mumewe alianza kuongea nae,
“Yani Erick jana bhana, niliondoka hapo na mkeo ili anisaidie kupika, uwiii vitu alivyopika huku jamani ni Mungu pekee anajua yani wageni wangu wamejilamba haswaa”
“Oooh huyo ndio mke wangu bhana”
“Ndiomana unampenda”
“Nampenda ndio ila sio sababu ya kupika tu hapana, hiyo kupika ni ziada ila ninampenda mke wangu kwasababu zangu mwenyewe”
Basi waliongea pale na kukata ile simu kisha baba Angel alimuangalia mkewe na kumwambia,
“Na mimi nataka unipikie hiko chakula ulichopika kwa Tumaini, sio nje huko mnaenda kuwapikia mapochopocho halafu ndani unasahau maana naona toka tuje na Vaileth basi kila siku kula chakula cha Vaileth tu, nimekumbuka chakula chako mke wangu”
“Basi kesho nitapika”
Wakaongea ongea na kuamua kulala pale.

Kesho yake wakati wakina Angel wameenda shuleni, basi mama yao aliamua kubaki nyumbani na muda huo alitaka kusaga juisi.
Akaenda jikoni na kukuta kidude cha kuchomeka kwenye soketi hakipo basi alimuuliza Vaileth nae akamjibu,
“Oooh hiko nilimuona nacho Erick, nadhani alienda nacho chumbani kwake”
“Aaaah huyu mtoto nae na vidude vya umeme jamani ni hatari’
Basi alitoka pale na moja kwa moja kuelekea chumbani kwa Erick, wakati akiangaza macho yake akaona barua mezani kwa Erick basi akaenda kuichukua na kuisoma, yani alishtuka sana kuona ni barua kutoa kwa Samir kwenda kwa Angel,
“Mmmh sasa inafanya nini humu chumbani kwa Erick jamani!!”
Basi akaisoma mara mbilimbili akakuta ujumbe wa chini ukisema,
“Kesho nitakuja kwenu Angel, nitasimama pembezoni mwa ukuta wenu naomba uje tu unikumbatie yani hiyo itakuwa ni furaha yangu, nakupenda sana Angel mpenzi wangu”
Huyu mama akapumua kidogo na kusema,
“Yani hiyo kesho si ndio leo? Jamani hawa watu wanataka kunifanyeje mimi? Kwanini wananifanyia hivi!!”
Basi mama Angel alitoka nje na kukaa mitaa ile ile ya nje ya nyumba yao huku akisubiri kwa hamu kama gari itapiga honi basi atajua kuwa Angel amefika na atakimbilia nje kabisa ili Angel asiende huop upande uliotajwa na Samir, na kweli alitoka pale nje mara kadhaa bila kumuona huyo Samir kwahiyo aliamua tu kungoja pale ndani ya geti, yani hakufanya chochote tena zaidi ya kungoja Angel arudi. Ila alipoona Erica na Erick wamerudi akaona ni vyema nay eye akitoka nje kabisa.
 
SEHEMU YA 72

Wakati Angel anarudi, basi karibu na kufika kwao gari yao ilipata pancha, basi dereva akamwambia asubiri abadili tairi lingine,
“Khaa jamani huu ni ujinga sasa, nyumbani ni pale napaona halafu nisubirie uweke tairi lingine kweli!! Subiri nishuke niende nyumbani tu, wewe tengenezaga”
Basi yule dereva alibaki kupachika tairi lingine wakati Angel akishuka na kutembea kuelekea kwao, ila kabla hajasogea vizuri alishangaa akivutwa mkono na aliposhtuka aliona mkono ule kavutwa na Samir basi alimuangalia tu bila ya kusema chochote, Samir alimvuta Angel hadi pembezoni mwa ukuta wao na kumkumbatia huku akimbusu na kumwambia ni jinsi gani anampenda, muda ule ule mama Angel nae alionekana eneo lile akiwashangaa yani alijikuta akiishiwa hadi nguvu.



Basi yule dereva alibaki kupachika tairi lingine wakati Angel akishuka na kutembea kuelekea kwao, ila kabla hajasogea vizuri alishangaa akivutwa mkono na aliposhtuka aliona mkono ule kavutwa na Samir basi alimuangalia tu bila ya kusema chochote, Samir alimvuta Angel hadi pembezoni mwa ukuta wao na kumkumbatia huku akimbusu na kumwambia ni jinsi gani anampenda, muda ule ule mama Angel nae alionekana eneo lile akiwashangaa yani alijikuta akiishiwa hadi nguvu.
Ila muda ule ule anapatwa na hasira ya gafla na kujikuta akipiga kelele, ila kile kitendo kinafanya Angel na Samir wamshangae yani Samir hakukimbia wala nini hadi mlinzi wa wakina Angel alipotoka na kumkamata Samir kwani alihisi ndio tatizo, kisha mama Angel alinyamaza kupiga kelele na kumtaka mlinzi ampeleke Samir ndani, ambapo yule mlinzi alifanya kama alivyoambiwa na bosi wake.
Basi mama Angel alimvuta Angel na kuingia nae ndani kisha alimwambia,
“Yani leo utaona ambacho huwa namaanisha ni kitu gani?”
Kisha mama Angel alichukua simu na kupiga mahali, na baada ya muda walikuja askari na kumkamata Samir, kwakweli Angel aliumia sana moyo, yani kwa mara ya kwanza alijikuta moyo wake ukiwa kama na vidonda vile, alitamani kumuhoji mama yake kuwa kwanini amefanya vile ila mama yake alimfokea na kumfukuzia ndani, Angel aliingia ndani huku akilia kwakweli hadi Vaileth alimuonea huruma.
Muda huu mama Angel aliondoka na wale askari ili akamuandikie mashtaka Samir na awekwe rumande.
Basi Angel alikuwa amejifungia ndani huku akilia, Vaileth aliamua kumfata ili amnyamazishe na kuanza kuongea nae,
“Mdogo wangu, kulia hakutokusaidia kitu chochote”
“Ila Samir hana kosa jamani”
“Natambua hilo mdogo wangu, ila kuna kitu nataka nikushauri”
“Kitu gani dada?”
“Kwanini usiwasiliane na baba yako? Huwa naona ni muelewa sana, hebu mtafute hewani, nenda kampigie simu atakuelewa”
Angel nae aliona ni jambo jema kama akimwambia baba yake maana baba yake ni mtu muelewa sana, basi akatoka chumbani na kwenda kumpigia baba yake simu sebleni kwenye simu ya mezani, na kwa muda kidogo tu baba yake alipokea,
“Baba, mimi ni Angel, samahani kwa hili baba”
“Lipi hilo?”
“Baba, leo wakati natoka shule gari yetu iliharibika karibu na nyumbani basi nikashuka ila kumbe pale kwetu alikuja Samir na kunivuta mkono basi mama alikuja muda huo huo na kutuona kisha akaita askari basi Samir kakamatwa na kupelekwa polisi”
“Sasa wewe Angel unatakaje? Yani unataka mimi nifanye nini?”
“Baba, Samir hana kosa lolote”
“Ila mwenye kosa ni wewe?”
“Hata mimi sina kosa baba”
“Usinichanganye na hayo mambo yasiyoeleweka, nina kazi zangu muda huu”
Kisha baba yake alikata ile simu na kumfanya Angel alie zaidi, basi Vaileth alienda tena kumbembeleza,
“Angel jamani usilie sana”
“Baba nae hataki kunielewa, baba na mama lao moja wale, sasa kosa la Samir ni nini?”
“Kosa lake ni kuja hapa kwenu, ila wazazi wako wapo sahihi Angel, kwahiyo tuwaachie wenyewe tu wanajua cha kufanya ambacho ni sahihi zaidi”
Basi Angel alienda tena chumbani akilia, na baada ya muda Erick na Erica nao waliamka maana walikuwa wamelala kwa muda wote kwahiyo hata hawakuelewa kilichoendelea hapo kwao.
 
SEHEMU YA 73

Mama Angel akiwa anakaribia kuondoka pale polisi baada ya kuandikisha maelezo, alishangaa akipigiwa simu na mumewe na kutoka nje ili aongee nayo,
“Uko wapi muda huu mke wangu?”
“Niko hapa kituo cha polisi”
“Kipi hicho?”
“Hapa karibu na kwetu”
“Nisubirie hapo hapo nakuja”
Basi baba Angel alikata simu kwakweli mama Angel alimshangaa sana mume wake kuwa anaenda kituoni kufanya kitu gani? Basi ilibidi tu amsubirie kama alivyosema.
Baada ya muda kidogo baba Angel aliwasili na kumsogelea mke wake huku akimuuliza ni kitu gani kimempeleka polisi,
“Mume wangu, yani leo Angel na huyo Samir wake wamenishinda tabia kabisa, huwezi amini leo Samir alikuja tena nyumbani na kumkumbatia Angel, yani nilitoka na kuwaona hadi nguvu ziliniisha nikatamani hata niwameze”
“Kwahiyo uamuzi wako wa mwisho mke wangu ni kumfunga Samir?”
“Ndio ili adabu imshike”
“Basi mimi naomba mke wangu tukafute hiyo kesi na kumuachia Samir ila tutapa onyo”
“Kheee unasemaje mume wangu, yani nilipe tena hela za kufuta kesi?”
“Nitalipa mimi kwani tatizo liko wapi?”
Mama Angel alichukia sana ila hakuwa na namna zaidi ya kwenda kufuta kesi, na mumewe akalipa kila kitu halafu Samir akaachiwa, kisha baba Angel alimchukua Samir na kwenda nae pembeni kisha akamuuliza,
“Hivi kwanini umekuwa msumbufu hivyo!”
“Nisamehe mzee”
“Nisamehe yako unafikiri itasaidia kitu gani? Hivi hujihurumii kuwa bado ni mwanafunzi tena upo kwenye darasa gumu, unadhani ukifeli huyo Angel atakukubali? Sisi wenyewe hatuhitaji wanaume waliofeli katika maisha yetu, sawa kufeli kupo ila mfeli kwa bahati mbaya hata wazazi tuseme kweli juhudi zilikuwepo ila haikuwa ridhiki sio mfeli kwa makusudi, muda kama huu inatakiwa kuwa makini sana na masomo ila na ujinga wao unawaza mapenzi, unadhani huyo Angel atakusaidia nini wewe katika maisha yako? Unatakiwa upambane kama mwanaume, kwanza pambana na utafute pesa za kutosha kisha uje kwetu kumfata Angel uone kama tutakukatalia mjinga wewe, nimekuhurumia tu kuwa utaozea huko jela bila kupata msaada wowote kwa ujinga wako wa mapenzi. Haya ondoka, ila safari ijayo ukifumwa nitashughulika na wewe mimi mwenyewe na hapo ndio utanijua vizuri”
“Asante mzee wangu”
Kisha Samir akaondoka mahali pale na baba Angel alisogea kwa mama Angel na kumtaka waondoke ila mama Angel alikuwa amenuna sana, yani aliondoka na mumewe ilimradi tu ila alikuwa kanuna.
Basi wakiwa ndani ya gari akamuulza,
“Ila kwanini umeamua kumtoa Samir? Unafurahia jinsi anavyomsumbua Angel? Kwa mfano Angel angekuwa Erica ungejihisi vipi?”
“Kheee wee mwanamke hebu acha gubu, toka lini katika maisha yetu nimemtenga Angel? Toka niliposema kuwa mimi ndiye nitakuwa baba yake, lini umesikia nimemtenga? Ulipowazaa Erica na Erick je nlimtenga Angel? Alibaki kuwa ni mwanangu wa thamani sana, nampenda kuliko unavyofikiria, nampenda kuliko hata huyo babake mzazi angefanya, hebu wanawake muda mwingine muelewe mnaongea kuhusu nini sio mnavyojisikia kuropoka basi mnaropoka. Unajua ni kwanini wanawake wengi wanaachwa walee watoto wenyewe? Sababu ya midomo, yani hakuna mwanaume anayeweza kuvumilia kila siku unamsema jambo moja wakati yeye anajitahidi kulifanya sahihi, nadhani katika ulimwengu huu ni mimi tu ninayeweza kuvumilia”
Kisha akacheka ila mama Angel akamwambia,
“Naomba nisamehe kwa maneo yangu”
“Nakuelewa mke wangu, yani huwa nakuelewa kuliko unavyofikiria, nakuelewa sana tena sana, ila mke wangu jaribu kuangalia ninachokifanya, hivi mfano Erick awekwe rumande sababu ya kumfatilia mwanamke utajisikiaje?”
“Aaah Erick hawezi kufanya hivyo”
“Sawa, mfano mimi kipindi kile nakufatilia wewe ningewekwa ndani sababu ya kukufatilia unajua ningeumia sana, nilifukuzwa shule bado niliumia sana”
“Ila hawa ni wadogo sana kuanza kupendana”
“Hakuna cha udogo wala nini, nakumbuka mimi nilikupenda kwa mara ya kwanza kukuona tukiwa kidato cha pili, mbona tulikuwa wadogo sana ila nakupenda hadi leo. Ila hii sio point yangu wala nini, unachofabnya si kibaya ila jaribu kukifanya kwa nja sahihi. Kumfunga Samir hakutasaidia chochote kile, ila ni Angel kuijua thamani yake na kuithamini, unatakiwa kukaa na Angel na kumfundisha ajijue kuwa yeye ni mtu wa aina gani”
“Inamaana mimi nimeshindwa kumfundisha Angel?
“Sijasema umeshindwa, ila sidhani kama tunaelewana mke wangu naomba tuache huumjadala”
“Ila Tumaini alisema Jumatano atakuja kumchukua Angel na kwenda kuishi nae kwake hadi atakapomaliza kidato cha nne”
“Sawa hakuna tatizo”
Basi walirudi hadi nyumbani ambapo Angel alikuwa kajifungia ndani tu muda wote.
 
SEHEMU YA 74

Usiku wa siku hiyo baba na mama Angel wanaamua tu kulala bila ya kuzungumza na watoto wao maana walihisi kuwa huenda wamechoka.
Basi kulivyokucha, Erica na Erick walijiandaa na kwenda shule ila Angel siku hii hakujiandaa wala nini, ilibidi mama yake aende kumuuliza kuwa kwanini hajaenda shule, alishangaa kumkuta binti yake macho yamemvimba kwa kulia, yani mama Angel alisikitika sana na kumwambia Angel,
“Ama kwa hakika nimepata binti mjinga sana na asiyejielewa hata kidogo halafu wewe ndio mtoto wangu wa kwanza, hivi Angel unafundisha nini wadogo zako? Unataka nao wawe wasumbufu kama wewe? Kwanini Angel kunitenda hivi mama yako jamani? Mbona mtoto huna huruma wewe loh!!”
“Mama, wewe ndio huna huruma sasa mimi nina raha gani hapa nilipo ikiwa Samir amelala ndani”
“Jamani Angel kalala ndani kivipi? Mbona baba yako alimtoa tayari, hata kama angelala ndani ndio sababu ya wewe kulia hadi kuvimba macho, kwahiyo unampenda Samir kuliko sisi wazazi wako?”
Angel alikaa kimya, kisha mama yake akaenda kuchukua ile simu aliyokuwa anatumia na kumwambia,
“Haya mpigie Samir hapo akwambie kama yupo rumande au yuko wapi”
Basi Angel alichukua ile simu na kumpigia kweli Samir ambapo baada ya muda mfupi Samir alipokea ile simu,
“Oooh siamini, leo Angel umenipigia”
“Uko wapi Samir?”
“Nipo shule”
Muda huo huo Angel alisikia sauti upande wa pili ikisema,
“Yani Samir, wenzio wapo darasani na wewe upon je unaongea na simu!! Leo ni mara ya tatu nakufuma, twende ofisini sasa”
Kisha ile simu ilikatika, inaonyesha ni mwalimu alimbamba Samir akiongea na simu, basi Angel pia alishusha ile simu na kumkabidhi mama yake kisha mama yake akamwambia,
“Umeamini sasa kuwa Samir alitolewa? Basi jiandae maana kesho shangazi yako mama Leah anakuja kukuchukua, kwahiyo jiandae ila nitaongea nae aje akuchukue leo tu ili kesho utokee kule kwenda shuleni”
“Nimeamini mama, ila huko kwa shangazi naenda kutembea tu au?”
“Unaenda kuishi huko hadi umalize kidato cha nne yani ni mimi na nduguzo ndio tutakuwa tunakuja kuwaona, ila mara kwa mara nitakuwa nawasiliana na shangazi yako”
Halafu mama yake alitoka kule chumbani, basi Angel akawa akijitafakari haswaaa maneno ya mwalimu kuwa ile ilikuwa ni mara ya tatu kumbamba Samir akiongea na simu, basi akajiuliza,
“Je mara zote hizo huwa anaongea na nani?”
Akakosa jibu na kuamua kwenda kuoga ili kupata nguvu ya kupanga nguo zake kama alivyoambiwa na mama yake.
 
SEHEMU YA 75

Samir alipelekwa ofisini na mwalimu wa nidhamu na kuanza kuongea nae kwanza,
“Unajua Samir kutenda kosa si kosa bali kurudia kosa, nilikuhurumia sana mwanzoni kuwa mtoto huyu itakuwa kakosea, Samir nilimfuma Angel akiwa anatumiana na mtu ujumbe darasani, na ukaja mwenyewe kusema kuwa anawasiliana na wewe, nikakupa onyo, ile ilikuwa mara ya kwanza, mara ya pili nilikukuta ukiongea na simu na nilipokubana ulisema ulikuwa unawasiliana na mamako ana matatizo, nikakusamehe ila nikwambia isijirudie tena na nikakwambia kuwa simu haziruhusiwi shuleni, acha simu yako nyumbani kwenu. Ulinikubalia na uliandika barua ya maelezo, haya na leo tena na kufuma na kosa lile lile, kwakweli sitasikiliza mjadala, sijali kuwa hili ni darasa gumu wala nini bali nakuandikia barua ya kusimamishwa shule”
“Jamani mwalimu!!”
“Hakuna cha jamani, unatakiwa kuzingatia masomo sio kuleta mambo ya kijinga shuleni, yani kaa ukijua muda huu ndio siku yako ya mwisho kuonekana hapa shuleni”
Basi Samir alijitahidi kumbembeleza mwalimu ila alishindwa kwani yule mwalimu hakukubali wala nini kwahiyo ilibidi Samir akachukue begi lake na aende kuchukua barua yake na kurudi nyumbani tu.
Muda Samir anaondoka, Erica nae alikuwa akienda chooni kwahiyo Samir alikutana nae na kumwambia Erica,
“Mwambie Angel kuwa nimefukuzwa shule, ila siku zote nitampenda hadi mwisho wa maisha yangu, hata nisipomuona nitaendelea kumpenda tu. Mwambie kuwa nampenda sana”
Basi Erica alimuangalia huyu Samir na kumuitikia tu bila ya kusema kitu kingine chochote kile, basi Samir akamuaga na kuondoka zake.

Mama Angel anawasiliana na wifi yake kuwa aende kumchukua Angel siku hiyo hiyo kwani hakutaka aendelee kukaa hapo nyumbani, ukizingatia alishaona jinsi binti yake alivyoathiriwa na mawazo juu ya Samir.
“Wifi naomba uje leo kumchukua Angel, nishamwambia ajiandae”
“Oooh sawa, halafu nilikuwa na safari ya kuja huko huko, ila siji na gari”
“Hakuna shida, dereva atawapeleka maana ndio atakuwa anakuja kumchukua Angel na kumpeleka shuleni”
“Sawa, hakuna tatizo”
Basi mama Angel aliona ni afadhari iwe vile maana hakutaka matatizo tena na Angel, na alijua kwamba Angel akienda kwa shangazi yake basi ataepuka vitu vingi sana vya kuhusu Samir.
Baada ya muda kidogo wifi wa mama Angel aliwasili na kuanza kuzumza nae,
“Eeeeh huyo Angel kashajiandaa lakini?”
“Kashajiandaa ndio”
“Basi hakuna tatizo, leo kuna mahali nilikuwa naenda jioni ndiomana nikakwambia nimpitia kabisa saa hizi, vipi mbona hajaenda shule”
“Mmmh alichelewa kuamka”
“Jamani Angel nae loh! Kwangu atakuwa anwahi huyu vizuri tu”
Hakutaka kumueleza wifi yake kuhusu yaliyotukia jana, ila aliacha kama kujishuhudia basi akajishuhudie mwenyewe huko huko.
Basi mama Angel alienda tu kumshtua Angel ilia toke ndani na aondoke na shangazi yake ambapo alifanya hivyo na kutoka na begi lake la madaftari pamoja na begi lake dogo la nguo zake. Kisha akamsalimia shangazi yake pale na kumwambia mama yake,
“Mama, mimi nabeba hizi nguo kidogo tu zibebi nyingi”
Shangazi yake akasema,
“Ubebe nyingi za nini? Hizo hizo kidogo zinakutosha maana zitafanya uwe makini zaidi”
Basi mama yake alipiga simu kwa dereva wao ambaye alifika kuwachukua, pia alimpa maagizo kuwa toka siku hiyo atakuwa akimfata Angel huko kwenda shuleni na atakuwa akimrudisha huko huko, basi yule dereva alikubali na kuondoka nao.
 
SEHEMU YA 76

Wakina Erica walirudi shuleni, basi kwavile Erica alikuwa na ujumbe kwa dada yake akamsubiri arudi ndio amwambie maana yeye alijua kuwa dada yao kaanda shuleni, ila alishangaa kuona hadi giza linaingia bila dada yao kurudi nyumbani, ikabidi akamuulize dada yao wa kazi vaileth,
“Eti dada samahani, dada Angel mbona leo kachelewa kurudi shule?”
“Sio kachelewa ila hayupo”
“Khee hayupo? Kivipi?”
“Kaja hapa shangazi yenu kumchukua, kwahiyo ameenda kuishi kwa shangazi yenu!”
“Jamani!!”
Erica akasononeka, basi Vaileth akawahadithia kisa cha jana yake na hapo kumfanya Erica aelewe kuwa ile barua ilibambwa na mama yao, ila moja kwa moja alihisi mtu mbaya ni Erick tu kwenda kupeleka barua kwa mama yao, basi akamfata Erick chumbani, alipofika alifungua tu mlango na kumkuta Erick ametoka kuoga yani ndio kalifungua taulo ili avae nguo, basi Erica alishtuka sana ambapo Erick nae alijifunga na taulo kisha akamkaribisha dadake ambaye alikuwa ameduwaa pale mlangoni,
“Kilichokufanya ushangae hivyo ni nini?”
“Kumbe Erick ndio upo hivyo!!!”
“Wewe nawe, si nimekuwa unadhani nitaendelea kuwa vile vile kama zamani! Hujioni wewe umetokwa na maziwa kifuani mbona mimi sisemi kitu!”
“kheee nisamehe basi”
“Mi nilishakusamehe ila sidhani kama ni vibaya kwa pacha wako kukuona ulivyo, angeniona mtu mwingine ingekuwa vibaya ila kwa pacha wangu sio vibaya”
“Haya, tuachane na hayo. Eeeh ile barua ya da Angel aliyoandikiwa na Samir ulisema utaificha imekuwaje imemfikia mama?”
Ndipo Erick akakumbuka sasa sehemu aliyoweka hiyo barua, basi akaanza kuangalia bila kuikuta na kusema,
“Oooh kumbe niliiacha mezani, mmmh inamaana mama aliingia humu chumbani!”
“Yani na wewe ukaweka mezani kweli! Unasahau kama mama huwa naingia kwenye vyumba vyetu kama chumbani kwake, na anapekua atakacho, basi ndio mama imemfikia hivyo”
“Wewe umejuaje?”
Akamsimulia jinsi ambavyo alisimuliwa na Vaileth kuhusu yaliyotokea jana,
“Khee tulikuwa wapi kwani? Mbona hatujasikia hayo?”
“Nadhani ni muda ambao tulikuwa tumelala, mfano mimi jana nilichoka sana jamani”
“Hata mimi jana nilichoka sana, ila ndio inavyokuwaga Jumatatu. Pole kwa dada Angel jamani maana nahisi aliambulia kipigo tena”
“Hapana, angepigwa basi tungesikia tu. Ila mama kachukia hadi leo da Angel kapelekwa kwa shangazi ujue”
Erick akashangaa na kutaka kuelezwa zaidi basi Erica alimueleza vile ambavyo alielezwa na Vaileth, kwakweli Erick alisikitika sana kwa dada yake kuondolewa sabau ya uzembe wao.
Kisha alimuuliza jambo Erica,
‘Vipi Elly hajambo?”
Erica alicheka na kumwambia kaka yake,
“Maajabu, leo umemkumbuka Elly?”
“Nimemkumbuka ndio, sababu leo hujaleta swaga zako za kusema Elly kafanya hiki mara kafanya kile ndiomana nimekuuliza”
“Mmmh leo hajaja shule ujue”
“Khee anaumwa?”
“Sijui, ila kesho nitajua”
“Basi utampa pole”
Erica alitoka chumbani kwa kaka yake ila alishangaa sana kwa kaka yake kumuulizia Elly wakati huwa hathubutu kabisa kumuulizia Abdi, ila Elly alimuulizia na kusema mpe pole kama anaumwa, kwakweli Erica alishangaa sana ila aliondoka tu kuelekea chumbani kwake.
 
SEHEMU YA 77

Tumaini akiwa na Angel nyumbani kwake, anaanza kumpa Angel masharti ya nyumba yake hiyo, na kipi hataki kitokee au kitendeke kwenye nyumba yake,
“Angel mwanangu, karibu kwenye himaya yangu, nyumba hii mwanangu ina masharti yake. Upo tayari uyasikiliza”
“Nipo tayari shangazi”
“Haya, humu ndani kila siku ina kitu chake cha kufanya, kwanza kuna muda wa kuamka, kuna muda wa kulala, kuna muda wa kujisomea, kuna muda wa kuangalia Tv, kuna muda wa kucheza na kuna muda wa kula. Kwa kifupi kila kitu kinafanywa kutokana na ratiba ya humu ndani, ila kutoka Jumatatu hadi Ijumaa hakuna mtoto au mwanafunzi yoyote anayeruhusiwa kuangalia Tv kwa muda wowote, yani muda wa kuangalia Tv upo Jumamosi na Jumapili ingawa hapo kuna muda wake pia kwani sio siku nzima unatumbulia macho Tv. Hiyo ni sheria namba moja, huwa sina kawaida ya kutuma watoto dukani ila huwa ikitokea nataka uende moja kwa moja ninapokutuma na kurudi nyumbani ni hivyo hivyo kama una kitu unahitaji kununua, hata hivyo huwa napenda niandikiwe mahitaji yote ili niyanunue na yawepo nyumbani. Hapa kutoka haitakiwi izidi saa kumi na mbili yani saa kumi na mbili jioni inavyogonga basi hairuhusiwi kutoka hata nje ya geti langu lile, naonekana mkali sana ila nalinda uzao wangu maana watoto wangu wote ni wakike, nikicheza basi nimewapoteza. Umenielewa Angel”
“Nimekuelewa shangazi”
“Ukitoka shule ni nyumbani na ukifika nyumbani hakuna kutoka tena, utafata ratiba tu inasemaje kwa muda huo hadi pale unapoenda kulala, ujinga nyumbani kwangu sitaki, sijui kusikia mambo uliyokuwa ukiyafanya kwenu kuyaleta hapa sitaki. Mimi ni shangazi yako kwahiyo kuwa makini sana na mimi na uniheshimu”
“Sawa shangazi”
“Haya, twende nikakuonyeshe chumbani”
Basi Angel alipelekwa hadi chumbani na kuweka begi lake na muda huo huo aliambiwa asome ratiba ya siku hiyo inasemaje, yani ratiba ilikuwa imebandikwa nyuma ya mlango wa kile chumba, kwakweli Angel alihisi kama yupo kwenye kifungo vile ila ilibidi tu akubaliane na hali halisi na kufanya vile ambavyo ratiba ya kile chumba ilisema.
Watoto wa shangazi yake waliporudi kutoka shule wala hawakuonekana kuwa na hofu na ile ratiba kwani waliizoea tu, basi walimsalimia dada yao pale na kuanza kuvua sare zao za shule, basi Angel akaenda kwa shangazi yake na kumwambia,
“Sasa shangazi, mimi nitalaleje na watoto ndani?”
“Ndio ujinga ambao mama yako kakufundisha, ndiomana unafanya vitu kinyemela. Sawa sio taizo, nakuhamisha chumba ila kuwa makini sana”
Basi Tumaini akaenda kumuonyesha Angel chumba kingine cha kulala ambacho katika nyumba yake huwa ni chumba cha kulala wageni, ila aliona kwa kipindi hiko kitamfaa Angel, kisha akamwambia Angel,
“Ila nilikuwa nakujaribisha u mule kuwa utasemaje, haa hukujiuliza kuwa kule ungelalaje? Na ungelala wapi? Nilikuwa nakujaribu tu mule, ila chumba chako kitakuwa ni hiki ila napo nitakuja kukubandikia ratiba nzima ya kuishi humu ndani”
“Sawa shangazi”
Basi Angel akaweka tena vitu vyake vizuri huku akitaakari yale yaliyopo.
 
SEHEMU YA 78

Kulipokucha Angel alijiandaa kwenda shuleni na alienda shuleni kama kawaida na kukua mama yake kumbe alishaoa maelezo ya kwanini jana yake hakufika shuleni basi wote walibaki kumpa pole maana alisema kuwa anaumwa.
Basi alishiriki vizuri kabisa kwenye masomo na alipenda wanafunzi wa shule ile jinsi walivyokuwa na ushirikiano kwani waliweza kumuelekeza kila kitu ambacho kilifundishwa siku ya jana ambayo hakufika shuleni. Kuna mdada alimzoea kidogo kwahiyo akawa kama rafiki yake hapo shuleni, aliiwa Husna, aliipenda sana tabia yake kwani alionekana kupenda kusema ukweli muda wote, basi siku hiyo muda wa mapumziko akawa anaongea nae,
“Kwakweli Angel wewe ni mzuri sijui kama unatambua hilo!”
Angel alikuwa akicheka tu, kisha Husna alimwambia jambo lingine,
“Ila uzuri unakamilika ukiwa na akili timamu, wazungu wansema beut with brain, kwahiyo unatakiwa uwe mzuri na uwe na akili ili uzuri wako uthaminike”
“Akili ya kufanyeje?”
“Aili ya kuitambua thamani yako, mama yangu huwa ananifundisha jambo moja sana kuwa mimi ni wa thamani sana, natakiwa muda wote nitambue thamani yangu, nisikubali kitu chochote kuvuruga thamani niliyokuwa nayo. Siku tukipata muda vizuri nitakuelekeza mambo mengi Angel, ia kiukweli nimekupenda bure, maana wewe ni mzuri halafu muelewa, halafu una akili, nimekupenda bure kwakweli”
Basi Angel alifurahi sana kusikia vile na kumfanya aishie kutabasamu tu.
Muda wa masomo uliisha na kurudi nyumbani kwa shangazi yake bila tatizo lolote, na alikuwa akienda shuleni kwa muda na kurudi muda unaotakiwa hadi shangazi alihisi kuna mambo Angel alikuwa akisingiziwa.

Ilikuwa siku ya Ijumaa ambapo kama kawaida, Angel alienda shule na kama kawaida ile asubuhi kabisa waliwahi darasani na kufanya jaribio la siku maana katika ile shulle ilikuwa kila siku kuna jaribio asubuhi, kwahiyo aliwahi na kufanya vizuri kabisa.
Kwenye mida ya saa mbili na nusu asubuhi wakiwa wametulia darasani wakijisomea, mara aliingia mwalimu na mwanafunzi mgeni ila hakutaka wainuke kumsalimia ili asiharibu umakini wao na muda huo Angel ndio alikuwa makini na kitabu chake akisoma tu, basi mwalimu alitangaza,
“Jamani tumepata mwanafunzi mgeni, kwahiyo nahitaji ushirikiano wenu mwema kwake. Anaitwa Samir”
Angel alihisi moyo wake ukifanya paaa, na kuinua sura yake, kwakweli hakuamini kwani macho yake yaligongana na macho ya Samir kwa muda huo.
 
SEHEMU YA 79


Walijikuta wakiangaliana kwa muda kidogo kisha kila mmoja kuendelea na mambo yake ambapo Samir alikaribishwa vizuri na kiongozi wa

darasa na kuonyeshwa sehemu ya kukaa na kuendelea na masomo.
Ila leo Samir hakumfata Angel wala nini yani ilikuwa kama vile yeye na Angel ni watu wasiofahamiana kabisa, muda kidogo Samir alikuja

kuitwa na mwalimu ambapo mama yake mzazi alikuwa amekuja tena pale shuleni, ingawa ni yeye alimtafutia Samir hiyo shule ila aliamua

kurudi tena kuongea nae, basi wakaingia ofisini na kuanza kuongea na Samir ambapo mama yake alianza kumwambia,
“Naona nyumbani nimeshasema sana hadi pumu imenishika, leo nimekuleta hapa shuleni, huwezi amini nimeenda hadi stendi ya daladala

ila sijapata hamu ya kupanda gari nimeamua kuja tu kuongea na wewe, si unajua mume wangu ana usafiri lakini leo alifungia magari yote

maana hataki kusikia huu ujinga wako. Jamani Samir, leo naongea na wewe kwenye hii ofisi kwa mara ya mwisho, naongea kama mama

mwenye uchungu na mtoto wake, Samir tafadhari sitaki ujinga, yani sitaki ujinga kabisa yani kile leo nakuhamisha shule sababu ya ujinga

wako, ile shule ya kwanza ulimshika mwalimu makalio ukafukuzwa, shule ya pili ulimpiga mwanafunzi mwenzio ukafukuzwa, sasa shule ile

ya tatu umeanza kuongea na simu shuleni jamani na skendo za mapenzi zimekufukuzisha, hivi Samir akili yako ikoje? Nani aliyekuroga?

Hebu soma mwanangu, upate kazi nzuri uone kama kuna mwanamke yoyote wa kukukataa wewe Kwakweli Samir ukifanya ujinga wako na

shule hii ujue sina dhamana na wewe, yani ufukuzwe shule basi tutabaki nyumbani tukiangaliana, ujinga sitaki jamani!”
“Sawa mama, nimekuelewa na haita jirudia tena”
“Haya nipe simu yako, yani umefanya kila mtu anitukane kuwa sina malezi bora kwako hata mume wangu kanitukana mjinga wewe

umeniletea balaa tu katika maisha yangu”
Basi Samir akaitoa simu aliyokuwa ameiweka kwenye mfuko wa suruali yake, kisha kumkabidhi mama yake ambaye aliichukua na kuiweka

kwenye mkoba wake kisha Samir akaambiwa arudi darasani, kisha walimu wakaanza kumsema mama Samir,
“Ila na wewe una makosa, utamuachaje mtoto anakuja shuleni na simu? Yani sisi tungemkamata nayo u basi tusingejari ni hela ngapi

umetoa zaidi zaidi tungemfukuza shule, inaonyesha kijana wako ni kiburi sana”
“Jamani walimu naomba mnisaidie tafadhari, naomba mnisaidie, natambua kuwa nyie pia ni walezi naomba mnisaidie yani huyu mtoto

anafanya niumwe kichwa kila kukicha jamani, naomba mnisaidie walimu. Muwe nae karibu tafadhari”
Akajitokeza mwalimu mmoja na kusema,
“Usijali mama Samir, mimi nitakuwa na huyu bega kwa bega”
“Asante sana mwanamke mwenzangu, Napata shida mimi”
“Basi usijali, yani mimi ndiye mwalimu ninayeogopewa na wanafunzi wote hapa shuleni, kwahiyo usijali wala nini”
“Asante sana”
Basi mama Samir aliaga wale walimu na kuondoka zake.

Muda wa kukaribia kutoka, mwalimu ambaye alijulikana shuleni kwa jina la madam Hawa, alimuita Samir na kuanza kuongea nae,
“Sasa Samir, mimi ndio nimeachiwa wewe hapa shuleni nikuangalie na kukulea, nasikia kichwa chako hiko ni kitupu basi mimi nitakijaza maji

na mchanga ili upande uwa kichwani. Sikia nikwambie kitu, unapokuja shuleni unatakiwa uje kuniona mimi na unapoondoka shuleni

unatakiwa kuja kuniona mimi pia. Hilo sio ombi bali ni amri, sijui tumeelewana”
“Nimekuelewa ndio”
“Haya unaweza kwenda sasa”
Katika shule hii hapakuwa na usafiri kama shule zingine, kwahiyo wanafunzi waliondoka na kwenda kupanda madaladdala kurudi nyumbani

kwao niomana hata Angel alikuwa akipelekwa na dereva na kufatwa na dereva, mama Angel hakupata nafasi ya kumpeleka Angel kwenye

shule atakazo kwahiyo ilibii ampeleke kwenye hiyo shule kwani alisikia nayo inafundisha vizuri.
Basi Samir aliondoka ili kurudi kwao ila aliongozana na yule kiranja wa darasa ambaye alimkaribisha na alikuwa akiitwa Adam basi alianza

kuongea nae,
“Naona madam Hawa alikuita?”
“Ndio, alikuwa akinipiga mikwara yake”
“Ana mikwara yule madam hatari sababu anajua wanafunzi wengi tuna muogopa, ila yule madam tatizo lake hana mume”
“Kheee kwanini?”
“Sijui alitendwa huko anajua mwenyewe, yani madam ana hasira yule sijapata kuona, ukimsogelea tu utashangaa umenaswa kofi, sasa

kama kashakupiga mikwara basi ujipange ndugu yangu”
“Aaaah sawa, nimekuelewa”
Basi waliongozana na kuongea hadi stendi ya daladala na kila mmoja alipanda daladala ya kuelekea nyumbani kwao.
 
SEHEMU YA 80


Leo baba Angel alirudi mapema nyumbani kwake na alimuita mkewe chumbani ili kuzungumza nae mawili matatu,
“Mke wangu jamani nataka watoto”
“Kheee bado una mambo hay ohayo jamani!”
“Ndio, furaha ya ndoa ni watoto. Kwa mama yangu nimezaliwa peke yangu, na kwa baba yangu tumezaliwa waaili tu kama jicho, kwakweli

nahitaji kupata watoto ili tufurahi pamoja na familia iwe kubwa mahali hapa”
“Sawa, mfano je nikiwa sina uwezo tena wa kushika mimba?”
“Ukiwa huna uwezo wa kushika mimba hiyo inajulikana mke wangu na wala sio sababu ya mimi kuchukia ila mke wangu najua uwezo huo

unao sema unatumia zile njia zenu za uzazi wa mpango, mke wangu ulipozaa tu watoto wetu mapacha ukaweka kitanzi, nikatulia tuli miaka

kumi na mbili ikapita na wala huna mashaka wala wasiwasi wowote kuwa nimzalie tena mume wangu, zaidi zaidi kumsema dada yangu

kuwa kazaa kama panya, sawa kazaa kama panya ila ni furaha kubwa kwa mumewe ambaye ni kaka yako, tunawasema sasa ila badae

tutawafurahia. Mke wangu mambo ya kitanzi sijui ndio ukayachoka, umeenda kuweka kijiti kweli jamani ni haki hiyo? Halafu unasema kama

huna uwezo wa kushika mimba je wakati uwezo huo unao jamani mke wangu, mimi nataka watoto”
“Jamani Erick, mimi nimechoka kulea mimba”
“Kwani hiyo mimba utailea mwenyewe? Si tutakuwa sote katika kulea? Na safari hii nakwambia nitakuwa nawe bega kwa bega, nakupenda

sana mke wangu kwakweli nahitaji mtoto. Kama kuna kitu nilikukosea kwenye mimba ile ya mapacha naomba unisamehe”
“Unadhani nasahau uliyoyafanya kipindi nakaribia kujifungua? Ndiomana sina hamu hata ya kubeba mimba”
“Naomba unisamehe mke wangu na hayo yapite, haitojirudia tena”
Baba Angel alipiga na magoti kabisa, ilionyesha ni kwa jinsi gani alikuwa na uhitaji wa watoto wengine toka kwa mke wake, basi mama

Angel alimjibu kuwa amaemuelewa.
“Sawa nimekuelewa”
“Eeeh na ile ahadi ya kunipikia kile chakula kizuri imekuwaje? Maana tatizo lako mke wangu muda wote kuchunga watoto hata unasahau

kuhusu mumeo”
“Nisamehe kwa hilo mume wangu, ngoja nikakuandalie leo”
Basi aliinuka na kumuacha mumewe chumbani kisha alienda kumuandalia chakula anachokitaka.

Angel alirudi kwa shangazi yake, na aliporudi tu shangazi yake alimuita na kumuuliza,
“Ni kitu gani kimetokea leo shuleni?”
“Jamani shangazi hata salamu!! Shikamoo”
“Marahaba, nasikia kuna mkaka aliingia darasani kwenu mkaangaliana sana”
Angel alishangaa kuwa shangazi yake amejuaje tukio lile, basi alinyamaza kimya tu kisha shangazi yake akaendelea,
“Angel, kuwa makini na masomo yako, mama na baba yako sio wajinga kuhangaika na wewe kila siku yani kila siku wimbo ni Angel tu

kwakweli tumechoka, kuwa makini na masomo na sitaki kusikia habari za wewe kumuangalia tena kijana hivyo”
Basi Angel alienda chumbani ila alikuwa na maswali mengi sana kuwa kwanini shangazi yake ameelewa kile kilichotokea shuleni kwa siku

hiyo? Ila hakuwa na jibu wala nini zaidi ya kuamua kwenda ndani na kufanya mambo kama ratiba inavyosema.
Kulipokucha alijiandaa na kwenda shuleni kama kawaida ila leo Husna alimwambia jambo lingine,
“Unajua Angel unapitwa na vitu vingi kwa unavyoletwa na gari na kufatwa na gari? Utajifunza lini jinsi jamii ilivyo?”
“Sasa mimi nifanyeje unadhani?”
“Ongea na kwenu wapunguze gharama za wewe kufatwa na gari kila siku, bora kuletwa tu ili usichelewe shule ila kufatwa na gari jamani

mambo mengi sana unayakosa Angel”
“Mmmh nitafikiria uyasemayo”
Basi waliendelea na masomo ila Angel alijikuta akimuangalia Samir kwa macho ya wizi ila hata Samir nae alionekana akimuangalia Angel

kwa macho ya wizi kiasi kwamba kila muda walijikuta wakigongana macho yao na kushusha sura zao chini.
Muda kidogo aliingia madam Hawa na kumuita Samir ambaye aliinuka na kumfata madam Hawa.
Kiukweli Angel hakupenda ile hali ila ilibidi atulie tu kwani alikumbuka maneno ya shangazi yake kuhusu kutulia na kuangalia maisha yake.

Ila muda ule ule Husna alimuuliza tena Angel,
“Mbona kama umeshtuka kwa mwalimu Hawa kumuita Samir? Unafahamiana na Samir”
“Mmmh hapana, sifahamiani nae. Halafu sijashtuka hicho bali nilikuwa na mawazo yang utu”
“Aaah nilijua labda unafahamiana nae”
“Hapana simfahamu”
Angel aliona ni vyema kwake kukataa kuhusu kufahamiana na Samir ili abaki kuwa huru katika fikra zake.
 
SEHEMU YA 81


Muda wa kutoka kama kawaida, dereva alifika kumchukua na kumrudisha kwa shangazi yake na alivyofika tu kama kawaida shangazi nae

alianza kumuuliza za shule, naye alimjibu vyema tu kisha shangazi yake akamwambia,
“Leo nimefurahi maana sijasikia chochote kibaya kuhusu wewe, ila ngoja nikwambie jambo moja kwenye nyumba hii kufaulu ni lazima na sio

hiyari, yani lazima ufaulu mitihani yako”
“Nakuhakikishia nitafaulu shangazi, si unaona hata mitihani ya kawaida ninavyofanya!”
“Nimeona ndio”
Basi Angel alienda ndani ila kiukweli ratiba ya hapa kwa shangazi yake ilikuwa ikimchosha, maana hakuna ratiba kusema atapika, kufua au

kuosha vyombo, ila tu huwa anakuta sare zimefuliwa na msichana wa kazi, chakula kimepikwa na vyombo vimeoshwa. Kwavile hakupenda

aina ile ya maisha aliamua kwenda kuongea na shangazi yake,
“Shangazi nina ombi moja”
“Niambie ni ombi gani?”
“Shangazi, unajua mimi na wakina Leah tupo tofauti sana, mimi ni mkubwa na wakina Leah ni wadogo kwahiyo si vizuri ratiba yangu iwe

sawa na wakina Leah. Shangazi, kwenye ratiba yangu hakuna kupika, kufua wala kuosha vyombo na hizo ndio kazi za kike shangazi, sasa

mimi nitakuwa nakaa tu kila siku bila kufanya kazi yoyote?”
“Ndiomaana nina wafanyakazi wawili, mwingine anakuja kila siku na mwingine analala hapa hapa”
“Hata kama shangazi, ila kuna ulazima wa mimi kuwasaidia kazi au la punguza mfanyakazi mmoja. Jamani pale kwetu mama kaweka

mfanyakazi hivi karibuni ila tumekuwa pale bila mfanyakazi yoyote yule, shangazi tafadhari naomba hata kwa Jumamosi tu raiba yangu

isome kupika au kuosha vyombo au kufua tafadhari”
“Sawa nitafikiria na hilo, kuna lingine?”
“Ndio shangazi, ningeomba huyu dereva anayenipeleka, mpunguze gharama kidogo yani asiwe anakuja kunichukua shuleni”
“Kheee wee mtoto una wazimu eeeh! Hakuna kitu kama hiko, hebu sahau kuhusu hilo”
Basi Angel akainuka tu na kuondoka wala hakuongea kingine chochote na shangazi yake.
 
SEHEMU YA 82

Erica akiwa getini kutoka shuleni, alishtuka kuona mtu kamziba macho kwa nyuma, basi akaanza kukisia,
“Nani wewe jamani, ila vidole vyako ni vya Erick”
Alikuwa akimpapasa mikono ili akisie ni nani, basi Erick alimuachia huku akicheka sana na kusema,
“Kweli unanijua, hadi vidole Erica wangu jamani”
Erica nae akacheka na kusema,
“Yani mchezo huo anao Elly shuleni, sasa kumbe na wewe unao”
“Hivi Elly nani? Mbona vitu vingi vyangu unasema ni kama vya Elly?”
“Elly nae ni kaka yangu, wewe si uliondoka kunilinda hukutaka tena, basi akapatikana Elly”
Wakaingia ndani huku wakiongea ongea, ila Vaileth aliwauliza,
“Jamani nyie mnasoma shule tofauti ila kila siku mnarudi pamoja, huwa mnaambizana au inakuwaje?”
Erick akajibu,
“Hii inatokea tu wala huwa hatuambizani”
“Oooh ni sababu nyie ni mapacha eeeh!”
Wote wakacheka na kila mmoja kwenda chumbani kwake kwaajili ya kubadili sare za shule.
Leo walipotoka kubadili sare zao walirudi sebleni na kuanza kuangalia Tv, yani hadi muda mama yao anarudi aliwakuta sebleni wakiangalia

Tv, basi alikaa chini na kusema,
“Haya ndio malezi ambayo wifi yangu hayataki kwakweli, hivi Erica na Erick huwa hamna homework? Huwa hamna vitu vya kujisomea kweli?

Kile chumba cha kujisomea niliweka cha nini jamani! Haya sitaki kuwaona hapa, muende mkajisomee”
Basi Erica na Erick waliondoka zao na kuelekea kwenye vymba vyao, hata hawakuelekea kwenye chumba cha kujisomea.
Muda kidogo baba Angel nae alirudi ikabidi mama Angel aende na mumewe chumbani basi walisalimiana pale na kuanza kuongea ya hapa

na pale ambapo baba Angel alimuuliza,
“Leo usiku tunakula chakula gani?”
“Mmmh hata sijaangalia, ngoja nikamuulize dada”
“Oooh huyu sio mke wangu jamani”
“Kwanini?”
“Unajua sijakuzoea hivi kabisa! Chakula ukamuulize dada kweli jamani! Nahitaji uniandalie wewe chakula”
“Umeanza sasa, ndio unataka nibebe na mimba jamani, hiyo mimba nitaibeba mgongoni au? Ili nibebe na niwe nakuandalia chakula”
“Mbona kipindi una mimba tulikuwa tunapika wote na kula wote, itakuwaje kwasasa nishindwe!”
“Halafu mambo ya biashara kule yananitinga mume wangu, kwahiyo narudi nimechoka”
“Jamani, jamani kwani huwa nasemaje mimi!! Sawa tuache hayo, ila kwa leo sili chakula kilichoandaliwa na Vaileth, nataka uniandalie wewe”
Mama Angel alitoka chumbani akiwa amechukia kiasi ila hakuwa na namna zaidi ya kwenda kumuandalia mumewe chakula, aliona kama

anampa adhabu vile, akajiuliza kuwa labda kwavile hajabeba mimba maana alishindwa kumuelewa mumewe kuwa analengo gani naye

mpaka amwambie kwenda kumpikia kwa muda huo.
Basi alipomaliza alimuandalia mumewe na kumkaribisha chakula, basi mumewe alifurahi sana na kusema,
“Huyu sasa ndio mke niliyemuoa”
Akatabasamu na kukaa pamoja na mumewe wakila kile chakula, kwakweli hata Vaileth alijikuta akitamani sana maisha ambayo baba Angel

na mama Angel walikuwa wakiyaishi, hata alijiuliza kama huwa wanagombana kwa jinsi walivyokuwa wakila kwa pamoja na kutabasamu

pale mezani.
Muda huo Erica na Erick pamoja na dada yao walikuwa wameshakula kwahiyo walikaa sebleni huku wakiongea kwa chini chini ambapo

Vaileth ndio aliyaanzisha maongezi yale,
“Wazazi wenu wanaonyesha kupendana sana, hivi wamewahi kugombana?”
“Mmmh hapana, hatujawahi kusikia wakigombana”
Kisha Erica na Erick waliinuka na kwenda chumbani ambapo nao wazazi wao walimaliza kula na waliinuka na kwenda chumbani pia.



 
SEHEMU YA 83

Muda wa kulala, Erica alienda chumbani kwa Erick na kuanza kuongea nae kuhusu wazazi wao,
“Mama na baba wanapenda sana kama dada Angel na Samir vile”
“Ila wewe Erica kuna muda una wazimu ujue, yani mama na baba ukawafananishe na Angel na Samir kweli?”
“Aaaah basi nimesemea tu”
“Haya niambie, huu ni muda wa kulala kwani unakuja kulala chumbani kwangu leo?”
“Kheee jamani Erick loh!! Mimi niliona nimeboreka na usingizi sina ndiomana nikaja huku, nitalalaje chumbani kwako sasa?”
“Unadhani kuna ubaya wowote? Hakuna ubaya wala nini, vipi Abdi hajakupa tena karata tucheze? Ila hata hivyo kesho ni shule ujue”
“Sawa, ngoja nikalale tu”
Erica aliondoka na kwenda chumbani kwake kulala, basi Erick alibaki akijiuliza,
“Huyu dada yangu ana nini lakini? Muda huu alikuja kufanya nini? Nakumbuka hapo nyuma ni mimi nilikuwa msumbufu kwake ila kwanini

kwasasa yeye ndio kawa msumbufu?”
Akaachana na mawazo na kuamua kulala tu.
Kulipokucha kama kawaida walijiandaa na kwenda shuleni ila Erica alipofika leo alizibwa macho na Elly yani kama jana yake alivyofanyiwa

na Erick basi akacheka na kusema,
“Nimekugundua ni Elly wewe”
Basi Elly alimuachia na kucheka pia huku akimwambia,
“Mwanzoni nilikuwa nikikugusa lazima ukosee ila leo umesema upesi upesi kuwa ni Elly”
“Ndio maana shuleni ni wewe ndio mwenye mtindo wa kuniziba macho na nyumbani ni Erick ndio mwenye mchezo huo”
Basi walicheka kwa pamoja na kuingia kwenye kipindi vizuri.
Kitendo cha Erica kuwa karibu na Elly kilikuwa kinamkera sana Abdi, na kuona kamavile Elly kaja kumzibia nafasi yake kwa Erica, basi

akasogea alipo Erica ingawa kashapewa onyo mara nyingi tu na Elly ila alisogea na moja kwa moja alimpa Erica karata maana alitambua

ndio ugonjwa wake,
“Erica, nimekuletea karata leo”
“Oooh Abdi jamani, asante sana. Nashukuru kwa hili”
Elly alimuangalia Abdi na kumwambia,
“Nilikwambiaje?”
Erica akasema,
“Jamani Elly achana na hayo mambo, Abdi ni rafiki yangu mkubwa kama ulivyokuwa wewe, kwahiyo hata usiwe na mashaka na Abdi.”
Kisha akamuangalia Abdi na kumwambia,
“Nashukuru sana kwa karata Abdi”
Basi Abdi akasogea na kumnong’oneza kitu Erica ambapo Erica alicheka tu.



 
SEHEMU YA 84

Angel nae akiwa shuleni bado Husna alimwambia umuhimu wa kurudi na kuongozana na wenzie yani asiwe anatumia usafiri kila leo,
“Angel, unapitwa na kuona mengi na kujifunza mengi pia. Unajua mimi napenda utambue dunia imezungukwa na vitu gani? Na watu gani?

Watoto wengi wa matajiri huwa hampati nafasi ya kujifunza mambo mengi yanayoizunguka jamii, jaribu kuongea na dereva wenu ili upate

nafasi na wewe nya kutembea na wenzio, kuongea mambo mbalimbali”
“Sawa nimekuelewa, ila sijui kama nyumbani watanielewa”
“Wewe ongea na dereva tu, naamini atakuelewa. Tena kesho ni Ijumaa Angel, jitahidi tuondoke pamoja hadi stendi”
“Sawa, hakuna tatizo”
Basi muda huo huo alifika tena madam Hawa na kumuita Samir, yani ilikuwa ni kawaida kwa huyu madam kufika na kumuita Samir.
Muda wa kutoka ulipofika kama kawaida dereva alifika kumchukua Angel na kuondoka nae, walipokuwa njiani Angel akamwambia dereva,
“Sikia anko, kesho nipeleke tu shule ila usije kunichukua”
“Mmmh unadhani mama yako atanielewa?”
“Atakuelewa ndio, ila usimwambie nakuomba. Na mimi nahitaji kupanda daladala, yani kipindi mama na baba wamesafiri nilikuwa nafaidi

sana na kupanda daladala ila kwasasa kila sehemu dereva jamani nimechoka, naomba kesho usije kunifata bhana”
“Ila usimwambie mama yako ukweli”
“Sitomwambia, na leo usinifikishe nyumbani kwa shangazi kabisa ila nishushe karibu na pale nitembee kidogo”
Yule dereva alikubali na kweli walipofika karibu alimshusha Angel ambapo alianza kutembea kuelekea kwa shangazi yake, wakati

anakaribia getini, ilipita bajaji mbele yake kisha yule mwenye bajaji alisimamisha na kumwambia Angel,
“Oooh siamini kama leo nimekuona tena Malaika”
Kwakweli Angel hakuwa na kumbukumbu yoyote ya kuonana na huyu dereva bajaji kabla, kwahiyo alibaki akimuangalia tu, kisha yule

dereva akamwambia,
“Mimi naitwa Ally, niliwahi kumleta mama yako nyumbani kwenu kisha wewe ukaniletea hela. Uminikumbuka?”
Angel akajaribu kuvuta kumbukumbu, na kukumbuka lile tukio ila sura ya huyu dereva wa bajaji ilikuwa imemtoka na kumwambia,
“Nimekumbuka ndio, kumbe ni wewe?”
“Ndio ni mimi, naomba namba yako mrembo”
“Sina simu”
“Mmmmh mtoto mrembo kama wewe huna simu! Basi hakuna tatizo maana nitakuletea simu”
“Mmmmh hapana usiniletee maana nitaiweka wapi? Siruhusiwi kumiliki simu maana mimi ni mwanafunzi bado”
“Kheee maisha gani unayoishi hayo mrembo jamani, siku hizi mtoto wa miaka kumi anamiliki simu sembuse wewe jamani”
“Hapana, mimi siruhusiwi”
“Oooh basi nitakuwa nakuvizia mida kama hii ili angalau nikuone tu mrembo, mmmh watu wengine jamani kama hamjisaidii vile”
Angel aliondoka zake na kwenda kuingia ndani kwao ila leo shangazi yake hakuwepo nyumbani kwahiyo aliingia tu bila kuulizwa chochote

kile.



 
SEHEMU YA 85


Kama kawaida, Erick na Erica nao walirudi nyumbani kwao ambapo kila mmoja alienda chumbani kwake kuvua sare za shule, ila baada ya

muda kidogo tu Erica alienda chumbani kwa Erick na kumuonyesha zile karata, basi Erick alichukia na kumwambia,
“Ni Abdi kakupa eeeh!”
Alipoona kaka yake kachukia ilibidi abadili ukweli na kumwambia,
“Hapana, nimepewa na Elly”
“Oooh sawa, basi tutacheza hizo karata”
“Ila kaka mbona Elly huchukii ila Abdi unachukia?”
“Sijui ni kwanini ila Abdi simuamini hata kidogo nadhani imetokea tu hivyo”
“Basi naziweka kwako halafu kesho tuatacheza”
Erica aliziacha pale kwa kaka yake kisha yeye alienda chumbani kwake.
Siku hiyo hawakuweza kucheza karata kwani kila mmoja alikuwa kachoka kwahiyo usiku walilala tu ndiomana walisema kuwa karata

wangecheza kesho yake usiku.
Kulipokucha kama kawaida walijiandaa na kwenda shuleni basi wakiwa shuleni, Erica alifatwa na Abdi leo ambapo alimuuliza,
“Ujumbe wangu kwenye zile karata umeuona?”
“Ujumbe? Ujumbe gani kwani?”
“Kuna ujumbe wako nimeuweka katikati ya zile karata”
“Ni mzuri au mbaya?”
“Kwani vipi?”
“Zile karata nimempa kaka yangu Erick aziweke kwanza”
“Oooh kwanini umefanya hiyo Erica jamani!! Naomba ukirudi tu kwenu ukazichukue zile karata na kuzichambua ili utoe ule ujumbe”
Erica alimuangalia Abdi aliyeonyesha kachukizwa kabisa kuhusu karata kuachiwa Erick wakati zina ujumbe wake.

Leo Angel akiwa shuleni basi hakuwa na mashaka sana kwani alishamwambia dereva kuwa asimfate na alikuwa na uhakika wa kuondoka

na Husna kama walivyopanga.
Ila muda kidogo Husna alianza kulalamika tmbo, yani tumbo likawa linamsumbua sana ikabidi hadi mwalimu ampe ruhusa ya kwenda

nyumbani kwahiyo Husna aliondoka na kwenda kwao na hivyo Angel kubaki mwenyewe.
Muda wa kutoka ilibidi Angel aondoke mwenyewe huku akifatiliza tu wanafunzi wenzie wanapoelekea, gafla akaitwa
“Angel”
Akageuka na kukuta ni Samir ndio alimuita ila alikuwa akihema, basi Angel alimuuliza,
“Mbona unahema hivyo?”
“Nilipokuona unaondoka mwenyewe nikaanza kukukimbilia, yani yule madam nae ananitesa balaa”
“Kwani anakuitiaga nini?”
“Yani acha tu, nikija shule lazima niripoti kwake na nikitoka lazima niripoti kwake pia”
“Pole sana”
“Asante kipenzi changu”
“Umeanza hivyo, mimi sitaki bhana, usiniite hivyo”
“Ila Angel, mimi na wewe inatakiwa tupate sehemu tuongee vizuri. Hata macho yako yanaonyesha kuwa unanipenda pia”
Angel akaona atembee tu bila kumjibu chochote Samir kwani alihisi kuwa anaanza tena kumshawishi.


 
SEHEMU YA 86

Mama Angel kwasasa aliona nafuu kidogo kwani hakupata malalamiko yoyote kuhusu Angel yani hakusikia chochote kinachoendelea juu ya

Angel, ila aliona ni vyema kama atapita shuleni kwao ili akamchukue mwenyewe na ajaribu kuongea nae mawili matatu na mwanae kwahiyo

alimtumia tu ujumbe dereva,
“Leo usiende kumchukua Angel, naenda mwenyewe”
Basi alikuwa kwenye gari yake na moja kwa moja alielekea shuleni kwakina Angel.
Alipofika alishangaa kukuta ndio muda huo wanafunzi wakiwa wanatoka shuleni, alishangaa mbele kuona Angel ameongozana na Samir

wakitembea kuelekea kwenye stendi ya daladala.


Alipofika alishangaa kukuta ndio muda huo wanafunzi wakiwa wanatoka shuleni, alishangaa mbele kuona Angel ameongozana na Samir

wakitembea kuelekea kwenye stendi ya daladala.
Kwakweli mama Angel alichukia sana na kutamani hata kushuka ili awafuate maana njia waliyopita huwa hayapiti magari, kwakweli alichukia

sana na kuwasha gari yake ili awakute stendi.
Ila alivyofika stendi tu na wao ndio walikuwa wakipanda daladala, yani alichukia mno na kupigia honi ile daladala ila wala haikusimama yani

alijikuta akijawa na hasira katika moyo wake balaa huku akisema,
“Huyu Samir ananitakia nini tena jamani, yani nimemuamisha Angel shule ila kamfata jamani!”
Wakati akiwaza hayo kumbe alikuwa kasimamisha gari barabarani na kusababisha foleni basi honi nyingi zikawa zinapiga kwake, akashtuka

na kuogopa ila alipoangalia hakuiona tena ile daladala kwani zilipita nyingi nyingi, basi hasira zilimzidi yani alikuwa akiendesha gari huku

ana mawazo na hasira aliamua kulipaki pembeni kwani kwa hali aliyokuwa nayo angeweza hata kupata ajali, akampigia simu tu dereva wao

ili apande bodaboda na aende mahali alipo ili waweze kuondoka.

Angel akiwa kwenye daladala na Samir, basi konda alipokuja kudai nauli Samir alilipa nauli ya watu wawili yani yeye na Angel, basi Angel

akamuangalia na kumwambia,
“Ila mimi nauli ninayo”
“Sijasema kuwa huna ila mimi ni mwanaume na lazima nikuhudumie”
“Kheeee makubwa”
“Usishangae Angel, mtu unapopenda kuna mambo unayafanya kama umechanganyikiwa vile”
“Pole”
“Sio pole tu, unatakiwa uonyeshe ushirikiano”
“Sasa ushirikiano gani?”
“Uwe unaniambia kuwa unanipenda pia ili nami nifurahie, najua unanipenda ila niambie”
Basi Angel alikaa kimya, na alipofika kituo anachoshuka alishuka ila Samir nae alishuka na kuongozana na Angel ambapo Angel alimuuliza,
“Kwani na wewe unaishi huku?”
“Hapana”
“Sasa mbona umeshuka?”
“Lazima nihakikishe kuwa unafika salama ndio nami niondoke”
“Mmmh hapana, usifike nami kwa shangazi, unataka kuniletea balaa wewe”
Basi Angel aliita bajaji ambapo alipanda na kumtaka dereva aondoke, kilikuwa ni kitendo cha haraka kwahiyo Samir hakuweza kupanda pia.
Basi Angel akiwa kwenye ile najaji alishangaa kukuta ni yule Ally ndio kambeba kwenye bajaji,
“Kheee kumbe ni wewe?”
“Ndio ni mimi, yani leo nahisi nitalala huku nikitabasamu kwa kumbeba mrembo kwenye bajaji yangu”
“Mmmh wewe nawe loh!!”
“Sio hivyo ila wewe ni mrembo sana”
Angel aliamua kukaa kimya tu mpaka walipofika getini kwa shangazi yake na kushuka huku akimuuliza yule dereva,
“Unanidai pesa ngapi?”
“Hapana sikudai mrembo, nimekubeba tu”
“Mmmh!”
Basi Angel aliingia kwenye geti lao na moja kwa moja alienda chumbani kwake maana hakumkuta shangazi yake pale sebleni.



 
Back
Top Bottom