Simulizi : Nguvu ya Mapenzi

Simulizi : Nguvu ya Mapenzi

SEHEMU YA 106

Basi yule mzazi wa Erica akaitwa, alipoingia tu ofisini, macho yake yaligongana na macho ya baba Abdi kwani ni watu waliofahamiana.
Kimya cha muda mfupi kikatawala mahali pale, kisha mwalimu akavunja ule ukimya kwa kusema,
“Tena sfadhari mzazi wa Erica umefika, maana hapa kuna ubishano kidogo juu ya mtu anayepaswa kutengeneza mlango wa choo”
Basi baba Abdi akasema,
“Ubishano upi tena mwalimu?”
“Si umekataa kuwa mwanao hahusiki? Na anayetakiwa kulipa ni Elly ambaye alimsaidia Erica? Bora amefika mzazi wa Erica maana ndio alitupigia simu na kutusema sana, na tukaona sio vizuri kweli sababu chanzo cha tatizo anajulikana”
Baba Abdi akasema tena,
“Kwani Abdi kavunja nini na nini?”
“Abdi hajavunja ila inasemekana kuwa alitaka kumbaka Erica, ndio huyu Elly akaenda kumsaidia kwahiyo ilibidi avunje mlango wa choo yani mwanao ilibidi ashtakiwe ujue”
“Jamani walimu ndio mnataka kukuza mambo kiasi hiki, haya mambo si ya kuyamaliza tu. Hebu niandikieni hapo gharama za huo mlango na nitazilipa ili mtengeneze”
Walimu wote walishangaa maana huyu baba alivyokuwa mpole muda huu utafikiri sio huyu ambaye alikuwa akiwabishia humo ofisini na kukataa kabisa kulipa ila muda huu anataka kupewa gharama na kuahidi kuwa atalipa za utengenezaji, walimu walidhani ni masikhara, basi wakasema pale,
“Ule mlangi inatakiwa laki mbili ndio utengenezwe”
“Aaaah kumbe!! Sasa si mngesema toka mwanzo tu jamani”
Kisha baba Abdi akatoa wallet yake na kutoa laki mbili taslimu pale na kumkabidhi mwalimu yani wote walikuwa wakishangaa tu ila walishangaa zaidi kwa mama Erica maana hakuongea jambo lolote zaidi ya kumvuta Erica na kutoka nae nje ambapo Elly nae alimfata nyuma.
Baba Abdi alipomaliza kulipa alitoka pia ambapo mwanae nae alimfata nyuma, halafu baba Erica alikuwa akimuita mama Erica,
“Erica, Erica, Erica”
Ambapo mtoto Erica ndio alikuwa akigeuka nyuma na kumwambia mama yake,
“Mama, baba Abdi ananiita”
“Twende nyumbani wewe, acha ujinga”
Basi wakaingia ndani ya gari ila kabla mama Erica hajaondoa ile gari yake alishangaa baba Abdi kukaa mbele ya ile gari kwa maana kuwa alikuwa radhi amgonge au amsikilize, kwahiyo ilibidi mama Erica ashuke kumsikiliza, kwanza alimuuliza,
“Una tatizo gani kwani?”
“Inamaana umenisahau Bahati wako?”
Mama Erica alicheka na kusema,
“Hivi unajua sisi ni watu wazima sasa, tuna familia zetu hebu acha mambo ya kijinga jamani”
“Nipe kwanza mawasiliano yako ndio nitaacha, kwakweli sijui nikwambiaje ila nilipokuona leo akili yangu yote imeruka na kupoteza uelekeo kabisa”
Mama Erica akaona isiwe tabu maana alimpa namba yake kisha kuagana nae ambapo kila mmoja alipanda gari lake na kuondoka zake.

Moja mwa moja mama yake Erica alitaka Elly ampeleke kwao ambapo Elly alifika nae hadi nyumbani kwao ila mama yake Elly hakuwepo basi mama Erica alimuuliza Elly,
“Kwani mama hako huwa anarudi muda gani?”
“Mama, hana muda maalum wa kurudi, kwahiyo sijui”
“Ooooh sawa, akija basi mwambie kuwa mama yake na Erica anahitaji sana kumuona”
“Sawa, nitamwambia”
Basi mama Erica alipanda kwenye gari na binti yake na kuanza kurudi kwao huku Erica akimwambia mama yake,
“Si nilikwambia mama, huwezi kuonana na yule mama yupo busy sana”
“Nimekuelewa mwanangu, ila huwezi jua ni kwanini nahitaji kumuona”
“Kwanini mama?”
“Bado mdogo kujua haya”
“Sawa, hivi na yule baba Abdi unafahamiana nae?”
“Achana na maswali hayo”
Basi waliendelea na safari ambapo Erica alikuwa akijiuliza mambo mengi sana kuhusi baba yake Abdi na mama yake, kwahiyo alipanga baba yake akirudi nyumbani amuhadithie yani yeye hata hakufikiria kama sio vizuri wala nini.
 
SEHEMU YA 107

Baba Abdi nae alikuwa akielekea kwake huku akitabasamu tu, mwanae alikuwa akimuuliza,
“Baba, mbona umelipa hela kubwa ya mlango wakati ule mlango matengenezo yake haifiki hata elfu hamsini”
“Nyamaza kimya kenge wewe, unafanya makosa halafu unajifanya kujieleza ujinga hapa”
Walipoingia tu nyumbani kwao, siku hiyo baba yake alipitiliza kulala tu, ilibidi mama aliyeishi nao kuanza kumuuliza Abdi,
“Leo hamjaokota mtoto mwingine wa kuja nae nyumbani?”
“Hapana mama, ila kuna jambo lingine limetokea”
“Jambo gani?”
“Wakati tupo shuleni, alifika mama yake na Erica”
“Mama yake nani?”
Baba yake nae alitoka chumbani na kumuita Abdi ambapo Abdi alienda kumsikiliza baba yake, alimfunga mlango na kumwambia,
“Yani wewe umefanya makosa, umefanya nilipe pesa isiyokuwa na sababu halafu saa hizi upo nyumbani kuchonga mdomo kwa mama yako. Unamweleza hayo ili iweje? Unataka aondoke halafu hapa atawalea nani wajinga nyie”
Kisha akachukua mkanda wake wa suruali na kumtandika nao sana yani hadi mama yake alienda kumuombea msamaha ndio akamuachia.
Basi mkewe akamuuliza,
“Nini sababu ya kumpiga hivyo mtoto jamani!”
“Huyu mtoto ni mjinga sana, unajua alichofanya shuleni?”
“Eeeeh kafanyaje?”
Baba Abdi alianza kumueleza mkewe kile alichoambiwa na walimu, yani kile alichokuwa anakibishia ndio alichomueleza mkewe, basi mkewe alikuwa akishangaa tu na kuona kuwa mumewe alikuwa sahihi kumuadhibu mtoto huyo ila kwa muda huo alikuwa ameshaachana na mada ya mtoto wake kuwa alipofika mama Erica ilikuwaje.

Erica akiwa nyumbani alimuhadithia Erick kuhusu kilichotokea shuleni halafu akamwambia jinsi alivyomuuliza mama yake na jinsi alivyomshushua, kisha akamwambia Erick,
“Sasa mimi nitaenda kumuuliza baba”
“Ukisikia umbea ndio huo, dada Angel alikuwa akigombana nawe kila siku hapa sababu ya huo umbea kwani Erica huwa huwezi kupotezea kitu? Hata kama wakifahamiana, wewe mtoto inakuhusu nini au itakusaidia nini? Je utayafahamu maisha ya wazazi wetu kipindi hiko? Maisha yao yalivyokuwa ni siri yao pekee, sisi watoto hayatuhusu, kama mama kasema achana na habari hizo basi achana nazo”
“Mmmh jamani!”
“Ndio, mimi nakupenda ndiomana nakwambia ukweli Erica, sio jambo jema kufatilia mambo yanayofanywa na wazazi”
“Basi sifatilii tena, nitakuwa nafatilia mambo yako”
“Ndio, yangu ukifatilia ni sawa kabisa. Tena anza muda huu huu kufatilia, ila sio mambo ya wazazi kwanza hawatapenda wakigundua hilo, pili sio tabia nzuri”
Basi ile ikawa kama dawa, maana alivyoambiwa tu vile, hakutaka tena kujihusisha na mambo yasiyomuhusu. Basi kaka yake alimwambia tena,
“Kesho ni Ijumaa mdogo wangu una mpango gani?”
“Mpango gani kivipi?”
Mara Vaileth alienda kuwaita maana walikuwa kwenye kile chumba cha kusomea,
“Nyie mnaitwa na wazazi wenu kwenda kula huko”
Basi wakainuka na kuelekea sebleni ambapo baba na mama yao walikuwa mezani wakila, kwahiyo waliulizia kama na wao wamekula ndiomana waliwaita, basi waliwasalimia pale na kuchukua chakula na kuanza kukila.
Wakati wa kula simu ya mama Angel ambayo alikuwa ameiacha kwenye kochi iliita sana basi akamwambia Erica akamchukulie ili aangalie nani anapiga ila Erick akamwambia mama yake,
“Mama, siku zote huwa unatufundisha kuwa si vizuri kuongea wakati wa kula. Pia sidhani kama ni vizuri kupokea simu wakati wa kula”
Baba Angel nae akasapoti na kusema,
“Kweli kabisa alichosema mtoto”
Basi wote waliendelea kula, ila yule mpigaji inaonyesha aliamua kupiga maana simu ilikuwa ikiita tu, yani ikikatika inaanza tena kuita hadi kero.
Ikabidi tu mama Angel ainuke na kuizima ile simu kisha alirudi kula na walipomaliza waliagana pale ambapo moja kwa moja walienda vyumbani.
 
SEHEMU YA 108


Baba Angel alimuuliza mke wake kuhusu ile simu iliyokuwa ikipigwa muda wote,
“Ni nani aliyekuwa akipiga vile?”
“Sijui, ni namba mpya”
“Labda ni mtu wa maana au labda kuna tatizo maana kapiga sana mke wangu, hebu jaribu kumtafuta usikie, huwezi jua”
Basi mama Angel aliwasha tena ile simu na kuipiga ile namba ambayo muda ule ule ilipokelewa na sauti ya kika,
“Nani mwenzangu”
“Nikuuliza wewe uliyepiga ni nani?”
“Oooh niliona umenipigia sana, ndiomana nikakupigia ili kujua ni nani?”
“Hebu niambie kuwa ni nani wewe maana hii ni simu ya mume wangu”
“Oooh samahani”
“Samahani ya nini? Wewe ndio kimada chake eeh!”
Mama Angel alikata ile simu na mumewe alimuangalia na kumuuliza,
“Nani sasa?”
“Nadhani alikosea namba maana namuuliza nani na yeye ananiuliza nani”
“Oooh achana nae, tufanye yet utu mke wangu. Kesho kuna mahali nataka twende pamoja”
“Wapi huko mume wangu?”
“Mmmh ila tutarudi Jumapili”
“Inabidi tuwaage watoto basi”
“Tutawaaga kesho asubuhi, hakuna tatizo”
“Sawa, na hiyo Jumapili tutarudi asubuhi au jioni?”
“Jioni mke wangu”
“Sawa, hakuna tatizo”
Kisha wakaamua kulala tu kwa muda huo.
Kulipokucha, mama Angel na baba Angel walishajiandaa kwahiyo wakati wanatoka walikuta watoto wao nao wamejiandaa basi waliwaaga kuwa wanasafiri na wangerudi Jumapili jioni, Vaileth nae alikuwepo pale basi alimkumbusha mama Angel safari yake ya kesho kwa ndugu zake,
“Mama, je mimi naweza kesho kwenda kwa shangazi yangu kumsalimia?”
“Hakuna tatizo ilimradi jioni utakuwa umerudi dada”
Basi Vaileth alishukuru na kuwatakia safari njema, basi waliondoka zao na watoto wao walienda shuleni kama kawaida yao.
 
SEHEMU YA 109


Erica akiwa shuleni leo alishangaa mno kuona Elly akiwa kama kavimba mkono vile, basi muda wa mapumziko aliamua kumuuliza kuwa imekuwaje,
“Elly, tatizo nini jamani? Mbona mkono umevimba?”
“Toka udogo wangu sijawahi hata mara moja kupigwa na mama yangu ila jana amenipiga hadi nilijihisi kizunguzungu”
“Kheee kwanini sasa mamako alikupiga jamani Elly?”
“Sijui kwanini ila mama kachukia sana nilipomwambia kuwa nilienda na mama yako nyumbani, na nilipomwambia kuwa mama yako anataka kufahamiana nae, nilishangaa mama akichukia na kunipiga sana, sasa wakati nakimbia ndio kuna kitu alinitupia kikanipata hapa mkononi hadi mkono ukavimba hivi. Kwakweli nimeshangaa sana, sijui kwanini mama kachukia kiasi hiki jamani! Tena kasema nisirudie tena na pale tunapoishi tutahama”
“Mmmh, kwahiyo mama yako hataki kuonana na mama yangu jamani!”
“Sio mama yako tu ila mama huwa hataki kuonana na mtu yeyote asiye ndugu yetu, naomba Erica usimwambia haya mama yako tafadhari, nakuomba sana”
“Usijali Elly, ila dah nakuhurumia sana. Sasa dawa gani umetumia?”
“Dada alinikanda”
“Dada yako yupi?”
“Ni mtoto wa makubwa, basi ndio kanikanda mkono, kiukweli mama alikuwa na hasira sana, hadi muda analala alikuwa amenuna na leo asuhubi hata sijaongea nae. Roho inaniuma sana, mama yangu ni kila kitu katika maisha yangu hata sijui ni kwanini amechukia kiasi hiki”
“Pole sana Elly, nakuahidi sitomwambia mama na wala sitotaka tena kuja nae kwenu kuonana na mama yako. Pole Elly jamani”
Basi waliingia darasani ila Erica alikuwa akijiuliza vitu vingi sana kwani hakuona mantiki ya Elly kupigwa na mama yake.
 
SEHEMU YA 110

Angel leo akiwa shuleni, basi Husna alikaa nae karibu wakijisomea, ila muda wa mapumziko siku hiyo walishangaa sana Samir kuelekea ofisini, na aliweza kumuona maana yeye na Husna walikaa karibu na ofisi kwahiyo waliona kila kitu, na baada ya muda mwalimu aliwaita basi Husna na Angel walienda, akawaambia watoe vile vyombo na kupeleka kwenye jiko la shule.
Basi waliingia na kutoa vile vyombo, ila Samir nae alikuwepo mule ofisini na alikaa meza moja na madam Hawa, kwahiyo walitoa vile vyombo na kupeleka jikoni. Ila roho ya Angel iliumia sana, basi alimuuliza Husna,
“Inamaana madam Hawa ana mahusiano na Samir?”
“Mmmh sijui, lakini inawezekana maana madam Hawa hajawahi kuwa karibu kiasi hiki na mwanafunzi yoyote yule”
“Kwahiyo inamaana yupo nae?”
“Mbona unaulizia hivyo Angel? Unamtaka Samir?”
“Hapana, nimeuliza tu”
“Hawa wavulana shuleni ukitaka kusoma kwa raha waone wote kama kaka zako, inamaana hata akifanya nini haitakuumiza moyo maana unaona kama kaka yako ndio amefanya. Una kaka nyumbani Angel?”
“Ndio, yupo mdogo wangu wa kiume anaitwa Erick”
“Basi ukitaka kufaulu vizuri muone kila mvulana shuleni kama mdogo wako Erick”
“Ila sijasema kuwa namtaka Samir”
“Hata mimi sijasema kuwa unamtaka ila nimeongelea tu rafiki yangu”
Basi walirudi darasani na baada ya muda Samir nae alirudi darasani na kuendelea na masomo.
Muda wa kutoka ulivyofika, leo madam Hawa alifika mwenyewe darasani kwakina Angel na kumuita Samir, ambapo alimwambia,
“Samir, jiandae tuondoke”
Basi Samir alibeba begi lake na kuondoka na yule madam, yani kitu hiko kiliumiza sana moyo wa Angel, aliumia na fikra zake zote.

Angel aliporudi nyumbani alikuwa na mawazo sana, shangazi yake alipomuona alielewa tu kuwa Angel hayupo sawa basi alimuita kabla ya kwenda chumbani na kuanza kuongea nae,
“Angel, ni kitu gani kinakukosesha raha malaika wangu?”
“Shangazi sijui nisemeje, ila swala la kumuona Samir akiwa karibu na madam Hawa, naumia sana moyo”
“Ngoja nikuulize swali mwanangu, umeenda shule kwaajili ya kusoma au kwaajili ya Samir?”
“Kwaajili ya kusoma shangazi”
“Basi soma, unamfatilia Samir ni nani katika maisha yako? Na atakusaidia kitu gani? Je Samir ndio atasaidia kuongoza maisha yako? Bila Samir huwezi kuishi?”
“Hapana shangazi”
“Basi achana na mawazo ya Samir kabisa, kwanza hakufai mtoto mdogo anatembea na wamama watu wazima, yani hakufai kabisa mwanangu. Zingatia masomo yako”
“Asante shangazi”
Basi Angel muda huu alienda chumbani kwake tu na kuanza kufanya mambo mengine yaliyokuwa kwenye ratiba yake, ila kwavile hakumaliza vizuri mawazo yake basi muda huo alitoka tena nje, na siku hiyo kwa mara ya kwanza alikaa nje ya geti na muda kidogo ni kamavile aliambizana na yule dereva wa bajaji kwani alifika muda ule ule pale getini kwakina Angel na kuanza kumsalimia,
“Mrembo uhali gani?”
“Mmmh wewe nawe loh!!”
“Wewe nawe nini, yani sijui ni kitu gani kimenipitisha hapa, nadhani ni moyo wangu ndio umenipitisha hapa. Nakupenda sana Angel”
Mara shangazi wa Angel alitoka nje na kushangaa sana,
“Kheee kumbe wewe upon je badala ya kukaa chumbani kwako”
Kisha akamvuta mkono na kuingia nae ndani, kisha akamchapa makofi ya kutosha na kumwambia,
“Angel huwa sipendi kupiga ni mpaka mtu anipe sababu ya kupiga, na kwa unachofanya Jumatatu nitaenda shuleni kwenu nikaseme kinachoendelea juu yako. Usinitie uchizi mie”
Angel alinyong’onyea na kumwambia shangazi yake,
“Nisamehe shangazi tafadhari, usiende shule”
“Unaniahidi kitu gani?”
“Nakuahidi shangazi hii kitu haitajirudia tena, nisamehe shangazi”
“Haya rudi chumbani kenge wewe”
Basi Angel alitia huruma sana na moja kwa moja alielekea chumbani kwake.
 
SEHEMU YA 111

Erica leo alivyorudi nyumbani kwao tu, wakati amekaa sebleni na Erick alimuhadithia juu ya Elly kupigwa na mama yake, kwakweli hata Erick alishangaa sana,
“Jamani, kwanini sasa? Kisa kutokufahamiana na mama yetu?”
“Ndio, Elly kasema kuwa mama yake hataki kuonana na mtu yeyote mgeni kwake zaidi ya ndugu zake”
Vaileth nae aliyasikia hayo na kumuuliza Erica,
“Kama huyo mama hataki kuonana na mama yenu, kwanini alimpa Elly visheti akuletee ili ulete nyumbani?”
“Mmmh sijui”
“Kuwa makini sana Erica, sio kila unachopewa basin i cha kuleta nyumbani, kuwa makini sana utaangamiza wazazi wako”
“Inamaana mama yake Elly ni mbaya?”
“Sina maana hiyo, ila tu nimekwambia kuwa makini basi”
“Sawa dada, nimekuelewa”
Basi Erica aliendelea kuongea na kaka yake ambaye kwa muda huo waliinuka na kwenda ndani kucheza zile karata za Abdi, basi wakati wanacheza ndipo Erick akamtania Erica,
“Hizi karata ndio zingesababisha ubakwe Erica”
“Toka zako huko, halafu baba yake Abdi sijui yukoje, eti akaniuliza umewahi kubakwa?”
Erick alicheka sana na kumuuliza,
“Ulimjibuje?”
“Nilikaa kimya tu”
“Siku nyingine wakikuuliza hivyo waambie nimewahi ndio kubakwa na kaka yangu”
“Kheee Erick unaongelea nini kwani?”
“Kwani hapa tunaongelea nini?”
“Kheee basi, tucheze tu karata”
Basi waliendelea na kucheza zile karata huku wakiendelea kuambizana mambo mbalimbali, muda wa kulala ulifika na kujikuta wote wakiwa wamelala sehemu moja yani chumbani kwa Erica maana ndipo walipokuwa wakicheza karata humo.
Erica alishtuka usiku wa maneno na kuhisi njaa sana ila Erick alikuwa amelala hoi, ilibidi amuamshe maana alijua pia lazima na yeye ana njaa.
Na kweli alivyoamka pia alikuwa na njaa na siku hiyo waliona umuhimu wa mama yao kuwa nyumbani kwani yeye huwa anawakumbusha kila siku muda wa kula ila leo dada yao aliwaacha waendelee kulala tu, basi waliamka na kwenda jikoni ambapo walipakua chakula na kula, ila waliposhiba hawakuwa na usingizi kabisa, hivyo waliamua kuwasha Tv na kuanza kuangalia ambapo walilala pale pale sebleni.
 
SEHEMU YA 112


Vaileth alipoamka asubuhi kwakweli alicheka sana kukuta wamelala sebleni, aliwashtua na kuwauliza kuwa imekuwaje, Erica alianza kusema,
“Ila dada una tabia mbaya jamani, yani umeacha kutuamsha jana tuweze kula”
“Jamani, nilijua labda hamna njaa ndiomana mlienda kulala mapema. Kwahiyo ndio mliamka usiku na kuja kula”
“Ndio, na usingizi ulikata na tulipokaa sebleni ndio tukajikuta tukilala tena”
“Ila nyie jamani, hivi mama yenu angekuwepo mngefanya ujinga wa namna hii eeeh!”
Basi Erick akaondoka zake kuelekea chumbani kwake, kwahiyo ilibidi vaileth amuage Erica kuwa siku hiyo atatoka ila badae atarudi.
Baada ya hapo Vaileth alifanya usafi wote wa ile nyumba na kisha kujiandaa na kuondoka, muda huo Erica na Erick wamelala maana baada ya pale kila mmoja alienda chumbani kwake kulala tena.
Basi Erick alipoamka aligundua kuwa yule dada yao hakupika hata chai wala nini, ikabidi akapike mwenyewe maana hakikuwa kitu kigumu kwake, tena siku hiyo alipika chai, alichemsha mayai na kwenda kununua mkate wa kula yeye na Erica, yani Erica alipoamka alikuta kaka yake ameshaaandaa kila kitu akatabasamu na kumwambia,
“Kwa hakika mke utakayemuoa atakuwa na raha sana”
“Sidhani kama nitakuja kuoa mimi”
“Kwanini?”
“Sababu ninayempenda hawezi kuwa mke wangu”
“Mmmh kumbe kaka yangu ushapenda tayari, nidokezee basi nimjue wifi yangu ni nani na kwanini hutoweza kumuoa?”
“Hebu njoo tu tunywe chai, maswali mengine hayana msingi hayo”
Basi walikaa na kuendelea kunywa chai.
 
SEHEMU YA 113

Vaileth alifika kwa shangazi yake na kupokelewa kwa kofi kwanza, yani alibaki tu kushangaa na kumwambia shangazi yake,
“Jamani shangazi, hilo kofi ndio salamu?”
“Ndio, mjinga sana wewe yani unaishi kwenye nyumba ya kifahari halafu wazazi wako tunaishi kwenye nyumba ya shida hivi ndio unaona vizuri? Bora hata wifi asingekuzaa toto jinga kama wewe”
Prisca alienda na kusema,
“Bora shangazi useme wewe, yani mimi kwakweli kwa jinsi nilivyoiona ile nyumba hadi nilisisimka na kujiuliza hivi Nyanda anafanya kitu gani?”
Basi shangazi yake akasema tena,
“Mwanangu Vaileth kama ulivyojiita jina zuri la kizungu ila mbona unakosa akili kwenye bichwa lako hilo?”
“Sasa shangazi, mimi nitafanya kitu gani?”
“Kumbe hujui eeeh! Mbona swala ni jepesi sana, ni kumtega yule baba mwenye nyumba na kumuweka kwenye kumi na nane zako”
“Mmmmh yule baba mwenye nyumba hana mambo hayo kabisa”
“Basi hata kwa ndumba mwanangu, kuna mtaalamu huyo yuko vizuri yani ni swala tu la wewe kuweka dawa mara moja kwenye chakula cha huyo baba halafu kwisha habari yake”
“Mmmh!”
“Sio mmmh ndiomana nilikupigia simu ile asubuhi kuwa uwahi kuja ili twende huko. Haya tuondoke”
Yani Vaileth alikuwa akishangaa tu kwakweli, kisha yule shangazi aliondoka nae na kwenda kupanda daladala ambapo walienda mbali kidogo na pale na kulikuwa na bibi wa makamo ambaye ndio alikuwa mganga, basi alianza kuongea nao,
“Kwanza huyu mwenye nyumba mnayemtaka kafatiliwa na wadada wengi sana, nikikupa idadi ya wanawake ambao wamemfatilia huyo baba basi utabaki tu na mshangao, na hajaanza kufatiliwa leo bali siku nyingi sana ila huyo baba anampenda sana mkewe”
Shangazi wa Vaileth akachukia na kusema,
“Jamani jamani, kwahiyo haiwezekani kwa Nyanda kumpata?”
“Imefika kwangu jua kwamba inawezekana, kwanza wenye nyumba hao wamesafiri, si ndio”
Vaileth akajibu,
“Ndio”
“Basin i vizuri kwani nakupa dawa kwanza ambayo utatakiwa kuiweka getini yani inatakiwa ikae masaa kumi na nane ndio ianze kufanya kazi, kwamaana hiyo ni kwamba, watakaporudi kesho na kukanyaga hiyo dawa basi itakuwa ndio njia ya kwanza kumteka, halafu nitakupa dawa nyingine ya kuweka kwenye chakula”
“Sawa”
“Ila fanya kama nitakavyokuelekeza, kwanza wakati unaiweka usiruhusu mtu yoyote kuiona”
Basi yule bibi alifanya dawa zake na kumkabidhi Vaileth zile dawa ambapo shangazi yake alimpa onyo kuwa asipuuze kufanya hizo dawa,
“Yani ukipuuza Vai ujue huna ndugu katika maisha yako”
Basi na muda huo huo walimtaka Vaileth aondoke aelekee kwa bosi wake, yani Vaileth aliondoka huku akiwa na mawazo sana, kwani kile kitu hakuwahi kukifikiria na wala hakutaka kukifanya kabisa ila kila akikumbuka maneno ya shangazi yake aliogopa sana, maana hadi anaondoka aliambiwa ole wake asifanye hiyo dawa.
 
SEHEMU YA 114

Erica na Erick muda huu walitulia sebleni wakiangalia Tv, mara kwenye Tv kulikuwa na tamthilia ambayo ilionyesha mwanamke akimuwekea limbwata mume wake, basi Erick akasema,
“Yani wanawake akili zenu ni mbovu sana, sasa huyu akimloga mume wake ndio anapata faida gani?”
“Mmmh sio wanawake wote, mbona mama hayupo hivyo?”
“Haya badili kipindi basi, mimi mavitu ya ushirikina hayo sitaki kuyaangalia”
“Sibadili”
Basi walianza kugombana sababu Erica ndio alishika ile rimoti ya Tv, na wakati wanagombana Erica aliinuka na kuanza kukimbia ambapo Erick alikuwa akimkimbiza, cha kushangaza erica alikimbia kwa kuelekea nje wakati sio kawaida yao kutoka nje ya geti ila wakati kafungua geti alijikuta akimsukuma Vaileth na kumfanya aangukie huko hadi vitu vya kwenye mkoba wake kuanguka, ni pale walipoanza kushangaa wakati wanaviokota, Erica alivishika na kumuangalia dada yao kisha akamwambia,
“Dada, kumbe wewe ni mshirikina!!”
Vaileth alishtuka na kuogopa sana, kile kitendo cha mshtuko kilifanya aanguke na kuzimia.


Basi walianza kugombana sababu Erica ndio alishika ile rimoti ya Tv, na wakati wanagombana Erica aliinuka na kuanza kukimbia ambapo Erick alikuwa akimkimbiza, cha kushangaza erica alikimbia kwa kuelekea nje wakati sio kawaida yao kutoka nje ya geti ila wakati kafungua geti alijikuta akimsukuma Vaileth na kumfanya aangukie huko hadi vitu vya kwenye mkoba wake kuanguka, ni pale walipoanza kushangaa wakati wanaviokota, Erica alivishika na kumuangalia dada yao kisha akamwambia,
“Dada, kumbe wewe ni mshirikina!!”
Vaileth alishtuka na kuogopa sana, kile kitendo cha mshtuko kilifanya aanguke na kuzimia.
Basi Erick na Erica walimuita mlinzi wao ambaye alimuinua Vaileth na kumuingiza ndani, ila Erick alikusanya zile dawa za Vaileth na kwenda kuzitupa kwenye mtaro halafu akarudi tena nyumbani kwao ambapo Vaileth alikuwa amezinduka ila walipomuuliza alikuwa akilia tu.
Basi walimpeleka ndani kabisa ambapo Erick na Erica walikaa nae na kumuhoji, kwani Erica bado alikazania lile lile swala,
“Dada, tuambie ukweli, wewe ni mshirikina?”
Vaileth alikuwa akilia tu, kisha aliwajibu,
“Jamani mimi sio mshirikina ila zile dawa nimepewa na shangazi yangu amesema za kunikinga”
“Kwani dada huamini kuwa Mungu pekee ndio kinga ya kweli?”
“Naamini wadogo zangu, haikuwa nia yangu kuwa na zile dawa, ni shangazi kanipa”
“Sawa dada, basi kesho twende wote Kanisani”
“Sawa tutaenda, naomba mnisamehe sana wadogo zangu”
Kisha Vaileth alienda chumbani, kiukweli alikuwa akijutia mno kile kitendo, alijikuta akilaani mno kuhusu shangazi yake kumpeleka kwa mganga na kupewa zile dawa, yani alikuwa kajifungia tu chumbani akilia.
Basi Erick na Erica walikuwa sebleni ambapo Erica alimwambia Erick,
“Lazima nimueleze mama kuhusu swala hili”
“Wewe nawe, kashatuomba msamaha, sasa mama umueleze kitu gani?”
“Yani wewe Erick unapinga kila kitu, una uhakika gani kuwa zile dawa ni zake mwenyewe? Unajua tutadhurika humu ndani? Dalili ya mvua ni mawangu”
“Hata kama ila subiri kwanza mdogo wangu, tusiwe hivyo jamani, mtu kaomba msamaha halafu tumfanyie hivyo kweli!!”
“Mmmh haya, maana wewe kila kitu unapinga jamani”
Basi na wao waliendelea na mambo mengine.
 
SEHEMU YA 115

Mama Angel na baba Angel walikuwa mahali ambapo baba Angel alichagua ili yeye na mkewe wakae kwa karibu zaidi na kusahau yale yanayowafanya muda wote wasifikirie mambo yao zaidi ya biashara tu wanazofanya,
“Jamani mume wangu si ungeniambia sasa!”
“Aaaah kumbe hujui eeeh! Safari za kushtukizana ndio nzuri mpenzi. Mimi na wewe tunapendana, kwahiyo naweza panga safari yoyote kwa muda wowote kwani najua huwezi kukataa. Je hujafurahia huku mke wangu?”
“Nimefurahi sana yani, mara nyingine watoto nao wanachanganya sana akili, mtu ukipata sehemu kama hii unashukuru sana kwakweli”
Mara simu ya mama Angel ilianza kuita, kuangalia ni ile namba ya siku ile, wasiwasi wake ni kuwa huenda mpigaji wa ile simu ni baba Abdi sababu siku ile ni mkewe aliongea na kwa haraka haraka alihisi ile sauti kama ni sauti ya Fetty vile, basi mumewe akamwambia kuwa apokee,
“Pokea mke wangu, huwezi jua ingawa sikupenda tukiwa huku tusumbuliwe na simu”
Basi mama Angel alipokea, na kama alivyohisi ni kweli baba Abdi ndiye aliyekuwa akimpigia ile simu,
“Oooh asante sana kwa kupokea simu yangu, ujue nimekumiss sana wewe mwanamke”
“Kwani wewe una matatizo gani jamani!!”
“Sina matatizo yoyote, wewe ndio chanzo cha mimi kuoa mwanamke asiyeeleweka, na wewe ndio chanzo cha yule mwanamke kunifanyia dawa mimi hadi nikazaa hovyo, na wewe ndio chanzo cha mpaka sasa siishi kwa amani na mke wangu maana muda wote nakukumbuka na kukutaja sana kwani ungeishi nami najua watoto wangu wangepata malezi mazuri sana”
“Una wazimu wewe”
Kisha mama Angel alikata ile simu na mumewe alimuuliza, ambapo hakutaka kumficha kwani alimwambia ukweli wote,
“Kheee jamani, hivi huyu si ndio kwenye harusi yetu aliongea sana nikajua yameisha mke wangu, bado tu anakufatilia!! Nahitaji kuongea nae kiume”
“Hata mimi namshangaa, eti analalamika maisha yake yameharibika sababu yangu”
“Huyu ni mjinga, maana mtu unaharibu maisha mwenyewe na sio mtu mwingine, kwani wewe umeharibu vipi maisha yake?”
Mama Angel alimwambia mumewe waachane tu na habari hizo na waendelee kufurahia kilichowapeleka kule kwani hakutaka kuongea yaliyopita.

Leo ndio ilikuwa Jumamosi ambayo Samir alienda nyumbani kwa madam Hawa, ambaye alisema kuwa siku hiyo ndio aende akaongee nae vizuri, kiukweli hata yeye huwa haelewi mantiki ya kinachofanywa na yule madam kwahiyo anachukulia kawaida tu, basi alienda kumsikiliza,
“Madam, nimeitikia wito”
“Maisha unayoishi sasa yani mimi nikionekana kama mzazi wako unayaonaje?”
Samir alinyamaza kimya kidogo, kumbe kile alichokuwa akifanyiwa ni kama mtoto wa mwalimu, basi alipumua kidogo na kujibu,
“Nimeyapenda”
“Mbona umewaza sana? Ulikuwa ukifikiria ni kitu gani? Au ulifikiria kuwa nakutaka?”
“Hapana madam”
Kisha madam hawa akacheka na kusema,
“Siwezi katika maisha yangu yote kuwa na mahusiano na kujana mdogo kama wewe, yani maisha ninayokupa shuleni nahitaji ujione kama mtoto wa mwalimu na usome kwa bidii na uache kumfatilia Angel yani ukitaka kufanya ujinga ujue kuwa mama yangu yupo hapa shuleni ananiona. Mimi sikuhitaji kwakweli, na walimu wote wanaelewa kuwa kwanini nafanya hivi, nakuweka vizuri kisaikolojia. Haya niambie kwasasa, unasumbuliwa sana na mawazo ya Angel?”
“Hapana”
“Sawa, mara nyingi huwa unafanya nini?”
“Mara nyingi umekuwa ukinipa zoezi na maswali ya kufanya, kwahiyo nikirudi nyumbani nakosa muda wa kukaa na kuwaza maana asubuhi huwa unahitaji nikupatie hayo maswali, na moja kwa moja huwa unakuja na kuniita darasani kwahiyo nimejikuta nikiwa busy sana”
“Na hiko ndio nilichokuwa nakitaka toka mwanzo, nilitaka wewe ukazanie masomo na sio kitu kingine chochote. Kama ulikuwa unawazo kuwa madam Hawa anakutaka kimapenzi naomba usahau kabisa kabisa, maana mimi nakupenda kama mtoto wangu ndiomana niliongea na mama yako aniruhusu nianze kukulea mwenyewe shuleni ili kukurudisha kwenye mstari, si vizuri kufanya mzazi atupe hela kila siku sababu ya kukuhamisha wewe shule, si vizuri kwakweli mnatuumiza wazazi, niliumia sana wakati mama yako akiongea ndiomana nikabeba jukumu la kuwa nawe bega kwa bega”
“Asante sana madam”
“Sasa nadhani utakuwa huru zaidi maana mwanzoni ulikuwa na mashaka kuwa sijui huyu madam ananitaka sijui nini na nini, ondoka kabisa hayo mawazo maana mimi ni kama mama yako tu”
Basi Samir aliitikia ambapo yule madam alimpa maswali mengine na kuagana nae kuwa arudi kwao.
“Moja kwa moja nyumbani Samir, nitawasiliana na mama yako maana anajua kama ulikuja kwangu”
“Sawa madam”
Basi Samir aliondoka muda ule na kuelekea kwao.
 
SEHEMU YA 116


Samir alipofika kwao alimuona mama yake akimsindikiza mwanaume, kwahiyo alisimama akimuangalia hadi pale mama yake aliporudi na kumuuliza,
“Mama, na yule ni baba yangu?”
“Hebu kuwa na adabu wewe mtoto, kila mtu baba yako jamani eeh! Nisiongozane na mwanaume basi ndio kashakuwa baba yako, kwani baba yako ninayeishi nae hakutoshi?”
“Mama, yule baba ana kisirani sana”
“Hata awe na kisirani ndio kashakuwa baba yako, usinipangie maisha”
“Sawa mama, sikupangii maisha ila ni vizuri mimi kumjua baba yangu wa ukweli”
“Aliyekwambia kuwa huyu sio baba yako wa ukweli nani? Mimi ndio mama yako na mimi ndio niliyekuonyesha huyu, kwahiyo heshima na adabu ifate mkondo wake”
“Ila mama hujui tu ni kwanini simtaki huyu baba”
“Kwanini?”
“Jamani baba ana watoto kila sehemu, mwisho wa siku ndio mambo ya kujikuta nimeoana na dada yangu, baba gani huyu, kila kina ana mtoto. Nina uhakika watoto wake wengine hata hafahamu wako wapi na wanaishije, mimi ningeweza ningejibadilishia baba”
“Punguani mmoja wewe, usumbue, uhangaishe ila mimi na baba yako bado tupo pamoja na wewe. Tena kuna muda huwa nimekata tamaa kabisa ila baba yako utasikia tusimuache mtoto nyumbani, aende shule, halafu mjinga kama wewe unadai unamtaka baba mwingine. Kama umejizaa tafuta baba mwingine, ungejua hadi kuzaliwa kwako ni nini kilifanyika hata usingejiongelesha hapo”
Huyu mama ilionyesha amechukizwa na kumsonya mwanae kisha akaenda ndani kujiandaa na kumuaga kuwa anaenda kazini, muda huu Samir alikuwa na dada yake aliyeitwa Samia basi akamwambia,
“Kwakweli mimi nikiwa mkubwa siji kuoa mke dizaini ya mama kabisa”
“Kwanini?”
“Muda wote kazini, yani yeye hana cha usiku wa manane, asubuhi, mchana wala jioni. Haya saizi kashaondoka eti anaenda zamu, jamani si jioni hii basi atarudi kesho asubuhi, kwakweli siji kuoa mke dizaini ya mama kabisa”
Kisha akaingia zake ndani na kuanza kufanya kazi ambayo alipewa na madam Hawa.
 
SEHEMU YA 117

Leo Jumapili baada ya kutoka Kanisani, shangazi wa Angel alifika na mama mmoja nyumbani kwake na kumuita Angel kisha akamtambulisha kwa mama yule,
“Huyu anaitwa mama Sarah, ni mwalimu mzuri sana. Nimemuomba awe anakufundisha hesabu maana nimejaribu kupitia madaftari yako nimeona kidogo inakupiga chenga, kwahiyo nakubadilishia ratiba maana ukitoka tu shule huyu mama atafika hapa nyumbani na kukufundisha, tumeelewana?”
“Ndio shangazi, asante”
Kisha Angel akarudi chumbani huku shangazi yake akiendelea kuongea na yule mama Sarah, kisha aliamua kumsindikiza, ila wakati ametoka kumsindikiza alikutana na mtu ambaye hakutarajia kabisa kukutana nae, yule mtu alimuita,
“Tumaini”
Basi aligeuka na kumuangalia, alishangaa sana na kusema,
“Kheee Derrick, siamini kama nimekuona tena”
“Kwahiyo ulijua nimekufa?”
“Niliposikia umeathirika moja kwa moja nilijua kifo kinakunyemelea, kwahiyo mtu angesema umekufa wala nisingeshangaa”
“Acha fikra potofu dada yangu, ukimwi sio mwisho wa maisha cha muhimu ni kujikubali na hali halisi na kula vizuri na kutumia dawa vizuri. Je ukiniona hivi unaweza kusema nimeathirika?”
“Ndio nakushangaa hapa maana unaonekana kuwa na afya nzuri kabisa”
“Basi kuathirika sio mwisho wa maisha, mtu anakufa kwa maradhi mbalimbali kwanza ukimwi hauuwi mtu ila magonjwa nyemelezi ndio yanaua, ndio utasikia mara kafa na presha, sijui malaria, sijui kisukari ila ukimwi tunauandama tu. Mimi nadundika bado”
“Eeeeh vipi, mkeo na watoto hawajambo”
“Basi nilioa nikakaa na huyo mke dada yangu!! Sijui nina gundu gani, kamke kenyewe kalikuwa kashirikina hatari, nilikaoa na nikakaambia wazi kuwa mimi nimeathirika na alikubali vile vile na hali yangu, cha kushangaza eti ananifanyia limbwata nimpende sana, jamani mtu nishapigwa na ukimwi halafu atake tena kunipiga na malimbwata loh! Nikakapa talaka na kalisepa bhana”
“Kwahiyo watoto je?”
“Sikuzaa nae, ila bhana kumbe nina mtoto mkubwa hatari, kuna mwanamke alibeba mimba yangu wakati nipo chuo ila niliikataa basi ndio mtoto nimemuona sasa yani kafanana na mimi mweeeh ila nimegomewa kuishi nae kisa nilimkataa. Unaishi wapi Tumaini?”
“Twende, karibu kwangu, sio mbali kutoka hapa”
Basi wakaongozana hadi nyumbani kwa Tumaini ambapo waliongea ongea kisha Tumaini akamuita Angel amtambulishe mjomba wake huyo maana huyu Derrick alikuwa na undugu na mama Angel ila Tumaini alisoma nae ndiomana wakafahamiana.
Basi Angel alitoka na kutambulishwa kwa mjomba wake huyu, ila huyu mjomba alionekana kumuangalia sana Angel hadi alikuwa akijiramba midomo, basi Tumaini akamshtua hivi,
“Kheee wewe Derrick huachi tamaa zako jamani, mwanao huyu ujue!!”
Mara Derrick alianza kulia na kumfanya Tumaini amwambie Angel arudi ndani kisha kumuuliza Derrick kwanini analia,
“Erica alitoa mimba yangu, mtoto wetu angekuwa mkubwa kuliko huyu”
“Hivi wewe Derrick una kichaa au kitu gani jamani!! Erica si dada yako wewe? Inamaana ulitembea na dada yako hadi kupeana mimba?”
“Alikuwa ni mpenzi wangu kabla hatujajua ni ndugu”
“Kheee mbona umeniambia mapya leo, kwahiyo kipindi kile chuo ni hadi ulitembea na Erica?”
“Ndio, muulize Dora anaelewa kila kitu”
“Duh!! Naomba uende Derrick, kwanza tutakuja kuongea siku nyingine”
Basi Derrick aliinuka na kuondoka ila kiukweli lile jambo lilimuacha Tumaini akiwa na maswali sana.
 
SEHEMU YA 118

Erica toka tukio la jana alikosa imani kabisa na dada yao vaileth kiasi kwamba akiwa anapika jikoni basi anakuwa nae kwenye mapishi, yani yeye haamini kabisa kuwa zile dawa ni za kumsaidia yeye, anahisi kuwa lazima dada yao huyo ana dawa zingine.
Basi hioni ya siku hiyo alikuwa akipika nae jikoni, kuna muda alimuagiza chumvi ambayo waliisahau kwenye meza ya chakula basi na yeye alimuita Erick ili alete ile chumvi maana hakutaka hata kidogo kumuacha dada yao apike mwenyewe jikoni, basi Erick alipeleka ile chumvi huku akicheka kwani alijua ni kwanini Erica anafanya vile.
Ila Vaileth alimuuliza Erics,
“Mbona na wewe umemuagiza Erick?”
Erica huwa hawezi kuficha jambo milele maana muda ule ule alimwambia,
“Unafikiri yale madawa yako ya jana nakuamini? Yani sikuamini hata kidogo, ni kwavile tu Erick kasema nisiseme kwa mama ila lazima ningesema tu, yani sikuamini dada”
Vaileth alikaa kimya kwani aliona aibu sana, muda kidogo walifika wazazi wao basi Erick na Erica walienda kuwapokea huku Vaileth nae akiwa nyuma yao na kuwakaribisha, sema roho yake ilimsuta sana.
Basi mama Angel na baba Angel walikuwa wamekuja na zawadi na kuwapatia watoto wao, ilikuwa ni saa zinazofanana, basi Erica na Erick walifurahi sana na kwenda kuweka zile zawadi zao chumbani, mama Angel hakumsahau Vaileth kwani alimletea zawadi ya heleni na mkufu pamoja na kitenge, basi nae aliwashukuru na kufurahi sana kisha akapeleka chumbani kwake.
Yani vaileth kila alipokuwa akitembea mule ndani basi roho yake ilimsuta sana na kujilaumu sana kusikiliza matakwa ya shangazi yake, maana kama hivyo uaminifu tena umefutika kabisa, ukizingatia wakina Erica hawakumuamini tena.

Basi muda wa kula chakula cha usiku uliwadia na chakula kiliwekwa mezani kwanza na wote walienda mezani ila kabla ya kuanza kula kile chakula Erica akaongee,
“Jamani dada Vai ndio apakue chakula kwanza kuonja halafu ndio tuendelee na chakula”
Mama yake alimshangaa na kumuuliza,
“Kwanini Erica?”
“Kwani mama hujui? Mfalme na Malikia hawapaswi kula chakula kabla hakijaonjwa na mpishi kwahiyo mpishi anatakiwa kuwa wa kwanza kuonja halafu ndio mfalme na malkia wafatie”
“Kheee kwahiyo humu ndani nani ndio mfalme na nani ndio malkia?”
“Baba na mama nyie ndio mfalme na malkia halafu mimi na Erick ni Prince na Princes kwahiyo wote hatutakiwi kula chukula kama hakijaonjwa ili tusipate madhara”
Basi mama yake alicheka na kutikisa kichwa tu kisha akamwambia Vaileth,
“Haya, hebu onja mpishi”
Ilibidi Vaileth apakue kidogo na kula kile chukula halafu wao ndio wakapakua na kula kile chakula na baada ya hapo waliongea ongea kidogo na kuinuka kwaajili ya kujiandaa na kulala.
Basi Erica akiwa chumbani alifatwa na Erick ambaye alimuuliza na kumlaumu,
“Kwanini unafanya hivyo sasa Erica jamani! Unajua unamkosesha raha yule dada Vai!”
“Hata yeye alitakiwa kukosa raha kwanza wakati kabeba kifurushi cha zile dawa”
“Si alishasema ni za kwake?”
“Hatakama kasema ni za kwake yani mimi bado haijaniingia akilini kwakweli, najua lazima zile dawa alikuwa akileta kwaajili yetu humu ndani”
“Kwanini unasema hivyo?”
“Hebu angalia baada ya kumbamba nini kilitokea? Alilia mwanzo mwisho, yani anajuta kwanini tumembamba, halafu pili yupo na wasiwasi muda wote, halafu tena akituona tu anashtuka si anataka kufanya kitu huyo”
“Haya leo umemsimamia jikoni na bado hujamuamini kwani hadi umeomba aonje kwanza chakula yeye, kwanza nikuulize je siku zote utakuwa ukimsimamia? Je wakati tupo shuleni ni nani atamsimamia?”
“Nilichofanya leo ni kumuweka wazi kuwa kuanzia sasa nimeanza rasmi kumfatilia kwahiyo asishangae kuwa siku nimemmwagia chakula usoni yani nikiwa na mashaka nae tu ajue ameisha. Nawapenda wazazi wetu ujue, hivi wakifa kizembe unadhani nani wa kulaumiwa?”
“Unamaana anataka kuua wazazi wetu? Mbona sura yake ya upole sana?”
“Usimuamini mtu kwa kumuangalia usoni”
Basi Erick aliona watabishana sana, badala yake aliagana na Erica na moja kwa moja kwenda kulala.
Ila Erica alibaki na msimamo wake tu wa kumfatilia Vaileth kwani hakumuamini tena toka simu wambambe na zile dawa, aliona kamavile zile dawa alileta ili awaangamize mule ndani haswaa akikumba maandishi ya kwenye zile dawa, kuwa weka kwenye chakula, mwaga mlangoni basi hakuwa na imani kama zile dawa zilikuwa kweli za kumkinga yule dada tu.
 
Back
Top Bottom