Abdallahking
JF-Expert Member
- Mar 19, 2018
- 3,985
- 10,840
- Thread starter
- #281
SEHEMU YA 240
Basi usiku wa siku hii, baba Angel aliongea na watoto wake maana Erica alienda kuomba kuwa hiyo safari ya ufukweni iwe kesho, na kwavile alijihisi uchovu sana akaona hakuna tatizo kwahiyo aliwaambia tu kuwa kesho yake wataenda huko ufukweni kutembea, ila ilikuwa nu furaha kubwa. Basi siku hiyo walilala huku wakiwaza uhuru ambao kesho yake watakuwa nao.
Basi kulipokucha, baada ya kazi za hapa na pale ndio walienda kujiandaa sasa na walipokuwa tayari ndio walienda kuchukua ruhusa mapema naye aliwaruhusu na kuwapa pesa kwaajili ya matumizi ya huko watakapokuwa kutembea ila baba yao aliwaambia,
“Ila kule ni kuzuri sana mwisho wa wiki, sema leo siku ya kawaida mtakuta kumepooza sana”
“Aaaah baba, sisi hatuna tatizo ni bora tukashuhudie maji tu”
Basi akawaruhusu na wao wakaondoka kisha pale nyumbani alibaki na mkewe tu huku wakiongea na kupanga mambo mbalimbali.
Muda huu mama Angel ndio alikuwa na simu ya mume wake, basi ujumbe mara ukaingia kwenye simu ya mume wake,
“Baba Elly, mbona unafanya hivyo?”
Moja kwa moja mama Angel alitambua kuwa aliyetuma ujumbe ule alikuwa ni Sia, basi alimuangalia mumewe na kumuuliza,
“Eeeeh mume wangu huyu Sia ana ajenda gani za kukuita baba Elly?”
Akampa simu mumewe ambapo naye aliangalia ule ujumbe na kumwambia mke wake,
“Aaaah si mjinga huyu, hutambui hilo mke wangu. Naomba usifatilie mambo ya huyu”
“Ila amekazana sana mume wangu?”
“Achana nae, yani yeye ilimradi kapata namba zetu basi anaona cha kufanya ni kutusumbua tu, usimjali kwa lolote huyu mtu mke wangu”
“Na akija tena hapa nyumbani!”
“Hawezi, nishamwambia mlinzi kuwa sitaki kuiona ile takataka hapa nyumbani kwangu, hebu tufanye vitu vya muhimu mke wangu. Eeeh watoto wote wameondoka, leo tutakula nini?”
“Mmmh hata sijui halafu naona uvivu kupika leo hatari”
“Hakuna tatizo mke wangu, basi leo nitakupikia naamini utapenda chakula changu”
Mama Angel alicheka na kumkumbusha kitu mume wake,
“Ndio unipikie kama ugali aliopika dada yako nyumbani kwetu, na maharage yenye macho”
Baba Angel alicheka sana, yani alicheka muda huo na kusema,
“Yani Tumaini kashasahau ujue kama alikuwa hajui kupika, saivi anajiona ndio mwenyewe wakati aliumbuka ukweni. Ila kwenu sio watu wazuri, yani kumfanyia vile dada yangu dah! Haya sasa nikupikie nini mke wangu?”
“Chohote utakachokipenda wewe basi nami nitakipenda tena leo nimepikiwa na mume wangu basi nitakulaje!”
Wakacheka pale na kuendelea na mambo mengine.
Wakina Erick walifika ufukweni walikokuwa wakienda, basi baada ya kufika pale Junior akawaambia,
“Jamani, mimi nitatembea na Vaileth huku nikimuonyesha mandhari ya ufukwe halafu nyie kaka na dada ongozaneni huko kwingine sio tuanze kufatana fatana”
Erick na Erica wakaguna ila wakakubaliana nae tu na moja kwa moja Junior aliongozana na Vaileth ila kwakweli Vaileth hakutaka kuongozana na Junior sema tu hakutaka Erick na Erica watambue chochote kile.
Vaileth na Junior waliongozana huku Junior akijifanya kumuonyesha Vaileth baadhi ya vitu vya ufukweni, kisha alimuomba wakae mahali kwenye mchanga ili amuonyeshe vizuri, na walipokaa tu alianza maongezi nae,
“Kwanza kabisa Vaileth, ni kwanini umenichukia?”
“Hivi unadhani kuna mtu anaeweza kufurahia ujinga Junior, sikia umenidanganya mimi kuwa unanipenda kumbe una wanawake zako kibao. Najua unanifanyia yote haya sababu unaniona mimi mjinga kwakuwa ni mtu mzima halafu nimekupenda wewe kijana mdogo”
“Ngoja nikukatishe kuhusu umri wako, kwanza kabisa tambua kuwa umri ni namba tu, mapenzi hayaangalii umri wala nini. Halafu unaweza kuona mimi ni mdogo ila nikawa natambua mambo mengi sana katika mapenzi kutokana na niliyopita. Siwezi kukataa hili, ni kweli mimi nilikuwa muhuni sana na nilikuwa na wanawake wengi, ila nilipokupata wewe nikasema kwanini nihangaike na wanawake wengine wakati wewe nakupenda! Sasa yule msichana niliachana nae kitambo sana na alisema kuwa ana mimba yangu na anahitaji kuitoa, basi nilimpatia pesa za kuitoa na hapo nikamwambia kuwa mimi na yeye ndio basi. Sasa hata namshangaa kunitafuta tena sijui damu zinamtoka, kwanza kabisa mimba alikuwa nayo yeye na sio mie, halafu ni yeye ndio aliyeenda kutoa, sasa anamlalamikia nani kuwa damu zinamtoka? Achana na yule msichana, kwanza nilimwambia kuwa mimi nina mke aniheshimu ila hataki ndiomana kafanya huo ujinga, jamani Vai nakupenda sana”
“Mmmh kwa mtindo huu ndio tutakuwa kama mama na baba kweli kule nyumbani! Wale wanapendana kwa dhati na wala baba hana uhuni kabisa”
“Sikia nikwambie, mama yangu nilimsikia akiongea na baba na walikuwa wakiongea kuhusu bamdogo huyo, nasikia alikuwa ni malaya tena malaya koko, hata mbwa mwenyewe akasome”
“Jamani Junior, punguza ukali wa maneno”
“Aaah basi, ila usione watu wametulia kwenye ndoa zao ukadhani wameibuka tu, penzi la kweli linatengenezwa na maelewano mema na masikizano, sasa unanifungia mlango kabisa hutaki hata kusikia upande wangu naongea kuhusu nini au nitajitetea vipi ila unabaki kuumia moyo na kunilaumu. Jamani Vaileth mimi nakupenda sana”
“Mmmh lakini swala la kusema baba alikuwa muhuni nakukatalia”
“Haya, endelea kukataa tu ila wanaomfahamu wenyewe wanasema, kuwa alikuwa ni kiwembe balaa kinakata kulia na kushoto, unaambiwa akiwa anatembea na wewe mdada na ukamtambulisha rafiki zako basi jua wote hao atawapitia”
“Duh!!”
“Mbona mimi mstaarabu sana, ila maisha huwa yanabadilisha mtu. Muangalie sasa, katulia na ndoa yake, hanywi pombe na unaambiwa alikuwa analewa yule hadi anazima”
“Junior! Nani kakwambia maneno hayo?”
“Yani licha ya kumsikia mama ila kuna mama mmoja hivi, sijui alikuwaga mwanamke wa zamani wa bamdogo basi huwa nikikutana nae ananiambia mambo mengi sana ya bamdogo kipindi hiko”
“Kwahiyo na yeye alimvumilia tu! Yani mwanaume analewa hadi anazima, anatembea na rafiki zako wote, bado alimvumilia tu”
“Si alimpenda, tena sio marafiki tu hata ndugu zako ikiwezekana anatembea nao. Unajua ukiona mwanaume wa hivyo tambua kabisa hakupendi kwani mwanaume anayekupenda atawaheshimu ndugu zako, atawaheshimu rafiki zako na atakuheshimu na wewe pia. Yule mmama nilimwambia kuwa basi hakukupenda, ila yule mama anavyoongea kwa uchungu hata nina mashaka nae”
“Ni mama gani huyo?”
“Siku moja nitakuonyesha, nikimuona tu nje ya geti basi nitakuita ili tuongee nae, kiukweli utabaki unamuangalia tu. Ila sijui alinihadithia mimi tu au huwa anawahadithia wengi sijui. Kiukweli siwezi kumueleza bamdogo yale maneno najua atachukia sana”
“Ila kwakweli imenishangaza sana, kwahiyo wewe unanipenda kweli?”
“Vaileth jamani, mimi ninakupenda sana tu, kiasi kwamba hata siwezi kumtamani mwanamke mwingine zaidi yako. Naomba unisamehe na tuanze kurasa mpya ya mapenzi yetu”
Vaileth alitabasamu tu na kumfanya Junior atambue kuwa pale ameshasamehewa kwahiyo ilikuwa ni furaha sana kwake kwani alitamani mno kusamehewa na Vaileth.
.
.
.
.
.
ITAENDELEA ALHAMISI