Simulizi : Nguvu ya Mapenzi

Simulizi : Nguvu ya Mapenzi

SEHEMU YA 240


Basi usiku wa siku hii, baba Angel aliongea na watoto wake maana Erica alienda kuomba kuwa hiyo safari ya ufukweni iwe kesho, na kwavile alijihisi uchovu sana akaona hakuna tatizo kwahiyo aliwaambia tu kuwa kesho yake wataenda huko ufukweni kutembea, ila ilikuwa nu furaha kubwa. Basi siku hiyo walilala huku wakiwaza uhuru ambao kesho yake watakuwa nao.
Basi kulipokucha, baada ya kazi za hapa na pale ndio walienda kujiandaa sasa na walipokuwa tayari ndio walienda kuchukua ruhusa mapema naye aliwaruhusu na kuwapa pesa kwaajili ya matumizi ya huko watakapokuwa kutembea ila baba yao aliwaambia,
“Ila kule ni kuzuri sana mwisho wa wiki, sema leo siku ya kawaida mtakuta kumepooza sana”
“Aaaah baba, sisi hatuna tatizo ni bora tukashuhudie maji tu”
Basi akawaruhusu na wao wakaondoka kisha pale nyumbani alibaki na mkewe tu huku wakiongea na kupanga mambo mbalimbali.
Muda huu mama Angel ndio alikuwa na simu ya mume wake, basi ujumbe mara ukaingia kwenye simu ya mume wake,
“Baba Elly, mbona unafanya hivyo?”
Moja kwa moja mama Angel alitambua kuwa aliyetuma ujumbe ule alikuwa ni Sia, basi alimuangalia mumewe na kumuuliza,
“Eeeeh mume wangu huyu Sia ana ajenda gani za kukuita baba Elly?”
Akampa simu mumewe ambapo naye aliangalia ule ujumbe na kumwambia mke wake,
“Aaaah si mjinga huyu, hutambui hilo mke wangu. Naomba usifatilie mambo ya huyu”
“Ila amekazana sana mume wangu?”
“Achana nae, yani yeye ilimradi kapata namba zetu basi anaona cha kufanya ni kutusumbua tu, usimjali kwa lolote huyu mtu mke wangu”
“Na akija tena hapa nyumbani!”
“Hawezi, nishamwambia mlinzi kuwa sitaki kuiona ile takataka hapa nyumbani kwangu, hebu tufanye vitu vya muhimu mke wangu. Eeeh watoto wote wameondoka, leo tutakula nini?”
“Mmmh hata sijui halafu naona uvivu kupika leo hatari”
“Hakuna tatizo mke wangu, basi leo nitakupikia naamini utapenda chakula changu”
Mama Angel alicheka na kumkumbusha kitu mume wake,
“Ndio unipikie kama ugali aliopika dada yako nyumbani kwetu, na maharage yenye macho”
Baba Angel alicheka sana, yani alicheka muda huo na kusema,
“Yani Tumaini kashasahau ujue kama alikuwa hajui kupika, saivi anajiona ndio mwenyewe wakati aliumbuka ukweni. Ila kwenu sio watu wazuri, yani kumfanyia vile dada yangu dah! Haya sasa nikupikie nini mke wangu?”
“Chohote utakachokipenda wewe basi nami nitakipenda tena leo nimepikiwa na mume wangu basi nitakulaje!”
Wakacheka pale na kuendelea na mambo mengine.

Wakina Erick walifika ufukweni walikokuwa wakienda, basi baada ya kufika pale Junior akawaambia,
“Jamani, mimi nitatembea na Vaileth huku nikimuonyesha mandhari ya ufukwe halafu nyie kaka na dada ongozaneni huko kwingine sio tuanze kufatana fatana”
Erick na Erica wakaguna ila wakakubaliana nae tu na moja kwa moja Junior aliongozana na Vaileth ila kwakweli Vaileth hakutaka kuongozana na Junior sema tu hakutaka Erick na Erica watambue chochote kile.
Vaileth na Junior waliongozana huku Junior akijifanya kumuonyesha Vaileth baadhi ya vitu vya ufukweni, kisha alimuomba wakae mahali kwenye mchanga ili amuonyeshe vizuri, na walipokaa tu alianza maongezi nae,
“Kwanza kabisa Vaileth, ni kwanini umenichukia?”
“Hivi unadhani kuna mtu anaeweza kufurahia ujinga Junior, sikia umenidanganya mimi kuwa unanipenda kumbe una wanawake zako kibao. Najua unanifanyia yote haya sababu unaniona mimi mjinga kwakuwa ni mtu mzima halafu nimekupenda wewe kijana mdogo”
“Ngoja nikukatishe kuhusu umri wako, kwanza kabisa tambua kuwa umri ni namba tu, mapenzi hayaangalii umri wala nini. Halafu unaweza kuona mimi ni mdogo ila nikawa natambua mambo mengi sana katika mapenzi kutokana na niliyopita. Siwezi kukataa hili, ni kweli mimi nilikuwa muhuni sana na nilikuwa na wanawake wengi, ila nilipokupata wewe nikasema kwanini nihangaike na wanawake wengine wakati wewe nakupenda! Sasa yule msichana niliachana nae kitambo sana na alisema kuwa ana mimba yangu na anahitaji kuitoa, basi nilimpatia pesa za kuitoa na hapo nikamwambia kuwa mimi na yeye ndio basi. Sasa hata namshangaa kunitafuta tena sijui damu zinamtoka, kwanza kabisa mimba alikuwa nayo yeye na sio mie, halafu ni yeye ndio aliyeenda kutoa, sasa anamlalamikia nani kuwa damu zinamtoka? Achana na yule msichana, kwanza nilimwambia kuwa mimi nina mke aniheshimu ila hataki ndiomana kafanya huo ujinga, jamani Vai nakupenda sana”
“Mmmh kwa mtindo huu ndio tutakuwa kama mama na baba kweli kule nyumbani! Wale wanapendana kwa dhati na wala baba hana uhuni kabisa”
“Sikia nikwambie, mama yangu nilimsikia akiongea na baba na walikuwa wakiongea kuhusu bamdogo huyo, nasikia alikuwa ni malaya tena malaya koko, hata mbwa mwenyewe akasome”
“Jamani Junior, punguza ukali wa maneno”
“Aaah basi, ila usione watu wametulia kwenye ndoa zao ukadhani wameibuka tu, penzi la kweli linatengenezwa na maelewano mema na masikizano, sasa unanifungia mlango kabisa hutaki hata kusikia upande wangu naongea kuhusu nini au nitajitetea vipi ila unabaki kuumia moyo na kunilaumu. Jamani Vaileth mimi nakupenda sana”
“Mmmh lakini swala la kusema baba alikuwa muhuni nakukatalia”
“Haya, endelea kukataa tu ila wanaomfahamu wenyewe wanasema, kuwa alikuwa ni kiwembe balaa kinakata kulia na kushoto, unaambiwa akiwa anatembea na wewe mdada na ukamtambulisha rafiki zako basi jua wote hao atawapitia”
“Duh!!”
“Mbona mimi mstaarabu sana, ila maisha huwa yanabadilisha mtu. Muangalie sasa, katulia na ndoa yake, hanywi pombe na unaambiwa alikuwa analewa yule hadi anazima”
“Junior! Nani kakwambia maneno hayo?”
“Yani licha ya kumsikia mama ila kuna mama mmoja hivi, sijui alikuwaga mwanamke wa zamani wa bamdogo basi huwa nikikutana nae ananiambia mambo mengi sana ya bamdogo kipindi hiko”
“Kwahiyo na yeye alimvumilia tu! Yani mwanaume analewa hadi anazima, anatembea na rafiki zako wote, bado alimvumilia tu”
“Si alimpenda, tena sio marafiki tu hata ndugu zako ikiwezekana anatembea nao. Unajua ukiona mwanaume wa hivyo tambua kabisa hakupendi kwani mwanaume anayekupenda atawaheshimu ndugu zako, atawaheshimu rafiki zako na atakuheshimu na wewe pia. Yule mmama nilimwambia kuwa basi hakukupenda, ila yule mama anavyoongea kwa uchungu hata nina mashaka nae”
“Ni mama gani huyo?”
“Siku moja nitakuonyesha, nikimuona tu nje ya geti basi nitakuita ili tuongee nae, kiukweli utabaki unamuangalia tu. Ila sijui alinihadithia mimi tu au huwa anawahadithia wengi sijui. Kiukweli siwezi kumueleza bamdogo yale maneno najua atachukia sana”
“Ila kwakweli imenishangaza sana, kwahiyo wewe unanipenda kweli?”
“Vaileth jamani, mimi ninakupenda sana tu, kiasi kwamba hata siwezi kumtamani mwanamke mwingine zaidi yako. Naomba unisamehe na tuanze kurasa mpya ya mapenzi yetu”
Vaileth alitabasamu tu na kumfanya Junior atambue kuwa pale ameshasamehewa kwahiyo ilikuwa ni furaha sana kwake kwani alitamani mno kusamehewa na Vaileth.
.
.
.
.
.
ITAENDELEA ALHAMISI
 
SEHEMU YA 241


Erick na Erica nao walikuwa wakitembea tembea pembezoni mwa maji huku wakichezea maji na kukimbizana, basi Erica akasema,
“Jamani, mimi huwa nikimuona Sarah yupo karibu na wewe basi roho huwa inaniuma sana”
“Kwanini?”
“Hata sijui kwakweli”
“Sikia basi tufanye kitu kimoja”
“Kitu gani?”
“Mimi na wewe tupeane ahadi ya jambo moja ambalo wewe hutolifanya katika maisha yako na mimi sitolifanya katika maisha yangu”
“Jambo gani”
“Iwe hivi, yani mimi nisiwe na rafiki yoyote wa kike zaidi yako yani wewe uwe ndio rafiki yangu na kila kitu kwangu, na wewe usiwe na rafiki yoyote wa kiume zaidi yangu yani mimi niwe kila kitu kwako”
“Unamaanisha hata kuongea nao tusiongee nao!”
“Unaweza kusalimiana nao tu ila ukiona wanaleta maongezi mengi unaachana nao na mimi iwe hivyohivyo, unajua na mimi naumia sana moyo nikimuona yule Bahati na unavyoongea nae vizuri kwakweli naumia sana. Sisi ni mapacha, yatupasa tupendane”
“Kweli kabisa, kwahiyo tule kiapo?”
“Ndio”
“Sasa kiapo hiko tunakulaje?”
Twende pale kwenye ukingo wa bahari nikuelekeze cha kufanya”
Basi Erick na Erica wakaongozana hadi kwenye ukingo wa bahari na kwenda kuelekezana namna ya kula kiapo.

Muda huu Tumaini alikuwa ametoka kwenye shughuli zake ila njiani alimuona Sian a kumfanya asimamishe gari ili aongee nae maana mama Erick alishampigia simu kwa kumwambia kuwa inatakiwa wamshawishi baba Angel kwenda kupima DNA na mtoto wa Sia.
Basi alishuka kwenye gari na kusimama nae nje huku akiongea nae,
“Eeeh Sia, nimesikia ishu za kwenda kupima DNA sijui Erick na mtoto wako, jamani Sia rafiki yangu mbona una makubwa wewe, unajua wazi mtoto sio wa Erick, kitu gani kinakusumbua lakini”
“Tumaini, najua huelewi uchungu ambao upo katika moyo wangu ndiomana unasema hivyo”
“Huo uchungu ni uchungu gani wa miaka hiyo hadi leo! Inamaana wewe huwezi kupata mwanaume zaidi ya Erick, kwani Sia una kasoro gani wewe hadi ukose mwanaume? Unachong’ang’ania kwa Erick ipo siku utakipata”
“Ndio, nataka sana anioe”
“Hilo swala la Erick kukuoa hebu lifute katika mawazo yako, halipo na kamwe halitakuwepo. Unajua na mimi nimeolewa kwahiyo naujua uchungu wa mume, usitake Erica aone ndoa yake chungu eti sababu yako Sia. Hebu acha wenzio wafurahie ndoa yako, sijui umeibuka wapi wewe”
“Sijaibuka ila nampenda sana Erick”
“Oooh tena kabla sijasahau, Erick alinipigia simu kasema…..”
Kabla Tumaini hajamalizia mara kuna mkaka alitokea mbele yao na kumzaba kibao Sia halafu akamkunja pale na kumwambia,
“Wewe mwanamke nataka mtoto wangu, nishapata habari zako unachokifanya kwa mwanangu namtaka”
Tumaini alibaki ameduwaa kwani hakuelewa ni kitu gani kinaongelewa pale.
Kabla Tumaini hajamalizia mara kuna mkaka alitokea mbele yao na kumzaba kibao Sia halafu akamkunja pale na kumwambia,
“Wewe mwanamke nataka mtoto wangu, nishapata habari zako unachokifanya kwa mwanangu namtaka”
Tumaini alibaki ameduwaa kwani hakuelewa ni kitu gani kinaongelewa pale.
Yule mwanaume aliendelea kumkunja Sia na kumfanya Sia aanze kumlalamikia,
“Hebu niachilie jamani, yani huwezi kuongea kistaarabu!!”
“Kistaarabu gani na mwanangu napata habari kuwa umemfanya ombaomba huko”
“Jamani nimemfanya ombaomba wapi una uhakika? Mbona unaongea maneno ambayo huna ushahidi nayo?”
Muda huu Tumaini alisema,
“Mtajuana wenyewe”
Kisha akaingia kwenye gari lake na kuondoka zake.
Kwahiyo Sia alibaki na yule mwanaume akibishana nae,
“Kwanza hebu niachilie halafu ndio tuongee”
Yule mwanaume alimuachilia Sia ili kumsikiliza anasemaje ila muda ule ule Sia alimkimbia yule mwanaume na mbele kupanda pikipiki yani yule mwanaume hakuweza kumpata tena Sia, kitendo hiko Tumaini alikiona wakati akigeuza gari yake na kumfanya ajiulize sana kuwa kuna nini kati ya Sia na yule mwanaume? Ila kwa mawazo yake akahisi kuwa huenda Sia amezaa na yule mwanaume, tena akahisi kuwa huenda Elly ndio mtoto ambaye yule mwanaume anamdai maana mtoto huyo inaonekana Sia kamfanya kitega uchumi, ukizingatia mama Angel alimuelezea kuhusu lile swala la Sia kumtuma mtoto nyumbani kwake kuwa anaumwa, basi moja kwa moja alihisi kuwa yule mwanaume alikuwa akidai mtoto Elly tu kwa Sia.

Muda huu Erica na Erick walivyokubaliana na kumaliza kula kiapo, ila waliona kuwa muda umeendaenda kwahiyo waliona ni vyema wakaungane na wakina Junior ili kuangalia kama watarudi nyumbani muda huo.
Basi waliwafata wakina Junior pale ambao walionekana wamepatana huku wakifurahi sana, basi waliwashtua na kukaa nao karibu ambapo Junior aliwauliza,
“Kheee kwahiyo ndio mshamaliza kutembea tembea!”
Erica akamjibu,
“Kheee jamani, unataka tutembee tembee hadi muda gani? Sisi tushamaliza kilichotuleta huku”
“Kitu gani hicho?”
“Leo tumeamua kula kiapo”
Junior akashangaa,
“Kiapo, kiapo gani”
Basi Erick alikuwa akimtonya Erica asielezee ila Erica hakuona kama kuna tatizo au ubaya wowote na kuanza kuelezea,
“Mimi na Erick tumeamua jambo moja, yani yeye hatokuwa na rafiki mwingine wa kike zaidi yangu, siri zake na kila kitu chake atakuwa ananiambia mimi. Na mimi sitokuwa na rafiki yoyote wa kiume zaidi yake, siri zangu na kila kitu change basi namshirikisha Erick”
Junior na Vaileth waliangaliana kwa mshangao, kisha Junior akasema,
“Hivi hamjui kama ni ndugu nyie!”
“Kwani ndugu hawapaswi kula kiapo?”
“Sijasema hivyo ila nimesema kutokana na aina ya kiapo chenu, nyie ni mapacha hilo sikatai wala sipingi ila sio kwamba ndio mtakuwa kila kitu mnafanya pamoja. Hapo badae Erica utaolewa na Erick ataoa, sasa mtawezaje kuoa na kuolewa bila kuwa na urafiki na wenzi wenu sababu tu mmesema mtakuwa marafiki wenyewe! Hivi mmefikiria hili kwanza kabla ya kula hiko kiapo chenu!”
Erick akajibu,
“Katika maisha yangu sitegemei kuja kuoa”
“Kheee usinishangaze Erick, kwahiyo wewe ni Padri?”
“Na mimi sitegemei kuolewa”
“Kheee nyie watoto mnanivuruga mjue, kwahiyo Erica ni Sister halafu Erick ni Padri, nyie wawapi jamani! Mbona mnanishangaza sana”
“Sasa tunachokushangaza ni kitu gani? Kula kiapo au kitu gani?”
“Ila sio kosa lenu ni utoto tu unawasumbua, najua mkikua na kufikia kwenye rika kama langu basi mtaona umuhimu wa marafiki mbalimbali. Siwashangai sana maana ni utoto tu huo unawasumbua, haya twendeni tukale pale kwenye hoteli halafu ndio turudi nyumbani yani tunafika tukiwa tumeshiba kabisa sio kuanza kutafuta chakula nyumbani tena”
Kisha waliinuka wote na kuelekea kwenye hoteli ya karibu na pale ufukweni ili kupata chakula.
 
SEHEMU YA 242

Muda huu baba Angel akiwa yupo kuzunguka zunguka kwenye nyumba yake ili kuangalia maeneo ya bustani yake vizuri, akapigiwa simu na dada yake na kuanza kuongea nae,
“Jamani Erick, leo njiani si nikakutana na Sia halafu akaanza zile mada zake za mtoto ila Mungu si Athumani jamani akatokea mbaba yule sijui wa wapi, akamzaba vibao Sian a kumkunja huku akimdai mtoto wake, yani mwanamke mbaya yule jamani! Kutaka kutudanganya tunaona hivi ndio nini!”
“Kwahiyo na wewe ulikuwa unaamini kuwa mtoto ni wangu?”
“Hapana, mimi nilikuwa siamini na ndio nilikuwa naongea nae anakazana tukapime DNA ndio mara katokea huyo mbaba, jamani Sia yule asipoangalia anafia kwenye mikono ya watu halafu sijui alimponyokaje yule baba maana tu nilimuona akipepea na bodaboda, jamani Sia kawa mbaya sana”
“Ila ni vizuri umetambua hilo dada yangu maana nilikuwa naumia sana kuona mnamuamini yule mjinga”
Tumaini aliongea na ndugu yake kwa furaha sana, na ile simu ilipokatika basi baba Angel alienda kumpelekea mama Angel ujumbe ule na kumfanya mkewe ajihisi vizuri sana kwani siku zote alihisi kuumizwa kichwa sana na Sia, kwahiyo kupata habari kama hiyo kwake ilikuwa nafuu sana.
“Mke wangu, kesho nitaenda kazini ila nitawahi kutoka na kwenda kumuona Angel kwa mama”
“Oooh utakuwa umefanya jambo jema sana mume wangu, nashukuru kwa hilo”
Basi waliongea pale huku wakipanga ratiba vizuri tu.

Muda huu ndio wakina Junior walikuwa wanarudi nyumbani, na kweli walishashiba kwahiyo walifika tu na kuwashuku wazazi wao kwa kuwaruhusi siku hiyo kwenda kutembea na moja kwa moja walienda kulala kwani kila mmoja alikuwa amechoka sana ila kama kawaida leo Junior aliweza kwenda chumbani kwa Vaileth tena maana walikuwa wamepatana, basi akamwambia,
“Nakuomba kitu kimoja mke wangu, tuaminiane yani mimi na wewe tuwe letu moja”
“Ila kuna jambo mimi nataka”
“Jambo gani?”
“Erica na Erick ni mapacha ila wamekula kiapo cha kuwa marafiki wao wawili tu daima na milele, tumewaponda ila kiukweli nimependa maamuzi yao. Basi nilikuwa naomba mimi na wewe tule kiapo pia cha kuwa pamoja milele na kutokusalitiana yani usinisaliti na nisikusaliti”
“Hakuna tatizo mke wangu, tutakula tu hiko kiapo”
“Ndio tule muda huu, ni kiapo cha damu”
“Mmmh jamani Vai, mambo gani hayo yakutoana damu tena! Unajua mimi ni muoga sana, tutakula kiapo kama cha wakina Erick”
“Sasa mpaka twende ufukweni ni lini tena! Wakati kiapo cha damu ni rahisi tu hapa”
“Mke wangu napenda sana tule hiko kiapo ila mimi ni muoga sana kutobolewa na kitu yani nikiona damu inatoka basi Napata hofu maradufu, nakuomba mke wangu niamini halafu mimi na wewe tutakula tu kiapo. Amini nakupenda sana Vaileth, leo tumechoka sana mama njoo tulale, maswala ya viapo tutakula tu hakuna tatizo”
Basi Junior akafanya kumpapasa pale Vaileth ili asahau ile ajenda yake na kweli mwisho wa siku waliamua kulala tu.

Kwenye mida ya saa nne asubuhi, Angel akiwa na bibi yake basi bibi yake kulikuwa na watu anahitaji kuwasalimia ila simu yake haikuwa na salio hivyo ilimbidi amuagize Angel kununua vocha, kwakweli Angel alifurahi kwa kiasi Fulani aliyapenda maisha ya kwa bibi yake ingawa kuna muda huwa anakosa raha sana ila aliyapenda maisha yale sababu hata alikuwa anapata uhuru wa mwenda dukani, kwaniyo kwake ilikuwa ni furaha.
Aliondoka muda huu na kuelekea dukani alikotumwa na bibi yake, moja kwa moja alienda kununua vocha ila alipotoka tu kununua vocha alishikwa bega akashtuka kugeuka akamuona yule Ally ambaye ni dereva bodaboda, kwakweli alimshangaa sana na kusogea pembeni huku akisalimiana nae,
“Kheee Ally, umefikaje huku?”
“Hata mimi sijui nimefikaje huku ila nadhani ni kusudi la Mungu ili mimi na wewe tupate kuonana”
“Kheee!”
“Kweli Angel, nilikuwa naumia sana kwa kutokukuona maana furaha yangu ni kukuona tu kwahiyo swala la kutokukuona lilikuwa linaniumiza sana”
“Oooh pole, mimi nawahi nyumbani nampelekea bibi vocha”
Basi Angel akawa anaondoka huku Ally akimfata nyuma na kumuongelesha,
“Kwahiyo unaishi huku siku hizi!”
“Ndio, naishi na bibi yangu”
“Natumai bibi yako hatachukia nikimfahamu”
“Mmmh sio leo, hapana jamani usiniletee matatizo bure”
“Kwanini?”
“Kwanza bibi yangu hapendi kabisa niwe na marafiki wanaume, kwahiyo nisamehe tafadhali”
Angel alifika kwa bibi yake na kuingia na moja kwa moja kumpelekea bibi yake vocha ambaye alimuuliza kidogo,
“Mbona umechelewa Angel, ulisimama na wanaume eeeh!”
“Hapana bibi”
“Maana mkishaona mna rangi rangi na vinywele vya kuongopea wenzenu basi ndio mnajifanya mnamiliki dunia sababu ya kujiona nyie ndio wazuri dunia nzima. Angel mjukuu wangu, sifa ni ile tutakayokupa sisi tu na si mtu wa njiani, atakwambia mzuri kumbe anakusabifu, sisi tukikusifia inatosha mjukuu wangu. Haya niwekee hiyo vocha na uniungie kifurushi”
Basi Angel alifanya hivyo ila alipomaliza alituma ujumbe kwa Samir,
“Nimekumiss sana Samir, ila bibi bado hajanipa simu yangu. Akinipa nitakushtua ili tuwasiliane, usinijibu hapa maana hii simu ya bibi”
Akamtumia na kuifuta ile meseji kisha kumpa simu bibi yake ambapo alianza kuitumia kwa kuwapigia aliotaka kuwapigia.
 
SEHEMU YA 243

Baba Angel leo akiwa ofisini tu, muda kidogo akafatwa na madam Oliva ambaye alikuwa akilalamika kwanza,
“Jamani baba Erick, kumbe jana ulipanga kutokuja ofisini! Basi mwenzio nikaja nikakukosa, niliumia moyo ujue!”
“Oooh pole sana, ulikuwa na ujumbe gani madam?”
“Nina ujumbe basi!! Nilikuwa nataka kukusalimia tu, yani mimi huwa napenda sana kuongea na wewe maana wewe ni mwanaume ambaye una maneno yenye busara sana, halafu huwa unanipa moyo sana yani nikiongea na wewe basi najihisi vizuri kwenye moyo wangu”
“Nafurahi kusikia hivyo, karibu sana”
“Asante, leo una ratiba gani? Maana nilitaka twende kwangu ukapafahamu”
“Madam tutaenda siku nyingine, maana leo nahitaji kwenda kumuona mwanangu kwa bibi yake”
“Sawa hakuna tatizo, mwanao huyo ni wa kike au wa kiume?”
“Ni wa kike, anaitwa Angel”
“Oooh nimefurahi kufahamu hilo swala, basi ni hivi ngoja nitoke kidogo halafu nitarudi muda sio mrefu naomba usiondoke kabla sijarudi”
Basi madam Oliva aliondoka, kiukweli baba Angel hata hakujua ni kitu gani huyu madam anahitaji kufanya, kwahiyo yeye aliendelea na kazi zake tu kama kawaida.
Muda kidogo madam Oliva alirudi akiwa na kimfuko na kumkabidhi baba Angel, kisha akamwambia,
“Humo kuna zawadi ya Angel, naomba usifungue yani mpelekee Angel mwenyewe kisha umwambie kuwa umepewa na madam Oliva”
“Asante sana kwa kumkumbuka mwanangu”
“Yani mimi kwa jinsi ninavyokuona hadi naona watoto wako wote kama watoto wangu jamani. Ila hakuna tatizo, sema tu kumbuka hilo kuwa mfikishie zawadi yangu hiyo Angel”
“Nitaifikisha madam, hakuna tatizo lolote”
“Haya, mwambie Angel kuna siku ataniona naamini atanipenda sana”
Madam alikuwa akiongea haya huku akitabasamu kwani alijihisi raha sana kwenye moyo wake na alitamani watoto wote wa baba Angel wampende yeye ili kama atazungumza nao chochote kile wapate kumsikiliza na kumuelewa.
Basi baba Angel nae aliinuka pale kwani aliona kuwa muda wake umefika wa kwenda kumtembelea mama mkwe wake kama alivyopanga, kwahiyo waliachana na madam Oliva nje ya ofisi halafu moja kwa moja baba Angel alipanda kwenye gari na kuondoka zake.

Fetty leo ndio aliweza kumshawishi mumewe ili waende kwa mama Erica yani bibi Angel maana alishamshauri muda kufanya hivyo ili wakapate ushauri wa ziada.
Basi walijiandaa na kutoka ambapo moja kwa moja walienda mpaka kwa bibi Angel na kufika mpaka mlango wa mbele ya nyumba hiyo na kubisha hodi huku mume wa Fetty akisema,
“Ila pamebadilika sana siku hizi”
“Lazima pabadilike ni muda mrefu umepita”
Basi walifunguliwa mlango na Angel na kukaribishwa ndani, walimkuta bibi Angel amekaa na mgeni ambaye alikuwa ni baba Angel ila kiukweli mume wa Fetty alipomuona huyu mtu yani baba Angel alijihisi vibaya sana moyoni, basi waliingia na kuwasalimia na kuongea mawili matatu baada ya muda mume wa Fetty alitoka nje na aliporudi ndani alisema kuwa kuna mahali kaitwa kwahiyo ilibidi tu awaage, kwahiyo hata mkewe hakuwa na namna zaidi zaidi ya kuongozana nae tu.
Bibi Angel aliwaambia pale,
“Jamani, Fetty ungebaki jamani, si ni yeye ndio anawahi!”
“Aaaah mama usijali, tutakuja siku nyingine yani lazima tuje, usijali mama”
Basi wakaagana nao pale na moja kwa moja walitoka na kwenda kupanda gari yao na kuondoka ila njiani mume wa Fetty alinza kusema,
“Na bahati yako hujakubali kubaki maana ungekubali ndio ungenieleza ajenda yako vizuri”
“Ajenda kivipi?”
“Unafikiri yule Erick namuamini basi! Sina imani nae”
“Huna imani nae wapi? Si useme tu ukweli kuwa bado unampenda Erica, hivi lini Bahati akili yako itakuwa kawaida jamani! Unajua siku ya harusi ya Erick na Erica ulitoa risala ambayo binafsi nilifurahishwa nayo na kuona ni kweli mume wangu kawa muelewa sasa, yani ulitoa risala nzuri sana kama mwalimu wa mapenzi ila leo hii wewe ndio wa kuwaonea wivu Erick na Erica kweli!”
“Aaaah hapana, sio hivyo ingawa ni kweli Erica nilimpenda”
“Basi ule upendo ambao ulikuwa nao kwa Erica uonyeshe kwangu, unashindwa nini? Au ngoja nikuulize ni kitu gani kinakufanya umpende Erica hadi leo yani hadi mume wa Erica pale umuonee wivu maana naelewa wazi kuwa huna safari wala hujaitwa popote ila umeona tuondoke tu”
“Ni kweli mke wangu hata sio utani, yani nilipomuona Erick tu nimeshangaa kuwa sipendi tena kuwa eneo hilo kabisa, nisamehe kwa hilo tafadhari”
“Haya niambie, ni kitu gani kinakufanya uone wivu au ni kitu gani kinakufanya umpende sana Erica mpaka ushindwe kumsahau”
“Nadhani sijawahi kukwambia haya, ni hivi. Mimi kwa Erica nilikuwa ni mwanaume wake wa kwanza kabisa, hiyo inaonyesha jinsi gani Erica alijitunza kwaajili yangu, hiko kitu kinafanya nimpende sana Erica na nishindwe kumsahau”
“Wewe ulijuaje kuwa ulikuwa mwanaume wa kwanza kwa Erica?”
“Yani siku namuingilia, Erica alikuwa akilalamika maumivu tu, na Erica hakujua mambo yoyote ya mapenzi, kwakweli najivunia kuwa mwanaume wa kwanza kwa Erica”
“Mmmh! Kwahiyo roho ikakuuma sana kunipata mimi gumegume”
“Hapana mke wangu sina maana hiyo”
“Haya kingine”
“Kingine ni kuwa, mimi kwa hali niliyokuwa nayo mwanzoni ilikuwa ni ngumu sana kukubaliwa na mwanamke mrembo kama Erica, ila Erica alikubaliana na hali yangu na kuwa na mimi na huo ni upendo wa dhati alionionyesha, sikuwa na kitanda mimi ila Erica alikubali kulala na mimi kwenye godoro chini, vitu vingi sana sikuwa navyo ila Erica alinikubali na umasikini wangu. Kitu kingine, Erica aliniambia wazi, anapenda mwanaume wake awe hivi na vile na vile ila kwakuwa mimi sikuwa na pesa basi kuna mambo mengine nilitamani kuyafanikisha lakini nilishindwa ila asilimia tisini ya mafanikio yangu katika maisha basi imefanikishwa na Erica, alianza kuninunulia vitu vya ndani ya nyumba na kufanya chumba change kivutie, Erica alinipa mtaji wa kufuga samaki, Erica alinipa mtaji wa kufuga kuku, Erica alinipa mtaji wa kufungua lile duka langu kubwa la samaki na kuku, kwakweli siwezi kumsahau Erica katika maisha yangu. Hapo ndio msemo wanaosema kwenye mafanikio ya mwanaume basi mwanamke yupo nyuma, nauona kuwa ni kweli maana mafanikio yangu yamewezeshwa na Erica. Sasa roho iliniuma kipindi nimekuwa na pesa, na mimi naweza kutembea kwa kujitapa nikamuona jamaa Erick kaniibia mwanamke aliyenitengeneza kwa muda mrefu!! Kwakweli roho iliniuma sana. Nisamehe mke wangu ila siwezi kuficha hili, nampenda sana Erica”
Fetty akapumua kidogo na kumwambia mumewe,
“Unampenda sana, ila kumbuka hata yeye anampenda sana Erick na ndio kaamua kuolewa nae na kweli wanapendezana hata upendo wao tunaweza kuuona machoni. Hata kama Erica alikupenda basi hakuweza kukupenda kama ambavyo amempenda mume wake. Kuhusu kukutengeneza kimaisha, Mungu alijua ni kwanini Erica kafanya vile maana kumbe alikutengeneza kwaajili yangu”
“Ushaanza kujipigia debe, yani kuna mambo nakumbuka na moyo unaniuma sana. Ile nyumba yangu niliyoamua kupangisha, basi ile nyumba ndio niliyojenga ili niishi na Erica, kiukweli bila fitna za ndugu zangu basi kwasasa Erica angekuwa mke wangu”
Fetty hakutaka kuongeza neno kwa hapo kwani alijua maneno mengine atakayoongea mume wake yatamkarahisha tu.
 
SEHEMU YA 244

Baba Angel alipomaliza yale maongezi, akaenda kuitoa ile zawadi aliyokabidhiwa na madam Oliva na kumpa Angel ila Angel alifurahi sana

maana huyu mtoto alikuwa na kawaida ya kufurahi na alipenda sana kufurahi kwahiyo yeye alifurahi kabla hata ya kujua kuwa ni zawadi

gani ambayo imewekwa kwenye mfuko.
Basi kwa muda huo baba Angel aliwaaga na kuondoka zake. Angel alienda chumbani kwake ili kuangalia ule mfuko umebeba vitu gani,

kwanza alikuta kitabu kimoja kidogo halafu alikuta hereni, cheni na bangili. Basi akakisoma kile kitabu kidogo ambacho kiliandikwa juu
“Mtoto wa kike jithamini, wewe ni wa thamani sana”
Yale maneno yalimvutia na kujikuta akianza kusoma, kile kitabu kilielezea namna ya mtoto wa kike anavyopaswa kuwa msafi na namna

ambavyo wanaume wanaonyesha tamaa kwa watoto wa kike, basi alikuwa akisoma na kwenda nacho kwa bibi yake na kumuonyesha,

kwakweli alipomsomea kidogo tu bibi yake nae alipenda sana na kuuliza,
“Ndio nani kakupa mjukuu wangu?”
“Baba kasema ni madam Oliva”
“Natamani kumfahamu kwakweli, amefikiria nini kukuletea kitabu kama hiki!! Jamani Angel maneno yangu hayakukai, umeletewa kitabu sasa

na kama bado maneno yake hayakukai basi hapo sijui ni shetani gani atakuwa kwako”
Angel alitabasamu tu, na bibi yake akasema tena,
“Labda shetani mwenye vichwa saba, ila nitaongea na baba yako kuwa atuletee huyo madam Oliva tumfahamu”
“Oooh bibi, tena nina hamu kweli ya kumfahamu ngoja nikakuonyeshe vingine alivyoniletea”
Angel alienda kumletea bibi yake ambaye aliviangalia vile vitu na kuvipenda sana huku wakimsifia madam Oliva kuwa ni mtu mzuri sana.

Baba Angel anarudi nyumbani kwake na kumuelezea taarifamkewe kuhusu sehemu aliyotoka, yani mama Angel akafurahi sana kwa

mumewe kuitimiza hiyo ahadi, kitu pekee ambacho baba Angel hakukisema ni kuhusu kumpelekea Angel zawadi iliyotoka kwa madam Oliva,

hakuona umuhimu wa jambo lile ndiomana hakusema wala nini, baada ya hapo aliulizia mambo ya watoto,
“Eeeeh watoto hapa nyumbani wameshidaje?”
“Uuuh leo maajabu, jamani baba Angel huwa huna kawaida ya kuulizia hali ya watoto kabisa, yani leo ni maajabu yamefanyika,,

wamwshinda salama mume wangu hawajambo”
“Oooh jana si walienda ufukweni nikajua Erica kakuletea mada za huko”
“Halafu namshangaa safari hii hajaja kusema, yani Erica hata angeona mchanga unagongana anagekuja kusema. Hivi huyu mtoto katoa

wapi hizi tabia za umbea jamani! Yani hadi huwa nashangaa na kujiuliza sana. Unajua kwetu hawapo watu wa namna hii na kwenu pia, sasa

Erica kaitoa wapi tabia hii ya umbea?”
“Hilo hilo jambo ilitakiwa mimi ndio niwe nashangaa ila sio wewe mama Angel jamani, yani wewe hata usingeshangaa ila tu ungemuweka

mtoto vizuri asizungumze umbea kupitiliza maana itafikia hatua atatoa siri zake mwenyewe”
“Kwahiyo katoa wapi umbea hadi unasema wewe ndio wa kuniuliza mimi?”
“Kwani Derrick yukoje jamani! Yani Derrick ni mbea sana tena Derrick ni mbea na muongo, tumuombee tu Erica asianze uongo na huo

umbea apunguze maana atagombanisha watu. Yani wewe muangalie ndugu yako Derrick vizuri, angalia umbea aliokusambazia wewe tena

Derrick ni mtoto wa kiume kumbeka, ila Erica ni mtoto wa kike. Yani kwenye ukoo wenu huko lazima kuna mtu yuko hivi ndio anarishisha

hawa watu”
Mama Angel alisikitika kidogo kwani alimkumbuka huyu ndugu yake Derrick ambaye hadi sasa hawapatani sababu ya mambo ambayo

Derrick amemfanyia, basi akasema,
“Ila kweli, sema mwanangu asiwe kama Derrick jamani! Unajua yule Derrick ilivuka mipaka jamani!”
“Ni wewe kukaa chini na Erica na kumwambia cha kusema na kutokusema, ila naona ameanza kukua maana jana alivyotoka ufukweni tu

angekuja kukueleza kila kitu kilichotokea”
“Ila mimi huwa napenda sana ambavyo anasema maana kuna mambo yamejificha ila Erica ananiletea habari na kunifungua macho”
“Aaaah kumbe unapenda umbea wake eeeh!”
Mama Angel alicheka pale kwani kuna baadhi ya maneno ya mwanae aliyaona kuwa yapo sawa kabisa.

Kulipokucha, mapema kabisa baba Angel alienda zake kwenye kazi yake na kuanza kufanya kazi zake basi alikuwa pale kwenye kazi muda

wote, na kama kawaida yake yani alisahau hata kula kwa muda huo maana alijiona kuwa kuna kazi lazima aimalize kwanza na kweli

alifanya juu chini hadi aliimaliza.
Ila alipoimaliza tu, alifika madam Oliva, yani kama alivizia vile kuwa muda huu baba Angel atakuwa kamaliza kazi, basi alimsalimia pale na

kumwambia,
“Jamani, hivi na leo umekula kweli?”
“Aaah kuna kazi iliniweka busy sana siku ya leo, hivyobasi hata kula sijala ila hakuna tatizo sababu muda sio mrefu narudi kwangu kwahiyo

nitakula nyumbani”
“Aaaah jamani, nimekuletea matunda haya”
Basi madam Oliva alitoa yale matunda na kumpa baba Angel, ila kiukweli baba Angel alikuwa akipenda sana matunda basi alimshuru pale

na kula yale matunda, huku wakiongea ongea,
“Leo baba Erick nahitaji ufike nyumbani kwangu ili upafahamu. Nakuomba sana”
“Aaaah madam Oliva sio kwa leo”
“Lini sasa jamani baba Erick? Wewe mwenyewe muda wako unajua jinsi ulivyo, mimi nitakufahamisha kwangu lini? Unajua binadamu ni

kufahiana eeeh! Yani inatakiwa ufahamu kwangu kama nilivyofahamu kwako. Nakuomba tafadhari ufike kwangu leo”
“Ila sitakaa sana”
“Hamna tatizo yani swala la wewe kufika tu kwangu linatosha”
Baba Angel alikubali na baada ya muda kidogo aliinuka na kufunga ile ofisi yake kisha kuondoka na madam Oliva.
 
SEHEMU YA 245

Wakiwa njiani na madam Oliva alimuona mtu kama Sia kwenye bodaboda tena ikienda kwa kasi sana ila hakutilia maanani ukizingatia huwa

anakerwa sana na mtu huyu, kwahiyo aliendelea tu na maongezi na madam Oliva basin a mwisho wa siku walifika hadi kwa madam Oliva.
Aliweza kuiona nyumba ya madam huyu ambayo ilikuwa ni nzuri ila ndani hapakuwa na mtu mwingine yoyote zaidi ya mlinzi ambaye alikuwa

getini yani madam Oliva ndani ya nyumba yake hapakuwa hata na msichana wa kazi, basi baba Angel akauliza,
“Mbona kimya hivi? Wanao wako wapi?”
“Nina mtoto mmoja tu, ila bibi yake huwa anamng’ang’ania sana, kwahiyo yupo kwa bibi yake na hapa naishi mwenyewe tu”
“Aaaah nimekuelewa hapo”
Basi madam Oliva alimkaribisha baba Angel sebleni na kwenda jikoni kuleta juisi ili waweze kunywa kidogo ila muda huo alivyoenda kuleta

juisi baba Angel alipigiwa simu na Steve na kufanya aipokee,
“Bosi, ni hivi. Sia alikuja tena dukani leo ila kilichotokea sasa ni kimoja kuna wale walinzi uliwaweka na kusema kuwa Sia asiingie dukani

kabisa, basi walimzuia ila Sia alisisitiza kufanya hivyo na wale walinzi wamempiga Sia ameanguka hata sijui imekuwaje maana hatingishiki”:
Ile habari kidogo ilimshtua sana baba Angel na muda huo huo akasimama na kutoka nje ya nyumba ile.

Basi madam Oliva alimkaribisha baba Angel sebleni na kwenda jikoni kuleta juisi ili waweze kunywa kidogo ila muda huo alivyoenda kuleta

juisi baba Angel alipigiwa simu na Steve na kufanya aipokee,
“Bosi, ni hivi. Sia alikuja tena dukani leo ila kilichotokea sasa ni kimoja kuna wale walinzi uliwaweka na kusema kuwa Sia asiingie dukani

kabisa, basi walimzuia ila Sia alisisitiza kufanya hivyo na wale walinzi wamempiga Sia ameanguka hata sijui imekuwaje maana hatingishiki”:
Ile habari kidogo ilimshtua sana baba Angel na muda huo huo akasimama na kutoka nje ya nyumba ile.
Kiukweli alitoka nje na kuondoka akielekea dukani kwake ambapo kaambiwa kuwa kuna tatizo, basi madam Oliva muda huo alitoka jikoni na

glasi za juisi ila hakumkuta baba Angel, ikabidi akamuulize mlinzi wake ambaye alisema kuwa yule mgeni kaondoka zake, basi madam Oliva

alirudi ndani na kupiga simu ya baba Angel na kuanza kuongea nae,
“Jamani baba Angel ndio hata kuaga hakuna!”
“Aaah samahani madam, kuna tatizo kidogo limetokea ndio naenda kushughulikia”
Kisha baba Angel akaikata ile simu kwakweli madam Oliva hakujihisi vizuri kabisa na muda huo alimpigia rafiki yake simu,
“Jamani shoga yangu kumbe kumpata mume wa mtu ndio kazi hivi!!”
“Kivipi!! Kwanza kabisa hakuna mwanaume rahisi kumpata kama mume wa mtu sababu wengi wao huwa wanakuwa na stress za kutosha

walizopewa na wake zao”
“Jamani huyu mume wa mtu ananipa mawazo haswaa, leo nimekuja nae hadi nyumbani basi nikaenda kufanya vile ulivyosema, nafika

sebleni hayupo kumbe kapata dharula kaondoka, jamani dharula gani muda huu huu!”
“Uikate tamaa madam, hiyo moja imeshindikana ila endelea kujaribu”
Aliongea na mwenzie pale aliyeonekana kumpa ushauri mbalimbali.

Basi baba Angel alifika dukani na kuulizia kuwa Sia yuko wapi, alikuta wamemuhifadhi mahali kwani pale waliogopa watu wangeweza kujaa,
“Mmmmh nyie mbona mna akili mbovu hivyo, yani mtu alianguka halafu nyie mmenda kumuhifadhi mahali? Akitufia huko je! Hata kama

nilisema mumfukuze ila sio kwa stahili ya kumpa kipigo mpaka kuzimia”
“Ila bosi, hatujampiga hivyo unavyodhani!”
Baba Angel alichukia, ingawa hakumpenda Sia ila bado hakupenda yeye awe chanzo cha kifo cha Sia, kwahiyo alichukia sana,

akaonyeshwa sehemu waliyomuweka Sia na hapo alimbeba na kumpeleka kwenye gari yake kisha na yeye akapanda ili aelekee nae

hospitali.
Wakati gari inaondoka akamsikia Sia akiongea,
“Habari yako Erick”
Baba Angel alishtuka sana hadi alisimamisha gari pembeni na kuita,
“Sia!!”
“Ndio ni mimi ulidhani imekuwaje?”
“Umenishtua sana”
“Kheee ulidhani nimekufa! Hapana sijafa, bado nipo hai”
“Sasa ilikuwaje kwani?”
Kwavile baba Angel alimlaza Sia siti za nyuma ya gari, kwahiyo Sia akaruka na kukaa ile siti ya mbele ili aonane nae vizuri zaidi, kisha

alianza kuongea nae,
“Unajua sikujua kama bado utanijali kiasi hiki baada ya yote yale”
“Sikuelewi”
“Huwezi ukanielewa, ni hivi. Mimi sikuzimia kama kuzimia ila nilikuwa nimeigiza tu, na nilijua kuwa wale vijana watafanya vile ila nilikuwa

namuomba Mungu ukipigiwa simu basi ufanye hima kufika. Unajua wale vijana wamenizaba kibao kimoja tu, kiukweli siwezi kuzimishwa kwa

kibao kimoja labda kama kuna namna nyingine”
“Kwahiyo Sia ulikuwa unaigiza kuzimia ili iweje?”
“Sikia nikwambie Erick, unajua mimi huwa nakufatilia sana. Ipo hivi na huwezi kuibadilisha. Mimi sio adui yako na wala sio adui wa Erica,

mna maadui wengine tu ila sio mimi na kama kutumiwa na maadui zenu basi nilitumiwa mwanzoni. Mimi siwezi kumuumiza mtoto wako, bora

hata mtoto wa Erica”
“Unamaanisha Angel!”
“Nimesemea tu, ila mimi siwezi kumuumiza mtoto wako wa aina yoyote. Kuna vitu vingine nafanya vinakukera haswaa, sema kuna wakati

mwingine nakuwa na uhitaji wa pesa ndiomana nafanya vile. Nilikwambia kuwa Erick ni mwanangu hujawahi kuniamini, nikasema Elly

nimezaa na wewe hujataka kuniamini wala sihitaji uniamini wala nini kwani sina ugomvi na wewe ila mara nyingine ni pesa inanitesa sababui

sina pesa. Ila kwasasa ningeomba basi umuhudumie Elly kama unavyomuhudumia Angel yani uwe unamsaidia tu, mbona Angel unajua fika

sio mwanao lakini unampenda, unamjali, unamthamini na kumlinda! Naomba iwe hivyo na kwa Elly pia”
“Unajua wewe mwanamke una wazimu, kwahiyo Elly mwanangu sio mwanangu?”
“Aaaah tusiongee hayo kwa wakati huu hata nikikwambia hutonielewa”
“Sikia kwanza, kuhusu swala la Angel natambua wazi kuwa sio wangu ila nilishamkubali yule mtoto toka mdogo na nilimwambia mama yake

kuwa Angel nitamlea siku zote kama mwanangu na siku zote ataishi hivyo na ndugu zangu wote hata waseme kitu gani ila wanatakiw

akukubaliana na kauli yangu kuwa Angel ni mwanangu. Mwanzoni walisema sema hadi kutaka nikapime damu na Angel sasa nipime damu

gani wakati ukweli naujua? Ila mimi nilibaki na msimamo wangu kuwa Angel ni mwanangu na maisha yanataka uwe na msimamo. Ila wewe

naona upo kujikanyagakanyaga, mara Erick mwanao tukikuuliza kivipi unajiuma uma, mara Elly mwanangu na sasa umekuja na hoja mpya

sijui nimsaidie Elly kama ninavyomsaidia Angel. Dah! Wewe mwanamke wewe aliyekuroga kiukweli amekufa jamani. Kwahiyo hiko kitu cha

kuomba msaada kuhusu Elly ndio kilikufanya uzimie?”
“Hapana, hiko wala kisingenifanya nizimie kwani ningejua ni wapi pa kukuvizia hadi tukaongea pamoja, ila kilichonifanya nifanye hivi ni hiki.

Nilikuona wewe na yule madam mnaondoka na kwa haraka haraka nilihisi tu mnaenda nyumbani kwa yule madam, inawezekana hujui au

unajifanya hujui wakati dalili zote zinaonekana, yule madam anakutaka Erick ndiomana yupo karibu sana na wewe. Nimefatilia muda,

anakuletea matunda sijui nini, anawapeleka wakina Erica kusuka, anakupa zawadi umpelekee Angel, nimemfatilia sana, utajua wewe ni

muda gani nimetumia kumfatilia ila nilishamfatilia sana. Na nilishawahi kumsikia akiongea na mwenzie yani mwenzie alikuwa akimpa mbinu

ya kukupata wewe kuwa ukienda nae kwake akuleweshe kisha ungelala nae na yeye ingekuwa ndio njia moja wapo kwanza ya kukupata

maana ukilala nae sasa ndio ataanza kufanya mazoea ya kulala nawe mara kwa mara”
“Mmmh!”
“Ndio hivyo, kwahiyo nilivyokuona nikaona njia pekee ya kufanya ni kujifanya nimeenda kufanya fujo dukani kwako kwani naelewa wazi

kuwa umeweka walinzi kwaajili yangu nami nilijifanya nataka kuingia kwa nguvu basi wakanizaba kibao nami nikazimia ila dah kibao

kinauma kile, wale walinzi wamekomaa sana.”
Baba Angel alicheka kidogo na kutikisa kichwa maana huyu mwanamke kiukweli alikuwa akiumiza sana kichwa chake, kisha Sia aliendelea

kuongea,
“Basi ndiomana nikafanya vile sababu nilijua wakikutaarifu utakuja na kuachana na yule mwanamke. Erick ngoja nikwambie kitu, kipindi upo

na mimi ulikuwa ni mwanaume muhuni sana, ulikuwa na wanawake wengi na wengine nakufumania nao kitandani ila bado nilivumilia, ila sio

kwamba niliipenda ile hali sikuipenda hata kidogo sema tu nilivumilia sababu nakupenda. Namfahamu Erica alivyo, nafahamu udhaifu wake,

pia nafahamu kuwa Erica anapenda sana kulia. Jamani aje agundue kwasasa upo na yule madam utamfanya mwenzio alie hata siku mbili

kama ana msiba vile, ukizingatia kwake unaishi kama mwanaume wa tofauti kwani umebadilisha tabia zote na wala hawezi kukuhisi vibaya,

ila gafla sikie mumeo anatoka na yule madam kiukweli ataumia sana na utamuweka kwenye wakati mgumu sana, ndiomana mimi nikafanya

vile kukuokoa wewe na kuokoa ndoa yenu. Mimi nilikuomba unioe ila sikukuomba uachane na Erica, ila najua pia kuwa swala hilo ni gumu

kutokana na mlivyokubaliana wakati wa ndoa kuwa ndoa yenu ni ya mke mmoja na mume mmoja, ila ombi langu mimi ni ndoa tu. Sema

tuachane na hilo kwanza, ila tuongelee hili la leo, kwahiyo hiko ndio kitu kilichotokea, nisamehe bure, nisamehe kwa kukukwaza ila sikuwa

na jinsi zaidi ya kufanya hivyo”
“Sasa madam Oliva alitaka anileweshe na kitu gani?”
“Sijui ila alitaka kukulewesha, na ungelewa tu basi kwisha habari yako, kwanza yule madam ana uchu wa muda mrefu sana. Ungelewa

wewe mbona ingekuwa balaa humo ndani, na ninavyokufahamu ukilewa mmh! Sema umeacha pombe tu siku hizi”
“Hebu acha habari zako hizo, ila hata sijui niseme kitu gani? Haya cha kukusaidie kwasasa nitakurudisha tu kwako”
Sia alifurahi sana, na muda huo huo alianza kumuelekeza baba Angel nyumbani kwake ambapo ni kweli baba Angel alimfikisha Sia hadi

nyumbani kwake na hapo palikuwa na Elly ambaye aliona lile tukio na kumfanya atabasamu pia, kwani alikuwa akiumia sana kuona hakuna

hata mwanaume anayeongozana na mama yake, kwahiyo alivyomuona vile mama yake alifurahi sana huku akijisemea,
“Hata kama baba yangu amekufa, ni heri mama akanipatia baba wa kambo kama hivi”
Basi Sia alipokuwa anashuka alimwambia baba Angel,
“Ila Erick samahani, hapa ndani kwa siku ya leo kidogo biashara zangu hazijaenda vizuri na sina chakula”
“Unajua kuna kipindi una wazimu wewe mwanamke”
“Jamani, kwanini Erick?”
“Haya, unahitaji mtaji wa kiasi gani ili kuboresha biashara yako na uache kuisumbua familia yangu”
“Ningepata milioni moja, ingenisaidia sana”
“Basi subiri hapo nitakuja muda sio mrefu”
Sia alishuka na baba Angel muda huo alienda hadi benki na kutoa pesa kisha akaweka kwenye bahasha na kumpelekea Sia kisha

akamwambia,
“Sihitaji tena kuona ukiisumbua akili yangu au familia yangu”
“Ila naomba usinikataze kufatilia kama kuna wanawake wanaokuvizia kama madam!”
“Dah! Unajua wewe jamani! Usiniumize kichwa, yani acha kunifatilia kabisa. Kwaheri”
Baba Angel alirudi kwenye gari yake na muda huo moja kwa moja alienda nyumbani kwake.
 
SEHEMU YA 246

Kwakweli, leo Sia alikuwa na furaha sana hadi Elly alifurahi pia jinsi mama yake alivyokuwa na furaha basi akaongea nae,
“Mama, leo nimefurahi sana jinsi ulivyofurahi. Sikutoka nje kumsalimia yule mgeni ila kama namfahamu hivi! Nitambulishe mama”
“Ni kweli unamfahamu, yule ni baba yake Erica”
Elly akashtuka kidogo kwani hakufahamu kama yule ni baba yake Erica wala nini ila kawahi kuonana nae mara kadhaa, kisha alimuuliza

mama yake,
“Mama, lakini si ulisema ile familia ya wakina Erica ni ndugu zetu lakini wanakuchukia kumbe hawakuchukii?”
“Ni hivi mwanangu, huyu baba hana roho mbaya hata kidogo ila mke wake kuna muda anakuwa kama mwendawazimu. Leo nimefurahi sana

kukutana naye”
“Nakuona mama”
Kisha Sia alitoa ile bahasha na kuweka zile hela kitandani na kuanza kuzihesabu, kwakweli alichekelea sana na kusema,
“Oooh furaha yangu ya leo, nitaipumzisha ile familia kwasasa hawatoniona maana nitakuwa makini na shughuli zangu. Oooh kumbe kanipa

milioni tatu na laki tano!! Aaaah nimefurahi sana”
Elly nae alifurahi sana maana kile kitendo cha kumuona mama yake akiwa na furaha kilimfanya afurahi pia kisha akamuuliza,
“Kwani mama umefanyeje leo hadi imekuwa hivyo!!”
“Yani mwanangu nilichokifanya leo hata sikutegemea kama kitaniletea matunda haya, ila mwanangu usijali kitu yani katika maisha ukitaka

kufanya kitu basi fanya tu huwezi jua muda kitu hiko kitakapofanikiwa kama mimi leo”
Sia alikuwa akiongea huku akitabasamu tu, kisha mama yake akasema,
“Hii milioni tatu nitaiwekeza kwenye biashara yangu halafu hii laki tano ndio itatuisaidia kwasasa hapa nyumbani. Unajua shule yako nayo

imenikomba sana hela, ila usijali kitu mwanangu yani mama anaweza kila kitu katika maisha maana yule baba yake Erica kaahidi

kukusomesha mwanangu”
“Mama, hiyo ni habari njema sana, nilikuwa naumia ukihangaika kulipa ada, nimefurahi sana”
“Usijali mwanangu, nikiwepo mimi basi kila kitu kinaenda kwenye mstari ulionyooka”
Basi siku hiyo aliamua kwenda kupika mapema kabisa ili ale na watoto wake maana kwenye nyumba yake kulikuwa na watoto wengine

anaishi nao zaidi ya Elly.

Baba Angel akiwa njiani kurudi nyumbani kwake, alisikia simu yake ikiita ila kwa muda huo hakuichukua kwani alikuwa makini na kuendesha

gari yake, basi alivyofika nyumbani na kuingiza gari ile simu ikaanza kuita tena ikabidi aichukue na kuangalia mpigaji alikuwa ni madam

Oliva, basi akaipokea na kuanza kuongea nayo,
“Baba Erick, ndio bado hujamaliza tu hilo tatizo?”
“Aaah nimemaliza, ila nimerudi nyumbani”
“Jamani kwanini lakini”
“Usijali madam, nimeshapafahamu kwako sidhani kama ni tatizo sana kwani kama kufahamiana tumeshafahamiana”
“Mimi nilihitaji angalau ule chakula na tuongee mawili matatu sababu nina biashara yangu nataka nikushirikishe”
“Oooh basi njoo ofisini kesho”
Kisha baba Angel hakukata simu, kuna muda alitaka kuamini maneno ya Sia kuhusu huyu madam ila kuna muda anaona maneno ya Sia

kuwa ni uzushi tu kwani alimuona madam kama ni mtu asiyekuwa na tatizo ambalo Sia alikuwa akilizungumzia.
Basi akaingia ndani kwake na kumkuta mkewe na kuendelea nae na mambo mengine ila kuhusu swala la Sia hakumwambia kabisa kwani

anamfahamu vizuri mkewe alivyo.

Kesho yake ilivyofika, baba Angel alijiandaa vizuri kabisa na kwenda kazini kwake, ila kuna mahali alikuwa na shamba halafu alikuwa

akihitaji kufanya ujenzi ila kutokana na shughuli zake kuona zitakuwa nyingi siku hiyo basi aliondoka pale nyumbani akiwa na Junior pamoja

na Erick na moja kwa moja alienda nao kwenye hilo eneo na kuwaelekeza cha kufanya kisha akawaacha hapo halafu yeye akaenda ofisini.
Yani ile anaingia tu ofisini kwake, na madam Oliva alikuwa kashawasili,
“Eeeh madam”
“Eeeeh nilikuwa nakusubiri ufike”
“Haya, karibu ofisini”
Basi waliingia ofisini na madam Oliva na kuanza kuongea nae mawili matatu,
“Eeeh kuna biashara ulisema unataka unishirikishe, ni biashara gani hiyo?”
“Mmmh kwanza mke wako anafanya kazi au ni mama wa nyumbani tu!”
“Aaaah nilioa msomi bhana, atakuwaje mama wa nyumbani! Yupo nyumbani sababu analea tu, sema kwa mimi huwa napenda mke wangu

awe nyumbani tu ila yeye hapendi. Yani mimi kitendo cha kurudi nyumbani na kupokelewa na mke wangu huwa najihisi raha sana, ila

akianza shughuli zake sasa hadi huwa namwambia pumzika sasa mama tule maisha.”
“Kheee kwahiyo mke wako angekuwa mama wa nyumbani ungefurahi zaidi?”
“Ndio, si mimi najishughulisha kwaajili yao! Yani yeye angekuwa anakaa tu nyumbani kulea watoto ningefurahi ila mke wangu hataki kabisa,

hata hivyo nilimkatalia kuwa na kazi ya kumfanya awe busy kwa muda mrefu kwahiyo kazi yake anayoifanya ni huru sana.”
“Oooh sawa, kuna biashara nataka nikushirikishe. Ushawahi kusikia biashara za mtandao?”
“Aaaah na wewe madam una mambo mengi sana, saivi unakuja na biashara za mitandao tena!”
“Ni nzuri sana, ukiianza hutojutia, watu wanatengeneza hadi milioni mia kwa wiki!”
“Jamani madam, ila kwa mimi biashara zangu hizi zinanitosha, wala usinishirikishe hiyo”
“Basi nitamwambia mke wako, ni nzuri sana kwanza unaifanya kwa muda wako wa ziada”
“Asante madam, mimi niletee biashara za kuona ila za mitandao zisiwezi kwanza sio mzuri sana kwenye mitandao mimi. Ila kwa leo nina kazi

nyingi sana sitaweza kuongea sana na wewe”
Basi madam Oliva aliamua kuaga tu kwani aliona kama ni ujanja tu baba Angel kautumia ili aondoke.
 
SEHEMU YA 247

Mama Angel akiwa nyumbani, kwahiyo aliyebaki alikuwa Erica tu sababu Erick na Junior waliondoka na Vaileth muda huo alikuwa akipika.
Basi alikaa sebleni pale na mwanae huyo, mara simu yake ikaita akaichukua na kuipokea, alikuwa ni dada yake Mage,
“Mdogo wangu nipigie, kuna jambo muhimu sana nataka tuongee”
Kisha ile simu ikakatika, basi mama Angel akaanza kupiga ila simu ikamwambia kuwa salio lako halitoshi kupiga simu na kumfanya achukie

sana,
“Aaaarggh kumbe sijaweka vocha, kehee sasa nitafanyaje jamani! Nitamtuma nani dukani kuninunulia vocha?”
Erica akamwambia mama yake,
“Nitume mimi”
Basi hakuwa na njia nyingine mama Angel zaidi ya kumtuma Erica vocha ambapo Erica alitoka huku akifurahia,
“Jamani, leo kama maajabu vile nimetumwa dukani. Ila mama anatufuga sana dah!”
Basi akaenda moja kwa moja hadi dukani na kununua vocha, ambapo yule muuza duka akamuuliza,
“Hivi wewe ni mtoto wa yule baba ambaye watoto wake hawatoki nje eeh!”
Erica alicheka kusikia kuwa mtaani wanaitwa kwa jina hilo, alitikisa kichwa na kuanza kuondoka. Ila kwa hatua chache tu akashikwa bega,

kugeuka akakutana na Elly kwakweli alifurahi sana na kuanza kuongea nae,
“Elly jamani, mitaa yetu umekuja kutafuta nini?”
“Aaah mama yangu ana mgahawa wa mama lishe maeneo ya huku, sasa leo nilikuwa nae maana tunapaboresha na kuanza tena biashara”
“Kumbe, hongereni”
“Ila unajua mama yangu kapata hela wapi?”
“Eeeh wapi?”
“Jana, mama kaletwa nyumbani na baba yako kisha baba yako akaondoka na baada ya muda alirudi na bahasha na kumkabidhi mama.

Tulipoenda kuhesabu zile hela zilikuwa milioni tatu na laki tano. Halafu nasikia baba yako kamuahidi mama kuwa atanisomesha mimi

kwahiyo ada hatolipa tena mama bali italipwa na baba yako”
“Mmmh kumbe!”
“Ndio, nasikia baba yako ana roho nzuri sana ila mama yako kuna wakati anapatwa na uwendawazimu!”
“Jamani Elly! Mama yangu hawezi kupandwa na uwendawazimu ujue!”
“Ndio mama alivyoniambia sasa, kasema mimi na nyie ni ndugu, na baba yako anatupenda sana wote kwa pamoja”
“Kheee haya, twende kwetu basi ukamsalimie mama”
“Siku baba yako akiwepo nitakuja, ila mama yako namfahamu maana hata siku ile aliniangalia kwa chuki sana. Ila hata hivyo kuna kazi

naimalizia na mama”
Basi Erica aliagana na Elly pale ila alikuwa akitembea huku akijiuliza maswali mengi sana kuwa baba yake imekuwaje hadi ampe pesa

mama Elly, akajiuliza,
“Hivi mama atakuwa anajua kweli? Hivi baba anaweza kufanya kitu mama asijue!”
Akaendelea kwenda nyumbani na alipofika alimpa mama yake ile vocha ambaye aliikwangua na kuanza kuiingiza kwenye simu yake basi

Erica akaanza kuongea,
“Basi leo dukani mama nimekutana na….”
Mama yake akamkatisha,
“Ushaanza umbea wako, nataka kwenda kuongea na simu mimi aaargh maana wewe hata ukikutana na mende unataka uje kunisimulia”
Kisha mama Angel aliinuka na kwenda kuongea na simu ile, kiukweli Erica hakupenda kabisa jambo lile yani aliona kama mama yake

kamfanyia makusudi, hakujua ni kwanini mama yake hakutaka kumsikiliza, basi akahisi huenda mama yake anafahamu hiko kitu ila

ilimuuma kushushuliwa kabla ya kusema umbea, hivyobasi akaamua kwenda kulala.

Mama Angel alimpigia simu dada yake na kuanza kuongea nae, ambapo walisalimiana kwanza kisha dada yake akaanza kumwambia

dhumuni la yeye kumtafuta hewani,
“Ni hivi mdogo wangu, unajua tukiacha mambo yote yaliyotokea baina yako na Derrick ila bado ni ndugu yetu yani hatutakiwa kulipinga hilo

maana Derrick ni mtoto wa baba yetu”
“Kwani unaongelea kitu gani dada?”
“Nasikia Derrick kawa tapeli”
“Mmmh jamani, Derrick kawa tapeli!”
“Ndio hivyo, Derrick ni tapeli. Sasa tusipoamka kama ndugu tutakaoumia ni sisi, inatakiwa mimi wewe, Bite na Tony tuungane na Derrick ili

tumsaidie kisaikolojia”
“Sikuelewi dada”
“Kitu gani ambacho hunielewi Erica jamani! Kumbuka Derrick ni ndugu yetu yani unavyomuona Tony unatakiwa kumuona hivyo hivyo na

Derrick”
“Kwakweli dada unanichanganya tu”
“Nakuchanganya na nini jamani, nakwambia Derrick kawa tapeli”
“Kwanini wakati kasoma na ana kazi nzuri tu”
“Aliyekwambia matapeli ni watu wasiosoma tu nani? Huoni kila leo wanagundua njia mpya za utapeli? Wengine wamesoma na wengine

hawajasoma ila utapeli ni tabia tu, mwingine utaona kavaa vizuri anapendeza kumbe tapeli ndio ilivyo kwa Derrick ni wengi kawaliza kwa

utapeli wake, tusiposhirikiana pamoja ili Derrick aache utapeli itakuwa ni kazi kwetu”
“Ila dada Derrick si ana kazi jamani!”
“Nasikia kuna matatizo yalitokea kazini kwao, kwahiyo Derrick hana kazi tena ila hiyo sio sababu maana nasikia utapeli kaanza toka yupo

kazini kwahiyo kwasasa ni kama anaendeleza tu. Kwakweli Derrick anaweza fanya mpango hata tutapeliwe sisi wenyewe, mdogo wangu

kama ndugu tunatakiwa tuwe na lengo moja ili tuweze kumuokoa Derrick, haijalishi ni kitu gani kilitokea kati yenu ila bado Derrick ni ndugu

yetu, tumpende, tumjali na tumthamini”
“Kheee haya dada nimekuelewa, hakuna tatizo utanipa taarifa basi”
“Sawa, wasalimie wanangu huko”
Kisha mama Angel aliagana na dada yake ila bado hakuafikiana nae wala nini kuhusu kumsaidia Derrick kwani kiukweli huwa mtu huyu

anamkera sana.

Usiku wa leo Erick akiwa kajilaza sababu alichoka sana kwa safari ambayo jana yake walienda na baba yao kwahiyo aliwahi sana kulala,

basi Erica akaenda moja kwa moja chumbani kwa kaka yake ambaye alimkuta amejilaza ila siku hii alisahau kufunga mlango wa chumba

cha Erick alivyoingia, kwahiyo alianza tu kumuamsha, basi Erick aliamka huku akiwa na usingizi na alimuangalia Erica kwa macho ya

usingizi halafu aliendelea kulala ambapo Erica alienda kumgusa tena, na kumfanya ageuke sasa akiendelea kumuangalia kwa jicho la

usingizi kisha akamwambia,
“Niambie malaika wangu nini tatizo”
“Wewe mimi sio Angel bhana, mimi ni Erica”
Erick aligeuka upande wa pili na kulala tena, basi Erica alichukia na kusema,
“Ndio shida yako ukilala unakuwa kama pono, sasa mimi huu umbea nitamwambia nani jamani! Mama hataki na wewe umelala jamani

mwenzenu nina maneno nataka niseme”
Ila muda huu Erick alikuwa amelala kabisa yani hana hata habari, basi Arica alianza kuongea peke yake yani aliongea tu hata kama kaka

yake amelala basi alianza kusema ila muda huu mama Angel nae alikuwa akipita pale karibu na chumba cha Erick na kukuta mlango uko

wazi, sema alielewa kuwa mwanae siku hiyo alichoka sana kwahiyo akasogea ili afunge mlango sema akasikia sauti ya Erica ikisema,
“Basi leo mama alinituma dukani, wakati natoka tu si nikakutana na Elly, tukasalimiana pale akaanza kuniambia kuwa baba na mama yake

wamepatana kiasi kwamba baba kampeleka mama yake nyumbani kwao, halafu baba akaondoka na kurudi tena kwao kisha akamkabidhi

mama yake hela kiasi cha milioni tatu na laki tano, kitu kingine baba kaahidi kumsomesha Elly na kila kitu kuhusu Elly kitakuwa juu ya baba.

Nilivyotoka dukani nikatamani nikumueleza mama ila nilivyoanza tu kanishushua balaa hadi nimejihisi vibaya mimi, halafu nakuja

kukwambia wewe unayenisikilizaga nawe unajifanya umelala. Ila ndio nishakwambia hivyo, ukiona kama ulikuwa unaota shauri yako ila mimi

ndio nishakwambia. Usiku mwema”
Erica akainuka na kumfunika kaka yake shuka vizuri halafu alitoka ila hakumkuta mtu mlangoni pale kwahiyo hakuelewa kama mama yake

alisikia kile alichokisema, basi alifunga mlango wa Erick na kuondoka zake.
 
SEHEMU YA 248

Mama Angel alienda chumbani kwake na kuwa na mawazo sana, yani alijikuta akikosa raha kabisa huku moyo ukimuuma sana kwani wivu

ulijengeka kwake, muda huu mumewe alikuwa ameenda kuoga, alikuwa amejiinamia tu kwa mawazo aliyokuwa nayo.
Gafla alisikia mlio wa meseji na hivyobasi akachukua simu ya mumewe na kuanza kuangalia ule ujumbe ulioingia, ilikuwa ni namba tu na

ujumbe ulisema,
“Erick, kwakweli jana nilifurahi sana. Ngoja nikupe matumizi ya ile hela, laki tano nimetumia nyumbani na milioni tatu kwenye biashara

yangu. Kwakweli asante sana, sitakufatilia wala kukusumbua kwasasa maana ahadi zako zimenitosha. Nitakupenda siku zote za maisha

yangu”
Mama Angel alirudia ujumbe huu mara mbili mbili huku akiumia sana moyo wake hadi machozi yalianza kumlengalenga.

Gafla alisikia mlio wa meseji na hivyobasi akachukua simu ya mumewe na kuanza kuangalia ule ujumbe ulioingia, ilikuwa ni namba tu na

ujumbe ulisema,
“Erick, kwakweli jana nilifurahi sana. Ngoja nikupe matumizi ya ile hela, laki tano nimetumia nyumbani na milioni tatu kwenye biashara

yangu. Kwakweli asante sana, sitakufatilia wala kukusumbua kwasasa maana ahadi zako zimenitosha. Nitakupenda siku zote za maisha

yangu”
Mama Angel alirudia ujumbe huu mara mbili mbili huku akiumia sana moyo wake hadi machozi yalianza kumlengalenga.
Baba Angel alitoka bafuni na kumshangaa mkewe akiwa na simu yake huku machozi yakimlengalenga, basi alimfata karibu na kukaa naye

kisha alianza kumuuliza,
“Tatizo liko wapi mke wangu? Mbona unaonekana haupo sawa?”
Kisha mama Angel alimpa baba Angel ile simu yake na kumfanya ausome ule ujumbe, moja kwa moja baba Angel alitambua wazi kuwa ule

ujumbe ulitoka kwa Sia, basi alimuangalia mke wake na kumwambia,
“Erica mke wangu, kweli ni wakati wa wewe kuchukia huu! Inamaana huniamini mume wako mpaka leo? Kweli nianze kuhangaika na

wanawake wa kazi gani, unatakiw akuniuliza kwanza tena kwa ustaarabu tu ila sio kutoa machozi mke wangu jamani”
“Nikuulize kitu gani wakati kila kitu kinaonekana hapo”
“Sikia mke wangu, ningekuwa ni mwanaume muhangaikaji kwanza kabisa nisingekuwa nakuachia simu yangu, ungekuta simu yangu ina

kufuli kila mahali ila simu yangu huwa naicha peupe kabisa sababu najiamini sana, kwanini wewe huniamini? Tumekuwa pamoja kwa miaka

sasa mpaka tuna watoto wanne ila bado huniamini jamani! Nifanye nini mke wangu?”
“Haya nieleze kwanza huyo mwanamke ulimpatia pesa kwa misingi ipi? Ni nani?”
“Huyu ni Sia mke wangu, sikuwa hata na nia mbaya ila nilimuuliza tu anachotaka ni kitu gani ili asiisumbue tena familia yetu, ndio akasema

nikimpa milioni moja basi hatotusumbua tena. Nikampa hiyo milioni tati na laki tani sababu sitaki usumbufu wake tena, sio kwamba sina

matumizi na hela, ninayo sana ila sikupenda vile anavyoikosesha amani familia yetu”
“Kwahiyo umeona kumpa hela ndio suluhisho? Na kumepleka kwake je? Kumuahidi kumsomeshea mwanae na kumtunza je! Hebu niweke

wazi Erick, ni kweli ulizaa na Sia?”
“Sikia mke wangu, kama ningezaa na Sia wala nisingekuwa na sababu ya kukataa ujue! Kwanza nikatae damu yangu ili iweje! Siwezi

kufanya hiko kitu hata kama simpendi mwanamke, ila Erica nakupenda wewe na ninachokwambia ni ukweli ila swala la kunichunguza hivyo

mke wangu inaonyesha wazi huniamini”
“Aaaagh Erick, nitolee swala la kutokukuamini kabisa eti nakuchunguza inamaana sikuamini naomba ulitoe. Katika mahusiano yetu tunaishi

siku zote kwa namna hii, ni kawaida kwangu kushika simu yako nawe ni kawaida kushika simu yangu hata kupokea pia, sasa mimi kusoma

ujumbe ndio kukuchunguza! Naomba jamani usianze kufanya niongee hadi asubuhi hapa, nataka tu kujua ajenda yako ya kumsomesha

mtoto wa Sia imekuwaje?”
“Hakuna kitu kama hiko mke wangu, sijapanga hivyo na Sia”
“Erick, nitajua tu ukweli. Unaona nalea ndio unafikiri siwezi kujua, najua unajua kama akili zangu zikoje, sishindwi kukuchunguza mimi tena

zaidi ya kukuchunguza kwa simu naweza yote, ila nahitaji tuendelee kuishi kwa amani, kuwa mkweli kwangu kama zamani. Mume wangu

najivunia kuwa nimekutengeneza na kukufanya uwe hivyo ulivyokuwa kwasasa, najua kuna wengi wanajiuliza ni kwanini wale wanadumu au

ni kwanini wana furaha ila ni sababu ya kukutengeneza na kujenga mazingira safi ya kupendana na kuaminiana. Kipi unachoniambia

nikapinga mimi? Kwanini sasa unanificha mambo kama haya kweli!! Jambo limetokea jana ulishindwa kuniambia hadi leo kweli!!”
“Oooh mke wangu nisamehe tafadhari, nakuomba tusimkaribishe shetani bure katika ndoa yetu, naomba unisamehe”
“Niahidi kuwa unaenda kubadilika, kiukweli sijapenda hii kitu yani sijapenda kabisa. Naomba chochote kinachotokea uwe unaniambia kama

zamani”
“Sawa mke wangu, naomba tena msamaha”
Mama Angel aliitikia ila bado alionekana kuwa na kinyongo moyoni mwake, hivyo mumewe ilibidi aanze kumbembeleza ili arudi katika hali

ya kawaida.
Basi wakaamua kulala, sema kwavile baba Angel nae alikuwa amechoka sana kwahiyo alivyojilaza tu akapitiwa na usingizi ila kwa mama

Angel ilikuwa tofauti kwanza alikuwa na mawazo na pia huwa analala sana mchana na mtoto kwahiyo alijikuta akiwa macho, kwani bado

moyo wake ulikuwa ukiumia kwahiyo alichukua simu ya mume wake na kuanza kuwasiliana na Sia yani akijifanya kama yeye ndiye baba

Angel,
“Umelala Sia? Ile hela inakutosha lakini?”
“Oooh Mungu yu mwema, umenikumbuka leo jamani naona maombi yangu yanaanza kujibiwa. Imenitosha ndio, nilikuwa nalala hapa ila

niliposikia ujumbe ndio naangalia naona ni wewe nimeshtuka sana. Nashukuru, leo umechat na mimi mkeo hakuoni au?”
“Aaah kalala, yupo hoi si unajua analea?”
“Oooh naelewa ndio, sasa huu ndio muda muafaka ungekuwa na mimi wakati mkeo analea. Unajua ndiomana wenzetu kuna sharia ya

mwanaume kuoa wake wengi, achana na imani hiyo ya mke mmoja, twende tufunge ndoa hata bomani ili tusizini”
Mama Angel akapumua kidogo na kuendelea kuwasiliana na Sia,
“Aaah jamani, ndoa nyingine mke wangu hawezi kukubali”
“Naelewa hilo sababu Erica ana roho mbaya, na akijua kuwa umenipa pesa kama namuona atakavyonuna hata kutamani kujiua”
“Hahaha, mke wangu hayupo hivyo bhana. Hawezi kuchukia, mbona ana roho nzuri tu huyu”
“Kama ana roho nzuri mwambie nataka kuongeza mke wa pili, nataka kumuoa Sia uone patakavyochimbika hapo bila jembe”
“Basi nitamwambia hakuna tatizo, vipi mtoto kalala?
“Kalala ndio, leo maajabu umeulizia hadi kuhusu mtoto?”
“Ndio, mwanangu huyo”
“Mmmh jamani, Erick wewe au mwingine. Wewe kirahisi tu hivyo useme Elly mwanao! Au leo umekunywa kidogo?”
“Aaah hapana, nitamlea Elly”
“Kheee jamani usinifanye nishindwe kulala kwa furaha, miaka yote hii natafuta wa kunisaidia kulea mtoto, unajua nani alikuwa akinisaidia?

Simtaji hadi unioe”
“Nakutania jamani usichukulie serious maneno yangu, usiku mwema.”
“Nakupenda Erick, na nitakupenda siku zote za maisha yangu yani leo nalala huku natabasamu kwa kuwasiliana tu na wewe maana

sikutegemea kitu cha namna hii. Nakupenda sana”
Mama Angel alikuwa akisoma hizi jumbe mara mbilimbili ila ni yeye mwenyewe zilikuwa zikimuumiza maana mumewe alilala muda huo hana

hata habari, kisha mama Angel alizifuta zile jumbe na kuweka simu pembeni, ila kitu ambacho kilimpa amani ni kule kugundua kuwa

mumewe hajasema swala la kuhudumia mtoto wa Sia, wala hajakubali kuwa mtoto wa Sia ni wake, kisha akalala kwa muda huo.
 
SEHEMU YA 249

Kulipokucha, na leo baba Angel aliwachukua Junior na Erick na kuondoka nao kuelekea kwenye sehemu yake ya ujenzi kwani bado alikuwa

na kazi ofisini na alihitaji sehemu ile isimamiwe kwa ukaribu sana kwahiyo aliwaamini watoto wake hao kuwa watafanya vizuri sana.
Basi yeye alifika ofisini na kuanza kazi zake, wakati akiendelea ujumbe kwenye simu yake ukaingi na namba mpya ila aliitambua kuwa ni

namba ya Sia,
“Umeamkaje Erick kipenzi cha moyo wangu, yani jana usiku nimefurahi sana kuwasiliana na wewe. Hizi meseji zako nazipitia tu leo na

zinanipa nguvu sana ya kuendelea mbele, nakupenda sana Erick”
Kwakwlei baba Angel alishtuka sana kwani hajawasiliana na Sia kw anjia ya ujumbe kwa siku nyingi sana, kwani siku zote huwa anapuuzia

jumbe zake kwahiyo siku hiyo alishangaa sana na kuona kweli Sia ana wazimu, basi akaamua kumpigia simu,
“Ila Sia una wazimu au kitu gani? Mimi na wewe tulikubaliana nini kwani? Si ulisema hutoisumbua familia yangu tena, imekuwaje sasa?

Unaanza uongo, mimi nimeongea nawe saa ngapi jana na kuhusu nini?”
Basi Sia alijaribu kumuelewesha jinsi jana alivyokuwa akiwasiliana nae, kwakweli baba Angel alishangaa sana sababu hakufanya hivyo, Sia

akamwambia,
“Hadi nilikuuliza umelewa leo?”
“Hebu nitumie hizo jumbe yani hata sikumbuki”
Basi Sia akamtumia zile jumbe ambazo alikuwa akiwasiliana nae jana usiku, baba Angel alizipitia na kujua moja kwa moja ni mke wake tu,

ila hakutaka Sia ajue kuwa ni mke wake ndio kaona, kisha akamwambia,
“Sia, mimi na wewe tumemalizana naomba uiache familia yangu na uache kunitumia jumbe za kijinga jinga”
Kisha baba Angel alikata simu na kukaa sasa akimtafakari mke wake kuna mke wake ana tatizo gani ambalo yeye binafsi halielewi,

alijisemea,
“Sijui ni kitu gani unaweza kumfanyia mwanamke naye akaona na kuamini kuwa hakuna mwanamke mwingine unayemuhitaji katika maisha

yako zaidi ya yeye, ningejua hiko kitu basi ningemfanyia mke wangu yani anachukia bila sababu ananichunguza bila sababu halafu

nampenda sana jamani”
Mara madam Oliva alifika ofisini kwa baba Angel ambaye alimkaribisha na kuanza kuongea nae,
“Oooh naona na leo umekuja madam”
“Yani mimi huwa nikikaa ofisini kwangu na kujiona nimeboreka, naona ni vyema nije tu huku ili tuongee mawili matatu”
“Haya, karibu”
“Asante, hivi baba Erick ni kitu gani unakipenda kwa mwanamke?”
“Dah hilo swali ni gumu sana, ila nadhani siku ukikaa sana na mke wangu halafu muangalie alivyo basi utapata jibu ya swali lako maana

ninachopenda kwa mwanamke basi vyote anavyo mke wangu ndiomana nampenda sana”
“Oooh mke wako ana raha sana, yani kupata mume kama wewe kwakweli ana raha sana tena ana Bahati sana. Haya, ngoja nikuulize swali

jingine ukiambiwa kitu ufanye na mama yako halafu mke wako akakwambia kitu kingine utafanya kipi?”
“Sijui lengo lako ni nini kuniuliza maswali hayo, ila katika maisha kila kitu kina wakati wake, kipindi nikiwa mdogo nakuwa chini ya mama na

mama yangu ndio anakuwa kila kitu kwangu, ila kwasasa nimeoa basi niko chini ya mke wangu, yani mke anatakiwa kuniongoza mimi

ndiomana kuna usemi unakwambia katika maisha kosea vyote ila usikosee ndoa, kwani ndoa ndio inatufanya tuwe jinsi tulivyosasa,

mwanamke mwenye busara basi atamthamini mama mkwe wake kama mama yake mzazi kwahiyo atamuheshimu na kumthamini mama

yangu, kiasi kwamba mama akitaka jambo na yeye akitaka kwa muda huo huo basi atatumia busara yani hata yeye yupo radhi kusubiri

maana anamuona mama kama mama yake, labda mimi mwenyewe tu nikengeuke. Na ndivyo ilivyo kwa mke wangu, yani ndugu zangu ni

ndugu zake, wazazi wangu ni wazazi wake, anawapenda, anawaheshimu na kuwathamini halafu kingine mimi ninavyompenda, kumjali na

kumthamini mke wangu ndivyo ninavyowajengea chachu ndugu zangu kumjali mke wangu pia, ila mimi nikimchukia hao ndugu watampenda

kitu gani kama sio unafki!”
“Ooooh baba Erick unaongea, hata sikutegemea. Ila samahani kwa maswali yangu, hivi mwanamke akikutongoza unajisikiaje?”
“Kipindi cha ujana wangu, nikitongozwa na mwanamke nilikuwa naona ufahari sana na kumkubali muda huo huo ila tangu nimeoa, basi

nikitongozwa na mwanamke nampa onyo kuwa mimi ni mume wa mtu asinisumbue, kama hasikii huwa namueleza kila kitu mke wangu ili

naye ajue kilichopo”
“Kheee hadi hayo mambo huwa unamwambia mkeo!”
“Nisipomwambia yeye nitamwambia nani tena”
Simu ya baba Angel iliita na alihitajika kule kwenye ujenzi kwahiyo aliona vyema kuagana na madam Oliva, ila kiukweli huyu madam

humfanya asimamishe kazi zake maana akiwa na mazungumzo nae basi hujiona akiongea nae ujinga tu.

Junior na Erick wakiwa kwenye usimamizi mahali pale, baba yao alifika na kufanya wenyewe kuanza kuzunguka kidogo kiwanja kile

ambacho kilikuwa ni kikubwa sana, ila wakati wanazunguka kuna mtu walimuona akipita na mtu huyu walimfahamu, alisogea kuwasalimia,

alikuwa ni Samia, basi Junior akamuuliza,
“Samia, kwani kwenu ni huku!! Si uliniambia sehemu nyingine!”
“Huku sio kwetu, huku ni kwa bibi yangu mzaa baba. Saivi si tupo likizo basi ndio hivi nipo kwa bibi”
“Aaah kumbe, kwahiyo kwa bibi yako sio mbali na hapa?”
“Eeeh sio mbali wala nini, ni hapo tu mbele kidogo. Bibi alinituma kumuita kaka yangu ndio nilienda kumuita”
Basi yule kaka yake nae alisogea na kumfanya Samia kuanza kuwatambulisha wakina Junior,
“Kaka, huyu anaitwa Junior na huyu ni Erick ni kaka zake na rafiki yangu Erica. Jamani huyu ni kaka yangu anaitwa Rahim”
Basi wakashikana mikono pale kisha Rahim akatangulia kuondoka na kuwaacha pale wakiwa wamesimama na Samia, ila muda kidogo Erick

aliitwa na baba yake kwahiyo alibaki Junior na Samia ambapo Samia aliaga ila Junior aliamua kumsindikiza Samia hadi kwa bibi yake,

kwahiyo njiani walikuwa wakiongea,
“Eeeh Samia, yani huwa napenda unavyoongea, unavyotabasamu napenda sana. Mimi nakupenda kiukweli”
“Kheee makubwa”
“Makubwa yapi Samia? Mimi nakupenda, natamani tuwe na mahusiano ila mahusiano ya siri”
“Unanipenda kweli?”
“Ndio nakupenda”
“Baba aliniambia kuwa, ikiwa kuna mwanaume kaja kukwambia anakupenda mwambie akupe pesa”
“Kheee hela ya nini jamani Samia? Mapenzi sio pesa”
“Hiyo ni kutokana na wewe ila kwa mimi nasema nilichoambiwa na baba yangu, kaniambia kuwa mtu akisema ananipenda nimwambie kuwa

anipe pesa”
“Kwahiyo nikikupa pesa ndio utanikubali?”
“Nitakufikiria”
“Jamani Samia mbona unanifanyia hivyo mtoto wa mwanamke mwenzio? Haya basi chukua hii elfu tani ya vocha”
Junior alitoa elfu tano na kumpa Samia ambaye aliipokea ila akamwambia,
“Hii hela ndogo hainitoshi”
“Kheee kwahiyo unataka pesa ngapi?”
“Nipe kuanzia laki tano, baba yangu hapendi nije kuolewa na masikini. Kwahiyo ukinipa hela nitajua kuwa wewe ni tajiri na unafaa”
“Kheee Samia, unajua wewe bado ni mtoto mdogo!”
“Nina miaka kumi na nne, ni mdogo kweli ila hakuna cha kunidanganya maana nishafundishwa kila kitu na ninaelewa kila kitu”
“Kwahiyo nikikupa laki tano ndio utanikubalia? Ulishawahi kuwa na mpenzi?”
“Sijawahi sababu huwa wanashindwa kutafuta hiyo laki tano ya kunipa mimi kwahiyo sijawahi kuwa na mchumba na nadhani itakuwa hivyo

hadi nimalize shule”
“Ila unaonekana mjanja sana wewe”
Walikuwa wamefika kwa bibi yake Samia, hivyobasi Junior aliagana na Samia pale hukua akiahidi kumtafuta tena tu,
“Ukinitafuta tena iwe tunaongelea maswala ya kawaida ila kama unataka kunitongoza bila hiyo laki tano hapana kwakweli”
Kisha Samia akaingia kwa bibi yake halafu Junior akarudi kule ambako ujenzi unaendelea na kumkuta Erick,
“Ulimsindikiza Samia?”
“Ndio, nimempeleka hadi kwa bibi yake, ila wewe naona huwa unamfagilia yule Sarah maana akifika nyumbani huwa lazima umsindikize ila

huyu Samia wala huwa hujiangaishi nae”
“Aaaah tatizo Sarah nimemzoea sana ila Samia sina mazoea nae kivile wala nini”
Baba yao alifika na kuwauliza maswali matatu pale kuwa wanauonaje ujenzi na mengine mengine. Walipomaliza jioni kabisa ndio

waliondoka kuelekea nyumbani kwao maana walikuwa wameshachoka.
Kwkweli Erick ndio alikuwa anaongoza kwa kuchoka sana ukizingatia bado kukurukakara kama hizi hajazizoea tofauti na Junior kidogo

mambo yale kayazoea.
Basi kwenye gari ni Junior tu na baba Angel ndio walikuwa wakiongea ongea ila Erick alikuwa amelala muda tu kwa uchovu,
“Baba si unaona Erick hajazoea haya mambo, mwambie mamdogo aache kumkalisha ndani hadi Erick kama watoto wake wengine wakike”
“Aaaah atazoea tu, ndio kama hivi nampa mpa zoezi la kazi”
“Sawa, bamdogo”
Basi waliendelea tu na safari ila kichwani kwa Junior muda huo ilikuwa ni kupata tu laki tano ambayo aliona ingemsaidia sana.
 
SEHEMU YA 250

Leo Angel na bibi yake wakiwa wanajiandaa kulala, Angel alimuomba bibi yake simu kwa siku hiyo ili aweze kuwasiliana na rafiki zake,
“Angel, sio ndio uanze kuwasiliana tena na wakina Samir jamani!”
“Siwezi bibi, kwanza kile kitabu kimenifungua sana siwezi kufanya hivyo bibi nawasiliana tu na marafiki zangu wa kawaida yani wakina

Husna, Yusna, Hanifa nimewakumbuka sana”
Basi bibi yake akampa simu na kumfanya Angel afurahi sana na kuanza kwenda nayo moja kwa moja chumbani kwake. Ila bibi yake

akamkumbusha jambo moja,
“Ila si unajua kuwa huu ni muda wa kulala?”
“Najua bibi, nawasiliana nao kidogo tu halafu nakuletea simu”
“haya, saa nne kamili ulete simu chumbani kwangu siwezi kuacha uitumie hadi asubuhi”
“Hakuna tatizo bibi yangu”
Basi Angel alienda nayo chumbani kwake huku akijisemea kuwa siku hiyo kweli hatomtafuta Samir wala nini na alikuwa na mpango kweli wa

kutafuta rafiki zake wa kike ila muda alipoiwasha tu ile simu alipokaa kidogo tu kuna ujumbe ukaingia kutoka kwa Samir, hata yeye

alishangaa kuwa Samir kajua vipi kuwa kashika simu kwa muda huo, ujumbe ulimwambia
“Najua mpenzi unaupata ujumbe wangu muda huu, ni kwamba nakupenda sana”
Basi akamjibu kwa kumuuliza,
“Umejuaje kama nitakuwa na simu muda huu?”
“Ni Mungu tu ambaye ameunganisha mioyo yetu Angel, mimi nakupenda sana”
“Mmmh!”
“Sasa unaguna nini Angel”
“Wewe ungekuwa unanipenda siku ile usingekimbia baada ya kumuona bibi yangu na ungebaki kunitetea”
“Aaaah kumbe unahitaji hiyo kitu kutoka kwangu, usifikiri siwezi Angel, yani naweza sana hata kuwa nakuja hapo. Kwani bibi yako

hanifahamu mimi? Ananifahamu huyo toka udogo wangu, ila nitaanza kuwa nakuja sasa”
“Ndio, onekana kwa bibi na usimuogope ndio nitajua ni kweli unanipenda”
“Sawa, hakuna tatizo lolote”
Kisha waliendelea kuwasiliana kwa vitu mbalimbalia na kwavile hakuwakuwasiliana kwa siku nyingi kwahiyo wakajikuta wana mada nyingi

sana za kuongelea mwisho wa siku Angel alijikuta amelala akiwa na ile simu mkononi.
Kuja kushtuka ni wakati pamekucha kabisa, basi aliwasha ile simu na kufuta jumbe zote kisha kuizima halafu alinyata na kuipeleka

chumbani kwa bibi yake ambaye alimkuta kashaamka na yupo nje maana bibi yake huwa anawahi sana kuamka.
Alivyoiweka ile simu akarudi chumbani kwake na kuendelea kulala, baada ya muda kidogo tu bibi yake alienda kumuamsha,
“Wewe Angel hebu amka huko, nadhani ndio umetumia simu hadi usiku sana maana hujanirudishia na umelala mpaka muda huu, simu iko

wapi?”
“Jamani bibi, mbona simu niliirudisha saa nne usiku kama ulivyosema”
“Umeiweka wapi sasa?”
“Pale mezani kwako bibi”
Bibi aliwaza ila hakuwa na kumbukumbu kama aliangalia mezani, basi alienda chumbani kwake na kweli aliikuta mezani kwake kwahiyo

akaona kuwa Angel alikuwa akisema ukweli na kuamini maneno yake.

Leo, Angel na bibi yake walitembelewa na mgeni ambaye alikuwa ni mama mkubwa wa Angel, basi walimkaribisha pale vizuri kabisa na bibi

Angel alianza kumlaumu,
“Yani Mage kuja kwangu siku hizi naona hutaki kabisa hadi usikie mama yako nimekufa!”
“Hapana mama, sio hivyo tatizo ni nyie wenyewe yani naona kwasasa maisha yako yote yapo kwa Erica”
“Kwanini jamani?”
“Nyumbani kwa Erica ndio unapoweza kwenda kukaa hata mwezi ila kwangu huji wala kwa Bite nasikia huendagi”
“Hizo lawama sasa, mimi nilienda kukaa kwa Erica sababu ya uzazi. Kwanza nakushangaa unajilalamisha wakati mdogo wako toka

ajifungue hujawahi kwenda kabisa, ila upo hapa kulalamika kwanini sikutembelei, ukiacha mambo yako na kuja kunitembelea mimi

unapungukiwa na nini? Kumbuka mimi ni mama na nitabaki kuwa hivi, huwezi kukaa chini na kusema mama sijui alifanya hivi basi na mimi

nafanya vile, kila mtu atakushangaa kutaka kushindana na mama yako”
“Basi nisamehe mama”
“Sio basi nisamehe, yani unastahili kuniomba msamaha tena haswaaa. Ni kweli kulikuwa na matatizo baina yetu ila yaliisha, yani

nakushangaa sana Mage, wewe habari za ndugu wa baba yako ndio unazo, unaenda huko kuwasalimia muda wote na kufanya nao kila kitu

ila kuja kunisalimia mimi unaona shida, mdogo wako kajifungua pale hujaenda hadi leo! Hata Bite na mumewe wamekushinda kwani

walikuwa wa kwanza kuja, hata Tumaini kakushinda yani mwanangu umekuwa na roho ya ajabu sana. Ila nishakusamehe tayari maana

mtoto akinyea kiganja huwezi kukata”
“Jamani mama, nashukuru kwa kunisamehe lakini. Ila leo nimekukumbuka sana, na licha ya kukukumbuka kuna jambo nataka tuongee”
“Jambo gani?”
Basi Mage alianza kumueleza mama yake kuhusu Derrick na kumuomba awaombe ndugu zake yani Erica, Bite na Tony wakubali kukutana

nae na kufanya kikao cha namna ya kumsaidia,
“Unaona sasa Mage, hayo ndio mambo unayoyaweza wewe. Sijui Derrick imekuwaje sijui imekuwaje, jamani yule si ana mama yake? Si ana

ndugu zake huko watamsaidia”
“Ila mama kumbuka kuwa Derrick ni mtoto wa baba yani ni ndugu yetu”
“Ndio ni ndugu yenu nyie ila sio mimi, simtambui Derrick mimi. Sijawahi kumtambua na sitomtambua kamwe”
“Ila mama kigeugeu wewe, mamake Derrick si aliwahi kufika hapa tena alikuwa anakuja na unaongea nae vizuri tu kumbe una kinyongo hadi

leo!”
“Sina kinyongo ila usitake kunichanganya tafadhari Mage, usinichanganye kabisa. Kama umepanga kukutana na ndugu zako basi kutana

nao uzungumze nao kuhusu hilo ila mimi mniache kama nilivyo, ya kwangu yananitosha”
Kiukweli Mage huwa kuna wakati anamshangaa sana mama yake, kuwa anamchukia kiasi hiko mtoto ambaye baba yao alizaa nje ya ndoa,

yani Mage hakuona kama kuna sababu ya kumchukia wakati ni ndugu yao ila ikabidi tu abadilishe mada.
Muda kidogo alisogea msichana wa kazi kwa Angel na kumwambia kuwa kuna mgeni wake nje, ikabidi Angel atoke ili akaonane na huyo

mgeni.
 
SEHEMU YA 251

Angel alitoka na kushangaa kumuona Ally, maana kwa haraka haraka alihisi ni Samir sababu jana yake aliongea nae kuwa ataanza kumtembelea kwahiyo alishangaa sana kumuona Ally basi ikabidi asalimiane nae na kumuuliza,
“Jamani, umekuja hadi kwa bibi yangu!”
“Ndio, sababu nakupenda kwahiyo lazima nije ulipo”
Angel alitabasamu na kumuuliza,
“Kwahiyo Ally unamaanisha unataka kuwa mpenzi wangu?”
“Ndio, nahitaji tuwe pamoja”
“Wewe si dereva wa bajaji!!”
“Haijalishi, leo utaona naendesha bajaji ila kesho utaona naendesha hummer”
“Khaaa jamani, wanaume mna swaga duh!! Ila Ally hapana jamani, mimi nina mpenzi”
“Aaaah Angel usiseme hivyo, hebu ona tunavyoendana, pale Angel hapa Ally yani mimi na wewe tumeumbiwa kuwa pamoja kabisa”
Angel akacheka tu, ila muda huo mamake mkubwa yani Mage alitoka ndani akiwa na bibi yake inaonyesha alikuwa ameaga, ila alipofika pale nje ambapo Ally kasimama na Angel aliwaangalia kwa mshangao na kusema,
“Jamani Ally umefika hadi huku kweli kufata mwanamke!”
Bibi Angel alishangaa pia na kuuliza,
“Kwani ni nani huyu?”
Mage alimuangalia mama yake na kusema,
“Mama, kuna haja ya Angel kujua ukweli wa uhalisia wake bila hivyo atatembea na ndugu zake na kuleta mabalaa aliyoleta mama yake”
Kisha akawaangalia Angel na Ally na kusema,
“Nyie ni ndugu wajinga nyie, mmesimama hapo kutamaniana tu”
Angel na Ally walishangaa sana kusikia kuwa wao ni ndugu.

Mage alimuangalia mama yake na kusema,
“Mama, kuna haja ya Angel kujua ukweli wa uhalisia wake bila hivyo atatembea na ndugu zake na kuleta mabalaa aliyoleta mama yake”
Kisha akawaangalia Angel na Ally na kusema,
“Nyie ni ndugu wajinga nyie, mmesimama hapo kutamaniana tu”
Angel na Ally walishangaa sana kusikia kuwa wao ni ndugu.
Basi waliuliza kwa mshangao,
“Sisi ni ndugu!!”
Bibi yake Angel aliingilia kati pale ili yule mwanaume aondoke,
“Wewe kijana ondoka nyumbani kwangu sitaki ujinga, halafu Angel rudi ndani”
Ila bado Angel na Ally walisimama pale pale kwani walitaka kusikia ile kauli juu ya undugu wao iko vipi, ikabidi bibi aongee kwa ukali zaidi na ambapo alivyoona hawamsikii akamshika Angel mkono na kumuingiza ndani kisha alifunga mlango kwa nje ili Angel asitoke kabisa, kisha alivyotoka nje akamtimua Ally na kumvuta Mage kwa pembeni na kuanza kuongea nae,
“Wewe Mage wewe, wale ni ndugu kivipi? Badala uwafokee wewe unasema ni ndugu!!”
“Ni ndugu ndio mama, ni sababu tu Ally kafanana na mama yake, ila huyo Ally pia ni mtoto wa Rahim”
“Kheee huyo Rahim alikuwa anazaa zaa hovyo hovyo eeeh!”
“Ndio, Rahim ana watoto wengi sana. Kwahiyo kuna umuhimu mkubwa sana wa Angel kuujua uhalisia wake, la sivyo atatembea na kaka zake”
“Ila Erica hataki kabisa hilo lifanyike, hataki Angel atambue ukweli”
“Mama, hata sisi tumwambie tu Angel ukweli. Unajua haijalishi baba wa mtoto alikufanya nini ila kuna ulazima wa mtoto kutambua baba yake halisi ni nani, kwahiyo kama Erica hawezi hata sisi tumwambie Angel”
“Mmmh mwanangu, unajua mapenzi ya watu tena. Erick na Erica wenyewe walikubaliana juu ya Angel halafu sisi tufungue midomo mipana kama funiko la choo kumwambia Angel kuwa baba yako sio Erick ni Rahim! Jamani itakuwa tuna wazimu eti”
“Ila mama kwani siri hapo iko wapi, hivi huyo Angel hakuna hata kimoja alichofanana na Erick, halafu mseme mnatunza siri, hadi lini mambo hayo? Mwambieni Angel ukweli na aamue mwenyewe kusuka au kunyoa ila mwambieni ukweli kuwa Erick sio baba yake mzazi. Kwanza namshangaa sana Erica, yani mtoto baba yake mzazi ni mwingine halafu kaenda kumuandikisha jina la mwanaume mwingine! Yani mapenzi ni uchizi sana, kuna mambo mtu anafanya kama anawazimu vile”
“Ngoja nikuombe kitu mwanangu, naomba kuhusu hilo uwe na busara na uwe mstahimilivu, hebu kwanza kumbuka mdogo wako wakati ana mimba ya Angel alikuwa na hali gani? Hakuwa na raha kabisa mpaka nimembamba akajifungua, baada ya hapo ni kulia tu kila akikaa mwenyewe chumbani basi ujue analia na kumkuta amevimba macho tu, ila Mungu ni mwema akatokea Erick na kumfuta machungu yote na kuanza kumlea Angel na kumuhudumia kama mwanae, je Erica angefanyeje zaidi ya kutimiza matakwa ya Erick na kumuandika Angel jina la Erick? Unadhani Erica angefanyeje? Alikuwa kwenye wakati mgumu sana, nilimsema mno nakumbuka ila badae nilielewa ni kwanini alifanya vile. Huyo Rahim si ndio wale wanaume wanaozaa hovyo na kusema mtoto akikua basi atanitafuta, hivi huwa inatokeaje kwa wanaume wa aina hiyo? Si ndio mama anaamua tu kumpa mtoto ubini wake! Sasa kama huyo Rahim ana watoto wengi basi ni lazima mwisho wa siku watoto wake wataoana tu”
“Ila mama umeongea mengi sana, sema mada yangu sio hiyo ila mada yangu ni Angel aujue ukweli”
“Sasa ukweli huo ataambiwa na mama yake na sio sisi watu wengine, nadhani umenielewa Mage? Tafadhari muache Erica afanye maamuzi yake mwenyewe kwa watoto wake”
“Mmmhhh”
“Usigune, ndio hivyo. Mwache mdogo wako afurahie ndoa yake na watoto wake, muda ukifika na akiamua kusema ukweli basi atausema tu”
Muda huu bibi Angel alighairi hata kumsindikiza Mage kwahiyo Mage aliondoka mwenyewe na bibi Angel alirudi nyumbani.
 
SEHEMU YA 252

Kisha bibi Angel moja kwa moja alienda ndani na kumkuta Angel kajiinamia tu, basi akamsogelea na kumuuliza,
“Angel mjukuu wangu jamani tatizo ni nini kwani?”
“Nahitaji kujua ukweli bibi, yule Ally ni ndugu yangu kivipi? Je naye ni mtoto wa baba?”
“Mwanangu, huyu mamako mkubwa usimuone hivi ni ana matatizo mengi sana, kwanza ushawahi kumuona akija kwenu mara kwa mara?”
“Huwa haji”
Mara simu ya bibi Angel ikaanza kuita, kuiangalia aliyekuwa anapiga ni Mage, basi akaipokea na kuanza kuongea nayo,
“Kwakweli mama, mimi sina amani natamani Angel aujue ukweli yani sina amani kabisa. Narudi mama kumwambia Angel ukweli”
“Kwani uko wapi muda huu?”
“Nipo stendi ila narudi, nahitaji Angel aujue ukweli jamani mama mtamficha Angel hadi lini? Inapaswa mtoto ajue ukweli”
“Ila Mage una wazimu au ni kitu gani lakini”
“Hapana mama ila lazima Angel ajue ukweli”
Mage akakata simu, yani kwa muda huo bibi Angel hakuelewa cha kufanya na kuhisi kama kuchanganyikiwa kwani hakuona kama ni sahihi kwa wao kumwambia Angel ukweli wakati wazazi wa mtoto wapo.
Basi na Angel nae akaendelea na maswali kwa bibi yake,
“Nielezee basi bibi”
“Mjukuu wangu, natoka kidogo nikirudi nitakuja kukwambia uchizi wa huyu mamako mkubwa”
Kwa muda huo aliona kitu pekee cha kumzubaisha nacho Angel ni simu, basi akampa Angel simu na kweli Angel alifurahi sana na kwenda nayo chumbani kwake. Muda huo bibi Angel aliwahi kutoka nje ili akutane na Mage, na ile anafika tu nje na Mage nae alikuwa amefika, kwavile bibi Angel alikuwa amechukizwa akamnasa Mage kibao na kumwambia,
“Hivi wewe mtoto una nini lakini? Kwanza huna mazoea ya kwenda kwa mdogo wako ingawa mdogo wako hakujali chochote kuhusu kwako na kuja mara kwa mara ila wewe huna mazoea”
“Kwani kwani kuna nini?”
“Unafikiri kuwa na watoto wengi vile kama timu ya mpira kuna mgeni yoyote anapenda? Ulikuwa nao wanne na sasa una watoto sita Mage, kuna mgeni anapenda? Na bora ungekuwa na nyumba kubwa, kwa nyumba gani ile mgeni anarundikana na mitoto yote chumbani”
“Mama, sasa naona umeamua tu kunidhalilisha. Kwani kuwa na watoto wengi ni dhambi? Mume wangu tumetulia nae kwa miaka na miaka, kwanini nisimzalie akafurahi! Kwahiyo ndiomana unaenda kwa Erica sababu ana jumba kubwa, ila huo ni ujinga kwani hilo jumba ataikwa nalo! Mnaacha kumwambia Angel ukweli sababu ya mali za huyo Erick, kama mali Angel akazitafute kwa babake huko mwenye watoto kama kumbikumbi ila sio kujidanganyishia kwa Erick, na yule mwanao alivyo na wivu najua pale hata asikie Erick ana mtoto mwingine atatamani hata kujiua na kusahau yote ambayo Erick amemtendea yeye. Jamani hebu muhurumieni na huyo Erick, kashamlea sana huyu Angel, kwanza nilivyomkuta kwako huku nimeshukuru Mungu, kuna siku Erick atambaka huyu Angel kufidia mali zake”
Mama yake akamzaba tena kibao na kumwambia,
“Hivi wewe Mage una wazimu au kitu gani? Sikia nikwambie, kuolewa ni Bahati ila kuolewa na mwanaume kama Erick ni Bahati zaidi, hebu muache mdogo wako aishi kwa amani. Kwahiyo yale maisha ya kwenda huko kijijini na kufanyiwa mila ulikuwa unayapenda? Hebu muache, Erick kamkubali mwenyewe mtoto, na yeye mwenyewe alisema kuwa mtoto awekwe jina lake na siku zote anamjali na kumpenda, huyo baba yake angafanya nini?”
“Ila mama, nashukuru kwa vibao ulivyonipiga wala siwezi kuvirudisha kwani wewe ni mama yangu, ila mimi nitasimama kwenye ukweli tu Angel lazima amtambue baba yake. Hata kama ukinizuia leo jua kuna siku nitakuja na kumwambia Angel ukweli kuhusu baba yake mzazi”
Kisha Mage akaondoka, kwakweli mama yake akasikitika sana na akaona kuna umuhimu wa kumwambia mwanae Erica ili ajue kuwa dada yake anataka kufanya nini yani bibi Angel aliingia ndani akiwa na mawazo sana ila kitu kikubwa alichowaza ni swala la kumpa Angel simu kwa muda huo, akawaza huenda Angel akimuuliza mama yake kuhusu lile swala basi mama yake anaweza kupaniki ni bora yeye mwenyewe kumueleza mama yake Angel ilivyokuwa kwahiyo aliona ni vyema akamnyang’anye Angel ile simu.

Angel alitulia na simu yake huku akiwasiliana na watu mbalimbali na siku hiyo akabahatika kuwasiliana na Mussa pia,
“Nimekukumbuka sana Angel”
“Unajua mimi ni shemeji yako kwa Samir”
“Aaaah Angel, achana na Samir kwakweli utajutia, ni ndugu yangu yule namjua vizuri tu. Unamuona Samir kuwa kijana mwenzio ila ana mambo makubwa kushinda huo ujana wenyewe, kwakweli Angel huyo Samir hakufai kabisa”
“Mmmmh!”
“Usigune Angel, lini tukutane tuyajenge?”
“Aaaah mimi naishi kwa bibi halafu siruhusiwi kutoka kwahiyo ni ngumu kwa sisi kukutana”
“Nielekeze kwa bibi yako basi nije”
Wakati huo kuna ujumbe uliingia pia kutoka kwa Samir ukisema,
“Angel mpenzi wangu nimekukumbuka kweli yani, sijui nije lini kukuona”
Sasa Angel hakusoma vizuri na kujua ni Mussa ndio kaandika vile basi akajibu na kumwambia,
“Mussa, acha zako jamani uje wapi wakati huku hupajui?”
Muda huo huo Samir alianza kupiga simu maana tayari na yeye alishahisi kuwa Mussa bado anamnyemelea mpenzi wake, ila muda huu bibi Angel nae alienda chumbani kwa Angel na kumtaka ampe ile simu, basi Angel hakuwa na namna aliizima tu na kumpa bibi yake kisha akamuuliza,
“Eeeh bibi kwahiyo hujanimalizia mambo ya mamkubwa Mage”
“Aaaah ila Angel nimekumbuka kile chakula chako cha siku ile, naomba unipikie tena mjukuu wangu”
Kwahiyo bibi aliamua kumzuga Angel kwa namna hiyo kwani alijua lazima kile chakula kitachukua muda wake wa kutosha kisha akamwambia kuwa akimaliza kupika atampa simu ili aendelee kuwasiliana na marafiki zake, kwakweli Angel alifurahi na kwenda kuanza kupika ila wakati huo tu akafika mama Junior yani mama mkubwa mwingine wa Angel, basi walifurahiana pale kisha mama Junior alienda kumsalimia mama yake ambaye alifurahi sana na kusema,
“Naona leo nimekumbukwa sana jamani, wanangu mmeniota nini?”
“Aaaah mama jamani, nimekukumbuka tu”
“Haya, karibu mwanangu tena bora umekuja maana nina dukuduku hatari”
“Lipi tena hilo mama?”
“Niambie kwanza ya kwako”
“Ya kwangu ni kuhusu dada Mage na habari zake za Derrick, kiukweli huwa simuelewi kabisa Mage akianza habari za huyo mtu”
“Kwanza nikukatishe, twende nje kuzungumza hayo”
Basi mama Junior alitoka nje na kuamua kuaga kabisa kwani muda nao ulikuwa umeenda kwahiyo aliona ni vyema kuongea na mama yake nje na kuondoka moja kwa moja.
Walipofika nje ndipo walipoanza kuongea,
“Kwanza huyo Mage kaniudhi hatari, bora umekuja nikwambie hili dukuduku na ujue cha kufanya”
Kisha bibi Angel alianza kumuelezea mama Junior mambo yote yaliyotokea siku hiyo, muda huo walikuwa wakiongea huku wakitembea kuelekea stendi na walifika mahali wakasimama, bibi aliamua kufanya hivyo ili Angel asisikie yale maongezi yao, basi alivyomueleza kila kitu mama Junior akamwambia,
“Mama, kwahiyo tumekuja kuongelea huku barabarani kwanini lakini wakati tungeweza hata kuongea chumbani kwako au hata nje ya geti?”
“Nimehofia mwanangu, Angel asije akatusikia”
Mama Junior alicheka na kusema,
“Jamani mama, unajua Angel hana tabia za kimbea hata kidogo yani yule mtoto anaishi kizungu, umbea ni mtu ampelekee mwenyewe. Hapo angekuwa Erica uwiii hata huku barabarani angekuja kutusikiliza tu, kitoto kimbea kile nahisi hadi anakaribia kupewa medali. Jana niliongea na mama yake anasema Erica akiwa na umbea asiposikilizwa basi anaanza kuongea mwenyewe, yani angekuwa Erica ningekwambia wazi kuwa hakuna la kuficha ila kwa Angel hakuna tatizo lolote maana Angel sio mfatiliaji wa mambo yasiyomuhusu”
“Ila haya yanamuhusu mwanangu!”
“Hata kama, bado Angel hawezi kuja kutegesha sikio sehemu asiyoitwa kuja kusikiliza mazungumzo yani Angel hayupo hivyo, na kuhusu huyo Mage tulia mama yani tulia kabisa, wote ndani hatumuwezi Mage maana akiamua lake kaamua ila kiboko yake ni mama Angel tu. Nitamueleza mama Angel kila kitu hata usihofu na huyo Mage ajipange maana mama Angel ndio huwa wanawezana wale. Unafikiri mama unaweza kumwambia chochote Mage akakuelewa akishaamua lake? Huwa haelewi kitu, ila unadhani ni kwanini hajasema ukweli wa kuhusu Angel hadi leo? Tulia mama, tena ngoja nianze na hilo halafu hili la Derrick litafatia. Rudi tu nyumbani mama ngoja niondoke mimi”
Basi wakaagana pale na bibi Angel akarudi zake nyumbani kwake.
 
SEHEMU YA 253

Baba Angel akiwa nyumbani leo ilibidi amuelezee mke wake kuhusu ujenzi unaoendelea maana kila siku amekuwa akiondoka na wakina Junior halafu mkewe anajua tu kuna ujenzi ila hajui ni sehemu gani,
“Mke wangu, ngoja nikuelezee kuhusu ujenzi unaoendelea”
“Kwanza ni ujenzi wa nini?”
“Unajua unapoamua kuwa mjasiriamali basi lazima uwe mbunifu yani ujaribu kuona vitu vinavyoingiza hela zaidi, nimefanya sana biashara za maduka ya nguo za watoto, nimefanya sana biashara za magari ila pale ninajenga kiwanda kidogo kwa kuanzia kwani nimeona uhitaji wa watu wa eneo lile. Ila nataka pia kuanza kumfundisha Erick ili asiwe mzembe, nahitaji Erick awe kama mimi”
“Oooh ni vizuuri ila ni eneo gani hilo?”
Baba Angel alimtajia eneo ambalo anafanya ujenzi huo na kumfanya mama Angel ashtuke sana, basi mumewe akamuuliza,
“Mbona umeshtuka hivyo mke wangu?”
“Mmmh sijui, unajua nini hiyo sehemu ndio ambako wanaishi yule mr.Peter na mke wake”
“Unamaanisha wazazi wa Rahim?”
“Ndio”
“Aaaah watajijua wenyewe, cha muhimu sie tunafanya mambo yet utu. Yani tusindwe kutafuta sehemu bora za biashara sababu yao! Watajijua wenyewe”
Huwa baba Angel hapendi kufanya akili yake iwaze mambo kama hayo yani huwa hapendi kabisa ukizingatia ana mambo mengi ya kuwaza.

Wakati wote wameondoka nyumbani kwa siku hii, alibaki tu mama Angel na Vaileth na muda huu Erica alikuwa amelala ila mama Angel alipigiwa simu na mama Junior ambaye alimpa habari ya dada yao mkubwa Mage, basi aliamua kwenda chumbani kuongea nae,
“Hivi kwani dada ananitakia nini mimi jamani? Unajua mistake kunikumbusha mambo ya ajabu ambayo mnataka kunifanyia, hivi mtoto wangu wa kwanza si angekuwa wa Erick kama msingeenda kunitoa ile mimba? Sasa tatizo liko wapi nikimpa Angel Erick? Na hata isingekuwa hivyo bado Erick yupo upande wangu sana, kaifuta aibu yangu na fedheha, tatizo liko wapi nikimtunuku mtoto ambaye baba yake haeleweki. Yeye kinamuuma nini ikitokea Angel katembea na kaka yake? Kwanza asinichanganye kabisa, huyo Rahim ana watoto kila kona ya nchi halafu na mwanangu nimdumbukize huko, halafu huyo dada Mage, ni siku nyingi haji kwangu kumbe ana yake ameyatunza, anitolee balaa mie”
Basi aliongea nae ila mama Angel alichukia sana ila hakutaka hata kumpigia simu kwa siku hiyo dada yake.
Alivyokata ile simu alirudi sebleni, na kutoka nje ila alimkuta Vaileth amejiinamia tu basi alianza kumuuliza pale kuwa tatizo ni nini,
“Yani huko nyumbani wamenipigia simu kuwa mvua zimeanza na nyumba ya wazazi wangu inavuja, natamani ningekuwa na pesa niwaweke bati wazazi wangu”
“Oooh pole jamani Vaileth, ila usijali nitajadili na mume wangu jioni ya leo”
“Oooh asante sana mama, nashukuru kwa hilo ila pia mama kuna ndoto ambazo sio nzuri nazipata”
“Ndoto gani hizo Vaileth?”
“Samahani mama kama nitakukwaza, ni kuhusu huyu madam Oliva, yani nikilala nahisi kama kuna mambo anataka kumfanyia baba, nahisi kama anataka kumvuta baba”
“Mmmh asante kwa ujumbe Vaileth”
Kisha muda huo huo mama Angel alirudi ndani kwani aliona akili yake ikianza kuchanganyikana sasa.

Baba Angel akiwa kazini siku ya leo akiendelea na kazi zake, mara kama kawaida alifika madam Oliva na kumsalimia pale huku akijiongelesha mambo mbalimbali kisha akatoa bakuli ambalo aliweka matunda, ni kweli yale matunda yalikuwa yanavutia sana kiasi cha kumfanya baba Angel kuyatamani, basi madam Oliva huku akitabasamu akamwambia,
“Leo nimeona utakuwa na hamu sana na matunda baba, nimekuletea haya”
“Oooh nashukuru sana madam Oliva”
“Ni matamu sana, hebu onja kidogo”
Mara simu ya baba Angel kuna ujumbe uliingia, basi akaangalia na kuona kuwa ujumbe ule umetoka kwa mke wake basi alianza kuusoma,
“Erick nakuomba mume wangu usiwe karibu na madam Oliva, nakuomba sana usile chochote kile anachotaka ule. Kama unataka chochote utakipata nyumbani mume wangu, nakupenda sana”
Kwanza kabisa baba Angel alitabasamu kwani ujumbe wa namna hii umekuwa adimu sana kwake toka kwa mke wake toka wawe ndani ya ndoa, kwahiyo akajikuta anafuraha sana kisha akamuangalia madam Oliva na kumwambia,
“Oooh madam samahani, nimekumbuka kitu jamani dah! Uroho huu, kumbe nimefunga leo”
“Khaaa kumbe huwa unafunga baba Erick! Ila kwenye kufunga wanasema ukitamani kit utu umefungulia kwahiyo ni bora ule tu”
“Aaaah hapana bhana, mimi nishakubaliana na mke wangu kuwa tutafungulia jioni nikiwa nyumbani, hata kama nimetamani basi nitatubu tu mbele za Mungu ila kula siwezi kwakweli, nisamehe sana madam”
“Mmmh jamani, sawa basi”
Madam Oliva hakutaka hata kukaa zaidi kwani aliaga na kubeba bakuli lake la matunda na kuondoka zake.
Baba Angel alikaa kwa muda akimtafakari mke wake, yani alijihisi amani kubwa sana katika moyo wake na kujisemea,
“Oooh leo nitaenda tena kwenye duka lile kumnunulia mke wangu zawadi”
Na muda huo huo aliinuka na kutoka ofisini kwake, na moja kwa moja alipitia kwanza kwenye lile duka kununua zawadi halafu ndio aende kwenye ujenzi, aliwakuta baba Emma na Mama Emma wapo kama kawaida ila hawa wana ndoa nao walionekana kufurahiana sana kuwa pamoja na kufanya shuguli pamoja, basi walimkaribisha vizuri sana na moja kwa moja aliongea nao kuwa anahitaji zawadi nyingine ya mke wake, basi baba Emma akamshauri,
“Leo mchukulie mkoba, anaweza kuwa na mikoba mingi sana ila utakaomchukulia wewe ndio atauona maridadi. Na ubora wa mikoba yetu ya hapa ni lazima mke wako apende”
Baba Angel akatabasamu na kuuliza,
“Sasa nitamchukulia mkoba gani jamani!”
Baba Emma alionyesha mkoba ambao hata mama Emma aliupenda na hata baba Angel aliupenda pia basi walimfungia na kuondoka nao kwani alitaka kumpelekea mke wake.

Junior na Erica kwenye ule ujenzi, muda mwingi Junior alionekana na mawazo kiasi na kumfanya Erick amuulize,
“Kwani tatizo nini Junior?”
“Hivi katika maisha yako umewahi kupenda?”
“Ndio kusema unampenda hivyo dada Vai?”
“Nampenda ndio ila…!”
Baba Angel alifika muda ule na kuangalia nao ujenzi na kufatilia ya hapa na pale kisha baada ya hapo kuwataka wote warudi nyumbani.
Walipofika nyumbani tu baba Angel alimkabidhi mke wake ile zawadi na kumfanya mke wake afurahi sana,
“Asante kwa zawadi mume wangu, naona siku hizi unapatia sana ninavyovipenda”
“Ndio, sababu wewe ni mke wangu wa pekee”
Mama Angel alikuwa akitabasamu tu kisha mumewe akamwambia,
“Unajua ujumbe wako wa leo umenihamasisha sana, jamani mama kuwa hivi hivi kwangu na ikiwezekana ongeza zaidi ili nipagawe mtoto wa mwanamke mwenzio”
Mama Angel alicheka na muda huo aliamua kumwambia pia swala la Vaileth ila sababu baba Angel alikuwa na furaha sana akamwambia mke wake,
“Kuna hela nilitaka kwenda nazo kesho mahali, ila naenda kumpatia Vai ili atume kijijini kwao, maana kumbuka tuliahidi kumsaidia, naomba mke wangu usikatae”
“Mmmh sikatai, ni kiasi gani?”
“Milioni mbili”
“Jamani yote hiyo mume wangu!”
“Aaaah jamani mke wangu kumbuka huyu kabeba dhamana zetu, huyu anatutunzia nyumba yetu kwasasa, anatuandalia chakula na kutufanyia mambo mengi sana”
Kisha baba Angel alimsogelea mke wake na kumbusu halafu akamuuliza tena,
“Tumpe ngapi mke wangu?”
“Hakuna tatizo, mpe tu hiyo uliyosema”
Basi baba Angel alimkabidhi ile pesa mke wake ili akampe yeye mwenyewe, kwahiyo mama Angel alitoka na kwenda kuongea na Vaileth na kumkabidhi ile pesa, kwakweli Vaileth alifurahi sana maana aliona kama ndoto vile.
Vaileth alimshukuru sana baba Angel na mama Angel kwa moyo wao wa kipekee sana.
 
SEHEMU YA 254

Usiku wa siku hiyo, wakati Junior yupo na Vaileth, alimuona akiwa na furaha sana na kumuuliza kilichomfyrahisha vile basi Vaileth alimueleza kile kilichotokea kuhusu pesa aliyopewa na bosi zake,
“Oooh jambo jema hilo mke wangu jamani, ila kuna kitu nataka nikuombe”
“Kitu gani hiko?”
“Katika hiyo hela naomba unikopeshe laki tano maana kuna mambo ya maendeleo nataka kufanya ila niliwaza kuwa pesa nitapata wapi, sema Mungu ni mwema sana naomba unifanyie hivyo Vai”
“Mmmh jamani Junior!”
“Kwani hunipendi Vai!”
“Nakupenda sana Junior”
“Basi naomba nifanyie hivyo”
Vaileth hakuwa na namna zaidi ya kumpa hizo laki tano Junior ambaye alifurahi sana na siku hiyo alimpa Vaileth mapenzi mazito sana maana hela aliyokuwa akiitaka aliipata tayari.
Kulipokucha tu siku hiyo Junior na Erick waliondoka mapema sana kwani walitakiwa kuondoka na dereva ila baba Angel alikuwa bado kalala kwani hakupanga kuwahi kwa siku hii.

Ile asubuhi mama Angel aliongea na mumewe wakati akijiandaa kwenda kazini,
“Ila unajua mume wangu hatujafanya kitu kizuri kumpa pesa mkononi Vaileth”
“Sasa tungefanyeje mke wangu?”
“Yani tulitakiwa kuongea nae halafu tuwatumie wazazi wake moja kwa moja na kama nyingine ya kumuwekea tumuwekee ila hivi tulivyofanya hatujafanya vizuri maana yeye mpaka aende kutuma kwenye simu huko, wakimuibia je!”
“Nimekuelewa mke wangu, ila hakijaharibika kitu muite Vai akupatie ile pesa ili mimi nikaweke kwenye simu yako kisha wewe utamtumia kwa namba za ndugu zake hapa au tufanyeje?”
“Sawa mume wangu”
Basi mama Angel alienda kumuita Vaileth na kumwambia,
“Vai, naomba ile hela ya jana ili tuitume moja kwa moja”
Vaielth alipumua na kuangalia tu chini kimya

Basi mama Angel alienda kumuita Vaileth na kumwambia,
“Vai, naomba ile hela ya jana ili tuitume moja kwa moja”
Vaielth alipumua kwanza huku akimkodolea macho tu mama Angel.
Mama Angel alimshangaa na kumwambia tena,
“Wewe Vai hunisikii au ni kitu gani?”
“Nakusikia mama”
“Sasa unangoja nini kutekeleza?”
Vaileth akaondoka na kwenda chumbani kwake na kuzitoa zile milioni moja na laki tano huku akiwaza kuwa itakuwaje, aliwaza kwa muda sana kule chumbani hadi mama Angel alimuita tena kwa nguvu na kurudi na zile pesa, basi mama Angel akamuuliza,
“Vipi wewe upo sawa?”
“Nipo sawa mama”
“Haya, zilete”
Muda huo baba Angel alitoka chumbani pia na aliuliza,
“Zipo zote?”
Vaileth alijiuma uma tu na kujibu,
“Zipo milioni moja na laki tano”
Mama Angel alishangaa sana na kumuuliza,
“Laki tano nyingone iko wapi?”
Vaileth aliinama tu chini bila ya kujibu chochote, basi baba Angel akasema,
“Itakuwa kaiweka kwaajili ya matumizi yake”
“Matumizi gani ndani ya nyumba hii laki tano jamani! Eeeh Vain i matumizi gani hayo?”
Vaileth alikuwa kimya tu, kiukweli hata jinsi ya kuanza kujieleza hakujua kuwa aanzie wapi maana wakimwambia hata alete wazione ni kazi bure maana hana hizo pesa, basi baba Angel ikabidi akate yale maneno na kumuomba mke wake asifoke sana kisha akachukua zile pesa na kuondoka nazo ili kwenda kufanya kama ambavyo aliahidi.
Walibaki mama Angel na Vaileth sasa ambapo mama Angel alimwambia Vaileth,
“Vaileth, mimi ndio ningekuwa wewe nimepata kazi mahali kama hapa ambapo mabosi wana upendo basi ningepatumia kama njia kwangu ya kupata maendeleo. Unashindwa kusema kuwa jamani ninahitaji kitu Fulani au kitu Fulani unashindwa Vai? Unashindwa hata kusema naomba mnifungulie akaunti ili niweke japo hela zangu humo kuna leo na kesho ujue, unatakiwa kujiandaa katika maisha. Shauri yako, kaa na pesa upigiwe simu zisizoeleweka kukukopa hizo hela, oooh nimekumbuka kitu kwanza simu yako ninayo mimi taarifa za ndugu zako ulizipata wapi?”
“Niliwapigia kwa simu hiyo ya mezani mama”
Basi mama Angel alienda ndani kwake na kutoa ile simu ya Vaileth na kumkabidhi maana tangu ameichukua kipindi kile hakuirudisha.

Leo walivyofika tu kwenye ujenzi baada ya muda kidogo Junior aliondoka, yani hata Erick hakujua kuwa Junior ameenda wapi ila muda huo Junior moja kwa moja alienda kwa bibi yake Samia ili kuonana na Samia.
Alifika pale na kugonga geti halafu akaamuulizia Samia ambaye aliitwa na kutoka ndani na kumkaribisha junior,
“Karibu sana Junior”
“Asante, nakupenda sana Samia”
“Oooh kumbe hunielewi au? Nilikwambia kunitongoza mimi ni laki tano”
“Nimekuletea Samia”
“Wow, iko wapi?”
Junior akamtolea Samia hela ambayo alienda nayo kwa lengo la kumpa na Samia akafurahi sana kisha Junior akamwambia,
“Sasa Samia, inatakiwa mimi na wewe tupate sehemu ya kuzungumza vizuri ili tuyajenge”
“Sehemu gani?”
“Ikiwa guest itapendeza zaidi”
“Mmmh guest? Hapana, siwezi kupelekwa guest mimi”
“Kwahiyo wapi unataka?”
“Nataka twende labda hotelini”
“Mmmh jamani Samia mbona unapenda vitu vya gharama hivyo?”
“Sababu na mimi ni wa gharama, baba yangu huwa ananiambia kuwa mimi ni wa gharama sana. Ngoja nikutajie hoteli ya kwenda, sitaki za ajabu ajabu”
“Mmmh hoteli gani hizo?”
Samia akamtajia na kumfanya Junior ashtuke kidogo ambapo Samia akamwambia,
“Yani nimekutajia hoteli ya chumba cha kulala laki moja umeshtuka hivyo ningekutajia zaidi je ingekuwaje?”
“Hamna Samia, sijashtuka kwa ubaya mpenzi wangu. Ila Samia ni kweli hujawahi kuwa na mahusiano wewe? Hujawahi kulala na mwanaume?”
“Ndio sijawahi, unanionaje kwani? Mimi siwezi kuwa na mwanaume mtu mzima, na wanaume wadogo wengi hawana hela, huwa nikiwaambia waniletee laki tano wanajiuma uma ila naona wewe umeweza, na kwa hakika utakuwa mpenzi wangu tu”
“Basi Samia, naomba Jumamosi hii tukutane”
“Aaaah sio Jumamosi, fanya Ijumaa maana Jumamosi nahisi kamavile baba atakuwepo”
“Sawa hakuna tatizo, basi Ijumaa tutakutana ila naomba umaanishe Samia”
“Usijali, tutakuwa tunawasiliana basi”
Na muda ule Samia akampa Junior namba anayotumia kwa siku hizo na kumfanya Junior afurahi sana basi waliongea sana pale na kuagana ambapo Junior akamwambia Samia,
“Jamani hata kunikumbatia au kunibusu?”
“Mmmh haiwezekani kwa muda huu, itawezekana Ijumaa”
Basi Junior hakuwa na namna ila alichotaka ni kumpata Samia tu, yani yeye alihisi kuwa akishalala nae tu basi ataridhika na roho yake.
Alirudi kule kwenye ujenzi na kumkuta Erick na baba Angel basi baba Angel alimuuliza,
“Kheee Junior ndio ushazoea huku na kuanza kuzurula?”
“Hapana bamdogo ila kuna rafiki yangu hakai mbali na hapa nikaona ni vyema nikienda kumsalimia”
“Oooh sawa hakuna tatizo”
Basi waliendelea na kazi ndogo ndogo za pale na walipomaliza tu waliondoka na kurudi nyumbani.
Wakiwa njiani kurudi nyumbani, leo Erick alimuona Elly na binti mwingine ambaye alikuwa kama kipofu ila Erick hakumshtua baba yake kuhusu hilo na kukaa kimya tu hadi wanaingia nyumbani kwao hakusema lolote kama kuna mahali kamuona Elly.
 
SEHEMU YA 255

Basi usiku wa leo, baba Angel aliwaita Junior na Erick na kuwaambia kuwa kesho yake watapumzika kwenda kwenye ujenzi halafu wataenda tena kesho kutwa,
“Kesho Alhamisi mtapumzika ila Ijumaa kuna kazi kubwa kidogo kwahiyo inabidi twende mapema sana, yani Ijumaa hata mimi sitaenda ofisini”
Waliitikia pale ila Junior alikuwa na miadi yake Ijumaa kwahiyo aliwaza jinsi gani ataikwepa siku ya Ijumaa ili aweze kwenda kukutana na Samia na hata hivyo alihitaji pesa za kufanya hivyo, basi akiwa anawaza baba Angel akawaambia jambo lingine,
“Ila Ijumaa baada ya kazi ile nitawapa pesa ili Jumamosi kila mmoja akajinunulie kitu anachokitaka”
Ile ilikuwa ni habari njema sana ila kwa upande wa Junior kidogo haikukaa vizuri kwani alikuwa na mawazo mengi sana juu ya Samia ila aliitikia tu kwani aliwaza kumshawishi Samia ili wakutane Jumamosi.
Kwahiyo baada ya kuwaambia hayo kila mmoja alirudi chumbani kwake, na Junior kitu cha kwanza kabisa ni kuwasiliana na Samia ili amsikie atasemaje,
“Samia mpenzi wangu, naomba tuonane Jumamosi”
“Mmmh si nimekwambia Junior kuwa Jumamosi haitawezekana, ni Ijumaa tu”
“Unajua Ijumaa kuna dili la hela nyingi sana nataka kufanya ili Jumamosi nikununulie zawadi nzuri sana Samia”
“Oooh sasa utaangalia mwenyewe kati ya hilo dili na mimi kipi ni cha muhimu, kwahiyo utaamua kama kukutana na mimi au kwenda kwenye hilo dili. Sina maneno mengi mimi nimemaliza”
“Mmmh jamani Samia mbona unakuwa hivyo!!”
“Sio kosa langu ila ni baba yangu ndio kanifundisha jinsi ya kumchunguza mwanaume”
“Mmmh ila jaribu basi iwe Jumamosi”
“Nishakwambia Jumamosi haiwezekani mbona hunielewi Junior!”
“Basi malkia wangu, tutakutana Ijumaa”
Yani muda huo akili ya Junior inagonga mwamba tu kila muda, kiukweli hakuelewa kabisa cha kufanya kwake ilikuwa moja haikai wala mbili haikai akajikuta siku hiyo hata anasahau kwenda kulala chumbani kwa Vaileth wakati ni kawaida yake kwenda kulala chumbani kwa Vaileth.
Alijikuta akiwa na mawazo hadi usingizi ulimpata na kushtuka wakati pamekucha kabisa, akawaza cha kufanya kwa muda huo,
“Nitapata wapi hiyo laki moja ya kukodi chumba? Ila lazima niipate maana kale kajinga kashamaliza laki tano yangu! Na nikimpata huyu binti atasimulia ukoo wake mzima”
Basi likamjia wazo kuwa aende kwa mama yake kumuomba hela ila hakuwa na uhakika kama mama yake angempatia pesa kwa siku hiyo, yani akachekecha akili yake sana, akachukua simu yake na kukutana na ujumbe toka kwa Vaileth,
“Jana ndio ulichoka sana Junior? Mbona hukuja chumbani kwangu, nilitaka uje ili tuongee kuhusu hili swala”
Alijua kuwa alifanya makosa na kujisema,
“Ila sisi wanaume loh! Kwa Vai Napata kila kitu yani hakuna ambacho sipati na ninaishi nae kama mke wangu ila nimechukua na laki tano yake kwenda kumpelekea mwanamke mwingine ili tu nikamuonje huyu mwanamke, sijui tamaa nitaacha lini mimi! Nitaacha hadi nikilala na Samia kwakweli, huyu mtoto kaniingia sana akilini”
Basi akaamka na kuoga na kujiandaa ili aende kwa mama yake.

Ila moja kwa moja Junior alienda kwanza jikoni ili kumpooza Vaileth kwani anajua kuwa amechukia, basi alimkuta jikoni na kumbusu ambapo Vaileth alishtuka kidogo halafu alianza kumwambia kwa sauti ya chini,
“Nisamehe mpenzi wangu, yani jana nilichoka sana halafu usiku nikajiwa na ndoto mbaya kuwa mama yangu ni mgonjwa, nikaamua kumpigia simu na kukuta kweli anaumwa ila hakutaka nimueleze mtu yoyote kuhusu kuumwa kwake kwahiyo hata mamdogo usimwambie, namuaga tu kuwa naenda kumsalimia mama si unajua mimi ni mtoto wa pekee kwetu”
“Naelewa hakuna tatizo”
“Basi kwaheri”
Junior akambusu tena Vaileth na kutoka ila kwenye mlango wa kuingia jikoni akapishana na Erica ambaye alikuwa anaenda jikoni pia ila hakufikiria kama Erica amesikia chochote kile maana alikuwa akiongea na Vaileth kwa sauti ndogo sana.
Basi alisalimiana nae tu na kuondoka zake na hata Erica jikoni hakumuuliza chochote kile Vaileth zaidi ya kuanza kumsaidia kazi tu.

Junior alienda kumuaga mama Angel kuwa anaenda kumsalimia tu mama yake, naye mama Angel hakumkatalia zaidi ya kumpatia Junior nauli tu ya kwenda huko kwa mama yake.
Basi Junior aliondoka ila huku akiwaza vitu mbali mbali vya kufanya, aliwaza kupata pesa kwa mama yake na kuona ni kazi ila akasema acha aende kujaribu tu.
Junior alivyofika tu alimkuta mama yake nyumbani na kukaribishwa vizuri tu,
“Oooh naona mwanangu umenikumbuka leo”
“Ndio, nimekukumbuka mama”
Basi baada ya maongezi ya hapa na pale, Junior akamjaribu mama yake,
“Halafu mama, nilikuwa na shida na kama laki moja hivi!”
Mama Junior akashtuka kidogo na kumuuliza,
“Weee Junior, laki moja ya nini tena?”
“Nina shida nayo mama”
“Junior mwanangu, naona huko kwa babako mdogo kunakuchanganya akili jinsi unavyowaona wanamiliki pesa nyingi, mwanangu pesa zinatafutwa kwa kufanya kazi. Sasa wewe laki moja unataka ya nini jamani! Mara mwisho umesema sherehe, haya leo ya nini?”
“Mmmh mama na wewe jamani, angekuwa mamdogo hapa angenipa haraka sana”
“Mbona hujamuomba sasa umekuja kwangu!”
“Jamani, wewe ndio mama yangu yani nitegemee kwa mama mdogo kila kitu kweli! Wewe ndio mama yangu na unajukumu la kunihudumia sababu mimi ni mwanao”
“Ila sio kwa huduma hizo za kukupa laki moja, mimi sina hela kwanza hapa nilipo nina kadi za michango ya harusi kibao ndani kwangu hata sielewi itakuwaje, na wewe unazidi kuniumiza kichwa tu. Sina hela Junior”
“Sawa mama, sijakulazimisha ila leo nipo hapa nitalala hapa kwahiyo kwa mamdogo nitarudi kesho”
“Oooh sawa”
Junior akampigia tu simu mama yake mdogo kumtaarifu kuwa siku hiyo hatorudi nyumbani sababu analala kwa mama yake, naye mama Angel alimuelewa sababu ni muda kidogo Junior hakwenda nyumbani kwao.

Basi leo baba Angel akiwa yupo kazini akiendelea na shughuli zake za kikazi maana huwa lazima azimalize kwanza halafu ndio aende kwenye ujenzi wake, akatembelewa na madam Oliva ila huyu madam leo alionekana kutabasamu sana kanakwamba sio yule aliyekataliwa matunda, kisha madam Oliva bila hata salamu alimwambia baba Angel,
“Nina habari njema kwako”
“Eeeh habari gani hiyo?”
“Matokeo ya kidato cha nne yametoka, halafu Angel na Junior wamefaulu vizuri tu”
“Oooh hizo ni habari njema kweli, kumbe majina ya wanangu unayajua eeh!”
“Ndio nayajua, nimewafatilia maana niliwauliza shule walizokuwa wakisoma. Basi nilipoona tu matokeo yametoka ikawa ndio kitu cha kwanza kabisa kuangalia matokeo yao”
“Nashukuru sana madam kwa kujitoa kwako”
“Kwahiyo ni muda wa kushereke, unajua watoto wakifaulu ni furaha sana kwa wazazi, inatakiwa kusherekea na kuwatafutia watoto zawadi”
“Ni kweli, ni jambo jema sana, ila mimi nina shughuli nyingi mno, hata muda wa kuwatafutia zawadi watoto huwa sina”
“Mke wako je!”
“Oooh yule ni wa muhimu sana kwangu, yani siwezi fanya kitu bila kumfikiria yeye. Nikimuahidi zawadi hata kama nimetoka kwenye shughuli zangu saa tano usiku basi hiyo zawadi nitaitafuta tu. Nampenda sana mke wangu”
“Mmmh!”
“Unaguna nini madam?”
“Unajua wewe ni mwanaume wa tofauti sana, jamani ni ngumu kwa mwanaume kumsifia mke wake mbele ya mwanamke mwingine, ni ngumu sana. Ila wewe muda wote utamsifia mke wako na utasema jinsi gani unavyompenda”
“Mbona hivi bado sijamsifia kabisa, hizi sio sifa, nikianza kutoa sifa za mke wangu mimi utabaki umeduwaa tu, kwanza mke wangu ana akili sana, mke wangu ni mcha Mungu, mke wangu sio malaya, mke wangu sio mchafu, mke wangu ni mzuri, mke wangu ana upendo, mke wangu….”
“Eeeeh basi jamani, hukawii kusema mkeo ndio bora zaidi hata chumbani kuliko wanawake wote”
“Ni kweli, mke wangu ni namba moja kuliko wanawake wote, acha nimpende mke wangu maana kakamilika kila kitu”
Madam Oliva akapumua kidogo ila hata hakutaka kukaa sana na kusema,
“Shule walizopangiwa zikitoka nitakuja kukwambia, kwaheri”
Basi madam Oliva aliinuka na kutoka nje ya ile ofisi ila baba Angel hakujali kitu chochote maana yeye aliona ni kawaida kwake kumsifia mke wake.
 
SEHEMU YA 256


Kwakweli madam Oliva aliumia sana kwa siku hii kupata siku zozote anazoongea na baba Angel na kwa muda huo aliamua kwenda mahali ili kupumzisha akili yake, ila akiwa huko akakutana na rafiki yake ambaye nae alikuwa sehemu hiyo kwahiyo walifurahiana na kuanza kuongea mawili matatu,
“Kumbe na wewe Oliva huwa unakuja huku!!”
“Mimi mwenzio bachela, nikushangae wewe mke wa mtu unafanya nini huku?”
“Aaaah mke wa mtu bongo!! Mimi nipo huku kutuliza mawazo, wee ndoa hizi ziachege tu yani mambo ya ndoa jamani loh!”
“Nini tena wakati tusio na ndoa tunatamani kuingia kwenye ndoa!!”
“Ingia tu shoga yangu ila kuna watu tuna mawazo hadi tunatamani kutoka, sema watoto wangu ndio wananiumiza kichwa inabidi tu nivumilie. Eeeh vipi Oliva ni shemeji gani huyo umempata? Nakumbuka wakati tupo Sekondari ulikuwa ukiponda wanaume wewe, nadhani ndio sababu ya kutokuolewa hadi leo. Hata ulipozaa kila mtu alijiuliza imekuwaje kwa Oliva kuzaa jamani, hata baba mtoto wako hutaki kumuonyesha, sasa nani huyo kapata Bahati ya kukubaliwa na wewe kwenye swala la ndoa?”
Madam Oliva alicheka na kusema,
“Mwenzangu, nihurumie tu mwenzio nampenda mume wa mtu”
“Aaai shoga yangu, mume wa mtu tena!! Aaah hata sikushauri jamani, mume wa mtu wa kazi gani jamani! Kuna wanaume wengi tu wapo hawajaoa, sasa wewe ukazane na mume wa mtu wa nini?”
“Ana mapenzi ya dhati shoga yangu, katika maisha yangu sijapata kuona mwanaume wa aina yake, kiukweli nahitaji kuolewa nae, natamani akubali niwe hata mke wa pili jamani nimezama shoga. Ila tatizo lake kila ukikutana nae ni kumsifia mkewe tu”
“Nimekwambia shoga hebu acha hayo mambo utajiumiza kichwa bure, wewe ni mwanamke msomi na una pesa kwanini uhangaike na mume wa mtu jamani. Mke wake akijua unajua atakudhalilisha, hebu achana na mambo hayo. Kwanza ndoa haina maana yoyote. Mwenzio hapa mume wangu ananiletea watoto kila siku nyumbani, karibia tunakuwa na timu mbili za mpira tuanzishe mechi mule mule ndani”
“Mmmh Fetty usiniambie jamani, mbona shemeji anaonekana mpole!”
“Wapole hao waogope shoga yangu, hawana maana hata kidogo, waogope kabisa. Najuta mimi ila nitafanyeje sasa, navumilia tu”
Basi wakaongea pale na kuanza kukumbushana mambo ya zamani ya shuleni na kucheka sana kisha kuamua kuondoka, na muda huu madam Oliva aliamua kumpa lifti rafiki yake hadi nyumbani kwake.

Siku hii baba Angel alichelewa kiasi kurudi nyumbani ila alimpa mke wake ile habari ya kufaulu kwa Junior na Angel, naye mama Angel alifurahi sana hata kutamani kupiga simu muda huo ila sababu aliona muda umeenda akasema kuwa atapiga kesho yake, basi baba Angel alimuulizia Junior na kuelezwa kuwa Junior kaenda kwao,
“Aaah jamani Junior nae, kwanini lakini wakati tulipanga vizuri, basi nitaenda na Erick tu”
Ila sababu baba Angel alikuwa amechoka sana akaamua tu kulala muda huo.
Kulivyokucha, ikabidi baba Angel aondoke na Erick tu maana Junior hakuwepo wala nini.
Basi nyumbani walibaki wale wale wa siku zote, baada ya kazi zake mama Angel aliamua kwend kukaa sebleni na kuangalia Tv ila muda huo alishasahau habari za matokeo ya wakina Angel na Junior.
Kwa muda huo alikuwa amekaa na Erica tu, mara kuna habari ilipita,
“Matokeo ya kidato cha nne mwaka huu, wasichana wang’ara”
Erica akamshtua mama yake,
“Mama, je matokeo ya kaka Junior na dada Angel yakoje?”
“Oooh nilisahau eti, wamefaulu maana baba yenu aliangalia tena ngoja nimpigie bibi yenu ili Angel apate habari juu ya ufaulu wake, halafu nimpigie mama Junior”
“Mmmh!”
“Mbona umeguna Erica?”
Erica akasogea karibu kwa mama yake na kuanza kumwambia,
“Basi nikwambie mama, mama Junior anaumwa ndiomana Junior kaenda huko jana na hajarudi”
“Kheee dada yangu anaweza akaumwa kweli na mimi nisipate habari!”
“Kweli mama, ila nasikia wamesema usiambiwe wewe ni siri”
“Hivi kuna ugonjwa wa siri jamani! Hebu kaniletee simu yangu washanichanganya tayari, kweli dada yangu anaumwa kimya kimya jamani loh!”
Erica akaenda kumletea mama yake simu ila alipiga aliona simu inakatwa na kumfanya achukie sana, yani akatamani hata kwenda ili akaangalie mwenyewe hali ya dada yake.

Muda huu Junior alikuwa na mama yake, na aliona dalili ya kupata pesa kwa mama yake ilikuwa ni ndogo mno, basi akaamua kumuomba simu mama yake,
“Mama, samahani naomba simu nimpigie mamdogo maana alisema nikitaka kutoka huku nimtaarifu”
Basi mama yake alimpatia simu yake halafu yeye akaenda kuendelea na kazi zake zingine, basi Junior alipekua majina ya ile simu akakuta kuna namba mama yake kaandika ‘Daktari’ Junior akatabasamu kisha akatuma ujumbe kwenye ile namba,
“Ndugu yangu nina shida sana, nimekwama hapa na ninahitaji sana pesa. Naomba uniazime laki mbili, kwenye siku mbili hizi nakurudishia ndugu yangu”
Basi ujumbe ukarudishwa muda huo huo,
“Usijali mama Junior, shida yako ni kama yangu nakutumia muda sio mrefu”
Na kweli muda sio mrefu ikaingia laki mbili kwenye simu ya mama Junior, basi muda huo huo Junior akairusha kwenye simu yake na kuandika ujumbe mwingine,
“Asante sana ndugu yangu, yani ndani ya siku mbili hizi nakurudishia”
Mara simu ile ilianza kuita, kuangalia akaona ni mama yake mdogo anapiga, basi akawa anaikata ili isimsumbue, kisha ukaingia ujumbe toka kwa yule daktari,
“Hakuna tatizo Bite, wewe ni kama ndugu yangu”
Basi Junior alifuta zile jumbe zote kisha akamrudishia mama yake simu na kumuaga kwani muda huo huo aliondoka zake ukizingatia alishapata hela aliyokuwa akiitaka tena na zaidi.

Junior alifika kwenye hoteli ambayo kapanga na Samia, basi alikodi chumba na kununua vinywaji halafu akakaa chumbani sasa akimsubiria Samia huku akiwasiliana nae,
“Samia mpenzi, mimi nishafika tayari”
“Oooh vizuri sana Junior, nipe kama nusu saa nitakuwa hapo, ila ushakodi chumba?”
“Ndio, nipo chumbani sasa”
“Hapo sawa, nakuja basi muda sio mrefu si unajua mimi bado mdogo sio vizuri tukionekana nje, ni bora umekodi chumba”
“Nakusubiri basi kipenzi changu”
“Yani nusu saa tu, usijali Junior”
Basi Junior alikuwa akimsubiria Samia ila yalipita masaa mawili bila ya Samia kuonekana wakati kamwambia ndani ya nusu saa, akaanza kupiga simu ya Samia ila ikawa haipokelewi wala nini yani Junior alichukia sana, mara ukaingia ujumbe toka kwa Samia,
“Samahani Junior, baba alikuja na kunilazimisha kwenda kuswali. Na sasa nipo nae nyumbani kwahiyo sitaweza kuja leo, nisamehe sana”
 
SEHEMU YA 257

Basi Junior alikuwa akimsubiria Samia ila yalipita masaa mawili bila ya Samia kuonekana wakati kamwambia ndani ya nusu saa, akaanza kupiga simu ya Samia ila ikawa haipokelewi wala nini yani Junior alichukia sana, mara ukaingia ujumbe toka kwa Samia,
“Samahani Junior, baba alikuja na kunilazimisha kwenda kuswali. Na sasa nipo nae nyumbani kwahiyo sitaweza kuja leo, nisamehe sana”
Junior alisoma huu ujumbe wa Samia mara mbili mbili na kuhisi akili yake ikiruka kabisa, basi aliamua kumpigia simu ila simu iliita tu bila kupokelewa na mwisho wa siku simu ilikuwa haipatikani, kwakweli Junior alichukia sana na kujisemea,
“Kwakweli mimi ni lofa, tena bonge la lofa, nimechukua hela kwa Vaileth mwanamke anayenipa mapenzi yote na kumpelekea yule mjinga Samia, na sasa nimeenda kumuwekea mama yangu deni ili nije kujivinjari na Samia, kwakweli mimi ni lofa sana. Yani Samia anajifanya mtoto wa mjini eeeh! Kweli maisha ni tofauti sana, Vaileth ni mkubwa ila mengi hayajui, ila Samia ni mdogo na mengi anayajua. Dah huyu dogo kaniweza ila lazima nitamkomesha tu”
Basi alikuwa akijifikiria pale, roho ilimuuma sana kwani tayari alishatoa hela pale ya chumba, na tayari alishanunua vinywaji yani akili yake haikufanya kazi kabisa, akawaza tena,
“Au niende kununua changudoa nije kulala nae humu! Jamani, hela yangu iende bure bure tu”
Hapo akaona ni vyema akanunue wanawake wa kujiuza ili hela yake isiende bure.

Bado mama Angel alikuwa akijiuliza sana kuwa ni kwanini dada yake amfiche kuhusu ugonjwa, basi muda huo aliamua kumpigia tena simu ila muda huu mama Junior alipokea na kusalimiana nae pale,
“Dada nasikia unaumwa ila unafanya siri, kwanini dada jamani!”
“Kheeee jamani niumwe halafu nifanye siri!! Haiwezekani kwakweli, nani huyo aliyekupa hizo habari?”
“Nasikia ndivyo Junior alivyosema jana”
“Jamani Junior niliongea nae muda gani mimi! Kwanza jana nilionana nae huku nyumbani ila kabla ya hapo hakuna chochote ambacho niliongea nae, mimi ni mzima wa afya njema kabisa”
“Sawa dada, yani nilishtuka sana kusikia unaumwa ila unafanya siri”
“Siwezi kufanya hivyo mdogo wangu”
Basi mama Angel aliagana na mama Junior na kumuita Erica sababu alitaka kujua kuwa Erica maneno hayo kayatoa wapi, alitambua kama mwanae ni mbea ila katika swala la uongo hakumuweka maana huwa mara nyingi anasema kitu alichokisikia, basi Erica akaenda,
“Eeeh na wewe, hiyo habari kuwa mama Junior anaumwa ila anafanya siri umeitoa wapi? Nimempigia simu ni mzima wa afya njema, jamani mwanangu mbea wewe hadi unachukua habari sio zenyewe. Haya umeitoa wapi?”
“Mama, ngoja nikwambie ukweli. Asubuhi nilikuwa naenda jikoni ila nikasikia sauti ya Junior jikoni basi nikasogea taratibu na kusikiliza ndio nikasikia Junior akimwambia dada Vaileth kuwa yeye anaenda kumuona mama yake sababu mama yake ni mgonjwa ila hataki watu wajue”
Mama Angel aliamua kumuita Vaileth, sababu hakuelewa kabisa, basi Vaileth alipofika alimuuliza,
“Vai, jana asubuhi Erica alikusikia wewe na Junior mkiongea jikoni yani Junior alikuwa akikwambia kuwa anaenda kumuona mama yake sababu alikuwa mgonjwa ila hataki watu wajue, je ni kweli?”
Vaileth alinyamaza kimya hadi mama Angel aliamua kumuuliza kwa ukali zaidi ndipo alipojibu,
“Ni kweli mama”
“Sasa Junior alikuwa ni misingi gani kusema hivyo jamani!”
Erica akauliza,
“Kwani mama yake haumwi kweli?”
“Haumwi wala nini, na unaambiwa Junior katoka kwao muda mrefu sana kasema anakuja huku ila hadi jioni hii hajafika huku jamani, huyu Junior anamaana gani sijui”
Basi Vaileth alinyanyuka na kuwa kama anaenda jikoni ila alienda chumbani kwake kwani kwa muda huo alijikuta akijiuliza maswali mengi sana,
“Kwani Junior kaenda wapi? Na kwanini anidanganye kuwa mama yake anaumwa?”
Akaanza kuvuta matukio kwanza, alivuta tukio la Junior kurudi akiwa na mawazo sana, pia alivuta tukio la Junior kuomba laki tano yake, alivuta tukio la Junior kudai kuwa amechoka sana na kulala chumbani kwake, akavuta pia tukio la kudanganywa kuwa mama Junior ni mgonjwa, akajikuta machozi yakimtoka kwani alihisi kuwa Junior anamsaliti.
“Kwanini Junior ananifanyia hivi lakini? Mbona mimi nampenda sana, mbona namjali, kwanini ananifanyia hivi!! Junior hata angechoka vipi ni lazima angekuja chumbani, kwanini Junior kabadilika? Lazima kuna mwanamke mwingine kampata tu”
Kwa muda huo huku machozi yakimtoka alikuwa akiwaza kuwa ampigie simu Junior kumuuliza au afanye kitu gani, yani alijikuta kuwa na mawazo sana ila kwa muda huo aliampigia simu kwanza ndugu yake Prisca maana simu ya awali alikuwa nayo,
“Oooh leo Nyanda umenikumbuka, nimefurahi sana”
“Jamani wewe, huzoei tu kuniita Vaileth jamani!!”
“Samahani Vaileth jamani, mazoea yana tabu nishazoea nyanda mimi”
“Hivi kwa mfano una mwanaume wako, akakukosea unatakiwa kufanya kitu gani?”
“Kheee ushapata mwanaume au yule baba mtoto wako karudi? Unataka ushauri gani kwangu? Ushauri wa kawaida ni kuwa kama mwanaume wako kakukosea mchambe tu tena umchambe haswaaa hadi ahisi kizunguzungu. Ila ushauri wenye busara na wa kudumisha mahusiano, kama mwanaume wako kakukosea, kwanza kabisa huwezi jua ni kwanini kakukosea, unatakiwa kumbembeleza, mnyenyekee muulize kwa ustaarabu, muonyeshe mapenzi na yeye atajishtukia kwa makosa yake. Kwahiyo utachagua wewe!”
“Mmmh ingekuwa wewe ungechagua nini?”
“Inategemea na aina ya mwanaume, kama anayenipa pesa nitamnyenyekea hata kama kanikosea ila mwanaume ngonjwa ngojwa akinikosea namchamba hadi anasahau jina la mama yake mzazi”
“Mmmh jamani!”
“Kwanza nimefurahi sana upo hewani kwasasa”
“Basi nitakupigia tena tuongee”
Vaileth alikata ile simu huku akijiuliza kama ampigie simu Junior au vipi.

Kwa muda huu, Junior alikuwa ameshafanikiwa kumpata mwanamke mmoja anayejiuza ambaye alikubaliana nae kumlipa elfu ishirini, basi alienda na yule mwanamke kwenye ile hoteli na mwanamke akasema,
“Kheee kumbe una hela jamani, sasa mbona hukusema hadi nimepanga dau dogo hivyo!! Nilikuona mdogo kumbe una mawe, utaongeza dau ili tuwe wote hadi asubuhi”
Mara simu ya Junior ilianza kuita, basi aliichukua na kuona mpigaji ni Vaileth, kiukweli aliumia moyo wake na kuamua kupokea ile simu,
“Junior mpenzi wangu, upo wapi?”
“Karibia narudi nyumbani”
“Nakuomba mpenzi, ukihisi kutamani mwanamke mwingine jua kuwa mimi nipo na ninakupenda sana mpenzi wangu, maradhi ni mengi sana siku hizi”
“Nimekusikia”
“Nakupenda sana, naomba urudi nyumbani Junior. Natamani sana kukuona mpenzi wangu”
Basi ile simu ikakatika ila kwa muda huo Junior alihisi moyo wake kuumia sana jinsi akimfikiria Vaileth, basi akamuangalia yule kahaba aliyemuita na kumwambia,
“Subiri nikanunue kinga”
“Hakuna tatizo”
Junior alitoka ila bado kauli ya Vaileth ilifanya kazi kichwani kwake kuwa rudi nyumbani moenzi wangu, alijihisi kuwa na hatia sana. Basi alivyofika nje, alisimamisha bodaboda na kuondoka nayo kuelekea nyumbani kwa muda huo, hata hakumjali tena yule Kahaba aliyemchukua.
 
Back
Top Bottom