Abdallahking
JF-Expert Member
- Mar 19, 2018
- 3,985
- 10,840
- Thread starter
- #141
SEHEMU YA 122
Kisha akamuangalia Derick na kumwambia,
“Khee Derick umekuwa jamani, karibuni nyumbani. Kweli damu nzito kuliko maji yani Erica na Derick mmekumbukana? Karibuni sana nyumbani”
Erica alipigwa na mshangao kwa muda kidogo maana alijiona haelewi kabisa, kuwa Derick ni ndugu yake kwakweli hakuelewa.
Mshangao aliokuwa nao Erica ni sawa na mshangao aliokuwa nao Derick, huyu mdada alimfahamu ila Erica hakumfahamu hata akashangaa kuwa undugu wake na Erica umetokea wapi, kisha Mage ndio akawaondoa kwenye mshangao na kuwaambia kuwa wakaribie nyumbani kwake.
Waliongozana na Mage hadi nyumbani kwake, muda wote si Erica wala si Derick aliyekuwa akiongea chochote zaidi ya Mage.
Alifika nao nyumbani kwake na kumwambia Derrick,
“Derick, hapa ndio nyumbani kwangu. Jisikie upo huru, najua siku zote ulijiuliza kuwa Yule dada anaishi wapi, ila naishi hapa. Karibu sana”
Akashukuru na kisha Mage kuwauliza,
“Mmekutana wapi jamani na mmekumbukana vipi? Nakumbuka mara ya mwisho nyie kuonana mlikuwa wadogo sana, toka hapo Derick hukuweza tena kufika kwetu. Sasa sijui mmefahamiana vipi? Najua utajiuliza kuwa kwanini mimi sijafika kwenu kwa siku nyingi ila mamako alihama bila hata ya kuniambia, ila upendo wangu upo pale pale. Kwakweli Mungu mkubwa jamani, mmefahamiana vipi?”
Muda wote Erica alikuwa kimya kabisa, ila muda huu aliamua kumuuliza dada yake kwa mshangao,
“Dada, mimi na huyu Derick tunasoma chuo kimoja ndio tulikofahamiana, ila huo undugu na huyu uko vipi maana hata sielewi”
“Kwahiyo hamkuwa mnakuja kwangu eeh!”
“Ni kweli hatukuwa tunakuja kwako”
“Mlikuwa mnaenda wapi?”
“Tuachane na hizo habari kwanza dada, ila tueleweshe undugu wetu uko vipi”
Erica alitaka kujua undugu wake na Derick ukoje maana hakuelewa kabisa,
“Iko hivi, baba yetu alizaa mtooto mwingine nje yani huyu Derick kazaliwa umepishana nae mwaka mmoja tu. Mwanzoni wakati wewe una miaka mine huyu Derick aliletwa nyumbani ila mama alimkataa sababu hakutaka mtoto wa nje ya ndoa, ila baba alikuwa akimuhudumia tu vizuri na ni mimi aliyekuwa ananituma nipeleke hela za matumizi kwakina Derick, yani hadi kipindi baba anakufa alisema nimuangalie sana Derick na ndio sababu ya mimi kwenda mara kwa mara kumuona Derick ila sikumwambia mama kwani sikupenda ajue kuwa naendaga, nimeacha kwenda mwaka juzi maana mama yake Derick alihama pale alipokuwa anakaa na sikuwa na mawasiliano nae”
“Kwahiyo dada unamaanisha kuwa mimi na Derick ni watoto wa baba mmoja?”
“Ndio, na ndiomana nikasema damu nzito. Yani wewe na Derick ni baba mmoja ila mama mbalimbali, yani Derick ni ndugu yetu kwa mama mwingine, tumechangia baba”
Alishangaa kuwaona wote wakiinamia chini yani Derick na Erica, ikabidi awaulize,
“Vipi kwani, hamkupenda muwe ndugu? Nisamehe mimi Derick nilisema ningekuja kukuchukua ufahamu ndugu zako wengine, ila sio kosa langu, ni sababu mama yako alihama”
“Ila kwanini baba hakutaka tufahamiane?”
“Erica, sio kosa la baba ni kosa la mama. Baba hakuwa na sauti yoyote kwa mama, kwahiyo kila alichoambiwa na mama alikubali”
“Kwanini?”
“Erica, hujui mambo mengi katika ujana wa mama na baba nasikia nyumbani kwakina mama walikuwa na uwezo sana hata zile nyumba ni mama amejengewa na wazazi wake, kwahiyo baba hakuwa na kauli yoyote, pale mama aliposema sitaki kukiona hiki kitoto nyumbani kwangu, ilibidi atii amri tu. Ila sio kosa lao wote, nakumbuka babu yani baba yake mama alikuwa mkali sana na alimwambia mama asikubali mtoto wa nje kwenye nyumba aliyojenga yeye. Nakumbuka baba aliniomba nifanye siri hata swala la kumtembelea Derick na kupeleka hela ya matumizi, ndiomana hata baada ya kifo cha baba bado haikuwa rahisi kwa mama Derick kuja kudai mirathi ya mwanae”
Kwa kiasi Fulani Erica alisikitika na Derick nae alisikitika, ila dada yao Mage aliendelea kuzungumza,
“Ndiomana mama habari zake huwa anasisitiza watoto wake kuolewa na wanaume wanaojiweza maana anasema kuwa mwanaume kudharauliwa na ukoo inauma sana, inasemekana ukoo wa mama walimdharau sana baba”
Derick alitokwa na machozi maana zile habari kuwa baba yake alidharaulika zilimuumiza na kilichomuumiza zaidi ni kitendo chake cha kutembea na dada yake bila ya kujua alijihisi maumivu sana moyoni, dada yao hakuelewa ila wadogo zake waliinama chini kwa muda na kushindwa kuongea chochote.
Derick aliinua kichwa na kuamua kumuaga dada yao kuwa anawahi chuoni, Erica nae alimuaga dada yake. Mage hakuwaelewa kwakweli ila yeye aliendelea kuwakaribisha tu nyumbani kwake, na kuchukua mawasiliano ya Derick pamoja na mawasiliano ya mama Derick ila Derick aliinuka kuondoka mpaka pale Mage alipomsimamisha kuwa awasindikize wote, walipofika stendi walipanda gari moja ila hakuna mmoja aliyemuongelesha mwenzie.
Mage aliwaacha wamepanda gari ila hakuwaelewa kwakweli kiasi kwamba alijiuliza maswali mengi bila majibu.