Simulizi: Nini maana ya mapenzi

Simulizi: Nini maana ya mapenzi

SEHEMU YA 122



Kisha akamuangalia Derick na kumwambia,
“Khee Derick umekuwa jamani, karibuni nyumbani. Kweli damu nzito kuliko maji yani Erica na Derick mmekumbukana? Karibuni sana nyumbani”
Erica alipigwa na mshangao kwa muda kidogo maana alijiona haelewi kabisa, kuwa Derick ni ndugu yake kwakweli hakuelewa.
Mshangao aliokuwa nao Erica ni sawa na mshangao aliokuwa nao Derick, huyu mdada alimfahamu ila Erica hakumfahamu hata akashangaa kuwa undugu wake na Erica umetokea wapi, kisha Mage ndio akawaondoa kwenye mshangao na kuwaambia kuwa wakaribie nyumbani kwake.
Waliongozana na Mage hadi nyumbani kwake, muda wote si Erica wala si Derick aliyekuwa akiongea chochote zaidi ya Mage.
Alifika nao nyumbani kwake na kumwambia Derrick,
“Derick, hapa ndio nyumbani kwangu. Jisikie upo huru, najua siku zote ulijiuliza kuwa Yule dada anaishi wapi, ila naishi hapa. Karibu sana”
Akashukuru na kisha Mage kuwauliza,
“Mmekutana wapi jamani na mmekumbukana vipi? Nakumbuka mara ya mwisho nyie kuonana mlikuwa wadogo sana, toka hapo Derick hukuweza tena kufika kwetu. Sasa sijui mmefahamiana vipi? Najua utajiuliza kuwa kwanini mimi sijafika kwenu kwa siku nyingi ila mamako alihama bila hata ya kuniambia, ila upendo wangu upo pale pale. Kwakweli Mungu mkubwa jamani, mmefahamiana vipi?”
Muda wote Erica alikuwa kimya kabisa, ila muda huu aliamua kumuuliza dada yake kwa mshangao,
“Dada, mimi na huyu Derick tunasoma chuo kimoja ndio tulikofahamiana, ila huo undugu na huyu uko vipi maana hata sielewi”
“Kwahiyo hamkuwa mnakuja kwangu eeh!”
“Ni kweli hatukuwa tunakuja kwako”
“Mlikuwa mnaenda wapi?”
“Tuachane na hizo habari kwanza dada, ila tueleweshe undugu wetu uko vipi”
Erica alitaka kujua undugu wake na Derick ukoje maana hakuelewa kabisa,
“Iko hivi, baba yetu alizaa mtooto mwingine nje yani huyu Derick kazaliwa umepishana nae mwaka mmoja tu. Mwanzoni wakati wewe una miaka mine huyu Derick aliletwa nyumbani ila mama alimkataa sababu hakutaka mtoto wa nje ya ndoa, ila baba alikuwa akimuhudumia tu vizuri na ni mimi aliyekuwa ananituma nipeleke hela za matumizi kwakina Derick, yani hadi kipindi baba anakufa alisema nimuangalie sana Derick na ndio sababu ya mimi kwenda mara kwa mara kumuona Derick ila sikumwambia mama kwani sikupenda ajue kuwa naendaga, nimeacha kwenda mwaka juzi maana mama yake Derick alihama pale alipokuwa anakaa na sikuwa na mawasiliano nae”
“Kwahiyo dada unamaanisha kuwa mimi na Derick ni watoto wa baba mmoja?”
“Ndio, na ndiomana nikasema damu nzito. Yani wewe na Derick ni baba mmoja ila mama mbalimbali, yani Derick ni ndugu yetu kwa mama mwingine, tumechangia baba”
Alishangaa kuwaona wote wakiinamia chini yani Derick na Erica, ikabidi awaulize,
“Vipi kwani, hamkupenda muwe ndugu? Nisamehe mimi Derick nilisema ningekuja kukuchukua ufahamu ndugu zako wengine, ila sio kosa langu, ni sababu mama yako alihama”
“Ila kwanini baba hakutaka tufahamiane?”
“Erica, sio kosa la baba ni kosa la mama. Baba hakuwa na sauti yoyote kwa mama, kwahiyo kila alichoambiwa na mama alikubali”
“Kwanini?”
“Erica, hujui mambo mengi katika ujana wa mama na baba nasikia nyumbani kwakina mama walikuwa na uwezo sana hata zile nyumba ni mama amejengewa na wazazi wake, kwahiyo baba hakuwa na kauli yoyote, pale mama aliposema sitaki kukiona hiki kitoto nyumbani kwangu, ilibidi atii amri tu. Ila sio kosa lao wote, nakumbuka babu yani baba yake mama alikuwa mkali sana na alimwambia mama asikubali mtoto wa nje kwenye nyumba aliyojenga yeye. Nakumbuka baba aliniomba nifanye siri hata swala la kumtembelea Derick na kupeleka hela ya matumizi, ndiomana hata baada ya kifo cha baba bado haikuwa rahisi kwa mama Derick kuja kudai mirathi ya mwanae”
Kwa kiasi Fulani Erica alisikitika na Derick nae alisikitika, ila dada yao Mage aliendelea kuzungumza,
“Ndiomana mama habari zake huwa anasisitiza watoto wake kuolewa na wanaume wanaojiweza maana anasema kuwa mwanaume kudharauliwa na ukoo inauma sana, inasemekana ukoo wa mama walimdharau sana baba”
Derick alitokwa na machozi maana zile habari kuwa baba yake alidharaulika zilimuumiza na kilichomuumiza zaidi ni kitendo chake cha kutembea na dada yake bila ya kujua alijihisi maumivu sana moyoni, dada yao hakuelewa ila wadogo zake waliinama chini kwa muda na kushindwa kuongea chochote.
Derick aliinua kichwa na kuamua kumuaga dada yao kuwa anawahi chuoni, Erica nae alimuaga dada yake. Mage hakuwaelewa kwakweli ila yeye aliendelea kuwakaribisha tu nyumbani kwake, na kuchukua mawasiliano ya Derick pamoja na mawasiliano ya mama Derick ila Derick aliinuka kuondoka mpaka pale Mage alipomsimamisha kuwa awasindikize wote, walipofika stendi walipanda gari moja ila hakuna mmoja aliyemuongelesha mwenzie.
Mage aliwaacha wamepanda gari ila hakuwaelewa kwakweli kiasi kwamba alijiuliza maswali mengi bila majibu.
 
SEHEMU YA 123


Erica alifika njiani na kushuka kwenye lile gari kwani alipanda gari la kwenda kwao, ila Derick hakumuuliza chochote kile Erica.
Alienda hadi kwao na kukuta mama yake ametoka, alitulia akimsubiri kwa hamu kwani alijikuta ana maswali mengi sana kwa mama yake bila hata majibu, alijiuliza kuwa hata kama babu yao alikataa yeye alitakiwa awe na uamuzi wa mwisho, kwanini amfanyie hivyo mtoto wa baba yao asiye na hatia? Alikosa jibu kwakweli, pia alimlaumu baba yao kuwa walikuwa na haki ya kufahamiana hata kwa siri na sio kufahamishwa kwa mtoto mmoja tu.
Alimsubiria mama yake afike kwa hamu sana, na baada ya muda kidogo mama yake alifika na kumshangaa sana kuwa vipi yupo nyumbani muda wa kuwa chuo,
“Mama, sina hata hamu ya kuwa chuo ndiomana nimerudi”
“Kivipi?”
“Nimekutana na mtoto mmoja anaitwa Derick, kumbe ni mtoto wa baba jamani? Kwanini hukuniambia?”
“Kwahiyo kukutana na mtoto wa baba yako sijui ndio kukukoseshe hamu ya kuwa chuoni?”
“Hapana mama”
“Ila nini?”
“Mama, dunia ina mambo mengi sana kama watoto tunapaswa kufahamiana maana kuna leo na kesho, naweza patwa na matatizo au yeye akapatwa na matatizo tukashindwa kusaidiana kumbe ni ndugu, ilitakiwa tufahamiane. Na ni nyie ndio wazazi wa kutufahamisha watoto wenu”
“Erica, usiwe unaongea kama unatapika kama kitu hujui bora kuuliza kuliko kunipa lawama za kijinga”
“Nisamehe mama, ila ningependa kujua”
“Najua sasa umekuwa na unaweza kuelewa, baba yenu nilimpenda tena nilimpenda sana na yeye alinipenda sana. Aling’ang’ania kutaka kunioa ila kwetu walimkataa sababu ukoo wao hawakuwa na hela za kutosha ila mimi nilimpenda na kung’ang’ania kuwa wakubali niolewe. Ikawa wamekuja kwetu na kukubaliwa kunioa, wakatajiwa mahali, ila ilikuwa ni kubwa sana kwa upande wa baba yenu ila kuna kitendo nilifanya nyumbani. Babu yangu mimi alikuwa na ng’ombe wengi sana, nilitumia kumlaghai Yule mchunga ng’ombe hadi nikafanikiwa kuuza ng’ombe watano, kisha pesa nilimpelekea baba yenu na kufanikisha swala la mahali hadi swala la kuoana. Baba hakutaka niishi kwenye mazingira magumu alinizawadia nyumba na kiwanja. Nyumba hii alinijengea mwenyewe alisema niishi kwenye nyumba ya kisasa, kwahiyo nyumba aliyonizawadia tulipangisha pia na tukaweza kujenga nyingine mbili hapo na kupangisha. Nilimpenda baba yenu, nilimuamini na nilifanya chochote alichotaka ila alinichefua siku moja nilipoletewa mtoto hapa nyumbani kwangu kuwa kazaa na mwanamke mwingine. Nilijiuliza hivi huyu mwanaume kakosa nini kwangu? Kama watoto nilimzalia, wakike kwa wakiume, kwakweli kama nisingekuwa nimezaa na baba yenu ningemkimbia. Kwakweli hakuna cha kusema sijui masikini ana mapenzi ya dhati, baba yenu alikuwa masikini na nilimpenda na kufanya chochote alichosema ila bado alinisaliti ndiomana huwa nawaambia watoto wangu sitaki mwanaume masikini hapa kwangu.”
Kwa kiasi Fulani maneno ya mama yake yalimuingia akilini, ila mama yake aliendelea kuongea
“Hivi mwanaume nimsaidie, nimzalie watoto, nilee watoto halafu aniletee mtoto kazaa wapi sijui nilee. Samahanini sana huo upuuzi siwezi kufanya, nilisikia ushauri wa baba yangu kuwa nyumba yake asikae mtoto wa kufikia, nilimwambia baba yenu kama kidume basi ajenge nyumba ya kuweka hao watoto wake aliowaokota kwenye umalaya. Toka kipindi hiko nilimchukia baba yenu yani nilikuwa nae tu sababu ni mume wangu, nikikumbuka vijana wengi walinitaka enzi za ujana wangu, vijana waliokuwa na pesa zao ila sikuwakubali sababu ya kuamini kuwa yeye atakuwa muaminifu kwangu. Wanaume uhuni wameumbiwa”
“Kwahiyo mama, hukumpenda baba hadi amekufa?”
“Niavche Erica. Si kweli. Upendo ulipungua ila haukutoka kwani siku zote atabaki kuwa mwanaume niliyempenda sana, na hakuna pigo nililopata maishani kama kifo cha baba yenu. Ukizingatia hapa mwishoni ndio alianza kujitahidi kweli kusaka pesa ila ndio hivyo akafa. Nikikumbuka kifo cha baba yenu naumia sana”
“Ila mama kwanini baada ya kifo cha baba usimuenzi kwa kututambulisha kwa huyo mtoto wake?”
“Erica, mama wa huyo mtoto hajawahi kuwa karibu na mimi wala baada ya kifo cha mume wangu bado hakuweza kujileta kwangu ili tumalize tofauti zetu. Siwezi kujipendekeza mimi sio mwenye shida, aje mwenyewe kumleta mwanae ajuane na watoto wangu”
Erica hakuwa na maswali zaidi kwa mama yake kwani aliona hata akiendelea kumuuliza ni kazi bure kwani mengi ameshajibiwa.
 
SEHEMU YA 124


Erica alienda chumbani kwake, alioga na kubadilisha nguo. Alikuwa akitafakari sana vitu ambavyo hakuwa na majibu navyo, alitafakari sana kuhusu mapenzi.
“Nimetembea na kaka yangu sababu ya mawazo ya mapenzi, najuata kufanya vitu bila kufikiria na kusema ukweli siwezi kabisa. Hivi Yule Bahati ananipenda kweli? Mama kasema wanaume wote ni wasaliti haijalishi ni tajiri au ni masikini, ukiangalia Rahim ameshindwa hata kunitambulisha kwa mama yake, mmh ananipenda kweli? Ila yote ni Erick wangu jamani, kaamua kweli kuwa na mwanamke mwingine? Hapana jamani, Erick nakupenda, nimetembea na kaka yangu mimi hata sijui nitamuangaliaje?”
Aliwaza sana ila aliona kichwa kikimzunguka tu, leo alipigiwa simu na namba mpya, alipoiangalia ilikuwa ni namba ya nchi nyingine, akapokea,
“Erica, mimi ni Rahim. Mbona kimya hivyo mpenzi? Nini nimekukosea?”
“Hujanikosea chochote kile Rahim, ni masomo tu yalinibana”
“Ila ukiwa na tatizo lolote niambie Erica, nipo kwaajili yako”
“Sawa Rahim, nimekuelewa”
“Naomba tuwasiliane basi Facebook”
“Sawa”
Erica alikata simu ya Rahim ila kiukweli kwa muda huo kama angepigiwa simu na Erick basi angejisikia vizuri sana, lakini haikuwa hivyo aliamua kuwa mpole tu na kwenda kujilaza kwani alikuwa na mawazo kupitiliza.
Alilala sana siku hiyo yani kuja kushtuka ni usiku wa saa tatu na kichwa chake kilikuwa kizito sana, akatambua kuwa hata kula hakula, akamsikia tu mama yake akimuita kwa kulalamika,
“Wewe mtoto ndio kuchoka gani na masomo huko jamani, yani unalala kama mzigo hadi unapitiliza. Nishakuamsha sana hadi nimetamani nikaite daktari, hebu amka ule”
Erica alijinyoosha nyoosha na kwenda kula ila alikula kidogo sana kwani alihisi mwili kuchoka vilivyo, alimaliza na kwenda tena kuoga kisha kurudi kitandani,
“Itakuwa Yule mwanaume jana alinipindua pindua vilivyo, mmh Mungu wangu ni kaka yangu eti! Aibu hii sijui nitaiweka wapi”
Akashangaa kuona Derick akimpigia simu, ila kwa uoga na aibu akaipokea
“Erica, naomba tusameheane ila sio kosa langu na wala sio kosa lako, sijui ni namna gani ya kukutazama tena ila sitaki kuamini kuwa wewe ni dada yangu”
“Derick, sisi ni ndugu kweli. Ni wakati kwa wazazi wetu kuwa pamoja na kutukutanisha ila kwa kilichotokea kwetu naomba ibaki kuwa siri yetu”
“Hata mimi nilitaka kukwambia hivyo hivyo, sikulala na wewe kwa kutaka Erica ila ni pombe ndio zilipelekea kufanya vile naomba unisamehe ila ibaki kuwa siri yetu milele”
“Sitamwambia yeyote siri hii, kwanza ni aibu sana yani nililala na ndugu yangu? Hapana sitaki kuamini kabisa, naomba tusionane Derick hadi mambo haya yakae sawa”
“Nimekuelewa Erica”
“Siku tukija kuonana iwe kama dada na kaka yani kama hakuna kitu kilichotokea kati yetu tusahau kabisa”
“Ni ngumu kusahau ila nitajitahidi”
Simu ilikatika ila Erica alizidi kuwa na mawazo yani kuna vitu alikuwa akijiuliza bila ya kupata majibu,
“Baba kuwa na mtoto mwingine si vibaya wala si dhambi, mimi kumfahamu mtoto wa baba si vibaya kwani ni ndugu yangu ila kwanini mimi na Derick tufahamiane kwa njia hii? Kwanini Derick anipende dada yake? Hivi hapakuwa na njia nyingine ya kunifahamisha mimi kwa Derick zaidi ya njia ya kufanya naye ngono? Sielewi jamani yani sielewi kabisa, hivi Derick alianzaje kuwa na hisia na dada yake jamani? Aaah Erica mimi yani kuna muda hata sijui nifanyeje”
Alijiona tu hana raha, na akakumbuka kuwa Rahim alimwambia awasiliane nae facebook ila hata hakuwa na hamu ya kufanya hivyo maana bado akili yake ilizingirwa na mambo mengi sana. Akaamua kulala tena tu.
 
SEHEMU YA 125


Kesho yake akajiandaa na kwenda chuoni ila kiukweli hakupanga kabisa kuonana na Derick, kiasi kwamba alikuwa akimaliza kipindi tu anarudi kwao yani hata harandirandi maeneo ya chuo kwani bado aibu na dhamira ya moyo wake vilimsuta.
Akiwa nyumbani, akaingia facebook ili aweze kuwasiliana na Rahim atulize mawazo yake, akakuta kuna jumbe alitumiwa na Tumaini, kufungua jumbe zile zilikuwa ni picha zikimuonyesha Erick na huyo mwanamke wake mpya, kisha Tumaini akamuandikia ujumbe,
“Huyo ndio wifi yangu, mwanamke mpya wa Erick yani kwangu ni raha tu kila siku”
Erica hakujibu ule ujumbe kwani ulikuwa ukimkera tu, alijiuliza kuwa pengine huyu Tumaini anamfanyia makusudi,
“Mmmh lakini haiwezekani maana hanijui jamani kama ni mimi niliyekuwa na mahusiano na Erick, anawezaje kunifanyia vitu vya kuniumiza moyo? Itakuwa anajisikia tu”
Ila aliona cha muhimu ni kuacha kabisa kuwasiliana na Tumaini kwenye mtandao wa kijamii ili asiendelee kuumiza kichwa chake kwa picha za Erick na mwanamke wake.
Alikaa vile vile mwenye mashaka moyoni kwa mwezi mzima yani anaenda chuo na kurudi kwao, hakutaka kulala hosteli kabisa kwani alihisi kama akilala hosteli huenda akaonana na Derick.
Siku hiyo akiwa nyumbani, chumbani kwake, mama yake alienda kumuita
“Erica, Yule muuza samaki amekuja tena kuulizia”
Erica moyo ulilia paaa kwani alijua kwa vyovyote vile ni Bahati, na kweli alitoka na kumkuta Bahati, kwa kipindi chote hiko alijiona amepumua kwa Bahati na wala hakujua kama Bahati angejitokeza tena katika maisha yake.
Akamvutia nje Bahati ilia aongee nae, ambapo walivyotoka tu nje Bahati alianza kwa kulalamika,
“Kwakweli Erica ulichonifanyia sio haki kabisa, mimi nilifungwa kwaajili yako ila wewe hata siku moja ya kuja kuniona hakuna? Hata kutaka kujua kuwa kipi kilinikuta hakuna? Erica kweli unanifanyia hivi binadamu mwenzio?”
“Bahati, kwanza pole ila na wewe hujui kuwa ugomvi wako pale hosteli umenisababishia matatizi gani mimi. Unaniona sikai tena hosteli sababu ya ukorofi wako ulioufanya yani hadi napaona hosteli kama kituo cha polisi. Hapana kwakweli”
“Ila Erica bado nakupenda”
“Kheee, wewe mwanaume hivi umerogwa au?”
“Nimekuletea na samaki, hizi”
Bahati akachukua mfuko aliofika nao ulikuwa na samaki akamkabidhi Erica, ila Erica alipopokea tu ule mfuko gafla akajihisi kichefuchefu cha hali ya juu na kwenda kutapika sana.
Bahati alishangaa na kuuweka ule mfuko wenye samaki pembeni,
“Bahati, ondoka na samaki zako sizitaki”
“Kwani una matatizo gani Erica? Mbona samaki huwa unazipenda tu”
“Nimekwambia ondoka na samaki zako”
Ila Bahati hakukubali bali alienda tena ndani kwakina Erica na kuacha ule mfuko wake wa samaki mezani kisha akatoka nje alipo Erica huku akimpa ushauri kuwa waende hospitali,
“Hospitali nikafanye nini? Kwani kutapika ndio kuumwa? Labda ni minyoo”
“Sawa, ila hata kama ni minyoo Erica unatakiwa kupima”
“Aaah na wewe hebu achana na mimi, tutaongea siku nyingine kwa muda huu naenda kupumzika ndani”
Erica alionekana kuchukizwa kabisa, na kwenda ndani kwao ikabidi Bahati aondoke tu.


Mama yake Erica alishangaa kukuta mfuko wa samaki mezani,
“Yani Erica umeshindwa hata kuwashughulikia hawa samaki jamani! Yani umeletewa na kuwaacha hapa mezani?”
Erica alienda kuwachukua kwa kinyaa sana ili akawashughulikie, ila kabla ya kufanya chochote alitapika sana mpaka mama yake akaenda kumdaka,
“Una tatizo gani Erica”
“Najisikia vibaya tu mama”
“Basi twende hospitali”
“Ngoja nikajiandae”
Erica aliingia ndani kama anajiandaa kwaajili ya kwenda hospitali ila alifika kitandani na kujilaza, na usingizi ukampitia pale pale. Mama yake alisafisha wale samaki na kuwapika ila Erica alikuwa bado kalala, ikabidi hadi mama yake amuamshe ila alidai ni uchovu tu wala hajihisi vibaya kiasi cha kwenda hospitali.
Ila kesho yake aliamua kwenda mwenyewe hospitali kupima minyoo, ila daktari alimshauri wapime na ujauzito.
Majibu yalipotoka yalionesha kuwa Erica ana mimba, yani swala hilo likaichanganya kabisa akili yake.

ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 122



Kisha akamuangalia Derick na kumwambia,
“Khee Derick umekuwa jamani, karibuni nyumbani. Kweli damu nzito kuliko maji yani Erica na Derick mmekumbukana? Karibuni sana nyumbani”
Erica alipigwa na mshangao kwa muda kidogo maana alijiona haelewi kabisa, kuwa Derick ni ndugu yake kwakweli hakuelewa.
Mshangao aliokuwa nao Erica ni sawa na mshangao aliokuwa nao Derick, huyu mdada alimfahamu ila Erica hakumfahamu hata akashangaa kuwa undugu wake na Erica umetokea wapi, kisha Mage ndio akawaondoa kwenye mshangao na kuwaambia kuwa wakaribie nyumbani kwake.
Waliongozana na Mage hadi nyumbani kwake, muda wote si Erica wala si Derick aliyekuwa akiongea chochote zaidi ya Mage.
Alifika nao nyumbani kwake na kumwambia Derrick,
“Derick, hapa ndio nyumbani kwangu. Jisikie upo huru, najua siku zote ulijiuliza kuwa Yule dada anaishi wapi, ila naishi hapa. Karibu sana”
Akashukuru na kisha Mage kuwauliza,
“Mmekutana wapi jamani na mmekumbukana vipi? Nakumbuka mara ya mwisho nyie kuonana mlikuwa wadogo sana, toka hapo Derick hukuweza tena kufika kwetu. Sasa sijui mmefahamiana vipi? Najua utajiuliza kuwa kwanini mimi sijafika kwenu kwa siku nyingi ila mamako alihama bila hata ya kuniambia, ila upendo wangu upo pale pale. Kwakweli Mungu mkubwa jamani, mmefahamiana vipi?”
Muda wote Erica alikuwa kimya kabisa, ila muda huu aliamua kumuuliza dada yake kwa mshangao,
“Dada, mimi na huyu Derick tunasoma chuo kimoja ndio tulikofahamiana, ila huo undugu na huyu uko vipi maana hata sielewi”
“Kwahiyo hamkuwa mnakuja kwangu eeh!”
“Ni kweli hatukuwa tunakuja kwako”
“Mlikuwa mnaenda wapi?”
“Tuachane na hizo habari kwanza dada, ila tueleweshe undugu wetu uko vipi”
Erica alitaka kujua undugu wake na Derick ukoje maana hakuelewa kabisa,
“Iko hivi, baba yetu alizaa mtooto mwingine nje yani huyu Derick kazaliwa umepishana nae mwaka mmoja tu. Mwanzoni wakati wewe una miaka mine huyu Derick aliletwa nyumbani ila mama alimkataa sababu hakutaka mtoto wa nje ya ndoa, ila baba alikuwa akimuhudumia tu vizuri na ni mimi aliyekuwa ananituma nipeleke hela za matumizi kwakina Derick, yani hadi kipindi baba anakufa alisema nimuangalie sana Derick na ndio sababu ya mimi kwenda mara kwa mara kumuona Derick ila sikumwambia mama kwani sikupenda ajue kuwa naendaga, nimeacha kwenda mwaka juzi maana mama yake Derick alihama pale alipokuwa anakaa na sikuwa na mawasiliano nae”
“Kwahiyo dada unamaanisha kuwa mimi na Derick ni watoto wa baba mmoja?”
“Ndio, na ndiomana nikasema damu nzito. Yani wewe na Derick ni baba mmoja ila mama mbalimbali, yani Derick ni ndugu yetu kwa mama mwingine, tumechangia baba”
Alishangaa kuwaona wote wakiinamia chini yani Derick na Erica, ikabidi awaulize,
“Vipi kwani, hamkupenda muwe ndugu? Nisamehe mimi Derick nilisema ningekuja kukuchukua ufahamu ndugu zako wengine, ila sio kosa langu, ni sababu mama yako alihama”
“Ila kwanini baba hakutaka tufahamiane?”
“Erica, sio kosa la baba ni kosa la mama. Baba hakuwa na sauti yoyote kwa mama, kwahiyo kila alichoambiwa na mama alikubali”
“Kwanini?”
“Erica, hujui mambo mengi katika ujana wa mama na baba nasikia nyumbani kwakina mama walikuwa na uwezo sana hata zile nyumba ni mama amejengewa na wazazi wake, kwahiyo baba hakuwa na kauli yoyote, pale mama aliposema sitaki kukiona hiki kitoto nyumbani kwangu, ilibidi atii amri tu. Ila sio kosa lao wote, nakumbuka babu yani baba yake mama alikuwa mkali sana na alimwambia mama asikubali mtoto wa nje kwenye nyumba aliyojenga yeye. Nakumbuka baba aliniomba nifanye siri hata swala la kumtembelea Derick na kupeleka hela ya matumizi, ndiomana hata baada ya kifo cha baba bado haikuwa rahisi kwa mama Derick kuja kudai mirathi ya mwanae”
Kwa kiasi Fulani Erica alisikitika na Derick nae alisikitika, ila dada yao Mage aliendelea kuzungumza,
“Ndiomana mama habari zake huwa anasisitiza watoto wake kuolewa na wanaume wanaojiweza maana anasema kuwa mwanaume kudharauliwa na ukoo inauma sana, inasemekana ukoo wa mama walimdharau sana baba”
Derick alitokwa na machozi maana zile habari kuwa baba yake alidharaulika zilimuumiza na kilichomuumiza zaidi ni kitendo chake cha kutembea na dada yake bila ya kujua alijihisi maumivu sana moyoni, dada yao hakuelewa ila wadogo zake waliinama chini kwa muda na kushindwa kuongea chochote.
Derick aliinua kichwa na kuamua kumuaga dada yao kuwa anawahi chuoni, Erica nae alimuaga dada yake. Mage hakuwaelewa kwakweli ila yeye aliendelea kuwakaribisha tu nyumbani kwake, na kuchukua mawasiliano ya Derick pamoja na mawasiliano ya mama Derick ila Derick aliinuka kuondoka mpaka pale Mage alipomsimamisha kuwa awasindikize wote, walipofika stendi walipanda gari moja ila hakuna mmoja aliyemuongelesha mwenzie.
Mage aliwaacha wamepanda gari ila hakuwaelewa kwakweli kiasi kwamba alijiuliza maswali mengi bila majibu.
 
.IV KAMA MWANDISHI HUYU ALIKUWA NA STORY INGINE INAITWA JINSI FACEBOOK IMEHARIBU MAISHA YANGU KAMA SJAKOSEA,NAOMBA LINK KAMA IPO

Hapana mkuu, Facebook imeharibu maisha yangu ni ya George Iron Mosenya.

Niliirusha sema account zilipewa Ban kwasabb ya links. Kesho nitairusha tena
 
SEHEMU YA 126




Ila kesho yake aliamua kwenda mwenyewe hospitali kupima minyoo, ila daktari alimshauri wapime na ujauzito.
Majibu yalipotoka yalionesha kuwa Erica ana mimba, yani swala hilo likaichanganya kabisa akili yake.
Daktari alimuangalia sana kwa makini Erica alivyokuwa amechanganyikiwa, akamuuliza,
“Vipi hukutarajia au?”
“Sikutarajia dokta na hata sijui nifanye nini mimi!”
“Kama huna mpango na hiyo mimba nakushauri utoe”
Yani huu ushauri ulipenya vilivyo kwenye akili ya Erica na aliona kuwa unamfaa sana, akamuangalia dokta kwa makini na kumuuliza,
“Kwahiyo inawezekana kutoa?”
“Ndio, inawezekana, ila kuna gharama zake”
“Shilingi ngapi”
“Sababu mimba yako ina zaidi ya wiki nne ni laki moja na nusu”
“Duh!”
“Ndio, hivyo. Kutoa mimba ni gharama, nenda jipange ila usichelewe sana maana kadri inavyozidi kukua ndivyo gharama inavyoongezeka”
Erica alimuaga Yule dokta ila kiukweli alikuwa kachanganyikiwa na hakujua hata aanzie wapi na aishie wapi, akijangalia hakuwa na hela hiyo kwa kipindi hiko na hakujua ni wapi ataipata. Akasogea mahali na kuamua kumpigia simu Derick na kumuomba kuwa waonane siku hiyo ana mazungumzo nae.

Walikutana na Derick ila hata Derick aliweza kuona mashaka aliyokuwa nayo Erica, alimuuliza kwa makini kuwa tatizo ni nini,
“Nimetoka hospitali kupima nimekutwa na mimba”
“Una mimba?”
“Ndio nina mimba”
“Ya nani?”
“Ya kwako Derick”
“Yani siku moja tu erica ndio upate mimba kweli? Haya sasa tunafanyaje”
“Nataka kutoa”
“Kutoa? Unajua kama kutoa mimba si vizuri!”
“Haya ngoja nikuulize, mimi na wewe ni ndugu, je huyo mtoto atatuitaje unajua mambo mengine yalifanywa bila ya kufikiria! Naomba sapoti yako Derick, nisaidie nitoe hii mimba”
“Sasa mimi nitakusapoti vipi?”
“Unipatie hela nikatoe, dokta kaniambia ni shilingi laki moja na nusu”
“Kheee laki na nusu? Hela yote hiyo, si bora uzae tu. Kwanza sina hiyo hela”
“Sasa kama laki na nusu ya kutolea huna, hiyo hela ya kulea mtoto utakuwa nayo? Umeniharibia maisha yangu Derick halafu unagoma hapo, unataka ndugu zetu wajue kama tulikuwa na mahusiano”
“Ila Erica, hebu kuwa mkweli basi hiyo mimba ya nani? Yani mimi siku moja tu nikupe mimba kweli?”
Erica aliona huyu Derick anamfanyia masihara wakati yeye alishachanganyikiwa na swala lile la mimba, alimuangalia kwa gadhabu sana na kumwambia,
“Hivi aliyekwambia mimba inaingia ukifanya mapenzi wiki nzima nani? Mimba inaingia siku moja tu na wakati mmoja”
“Kama ndio hivyo basi zaa halafu nitaangalia mtoto kama atafanana na mimi”
“Katika watu waliowahi kunichefua katika maisha yangu, wewe ni namba moja. Kwaheri”
Erica aliondoka zake, alisimamisha bodaboda na kwenda kwao huku ana mawazo tele akiwaza kuwa atafanya nini na ile mimba maana hakutaka mama yake ajue na hawezi kwenda kumuomba hela dada yake Bite maana atauliza tu kuwa hela ya nini, alihisi kuchanganyikiwa kabisa.
 
SEHEMU YA 127


Usiku ulifika ila hakuwa na usingizi, mawazo yalijaa kwenye akili yake maana aliwaza kuhusu ile mimba, yani kwa akili iliyojaa kichwani mwake ni kutoa tu ile mimba na si vinginevyo.
Alichukua simu yake na kuingia facebook, akamuona Rahim yuko hewani akaamua kumtumia ujumbe,
“Nina shida na laki moja na nusu”
Akaituma kisha akaizima kabisa simu huku akiwaza maswali kadhaa,
“Lazima ataniuliza ya nini, sijui nitamjibu vipi mimi? Akisema sina, oooh nitakuwa nimeumbuka mimi Erica”
Akachukua simu yake ya kawaida na kuandika ujumbe mfupi, kisha akamtumia Tumaini,
“Naomba nikopeshe laki moja na nusu”
Akatuma huku akiwaza pia kuwa lazima Tumaini atamuuliza kuwa ana shida nayo ipi, na kweli ujumbe toka kwa Tumaini uliingia ukimuuliza,
“Una shida gani na hiyo hela Erica?”
Hakuweza kujibu kwani hata hakujipanga kuwa aseme ana shida ipi na hiyo hela, badala yake akatuma ujumbe kwa dada yake Bite,
“Dada, naomba laki moja na nusu nina shida nayo”
Muda kidogo baada ya kutuma, dada yake alianza kumpigia na kumfanya ashindwe kupokea kwani bado hakujipanga na maelezo. Ikabidi sasa aanze kujifikiria kuwa akiulizwa hiyo laki moja na nusu ya nini atafute uongo wa kusema, alijiuliza sana na kukosa jibu. Aliamua kutokuangalia simu yake kuwa ni ujumbe gani amejibiwa au ni nani anampigia, ila kuna muda simu yake iliita sana na kila ilipokatika ilianza kuita tena ikabidi aichukue kuipokea maana alipoangalia alikuwa na Bahati na akaona asipopokea Yule Bahati hatoacha kumpigia na kama akizima simu basi dada yake atamuuliza kuwa kwanini alizima simu,
“Erica mpenzi wangu una matatizo gani?”
“Usiniulize bhana nina matatizo gani, mimi nina shida na hela”
“Shilingi ngapi unataka mpenzi wangu?”
“Nahitaji laki moja na nusu”
“Duh hela yote hiyo ya nini mama?”
“Kama huna sema huna sio kuniuliza hela yote ya nini”
“Erica, wewe ni mpenzi wangu na nina wajibu wa kuhoji kuwa una tatizo gani. Hata hivyo hiyo hela sina, ila nina elfu ishirini, naomba nikutumie huenda ikakusaidia kidogo”
“Haya tuma”
Kisha Erica alikata simu, na baada ya muda kidogo alikuwa ametumiwa elfu ishirini na Bahati,
“Yani angekuwa na hela huyu ningefaidi sana, ila sema mtu mwenyewe masikini”
Alipigiwa tena simu na Bahati na kupokea,
“Hata kama hujataka kuniambia kuwa una tatizo gani, ila nipo tayari kukusaidia. Kesho nitajitahidi kupambana na nitakachopata nitakutumia mpenzi wangu”
“Haya asante, usiku mwema”
Kisha Erica akakata simu na kulala, ila kiukweli usingizi bado haukuja kabisa maana alikuwa akiwaza kuhusu ile mimba na atafanya kitu gani aweze kupata pesa za kuitoa, hakuwa na marafiki wengi na wachache alionao hawakuwa na uwezo wa kumkopesha laki na nusu, mwenye uwezo ni Tumaini ila hakuweza kumwambia tatizo lake kwani Tumaini anapinga vikali swala la kutoa mimba.
Akawaza kuwa amuulize Johari, akaona hapana maana hapo siri zake za kutoa mimba zitajulikana, akakumbuka kuna siku aliwahi kusikia watu wakisema kuwa kunywa majivu kunatoa mimba. Akainuka na kwenda jikoni, akakoroga majivu kwenye kikombe na kunywa kisha akarudi chumbani ili kusikilizia matokeo ya majivu yale.
 
SEHEMU YA 128


Hadi kesho yake hakuona dalili yoyote ile na kuhisi huenda ni dawa ya uongo au hakusikiliza vizuri kuhusu njia za kutolea mimba kwa kutumia majivu.
Akawasha tena simu yake na kuingia facebook ili kuona kama Rahim kamjibu ila akaona hajajibiwa, akakosa raha kabisa, muda kidogo aliona ujumbe facebook kutoka kwa Rahim,
“Yani leo ndio nimeingia kwenye mtandao na kukuta una shida na hiyo pesa, naomba kesho nikutumie kwa western union, nitumie tu details zako Erica”
Yani Erica alisoma ule ujumbe mara mbili, hakuamini macho yake hata akawaza kuwa aandike kwanza asante au atume taarifa zake kwanza, alihisi kuchanganyikiwa maana kati ya wote aliowaomba ni Rahim tu ambaye hakumuuliza kuwa pesa ile anaihitaji ya nini, alichukua simu yake na kumtumia taarifa zake kisah chini yake kumshukuru ila Rahim alimjibu,
“Usijali, hayo ni mambo madogo sana kwangu”
Erica alitabasamu na kuweza kuendelea na shughuli zake zingine maana alikuwa na uhakika wa kuipata ile pesa.
Jioni yake alitafutwa na Bahati pia kwenye simu, akaamua kupokea simu yake,
“Erica mpenzi wangu, nimepambana kadri niwezavyo, nimemkopa rafiki yangu na nimepata elfu hamsini tu naomba nikutumie tafadhali”
Erica akaona kama akikataa basi atamfanya Bahati ajisikie vibaya, kwahiyo alimkubalia na baada ya muda mfupi Bahati alimtumia ile elfu hamsini kwahiyo ikawa jumla elfu sabini ukiongeza na ile elfu ishirini ya jana yake, kiukweli alijua ni wazi kabisa kama Bahati angekuwa na hela za kutosha basi angemsaidia ni kwavile tu hakuwa na hela za kutosha. Akamshukuru pia huku akingoja hela atakayotumiwa na Rahim kesho yake.
Usiku wake Rahim alimtumia taarifa za kwenda kuchukua hela zake, na kusema kuwa kesho asubuhi angeenda kuchukua.
Na kweli alienda kuchukua na kushangaa sana, maana alijua Rahim kakosea kusema nimetuma laki tano, akakuta kweli anapewa laki tano, alistaajabu sana na kuona ni kweli anapendwa sana na Rahim, moja kwa moja alienda kule hospitali alipoahidiana na Yule dokta na kupewa muda wa kufanyiwa tukio la kutoa mimba.
Muda ulipofika alielekea alipoambiwa ila moyoni mwake alijiapia,
“Hii itakuwa ni mimba ya mwisho kutoa katika maisha yangu yote, nikija kupata mimba tena nitazaa bila kujali chochote. Nimejifunza sasa na sitarudia tena”
Daktari alifika na kumfanyia ile shughuli, maumivu aliyoyapata siku hii yalikuwa makali sana ila dokta alimaliza kumtoa mimba na kumuandikia dawa kisha kumuacha apumzike kidogo.
 
SEHEMU YA 129


Alirudi nyumbani sasa na kwenda kulala ila alishukuru sana kwa kufanikisha swala lake la kutoa mimba, ila akajisemea kuwa hataki tena kujihusisha na maswala ya ngono,
“Ilimradi mwanaume anipendaye yupo nje ya nchi basi akirudi labda ndio nitakuwa nae pamoja, ila kwasasa sitaki kuwa karibu na mwanaume yoyote Yule. Bahati naweza kummudu, ni msumbufu sana ila naweza kummudu najua nikimwambia sitaki hawezi kunilazimisha ila sitakaa na mwanaume yoyote Yule kwenye maeneo hatarishi”
Lile lilikuwa somo kubwa sana kwake maana kutembea na kaka yake lilikuwa swala la ajabu na aibu sana katika maisha yake.
Alijifikiria kuhusu elfu sabini aliyopewa na Bahati akaona kama atamrudishia basi Bahati atajisikia vibaya sana, akaona ni vyema amnunulie Bahati zawadi kwa ile hela au aongezee kidogo ampatie ila swala la kumrudishia litamfanya Bahati ajisikie vibaya, akajifikiria sana kuwa ampatie zawadi gani Bahati, akakumbuka kuwa ndani kwa Bahati kuna jiko la mkaa tu kwahiyo akawaza kuwa amnunulie jiko la gesi.
Akalala muda huo akiwa na amani moyoni mwake, alikuja kushtuka wakati usiku umeshaingia mama yake ndio alienda kumuamsha,
“Una matatizo gani siku hizi mwanangu, unajua sikuelewi? Toka umerudi yani hueleweki kabisa, una tatizo gani, niambie unajua mimi ni mama yako”
Muda ule ulke simu ya mama yake ikaita, na akaipokea ilionyesha kuwa alikuwa akiongea na Bite kwani alikuwa akimueleza matatizo aliyokuwa nayo Erica kwa kipindi hiko, Erica akainuka na kwenda kuoga kwani alijua baada ya hapo angeitwa tu na mama yake kuulizwa kuwa ana tatizo gani tena.
Na kweli baada ya kumaliza tu kuoga, mama yake alimuita na alipoenda alianza kumuuliza,
“Ulimuomba dada yako laki moja na nusu ya nini?”
“Mmmh jamani dada Bite nae, yani kakwambia”
“Ndio lazima aniambie mimi ndio mama yenu, na amekuuliza ya nini hujamjibu. Haya niambie sasa hiyo hela ulitaka ya nini?”
“Mama, kuna rafiki yangu anaolewa sasa nilikuwa nataka hela ya mchango maana nilimuahidi nitamchangia yani sikuwa na furaha sababu sherehe yake imepita jana”
“Hivi wewe kama kuna jambo kama hilo kwanini usiseme mapema?”
“Mama, yani sikuelewa nimekuja kushtukia tu siku zimeisha na nimeogopa kumwambia dada sababu najua angenishushua”
“Ndio lazima akushushue, mtu unasoma halafu unataka kuanza kujishughulisha na kuchanga michango mikubwa hiyo ya harusi. Ujinga huo, michango waniambie mimi”
Erica alishukuru mama yake akubaliana na uongo aliomdanganya kwani muda wote alikuwa anatafuta uongo wa kusema kuhusu kukaa na mawazo vile na kuomba hela.
 
SEHEMU YA 130


Kesho yake alienda kwenye maduka ya gesi na kununua mtungi mdogo wa gesi uliokuwa na kila kitu kwa elfu tisini, kisha akakumbuka kuwa ndani kwa Bahati kuna joto sana, aliamua kumnunulia na feni ya chini ya elfu sabini maana hela alikuwa nazo kwa kipindi hiko. Akakodi bajaji hadi alipokuwa akiishi Bahati maana alifanya kwa kumshtukiza tu.
Alimkuta Bahati anafua, yani Bahati hakuamini kile alichokiona kuwa Erica kamnunulia zawadi, Erica alishusha zile zawadi na kumwambia Bahati kuwa anawahi chuo ila hakujua kama kile kitu kimetengeneza kitu gani kwenye moyo wa Bahati, kwani Bahati alijiona kuwa ni mwanaume anayependwa na Erica kuliko watu wote duniani kwani hakufikiria kama inawezekana kwa mwanamke asiyekupenda kukufanyia vile, ukizingatia hata hela aliyompa Erica haikufikia vitu ambavyo Erica alimnunulia.
Erica hakutaka kukaa sana kwa Bahati kwani aliogopa maswala ya kujikuta akiingia tena kwenye uzinifu kwa kushawishiwa, alishajisemea kuwa hatokuwa kwenye mazingira hatarishi tena kwahiyo alijizuia hata kuingia ndani kwa Bahati.
Alipokuwa chuoni, jioni yake alifatwa na Bahati, hakupinga kwenda kuongea nae,
“Kwakweli Erica nimeamini unanipenda, na nakuahidi kukupenda hadi pumzi yangu ya mwisho”
Erica alimuangalia tu Bahati, huku Bahati akiendelea kuongea,
“Sasa lini utahitaji nikufurahishe kwa mapenzi mpenzi wangu?”
“Naomba nikwambie jambo hili Bahati, sitaki tena ngono hadi pale nitakapoingia kwenye ndoa”
“Hilo sio tatizo Erica, si ukubali tu nikuoe hata sasa”
“Hapana siwezi kuolewa hadi nimalize chuo, kama unanipenda basi kubaliana na mawazo yangu, sitaki kufanya chochote tena hadi ndoa”
Bahati hakuwa na usemi zaidi ya kukubali kile ambacho Erica alisema kwani alimpenda sana Erica,
“Pia naomba usiwe unakuja mara kwa mara hapa hosteli nakuomba”
“Sawa, hakuna shida”
Kisha Erica akaagana nae, hakutaka kuendelea kumkataa wakati mtu bado anajilazimisha kwake akaona njia pekee ni kumuomba asiwe anaenda mara kwa mara pale hosteli, na alishukuru kuona vile amekubali.
Kitu ambacho hakukifahamu Erica ni kuwa watu wengi pale chuoni walikuwa na habari zake mbali mbali nzuri na mbaya, alizozijua na asizozijua, sababu hakutaka kuwa karibu na marafiki maana siku zote walitumika kuumiza moyo wake, ilikuwa ni ngumu sana kujua habari yoyote inayoendelea juu yake pale chuoni, alichojali yeye ni kufanya masomo yake tu.
 
SEHEMU YA 131


Mawasiliano ya Erica na Rahim yalipamba moto kiasi kwamba walijikuta hadi wakipanga mipango ya ndoa kwenye simu na idadi ya watoto watakaowazaa, Erica alianza taratibu kuuweka moyo wake kwa Rahim kwani aliona ndiye mwanaume ampendaye.
Siku hiyo akiwa anawasiliana nae kwa njia ya ujumbe facebook kama kawaida yao, alishangaa kuona kuna mtu kamtumia ombi la urafiki, kumuangalia mtu Yule akaona ni Erick, moyo ulimlipuka paa, akamfungua mtu huyo na kuangalia picha zake vizuri, akaona ni Erick Yule Yule anayempenda siku zote, alihisi akili yake kuhama kwakweli maana kila akimfikiria mtu huyu huwa anashindwa kuelewa kama anaweza kukubali kuolewa na mwanaume mwingine ikiwa Erick hajaoa, ingawa taarifa za kuambiwa kuwa Erick ana mwanamke zilimuumiza sana na kujiapia kuwa atamsahau ila kitendo cha kuona kamuomba urafiki facebook kilihamisha akili yake kabisa na kujikuta akikubali ombi la urafiki wa Erick huku akitamani kumtumia ujumbe ila kabla hajamtumia alishtukia tu kuna ujumbe ukitoka kwa Erick kwenda kwake,
“Hongera Erica, ulinitafuta ilihali ukijua kuwa umeshaolewa? Iliniuma sana kuongea na mume wako”
Erica alishangaa sana na kumuandikia ujumbe,
“Hizo habari za mimi kuolewa umezitoa wapi Erick? Mimi sijawahi kuolewa na wala simu yangu haijawahi kushikwa na mwanaume”
“Acha uongo Erica, mwanaume wako alipokea hadi usiku akisema umelala nae, niliumia sana Erica yani wewe msichana unaumiza akili yangu”
Sasa muda huo wakati anasoma huo ujumbe kuna ujumbe uliingia kutoka kwa Tumaini ukimwambia,
“Erica toka siku ile hujanijibu hadi leo kuwa hela ile ulikuwa unataka ya nini, halafu ni mwezi sasa hatujaonana kwanini mdogo wangu? Una matatizo gani? Usinifiche, kuna habari nyingi sana nimesikia kuhusu wewe, ndiomana nakuuliza kwa makini ikiwezekana tuonane na tuongee kuhusu hizi habari kama zina ukweli maana zinaniumiza sana”
Aliisoma na kujiuliza sana kuwa ni habari gani hizo ila hakupata jibu, ila akaona ni vyema amjibu Erick kwanza, halafu ndio aendelee kuulizana na Tumaini
“Unajua ninavyokupenda Erick, siwezi kufanya huo upuuzi”
Akatuma, na kushtuka kwani aligundua kuwa ule ujumbe ametuma kwa Tumaini na sio Erick.
 
SEHEMU YA 133



Kesho yake kama kawaida alienda chuo kwenye kipindi, na alipotoka tu kwenye kipindi alitafutwa na Tumaini na kutajiwa mahali ambako Tumaini yupo kisha akaenda kumsikiliza. Alimkuta na kumsalimia ila Tumaini hakuitikia salamu ya Erica, akamuuliza
“Haya sasa nionyeshe huyo Erick uliyekuwa unamwambia kuwa unampenda facebook”
Erica hakutaka kumdanganya Tumaini ila pia hakutaka kumwambia ukweli kama ni yeye ndiye aliyekuwa anasemwa na Erick, kwahiyo akamwambia
“Ni kweli niliyekuwa nawasiliana nae ni Erick mdogo wako ila sikutaka kukwambia ukweli maana ulishachukia tayari”
Tumaini akamzaba kibao Erica na kumuuliza,
“Ni lini umeanza kumpenda mdogo wangu?”
Erica alikuwa akijishika shika shavu pale alipozabuliwa kofi,
“Ni tangia nilipomuona kwako”
“Nilijua tu mwanaizaya wewe, mtoto shetani kabisa wewe. Kwan je unaonekana mstaarabu kumbe mbwa mwitu, kwahiyo siku ile ulitulaghai na Sia ili uchukue namba ya mdogo wangu na uanza kumchombeza? Ndiomana kila nikikwambia kuhusu mchumba wa Erick unapata kimuhemuhe na kuaga”
“Nisamehe dada”
“Nikusamehe nini shetani mkubwa wewe, ninachotaka ni uachane na mdogo wangu atulie na mchumba aliyempata kwanza ni mzuri sana. Sitaki mdogo wangu aanze kuhangaika na watanzania tena, haswaa mtu kama wewe mwenye skendo kila kona ya chuo hiki”
“Ila dada kwani mimi nina skendo gani?”
“Tena utulie, unafikiri mambo yako ni siri? Kila mtu hapa chuo anayajua mambo yako, ulisababisha vijana wawili wapigane hosteli sababu yako, hapo ulipo ushabakwa na wanaume wane unafikiri ni siri? Kila mtu anajua, tena ulivyomzoefu wa hayo mambo yani ulibakwa na kuonekana kujionea sawa tu. Na zaidi ya yote nimepata habari kuwa ulikuwa na mahusiano na Derick, hakuna asiyejua hapa chuoni kama Derick ni mwanaume Malaya chuo kizima yani kazi yake ni kubadilisha wanawake tu, ila kwako akakuzoa maana ushazoea kuzolewa na wanaume. Hivi wa kumtaka mdogo wangu wewe? Hapo ulipo unanuka zinaa, mwanaharamu wewe”
Erica alikuwa kimya kabisa maana hakuamini kama maneno haya yanaongelewa na Tumaini, aliyemuona kama dada yake hapo chuoni, aliona kuwa amepata ndugu na si rafiki na ndiomana akawa nae karibu, ila leo amemwambia maneno makali sana ambayo alibaki kuyashangaa tu. Kitendo cha Erica kuwa kimya kilimfanya Tumaini aendelee kuongea,
“Nakuomba Erica uachane na mdogo wangu tafadhali, au kwavile kwetu nilikwambia tuna uwezo? Achana na Erick nakuomba, achana nae kabisa. Niahidi sasa hivi kuwa utaachana na Erick”
“Nakuahidi dada, sitaendelea nae tena”
“Yani wewe loh”
Akatema na mate chini na kuendelea kuongea,
“Unatia hata kichefuchefu yani, msichana mzuri hivyo, unaonekana mpole tena binti mlokole kumbe hakuna kitu ni jamvi la wageni yani wewe kila anayekutaka anakupata, na isitoshe ushabakwa na watu zaidi ya wanne halafu bila haya unamwambia mdogo wangu unampenda, na nitamtafuta Erick nimwambie skendo zako ili hata asikukubali mwanaizaya wewe”
Tumaini akaondoka na Erica akaondoka pia bila ya kumjibu chochote maana alikuwa akishangazwa tu, kichwa chake kilijaa mawazo ya kila aina na kufanya akose raha kabisa huku akijiuliza kuwa ni wapi alipokosea maana hakuelewa kabisa, swala lake la kutafuta penzi la kweli limemfanya aonekane Malaya na hafai kabisa kwa jamii, Erick ni mwanaume anayempenda sana ila dalili ya kumpata tena hakuwa nayo kwa zile skendo alizosikia kuhusu yeye.
 
SEHEMU YA 134


Alirudi hosteli akiwa na mawazo sana, akaona kuwa atawaza sana bila ya kuwa na majibu yanayoeleweka, akajiangalia ni kweli hakuwa na rafiki pale chuoni sasa ni nani anayeweza kumwambia ukweli kuwa zile kashfa za ajabu ajabu kwake zimeenezwa na nani na zimeanza vipi, akamkumbuka Fetty kuwa anaongeaga ongeaga nae, akatoka kwenda kumuulizia kwenye chumba chake ili akaongee nae maana alimuona kuwa na maneno mengi sana na kwa vyovyote vile lazima atakuwa ni binti mbea.
Alienda kumuulizia na kweli alimkuta na kwenda nae nje kwenye kivuli kisha akaa nae ili kuzungumza nae,
“Samahani Fetty, eti ni habari gani zinazoenea kuhusu mimi?”
“Tatizo lako Erica huna marafiki na ndiomana huwezi kujua kitu chochote kinachoendelea kuhusu wewe, ila kiukweli habari zako ni mbaya sana yani ningekuwa wewe hata chuo ningehama”
“Niambie Fetty ni habari zipi hizo?”
“kwanza kabisa, lile swala lako la wanaume kupigana sababu yako limeenea hosteli hapa kote na sio hosteli tu hadi chuoni habari hizo wanazo yani hakuna mtu anayejua, halafu swala lako la kubakwa na wakaka wane limeenea kote”
Erica alimkatisha kwanza Fetty na kumuuliza kwa makini,
“Nimebakwa! Jamani hizo habari kazieneza nani? Mbona mimi sikubakwa jamani!”
“Erica, wewe unasema hujabakwa ila wakaka waliokubaka wameeneza habari hosteli kote hya kwamba walikubaka siku hiyo saa nne, eti ulijichelewesha kuondoka na kuna jamaa yako ulikuwa unamsubiri ila hakutokea, na wale walikuwa wamekuvizia maana ulishawadanganya wote na umekula hela zao, kwahiyo wakakubaka”
“Jamani jamani loh! Hiki chuo kina mambo ya ajabu jamani, sijawahi kubakwa mimi, sijawahi kubakwa kabisa katika maisha yangu. Na kuhusu Derick je maana nimesikia sikia habari”
“Shoga, Derick ni Malaya koko ila sikutaka tu kukwambia siku ile maana sijui kama ungenielewa ila Derick ni Malaya koko. Sasa kitendo cha wewe kuwa na mahusiano na Derick kimejulikana chuo kizima yani watu wamekuzania kuwa na wewe ni malaya maana kumkubali Derick anayejulikana chuo kizima kuwa ni malaya ni swala la ajabu”
“Jamani! Kumbe Derick ni malaya? Sikujua Fetty”
“Utajulia wapi na hauna mashoga, katika maisha unatakiwa kuwa na marafiki ili kutambua vitu kama hivi, watu wanakuwa na marafiki ili kujua mambo mbalimbali. Kidole kimoja hakivunji chawa shoga yangu, unatakiwa kuwa na marafiki ili kuweza kuisafisha sifa yako. Sasa swala la kubakwa ungekuwa na marafiki hata wangekutetea kwa watu kuwa hukubakwa ila marafiki huna na habari imeenea chuo kizima kuwa ulibakwa”
Erica alipumua kidogo huku akijiuliza kuwa ni nani aliyeeneza habari zake kuwa alibakwa wakati hakubakwa, kiukweli hakupendezewa kabisa na zile habari ila alimshukuru Fetty kwa kumwambia ukweli,
“Tena nasikia kuna habari yako hiyo kubwa kuliko zote ila bado mwenye nayo hajapata ushahidi vizuri”
“Habari gani hiyo?”
“Sijui, ila wanasema tu kuna habari yako mbaya inakuja kuenea chuoni. Erica kuwa makini sana, kuwa makini na watu unaoanza nao mahusiano ya kimapenzi, nahisi habari zako nyingi zinaenezwa na Derick, kuwa nae makini sana, ni mvulana malaya Yule na anapenda kumchafulia sifa msichana ndiomana wengi wanamkwepa kuwa nae kwenye mahusiano.”
“Nashukuru sana Fetty, inatosha kwa uliyoniambia asante”
Erica aliondoka na kuingia ndani hosteli, akapabeba mkoba wake na kuondoka zake, yani muda huo aliondoka na kwenda nyumbani kwao kabisa kwani zile habari hazikumfurahisha kabisa.
 
Back
Top Bottom