NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE
MTUNZI :
Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHILINI NA TATU: Deus akiwa kwenye korido refu la ndege hii ya kisasa, akatazama kushoto na kulia kutazama seat itakayo mfaa, mpaka alipovutiwa na seat moja ya pembeni ya seat ambayo ilikaliwa na mschana mrembo kweli kweli mwenye asili ya Ethiopia, ambae muda huo alikuwa anasoma kitabu, “lazima atakuwa anaongea kiingeleza anafaa kuwa kampani yangu huko Congo” alijisemea Deus, huku anaisogelea ile seat, pasipo kujuwa huo ndiyo mwanzo wa kubadili maisha yake kutoka kuwa askari hodari mpaka kijana anaeshiriki uharifu……ENDELEA……
Deus aliembea taratibu, kuisogelea ile seat ya karibu na yule mrembo, ambae licha ya kufunika nywele zake kwa kitambaa maalumu cha kichwani, lakini zilionekana wazi upande wa mgongoni, jinsi zilivyo nyeusi na ndefu, huku macho yake yakiwa kwenye kitabu alicho kuwa anasoma, huku moyoni mwake kijana Deus, akiwaza namna ya kumkabiri mschana huyu mrembo, kwa lugha ya kiengereza, ambayo yeye alikuwa anaifahamu kwa juu juu, nasiyo kwa undani zaidi.
“Hi” alisalimia Deus huku anakaa kwenye seat ya pembeni ya mschana yule, ambae kimtazamo, ni kama alikuwa na miaka ishirini sita au saba, hivyo angekuwa amemzidi kijana wetu miaka kati ya mitatu au minne, ambae aligeuza uso wake na kumtazama kijana Deus, ambae wakati huo alikuwa amevalia mavazi yake nadhifu ya kijeshi, yaliyomkaa vyema kwenye mwili wake na kufanya umbo lake la mazoezi, lililo shabihishwa na urefu wa kijana huyu wakupendeza vionekane vyema.
Ilitumi kama sekunde nne kwa mschana yule, mwenye mwonekano wa kihabeshi usoni pake, huku umbo lake likiwa la kuvutia, maana alimtazama juu mpaka chini, kisha akapandisha tena uso wake na kumtazama kijana usoni, “mambo” alijibu yule mwanamke kwa lugha adhimu ya Kiswahili iliyo nyooka, kiasi cha kumfanya Deus atabasamu kidogo, “ni bahati kumbe wewe ni mtanzania?” aliuliza Deus akionyesha wazi kufurahia jambo lile, “kwani uwezi kuongea na mtu toka taifa jingine?” aliuliza yule mschana, kwa sauti kavu, huku akimtazama Deus kwa macho ya ukali, akionyesha wazi kuwa hakupendezwa na maneno ya kijana wetu Deus.
Hapo Deus akatuliza akili na kumtazama mschana huyu, akijaribu kuisoma hali yake kwa muda ule, ukweli ukimtazama kwa macho, usingekubali hata kwa viboko, kuwa ni mtanzania, maana mwonekano wake ulionyesha wazi ni raia wa Ethiopia, lakini Kiswahili chake, ndio kinge kuweka njia panda, maana ungesema umekutana nae tegeta au msata.
Deus aligundua kuwa, mschana huyo, alikuwa amechukizwa na kauli ile yenye mtazamo wa kibaguzi, “haaaaa….hapana… ila tu.. niliiii….nilikuwa na hofia kuwa tusinge elewana lugha” alisema Deusi kwa namna ya kujitetea, japo kiukweli hiyo ndiyo sababu halisi ya kufurahi kwake.
Yule mschana mrembo, hakuongea tena neno jingine zaidi akatazama kitabu chake, ambacho jarada lake lilikuwa limeandikwa HELLO DOCTOR, hapo Deus akawa mpole kidogo, na kuanza kuwanza jinsi atakavyo sawazisha makosa yake, japo hakuwa na uzoefu mkubwa wa kucheza na akili za waschana, lakini alijaliwa busara.
Kwanza Deus akatoa simu yake na kuanza kujifanya anaperuzi, wakati hakuwa na network, huku akili yake ikiwa ni ataanzaje kuongea na mschana huyu, ambae siyo tu uzuri wa sura yake, ila pia alionekana kuwa ni mtu mwenye heshima zake, hasa kutokana na mavazi aliyo ya vaa, pia utulivu wake, na hata ukimtazama kwa macho, ungejuwa ni mtu mwenye taaluma flani, kiwango cha juu, maana ukiachilia vijimiwani vyake vya macho alivyo vivaa, pia alikuwa amefunika nywele zake, kwa kitambaa cha rangi ya maziwa, kilichofanana rangi na suit ya kike aliyoivaa, suit iliyo mkaa vyema mwili mwake, huku akiongeza na vito vya thamani alivyo vaa mwilini mwake, kama vile hear ring, pete na mkufu, hata viatu vyake vya kumbukiza, vyeusi vilikuwa vizuri sana.
Baada ya kuwaza kwa muda flani, Deus akapiga moyo konde, na kumvaa yule mschana, “samahani dada naitwa Deus kutoka Tanzania, naelekea DRC, napenda kukufahamu kama hutojari” alisema Deus, kwa sauti tulivu ya upole, huku anamtazama mschana yule kwa macho yake, ambayo siku zote, huwa yanamtambulisha tabia yake ya utulivu na upole.
Yule mschana alifunika kitabu chake, na ukilaza kwenye paja lake pana, kisha akamtazama Deus, “kaka nivyema kama ungeweka mawazo yako kule unakoelekea, kuliko kuanza kuhitaji kujuwa majina ambayo hayatokusaidia” alisema yule mschana mrembo, kwa sauti ya chini tulivu, kisha anageuka na kuchukuwa mkoba wake mdogo, ambao ulikuwa pembeni yake, akaufungua na kutoa simu yake ya kisasa, na ear phone, ambayo aliichomeka masikioni, na kuweka music flani, ambao Deus hakupata bahati ya kuusikia, kisha akafunua kitabu chake, na kuendelea kusoma.
Hapo Deus akaona tayari amesha poteza haki ya kuongea na mschana yule mrembo, hivyo na yeye akainamia simu yake, na kuanza kutazama picha alizopiga akiwa katika mzeozi ya kijeshi, katika vyuo mbali mbali, kabla hajasikia tangazo toka kwenye speeker za ndege ile, ikiwashauri wa funge mikanda, tayari kwa kuanza safari.*******
Naam masaa mawili ambayo ndege ilikuwa hewani, yalimuwia vigumu sana kijana Deus, ambae japo Deus hakuwa mwongeaji sana, ila alijihisi unyonge sana, na kutamani ndege ifike haraka, ashuke, na yule mschana aendelee na safari.
Japo mawazo na matamanio yake yalikuwa tofauti, maana baada ya ndege kutua, katika uwanja ndege wa Goma, jirani kidogo na kitongoji cha bhilelee, pembezoni mwa barabara iendayo kaskazini mwa jimbo la kivu ya kaskazini, yaani mikoa ya Bhutembo na Beni, kupitia mbuga za wanyama za Vilunga, kilomita zaidi ya ishirini toka mlima mrefu wa Volocano, wa nyilagongo, ukanda ambao kwa kiasi kikubwa, ulikuwa umekaliwa na waasi wa M 23
Wakati Deus akiwa anashuka toka ndani ya ndege, akiongozana na wale makamanda wenzake, yani wa kutoka Tanzania, na wale wanchi nyingine, akashangaa kuona yule mschana mrembo wakihabeshi, akishuka toka ndani ya ndege, akiwa ameongozana na wanaume wawili, nao wenye mwonekano wa ki-Africa, ambao walipokelewa mabegi yao makubwa, nakuongozwa, kuelekea upande ambao, kulikuwa na magari mawili, moja likiwa ni bus dogo aina ya Toyota Coster, lenye maandishi makubwa meusi, UN na pembeni yake kukiwa na nembo ya umoja wa mataifa ya rangi ya blue, pamoja na maandishi ya blue, MUNOSCO, huku jingine likiwa ni gari dogo, aina ya Toyota land Cruizer, nalo jeupe, lenye maandishi makubwa ubavuni, kama lile bus, UN lakini hili yalikuwa ya rangi ya blue, na mbele ya maandishi hayo kulikuwa na nembo ya UN WHO, nayo ya blue.
Kitu ambacho kilimfanya Deus ajihurumie nafsi yake, ni pale alipowaona wale watu watatu, wakiongozwa na wale waliowapokea mizigo, wakielekea moja kwa moja, kwenye lile gari dogo, Toyota Land Cruize, na kuingia ndani ya gari hilo, huku yule mschana mrembo akienda kukaa kwenye seat ya mbele upande wa abiria, kisha lile gari kuondoka zake, wakiwaacha wao wanachukuwa mizigo yao na kuelekea kwenye lile bus dogo, yani Toyota Coster, ambalo lilikuja kuwapokea wao, maana hata derva wa gari lile, alikuwa ni askari mwenye cheo cha koplo, toka nchini Nigeria.
Deus aliambatana na wenzake, ambao ni wakubwa wake kwa cheo, kuingia ndani ya gari, na kuanza safari kuelekea, kwenye ofisi za makao makuu ya umoja wa mataifa, pale goma, huku akiombea kuwa, asikuane tena na yule mwanamke, mwenye malingo na dharau, ambae yeye pasipo kujuwa kuwa ni afisa wa UN, alianza kumchombeza kule ndani ya ndege.
Naam Deus alidhania kuwa ni bahati yake, maana alihisi kuwa mambo yameenda kama alivyo tamani yawe, maana week nzima aliyo kuwepo pale Goma, hakuwahi kumwona yule mwanamke wala wale wenzake, na tayari walisha patiwa vitambulisho vya umoja wa mataifa chini ya MUNUSCO, pia yeye kwa upendeleo, akapangiwa kuishi ndani ya kambi moja la jeshi, la pale pale mjini Goma, la MUNIG BASE, lililopo kilomita kama tisa toka mjini, ambalo lilikuwa linakaliwa na askari wa kutoka nchi mbili, wenye jukumu moja, yani platoon mbili za Tanzania, na platoon mbili za kutoka afrika ya kusini.
Bahati aliyokuwa nayo Deus nikwamba, hakutakiwa kulipia nyumba, maana aliishi kama askari wenzake, na hata chakula alipewa kipaumbele na kula chakula cha pekee, pale kambini, na pia tayari alisha kabidhiwa gari, ambalo alikuwa anawaendesha wale maafisa aliokuja nao toka Tanzania, ambalo lilikuwa lina lala pale Munig Base, na alifanya majukumu hayo akiombea asije akakutana na yule mwanamke wa kihabeshi, ambae mpaka hapo hakuwa anajuwa anahusika na nini katika UN.
Sasa tayari kijana Deus alishabadili line ya simu, na kuweka mtandao wa kule Congo, ambao ulimsaidia kupata network ya kuwasilina na wapendwa wake Tanzania, akiwa pamoja na rafiki yake wa simu, Pacha, japo pia aliweza kuwasiliana kwa line yake aliyotoka nayo Tanzania, ila kwaajili ya kupokea simu tu, endapo angepigiwa na mtu toka tanzania.
Deus alizidi kujiona mwenye bahati zaidi, week moja baadae, baada ya kupata safari ya kuelekea mkoa wa ben, kuwapeleka wale maafisa wake, japo barabara ilikuwa ni ngeni kwake, lakini kwa uwezo mkubwa ambao kijana huyu alikuwa nao katika kuendesha gari, alitumia masaa kumi na moja, pasipo kujari ubovu wa barabara ile, kuingia Ben na kisha moja kwa moja mpaka uwanja wa ndege wa Ben Mavivi, kwenye kambi ya jeshi chini ya UN, inayokaliwa na majeshi ya MONUSCO, toka nchi za Filipino na India, kilometer kumi toka mjiniBen.
Upande huo, ni upande ambao umezungukwa na misitu mikubwa sana, ya kaskazini mashariki mwa Kongo, ni upande ambao, ulikuwa umetawaliwa na tishio la uwepo wa kikundi cha waasi wa zamani wa Uganda, wa IDFNALU, ambao kwa kiasi kikubwa walikuwa wanahusishwa na matukio yote mabaya ya upande huo wa Congo, kama vile, utekaji nyara, mauwaji ubaki na uporaji wa mali za raia na serikali.
Hapo Deus akajiona kuwa yupo sehemu salama, japo ilimuwia vigumu kuishi na watu mafia mengine ambao hata lugha walikuwa hawaelewani, na ukichulia kuwa wale wakubwa wake, muda mwingi walikuwa maofisini, wanafanya majukumu yao, na mbaya zaidi ofisi zilikuwa pale pale kambini, kiasi kwamba, muda wote yeye Deus alikuwa ametulia kwenye sehemu aliyofikia, akiperuzi mtandaoni, na kuchat na rafiki yake aliemwita Pacha, kutokana na kufanana kwa tarehe yao ya kuzaliwa. maana hakuwa na haja hata ya kuwapeleka wakuu wake ofisini, kutokana na ukaribu wa ofisi.******
Naam! kijana Deus akiwa anaamini amesha kaa mbali na sehemu ambayo yupo yule mwanamke mjivuni, siku tatu baadae, mida ya saa mbili, za asubuhi, Deus akiwa ametulia chumbani kwake anatazama tv, huku mara chache akichat na mwanamke aliemsevu kwa jina la pacha, kwenye simu yake, mara akasikia mlango wa chumba chake unagongwa, akainuka na kwenda kuufungua, hapo akakutana na kijana mmoja wa kiafrika alieshika karatasi mkononi, “mambo vipi rafiki, biko Bien?” alisalimia yule kijana kwa sauti yenye rafudhi ya wenyeji wa pale Congo. …….....ilikufahamu kilicho tokea mpaka kijana Deus akaamuwa kuwa kama alivyo sasa, endelea kuwatilia mkasa huu wa #NYUMA_YA_MLANGO_WA_ADUI, inayo kujia hapa hapa
jamii forums