Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

MA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA KUMI NA SITA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA TANO: Mama Frank akiwa na tochi mkononi, akaingia ndani ya kiji mlango kile, kwa kutanguliza miguu, ambapo miguu yake iligusa ngazi, na baada ya hatua mbili, akakanyaga aridhi, “mpokee huyo” alisema bwana Frank, huku anampatia mtoto Deusi, ambae muda wote alikuwa anatazama kila kilichokuwa kinatokea usiku ule, hakika ilikuwa jambo geni na la kutisha sana kwake, lakini uwezi kuamini ujasiri wa mtoto huyu, ambae akuonyesha uoga wala wasi wasi, uso macho yake yakiwa makavu kabisa, pasipo dalili ya machozi wala kilio. …..ENDELEA…..


Baada kuhakikisha kuwa, tayari familia yake imeingia ndani ya shimo hilo, hapo bwana Frank akachukuwa, panga lake na ile tochi, aka ingia ndani ya lile shimo, “pumbavu jamaa wametuzidi akili” ilisikika sauti, toka upande wajikoni kabla bwana Frank ajafunga kile kimlango taratibu na kwa umakini mkubwa sana, “haraka sana watu wasambae mji mzima, askari wakae kwenye barabara zote, kabla hajavuka na kutoka nje ya jiji, kumbuka mtu huyu hatakiwi kufika asubuhi akiwa anapumua” ilisikika kwa mbali sauti, hiyo toka upande wa jikoni, Frank hakujari tena sauti hizo, zaidi aliiongoza familia yake, mle ndani handaki lenye upanda hafifu, na hewa nzito.********


Naam askari walionekana wametapakaa ndani ya jiji la TT, ambalo sasa hakukuwa na raia wa kawaida alie kuwa anazunguka, kutoka na mvua kali iliyokuwa inanyesha kwa nguvu na kuogofya, pengine ungeona gari moja moja likikatikiza kwa mwendo wa taratibu, kutokana na mvua nyingi iliyokuwa inanyesha, na kusababisha ukungu mwingi sana.


Bwana Frank Nyati na familia yake waliibuka mita kama hamsini toka kwenye nyumba yake, usawa wa kichaka cha mauwa kilicho pandwa kama fensi ya eneo lile, la nyumba ya bwana Frank, ambae yeye alikuwa ndie wa kwanza kuibuka, na kuangalia pande zote, kujiridhisha, kama ilikuwa ni sehemu salama, kwa yeye na familia yake kutoka shimoni, lakini wakati anatazama eneo lile, upande wa nyumbani kwake, akaona miili ya watu kadhaa ikiwa imelala eneo la mbele la nyumba yake, ikiwa ni matokeo ya Uzi gan, “sidhani kama kuna cha kusubiri hapa, cha msingi hakikisheni huyu mpuuzi anapatikana na muna muuwa yeye na familia yake yote” wakati huo huo, Frank akasikia sauti toka upande wa barabarani.


Alipo tazama upande huo, kwa tabu sana, akaweza kuona watu kadhaa waliosimama pembeni ya magari binafsi aina ya land rover mia na kumi, yanayofanana na magari yanayotumiwa na jeshi lao, jeshi la nchi hii ya #mbogo_land, waliozuiwa na vichaka vile vya maua, hivyo Frank akatoka na kutambaa usawa wa maua yale mpaka alipo pata sehemu nzuri ya kuwaona watu hao, ambao sasa walikuwa wananyeshewa na mvua, “vipi kuhusu miili ya wenzetu?” aliuliza mmoja kati ya watu wale, aliesimama na mwenzie mmoja alie valia koti refu la mvua, wakiwa ubavuni mwa moja kati ya magari yale matatu, nawasiliana na boss yeye atajuwa la kufanya, nyie wahini mkamsake huyu mpuuzi” alisema yule jamaa mwenye kuvalia koti refu, ambae sauti yake haikuwa ngeni masikioni mwa Frank.


Baada ya hapo Frank akawaona watu wale wenye kuvalia nguo nyeusi, wakiingia kwenye magari, mawili na kuondoka zao, huku wakimwacha yule mwenye kuvalia koti ra mvua, akiwa pamoja na derea wa gari moja lililobakia, Frank alimwona yule jamaa mwenye sauti anayo ifananisha, mtu ambae ni wazi kabisa kuwa ndie aliekuwa mkubwa wao pale walipokuwepo, akitembea kuja upande alipokuwa yeye, hapo Frank anajiweka sawa na panga lake mkononi, tayari kwa lolote.


Frank, anamkazia macho mtu yule kwa lengo la kumtambua, mpaka anapomwona anasimama mita chache, pembeni ya barabara, mita kama sita toka kwenye kile kichaka alichokuwepo yeye, kisha anafungua zip ya suruali yake na kutoa kifaa chake cha kukojolea, kisha anaanza kuumwaga mkojo, Frank hajari kuhusu kifaa hicho, ambacho hata yeye anacho pia, yeye anatazama uso wa jamaa huyu, ambae kiukweli uso wake una gubikwa na giza, na kushindwa kumtambua.


Lakini haikuwa hivyo muda wote, maana baada ya kusubiri kujitahidi kumtambua mtu yule, na kushindwa, Frank akaona kuwa anaweza kumkabili peke yake yule jamaa kwa kutumia upanga wake, maana mpaka muda yule, jamaa alikuwa pake yake, yani mbali na gari, ambalo kulikuwa na dereva peke yake.


Sasa basi, Frank hakumsubiri jamaa amalize kumwaga haja ndogo, aka hesabu “moja… mbili… tat..” kabla haja maliza tatu, mara ghafla mwanga mkali wa gari uka angaza eneo lile, likitokea mjini, na kumfanya jamaa huyu ageuke kulitazama gari lile, Frank akabonyea zaidi kukwepa mwanga, na kuelekeza macho kule alikokuwepo yule, jamaa ambae bila shaka, alikuwa analitarajia gari lile.


Maana yule jamaa alimaliza kukojoa na kukugeuka tena, kulitazama lile gari, ambalo lilikuwa limesha sogea na kupunguza mwendo, huku mwanga wagari lile dogo la kifahari, ukimuangazia usoni, kamanda huyu, alievalia koti kubwa jeusi la mvua, na kwa msaada wa mwanga huo ndipo Frank alipo pata nafasi ya kumtambua mtu huyu, utambuzi ambao ulimstua na kumshangaza bwana Frank, ambae alijikuta anatoa macho ya mshangao wa kutokuamini macho yake.


Huyu alikuwa ni Canal Erasto Kadumya, afisa mtoro wa jeshi, anae kiongoza kikundi cha wahasi wa UMD, ambacho sasa mamluki wake wanasakwa kwa udi na uvumba ndani ya serikali, sasa inakuwaje anamwona kati ya watu wanao msaka yeye, kwa tuhuma za uhaini, wakati kiongozi wa zoezi hili ndie muasi mkubwa sana, anae tafutwa usiku na mchana na jeshi la serikali, ambae sasa alikuwa analisogelea gari lililokuwa limesimama, na mlango wa upande wa dereva ukafunguliwa.


Ukweli ungeweza kusema kuwa, kumwona Erasto Kadumya, akishiriki operation hii ya kusaka wa saliti, kuwa ndio ulikuwa mshangao mkubwa sana, kwa bwana Frank, lakini hapana, sikuwa hivyo, ukweli ni kwamba, mshangao mkubwa ulikuwa ni pale, alipomwona mtu alieshuka toka garini, mtu mfupi kiasi, alie valia koti refu la mvua, kama la Bwana Kadumya, “mawazo yangu yalikuwa sawa, huyu mpuuzi anajaribu kuiangusha serikali” alinong’ona, Frank huku anawatazama wawili wale, walio salimia kwa salamu za kijeshi.


Huyu alikuwa ni Major Chitopelah, mkuu wa operation ya kuwasaka wahasi ndani ya serikali, yani amempumbaza mfalme, huku anaendelea kumpunguzia nguvu ya watu ambao wengemsaidia kuzuwia mapinduzi” alijisemea Frank, huku anaendelea kuwatazama wawili wale, “Erasto kumbuka uzembe hautakiwi kabisa, katika swala la Frank, maana ni mtu hatari sana” alisikika Chitopela, ambae kijeshi alikuwa na cheo kidogo kuliko Kadumya, lakini pale alionekana kuwa ndie mwenye madaraka makubwa zaidi ya Kadumya, “hakika afande, wala usiwe na wasi wasi, nitamnasa ndani ya usiku huu, na nitakuonyesha mwili wake” alisema Kadumya kwa kujiamini.


Baada ya maongezi mafupi, Frank aliwaona wawili wale wakimaliza maongezi yao, na bwana Dickson Chitopelah, akifungua tena mlango wa gari lake na kutoa bagi dogo, ambalo alimpatia Kadumya, “hii ni motisha kwa vijana, zidi kuwapa moyo kuwa, endapo tutafanikiwa kuichukuwa nchi, watakuwa na maisha mazuri sana” alisisitiza Chitopelah, kabla awajaagana na kila mmoja kuondoka na gari lake.


Hii ilimpatia picha pana sana bwana Frank, ambae aligundua kuwa uasi ulikuwa katika vitengo nyeti vya serikali, ikiwa na kiengo cha siri cha mawakala wa usalama wa taifa ili tajiri, linalo tawaliwa katika mfumo wa kifalme, na kwa haraka Frank alijuwa fika kuwa singweza kubadilisha hisia za king Eugen juu yake, na kumwaminisha kuwa Chopelah, alikuwa ndie muasi na msaliti.


Hapo ndipo bwana Frank alipochukuwa familia yake na kuitorosha kuelekea nje ya nchi, na njia aliyo itumia, ilikuwa ni njia ngumu sana, njia ambayo, katika hali ya kawaida, asinge kubali kuipitisha familia yake, maana ukiachilia, hatari ya kuwepo kwa waasi, pia msitu huu, ulikuwa unaongoza kwa wanyama hatarishi, kama vile simba, chui, na wegine wa jamii hiyo pasipo kusahau nyoka wakubwa, sana wakila aina, na wanyama wakubwa ambao siyo rafiki sana kwa binadamu, kama vile faru na tembo.


Mito mikubwa, ambayo ilikuwa inatiririsha maji kwa fujo, huku mvua na milipuko ya radi, ikiendelea kulindima, hakika iligopesha tochi zote zilisha zima, na sasa walitembea kwa kutegemea mwanga wa radi, sidhani kama kuna sehemu ambayo haikulowa katika miili yao, Deus na mama yake walikuwa wanatetemeka kwa baridi kali, kiasi cha meno kugongana, huku bwana Frank akifyeka vicha na magugu marefu, ndani ya madimbwi, ya maji, akitengeneza njia kwakutumia panga kali, mfano wa jambia, alilokuwa amelishika mkononi, mke wake akimfwaa nyuma, akiwa amembeba mtoto.


Ndani ya masaa matatu, tayari walisha vuka mpaka wa inua kisigino, wa kuelekea Tanzania, mpaka ambao, kila mtu huuchukulia kama mpaka mgumu sana kwa mtu kuupitia, kutokana na vikwanzo vya eneo hilo lenye milima na mabonde….…..#NYUMA_YA_MLANGO_WA_ADUI, inayo kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA KUMI NA SABA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA SITA: Ndani ya masaa matatu, tayari walisha vuka mpaka wa inua kisigino, wa kuelekea Tanzania, mpaka mbao, kila mtu huuchukulia kama mpaka mgumu sana kwa mtu kuupitia, kutokana na vikwanzo vya eneo hilo lenye milima na mabonde….ENDELEA….


Nakuingia upande wa Tanzania, wakipitia sehemu hiyo hatari, ya Makalio ya Semi, na kuanza kukabiriana na mbuga kubwa tambalale, sasa hatari ilikuwa kwao, ni kuhusu wanyama wakali na hatari kwa binadamu, ambao walikuwa wanaejaa katika mbuga ya wanyama ya selous, kwa usiku ule iliwapasa kuafuta pango moja salama, na kupumzika mpaka asubuhi, ambapo iliwapasa kutembea mchana ili waweze kukabiliana na hatari zanazowakabiri.


Safari ili tumia siku tatu, huku siku moja wakilala porini, na siku mbili kwenye vijiji, na siku ya tatu walijikuta katika kijiji kidogo cha Kilima sela, kilichopo mpaka mwa wilaya ya Seongea vijijini, (sasa Namtumbo) na wilaya ya Tunduru, kijiji ambacho kipindi hicho kilikuwa ni kidogo chenye idadi ya nyumba ishirini tu, na kijiji ambacho umbali wake toka vijiji vingine, vinavyo pakana navyo, kama mchomoro na Namwinyu, ni umbali mrefu sana, yapata kilomita kati ya ishirini mpaka thelasini, vikitenganishwa na misitu minene yenye wanyama wakali na hatari.


Ilikuwa ni sehemu nzuri sana kwa bwana Nyati kujificha na familia yake, lakini ugumu ukaja kwenye aina ya maisha ambayo wangeishi, maana ukiachilia kuwa asingekuwa na fedha yoyote ya kutumia, sababu asingeweza kuchenji fedha zake za #mbogo_land, au kuuza dhahabu zake alizokuwa nazo, kutokana na sehemu hiyo kukosa huduma hizo, kikubwa ni kwamba, licha ya kuhitaji kuishi kwa kificho, lakini alihitaji familia yake ipate huduma zote muhimu, na maisha mazuri.


Hivyo basi, pale kijijini alikaa kwa siku tatu, akihifadhiwa kwenye nyumba ya mwenyekiti wa kijiji kile kidogo, akapata usafiri wa gari kubwa la mizigo, lililo kuwa linaelekea songea mjini, ambako kuna sehemu alisha ilenga kwenda kufikia, maana licha ya kuwa raia wa #mbogo_land, lakini alikuwa anayafahamu vizuri maeneo ya Tanzania, ikiwemo mkoa huu wa Ruvuma.******


Yap! safari yao ilichukuwa siku mbili, ni kutokana na ubovu wa barabara, (kipindi hicho ni barabara ya vumbi) maana ilikuwa imechafuka kwa tope, lililolazimisha gari kukwama mara kwa mara, siku ya tatu mida ya saa nne za asubuhi, waliingia songea na bwana Frank akaenda kwenye ofisi za poster kwaajili ya kubadiri fedha alizokuwa nazo, toka kwenye ML Sh kuja kwenye Tsh, alipofanikiwa, alienda kulipia hotel na kupata sehemu ya kuoga kula na kupumzika.


Frank alikaa hotelini kwa muda wa week nzima, huku akifanya mpango wa kununua eneo maeneo ya Making’nda, kando kando ya mto lipupuma, na kutengeneza kibanda kidogo, cha tofari za kuchoma, ambacho alifanikiwa kuweka vitu muhimu, na kuhamia hapo, pamoja na familia yake, kisha kuendeleza ujenzi wa nyumba kubwa, lakini siyo ya kisasa wala ya kifahari, pamoja na kujishugurisha na kilimo, japo hakikuwa muhimu kwake, sababu alikuwa na akiba ya fedha na mali ambayo angeweza kuitumia kuishi maisha ya kifahari, kuwa na nyumba nziri eneo la mjini, na kununua gari zuri aina ya voxwagon, (taxi kobe) wakati huo ni moja kati ya magari mazuri.*******


Naam siku zilienda, miaka ikakatika, mara chache bwana Frank alifanya safari za siri kwenda #mbogo_land, ambako alichunguza maendelea ya kundi hatari la UMD lililoamini kwa Uhuru kwa Mapinduzi ya Damu, japo wananchi wote wa nchi hiyo ya Mbogo Land walishangaa sela za kundi hilo, na kulichukulia kama janga jipya kwa taifa lao.


Bahati nzuri miaka mitatu baadae, tetesi na za uwepo kwa kundi hilo, na usaliti ndani ya #Mbogo_land ulianza kutoweka Taratibu, huku bwana Chitopelah akipewa sifa za kuwa, yeye ndie aliefanikiwa kutokomeza kundi la UMD ambalo lilichukuliwa kama kundi hatarishi kwa usalama wa taifa, sifa ambazo zilienda sambamba medali mbali mbali, zikiwepo utumishi uliotukuka, nidhamu na utii katika utumishi, ushujaa na kujitolea kaika taifa, na tuzo ya uzalendo, huku akipandishwa vyeo mfululizo, yani ndani ya miaka mitatu, alisha pandishwa vyeo mara tatu, toka major mpaka brigadie general, cheo ambacho kilitosha kumkabidhi madaraka aliyokuwa nayo, yani mkuu wa kitengo cha mawakala wa siri wa usalama wa taifa hilo.


Lakini licha ya hayo yote kufanyika, lakini bado taifa liliendelea kuwa hesabu wote waliokimbia nchi kuwa ni waasi, yaani kuanzia Canal Kadumya, mfanyabiashara mkubwa na tajiri James Carvin, pia askari Canal Frank Nyati, huku ikitolewa amri kuwa, siku watakapo ingia nchini humo wakamatwe na kufikishwa mahakamani, kujibu kesi ya uhaini.


Katika hali ya kawaida kila mmoja alidhania kuwa swala hilo limeisha, na kwamba waasi wameshaamua kuondoka nchini Mbogo Land, hivyo ndivyo hata bwana Frank alivyo hisi, na kuamua kuachana na habari za mbogo land, na kuanza kuishi maisha yake akiwa kama raia wa kawaida ndani ya nchi ya Tanzania, huku akizidi kuboresha maisha yake, ikiwa pamoja na kuweka vizuri nyumba yake, pamoja na kununua gari aina ya land rover 109, ambalo alilitumia kwa safari zake za hapa na pale, huku akijipatia silaha kadhaa kwaajili ya kujilinda mwenyewe, akimini kuwa endapo Chitopela, atagundua sehemu aliyopo, anaweza kumfwata na kumwangamiza, hivyo nilazima ajilinde yeye na amfundishe mwanae namna ya kujilinda yeye mwenyewe.


Lakini licha ya kuamua kusahau kila kitu, lakini alitumia muda mwingi, kumwandaa mtoto wake Deus, kielimu na ujuzi mbali mbali, ambazo mwanadamu wakisasa anapaswa kuupata, pamoja na jinsi ya kujilinda mwenyewe ambapo mpaka anafikia kidato cha nne, tayari kijana Deus aliekuwa na miaka kumi na nane, alikuwa na uwezi wa kufanya mambo mengi sana, na licha ya hivyo alikuwa mtu hatari sana, japo hakutumia uwezo wake vibaya,


Ukiachilia uwezo wa kuendesha gari kwa ufundi wa hali ya juu, na kurekebisha matatizo madogo madogo ya gari, pia alikuwa na uwezo wa kutumia computer, pia alikuwa na uwezo mkubwa wa kujilinda na kushambulia kwa mikono mitupu, katika kiwango cha hali ya juu sana, huku akiwa na uwezo wa kutumia silaha za aina nyingi sana, alizofundishwa kwa siri na baba yake namna ya kuzitumia.


Deus ambae matokeo yake ya kidato cha nne haya kuwa mazuri, nyota yake inaanza kung’aa mwaka 2010, mwezi wa nne, msimu wa sikukuu za pasaka, Deus akiwa na miaka 20, alikuwa anasafiri kuelekea Dar es salaam, alikotumwa na baba yake, kwenda kufwata gari jipya, walilo linunua.


Safari ilianzia songea na alipofika njombe, akaona dalili za uwepo wa usafiri ambao siku zote amekuwa akiutamani siku nyingi, usafiri wa gari moshi, ambao amekuwa akiusikia tu! na alisha jaribu kuuvizia mara kwa mara, bila mafanikio, lakini leo alipoona kuna watu kadhaa kwenye ofisi za TAZARA, akaona siyo mbaya endapo atashuka toka kwenye bus la abiria, na kwenda kuulizia, “yes leo kuna trean saa kumi na moja jioni, linatoka zambia, ila ni express first class” alisema mhusika wa pale Tazara, “afadhari maana nilikuwa natamani sana kupanda trean” alisema Deus, alie beba begi lake mgongoni, kwa sauti iliyojawa na furaha, “ok! bei gani mpaka dar?” aliuliza Deus, huku anatoa begi lake toka mgongoni, na kufungua zip ndogo ya pembeni “elfu ishilini behewa la kwanza, la pili elfu kumi na tano, na la tatu elfu kumi, sijuwi unaitaji lipi?” aliuliza yule mtu, wa pale mapokezi, “nipatie ya pili” alisema Deus, huku anatoa noti mbili za elfu kumi kumi, na kumpatia yule jamaa, ambae alipokea na kuandika andika, kwenye kitabu cha tiketi, “trean inapita saa kumi na moja” alisema yule jamaa, huku anampatia tiketi yake kijana Deus.


Ukweli ilikuwa ni furaha kubwa kwake, alitembea kwa furaha, akiondoka eneo lile ili akatafute sehemu ambayo angeweza kukaa mpaka mida hiyo ya saa kumi na moja, na wakati anaendelea kutembea mara akasikia, sauti ya kike, toka nyuma yake, “kaka umepata tiket kwa shilingi ngapi?” Deus akuijali sauti ile, maana alidhania kuwa mtu huyo hakuwa anaongea na yeye, sababu mahali pale, kulikuwa na watu wengine, ndio kwanza alikuwa anatoa simu yake, ili aweze kumjulisha baba yake juu ya kutimiza ndoto yake ya kupanda gari moshi.


Lakini kabla hajapiga simu, akashtuka anashikwa bega, “anko samahani nilikuwa nauliza umepata tikeyi kwa shilingi ngapi” ilikuwa sauti ile ile ya kike, aliyo isikia mwanzo, Deus akageuka na kumtazama mtu mwenye sauti nzuri, aliemsemesha.


Nikweli alikuwamschana, tena mschana mdogo, mwenye sura na umbo zuri sana, wa kati ya umri wa miaka 14 au kumi na tano, alie valia nguo nzuri za kike, mwenye kuburuza begi kubwa kwa mkono wake wa kulia, huku mkono wa kushoto akiwa ameshikilia tiketi, “mimi nimechukuwa daraja la pili elfu kumi na tano” alijibu Deus huku anamtazama mschana huyu mdogo, ambae pia alikuwa anamtazama usoni, pasipo kukwepesha macho, “hooo nisawa, mimi nimechukuwa daraja la kwanza, nilizania wameniibia” alisema yule mschana ambae kwa kumtazama tu, ungejuwa ni mtoto kutoka familia bora, ambae sasa alikuwa anahifadhi tiketi yake, kwenye mkoba wake mdogo mzuri wa gharama kubwa, alio uweka kwapani.


Baada ya hapo Deus akaendelea kubofya simu yake huku anatembea kuelekea barabarani, kupanda gari la kuelekea mjini makambako, ambako angekaa mpaka jioni, mida ya trean kupita, “samahani anko nisubiri na mimi naenda mjini” alisema yule mschana mdogo, huku anamfwata Deus, akiwa anakokota begi lake kubwa, kuliko hata yeye mwenyewe.


Hapo Deus akasimama na kumtazama yule mschana mdogo lakini mrembo, “mimi naenda Makambako mjini, sasa utabeba begi mpaka huko?” aliuliza Deus, huku anamtazama mschana huyo mdogo, ambae alitazama begi lake, kisha akamtazama Deus, “kwahiyo niliache hapa?” aliuliza kwa sauti yake ya kischana, “ndiyo unaweza kuwaachia watu wa pale mapokezi, ukalikuta baaadae” alijibu Deus, na hapo mschana yule akalitazama tena begi lake, kisha aka tazama kwenye jengo la mapokezi, ambako palikuwa na watu wachache wanakata waliokuwa wanaendelea kukata tiketi zao, kisha akamtazama Deus Frank, ambae alikuwa anamtazama mschana huyu, na kuisoma akili yake, kwamba anahisi yeye ataondoka zake na kumwacha, “nisawa wacha niliache hapa, lakini naomba unisubiri” alisema yule mschana kwa sauti ya kuomba na kubembeleza.


Hapo Deus akatabasamu kidogo, “kwanini nilazima uongozane na mimi, inamaana upo peke yako?” aliuliza Deus huku anamsogelea yule mschana, ambae alikuwa anatabasamu kwa aibu kidogo, “ndiyo nipo peke yangu natokea shule huko Kifanya, na ni mara yangu yakwanza kusafiri na tren” alijibu yule mschana, huku anamtazama Deus, ambae sasa alilinyakuwa begi la mschana yule na kuliweka begani, “kwanini usinge panda bus, mbona elfu ishilini inatosha kufika dar?” aliuliza Deus, akianza kutembea kueleka mapokezi, na begi begani, huku yule mschana mdogo akifwata nyuma, “nimetamani tu kusafiri na tren” alijibu yule mschana, na kumfanya Deus acheke kidogo, maana akili zao ziliendana.


Naam utaratibu wa kuifadhi begi ulichukuwa muda mfupi sana, kisha wakatoka nakuelekea barabarani, ambako walipanda bus dogo litokalo nyororo, kuelekea makambako mjini, huku muda wote mschana mdogo akiwa karibu kabisa na Deus, ungesema ni mtu na mdogo wake, au ni watu wanao fahamiana kwa siku nyingi sana, ilifikia wakati Deus aliona kuwa bahati yake mbaya, “angekuwa mkubwa kidogo, leo ninge jilia kitu mpaka nichoke” nadhani mawazo hayo angeyapata mwanaume yoyote, ambae angeng’ang'aniwa na na mschana huyu mdogo…..kujuwa kilichotokea kwenye hii safari endelea kufwatilia mkasa huu wa.…..#NYUMA_YA_MLANGO_WA_ADUI, inayo kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA KUMI NA NANE
MTUNZI : Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA SABA: Naam utaratibu wa kuifadhi begi ulichukuwa muda mfupi sana, kisha wakatoka nakuelekea barabarani, ambako walipanda bus dogo litokalo nyororo, kuelekea makambako mjini, huku muda wote mschana mdogo akiwa karibu kabisa na Deus, ungesema ni mtu na mdogo wake, au ni watu wanao fahamiana kwa siku nyingi sana, ilifikia wakati Deus aliona kuwa bahati yake mbaya, “angekuwa mkubwa kidogo, leo ninge jilia kitu mpaka nichoke” nadhani mawazo hayo angeyapata mwanaume yoyote, ambae angeng’ang'aniwa na na mschana huyu mdogo….


Yap mida ya saa sita mchana, iliwakua makambako mjini, ambako walitafuta sehemu nzuri ya chakula, na kukaa hapo wakiagiza vinywaji na vyakula, ambapo tofauti na vile alivyo dhania Deus, kwamba gharama za binti huyu zitakuwa zake, lakini ndio kwanza, wakawa wanagombaniana kulipia, hakika mschana yule, alionekana kuwa na malezi tofauti kabisa, na watoto wengi, hakupenda kuwa tegemezi, wala kuhudumiwa kama waschana wengi wanavyopenda, hasa wanavyopata mtu mwema kama huyu, wakati huo wingu lilionekana kutanda angani, ikiashilia kuwa kuna baadhi ya sehemu mvua zilikuwa zinaendela kunyesha.


Walitumia muda mwingi kula, huku wakiongea hili na lile, na kufahamiana majina, ambapo Deus alifahamu kuwa mschana huyu mdogo anaitwa Caroline, alikuwa anasoma kidato cha kwanza shule ya sekondari ya Kifanya, ya wanawake, inayo milikiwa na taasisi moja ya kidini, na pasipo kutambulisha uwezo wa familia yake, lakini aliweza kuona wazi kuwa binti huyu mdogo alikuwa anatokea kwenye familia tajiri, maana ukiachilia matumizi yake kwenye upande wa fedha, pia alikuwa anamiliki simu nzuri ya kisasa, yenye kutumikisha internet (smart phone, wakati huo waliokuwa nazo ni wachache, kweli kweli, lakini mschana huyu, alionekana akiwasiliana mara kwa mara na mama yake, “ndiyo mama nipo na kaka Deus, siwezi kuachwa na tren….. anakuja dar, nimekutana nae hapa njombe…. wala usiwe na wasi wasi, nitakupigia uje unipokee TAZARA” aliongea kwa kujiamini maschana Caroline, “Caroline, kwanini umenizowea kwa haraka hivyo, huogopi kama nikiwa mtu mbaya kwako?” aliuliza Deus, huku akiishangaa tabia ya Caroline kumdaka juu kwa juu, na kujenga nae mazowea.


Swali lile halikumshtua Calorine, ambae ninapo zungumzia kuwa ni mschana mzuri, ni mzuri kweli, “nimekuona tu, nikajuwa wewe siyo mtu mbaya” alijibu Caroline, huku anatabasamu, Deus alimtazama Carlo kwa sekunde kadhaa, hata Carlo alipomtazama Deus macho yao yakagongana na wote wakatabasamuliana, “hivi Carlo, nyumbani kwenu, kuna ndugu zako wengine au umezaliwa peke yako?” aliuliza Deus, ambae muda wote uongea taratibu na kwa upole, hata macho yake hutazama kwa upole na kuisadifu sura yake ionekane tulivu ya upole, wakati huu mvua ilikuwa inanyesha pale Makambako.


Swali la Deus lilimfanya Caroline acheke kidogo, “ndiyo mimi ni mtoto wa pili, kuna mdogo wangu yupo darasa la nne, na dada yangu yupo chuo mwaka wakwanza, watu wanasema na mimi nikiwa mkubwa nitakuwa mzuri kama yeye” alisema Caroline, na wote wakacheka, “vipi kuhusu wewe, una mdogo wako wakiume” aliuliza Caroline, kwa sauti ambayo ungesema ni utani, “nipo mwenyewe, nilizaliwa peke yangu” alijibu Deus, huku akicheka kidogo.*****


Naam maongezi yaliendelea mpaka saa kumi, za jioni, waliponunua baadhi ya vyakula kwaajili ya safari, na kuelekea TAZARA ya Makambako, tayari kwaajili ya safari, mida hii mvua ilikuwa imesimama, lakini bado wingu lilikuwa zito angani.


Lakini wawili hawa walipofika pale stesheni, hawakukuta kama walivyotegemea, yaani walidhania wangekuta mkusanyiko wawatu waliokuwa wanasubiri tren, baada yake walikuta peupe, zaidi ni wafanyakazi wawili watatu, waliokuwa wanapakiza mizigo kwenye behewa la tren moja la kizamani, la kubabea mizigo, lilo onyesha lilitarajia kufanya safari muda mfupi ujao, “tutakuwa tumeachwa au?” aliuliza Deus, huku anatazama saa ya kwene simu yake ya kitochi, kama ambavyo ungeweza kuiita kwa sasa, “saa kumi na nusu, muda bado kabisa” alisema Caroline, ambae pia alikuwa anatazama muda kwenye simu.


Kitu ambacho Deus hawezi ni kuandikia mate, kungali na wino upo , hivyo akaenda moja kwa moja mapokezi, na kuuliza kama bado wapo ndani ya muda, “hoooo tulikuwa tuna watafuta sana, bahati mbaya hatukuchukuwa namba zenu za simu, kutokana na hali ya hewa express imekwama njiani, hivyo leo hakuna usafiri” alisema yule mkata tiket huku anatoa fedha na kuwapatia wakina Deus kila mmoja kutokana na alivyokata, “kwahiyo hakuna tren jingine, maana sasa hivi hatuwezi kupata bus la kwenda dar, nilazima tulale?” aliuliza Deus, ambae alidhania kuwa leo ndiyo siku yake ya kufurahia usafiri wa gari moshi.


Yule jamaa wa mapokezi alionyesha kuwa muelewa kidogo, maana aliinamisha kichwa kidogo na alipoinua uso wake, akatazama kule ambako kulikuwa na wale wafanyakazi wanapakiza mizigo kwenye tren “ngoja kwanza niwaombee lift kwenye hiyo hapo, japo siyo ya abiria, ina sehemu chache za kukaa watu” alisema yule jamaa, ambae juhudu zake zilizaa matunda na wawili hawa wakapata nafasi, na kuingia ndani ya tren hii,ambayo ilikuwa na behewa kumi na tano, moja tu, likiwa kwaajili ya kukaa wafanyakazi, mengine kumi na nne yalikuwa yamesheheni mzigo wa mbao.


Saa mbili kasoro za usiku, safari ilianza kueleka dar es salaam, Deus na mtoto Caroline, wakiwa ndani ya behewa la kwanza toka kwenye kichwa cha gari moshi, safari hii wakiwa hawajalipa hata shilingi moja, kwaajili ya usafiri, angalau walipata sehemu nzuri za kukaa, ambazo wangeweza hata kulala pale ambapo wange hitaji kufanya hivyo, bahati nzuri kwao walikuwa wamebeba chakula, japo hawakuwa na uhakika kama kita wasaidia mpaka kesho usiku watakapo ingia dar es salaam, cha kufurahisha ni kwamba Deus kijana mwenye miaka ishirini, na mschana Caroline mwenye miaka kumi na nne, walikuwa wakiongea kwa furaha, na kucheka kwa pamoja, kitu ambacho kilifanya safari yao ianze vizuri, huku kila mmoja akiwataarifu wazazi wake, juu ya usafiri huu mpya, ambao kwa upande wa Deus baba yake aliipokea kawaida tu, yani hakuwa na wasi wasi na kijana wake, ambae siyo tu uelewa wa vitu vingi, pia alikuwa tayari kukabiriana kwa lolote wakati wowote.


Tofauti ilikuwa kwa upande wa Caroline, ambae mama yake alimlaumu sana kwa kitendo cha kuamua kupanda tren ya mizigo, “ilitakiwa upande bus baada ya kuona umeikosa hiyo tren, huoni hali ya hewa ilivyochafuka, mvua inanyesha kila kona” alalamika mama yake Caroline, “usihofu mama nitafika salama, hata hivyo sipo peke yangu nipo na kaka Deus…” alisema Caroline, jambo ambalo niwazi alikumpendeza mama yake, “yani mtu umekutana nae leo, una mwamini vipi, hivi Carlo unajuwa kuwa baba yako amesafiri? ukipata tatizo ni tamwambia nini akirudi?” aling’aka mama Caroline, ambae ukiachilia kutopendezewa na kitendo kile cha binti yake kupanda tren ya mizigo, pia alipiga mara kwa mara kuulizia walikofikia na kama binti yake huyo yupo salama, hata walipofika sehemu ambazo hazikuwa na network, nikama ilikuwa afadhari kwa mschana huyo,


Saa sita za usiku Caroline alipitiwa na usingizi, Deus alihakikisha anakaa macho kumtazama mschana huyu akilala vizuri juu ya seat nyembamba, pasipo kuanguka, hata kulipokucha asubuhi, na mschana huyu kuamka ndipo Deus alipopata nafasi ya kupumzika kidogo, japo ilikuwa I kwa taabu sana, maana kila mara Caroline alimsemesha, na kumtoa kwenye usingizi.


Naam mida ya saa tisa jioni siku ya pili, wakiwa wanakatiza maeneo ya morogoro, huku mvua ikiwa ikiwa inaendela kunyesha, ndipo kwa mbali sana, dereva wa tren alipo pokea mawasiliano ya kwenye tren, kwa njia ya redio call, yakimjulisha kuwa, huko mbele sehemu ya daraja, njia ya tren imesombwa na maji, na kiukweli walikuwa wamebakiza hatua chache sana kufikia sehemu hiyo… .…..#NYUMA_YA_MLANGO_WA_ADUI, inayo kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA KUMI NA NANE
MTUNZI : Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA SABA: Naam utaratibu wa kuifadhi begi ulichukuwa muda mfupi sana, kisha wakatoka nakuelekea barabarani, ambako walipanda bus dogo litokalo nyororo, kuelekea makambako mjini, huku muda wote mschana mdogo akiwa karibu kabisa na Deus, ungesema ni mtu na mdogo wake, au ni watu wanao fahamiana kwa siku nyingi sana, ilifikia wakati Deus aliona kuwa bahati yake mbaya, “angekuwa mkubwa kidogo, leo ninge jilia kitu mpaka nichoke” nadhani mawazo hayo angeyapata mwanaume yoyote, ambae angeng’ang'aniwa na na mschana huyu mdogo….


Yap mida ya saa sita mchana, iliwakua makambako mjini, ambako walitafuta sehemu nzuri ya chakula, na kukaa hapo wakiagiza vinywaji na vyakula, ambapo tofauti na vile alivyo dhania Deus, kwamba gharama za binti huyu zitakuwa zake, lakini ndio kwanza, wakawa wanagombaniana kulipia, hakika mschana yule, alionekana kuwa na malezi tofauti kabisa, na watoto wengi, hakupenda kuwa tegemezi, wala kuhudumiwa kama waschana wengi wanavyopenda, hasa wanavyopata mtu mwema kama huyu, wakati huo wingu lilionekana kutanda angani, ikiashilia kuwa kuna baadhi ya sehemu mvua zilikuwa zinaendela kunyesha.


Walitumia muda mwingi kula, huku wakiongea hili na lile, na kufahamiana majina, ambapo Deus alifahamu kuwa mschana huyu mdogo anaitwa Caroline, alikuwa anasoma kidato cha kwanza shule ya sekondari ya Kifanya, ya wanawake, inayo milikiwa na taasisi moja ya kidini, na pasipo kutambulisha uwezo wa familia yake, lakini aliweza kuona wazi kuwa binti huyu mdogo alikuwa anatokea kwenye familia tajiri, maana ukiachilia matumizi yake kwenye upande wa fedha, pia alikuwa anamiliki simu nzuri ya kisasa, yenye kutumikisha internet (smart phone, wakati huo waliokuwa nazo ni wachache, kweli kweli, lakini mschana huyu, alionekana akiwasiliana mara kwa mara na mama yake, “ndiyo mama nipo na kaka Deus, siwezi kuachwa na tren….. anakuja dar, nimekutana nae hapa njombe…. wala usiwe na wasi wasi, nitakupigia uje unipokee TAZARA” aliongea kwa kujiamini maschana Caroline, “Caroline, kwanini umenizowea kwa haraka hivyo, huogopi kama nikiwa mtu mbaya kwako?” aliuliza Deus, huku akiishangaa tabia ya Caroline kumdaka juu kwa juu, na kujenga nae mazowea.


Swali lile halikumshtua Calorine, ambae ninapo zungumzia kuwa ni mschana mzuri, ni mzuri kweli, “nimekuona tu, nikajuwa wewe siyo mtu mbaya” alijibu Caroline, huku anatabasamu, Deus alimtazama Carlo kwa sekunde kadhaa, hata Carlo alipomtazama Deus macho yao yakagongana na wote wakatabasamuliana, “hivi Carlo, nyumbani kwenu, kuna ndugu zako wengine au umezaliwa peke yako?” aliuliza Deus, ambae muda wote uongea taratibu na kwa upole, hata macho yake hutazama kwa upole na kuisadifu sura yake ionekane tulivu ya upole, wakati huu mvua ilikuwa inanyesha pale Makambako.


Swali la Deus lilimfanya Caroline acheke kidogo, “ndiyo mimi ni mtoto wa pili, kuna mdogo wangu yupo darasa la nne, na dada yangu yupo chuo mwaka wakwanza, watu wanasema na mimi nikiwa mkubwa nitakuwa mzuri kama yeye” alisema Caroline, na wote wakacheka, “vipi kuhusu wewe, una mdogo wako wakiume” aliuliza Caroline, kwa sauti ambayo ungesema ni utani, “nipo mwenyewe, nilizaliwa peke yangu” alijibu Deus, huku akicheka kidogo.*****


Naam maongezi yaliendelea mpaka saa kumi, za jioni, waliponunua baadhi ya vyakula kwaajili ya safari, na kuelekea TAZARA ya Makambako, tayari kwaajili ya safari, mida hii mvua ilikuwa imesimama, lakini bado wingu lilikuwa zito angani.


Lakini wawili hawa walipofika pale stesheni, hawakukuta kama walivyotegemea, yaani walidhania wangekuta mkusanyiko wawatu waliokuwa wanasubiri tren, baada yake walikuta peupe, zaidi ni wafanyakazi wawili watatu, waliokuwa wanapakiza mizigo kwenye behewa la tren moja la kizamani, la kubabea mizigo, lilo onyesha lilitarajia kufanya safari muda mfupi ujao, “tutakuwa tumeachwa au?” aliuliza Deus, huku anatazama saa ya kwene simu yake ya kitochi, kama ambavyo ungeweza kuiita kwa sasa, “saa kumi na nusu, muda bado kabisa” alisema Caroline, ambae pia alikuwa anatazama muda kwenye simu.


Kitu ambacho Deus hawezi ni kuandikia mate, kungali na wino upo , hivyo akaenda moja kwa moja mapokezi, na kuuliza kama bado wapo ndani ya muda, “hoooo tulikuwa tuna watafuta sana, bahati mbaya hatukuchukuwa namba zenu za simu, kutokana na hali ya hewa express imekwama njiani, hivyo leo hakuna usafiri” alisema yule mkata tiket huku anatoa fedha na kuwapatia wakina Deus kila mmoja kutokana na alivyokata, “kwahiyo hakuna tren jingine, maana sasa hivi hatuwezi kupata bus la kwenda dar, nilazima tulale?” aliuliza Deus, ambae alidhania kuwa leo ndiyo siku yake ya kufurahia usafiri wa gari moshi.


Yule jamaa wa mapokezi alionyesha kuwa muelewa kidogo, maana aliinamisha kichwa kidogo na alipoinua uso wake, akatazama kule ambako kulikuwa na wale wafanyakazi wanapakiza mizigo kwenye tren “ngoja kwanza niwaombee lift kwenye hiyo hapo, japo siyo ya abiria, ina sehemu chache za kukaa watu” alisema yule jamaa, ambae juhudu zake zilizaa matunda na wawili hawa wakapata nafasi, na kuingia ndani ya tren hii,ambayo ilikuwa na behewa kumi na tano, moja tu, likiwa kwaajili ya kukaa wafanyakazi, mengine kumi na nne yalikuwa yamesheheni mzigo wa mbao.


Saa mbili kasoro za usiku, safari ilianza kueleka dar es salaam, Deus na mtoto Caroline, wakiwa ndani ya behewa la kwanza toka kwenye kichwa cha gari moshi, safari hii wakiwa hawajalipa hata shilingi moja, kwaajili ya usafiri, angalau walipata sehemu nzuri za kukaa, ambazo wangeweza hata kulala pale ambapo wange hitaji kufanya hivyo, bahati nzuri kwao walikuwa wamebeba chakula, japo hawakuwa na uhakika kama kita wasaidia mpaka kesho usiku watakapo ingia dar es salaam, cha kufurahisha ni kwamba Deus kijana mwenye miaka ishirini, na mschana Caroline mwenye miaka kumi na nne, walikuwa wakiongea kwa furaha, na kucheka kwa pamoja, kitu ambacho kilifanya safari yao ianze vizuri, huku kila mmoja akiwataarifu wazazi wake, juu ya usafiri huu mpya, ambao kwa upande wa Deus baba yake aliipokea kawaida tu, yani hakuwa na wasi wasi na kijana wake, ambae siyo tu uelewa wa vitu vingi, pia alikuwa tayari kukabiriana kwa lolote wakati wowote.


Tofauti ilikuwa kwa upande wa Caroline, ambae mama yake alimlaumu sana kwa kitendo cha kuamua kupanda tren ya mizigo, “ilitakiwa upande bus baada ya kuona umeikosa hiyo tren, huoni hali ya hewa ilivyochafuka, mvua inanyesha kila kona” alalamika mama yake Caroline, “usihofu mama nitafika salama, hata hivyo sipo peke yangu nipo na kaka Deus…” alisema Caroline, jambo ambalo niwazi alikumpendeza mama yake, “yani mtu umekutana nae leo, una mwamini vipi, hivi Carlo unajuwa kuwa baba yako amesafiri? ukipata tatizo ni tamwambia nini akirudi?” aling’aka mama Caroline, ambae ukiachilia kutopendezewa na kitendo kile cha binti yake kupanda tren ya mizigo, pia alipiga mara kwa mara kuulizia walikofikia na kama binti yake huyo yupo salama, hata walipofika sehemu ambazo hazikuwa na network, nikama ilikuwa afadhari kwa mschana huyo,


Saa sita za usiku Caroline alipitiwa na usingizi, Deus alihakikisha anakaa macho kumtazama mschana huyu akilala vizuri juu ya seat nyembamba, pasipo kuanguka, hata kulipokucha asubuhi, na mschana huyu kuamka ndipo Deus alipopata nafasi ya kupumzika kidogo, japo ilikuwa I kwa taabu sana, maana kila mara Caroline alimsemesha, na kumtoa kwenye usingizi.


Naam mida ya saa tisa jioni siku ya pili, wakiwa wanakatiza maeneo ya morogoro, huku mvua ikiwa ikiwa inaendela kunyesha, ndipo kwa mbali sana, dereva wa tren alipo pokea mawasiliano ya kwenye tren, kwa njia ya redio call, yakimjulisha kuwa, huko mbele sehemu ya daraja, njia ya tren imesombwa na maji, na kiukweli walikuwa wamebakiza hatua chache sana kufikia sehemu hiyo… .…..#NYUMA_YA_MLANGO_WA_ADUI, inayo kujia hapa hapa jamii forums
Nyota iling'aaje sasa
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA KUMI NA TISA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA NANE: Naam mida ya saa tisa jioni siku ya pili, wakiwa wanakatiza maeneo ya morogoro, huku mvua ikiwa inaendela kunyesha, ndipo kwa mbali sana, dereva wa tren alipo pokea mawasiliano ya kwenye tren, kwa njia ya redio call, yakimjulisha kuwa, huko mbele sehemu ya daraja, njia ya tren imesombwa na maji, na kiukweli walikuwa wamebakiza hatua chache sana kufikia sehemu hiyo…ENDELEA…..
Ambayo inafahamika kwa jina la Mbingu, “jamani kuweni tayari mbele kuna daraja limebebwa na maji” alipiga kelele aliekuwa anendesha gari moshi, huku akivuta brake kwanguvu, na kufanya vyuma vianze kusagana, huku Tren ikisota kwa nguvu kuelekea mbele, pasipo kupunguza mwendo, “njoo unisaidie kuvuta brake, alipiga kelele yule dereva wa tren, akimwambia mwenzie amsaidie, nae akaenda haraka na wote kwa pamoja wakajiweka sawa na kuanza kuvuta tena zile chuma za brake, ambazo zilikuwa mbili, “aya moja, mbili tatu” alihesabu yule dereva, na wote kwa pamoja wakazivuta vile vyuma, kwa nguvu zao zote.


Naam kwa bahati mbaya chuma kimoja kikakatika, na huku tren ikiendelea kushika kasi ya ajabu, maana sasa haikuwa na brake yoyote, “mugu wangu tunakufa huku tuna jiona” alisema yule mwingine, huku akichungulia nje ya tren, ambako sasa palionekana jinsi miti mawe na mataruma wima yalivyo kuwa yana kimbia kurudi nyuma, ikionyesha wazi jinsi tren ilivyokuwa katika kasi ya ajabu.


Wakati hayo yanaendelea, mschana Caroline ambae tayari alikuwa ameshajuwa kinacho endelea, sasa alianza kukumbuka maneno ya mama yake, kwamba haikuwa vizuri kusafiri na tren kipindi hiki cha mvua, wakati anakumbuka hilo akamwona mmoja kati ya wafanyakazi wa ile tren akifungua mlango na kujirusha, kwa lengo la kujiokoa, nao wakitumia dirisha waliweza kumwona mtu huyo, anajipiga vibaya aridhini na kubiringika mara kadhaa, kabla ya kujibamiza tena kwenye jiwe bembezoni kabisa mwa mataruma mlalo yatumikayo kama barabara ya tren, wakashuhudia damu nyingi ikimwagika kichwani mwa mtu huyo ambae alitulia, hapo hapo akiwa amesha umaliza mwendo.


Hakika lilikuwa ni tukio la kugofya sana machoni pa Carlo, ambae alianza kuangua kilio cha kukata tamaa, “kaka Deus tunakufa leo” alisema Caroline, kwa sauti iliyojaa uoga na wasi wasi, sambamba na kilio cha kukata tamaa, “usiogope Carlo, omba mungu tutatoka salama” alisema Deus, kwa sauti tulivu, kama vile hakukuwa na kitu cha hatari kinatokea mbele yao.


Wakati wao wanaendelea kuwaza hayo na Tren ikiwa inakaribia kabisa, sehemu ambayo daraja lilikuwa limesombwa, watu wengine wawili wakajirusha, mmoja wao akiwa ni yule msaidizi wa dereva, nao hali ilikuwa ni kama ile ya yule wa mwanzo, japo hawa ilikuwa tofauti kidogo, mmoja alipoteza maisha, huku mwingune akivungika miguu yote miwili.
Hapo sasa tren ilikuwa imebakiwa na watau wanne tu, yani Deus Frank Caroline, na Dereva wa tren na fundi mmoja wa ile tren, wote wakajikusanya kwenye behewa la wafanyakazi, huku wakitazama kwa macho ya kukaa tamaa, kasoro Deus ambae aliwatazama mmoja baada ya mwingine, kama vile anapima hofu yao, “naomba muwe waulivu, hapa tuna toka mmoja baada ya mwingine” alisema Deus na wale wawili wakamtazama kwa macho ya kumpuuzia, huku wakiamini kila wanacho kifikiria, kuwa ni muda wa kutubu dhambi zao, na kujiandaa kwa maisha mapya ya ulemavu, wa kiungo chochoe cha mwili, labda Caroline peke yake ambae ndie alie onyesha kumwamini japo kidogo kijana huyu.


Kauli ya Deus haikuonyesha kuwatuliza wale jamaa ambao niwafanyakazi wa tren, hapo Deus akajuwa kuwa lazima kuna hitajika kazi ya ziada ili kuwanusuru hawa jamaa wengine, maana kuhusu Caroline, ambae kwa asilimia kubwa alikuwa anamtegemea yeye, kutoka kwenye tren,


Deus akamtazama yule dereva, ambae sasa alikuwa ana haha, kutafuta pakutokea, kama wenzake walivyofanya, kisha akamtazama Caroline, ambae alikuwa amesimama karibu yake kabisa, huku ana tweta kwa hofu, “tulia Carlo, utafanya kama nitakavyokuambia” alisema Deus huku ana mtazama Caroline ambae aliitikia kwa kichwa.


Sasa Deusi akawatazama tena wale wafanyakazi wa tren ambao umri wao ulikuwa mkubwa kuliko wa yeye Deus, sikieni wazee, hauwezi kubakia humu, na wala hatuwezi kutoka kama mnavyo fanya nyie, kama mnapenda kupona nisikilizeni” alisema Deus, kwa sauti ya ukali na ya juu kidogo, ambayo iliwafanya wale jamaa wamtazame Deus, japo bado walikuwa wamejawa na hofu kubwa, hasa baada ya kuona kilichowatokea wenzao waliojaribu kuruka, nje ya tren.******


Taarifa ya uharibifu mkubwa uliofanywa na mvua inayoendelea kunyesha, ilisambaa kwa haraka sana, huku tazara morogoro, wakitangaza kupotea kwa mawasiliano ya tren moja ya mizigo, iliyokuwa inasafiri toka makambako, kwenda dar es salaam.


Japo ilikuwa ni tren ya mizigo, lakini hofu kubwa ilitanda, baada ya kusikika kuwa kulikuwa na watu wapatao saba ndani ya tren, waliokuwa wanasafiri na tren hiyo ya mizigo.


Serikari ikawahakikishia wanachi kuwa inatuma vyombo vya ulinzi na usalama, kwenda kuitafuta tren hiyo, wakati TAZARA yenyewe inafanya juhudi ya kuwasiliana na vituo vyote, ili kuzuia tren nyingine zilizopo njiani.


Naam lisaa limoja baadae toka serikali itangaze, ikiwa ni lisaa la pili toka tren ipoteze mawasiliano, magari ya jeshi la ulinzi, na vikosi vya uokoaji vya zima moto, vilifika pale Mbingu, vikiwa vina ongozwa na Kanali Eric Mbelya. wakakuta mabehewa ya mbele ya tren yamezama kwenye mto, huku yale ya nyuma yakiwa yamefunika eneo lote la juu, huku mbao zikiwa zinaelea juu yamaji, na nyingine zikining’inia kwenye mahewa, yaliyo kuwa yamekaa kila moja kwa mkao wake, “ni ajali mbaya sana, kama ingekuwa ni ajali ya tren la abiria, na hata kwa wafanyakazi wa tren hii sidhani kama kuna alietoka salama” alisema Canal Mbelya, wakati akiwa anaongea na viongozi wasaidizi wake wawili wa jeshi la wanachi na mmoja wa jeshi la zimamoto, “ni hatari kubwa afande, sijuwi kwanini hawakupata taarifa mapema, juu ya ubovu wa barabara” alichangia mkuu wa zimamoto.


baada ya maongezi ya hapa na pale, Canal Mbelya akatoa majukumu, chamsingi askari watoe mbao kwenye maji, kisha watazame kama kuna miili itaonekana, wakati huo yafanyike mawasiliano na shirika la TAZARA walete winch lile lisaidie kuinua behewa na hizo mbao zitakazo bakia” aliagiza Canal, na wakati huo huo, akasikia kelele, “jamani tunaomba msaada wenzetu wame umeumia sana wanahitaji kufikishwa hospital haraka” wote waligeuka na kutazama kule ilikotokea kelele huyo.


Ulikuwa ni upande wa kulia kama unatokea mjini, yani upande wa iringa, ambako waliweza kumwona kijana mmoja mdogo, lakini mwenye mwili wa kimazoezi, akiwa amembeba mtu mmoja mtu mzima, alie kuwa anavuja damu miguuni, yupo hoi kwa upotevu wa damu, huku nyuma yao wakifwatia watu watatu, wanaume wawili na mwanamke mmoja.


Hapo hapo askari kadhaa wa jeshi la ulinzi pamoja na zimamoto, wakaenda kumpokea mtu yule, na kumsogeza kwenye gari la wagonjwa, ambalo walikuwa wamekuja nalo, likiwa ni mali ya jeshi la ulinzi.


Inamaana nyie pia mlikuwa katika hii tren, aliuliza canal Eric Mbelya, “ndiyo sisi ni ma-crew wa hii tren na huyu kijana na huyu mschana, tuliwapa lift baada ya kukosa tren ya express, wengine wawili wapo huko nyuma wamekufa” alisema yule dereva wa tren, hapo kiongozi mmoja wa jeshi akatoa amri, askari wasambae kusaka miili ya watu huko njiani, pembezoni mwa barabara tren, huku yeye mwenyewe akiongoza, “likuwa wangapi ndani ya tren?” aliuliza Canal Mbelya, akimwuliza yule dereva, “tulikuwa saba, wamekufa wawili” alisema yule dereva ambae bado alikuwa katika hali ya taharuki, kama ilivyokuwa kwa wezake pamoja na mschana Caroline, ni kutokana na kilicho tokea, kasoro kijana Deus ambae alionekana kuwa kawaida tu.


Hapo kidogo Canal alionekana kupatwa na mshangao kidogo, “unasema mlikuwa saba, na hapa nimewaona watano, na umesema wawili wamekufa?” aliulizia Canal Eric, huku anamtazama yule dereva, “ndiyo hatukuwa na mtu mwingine zaidi yetu” alisema dereva, na hapo yule canal na wakubwa wenzake waliwatazama wale wakina Deus, kwa awamu na mwisho macho yao yaka gota kwa mschana mdogo wa miaka kumi na nne, ambae bado alionekana kuwa katika hali ya kuweweseka, kama wale wengine, “hebu subiri kwanza, nyie mlitokaje ndani ya tren?” aliuliza canal Mbelya, huku anawatazama mmoja baada ya mwingine, kuona nani atakae toa jibu.


lakini hakupata jibu, zaidi ya kuwaona wale wote watatu, wakimtazama kijana mdogo Deus, na wao wakamtazama, ‘eti dogo, mmetokaje ndani yah hii tren, tena mkwa hamja pata majeraha yoyote?” aliuliza yule mwanajeshi wa jeshi la ulinzi wenye cheo cha Canal, huku anamkazia macho Deus, ambae alikuwa tofauti na wale wengine, kwamaana akuonyesha dalili ya wasi wasi, wala taharuki ya ajari….… .…..#NYUMA_YA_MLANGO_WA_ADUI, inayo kujia hapa hapa, Jamii Forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA ISHIRINI
MTUNZI : Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA TISA: lakini hakupata jibu, zaidi ya kuwaona wale wote watatu, wakimtazama kijana mdogo Deus, na wao wakamtazama, ‘eti dogo, mmetokaje ndani ya hii tren, tena mkwa hamja pata majeraha yoyote?” aliuliza yule mwanajeshi wa jeshi la ulinzi wenye cheo cha Canal, huku anamkazia macho Deus, ambae alikuwa tofauti na wale wengine, kwamaana akuonyesha dalili ya wasi wasi, wala taharuki ya ajali….…endelea….


“tuliruka tu, hakuna cha zaidi tulichotumia” alijibu Deus Frank, ambae kama ungemkuta pale usingedhania kama alikuwepo ndani ya ile tren, labda kule kuchafuka kwake ndio ungegundua kuwa alikuwa mmoja wa walionusulika toka kwenye ajali.


Kwa jibu hilo yule Kanali alievalia sare za kijeshi zile za kivita, alimtazama yule kijana toka juu mpaka chini, halafu akatazama Caroline, kabla hajawatazama wale wengine watatu, na kisha akarudisha macho yake tena usoni kijana Deus, “lakini wewe siyo mfanyakazi ndani ya hii tren?” aliuliza yule Kanali, huku anamkazia macho Deus, ambae alitabasamu kidogo, huku anakwepesha macho yake ya upole, “ndiyo mzee huyo na huyu mschana ni abilia waliokosa express, tukawapa lift, ila yeye ndie alietusaidia kuruka toka kwenye Tren” alisema yule dereva wa Tren kwa msisitizo, wakati huo tayari wanajeshi walioenda kusaka miili ya watu walioruka kule nyuma, walikuwa wanarudi huku wamebeba watu wawili pamoja na begi kubwa la mschana Caroline, naamini tutafahamu kwanini waliliacha.


Hapo wanajeshi wote pamoja na wale wa jeshi la ukoaji, wakamtazama Deus kwa mshangao, “kwa hiyo walioumia na kufa hukuwapa maelekezo, au hawakufata maelekezo yako, “aliuliza yule Kanal ambae kwenye shati lake, juu ya mfuko wa kifuani, upande wa kushoto kulikuwa na neno Tanzania, na upande wa kulia kulikuwa na neno JP KASUBA, huku mabegani mwake kukionekana nyota mbili chini ya ngao ya taifa, wengi huiita bibi na bwana, kushoto na kulia, “waliruka mapema, kabla hatuja elezana chakufanya” alisema Deus, kwa sauti yake tulivu.


Wakati maongezi yanaendelea, mara akaja askari wa jeshi la ulinzi, huku akiwa amevalia groves za kitabibu mikononi mwake, ilionyesha wazi kuwa ni muuguzi, alipofika alipiga salut na yule Kanali Kasuba akaitikia kwa salut, “afande tupo tayari kuondoka, kumwaisha yule majeruhi, amevuja damu nyingi sana” alisema yule askari mwenye alama ya yota mbili mabegani mwake, “ok! sawa wachukuwe na hawa wanne, huyu bado nina maongezi nae” alisema Kanal, pasipo kupepesa macho, huku anamtazama kijana Deus, kwa macho kama ya kutaka kubaki pamoja nae, na hapo mschana Caroline pia akamtazama Deus, ambae pia alikuwa anamtazama kwa macho ya tabasamu, “usijali mdogo wangu, tutaonana tu” alisema Deus kwa sauti tulivu, “usijari binti tangulia tu, yeye anakuja, tuaongea mambo ya kikazi” alisisitiza Kanali, safari hii kama vile anamwondoa wasi wasi Caroline, ambae alikubali kuongozana na yule askari pamoja na wale wafanyakazi wa TAZARA, mpaka kwenye gari la wagonjwa, ambako alilikuta begi lake.


Kanali Kasuba pamoja na askari wengine, wakiwa na Deus ambae pia alikuwa na begi lake dogo mgogoni, wakiwa wana wasindikiza kwa macho wakina Caroline, ambao walipolifikia gari, nikama walikuwa hawaamini kilicho watokea, kila mmoja kwa wakati wake aliweza kusimama na kugeuka kutazama kule alipokuwepo Deus, kisha kuingia kwenye gari.


Caroline yeye alivunja record, maana alipogeuka na kumazama Deus, akajikuta anapunga mkono, hata wakina Kasuba wasijuwe anapungiwa nani, “dogo punga mkono” alisema Kasuba akimlenga Deus, ambae alipunga mkono huku anatabasamu, na hapo kidogo Caroline akaachia kijitabasamu, kilicho ambana na simanzi, niwazi alihisi asingeweza kumwona tena kijana huyu, ambae amekuwa msaada mkubwa kwake, katika ajali hii.


Naam wakina Caroline waliingia garini, na gari likaondoka kuelekea mjini, na wakina Kasuba wakilisindikiza kwa macho mpaka lilipotoweka, “imeisha hiyo, niwazi umekuwa muhimu kwao, kiasi kwamba kila mmoja anahitaji muendelee kuwa wote mpaka mwisho wa safari yenu” alisema kanal Kasuba na wote wakacheka kidogo, huku Kasuba anamgeukia Deus, “dogo unaweza kutueleza ilikuwaje ukaweza kuwasaidia hao wote kutoka ndani ya tren?” aliuliza Kasuba, na wenzake wote wakatega masikio macho kumsikiliza kijana Deusi, ambae alianza kutoa maelezo mara moja.*******


Naaam ilikuwa hivi, baada ya kuwatuliza wale wafanyakazi wa TAZARA nao kuacha kila walicho kuwa wanakifanya na kumtazama Deus, huku Tren ikizidi kukaribia daraja, ndipo Deus, akamtazama yule dereva, “mzee kuna namna ya kupanda juu ya behewa?” aliuliza Deus, na yule dereva wa Tren akajibu haraka, “behewa hili hauwezi kupanda labda linalofwata, hilo lipowazi” Deus hakusubiri huyu mzee amalize kujibu, “twendeni haraka, kwenye hilo behewa tumekaribia daraja, alisema Deus, ambae kwa upande wake tayari alikuwa amesha vaa begi lake dogo mgongoni, maana ukiachilia nguo chache zilizo kuwepo, pia kulikuwa na vitu muhimu kwake, kama vile Fedha, vyeti vyake vya shule, na bastora ndogo, ya kisasa aina ya Walther P99, inayotumia risasi yenye mzingo wa mm 6, ambayo anaimiliki kinyume cha sheria, maana hakuwa na kibali cha kumiliki, japo siyo ya kufanyia maovu, hii alipewa na baba yake kwaajili tu, ya kuhakikisha anaitumia kukabiliana na lolote la unyang’anyi litakalo toke akiwa njiani na gari ambalo anaenda kulifwata.


Deus akamshika mkono Caroline ambae licha ya kuwaona wale wafanyakazi wa tren wanaelekea upande wa nyuma wa behewa lile fupi la wafanyakazi wa Tren, yeye alikuwa anamtazama Deus, “begi langu” alisema Caroline, na hapo Deus ambae licha ya kumshangaa mschana huyu kwa kukumbuka begi lake, katika hali ya hatari kama hii, lakini hakumsemesha chochote mschana huyu, zaidi ya kumwachia mkono, na kulishika lile begi kubwa na zito la mschana yule, kisha aka sogea mlangoni akafungua mlango na kulitupa lile begi, pasipo kuangalia lilipo dondokea, kisha akamfwata Caroline, na kumshika mkono kisha kuelekea kule ambako wengine walielekea, ambao sasa walikuwa wamesha fungua mlango na kutoka nje.


Nawalipotoka nje waliwakuta wale jamaa watatu wamesha panda juu ya behewa lenye mbao, na kumsubiri, Deus, ambae alimsaidia Caroline kupanda kwenye mbao za kwenye behewa, huku wale wengine wakimpokea kule juu, kisha Deus nae akapanda juu, ya behewa lile, wakati huo tayari kichwa cha Tren kilikuwa kimebakiza mita kama mia mbili na nusu kuingia darajani, daraja ambalo lilikuwa limesha sombwa na maji, jamani sikilizeni, kosa lolote litagharimu maisha yako au ulemavu wa kudumu, hivyo fanyeni kama niakavyo waeleza” alisema Deus huku anamshika mkono, Caroline, na kuanza kukimbia juu ya mbao, kurudi nyuma zaidi ya Tren, hata wale jamaa watatu pia wakakimbia kuwafwata, mpaka karibu na mwisho ambapo Deus alisimama, akiwa bado amemshika Caroline, nawao wakasimama.


“jamani hatuna muda wakupoteza, mtaruka juu kwa kuelekea nyuma pembeni kidogo ya usawa wa behewa, unapotuwa jilegeze kiasi, mme elewa?” alipiga kelele Deus, “ndiyo” japo walijibu kwa pamoja, lakini kiukweli zilikuwa sauti za chini, ambazo zilikosa matumaini, “haya kila mtu kwa wakati wake, kumbuka kosa moja unapoteza maisha” alisema Deus, na hapo watu hawa kama vile hawaja mwelewa Deus, wote wakamtazama, wakamtazama Deus kisha akamshika Caroline, na kunyanyua kama mtoto, kifuani kwake, kisha akapiga hatua tatu upande wa kulia wa behewa na kuruka juu, Caroline alijikuta akipiga ukelele mkubwa wa uoga, huku anafumba macho kwa uoga, huku akijikuta wakielea kwa sekunde kadhaa hewani, kabla hawaja tuwa chini na kwenye vidimbiwi vidogo vya maji pasipo kupata jeraha hata moja.


Na wale wengine lipoona hivyo, nao wakaruka kama alivyofanya Deus, japo walipata vimichubuko vidogo, wakati huo huo waliweza kuona kichwa cha tren kikiacha njia yake na kutumbukia mtoni, na mkia wake ukifwatia, “baada ya hapo ndio tuka rudi kwenda kuwaangalia wale walioruka mwanzo, pamoja na begi la yule mschana, ambalo tulilikosa, likaja kuonwa na hawa askari” alisema Deus, akimaliza kumweleza Kanali Kasuba.


Ukweli simulizi ilikuwa ni yakusisimua, siyo tu kwa Kanal Kasuba, ila pia kwa wengine wote waliokuwa wanasikiliza, “kijana kwanini unaficha utambulisho wako?” aliuliza Kanali Kasuba, huku anamtazama Deus machoni, lakini Deus ambae alikuwa anamtazama Kasuba, alionekana kutoa macho ya mshangao.


Naweza kuona kitamburisho chako?” aliuliza kanal huku anamtazama Deus, huku amenyoosha mkono tayari kupokea kitambulisho….…..#NYUMA_YA_MLANGO_WA_ADUI, inayo kujia hapa hapa jamii forums
 
Back
Top Bottom