Abou Shaymaa
JF-Expert Member
- Oct 19, 2022
- 1,479
- 3,229
- Thread starter
- #181
NYUMA YA MLANGO WA ADUISasa hivi sitaki ujinga wa kuifuatilia sijui hadithi au simulizi flani hivi sijui nini.
Hawa wasimuliaji wanatuona sisi kama wajinga flani hivi.
Kumbe wangeleta simulizi zao kwa wakati wangenufaika wao kwa kupata followazi wengi na kufanya biashara yao baadae.
Wasimuliaji kama huyu ni watu wa kuwapotezea tu.
Yako maisha mazuri nje ya hawa wapumbavu
SEHEMU YA ALOBAINI NA NNE
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
ILIPOISHIA SEHEMU YA ALOBAINI TATU: “wacha nikufanyie wepesi kisonge” alisema Deus huku anatazama upande kushoto ambako kuna uwanja wa ndege, akaona kama upande huo sio mzuri kwake, akatazama upande wakulia, akaona chochoro moja yenye giza ya kati ya nyumba na nyumba zile zenye maduka upande huu wa barabara, hapo Deus akakata kona na kuingia upande ule, na kupotelea gizani, Unajuwa nini kilikuwa kinaendelea, basi hebu turudi siku mbili nyumba siku ambayo Deus aliingia ofisini pale MONUSCO, mara baada ya kuingia ghoma akitokea ben,……… ….endelea….
Naam taarifa za maamuzi ya mahakama kuu ya kijeshi iliyoendeshwa kwenye bwalo la mikutano, huko Ben mavivi ya kuondolewa kwa hadhi ya kuwa afisa wa MONUSCO ya askari Deus flank Nyati, zilifika kwa bwana Seveline Khbango anae fanyia kazi katika ofisi ya mipango na ushirikiano pale makao makuu ya MONUSCO mjini Ghoma, ambae alimtaarifu mkuu wake aliekuwa anaishi nchi Rwanda na kuwaeleza habari hiyo inayo muhusu mtu alievuruga mipango yao ya kuwateka madoctor kule Ben, “Seveline, huu ndio wakati ambao tulikuwa tuna usuburi, lazima tumtumie huyu askari kuuwa ndege wawili kwa jiwe moja” alisema Chief wa kutoka Rwanda, (neno Chief watu wa kongo, hulitumia baada ya neno Boss.
Hapo Chief akaanza kufafanua, kwamba waandae vijana kadhaa ambao watashiriki kumkamata Deus, ambae akisha kamatwa wata tangaza katika mashirika makubwa ya habari duniani wakijinadi kuwa wamemteka askari wa Tanzania, hiyo ingewapatia heshima kubwa na kuwa tishio kwa ukanda huu wa Kivu ya kaskazini, na pili watatumia nafasi hiyo kudai mamilioni ya fedha ili wamwachie askari huyo ambae miezi michache iliyopita alijizolea sifa kubwa kama askari shujaa alie waokoa madoctor watatu, toka mikononi mwa waasi wa IDFNALU.
Na kwa kutekeleza mpango huo wakaweka watu kila kona ili kuhakikisha wanamfwatilia Deus kila hatua, ili iwe rahisi kumnasa pindi atakapofika Goma.********
Ilikuwa ni mida ya saa mbili kasoro dakika chache sana, kaskazini nje kidogo ya jiji la goma Kanyaluchina ni neno la moja ya makabila ya mashariki ya Congo, nimeandika kama inavyo tamkwa kilomita nne toka airport pia ni kilomita mbili toka MUNIG Base, lililopo karibu kabisa na Kibhati, hapo tunazungumzia eneo ya opelapee (sio mandishi sahihi ila ndivyo inavyo tamkwa, hiloni neno la kifaransa) eneo ambalo limechangamka sana, hasa kwa kipindi hiki ambacho waasi wa M-23, walikuwa wamesha ondolewa.
Mita kama khamsini hivi toka kwenye geti la ushuru linalo simamiwa na jeshi la serikali ya jamuhuri ya watu wa Congo, walionekana vijana wawili waliokuwa wamesimama pembeni ya piki piki, huku macho yao yakielekea upande wa Munig, ni wazi kuna kitu walikuwa wana kitarajia.
Nawakiwa wamesimama mahali pale, mmoja alie valia shati jekundu na kuchomekea kwenye suruali ya kitambaa aliyofungia mkanda maeneo ya tumbo kichwani akiwa amejivesha kofia nyeusi na kuziba sura yake kwa kepu ndefu ya kofia hiyo, aliweka simu yake sawa, iliyokuwa mkononi mwake na kubofya namba fulani ambayo ilikuwa juu kabisa, kwa maana ilikuwa ndiyo ya mwisho kuipiga iliyoifadhiwa kwa jina la Chief Seveline Khabango, kisha akaiweka sikioni akaisikilizia dakika kadhaa, halafu akaanza kuongea, “chief, una uhakika kweli kuwa wanaingia leo goma, maana kutoka ben mwa leo na kufika mwaleo leo, ni vigumu” aliuliza yule jamaa mwenye kuvalia suruali tumboni, “Kisonge nimepata taarifa wamepita Kibumba muda mrefu, sasa hivi wanaingia goma waenda mbio sana, chunga hapo mpaka wapite na kisha muwafuate mkaone wanaenda kufikia wapi” ilisikika sauti toka upande wapili wa simu, yaani kwa chief Seveline Khabango, “sawa chief sisi tupo hapa tuna chunga (kusubiri)” alisema yule kijana ambae sasa unaweza kumtabua kuwa ni Kisonge, ambae muda wote amekuwa akitafutwa kule ben, kisha akakata simu ambayo hakuiweka mfukoni, aliendelea kuishika mkononi.
“Sijui kama ni kweli, yaani hawa watanzania wanaendeshaje gari, watumie siku moja, toka ben mpaka hapa ghoma, nadhani amefananisha gari” alisema Kisonge, akimweleza yule mwenzie ambae alikuwa bado anatazama barabara, upande wa munig, “mh! ngoja tuone maajabu” alisema yule mwinzie na Kisonge, aliekuwa amevalia koti la baridi na kofia ngumu ya kuendeshea pikipiki, hayo maajabu yaanzaje kuto….” alisema Kisonge na kabla hajamalizia kuonggea akajikuta akitoa macho kwa mshangao, akitazama upande ule ule wa Munig, ambako waliweza kuona mwanga wa taa za gari, lililokuwa linakuja kwa mwendo wa kasi sana kulisogelea geti la ushuru.
Hawakuhitaji tochi wala mkalimani, kuwaeleza kuwa lile ndilo gari walilokuwa wanalisubiri, yaani gari la MONUSCO toka ben, iliwashangaza sana, wakajikuta wanatazamana kwa mshangao, “kweli hawa ni majeshi” alinong’ona yule mwenye kofia ngumu huku wote wakitazama tena kule lilikokuwa linatokea lile gari, ambalo sasa lilikuwa limesha karibia geti la ushuru, na kupunguza mwendo, kwaajili ya kupita kwenye sehemu ndogo iliyoachwa pale getini kwaajili ya kupita magari yasiyo husika na ushuru.
Wakina Kisonge walilishuhudia gari lile aina ya Toyota Land Cruizer likipita pale getini na kisha kuongeza mwendo kuelekea jijini, walilisindikiza kwa macho mpaka lilipotokomea upande ghoma mjini, huku Kisonge akishtuka na kukumbuka kuwa anatakiwa kulifwatilia lile gari, “washa pikipiki tuondoke haraka” alisema Kisonge huku anaiweka simu yake sawa na kupiga kwa chief Seveline, wakati huo yule mwenzie, akiwa anapanda piki piki na kuiwasha, “Chief, nikweli wamepita” alisema Kisonge huku na yeye anapanda piki piki, ambayo haikuchelewa kuanza safari kuelekea mjini kwa mwendo mkali sana, huku wakiwa wamesha lipoteza gari mbele yao, “wafuatilieni mkajuwe wamefikia wapi, lazima huyo mjinga alipie alichokifanya, hii itawafanya UN na askari wenzake waiogope NALLU” ilisikika sauti ya Chief Seveline, “namimi mwenyewe ninahasirea nae sana, ameniharibia mambo mengi sana” alisema Kisonge kisha wakakata simu huku pikipiki yao ikizidi kushika kasi.
Naam licha ya kukimbia na pikipiki yao, lakini hawakufanikiwa kulipata gari lile, walilolisubiri kwa masaa kadhaa, zaidi walijikuta wamesimama njia panda ya Bhilelee pasipo dalili yoyote ya gari la UN, ndipo Kisonge alipopiga simu kwa Chief Seveline na kumweleza kilicho tokea, “hakuna shida Kisonge, kesho lazima wata kuja hapa ofisini ndipo tutanza kumfuatilia mimi nitampigia Chief aandae vijana wakumshughurikia, maana chief anamtaka akiwa hai ili kuwafanya watanzania watoe fedha nyingi, na pia kutoa tishio kwa majeshi yote ya MONUSCO, na UN kwa ujumla na itakuwa aibu kwao na watatuheshimu” alisema Chief Seveline, kabla hawajakata simu.
Naam siku ya pili ndipo wakaanza kumfwatilia Deus, na kuhakikisha wanafahamu kila anacho kifanya, huku upande mwingine wakiwa wamewaandaa vijana watano walio waamini kuwa wanauwezo mkubwa wakupambana, ambao wange mkamata Deus, huku mmoja akiambatana na Kisonge kumfwatilia Deus na wengine wakisubiri muda muafaka wa kumkamata kijana huyo kabla hajapanda ndege kuelekea nchini kwao, kitu ambacho walifanya watu hao toka kundi hatari la IDFNALU, nikwamba, askari hao watano wa IDFNALU, licha ya kuwa walikuwa wanajiamini kuwa wanauwezo mkubwa kuliko Deus, lakini pia walikuwa na silaha muda wote, ambazo ni AK 47, visu na bastora ili iwe rahisi kwao kumdhibiti kijana huyo.
Siku ya pili ambayo ndio siku ambayo Deus alikuwa amesha kamilisha taratibu za kuvunjiwa mkataba na UN, Seveline aliekuwa ndani ya ofisi za Monustco, alifwatilia kila kitu na hata alipokuwa anatoka pale MONUSCO, akapiga simu kwa Kisonge,
aliekuwa anasubiri nje ya uzio wa ofisi zile, pamoja na askari mmoja toka kwenye kikundi cha waasi, abae sasa ndie alikuwa anaambatana nae katika tracking yao.*****
Wakiwa wanaamini kuwa Deus hakuwa amewaona walimfuatilia mchana kutwa, pale jijini Goma, wakati Deus anafanya manunuzi hata giza lilipoingia na Deus kuamua kurudi kambini, ndipo na wao wakaona kuwa sasa ndio muda muafaka wa kumnasa kijana yule, Kisonge akapiga simu kuwajulisha wale wenzao wanne, kwamba sasa windo lao linaelekea nachinjioni.
Nakile ambacho walikiona kuwa ni kujiingiza kwenye kilengeo kwa Deus, ni baada ya kumwona kijana huy aliekuwa anafuata barabara ya kibati, akichepuka na kuingia kwenye chochoro za mtaa wa bilele, bahati nzuri kwa Kisonge,
kama sio bahati mbaya kwao, tayari wale vijana wanne, walikuwa karibu na eneo la tukio, na kupewa maelekezo ya kujipanga vyema ili kumzunguka Deus waweze kukamata.
Yap! nadhani sasa ndio wakati wa kushuhudia kile kilichotokea, kwa Kisonge na wenzake, hapa mitaa ya Bilele (bilele tafsiri yake ni migomba ya ndizi)
Naam Kisonge akiwa na yule wenzie anaendesha pikipiki walikuwa wamesimama karibu na uchochoro ule wote wakashuka, “sasa sikia Kisonge baki hapa na pikipiki” alisema yule jamaa huku anafungua zip ya koti lake la baridi, na kutoa bunduki aina ya AK 47, ambayo kitako chake kilikuwa kimeondolewa na kuikoki, wakati huo mita kama hamsini toka pale waliposiama, llisimama gari dogo aina ya Toyota spacio, lilisimama na wakashuka vijana wanne wakiwa na Bunduki kaa ile aliyoishika yule mwingine, kisha wakamtazama yule alie simama na Kisonge, ambae aliwaonyesha ishala kuwa ameingia kwenye chochoro iliyokuwa jiani yake.
Hapo mmoja kati ya wale wanne akamwonyesha ishara, yule aliesimama na kisonge kuwa aingie pale chochoroni, kisha akawagawa wale wenzake kwamba waingie kwenye chochoro inayofwata, yani iliyopo pale jirani na waliposimama nao kwa pamoja wakafanya hivyo, yaani yule mmoja akaingia kwenye chochoro aliyoingia Deus, na wale wanne wakaingia kwenye chochoro moja, na walipovuka nyumba mbili wakakutana na chochoro nyingine ambapo wawili wakaingia kwenye chochoro ile na wawili wakaendelea kufwata chochoro iliyonyooka hawakujuwa kuwa wanachokifuata ni kitu kibaya sana.
Huku upande wa barabarani, bwana Kisonge alipiga simu kwa Chief Seveline, ambae hakuchelewa kupokea, “Chief tayari vijana wanamkamata tupo hapa bilele” alisema Kisongea kwa sauti ya chini, “safi sana Kisonge, hakikisha safari hii hakuna makosa zaidi, nisubiri hapo nakuja sasa hivi” alisema Chief Seveline, kwasauti iliyojawa kihoro, na kukata simu. ….endelea…. kufwatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums