Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA HAMSINI NA TATU
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA MBILI: Walikuwa wamechoka haswaa, walitulia dakika kadhaa wakihema kwa kumaliza mbio ndefu, kabla hawajashtuliwa na simu ya mezani toka mapokezi, ambayo ilipokelewa na Neela mwenyewe, ikiulizia kama wapo tayari kuletewa chakula, jambo lililo kubaliwa na Neela kwamba chakula kiletwe..endelea….


Baada ya hapo wakaingia bafuni kumalizia kuoga, kisha wakaenda kutulia pale kwenye kibaraza cha nje wakisubiri chakula kilicholetwa mara moja na wao kuendelea kula mpaka sisi tulipowakuta wakiwa hapa wakiendelea kuonek
ana aibu kwa kile walichokifanya kule ndani.******


Naam twendeni #Mbogo_land, moja kwa moja Golden House, ambapo tuna muona waziri wa ulinzi bwana Chitopelah akitoka nje ya jengo hilo ni wazi alikuwa amesha maliza kikao na mfalme, na moja kwa moja akaelekea kwenye maegesho ya magari ya wageni VVIP, ambao wengiwao ni mawaziri.


Lakini wakati anakaribia gari lake, simu yake ikaanza kuita akaitoa mfukoni na kuitazama, alipoona jina la mpigaji akatazama kushoto na kulia, aliporidhika kwamba alicho kitazama kipo katika hali inayo mruhusu kupokea simu akaipokea na kuiweka sikioni, “niambie Kadumya, kuna taarifa yoyote” aliuliza Chitopelah kwa sauti ya chini huku anaendelea kutembea kulifikia gari alililo likusudia, “ndiyo boss, tayari vijana wameshakabidhi mzigo, dhahabu kilo hamsini, kama ulivyoagiza shambulio la kwanza ni kilomita nne kabla ya kuingia Ndanda, itatengenezwa ajari, kisha vijana watachukuwa box na kuondoka nalo, bwana Tshen hatofahamu kama tumechukuwa sisi ataamini kuwa mzigo umeibiwa baada ya ajari” ilisikika sauti upande wapili wa simu, “mpango mzuri, tunachojari sisi ni kwamba, tayari ameshaweka fedha kwenye account yetu ya siri, itasaidia kuwapatia posho vijana, ila tuna jambo la kuongea jioni ya leo, naona mfalme ameanza kutia mashaka juu ya utoro wa askari” alisema Chitopela kwa sauti ya chini.


“vipi kuhusu mpango wapili wa kurudisha mzigo” aliuliza Kadumya, “ufanyike kama tulivyopanga, wasiliana na vijana wa dar es salaam, wahakikishe mzigo haupandi ndege, kisha wakati wanahangaika kutafuta njia nyingine ya kusafirisha, waupore na kuurudisha mikononi mwetu, maana tukiupoteza itakuwa vigumu kupata mzigo kama huo, kwa sasa uthibiti ni mkubwa sana wa madini toka hapa nchini” alisema Chitopela, ambae tayari alisha lifikia gari alilokuwa analifuata na kukata simu, kisha akaingia ndani ya gari lile kisha gari likaondoka, wakipisana na gari moja aina ya land lover Puma, lenye rangi ya kijani, lenye namba 2008MLA 6202 , mali ya jeshi la #mboogo_land, ambalo lilikuwa linaingia pale Golden House huku ndani likiwa na watu watatu waliovalia nguo za kijeshi maalumu kwaajili ya vita, yaani vazi la vita, kama wazungu wanavyoita combati dress, huku mmoja kati yao aliekaa seat ya mbele kushoto, akionekana kuwa na cheo cha major general, na kwenye ukosi wake (kola), vikionekana vialama vyekundu, alionekana kuwa ndie mkubwa wao.


Naam gari liliingia kwenye maegesho ya VVIP, nakusimama pale pale lilipotoka gari la waziri wa ulinzi, Dickson Chitopelah, kisha akashuka yule major gen, ambae kwa muonekano ni mtu ambae alijaaliwa umbo na mwonekno wa kijeshi, ukiachilia misuri ya mikono iliyoonekana vyema baada ya kukunja shati lake la kombati, pia alikuwa mrefu mwenye kifua kipana, mweusi alie valia miwani meusi ya jua na kofia nyeusi kichwani mwake, ikiwa ni ishara ya askari wa kikosi cha mizinga mikubwa, mfano Tank yani vifaru mizinga mikubwa kama vile D 30 na mingineyo, pia BM -12 Grad, ikiwa ni silaha toka Urusi, yenyewe inayoitwa Boyevaya Machina, na pia hutumiwa na askari wapelelezi wa kivita, Amoured Reccenasence.


Ambae alianza kutembea kwa mwendo wa haraka kuelekea kwenye lango la kuingilia kwenye jengo ilikuwa la kipekee lenye ofisi za mfalme, ndani ya makazi ya mfalme Elvis wa kwanza, huku akionekana kupendeza kwa nembo ya dhahabu, iliyoonyesha picha ya mwewe, ikimaanisha ni kiumbe ambacho hufanya uchunguzi mkali kwenye mawindo yake kabla ya kufanya uvamizi, lilokaa juu ya mfuko wa kulia wa shati lake chini ya jina lake, lililoonyesha kuwa alikuwa ni AR kwa maana ya kwamba Amour Racce.


Huyu anaitwa Major Gen Sixmond Mbedo, mkuu wa kitego cha upelelezi kivita, ambae siyo tu kukubalika kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kupanga na kufanikisha uchunguzi wa ndani na nje ya nchi, pia alikuwa na Elimu kubwa sana ya fani hiyo ya uchunguzi wa kivita, kiasi kuaminiwa na king Elvis, hata kupewa kibari cha kuingia kwa mfalme mara kwa mara anapokuwa na taarifa muhimu.


Dakika tano baadae tayari major Gen Sixmund, alikuwa amesha ruhusiwa kuingia ndani ya ofisi kubwa ya mfalme Elvis wa kwanza, aliemkuta anamsubiri, baada ya kupewa taarifa na watu wa mapokezi na baada ya salamu zote za heshima, ndipo major Gen Sixmund akaeleza kilicho mleta “mtukufu mfalme, hii ni taarifa nyeti sana,
toka kwa wachunguzi wa mipakani na maeneo ya jirani” alisema Gen Sixmund, kwa kituo, “endelea, nakusikiliza Gen” alisema mfalme Elvis kwa sauti tulivu, “mfalme, wachunguzi wetu wamegundua uwepo wasiri wa kundi la Uhuru kwa Umwagaji Damu, yaani UMD, kikundi ambacho kilidhaniwa kimesha tokomezwa mwaka 1992, na lengo lao ni kufanya mapinduzi ya serikali yako tukufu” alisema Gen Sixmund, akionyesha kuhuzunishwana taarifa zile alizo zileta.


Kama Six alihuzunishwa na taarifa aliyoileta yeye mwenyewe basi ilikuwaje kwa mfalme Elvis, imekuwaje hilo kundi likarudi tena hata baada ya operation kubwa iliyofanyika miaka hiyo ya tisini?” aliuliza king Elvis kwa mshtuko mkubwa sana, “mtukufu mfalme, kundi hilo lililoanzishwa mwanzoni mwa miaka ya tisini, na kutoweka ghafla mwaka 1992, lilizusha wimbi kubwa la usaliti ndani ya serikali ya mfalme Eugen, ndipo serikali ikitumia kitengo cha MLSA, ilianzisha msako mkali wa wasaliti wote waliojificha serikalini, na kuwaangamiza kwa siri wao na familia zao” ,alieleza Gen Sixmund, kabla king Elvis hajamkatiza, “Gen, ni kwanini familia zao zilihusishwa na nani alitoa wazo hilo?” aliuliza King Elvis, ambae alionekana kusikitishwa na kitendo kile.


Hapo Gen Sixmund akaeleza kilicho tokea, “mtukufu mfalme, ukweli jambo hilo lilimshangaza kila mmoja, hata baadhi ya mataifa makubwa yalilipigia kelele swala hilo, lakini mfalme alikanusha vibaya na kuzuia waangalizi wakijeshi, japo wengi tunaamini kuwa mpango ule uliokuwa chini ya bwana Chitopela ulisaidia, lakini bado wakosoaji walisema kuwa wengi waliuwawa kimakosa na mbaya zaidi walikuwa ni viungi muhimu serikalini” alieleza Sixmund, “sasa Gen, ushauri wako ni upi” na kikundi hicho kipo wapi?” aliuliza mfalme, kwa maana unapotoa report unatakiwa kutoa ushauri.


Hapo Sixmund akatulia kidogo na kujiweka sawa, kwa maana alitakiwa atoe ushauri ambao ungekuwa na faida kubwa kwa mfalme na serikali yake, “mtukufu mfalme, bado kikundi hakijulikani, kipo sehemu gani, kwa maana hizi ni taarifa za awali, lakini sehemu ambayo wanakaa na kuratibu mambo yao inasemekana ni dar es salaam Tanzania, ambako ndio makazi ya viongozi wao, ushauri wangu mtukufu mfalme ni kwamba, nitateuwa mtu ambae anaweza kusimamia kikundi kidogo cha jeshi cha uchunguzi toka ndani ya jeshi letu la ulinzi, kitengo cha AR, ambacho kitachunguza kwa siri, mienendo na mipango ya UMD, ili tujuwe namna ya kuwadhibiti” alisema Sixmund, “sawa kibari kimetolewa, teuwa kikundi na msimamizi, lete bajeti yako, kwaajili ya kikundi, nahitaji taarifa za mara kwa mara kujuwa kila kinachoendelea” alisema mfalme Elvis, kabla ya kuagana na Sixmund, ambae aliondoka zake na kwenda kuandaa kikundi hicho cha siri, ndani ya kitengo chake cha AR.*******


Kampala Uganda, Hotel Ajun Serasie, wakati Neela na Deus wanaendelea kula, huku Neela akionekana wazi kuzidi kujawa na hisia za mapenzi, mara ghafla Neela akasogeza mkono wake na kuushika mkono wa Deus, kisha akamtazama kwa macho tulivu yenye hisia kali za mapenzi, “Deus nilidhania hii inaweza kuwa ishara ya neno asante, maana mwili wangu huwa siutoi kwaajili ya burudani kwa mtu, niliutoa mara chache kwa mwanaume aliesema atakuwa mume wangu, ni kutoka Tanzania, nilikutana nae wakati nasoma chuo pale muhimbili, akakosa uvumulivu na kunisaliti ndio maana nilikuchukia siku ya kwanza tulipokutana, niliona kuwa wanaume toka Tanzania sio waaminifu, nikaamua kukupa kama asante kwa kuniokoa toka kwenye mikono ya wale majambazi washenzi, lakini nimegundua kuwa, nilichokipata kwako ni zaidi ya kile nilichokupatia, hakika bado nina deni kwako” alisema Neela na kumfanya.


Deus alitabasamu kidogo, kisha akaongea kwa sauti tulivu iliyojaa mahaba, “hapo mwanzo sikuwahi kujaribu mapenzi, ila nimeshangazwa na kile nilichokiona kwako, sikutegemea kama mapenzi ni matamu hivi, umekuwa mwalimu wangu mzuri sana” alisema Deus, huku tabasamu likiendelea kutawala usoni mwake, “wewe umenifanya niyafanye yote ulio yaona, japo niliwahi kushiriki mapenzi, lakini Deus, leo ndio nimefanya mapenzi kiukweli, yaani kamavile kulikuwa na mwalimu pembeni yetu, yaani kama mwanaume wangu wa zamani angepata kuniona wakati ule, angeshangaa sana” alisema Neela huku uso wake ukijawa na tabasamu lililojaa aibu ya kike na kumalizia kwa kicheko cha chini, huku anakwepesha macho yake yasitazamane na macho ya Deus.


Wakati wanaongea hili na lile, mara simu ya Neela ikaanza kuita, wote wakaitazaa na kuona jina la mpigaji likiwa limeandikwa BABA, Neela akaipokea haraka na kuiweka sikioni, kisha akaanza kuongea kwa lugha ambayo Deus hakuielewa, mpaka walipomaliza na kukata simu, “alikuwa baba yangu, yupo na mama wanaondoka Ethiopia sasa kwa ndege binafsi, wanakuja kukuona mwanaume ulieyakoa maisha yangu, nilikuambia mwanzo kuna watu wanahitaji kukuona” alisema Neela, kitu ambacho kilimshangaza sana, Deus, “kwanini lakini mbona ni kitu cha kawaida tu, kwanini wazazi wako wanakuja toka Ethiopia?” aliuliza kwa mshangao Deus na kumfanya Neela acheke kiogo, kisha kuanza kumueleza jambo alisilolijuwa kuhusu yeye na familia yake.*******


Naam Gari aina ya BMW lilioekana likikatiza kwenye barabara ya tunduru masasi, kuelekea upande wa mashariki, yaani kwenye mji wa masasi uliopo mkoa wa mtwara kwa speed kari sana ya kilomita mia moja themanini kwa saa, na sasa lilikuwa limebakiza kilomita chache sana kuingia masasi mjini.


Ndani ya gari hilo anaonekana mtu mmoja tu, ambae ndie dereva, tena ni mschana mrembo, mwenye umri kati ya miaka 24 au 25 hakika ingekushangaza sana, kwa mschana mdogo kama huyu kuendesha gari kwa speed kama hii, gari lilikuwa la kisasa, ambalo lina mambo mengi sana, ukiachia seat zake kuwa nzuri zenye kustarehesha msafiri, pia screen dogo ya video kila seat, huku dash board yake yenye mambo mengi sana, ikizidi kueleza kuwa iligari aina BMW 7, sio la kawaida, kuanzia speed yake ya mwisho kuwa 280, pia vitufe vingi vya kuongozea gari, pamoja na kioo kiogo chenye ramani ya sehemu anayoenda ikionyesha kilomita na hali ya hewa.


Naam wakati mschana huyo mrembo wa sura na umbo alikuwa anapunguza mwendo kuingia mjini masasi mara simu yake ikaita, nae akabiofya kitufe flani kwenye dash board ya gari lake la kisasa, sehemu ya kioo cha video ndogo pale mbele, ambapo kuna jina la mpigaji wasimu lilionekana limeandikwa Boss Atshen na kuanza kuongea. “naam boss, ndio naingia masasi sasa” alisema yule mschana, mrembo, ambae hata sauti yake ni nzuri, “sikia Sheba, ramani inaonyesha mbele yako kuna njia panda, barabara tatu za lami, mbele kulia na hiyo unayotoka, na moja ya kushoto ni ya vumbi, ifuate hiyo sina uhakika na hawa washenzi, wanaweza kubadili mchezo muda wowote” ilisikika sauti toka kwenye ile screen na ile kutazama vizuri tayari alikuwa anaivuka ile njia panda, hivyo akapunguza mwendo zaidi na kuingia kwenye kituo cha mafuta kilichopo pembezo mwa njia panda, upane wa kushoto mtu yeyote angejuwa kuwa gari hili linaingia kuweka mafuta, lakini haikuwa hivyo, lilipitiliza moja kwa moja mpaka njia ya kutokea na kuingia kwenye ile barabara aliyo elekezwa. ..…….endelea…. kufwatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
muendelezo tafadhali.
SEHEMU YA HAMSINI NA NNE
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA TATU: moja ya kushoto ni ya vumbi ifuate hiyo, sina uhakika na hawa washenzi, wanaweza kubadili mchezo muda wowote” ilisikika sauti toka kwenye ile screen na ile kutazama vizuri tayari alikuwa anaivuka ile njia panda, hivyo akapunguza mwendo zaidi na kuingia kwenye kituo cha mafuta kilichopo pembezon mwa njia panda, upande wa kushoto, mtu yoyote angejuwa kuwa gari hili linaingia kuweka mafuta, lakini haikuwa hivyo, lilipitiliza moja kwa moja mpaka njia ya kutokea na kuingia kwenye ile barabara aliyo elekezwa. ..…….endelea….


“boss tayari nimeingia barabara ya kushoto” alisema mschana huyo anaitwa Sheba, kuna kilomita 47 mbele yako barabara chafu sana, kalale nachingwea Nyumbani lodge ndiyo sehemu salama, ondoka kesho mapema, kuna kilomita nyingine 45 kufikia njia panda ya barabara ya lami” ilisikika ile sauti toka kwenye simu ya kwenye gari, “umesikika boss” alisema yule mschana, “ok! safari njema, mzigo ufike salama” alisema Tshen na simu ikakatika.


Hapo mschana Sheba, akalegeza kidogo mguu wake wa kulia ambao ulikuwa umekanyaga peder ya mafuta na kupeleka mkono wake wa kulia, chini ya seat upande wa mlango wa gari na kuibuka na bastora yake, akiliacha gari linaendelea kusonga mbele yeye akaachia stearing, yaani mshikanio na kuikoki ile bastora yake kisha akairudisha bastora mahali pake huku anashika mshikanio na kukaza mguu wa kulia kwenye peder ya mafuta na gari likaongeza speed, japo gari hili lilikuwa na mifumo miwili ya gia, yaani manual transmission gear, na automatic transmission gear, lakini mwanadada Sheba, alikuwa anatumia automatic peke yake, na baada ya kukanyaga kwa sekunde ishirini juu barabara hii ya vumbi, tayari alikuwa anakaribia speed mia arobaini na kujikuta akipunguza speed yeye mwenyewe na kufikia speed mia na wakati mwingine tisini ni baada ya kukutana na baadhi ya vikwanzo vya mashimo na mawe yaliyo simama na kuchongoka kama kisu cha ngariba, na kufikia speed themanini, angalau aliweza kuyaona mashimo, lakini kuhusu mawe gari hili lenye mneso wa nguvu, alikusikia jiwe la aina yoyote.******


Naam Neela ni binti pekee wa bwana Ajun Serasie, barozi wa zamani wa Ethiopia nchini Tanzania, ambako aliishi kwa miaka kumi na moja, ukiachilia kuwa barozi na mfanyakazi wa serikali pia ni mfanya biashara tajiri mkubwa sana Adis ababa, pia aliweleza katika biashara ya hotel nchini Uganda, yani Ajun Serasie Hotel, kwa maana hiyo hotel waliyofikia wakina Neela ni hotel ya baba yake Neela, ambae pia anawashirika wengine na wakubwa wakibiashara, iwe ndani ya nchi au nje ya nchi yao ya Ethiopia, ikiwa ni wafananya biashara kwa njia halali na zile njia ambazo hazitambuliwi na serikali.


Ukiachilia kumiliki mahotel makubwa ya hadhi ya nyota tano katika nchi kama Tanzania, katika majiji makubwa kama vile Arusha dar es salaam na kisiwani Zanzibar zote zikiwa zenye hadhi ya nyota tano, pia alikuwa anamiliki kampuni ya usafirishaji kwa njia ya anga, yaani ndege, akiwa na ndege kumi na mbili kumi zikiwa ndege ndogo za abiria na mbili zikiwa ni ndege kubwa za mizigo, ambazo pia anazitumia kusambaza vyakula kwenye tenda zake alizopata kwenye mashirika ya UN, ikiwa ni kwa walinda amani wa nchi mbali mbali, kama vile Sudan, Africa ya kati, na DRC.


Ukiachilia hayo yote bwana Ajun Serasie, alijaliwa kupata mtoto mmoja tu wakike, ambae ndie huyu Neela, ukweli anampenda kuliko hata utajiri wake, hata aliposikia kuwa ametekwa na waasi wa mashriki ya Cngo, alipatwa na mshtuko mkubwa sana, alikuwa tayari kutoa fedha ambayo waasi waliitaka, yaani dollar mia tano za kimarekani, ambazo ni sawa na Tanzania shilingi bilioni moja na laki tatu (kwa wakati huo) japo alifahamu fika kuw hata kama angelipa fedha hizo, lakini binti yake asinge toka salama, angekumbana na hatari ya kubakwa kunyanyaswa na kuteswa sana.


Na hata alivyosikia kuwa, kuna kijana amemuokoa Neela na madoctor wenzake, walifurahi sana na kupanga kwenda nchini Congo, kukutana na askari huyo wa kitanzania, kumshukuru pamoja na kumpatia zawadi kama shukrani na wakati wanajiandaa kwenda DRC, Neela akawajulisha kuwa Deus alikuwa katika kesi ya jaribio la kubaka.


Iliwashtua na kuwashangaza sana, wazazi wa Neela, walimuona Deus mtu wa ajabu sana kwa kitendo hicho cha kujaribu kubaka, lakini Neela alipowafafanulia kuwa ilikuwa ni mpango wa kutengenezwa ili kumkomoa Deus kwa kitend cha kuvuruga mpango wa waasi, ule wa kuwateka wakina Neela, ndipo wazazi wa Neela walipoona kuwa kuna haja ya kumsaidia kuepukana na kesi hiyo na kwamba hiyo ndio nafasi yao ya kutoa shukrani kwa kijana huyu kwa kile alicho mfanyia binti yao.


Lakini kabla hawajafanya lolote, wakasikia kuwa Deus alikuwa na ushaidi wakutosha na wenye nguvu wa kumuondolea hatari ya kupatikana na hatia, japo baadae alipatikana na kosa la kisheria, la kufanya kazi nje ya mkataba wake na MONUSCO, hivyo akasitishiwa mkataba, huku wakitambua kuwa lazima akakutane na adhabu kali huko nchini kwake Tanzania kutokana na sheria kali zilizopo katika jeshi hilo, ambalo ni moja kati ya majeshi yenye nidhamu ya hali ya juu katika nchi tatu za Africa, huku ikionekana katika orodha ya nchi hamsini zenye majeshi yenye nidhamu duniani.


Ndipo na wao wakapanga kukutana nae, pindi atakaporudi Tanzania, iliweze kumshukuru, maana niwazi ule msaada alioutoa kwa binti yao, ndio chanzo cha Deus kuharibu Malengo yake, na kwa bahati nzuri binti yao akawajulisha kuwa Deus alikuwa anaelekea Tanzania, huku na yeye pia ambae alikuwa na nia ya dhati ya kumshukuru kijana huyu, ambae siyo tu, anavutia kwa umbo lake la kimazoezi na sura yake ya upole, pia alitokea kumpenda na kupanga kumshukuru kwa namna ya kipekee kwa kumpatia kile ambacho kijana huyo alionyesha kukitamani toka siku ya kwanza walipokutana pale Entebe ndani ya ndege.********


Mida hii Chitopelah, alikuwa ofisini kwake ana waza na kuwazua, namna atakavyo fanikisha kuingiza silaha na kuivamia nchi, ambayo inamuamini kuwa kiongzi mzalendo mwenye kujitolea nchini kwa moyo wake wote, kuilinda nchi yake, “sio kwamba hakuwa na silaha nyingine, ukweli ni kwamba yeye na kundi lake la UMD, walikuwa na silaha japo ni chache, lakini zilikuwa za kisasavna zenye uwezo mkubwa na nzuri kwa malengo na kushambulia, ambazo pia zingeshiriki kumuondoa mfalme madarakani, pasipo kujali maisha mazuri wanayoishi wanachi wa nchi hii, ambao toka zama za mfalme Eric wa kwanza, yaani baba yake Eugen, alipoweka utaratibu wa kumfungulia account ya benk kila mzaliwa wa nchi hii anapo fikisha miaka miwili, account ambayo huwekewa fedha za kujikimu, kila baada ya miezi mitatu, huku huduma zote muhimu katika nchi hii, yani kama vile maji umeme Elimu kuanzia ngazi ya chekechea mpaka chuo kikuu, pia matibabu yasiyozidi laki nane za kitanzania zikiwa ni bure kabisa, hata pale matibabu ya mwanachi yoyote yanapozidi laki nane, basi serikali ingechangia asilimia hamsini ya gharama iliyozidi, walifanikiwa hilo katika mpango wa bia ya afya, ambayo wanachi hupatiwa bure kabisa toka pale anapozaliwa tu.


Ukiachilia hayo, pia serikali iligharamia harusi za wachumba, ambao walichaguana siku ya mwenyewe kijana kuchagua chumba, (soma #UMEKOSEA_LAKINI_TAMU) uanza kwa kulipia mahali mpaka kugharamia sherehe za harusi, na kama wanandoa hawakuwa na uwezo wa kujenga nyumba binafsi, basi huenda kuishi kwenye nyumba za kisasa zenye kila kitu, zinazo milikiwa na serikali, uondolewa pindi tu wanapoachana, ila wakidumu ndoani, basi wangeishi hapo maisha yao yote.


hayo yote yalifanyika kwa fedha zilizopatikana katika mapato ya ndani ya nchi, ya #mbogo_land, ambayo kwa asilimia themanini na tano, yanapatikana kwa kutegemea madini yanayopatikana nchini hapo.


“Mpango ukifanikiwa nitakuwa tajiri mkubwa sana, sio hapa Africa mashariki au Africa kwa ujumla, ila nitakuwa tajiri mkubwa duniani” aliwaza Chitopela huku amekaa kwenye kiti chake kwa kuegemea kivivu, “yani watu tunatafuta fedha halafu mjinga mmoja anagawa fedha hovyo kwa wananchi majinga wasiotaka kulima na kubeba zege” alijisemea Chitopela, ambae kiukweli alitamani kuona fedha na mali ya nchi hii, ambayo sasa vina nufaisha wanachi, vikiwa katika mikono yake, lazima nipate fedha ya kuingizia mzigo nchini, ili mambo mengine yaendelee” alijisema chitopelah na wakati huo huo simu yake ikaanza kuita, alipoitazama akaona jina la mpigaji kuwa ni Kadumya.


Chitopela akaipokea haraka na kuiweka sikioni, “niambie Kadumya, mmesha fanikiwa?” aliuliza Chitopela kabla hata hajasalimia, “boss dakika thelathini sasa, vijana wanasema, bado gari halijaonekana ndanda, na mara ya mwisho, lilionekana linakaribia masasi, sijuwi kwanini halijafika mpaka sasa” alisikika Kadumya upande wapili wasimu, “endeleeni kusubiri, ikiwezekana wengine wakakae njia panda ya Nanganga” alisema Chitopela kwa sauti ambayo haikuonyesha wasi wasi, juu kama mtego wake umeshindikana, sawa boss tutafanya hivyo” alijibu Kadumya na hapo simu ikakatwa, “mtu atoke kwao huko aje ajifanye mjanja kwetu, hawezi kutukimbia hata kidogo” alisema Chitopela hukua anaweka simu mezani.*******


Dakika ishirini na saba, ndio muda ambao Sheba aliutumia kutembea toka masasi mpaka Nachingwea na sasa alikuwa anazunguka round about ya askari mchafu, sanamu ambalo lina mfanano na lile la poster, japo kwasasa (sanam hilo halipotena sehemu ile), na kubakia jina tu, kisha BMW lina fwata uelekeo wa upande wa kulia, na kuingia barabara ya vumbi, iendayo Lindi mjini, ambako ndiko makao makuu ya mkoa huu, lakini baada ya kilomita kama mbili nanusu tu, akiwa ameshapita chuo cha ualimu cha nambambo, Sheba anapunguza mwendo, na kuingia kwenye barabara ndogo ya vumbi, lakini iliyotengenezwa vizuri kwaajili ya kupita gari la aina yoyote.


Gari lina seleleka taratibu likipita eneo la mita kama mia mbili, lenye mandhari nzuri, ya kijani, iliyopambwa na miti mifupi mifupi ya asili, ambayo makazi ya ndege wa kila aina walioonekana wakiruka na kupendeza kwa rangi zao walizo jaliwa……..…….endelea…. kufwatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
Pamoja mkuu zije kwa wing arosto n hatari kwa afya ya wasomaji.
 
Huyu jamaa anatutia arosto sanah
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA HAMSINI NA TANO
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA NNE: Gari lina seleleka taratibu likipita eneo la mita kama mia mbili, lenye mandhari nzuri ya kijani, iliyopambwa na miti mifupi mifupi ya asili, ambayo ni makazi ya ndege wa kila aina walio onekana wakiruka na kupendeza kwa rangi zao walizo jaaliwa……..…….endelea….


Burudani hii haikudumu kwa muda mrefu, maana Sheba anaibuka kwenye maungio ya barabara nyingine, nae anafuata upande wa kushoto na mita hamsini mbele yake anaona ukuta mkubwa wa usalama wa majengo yaliyopo ndani, wenye bango kubwa liloandikwa Nyumbani Lodge Village, nae anaenda kuingiza gari ndani ya uzio ule mkubwa na kuweza kujionea jinsi hotel ile ya kisasa nzuri yenye utulivu jinsi viunga vyake vilivyopendezeshwa kwa sakafu ya tofari ndogo ndogo za rangi ya seruji na nyekundu, sambamba na maua ya kila aina yaliyostawi juu ya koka za kijani, zilizo zunguka midhurungi mizuri kwaajili ya wateja waliokuwa wanajipatia burudani ya vinywaji na vyakula vizuri, vinavyopatikana mahali pale, vilivyopo pembezoni mwa eneo la mbele la majengo ya hotel hii mfano wa kijiji fulani kwa jinsi nyumba zake zilivyokaa, ukiachilia jengo kubwa lenye vyumba kwaajili ya wateja na ukumbi mmoja mkubwa wa wastani kwaajili ya vyakula na kuangalia sinema, pia kulikuwa na vyumba vilivyo jitegemea kwa kujitenga, ungesema ni nyumba ya kupanga, ilikuwa ni chumba na sebule chenye kila kitu, kuanzia sofa set ya kitanda kikubwa chumbani, bafu friji TV na baadhi ya vifaa ambavyo ungeweza kupatia huduma ndogo ndogo muhimu kwa binadamu, “pana faa kwa usiku huu” alijisemea Sheba huku anasimamisha gari mbele ya jengo la utawala la hotel hii.********


Saa mbili usiku, Deus na Neela walikuwa kwenye ukumbi mdogo wa VIP ndani ya hotel Ajun, wakiongea na mzee Ajun na mke wake, ambao walishaingia pale toka lisaa limoja lililopita, “kwakweli kijana tulihuzunika sana, kwa kile kilicho kutokea baada ya pale, lakini ni kawaida ya Serikali nyingi kuto kuangalia utumishi wa mtumishi wao zaidi ya kuangalia raia watasemaje, hauna budi kukubaliana na hilo” alisema mzee Ajun na kila mmoja akakubaliana kwa kichwa kwa kile alicho kisema, ila siyo mbaya nadhani hauto kwama kwa lolote, bado ni kijana mdogo una nafasi ya kuanza upya, hata kama ikitokea ukaachishwa kazi” alisema mzee Ajun na hapo Deus akaitikia kwa kichwa kukubaliana nae,


Wakati huo hapo mezani walikaa kwa mtindo wa urafiki yaani mzee Ajun akiwa amekaa karibu kabisa na mke wake upande mmoja wa meza, yaani hapa na hapa, wakitazamana na wakina Neela na Deus, ambao walikaa kama Ajun na mke wake japo wao hawakukaribiana sana, “mwanangu ukifika Tanzania msalimie sana mama yako, pia mpe hongera nyingi sana mwambie amepata mtoto ambae wengi wanamuhitaji” alisema mama Neela, ambae hakuishia hapo, “utampelekea zawadi kidogo pamoja na baba yako, tayari mizigo ipo airport, utakutana nayo kesho wakati unaondoka” alisema mama Neela kwa sauti iliyojaa upendo na shukrani, “asante sana mama nitafikisha salamu” alijibu Deus kwa sauti yake tulivu na ya upole huku akitabasamu.


Kabla hawajaingia kwenye aongezi ya kawaida, mzee Ajun alimkabidhi Deus bahasha yenye fedha ambazo hakuzitaja kiasi chake, zikiwa ni dollar za marekani, “pia ukiwa na shida yoyote, unaweza kuwasiliana na mimi moja kwa moja” alisema mzee Ajun, ambae kimuonekano hakua mzee sana, huku anampatia Deus card yenye namba za simu, ikiwa ni kadi maalumu kwa watu wa karibu na familia yake, huku akisisitizwa kuwa kesho akifika airport atakuta kuna mizigo yake, na tayari amesha fanyiwa taratibu za usafiri wa kwenda Tanzania.*******


Mpaka saa tatu usiku, bado taarifa ya kuto kuonekana kwa BMW 7, zilikuwa zinaedelea kumfikia bwana Chitopleah, ambae sasa alikuwa kwenye nyumba moja tulivu, iliyopo kwenye kitongoji cha Nyayo ya Chifu Kube, sehemu ambayo wakazi wake ni wahamiaji, yaani vijana toka nchi za jirani, waliokuja kutafuta maisha katika nchi hii.


Chopelah ambae ujio wake ulikuwa siri sehemu hii, hakuwa peke yake alikuwa na watu nane, mmoja wapo alikuwa ni bwana Kadumya, kanal mtoro wa MLA, “sijali nini kimetokea, ninachotaka ni dhahabu zangu, siwezi kupoteza kilo hamsini, bado tunahitaji fedha zaidi, kumbukeni kuna mzigo unatakiwa kusafirishwa na wale hatuwezi kuwafanyia uhuni hata mara moja” alisema Chitopelah kwa sauti ya ukali, “boss tayari nimesha wasiliana na Mbwambo awatume vijana waende kusubiri airport ya dar es salaam, huku wakiongea na watu wetu wa pale airport, ambao watazuia mzigo na kuuteka moja kwa moja ” alisema Kadumya, akionyesha kuwa na uhakika mkubwa.


Hapo Chutopelah akaoneka kuridhika na jibu la Kadumya, “sasa nimewaita hapa, kuwaeleza juu ya mambo yanavyo endelea” alisema Chitopelah kwa kituo, huku anawatazama wale vijana waliosimama mbele yake, ambao uvaaji wao walionyesha kuwa kama sio wametokea porini, basi kazi zao ni ngumu, kutokana na mavazi yao ya kufanana na walivyovaa, yaan suruali nyeusi chakavu na tishert nyeusi nazo zilizo choka choka, tofauti na Kadumya ambae ukiachilia mindevu yake iliyozunguka mdomo wake, na kujaa kidevuni na licha ya kuvaa nguo alionekana kuwa mwenye hali nzuri tu, kuanzia mavazi ambayo ni suruali nyeusi na tishrt nyeusi, kama wenzake, ila yeye mavazi yake yalionekana kuwa mapya,


“kwanza kabisa, silaha tumesha lipia, zitaingia hapa baada ya miezi mitatu, hivyo askari waendelee kufanya mzoezi, na kuisoma vyema ramani ya ngome ya mfalme na makambi yote ya jeshi yaliyopo mipakani na hapa TTC (Trench Town City) hasa yale yenye silaha nzito” alieleza Chitopelah, ambae alikuw amevalia koti refu jeusi, na kofia kubwa yenye masikio ya duara, yaani jangle hut, “kikubwa cha kuzingatia ni kwamba usiri uongezwe maana mfamle ameanza kuhoji juu askari wanao ondoka jeshini, hakikisheni habari za kikundi chetu hazivuji hata kidogo,” alisisitiza Chitopelah, ambae kiukweli ana tamaa ya kuitawala nchi hii yenye utajiri kubwa.


Tamaa ambayo alipewa na wafanya biashara na matajiri, ambao pia kwa namna moja au nyingine, walikuwa wanazitamani mali za nchi hiyo ya #mbogo_land, ambayo inaongozwa kifalme, ni baada ya kukosa njia ya kuzipora mali za nchi hiyo, ambayo haijawahi kuongozwa na kiongozi mwenye tamaa, ambae angeweza kuuza hovyo mali za nchi yake.


Chitopela baada ya kupewa mchongo huo, huku akiahidiwa kupewa msaada, mara baada ya kuanza mapinduzi, anaamua kuanza harakati za mapinduzi, ambazo kwake ilikuwa rahisi sana kulianzisha jambo hilo, mwanzo aliwashawishi baadhi ya askari wenzake na wenye tamaa, pasipo kujali ukubwa wa vyeo na kufanikiwa kumpata Kadumya, ambae alikubali kuingia kwenye mchakato huo, na baada ya hapo akapanga mpango wakupunguza nguvu ya ulinzi ya nchi hii, ambapo alitengeneza uzushi wa uwepo wa wasaliti serikalini na kumshawishi mfalme kutoa kibali cha kuwa maliza wasaliti wote.


Kibali kile kilipokubaliwa ndipo Chitopela, alipochukuwa faida na kuanza kuuwa watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama, ambao kwa namna moja au nyingine ni viungo muhimu na msaada mkubwa katika nchi hii ya #mbogo_land, huku akiongeza ya kwake na kuzifyekelea mbali familia za wapiganaji hao, ili asitokee hata mmoja kuja kulipiza kisasi hapo
siku za baadae, na ukiachilia kupunguza nguvu ya ulinzi na usalama, ambayo ingekuwa kikwazo kwake.


Chitopela alihakikisha kuwa matukio ya operation ile, yana mchafua mfalme Eugen na kuharibu sifa ya serikali yake, kwa kuuwa wanausalama na familia zao, kitu ambacho kilifanikiwa na baraza la usalama la umoja wa mataifa kutoa onyo kali kwa mfalme Eugen, ambae alipinga vikali tuhuma hizo, sababu hakuwa anafahamu lolote juu ya uonevu na mauwaji ya familia za wanausalama wake, nakuonya baraza ilo lisiingilie maswala ya nchi yake, akidai kuwa, ndiyo chanzo cha migogoro na vita visivyo isha, huku mfalme huyo akiamini kuwa pengine umoja wa mataida ndio chanzo cha kikundi hicho kinachodai serikali ya uongozi wa Democrasia.


Naam baada ya kuhakikisha amesha punguza wanausalama ambao wangekuwa kikwanzo kwake, pia alihakikisha anapandikiza chuki kati ya mfalme na tajiri mmoja mkubwa, ili aichukie serikali na badae amshike akili, ili aweze kumsaidia katika kuhudumia askari wake katika mapinduzi ya serikali ambayo tayari atakuwa anaichukia.


Na hapo ndipo Chitopela askari aliesomea propaganda na ushawishi, katika chuo cha uongozi na siasa cha P R C huko ujerumani, alipo mwingiza bwana James Stiven, tajiri mkubwa sana pale #mbogo_land, katika orodha ya wahusika na wanachama wa UMD, kama mfadhiri mkuu, huku akijuwa fika kuwa yeye ndie mkuu wa chama hicho na baada ya kuhakikisha ameingia kwenye orodha ya watu wanao tafutwa kama wahaini, akamtuma mtu amjulishe tajiri James juu ya msako unaona muhusu, na yeye kumshauri akimbie kabla haja kamatwa.


Baada ya kuhakikisha amekamilisha mipango ya mwanzo, bwana Chitopela akatulia kusahaulisha serikali swala hilo na kuaminisha serikali kuwa ameweza kudhibiti waasi na wasaliti, lakini miaka ishirini baadae akiwa amesha kabidhiwa uwaziri wa ulinzi wa nchi hii tajiri, ndipo alipoamua kuiba baadhi ya silaha toka jeshini, huku anakusanya vijana wa nchi jirani, walioingia #mbogo_land, kwaajili ya kusaka maisha na kuwaingiza kwenye jeshi lake kwa ushawishi wa kuwa na maisha mazuri wakati huo huo akiendelea kushawishi askari wengine ambao ni vijana kutoroka jeshini, na kwenda kuwa wakufunzi na wapelelezi katika jeshi lake, akiwahaidi madaraka na maisha mazuri katika serikali yake mpya.*******


Naam saa nne usiku ndio mida ambayo, Neela na Deus, waliagana na mzee Ajun na mke wake na kila mtu kuelekea sehemu ambayo alipaswa kulala na hapo ndipo Deus alipogundua kuwa heshima katika familia hii tajiri ya bwana Ajun ni ya hali ya juu, maaana walitakiwa kudanganya kuwa kila mmoja analala chumba chake kwa kuendelea kukaa pale ukumbini, wakiendelea kupata vinywaji vyao na baadae wakaingia chumbani ambako hakukuwa na muda wa kuangalia video maana muda wote walikuwa wanapeana dudu ungesema wametoka jela.*******


Naam siku ya pili wa kwanza kuamka ni Sheba, ambae mpaka saa mbili asubuhi alikuwa amesha tembea zaidi ya kilomita mia mbili hamsini, alisha pita nangukurukuru na sasa alikuwa analitafuta Daraja la mkapa lililopo kwenye mto mkubwa sana wa Rufiji, akielekea jijini dar es salaam kwa speed ya ajabu, akiwagi ndge ambayo ilikuwa inatarajiwa kushuka muda mfupi ujao katika uwanja wa kimataifa wa walimu Nyerere. nakukabidhi gari kweye ofisi za kampuni ya ndege ya bwana Ajun.


Pia huyo ndio mida ambayo, kijana wetu Deus na mschana Neela wakiwa na wazazi wa Neela, walikuwa wamesha fika entebe uwanja wa ndege, ambako Deus alikuta tayari mizigo aliyoletewa na wazazi wa Neela tayari ilikuwa imesha pakiwa kwenye ndege ambayo Deus angeondoka nayo dakika chache zijazo. .…….endelea…. kufwatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA HAMSINI NA SITA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA TANO: Pia huo ndio mida ambayo, kijana wetu Deus na mschana Neela wakiwa na wazazi wa Neela walikuwa wameshafika entebe uwanja wa ndege, ambako Deus alikuta tayari mizigo aliyoletewa na wazazi wa Neela tayari ilikuwa imesha pakiwa kwenye ndege ambayo Deus angeondoka nayo dakika chache zijazo. .…….endelea….

Saa tatu kasoro ndege binafsi ya bwana Ajun iliachia ardhi na kuelekea usawa wa anga la sudan ya kusini mpaka Ethiopia ikifuatiwa na ndege ambayo ilikuwa imewabeba wakina Deus, ambayo iliondoka saa tatu na dakika tano, ikitumia dakika arobaini na tano kutua dar es salaam, dakika kumi na tano kabla Sheba hajasimamisha gari kwenye geti la DIA, Dar es salaam Internatonal Airport, akitarajia kusafiri dakika thelathini zijazo na ndege aliyokujanayo Deus.

Naam ile Deus anashuka tu toka kwenye ndege, akaliona gari la jeshi la ulinzi lenye rangi ya kijani, mstari mwekundu katikati na maandishi makubwa mawili yenye langi nyekundu MP, pembeni yake wakiwa wamesimama askari wa jeshi la ulinzi waliovalia mavazi yao ya kijeshi na kofia ngumu za rangi yeupe na maanishi mekundu ya MP kama wanne hivi, walishikilia marungu na pingu wakiwa wamesimama wanatazama ngazi za ndege ile ambayo ilibeba waheshimiwa.

Ile Deus anashuka tu wale askari nao wakamfwata, “Private Deus Nyati, upo chini ya ulinzi wa polisi Jeshi safari mahakama kuu ya jeshi, utakiwi kufanya lolote la kijinga, vinginevyo utatengeneza picha mbaya mbele ya raia” alisema askari mwenye cheo cha sajent, tayari Deus alikuwa amesha lijuwa hilo kuwa litamtokea, “ndiyo afande lakini kuna mizigo yangu kidogo, bado haijashushwa toka kwenye ndege” alisema Deus ambae hakujuwa mizigo hiyo ipo mingapi, “hakuna shida mizigo yako itasubiriwa” alijibu yule sajent, kisha Deus akaongozana na MP, kuelekea kwenye gari, ambako alipakizwa nyuma ya gari lile la wazi na kusubiri mizigo ishushwe toka kwenye ndege.

Naam dakika chache baadae, mizigo ikaanza kushushwa toka kwenye ndege, huku MP wawili wakisimamia mizigo ya Deus, ambayo hata Deus mwenyewe hakuwa ameiona hapo mwanzo, MP wakashuhudia mzigo ikiendelea kushushwa, ambayo pasipo kujuwa mizigo ya nini, zaidi waliona mabegi machache ya ukubwa wa wastani na masanduku kumi makubwa yenye kufanana, huku mabegi yakichukuliwa nakupakizwa kwenye viberenge na kupelekwa kwenye jengo la VIP huku masunduku yakipangwa pembeni.

Naam baada ya kumaliza kupanga masanduku yale, mfanyakazi mmoja wa ndege akasogelea gari la jeshi, “samahani mheshimiwa mizigo ipo tayari, unaweza kusogeza gari ipakizwe” alisema yule mhudumu wa ndege upande wa mizigo, yani cargo huku anamtazama Deus.

Mpaka hapo tayari Deus na wale askari wenzake walisha juwa ni mizigo ipi inazungumziwa, hata Deus mwenyewe alishangaa, maana hakutegemea kuwa mizigo yenyewe ingekuwa mingi na mikubwa namna ile.

Dakika kumi zilitumika kupanga mizigo ndani ya gari lile, aina ya land rover diffender na safari ya kuelekea makao makuu ya jeshi ikaanza, gari lilitembea taratibu kupitia upande wa kambi la jeshi la wanaanga, wote walikuwa kimya ndani ya gari, kila mmoja akitafakari ya kwake, wakti wale askari waliomfwata Deus wakiwa wanawaza juu ya masunduku aliyokuja nayo Deus, ambae alikaa kwa muda mfupi nchini Congo, wakati huo huo Deus yeye alikuwa anawaza kinachoenda kumkuta huko makao makuu ya jeshi.

Naam! gari lilitoka nje ya geti la askari wa anga, na kuingia barabara kuu itokayo ukonga na kuanza kushika barabara kuelekea upande wa kulia, yaani kuelekea tazara sambamba na magari mengine yaliyokuwa yanaelekea mjini, Deus alipata kuyaona mazingira ambayo, alikuwa hajayaona kwa miezi kadhaa, mji ulikuwa umechangamka, watu wanaendelea pilika zao, wengine kwa miguu wengine piki piki na magari, kitu kilicho amsha hisia zake na kukumbuka ndoto zake ni walipopishana na gari dogo jeusi, aina ya BMW S7, walilopishana nalo wakati wanakatiza maeneo ya geti la uwanja wa ndege, ambapo aliliona gari la ndoto yake lililokuwa lina ingia hapo airport.

Lilikuwa gari zuri sana, jipya gari ambalo unaweza kuzurula wezi mzima pasipo kuliona, hapa jijini Dara es salaam, gari ambalo Deus alipanga hatokwenda kwao songea pasipo kuwa nalo, kwa maana mara tu baada ya kumalizana na wakubwa wake makao makuu, angeenda kwenye tawi la BMW kuaanza taratibu za kununua gari hilo, kwa mawazo hayo, Deus alijikuta anatabasamu huku analisindikiza kwa macho gari lile la kisasa na lenye nguvu.

Huyo alikuwa mschana Sheba, ambae sasa alikuwa anasogelea gate, huku ndani ya eneo la maegesho la magari la uwanja wandege, teminal namba moja, akiona magari mawili meusi yaliyo pandishwa vioo vyeusi mpaka juu, watu wanne wakiwa wamesimama nje ya magari hayo, macho yao yakizibwa na miwani meusi kama suit zao nyeusi walizo vaa, lakini ghafla simu yake ikaanza kuita, akatazama kwenye dash board ya gari kuona jina la mpigaji, akagundua kuwa alikuwa ni Boss Atshen, akaipokea simu huku gari likiwa linaenda taratibu kusogelea geti, “Sheba, usiingize gari uwanja wa ndege, kuna taarifa kuwa tayari wanausalama wa wapo hapo wanataka kukukamata, na inawezekana kabisa kuwa wanahitaji hizo dhahabu” ilisikika sauti ya Atshen, akiongea kwa haraka na wasi wasi, “boss nipo getini na nina waona watu ambao nadhani ndio wenyewe, nifanyaje?” alisema Sheba, huku anasimamisha gari mita chache toka lilipo gate, na kutazama kwenye side mirror, kuangalia kama anaweza kugeuza kwenye ile njia ya kuingilia, ambako kulikuwa na magari kadhaa, ambayo nayo yalikuwa yamesimama, “fanya unachoweza kuokoa huo mzigo, tumeweka fedha nyingi sana” ilisikika sauti ya upande wapili sauti ambayo ni ya bwana Atshen na wakati huo zilisikika honi za magari ya nyuma.

Ni kweli nyuma kulikuwa na magari kadhaa, ambayo nay yalikuwa yamesimama yakisubiri kuingia, “nafahamu boss, lakini nashindwa kugeuka magari yameziba nyuma” alisema Sheba, huku anatazama kule kwenye geti, ambako kulikuwa na mlinzi wa geti lile aliekuwa anasogelea gari la sheba, yaani BMW 7, “sikia sheba, jitahidi kutoka hapo nenda kwenye maficho yeu ya kule relini” alisema Atshen na hapo sheba akapeleka mkono kwenye vungu ya seat na kutoa bastora yake na kuiweka pembeni ya seat, karibu na gia, kisha akaachia brake ya gari nalo likaanza kutembea taratibu, likisogelea geti hata yule mlinzi alipoona hivyo, akasimama na kurudi getini.

Sheba alifika getini, na kulipia fedha ambayo ilitakiwa geti likafunguka na yeye akaingia ndani yageti, lile huku macho yake yakiwatazama wale jamaa waliosimama nje ya magari yao, wakimtazama kwa umakini mkubwa, Sheba akaendesha gari taratibu kwa mtu ambae alikuwa analitazama gari lile angesema kuwa dereva alikuwa anatafuta sehemu ya maegesho.

Kitu ambacho msomaji unapaswa kufahamu kuwa kuna watu walikuwepo hapo uwanjani wakiwa wameelekeza macho yao, kwenye BMW jeusi huku muda wote wakiongea kwa sauti za chini na ishara, “oya, msiwe na haraka subirini mpaka asimame ashushe mzigo ndio tunamfuata” alisema mmoja wao, huku wakiwa wanalitazama gari lile, ambalo sasa lilikuwa linaelekea upande wa kulia wa maegesho, ambako ndio upande wa kushoto wa eneo lile, kama ukiwa ndani na ndiko kwenye barabara ya kutokea.

Taratibu waliliona gari linaenda moja kwa moja mpaka karibu na lango la kutokea, kisha likasimama mita kama kumi hivi toka getini, wakiwa wanasikilizia dereva ashuke, mara wakamuona mlinzi wa geti la kutokea akilifwata lile gari, kama vile aliitwa na dereva, akasimama kwa muda mfupi kwenye dirisha la gari upande wa dereva kisha akarudi getini, akiliacha lile gari limesimama pale pale, huku jamaa wenye magari meusi na Suit nyeusi wakiamini kuwa kutokana na ugeni Dereva alikuwa anaulizia sehemu anayotakiwa kuanzia utaratibu wa kukabidhi mzigo.

Lakini haikuwa hivyo, ukweli ni kwamba, mara baada ya kusimamisha gari, Sheba akashusha akaificha bastora yake na kushusha kioo, halafu akamuita mlinzi, ambae alimfuata mara moja, “samahani kaka sikujuwa kama huku ni uwanja wa ndege, nahitaji kutoka” alisema Sheba kwa sauti nyororo ya yenye kuombeleza, yule mlinzi akacheka kibwege, “hahahaha, unapoteaje sasa, ila sishangai maana wengi wanapoteaga” alisema yule mlinzi huku akimalizia kicheko chake, Sheba nae akacheka kidogo, “ok! sogeza gari” alisema yule mlinzi huku anaanza kutembea kuelekea getini,

Naam ile mlinzi alipolifikia mara ghafla wakamuona mlinzi akifungua geti, na hapo wale waliovaa suti nyeusi wakaliona gari aina ya BMW, likichomoka kwa speed, kama vile dereva amekanyaga mafuta kwa bahati mbaya, na kupita pale getini kwa speed ile ile, “oya! ingieni kwenye gari anaondoka yule” alisema mmoja wao na hapo wakaanza wote wanne wakaingia kwenye magari yao, ambamo mlikuwa na madereva, ambao tayari walikuwa wameshawasha magari, “endesha gari haraka, atakuwa ameshashtuka yule” alisema mwingine wakati magari yao yanaondoka kuelekea kwenye geti la kutokea.

Mpaka wanavuka geti hawakuweza kuliona gari lile wala alama yake kwa mbali lilikuwa limetoka eneo lile, hakika ilikuwa ni kasi ya ajabu, “tumesha mpoteza” alisema mmoja wao kwa sauti iliyojaa ghadhab, “lakini bwana Mbwambo, si ulisema mchongo huu dereva hawezi kuukwepa sababu hajuwi chochote, sasa mbona ameshtukia kama anafuatiliwa?” aliuliza mmoja kati ya wale waliovaa suit nyeusi, “tumuulize Enock yeye ndie aliesema kuwa dereva hajui lolote” alisema yule alieitwa Mbwambo, ambae hata kwa umri, alionekana mtu mzima, “lakini si niliwaambia kuwa kadumya ndie alie eleza hivyo” alijibu Enock, ambae muonekano wake ni kijna wakati ya miaka 24 au 25, “tunafanyaje sasa?” aliuliza Mbwambo, huku wakiegesha gari pembeni na jingine la nyuma yao nalo lika simama nyuma yao kwenye kituo cha dala dala cha poster ya Ukonga, “ni kitu rahisi sana, tutawanyike jiji zima kulisaka lile gari, yapo machache sana hapa dar es salaam, isitoshe dereva wake ni wakike, tutalitambua kwa haraka sana” alisema yule kijana.

Huyo ni luten Enock Kafulu, askari mtoro wa jeshi la ulinzi la#mbogo_land, alie bobea katika ushushu, yani upelelezi wakificho na ujasusi …….endelea…. kufwatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
wewe niwakupigwa makwenzi
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA HAMSINI NA SABA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA SITA: aliuliza Mbwambo huku wakiegesha gari pembeni na jingine la nyuma yao nalo likasimama nyuma yao kwenye kituo cha dala dala cha poster ya Ukonga, “ni kitu rahisi sana, tutawanyike jiji zima, kulisaka lile gari, yapo machache sana hapa dar es salaam, isitoshe dereva wake ni wakike, tuta litambua kwa haraka sana” alisema yule kijana, Huyo ni luten Enock Kafulu, askari mtoro wa jeshi la ulinzi la#mbogo_land, aliebobea katika ushushu, yaani upelelezi wakificho. …….endelea….


Ndie yule ambae utoro wake umemshtua king Elvis wa #mbogo_land, “basi lifanyike haraka hilo, si unajuwa inabidi ukakutane na mchumba wako leo mchana” alikumbusha bwana Mbwambo, ambae kwa hapa dar es salaam yeye ndie mwenyeji kuliko wengine wote na hapo wakaanza kupanga muundo wao na barabara watakazo pitia katika msako wa BMW S 7, linaloendeshwa na mwanamke.*******


Naam, gari aina ya Land Rover defender lilienda moja kwa moja mpaka upanga na kuingia ndani ya uzio wa eneo hili la makao makuu ya jeshi, na wote wakashuka, baada ya hapo Deus akapewa nafasi ya kubadili nguo zake toka zile za kiraia na kuvalia sare za kijeshi, ambazo alikuwa naz kwenye begi lake kubwa aliloltokanalo Congo, kisha akapelekwa moja kwa moja mpaka kwa mkuu wa polisi jeshi, ambae jakujiuliza mara mbili, aliagiza Deus Frank afikishwe mahakani sita kamili.


Kitu ambacho hakuna alieamini, hata wale MP waliomfuata airport ni mwenendo mzima wa kesi ya Deus ya kuharibu sifa na taratibu za jeshi, ambapo mpaka kufika saa saba mchana, tayari alikuwa amesha hukumiwa kuachishwa jeshi kwa utovu wa nidhamu, hukumu ambayo ilimtaka Deus Nyati ajaze form maalumu ya kuachishwa kazi, ambayo itaelekeza baada ya hapo ataenda kuishi wapi, akapewa millioni mbili ambazo ni nauli yake peke yake ya kurudi kwao, maana hakuwa na vitu vya kusafirisha wala familia, kwa hiyo alikuwa askari kapela, au unaweza kusema ni Single (Singo)*******


Naam nje ya mji wa kisarawe kwenye vichaka vya Mdidimue, kilomita moja toka barabara itokayo kisarawe kwenda Kibaha, pembezoni mwa njia ya treni, yani reillway, nikama mita mia mbili toka ilipo njia hiyo ya tren ya kati, yani TRC, ilionekana nyumba moja ndogo, ambayo licha ya upya wake, lakini ilionekana chakavu, ni kutokana na kutokumaliziwa ujenzi.


Madirisha yalikuwa na nguzo zenye nondo tu, pasipo vizingiti, mlango ulikuwa dhaifu, haikuwa na sakafu wala kuta hazikuwekwa plasta, huku nyumba hii ikiunga nishwa na maegesho ya magari ambayo kiukweli ungesema linafugiwa mifugo flani, kama vile ng’ombe au mbuzi, maana halikuwa na hadhi ya kulala gari lolote hata Vitz la mbogo Edgar, ukiachilia lango lake la bati, lililkuwa limeshikiwa kwa kamba ya katani, pia bati zile zilikuwa zimechakaa kama bati la paa la jiko la shule au choo cha shimo.


Achana na muonekano wa nje wa nyumba hii, ambayo ilikuwa imezungukwa na vichaka, ndani kulikuwa na vyumba vinne vya kulala, na jiko, choo cha na bafu, katika vyumba vile vinne ni kimoja tu ndio kilikuwa na mlango, tena mlango wa bati ambao hata mtoto akiusukuma ungefunguka bila kikwazo chochote.


Naam tunapoingia ndani ya chumba hiki chenye kitanda kidogo, chenye kuwekewa neti na kutandikwa shuka chakavu, basi tunakumbuka, kuna mtu aliwahi kuingia ndani ya chumba hiki, wacha nasisi tutumie njia aliyopita yeye.


Tunainua kitanda na kugusa sehemu ya fulani kwenye sakafu ya uvunguni mwa kitanda, ardhi ina sogea pembeni kidogo na hapo tunaona ngazi zinazo elekea kule chini ambako kuna giza kweli kweli, hatuna budi kukabiliana nalo, maana tunahitaji kujuwa kilichopo hum ndani, hivyo tuna shuka nalo, tuna papasa ngazi, lakini kila tunapozidi kushuka ndivyo tunavyoweza kuona mwanga, nikama kuna nyumba nyingine huku chini.


Jibu tunalipata baada ya kukuta mlango mwingine na kuufungua, tuna kutana na sehemu kubwa ya wazi yenye mwanga wa kutosha, sehemu ambayo sio tu kuwa na mfanano na sehemu ambayo inaweza kutumika kama sebule, kwa jinsi ilivyotengenezwa kwa vigae vya kung’aa (taylez) na kung’alishwa kwa ranginzuri kwenye kuta zake, pia ilikuwa pana yenye taa nzuri za kupendeza.


Lakini cha kushangaza, sehemu hii tunalikuta gari aina ya BMW S7 jeusi, nilile ambalo tulianza kuliona mtambaswala kule masasi, ndio lile analoendesha Sheba, ambae lisaa limoja lililopita, alikuwa ana wakimbia wakina Mbwambo, kule airport, sasa yenye mwenyewe yupo wapi.


Hapo tuna fungua mlango mmoja na kuibukia kwenye sehemu kubwa ambayo ni wazi kuwa inatumika kama sebule, maana palikuwa na kila kitu ambacho nikielelezo cha kuwa hii ni sebule, yanye seating room dianing room na jiko, ilikuwa ni ramani nzuri sana, yenye muonekano wa mkazi asie na mambo mengi, palikuwa na makochi mazuri ya kisasa, meza nzuri ya kioo, TV kubwa ya kisasa, seti ya music, pia kulikuwa na meza kubwa ya chakula ya kisasa, iliyozungukwa na viti sita vya kisasa vilivyopo karibu na meza kubwa mfano wa counter iliyo tenganisha jiko lenye kila kitu na ukumbi huo wa chakula, huku upande wakulia wa meza ile ndefu, kukiwa na kabati moja zuri la ukutani, lenye vinywaji vya kila aina, vingi kiwa ni pombe sambamba na friji dogo la vinywaji.


Lakini hapo hatumuoni Sheba, tuna tazama milango mitano inayoonekana mbele ya macho yetu, ukiachilia ule ambao tumeingilia toka kwenye ukumbi wenye gari, tuna chagua mlango mmoja ambao tunaufungua na kukutana na chumba ambacho kinafanana kabisa na chumba cha matibabu, ambacho ukiachilia kitanda cha kupumzishia mgonjwa pia kina vifaa vingi vya kitabibu na makopo na box za dawa, mashine za vipimo na vifaa vya kimaabara, lakini Sheba hayupo.


Tuna toka na kuingia chumba kingine, ambacho tuna kutana na chumba kikubwa mfano wa ghala, ambalo lilikuwa tupu, hii inaonyesha kuna mizigo kama sio huwa unaifadhiwa humo, basi ilikuwa inahifadhiwagwa humo, hatuna budi kutoka na kufungua mlango wa tatu, ambao ni choo na bafu, hatukai tuna toka na kuingia chumba cha nne, ambacho ni chumba kikubwa cha kulala, chenye vitanda viwili, vya dabo deck, yaani kila kitanda kilikuwa na sehemu mbili za kulala, juu na chini, pia kulikuwa na bafu na choo, TV na meza ndogo, kabati la nguo na kioo kikubwa, lakini Sheba hayupo, tunaingia chumba cha tano.


Hiki nacho ni chumba cha kulala, chenye kitanda kimoja tu, kikubwa cha kisasa, kochi moja dogo la watu wawili kabati kubwa la nguo, meza ya kioo, friji dogo, TV pia bafu na choo, na kila sehemu tuliypita kulikuwa na kiyoyozi, yani A/C, kwa maana ya air condition.


Ndani ya chumba hiki kikubwa tunamkuta Sheba, mschana mrembo mwenye asili ya kihabeshi, alie kuwa amejilaza kwenye kitanda kile kikubwa, huku amevalia suruali nyeusi ya kubana na kijinguo fulani ambacho, ungeweza kusema ni gauni tishet, lakini lenye kuishia mapajani mwa mschana huyu aliejaliwa uzuri wa umbo na sura, na hata pale kitandani alipojilanza chali, akikunja miguu yake kwa mtindo wa nne, huku ameweka simu sikioni kwa maana ya kungea na mtu, ungeweza kuona jinsi hips zake zilivyo tawanyika na kuchomza pembeni.


Tuachane na hips za Sheba, tuwe makini na simu aliyokuwa anaongea nayo, “boss mpaka sasa hatuja juwa ni nani anaetufutilia, na kama ni wanausalama, basi hivyo na ninavyojuwa kwa hapa Tanzania muda si mrefu watagundua maficho yetu na kunikamata na ukichukulia kuwa tayari airport siwezi kuingia” alisema yule mschana kwa sauti yake tamu ya kulalamika, “sikia Sheba, kama unavyojuwa airport imeshindikana, lakini usiwe na wasi wasi ndani ya masaa machache yajayo tutakuwa tumesha pata njia ya kuondoa hizo dhahabu hapo Tanzania, ilisikika sauti nzito upande wapili, ambayo tuna ifahamu kuwa ni sauti ya Atshen, “mh! boss ni njia gani nyingine ya kusafirisha dhahabu kilo hamsini?” aliuliza Sheba kwa sauti yenye mshangao, “hatuna njia nyingine zaidi ya njia ndefu ambayo ni njia ya barabara” alisema Atshen,


Lakini ilionekana kuwa ni ngumu kwa Sheba, “boss, ukweli ni kwamba, hii inaweza kuwa hatari sana, tafuta njia nyingine, hii itafanya maadui zetu watufikie kirahisi sana” alisema Sheba, huku kwa sauti yenye kuonya, “Sheba, vyovyote itakavyokuwa, lazima mzigo ufike ukiwa salama, nitakupigia baadae kukupa mpango kamili” alisema Atshen kwa sauti yenye hali ya kutoa amri na kulazimisha, “lakini Boss, itawezekana kweli kilo hamsini za dhahabu, tusafirishe kwa gari?, polisi maliasili majambazi na wanyang’anyi wote nitawakwepaje, na vipi hawa walioanza kunifuatilia nita waepuka vipi?” aliuliza yule mschana huyo ambae kiukweli hata ukimtazama kwa macho umri wake bado mdogo, lakini tayari simu ilikuwa imesha katika.


Saa nane na nusu ndio muda ambao tayari Deus alikuwa ameshatoka nje ya lango la makao makuu ya jeshi akiwa kama raia wa kawaida, tayari alikuwa amesha kabidhi nguo na vifaa vyote vya jeshi, alishapewa fedha ambayo angetumia kama nauli ya kufika nyumbani kwa wazazi wake huko songea sasa Deus, alikuwa amesha pakiza mizigo ile kwenye bus liendalo mkoani, kipindi hicho katika stendi ya ubungo, maana aliona itakuwa vyema kama atasafirisha mizigo ile kuelekea songea, maana yeye alikuwa na mpango wa kununua gari dogo, ambalo lisingeweza kubeba mizigo ile yote.


Baada ya kumaliza hayo yote, Deus akiwa na begi lake kubwa la mgongoni, akatoka nje ya stendi kwaajili ya kuangalia sehemu ya kwenda kupumzika, yaani Hotel ilikesho aanze taratibu za kununua gari, lakini kabla hajafanya lolote akasikia simu yake ikianza kuita, alipoitazama ile namba akashtuka kidogo, maana ukichilia namba ilikuwa ngeni, lakini pia ilikuwa ni kutoka nje ya nchi, kutokana na uelewa mdogo wa code namba, za nchi mbali mbali hakuweza kuitambua ile namba ni ya nchi gani, hivyo akahisi kuwa ni kutoka Congo, kwa kina Major Felix, hivyo akaipokea, “hello afande tayri nipo nje ya game” alisema Deus, mara baada ya kupokea simu, “hapana Deus mimi naitwa Atshen, toka Adis ababa” ilisikika sauti tulivu toka upande wapili wa simu…..…….endelea…. kufwatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA HAMSINI NA NANE
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA SABA: akasikia simu yake ikianza kuita, alipoitazama ile namba akashtuka kidogo, maana ukichilia namba ilikuwa ngeni lakini pia ilikuwa ni kutoka nje ya nchi, kutokana na uelewa mdogo wa code namba, za nchi mbali mbali, hakuweza kuitambua ile namba ni ya nchi gani, hivyo akahisi kuwa ni kutoka Congo, kwa kina Major Felix, hivyo akaipokea, “hello afande tayari nipo nje ya game” alisema Deus, mara baada ya kupokea simu, “hapana Deus mimi naitwa Atshen, toka Adisababa” ilisikika sauti tulivu toka upande wapili wa simu…..…….endelea….


Ilimshtua kidogo Deus, maana angetegemea kupigiwa na mtu kama Neela au baba yake Neela, lakini sasa anapigiwa na mtu tofauti kabisa toka Ethiopia, “unanifahamu vipi na unashida gani na mimi” aliuliza Deus alikuwa amesimama mbele ya eneo la stendi ya mkoa, pale Ubungo macho ameyaelekeza barabarani, akitazama namna ambavyo anaweza kuvuka barabara ili aende upande wa pili, akapande gari la kuelekea Kimara, ambako alipanga kukodi chumba kwenye hotel fulani, “nimepewa namba yako na bwana Ajun Serasie, nina kazi na wewe kuna gari nahitaji uliendeshe mpaka Longai mpakani, utanichaji bei gani?” aliuliza mpigaji wa simu, ambae kwa sauti yake, tuna mfahamu kuwa ni bwana Atshen, boss wake Sheba, “taja siku ya safari jina lako lengo la safari na malipo yangu” alisema Deus, ambae bado alikuwa amesimama, pale pale, “jina hakuna, safari muda wowote kuanzia sasa, nipale tu tutakapo kuwa tume kubaliana, lengo la safari ni kumsafirisha mschana ambae utamkuta na gari, malipo ni million hamsini cash” hayo ndiyo maelezo ya upande wa pili.


Deus akatulia kidogo akitafakari juu ya jambo lile, alitumia sekunde kama therasini, “million hamsini kumsafirisha mschana?” alijiuliza Deus, kabla haja ongea kwa mara nyingine, “je mzee Ajun, anafahamu juu ya hili?” aliuliza Deus kwa sauti yake tulivu, “yah! anafahamu, yeye ndie alienishauri kuwa nikutafute wewe, maana ni dereva mzuri na pia ni mlinzi mzuri” alisema mtu ambae sisi tuna mfahamu kama Atshen, “ok! kwa heshima ya Ajun, nimekubali, lakini nusu ya malipo yangu kabla ya kuanza safari” alisema Deus kwa sauti tulivu, pasipo kujali fedha nyingi alizokuwa nazo na hakuwaza kwa nini malipo makubwa kwa kazi ndogo, “ok! imekubaliwa, kazi inaanza sasa elekea kiluvya madukani, nusu saa ijayo uwe hapo, kisha subiri hapo hapo” alisema Atshen kisha simu ikakatika.


Naam Deus aliejiona mwenye bahati, aliweka simu mfukoni na kuvuka barabara wakati huo ujenzi wa barabara ya mwendo kasi ukiwa unaendelea, magari yalikuwa mengi upande wapili, lakini yalikuwa yamejaa abiria na alihitaji dakika thelathini tu kufika kiluvya madukani, sehemu aliyoelekezwa, kwa kulijuwa hilo, akaona itakuwa vyema kama ata kodi Taxi, hivyo moja kwa moja akasogea kwenye maegesho ya Taxi, na kuingia kwenye moja kati ya magari yale, “nipeleke kiluvya madukani” alisema Deus huku anajiweka sawa kwenye seat ya nyuma ya abiria.******


Msako ulikuwa mkali sana, kwa kina Mbwambo, waliojigawa makundi matatu, kila kundi likiwa na gari lake, na kila gari likiwa na watu wasiopungua wanne, na kila kundi likiwa upande wake, katika jiji hili la dar es salaam, walizunguka kila kona na kila chochoro, pasipo mafanikio yoyote, simu ziliendelea kumiminika #mbogo_land, kwa Kadumya akisisitiza kuhusu umuhimu wa kupatika kwa zile dhahabu, ambazo zingesaidia kupatika kwa fedha za posho za askari wao waliopo msituni, na wengine ambao walikuwa wanaendelea kushawishiwa na kujiunga na kikundi chao.


Taarifa hizo hizo, zilizidi kumshanga na kumvuruga waziri Chitopelah, ambae kiukweli, hakutaka kuamini kuwa kilo hamsini za dhahabu, anapishana nazo, kirahisi vile, japo fedha ya mzigo ule alishalipwa, lakini alikuwa na uhitaji mkubwa wa fedha, kwa kipindi hiki cha maandalizi ya mapinduzi, aliyopanga kuyatekeleza miezi mitatu ijayo.


Chitopela kwa kuona kuwa anakaribia kupoteza dhahabu, kilo hamsini, akaona kuwa inafaa atumie akili zaidi, nayo ni kushirikisha mtu mwingine nje ya UMD, hapo akawasiliana na rafiki yake bwana Keneth Paul Ulenje, kamanda wa polisi, mkoa wa kipolisi wa Ilala, ambae alifahamiana nae katika kikao cha ulinzi na usalama wa bahari ya kusini mashariki mwa afrika, kilicho jumuisha wajumbe toka nchi za Tanzania #mbogo_land na Msumbiji, na kumweleza juu ya jambo linalo msumbua, “bwana Chitopela umebugi sana, kitu ambacho umesahau ni kwamba, kuna njia nyingi za kutokea hapa dar es salaam na hata Tanzania kwa ujumla, lakini hatujachelewa, ngoja tuzuwie njia zote zinazoenda kwenye miji yenye viwanja vikubwa vya ndege, ikiwa pamoja na mwanza na Kilimanjaro, pia mipaka ya karibu, tanga na kilimanjaro na arusha, we andaa posho kwaajili ya vijana, pia nitumie muonekano wa gari na namba zake” alisea CP Ulenje, kwa kujiamini kabisa, akimpa uhakika bwana Chitopelah, matumaini ya kupata mzigo wake.*******


Makao makuu ya jeshi, mida hii ya saa nane na dakika ishirini na nne kuelekea ishirini na tano, watu walionekana wakiwa wamejaa kwenye ubao mkubwa wamatangazo ambayo utolewa kila siku, kama amri namba moja ya kila siku, tofauti na siku nyingine ambazo, askari husoma tangazo hilo kwa uchache na wengine huagiza wasomewe, lakini leo watu walikuwa wamejaa kwa wingi wakisoma kipengele cha matokeo ya mahakaman ya askari Deus Nyati, ambae alihukumiwa kufukuzwa kazi,


Hakika habari hii, ili msisimua kila mmoja, aliekuwepo eneo lile, ni kutokana na watu wengu kufahamu kilichomtokea huko DRC, hakika kila mmoja alilipokea kwa namna yake swala hili, wapo walio ona kuwa Deus, hakutendewa haki, maana mahakama ilisha thibitisha kuwa Deus hakuwa na hatia, ni baada ya mschana aliedaiwa kunusurika kubakwa, kueleza mahakama kuwa, alilazimishwa kusema hivyo, ilihali hakuwa amefanyiwa kitendo hicho na bwana Deus, huku wengine wakisema kuwa, jambo hili lilihitaji busara zaidi na sio kuchukua maamuzi kwa haraka, na wapo walio ona alistahili adhabu ile, kwanini aliamua kusaidia watu baada ya kuzingatia jukumu lililo mpeleka huko DRC.


Wakati askari wa kawaida wakijadili jambo hilo, kutokana na upeo wao, lakini wakati hu huo, katika jengo la idara ya mafunzo na utendaji kivita, mlango wa ofisi ya mkuu wa idara hiyo, Major general, Mbike Kifimbo, ulifunguliwa kwa ghafla na kwa nguvu, ungesema ndani ya ofisi hiyo kulikuwa na watu wanagombana, kiasi cha kumshtua hata secretary wake, aliekuwa anamalizia kazi na kujiandaa kuondoka, maana muda wakazi ulibakiza dakika chache sana, “Stella, kuna taarifa yoyote ilikuja hapa kuhusu hii mahakama ya Deus Nyati?” aliuliza gen Kifimbo, kwa sauti ambayo ilionekana wazi kuwa na ghadhab ya hali ya juu, “hapana afande, hata mimi nimeona kwenye tangazo kuwa Deus Nyati amehukumiwa kufukuzwa kazi” alijibu askari wakike aliekuwepo kwenye kile chumba cha karani wa mkuu huyu wa mafunzo jeshini, ambae alionekana kuchukizwa zaidi.


Gen akarudi ndani ya ofisi na kufunga mlango, kisha akasogelea meza yake kwa lengo la kuchukuwa simu, kwa maana alitaka kupiga sehemu, lakini ile anaishika tu na simu yake ikaita, alipo itazama simu, Gen Mbike alijihisi kutetemeka, maana aliona jina limeandikwa, Afande CDF, ikimaanisha ni simu toka kwa Chief Of Difance Force, yani mkuu wa majeshi, Mbike akaipokea ile simu na kuiweka sikioni, “jambo afande” alisalimia Gen Mbike, na hata kabla salamu haijajibiwa tayari akakutana na swali, “kwahiyo umempokea askari kimya kimya, halafu ukamhukumu kimya kimya, ukakubaliana na mkuu wa uajili mumfukuze kazi, na mimi muna nipa taarifa kuwa askari amefukuzwa kazi, sasa mimi kazi yangu ni ipi? na mataifa mengine yatatuonaje hata baaa ya askari kufanya makubwa yaliyo tuletea sifa jeshi na nchi yetu, bado mna mfukuza kazi kwaajili ya kosa la kipuuzi la kufanya kazi nje ya jukumu alilopewa, kwani nyie hamna maduka mitaani?, hamlimi mashamba yenu,? hamsaidii watu bila kulitaarifu jeshi” ilikuwa ni sauti kali yenye ukali wa hali ya juu, ikionyesha wazi ilikuwa imejaa hasira.


Ukweli ilimshangaza hata Gen Mbike, maana kwa jinsi ilivyo, ilikuwa lazima Deus, atariport kwenye ofisi yake, mara tu baada ya kufika nchini, na baada ya hapo ndipo mambo mengine yaendelee, “afande hata mimi nimeshangazwa na jambo hili, sina taarifa zozote za mwanzo, zaidi nime kuja kusikia mchana huu, kuwa askari huyu tayari ameshaachishwa jeshi, nilidhania kibali kimetoka kwako” alisema Gen Mbike, kwa sauti yenye unyenyekevu, huku akionekana kutokupendezwa na jambo hilo, “sijaidhinisha mimi afisa utawala, ndie alieidhinisha, lakini ni baada ya kuletewa ombi toka kwenu na yeye hakuwepo kwenye kikao chetu cha mwisho, ni nani alietoa wazo la kutoa hukumu kama hii?” aliuliza CDF, ambae mara ya mwisho alieleza kuwa askari Deus, asifukuzwe kazi, ila akifika taratibu za kimahakama zifuatwe na kama ni adhabu apewe ya kawaida tu, ambayo ataitumikia na kuendelea na kazi na ikiwezekana apewe onyo, ambalo pia uhesabika kama adhabu.


“ni upuuzi, hebu fuatilia ni nani alie jichukulia maamuzi hayo, kisha nipe jibu kesho saa mbili asubuhi kwenye kikao, na huyo askari atafutwe haraka kesho ariport hapo ofisini kwako, na kufutiwa adhabu hiyo” alisema CDF kwa sauti iliyo onyesha kuwa ilikuwa na hasira kali sana, kisha akakata simu, akimuacha COT, yani Chief of Treaning akiwa ameacha mdomo wazi kwa mshangao, jinsi haya mambo yalivyoenda…..…..…….endelea…. kufwatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA HAMSINI NA NANE
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA SABA: akasikia simu yake ikianza kuita, alipoitazama ile namba akashtuka kidogo, maana ukichilia namba ilikuwa ngeni lakini pia ilikuwa ni kutoka nje ya nchi, kutokana na uelewa mdogo wa code namba, za nchi mbali mbali, hakuweza kuitambua ile namba ni ya nchi gani, hivyo akahisi kuwa ni kutoka Congo, kwa kina Major Felix, hivyo akaipokea, “hello afande tayari nipo nje ya game” alisema Deus, mara baada ya kupokea simu, “hapana Deus mimi naitwa Atshen, toka Adisababa” ilisikika sauti tulivu toka upande wapili wa simu…..…….endelea….


Ilimshtua kidogo Deus, maana angetegemea kupigiwa na mtu kama Neela au baba yake Neela, lakini sasa anapigiwa na mtu tofauti kabisa toka Ethiopia, “unanifahamu vipi na unashida gani na mimi” aliuliza Deus alikuwa amesimama mbele ya eneo la stendi ya mkoa, pale Ubungo macho ameyaelekeza barabarani, akitazama namna ambavyo anaweza kuvuka barabara ili aende upande wa pili, akapande gari la kuelekea Kimara, ambako alipanga kukodi chumba kwenye hotel fulani, “nimepewa namba yako na bwana Ajun Serasie, nina kazi na wewe kuna gari nahitaji uliendeshe mpaka Longai mpakani, utanichaji bei gani?” aliuliza mpigaji wa simu, ambae kwa sauti yake, tuna mfahamu kuwa ni bwana Atshen, boss wake Sheba, “taja siku ya safari jina lako lengo la safari na malipo yangu” alisema Deus, ambae bado alikuwa amesimama, pale pale, “jina hakuna, safari muda wowote kuanzia sasa, nipale tu tutakapo kuwa tume kubaliana, lengo la safari ni kumsafirisha mschana ambae utamkuta na gari, malipo ni million hamsini cash” hayo ndiyo maelezo ya upande wa pili.


Deus akatulia kidogo akitafakari juu ya jambo lile, alitumia sekunde kama therasini, “million hamsini kumsafirisha mschana?” alijiuliza Deus, kabla haja ongea kwa mara nyingine, “je mzee Ajun, anafahamu juu ya hili?” aliuliza Deus kwa sauti yake tulivu, “yah! anafahamu, yeye ndie alienishauri kuwa nikutafute wewe, maana ni dereva mzuri na pia ni mlinzi mzuri” alisema mtu ambae sisi tuna mfahamu kama Atshen, “ok! kwa heshima ya Ajun, nimekubali, lakini nusu ya malipo yangu kabla ya kuanza safari” alisema Deus kwa sauti tulivu, pasipo kujali fedha nyingi alizokuwa nazo na hakuwaza kwa nini malipo makubwa kwa kazi ndogo, “ok! imekubaliwa, kazi inaanza sasa elekea kiluvya madukani, nusu saa ijayo uwe hapo, kisha subiri hapo hapo” alisema Atshen kisha simu ikakatika.


Naam Deus aliejiona mwenye bahati, aliweka simu mfukoni na kuvuka barabara wakati huo ujenzi wa barabara ya mwendo kasi ukiwa unaendelea, magari yalikuwa mengi upande wapili, lakini yalikuwa yamejaa abiria na alihitaji dakika thelathini tu kufika kiluvya madukani, sehemu aliyoelekezwa, kwa kulijuwa hilo, akaona itakuwa vyema kama ata kodi Taxi, hivyo moja kwa moja akasogea kwenye maegesho ya Taxi, na kuingia kwenye moja kati ya magari yale, “nipeleke kiluvya madukani” alisema Deus huku anajiweka sawa kwenye seat ya nyuma ya abiria.******


Msako ulikuwa mkali sana, kwa kina Mbwambo, waliojigawa makundi matatu, kila kundi likiwa na gari lake, na kila gari likiwa na watu wasiopungua wanne, na kila kundi likiwa upande wake, katika jiji hili la dar es salaam, walizunguka kila kona na kila chochoro, pasipo mafanikio yoyote, simu ziliendelea kumiminika #mbogo_land, kwa Kadumya akisisitiza kuhusu umuhimu wa kupatika kwa zile dhahabu, ambazo zingesaidia kupatika kwa fedha za posho za askari wao waliopo msituni, na wengine ambao walikuwa wanaendelea kushawishiwa na kujiunga na kikundi chao.


Taarifa hizo hizo, zilizidi kumshanga na kumvuruga waziri Chitopelah, ambae kiukweli, hakutaka kuamini kuwa kilo hamsini za dhahabu, anapishana nazo, kirahisi vile, japo fedha ya mzigo ule alishalipwa, lakini alikuwa na uhitaji mkubwa wa fedha, kwa kipindi hiki cha maandalizi ya mapinduzi, aliyopanga kuyatekeleza miezi mitatu ijayo.


Chitopela kwa kuona kuwa anakaribia kupoteza dhahabu, kilo hamsini, akaona kuwa inafaa atumie akili zaidi, nayo ni kushirikisha mtu mwingine nje ya UMD, hapo akawasiliana na rafiki yake bwana Keneth Paul Ulenje, kamanda wa polisi, mkoa wa kipolisi wa Ilala, ambae alifahamiana nae katika kikao cha ulinzi na usalama wa bahari ya kusini mashariki mwa afrika, kilicho jumuisha wajumbe toka nchi za Tanzania #mbogo_land na Msumbiji, na kumweleza juu ya jambo linalo msumbua, “bwana Chitopela umebugi sana, kitu ambacho umesahau ni kwamba, kuna njia nyingi za kutokea hapa dar es salaam na hata Tanzania kwa ujumla, lakini hatujachelewa, ngoja tuzuwie njia zote zinazoenda kwenye miji yenye viwanja vikubwa vya ndege, ikiwa pamoja na mwanza na Kilimanjaro, pia mipaka ya karibu, tanga na kilimanjaro na arusha, we andaa posho kwaajili ya vijana, pia nitumie muonekano wa gari na namba zake” alisea CP Ulenje, kwa kujiamini kabisa, akimpa uhakika bwana Chitopelah, matumaini ya kupata mzigo wake.*******


Makao makuu ya jeshi, mida hii ya saa nane na dakika ishirini na nne kuelekea ishirini na tano, watu walionekana wakiwa wamejaa kwenye ubao mkubwa wamatangazo ambayo utolewa kila siku, kama amri namba moja ya kila siku, tofauti na siku nyingine ambazo, askari husoma tangazo hilo kwa uchache na wengine huagiza wasomewe, lakini leo watu walikuwa wamejaa kwa wingi wakisoma kipengele cha matokeo ya mahakaman ya askari Deus Nyati, ambae alihukumiwa kufukuzwa kazi,


Hakika habari hii, ili msisimua kila mmoja, aliekuwepo eneo lile, ni kutokana na watu wengu kufahamu kilichomtokea huko DRC, hakika kila mmoja alilipokea kwa namna yake swala hili, wapo walio ona kuwa Deus, hakutendewa haki, maana mahakama ilisha thibitisha kuwa Deus hakuwa na hatia, ni baada ya mschana aliedaiwa kunusurika kubakwa, kueleza mahakama kuwa, alilazimishwa kusema hivyo, ilihali hakuwa amefanyiwa kitendo hicho na bwana Deus, huku wengine wakisema kuwa, jambo hili lilihitaji busara zaidi na sio kuchukua maamuzi kwa haraka, na wapo walio ona alistahili adhabu ile, kwanini aliamua kusaidia watu baada ya kuzingatia jukumu lililo mpeleka huko DRC.


Wakati askari wa kawaida wakijadili jambo hilo, kutokana na upeo wao, lakini wakati hu huo, katika jengo la idara ya mafunzo na utendaji kivita, mlango wa ofisi ya mkuu wa idara hiyo, Major general, Mbike Kifimbo, ulifunguliwa kwa ghafla na kwa nguvu, ungesema ndani ya ofisi hiyo kulikuwa na watu wanagombana, kiasi cha kumshtua hata secretary wake, aliekuwa anamalizia kazi na kujiandaa kuondoka, maana muda wakazi ulibakiza dakika chache sana, “Stella, kuna taarifa yoyote ilikuja hapa kuhusu hii mahakama ya Deus Nyati?” aliuliza gen Kifimbo, kwa sauti ambayo ilionekana wazi kuwa na ghadhab ya hali ya juu, “hapana afande, hata mimi nimeona kwenye tangazo kuwa Deus Nyati amehukumiwa kufukuzwa kazi” alijibu askari wakike aliekuwepo kwenye kile chumba cha karani wa mkuu huyu wa mafunzo jeshini, ambae alionekana kuchukizwa zaidi.


Gen akarudi ndani ya ofisi na kufunga mlango, kisha akasogelea meza yake kwa lengo la kuchukuwa simu, kwa maana alitaka kupiga sehemu, lakini ile anaishika tu na simu yake ikaita, alipo itazama simu, Gen Mbike alijihisi kutetemeka, maana aliona jina limeandikwa, Afande CDF, ikimaanisha ni simu toka kwa Chief Of Difance Force, yani mkuu wa majeshi, Mbike akaipokea ile simu na kuiweka sikioni, “jambo afande” alisalimia Gen Mbike, na hata kabla salamu haijajibiwa tayari akakutana na swali, “kwahiyo umempokea askari kimya kimya, halafu ukamhukumu kimya kimya, ukakubaliana na mkuu wa uajili mumfukuze kazi, na mimi muna nipa taarifa kuwa askari amefukuzwa kazi, sasa mimi kazi yangu ni ipi? na mataifa mengine yatatuonaje hata baaa ya askari kufanya makubwa yaliyo tuletea sifa jeshi na nchi yetu, bado mna mfukuza kazi kwaajili ya kosa la kipuuzi la kufanya kazi nje ya jukumu alilopewa, kwani nyie hamna maduka mitaani?, hamlimi mashamba yenu,? hamsaidii watu bila kulitaarifu jeshi” ilikuwa ni sauti kali yenye ukali wa hali ya juu, ikionyesha wazi ilikuwa imejaa hasira.


Ukweli ilimshangaza hata Gen Mbike, maana kwa jinsi ilivyo, ilikuwa lazima Deus, atariport kwenye ofisi yake, mara tu baada ya kufika nchini, na baada ya hapo ndipo mambo mengine yaendelee, “afande hata mimi nimeshangazwa na jambo hili, sina taarifa zozote za mwanzo, zaidi nime kuja kusikia mchana huu, kuwa askari huyu tayari ameshaachishwa jeshi, nilidhania kibali kimetoka kwako” alisema Gen Mbike, kwa sauti yenye unyenyekevu, huku akionekana kutokupendezwa na jambo hilo, “sijaidhinisha mimi afisa utawala, ndie alieidhinisha, lakini ni baada ya kuletewa ombi toka kwenu na yeye hakuwepo kwenye kikao chetu cha mwisho, ni nani alietoa wazo la kutoa hukumu kama hii?” aliuliza CDF, ambae mara ya mwisho alieleza kuwa askari Deus, asifukuzwe kazi, ila akifika taratibu za kimahakama zifuatwe na kama ni adhabu apewe ya kawaida tu, ambayo ataitumikia na kuendelea na kazi na ikiwezekana apewe onyo, ambalo pia uhesabika kama adhabu.


“ni upuuzi, hebu fuatilia ni nani alie jichukulia maamuzi hayo, kisha nipe jibu kesho saa mbili asubuhi kwenye kikao, na huyo askari atafutwe haraka kesho ariport hapo ofisini kwako, na kufutiwa adhabu hiyo” alisema CDF kwa sauti iliyo onyesha kuwa ilikuwa na hasira kali sana, kisha akakata simu, akimuacha COT, yani Chief of Treaning akiwa ameacha mdomo wazi kwa mshangao, jinsi haya mambo yalivyoenda…..…..…….endelea…. kufwatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
🪑
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA HAMSINI NA TISA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA NANE: “ni upuuzi, hebu fuatilia ni nani aliejichukulia maamuzi hayo kisha nipe jibu kesho saa mbili asubuhi kwenye kikao na huyo askari atafutwe haraka kesho areport hapo ofisini kwako na kufutiwa adhabu hiyo” alisema CDF kwa sauti iliyo onyesha kuwa ilikuwa na hasira kali sana, kisha akakata simu akimwacha COT, yaani Chief Of Treaning akiwa ameacha mdomo wazi kwa mshangao jinsi haya mambo yalivyoenda…..endelea…


Gen Mbike hakutaka kupoteza muda kushangaa, hapo hapo akapiga simu kwenda kwa Chief Of Defance MP, na simu ikaanza kuita mara moja.*****


Wakati huo huo kijana wetu Deus, akiwa ndani ya gari waliingia kiluvya madukani na kwenda kusimama njia panda ya kuelekea kisarawe sehemu aliyoelekezwa na na mtu aliempigia simu.


Deus alilipa kiasi cha Tsh 15000 kama malipo ya usafiri, kisha akashuka na kuchukuwa begi lake kubwa la mgongoni na kusimama pembeni ya barabara iendayo kisarawe kisha akatazama kama angeona kitu chochote ambacho kingempa ishara ya gari au mtu ambae anatakiwa asafiri nae, lakini hakuona dalili yoyote zaidi ya watu waliokuwepo eneo lile wakiendelea na shughuri zao za kibiashara, kama vile boda boda mama ntilie wa mama wauza samaki na wasafiri waliokuwa wanaendelea kusubiri daladala, huku wapiga debe wakiendelea kuwashawishi kupanda magari yale, japo nilazima wangepanda hata bila ushawishi ule wa wapiga debe.


Baada ya kuona hivyo Deus akaona kuwa ule ndio wakati ambao angeutumia kuwasiliana na wazazi wake, kuwaeleza kilichotokea kwake mara baada ya kuingia Tanzania ya kwamba amefukuzwa kazi na pia awajulishe kuhusu mizigo ambayo ameituma kwenye bus, hivyo waende kuipokea siku baada ya kesho, ambayo kwa Kiswahili inaitwa keshokutwa.


Naaam wakati Deus anaendelea kuongea na simu yake mara akaliona gari dogo aina BMW S7 jeus, likiwa linaingia pale njia panda likitokea upande wa kisarawe, macho yalimtoka akilitazama lile gari ambalo kiukweli ndiyo gari la ndoto yake, gari ambalo kuna muda fulani aliliona maeneo ya airport japo hakuwa na uhakika kama ndiyo lile lile au la, ila kwa hakika alikjikuta anazidi kutamani kumiliki gari kama lile, na wakati anaendelea kuongea na simu, mara simu yake ikaanza kutoa ishara ya simu nyingine kutaka kuingia kwenye simu yake, akaitoa sikioni na kutazama mpigaji wa simu ya pili.


Kwa macho yake akaona ile namba ngeni ya nchi za nje, namba ambayo ilitoka kumpigia dakika ishirini na saba au nane zilizopita, “baba subiri kidogo nitakupiga baadae” alisema Deus na kukata simu ya kwanza kisha akapokea ile ya pili.******


Mkuu wa polisi jeshini Brigedia SS Chawe, mida hii alikuwa ndani ya gari la jeshi analotembelea siku zote, ikiwa ni safari ya kuelekea nyumbani kwake huku moyoni akijisifu kwa kumaliza jukumu la kufungua mashitaka na kumaliza kesi ya askari mtovu wa nidhamu, yaani Deus Nyati, ambae kisheria adhabu yake ni kufukuzwa jeshi kwa kulitia aibu jeshi hilo lenye kusifiwa kwa nidhamu, “hivi afande unadhani ni sawa kumfukuza jeshi privae Deus Nyati?” aliuliza msaidizi na mwangalizi (mpambe) wa mkuu wa polisi jeshi, mwenye cheo cha luteni, “hakuna mtu muhimu jeshini, kama amefanya makosa basi sheria lazima ichukuwe mkondo wake” alisema brigedia yule, ambae juu ya mfuko wake wakulia wa shati la kombani, kulikuwa na jina SS Chawe yaani Salum Said Chawe, “lakini afande UN ilibaini kuwa hakuwa na kosa zaidi ya kuvunja taratibu ndogo ambazo askari wengi huzivunja” alisema yule msaidizi.


Hiyo ilimfanya Chawe akasirike, “kwahiyo unanifundisha majukumu yangu” aliuliza Chawe kwa sauti kavu, huku wakitazama jengo la diamond jubilee, kwa maana walikuwa wanakatiza hapo na wakati huo huo simu ya mkononi ya Chawe ikaanza kuita, akaichukuwa haraka na kuitazama, mpigaji alikuwa ni major General Mbike, yaani COT, moyo wa Chawe ukalipuka kwa mshtuko, maana alikumbuka kuwa licha ya kumpokea na kumshtaki Deus, lakini hakuwa amepeleka taarifa yoyote kwa Mkuu wa mafunzo.


Chawe akaipokea haraka simu ile na kuiweka sikioni, “jambo afande” alisalimia brigedia Chawe, “Chawe toka lini umepewa jukumu la kupokea watu wanaotoka operation nje ya nchi?” aliuliza Mbike kwa sauti iliyojilazimisha kuzuwia jazba, “afande huyu ni tofauti kidogo, huyu ni mwalifu, hivyo ni jukumu la MP kwenda kumuweka chini ya ulinzi” alijibu Chawe kwa sauti yenye uzito mkubwa wanidhamu, “uliagizwa na nani brigedia, ofisi yangu si ndiyo yenye jukumu la kukuagiza kuwa fulani akamtwe, maana bado alikuwa chini yangu” aliuliza Mbike, safari hii akiongeza sauti kidogo na kuwa yenye ukali, “afande nadhani msaidizi wangu ndie aliamua kujiongeza baada ya kuona taarifa inachelewa, sababu mimi nililetewa akiwa amesha toka airport” alisema Chawe kwa sauti ya kujitetea “kwahiyo jukumu la kufungua mashaka nalo ulijiongeza au uliagizwa na nani?” aliuliza Mbike, kwa sauti yenye hasira ya wazi na hapo ndipo Chawe alipokumbuka maneno ya huyu msaidizi wake (mpambe)


“afande tulitoa taarifa kwa mnadhimu, tukiomba kibali cha kufungua mahakama, nae akakubali, na sisi tukafanya hivyo” alijibu Chawe, na hapo kikasikika kicheko cha uchungu, “Chawe ulikuwa na maslahi yoyote kwa kumshtaki Deus, mbona ulikiuka sheria na nidhamu ya kijeshi ambayo unaisimamia kila siku, ni kweli ulitakiwa uende kwa mnadhimu kabla yangu? wewe ndie ulietakiwa ukampokee Deus airport na siyo mimi, hata jukumu la kumshtaki Deus, lilikuwa la kwangu, hakika hii imekuchafua, anyway jiandae kwa kile kitakacho kutokea kwa kosa la kufukuza askari ambae bado jeshi lilikuwa linamuhitaji” alisema Mbike na kukata simu, akimuacha Chawe ameshikilia simu huku macho ameyatoa kama vile amefumaniwa.******


Yap! Saa nane na nusu, ndio muda ambao, Sheba alisimamisha gari maeneo ya kiluvya madukani, akitokea upande wa kisarawe kupitia barabara ya tondoroni mpaka mdidimue, Sheba kama alivyoelekezwa na boss wake Atshen akasimamisha gari mita chache toka barabara hiyo iendayo Morogoro, ambapo aliambiwa kuwa atampata mtu mwenye uwezo mkubwa wa kuendesha gari na pia ni mpiganaji mkubwa sana mwenye uwezo mkubwa.


Sheba akatazama kushoto na kulia mwa barabara ya vumbi ya kiluvya madukani kama angemuona mtu analifwata gari lile, lakini hakuona mtu yoyote anae lifuata gari lake, zaidi aliwaona watu wengi wakiwa wanaendelea na shughuri zao, wakiwa wauza samaki, mama nitilie wapiga debe wa daladala, pia madereva wa boda boda na watu waliokuwa wanafika pale kutafuta mahitaji au usafiri wa kwenda maeneo mbali mbali ya mji.


Wakati Sheba anatazama kushoto na kulia, mara macho yake yakakwama kwa kijana mmoja mrefu wa wastani, mwenye umbo fulani ambalo lilimtambulisha kuwa ni kijana aliependa mazoezi, au kufanya mazoezi kwa muda mrefu siku za hivi karibuni, ambae alikuwa amebeba begi kubwa mgongoni mwake, “mh! mbona sikuwhai kuona kijana mtanzania mwenye kufanana na wewe” aliwaza Sheba, ambae sio kwaajili ya lile begi, ila ni kwaajili ya uso wa upole wakijana huyu, ambae sasa alikuwa anaongea na simu, huku macho yake anapepesa kushoto na kulia na mwisho macho yake yakaganda kwenye gari lake, ambalo alilitazama kwa muda mrefu kidogo huku anaendelea kuongea kwa simu yake.


Dakika moja baadae, akamuona kijana yule, akibofya simu yake na kuiweka tena sikioni, ilionyesha wazi kuwa kuna simu nyingine ilikuwa imeingia wakati akiwa anaongea na hata alipoongea na ile simu ya pili alionekana akitazama tena gari la Sheba, na kuanza kutembea kulifuata, mpaka alipolifikia gari lile, hapo Sheba akajikuta anatabasamu, maana alishajuwa kuwa kijana huyu mwenye umbo la pekee, ndie mtu aliekusudiwa kuwa dereva na mlinzi wake katika safari mpya ya kuelekea kaskazini mwa Tanzania,


Kijana yule alipolikaribia gari, Sheba akafungua mlango na kushuka akiliacha lina unguruma, na kuzunguka upande wa kushoto wa gari, akaingia kwenye upade huo kwa maana seat ya abiria wa mbele na Deus nae hakujiuliza, akausogelea mlango wa abiria wa nyuma na kuufungua mlango ule akaliona begi dogo ambalo hakulijali, yeye akaweka begi lake na kuufunga mlango ule, kisha akaingia kwenye seat ya dereva, ambayo mlango wake ulikuwa wazi.


Baada ya kuingia akafunga mlango na kumtazama Sheba, “habari yako dada” alisalimia Deus kwa sauti yake ya upole, “nzuri, nadhani maelekezo unayo, mzigo wako huo hapo seat ya nyuma” alisema Sheba, huku akionyesha lile begi dogo lililopo seat ya nyuma, Deus alilitazama lile begi dogo, kisha akalinyoosha mkono na kulichukuwa, halafu akafungua lile begi, ambalo ndani yake kulikuwa na bando za fedha za kitanzania, noti za elfu kumi kumi, akafunga na kulirushia tena kule nyuma, “ok! boss wako yupo vizuri, anaenda na muda na mkweli anatimiza ahadi” alisema Deus, huku anatazama dash board ya gari lile ambao leo ni mara yake ya kwanza kuingia ndani yake, “una uhakika tutafika salama?” aliuliza Sheba kwa saut ya kutilia mashaka, maana kwa muonekan wa sura na muonekano wa Deus, upole wake na uongeaji wake, usingemuweka katika kundi kama hili.


“Tuna BMW S7, sina wasi wasi” alisema Deus, huku anapachika gia na kuondoa gari taratibu, kuingia barabara kuu, usingewaza kama walikuwa na safari ya mbali kiasi hicho, zaidi ya kilomita mia tatu, taratibu gari liliingia barabara ya morogoro na kushika uelekeo wa kushoto, ambao ni wa morogoro, likitembea kwa speed ndogo, kama linaishia mzani, wakati huo hapo, pale kibaha mpakani hawakujuwa kuwa, mita chache toka pale njia panda ya kisarawe walipokuwepo, kuna askari wa jeshi la polisi alievalia nguo za kiraia alikuwa analitazama gari lile la kisasa, lenye mwonekano wa upya…....…….endelea…. kufwatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
Back
Top Bottom