NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA THEMANINI NA SITA
MTUNZI :
Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA TANO: Nadhani Ulenje alikereka na kelele za Songoro, maana alikata simu mara moja, “hivi huyu mjinga anapata wapi kiburi cha kunikatia simu?” aliuliza Songoro kwa sauti yenye mshangaobhuku anapiga tena simu kwa Ulenje, simu ambayo safari hii haikupokelewa hata kwa bahati mbaya, “inamana tumeanza kudharauliana kiasi hicho Ulenje, umesahau mimi ndie ninae kuweka mjini, au kwa sababu una washirika wengine wenye wanaokupa dhahabu za #mbogo_land, aliuliza Songoro huku anapiga tena simu kwa Ulenje, ambae licha ya kupigiwa mara kadhaa lakini hakuipokea. ….ENDELEA…
Hapo sasa akiwa mwenye hasira kali, Songoro akaiweka simu mezani na kumtazama mmoja kati ya wale vijana waliokuwa wamesimama, “Side hivi unamfahamu huyu mtoto mwenye BMW jeusi anapatikana vipi?” aliuliza Songoro kwa sauti iliyoonyesha hamu kubwa ya kumpata dereva wa BMW jeusi, “boss nilishawahi kusikia habari zake, lakini sikuwahi kufahamu anakoishi” alijibu Side, ambae ni mmoja kati ya vijana waliotoka kwa Eze kuja kuziba pengo la wale vijana waliopigwa na dereva jana usiku.
Jibu la Side nikama lilizidi kumtia hasira Songoro, ambae alishika kichwa chake kwa mikono yote miwili na kujikuna nywele, “nitakukamata tu we mshenzi” alipiga kelele Songoro nakuwafanya wakina Side wamtazame mzee huyo mwenye hasira kali****
Mbogo Land, ndani ya jiji la TT waziri Chitopelah, alikuwa nyumbani kwake anasubiria matokea ya mambo yanayo endelea nchini Tanzania, kwa maana ya utekelezwaji wa mipango miwili ambayo mmoja wapo ungewezesha kupatikana kwa fedha za kufanyia malipo ya silaha ambazo zinatarajiwa kutumiwa katika mapinduzi ya kijeshi kuung'oa uongozi wa kifalme chini ya mfalme Elvis wa kwanza.
Wakati anawaza hayo waziri huyu, ambae alipewa uwaziri akiwa na cheo cha brigediaa general, mara akasikia simu yake inaita, akanyakuwa haraka na kutazama mpigaji, akajikuta anaipokea kwa pupa, “niambie Chiro, vipi wamesha fika?” aliuliza Chitopela, akiwa mwenye shauku ya kujua jambo, “ndiyo boss, wapo kumi na sita wameriport ubalozini na wamesha pelekwa Angoni ams hotel kule msamala” alisema huyo mtu alieitwa Chiro, “kwahiyo umejaribu kudodosa wamefuata nini huko Tanzania?” aliuliza Chotopelah, boss kwa kweli mpaka sasa hivi ninavyoongea na wewe, nawaona askari watatu, wamevaa nguo za kiraia wanaingia kwenye gari moja wanatoka hapa hotelini, sijajua wanaelekea wapi, ndio najaribu kuwa fuatilia” alisema Chiro, kabla hawajaagana na kukata simu, ikitanguliwa na maagizo ya kutokuacha kuwafuatilia, yaliyotolewa na Chitopelah.
Huyo bwana anaitwa Chiropo, kwa lugha ya asili ya mbogo Land maana yake mtoto wa kiume mropokaji, kwa mtoto wakike ungesema Kiropo, na kwa mwanaume mtu mzima ungesema Muropo, na kwa mwanamke mkubwa ungesema Tiropo.
Huyu ni mfanyakazi wa serikali katika kitengo cha MLA ya Mbogo Land, alieletwa nchini Tanzania, kama mmoja wa watunza nyaraka wa ubalozi wao, lakini tayari alishakutana na ushawishi wa bwana Dickson chitopelah, na kuwa jicho lake pale kwenye ubalozi mdogo wa Songea, kama alivyofanya sehemu nyingine, nje na ndani ya nchi, serikalini na kwenye sekta binafsi, ambazo aliamini kuwa zinahusika kwa namna moja au nyingine na mpango wake.**********
Turudi Dar es salaam, mida hii ya saa tatu, jiji lilikuwa limechangamka kweli kweli, ungesema ni saa moja za jioni, maana pilika zilishamili, watu walionekana kukatiza barabarani, pia magari yakiwa ni yale binafsi ya serikali na yale mabasi madogo ya abiria yaliyojaza abiria, yakiingia na kutoka katikati ya jiji, bila kusahau pikipiki na bajaji zilizo onekana kuwa kama kivutio cha macho ya abiria waliopo kwenye magari ya abiria na magari binafsi, au watu walio kuwa wanatembea kwa miguu na walio kuwa wametulia pembezoni mwa barabara wakiuza au kununua biashara za jioni, kama vile mahindi ya kuchoma yale ya kupaka chumvi, mihogo au mishikaki, waliojionea jinsi vyombo hivyo vya usafiri vikipenya mbavuni mwa magari pasipo kujali hatari yoyote ambayo inaweza kuwatokea wao madereva na abiria wao.
Sisi twendeni maeneo ya shekilango, mita chache toka barabara ya morogoro, pembezoni mwa barabara iendayo Bamaga, nje ya jengo kubwa la Sisterfada Hotel, tunalioona gari aina Toyota V 8, likiingia kwenye maegesho ya chini ya jengo lile.
Baada ya taratibu zote za kuzima gari hilo kufanyika, mlango wa dereva unafunguliwa na anashuka mzee James Kelvin na mkoba wake, kisha anabonya kiongozea mbali cha gari lake kwa kufunga gari lake, ambalo linajifunga kisha anaweka funguo mfukoni na kuanza kutembea kuelekea upande wa kutokea pale kwenye maegesho na kulifuata lango lakuingilia ndani ya hotel hii yenye hadhi kubwa, ambayo ukitazama muonekano wa pale mbele, ungeona kuna watu wachache waliokuwa wakiingia ndani, huku wakipokelewa na wanausalama wa hotelini pale waliovalia suruali ya dark brue na mashati meupe, huku viatu vyao vikiwa vyeusi.
Kama ilivyokuwa kwa wale wageni wengine, pia bwana James anapokelewa na walinzi, “karibu muheshimiwa” anasema mlinzi mmoja kwa sauti iliyojaa unyenyekevu, ni wazi kwamba alimtambua tajiri huyu mkubwa, “Asante sana” aliitikia bwana James, huku anakatiza kwenye lango kubwa la vioo na kuanza kutembea kuelelekea kwenye lift, huku macho yake yakikutana na macho ya kijana mmoja aliekuwa amekaa kwenye viti vya wateja wasubiriao huduma, yeye hakumjali akaingia kwenye lift na kubonya namba tatu, akimaanisha kuwa ni ghorofa ya tatu, lift inafunga mlango.
Sekunde chache baadae lift inafungua mlango wake, kisha mzee James anatoka na kuelekea mpaka kwenye mlango wa chumba namba nane wa ghorofa hili la tatu, mlango ambao wanaonakena vijana wawili waliovalia suit nyeusi, na kila mmoja akiwa ameshika begi kubwa mkononi ana wasalimia, “habari zenu vijana” nao wanaitikia, “salama karibu” ni sauti kavu toka kwa mmoja kati yao, huku yule mwingine anafungua mlango wa chumba namba nane, mzee James nae anaingia ndani akikutana na moshi mzito wa siraga bwege..
Naaam ile mzee James anaingia ndani ya chumba, anashikwa na mshangao mkubwa sana, mapigo ya moyo yanaanza kwenda mbio, wasi wasi unamshika mzee huyu, ni kwaajili kile anacho kiona mbele yake, sio tu ukubwa wa chumba kile kikubwa chenye kitanda kikubwa sana na makochi mawili mazuri makubwa, nasiyo ule moshi wa bangi ulio sambaza harufu mle ndani.
Ila ni watu watano, aliowakuta mule ndani, “karibu mheshimiwa, sikufikiria kama utakuja kwa wakati” lilikuwa ni karibisho toka kwa mtu mmoja aliekuwa amekaa kwenye moja kati ya yale makochi mawili, ambae licha ya kuvaa suit yake nyeusi yenye kufanana na wale vijana wawili nje ya mlango, lakini alikuwa anavuta bangi, akisindikizia kwa pombe kali iliyokuwa mezani.
Mzee James anashindwa kuitikia karibisho toka kwa yule jamaa, baada yake anatazama kushoto na kulia na mbele yake upande wa dirishani, ambako, kulikuwa na vijana wanne walio valia suit nyeusi kama wenzao, walio simama kwa mtindo wa kuwazunguka, mkononi mwao walikuwa wameshikilia bunduki aina ya H&K G95 ASSAUL RIFLE, yani HECKLER &KOCH G95 TOKA GERMANY ASSAULT RIFLE 5.56MM toka ujerumani, wawili wakiwatazama na wawili wakiwa wamesimama upande wa dirishani, wakitazama upande nje, ambao ni upande wa ubungo plaza yani sio upande wa barabarani.
Taswira ilikuwa ni kama watu fulani wanaigiza filamu ya kijambazi, “asante mheshimiwa, lakini samahani jamani nadhani nimekosea chumba” alisema mzee James, kwa sauti tulivu ya unyenyekevu huku anageuka na kuutazama mlago ambao tayari ulikuwa umesha fungwa, “hujakosea bwana James, sisi ni wajumbe wa mheshimiwa Chitopelah, toka #Mbogo_land, tupo hapa kuongea na wewe” alisema yule aliekuwa amekaa kwenye kochi anaburudika kwa mchanganuo wa bangi na pombe kali.
Hapo bwana James ambae mpaka sasa hakuona dalili ya maongezi ya kibiashara, aligeuka na kuwatazana wake wajumbe wa Chitopelah, ambao walikuwa wamekaza sura zao wakimtazama, kasoro wale waliokuwa wanatazama nje kupitia dirishani, na huyu alie kaa, ambae alionekana kuachia tabasamu la sanifu, kwamba bwana James ameshaingia mikononi mwao, hivyo nilazima akubaliane nao.
Kiroho shingo upande na mashaka makubwa, bwana Jamaes akaenda kukaa kwenye lile kochi lililokuwa tupu, “ok! nakusikiliza mheshimiwa” alisema james, ambae alikuwa ameukumbatia mkoba wake, huku kichwani yakimjia maswali mfululizo, yote yakiwa yana jiuliza nia kubwa ya bwana Chitopelah kufanya biashara ya siri ni nini.*******
Twende Makuti pub kule mbezi luis au mbezi mwisho kama unavyoweza kuita, bado anaonekana Veronica akiwa amekaa kwenye meza yake anakunywa wine taratibu, macho ameyaelekeza sehemu ya kutokea, huku mara kwa mara akitazama simu yake na kujaribu kuipiga namba ya JJ, ambayo haikupokelewa, “dakika kumi zikipita naondoka zangu” alijisemea Veronica huku anabofya simu yake na kuweka kwenye sehemu ya kuandikia ujumbe wa whatsapp, anagusa namba ya mchoraji wake unakuja uwanja wa ujumbe, halafu anaanza kuandika, “huyo mteja ulienae busy ni wakike au wa kiume?” anamaliza kuutuma kwenda kwa mchoraji, kisha akatulia akaandika mwingine wakati huo huo na sehemu hiyo hiyo ya mchoraji, “maana naona umetumia muda mrefu sana” safari hii anamalizia kwa vikaragosi vya mshangao, kisha akautuma na kuweka simu mezani.
Naam Vaeronica anakaa tena dakika kumi nyingine, huku mara kwa mara akijaribu kupiga simu pasipo mafanikio na hapo Veronica anakosa uvumilivu, pasipo kujali kwamba chupa yake ya wine ipo nusu, akainuka na tayari kuondoka.
Lakini kabla hata hajapiga hatua moja akashkwa mkono, “ni vyema kama ukikaa chini na kusikiliza ujumbe wako” ilisikika sauti ya mwanaume alie mshika mkono, Veronica anageuza uso wake na kumtazama aliemshika mkono, ambae anamtambua kuwa ni yule aliempokea mwanzo pale kwenye maegesho, lakini safari hii hakuwa mwenye lile tabasamu la uongo, “kwani kuna tatizo gani, John amepatwa na tatizo?” aliuliza Veronica, huku anakaa tena kwenye kiti chake, akionyesha kupatwa na wasi wasi, “sikia dada, unatakiwa kuwa mpole na kunisikiliza” alisema yule jamaa na Veronica akatulia kumsikiliza.
Hapo yule jamaa akatoa simu na kufungua kwenye hifadhi ya video na picha, anaigusa moja kati ya Video ambayo inaanza kucheza, huku Veronica anaitazama video ambayo inawaonyesha wanaume wawili wakiwa ndani ya jengo moja kubwa lisilomaliza ujenzi, huku mwanaume mwingine anaonekana akiwa amelala chini, huku nguo zake zikiwa zimechafuka damu chapa chapa, wasi wasi mkubwa unamshika Veronica mapigo ya moyo yanamwenda mbio, “ni nani huyu, usiniambie kama ni John” alisema Verionica kwa sauti yenye kujawa na wasi wasi na mshtuko, “ni yeye, wala hujakosea” alisema yule jamaa, wakati huo video inaonyesha kwa ukaribu zaidi tukio lile na kuivuta sura ya mtu alielala pale chini. Naam mbona kama JJ nae yupo matatizoni?Itakuwaje sasa? ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa
NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa
jamii forums