Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

Simulizi: Nyuma ya mlango wa adui

NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA THEMANINI NA NNE
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA TATU: “mutapokelewa na balozi mdogo katika ubalozi wa Songea, kuhusu maelekezo yote mutayapata huko, usiri ni kitu muhimu na ndio daraja la jukumu lenu, muda wote mutawasiliana na mimi” alisema general Sixmund kwa sauti ya chini, huku kwa macho ya wizi anatazama lile gari la kati la kiraia, ambapo sasa alionekana anashuka waziri chitopelahvakiwa anashuka toka kwenye gari. “bila shaka afande naamini kila kitu kitaenda sawa” alisema captain Makey kwa sauti ya chini huku anatazama kule ambako waziri Chitopelah alikuwa anatokea. ….ENDELEA…


Hapo kikapita kimya kifupi huku wote wakimtazama vizuri huyu waziri wa ulinzi wa serikali ya kifalme ya #mbogo_land, ambae pia walikuwa nae katika msafara wao, “General Six, hii imekuwa ghafla sana, mume weza kuwaandaa vyema hawa askari na kwamba hawato tuangusha?” aliuliza waziri Chitopelah mara alipowafikia askari wale, akionyesha wazi kuwa anaamini kuwa askari wale wa jeshi la ulinzi la #Mbogo_Land, wanaenda Tanzania kushiriki zoezi la pamoja, mazoezi ambayo hutokea mara nyingi kwa nchi za jirani kama hizi, “kuhusu maandalizi hilo sina shaka, ni kutokana na utayari wa kikundi chetu mheshimiwa” alisema general Sixmund kwa kujiamini, “sawa nina waamini na nina jivunia nyie kwamba hamto tuangusha, naamini kila kitu kipo sawa, kama kuna mapungufu basi mutatoa taarifa mapemaa” alisema Chitopelah huku ana watazama maafisa wale wa kikosi cha kijeshi kinacho husika na mambo ya uchunguzi wa kivita, “ndiyo afande” walijibu wote kwa pamoja.


Baada ya hapo Chitopelah, akamtazama Sixmund, “sina la kuongea zaidi, nadhani wanaweza kuingia kwenye ndege ili waanze safari” alisema Chitopelah, na hapo general Sixmund, akapiga salut, kisha akamgeukia captain Amos David Makey, “captain ongoza kikundi kuingia kwenye ndege” alisema Sixmund, na hapo Makey, akaanza kuongoza askari wake kuelekea kwenye ndege, ambayo ilikuwa imesimama sehemu ya kupandia ndege za VIP, wakiwaacha wakina Sixmund wakiwatazama kwa kila hatua waliyokuwa wanapitia pale uwanja wa ndege, huku kila mmoja wao, kati ya general Six na Waziri Chitopelah akiwaza la kwake.


Wakati General akiwa anawaza juu ya namna atakavyoweza kutunza siri, waziri asijuwe, na sio kwamba alimshuku kwa lolote, hapana, ni vile alikuwa anatimiza walichopanga na mfalme Elvis Mbogo wa kwanza, kwamba daraja la operation hiyo siri, “bora asiwe mdadisi huyu mtu” aliwaza Sixmund huku macho ameyakaza kule ambako iliko ndege.


Wakati huo waziri Chitopelah pia alikuwa anawaza juu ya ughafla wa safari ya askari wa MLA kwenda nchini Tanzania, sehemu ambayo yeye anaitumia kama sehemu ya kukamilishia mipango yake, “hivi Six, kwanini nimechelewa kupata taarifa ya zoezi hili na kwanini limekuwa ghafla sana” aliuliza Chitopelah kwa sauti yenye mashaka ya wazi, huku macho yake yana hama toka kwenye ndege ambako wale askari tayari walikuwa wamesha ingia ndani yake, “ukweli mheshimiwa ughafla huu umetushangaza wengi, lakini hauwezi kuwa sababu ya kushindwa au kufanya vibaya kwa askari wetu katika zoezi hilo” alisema general Six, huku wakiitazama ndege, ambayo sasa ilikuwa inaanza kutembe taratibu kwenye njia za kurukia, “lakini General mara nyingi taarifa za mazoezi toka nje huwa yanapokelewa na ofisi yangu, inakuwaje hii imekuja moja kwa moja kwenu na mimi napewa taarifa na mfalme?” aliuliza mheshimiwa Chitopelah kwa sauti ya mashaka.


Naam kabla hata Six hajajibu, simu ya mfukoni ya Mheshimiwa Chitopelah, ikaanza kuita toka mfukoni wake, Chitopelah akaitoa na kutazama jina la mpigaji, alipoliona ghafla akamtazama Sixmund, “naona kuna watu wananihitaji huko, kama kunalolote utanijulisha” alisema Chitopelah, huku anaelekea kwenye gari lake na simu yake mkononi, “ndiyo mheshimiwa” alijibu sixmund huku anamsindikiza waziri huyu kwa macho, mpaka alipo ingia kwenye gari, huku walinzi na watu aliokuwanao wakiingia kwenye magari pia.*********


Yap! sasa turudi dar es salaam Tanzania, tabata kinyerezi mwisho, nyumbani kwa tajiri mkubwa bwana James Kelvin, anaonekana mschana mmoja mrembo, akiwa amekaa kwenye kochi moja kubwa huku ameshika simu yake anaperuzi kwenye mitandao ya kijamii, “hivi kwanini huyu kaka hajaonekana mpaka leo” anajiuliza mschana huyu huku anabadili kurasa nyingine,


Mara anaibuka mzee James, alievaa nguo nadhifu ni wazi alikuwa anaenda sehemu muhimu usiku ule, akiwa ameongozana na mke wake, alie valia nguo za kawaida za nyumbani huku amebeba mkoba mdogo mweusi wa kiume, ambao mume wake hupenda kubeba anapokuwa anakikao au mkutano muhimu na wakibiashara, “lakini kwa nini iwe biashara ya siri kati yako na mheshimiwa Chitopelah?” aliuliza mke wa mzee James, “mh! hata mimi imenishtua sana, ila pengine inaweza kuwa ndiyo safari ya sisi kurudi nyumbani #mbogo_land, nchi tuliyozaliwa” alisema mzee James, huku anasimama pale sebuleni.


Maongezi hayo ni kama yalimvutia binti yao mdogo, aliekuwa amejilaza kwenye kochi, “itakuwa safi sana, lakini tunahitaji kuwa makini sana, maana hao hao ndio waliokusingizia kuwa wewe ni mfadhili wa waasi” alisema mama Veronica, yani mke wa James kwa sauti tulivu yenye tahadhari nyingi, “baba, bado unataka kukutana na watu wa #mbogo_land, lakini si ulisema ilibakia kidogo wakuuwe wewe mama na dada Vero?” aliuliza yule mschana mrembo juu ya kochi, huku anawatazama wakina mzee James na mke wake, “hapana Carlo, ni maswala ya kibiashara, inaweza kuwa ndio nafasi ya mimi kujisafisha na pengine kurudi nchini kwetu” alisema mzee James akimtazama binti yake.


Huyo ni Carloline James, binti mdogo wa mzee James, huyu ndie mschana alieokolewa na Deus kwenye ajali ya tren miaka kadhaa iliyopita, huyu ndie mdogo wa doctor Veronica au pacha, kama Deus anavyomuita.


Na hapo ni kama mschana huyu Carloline alielewa alichoelezwa na baba yake, “sawa baba nakutakia kikao chema” alisema Carlo na hapo wakaagana na mzee James akachukuwa mkoba wake na kutoka nje, akiwaacha mama na mwana pale sebuleni wakiendelea na maongezi yao, “vipi Carlo, umepata chochote juu ya yule kijana?” aliuliza mama Vero huku anacheka kidogo, “sijui anaishi wapi yule mwanaume, yani mwezi wa pili sasa sijasikia habari zake” alisema Carlo kwa sauti ya kujilalamisha,******


Naam mara baada ya kuingia kwenye gari lake, pasipo kusubiri ndege ipotee angani, “tuondoke” Dickson Chitopelah, anamuamuru dereva wake aondoe gari, nae akafanya hivyo kwa kuondoa gari kutoka nje ya eneo la uwaja wa ndege, huku simu yake bado ilikuwa inaendelea kuita, akaipokea “niambie” alisema Chitopela mara baada ya kuweka simu sikioni, “boss tayari tumesha weka mambo sawa, na sasa tunaelekea SisterFada kwenye kikao na James” ilisikika sauti toka upande wa pili wa simu, “ok! sawa ila sasa kuweni makini na kila hatua, halafu kuna jambo ilikuwa lazima tuongee” alisema Chitopelah, ambae alionekana kuongea kwa namna ambayo, hakutaka walinzi wake wajue lolote, “tuna weza kuongea sasa boss, maana bado nipo njiani” ilisikika ile ya upande wa pili, “sikia, kuna askari wanaondoka mida hii hapa TT, wanaelekea songea kuna zoezi la kijeshi, toa mtu mmoja wa kuwatazama kila kinachoendelea na niwe napata taarifa zote kwa wakati” alisema Chitopelah kwa msisitizo, kisha wakakata simu kwa ahadi ya kwamba, watawasiliana baadae.


Naam turudi tena nyumbani kwa mzee James, ambako bado tuna muona Carloline na mama yake bado wapo sebuleni wanaendelea na maongezi yao, “lakini wewe bado unasoma hivi huyo manaume utafanya nae nini, kwani hutaki kuwa kama dada yako?” aliuliza mama Vero na kabla Carloline hajajibu wote wakasikia sauti ya viatu vyenye visigizo virefu ikitokea upande wa koridoni, wakageuza macho yao kutazama alie kuwa anakuja.


Naam sekunde chache baadae, wakamuona mwanamke mzuri aliependeza mfano wa malaika akija kwa mwendo wa taratibu, huku uso wake ukiwa umepambwa na tabasamu mwanana lililozidisha uzuri wake mara dufu, “naonekanaje hapo?” aliuliza mwanamke yule, ambao gauni lake jekundu lilikaa vyema kwenye umbo lake zuri la kupendeza.


Hapo calroline na mama yake walitumia dakika nzima kumtazama mwanamke huyo kabla hawajatoa maoni yao, “ndiyo maana wanaume wanachanganyikiwa kila wanapokuona dada yangu” alisema Carloline huku anainuka toka kwenye kochi na kumsogelea dada yake huyo mrembo nakujaribu kuligusa gauni lake, huku mama yao akiwa anaendelea kumtazama mwanamke huyo ambae kwa haraka haraka ungesema ni siku yake ya ndoa au send off, “Vero umesema unaenda kukutana na John, huoni kama ni hatari sana usiku kama huu na hivyo ulivyopendeza?” aliuliza mama yao, huku akiendelea kuumtazama binti yake, ambae alicheka cha kicheko chini chini kilicho tawaliwa na aibu fulani ya kujishuku, “hapana mama, tena tunaenda kukutana hapo mbezi tu, sehemu ya wazi” alisema doctor Veronica, ambae alijuwa fika anaenda kujaribu kitu ambacho hajawahi kujaribu, yani kuridhishana kimapenzi na mchumba wake pasipo kukutanisha sehemu zao za haja ndogo.


Ni kama mama Vero hakuridhika kwa roho safi, japo aliagana na binti yake, kisha doctor Veronica akaondoka zake na kutoka nje, akaingia kwenye gari lake aina ya Toyota wish, kisha akawasha na kuondoka zake huku akipiga simu kwa mchumba wake, mwanaume anaitwa John Joseph Daud, simu iliita kwa muda mfupi na kupokelewa, “niambie mpenzi, umesha toka” ilisikika sauti iliyochangamka kwa furaha, toka upande wa pili wa simu. ….ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA THEMANINI NA TANO
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA NNE: Nikama mama Vero hakuridhika kwa roho safi, japo aliagana na binti yake, kisha doctor Veronica akaondoka zake na kutoka nje akaingia kwenye gari lake aina ya Toyota wish, kisha akawasha nakuondoka zake, huku akipiga simu kwa mchumba wake, mwanaume anaitwa John Joseph Daud, simu iliita kwa muda mfupi na kupokelewa, “niambie mpenzi, umeshatoka” ilisikika sauti iliyochangamka kwa furaha, toka upande wa pili wa simu. ….ENDELEA…

Kwanza Veronica akacheka kicheko hafifu chenye kutawaliwa na aibu, “yani unavyofurahia, nimesha toka nyumbani nikukute basi hapo makuti hotel” alisema Veronica kwa sauti ya kama sitaki nataka, “naanzaje kuchelewa wakati nimeshafika, we njoo moja kwa moja utanikuta hapa” alisema JJ akionyesha wazi kufurahia jambo, “sawa, ila pia sitochelewa kurudi nyumbani” alisema doctor Veronica, kabla hajakata simu na kusimamisha gari, kisha akaingia Whatsapp na kuanza kuandika ujumbe, “upo wapi mchoraji?” kisha akaituma kwenda kwenye namba iliyoandikwa mchoraji wangu, kisha akaondoa tena gari.

Alipofika karibu na barabara kuu akasimamisha gari na kutazama kama kuna ujumbe umeingia, akaona kuna jumbe mbili toka mchoraji, “nipo mwenge napeleka vyombo kwa mteja wangu” ndvyo ulivyosema ujumbe wake wa kwanza, na ujumbe wa pili ulisema hivi, “nitakutafuta baadae kwa sasa nitakuwa busy kidogo” hapo Veronica akacheka kidogo, “vyombo gani usiku huu, sema wivu unakusumbua” alijisemea Veronica, huku anaendesha gari kueleka upande wa mbezi kupitia malamba mawili, moyoni akiwaza hicho kitu watakacho kifanya na kumaliza hajazao pasipo kuingiliana, wakati huo maneno ya mchoraji yakimjia kichwani, “mh! sina hakika kama unacho kifikiria kitu cha kweli, nakushauri ujiandae kwa mabadiliko ya ratiba” ilitisha kidogo, lakini Veronica akajipa moyo, “J hawezi kufanya hivyo bwana, hisia za wivu tu za mchoraji” alijisemea Veronica huku safari inaendelea.********

Naaam mida ya saa mbili na nusu za usiku, maeneo ya mwenge Dar es salaam Deus Frank Nyati, alikuwa amesimamisha gari nje Mama P Saloon na dakika hiyo hiyo akatoka mschana mmoja toka saloon akiwa amebeba box moja dogo mkononi mwake, akasogelea gari na Deus akafungua kioo na kupokea lile box, kisha akaondoa gari kuelekea mjini huku anapandisha kioo.******

Kimara kichungwani, nyumbani kwa bwana Ezze tunamkuta akiwa ametulia sebuleni anatazama taarifa ya habari, huku mara kwa mara anaitazama simu yake kama ataona ujumbe au simu toka sehemu fulani.

Hakika kama ungemuona bwana Eze aliekaa kochini kwa muonekano wa mtoto wa miaka kumi au kumi na mbili, ungefahamu kuwa bwana Eze hakuwa anaelewa chochote kinachoendelea kwenye television, zaidi ni kwamba alikuwa anasumbuliwa na jambo fulani kichwani mwake, “hawa wapuuzi mbona hawaleti taarifa, au mpaka atombw.. ndio wanipe taarifa” aliwaza Eze kimoyo moyo huku anachukuwa sim yake kochini na kuitazama, hakuona chochote zaidi ya tarehe na saa, ilikuwa ni tarehe ishirini na saba ya mwezi wa pili, muda ni saa mbili na dakika arobaini na nane, “ona sasa, muda unazidi kwenda, halafu wao hawaniambii chochote” aliwaza mtu mfupi Eze, huku anarudisha simu juu ya kochi pembeni yake.

Lakini sasa, ile anaweka simu tu, nayo ikaanza kuita, Eze akiwa mwenye kihoro akaichukuwa simu yake haraka na kutazama jina la mpigaji, akaona kuwa mpigaji ni Inno, “yes” alinong’ona Eze huku anatazama upande wake wa kulia, kule ambako kuna kolido la kutokea upande wa vyumbani ambako wakati ule mke wake alikuwa ameelekea, alipoona hakuna mtu akaipokea simu na kuiweka sikioni, “niambie Inno, amefikia wapi huyo?” aliuliza Eze kwa sauti ya chini, “boss mama P yupo ameingia hapa Sisterfada hotel, yupo chumba namba nane ghrofa ya pili, lakini yupo peke yake” ilisikika sauti toka upende wa pili wa simu, “msiondoke angalieni yoyote ambae ataingia humo, akiwa mwanaume hakikisheni muna muwahi kabla hajafanya lolote, mchukueni huyo fala kwa namna yoyote mpelekeni shamba tukampe somo” alisema Eze na wakati huo huo akasikia vishindo vya mtu akitokea upande wa vyumbani.

Hapo moja kwa moja Eze akajuwa kuwa anaekuja ni mke wake, “sawa boss, sisi tupo hapa hotelini tumejipanga vyema, mmoja yupo nje mimi nipo mapokezi, mmoja yupo kwenye gari na mwingine yupo ghorofa ya nne anaangalia kama kuna mtu ataingia” alisema Inno, wakati huo Eze anatazama upande wa korido ambako mke wake alikuwa ndio anaibukia sebuleni, “haya niambie, nani huyo apotezwe?” aliuliza mke wa Eze, huku anaenda moja kwa moja kukaa pembeni ya mume wake na kumuwekea miguu yake minene mapajani na kufanya Eze akunje sura kwa uzito wa mzigo, “hoooo! Ino baadae bwana, msisahau kunipa taarifa” alisema Eze kwa sauti iliyoonyesha amelemewa na mzigo kisha akakata simu.*******

Yap! mida hii ya saa tatu kasoro, ndio mida ambayo mwanadada Veronica alipo simamisha gari lake kwenye maegesho ya magari ya hapa Makuti bar iliyopo maeneo ya mbezi mwisho, karibu kabisa na kituo cha mabasi ya malamba mawili, kabla hajazima gari Veronica akatoa simu yake na kupiga kwa JJ na simu ikaanza kuita.

Simu iliita kwa muda mrefu sana bila kupokelewa, “mh! napiga mara ya mwisho asipo pokea naondoka zangu” alijisemea Veronica huku anabonyeza tena kipigio, lakini kabla simu haijaanza kuita, akashtuka mtu anagusa kioo cha gari lake kwa maana ya kuomba ashushe kioo.

Huyu alikuwa ni kijana mmoja mrefu kiasi, alie valia suruali ya jinsi na tishet nyeusi, Veronica akakata simu na kushusha kioo, “habari yako dada” alisalimia yule kijana, huku anamtazama Veronica kwa macho fulani yenye tabasamu ambalo kama ni mjuzi wa uchunguzi, ungegundua kuwa, alikuwa na kitu fulani sio cha kawaida ndani yake, “salama habari” alisalimia Veronica ambae kama ujuavyo uzuri wake ni wenye kuchanganya, “poa tu dada yangu, samahani dada wewe ndie doctor Veronica James” aliuliza yule jamaa kwa sauti ambayo ilionyesha urafiki, japo kama Veronica angekuwa makini angegundua kitu kwa huyu jamaa,

Hapo Doctor Veronica akagundua kuwa huyu jamaa ni mjumbe wa mchumba wake John Joseph, “yes ndio mimi, vipi una ujumbe wangu wowote?” aliuliza Veronica huku anaachia tabasamu pana, “ndiyo dada yangu, John anamaongezi fulani hapo nyuma, hivyo amesema nikakuonyeshe pakukaa umsubiri mpaka atakapokuja” alisema yule kijana na hapo Veronica akacheka kidogo, “ndio maana hapokei simu, ningeondoka zangu mimi” alisema Veronica huku anapandisha kioo cha gari kabla hajalizima na kushuka toka kwenye gari kisha akaongozana na yule kijana ambae alienda mpaka kwenye ukumbi wa ile bar, akimchagulia sehemu moja tulivu yenye mwanga hafifu yenye watu wachache waliokaa kwa kuachiana nafasi kubwa, “unaweza kukaa hapa ukamsubiri” alisema yule kijana kisha akaondoka zake akipishana na mhudumu alie kuja kumuuliza kuwa anahitaji nini.

Hapo Veronica akawaza kidogo, juu ya kinywaji, kwamba anywe soda au juice, atawezaje kukabiliana na mishikoshiko ya JJ akiwa na akili zake timamu na vipi kama akiagiza wine ya kuondoa aibu na akalewa sana kisha JJ akapata faida kutokana na ulevi wake, “nitakunywa kidogo bwana” alijisemea Veronica ambae aliagiza #mbogo_land coco wine, ambayo pia sio nzuri sana kuitumia ukiwa peke yako.

Mhudumu aliondoka na kufuata kinywaji, na hapo hapo Veronica akatoa simu yake na kuanza kupekuwa jumbe zilizoingia na zilizo na kipaumbele alizijibu huku nyingine akaziacha, lakini mpaka anamaliza, hakuweza kuona ujumbe toka kwa mchoraji wake, hivyo akaandika ujumbe wake, “ndio kusema bado upo busy na mteja wako, usikute ni mke wa mtu” aliandika Veronica akiweka na vikaragosi kicheko kisha akatuma kwenda kwa mchoraji na kuiweka simu mezani akitarajia muda wowote kuona ujumbe ukiingia simuni, na wakati huo muhudumu alikuwa anakuja na kinywaji alichokiagiza, na hapakuwa na dalili ya kuonekana kwa mchumba wake JJ, masikini Veronica hakujua kuwa
kuna mtu alikuwa mita chache toka pale alipo anamtazama na kufuatilia kila anacho kifanya.*******

Yap!, sasa twendeni Kigamboni nadhani bado hujamsahau tajiri na muuzaji wa dawa za kulevya, bwana Uledi Songoro, mzee Matata muuzaji wa dawa za kulevya na jambazi kubwa mwenye asili ya DRC, ambae ni m’babe na mkatili, ambae masaa ishirini na nne yaliyopita alivamiwa na kijana mmoja anaendesha gari aina ya BMW Series 7, kijana ambae alimfanyia maangamizi ya kutisha na kuondoka na mschana Zamda mtoto wa bwana Simba, ambae alimchukuwa kwaaji ya kumbaka kwa lengo la kutoa onyo kwa mzee Simba kuhusu malipo ya fedha zake za mauzo ya dawa za kulevya.

Bwana Songoro, usiku huu bwana alikuwa ndani ya jumba lake la ufukweni anabugia pombe kama ng’amia mwenye kiu kali, huku pembeni yake akionekana mwanamke mmoja alievalia nusu utupu akiwa anamgusa gusa sehemu nyeti pasipo kujali vijana kadhaa waliokuwepo eneo lile wamesimama na na bastora zao viunoni mwao.

Bwana Songoro ambae alisha muachia CP Ulenje, jukumu la kumtafuta Dereva wa BMW jeusi, kama wanavyoita wenyewe kwa madai ya kwamba amemletea dharau na hasara kubwa sana, hakika alionekana kukosa raha sana, maana haikuwahi kutokea mtu akamletea dharau kama hizo, yaan kuingia ndani ya ngome yake na kupiga walinzi wake wote huku akifanya anachokitaka, “mbona sipati taarifa ya kukamatwa kwa huyu mpuuzi” alipiga kelele Songoro, alieonekana kujawa na hasira kali sana, huku anachukuwa simu yake na kupiga namba ya CP Ulenje, ambayo inaanza kuita mara moja.

Bahati ipo upande wake, simu iliita sekunde chache nakupokelewa mara moja, “Ulenje sijapata taarifa yoyote toka jana, inamaana umeshindwa kazi?” aliuliza Songoro kama vile anaongea na mfanyakazi wake, “tulia bwana Songoro, mbona una wasi wasi sana kama unaoga nje? tayari dogo ameingia kwenye mtego, ujuwe huyo dogo anaejiita dereva, ana maadui wengi sana, sio wewe peke yako yeye ndie alie kimbia na dhahabu ya wale watu toka #mbogo_land, hivyo bahati nzuri wamepata namba yake na sasa wamemuingiza kwenye mtego mkubwa sana, ni wazi leo lazima awe mwenye bahati mbaya” alisikika Ulenje toka upande wa pili wa simu akiongea kwa kujiamini, “lakini hilo sio lengo langu, mimi nataka awe mikononi mwangu, nimuuwe mwenyewe” alisema Songoro kwa sauti iliyojaa jazba, “ujue Songoro, mambo hayapo kama unavyodhania, hawa jamaa wananguvu kuliko wewe, ni bora ukawa mpole uangalie wanafanya nini, pengine inaweza kukusaidia baadae” alisema Ulenje kwa sauti fulani yenye kujaribu kumtuliza Songoro, “nani kakuambia nina tegemea nguvu ya mtu mwingine, sihitaji huo upuuzi Ulenje, namtaka huyo fala haraka” alipiga kelele Songoro.

Nadhani Ulenje alikereka na kelele za Songoro, maana alikata simu mara moja, “hivi huyu mjinga anapata wapi kiburi cha kunikatia simu?” aliuliza Songoro kwa sauti yenye mshangao, huku anapiga tena simu kwa Ulenje, simu ambayo safari hii haikupokelewa hata kwa bahati mbaya, “inamana tumeanza kudharauliana kiasi hicho Ulenje, umesahau mimi ndie ninae kuweka mjini, au kwasababu una washirika wengine wenye wanaokupa dhahabu za #mbogo_land, aliuliza Songoro huku anapiga tena simu kwa Ulenje, ambae licha ya kupigiwa mara kadhaa lakini hakuipokea, Kumbe Deus ile kazi aliombiwa saa mbili ni mtego! sasa itakuwaje? Na kuhusu doctor vero maan yashaanza mapicha picha itakuwaje tena! ENDELEA Kufuatilia mkasa huu NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
NYUMA YA MLANGO WA ADUI
SEHEMU YA THEMANINI NA SITA
MTUNZI : Mbogo EDGAR
WHATSAPP : 0743632247 (KWAMATUMIZI YA OFISI TU)
TULIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA TANO: Nadhani Ulenje alikereka na kelele za Songoro, maana alikata simu mara moja, “hivi huyu mjinga anapata wapi kiburi cha kunikatia simu?” aliuliza Songoro kwa sauti yenye mshangaobhuku anapiga tena simu kwa Ulenje, simu ambayo safari hii haikupokelewa hata kwa bahati mbaya, “inamana tumeanza kudharauliana kiasi hicho Ulenje, umesahau mimi ndie ninae kuweka mjini, au kwa sababu una washirika wengine wenye wanaokupa dhahabu za #mbogo_land, aliuliza Songoro huku anapiga tena simu kwa Ulenje, ambae licha ya kupigiwa mara kadhaa lakini hakuipokea. ….ENDELEA…

Hapo sasa akiwa mwenye hasira kali, Songoro akaiweka simu mezani na kumtazama mmoja kati ya wale vijana waliokuwa wamesimama, “Side hivi unamfahamu huyu mtoto mwenye BMW jeusi anapatikana vipi?” aliuliza Songoro kwa sauti iliyoonyesha hamu kubwa ya kumpata dereva wa BMW jeusi, “boss nilishawahi kusikia habari zake, lakini sikuwahi kufahamu anakoishi” alijibu Side, ambae ni mmoja kati ya vijana waliotoka kwa Eze kuja kuziba pengo la wale vijana waliopigwa na dereva jana usiku.

Jibu la Side nikama lilizidi kumtia hasira Songoro, ambae alishika kichwa chake kwa mikono yote miwili na kujikuna nywele, “nitakukamata tu we mshenzi” alipiga kelele Songoro nakuwafanya wakina Side wamtazame mzee huyo mwenye hasira kali****

Mbogo Land, ndani ya jiji la TT waziri Chitopelah, alikuwa nyumbani kwake anasubiria matokea ya mambo yanayo endelea nchini Tanzania, kwa maana ya utekelezwaji wa mipango miwili ambayo mmoja wapo ungewezesha kupatikana kwa fedha za kufanyia malipo ya silaha ambazo zinatarajiwa kutumiwa katika mapinduzi ya kijeshi kuung'oa uongozi wa kifalme chini ya mfalme Elvis wa kwanza.

Wakati anawaza hayo waziri huyu, ambae alipewa uwaziri akiwa na cheo cha brigediaa general, mara akasikia simu yake inaita, akanyakuwa haraka na kutazama mpigaji, akajikuta anaipokea kwa pupa, “niambie Chiro, vipi wamesha fika?” aliuliza Chitopela, akiwa mwenye shauku ya kujua jambo, “ndiyo boss, wapo kumi na sita wameriport ubalozini na wamesha pelekwa Angoni ams hotel kule msamala” alisema huyo mtu alieitwa Chiro, “kwahiyo umejaribu kudodosa wamefuata nini huko Tanzania?” aliuliza Chotopelah, boss kwa kweli mpaka sasa hivi ninavyoongea na wewe, nawaona askari watatu, wamevaa nguo za kiraia wanaingia kwenye gari moja wanatoka hapa hotelini, sijajua wanaelekea wapi, ndio najaribu kuwa fuatilia” alisema Chiro, kabla hawajaagana na kukata simu, ikitanguliwa na maagizo ya kutokuacha kuwafuatilia, yaliyotolewa na Chitopelah.

Huyo bwana anaitwa Chiropo, kwa lugha ya asili ya mbogo Land maana yake mtoto wa kiume mropokaji, kwa mtoto wakike ungesema Kiropo, na kwa mwanaume mtu mzima ungesema Muropo, na kwa mwanamke mkubwa ungesema Tiropo.

Huyu ni mfanyakazi wa serikali katika kitengo cha MLA ya Mbogo Land, alieletwa nchini Tanzania, kama mmoja wa watunza nyaraka wa ubalozi wao, lakini tayari alishakutana na ushawishi wa bwana Dickson chitopelah, na kuwa jicho lake pale kwenye ubalozi mdogo wa Songea, kama alivyofanya sehemu nyingine, nje na ndani ya nchi, serikalini na kwenye sekta binafsi, ambazo aliamini kuwa zinahusika kwa namna moja au nyingine na mpango wake.**********

Turudi Dar es salaam, mida hii ya saa tatu, jiji lilikuwa limechangamka kweli kweli, ungesema ni saa moja za jioni, maana pilika zilishamili, watu walionekana kukatiza barabarani, pia magari yakiwa ni yale binafsi ya serikali na yale mabasi madogo ya abiria yaliyojaza abiria, yakiingia na kutoka katikati ya jiji, bila kusahau pikipiki na bajaji zilizo onekana kuwa kama kivutio cha macho ya abiria waliopo kwenye magari ya abiria na magari binafsi, au watu walio kuwa wanatembea kwa miguu na walio kuwa wametulia pembezoni mwa barabara wakiuza au kununua biashara za jioni, kama vile mahindi ya kuchoma yale ya kupaka chumvi, mihogo au mishikaki, waliojionea jinsi vyombo hivyo vya usafiri vikipenya mbavuni mwa magari pasipo kujali hatari yoyote ambayo inaweza kuwatokea wao madereva na abiria wao.

Sisi twendeni maeneo ya shekilango, mita chache toka barabara ya morogoro, pembezoni mwa barabara iendayo Bamaga, nje ya jengo kubwa la Sisterfada Hotel, tunalioona gari aina Toyota V 8, likiingia kwenye maegesho ya chini ya jengo lile.

Baada ya taratibu zote za kuzima gari hilo kufanyika, mlango wa dereva unafunguliwa na anashuka mzee James Kelvin na mkoba wake, kisha anabonya kiongozea mbali cha gari lake kwa kufunga gari lake, ambalo linajifunga kisha anaweka funguo mfukoni na kuanza kutembea kuelekea upande wa kutokea pale kwenye maegesho na kulifuata lango lakuingilia ndani ya hotel hii yenye hadhi kubwa, ambayo ukitazama muonekano wa pale mbele, ungeona kuna watu wachache waliokuwa wakiingia ndani, huku wakipokelewa na wanausalama wa hotelini pale waliovalia suruali ya dark brue na mashati meupe, huku viatu vyao vikiwa vyeusi.

Kama ilivyokuwa kwa wale wageni wengine, pia bwana James anapokelewa na walinzi, “karibu muheshimiwa” anasema mlinzi mmoja kwa sauti iliyojaa unyenyekevu, ni wazi kwamba alimtambua tajiri huyu mkubwa, “Asante sana” aliitikia bwana James, huku anakatiza kwenye lango kubwa la vioo na kuanza kutembea kuelelekea kwenye lift, huku macho yake yakikutana na macho ya kijana mmoja aliekuwa amekaa kwenye viti vya wateja wasubiriao huduma, yeye hakumjali akaingia kwenye lift na kubonya namba tatu, akimaanisha kuwa ni ghorofa ya tatu, lift inafunga mlango.

Sekunde chache baadae lift inafungua mlango wake, kisha mzee James anatoka na kuelekea mpaka kwenye mlango wa chumba namba nane wa ghorofa hili la tatu, mlango ambao wanaonakena vijana wawili waliovalia suit nyeusi, na kila mmoja akiwa ameshika begi kubwa mkononi ana wasalimia, “habari zenu vijana” nao wanaitikia, “salama karibu” ni sauti kavu toka kwa mmoja kati yao, huku yule mwingine anafungua mlango wa chumba namba nane, mzee James nae anaingia ndani akikutana na moshi mzito wa siraga bwege..

Naaam ile mzee James anaingia ndani ya chumba, anashikwa na mshangao mkubwa sana, mapigo ya moyo yanaanza kwenda mbio, wasi wasi unamshika mzee huyu, ni kwaajili kile anacho kiona mbele yake, sio tu ukubwa wa chumba kile kikubwa chenye kitanda kikubwa sana na makochi mawili mazuri makubwa, nasiyo ule moshi wa bangi ulio sambaza harufu mle ndani.

Ila ni watu watano, aliowakuta mule ndani, “karibu mheshimiwa, sikufikiria kama utakuja kwa wakati” lilikuwa ni karibisho toka kwa mtu mmoja aliekuwa amekaa kwenye moja kati ya yale makochi mawili, ambae licha ya kuvaa suit yake nyeusi yenye kufanana na wale vijana wawili nje ya mlango, lakini alikuwa anavuta bangi, akisindikizia kwa pombe kali iliyokuwa mezani.

Mzee James anashindwa kuitikia karibisho toka kwa yule jamaa, baada yake anatazama kushoto na kulia na mbele yake upande wa dirishani, ambako, kulikuwa na vijana wanne walio valia suit nyeusi kama wenzao, walio simama kwa mtindo wa kuwazunguka, mkononi mwao walikuwa wameshikilia bunduki aina ya H&K G95 ASSAUL RIFLE, yani HECKLER &KOCH G95 TOKA GERMANY ASSAULT RIFLE 5.56MM toka ujerumani, wawili wakiwatazama na wawili wakiwa wamesimama upande wa dirishani, wakitazama upande nje, ambao ni upande wa ubungo plaza yani sio upande wa barabarani.

Taswira ilikuwa ni kama watu fulani wanaigiza filamu ya kijambazi, “asante mheshimiwa, lakini samahani jamani nadhani nimekosea chumba” alisema mzee James, kwa sauti tulivu ya unyenyekevu huku anageuka na kuutazama mlago ambao tayari ulikuwa umesha fungwa, “hujakosea bwana James, sisi ni wajumbe wa mheshimiwa Chitopelah, toka #Mbogo_land, tupo hapa kuongea na wewe” alisema yule aliekuwa amekaa kwenye kochi anaburudika kwa mchanganuo wa bangi na pombe kali.

Hapo bwana James ambae mpaka sasa hakuona dalili ya maongezi ya kibiashara, aligeuka na kuwatazana wake wajumbe wa Chitopelah, ambao walikuwa wamekaza sura zao wakimtazama, kasoro wale waliokuwa wanatazama nje kupitia dirishani, na huyu alie kaa, ambae alionekana kuachia tabasamu la sanifu, kwamba bwana James ameshaingia mikononi mwao, hivyo nilazima akubaliane nao.

Kiroho shingo upande na mashaka makubwa, bwana Jamaes akaenda kukaa kwenye lile kochi lililokuwa tupu, “ok! nakusikiliza mheshimiwa” alisema james, ambae alikuwa ameukumbatia mkoba wake, huku kichwani yakimjia maswali mfululizo, yote yakiwa yana jiuliza nia kubwa ya bwana Chitopelah kufanya biashara ya siri ni nini.*******

Twende Makuti pub kule mbezi luis au mbezi mwisho kama unavyoweza kuita, bado anaonekana Veronica akiwa amekaa kwenye meza yake anakunywa wine taratibu, macho ameyaelekeza sehemu ya kutokea, huku mara kwa mara akitazama simu yake na kujaribu kuipiga namba ya JJ, ambayo haikupokelewa, “dakika kumi zikipita naondoka zangu” alijisemea Veronica huku anabofya simu yake na kuweka kwenye sehemu ya kuandikia ujumbe wa whatsapp, anagusa namba ya mchoraji wake unakuja uwanja wa ujumbe, halafu anaanza kuandika, “huyo mteja ulienae busy ni wakike au wa kiume?” anamaliza kuutuma kwenda kwa mchoraji, kisha akatulia akaandika mwingine wakati huo huo na sehemu hiyo hiyo ya mchoraji, “maana naona umetumia muda mrefu sana” safari hii anamalizia kwa vikaragosi vya mshangao, kisha akautuma na kuweka simu mezani.

Naam Vaeronica anakaa tena dakika kumi nyingine, huku mara kwa mara akijaribu kupiga simu pasipo mafanikio na hapo Veronica anakosa uvumilivu, pasipo kujali kwamba chupa yake ya wine ipo nusu, akainuka na tayari kuondoka.

Lakini kabla hata hajapiga hatua moja akashkwa mkono, “ni vyema kama ukikaa chini na kusikiliza ujumbe wako” ilisikika sauti ya mwanaume alie mshika mkono, Veronica anageuza uso wake na kumtazama aliemshika mkono, ambae anamtambua kuwa ni yule aliempokea mwanzo pale kwenye maegesho, lakini safari hii hakuwa mwenye lile tabasamu la uongo, “kwani kuna tatizo gani, John amepatwa na tatizo?” aliuliza Veronica, huku anakaa tena kwenye kiti chake, akionyesha kupatwa na wasi wasi, “sikia dada, unatakiwa kuwa mpole na kunisikiliza” alisema yule jamaa na Veronica akatulia kumsikiliza.

Hapo yule jamaa akatoa simu na kufungua kwenye hifadhi ya video na picha, anaigusa moja kati ya Video ambayo inaanza kucheza, huku Veronica anaitazama video ambayo inawaonyesha wanaume wawili wakiwa ndani ya jengo moja kubwa lisilomaliza ujenzi, huku mwanaume mwingine anaonekana akiwa amelala chini, huku nguo zake zikiwa zimechafuka damu chapa chapa, wasi wasi mkubwa unamshika Veronica mapigo ya moyo yanamwenda mbio, “ni nani huyu, usiniambie kama ni John” alisema Verionica kwa sauti yenye kujawa na wasi wasi na mshtuko, “ni yeye, wala hujakosea” alisema yule jamaa, wakati huo video inaonyesha kwa ukaribu zaidi tukio lile na kuivuta sura ya mtu alielala pale chini. Naam mbona kama JJ nae yupo matatizoni?Itakuwaje sasa? ENDELEA Kufuatilia mkasa huu wa NYUMA YA MLANGO WA ADUI unao kujia hapa hapa jamii forums
 
Back
Top Bottom