Simulizi ya kichawi: Makaburi ya wasio na hatia (The Graves of The Innocents)

Simulizi ya kichawi: Makaburi ya wasio na hatia (The Graves of The Innocents)

Sehemu ya thelathini na mbili______32



ILIPOISHIA:

Wote waliacha kila walichokuwa wanakifanya, wakawa wananitazama kwa macho makali. Sikuelewa nini hasa kimetokea, wakati nikiendelea kuwatazama vizuri kwa mara ya pili, kuna jambo moja lilinishtua mno mpaka nikajikuta nimetoa mkono mfukoni, giza likarudi kama lilivyokuwa mwanzo.

SASA ENDELEA…

Japokuwa kulikuwa na giza, niliweza kuonamacho ya wale watu yaking’ara kama wanyama wakali wa porini, nikawa najilaumu kwa kile nilichokifanya. Hata sijui nini kilitokea kwani kuanzia mwanzo nilikuwa nimejiapiza kwamba siku hiyo sitaleta ujuaji wowote mbele ya watu hao lakini cha ajabu, ndani ya muda mfupi tu, tayari nilishakuwa nimewekwa mtu kati.

Sikujua safari hii wataniadhibu vipi lakini niliamua kupiga moyo konde, liwalo na liwe. Bado nilikuwa najiuliza maswali mengi kuhusu kile kilichokuwa kwenye mfuko wangu, sikujua ni nini na kilikuwa na uhusiano gani na ule mwanga uliotokeza ghafla mle ndani ya mahabusu.

Sijui nilipata wapi ujasiri lakini nilijikuta nikiingiza tena mkono taratibu mfukoni, nilipokigusa tu kile kitu mle mfukoni, ule mwanga ulirudi tena vilevile, wale watu ambao safari hii walikuwa wamejikusanya na kutengeneza kama nusu duara hivi, waliinua wote shingo zao na kunigeukia tena, nikakishika kile kitu kwa nguvu huku na mimi nikiwa nawatazama.

*Usiache kutembelea Simulizi za Majonzi

Katika hali ambayo sikuitegemea, nilishangaa wa kwanza akisimama na kukimbilia kwenye ile kona alipokuwa amekaa yule mahabusu ambaye awali alikuwa akipiga kelele. Safari hii alikuwa amelala, tena kwa kuinamisha kichwa mbele, katikati ya miguu yake.

Nikamuona yule mtu wa kwanza, mikono yake akiwa amejiziba sehemu nyeti, akisogea mpaka kwenye kona, alipoikaribia, aligeuka na kuanza kutembea kinyumenyume, akamkanyaga yule mahabusu kisha nikashangaa akipotelea kwenye ukuta.

Ni hapo ndipo nilipoamini yale maneno niliyowahi kuyasikia kwamba wachawi wanao uwezo wa kuingia na kutoka ndani ya nyumba hata kama milango imefungwa. Nilishindwa kuelewa ni nini hasa kilichofanya iwezekane kwa yule mtu kupotelea kwenye ukuta.

Nikiwa bado nimepigwa na butwaa, nilimuona mwingine naye akiinuka, akaanza kutembea kuelekea kwenye ile kona, wengine nao wakasimama, wakawa wanatembea huku wote wakiwa wananitazama kwa macho mabaya. Ni kama nilikuwa nimewavurugia mipango yao, nikazidi kukishikilia kile kitu mfukoni.

“Hiyo ndiyo nafasi yako ya kutoka mahabusu, hakikisha unamshika mmoja kati yao na kumvua usinga aliovaa shingoni kisha na wewe utatoka kama hao wengine walivyotoka,” nilisikia sauti masikioni mwangu ambayo niliitambua vizuri kwamba ni ya baba.

Bado sikuwa nimeelewa ni mbinu gani anayoitumia baba kuwasiliana na mimi kwa sauti ambayo hakuna mtu mwingine yeyote anayeisikia. Hata hivyo, sikutaka sana kuhoji, nilichokifanyailikuwa ni kufuata maelekezo.

Cha ajabu, wale watu walipoona nawafuata, walianza kukimbia lakini kwa sababu ya nafasi ndogo iliyokuwepo, walishindwa kutoka wote kwa mkupuo, nikafanikiwa kumkamata mmoja ambapo moja kwa moja nilipeleka mkono shingoni ambapo alikuwa amevaa kitu kama kamba nyembamba lakini iliyosokotwa kwa nywele, ikakatika na kubaki mkononi mwangu.

Kitendo hicho kilisababisha alie kwa sauti kubwa lakini cha ajabu sasa, sauti yake ilitoka kama zile sauti zinazotolewa na mapaka yanayolia usiku, akadondoka chini na kuendelea kulia kwa sauti kubwa kama paka.

*Usiache kutembelea Simulizi za Majonzi

Cha ajabu, wakati nikiwa nimeshageuka na kuupa mgongo ukuta, tayari kwa kufanya kile baba alichoniambia nikifanye, yule mtu aliinua uso wake huku akionesha ishara kwamba nimsamehe. Kilichonishtua ni kwamba sura yake ilikuwa ikifanana na mimi kwa kila kitu wakati awali hakuwa vile.

Nikiwa bado naendelea kumshangaa, nilisikia sauti ya baba ikinisisitiza kutoka haraka. Sikuwa nimewahi kushiriki uchawi mkubwa kiasi hicho, nikawa natetemeka nikiwa siamini kama kweli naweza kupita ukutani. Nilipiga hatua kurudi nyuma mpaka nilipoufikia ukuta.

Cha ajabu, nilipouegamia ulilainika kama pazia, nikapiga hatua nyingine na kujikuta nusu ya mwili wangu tayari ipo nje, nikapiga hatua nyingine, nikawa nimetoka nje kabisa. Nilibaki nimesimama kwenye maua yaliyopandwa pembezoni mwa ile mahabusu nikiwa bado siamini.

Niligeuka na kutazama huku na kule, hakukuwa na mtu yeyote eneo hilo, harakaharaka nikatembea na kupotelea kwenye kota za askari wa kituo kile, nikawa nazidi kutembea nikiwa sielewi naelekea wapi. Nilizimaliza kota hizo, kwa mbali nikawa nawasikia mbwa wakibweka, nikaongeza mwendo na muda mfupi baadaye, nilitokeza kwenye barabara ya lami.

Siwezi kuficha jinsi nilivyofurahi kutoka mle mahabusu. Hapohapo nikajikuta eti na mimi nikitamani kuwa mchawi ili nipate nafasi ya kufaidi mambo mengi kwenye hii dunia ambayo binadamu wa kawaida hawawezi.

Hebu vuta picha, hata kama ni wewe, yaani ndugu yako yupo gerezani anateseka halafu leo ukiambiwa kuna ujuzi ukifundishwa ndugu yako anaweza kutoka kiulaini, tena bila kutumia nguvu wala fedha, huwezi kutamani kweli?

Labda kamauna imani kali ya dini ndiyo unaweza kuukwepa mtego huo lakini kwangu mimi, siwezi kuficha kwamba nilifurahi sana na kutamani kuwa mchawi, tena niliyebobea. Nilijiapiza kwamba nitakapopata nafasi ya kuzungumza na baba, nitamueleza nia yangu bila kujali atanichukuliaje.

Niliendelea kutembea kufuata ile barabara ya lami huku muda mwingi tabasamu likiwa limechanua kwenye uso wangu. Tafsiri ya kile kilichotokea n kwamba asubuhi polisi wangeingia na kufanya ukaguzi mle mahabusu wangekuwa na imani kwamba bado nipo, labda watashtuka kwa nini sijavaa nguo kwa sababu yule mchawi hakuwa amevaa nguo.

*Usiache kutembelea Simulizi za Majonzi

Nilielewa kwa nini baba aliniambia nisitoe maelezo yoyote kwa sababu kama yule mtu niliyebadilishana naye na kumuacha mle ndani mahabusu atahojiwa, maelezo atakayoyatoa yatakuwa hayaungi chochote na tukio lililotokea kwa hiyo uwezekano wa baadaye kuja kuachiwa kwa sababu ya kukosekana ushahidi ulikuwa mkubwa.

Sikujua atasota kwa muda gani mle mahabusu, tena kesi yenyewe ikiwa ni ya mauaji lakini niliona kama anastahili maana ni uchawi wa aina gani watu wanaenda kuufanyia sehemu hatari kama mahabusu? Niliendelea kutembea huku mara kwa mara nikicheka mwenyewe maana nilijiona bonge la mjanja kuukwepa msala ule.

Nikiwa naendelea kutembea nikiwa sijui naelekea wapi kwa sababu kama nilivyoeleza, sikuwa naijua mitaa ya Jiji la Dar es Salaam, nilisikia vishindo vya mtu akija huku akikimbia akitokea nyuma yangu. Baba amewahi kuniambia kwamba ukiwa unatembea usiku, ni mwiko kugeuka nyuma.

Alizidi kunikaribia, nikawa najiuliza kama atakuwa ni mtu mbaya itakuwaje? Niliendelea kujikaza kisabuni, vishindo vikazidi kunikaribia na alipofika usawa wangu, nikasikia akipunguza mwendo. Kilichonifanya niamini kwamba hawezi kuwa mtu mbaya, ni jinsi manukato aliyokuwa amejipulizia mwilini yalivyokuwa yakinukia vizuri.

“Mambo,” sauti ya kike ilisikika, safari hii ikiwa usawa wangu kabisa, ikabidi nisimame, nikageuza shingo yangu upande wa kulia alipokuwepo mtu huyo aliyenisalimu. Muda huo kwa makadirio ilikuwa ni kama saa nane za usiku maana kuna sehemu nilipita nikasikia redio kwa mbali ikitangaza kwamba ni saa nane kasoro za usiku.

“Mbona umeshtuka Togo!” alisema huku akinisogelea. Siwezi kuficha, mshtuko nilioupata nusura nidondoke na kuzimia.

Je, nini kitafuatia?
 
Sehemu ya 33



ILIPOISHIA:

Muda huo kwa makadirio ilikuwa ni kama saa nane za usiku maana kuna sehemu nilipita nikasikia redio kwa mbali ikitangaza kwamba ni saa nane kasoro za usiku.

“Mbona umeshtuka Togo!” alisema huku akinisogelea. Siwezi kuficha, mshtuko nilioupata nusura nidondoke na kuzimia.

SASA ENDELEA…

Alikuwa ni yule msichana ambaye mchana wa siku iliyopita alinifia gesti tukiwa kwenye mechi ya kirafiki na kunisababishia matatizo makubwa mpaka nikapelekwa mahabusu nikikabiliwa na kesi kubwa ya mauaji.

Nilitaka kukimbia nikahisi mwili wangu ukiishiwa nguvu, nilitaka kupiga kelele lakini sauti ikawa haitoki, nikabaki nimesimama palepale nikitetemeka kama mbwa mbele ya chatu, akawa ananishangaa usoni kama anayejiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu.

“Wewe si ulikufa wewe?” nilisema huku safari hii miguu yangu ikiwa imeanza kupata nguvu, nikawa narudi nyuma nikiangalia upenyo wa kukimbia. Ni kama alishagundua ninachotaka kukifanya, akacheka na kunisihi nisikimbie bali kuna jambo la muhimu anataka kuniambia.

Maneno yake yaliingilia sikio moja na kutokea la pili, akili yangu ilinifanya niamini kwamba hakuwa yeye bali mzimu wake, akawa anazidi kunisogelea mwilini.

*Usiache kutembelea Simulizi za Majonzi

“Najua unafikiri labda mimi ni mzimu, siyo, nipo hai wala sijafa na leo nitakutajia mpaka jina langu,” aliniambia huku akizidi kunisogelea. Mazungumzo yake hayakuonesha kama alikuwa mzimu au alikuwa na nia mbaya na mimi lakini bado niliendelea kurudi nyuma, naye akawa anazidi kunifuata.

“Jina langu naitwa Isrina au wengi huwa wanapenda kuniita Isri. Nakuomba unipe japo dakika chache nikueleze kilichotokea leo na historia fupi ya maisha yangu, pia nataka nikueleze kitu ambacho hukijui kuhusu wewe ambacho kitakusaidia sana,” alisema kwa sauti ya upole.

Sijui nini kilitokea lakini nilijikuta nikishawishiwa na maneno yake matamu, nikasimama, akazidi kunisogelea mwilini na kunikumbatia kimahaba. Kitendo hicho kilisababisha hofu yote niliyokuwanayo iyeyuke ghafla kwa sababu nimewahi kusikia kwamba tofauti ya mtu na mzimu, ni kwamba mzimu unakuwa na mwili ambao japo unauona, hauwezi kuushika ukashikika.

Nimewahi kusikia kuwa miili ya mizimu inakuwa kwenye mfumo wa hewa, kwamba unamuona mtu lakini ukitaka kumkumbatia anakuwa kama hewa, hashikiki. Ili kuwa na uhakika, na mimi nilimshika kiuno chake, kweli kikashikika vizuri kabisa, tukawa tunatazamana usoni.

Tukiwa bado tunaendelea kutazamana, alinibusu kwenye shavu langu la kushoto, nikajikuta mwili mzima ukisisimka na ndani ya sekunde chache tu, ile hali iliyokuwa inanisumbua sana, ya kuwa na kiu kubwa ya kucheza mchezo wa kikubwa ilinianza tena.

Ni kama Isri alielewa nilichokuwa nakihitaji, alichokifanya ilikuwa ni kuendelea kunitoa hofu huku akiendelea kunichokoza hapa na pale, hali ikazidi kuwa tete kwa upande wangu.

Usiku huo kulikua kimya kabisa, hakukuwa na mtu yeyote aliyekuwa akuipita barabarani, kelele pekee zilizokuwa zinasikika zilikuwa ni za mbwa waliokuwa wakibweka mitaani. Ilibidi tusogee pembeni ya barabara, hakukuwa na muda wa kupoteza, kila mmoja alijiweka kwenye mkao wa kula na kazi ilianza palepale.

Kwa jinsi nilivyokuwa na ‘kiu’, nilimsambaratisha vilivyo Isri mpaka ikabidi aweke mpira kwapani. Hata hivyo, angalau kidogo nilianza kujisikia vizuri, akili yangu sasa ikahamia kwenye kutaka kuujua ukweli kwa sababu nilishahakikisha kwamba Isri hakuwa amekufa.

“Haya niambie kilichotokea.”

*Usiache kutembelea Simulizi za Majonzi

“Kwanza nashukuru,” alisema huku akinikumbatia na kunibusu huku tabasamu pana likiwa limechanua kwenye uso wake.

“Usijali, ahsante na wewe,” nilisema, akazidi kucheka. Alivuta pumzi ndefu na kunitazama usoni, Japokuwa ilikuwa ni usiku, kwa msada wa mbalamwezi niliweza kumtazama vizuri jinsi alivyokuwa ananiangalia kwa macho yaliyojaa ujumbe.

Alishusha tena pumzi ndefu kisha akanikumbatia na kujilaza kifuani kwangu, akaniambia kama sitajali, tutafute sehemu na kukaa kwa sababu alikuwa amechoka sana. Nilimkubalia, tukasogea kwenye nyumba ambayo ilikuwa ikijengwa lakini bado haijakamilika, tukakaa kwenye msingi na kuanza kuzungumza.

Aliniambia kwamba aligundua kwamba nina kitu fulani cha kipekee siku ya kwanza tulipokutana ndani ya basi, wakati tukisafiri kutokea Mbeya kuja Dar es Salaam. Aliniambia kwamba yeye amezaliwa katika ukoo wa kichifu kwani babu yake mzaa baba, alikuwa ni kiongozi wa mila wa Wanyakyusa waliokuwa wakiishi kandokando la Mlima Rungwe na alikuwa akiheshimika sana. Aliniambia kwamba hata babu yake huyo alipofariki, alimrithisha mikoba yake baba yake ambaye licha ya kuwa msomi, akiwa ni daktari kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, pia alikuwa akiendelea na shughuli za kimila na ndiyo maana yeye alikuwa na uwezo wa tofauti na watu wengine kwani ndani kwao yeye ndiye aliyekuwa wa kwanza kuzaliwa.

Maelezo hayo bado hayakuwa yamenisaidia kuelewa chochote, niliona kama ananizungusha tu lakini sikutaka kumkatisha, nikatulia na kuendelea kumsikiliza.

Aliniambia kwamba kwa kuwa yeye ndiye mtoto wa kwanza kwenye familia yao, na kawaida zile kazi za kimila huwa zinarithishwa kwa mtoto wa kwanza, baba yake alikuwa amefanya kitu kimoja kibaya sana kwenye maisha yake ndiyo maana siku aliponiona mimi alifurahi sana.

“Unamaanisha nini?”

“Mimi ni kaburi la wasio na hatia Togo, nimeamua kukueleza ukweli kwa sababu wewe ndiye mwanaume pekee ambaye umeweza kuuvuka mtego wa kifo,” aliniambia, nikawa simuelewi kabisa. Sikuelewa anamaanisha nini anaposema yeye ni kaburi la wasio na hatia na anamaanisha nini anaposema mimi nimeweza kuuvuka mtego wa kifo?

Nikiwa bado na shauku kubwa ya kutaka kumsikiliza alichomaanisha, nilipoinua uso wangu na kutazama upande wa barabarani, nilishtuka sana kuona kulikuwa na watu wengi wamekusanyika, wote wakiwa wanatutazama.

“Mungu wangu,” nilisema kwa mshtuko kwani ilionesha kuna jambo halikuwa sawa kwetu na ndiyo maana walikuwa wakitutazama. Tofauti na mimi, yeye alipowatazama wala hakushtuka, akaniambia ni haki yao kushangaa kwa sababu hatukuwa tukionekana wa kawaida.

*Usiache kutembelea Simulizi za Majonzi

“Unamaanisha nini?”

“Umewahi kusikia stori za majini?” aliniuliza, nikamgeukia na kumtazama usoni kisha nikawatazama tena wale watu, walikuwa wakizidi kuongezeka kwa wingi, safari hii baadhi yao wakawa wanatupiga picha kwa kutumia simu zao. Niliweza kuligundua hilo kwa sababu ya mwanga wa flash uliokuwa ukitumulika.

Nilimtaka tuondoke lakini akasema wala nisiwe na wasiwasi, hawawezi kutufanya jambo lolote na hawana uwezo huo. Alipoona situlii, aliniambia nimpe mkono wangu wa kushoto, nikafanya hivyo, akashika kidole changu cha mwisho kisha akaniambia na mimi nifanye hivyohivyo, nikamshika.

“Nahesabu mpaka tatu, nikifika tatu fumba macho na usifumbue mpaka nitakapokwambia,” alisema, nikatii kile alichoniambia. Alipofikisha tatu, nilifumba macho, nikashtukia ghafla tumehama pale tulipokuwa na kwenda upande wa pili, kule barabarani ambako watu wengi walikuwa wamesimama wakishangaa, tukajichanganya na wale watu.

“Hebu angalia wanachokishangaa,” alisema huku akinitaka nitazame pale tulipokuwa tumekaa awali. Macho yalinitoka nikiwa ni kama siamini.

Je, nini kitafuatia?
 
Sehemu ya 34




ILIPOISHIA:

Alipofikisha tatu, nilifumba macho, nikashtukia ghafla tumehama pale tulipokuwa na kwenda upande wa pili, kule barabarani ambako watu wengi walikuwa wamesimama wakishangaa, tukajichanganya na wale watu.

“Hebu angalia wanachokishangaa,” alisema huku akinitaka nitazame pale tulipokuwa tumekaa awali. Macho yalinitoka nikiwa ni kama siamini.

SASA ENDELEA…

Watu wawili, mmoja akionesha kuwa mwanamke na mwingine mwanaume, wakiwa watupu kabisa huku miili yao iking’aa sana, walikuwa wamekaa kwenye msingi wa nyumba, wakiwa wanazungumza. Macho ya kila mmoja yalikuwa yaking’aa sana na nyuso zao zilikuwa na gizagiza fulani ambalo lilifanya iwe vigumu kwa watu kuwatambua sura zao.

“Hivi ndivyo tulivyokuwa tukionekana ndiyo maana unaona hawa watu wote wamekusanyika hapa,” alisema Isri huku akiniegamia.

Nilibaki nimepigwa na butwaa huku nikiwatazama wale watu ambao wala hawakuwa na taarifa kwamba tulikuwa tumeshajichanganya nao. Nilitamani kumuuliza Isri kwamba sasa iweje wale watu wawe wanaendelea kutuona wakati tulishahama na kujichanganya nao? Kabla hata sijamjibu, ni kama alizisoma hisia zangu, akaniambia kile walichokuwa wakiendelea kukiona, ilikuwa ni kiini macho.

Akaniambia kwamba watu wengi hawajui lakini hakuna jambo la hatari kama kusimama usiku na kuanza kutazama vitu usivyovijua au visivyo vya kawaida kwa sababu kama ni watu wenye nia ovu, unapowatazama tu wanajua kwamba unawatazama na wanao uwezo wa kubadilisha kile unachokiona wewe na kukuonesha kitu cha tofauti kabisa.

*Usiache kutembelea Simulizi za Majonzi

Akaniambia ndiyo maana baadhi ya watu hupata matatizo makubwa sana baada ya kuona majini usiku, wengine huona watu warefu wenye kwato, wengine huona miti ikibadilika au huona viumbe vya ajabu wakati kiukweli ni kwamba wanakuwa wamewaona wachawi wakiwa kwenye maumbo yao ya kawaida lakini kwa kuwa wachawi nao wanakuwa wameshagundua kwamba wanatazamwa, wanawafanyia kusudi.

“Sijaelewa, kwa hiyo unamaanisha hata mimi na wewe ni wachawi?”

“Sijamaanisha hivyo.”

“Kwani wewe ulijua kwamba wanatutazama?”

“Ndiyo nilijua,” alinijibu Isri na kunifanya nipigwe na mshangao mkubwa. Watu walikuwa wakizidi kuongezeka na wengi walikuwa ni walinzi wa maeneo ya jirani na pale, wengine wakiwa ni Wamasai na wengine wakiwa ni wafanyabiashara wanaodamka alfajiri na mapema kuwahi kuchukua bidhaa zao.

“Sasa mbona wanazidi kuongezeka, itakuwaje? Ina maana hapa hawatusikii wala hawatuoni?” nilimuuliza, akatingisha kichwa kuonesha kukubali, akaniambia ipo namna ya kuwatawanya. Aliposema hivyo tu, mara nilishangaa wale watu ambao watu wote walikuwa wakiwatazama, wakibadilika na kuwa mbwa wawili wakubwa, dume na jike.

Wakaanza kubweka kwa hasira na kuanza kutimua mbio kulifuata lile kundi la watu. Kiukweli kwa jinsi mbwa hao walivyokuwa wakubwa, wenye hasira huku meno yao makali yakiwa yametoka nje, hata mimi mwenyewe nilijikuta nikiogopa mno. Kufumba na kufumbua, kundi lote lilianza kutimua mbio, kila mmoja kivyake.

Na mimi nilitaka kukimbia lakini Isri alinikamata mkono kwa nguvu, wale mbwa wakawa wanazidi kuja kwa kasi, ikabidi nisimame nyuma yake. Watu walizidi kutimua mbio huku wakipiga kelele na ghafla tukasikia breki kali za gari zikifuatiwa na kishindo kikubwa.

“Tayari!” alisema Isri lakini sikumtilia maanani, akili zangu zote zikawa kwa wale mbwa. Cha ajabu, japokuwa sisi tulikuwa tumesimama, walitupita kwa kasi kubwa na kuendelea kuwatimua wale watu.

“Tayari huko,” alisema Isri kwa mara nyingine, ikabidi nimuulize tayari nini? Akaniambia twende tukajionee wenyewe. Yeye alitangulia, mimi nikawa namfuata, tukanyoosha na ile barabara ya lami mpaka mahali palipokuwa na njia panda, akanionesha kwa kidole nitazame mwenyewe.

Gari dogo aina ya Toyota Carina lilikuwa limeacha njia na kugonga kingo za daraja na kuingia mtaroni, huku barabarani kukiwa na mtu amelala huku damu nyingi zikimtoka akionekana amegongwa na gari lile.

“Mungu wangu,” nilisema kwa mshtuko, akaniambia mtu huyo alikuwa miongoni mwa wale waliokuwa pale wakitushangaa na wakati akiwakimbia wale mbwa ndipo akaingia barabarani bila kutazama, hali iliyosababisha agongwe na gari hilo kisha na lenyewe likapoteza mwelekeo na kugonga kingo za barabara.

Yaani kwa jinsi Isri alivyokuwa akizungumza kirahisirahisi, ungeweza kudhani anasimulia stori au anazungumza masihara, alikuwa anarahisisha sana mambo hali ambayo ilinifanya nigeuke na kumtazama usoni.

Nilishtuka sana nilipomtazama usoni, macho yake yalikuwa yamebadilika rangi na kuwa mekundu sana na kung’aa huku kwenye kingo za mdomo wake kukiwa kama na michuruziko ya damu, meno makali kama ya wale mbwa yakiwa yametokea kila upande.

Mshtuko nilioupata ulikuwa hauelezeki, nikahisi na mimi nipo kwenye mtego mbaya wa kifo, sikusubiri chochote, nilikurupuka na kuanza kutimua mbio kwa kasi kubwa nikiwa hata sielewi naelekea wapi.

“Togo! Togo rudi nakwambia, ohooo!” alisema kwa sauti kali ya kutisha lakini wala sikuvijali vitisho vyake. Jambo ambalo najisifia, ni uwezo mkubwa wa kutimua mbio. Unajua maisha ya kule kijijini tuliyokulia, ilikuwa ni lazima tu ujifunze kukimbia kwa kasi kubwa, kwani kinyume na hapo usingeweza kuambulia chochote mnapoenda kuwinda wanyama wa porini.

Nilikimbia kisawasawa, dakika chache baadaye nikawa nimeshafika mbali kabisa, nikatokezea kwenye barabara kubwa ya lami ambayo japokuwa ilikuwa ni usiku, yenyewe ilikuwa na magari mengi yakiendelea kupita, hasa makubwa ya mizigo.

*Usiache kutembelea Simulizi za Majonzi

Kiukweli nilikuwa mgeni kabisa na jiji lakini niliona ni bora nipotee kuliko kuendelea kukaa karibu na Isri. Japokuwa alikuwa amenieleza mambo mengi kuhusu yeye, yale mambo aliyoyafanya dakika za mwisho, ikiwemo kuwabadilisha wale watu kuwa mbwa, jinsi alivyokuwa akichekelea ile ajali iliyosababisha maafa makubwa na jinsi alivyobadilika na kuwa kama mnyama mkali wa porini, yalinifanya nimuogope mno.

Nikawa naendelea kukimbia pembezoni mwa barabara nikiwa hata sijui naelekea wapi. Kwa mbali kulianza kupambazuka, nikaanza kuona watu wachache wakifanya mazoezi ya kukimbia pembeni ya barabara.

Niliamini hao ndiyo wanaoweza kunisaidia uelekeo wa kufika nyumbani kabla hakujapambazuka kabisa.

Cha ajabu, kila nilipokuwa nikimkaribia mtu yeyote anayefanya mazoezi, alikuwa akitimua mbio za ajabu kunikwepa, mwingine almanusra agongwe na gari kwani alikuwa akija kwa mbele, na mimi nikawa nakimbia taratibu huku nikionesha dalili za kutaka kusimama ili nimuulize lakini ghafla aliponiona, alipiga kelele na kuvuka barabara kwa kasi kubwa mpaka upande wa pili bila hata kutazama, lori kubwa likapiga honi kali na dereva akakata kona kali kumkwepa.

Ilibidi nisimame na kujitazama mwilini kwa nini watu wananikimbia. Jambo la kwanza ambalo lilinishtua, kumbe kwa muda wote huo nilikuwa nikikimbia kwa kutumia mikono na miguu, hata sijui kwa nini muda wote huo sikujishtukia, harakaharaka nikainuka na kusimama kwa kutumia miguu.

Nilipojitazama mwilini, nilishtuka mno kugundua kwamba kumbe nilikuwa na manyoya mengi kama mnyama wa porini, nilipojitazama mikono, nilizidi kupagawa baada ya kugundua kuwa kumbe mikono yangu ilikuwa imebadilika na kuwa kama ya mbwa.

Mara nilishtukia jiwe kubwa likirushwa na kunikosakosa, kabla sijatulia nikashtukia jiwe lingine likinikosakosa, nikaona naweza kuuawa bure, nikaanza kutimua mbio lakini nilipojaribu kukimbia kwa miguu nilijikuta nikishindwa, ikabidi nijaribu kutumia na mikono, nikaweza na kasi ilikuwa kubwa zaidi. Nilikimbia sana huku nikilia nikiwa sielewi nini itakuwa hatma yangu.

Ni hapo nilipogundua kwamba kumbe Isri alikuwa amenigeuza umbo langu na kuwa kama mbwa mkubwa, nilimlaani sana moyoni mwangu na kujikuta nikiyakumbuka maneno ya baba ambaye mara kwa mara alikuwa akinionya kuhusu msichana huyo.

Nikiwa naendelea kukimbia, nilishtukia mtu mmoja akija kwa kasi kubwa nyuma yangu, nikazidi kuongeza kasi lakini kabla sijafika mbali nilishtukia kamba nene ilipita shingoni mwangu na kunifunga kitanzi, nikadondoka chini kama mzigo.

Nikiwa bado hata sijui nini cha kufanya, nilishtukia nikifungwa mikono na miguu, nikajaribu kukurupuka lakini sikuweza kufanya chochote, ikabidi nitulie na kuanza kumtazama ni nani aliyenifanyia kitendo hicho na alikuwa na lengo gani kwangu maana niliona kifo changu kikiwa kimewadia. Na hata kama ningeuawa, kila mtu angeamini aliyekufa ni mbwa mkubwa.

Je, nini kitafuatia?
 
Sehemu ya 35




ILIPOISHIA:

NIKIWA bado hata sijui nini cha kufanya, nilishtukia nikifungwa mikono na miguu, nikajaribu kukurupuka lakini sikuweza kufanya chochote, ikabidi nitulie na kuanza kumtazama ni nani aliyenifanyia kitendo hicho na alikuwa na lengo gani kwangu maana niliona kifo changu kikiwa kimewadia. Na hata kama ningeuawa, kila mtu angeamini aliyekufa ni mbwa mkubwa.

SASA ENDELEA…

“MIMI sipendi mtu mkaidi, siku nyingine nitakuacha uwe mbwa koko, unafikiri unaweza kunikimbia mimi?” alikuwa ni Isri, akiwa anahema huku jasho likimvuja kwa wingi. Nilitaka nimuombe msamaha lakini sauti haikutoka, nikawa naendelea kutokwa na machozi kwa wingi.

Aliniinamia pale chini, akanionyesha ishara nifumbue mdomo, nikafanya hivyo, akaingiza mkono mfukoni na kutoa kichupa kilichokuwa na maji, akayamimina yote mdomoni mwangu. Yalikuwa machungu sana lakini nilivumilia, akanionyesha ishara kwamba niyameze.

Nilifanya hivyo, nikahisi kama mwili wangu wote unawaka moto kwa maumivu lakini kufumba na kufumbua, nilijikuta nikibadilika na kurudi kwenye hali yangu ya kawaida. Alinifungua ile kamba ya shingoni kisha mikononi na miguuni, akaniambia nisimame lakini nilishindwa kufanya hivyo kwani sikuwa na nguo hata moja mwilini, akafungua kimfuko alichobeba mgongoni na kunirushia nguo zangu.

>>>Usikose kutembelea Simulizi za Majonzi

Yaani kama kuna mtu anabisha uchawi haupo kwenye hii dunia, basi anajidanganya sana, kuna uchawi na wachawi na wengine wana uwezo mkubwa kuliko unavyoweza kufikiri. Sijui hata hizo nguo nilizivua saa ngapi na yeye alizipata wapi, sikutaka kuhoji, harakaharaka nilizivaa huku nikitazama huku na kule kama hakuna mtu yeyote anayetuona.

Bado mwili wangu ulikuwa na harufu ya mbwa-mbwa na mikono ilikuwa imechubuka nadhani ni kwa sababu ya kukimbia kama mbwa.

“Kwa nini unanifanyia hivi Isri? Kosa langu ni nini?”

“Sasa kwani mimi nimekufanyaje? Badala unishukuru unaanza kunilaumu tena.”

“Nikushukuru! Nikushukuru kwa lipi,” nilisema kwa hasira huku nikimsogelea Isri mwilini, mwili wangu ukitetemeka kwa jazba.

“Unataka kufanya nini Togo!”

“Nataka unieleze, kwa nini umenifanyia hivi? Unanijua au unanisikia?” niliwaka kwa jazba. Miongoni mwa vitu ambavyo nilikuwa najivunia na hata wenzangu kule kijijini walikuwa wakiniogopa, ni ubavu niliokuwa nao. Hakukuwahi kutokea ugomvi wowote wa kupigana halafu nikashindwa ingawa ilikuwa si rahisi kunikuta nikipigana mpaka mtu anichokoze sana.

“Mimi ni nani kwako?” Isri aliniuliza swali ambalo kidogo lilizifanya jazba zangu zitulie. Aliniuliza swali hilo kwa mara nyingine, halafu akaniuliza kama naamini yeye anaweza kunifanyia jambo baya kwa makusudi kwa jinsi alivyokuwa ananipenda mpaka kufikia hatua ya kunipa mwili wake wa thamani. Akaniuliza kama nimesahau mapenzi makubwa aliyonionyesha tangu siku ya kwanza ananiona, nikajikuta nikishusha pumzi ndefu na kujiinamia, mwili ukianza kupunguza kutetemeka.

“Twende huku,” alisema huku akinishika mkono, nilitaka kujichomoa lakini moyo ukasita, nikawa mpole kama kondoo anayepelekwa machinjioni, nikamfuata mpaka chini ya mwembe mkubwa uliokuwa jirani na pale tulipokuwa. Akaniambia nimpe mkono wangu wa kushoto, akaugeuza na kuutazama kwa muda kwenye upande wa nyuma wenye kucha.

>>>Usikose kutembelea Simulizi za Majonzi

“Unauona huu mshipa wa damu,” aliniambia huku akinionyeshea mshipa mkubwa wa damu uliokuwa unaonekana. Akaniambia kwamba nikifika nyumbani, kabla sijaingia ndani, natakiwa kuchukua kitu chenye ncha kali, iwe sindano au wembe na kujitoboa kwenye huo mshipa ili damu itoke.

“Damu ikiwa inatoka, hakikisha unaipakaza kwenye kingo mbili za mlango kisha ndiyo uingie ndani na usitoke mpaka giza liingie,” aliniambia huku akinipa pole kwa yote yaliyotokea, sikumjibu kitu kwani bado sikuwa najua nini itakuwa hatma yangu.

Baada ya hapo, aliniambia nifumbe macho, nikatii alichokisema, akaniambia nisifumbue mpaka atakaponiambia. Ghafla nikaanza kuhisi kama kimbunga kikali kinavuma pale chini ya mwembe tulipokuwa, sikuelewa tena kilichoendelea mpaka niliposikia sauti za watu ninaowafahamu wakilitaja jina langu, akiwemo Isri mwenyewe.

Ikawa ni kama nimetoka kwenye usingizi mzito ambao hata sielewi ulitokea wapi, nilipofumbua macho, nilishtuka mno kujikuta nipo nje ya nyumba ya akina Rahma huku mama na ndugu zangu wakiwa wamenizunguka lakin Isri hakuwepo. Yaani kuna mambo mengine yanatokea hata ukiulizwa yametokeaje, huwezi kuelezea.

“Vipi? Mbona umelala nje?” mama aliniuliza huku akiniinua. Sikutaka kuwa na maelezo marefu maana kila mtu angeniona mwendawazimu kama ningesimulia kila kitu kilichotokea. Kwa bahati nzuri, baba alitoka na kuja hadi pale nilipokuwa, nikiwa bado nimekaa chini kwenye maua.

Akanitazama usoni kwa makini kisha akawaambia ndugu zangu pamoja na mama wakaendelee na usafi kwa sababu ndiyo kwanza walikuwa wametoka kuamka na walikuwa wakifanya usafi wa mazingira na nyumba.

Waliondoka kwa shingo upande, mara kwa mara wakawa wanageuka na kunitazama, wakiwa na maswali mengi yasiyo na majibu. Walichokuwa wanakijua wao ni kwamba nilikuwa nimekamatwa na polisi na kwa jinsi taratibu za kisheria zilivyo, isingekuwa rahisi mimi kutoka bila kuja kuwekewa dhamana na hakukuwa na mtu mwingine wa kufanya hivyo zaidi ya baba na baba yake Rahma.

“Hebu simama,” alisema baba huku akinipa mkono, na mimi nikampa mkono wa kushoto. Wakati akinivuta kuniinua, nilimuona akiukazia macho mshipa wangu wa mkononi, uleule ambao Isri aliniambia nikifika nyumbani, kabla sijaingia ndani niutoboe kisha damu nizipake kwenye kingo za mlango.

“Umefanya nini? Hebu tuone?” alisema baba huku akizidi kuuvutia ule mkono wangu kwake, akautazama ule mshipa kwa sekunde kadhaa kisha nikamuona akiingiza mkono wake mmoja mfukoni, akatoa pochi yake na kuipekuakwa mkono mmoja, huku ule mwingine akiwa bado amenishikilia.

Nikamuona akitoa sindano ya kushonea nguo iliyokuwa na uzi mweusi, nikiwa bado najiuliza anataka kufanya nini, nilishtukia akinitoboa, nikaruka kwa maumivu, damu nyingi ikawa inaruka kwa kasi. Harakaharaka, akiwa bado amenishikilia, nilimuona baba akitoa kichupa kidogo mfukoni, cha ajabu eti akawa anakinga damu ambayo licha ya kutobolewa sehemu ndogo, ilikuwa ikiendelea kuruka kwa nguvu.

Sikuelewa kulikuwa na uhusiano gani kati ya ule mshipa wangu, damu iliyokuwa inanitoka na kile alichokisema Isri. Kile kichupa kidogo kilikaribia kujaa lakini cha ajabu, damu yenyewe ilikuwa nyeusi tii. Ilipopungua kutoka, baba aliniachia, akakifunga kile kikopo na bila kunisemesha kitu aliingia ndani haraka na kuniacha palepale nje.

Ndugu zangu waliokuwa wakiendelea kunitazama kwa macho ya kuibia, walibaki kunishangaa tu. Kwa kuwa baba hakuniambia chochote, na tayari Isri alikuwa amenipa maelezo fulani, nilijifuta ile damu iliyokuwa ikiendelea kunivuja, safari hii ikiwa imepungua, harakaharaka nikasogea mlangoni na kuipaka kwenye kingo za mlango, nikawa nageuka huku na kule kuhakikisha hakuna anayeona ninachokifanya.

Nilipofanya kitendo hicho tu, nilisikia kama masikio yamezibuka hivi, nikawa nasikia sauti za ajabuajabu kama miluzi hivi ambayo awali sikuwa naisikia, nikajikuta nikilazimika kuziba masikio kwa mikono, nikaingia ndani.

>>>Usikose kutembelea Simulizi za Majonzi

Cha ajabu, nilipoingia ndani tu, ile miluzi ilikoma kusikika, nikarudi kwenye hali yangu ya kawaida ingawa bado damu ilikuwa ikinitoka kidogo.

“Togoooo!” Rahma ambaye ndiyo kwanza alikuwa akitoka chumbani kwake baada ya kuamka, alisema huku akinikimbilia pale koridoni nilipokuwepo, akaja na kunikumbatia kwa nguvu huku akipiga kelele, akasema eti haamini kama ameniona.

“Mbona unatoka damu?”

“Nimeumia,” nilimjibu kwa mkato, akanipa pole sana na kunishika mkono, akawa ananipeleka kule chumbani kwake. Mwili wangu ulikuwa mchafu na nilikuwa nanuka lakini mwenyewe hakujali. Furaha aliyokuwa nayo, iliweza kabisa kuumaliza uchovu wa asubuhi aliokuwa nao, uso wake ukachangamka mno, akawa anatembea kwa madaha huku akijinyonganyonga.

Kabla ya kupatwa na yale matatizo siku iliyopita, hatukuwa tumeonana na Rahma kwa sababu asubuhi aliwahi sana kuamka na kuondoka na mama yake kufuatilia mambo ya chuo, hatukupata muda wa kuwa pamoja.

“Togoo!” nilisikia baba akiniita kwa sauti ya juu akiwa amesimama kwenye mlango wa chumba anacholala na mama.

“Naam baba,” niliitikia huku nikijaribu kumtoa Rahma maana alikuwa amenishika kimahaba, baba akaja mbiombio na kunishika mkono, akamwambia Rahma kuna kazi hatujamaliza kwa hiyo anisubiri, alinishika mkono na kuanza kunivuta kuelekea nje lakini tulipofika kwenye kingo za mlango tu, jambo la ajabu lilitokea.

Je, nini kitafuatia?
 
Sehemu ya 36



ILIPOISHIA:

“Naam baba,” niliitikia huku nikijaribu kumtoa Rahma maana alikuwa amenishika kimahaba, baba akaja mbiombio na kunishika mkono, akamwambia Rahma kuna kazi hatujamaliza kwa hiyo anisubiri, alinishika mkono na kuanza kunivuta kuelekea nje lakini tulipofika kwenye kingo za mlango tu, jambo la ajabu lilitokea.

SASA ENDELEA…

Kishindo kikubwa kilisikika, nikamuona baba akianza kuyumbayumba kama amelewa, na mimi nikaanza kusikia kizunguzungu kikali huku damu zikianza kututoka wote, mdomoni na puani. Muda huo tulikuwa tumeshavuka kizingiti cha mlango.

Sijui nilipata wapi ujasiri kwani ni muda huo ndipo nilipogundua kwamba kuna kosa nilikuwa nimelifanya, Isri aliniambia kwamba nisitoke nje mpaka giza litakapoingia, jambo ambalo nililikiuka kwa hiyo ili kurekebisha makosa, nilimvuta baba kwa nguvu, wote tukaangukia upande wa ndani wa mlango.

Kilisikika kishindo kingine kisha baba akawa ni kama amezinduka kutoka kwenye usingizi mzito.

“Nini kimetokea?” baba aliniuliza huku na yeye akiwa ni kama amepigwa na butwaa, akainua shingo na kutazama huku na kule, nikamuona akishtuka zaidi baada ya kuona damu zinamtoka mdomoni na puani pale chini.

“Hata mimi sijui,” nilimjibu huku nikisimama, na yeye akasimama kisha akawa anajifuta damu huku akitazama vizuri pale mlangoni. Aliangalia kwa sekunde kadhaa kisha akanigeukia na kunitolea macho ya ukali.

>>>Usikose kutembelea Simulizi za Majonzi

“Umeweka nini hapa?” aliniuliza kwa ukali.

“Hakuna kitu.”

“Una uhakika?” aliniuliza huku akinisogelea mwilini. Miongoni mwa sifa za baba, huwa hapendi kabisa mtu muongo, ni bora akikuuliza unyamaze kuliko kutoa majibu ya uongo. Ili kuepusha shari, nilinyamaza na kujiinamia.

“Si naongea na wewe?”

“Wakati naingia nilipakaza damu hapo kwenye mlango,” nilisema, akaonesha kushtuka mno, hakusema kitu zaidi ya kunishika mkono, akawa ananivutia ndani huku akiendelea kujifuta damu.

Tulienda mpaka kwenye kile chumba changu, tukaingia huku baba akiwa makini kuhakikisha hakuna mtu yeyote anayetutazama. Wakati naingia, nilitupia macho kwenye mlango wa chumba cha Rahma, nikamuona akiwa anatuchungulia. Nilimuonesha ishara kwamba anisubiri, akatingisha kichwa kuniitikia.

“Mimi ni nani kwako?”

“Ni baba yangu.”

“Haya nataka unieleze kila kitu, umetokaje mahabusu na nini kimetokea mpaka ukapaka damu kwenye mlango,” alisema baba kwa sauti ya chini, lakini akionesha kutokuwa na hasira na mimi.

Kabla sijamjibu, niliingiza mkono mfukoni na kutoa ile dawa ya ajabu ambayo kwa kiasi kikubwa ilinisaidia sana.

“Hiyo ni mimi nilikuwekea muda ule wakati polisi wanakuchukua, naamini imekusaidia sana,” alisema baba huku akiichukua ile dawa mikononi mwangu na kuiweka kwenye mfuko wa shati. Ni hapo ndipo nilipoanza kupata picha juu ya nini kilichotokea.

>>>Usikose kutembelea Simulizi za Majonzi

“Sasa baba, unataka nikueleze nini wakati kumbe unajua kila kitu na wewe ndiye uliyenielekeza jinsi ya kutoka mahabusu?”

“Unachokisema ni sawa lakini najua kuna mambo mengi yametokea ukiachilia mbali wewe kutoka mahabusu na ndiyo maana nimekutoboa mkono wako na kukinga damu yako, mimi ni baba yako na hakuna mtu mwenye uchungu na wewe kuliko sisi wazazi wako, ni lazima ujifunze kuniamini na kuwa muwazi kwangu,” alisema.

Kiukweli sikuwahi kumsikia baba akizungumza kwa busara na mimi kiasi hicho, yaani ni kama alikuwa akizungumza na mkubwa mwenzake na hata ule ukali wake wa siku zote, hakuuonesha kabisa.

Nilishusha pumzi na kukaa vizuri, sikuona sababu ya kuendelea kumficha, nilianza kumueleza kila kitu kilichotokea, kuanzia nilipofikishwa kituoni, wale wachawi waliokuja usiku kule mahabusu na jinsi yule mwingine alivyobadilika sura na kufanana na mimi.

Nilipofikia kipengele hicho, baba alinikatisha, akaniambia kwamba dawa aliyokuwa amenipa, ina nguvu kubwa ya kufanya chochote ninachokitaka. Akaniambia kwamba yule mchawi aliyebadilika sura, alishindwa kutoka mpaka asubuhi na askari walipoingia kwa ajili ya kufanya ukaguzi.

“Nasikia wameshtuka sana kumuona, wakadhani ni wewe lakini tofauti ikawa ni kwamba sura mmefanana lakini yeye ni mzee na amekutwa hana nguo hata moja, mtaani kote ndiyo gumzo na hata vyombo vya habari vimeanza kuripoti tukio hilo la ajabu,” alisema baba.

Kauli yake ilinifanya niwe na shauku kubwa ya kutaka kujua nini kimeendelea, akaniambia nisiwe na wasiwasi atanieleza lakini pia akaniambia kwamba anataka kumtumia yule mchawi kama funzo kwa watu wengine wenye tabia ya kufanya uchawi wa kijinga.

Aliposema uchawi wa kijinga, sikumuelewa anamaanisha nini, nikataka kumuuliza tena lakini aliniambia niendelee kumueleza kilichotokea. Nilimueleza kila kitu na jinsi nilivyokutana na yule msichana usiku ule.

“Lakini si nilishakukataza kuwa karibu na Isri?” alisema huku akinitazama usoni, nilishtuka kumsikia baba akimtaja jina. Kwa ilivyoonesha, kumbe baba alikuwa akimfahamu vizuri msichana huyo na hata aliponikataza kuwa naye karibu, alikuwa na maana yake.

“Huyo si ndiye aliyekusababishia matatizo mpaka ukakamatwa kwa tuhuma za mauaji? Ina maana wewe hukushtuka mtu amekufia mchana gesti halafu usiku unakutana naye tena? Akili zako zinafanya kazi sawasawa kweli?” baba alinibadilikia, nikawa nataka kujitetea lakini alinikatisha na kuniambia anaelewa kila kitu kilichotokea kati yetu.

“Hebu hiyo mikono yako,” alisema, nikasita kidogo lakini baadaye nilimpa, akaishika na kuanza kuitazama upande wa mbele kisha akanitazama usoni.

“Na wewe umeshakuwa kama yeye,” alisema huku akiniachia, akaniambia nifumbue mdomo wangu. Nilifanya hivyo, akawa anayatazama meno yangu kwa makini. Bado nilikuwa na maswali mengi kuliko majibu na ilionesha kwamba baba anamfahamu vizuri sana Isri.

Kitendo cha kutazama mikono yangu kisha wakati huohuo akaanza kukagua meno yangu, kilitosha kunifanya nielewe kwamba kumbe anajua jinsi msichana huyo alivyonigeuza na kuwa kiumbe wa ajabu.

“Umewapa ushindi maadui zangu kwa sababu ya mambo yako ya kipumbavu,” alisema baba huku akiinuka, bado damu zilikuwa zikimtoka puani ingawa safari hii haikuwa kwa wingi kama ilivyokuwa mwanzo.

Alipotaka kutoka, nilimuita, akageuka na kunitazama, nikamwambia Isri ameniambia nisitoke nje mpaka giza litakapoingia, akanijibu kwa kifupi kwamba anajua kisha akaondoka zake.

Harakaharaka niliinuka na kukimbilia bafuni kwani nilikuwa najisikia aibu kukutana na Rahma nikiwa na harufu mbaya kiasi kile, nikajifungia na kufungulia maji kwa wingi, nilivua nguo zangu kisha nikaanza kujimwagia maji huku nikijikagua kama hakukuwa na kitu chochote kisicho cha kawaida mwilini mwangu.

Mara nilisikia mlango wa bafu ukigongwa, nikahisi ni Rahma amenifuata, harakaharaka nikaufungua, nikakutana uso kwa uso na baba.

>>>Usikose kutembelea Simulizi za Majonzi

“Ogea hii,” alisema huku akinipa ile dawa ambayo aliwahi kunipa niogee, ambayo ukiogea mwili unatoa uchafu mweusi kama mkaa. Nilimshukuru na kufunga mlango, nikaendelea kuoga. Maji machafu, meusi tii yalianza kunitoka, safari hii nikawa sina wasiwasi maana nilikuwa naelewa kinachotokea.

Nilioga mpaka uchafu wote ukaniisha mwilini, nikachukua nguo zangu na kuzikung’uta sana kisha nikavaa na kutoka. Rahma alikuwa amesimama kwenye mlango wa chumba chake, akionesha kunisubiri kwa shauku kubwa.

Hakuwa amevaa chochote zaidi ya kujifunga upande wa khanga nyepesi, akawa ananitazama usoni kwa macho yake mazuri, ambayo yalikuwa ni kama yana usingizi kwa jinsi yalivyolegea.

Nilitazama huku na kule, nilipoona hakuna mtu anayetutazama, nilimsogelea, akanikumbatia kwa mahaba kisha akanivutia ndani. Hatukukumbuka hata kufunga mlango, kwa makusudi aliuachia ule upande wa khanga, ukadondoka chini, nikawa kama fisi aliyeona mfupa.

Je, nini kitafuatia?
 
Sehemu ya 37




ILIPOISHIA:

Nilitazama huku na kule, nilipoona hakuna mtu anayetutazama, nilimsogelea, akanikumbatia kwa mahaba kisha akanivutia ndani. Hatukukumbuka hata kufunga mlango, kwa makusudi aliuachia ule upande wa khanga, ukadondoka chini, nikawa kama fisi aliyeona mfupa.

SASA ENDELEA…

Harakaharaka nilichojoa magwanda yangu huku nikiwa na pupa isiyo na mfano, muda mfupi baadaye tulikuwa saresare maua, nikamnyanyua Rahma juujuu na kumbwaga kwenye uwanja wa fundi seremala. Mwenyewe alionesha kufurahia sana, akanibana kwenye kifua chake kilichojaa vizuri, tukagusanisha ndimi zetu.

Hata hivyo, tofauti na mara zote ninapokuwa kwenye mazingira kama hayo, ambapo ‘Togo’ wangu huwa mkali kama nyoka koboko, nilishangaa akiwa kimya kabisa, kama hajui ni nini kilichokuwa kinataka kutokea.

Kama nilivyoeleza tangu mwanzo, sikuwa najua chochote kwenye ulimwengu wa kikubwa na Rahma ndiye aliyekuwa wa kwanza kuniingiza kwenye ulimwengu huo, akifuatiwa na Isri, tena ndani ya siku chache tu. Kwa hiyo, sikuwa mzoefu na hicho kilichotokea, kilikuwa kitu kigeni kabisa kwangu.

Nimewahi kusikia kwamba, kwa mwanaume, hakuna aibu kubwa kama kuwa na mwanamke faragha halafu ukashindwa kazi, nikajikuta nikiwa na wasiwasi mkubwa kweli ndani ya moyo wangu. Sikujua Rahma atanichukuliaje, sikujua atanidharau kwa kiasi gani, nikajikuta kijasho chembamba kikinitoka huku akili ikiwa imehama kabisa.

“Togo, vipi?” aliniuliza Rahma baada ya kubaini mabadiliko niliyokuwa nayo. Swali lake lilinifanya nizidi kujisikia aibu, nilikosa cha kujibu na kiukweli sikuwa na majibu. Alipeleka mkono bondeni yaliko makazi ya ‘Togo’ na kujaribu kumpa hamasa kwa kutumia mikono yake laini lakini ilikuwa sawa na kazi bure.

“Mshukuru sana Mungu wako, ulikuwa unaenda kumuua mtoto wa watu, mshenzi sana wewe,” nilisikia sauti ya baba ikiniongelea sikioni kwa ukali, ikafuatiwa na msonyo mrefu, nikakurupuka kwa hofu kubwa, nikawa namtazama Rahma nikiwa nimekodoa macho, kijasho chembamba kikinitoka.

Nilikumbuka tukio lililonitokea na Isri, nilipokutana naye kwa mara ya kwanza faragha, ambapo tukiwa mchezoni, ghafla ‘alikata roho’ ingawa baadaye nilikutana naye tena akiwa mzima na ndiyo yakatokea yale yaliyotokea usiku uliopita. Alichokisema baba kilinifanya nihisi kwamba huenda kuna kitu kibaya mwilini mwangu ambacho ndiyo chanzo cha yote na nikifanya masihara, kweli Rahma atakufa na kusababisha msiba mzito kwa familia yake.

Nilikumbuka pia kauli ya Isri kwamba mimi ndiye mwanaume pekee niliyeweza kuushinda mtihani wa kifo baada ya kukutana naye kimwili.

“Togo, una nini mpenzi wangu,” alisema Rahma huku akisimama, naye akionesha kushangazwa na kilichotokea. Alinisogelea na kutaka kunikumbatia lakini nilijitoa harakaharaka, nikavaa nguo zangu huku nikiendelea kuhema kwa nguvu, nikamuona Rahma akikaa pembeni ya kitanda na kujiinamia, machozi yakaanza kumtoka.

Niliondoka haraka na kuelekea bafuni, nikajifungia mlango kwa ndani na kujiinamia, nikiwa hata sielewi nini cha kufanya. Ilibidi nijimwagie tena maji, mwili wangu ukapata nguvu, nikatoka na kwenda chumbani kwangu, nikawa nimejilaza huku nikiendelea kutafakari kilichotokea.

Kwa mbali ile kiu kali ya kukutana kimwili na mwanamke ilinianza upya, nikawa najiuliza, inawezekanaje muda mfupi tu uliopita nimeshindwa kabisa kufanya chochote na Rahma na kumuacha akiwa na huzuni kubwa kwenye moyo wake, halafu dakika chache baadaye niwe na hamu kali isiyoelezeka.

Nilipokumbuka ile kauli ya baba, niliona kabisa kinachoenda kutokea ni janga kubwa kwa Rahma kwa sababu muda si mrefu, mimi ningeenda chumbani kwake au yeye angekuja kwangu, tungeanza kubembelezana na mwisho tungeishia kuangukia dhambini, na matokeo yake dhambi ingekomaa na kuzaa mauti kwa Rahma, jambo ambalo lingenifanya niishi na hatia ya kukatisha maisha ya mtu asiye na hatia milele.

Nilichokifanya, harakaharaka niliamka pale kitandani, nikavaa viatu vyangu na kutaka kutoka lakini nilikumbuka kwamba giza halikuwa limeingia kwa hiyo kutoka nje kungemaanisha kwamba ningepata madhara makubwa kama Isri alivyonipa masharti.

Niliamua kwenda kukaa sebuleni, ndugu zangu pamoja na wadogo zake Rahma wakawa wananishangaa. Kwa muda mfupi tu tuliokaa hapo nyumbani, tayari nilishaonesha tabia za ajabu sana. Kila mtu akawa ananitazama kwa macho ya chinichini, haikuwa kawaida yangu kukaa sebuleni.

Nilijikaza kiume, nikakazia macho kwenye runinga, nikawa sina habari na mtu, ukimya ukatanda pale sebuleni. Baba na baba yake Rahma walikuwa wamekaa kwenye sehemu ya kulia chakula, wakiwa wanacheza bao huku mama na mama yake Rahma wenyewe wakiwa jikoni.

Muda mfupi baadaye, Rahma alikuja na kuchungulia pale sebuleni, alipochungulia tu, macho yangu na yake yakagongana, akanionesha ishara ya kuniita kwa mkono kisha nikamsikia akitembea kuelekea chumbani kwake.

“Mungu wangu, sasa itakuwaje?” niliwaza, nikaamua kujikausha kama sijamuona Rahma, nikawa naendelea kukazia macho kwenye runinga imngawa kiukweli wala akili zangu hazikuwa pale na sikuwa najua hata kunaoneshwa nini.

Muda mfupi baadaye, Rahma alikuja tena lakini safari hii, alikuja na kukaa kwenye kochi nililokuwa nimekaa mimi, uso akiwa ameukunja. Nilijua kwamba amekasirika lakini sikuwa na namna zaidi ya kujiepusha naye, nilikuwa nampenda Rahma na sikuwa tayari kuona anapatwa na jambo lolote baya.

Alikuwa amejifunga khanga nyepesi na ndani hakuwa na kitu kabisa, nikazidi kujikuta kwenye wakati mgumu, tukawa tunatazama runinga bila mtu yeyote kumsemesha mwenzake. Hata wale ndugu zetu nadhani nao waligundua kwamba hatupo sawa kwa sababu si kawaida ya mimi na Rahma kukaa sehemu moja bila kusemeshana, tena mara nyingi tulikuwa tukicheka na kufurahi.

Dakika kadhaa baadaye, Rahma alibadili mkao aliokuwa amekaa, akanisogelea halafu akawa ni kama ameniegamia kimtindo, haikuwa rahisi kwa watu wengine kuelewa kilichokuwa kinaendelea lakini kiukweli nilijikuta nikipata msisimko mkubwa sana.

Mwisho niliamua kukata shauri maana na mimi nilikuwa nateseka, nikaamua liwalo na liwe, nikamgeukia Rahma na kumtazama usoni, naye akanigeukia, tukawa tunatazamana machoni, nikampa ishara kwamba atangulie ndani, akaniitikia huku akinitazama kwa macho yenye hisia kali za mapenzi.

Aliinuka na kutembea kwa madoido, nikawa namsindikiza kwa macho, nikawaona watu wote pale sebuleni wakitazamana. Nilishusha pumzi ndefu na kukaa vizuri kwenye kiti, nikawa navutia kasi ili na mimi niinuke na kumfuata Rahma kule ndani, tukatii kiu zetu.

“Togoo,” nilisikia sauti ya baba akiniita, nikaitika na kusimama, ilibidi nijiweke vizuri maana ilikuwa aibu kwa wote waliokuwa pale sebuleni, nikaelekea kule walikokuwa wamekaa baba na baba yake Rahma.

“Wewe sasa hivi una mambo ya kikubwa, hutakiwi kuwa unachanganyikana na wenzako, inabidi uanze kukaa na sisi baba zako, vuta kiti kaa hapa,” alisema baba, akawa ametibua shoo nzima, nilitaka kutoa visingizio lakini hakutaka kusikia chochote kutoka kwangu, ikabidi nikae na kujiinamia, wote wakawa wananitazama.

Je, nini kitafuatia?
 
Sehemu ya 37




ILIPOISHIA:

Nilitazama huku na kule, nilipoona hakuna mtu anayetutazama, nilimsogelea, akanikumbatia kwa mahaba kisha akanivutia ndani. Hatukukumbuka hata kufunga mlango, kwa makusudi aliuachia ule upande wa khanga, ukadondoka chini, nikawa kama fisi aliyeona mfupa.

SASA ENDELEA…

Harakaharaka nilichojoa magwanda yangu huku nikiwa na pupa isiyo na mfano, muda mfupi baadaye tulikuwa saresare maua, nikamnyanyua Rahma juujuu na kumbwaga kwenye uwanja wa fundi seremala. Mwenyewe alionesha kufurahia sana, akanibana kwenye kifua chake kilichojaa vizuri, tukagusanisha ndimi zetu.

Hata hivyo, tofauti na mara zote ninapokuwa kwenye mazingira kama hayo, ambapo ‘Togo’ wangu huwa mkali kama nyoka koboko, nilishangaa akiwa kimya kabisa, kama hajui ni nini kilichokuwa kinataka kutokea.

Kama nilivyoeleza tangu mwanzo, sikuwa najua chochote kwenye ulimwengu wa kikubwa na Rahma ndiye aliyekuwa wa kwanza kuniingiza kwenye ulimwengu huo, akifuatiwa na Isri, tena ndani ya siku chache tu. Kwa hiyo, sikuwa mzoefu na hicho kilichotokea, kilikuwa kitu kigeni kabisa kwangu.

Nimewahi kusikia kwamba, kwa mwanaume, hakuna aibu kubwa kama kuwa na mwanamke faragha halafu ukashindwa kazi, nikajikuta nikiwa na wasiwasi mkubwa kweli ndani ya moyo wangu. Sikujua Rahma atanichukuliaje, sikujua atanidharau kwa kiasi gani, nikajikuta kijasho chembamba kikinitoka huku akili ikiwa imehama kabisa.

“Togo, vipi?” aliniuliza Rahma baada ya kubaini mabadiliko niliyokuwa nayo. Swali lake lilinifanya nizidi kujisikia aibu, nilikosa cha kujibu na kiukweli sikuwa na majibu. Alipeleka mkono bondeni yaliko makazi ya ‘Togo’ na kujaribu kumpa hamasa kwa kutumia mikono yake laini lakini ilikuwa sawa na kazi bure.

“Mshukuru sana Mungu wako, ulikuwa unaenda kumuua mtoto wa watu, mshenzi sana wewe,” nilisikia sauti ya baba ikiniongelea sikioni kwa ukali, ikafuatiwa na msonyo mrefu, nikakurupuka kwa hofu kubwa, nikawa namtazama Rahma nikiwa nimekodoa macho, kijasho chembamba kikinitoka.

Nilikumbuka tukio lililonitokea na Isri, nilipokutana naye kwa mara ya kwanza faragha, ambapo tukiwa mchezoni, ghafla ‘alikata roho’ ingawa baadaye nilikutana naye tena akiwa mzima na ndiyo yakatokea yale yaliyotokea usiku uliopita. Alichokisema baba kilinifanya nihisi kwamba huenda kuna kitu kibaya mwilini mwangu ambacho ndiyo chanzo cha yote na nikifanya masihara, kweli Rahma atakufa na kusababisha msiba mzito kwa familia yake.

Nilikumbuka pia kauli ya Isri kwamba mimi ndiye mwanaume pekee niliyeweza kuushinda mtihani wa kifo baada ya kukutana naye kimwili.

“Togo, una nini mpenzi wangu,” alisema Rahma huku akisimama, naye akionesha kushangazwa na kilichotokea. Alinisogelea na kutaka kunikumbatia lakini nilijitoa harakaharaka, nikavaa nguo zangu huku nikiendelea kuhema kwa nguvu, nikamuona Rahma akikaa pembeni ya kitanda na kujiinamia, machozi yakaanza kumtoka.

Niliondoka haraka na kuelekea bafuni, nikajifungia mlango kwa ndani na kujiinamia, nikiwa hata sielewi nini cha kufanya. Ilibidi nijimwagie tena maji, mwili wangu ukapata nguvu, nikatoka na kwenda chumbani kwangu, nikawa nimejilaza huku nikiendelea kutafakari kilichotokea.

Kwa mbali ile kiu kali ya kukutana kimwili na mwanamke ilinianza upya, nikawa najiuliza, inawezekanaje muda mfupi tu uliopita nimeshindwa kabisa kufanya chochote na Rahma na kumuacha akiwa na huzuni kubwa kwenye moyo wake, halafu dakika chache baadaye niwe na hamu kali isiyoelezeka.

Nilipokumbuka ile kauli ya baba, niliona kabisa kinachoenda kutokea ni janga kubwa kwa Rahma kwa sababu muda si mrefu, mimi ningeenda chumbani kwake au yeye angekuja kwangu, tungeanza kubembelezana na mwisho tungeishia kuangukia dhambini, na matokeo yake dhambi ingekomaa na kuzaa mauti kwa Rahma, jambo ambalo lingenifanya niishi na hatia ya kukatisha maisha ya mtu asiye na hatia milele.

Nilichokifanya, harakaharaka niliamka pale kitandani, nikavaa viatu vyangu na kutaka kutoka lakini nilikumbuka kwamba giza halikuwa limeingia kwa hiyo kutoka nje kungemaanisha kwamba ningepata madhara makubwa kama Isri alivyonipa masharti.

Niliamua kwenda kukaa sebuleni, ndugu zangu pamoja na wadogo zake Rahma wakawa wananishangaa. Kwa muda mfupi tu tuliokaa hapo nyumbani, tayari nilishaonesha tabia za ajabu sana. Kila mtu akawa ananitazama kwa macho ya chinichini, haikuwa kawaida yangu kukaa sebuleni.

Nilijikaza kiume, nikakazia macho kwenye runinga, nikawa sina habari na mtu, ukimya ukatanda pale sebuleni. Baba na baba yake Rahma walikuwa wamekaa kwenye sehemu ya kulia chakula, wakiwa wanacheza bao huku mama na mama yake Rahma wenyewe wakiwa jikoni.

Muda mfupi baadaye, Rahma alikuja na kuchungulia pale sebuleni, alipochungulia tu, macho yangu na yake yakagongana, akanionesha ishara ya kuniita kwa mkono kisha nikamsikia akitembea kuelekea chumbani kwake.

“Mungu wangu, sasa itakuwaje?” niliwaza, nikaamua kujikausha kama sijamuona Rahma, nikawa naendelea kukazia macho kwenye runinga imngawa kiukweli wala akili zangu hazikuwa pale na sikuwa najua hata kunaoneshwa nini.

Muda mfupi baadaye, Rahma alikuja tena lakini safari hii, alikuja na kukaa kwenye kochi nililokuwa nimekaa mimi, uso akiwa ameukunja. Nilijua kwamba amekasirika lakini sikuwa na namna zaidi ya kujiepusha naye, nilikuwa nampenda Rahma na sikuwa tayari kuona anapatwa na jambo lolote baya.

Alikuwa amejifunga khanga nyepesi na ndani hakuwa na kitu kabisa, nikazidi kujikuta kwenye wakati mgumu, tukawa tunatazama runinga bila mtu yeyote kumsemesha mwenzake. Hata wale ndugu zetu nadhani nao waligundua kwamba hatupo sawa kwa sababu si kawaida ya mimi na Rahma kukaa sehemu moja bila kusemeshana, tena mara nyingi tulikuwa tukicheka na kufurahi.

Dakika kadhaa baadaye, Rahma alibadili mkao aliokuwa amekaa, akanisogelea halafu akawa ni kama ameniegamia kimtindo, haikuwa rahisi kwa watu wengine kuelewa kilichokuwa kinaendelea lakini kiukweli nilijikuta nikipata msisimko mkubwa sana.

Mwisho niliamua kukata shauri maana na mimi nilikuwa nateseka, nikaamua liwalo na liwe, nikamgeukia Rahma na kumtazama usoni, naye akanigeukia, tukawa tunatazamana machoni, nikampa ishara kwamba atangulie ndani, akaniitikia huku akinitazama kwa macho yenye hisia kali za mapenzi.

Aliinuka na kutembea kwa madoido, nikawa namsindikiza kwa macho, nikawaona watu wote pale sebuleni wakitazamana. Nilishusha pumzi ndefu na kukaa vizuri kwenye kiti, nikawa navutia kasi ili na mimi niinuke na kumfuata Rahma kule ndani, tukatii kiu zetu.

“Togoo,” nilisikia sauti ya baba akiniita, nikaitika na kusimama, ilibidi nijiweke vizuri maana ilikuwa aibu kwa wote waliokuwa pale sebuleni, nikaelekea kule walikokuwa wamekaa baba na baba yake Rahma.

“Wewe sasa hivi una mambo ya kikubwa, hutakiwi kuwa unachanganyikana na wenzako, inabidi uanze kukaa na sisi baba zako, vuta kiti kaa hapa,” alisema baba, akawa ametibua shoo nzima, nilitaka kutoa visingizio lakini hakutaka kusikia chochote kutoka kwangu, ikabidi nikae na kujiinamia, wote wakawa wananitazama.

Je, nini kitafuatia?
Mzee alishausoma mchezo[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Back
Top Bottom