Simulizi ya Kijasusi: C.O.D.EX.

Simulizi ya Kijasusi: C.O.D.EX.

71.

"hahahahaha ukitaka kuwaongoza watu vizuri wagawe makundi" aliongea mtu mmoja ambae alikuwa amevaa gwanda za jeshi na kucheka kwa nguvu huku akiwa anaangalia video zilizowaonyesha wale wenzake na marehemu Marko wakigombana.
"Unahis vipi baada kumuondoa Marko katika uso wa dunia" swali la kwanza alilokutana nalo kutoka kwa Christine baada kufika tu hoteli. "ah kawaida tu, mbona kuuwa kwangu ni jambo dogo sana" alijibu Alex na kuelekea chumbani kwake, alijitupa kitandani huku akiwaza na kuwazua inakuaje Allen James anakuwa hatari kiasi kile. Maana zile mbinu nazotumia si mchezo, kuweza kulenga mita zaidi ya 70 bila kutumia darubini. Mwisho aliona atapasuka kichwa tu ikiwa ataendelea kuwaza, aliamua kuinuka na uingia chooni kwa ajili ya kujifanyia usafi. Alimaliza na kurudi chumbani, alivaa nguo za kawaida na kutoka.
Chakula kilikuwa kimeshaletwa walikaa pamoja na kuanza kula huku wakiongea mambo mengi. "kesho tutaelekea Uingereza na tutaondoka hapa asubuhi" Aliongea christine, "sawa hakuna shida" Alex alijibu kwa sababu alishajua mapema kuwa wangeondoka Urusi. Baada ya kula kila mtu alikwenda chumbani kwake na kuupitisha usiku ambao kwa Alex ulikuwa ni mzuri sana hasa ukizingatia kuwa kuna mtu ambae anamthamini kama mtu na sio mashine tu ya kufanyia mauaji.
Siku ya pili mapema waliondoka na kuelekea uingereza, katila ndege walipata viti vya mbali mbali. Alex alikaa na mtu mmoaja ambae alikuwa akisoma gazeti hivo hakufanikiwa kumuona sura. "naona tunakwenda Uingereza" Aliongea yule mzee na kumafanya Alex kushtuka kwa maana sauti hiyo aliifahamu kama ilikuwa ya Allen. "Allen unafanya nini humu" Alex aliuliza kwa sauti ya chini, "si nasafri kama abiria wengine" Allen alijibu huku akiondoa gazeti. Alex karibu acheke kwa nguvu maana kwa jinsi alivyokuwa Allen ni shida, alikuwa amebandika ndevu nyngi pamoja na sharubu kitu ambacho kama hujawaho kukutana nae lazima usingemjua.
"sasa sikia tupange mikakati, kwanza walioiteketeza familia yako ndio waanze kuangamia halafu ao wengine watafuata" aliongea Allen, "ah sasa si nimeshaanza kuwaondoa" Alex alijibu kwa kujiamini. "acha ujinga wewe yule uliemuua jana hahusiki na vifo vya familia yako" Allen aliongea na ghafla sura ya Alex ilibadilika na kuwa kama ameanza kukasirika. "mi nimekwambia unatumiwa kufanikisha kazi za watu" Allen aliendelea kusukuma msumari wa moto katika kifua cha Alex. "mbona sielewe elewi" Alex aliongea huku akionekana kuwa amechanganyikiwa, "ndio lazima usielewe kwa sababu unachezewa mchezo mchafu" Allen alijibu.
 
72.
"Sasa nisikilize kwa makini, huko tunapokwenda yupo mtu mmoja ambae alihusika moja kwa moja katika utekelezaji wa mauaji ya familia yako. Huyo mtu ni mjapan mwenye uraia wa uingereza na anaitwa Masaya Okinamoto. Ni mtu hatari na ili umfikie karibu lazima upitie mashindano maalum ya ngumi za haram, mchezo huo unaendeshwa na matajiri wengi sana pasi na serekali kushtukia. Na kwa sababu Masaya hajawahi kushindwa, hivyo fainali lazima utapambana nae na hapo ndio muda ambao nitaingilia kati na kumteka. Lakini hakikisha unamchakaza vya kutosha lakini usimuue" Allen alimaliza kuongea na kumuangalia Alex aliekuwa ametoa macho kama mjusi aliebanwa na mlango.
"Hivi kwanini umeamua kunisaidia" Alex aliuliza swali ambalo lilimshtua kidogo Allen, "kijana mimi ni mtu mzima sana, na katika maisha yangu sikuwahi kufanya jambo zuri kama hili. Nimekuwa katika mazingira mazuri sana na sikutegemea hata siku moja kama saahivi ningekuwa katika hali hiii. Nimeona nikusaidia kwa sababu kiupande fulani najiona mwenyewe nikikuangalia kwa jinsi maisha yalivyokufanyia na watu waliokutenda ubaya. Wao saa hivi wanaishi vizuri na familia zao hali ya kuwa wewe maisha yako yamejaa misukosuko kama nilioipata mimi" Allen aliongea huku akionekana kama kutonesha kidonda ambacho kilikuwa kimepona juu lakini ndani bado kilikuwa kibichi. Na hapo ndipo akaanza kumuelezea historia yake na mambo yote yaliomkuta kipindi hicho akiwatumika watu wasio na shukrani hata kiodogo. "kwakweli sikujua kama ulipitia mambo yote hayo na nisamehe kwa kuktonesha kidonda ambacho kilikuwa kimeshaanza kupona" Alex aliongea baada kugundua kuwa macho ya Allen James yalikuwa yashaanza kuja maji na hapo ndio akaona kwa nini mzee huyo amekubali kumsaidia wakati akijua kabisa mwisho wke hautokuwa mzuri. "kijana katika haya maisha kuna mambo mawili ya kuchagua aidha uishi kama mtu huru au usishi kama mtumwa lakini huwezi kuishi katikati ya mambo hayo mawili. Namaanisha ukubali kuendelea kutumika au uutafute uhuru wako na uendeshe maisha yako kama watu wengine na hakuna kitu kizuri kama kusihi ukiwa na amani" Allen alimsihi Alex achague njia ambayo itampa faida katika masiha yake yote..


Alex alikuwa kimya kwa muda akitafakari maneno ya mzee huyo ambe kwa nje alinekana mzee lakini ndani alikua ni kijana kabisa. "nimekuelewa, na usijali nitachagua njia nzuri tu ambayo hata wewe utaipenda" Alex aliongea huku akitabasamu, "na kitu kimoja pia ukae ukikijua kuwa kisasi si kizuri kabisa hata ukiwauwa watu wote waliokutendea ubaya lakini familia yako haitorudi tena duniani, pia kisasi ni kizuri ikiwa utafanikisha malengo yako kwa sababu utakuwa umeutuwa mzigo mzito uliokuwa umeubeba moyoni mwako" Allen alizidi kumpanga Alex kisaikolojia bila Alex kutambuwa hilo, "sawa nimekuelewa lakini kwangu mimi kisasi ni kizuri sana hapa ni mwendo kutengua viungo mpaka kieleweke" Alex aliongea na kumwangalia Allen ambae alionekana kutabasamu. Waliendelea kuongea mambo mengi tu huku wakipanga mikakati ya kuwakomesha wale wote wanaowachukua vijana na kuwafanya panya wa lab kwa kuwafanyia manyaribio mbali mbali. Hatimae ndege ilikanyaga ardhi ya uingereza mjini London, kila mmoja alishuka na kuelekea njia yake kama hawajuani kabisa. Na mbaya zaidi hata Christine hakushtuka kama ndan ya ndege hio hio moja kachezwa akili, akiongozna na Alex walitoka mpaka nje ya uwanja na kuchukua taxi kisha safari ikaanza
 
73.
. "tunakwenda wapi" Alex aliuliza, "we utapaona tu"Christine alijibu basi na Alex alijifanya mjinga bila kuuliza swali jingine lolote lile. Walitembea kwa muda wa nusu saa mpaka nje mji kidogo, Taxi ilisimama nje ya jengo kubwa sana na wakashuka. Christine aliomgoza njia huku Alex akimfata kwa nyuma, walifika mlangoni na Christine akatoa funguo na kufungua. Waliingia ndani na hapo ndipo Alex alishangaa maana jumba hilo lilikuwa nasafi ndani na haliakuwa lilikuwa halina mtu. Sasa aliamini mia kwa mia maneno ya Allen kama kuna kamchezo cha harufu mbaya kanachezwa. Hata hivyo hakuuliza chochote, Christine alimwangalia Alex kwa makini usoni na kugundua kitu kisicho kawaida lakini aliamua kufunga mdomo wake na kukaa kimya. "mmh kashaanza kushtuka nini" Alijiuliza moyoni, "na kama ni hivo basi utakuwa msala mkubwa sana" aliendelea kujisemea moyoni. Wakati huo hakushtka kama alikuwa akiitwa mpaka alipoguswa bega ndipo akshtuka kutoka katika mawazo yake.
"unavoonekana ulikwa mbali sana" Alex aliongea huku akimuangalia kwa makini usoni, "unajua nilikuwa sitaki kurudi kwenye nyumba hii" Christine aliongea huku akilisogelea kochi na kukaa. "kwanini sasa" Alex aliuliza huku akitafuta kochi la kukaa, "hapa ndio nyumbani kwetu nilipozaliwa na nilipokulia kabla ya wazazi wangu kuuwawa kikatili mbele ya macho yangu. na mimi nikafanyiwa unyama mkubwa sana, kwa umri niliokuwa nao lilikuwa pigo ambalo sikuwahi kufikiria kama lingewahi kutokea" Christine alishindwa kuendelea kuongea na kuanza kulia huku akikumbuke usiku wa matukio yote hayo yaliomkuta akiwa binti mdogo sana. Alex aljitahidi kumnyamazisha lakini wapi ilikuwa ni kutwanga maji kwenye kinu, kumbukumbu za Christine kubakwa na wanaume sita walioshiba zilizidi kumrudia kichwani mwake na kujikuta akiabana miguu yake kwa nguvu na kukunja ngumi. Alex alipoona hivyo alielewa nini kilimtokea binti huyo. Baada robo saa alinyamaza kimya na kumuangalia Alex ambae alikuwa ametulia akisubiria kitu anachoaka kukiongea . "kama sio yule mzee aliekuja kuniokoa leo hii ningekua marehemu" Christine aliongea, "Mzee gani huyo" Alex aljikuta akiuliza. "Alinambia anaitwa Jason CJ" Christine alilisema jina na ghafla Alex alijikuta kinyong'onyea. "nini sasa" aliuliza Christine, "wewe ndio Ms Rose" Alex aliuliza kwa mshangao. Christine alishtuka baada kusikia jina hilo kwani ni watu wachache tu waliokuwa wakilifahamu jina baada ya familia yake.
Kabla Alex hajajibu, Christne aliruka nyuma na kutoa bastola yake kiunoni "nambie umelijuaje hilo jina" alifoka huku akiikoki bastola yake. "duh" Alex alishangaa kwanza kwa maana hakutegemea kabisa kama mwanamke huyo angekuwa mwepesi kiasi hicho. "Jason CJ ni babaangu mzazi" ilibidi ajibu kwa maana alishaona hali ya hewa humo ndani ilikuwa imeshaanza kuchafuka, "kama unakumbuka siku ulioletwa uliokuja nyumbani na baba, mimi ndo nilikuwa wa kwanza kukupokea" Alex aliongea huku akiilia taiming ile bastola kwa maana alielewa ikiendelea kuwa mikononi mwa mwanamke huyo basi maisha yake talikuwa hatarini. Christine alijaribu kuvuta kumbukumbu zake na kukumbuka siku ile baada kuokolewa na Mr Jason CJ alielekea marekani na mzee huyo. Wakati akiwa katika mawzo hayo Alex hakuchezea nafasi alifyetuka alipokuwa amekaa na kuikwapua mikononi mwa mschana huyo. Christine alishtuka na kuwa mnyonge, huku akijikunyata taratibu kwa sababu alielewa sababu ya kutekea kwa familia nzima ya Alex ni yeye. Ilibidi arudi kwenye kochi akae maana alihisi kuanguka na kweli haukupita muda alipiga ukwenzi mmoja tu na kupoteza fahamu. Alex alijaribu kumuamsha lakini wapi Christine alikuwa amepoteza fahamu kabisa, Alex alimbeba na kumpeleka chumbani kisha yeye akarudi ukumbini huku kichwani akiwa na maswali mengi yaliokosa majibu. Alihisi mishipa ya kichwa ikianza kutanuka kutokana na kuwaza mambo mengi ambayoa alijaribu kutafuta majibu ambayo yalikuwa hayapo kabisa kichwani mwake. Alipoona hali inazidi kuwa mbaya alitoa simu na kumuandikia ujumbe Allen, na haukupita muda Allen alifika katika jengi na kuingia ndani. "sikiliza kijana maswali yako yote yatapata majibu lakini si kutoka kwangu, unachotakiwa ni kutuliza kichwa na upumzike, kesho asubuhi akiamka Christine utamuuliza" Allen aliongea huku akijaribu kumtuliza Alex ambae alionekana kuelemewa na msongo wa mawazo..
Alex alkubaliana nae na kuelekea katika chumba kingine ambacho alioga na kubadilisha nguo, lakini aliporudi sebeleni hakumkuta Allen badala yake alikuta karatasi ndogo yenye ujumbe "kesho nitakuja". Aliichana na kurudi zake chumbani baada kuhakikisha kila kitu kipo sawa, usiku huo kwake haukuwa rahisi kukatika kutokana na msongo wa mawazo uliokuwa ukimuandama. Alikuja kushtuka asubuhi baada kupigw na mwanga wa jua usoni, kwa kujizoazoa alishuka kitandani. Alielekea bafuni na kujifanyia usafi, baada hapo alitoka na kuelekea sebleni ambaoko alimkuta Christine akiwa amekaa kimyaa na alipomuona tu Alex alishtuka na kuangaliapembeni. "habari za asubuhi" Alex alisalimia, "n..zu..zuri" Christine alijibu kwa woga. Hakuongea neno jingine, aliekea jikoni na kuandaa kifungua kinywa. Alirudi akiwa na vikombe viwili vya kahawa na kimoja akampa Chrsitine, "leo kuna mtu nataka uonane nae" Alex aliongea baada ukimya wa muda mdupi kutawala. "umeshatafuta mtu wa kuniua" Christine aliongea huku akitabasamu.
 
74.


"hapana anakuja kutusaidia mawazo tu" Alex aliongea na alipomaliza tu mlango uligongwa. "ndo huyo atakuwa kashafika" Alex aliongea na kuinuka akaenda kuufungua, Allen aliingia na Christine alivomuona tu alikiachia kikombe cha kahawa na kuanza kutetemeka. Kiufupi Christine alikuwa amechanganyikiwa kiupande fulani, "karibu Allen" Alex aliongea na kumpa mkono kama ishara ya salamu. Walielekea ukumbini ambako walimkuta Christine akiwa anatiririka jasho kama, "Habari yako Rose" Allen alimpa salamu na kumuita jina lake halisi. Christine au Rose alikuwa kimya tu huku akiwa amekodoa macho kama mtu alikabwa na tonge la ugali wa moto kooni. "binti sikia, mimi siko hapa kwaajili ya kukudhuru bali nataka kukusaidia" Allen aliongea maneno hayo kumuhakikishia mschana huyo usalama, "ah nani asie kujua wewe" Christine aliongea huku akijifuta jasho, "najua nina historia mbaya sana huko nyuma lakini amini kwa wakati huu sina nia ya kukudhuru kabisa. Unadhani ningetaka kukudhuru ungekuwa hai muda, ungekuwa ushakufa muda mrefu tu" Allen alijibu na kumsogelea Christine ambae alikua bado anatetemeka kwa woga. Alianza kuongea nae katika mfumo ambao hata Alex alishindwa kufahamu alikuwa anamaanisha nini japo maneno aliyasikia vizuri tu. baada ya dakika tano Christine alirudi katika hali yake ya kawaida kabisa. "ok muda hakuna tuanze mazungumzo" Allen aliongea, "Christine unajua chochote kuhusu vifo vya familia yangu" Alex aliuliza.

"ndio najua kila kitu na watu wote waliohusika" alijibu Christine, "ok, hebu nieleze maana nna hamu kweli ya kujua" Alex aliongea tena. "ni hivi siku alioniokoa ndio siku ambayo alinunua matatizo kwa huruma yake, kwasababu ilipangwa katika familia yangu asibakie hata mtu mmoja hai.Nilikuja kugundua kuwa vifo vya wazazi wangu vilitokana na mikono ya watu wakubwa katika matiafa kadhaa, watu hao walikuwa wakiendesha kampeni za chini kwa chini kuwashishi watu wajiunge na kikundi ambacho kilijiita WANAMAPINDUZI. Na kila aliyekataa yalimkuta kama yalioikuta familia yangu na yako, wazazi waliuwawa pamoja na watoto wa kike. Watoto wa kiume walichukuliwa na kupelekwa katika makambi mbali mbali ya siri kwa ajili ya kufanyiwa majaribio ya kutengenezwa jeshi ambalo ni tiifu. Moja kati ya watoto hao ni wewe japo mwanzo nilidhani umekufa pamoja na kakaako katika moto ule uliowashwa nyumbani kwenu. Wewe ulikuwa katika kambai ilokuwepo bahari ya pacific marine base71, lakini kaa ukijua kuwa kuna makambi mengine kama hayo zaidi ya mia. Watu waliokuwepo huko ni watoto yatima, wahanga wa vita hasa kutoka nchi za mashariki ya kati na mbali pamoja na Africa. Ukweli kwa sasa hicho kikundi kina jeshi kubwa sana ambalo likipewa tu amri basi dunia nzima inatumbukia katika majanga na mito ya damu. Watu wanaohusika na matukio yote haya ni watu wa kitengo cha upelelezi nchini Marekani, Urusi, Uingereza, Ufaransa na kadhalika. Lakini mkuu wa kikundi nimemjua hivi karibu anajiita THE GREAT GENERAL au GENEARAL DAVID. Ndie huyohuyo unaemfikiria saa hivi, mtu ambae wewe unamuona kama Godfather wako ndie mtu alieingamiza familia yako. Najua atakuwa amekwambia babaako amekufa kwa mshtuko baada kuona nyumba yake ikitetekea kwa moto, si kweli huo ni uongo mkubwa kwa sababu yeye ndie aliemuua.
.
Babaako alikuwa ni simba, sio mtu wa kutetemeshwa na vifo vya familia yake. Katika maisha yake amepoteza watu muhimu sana lakini bado alisimama kwa miguu yake miwili na kusonga mbele, unajua babaako alimpoteza rafiki wa pekee ambae walijuana tokea wadogo sana. Huyo mtu aliuwawa mbele ya macho yake na wala hakutoa chozi, lakini upendo wake kwa mtu huyo ulikuwa hauna mfano kabisa. Huyo aliitwa Mr Robert Mc cannon ambae ni baba wa Allen James au David Robert kwa jina lake halisi" alimaliza kuongea na kuwaangalia wote wawili usoni, Alex alionekana kuvimba kwa hasira lakini Allen alikuwa kimya huku akitabasamu, tabasamu ambalo lilifuatwa na micheirizi ya machozi yalioshindwa kujizuia ndani ya macho yake.
"yaani sikupata hata kumzika babaangu, halafu leo ndio nagundua kuwa watu niliowatumikia kwa moyo wa kizalendo ndio waliouchukua uhai babaangu, ni aibu gani hii" Allen aliongea huku akikunja ngumi kwa nguvu, vidole vilisikika vikidata na mishipa ilivimba usoni. "haki ya Mungu watalipa kwa walichomtendea marehemu babaangu" alisema kwa nguvu na ghafla damu za pua zilianza kumtoka na wala hakushtuka kabisa. Upande wa Alex yeye ndo alikuwa ameishiwa nguvu kabisa maana alikuwa hoi hasa alipofikiria kuwa mtu aliekua akimuamini sana ndio chanzo cha matatizo yake yote. Christine aliendelea "ukweli wote huu niliusoma katika kitabu cha kumbukumbu cha babaako ambacho nilikiba siku alionipeleka katika nyumba za kulelea watoto yatima, na nilikifanya ndio muongozo wangu wa maisha na humo ndio nikakuta siri nyingi kuhusu hicho kikundi cha wanamapinduzi na ndipo nikaweka azma kuwa lazima nitajiunga kwenye hicho kikundi ili nikisambaratishe ndani kwa ndani" alimaliza na kukaa kimya. "unaweza ukanionesha hich kitabu chake cha kumbukumbu" Alex aliuliza kinyonge huku machozi yakimtoka.
 
75.
Cheistine aliinuka na kuelekea chumbani, alirudi akiwa na kitabu mkononi na kumkabidhi Alex. Alikipokea ka mikono miwili na kukifungua nakweli muandiko aliokuta ulifanana kabisa na a babaake, alikuta pia picha moja amayo ilikua ni ya familia nzima. Machozi hayakuacha kutiririrka machoni mwake na uchungu pamoja na hasira vilizidi kila alipokuwa akikisoma kitabu hicho cha kumbukumbu za babaake. Allen aliliona na kujua abisa huko wanapoelekea si pazuri hata kidogo hivyo aliinuka na kumsogelea Alex. "kijana okoa nguvu zako, acha kulia mi naelewa uchungu wa kupoteza familia kuliko unavoulewa wewe. Futa machozi na usimame na kitu kimoja tu kichwani nacho ni kisasi, mimi nitakua na wewe mpaka mwisho a mpambano huu" Allen aliongo huku akimpiga piga Alex begani. Alex alifuta machozi kama alivomabiwa na kuinuka kisha akaelekea chumbani kwake, baada dakika kumi alirudi akiwa kashabadilisha nguo. Christine na Allen walimshangaa maana alikuwa amebadilika kabisa na kiunoni alipambwa na mkanda flani hivi ulikua umejaa magazine za bastola yake ndogo. "tunaanza wapi" Alex aliuliza, "hapa inabidi tuanze na mtu mmoja anaitwa William maarufu kama Willy" Christine alianza kuongea. Alitoa picha ya Willy na kumuonyesha Alex na kumpa maelezo yote kama yalivyotakiwa. Baada hapo Alex na Allen waliinuka na kutoka nje huku Christine akiwa na jukumu la kuhakikisha matukio yote yatakayofanyika hayarikodiwi na kamera zozote zile. "twende kwangu kwanz halafu tutaelekea huko wa hicho kitoweo" Allen aliongea na kumfanya Alex acheke kidogo baada kusikia neno kitoweo. Alikubali ba safari ya kuelekea kwa Allen ikaanza, walitumia dakika kumi na tano mpaka kufika huko. Waliingia ndani na Allen akamwambia Alex amsubiri sebleni na yeye akaelekea chumbani kae baada dakika kumi alirudi akiwa katika mavazi yake ya kazi huku akiwa amebeba mashine kuba mgongni iliotembea kwa jina la AK 47. Kiunono alikuwa na bastola ndogo nne semmiauto. Pia alibeba begi dogo lililokuwa na vipande vya sniper yake.
**************************************


"ni miezi minne sasa bado hatujui Alex na huyo Allen wako wapi" Mr Clinton alifoka kwa hasira, "mkuu tunaendelea kuwasaka na pia tumeshatoa taarifa katika nchi rafiki zote ikiwa wataonekana basi tutajua tu" Helen aliongea kujaribu kumtuliza mkuu wake. "Mkuu tuna tatizo kubwa sana" Martin aliingia huku akihema kama mtu aliekuwa akifukuzwa na jini, "kuna nini tena" Mr Clinton aliuliza kwa sintofahamu. "Agent William ameuwawa" Martin aliongea huku akihitahid kuhemama sawasawa, "tobaa" Mr Clinton alishtuka ile mbaya. "hii ina maanisha nini" Aliuliza, "hii inamaanisha kuwa kama ni Alex basi tayari ameanza safari ya kutuwinda" Aliongea Helen huku akionekana kama alikuwa kitetemeka. "kuna ushahidi wowote juu ya mauaji hayo" Helen alihoji, "kwa bahati mabya sana hata kamera za ofisini kwake hazijarikodo tukio zima" Martin aliongea kwa masikitiko makubwa sana. "hebu niunganishe na ofisi zetu nchini uingereza" Alitoa amri Mr Clinton na bila kuchelewa Martin aliondoka na kwaajili kazi hiyo. Alrudi baada dakika tano " mkuu tayari" alitoa majibu, Mr Clinton alinyanyua mkonga wa simu "hebu nielezeni kwa kina nini hasa kimeetokea" aliongea lakini majibu aliyoyapata upande apili yalikua hayana tafauti na yale allioletewa na Martin.
Baada maandalizi kukamilika majemedari wawili waliondoka kuelekea sehemu ambayo ndio chakula chao kwa siku hiyo kilikuwa kinapatikana. " Alex wewe utaingia katika ofisi zao, mimi nitakaa katika jengo moja hapa nje kwa ajili ya usalama, hakikisha unafanya kazi haraka iwezekanvyo" Aliongea Allen na Alex alikubali. Walifika nje ya ofisi na hapo wakatengana na kila mtu akaelekea upande wake. Christine alicheza na mitambo ya ofisi hiyo na kufanikiwa kuzihack computer zote huku akimpa Alex njia rahisi ya kufika katika chumba ambacho ndo William alikuwepo, na kutokana na mavazi aliovaa yalitosha kueleza kuwa alikuwa na Agent kama alivyo William na kwa sababu mitambo yao ilikuwa imevamiwa walishindwa kumgundua kabisa kama ni mtu amnae muda si mrefu wametumiwa picha yake kuwa ni wanted. "karibu" William alimpokea akiamini ni miongoni mwa wenzake maana maagent kujuana ilikua ni kitu kigumu sana kutokana na protokoli haiwaruhusu kujitambulisha ka majina yao isipokuwa kwa wakubwa zao tu. Allen tayari alishafika katika sehemu amabayo aliweza kuwaona wawili hao wakiongea.

"nipe ripoti kamili kuhusu mauaji ya familia ya Jason CJ" Alex aliongea akiwa serious, kwa mtazamo wa haraka William aligundua kuwa ujio huo haukuwa wa amani kabisa, alijaribu kupeleka mkono kwenye droo ili atoe bastola lakoni wapi Allen alipiga shaba pemebeni kidogo na ilipokuwepo bastola hiyo. "Unadhani nitakwambia kitu sahau" William alijibu kwa kujiamini huku akibonyeza kitufe cha siri ambacho kinatumika nyakati kama hizo za hatari. Lakini hakuna kilichotokea, "Alex umeona hiyo pete mkononi, muue huyo mjinga na uchukue hiyo pete" Allen aliongea kupitia kifaa maalum cha mawasiliano. Alex aliinuka na kumfumua William risasi ya kichwa kisha akamvua pete na kutoka zake bila mtu yoyote kushtukiwa na yoyote yule, wote aliopishana nao alimpa ishara ya heshma.
 
76.


Allen alifunga vifaa vyake na kushuka, moja kwa moja mpaka kwenye gari na kusoge eneo ambalo walikubaliana wakutane baada ya kazi. Dakika moja baadae Alex alifika eneo hilo na kuingiakwenye gari na safari ya kurudi ikaanza. Walifika nyumbani kwa CHristine na kumkabodhi ile pete, na kwa sababu Christine alifanya kazi nao alijua kabisa kama hiyo pete ni kifaa maalum cha kuhifadhia mambo ambayo ni siri kubwa sana. Alichukua kifaa maalum na kuiweka kisha akaanza utundu wake wa computer, baada nusu saa alifanikiwa kuhack pete hiyo na hapo sasa mafaili yote yalifunguka na kuzianika siri zote hewani. Walianza kukutana na mambo ambayo kwa kweli yalitisha sana, mauaji yasio ya kitoto yalirikodiwa wakati yanafanyika. Yaani hapo ubaya wa kitengo cha upelelezi ulimwagika, mauaji yaliopita na yanayofanyika kwa wakati huo na yatakayofanyika baadae yote yalikuwa yameandikwa humo. Yaani kwa siku moja waliua zaidi ya watu 20, Alex, Allen na Christine walibaki mdomo wazi wakionyesha kutoamini baada kila mmoja kushuhudia vifo vya familia yake bila chenga. "washenzi sana hawa na sasa watakoma" Allen aliongea na kukunja sura kama mtu alilamba ukwaju. Ghafla ile pete ilianza kuwaka rangi nyekundu, "Alex mchukue Christine na tukutane 73:56, FBI hawako mbali na hapa na wanakuja pamoja na S.W.A.T" Allen aliongea na kutoa bastol mbli kisha akaelekea dirishani na kuchungulia na kweli hakukosea kwa mabli alisikia ving'ora. Alex alichukua vitu muhimu na kutoka mlango wa nyuma akiongozana na Christine. Allen alitoa mabomu madogo mawili na kuayaset dakika moja na nusu. Alichungulia tena na tayari nyumba upande wa mbele ilikuwa imeshazingirwa, alifumua risasi kadhaa ili kuwashtua kisha akakimbilia mlango wa nyuma na kutoka. Baada sekunde kidogo tu mabomu yaliripuka a kuusambaratisha mjengo mzima, mabomu hayo yalikuwa madogo lakini shughuli yake ilikuwa kubwa si mchezo.
Christine kwa mbali alishuhudia nyumba yake ikiwaka moto "bora uende zako maana kila siku unanitonesha kidonda ambacho huwa kishanza kupona" alijisemea. dakika chache baadae Allen alifika na kuingia kwenye gari na safari ikaanza, "wapi sasa" Alex aliuliza. "tunaelekea Amrica lakini kwa njia za panya, hatutaki washtukie ujio wetu" Allen aliongea na kuwasha computer katika gari hiyo, alitafuta kitu kama ramani hivi na kumwambia Alex ambae ndo alikua dereva kwa wakati huo "fuata hiyo ramani". Alex alitikisa kichwa na kukanyaga mafuta na kuzdi kutokomea nje jiji la London, huko nyuma yalikuwa majanga matupu maana askari wengi waliofika kwaajili ya msako walijeruhiwa vibaya sana na wachache walipoteza maisha.
********************

.
"mkuu kuna jambo nahitaji kukwambia" aliingia Robert katika ofisi ya boss wake ndani ya kambi ya kikundi cha wanamapinduzi, "habari njema au mbaya" aliuliza General David ambae ndie mkuu wa kikosi hicho hatari. "mbaya tena sana" alijibu Robert, "mh nambie" aliongea tena. "kwanza tumempoteza Agent William lakini kibaya zaidi kuhusu mtu aliemuuwa ni yule kijana Alex akisaidia na Allen James" aliongea Robert huku akimuangalia bosi wake ambae tayari sura yake ilishaingia makunyanzi ikiashiria kuwa amekasirika. "huyo kijana hana kosa, mwenye kosa hapo ni huyo Allen James. Unajua familia yake iko wapi" aliongea na kutwanga swali. "hapana mpaka sasa hatujafamikiwa kujua familia yake iko wapi lakini ninachojua tu ni kwamba mtoto wake mmoja yupo mafunzoni katika kambi maalum" alijibu Robert. "sasa cha kufanya ni kumuua Allen halafu kesi ya mauaji yake tumatupia Alex, baada hapo tunamuingiza mchezoni mtoto wa Allen. Unajua tukimuingiza huyo mschana kutakuwa na asilimia kubwa ya kumkamata Alex kwa sababu atachanganya hisia na kazi na hapo itakuwa ni vigumu kushindwa kazi hii kwa sababu ata fanya chochote ikiwezeakana hata kuvunja sheria ilimradi tu na yeye amuue Alex kama sehemu ya kulipa kisasi cha babaake. Na hapo tutakuwa tumeuwa ndege wawili kwa jiwe moja, maana atakapo kamilisha kazi hiyo na yeye tutamuua" Aliongea General David na kuachia tabasamu la kinafiki lililojaa ubaya.
Alex alizidi kukanyaga mafuta mpaka walipofika katika sehemu ambayo ramani ilimuelekeza, alisimamisha gari na wote wakashuka. Alipigwa na butwa baada kuona sehemu hiyo imejaa vyuma chakavu yakiwemo mabaki ya ndege, na vifaa vingine vya kivita. Allen aloingoza njia na wengine wakafuata mpaka alipofika sehemu na mumanyaga. GHaflaardhi ilianza kutikisika na ukafunguka mlango mkubwa katika ardhi, Allen aliingia na kuwafanyia ishara wengine wamfuate. Baada kuingia wote mlango ulijifunga na kukarudo kama mwanzo. Aliwasha taa na hapo sasa Alex alikaa kitako kwa mshangao maana chumba hicho kilikuwa kimejaa silaha za aina zote. "tutapumzika hapa kwa siku moja na kesho usiku tutasafiri kueleke mjini New York" Allen aliongea na kuwaonesha bafu lilipo kwa ajili ya kuoga. Walijisafisha na kubadili nguo lakini Christine alishangaa kupewa nguo za kike "hizi nguo ni za nani" aliuliza kwa mshangao. "ni za marehemu mke wangu" Allen alijibu huku akionekana kutotaka endelea kuongea chochote juu ya mwanamke huyo. Christine aliligundua hilo hivo na yeye hakuuliza tena swali, waliandaa chakula na kula kisha wakapumzika. Siku ya pili maandalizi ya safari yalianza, "sasa tunatumia usafiri gani" Alex aliuliza. "tutatumia usafiri wa pipe inayotembea chini ya bahari mpaka katika kambi yangu nyingine mjini Florida, baada hapo tutakodi ndege mpaka New York" Alifafanua Allen. Alex hakuwa na swali jingine alikaa kimya kumuachiwa nguli huyo wa vita afanye kazi yake. Usiku ulipowadia walikwenda mpaka sehemu kilipochombo cha kusafiria na wote wakapanda. Safari ikaanza kwa mwendo mdogo lakini kadri muda ulivyokwenda chombo hicho kiliongezeka kasi, na baada ya dakika tano kilikuwa katika kasi kubwa sana kiasi ya kwamba kama ingekuwa ni ndege basi hata rada zingeshindwa kusoma. Baada ya nusu saa kilianza kipinguza mwendo na hatimae kilisimama, "karibuni Florida" Allen aliongea. Alex alikuwa haamini kabisa kama ndani ya muda mdogo kiasi hicho wameshafika Florida.
"acha utani we mzee" Alex aliongea akidhania ni utani, "kweli tumeshafika" Allen alisistiza. Alex bado hakumini kabisa lakini ilibidi ashuke ili ajiamishe kuwa kweli wako Florida au laa, Allen aliongoza njia mpka kwenye mlango na kuufungua. Kwa vile ulikuwa ni usiku hata watu wengi hawakuwa njiani, Alex alitoka nje na hapo sasa aliamini kama kweli wako Florida. Bila kuchelewa usiku huo walifika katika kiwanja kimoja cha ndege za kukodi. Walikodi ndege lakini hawakukodi rubani, "rubani nitakuwa mimi mwenyew" Aliongea Allen na kuingia ndani ya ndege. Baada maandalizi yote kukamilika safari ya kuelekea New York ikaanza, Allen alikuwa ni bingwa katika urushaji wa ndege. "mh kiasi wamuogope huyu mtu" Alex alijisemea moyoni, walifika katika uwanja wa ndege wa kampuni ile ile waliokodi. "karibuni New York ni matumaini yangu kuwa ndege yetu haijawaletea tatizo lolote" aliongea mzee mmoja. "tunashkuru sana kwa kuwa na huduma nzuri" Allen alijibu na kumkabdhi mzee huyo pesa taslim kwa ajili ya kumalizia deni lake.
.
Walitoka nje ya uwanja huo na kuchuku taxi, walielekea mpaka katika nyumba moja hivi ya wastani. "karibuni hapa ni nyumbani kwangu" Allen aliongea huku akitabasamu, waliingia ndani na kuweka kila kitu sawa. Kutokana na uchovu wa safari wote walikuwa hoi na baada ya kula tu kila mmoja liingia ndani na kulala japo ilikuwa tayari ishakaribia asubuhi.
Mafunzo makali yaliendelea katika kambi ambayo Christina au Agent Darling alipelekwa kuongeza ujuzi. Wengi aliokuwa nao waliishia njiani na wachache waliaga dunia kabisa, lakini ilikuwa tofauti wa mwanamke huyo ambe tayari mwili wake ulishaweza kumudu mazoezi ya aina hiyo. "unajua umenakiza kiezi mingapi" Jeff alimuuliza Christina, "dah hata sijui kabisa maana ni balaa, hata tarehe ya leo siijui" Christina alijibu huku akiendelea kupasha. "umebakisha miezi minne tu, halafu utapewa mtihani maalum wa kukabidhia medali yako ya THE ONE AND THE ONLY" Jeff aliongea huku akitabasamu lakini ndani ya tabasamu hilo kulikuwa na sura ya wasiwasi maana alieulewa vizuri mtihani huo ambao una matokea mawili tu, aidha ushinde ama ufe. Lakini kwa Christina alikuwa ni mwenye furaha sana, na alichowaza ni kurudi nyumbani na kumuonesha babaake medali yake ambayo ingempa cheo kuliko mwanajeshi yoyote yule katika nchi yake. Upande wa wanamapinduzi kulikuwa na kikao kikiendelea, na agenda ya kikao hicho ilikuwa ni kuhakikisha kuwa Allen James anakufa na kesi anabambikiwa Alex. "usijali mkuu mimi kama raisi wa nchi hii, nitahakikisha kuwa Agent Darling anaingia kichwa kichwa katika mchezi huu" Aliongea mtu mmoja wa makamo amabe kwa cheo alikuwa ni raisi wa nchi hiyo, "nitakushkuru sana Mr Jackson" aliongea General David na kucheka kidogo.
 
77.
Wakati wao wakiendelea na kikao, upande wa kina Alex nao pia walikuwa wanapanga mikakati ya kuwaondoa mmoja mmoja duniani. "sasa leo tunaanza na Mr Clinton, na kazi hii ataifanya Christine" aliongea Allen. "kwanini nisiifanye mimi" Alex alihoji, "Alex niachie huyo mbwa nikammalize mwenyewe, maana alichokuwa akinifanyia acha kabisa" Christine alijibu swali la Alex. "wakati Christine anatekeleza kazi hiyo Alex utakua nje unafatilia tukio zima, na ikiwa ksaada utahiajika basi fanya hivo" Allen aliendela kuongea, huyu mzee alikuwa ni master mind si mchezo. "wakati nyinyi mukiendelea na hilo, mimi nitakwenda kudili na mjinga mwengine ili kupata taarifa zote juu ya vikao vinavyoendelea katika kambi za hao wanaojiita wanamapinduzi" Allen aliendelea kuonesha yake katika kupanga mikakati. "tukifanya hivo tutazidi kuwachanganya, maana kupoteza watu wawili ndani ya siSilaha zote mtakazo zitumia zipo humu ndani" aliongea n kuinuka, alisogea mpaka katika ukuta na kuweka kiganja. Ukuta ulifunguka na kisha akaingia huku nyuma akifatwa na Alex na Christine, "ninapoongea kuhusu silaha namaanisha hizi" aliongea huku akiikamata bunduki moja mfano wa sniper lakini hii ilikuwa tafauti kidogo. "silaha hizi hata jeshi la nchi halimiliki" aliongea na kuwafanyia ishara kila mmoja ajisevia mashine amabazo angehisi zingemfaa katika kukamilisha kazi yake. walipordhika walitoka katika chumba hicho na kurudi sebleni, "tukutane hapa jioni baada kukamilisha kazi zetu" Allen aliongea na kutoa fungu ya gari mfukoni na kumrushia Alex. "katika gereji kuna gari aina GT harness bullet proof, mutatumia hiyo. Maisha yenu ni muhimu kwa hiyo msife huko hata kama itabidi uuwe wengine ili uokoeke basi usisite" Alimaliza kuongea na kuwahusia kisha yeye akatoka zake bila kuongea neno jingine lolete.
Alex aliinuka na kuingia ndani kwake na alipotoka alikuwa tayari katika commbat ya kazi, Christine hakuwa nyuma nae alivaa nguo zake za kazi na kubeba kila kitu ambacho angehisi kingemsaidia. Walitoka na kuelekea gereji ambapo walichukuwa gari na safari ikaanza, kwasababu kwa Christine ilikuwa ni mara ya kwanza kuingia uwanjani kutoa uhai wa mtu basi moyo wake ulikuwa ukinda mbio kupita maelezo. Alex aliligundua hilo na kummuwekea mkono juu ya mkono wake kisha akamawambia "usijali wala usiwe na wasi wasi kabisa, una mimi na Allen tunakuahidi kuwa hakuna jambo litakalo kutokea". Hapo kidogo mapigo ya moyo yalipungua kasi na kurudi katika hali yake ya kawaida, Alex alikanyaga mafuta na kuwa makini na kamera za barabarani. Walifika mpka nje jengo ambalo kwa nje linaaminika ni sehemu ya kufanyia biashara, Christine alishuka na kuvaa beji yake kifuani na kuweka miwai ake vizuri. Alikuwa amevaa kiofisi zaidi na beji alioweka ilimzuia yoyote kumuuliza swali isipokuwa bosi tu wa ofisi hio ambae ni Mr Clinton. Aliingia kwenye lifti na kuanza kupandisha juu, lifti ilisimama na mwanadada huyo akatoka na kila aliepishana nae alimpa heshima yake. Alifika mpaka kwenye meza ya secretary, "nataka kuongea na bosi wako" alitoa amri. Maggy alinyanyua simu na kupiga, "unaweza kupita" alijibu baada ya kukata simu hio. Christine alishukuru na kuingia ndani katika ofisi hiyo, kwa umakini wa hali ya juu aliweka kifaa maalum kwenye mlango kilichokuwa na sumaku na mlango huo ukajitia loki wenyewe. "karibu Agent" aliongea Mr Clinto huku akiuthaminsha mwili wa Christine, na aliganda pale alipofika kifuani na kukuta dodo zikiwa zimebustiwa vizuri. Hakuishia hapo aliendelea kushuka chini mpaka kiunoni na kuanza kukagua hips sasa. Hili jinga muda wote lilikuwa linawaza ngono, "eh Mungu wee tokea alivyokufa Rose nimekosa kabisa mambo mazito kama haya" alijisemea moyoni huku ute wa hamu ya ngono ukimjaa mdomoni. .
"nitasimama mpaka saa ngapi" aliongea Christine na Mr Clintone alishuka kutoka katika ndoto yake ya mchana. "ah karibu ukae" alijibu huku akijiuma meno, Christine alisogea na kukaa kwenye kiti huku ndani kwa ndani hasira zikizidi kumjaa. Alex alikuwa kwenye garia akifatilia kila kitu kilichokuwa kinaendelea katika jengo hilo, "ok nini hasa kilichokuleta hapa" aliuliza Mr Clintone baada utambuliso wa muda mfupi. "tumesikia unashirikiana na kikundi cha wanamapinduzi kutaka kuanzaisha vita" aliongea Christine huku akimkazia macho, kijasho chembamba kilianza kumtoka Mr Clintone huku akitfuta neno la kujibu. "ha...hap..hapana mkuu" alijibu kwa kudodosa, "lakini unawafahamu wanaofanya kazi hio si ndio" Christine aliongea tena na wakati huu alizidi kumkazia. "hapana mimk sijui chochote, hata hicho kikundi sijawahi kukisikia" alijibu kwa kujiamini sasa. Christine alifungua koti lake na kutoa bastola ndogo mbili na kuziweka mezani, "sasa utanambia ukweli au nitafanya nilichoagizwa nikifanye" aliongea huku akimuangalia Mr Clintone ambae alikuwa hajui afanye nini maana alielewa agizo likitoka katika kitengo hicho cha Christine lina uwezo wa kumuua mpaka raisi. Baada kuona hakuna jinsi ilibidi acheuke ukweli wote bila kujua kuwa alikuwa kashaachezwa akili. "hivo nilivoeleza ndivo nnavo jua mimi" alijitetea baada kumaliza kuongea, "nashkuru kwa ushirikiano wako lakini kuna jambo la mwisho nataka kukuuliza" aliongea Christine. "hivi unamjua Rose" aliuliza swali hilo huku akikunja ngumi lakini kwa vile mikono yake ilikuwa chini ya meza Mr Clintone hakufanikiwa kuiona ngumi hio. "ndio namjua, alikuwa secretary wangu lakini alishakufa muda mrefu mbona" alijibu Mr Clintone, hapo Christine alisimama na kuvua wigi alilokuwa amelivaa. Mr Clintone alitokwa na macho baada kugundua kuwa mwanamke huyo ndie Rose, "leo nimekuja kuweka mambo sawa kati yetu" aliongea kwa hasira na kunyanyua bastola zale kisha akafyetua risasi kadhaa, lakini Mr Clintone alikuwa mwepesi sana hivyo alifanikiwa kuruak pembeni. Kabla hajatoa bastola yake Christine alimuwahi na kumpiga teke zitola uso na kwa kasi ya ajabu akamuwekea bomba mbili za bastola katika macho yote mawili na hakuuliza hata shikamoo akafyetua risasi zilizoteokea nyuma ya kichwa cha Mr Clintone. Mr Clintone alianguka chini kama mzigo, wakati akiwa anamuangalia mzee huyo alielala katika dimbwi la damu ghafla alisikia mlango ukisukumwa kwa nguvu. Hakutaka kulaza damu alishika kitu kwenye sikio lake na kuongea "64:90" kisha akavua ile sketi na kushusha surualia aliokuwa maevaa ndani hapo sasa alionekana kama Angelina Jolie katika Tomb Rider. Miongoni wa mwa vifungo vya shati lake kulikuwa kuna bomu dogo la kuvunjia kioo. Alikitoa kifungo hicho na kukiweka kwenye kioo na haiukupita hata dakika kioo kikavunjika, wala hakufikiria mara mbili alikimbia na kuruka kutoka gorofa ya thalathini na moja. Aligungua parachute na kuelekea sehemu walioubalina wakutane na Alex, mpaka wanafanikiwa kuvunja mlango waliambulia peupe.

"kwanini umeamua kutufanyia hivo lakini, nani mwingine atatupa muongozo pale tutakapo kwama" Alex alilalamika huku akizidi kulia, alijiona ni mkosa mbele ya muumba wake kwa kumuacha mtu mwenye mke na watoto kufa. Christine alijitahidi kumtuliza Alex japo yeye mwenyewe alikuwa hoi kwa kulia, Alex hakuonge kitu tena alisimama na kuelekea chumbani kwa Allen, Alitafuta droo aliloambiwa na kulifungua, alivichukua vichupa na kurudi navo ukumbini. "nifate" aliongea na Christine aliinuka na kumfata, alielekea pale alipoweka mkono Allen na yeye akaweka wa kwake. Mlango ulifunguka na wote wakaingia, alielekea mpaka alipoanmbiwa kuna mlango mwengine wa siri. Aliugusa mlango huo nao ukafunguka, huku ukisindikizwa na taa zenye mwanga mkali. Walishangaa kukuta macomputer mengi sana, alisogea mpaka kwenye meza moja ambayo alikuta karatasi yenye maelekezo jinsi ya kutumia kemikali hiyo hatari. Kila mmoja aliingia chooni na kuoga, walipomaliza walivaa yale magauni ya hospitali kisha Alex akamchoma ile kemikali Christine na yeye pia akajichoma. Kila mmoja alipanda kitandani na kujiwekea vifaa maalum ambavo vimeunganishwa na computer ambayo itakuwa inafuatilia mifumo yote ya mwili. Pia walichoma drip ambayo ilikuwa na maji yenye virutubisho vya aina zote. "nakutakia usngizi mwema na tukutane baada miezi mitano" Alex aliongea huku akimuangalia Christine. "nawe pia" Christine alijibu huku akitabasamu, na ghafla wote wawili walianza kuona kiza na haukupita muda wote wakachukuliwa na usingizi mzito.
*********************************
 
78.
(baada ya miezi mitano)
Bado Christina hakuamini kama babaake ameuwawa, maana alihisi kama anaota vile. Ni mwezi mmoja sasa tokea Chritina Allen atoke katika kozi maalum ya THE ONE AND THE ONLY. Alikuwa ni mwenye furaha sana lakini furaha hio yote ilitoweka baada kupokea taarifa za kifo cha babaake kipenzi. Taarifa hizo zilimuumiza sana na kujikuta akiapa kumuua Alex kwa mikono yake miwili, "kuna taarifa zozote kuhusu Alex" Christina aliingia ofisini kwake huku akiuliza. "bado mkuu,hatujafanikiwa kujua yuko wapi" alijibu Joe. "endeleeni kusachi hakikisheni hamuachi jiwe halijafunuliwa" Aliongea mwanamke huyo ambae kwa muonekano tuu ilitoosha kuonyesha kama alikuwa hatari kupita maelezo.
"Alex, Alex" Christine alikuwa wa kwanza kuamka na kuanza kumuamsha Alex ambae alikuwa kiweweseka kama mtu aliekuwa akiota ndoto mabaya. "Allen" Alishtuka huku akiita jina hilo, "karibu tena duniani" Christine aliongea kwa uchangamfu sana. "Christine ni wewe au" Alex ilibidi aulize kwanza maana alikuwa amebadilika kidogo, "yeah ni mim na kuanzia leo usiniite Christine, niite jina langu halisi ...ROSE" aliongea Rose, Alex alishuka kitandani mara akakosea kuanguka kutokana na kuwa alikuwa amelala muda mrefu sana. Alitembe mpaka kwenye kioo na kujiangalia, macho yalimtoka baaada kujiona alivokuwa amevimba misuli na pia kidevu chake kilikuwa kimechafuka ndevu ambao ziliota kwa wingi wakati akiwa usingizini.


Alikitoa kifungo hicho na kukiweka kwenye kioo na haiukupita hata dakika kioo kikavunjika, wala hakufikiria mara mbili alikimbia na kuruka kutoka gorofa ya thalathini na moja. Aligungua parachute na kuelekea sehemu walioubalina wakutane na Alex, mpaka wanafanikiwa kuvunja mlango waliambulia peupe..
Wakati Alex na Christine wakikamilisha kazi yao, Allen huku aliekea katika sehemu ambayo ndio alikuwa na ahadi ya kukutana na huyo mtu mwingine. Alipofika kwenye jengo hilo alitoa bastola zake na kujiweka sawa kisha akaingia kwa umakini wa hali ya juu sana. "Naona umekuja kufuata kifo chako si ndio" ilisikika sauti ikitokea kwenye ambacho alikuwa amekaa mtu mmoja lievalia suti matata sana. "Mimi nimekuja kuhukua uhai wako tu" alijbu Allen huku na yeye akivuta kiti na kukaa, "hivi kweli unadhani utanishinda" aliuliza Robert kwa kejeli. "Mbona unauliza jibu" Allen nae alijibu kwa swali, jibu hilo lilipelekea kutokea kwa makunyanzi usoni mwa Robert.
"Mimi naona hakuna haja ya kupoteza muda zaidi, na napenda twende kiuwanaume zaidi hakuna kutumia silaha" aliongea Robert kwa kujiamini sana. "Itakuwa vizuri sana maana nina muda kweli sijapata mtu mwenye uwezo kama wangu katika ulingo. Ni matumaini yangu mpambano huu hautaisha mapema" alijibu Allen na kuweka bastola zake kwenye meza pamoja na kisu kidogo. Robert hakutaka kupoteza muda tena, alifyetuka kutoka katika kiti kwa kasi ya ajabu kusukuma masumbiw kadhaa ambayo mtaalamu Allen aliyatoka na kumzawadia ngumi nzito ya uso. "Uzembe ndio unao waua wengi" aliongea huku akikaa sawa.
"Acha kuongea wewe" alijibu Robert na kumvaa tena, safari hii alikuwa makini sana, Allen alijitahidi sana kuyatoka bila kushambulia. Na alifanya hivyo kuusoma mchezo wa adui yake huyo, kwa bahati mbaya aliteleza na kujikuta akichezea ngumi tatu kali sana za kifua. Alirudi nyuma na kukohoa kidogo, kikohozi hicho kiliambatana na mchirizi wa damu kutoak mdomoni. "Wewe ndio wanakuita Project x, sasa mimi ni Human killing machine (HKM)" Robert alijitamba kidogo. "Sasa ndio nimepasha na kama hujui kwa nini wameniita Project X. Ni kwa sababu utakavyoigeza X itabakia kuwa X tu" aliongea Allen na bila kusubiri jibu alifyetuka kutoka alipo na kumvaa Robert.
Robert kabla hajafikiri afanye nini alijikuta yuko hewani na kujibamiza ukutani, Allen hakumuachia hata asimame. Alimsogelea pale pale chini na kuanza kumshishia kipigo kitkatifu, Robert alijitahidi alijiyahidi kuzuia makonde ya kiumbe huyo lakini alishindwa kutokana na kasi ya makonde hayo. Allen baada kuona mpinzani wake amechapika, alimshika kooni na kumuinua mpaka akasimama sawa kisha akamuegemeza ukutani. "Unajua baada kukuondoa wewe duniani, Alex atakuwa amepata njia nyeupe kuelekea ushindi" aliongea Allen akisogea kwenye meza ambako alikuwa ameweka kisu chake. Alimgeukia Robert na kasi kubwa akaanza kumfata lakini kabla hajafika, alihisi kitu kikipenya mgongoni na kutokea mbele huku kikifuatiwa na mlio wa risasi iliofyetuliwa kutoka nyuma. Hata hivyo risasi hiyo haikumzuia kutimiza kil alichokusudia. Alijirusha kwa nguvu zake zote zilizobakia na kutua katika koromeo la Robert huku kisu alichokishika kikitengeza njia kubwa katika shingo ya Robert.
Wote wawili walianguka chini huku kila mmoja akijaribu kutetea uhai wake lakini wapi. General David alisogea walipo wote wawili huku akiwa haamini kilichotokea mbele yake na yeye ndie aliempiga risasi Allen. "Alex kazi kwako sasa, nitimizie kisasi ambacho sijakifanikisha" Allen aliongea maneno hayo na kuachia pini ya Grenade alilokuwa amebeba. General David kuona alikimbia na kutoka nje ya jengo hilo ambalo sekunde chache tu baada ya kutoka jengo zima likaripuka. Alikuta machozi yakimtoka na kuongea "nenda kwa amani mwanangu Robert na nasikitika mpaka unaaga dunia hujajua kama ni babaako mzazi" kisha akaondoka eneo hilo.
Alex na Christine walifanikiwa kutoroka na kurudi nyumbani, lakini mpaka usiku unaingia Allen hakuonekana. Hapo ndio Alex akaanza kupata wasiwasi, aliinuka alipokaana na kuanza kutembea tembea sebuleni. Bado haikutosha akaelekea chumbani kwa Allen, alikuta flash mbili nyeusu juu ya kitanda moja ikiwa imeandikwa jina lake na nyingine imeandikwa Christina pamoja na karatasi yenye ujumbe, aliichukua na kuanza kuisoma. "hicho kimoja ni cha kwako na kimoja cha mwanangu Christina au Agent Darling. Fungua chako tu na kimoja mkabidhi mwanangu".
Alex alitoka na flash hizo na kuelekea ukumbini ambako aliunganisha flash hiyo kwenye computer na kuifungua, Christine alikuja kuungana nae kuangalia ni kitu gani hicho. "Alex ninakwenda lakini sijui kama nitarudi, maana ninaekwenda kupambana nae ni hatari sana. Na uwepo wake tu kuna hatarisha kazi yako. Si mwingine bali ni Robert, ni hatari sana hivyo basi mimi nakwenda kukusafisha njia kuelekea ushindi. Kama nitakufa basi kifo changu utapachikiwa wewe kuwa ndio muuaji na watamtumia mwanagu Christina au Agent Darling kukukamata. Hivi sasa yuko mafunzoni katika kambi maalum anchukua mafunzo ya hali ya juu kabisa kuliko hata makombando wa nchi hii. Hivyo kaa ukijua atakuwa kikwazo kikubwa sana katika kufanisha kazi yako lakini naomba mmchukulie kama mdogo wako anaetenda asilolijua. Ukipata nafasi nzuri mkabidi hiyo flash na fanya hivyo bila kuchelewa. Mwisho kabisa chumbani kwangu katika droo kuna vichup viwili vya kemikali iliozimuliwa ya CODE X. Tumia kimoja wewe na kingine atumie Rose maana muna kazi kubwa sana mbele, kumalizia ikiwa sitarudi nakuomba unitimizie kisasi changu kwa walionitenda. Familia ni kitu muhimu sana basi fanya ufanyalo lakini baadae uwe na familia. Alex wewe ni kama mwanangu na kaa ukijua kuwa nilikuwa nakupenda sana na sitakuacha peke yako katika hii kazi. Nitakuwa nawe hata kama nitakuwa mbiguni" mpaka ujumbe huo unaisha Alex alijkuta akimwagikwa na machozi kama mtoto mdogo..
"kwanini umeamua kutufanyia hivo lakini, nani mwingine atatupa muongozo pale tutakapo kwama" Alex alilalamika huku akizidi kulia, alijiona ni mkosa mbele ya muumba wake kwa kumuacha mtu mwenye mke na watoto kufa. Christine alijitahidi kumtuliza Alex japo yeye mwenyewe alikuwa hoi kwa kulia, Alex hakuonge kitu tena alisimama na kuelekea chumbani kwa Allen, Alitafuta droo aliloambiwa na kulifungua, alivichukua vichupa na kurudi navo ukumbini.
 
79.

Mabega yake yalizidi kuwa makubwa, misuli ya kifua ilikuwa pia imeongezeka kutanuka. Six packs tumboni zilizidi kukamaa kama matofali ya kuchoma. "we Alex huoni kama uko uchi" Alshtuka baada kuguswa mgongoni na Rose, "damn" aliliweka guo lake vizuri kisha akaelekea sehemu ya kutokea. Aliweka mkono na mlango ukafunguka . Alipofika sebeleni alishangaa kukuta nyumba ikikwa haina hata vumbi utadhani kulikuwa kuna mtu anaishi. Lakini wala hakulijali hilo alielekea chooni na kuanza kujifanyija usafi, Rose nae alifanya hivo. Baada ya nusu saa wote walikuwa wameshamaliza, walirudi ukumbini huku kila mmoja akiwa na nguo za kawaida. Walirudi tena katika kile chumba chenye silaha na kuanza kutafuta silaha za kufanyia kazi, wakati wanaendelea kutafuta walikuwa mfuko mweusi na walipoufungua ulikuwa nguo nzuri za kazi. Hapo walitabasamu na kila mmoja kuchukua na kwenda kubadilisha, hapo sasa ndio wakawa wamekamilika. Kila mmoja alichukua silaha zitakazomfaa na kutoka katika chumba hicho. "tunaanza wapi" Aliuliza Alex, "inabidi tutoke tukachunguze kwanza" ROse alimjibu na wakakubaliana hivo. Waliingia gereji na kutoka na gari moja kwa moja mpaka katika makao makuu ya kitengo cha upelelezi. Walifika na kuweka fgari pembeni, "tusishuke" Alex aliongea kwa sababu alishaanza kuhisi kitu tofauti, aliliangalia eneo hilo kwa makini sana na kugundua kuwa lina kamera nyingi sana zimefichwa. "fikiria hatua moja mbele" alihisi kama sauti ikimwambia, alitabasamu kidogo na kujua japo Allen ameaga dunia lakini bad yupo pamja nae. Aliangalia kiti cha nyuma na kuchukua laptop kisha akaanza kufanya yake, alifanikiwa kuzihack kamera zote za eneo hilo na kuziunganisha katika laptop hiyo. Baada hapo waliondoka na kurudi nyumbani kwao, "sasa hatuna haja ya kwenda tena kule kila kitu tutaona huku huku" Alex alijisemea na kukaa kwenye kochi na kutoa pumzi ndefu.
"mkuu, njoo uangalie" Joe aliingia ofisini kwa Christina na kuongea, Christina bila kuchelewa aliinuka na kumfata mtaalamu huyo wa IT. "umeona ile gari" Joe aliongea, "ina sadikika ilionkena eneo hili siku aliokufa Mr Clinton" Joe alizidi kufafanua. "ok nipatie kila kinachohusika na gari hio" Christina aliongea na kuondoka. Joe alianza mandingo yake lakini cha ajabu hakukuta hata rikodi moja ya gari hio, ni wapi ilipopita baada kuondoka hapo. Kiufupi kamera zote za barabarani zilikuwa haziioneshi gari hio, "duh huyu jamaa anaenekana mtaalamu sana wa computer" Joe alijisemea na kuinuka kisha akaelekea ofisini kwa Christina. "mkuu inavyoonekana tunapambana na mtu amabe si wa kawaida kwa sababu amefanikiwa kufuta video zilizorikodiwa na kamera za barabarani" Aliongea Joe, "usiniambie anakushinda wewe" Christina aliongea kwa hasira. "ah sijasema kama ananishinda mimi ila kwa Computer zetu za kawaida hatuwezi kujua chochote kwa sababu huyu jamaa anatumia Master Computer" Alijitetea Joe. "sasa nikupatie hiyo Computer" Aliuliza Christina. "we nipe pesa tu kwa sababu hiyo computer huwezi kuipata bali unatengenezesha sehemu maalum" Joe aliongea na hapo hapo Christina alito kadi yake ya bank na kumkabidhi Joe "1313" aliongea na Joe akaondoka. "hahaha hatua moja mbele" Alex alikua akicheka baada kumzidi akili mtu amabe ndie atakaemuwinda, "Rose unataka kujifunza shabaha"Alex aliuliza. "natamani sana hasa kwa sniper" Rose alijibu huku akitabasamu, "jiandae basi nishampata mtu amabe utaanza kujifunzia shabaha kichwa chake" Alex aliongea na kuinuka, Rose nae alikwenda ndani aliporudi alikuwa na sniper mkononi na kwa pamoja walitoka na safari ikaanza. Walifika mpaka kwenye jengo fulani na kupanda mpaka juu, "kuna mtu mmoja atakuja katika ofisi hio hapo mbele na atakaa kwenye kiti kile pale" Alex aliongea, Rose alianza kuipanga sniper yake kwa ajili ya kazi "weka risasi moja tu inatosha" Alex aliongea tena Rose nae akafanya hivo. Baada dakika kumi Rodriguez alifika katika ofisi hio na kukaa pale pale Alex aliposema atakaa. Alex alikuwa na darubini hivyo alimuoma vizuri, "haya kazi kwako, pumua taratibu na usipige risasi mpaka pale utakapohisi mapigo yako ya moyo yamerudi katika hali yake ya kawaida" alimpa maelekezo hayo kama alivyopewa na Allen. Rose alitulia huku akijitahidi kupumua taratibu mpaka mwisho mapigo yakakaa sawa, akaweka jicho kwenye darubini ya sniper na kuanza kulenga. "sehemu nzuri ya kupiga ni kichwani" Alex alimpa maelkezo tena, "Rodriguez, Mungu akakubanika" Rose aliongea na kufyetua risasi ilioingia katika paji la uso la mzee huyo. "kazi nzuri" Alex alimpongeza na kukunja vitu vyao na kutokomea eneo hilo.
.
Taarifa hizo za kifo cha Rodriguez ziliwafikia wengine na kujikuta katika wakati mgumu sana, bila kuchelwa waliitisha kikao kilichoongozwa na Hellen. "nahisi sasa ule muda wa kuishi kwa amani umeisha" Aliongea baada kufungua kikao, "una maanisha Alex kasharudi" Martin aliuliza. "ndio na inaonekana sasa amejipanga kisawasawa" Hellen alijibu. "inabidi tumwage vikosi vianze kazi ya kumsaka" Mtu mwengine aliongea."acha ujinga wewe kwani hujui kama ule muda wa kufanya mapinduzi umefika" alifoka mwanamke huyo kwa hasira. "sasa unataka tuendelee kufa au vipi" aliuliza tena yule mtu, swali hilo lilimkera sana Hellen na kujikuta akichomoa bastola yake ndogo na kumchapa risasi kadhaa za kifua. "kuna bweha mwingine yoyote bado anaogopa" Aliongea Hellen na wote wa kutingisha vichwa kuashiria kuwa hakuna aliekuwa anaogopa. Acha kabisa kifo bwana, waliendelea na kikao chao na mwisho walikubaliana kuwa kila mtu afanye lolote lile linalowezekana amtoroke Alex hata kama itabidi kukodi bodigadi wake binafsi. Upande wa Christina alivimba kwa hasira baada kusikiwa kuwa Alex kashaanza kazi halafu yeye amekaa anasubiria master computer. "una mikono yenye nguvu sana, sikutegemea kama ungefanikiwa kumpata kichwani" Alex alimwabia Rose wakati wanapata chakula cha usiku. "ah nimebahatisha tu" Rose aliongea huku akitabasamu, "hapana hujabahatisha, ile ni kutokana na kuzidisha umakini kwa sababu ulikuwa ukitambua kuwa kwenye sniper ulikuwa na risasi moja tu hivyo kama ungemkosa ilikuwa ni vigumu kuweza kuweka risasi nyingine" Alex alifafanua. Basi walimaliza kula na kila mtu alielekea chumbani kwake na kupumzika. Siku ya pili mapema waliamka na kufanya mazoezi yakiwemo ya ngumi kwa sababu walielewa kuwa kazi hiyo itazidi kuwa ngumu kadri siku zinavyokwenda.

Wiki sasa ilikuwa imekatika bila matukio yoyote yale na master cimputer ilikuwa imeshakamilika, "sasa tuone nani kama Joe kwenye computer" alijisemea moyoni na kukaa kwenye kiti kisha akaanza mautundu yake na baada dakika tano aliweza kuziunga camera zote za barabarani na kila kona katika computer yake alioipa jina la Samurai. "bingo" alipiga kelela na kuinuka kiksha akenda kumuita Christina, "hii ni video ya kifo cha Rodriguez" aliongea Joe na kuanza kuirusiha nyuma taratibu ili kutafuta risasi imetoka wapi na alifanikiwa. "kuna vivuli vya watu wawili mmoja amesimama na mwengine amelala" alifafanua Joe. Baada hapo alianza kusafisha picha mpaka kufanikiwa kuwaona watu hao vizuri sana, "washenzi mumekwisha" Christina aliongea huku akitabasamu, tabasamu amabalo lilikuwa na maumivu tele. "halafu inaonekana aliepiga si nguli sana" Alizidi kufafanua Joe baada kuchunguza kwa jinsi alivyolala mpigaji huyo. "na hawa wanawalenga wakuu wa kitengo cha upelelezi" Christina aliongea na kuweka alama ya kuuliza kichwani. Wakati wakiendelea kuchambua video hiyo, simu ya Christina iliita "hallo" aliipokea. "naona unahangaika, kuchambua video si ndio" Aliongea Alex upande wa pili. Christina hapo alimpa ishara Joe aitrack simu hiyo, "usipate shida ya kuitrack maana utajiudhi tu" Alex aliongea tena na kuachia kicheko cha chini kwa chini. "nilijuwa tu utafanya juu chini kujua taarifa zangu na ndio maana nikafanya makusudi mauajia ya Rodriguez na hio na kukupa taarifa kuwa hata ukusanye jeshi lote la nchi hii basi hamtaweza kunizuia nisifanye nilichokusudia kwa sababu nimempa mtu ahadi na kama unavojua ahadi ni deni basi na mimi sitokaa mpaka niitimize" Alex alimaliza kuongea na kukata simu bila kusubiri Christina ajibu chochote. "mkuu hii simu imepigwa humu humu ofisini" Joe alitoa majibu baada kuitrack simu hio. "eti nini" Christina alimaka kwa mshangao. "WELCOME TO THE DIRTY GAME" Alex aliongea baada kukata simu hiyo na kutabsamu kwa hasira na machungu ya hali ya juu.
 
80.

Christina alijikuta akifura kwa hasira na kila alipojitahidi kuzituliza ilikuwa kazi bure, mwisho aliona bora aondoke kabisa ofisini. Moja kwa moja lienda mpaka nyumbani kwake na kujitupa kitandani huku akiwa na mwazo kibao. Na yote ilikuwa ni kivipi atamkamata Alex na kulipa kisasi kama alivyoamini kuwa Alex ndie aliemuuwa babaake. "Lakini kwa nini aseme hata nikikusanya jeshi zima siwezi kumzuia asitekeleze ahadi aliomuahidi mtu" swali hilo liliibuka tu kichwani mwake. "ana uhusiano gani na viongozi wa kitengo cha upelelezi" swali jingine liliibuka, "mh kuna kitu kinanuka vumba lakini hio sio kazi yangu kabisa, maisha yake ni halali yangu kuyatoa" alijisemea huku akitokwa na machozi.


Na maumivu yalizidi pale alipokumbuka kipindi akicheza na babaake wakati ni mdogo sana. "Hivi unataka kuwa nani ukiwa mkubwa" aliuliza babaake, "nataka kuwa kama wewe baba" Christina alijibu kwa sauti ya kitoto huku akicheka na kumkumbatia babaake. Mapenzi aliokuwa nayo binti huyo kwa babaake yalikuwa makubwa sana hasa ukizingatia mamaake alikufa wakati yeye ni mdogo hivyo basu mapenzi yote aliyahamishia kwa babaake. "kwanini lakini ulirudi katika mazingira ya vita tena wakati uliniahidi kuwa wewe na silha basi tena" Christina alijisemea mwenyewe huku akimlaumu babaake kwak kuto timiza ahadi yake. "kila kitu nilichokifanya nilikifanya kukupa tabasamu usoni, sasa hizi medani zote nilizozipapta nani nitamuonyesha na nani atakae ziona za thamani sana" alizidi kulalamika. Wakati akiendelea kulia alihisi kitu kama kikimgusa begani na aliogeuka alishangaa kumuona babaake akitabasamu huku akimuonyesha ishara kuwa anyamaze na kuwa mkakamavu. Alitaka kumkumbatia kwa furaha lakini alijikuta akikumbatia hewa, kumbe yale yalikuwa ni mawazo yake tu. Na hiyo ilikuwa ni kawaida ya babaake kumgusa begani wakati anapokuwa na wakati mgumu sana na kushundwa kupata majibu.

Alex akijishangaa mwenyewe ni kwa jinsi hata uwezo wake wa kupanga matukio ulivokuwa mkubwa sana. "kweli hii kemikali ni balaa" alijisemea moyoni wakati akiendelea kupanga mikakati kuanza kuwaondoa maadui zake kwa kasi ya kubwa. Rose alikuwa katika chumba maalum akifanya mazoezi ya kujiweka sawa maana alielewa shughuli iliokuwa mbele yake ilikuwa si ya kitoto. Alex alikamilisha mipango na kuelekea chumba cha mazoezi, "naona umeiva sasa" aliongea huku akivua shati lake. "unataka spaling nini" Rose aliongea huku akitabasamu, "ah huniwezi wewe" Alex alijibu na kuvaa vigloves maalum vya spaling. "ntatumi mkono mmoja tu" Alex aliongea na kuweka mkono wake wa kulia nyuma, Rose alijiweka sawa na mpambano ukaanza. Uwezo wa Alex uliongezeka mara dufu kuliko mwanzo maana alivyokuwa akizitoka ngumi ilikuwa ni kama mtu anaepelekwa na mashine. Rose alijitahidi kupeleka masumbwi mazito lakini wapi Alex alikuwa level nyingine kabisa na kuna wakati alitabiri kabisa atapiga wapi. Baada dakika kumi Rose alikuwa hoi na hapo alikuwa anashambulia tu, Alex wala hakurusha ngumi hata moja. "kweli umeiva sana" Alex alimsifia baada zoezi hilo fupi, "ah wapi sijakupata hata ngumi moja" Rose aliongea huku akicheka. "usijali kuna watu kibao mikono yako tu, hadi utachoka mwenyewe kwani ndi kwanza safari imeanza" Alex aliongea na kutoka na kuelekea chumbani kwake kwa ajili ya kujifanyia usafi. Baada saa moja walirudi sebleni na kupata chakula cha usiku kisha wakaanza kuoanga mipango ya usiku huo. "kuna huyu jamaa anaingia leo kutoka Uingereza, anaitwa Masaya. Ni mjapani mwenye asili ya kiingereza na ni miongoni mwa watu waliotumika katika kuhakikisha familia zetu znatetekea" Alex aliongea na kuendelea "huyu jamaa ana ulinzi wa hali ya juu sana lakini tukimuondoa mchezoni huyu tutakuwa tumejisafishia njia kuelekea ushindi maana baada Robert kwa hatari anafata huyu".
.
"so tunampelekaje kuzimu" Aliuliza Rose huku akiwa amevaa sura ya kazi. "kwa karibu hatuwezi kumpata lakini itabidi tuwapunguze walinzi wake, ili yeye afanikiwa kutoroka na baada hapo tutamsubiri 98:11, hapo tunaishambulia gari yake na kuhakikisha hatoki mtu. Kwa hiyo leo tutabeba bastola tatu sniper, smg na ndogo ya dharura" Alimaliza kuongea na kila mmoja akachukua silaha zake na kutoka nje. "mbona kuna gari mbili" Rose aliuliza kwa mshangao baada kukuta ferari nyeusi nje, "ndio, nimesahau kukwambi kuwa kuanzia sasa kila mtu atakuwa na usafiri wake. Hii itatupa urahisi kusaidiana ikiwa mmoja wetu atakamtwa" aliongea Alex na kumkabidhi Rose fungo ya ferari na safari ikaanza. kila mmoja alionesha ufundi wake katika kumudi gari hizo ndogo zenye mashine kubwa sana, walipofika sehemu walipeana ishara na kila mmoja alichukua njia yake.
Katikati ya usiku, ndege binafsi ilituwa katika moja kati ya viwanja vyake nchini marekani. "karibu marekani mkuu" aliongea mtu mmoja wakati anamkaribisha, "asante" Masaya alijibu huku akishusha pumzi kwa kasi. "tafadhali nifate" aliongea yule mtu na Masaya aliimfata huku akizungukwa na walinzi wake, "Juliet, uko katika nafasi yako" Alex aliongea katika kifaa maalum cha mawasiliano. "ndio Romeo, Roger that" Rose alijibu huku akijiweka sawa. "Mlengwa anaelekea saa 7:00" Alex aliongea, "nimekusoma Romeo" Rose alijibu. "usishambulie mpaka nitakapokwambia, over and out" Alex aliongea. "mkuu kuna mtu mmoja anaengia leo kutoka uingereza, na nina wasiwasi Alex atakuwa anamfatilia maana nimefanikiwa kuvamia computer yake" Joe aliingia Ofisini na kutoa taarifa, "nindalie gari yangu" alitoa amri huku akianza kutoa mashine za kazi. "tunaanza kushambulia ndani ya tatu, mbili na moja" Alex alimaliza kuongea na hapo sasa walinzi wa Masaya walianza kuenda chini mmoja baada ya mwengine. "mkuu tafuta sehemu ujifiche kuna masniper hapa" aliongea mlinzi mmoja kabla ya kupasuliwa kichwa na risasi iliyotoka kwa Rose. Masaya alikimbia na kufanikiwa kuingia katika gari na kumwambia dereva wake aondoe gari. "Juliet Kimbiza" Alex aliongea na hapo hapo waliacha kushambulia na kushuka chini, kila mmoja aliingia kwenye gari yake na safari ikaanza.



"tembea 220 km/saa" Alex aliongea huku akizidi kukanyaga mafuta na Rose nae hakuwa nyuma. "namuona mlengwa" Rose aliongea alipoiona gari ya Masaya mbele yake, "mpite na umzingue" Alex aliongea na Rose alifanya hivo. Aliipita gari ya Masaya na kuanza kupunguza mwendo huku akijitahidi kuibania isipite, dereva wa Masaya alipoona hivo aliamua kuingia njia za ndani kwa ndani na hilo ndio kosa alilofanya. Alex alishatangulia mbele na kufunga njia kwa gari kubwa ambalo alikuwa ameliandaa. "mkuu hakuna tena njia huku" Aliongea yule dereva, "rudi nyuma" aliongea Masaya lakini dereva alipoangalia kwenye kioo cha pembeni alishtuka "mkuu kuna gari mbili nyum zimefunga njia" aliongea dereva. Alex na Rose walishukwa kwenye gari huku mkononi wakiwa na SMG na kuanza kuishambulia gari ya Masaya. Walimimina risasi za kutosha mpaka gari ikawa haitamaniki, waliporidhika taratibu waliisogelea gari hiyo na kufungua mlango. Walimkuta Masaya akihema juujuu huku akiwa na majeraha kadhaa. "nyie ni kina nani na mnatakat nini" Aliuliza kwa tabu, Alex wala hakumjibu alimsachi na kuchukua flash ndogo pamoja na pete. "Rose, halali yako huyo" aliongea Alex na kurudi nyuma, Rose alitabasamu na kumyandika Masaya ngumi ya koo. Masaya wala hakufurukuta alitulia tuli na kutoa upepo wa mwisho na kuaga dunia, walirudi kwenye gari na kuondoka eneo hilo. Wakati wanatoka katika kichochoro hicho uso kwa uso na Agent Darling, Alex alishusha kioo wakatia anapishana nae na kusema "Allen Jr umechelewa tena, unamuangasha babaako" kisha akapandisha kioo na kukanyaga mafuta. Agent Darling alikanyaga breki na kuserereka, alianza kumfukuza huku akiwa na hasira ile mbaya. Alex alipoona Gari ya Agent Darling inakuja akaongea "Juliet tukutane nyumbani", "umesomeka Romeo" Rose alijinbu na kupumguza mwendo. Gari ya Agent Darling ilimpita kwa kasi sana, alitabsamu kidogo na kubadilisha njia. Mtanange ulianza kati ya Alex na Agent Darling, "kama ulivyosema mkuu mwanao ni mbishi sana" aliongea Alex akimaanisha Allen. "leo haki ya nani sikuachi labda gari yangu ipinduke" Agent Darling aliongea huku akizidi kukanyaga mafuta na gari yake aina ya lambogini Galado ilitii amri na kuteleza barabarani kwa mwendo kasi wa hali ya juu sana.
Manguli hao wawili walizidi kuonyesha uwezo wao katika fani hio ya kuchoma matairi, Agent Darling alishusha kioo na kujaribu kuishambulia gari ya Alex lakini kutokana na mwendo kuwa wa kasi sana ilikuwa ni vigumu kuipata. Hivyo basi kwa sababu gari yake ilikuwa ni yenye kufunguka paa, alibonyeza kitufe na lile paa la gari likafunguka na alipoona linachelewa alilipiga ngumi na kuling'oa. Wakati wote Alex alikuwa akumuangalia kupitia kioo cha pembeni na kutabasamu "ni kweli ulioyasema Allen, binti yako ni mbishi sana" Alex aliongea maneno hayo huku macho yake yakianza kujaa maji. Agent Darling aliwasha computer ya gari yake na kuweka tracking mode, mfumo huo uliiwezesha gari yake kuikariri gari ya Alex. Kisha akabonyeza kitufe kingine kilichoandikwa auto drive, na baada hapo aliachia msukani na kusimama kwenye siti yake. Gari yake ilizidi kusonga mbele na wakati huo ilikuwa ikijiendesha wenyewe, alichukua bastola kubwa aina AK47 na kuanza kuishambulia gari ya Alex. Bastola hio ilikuwa ina nguvu sana kiasi cha kutengeza nyufa wakati risasi yake ilipopiga katika kioo cha gari ya Alex japo ilikuwa ni bullet proof. "mbili nyingine navunja kioo cha nyuma" Agent Darling alijisemea moyoni, alifyetua risasi ya pili ikaende kupiga pale pale ilipopiga ya kwanza na bila kuchelewa alifyetua ya tatu na hatimae kioo cha nyuma cha gari ya Alex kikavunjika.
 
81.




Alex alishtuka baada kioo hicho kuvunja na ndipo akakanyaga breki na kuizungusha gari na ikaelekeana uso kwa uso na gari ya Agent Darling. Aliweka gia ya kurudi nyuma kuanza kurudi nyuma kwa kasi kubwa sana kisha alishusha kioo cha na kutoa bastola yake ndogo na kuanza kujibu mashambulizi. Lakini wala hayakumtisha Agent Daeling badala yake alitabasamu na kutoa bastola ndogo na kuanza kumimina risasi. Alex aliangalia saa yake ya na kugundua kuwa muda umekwenda sana, "siku nyingine tutamalizia mpambano wetu" Aliongea na kutabasamu kidogo kisha akalenga tairi la upande wa kulia la gari ya Agent Darling na kulichapa risasi. Tairi hilo lilipasuka na kutokana na mwendo mkubwa wa gari ile ilianza kuyumbayumba na kupoteza muelekeo. Lakini kabla gari hiyo haijapinduka Agent Darling aliruka na kupiga sarakasi nyuma, alitua barabarani na kubiringitia kwa ufundu wa hali ya juu sana. Alex alishuhudia tukio hilo zima na kujikuta akikodoa macho kama mjusi aliebanwa na mlango na ilibidi asimamishe ari kwanza. Agent Darling alisimama na kuiangalia gari ya Alex kwa hasira "bahati yako mpumbavu wewe" alijisemea na kusonya kwa nguvu kisha akatoa simu yake na kupiga. Alex aligeuza gari yake na kuondoka eneo hilo.
Baada ya dakika tano ilifika ndege moja ambayo watu wengi hawakuwahi kuiona, ilitua alipokuwa Agent Darling na kushuka mtu mmoja ambae kwa mbali ni mtu aliejengeka vizuri kimaumbile. "pole kwa kazi ngumu" aliongea Jeff baada kufika alipokuwa amesimama mwanamke huyo, "ah pole ya kazi gani sasa wakati sijafanikiwa kumchuna japo kidogo" Aliongea kwa masikitiko makubwa sana. "usijali huo ni mwanzo tu, mbona muda si mrefu utamuingiza mkononi" Jeff alimjibu huku akimsogelea na kumkumbatia, kwa jinsi alivyomkumbatia ilionyesha wazi kuwa hao walikuwa ni mtu na mpenzi wake. Agent Darling alikuwa akilia sio kwamba ameumia au kwa sababu kuna mtu anamjali sana bali alikuwa akilia akijilaumua kwa nini amemuacha Alex amemtoroka mikononi mwake. Jeff alimshika mkono na kurudi katika ndege na ndege hiyo ikaondoka na kupotelea angani. Alex alifika nyumbani kwake na kuingiza gari ndani, lakini mpaka wakati huo bado ile picha ya Agent Darling namna alivyochomoka kwenye ile gari ilikuwa ikimrudia kichwani mwake. "inawezekanaje mtu kuweza kutoka katika gari inayokwenda karibu kilometa 180 kwa saa kisha atue bila hata kuumia au kuvunjika" hilo ndio lilikuwa swali alilokuwa akijiuliza. "mbona umechelewa" Rose aliuliza baada Alex kuingia ndani, "ah we acha tu nilichokiona huko ni balaa, na inabidi tuwe makini sana na huyu mtoto wa Allen maana huyu mtoto ni balaa" Alex alijibu huku akijitupa kwenye kochi.
CODE X 2: THE DIRTY GAME 25
Muda wote alikuwa hajamuangalia vizuri Rose, baada kukaa kwenye kochi ndipo akamuangalia. Alishtuka baada kuona nguo aliovaa inaonyesha vizuri na kumchora umbile lake lenye asili ya kilatini. Aljitahidi kupotezea lakini wapi, mwanaume ni mwanaume tu hata awe kauzu vipi. Rose alilishtukia hilo na kuinuka, moja kwa moja alikwenda na kukaa juu ya mapaja ya Alex na wakawa wanaangaliana uso kwa uso. "hivi Alex mpaka lini tutakuwa tunalala vyumba tofauti" Rose aliuliza kwa sauto ya kike zaidi, "Rose vipi umechanganyikiwa nini" Alex alijibu huku akijitahidi kuyaondoa macho yake katika kifua cha binti kilichochorwa na matiti ya wastani na yaliojaa. "Alex mimi sijanganyikiwa ila nimejitahidi sana kuzuia hisia zangu juu yako lakini kwakweli nimeshindwa" Rose alijibu huku akisogeza kichwa chake karibu zaidi na cha Alex mpaka kikafika sehemu wakawa kila mmoja anahisi mvuke wa pumzi ya mwenzake.
*****************************.
"huyu Alex anazidi kutuyia heka heka kwa kweli" Helen alioongea wakati wakiwa kwenye kikao, "unajua vitu alivyochukua kwa Masaya vina siri kubwa na nzito sana" Martin aliongea huku akikuna kichwa. "sasa tunafanyaje kumpunguza makali" Helen aliuliza, "nimewasiliana na mtu mmoja hatari sana na amekubali kutusaidia ikiwa tutamlipa hela ya kutosha" Jafar alijibu. "ni nani huyo mtu mwenyewe"aliuliza Martin."Huyo anaitwa Shadow jina lake la kazi na anamiliki kikundi kinachoitwa COBRA, ni kikundi hatari sana cha majambazi ya kimataifa" alieleza Jafar. "hivi wewe una akili timamu kweli" alifoka mtu mwengine aliekuwepo kwenye kikao hicho kisha akaendelea "kwanini tusitumie tu wanajeshi wa kawaida, hivi unadhani...."kabla hajamaliza ulisikika mlio wa risasi na yule jamaa akaanguka chini huku akiwa na tundu linalotoa damu kichwani. "kwenye vita hakuna sahihi wala kosa, yote ni sawa" Helen aliongea maneno hayo wakati anairudisha bastola yake mezani. "Jafar mpe kazi huyo jamaa na kuhusu malipo tutamlipa kiasi anachotaka" Helen aliongea na kusimama akimaanisha kikao kimefungwa. Kila mtu aliondoka na kurudi sehemu yake ya kazi, ule mzoga ulibebwa na kupelekwa sehemu ya kuchomea maiti. "Shadow, kazi kwako sasa" Jafar aliongea maneno hayo baada simu yake kupokelewa upande wa pili kisha akakata. "vijana ule muda tuliokuwa tunausubiri umefika sasa, maana mikono ilikuwa inawasha kweli. Hivi ni muda gani hatujamwaga damu ya mtu" aliongea Shadow na mwisho akauliza. "ni wiki sasa mkuu" alijibu kijana mmoja ambe alioenekana mkorofi sana maana baada kuambiwa tu kuna kazi alinza kuweka silaha zake vizuri. "huyu kwenye picha ni Alex na ndie tunaetakiwa kumuondoa duniani, inavyosemekana eti ni mtu hatari sana. Sasa sijui ni hatari kuliko sisi lakini hakuna mtu hatari kama sisi katika dunia hii" aliongea na kucheka kwa kejeli. "wale vijana wa kupeleleza naomba muingie kazini hakikisheni ndani ya siku mbili mnajua tunampata wapi" alitoa amri hiyo na vijana kumi wakaondoka kambini kwa ajili ya kusaka taarifa za Alex na wapi anapatikana.
Kabla hajakutanisha mdomo wake na wa Alex, Alex alimzuia na kumshusha mapajani mwake kisha yeye akainuka na kuelekea chumbani kwake. "huyu nae kama karogwa" aljisemea moyoni wakati anaingia chumbani kwake. Alivua nguo na kuingia chooni kwaajili ya kuoga, wakati anaendelea kuoga ghafla alihisi mikono laini ikitambaa mgongoni kwake na alipogeuka alishangaa kumuona Rose akiwa mtupu na hapo ndio akakumbuka kama alisahau kufunga mlango kwa ufunguo. Lakini mpaka hapo alipofikia tayari alishainua mikono na kumpokea mschana huyo kwa moyo mkunjufu kabisa na kujikuta wakitokomea katika ulimwengu furaha zisizo na mwisho. Walikuja kushtuka asubuhi kumeshakucha, "Alex mbona mpema hivo" Rose aliongea baada Alex kumtingisha. "nenda kamalizie usingizi chumbani kwako" Alex alimjibu, "chumbani ni humu humu siendi kokote" Rose alijibu. "wee kuanzia lini" Alex aliuliza kwa mshangao, "kuanzia jana usiku" Rose alijibu na kugeuka upande wapili kisha akaendelea kulala. Alex alishuka kitandani lakini alishangaa kwa jinsi alivyokuwa mwepesi asubuhi hiyo, "duh nimepungua uzito nini" alijisemea na kujicheka mwenyewe kisha akatoka chumbani na kuelekea jikoni. Alitengeza kahawa na kunywa kisha akenda kuchukua ile flash na kuichomeka katika laptop yake, mambo alioyakuta humo yalianza kumfanya atoke jasho. "lazima watu zaidi ya milion 100 wafe, ili wafahamu kuwa mapinduzi lazima" hayo ni miongoni mwa maneno yaliosikika katika video aliokuwa anaangalia. "karibu tena duniani" Jeff aliongea baada Christina kufungua macho, "hapa ni wapi" Christina aliuliza. "karibu katika GHOST CHAMBER" Jeff alimjibu huku akitabasamu, "nimelala kwa muda gani" Christina aliuliza tena. "ah ni usiku mmoja tu" Jeff alimjibu na kuinuka, alikwenda mezani na kurudi na vikombe viwili vya kahawa. Kimoja alimpa kimoja Christina na kimoja alikunywa yeye. "nahitaji kurudi ofisini" Christina aliongea huku akisimama, "kwa leo huwahi tena, subiri mpaka kesho nitakupeleka" Jeff aliongea huku akimrudisha kwenye kitanda. "sawa" Christina alikubali na kukaa, "dah gari yangu hata sijui iko katika hali gani" aliongea Christina huku akionekana kama mwenye majonzi. "usijali, ile ilikuwa ya mpito tu. kuna gari yako ya aina yake peke yake iko katika hatua za mwisho kukamilika, inaitwa DARLING" Jeff alijibu huku akimuangalia Christina usoni.
********************************
 
82.
"Masaya tumeshampoteza tayari halafu munanambia nikae chini nitulie, hivi nyie mnaaakili au mumechanganyikiwa" General David alifoka katika kilichokuwa kinaendelea kwa siri. "mkuu usijali kila ktu kitakuwa sawa muda si mrefu" mtu mmoj aliongea ili kumtia moyo bosi wao ambae alienekana kukasirishwa n avifo vya watu wake hasa wale wenye umuhimu mkubwa. "sasa nawapa wiki moja tu ikiwa hamujanileteza Alex hapa naingia mwenyewe kazini" alifoka na kusimama, "sawa mkuu na tunakuahidi kuwa ndani ya wiki moja tutamleta Alex kwako akiwa hai ama amaekufa" walijibu kwa pamoja na kikao hicho kikafungwa. "huyu Alex huyu ni maumivu shingoni", "lakini ilikuaje kuaje mpaka tukafikia hapa". "unamaanisha nini kusema hivyo", "yaani namaanisha kwanini tumeingia katika mkumbo huu wakati tuna vyeo vikubwa tu katika nchi zetu na watu walikuwa wakituheshimu na kututumikia sisi". Hayo yalikuwa ni mazungumzo kati ya viongozi wawili wa nchi fulani. "Alex, Alex, Alex kosa langu kubwa n kukuacha hai" General David aliongea mwenyewe huku akionyesha ni mwenye hasira sana, "lakini nakuahidi utakufa tu kama walivyokufa wengine" aliongea tena kucheka kicheko kilichojaa uasi, chuki na hasira.


"Christina nifuate" Jeff aliingia katika chumba alichokuwa amepumzika Christina na kuongea, Christina alinyanyuka na kumafata bila kumuuliza swali. Walietembea mpaka kwenye chumba kimoja kikubwa sana, kwa mbali kulikuwa na kitu kimefunikwa na turubai nyeupe. "nenda ukafunue" Jeff alimwambia na yeye akakaa pembeni, Chritina alitembea kwa mwendo wa haraka mpaka alipofika alipoambiwa afunue. Mapigo ya moyo wake yaliongezeka kasi mpaka akawa anayasikia masikioni mwake, taratibu alianza kufunua turubai hilo mpaka anamaliza alikuwa haamini macho yake kabisa na alijaribu kuyafikicha ili kama yupo kwenye ndoto basi aamke. "happy birthday Darling" Jeff aliongea huku akimkumbatia kwa nyuma, christina alifurahi sana maana hata yeye mwenyewe alikuwa amesahau siku hiyo muhimu kwake. "hiyi ndio zawadi yako ya siku ya kuzaliwa" Jeff aliongea na kumkabidhi funguo za gari yake mpya inayokwenda kwa jina la darling. "unaweza ukatest, gari hii ni ya kisasa na iko hii hakuna nyingine. Ni bullet proof na mifumo ya silaha na kila kitu huna haja ya kushusha kioo na kushambulia wakati unamkimbiza mtu. Unabonyeza tu ndani na mbele zitatoka bunduki na utashambulia ukiwa ndani ya gari hii" Jeff aliendelea kumpa maelezo juu ya gari hiyo mpya kabisa hata katika ulimwengu haijawahi kuonekana.
Alex alimaliza kuikagua flash ile na kugundua siri nyingi sana na kwa msaada wa Rose walifanikiwa kugundua mpaka makao makuu ya kikundi hichi haramu. "sasa kilichobaki itabidi tuongeze kasi ya mauaji ili tuikamilishe kazi hii kabla ile siku waliopanga haijafika" Alex aliongea na Rose alikubali. Wakati wao wakipanga mikakati hiyo, vijana wa Shadow waliripoti kambini na kutoa taarifa zote walizozipata. "kazi nzuri vijana wangu" Shadow aliwasifu kwa kazi nzueri waliofanya, alitoa amri maandalizi ya mavamizi yaanze. Kikosi hicho kilikuwa na vijana thalathini waliobobea katika mbinu za kivita chini ya Shadow kiongozi asie na huruma hata kidogo.
"ah nimesahau kukuambia kitu" Jeff aliongea wakati Christina anajiandaa kuondoka, "kitu gani tena2 Christina aliuliza. "chukua hii flash itakupa maelezo mazuri tu" Jeff aliongea na kumkabidhi flash hiyo. .

Waliagana na Christina akaondoka na kurudi zake ofisini, kila alippita watu waliishangaa gari yake wapo waliomsimamisha ili wapige picha na gari hiyo. Alifika Ofisini na moja kwa moja mpaka katika ofisi yake na kuwasha computer, alichomeka ile flash ili ajue ndani kuna nini. Macho yalimtoka baada kuona taarifa zote za Alex na mwenzake, alitabasamu kidogo na kujisemea "leo ndio leo asemae kesho muongo". Aliichomoa flash na kuivunja, "bosi ulikuwa wapi siku hizi mbili" aliingia Joe na kuuliza swali. "nilikuwa undercover kidogo, kulikuwa na kazi na fanya" Christina alijibu na jibu hilo lilionekana kumridhisha Joe ambae baada maongezi hayo alimkabidhi mafaili mawili kisha yeye akatoka. Christina aliayafungua mafaili hayo na kuyasoma baada hapo aliyafunga na kuyaweka katika droo. Alikaa ofisini akiisbiri jioni ifike kwa hamu ili aingie kazini, wakati yeye anawaza hivyo Shadow na vijana wake pia walikuwa wamepanga usiku huo wakamavamie Alex kwa sababu walishapajua anapokaa.
******************************
Alex alikuwa ametulia ukumbini lakini moyo wake ulikuwa hauna amani kabisa, mwisho aliamua kuinuka na kuelekea chumbani alipokuwa akilala Allen. Alianza kukagua kagua vitu mbali mbali mpaka alipofika kwenye kabati la nguo. Alilifungua na kukuta kijikaratasi chenye ujumbe "ukishaanza kazi nyumba hii haitokufaa tena, utabidi uondoke lakini kwenye kabati hili nyuma kuna mlango wa siri. Na kuna usafiri maalum utakaokupeleka mpaka katika nyumba yangu nyingine hapa hapa New York...Allen James" Alex alitabasamu na kurudi sebleni. Wakati anafika alioma vivuli kwa nje vikitembea tembea, bila kusita alielekea jikoni ambako Rose alikuwa anaandaa chakula cha usiku. "tumevamiwa" Alex alimnong'oneza masikioni na taratibu wote wawili wakatoka jikoni na kuelekea chumba cha silaha. Kila mmoja alichukua dhana zake za kazi na kukaa tayari kwa yoyote atakae imgia, Rose alipanda sehemu ya juu kabisa ya jumba hilo na kujibanza pahali akiwa na sniper.Alex alijibana ukutani na kusikilizia, ghafla kilipasuka na kitu kama chuma kikasikika kikilia wakati kina gusa ardhi na kuanza kutoa moshi mzito. Mlango ulivunjwa na vijana wa Shadow wakaanza kuingia kwa fujo, masikini watatu wa mwanzo wote walianguka chuni wakiwa na matundu ya risasi kichwani. "haka kamchezo katakuwa kazuri kweli leo" Rose alijisemea baada ya kuwachapa watati wa mwanzo. Alex alichomoka alipojibanza kwa kasi ya hali ya juu huku mkononi akiwa na bastola ndogo mbili, alianza kufyatua risasi bila mpango ili ajipe mwanya wa kuingia sehemu nyingine. Vijana wa Shadow walijibanza mpaka Alex alipoacha kupiga risasi. Ndipo walipojitkeza na kuanza kujibu mashambulizi, walilimimina risasi lakini walishangaa sana maana wao ndio waliokuwa wakishambulia lakini wao ndio waliokuwa wananguka chini wakivuja damu. "kuna mtu mwengine amejificha humu na anatumia sniper" Aliongea mmoja wao na wote wakarudi kujibanza ukutani. Mwengine alitoa bomu dogo na kulirusha upande ambao waliamini ndipo alipokuwa amejificha huyo anaeshambulia, bomu hilo lilitua pembeni kidogo na alipokuwa Rose lakini aliwahi kuondoka kabla halijalipuka.
Wakati mpambano ndani ya nyumba hiyo kubwa ukindelea Agent Darling ndio alikuwa anafika, lakini alishangaa baada kuona moto ukirindima ndani ya jengo hilo. "mshenzi gani huyo anaeingilia kitoweo changu" Alijiesemea huku akiuma meno kwa hasira, "Alex atakufa kwa mikono yangu tu" alijisemea kwa mara nyingine na kutchukua bastola yake kisha kshika gari na kuelekea katika jengo hilo. "Juliet uko sawa" Alex aliongea baada kusikia mlio wa bomu, "ndio usijali kuhusu mimi" Rose alijibu. Agent Darling alipitia dirishani na kuanza kushambulia, Alex alipoona hivyo alijitokeza na kuendelea na mashambulizi. Na risasi zilipomuishia alianza kutumia kisu chake, hapo ndio walipoisoma namba. Alex alikuwa mtaalum sana hasa katika kombat ya kujihami mwenyewe, kila aliekutana nae alikwenda chini akiwa na alama kisu mwilini mwake. Ghafla wakati anaendea na mpambano aligongana mgogo na mtu mwengine na alipogeuka ni ana kwa ana na Agent Darling. "nimefutahi kukuona tena Allen Jr" Alex aliongea na kurusha kisu kilichokwenda moja kwa moja mpaka katika paji la uso la kijana mmoja wa Shadow. "mshenzi we tukiwamaliza hawa, nakuungia na wewe" Agent Darling aliongea huku akiendeleza mshambulizi. Kila mmoja aliendelea kupambana na wengine kwanza, "Juliet elekea chumbani kwa Allen nikukute huko"Alex aliongea na Rose akaitika na kuelekea huko. Vijana wa shadow walipoona hali imezidi kuwa mbaya waliamua kuchapa ndala, na wakati huo Alex alikimbilia chumbani kwa Allen ambalo alimkuta Rose na bila kuchelewa alielekea kwenye kabati na kulifungua kisha akampa ishara amfate, waliingia na kulifunga kwa ndani kisha akafungua mlango wa siri wa kabati hilo na na kuingia, Kumbe io ilikuwa ni lifti na ghafla ilianza kushuka kwa kasi kuelekea chini. Ilisimama na kufunguka, walitoka na kuelekea katika kitu kama treni lakini ilikuwa ndogo. Waliingia ndani ya chombo hicho na safari ikaanza. Agent Darling baada kuwaaliza wale walioshindwa kutoroka alianza kumtafuta Alex bila mafanikio. Wakati anaendelea na zoezi hilo ghafla simu ya mezani ikaita, aliipokea "asante kwa msaada wako, lakini nasikitika kuwa ungwe yetu mimi na wewe bado muda. Ukifika muda wa kuonyeshana usije ukaniangusha na nimependa ushujaa wako" Alex aliongea upande wa pili na bila kusikiliza kitu alikata simu na kuivunja kabisa huku akitabasamu. "nataka uone sababu ya yote hayo" alijisemea moyoni na kumkubatia Rose ambae alikuwa ameumia kidogo..
 
83.
Treni hio ilisimama na mlango ukafunguka, Alex alimbeba Rose na kushuka. Mbele yake kulikuwa na mlango, alitebea mpaka katika malango huo na kuufungua. Alishangaa kuona nyumba ile ilivyokuwa imefanana na ile waliokuwepo manzo kila. Kutokana na ufanano huo hakupata shiada kujua maabara iko wapi. Alielekea katika Maabara na kumlaza Rose kisha akachukua vifaa na kuanza kumchunuza, baada kumpatai huduma ya kwanza alimuacha apumzike yeye akatoka na kuelekea katika chumba kimoja ambacho aliamini ndio kama chumba alichokiacha kule alipotoka. Aliingia na kuelekea chooni na kujimwagia maji, alipomaliza alielekea jikoni na kujiandalia chakula. Alipomaliza alipata maakuli kisha akaelekea maabara kumuangalia Rose ambae alikuwa amelala hajitambui. Alikaa pembeni ya kitanda hicho na kujipumzisha. kutokana na uchovu na kuchoka sana usingizi ulimchukua gubigubi. Alikuja kushtuka baada kuhis kama akiguswa na mtu, alipofumbua macho alikutana natabasamu zuri usoni mwa rose. Lakini alishangaa kumuona akiwa ameshabadilisha nguo, hata hivyo alipojaribu kumuongelesha hakumjibu kitu badala yake alikuwa akitabasamu tu ila ghafla alianza kutoka damu nyingi mdomoni. Alex alikurupuka kutoka usingizini huku akihema kama mtu aliekuwa akifukuzwa. Alimuangalia Rose ambae alikuwa bado amelala hajitambui, alianza kuziangalia mashine ambazo zilikuwa zikifuatilia maendeleo yake lakini aligundua mapigo ya moyo yalikuwa yanasomwa katika kiwango cha chini kabisa. Hofu ilianza kumtanda, alitoka maabara na kuelekea gereji. Alitoa gari na kuipeleka mbele ya nyumba, alirudi ndani na kumbeba na kumpeleka kwenye gari kisha safari ya hospitali ikaanza. Aliendesha mwendo wa kiasi mpaka akiafika, alishuka na ufungua mlango wa nyuma. alimbeba na kukimbia nae ndani ya hosipitali. Wahudumu walipomuona walichukua kitanda cha matairi na kumfata. Alex alimlaza kwenye kitanda na hapo alikimbizwa katika chumba cha matibabu ya dharura, na baada kufanyiwa uchunguzi wa awali ikagundulika kuwa yupo katika hali mbaya. Hivyo dakatari mkuu anaemsimamia alitoa amri ahamishiwe chumba cha wagonjwa mahututi na ikafanywa hivo. "kijana nakuomba utulie utuache tufanye kazi yetu" Daktari huyo aliongea na kuzama katika chumba hicho cha wagonjwa mahututi.


Agent Darling alipiga simu kituo cha polisi cha karibu na nyumba aliokuwa anakaa Alex, dakika tano baadae kilifika kikosi cha askari kikiambatana na gari la zima moto pamoja na gari ya kubebea wagonjwa. Alitoa maelezo yote hayo lakini hakuomtaja Alex. Baada ya hapo aliacha polisi wafanye kazi yao, yeye akarudi kwenye gari yake na kuondoka. Kwa sabau ulikuwa ni usiku alirudi nyumbani kwake na kupumzika lakini mawazo yake yote yalikuwa ni kutaka kuua wale waliomvamia Alex walikuwa wanahusika nae vipi. usiingizi ulimchukua bila hata kutegemea, alikuja kushtuka asubuhi baada ya saa yake kupiga kelele. Alipoangalia aligundua kuwa siku hiyo amechelewa kuamka, alikurupuka kiatanani na kuingia chooni. Alioga haraka na kutoka, alivaa nguo za kazi na kutoka bila hata kunywa chai. Aliingia kwenye gari na kuondoka, siku hiyo kamera za barabarani zilipiga picha za kutosha za gari hio kutokana na mwendo kasi. Alifika ofisini na kukuta wenzake wote wakimshangaa, "hebu acheni kunitolea mimacho" aliongea na kuingia katika ofisi yake.

*************************************
Daktari alotoka katika chumba hicho huku akionekana ni mwenye huruma "nambie mpenzi wangu anaendeleaje" alijikuta akimuita hivo wakati anauliza. "kijana nakuomba utulie kwanza kisha ndio nikueleze" Daktari aliongea huku akimuweka kitako Alex ambae aliokana kama kuchanganyikiwa. "pole kwanza kwa kilichowakuta, na kwa upande wa mgonjwa sisi tumejitahidi kadri ya uwezo wetu lakini uwezo wake wa kuishi ni mdogo sana". "unasemaje" Alex alipanik kusikia hivo, "tulia sasa, kwa nje anaonekana hakuumia sana lakini ameumia sana ndani, tumetoa vipande sita vidogo vidogo vya vyuma. Vilikuwa vimeganda katia moyo wake na kupelekea moyo kuoteza nguvu ya kusukuma damu hivo kupeleka sehemu nyingi katika mwili wake kukosa damu ya kutosha. Hiyo imepelekea kupata tatizo la ubongo na pia kibaya zaidi utapoteza watu wawili, tumemkuta na uja uzito siku chache. Mpaka sasa kiumbe kilichokuwepo tumboni mwake kimeshakufa. Na tunahitaji kauli yako ili tuziondoe mashine zinazomuweka hai, hakuna uwezekano wa kupona kutokana na kua karibu nusu na robo ya seli zake za ubongo zimeshakufa. Usifanye maamuzi ya haraka, fikiria kwa umakini mkubwa hili swala kwa sabau ni swala la kifo na uhai" Daktari alimaliza kuongea na kumpa pole Alex kisha akainuka na kuondoka. Machozi yalianza kumtoka japo alijitahidi kuyazuia, "kwa nini mimi kila siku" alijisemea moyoni. .
Aliinuka na kuelekea katika chumba alichwekwa Rose na kuomba kumuona, manesi walimruhusu na kuingia. Alikwenda pembeni na kumuangalia mwanamke huyo ambae alionekana kupauka, alikaa pembeni na kuanza kuongea "hivi hata wewe unaondoka unaniacha peke yangu, kwanini lakini wote mumeamua kuondoka mapema kiasi hichi. Basi ungesubiri japo nikupe zawadi yako" Alex alizidi kulalamika, wakati anendelea kuongea alihisi kama mkono ukimgusa. Aliinua macho na kumuangalia Rose ambae alionekana kutabasamu. Akampa ishara amuondole kifaa kilichokuwa mdomo ili aongee na Alex alifanya hivo "mbona bado sijafa, unaweza kunipa hata saa hivi hiyo zawadi yangu" Rose aliongea japo kwa shida kidogo, Alex alitabasamu huku akitokwa na machozi kisha akamuonyesha ishara kuwa amsubiri anakuja. Alimrudishia kile kifaa cha kupumulia na kutoka kisha yeye akatoka na kuomba kuonana na daktari. Alielekezwa ofisi kwa daktari na kuongea nae,baada dakika tano alitoka na kutoka kabisa hospitali hapo. Nusu saa baadae alirudi na boxi kubwa na kuwakabidhi manesi, na kwa sababu walikuwa washaambiwa na mkuu wao jambo litakalo kwenda kufanyika. waliingia katika chumba alichokuwa amelazwa Rose na kufanya kama walivyoelekezwa. Alex aliekezwa katika chumba kingine na kubadilisha nguo. Alivaa suti moja safi sana na kutoka "maandalizi yamekamilika" Daktari aliongea, na kuongoza njia mpaka katika chumba alichokuwa Rose. Waliingia ndani na kumkuta padri akiwa tayari ameshafika. "karibu kijana" aliongea mzee huyo, "asante" Alex alijibu kukaa pembeni ya Rose. "unajua kama unachotaka kukifaya ni kitu kikubwa sana" aliongea tena mzee huyo. "naelewa" Alex alijibu, taratibu zilifanyika na muda wa ndoa ukafika. "bwana Alex Jr Jason umekubali kumchukua bi Rose kuwa mke wako halali wa ndoa kuanzia leo hadi mwisho wa uhai wako", "nimekubali" Alex alijibu bila kusita. "bi Rose umekubali kumchukuwa bwana Alex kuwa mume wako halali wa ndoa kuanzia leo hadi mwisho wa maisha yako", "nimekubali" Rose alijibu. Basi Padri aliwatangaza wawili hao kuwa mume na mke rasmi kuanzia muda huo. Wote waliokuwa wakishuhudia tikio hilo walikuwa wakitokwa na machozi kwa sababu walielewa kuwa mwanamke huyo asingeweza kutoboa hata masaa matatu yajayo. "Rose hii ndio zawadi yako" Alex alijibu na kumkumbatia" walipigwa pica kadhaa kama kumbukumbu za tukio hilo.
Baada hapo Alex aliwaomba wote watoke ili abaki na mke wake, na wote wakatoka. Baada nusu saa Alex alitoka huku analia na kumwambia daktari kuwa tayari. Gakatari alielewa nini amemaanisha na kumsogolea Alex ambae alikuwa anashindwa kuyazuia machozi "pole kwa kumpoteza mtu unaempeda" aliongea huku akimpiga piga begani. Maiti ya Rose ilitolewa na kuplekwa kwa ajili ya maandalizi ya safari ya mwisho. Baada hapo taratibu za mazishi zilifanyika na waliohudhuria wengi walikuwa ni miongoni mwa wale wauguzi wa hospitali, baada ya kuzika watu wote walioondoka kasoro Alex alibakia pale pale na mvua ilianza kunyesha lakini wala hakujali hilo. "nisalimie Allen huko unakokwenda na usijali ombi nitalishughulikia kama ulivosema na nakuhakikishia hatobaki mtu hata kama itabidi nipambane na duni nzima nitafanya hivo" Aliongea kisha akondoka eneo hilo la makaburi na kurudi nyumbani kwake, nyumba hiyo aliiona kubwa sana.
*************************************
"Alex niahidi kuwa kifo changu hakitokwenda bila kulipwa", "nakuahid na wala usijali wote waliohusika na kifo chako na cha Allen watalipa kwa maisha yao, hatobakia hata mmoja". "nafurahi kusikia hivo" Rose aliongea huku akianza kukosa pumzi, "vipi unaumia" Alex aliuliza huku akimsogeza karibu, "hapana siumii kabisa, nitaumiaje wakati naondoka katika mikono ya mwanaume nnaempemda" Rose alijibu huku akimuangalia Alex usoni. Kadri muda ulivyokwenda ndivo hali yake ilivyozidi kuwa mbaya. "Alex muda wangu umefika" Rose aliongea huku akimgusa Alex usoni kwa mikono yake ambayo ilikuwa ishapoa tayari na haikupita hat sekunde tano ilianguka na hapo alitoa pumzi ya mwisho na kuaga dunia. Alex alilia kwa nguvu mpaka waliokuwepo nje ya chumba hicho walisikia na wao wakakijukuta wakitokwa na machozi lakini wangefanyaje na kazi ya Mungu haina makosa.
"umetumwa na nani" Agent Darling alikomaa na swali hilo, "unadhani nitakwambia" alijibu kijana mmoja miongoni mwa vijana wa Shadow alikamtwa wakati wakijaribu kutoroka. "narudia kwa mara ya mwisho, ni nani aliekutuma" alifoka sasa, "kama nilivokwambia mwanzo, huwezi kuoata chochite kutoka kwangu ni bora uniue tu" aliibu kijana huyo. Ilibidi kwanza Agent Darling atoke katika chumba hicho maalum cha mahojiano. "huyu jamaa amepewa mafunzo ya kuhimili maumivu ya aina yoyote ile" aliongea Agent Darling huku akiwa amekunja sura. "kuna taarifa zozote kuhusu Alex" alimuuliza Joe ambae alikuwa akindela kutafuta kitu atika computer yake. "hapana mkuu sijapata chochote mpaka sasa" Alijibu Joe, "dah ni wiki nzima sasa huyu kiumbe hajapnekana atakuwa amejificha wapi" alijisemea Agent Darling. .
 
84.
Upande wa pili kulikuwa kuna kikao cha siri kinaendelea "usijali mkuu yule kijana hatosema chochote kwa sababu katiba yao inasema hatoweza kutaja jina la alie muajiri katika mazingira yoyote yale" Aliongea Jafar kumpoza Helen ambae alionekana kuchanganyikiwa. "sawa, lakini huyu Agent Darling ni tatizo kwa kweli" aliendelea kuongea "hasa akija akigundua kuwa babaake hakuuliwa na Alex yaani hapo ndio patakuwa hapatoshi". "na haitotokea siku akajua" alijibu Hansen ambae amerudi muda si mrefu kutoka mishen ya siri nchini Somalia, "una uhakika gani" aliuliza Martin. "ni kwa sababu wakati atakaopambana na Alex atakuwa anapambana kihisia zaidi na hatokuwa tayari kusikiliza chochote kutoka kwa hasimu wake huyo" alifafanua Hansen. "basi sawa lakini hakikisheni wote wawili wanakufa" aliongea Helen na kufunga kikao. Kila mmoja aliyawanyika na urudi anapofanya kazi zake.
"eti nini" alifoka Shadow baada vijana wake wa taarifa kumfikishia taarifa kuwa hawajapata taarifa yoyote juu ya Alex. "mnajua amewauwa ndugu zetu wangapi" aliuliza na kukunja ndita usoni, "tunafahamu mkuu lakini tumesachi kila kona ya nchi hatujapata chochote" alijibu mmoja wao. "sawa na vipi kuhusu yule mwenzetu aliekamatwa" alihoji kijana mwengine, "nimeongea na mtu mmoja kati ya wale waliotupa kazi hii na amesema kuwa kesho atakuwa anapelekwa jela na hapo ndio utakuwa muda wetu wa kwenda kumuokoa" alijibu Shadow. "sawa mkuu" walijibu kwa pamoja na kutawanyika, "Alex hivi umejificha wapi mtoto wa mama" Shadow alijiemea moyoni na kukunja ngumi.
Siku ya pili mapema asubuhi kijana wa Shadowa alikuwa anapelekwa gerezani baada kukataa kabisa kutoa ushirikiano. Alisindikizwa na gari sita za kikosi maalum, tatu zikiwa mbele na tatu zikiwa nyuma. Safari hiyo ilianza bila kujua kuwa Vijana wengine wa Shadow walikuwa wanaifatilia kwa nyuma, na kwa sababu gereza hilo lilikuwa nje mji kidogo waliusubiri msafara huo utoke nje ya mji ndio waanze mashambulizi. Lakini kabla hawajafanya chochote walipitwa na gari ndogo aina ya ferarri nyeusi kwa kasi kubwa sana. Haikuishia hapo tu iliupita mpak msafara huo na kutokomea mbele, baada mwendo wa sejunde kumi msafara ulisimama ghafla kutokana na njia kublokiwa na mti ulioanguka.

Polisi walishuka kwa ajili ya kwenda kuondoa, walikuwa sita ghafla wote walianguka chini huku wakitoka damu shingoni baada visu vidogo kupenya. Mnyama Alex Jr alichomoka kuotoka kwenye kichaka na kuivamia gari ya mbele kabisa na kumuua dereva wake, aliendeleza mashambulizi hayo ya kinyama. Maana alikuwa hachagui ukipita mbele yake umekwisa, baada dakika tano kikosi kizima kilichokuwa kinamsindikiza kijana huyo kilikuwa chini. Alex alikwenda nyuma na kufungua gari hilo la wafungwa na kumshusha kijana huyo. Na hapo ndio vijana wa shadow walipojitokeza lakini walichokutana nacho wanajuwa wenyewe. Alex hakuwa yule wa kawaida, alikuwa amebadilika kabisa. Roho ya kikatili ndio iliotawala mwili wake hivyo alikuwa akiua tu bila kujali kabisa. Vijana wa Shadow walipoona moto umezidi kuwa mkali, walikimbia bila mafanikio yoyote yale ya kumuokoa mwenzao. Alex alimgonga kijana huyo shingoni na kumfanya amepoteze fahamu kabisa. Alimuingiza kwenye gari na kuondoka nae
Taarifa za msafara kuvamiwa zilimfikia Agent Darling na kitengo kizima, bila kuchelewa walitoka na kuelekea eneo la tukio. "haya mauaji ni ya kikatili sana" aliongea mtu mmoja baada kumuangalia polisi mmoja ambae alitobolwa macho yote mawili. "mh huyu aliefanya mauaji haya ni katili kupita maelezo"aliongea mwengine, "huyu aliefanya mauaji haya ni simba mwenye jeraha" Agent Darling aliongea huku akizichunguza maiti hizo, "nadhani namfahamu aliefanya mauai haya" Joe aliongea baada kukagua mwili mmoja, "huyu ni Alex" alijibu hivo na kuwafanya wote wageuke na kumuangalia. "umejuaje" aliuliza mtu mmoja, "kila mtu huwa anaacha alama za mauaji yake na Alex huwa anafanya mauaji ya aina hii" aliongea hivo na kuonnyesha maiti moja, "maiti zote hizi zina matundu ya risasi zilizopita mbele na kutokea nyuma, Alex hakushambulii akiwa nyuma yako bali anakuuwa wakati unamuona kabisa" alindelea kufafanua.
"kijana kiupole kabisa nambie ni wapi kwenye kambi yenu" Alex aliongea kiunyonge kabisa, "halafu nyinyi wote hamnielewi nimekwambia huwezi ambulia kitu kutoka kwangu" Alijibu kijana huyo kwa jeuri. "mara ya mwisho nambie kikundi chenu kipo wapi" Alex aliongea tena lakani wakati huu sauti yake ilikuwa na mikwaruzo. "mtu mzima hatishiwi nyau" aliongea kijana huyo na kucheka kwa dharau, "huwa ninapotaka kujua kitu basi huwa nakijua kwa gharama yoyote ile" Alex aliongea na kuinuka alipokuwa amekaa. Alimsogelea kijana huyo na kumuangalia usoni, kwa kweli alikuwa anatisha sana. Macho yake yalikuwa mekundu kama mtu aliekuwa amevuta bangi, alitoa kifaa kidogo kama kiwembe cha kukatia kucha. Alimshka mkono kwa nguvu na kumuuliza "utasema ama hutosema", "sise...." hajamalizia alipiga kelele baada Alex kumgoa kucha ya kidole gumba. "utasema au husemi", "sise.." hakumaliza tena akagolewa kucha ya kidole kingine. "unajua kama itabdi nikchune ngozi ndio nipate nnachokitaka nitafanya hivo" Alex aliongea kwa upole. "fanya unavotaka" Alijibu kijana huyo huku akilia kutokana na maumivu anayoyapata. Alex aliondoka na kurudi akiwa na pochi ndogo yenye vifaa kadhaa. Alibeba koleo na kumsogelea "we nambie tu wala sitakuuwa" Alex alimbembeleza, "nimesema hupati kitu kutoka kwangu" alijbu kijana huyo. Alex alimshika mdomo na kuufungua kwa nguvu kisha akakamata jino moja la chini kwa koleo na kuling'oa..
Masikini kijana wa watu alipiga kelele za maumivu lakini ilikuwa ni kama kumpigia mbuzi gita maana Alex wala hakushtuka kabisa na kelele hizo, alikamata jino la pili kwa koleo na kuling'oa. Kijana huyo alizidi kupiga kelele mpaka akapoteza fahamu. Alex aliinuka na kwenda kuchukua ndo ya maji ya baridi, alimwagia na kijana huyo akazinduka, "sema tu maana ndio wanza nimeanza" Alex aliongea huku akitoa kisu kidogo cha kukatia ngozi na nyama wakati wa opereshen. Yule kijana alicheka "sisemi" alijibu. "basi sawa" Alex aliongea na kumsogelea kisha akamshika mkono na kupitisha kisu, taratibu alianza kumchuna ngozi. Maumivu alioyapata hayakuelezeka "ntasema basi usiendelee nitasema" aliongea kijana huyo kwa nguvu baada kuzidiwa na maumivu. "mambo si hayo sasa, kama ungekubali mapema labda saa hivi tungekuwa mezani tunapata chakula" aliongea Alex na kuacha kumchuna ngozi. Yule kijana alianza kuongea kila bila hata kuficha chochote mpaka mwisho "nakuomba uniue tu" aliongea hivo baada kumaliza kuongea. "bado kufa muda wako ukifika utakufa tu" Alex alimjibu na kutoka katika chumba hicho. Alielekea chumba cha silha na kubeba za kutosha, alirudi kule alipomfunga yule kijana na kumfungua. Alimuingiza kwenye gari na safari ikaanza, kwa vile ulikuwa ni usiku hakukuwa na shida polisi.
"oya sio Jimmy yule" mmoja kati ya vijana walikuwa doria aliuliza, "ndio mwenyewe yule" mwenzake alimjibu. Lakini alikuwa akiwafanyia ishara wasimsogelee, masikini wee walishindwa kumuelewa na walipomfikia aliripuka na kufa nao wote wawili. "Rules have change (sheria zimebadilika)" aliongea na Alex na kuzama kambini, alianza kuuwasha moto sio wa kitoto "mkuu Alex ametufuata huku huku" aliingia kijana mmoja na kutoa taarifa "anaonekana kama mtu aliechanganyikwa kabisa. Shadow aliinuka na kutoa bastola yake kisha akatoka nje, macho yalimtoka baada kukutana na maiti za vijana wake zikiwa zimatapakaa kila kona. Wakati akiwa katika mshangao huo alishtuliwa na kelele za kijana wake aliesimama pembeni yake baada kucheze risasi kadhaa za kifua. Na alipotoka kushambulia alicheze risasi ya mkono na kuingusha bastola chini. "kama ungekuwa hujanifata kwangu, yasingekufika haya lakini kwa sababu ya pesa na tamaa zako umeuvamia moto wa volacano" Aliongea alex huku akipandisha ngazi kueleke alipokuwa Shadow. "wewe hukujiuliza kwanini serekali imekupa kazi hii wakati yenyewe ina vikosi vingi tu vya kupambana na mimi" Alex aliongea tena kwa hasira kisha akaendelea "sasa subiri nikuonyeshe kwanini serekali yenyewe imeshindwa kunitia mikononi".
Alex alikuwa amezama katika dibwi la kisasi, hakusikiliza chochote alimvaa Shadow kama mbogo na kuanza kumchakaza. Japo Shadow alikuwa ni mpambanaji mzuri lakini alijikuta katika wakati mgumu sana maana kila alipojaribu kujitetea alishindwa. Alex aliendelea kumpa kichapo mpaka Shadow akalegea kabisa, "muda wako wa kuga bado, kwanza huwezi kufa kirahisi rahisi hivo. Umemuona huyu kwenye hii picha ni mke wangu na wewe ndio sababu ya kumpoteza pamoja na mwanangu aliekuwa tumboni kwake" Alex aliongea huku akimuonyesha picha ya Rose katika siku zake za mwisho. Shadow alikuwa ametulia kama maji mtungini maana alielewa hasira ya Alex haijaisha bado maana macho yake tu yalitosha kuongea. Alex alianza kumburuza Shadow mpaka nje na kumuingiza kwenye gari, kisha alimgonga shingoni na kumfanya alale fofofo. Alirudi ndani ya kambi hiyo na uanza kutega mabomu na kutoka aliondoa kwa gari kwa mwendo kasi sana na baada ya dakika tano kambi nzima iliripuka na kuteketea kabisa. Siku ya pili taarifa ya kuripuliwa kambi maarufu ya majambazi sugu ilienea kama moto wa gesi huku watu wakionekana kufurahishwa na tukio hilo.
Helicopter ya binafsi ilitua juu kabisa ya jengo hilo la kitengo maalum cha upelelezi, General David alitoka na kuelekea mlangoni ambapo watu wengi walikuwa wakimsubiri. "karibu mkuu" Helen aliongea "asante, kila kitu kipo tayari?" alishukuru na kuuliza, "vijana wote na wawakilishi pamoja na wakuu wa nchi mbali mbali wameshafika" Helen alijibu huku akiongoza njia kuelekea katika chumba maalum ambacho ndipo mkutano huo wa siri ulipokuwa unafanyika.
 
85.
Watu wote waliokuwemo katika chumba hicho walisimama baada ya General David kuingia, aliwaangalia wote na kutabasamu isha akanyoosha mkono juu kama ishara ya kutoa salamu. Wote waliinamisha vichwa chini na kujibu salamu hio kwa kukunja ngumi ya mkono wa kulia na kuweka kwenye moyo pande wa kushoto. "Yatukuke mapinduzi" kwa pamoja bila kupishana walisema. General David alitikisha kichwa na kuelekea kwenye kiti chake na kufubgua kikao rasmi. "mkuu kambi zote zipo tayari na tunasubiria amri yako tu" aliongea mtu mmoja mwenye lafudhi ya kichina, "vizuri sana" General David aliitika kwa kutabasamu. "kwa jumla tuna kambi Mia moja za baharini, sabiini za jangwani na hamsini za mwituni na kila kambi ina wanajeshi Mia moja ambao kwa ujumla wao tuna wanajeshi maalum wa CODE X elfu ishirini na mbili" aliendelea kufafanua mtu huyo. Wote walipiga makofi kuashiria wamefurahishwa na idadi ya wanajeshi hao wenye uwezo mara dufu kuliko wanajeshi wa kawaida. "idadi hiyo inatosha kufanya mapinduzi, maana ikiwa mwanajeshi mmoja anauwezo wa kupambana na makomando watano peke yake, jee hao wote inakuaje" aliongea mtu mwengine na wote wakacheka. Wakati kikao kinaendelea ndani Agent Darling ndie alikabidhiwa jukumu la kuimarisha ulinzi maana tokea Alex ajitokeze kwa sura mpya watu wote waliiniwa na wasiwasi na kupelekea hata ulinzi kuimarishwa katika eneo hilo. "vipi hujahisi kitu chochote kisicho kawaida" Agent Darling alimuuliza mmoja kati ya watunguaji (sniper) kupitia kifaa cha mawasiliano. "negative" alijibu sniper huyo.

Agent Darling alienedelea kuwauluza wote waliokuwa wamejificha katika majengo hayo wakiwa wamejiandaa vya kutosha. "habari yako Allen Jr" alishtuka aliposikia sauti hiyo maana aliitabua kama ilikuwa ni ya Alex, "we mshenzi uko wapi" alifoka kwa hasira Agent Darling.
.
"ah mbona hivo sasa, mimi ninachokitaka ni uondoe vijana wako hao watunguaji kabla sijaanza kuwapeleka kuzimu mmoja baada ya mwengine kwa sababu sina uhasama nao" Alex aliongea na suati yake ilitosha kumueleza Aent Darling kuwa alikuwa hatanii hata kidogo. "kama kweli wewe mwanume uanejiamini jitokeze" Agent Darling alimjaribu, "yaani leo usijali, tutacheza mpaka utachoka lakini sitaki mtu asie na hatia afe kwa kumlinda mkosaji" alijibu Alex taratibu na kumfanya Agent Darling aingiwe na wasiwasi. "vikosi vyote kaeni tayari" alitoa amri hiyo na vikosi vyote vikajipanga, "naona umeamua kuwatoa kafara binaadamu wenzako" Alex aliongea na kukata mawasiliano na ghafla ikasikika milio sita ya bastola, Agent Darling alijaribu kuwasiliana na watunguaji wake lakini wapi alikuwa hajibiwi kitu na hiyo ilitosa kumueleza kuwa tayari walishaaga dunia. Kwa mbali aliona gari nyeusi ikija upande wake, "shambulieni hiyo gari" alito amri na bila kusita wanajeshi wakaanza kushambulia lakini gari hiyo ilikuwa ni bullet proof hivyo hakupenya hata risasi moja. Agent Darling aliingia ndani na kutoa taarifa kuwa Alex ameshafika, ile gari ilipofika karibu na wanajeshi iliripuka na wengi walijeruhiwa.Hapo ndio Alex akajitokeza akiwa katika mavazi yake ya kikomando, alianza mashambulizi ya kasi huku kila aliepita mbele yake alikwenda na maji. Alex Jr aliendelea na kazi yake ya mauaji bila kujali kuwa aliokuwa anapambana nao walikuwa wakitekeleza majukumu yao tu. "mkuu kuna tatizo unatakiwa kuondoka" Aliingia mlinzi wa General David na kutoa taarifa "tatizo gani wewe huoni kama tupo kati kati ya kikao" alifoka General David. "mkuu niamini nusu na robo ya vikosi vinavyohakikisha usalama vimeshateketea katika mikono ya Alex. Alipolitaja jina hilo tu ukumbu mzima ulizuka na tafrani. "nini, Helen nieleze kwa kina" aliongea General David, "nu...ku...ku..eleze nini mkuu, wakati hali ndio ushaiona hivi" Helen aliongea kwa kigugumizi cha ghafla. Wakati wakiendelea na majibizano Alex tayari alikuwa kashaingia mjengoni tena bila hata kuguswa huko nje, alianza kuwachakaza waliokuwemo ndani sasa. Yaani Alex alikuwa kavurugwa kisawasawa maana alikuwa akitowa dozi bila kipimo maalum.
"Finally, tumekutana uso uso kwa uso tena" Aliongea Agent Darling baada kuonana ana kwa ana na Alex, "nenda nyumbani ukanyonye leo ni siku mbaya sana" Alex aliogea huku akivua miwani yake nyeusi iliokuwa umeficha macho mekundu mithili ya mtu alievuta bangi. "hahaha...eti nini" Agent Darling aliongea kwa kejeli, "nasema nenda nyumbani ukanywe maziwa, siku ya leo hutakaa uisahau maishani mwako hivyo ni bora tu ufanye nnavyo kwambia" Alex alifoka sasa alipoona hawaelewani. "itabidi unipeleke" Agent Darling aliongea na kwa kasi ya ajabu alifyetuka alipokuwa na kumvaa Alex. Bila mategemeo alirudishwa alipotoka baada kutandikwa ngumi nzito ya kifua iliomfanya akohoe kidogo. "hivi wewe hunielewi nnapo kwambi siku ya leo ni mbaya sana" Alex alifoka tena na safari hii hakusimama alimfata kwa nguvu na kumtandika makonde sita ya nguvu ya kifua na uso mpaka Agent Darling akaanguka na kupoteza fahamu. "vizuri, watoto wazuri huwa wanalala mapema ili kuepuka kuingizwa katika ugomvi wa wazazi wao" Alex aliongea na kuondoka eneo hilo, aliingia kwenye lifti na kuelekea ghorofa ya juu kabisa ambapo ndio kikao kilikuwa kinafanyika. General David alionekana kuwa mbishi kuondoka, "mkuu huyu mtu si wa kawaida hebu angalia anavyopiga tena hatumii hata bastola lakini ngumu yake moja tu inatosha kuwa risasi tena ya Shotgun" alizidi kuongea mlinzi wake, "sasa nitamkimbia mpaka lini" General David aliongea. "mkuu tufanye leo humkimbii bali unakwenda kujipanga upya ili kukabiliana nae" alisisitiza mlizi. Helen na baadhi ya viongozi na wawakilishi wengine walitoka wakiwa na bastola mkononi. "shoot on site" Helen alitoa maelekezohayo akimaanisha kuwa yoyote atakae muona Alex amuue. "sawa" wote walijibu na kujibanza wakisubiri lifti ifunguke lakini ilipofunguka kulikuwa hakuna mtu ndani. "habari yako Helen, umenimiss eeh" Helen alisikia sauti hiyo ikitokea nyuma yake na alipogeuka alikutana na mdomo wa bastola ndogo na bila kuchelewa Alex aliyetua risasi na kumwaga ubongo. Wale wengine wote walivyoona vile walianza kupoteana huku kila mmoja akitafua njia ya kutorokea. Alex wala hakuwajali kwa sababu yeye aliekuwa anamtaka ni General David, aliingia katika chumba cha mikutano lakini kwa mbali aliona mlango ukifungwa hakufikiria mara mbili alianza kukimbia kuelekea ulipo mlango huo.
 
86.
General David na mlinzi wake walikuwa wanakaribia juu, "washa helicopter" mlinzi aliongea kupitia radio call. Walifika juu huku mlinzi akiwa nyuma akiimarisha ulinzi, lakini hatua chache kabla ya kufika kwenye helicopter mlinzi alianguka chini na kupoteza maisha baada kupigwa risasi ya kifua. "simama na geuka taratibu" Alex aliongea na General David alisimama na kuanza kugeuka huku akichomoa bastola yake, lakini kabla hajashambulia alipigwa risasi ya mkono na kuingusha bastola. "Alex, Alex, Alex kwanini tusikae kitako tukayamaliza" General David aliongea huku akiugulia maumivu mkononi, "hivi wewe kitu gani ulikikosa mpaka ukaamua kuingamiza familia yangu" Alex aliuliza kwa hasira. "unajua Alex sisi ni binaadamu na kila binaadamu huwa amepangiwa siku zake za kuishi duniani, hivyo basi iliandikwa na Mungu kuwa familia yako yote ife kwa mikono yangu na wewe ubakie. Sasa mimi nina kosa gani kutekeleza kilichopangwa na Mungu" aliongea General David. "yaanu huoni hata aibu kumsingizia Mungu upuuzi wako" aliongea Alex na kubadilisha magazine ya bastola yake kisha akakoki. Wakati anafanya hivo, alisikia mlio na ghafla kitu cha moto kilipenya mgongoni. "ukithubutu kufanya chochote nakumaliza" Agent Darling aliongea, Alex aligeuka kwa nguvu na kumnyooshea bastola lakini Agent Darling alifyetua tena risasi iliopenya kifuani mwa Alex na kumfanya apige magoti. General David aliona huo ndio muda muafaka wa kutoroka, alikimbia na kungia kwenye helicopter na rubani akaiondoa.
Alex alijitahidi kusimama huku akijishika sehemu alipigwa risasi na Agent Darling, kutokana na hasira alizokuwa nazo Agent darling alifyetua risasi nyingine na kumpata Alex kifuani tena. "imebakia moja tu ambayo ntaisukuma kichwani mwako na kukuvuruga hicho kichwa" aliongea Agent Darling huku machozi yakimtoka. "kwanini umemuaa babaangu" aliuliza, "ama kweli kama baba kama mwana" Alex aliongea huku akikohoa na kutema damu. "babaako alikuwa ni mtu shujaa sana sijui kwanini mambo yalikwenda vile" Alex aliongea na kumuangalia Agent darling, "hivi unadhani nilishindwa kukuua mwanzo, hapana nilikuwa na asilimia mia moja ya kukuuwa lakini sikufanya vile kwa sababu nilidhani ni mwerevu sana kuujua ukweli wa mchezo huu ambao umechezewa bila kujitambua. Kama uliwahi kusikia DIRTY GAME basi ujue wewe umekuwa jokeri na kicheko cha kila mtu" Alex alizidi kuongea maneno kunya bila kujali kuwa anaeongea nae ni mtu ambae yuko hapo kumuua. "acha kuongea upuuzi, sali sala yako ya mwisho kabla hujafa" alifoka Agent Darling, "hivi kweli maiti nakufa tena, maana mimi nilishakufa siku aliokufa mke wangu kipenzi pamoja na mtoto wangu aliekuwa tumboni. Kuanzia siku hiyo nilipoteza kabisa dira ya maisha na kama kuniuwa utarudhika na kuweza kumuona babaako siki ya mwisho basi fanya hivo maana utakuwa umenisaidia na mimi kwenda kumuona mke wangu na mwanangu mbinguni" Alex aliongea maneno hayo na kuiangusha bastola yake chini kisha akainua mikono na kuangalia juu. "muda kidogo tu nitaungana na wewe mpenzi wangu na mwanangu ili nitimize ombi la mwisho la Allen James la kuwa na familia yangu" aliongea tena kufunga macho. Mlio wa risasi ulisikika "PAA".
.
MWISHO WA SEASON 2
ENDELEA KUFUATILIA SEASON 3.

MWISHO.
 
1.jpg


Simulizi : C.O.D.EX. 3 (The Real Me)
Mwandishi : TARIQ HAJI
Imeletwa kwenu na: BURE SERIES


87.

"Niko wapi, niko mbinguni au" aliongea Alex baada kufumbua macho kutoka katka usingizi wa kifo, "tulia kijana, utafikaje mbinguni wakati hujafa" aliongea mzee mmoja wa makamo huku akitabasamu na kumuekea Alex mkono begani "uko mahali salama kabisa" aliendelea kuongea mzee huyo. Alex alijaribu kuzivuta kumbukumbu zake za mara ya mwisho. Na ndipo akakumbuka kuwa alipigwa risasi na Agent Darling, akaanza kuwaza ikiwa risasi ile hajapigwa yeye , je aliepigwa ni nani?. Swali hilo lilizuka ghafla kichwani mwake, "isije ikawa wamemuuwa hawa". "Alex karibu tena duniani" aliingia mwanamke mmoja aliekuwa amevaa kinyago nusu katika uso wake. "unanikumbuka" aliobgea mwanamke na kukaa pembeni kwenye kiti. "hapana sikukumbuki" alijibu Alex huku akijaribu kukaa, "hahaha kweli Alex umenisahau?" aliuliza tena huku akicheka. "subiri hiyo sauti kama naijua" Alex aliongea huku akivuta kumbkumbu zake vizuri ghafla akaruka "Scarlet ni wewe au". "kumbe bado kichwa chako kipo vizuri" alijibu Scarlet, "wema haupotei" aliendelea kuongea mwanamke huyo mwenye tabasamu lenye kumuweka simba kichaa chini. Alionekana kuwa mchangamfu kupita maelezo lakini kwa mtu ambe na uwezo wa kusoma sura vizuri basi angegundua kuwa uchamgamfu wake pamoja na tabsamu vilikuwa ni danganya toto tu. Mtu pekee alielielewa hilo ni General Griffin, ambae ni baba mlezi wa Scarlet. "Hebu nambie nimeokokaje" aliongea Alex, "usijali nitakwambia kila" alijibu Scarlet na kumuangalia Alex.

"Ni hivi, nilisikia kinachoendelea kupitia vyanzo vyangu vya habari na uchunguzi. Taarifa nilizipata wakati natoka Mexico katika kazi maalum niliyopewa na serekali, ndipo nikaskia kuwa kua mtu anaitwa Alex na ni muuaji mkubwa sana. Nikaanza kufatilia na ndipo nikagundua kuwa Alex mwenyewe ni wewe, na pia nilianza kufatilia kwanini ulikuwa unatekeleza mauji hayo. Sasa siku moja nilifika katika ofisi za kitengo maalum cha upelelezi kama mwandishi wa habari. Wakati nashuka gari niliona vikosi vingi sana vya kuimarisha ulinzi wakati nataka kudadisi ghafla nilipitwa na gari ndogo nyeusi ikielekea upande waliopo wanajeshi na ilipofka ikaripuka. Kwa mbali nikauona ukianza kugawa dozi, bila kuchelewa nilipiga simu makao makuu waniletee chopa niondoke. ilichukua muda kufika, wakati naondoka sasa ndipo nikakuona juu ya jengo ukiwa umepiga magoti na mbele alikuwepo mwanamke aliekuwa ameshikilia bastola. Nilichukua sniper na kabla hajakupiga wewe nikamuwahi yeye, sijui hata nilimpiga wapi maana sikulenga kwa makini. Baada hapo nilikuchukua na kukuleta huku" Alimaliza kuongea Scarlet na kumuangalia Alex ambae macho yalikuwa yamemtoka kam mjusi aliebanwa na Mlango.

*******************************

"mkuu, Christina amemka" aliigia mwanamke mmoja aliejiulikana kwa jina la Martina, jeff aliinuka alipokaa na kuelekea chumba alichokuwa amelazwa Christina. "vipi hali yako" Swali a kwanza kuuliza alipofika ndani ya chumba hicho, "Jeff nimefikaje hapa?" aliuliza Christina. "tulia utajua kila kitu lakini kwanza unajiskiaje" Jeff alimtuliza na kumuuliza tena swali la kwanza. "vizuri kiasi na maumivu kwa mbali katika bega la mkono wa kushoto" alijibu Christina huku akijiangalia mkono ambao ulikuwa umefungwa bendeg. "usijali unahitaji siku chache tu, mkono utapona kabisa" alijibu Jeff huku akimshika mkono, "nilikukuta juu ya gorofa ukiwa unavuja damu huku ukiwa umepoteza fahamu,ndipo nikakuchukua na kukuleta huku katika kambi maalum, na wala usijali hakuna mtu anaejua kama uko hai ama umekufa" aliongea Jeff huku akimuangalia kwa makini, kwa vipi atazipokea taarifa hizo. "na kwanini wasijue kama niko hai ama nimekufa" aliuliza kwa mshangao, "nilikuwa nategemea swali hilo kutoka kwako" alijibu Jeff na kuinuka, alisogea mpaka ukutani na kubonyeza pahali. Ukuta ulifunguka na kulikuwa na TV, "naomba usikilize mwenyewe kabla sijakueleza chochote" aliongea Jeff na kuwasha Tv hiyo kubwa kisha akarudi alipokuwa amekaa wali na kukaa.

ITAENDELEA
 
Back
Top Bottom