Simulizi ya kijasusi: Nafsi zilizotelekezwa

Simulizi ya kijasusi: Nafsi zilizotelekezwa

HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 81

“Makamu wa raisi ameuawa” Aaliyah alibaki ameganda
“Nani mwenye uwezo wa kumvamia makamu wa raisi na kumuua? Na kwanini afanye hivyo?”
“Sijui ila nimepigiwa simu na mlinzi wake mkuu ambaye bila shaka naye ameuawa” Aaliyaha aliangalia saa yake hapo ndipo aligundua kwamba miadi yake na kiongozi huyo ndiyo iliwafanya kuwa hapo mapema namna hiyo, ilikuwa saa kumi na mbili kasoro ya asubuhi. Alishangaa inawezekanaje makamu wa raisi kuuawa tena alfajiri kabisa?
“Tunatakiwa kwenda huko muda huu kabla mtu mwingine yeyote hajajua kinacho endelea huenda kuna vitu tutavijua” alikuwa amechanganyikiwa, alibeba kofia yake na kutoka nje ambapo Aaliyah alimfuata ili waweze kwenda huko. Hiyo ni habari mbaya ambayo ilikuwa wakati mbaya pia. Makamu wa raisi kuuawa lilikuwa ni zaidi ya tatizo hilo kwa usalama wa taifa tena akiuliwa nyumbani kwake? Wangewaeleza nini wananchi wakaelewa? Majibu huenda wangeyapata huko huko mbele ya safari.

Raisi wa Tanzania Faraji Asan alikuwa ndani ya bwana la kuogelea, kichwa kilikuwa cha moto asubuhi ya mapema kabisa hivyo aliamua kwenda kukipooza eneo hilo la bwana kwa maji safi. Akiwa ametoka na kukaa kwenye kingo ya bwawa hilo, alikuja msaidizi wake wa kazi akiwa anatembea kwa mwendo wa haraka kidogo.
“Bosi unasubiriwa wewe tu kila kitu kipo tayari” alimhitaji mlinzi wake ampatie taulo bila kujibu kitu juu ya jambo ambalo aliambiwa, alijifuta vizuri na kuvaa nguo yake nyingine ambayo aliovaa kuwahi huko ambako alikuwa anahitajika wakati huo. Ndani ya chumba kimoja ambacho kilikuwa kama maktaba ndiko ambako alielekea na baada ya kuingia huko aliwahitaji watu wengine wote wabaki nje kwani hakutaka bugdha pindi awapo huko.
Ndani ya chumba hicho ambacho kilipangwa kwa ustadi mkubwa, alikuwa amesimama mzee mmoja wa makamo ambaye umri wake ulikuwa umekwenda. Kwenye mkono wake mzee huyo alikuwa na begi jeusi ambalo lilifungwa kwa ustadi mkubwa.
“Professor Christopher Nyemo nimepewa habari kwamba kila kitu kipo sawa kama nilivyo kuagiza!”
“Ndiyo bosi, nimeandaa taarifa zote tena kwa usahihi kabisa kama ambavyo ulihitaji niziweke”
“Una uhakika taarifa zote zipo humo?”
“Ndiyo kiongozi, zipo zote tangu ule mwaka ambao umeuainisha wakati unanipa maagizo”
“Asante kwa kazi ambayo umeifanya kwa wakati wote huu na kwa hili, hakika sitakusahau Nyemo na hata taifa litaikumbuka kazi yako daima” raisi aliongea kwa masikitiko akiwa anaivuta droo ndogo ambayo ilikuwa kwenye meza ya pembeni. Aliitoa bastola na kumnyooshea mzee huyo ambaye alionyesha wasiwasi wa wazi kabisa mbele ya raisi.
“Mheshimiwa tafadhali usifanye hicho ambacho unahitaji kukifanya” aliongea kwa sauti ya upole ila ya kumaanisha kile ambacho alikuwa anakisema ama kukihitaji, bado maisha yake alikuwa akiyapenda hivyo raisi kuhitaji kuyachukua alikuwa anakwenda kumkatili pakubwa.
“Unajua kabisa mimi sikupenda kuwa hivi, mimi sikuhitaji kuishi haya maisha ya kupangiwa. Nipo Ikulu lakini ni kama raia wa kawaida ambaye naishi kwa kupokea maagizo kutoka kwa watu ambao hata siku moja hawakuhitaji kuja kuonana na mimi. Wewe ni miongoni mwa watu ambao waliwahi kunishawishi nikubaliane na jambo hili ili kuweza kuishi lakini baadae ukaja ukaanza kunisaliti kwa kutumika nao kuuza taarifa zangu. Nyemo nilikuwa naweza kukusamehe yote lakini sio la hili kugundua kwamba unanisaliti mimi, taarifa ambazo nilikuwa nazihitaji bila shaka umeziandaa kwa usahihi ili uendelee kunihadaa na kunifanya mjinga, kumbuka mimi ni raisi wa nchi”
“Mheshimiwa tafadhali usifanye hili, wewe ni raisi lakini upo chini ya watu, wewe umewekwa hapo kama kivuli na ndiyo yalikuwa makubaliano ya mara ya kwanza kabisa wakati umepiga magoti unalia uachwe hai. Leo unaniona mimi sikufai kwa sababu unataka kubadili njia ya kupita?”
“Siku zote mimi sikupenda kuwa hivi, nimeitafuta hii nafasi ya kuweza kutoka huko muda mrefu lakini sikuipta, kwa sasa nahisi nimepata mtu ambaye naweza kumuamini hivyo nahitaji kufanya naye kazi kuwamaliza wote”
“Hahaha hahaha hahaha hahaha Asani nina uhakika kwamba wewe ni smart zaidi ya hapo, kweli unaamini kwamba unaweza kuacha mambo yakaenda kirahisi namna hii kama unavyo hitaji wewe? Makamu wa raisi kuuawa sio tatizo kwa sababu atawekwa mwingine na wananchi watadanganywa kama kawaida ila hiki ambacho unataka kukifanya wewe? Hili ni kosa ambalo litakufanya ufe ndani ya wiki hii tu, tufanye kama hakuna kitakacho tokea na taarifa hizi sizipeleki popote ila usije ukathubutu tena kuweza kuninyooshea bastola kwenye uso wangu mpuuz…….” Sentensi ya mzee huyo Christopher Nyemo iliishia njia baada ya risasi mbili kupenya kwenye paji la uso wake. Alidondoka chini akiwa anavuja damu hata hivyo raisi alimalizia risasi zote kwenye bastola kwenye kifua cha mzee huyo ambaye alichakaa damu kwenye shati yake safi nyeupe ambayo ilikuwa ndani ya koti ya suti ya blue.
Muda huo huo waliingia walinzi na kuubeba mwili huo huku wengine wakisafisha ile damu ili chini pabaki safi kama palivyokuwa mwanzo. Mwanaume mmoja shababi kweli kweli aliinama kuiokota ile begi akamsogezea mheshimiwa raisi na kumkabidhi.
“Bosi una uhakika na hili?”
“Ndiyo, nimeamua kufanya hivi hata kama nitakufa basi nitafurahi nikiwa kwa kuwa mtu mwema. Nimechoka kuua watu wasio na hatia, nimechoka kuwa kibaraka wa mtu, nimechoka kuwadanganya waananchi na kuliendesha taifa kitapeli. Nahitaji kukutana na Edison kwa gharama yoyote ile”
“Edison amekufa bosi”
“Yupo hai, nitafutie Aaliyah Beka, hakikisha unamleta hapa Ikulu nadhani yule binti atanifaa kwa kazi hii. Nipo tayari kufa lakini nataka hawa watu wote ambao wamehusika wafe na kufutika kwa taifa hili, miaka zaidi ya ishirini ambayo wameliendesha taifa hili watakavyo wao imefika mwisho. Siwezi kuendelea kuruhusu huu ujinga uendelee kwenye taifa teule kama hili” Aliongea kwa kufoka ila sauti ya utulivu mheshimiwa akionekana kabisa kutofurahishwa na jambo hilo ambalo lilionekana kuwa kero kwake kwa kipindi kirefu ni kwa vile tu hakuwa na namna ya kufanya akaamua kuishi nalo kama lilivyokuwa.
Christopher Nyemo alikuwa ni mwanahistoria wa Ikulu kwa muda mrefu. Alikuwa miongoni mwa watu wachache ambao walikuwa wakiijua Ikulu kwa ukubwa kuliko watu wengi, ndiye ambaye alikuwa anatunza nyaraka za mhimu za Ikulu na kujua kila taarifa mahali inako patikana kuhusu nchi hii hususani viongozi, waliyoyafanya na awamu ambazo walidumu kwenye madaraka. Siku hiyo alikuwa amepewa kazi moja ya mhimu na raisi, kazi ya kuweza kumkusanyia taarifa zote za viongozi wa Ikulu tangu mwaka wa 1991 mpaka siku ambayo yeye alikuwa anaingia Ikulu, kuna mambo hakuona kama yapo sawa kwa upande wake hivyo alihitaji kuyajua.
Mr Nyemo alikuwa ni mtu makini kwenye kazi yake, hakuwahi kumuangusha bosi wake wala kuruhusu amhisi kwa lolote baya hivyo kila kazi ambayo alipewa alikuwa anaifanya kwa uhakiwa wa asilimia zote na raisi alilijua hilo. Aliamini kwamba mtu huyo anempa taarifa za kweli ili aendelee kumuamini ila habari hiyo ingewafikia watu ambao hakuwa akihitaji kabisa waweze kujua juu ya mpango wake mpya ambao ulichipua ghafla kwenye kichwa chake. Mwanahistoria huyo ni miongoni mwa watu ambao walichangia kwa kiasi kikubwa yeye kuweza kuingia Ikulu ila baadae aligundua kwamba mwanahistoria huyo alikuwa miongoni mwa watu na viongozi wa kuaminika ndani ya jamii ya siri ya LUNATIC SOCIETY ambayo hata yeye alikuwa mmoja wapo. Taarifa ambazo alizihitaji siku hiyo zilikuwa zinaainisha namna viongozi walivyo patikana ndani ya taifa la Tanzania na walichokuwa wanakifanya baada tu ya kuanguka kwa umoja wa nchi za Kisovieti.
Alihakikisha wamesafisha kila kitu hapo akamkonyeza mlinzi wake ambaye aliufunga mlango wa kuingilia kwenye chumba hicho, alihitaji kuwa mwenyewe. Alinyoosha mbele ambako kulikuwa na shelf kubwa ya kitabu, alitoa vitabu viwili akaviweka pembeni, mbele kulikuwa na kibox ambacho kilikuwa kinahitaji namba, aliingiza namba kadhaa shelfu la vitabu likajigeuza. Ulikuwa ni mlango wa kuingilia ndani zaidi, palifunguka akaingia huko kisha pakajifunga tena kama palivyokuwa mwanzo.
Alitulia kwenye meza na kutoa makablasha yale kisha akaanza kuyapitia moja moja huku kumbukumbu zake zikizama mbali miaka ya nyuma huko kabla hata hana hiyo ndoto ya kuja kuwa raisi wa Tanzania.

UKURASA WA 81 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 82

SURA YA NANE
REVIEWS OF TANZANIAN PRESIDENTS SINCE 1991 (MAPITIO YA MARAISI WA TANZANIA TANGU 1991)
Baada ya kuisha vya vita baridi na upande wa magharibi kuibuka na ushindi mkubwa ndipo Tanzania ilimpokea memba wa KGB, IRINA ESPANOVICH ambaye alikuja kuwa muasisi wa jamii ya siri ya LUNATIC SOCIETY. Mwanamke huyo alifanikiwa kumuweka kwenye mkono wake mdogo wa raisi Novack Nyangasa, raisi wa kipindi hicho Justin Nyangasa baada ya kugundua jambo hilo alichukia mno akamhitaji mdogo wake kuifuta shughuli hiyo ndani ya mwezi mmoja lakini amri yake hiyo ilimfanya kuishia kaburini.
Kufa kwake ikiwa ni shinikizo na mpango wa IRINA kumlaghai Novack ukawa mwanzo wa kusimika mizizi yao Ikulu kwa sababu Novack alikuwa ni mtu wa kuheshimika kwa kuwa mdogo wake na mkubwa wa nchi. Hivyo ilitumika nguvu yake kumtumia mwanamama ambaye alikuwa makamu wa raisi kipindi hicho Daniela Lopa ambaye aliapishwa kuwa raisi na kwa mara ya kwanza akawa ndiye raisi wa kwanza mwanamke ndani ya taifa hili la Tanzania. Raisi huyo aliambiwa kila kitu juu ya kile ambacho kilitokea kwa kaka yake Novack hivyo naye alikuwa na chaguo la kukubali kufanya kazi chini ya mtu huyo ambaye alikuwa na nguvu kubwa au naye alambishwe mchanga kama mwenzake kisha wamuweke mtu wao mwingine pale juu.
Daniela hakuwa mjinga, kushindana na mtu ambaye alimuua kaka yake wa damu tena raisi ambaye alikuwa na nguvu kubwa kimamlaka asingeshindwa kumuua yeye ambaye walikutana ukubwani tu tena kwenye kazi hivyo akakubali kufanya kazi chini ya Novack Nyangasa lakini hata Novack alikuwa chini ya mtu ambaye ni Irina Espanovich. Daniela ndiye raisi ambaye aliidhinisha kufa kwa Christian Edison, mwanasayansi bora zaidi kuwahi kuzaliwa ndani ya ardhi ya Tanzania kwa sababu ndiye ambaye alitoa idhini ya mtu huyo kwenda Israeli ambako hakwenda kufanya kazi kama walivyo danganya bali walikwenda kumuulia kwenye ardhi ya mbali ambako waliamini hata ushahidi usingekuja kupatikana kamwe. Habari ya mwanasayansi huyo iliishia hapo wao wakabaki kudanganya kwamba alikuwa hai.
Daniela aliifanya kazi yake kwa uaminifu mkubwa chini ya Novack, alikuwa akiripoti kila jambo ambalo lilikuwa mhimu na kuyafanyia kazi yale yote ambayo alikuwa akiyahitaji Novack mpaka siku ambayo alimaliza mhula wake mwaka 2000. Kutoka kwake Ikulu hawakuwa na uhakika kama angefanikiwa kutunza zile siri zote ambazo alitoka nazo Ikulu hivyo naye akatakiwa kupotezwa, uliandaliwa mpango wa kufa kwake ambapo ilionekana kwamba mama huyo alidondoka kwenye ngazi za ndani kwake wakati akishuka kwenye ghorofa kwani alivaa vazi refu ambalo lilinasa vibaya kwenye chumba ambazo zilikuwa kwenye kingo za ngazi hizo hali iliyo mfanya adondokee kichwa chake kikapasuka. Daniela habari yake iliishia hapo akaingia EBENEZA GEREZA mwanaume ambaye aliipenda dini isivyo kawaida.
Alikulia kwenye malezi ya dhehebu la wakatoliki lakini hiyo dini ilikuwa ni kwa ajili ya kuwazuga wajinga. Alikuwa ni miongoni mwa watu washenzi zaidi kuwahi kutokea nchini ndiyo maana Novack alimchagua na kuamua kumfanya kuwa raisi kwa sababu alijua angefanya kazi zake vyema na wakati huo wananchi walikuwa wakimuamini isivyo kawaida kwa sababu kila baada ya sentensi moja angemtaja Mungu kitu ambacho hakuwahi kukimaanisha. Ni awamu hiyo ambayo LUNATIC SOCIETY ilitengeneza mizizi mirefu na mizito kwenye kila kona ya nchi na hata nje ya nchi.
Kwanza walitengeneza mifumo ya pesa, walitengeneza mabilioni ya fedha kwa sababu kila biashara kubwa ilikuwa yao, kila mradi mkubwa ulikuwa upande wao. Baada ya kuhakikisha wana mfumo mzito wa pesa ambazo waliamini zisingekuja kuisha ndipo wakaanza kutafuta watu wenye uwezo mkubwa kila sehemu. Waliangalia wasomi wakubwa ambao waliheshimika, waliangalia watu ambao walikuwa na akili nyingi lakini pia waliangalia watu wenye vipaji vikubwa hususani kwenye tasnia ya mapigano. Huku ndiko waliwekeza nguvu kubwa kwa baadae kutengeneza viumbe vya ajabu kwa ajili ya kuja kutengeneza ngome ambayo hakuna mwanadamu angekuwa na uwezo wa kuja kuivunja.
Huu ndio wakati ambao alitafutwa mwanaume mmoja aliye itwa Nikolai Gibson. Mwanaume huyu maisha yake kabla ya kutafutwa na watu hao aliyatumia zaidi kwenye kazi ya nchi, aliwahi kuwa jasusi hatari sana kwa maisha yake ya nyuma. Aliwahi kufanya kazi kwenye misheni miamoja na kumi na hakuwahi kufeli hata moja ikiwemo ya kumuua raisi wa nchi ya Liberia na alifanikiwa bila kukamatwa wala kuacha hatua yoyote ile. Sifa zake ziliwafaa watu hao ndipo walimtafuta mwanaume huyo ambaye kwa wakati huo alikuwa amestaafu kufanya kazi hizo kwa sababu alidai alichoka kuua watu.
Alitafutwa na kukutana ana kwa ana na mwanamama mwenye ushawishi mkubwa Irina Espanovich ndiye ambaye alimshawishi kwa mdomo wake akiahidi kumtengenezea chuo kikubwa cha siri ambacho atakitumia kuwanoa vijana wengi na kutengeneza viumbe vya hatari kwa ajili ya baadae ya jamii hiyo endapo itakuja kutokea siku hata moja mambo yao yakawa yanaenda vibaya. Nikolai alipewa nafasi kubwa na kuahidiwa maslahi makubwa ambayo alikuwa akiyasikia kwenye biashara za madawa ya kulevya na ndipo ambapo mpango wa kuwatengeneza vijana ulianzia pale.
Sasa hao vijana angewapatia wapi? Ulianza msako kwa wanaume ambao walikuwa hawana cha kupoteza kwenye maisha yao, wengi ambao walipewa kipaumbele ni wale ambao hawakuwa na familia, ambao walikuwa jeshini lakini walikuwa wanapimwa uwezo wao kuanzia akili, kuweza kuhimili mambo, kuwa na uwezo wa kubadilika kulingana na mazingira pamoja na wale ambao walikuwa wamekata tamaa ya maisha, alijua kwamba hao wangekuwa bora zaidi kwa sababu mtu ambaye alishajikatia tamaa ya kuweza kuishi ukimhakikishia kwamba unaweza ukamrudishia tumaini la kuwa hai, anaweza kufanya jambo lolote lile ambalo utamuamuru aweze kulifanya hiyo ikawa safari ya kukutana na kijana ambaye alijivunia kumtengeneza kuliko vijana wote.
Alikuwa akizunguka na gari yake maeneo ya Kariakoo ambako yalikuwa yanajengwa majengo mapya ya masoko kwa ajili ya biashara, akiwa anakatiza kwenye mitaa hiyo alivutiwa na jambo moja jambo hilo lilikuwa ni ugomvi wa vijana kadhaa akaamua kusogea na gari yake pembeni kidogo kisha akatulia kuona kile ambacho kilikuwa kinaendelea. Kijana mmoja alikuwa anazongwa na wenzake huku wakimtembezea kipigo kikali lakini hakuwa mnyonge, alipambana mpaka akafanikiwa kumtoa mmoja jino. Mwingine wakati anakuja alimkita na jiwe la uso akazimia hapo hapo, aliinama kuokota pesa ambayo bila shaka alitaka kudhulumiwa kisha akatoka nduki nguo zake zikiwa na tope. Ilikuwa ni ishara kwamba vijana wale walikuwa wanafanya kazi ya ujenzi.
Alivutiwa na ujasiri wa kijana yule akaamua kumfuatilia kujua anaenda wapi, alimuona akiwa anapanda daladala, aliifuatilia ile daladala mpaka alipo ona kijana yule anashuka akaanza kumfuatilia kwa nyuma taratibu. Safari ya kijana yule iliishia Tandale kwa tumbo ambapo baada ya kutia tu mguu mtaani vijana wenzake walikuwa wakimtania lakini hakuwajali akaingia vichochoroni. Hakumfuatilia tena kwa sababu alijua kufahamika kwa kijana yule maana yake ilikuwa ndiyo mitaa yake hivyo angepata taarifa mapema tu.
Alipaki gari pembezoni mwa duka moja akaagiza maji, aliteta jambo hilo na muuza duka ambaye alijifanya kutomuona kijana yule ambaye wenzake walikuwa wanamtania basi ikamlazimu kumkunjulia noti kadhaa nyekundu, hakuwa na ujanja zaid ya kumwaga ubuyu wote juu ya kijana yule. Ile ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kukutana na kijana Joeli John na kuanza kumfuatilia kwa ukaribu mpaka ile siku ambayo alijitokeza kwake akiwa analia karibu na kile kibanda cha muuza dagaa, akampa somo la maisha na kumuachia begi la pesa yo siku rasmi ambayo ilifungua ukurasa wa kumtengeneza Yohani Mawenge, mwanaume ambaye alijikamatisha huko Uganda na baada ya kukamilisha kilichokuwa kimempeleka akarudi nchini.
Raisi Ebenezer alimaliza mhula wake salama na mpaka sasa alikuwa bado yupo hai na mzima wa afya. Mhula wake aliumaliza mwaka 2010 ambapo baadae aliingia madarakani raisi mwingine Shebius Ndabo. Raisi huyu licha ya kuwekwa Ikulu lakini hakupewa taarifa nyingi za ndani kuhusu jamii hiyo hali ambayo ilimfanya kuanza kujisahau na kufanya mambo yake na huyu ndiye ambaye alifanya makosa makubwa kiasi kwamba taarifa nyingi za uwepo wa jamii hiyo zilivuja japo zilikuja kuzimwa baadae. Alianza kufanya mambo kwa kujisikia mwenyewe akiungana na aliyekuwa mkurugenzi wake wa usalama wa taifa JANISON LEWELA.
Uwepo wao wote wawili ulichukuliwa kama sio salama kwa umoja huo hivyo ilitakiwa mmoja wao afe na ambaye aliuawa alikuwa ni mkurugenzi Janison, aliuawa na mdunguaji ambaye alimpiga risasi akiwa kwenye kibara cha nyumba yake ikiwa ni siku moja tu baada ya raisi kushinikizwa kumuengua kwenye nafasi hiyo akawekwa mtu mwingine. Kesi ya kufa kwa mkurugenzi huyo walipewa kundi la Al-Shabaab ambao walilipwa pesa nyingi kisha kukubali kuhusika na mauaji hayo kwa sababu ambazo hazikuwahi kuwekwa wazi hivyo vyombo vikasaidia kumchafua mtu huyo kwa kudai kwamba alikuwa akishirikiana na magaidi ndiyo maana raisi alimuengeua kwenye nafasi yake hivyo huenda magaidi wenzake walipoteza imani kwake kwani hakuwa na mamlaka tena wakaamua kumuua. Kiongozi huyo akaonekana kama alikuwa muasi kwa taifa, watu wakaichukia mpaka maiti yake hivyo hakuzikwa kama shujaa bali haini kwa nchi yake.

UKURASA WA 82 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 83

Kifo cha mkurugenzi Janison kilienda sawa na raisi kupewa virusi ambavyo vilimfanya kuwa mpole, watu hao walikuwa wakimpa dawa kwa mafungu ili siku akija kujifanya kutaka kufanya uhuni tena basi wanaacha vinammaliza, jambo hilo lilimfanya kuwa mbwa mtiifu mpaka siku anamaliza mhila wake ndipo alipo ingia madarakani Faraji Asani.
Raisi huyo alikuwa anazipitia takwimu hizo huku akili yake ikiwa mbali kwani awani zote hizo ambazo zlizosoma na mambo yote yalitokea akiwa amezaliwa na anaishi tayari hivyo kuna stori aliwahi kuzisikia tu na hakuwahi kuziamini ila baada ya kuingia kwenye mfumo husika kuna habari alizithibitisha lakini kuna zingine hakufanikiwa kuujua ukweli huenda angeujua ukweli huo baada ya kukutana na wahusika wenyewe moja kwa moja na sio kupitia makaratasi ambayo watu wangeweza kubadilisha sheria kwa matakwa yao ambayo walikuwa wanayahitaji wao binafsi.
Alishuhudia wenzake ambao walikuwa wasaliti kwa watu hao mambo ambayo yaliwapata hivyo huenda na yeye yangemkuta yale yale na alikuwa ameshafanya maamuzi tayari. Kumuua mwanahistoria yule ilikuwa na maana kwamba hakukuwa na kurudi nyuma tena, alijikuta anatokwa na jasho usoni ambalo lilidondokea kwenye yale makaratasi ila wakati huo hisia zake zilienda mbali na nyuma zaidi ya kule ambako zilimpeleka mara ya kwanza wakati anaendelea kusoma habari ambazo ziliandikwa kwenye zile nyaraka ambazo alipewa na Christopher Nyemo.

ISAMILO, NYAMAGANA MWANZA.

NYAKABUNGO, ni kijiji ambacho kilikuwa kinapatikana ndani ya kata ya Isamilo, manispaa ya wilaya ya Nyamagana mkoani mwanza. Kwenye kijiji hicho ilikuwepo familia ya mzee Hasan ambaye maisha yake yalitegemea kwa kiasi kikubwa shughuli zake za uvuvi ndani ya kisiwa cha Ukerewe. Kwa bahati iliyokuwa mbaya siku ambayo mkewe alikuwa akijifungua ndiyo siku ambayo alikufa lakini mtoto alifanikiwa kuishi. Bwana huyo kwa sababu alikuwa akimpenda mno mkewe alihisi kwamba kuzaliwa kwa mtoto huyo ilikuwa ni laana kwa familia ndiyo maana mkewe akafa hivyo akawa hamhitaji lakini sheria ya nchi ilimhitaji kila mzazi kuwajibika kwa damu yake.
Bwana huyo alijaribu mara kadhaa kumuua mtoto huyo lakini ilishindikana kabisa mpaka alipokata shauri la kumlea hivyo hivyo japo alikuwa na chuki mbaya na mtoto huyo kwenye nafsi yake. Mtoto huyo alianza kulipata fukuto la joto akiwa bado mdogo, miaka mitano tu ambayo alikuwa nayo ilimfanya kuitambua vyema dunia ilivyo chungu. Aliishi kwa shida nyumbani kwa baba yake mzazi tena hayo akifanyiwa na mzazi wake hali iliyo mfanya asipapende nyumbani kwao, alitamani angeishi mbali na hapo ila kwa umari wake angeenda wapi? Akakubali kuishi maisha hayo hayo mpaka alipofikisha miaka kumi aliamua kutoroka nyumbani.
Jina lake alikuwa akiitwa Fariji Hassan, kukimbia nyumbani kulimfanya akimbilie mpaka Nyegezi ambako alikuwa mtoto wa mtaani yaani chokoraa. Aliyakwepa mateso ya nyumbani akakumbana na yale mateso ya dunia lakini pia yeye kukimbia nyumbani ilikuwa furaha kubwa kwa baba yake kwani aliutua mzigo wa sumu ambayo alikuwa nayo kwenye moyo wake hivyo akamfuta mtoto huyo kwenye maisha yake na mtoto akafuta kwenye moyo wake kama hakuwahi kuwa na familia kabisa.
Alijipeleka kwenye kituo cha kulelea watoto yatima ya NIPENI TUMAINI LANGU huko Nyegezi Mwanza. Kwenye kituo hicho alijielezea kwamba yeye hakuwa na familia wala hakuwahi kuwa nayo hivyo alikuwa yeye kama yeye na alipo ulizwa jina alijibu kwamba alikuwa akiitwa Faraji Asani akiwa amelibadilisha jina lake halisi la kuzaliwa la Fariji Hassan. Kituo hicho kilimlea sawa na watoto wengine, walisomeshwa kwa ufadhili wa watu wa nje na kufanikiwa kufika mpaka elimu ya upili. Alikuwa na hasira na maisha kutokana na alikotoka nyuma ambako kiualisia hakuwa akitamani hata kukumbuka kabisa kwa mara nyingine kwenye maisha yake.
Tamaa ya maisha ilimpa elimu dunia kwamba pesa wanazo wachache na ili uzipate pesa hizo basi unatakiwa kuwa miongoni mwa hao wachache. Hao wachache ni akina nani? Aligundua kwamba wengi walikuwa ni wafanya biashara lakini msingi wa hao wachache walikuwa ni wanasiasa kwa sababu hata wafanya biashara kwa kiasi kikubwa walikuwa wakiwategemea wanasiasa ili kuendesha mambo yao na muda mwingine walilazimika kuweza kuwatumia wanasiasa hao kwa ajili ya hizo shughuli zao kwenda sawa.
Jibu lake ni kwamba alitakiwa kuingia kwenye siasa ili asije kuishi kwenye ule ukata mkali ambao ulimfanya mpaka kuwa chokoraa mtaani hapo akachagua kwa usahihi chama ambacho kilikuwa na nguvu na uhakika wa kula nchini. Hakujali kuhusu uwepo wa haki ndani ya chama hicho, hakujali kama kuna uhalali wa shughuli ambazo zilikuwa zinafanyika ndani yake lakini yeye alicho kijali ilikuwa ni kuipambania ile hali yake ambayo hakuwa tayari kuja kiyarudia tena yale maisha ya nyuma.
Licha ya kituoni kwao kupigwa vita kuhusu masuala hayo ya siasa lakini kwake ilikuwa fursa ya kipekee kabisa akaamua kuivaa siasa kwenye mwili wake na kuamua kuiishi kama maisha yake ya kila siku. Alipokuwa anakaribia kwenda elimu ya juu alikosana na walezi wake kwenye hicho kituo kwa sababu aiikumbatia siasa kuliko kitu chochote na wao misingi yao waliamini kwamba siasa ndiyo ilikuwa chanzo cha matatizo yote ambayo yalikuwa yanatokea nchini, waliamini kwamba kijana huyo kuingia huko kuna wakati ingemlazimu kuwa mtu mkatili hivyo angekuja kuwa muuaji tu lazima lakini aligoma kuwaelewa.
Alikubali kuachana na masomo akaipambania ndoto yake ya siasa, alianza kusikika maeneo mengi, licha ya kuanza kuupata umaarufu hakuna mtu ambaye angemkumbuka kwao kwa sababu alikuwa mtu mzima sasa wa zaidi ya miaka ishirini na kwao aliondoka akiwa mdogo, jina lenyewe alikuwa amesha badilisha kwahiyo hakutamani tena chochote kutoka kwenye maisha yake ya nyuma. Kuzipambania ndoto zake ndiko ambako kulimfikisha Ikulu na kumkutanisha na watu hao ambao ndio walimuweka hapo na kumfanya kuwa kama kibaraka wao hivyo hata yeye alikuwa chini ya watu fulani.
Alimaliza kusoma na kuzifikiria fikira zake hizo za huko zamani, aliyakusanya makablasha yote na kuyahifadhi kwenye begi. Alifikiria mahali pa kuanzia kwa mara nyingine kwa sababu alikuwa anaenda kuokolea moto kwa mkono wake ila hakuwa na namna maji alisha yavua alitakiwa kuyaoga huku kwenye moyo wake hesabu zake kubwa zikiwa ni kumtumia Edison kukamilisha jambo lake ambalo lilikuwa kama mchezo wa pata potea hakujua kama angeweza na kama angeshindwa maana yake alitakiwa kufa. Alimeza mate kwa wasiwasi na kutoka humo ndani kwenda kuitekeleza mipango ambayo halmashauri ya kichwa chake iliikubali.

Yohani Maewenge alionekana akipaki gari yake maeneo ya ukufweni mwa bahari, alishuka na kuangaza kila upande, hakukuwa na kitu zaidi ya upepo mkali ambao ulikuwa unasikika kila wakati. Aliyaangalia mazingira vizuri kuhakiki kama usalama ulizingatiwa ama kama kulikuwa na mtu anamfuatilia nyuma, alijihakikishiwa kwamba usalama ulikuwa wa hali ya juu.
Kwenye mkono wake alikuwa ameshika cigar ambayo ilikuwa inateketea taratibu wakati ambao alisogea kwenye mchanga kuyakaribia maji ya bahari ambayo ilikuwa inatisha isivyo kawaida. Aliangalia saa yake ya mkononi, ilikuwa inasoma saa tisa usiku, muda ambao inaaminika kwamba viumbe visivyo wanadamu ndio huwa vinapenda kujiachia maeneo ya bahari, inadaiwa kwamba mida kama hiyo kuwepo kwenye maeneo kama hayo unaweza kuona viumbe vya ajabu visivyo na uhai na mambo ya kutisha ambayo yapo kwenye mlango wa pili wa dunia ambao hauonekani kwa macho ya kawaida.
Kwake lilikuwa jambo la kawaida, hakuwahi kuziogopa nadharia hizo huenda kutokana na sababu za msingi kwamba hata yeye roho yake ilikuwa sawa tu na hao watu. Aligeuka upande wa kulia na kushoto lakini bado hakuona mtu yeyote wala alama ya uwepo wa mtu, alisonya na kutema mate mengi kwenye maji baada ya kubanja huku akiendelea kuiteketeza ile cigar yake taratibu bila papara. Aliyaelekeza macho yake baharini ambako kulikuwa na mwanga wa taa uliokuwa unamulika sehemu nyingi kutoka kwenye meli ambazo zilikuwa zimetia nanga umbali mrefu kutoka ndani ya maji zikisubiri tarehe zao za kuondoka kuelekea maeneo mbali mbali ya dunia.
Kuyaangalia maji hayo ndiko kulimfanya akumbuke mbali, enzi za maisha yake ya nyuma na ambako alitoka. Alijikuta anatabasamu kwa mbali mwanaume huyo ambaye ilikuwa ni mara chache unaweza kumkuta kwenye hali kama hiyo, maisha yake ya nyuma yalikuwa na utata mkubwa kiasi kwamba hata yeye alikuwa akiisikitikia nafsi yake ile ambayo iliyaishi yale maisha. Alirudi kwenye yale maisha ya nyuma kwa kutumia fikra zake.

UKURASA WA 83 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 84

Joeli John, waweza kumuita Joh alipata begi la pesa, pesa ambazo hakuwahi kuwaza kuwa nazo kwenye maisha yake huku akiambiwa kwamba alikuwa anaweza kufanyia jambo lolote lile ambalo angelitaka yeye. Alijihisi kuchanganyikiwa lakini hakuwa na namna kwa sababu pesa zilikuwa zake na aliruhusiwa kuzitumia kwa namna atakayo yeye, baada ya mtu ambaye alimletea pesa kuweza kuondoka, yeye alikimbia kuelekea kwenye kituo cha daladala, alipanda daladala akiwa ndiye binadamu mwenye furaha zaidi duniani kwa siku hiyo.
Safari yake ilimpeleka mpaka SHOPPERS, huko alienda kufanya manunuzi ya nguo mpya na za gharama kubwa. Alifika eneo hilo ambalo lina maduka mengi makubwa ya vitu vitu vya gharama, kuingia hapo kununua bidhaa kama nguo unatakiwa uwe ni mtu ambaye una uhakika wa milo mitatu ndani ya jiji hili na hauwazii kodi mara kwa mara mama mwenye nyumba anapo ipiga simu yake kwenda kwako. Hata badhi ya wahudumu walibaki wanashangaa, mteja ni mfalme ndiyo lakini hali yake ilikuwa ya kushangaza ila hata wachache ambao walimhoji hususani wateja wenzake kuhusu hali yake alidai kwamba alikuwa kwenye machimbo ya madini ila alikuwa amerudi zake mjini sasa.
Alinunua mavazi ya gharama na kuhitaji kuonyeshwa zilipo sehemu za gharama za kwenda kufanyiwa usafi hususani kuogeshwa na warembo pamoja na kufanyia masaji kwenye mwili wake, pesa ilikuwepo yanini ajitese Joel? Ulikuwa ni muda wake wa kuyafaidi maisha bhana pesa zilimkubali ndani ya jioni moja tu pekee. Kijana huyo alibadilika mwonekano wake ndani ya saa moja tu, kama ungebahatika kuonana naye halafu ukaambiwa kwamba alitoka kwenye maisha ya kimaskini basi nafsi yako isingekubaliana na hiyo hali kwani ungekuwa moja ya watu ambao wangegoma kukubali.
Safari yake iliishia Serena hoteli, alichukua chumba cha bei kubwa huku akihitaji kutafutiwa mrembo mkali zaidi ndani ya eneo hilo ambaye alitakiwa kukaa naye usiku huo na kama angempenda basi angempa ofa nyingine ya kuendelea kuwa naye usiku uliokuwa unafuata. Hoteli hiyo ya nyota tano alikuwa akiiona tu kwenye runinga hususani wakati wafanya biashara wanafanya mikutano yao na wasanii wakubwa, yeye alikuwa anaziishi moja ya ndoto zake usiku huo. Aliletewa mwanamke mmoja mrembo haswa, alikuwa ni Mhabeshi yule, unaijua Ethiopia wewe? Mhabeshi ikawa halali yake kuyadhalilisha mashuka na yalikoma usiku ule, mwanaume yule alikuwa amepania kufanya mapenzi na mwanamke mrembo kama huyo na aliapa siku akimpata basi angenyooka na usiku huo aliyadhihirisha maneno yake mpaka mhabeshi hakutaka kumuacha mwanaume huyo kwa show ambayo alimpatia.
Joeli alijiona mjinga mno alipo jitazama kwenye kioo, alikumbuka ni jana yake tu jioni alitaka kujiua kwa sababu ya mwanamke! Tena mwanamke wa kawaida tu huenda ni ugumu wake wa maisha ndio ambao ulimfanya amuone mrembo. Alijicheka na kujitia kibao, yaani Joeli mimi ndiye nilikuwa nalia, mimi ndiye nilitaka kujiua kwa sababu ya mwanamke wa Tandale tena kwa Tumbo? Aaaah fala mimi. Alijiongelesha wakati huo alikuwa akimwangalia mhabeshi kitandani, alipewa show nzito mpaka akapitiwa na usingizi. Mwanamke huyo alilala kihasara kiasi kwamba hata mwili wake ulikuwa umejiachia wazi kabisa hivyo akawa anaona kila kitu, ulikuwa ni uumbaji bora zaidi wa kiumbe kinacho itwa mwanamke kuwahi kuuona kwa macho yake. Mhabeshi alikuwa mrembo mpaka alihisi mama yake alifanya sifa kumzaa mwanamke huyo, aliivua nguo yake ya ndani na kurudi tena kitandani kuweza kuufurahia ulimwengu wa uumbaji.
Joeli maisha yalikaa upande wake, alikula starehe kama amechanganyikiwa. Baada ya wiki moja alirudi Tandale akiwa na gari kali, alikuwa amevaa mavazi ya gharama kali mno ili kwenda kuwanyoosha wanazi wake. Baada ya kufika mtaani alikuwa gumzo Joeli, kila mtu alidai kumfahamu yeye na kuwa rafiki yake, kila mtu alihitaji ukaribu na kijana huyo lakini hakuwa na hizo shobo, heshima ilitakiwa kufuata mkondo wake. Tena hakurudi mwenyewe, alirudi na wale watunisha misuli wa gym ili asisumbuliwe na wapenda kushobokea watu. Taarifa ile ilimfikia Tina aliyekuwa mkewe, mwanamke huyo kusikia habari hiyo alitoka anakimbia kiasi kwamba hata nguo zilikuwa zinamdondoka kumuwahi Joh wake ambaye aliambiwa kwamba kawa tajiri ghafla.
Wanawake na pesa tena? Ni kama Messi na mpira wake, mwanamke huyo hakukumbuka kwamba siku kadhaa nyumba alimdhalilisha Joeli mbele ya wanaume wawili waliokuwa wakifanya naye mapenzi kwa fujo tena mbele yake, eti siku hiyo alikuwa akimkimbilia mmewe, hahaaha wanawake wanawake! Mwanamke huyo licha ya kufika hapo na kushuhudia maajabu ya dunia, Joh mfanya vibarua alikuwa akilindwa lakini aliishia kuwa kama Mussa. Mussa aliambiwa kwamba utaiona nchi ya ahadi ila hautafanikiwa kuingia, hata Tina hakufanikiwa kumgusa mwanaume huyo ambaye alikuwa na ghadhabu naye kubwa, jambo hilo alilihifadhi kwenye moyo wake kama kiporo.
Licha ya Tina kulia na kugala gala akijifanya kujutia kitendo chake, Joeli hakuwa na muda na mwanamke huyo baradhuli. Aligawa pesa kwa baadhi ya watu mtaani hapo kisha akatoweka na watu wake akimuacha mwanamke huyo anaushangaza mtaa akijilalamisha kwamba alikuwa akimpenda mno mumewe na hakuwa tayari kumuacha, watu wakabaki wanamshangaa kwa sababu kila siku Joh alikuwa akisalitiwa eti kawa na pesa ndipo kampenda ghafla? Alidhalilika mtaani hapo binti huyo.
Joel alijisahau mno, alikula bata mpaka mji ukamshangaa lakini alisahau kwamba alipewa mwezi mmoja tu pekee. Huenda ni utamu wa yale maisha mapya ndio ulimfanya asikumbuke kwamba muda wake ulikuwa unakaribia kufika hivyo akawa anaendelea kuponda raha mpaka siku moja ambayo alipokea ugeni, ugeni ambao haukuwa mgeni kwake. Alikuwa baharini kwenye boti na warembo kumi akiponda raha ndipo ambapo alishangaa boti hiyo inageuzwa uelekeo na kuelekea ndani zaidi ya bahari jambo lililomfanya kumfuata nahodha amwambie sababu ya kwenda kinyume na yeye ambaye ndiye alikuwa anamlipa lakini nahodha huyo alimwambia kwamba muda wake ulikuwa umeisha hivyo kuna mtu alihitaji kuonana naye.
Boti hiyo ilifika mahali ambako kulikuwa na meli ilipaki hapo, wanawake wale walirudishwa kuendelea na mambo yao huku yeye akiingia ndani ya meli hiyo ambayo bila shaka ilikuwa imepaki kusubiri tarehe yake ya kuondoka. Ndani ya meli hiyo alikutana na yule mwanaume ambaye ndiye alimletea lile begi la pesa, alishtuka na hapo ndipo akagundua kwamba siku zake zilikuwa zimeisha kama ambavyo aliahidiwa. Alishangaa mtu huyo kumpata kirahisi lakini mwanaume huyo alimahkikishia kwamba mtu anapokuwa anazipata pesa kwa mara ya kwanza hususani kwenye mazingira ambayo hata yeye mwenyewe hakuyatarajia basi lazima atataka kutamba kwamba hivyo hata ukihitaji kumtafuta hautumii nguvu kwani anakuwa maarufu ghafla lakini mbali na hilo alimhakikishia kwamba alikuwa akimfuatilia kila hatua ambayo alikuwa anaipiga.
Ndipo alipo mkalisha chini na kumpa mpango mzima wa lengo kubwa la kukutana naye, aliahidiwa maisha safi lakini pia alikuwa anaruhusiwa kutojiunga nao kama akiweza kulipa zile pesa ambazo alizitumia kula starehe kwa ule mwezi mzima. Angeitoa wapi tena pesa ya kulipa Joh! Kukubali ndiyo ikawa njia sahihi kwake, hata hivyo bila kupewa sharti hilo bado alikuwa tayari kujiunga na watu hao kwa sababu ni njia pekee ambayo ingemuweka mbali na umaskini.
Alijiunga na chuo cha siri ambacho kilikuwa chini ya mwanaume huyo aliyejulikana kwa jina la Nikolai Gibson. THE FUTURE PROJECT, ndio ambao ulikuwa mpango rasmi wa kutekelezaji wa kuwafua vijana hao kwenye chuo hicho akiamini kwamba vijana hao ulikuwa ni mpango wa baadae wa jamii yao ya siri. Walitengenezwa vijana wengi shupavu huko ambapo waliokuwa wanaiva walikuwa wanafanyiwa majaribio kwa kupewa kazi za kuua kisha wanasajiliwa moja kwa moja na kuanza kupata malipo makubwa ambayo yaliwafanya waipende kazi yao na kuwa waaminifu lakini kulikuwa na sheria kali mno kiasi kwamba ambaye alikuwa anaenda kinyume na sheria hizo alikuwa anakufa na mkosaji aliwekwa wazi ili wengine wajifunze kwake.
Joeli John ndilo lilikuja kuwa zao bora zaidi kwenye mpango huo kwa sababu yeye alifundishwa moja kwa moja na Nikolai tena kwa mkono wake mwenyewe, alimtengeneza kwa misingi mikali mwanaume huyo ambaye alikuja kuwa binadamu hatari kwa sababu alikuwa anaifanya kazi kwa uchungu hususani kila alipokuwa anakumbuka maisha ambayo alikuwa ametokea. Miaka mitatu na nusu ilimfanya kuwa jabari la kutisha ambalo kila mwenzake ambaye alikuwa anye kwenye mafunzo hayo aliaanza kuliogopa. Joeli alitengenezwa akaiava haswa zaidi ya matarajio ya mwalimu wake na ndipo akapewa jina na utambulisho mwingine wa Yohani Mawenge ili asije kujulikana kwa mtu yeyote yule.

UKURASA WA 84 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 85

Alianza kuyaishi maisha yake kama Yohani ambapo baada ya kuhitimisha mafunzo alirudi tena mtaani kwake, alikuwa amebadilika na utambulisho wake mpya hakuna mtu ambaye alikuwa akimfahamu tena Yohani. Kurudi kwake hakukuwa kwa ajili ya wema, bali alirudi ili kulipa kile kisasi ambacho aliwahi kuambiwa na Nikolai kwamba alitakiwa kuja kumuua mwanamke huyo kwani kwa baadae ndiye ambaye angekuja kuwa udhaifu wake mkubwa, mapenzi huwa hayafi kirahisi huenda kuna siku angekuja kumkumbuka tu lakini hakutaka kuua kinyonge hivyo kumuua pekeyake, alihitaji kuua wote ambao walimletea maumivu ndipo akaanza kumpoteza mmoja mmoja kwa wale wote ambao waliwahi kumuumiza akiwa na mkewe, hata marafiki zake ambao waliwahi kufanya mapenzi na mkewe aliaua wote kisha akamalizia na mwanamke huyo ambaye aliikata shingo yake akakitupia kichwa juu ya bati mwili akiutupia chooni.
Kila ambaye aliliona tukio hilo aliogopa mno na kudai ndilo tukio la kikatili zaidi kuwahi kutokea duniani. Watu walianza kuogopa kuishi Tandale kwa tumbo kutokana na mambo ambayo yalikuwa yametokea, mauaji ambayo yalitokea ndani ya mitaa ile yalikuwa ni ya kutisha kiasi kwamba baadhi ya watu walihama. Yohani baada ya kutekeleza hilo alitoweka eneo hilo na kuapa kutokuja kurudi tena ndani ya hiyo mitaa na huo ukawa mwanzo wa maisha yake mapya kabisa ambapo alitakiwa kwenda Bambali huko Senegal.

BAMBALI, SENEGAL
Ni kijiji ambacho kinapatikana umbali mrefu kutoka ulipo mji mkuu wa nchi ya Senegali Dakar. Ni kijiji chenye maisha ya hali ya chini sana kwa sababu ya aina ya maisha ambayo wanaishi watu wa huko, wengi ni wale watu wa maisha ya hali ya chini mno, ubovu wa huduma za kijamii na ukosefu wa miundombinu bora ni moja kati ya chanzo kikali cha ugumu wa maisha kwenye hayo maeneo. Bambali ni miongoni wa vitovu vya umaskini ndani ya nchi hiyo, uchumi wake ni wa chini mno kiasi kwamba wengi mlo wao huwa ni mmoja na kwa wachache huwa wanakula milo miwili kwa siku nzima.
Mitaa yake huwa imechangamka kwa sababu watu wake walishakubali kuishi kwenye hiyo hali kwa maana hawana namna ya kufanya hivyo kama ukienda huko wewe ndiye ambaye unaweza ukawasikitikia ila wao maisha hayo wanayaishi kama kawaida na wamesha yazoea. Moja kati ya shughuli kuu ambazo zinawafanya waishi huko ni uvuvi kupitia mto Casamance lakini pia vijana wengine huwa wanautumia muda mwingi kwenye kuucheza mpira wa mtaani wakiamini kwamba ipo siku wangeweza kuzitimiza ndoto zao kupitia tasnia hiyo.
Huko ndiko ambako Yohani Mawenge alitakiwa kuelekea, kulikuwa na kazi ya kwenda kumuua mwanaume mmoja aliyefahamika kama Diouf Faye. Bwana huyo alikuwa ni miongoni mwa wacheza kamari wakubwa sana ndani ya jiji la Dakar, alifanikiwa kushinda mabilioni ya pesa ila akawa anatafutwa ili aweze kuuawa hivyo akaamua kwenda kujificha huko kuilinda nafsi yake akiwa na kiasi kikubwa hicho cha pesa. Pesa zilikuwa ni nyingi mno ambazo kwa wale ambao walikuwa wanafanya biashara zao kwenye lile soko haramu walikuwa wanajua juu ya jambo hilo ila kwa wale ambao walikuwa wanasubiri taarifa za mitandao wasingeweza kuwa na taarifa nyeti kama hizo.
Taarifa hizo ziliyatekenya masikio ya LUNATIC SOCIETY na ni kipindia ambacho walikuwa wanazitafuta pesa nyingi ili kujiimarisha kila kona hivyo pesa hizo wakawa wanazihutaji kwa udi na uvumba, zaidi ya bilioni thelathini za kitanzania. Kwahiyo ikawa ni oparesheni ya kwanza ya Yohani Mawenge kwenda kulikamilisha zoezi hiyo ili waweze kumpa mkataba ndani ya jamii hiyo. Alitakiwa kwenda huko, kuhakikisha anamuua mtu huyo bila kuacha ushahidi ila kabla ya kufanya jambo hilo alitakiwa kwanza kuipata akaunti ya benki ambayo ilitumika kuhifadhia pesa hizo pamoja na namba za siri za akaunti hiyo.
Ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Yohani kusafiri kwenda nje ya mipaka ya nchi yake tena kwa kutumia ndege ila hakuwa na namna, alikuwa ana shida kubwa na hiyo kazi hivyo hakuwa tayari kumuangusha mwalimu wake ambaye alimjua kabisa kwamba alikuwa anaweza kujua popote alipo hivyo kila kit chake alikuwa anakifanya kwa umakini mkubwa isivyokuwa kawaida. Kabla ya safari alipewa maelekezo ya mhimu juu ya safari yake ili asije akafanya kosa lolote lile kwa namna yoyote ile awapo huko.
Alipanda ndege kwenda ndani ya jiji hilo ambapo alielekezwa magenge kadhaa ambayo yalikuwa yanauza silaha ndani ya jiji la Dakar kwa sababu asingeweza kusafiri na silaha akafanikiwa kuvuka nazo kwenye viwanja vya ndege. Hakuwa na papara, alisafiri kwa huko ambako alifanikiwa kupata silaha na kukodi gari kuelekea Bambali kumtafuta mtu wake ambaye alikuwa ana picha yake, mwanaume mmoja shupavu ambaye alikuwa mweusi tii.
Kutokana na ubovu wa barabara, alitumia masaa saba mpaka kufika ndani ya kijiji hicho ambacho watu wake licha ya kuwa na maisha ya hali ya chini sana bado kulichangamka mno hususani eneo ambalo lilikuwa likitumika kuuzia samaki. Mida ya jioni alikuwa kwenye msako wa kumtafuta mtu wake ambapo alilazimika kujiunga na kundi moja la vijana wavuta bangi. Alimvutia chemba kijana mmoja na kumuonyesha pesa nyingi huku akimuahidi kumpatia zote kama angempata taarifa za mtu ambaye alimuonyesha kwenye picha kwa sababu alijua vijana hao wavuta bangi walikuwa wanayajua maeneo yote ya huko na kila genge.
Ugumu wa maisha ulimfanya kijana huyo kumpeleka kwa mkubwa wake ambaye naye alipewa pesa nyingi akakubali kumuuza mtu huyo Diouf. Usiku ulipofika ndio ulikuwa muda wa kwenda kukamilisha jambo lile ambalo lilimpeleka, Faye alikuwa ndani ya jengo moja bovu lililokuwa limechoka, huko ndiko aliyaweka makazi yake na baadhi ya vijana wake. Yohani alivamia eneo lile ambapo alifanikiwa kumuua Faye na kuipata ile kadi na namna ya siri lakini wakati huo aliokuwa amekamilisha jambo lake tayari eneo hilo lilizingirwa na polisi kwa sababu taarifa za uwepo wa mgeni kwenye eneo hilo zilikuwa zimevuja.
Jambo alilolifanya ni kuua polisi wote na kukimbia, taarifa zilianza kusambaa lakini alikuwa amefanikiwa kutoweka kwenye hilo eneo na bahati ilikuwa kwake hakukuwa na kamera zozote ndani ya kijiji hicho hivyo misheni yake ya kwanza ikawa imefanikiwa, akarudi Tanzania kwa ushindi na kupewa sifa nyingi. Nikolai alijivunia kuwa na kijana kama yule, kijana ambaye aliamini angekuja kuibeba baadae ya jamii yao.
Utendaji wake mzuri wa kazi ndio ambao ulimpa nafasi ya kuja kuwa mlinzi ya msimamizi wa jamii hiyo ya siri Madam Kate, mwanamke ambaye alitengenezwa na watu hao na kuwa na mafanikio makubwa ya kibiashara ili kuhakikisha shughuli zao zote zinaenda kama zilivyokuwa zimepangwa na wao wenyewe. Hiyo ilikuwa safari ya maisha ya Yohani Mawenge waweza kumuita Joel John mpaka anafanikiwa kuwa na jina kubwa pamoja na maisha safi kiasi kwamba aliaminika sana na viongozi wake na wakati huo ndiye alikuwa mlinzi mkuu wa Madam Kate na kijana wa kuaminika zaidi kwake na haikuwa kwake tu bali kwa jamii yao yote ya siri.
Alitabasamu baada ya kutoka kwenye kumbukumbu hizo akiwa ufukweni upepo ukiendelea kupuliza kiasi cha kutokumboa Yohani. Alitumia nusu saa nzima kuzama kwenye hizo kumbukumbu zake na ndipo alipo angaza mkono wake wa kushoto, kwa mbali aliona taa ya mwanga ikumulika, alitabasamu na kuitupa Cigar yake ambayo ilibakia kupisi kidogo kuisha, alitema funda la mate na kuanza kuzitupa hatua zake kuelekea ule upande wa ule mwanga, bila shaka kuna mtu alikuwa amekuja kuonana naye hapo na muda wote huo alikuwa akimsubiri yeye.
Hatua zake zilimpeleka mpaka pembezoni mwa mwanaume mmoja ambaye alikuwa kwenye suti ya gharama, umri wake kidogo ulikuwa umeenda kuliko yeye lakini alikuwa shupavu bado. Kama kawaida mtu huyo alikuwa na cigar yake mdomoni moshi akiwa anautolea puani na kuusindikiza kwa macho ukiwa unateteketea baharini, Nikolai Gibson ndiye ambaye alikuwa ametia mguu wake kukutana na Yohani Mawenge. Huyo ndiye mwanaume ambaye alimtoa kwenye umaskini wa kutupwa na kumpa maisha, huyo ndiye alikuwa mwalimu wa maisha yake pamoja na kila kitu lakini pia huyo ndiye ambaye alimtengeneza yeye na kuwa kiumbe hatari mno hivyo alikuwa akimheshimu na kumuogopa sana kwa sababu alikuwa na taarifa zote za binadamu huyo ambaye alikuwa ana muda mchache wa kutabasamu kuliko kuua.
“Ni muda sana tangu mara ya mwisho tuonane mimi na wewe, ni imani yako kwamba kila kitu kipo safi kabisa kwa upande wako!”
“Ndiyo kiongozi kila kitu kipo sawa, umenitenga kiasi kwamba huwa hauwezi hata kunipigia simu kijana wako”
“Maisha yanatufunza namna nyingi za kuweza kuishi Yohani, muda mwingine mtu ili ujue kwamba anakupenda sio lazima awepo kila unapo hitaji wewe au akupigie simu kila siku, mtu anaye kupenda anaweza kupotea kwenye macho yako ila ukiwa unamhitaji kwenye nyakati ngumu kwako ataacha mambo yake na kujitokeza kwako. Nafurahishwa na kazi yako bora ambayo unaifanya kwa umakini hususani ila ya Uganda na hii ya juzi ya kumuua Namaki Prasad lakini sifurahishwi na bosi wako na hata wakubwa hawafurahishwi naye” aliongea mwanaume huyo aliirushia Cigar yake baharini kwani ulikuwa ni wakati wa kuongea mambo ya mhimu.

UKURASA WA 85 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 84

Joeli John, waweza kumuita Joh alipata begi la pesa, pesa ambazo hakuwahi kuwaza kuwa nazo kwenye maisha yake huku akiambiwa kwamba alikuwa anaweza kufanyia jambo lolote lile ambalo angelitaka yeye. Alijihisi kuchanganyikiwa lakini hakuwa na namna kwa sababu pesa zilikuwa zake na aliruhusiwa kuzitumia kwa namna atakayo yeye, baada ya mtu ambaye alimletea pesa kuweza kuondoka, yeye alikimbia kuelekea kwenye kituo cha daladala, alipanda daladala akiwa ndiye binadamu mwenye furaha zaidi duniani kwa siku hiyo.
Safari yake ilimpeleka mpaka SHOPPERS, huko alienda kufanya manunuzi ya nguo mpya na za gharama kubwa. Alifika eneo hilo ambalo lina maduka mengi makubwa ya vitu vitu vya gharama, kuingia hapo kununua bidhaa kama nguo unatakiwa uwe ni mtu ambaye una uhakika wa milo mitatu ndani ya jiji hili na hauwazii kodi mara kwa mara mama mwenye nyumba anapo ipiga simu yake kwenda kwako. Hata badhi ya wahudumu walibaki wanashangaa, mteja ni mfalme ndiyo lakini hali yake ilikuwa ya kushangaza ila hata wachache ambao walimhoji hususani wateja wenzake kuhusu hali yake alidai kwamba alikuwa kwenye machimbo ya madini ila alikuwa amerudi zake mjini sasa.
Alinunua mavazi ya gharama na kuhitaji kuonyeshwa zilipo sehemu za gharama za kwenda kufanyiwa usafi hususani kuogeshwa na warembo pamoja na kufanyia masaji kwenye mwili wake, pesa ilikuwepo yanini ajitese Joel? Ulikuwa ni muda wake wa kuyafaidi maisha bhana pesa zilimkubali ndani ya jioni moja tu pekee. Kijana huyo alibadilika mwonekano wake ndani ya saa moja tu, kama ungebahatika kuonana naye halafu ukaambiwa kwamba alitoka kwenye maisha ya kimaskini basi nafsi yako isingekubaliana na hiyo hali kwani ungekuwa moja ya watu ambao wangegoma kukubali.
Safari yake iliishia Serena hoteli, alichukua chumba cha bei kubwa huku akihitaji kutafutiwa mrembo mkali zaidi ndani ya eneo hilo ambaye alitakiwa kukaa naye usiku huo na kama angempenda basi angempa ofa nyingine ya kuendelea kuwa naye usiku uliokuwa unafuata. Hoteli hiyo ya nyota tano alikuwa akiiona tu kwenye runinga hususani wakati wafanya biashara wanafanya mikutano yao na wasanii wakubwa, yeye alikuwa anaziishi moja ya ndoto zake usiku huo. Aliletewa mwanamke mmoja mrembo haswa, alikuwa ni Mhabeshi yule, unaijua Ethiopia wewe? Mhabeshi ikawa halali yake kuyadhalilisha mashuka na yalikoma usiku ule, mwanaume yule alikuwa amepania kufanya mapenzi na mwanamke mrembo kama huyo na aliapa siku akimpata basi angenyooka na usiku huo aliyadhihirisha maneno yake mpaka mhabeshi hakutaka kumuacha mwanaume huyo kwa show ambayo alimpatia.
Joeli alijiona mjinga mno alipo jitazama kwenye kioo, alikumbuka ni jana yake tu jioni alitaka kujiua kwa sababu ya mwanamke! Tena mwanamke wa kawaida tu huenda ni ugumu wake wa maisha ndio ambao ulimfanya amuone mrembo. Alijicheka na kujitia kibao, yaani Joeli mimi ndiye nilikuwa nalia, mimi ndiye nilitaka kujiua kwa sababu ya mwanamke wa Tandale tena kwa Tumbo? Aaaah fala mimi. Alijiongelesha wakati huo alikuwa akimwangalia mhabeshi kitandani, alipewa show nzito mpaka akapitiwa na usingizi. Mwanamke huyo alilala kihasara kiasi kwamba hata mwili wake ulikuwa umejiachia wazi kabisa hivyo akawa anaona kila kitu, ulikuwa ni uumbaji bora zaidi wa kiumbe kinacho itwa mwanamke kuwahi kuuona kwa macho yake. Mhabeshi alikuwa mrembo mpaka alihisi mama yake alifanya sifa kumzaa mwanamke huyo, aliivua nguo yake ya ndani na kurudi tena kitandani kuweza kuufurahia ulimwengu wa uumbaji.
Joeli maisha yalikaa upande wake, alikula starehe kama amechanganyikiwa. Baada ya wiki moja alirudi Tandale akiwa na gari kali, alikuwa amevaa mavazi ya gharama kali mno ili kwenda kuwanyoosha wanazi wake. Baada ya kufika mtaani alikuwa gumzo Joeli, kila mtu alidai kumfahamu yeye na kuwa rafiki yake, kila mtu alihitaji ukaribu na kijana huyo lakini hakuwa na hizo shobo, heshima ilitakiwa kufuata mkondo wake. Tena hakurudi mwenyewe, alirudi na wale watunisha misuli wa gym ili asisumbuliwe na wapenda kushobokea watu. Taarifa ile ilimfikia Tina aliyekuwa mkewe, mwanamke huyo kusikia habari hiyo alitoka anakimbia kiasi kwamba hata nguo zilikuwa zinamdondoka kumuwahi Joh wake ambaye aliambiwa kwamba kawa tajiri ghafla.
Wanawake na pesa tena? Ni kama Messi na mpira wake, mwanamke huyo hakukumbuka kwamba siku kadhaa nyumba alimdhalilisha Joeli mbele ya wanaume wawili waliokuwa wakifanya naye mapenzi kwa fujo tena mbele yake, eti siku hiyo alikuwa akimkimbilia mmewe, hahaaha wanawake wanawake! Mwanamke huyo licha ya kufika hapo na kushuhudia maajabu ya dunia, Joh mfanya vibarua alikuwa akilindwa lakini aliishia kuwa kama Mussa. Mussa aliambiwa kwamba utaiona nchi ya ahadi ila hautafanikiwa kuingia, hata Tina hakufanikiwa kumgusa mwanaume huyo ambaye alikuwa na ghadhabu naye kubwa, jambo hilo alilihifadhi kwenye moyo wake kama kiporo.
Licha ya Tina kulia na kugala gala akijifanya kujutia kitendo chake, Joeli hakuwa na muda na mwanamke huyo baradhuli. Aligawa pesa kwa baadhi ya watu mtaani hapo kisha akatoweka na watu wake akimuacha mwanamke huyo anaushangaza mtaa akijilalamisha kwamba alikuwa akimpenda mno mumewe na hakuwa tayari kumuacha, watu wakabaki wanamshangaa kwa sababu kila siku Joh alikuwa akisalitiwa eti kawa na pesa ndipo kampenda ghafla? Alidhalilika mtaani hapo binti huyo.
Joel alijisahau mno, alikula bata mpaka mji ukamshangaa lakini alisahau kwamba alipewa mwezi mmoja tu pekee. Huenda ni utamu wa yale maisha mapya ndio ulimfanya asikumbuke kwamba muda wake ulikuwa unakaribia kufika hivyo akawa anaendelea kuponda raha mpaka siku moja ambayo alipokea ugeni, ugeni ambao haukuwa mgeni kwake. Alikuwa baharini kwenye boti na warembo kumi akiponda raha ndipo ambapo alishangaa boti hiyo inageuzwa uelekeo na kuelekea ndani zaidi ya bahari jambo lililomfanya kumfuata nahodha amwambie sababu ya kwenda kinyume na yeye ambaye ndiye alikuwa anamlipa lakini nahodha huyo alimwambia kwamba muda wake ulikuwa umeisha hivyo kuna mtu alihitaji kuonana naye.
Boti hiyo ilifika mahali ambako kulikuwa na meli ilipaki hapo, wanawake wale walirudishwa kuendelea na mambo yao huku yeye akiingia ndani ya meli hiyo ambayo bila shaka ilikuwa imepaki kusubiri tarehe yake ya kuondoka. Ndani ya meli hiyo alikutana na yule mwanaume ambaye ndiye alimletea lile begi la pesa, alishtuka na hapo ndipo akagundua kwamba siku zake zilikuwa zimeisha kama ambavyo aliahidiwa. Alishangaa mtu huyo kumpata kirahisi lakini mwanaume huyo alimahkikishia kwamba mtu anapokuwa anazipata pesa kwa mara ya kwanza hususani kwenye mazingira ambayo hata yeye mwenyewe hakuyatarajia basi lazima atataka kutamba kwamba hivyo hata ukihitaji kumtafuta hautumii nguvu kwani anakuwa maarufu ghafla lakini mbali na hilo alimhakikishia kwamba alikuwa akimfuatilia kila hatua ambayo alikuwa anaipiga.
Ndipo alipo mkalisha chini na kumpa mpango mzima wa lengo kubwa la kukutana naye, aliahidiwa maisha safi lakini pia alikuwa anaruhusiwa kutojiunga nao kama akiweza kulipa zile pesa ambazo alizitumia kula starehe kwa ule mwezi mzima. Angeitoa wapi tena pesa ya kulipa Joh! Kukubali ndiyo ikawa njia sahihi kwake, hata hivyo bila kupewa sharti hilo bado alikuwa tayari kujiunga na watu hao kwa sababu ni njia pekee ambayo ingemuweka mbali na umaskini.
Alijiunga na chuo cha siri ambacho kilikuwa chini ya mwanaume huyo aliyejulikana kwa jina la Nikolai Gibson. THE FUTURE PROJECT, ndio ambao ulikuwa mpango rasmi wa kutekelezaji wa kuwafua vijana hao kwenye chuo hicho akiamini kwamba vijana hao ulikuwa ni mpango wa baadae wa jamii yao ya siri. Walitengenezwa vijana wengi shupavu huko ambapo waliokuwa wanaiva walikuwa wanafanyiwa majaribio kwa kupewa kazi za kuua kisha wanasajiliwa moja kwa moja na kuanza kupata malipo makubwa ambayo yaliwafanya waipende kazi yao na kuwa waaminifu lakini kulikuwa na sheria kali mno kiasi kwamba ambaye alikuwa anaenda kinyume na sheria hizo alikuwa anakufa na mkosaji aliwekwa wazi ili wengine wajifunze kwake.
Joeli John ndilo lilikuja kuwa zao bora zaidi kwenye mpango huo kwa sababu yeye alifundishwa moja kwa moja na Nikolai tena kwa mkono wake mwenyewe, alimtengeneza kwa misingi mikali mwanaume huyo ambaye alikuja kuwa binadamu hatari kwa sababu alikuwa anaifanya kazi kwa uchungu hususani kila alipokuwa anakumbuka maisha ambayo alikuwa ametokea. Miaka mitatu na nusu ilimfanya kuwa jabari la kutisha ambalo kila mwenzake ambaye alikuwa anye kwenye mafunzo hayo aliaanza kuliogopa. Joeli alitengenezwa akaiava haswa zaidi ya matarajio ya mwalimu wake na ndipo akapewa jina na utambulisho mwingine wa Yohani Mawenge ili asije kujulikana kwa mtu yeyote yule.

UKURASA WA 84 unafika mwisho.
Ubarikiwe mno kiongozi, wacha ninogeshe safari yangu sasa ya kurudi home
 
Back
Top Bottom