Simulizi ya kijasusi: Nafsi zilizotelekezwa

Simulizi ya kijasusi: Nafsi zilizotelekezwa

Nadhani hauna wachangiaji huu uzi hivyo huwa nausahau mara kwa mara....

Huwa naukumbuka tu wa IDAIWE MAITI YANGU...

Leo nitajitahidi tusome angalau episodes hata 5 ✍️
Ni rahisi sana ku pata attention ni kurekebisha tu approaching style yako. Mfano badala ya kutuma kwa wiki mara moja jaribu kufululiza hata kwa wiki mbili tu kutuma kila soku episode moja alafu utupe mrejesho ila hii ya mara moja moja kwa wiki inachosha Sema basi tu
 
Ni rahisi sana ku pata attention ni kurekebisha tu approaching style yako. Mfano badala ya kutuma kwa wiki mara moja jaribu kufululiza hata kwa wiki mbili tu kutuma kila soku episode moja alafu utupe mrejesho ila hii ya mara moja moja kwa wiki inachosha Sema basi tu
Ushauri wako ni mzuri ila hiyo approach ambayo unaisema nimeifanya kwa muda mrefu sana na ndiyo nilianza nayo tangu siku ya kwanza naleta simulizi yangu ya kwanza kuiandika ambayo wengi husema ndiyo bora zaidi ULIMWENGU WA WATU WABAYA.....

So naelewa mkuu.
 
Sawa, nilihisi ulisha potezewa nikausahau kabisa.....

Nimeukumbuka baada ya kuona notifications zake
Hapana mkuu hii simulizi kali sana. Tupo tunaifatilia, mimi huwa sipendi sana kutoa comment simulizi ikiwa haijaisha na mara nyingi huwa sisomi ambazo hazijafika mwisho ila bidii yako ya kuweka ndo ilinishawishi niusome uzi wako.
Baada ya kuona uko kimya sana uzalendo ukanishinda ikabidi tukuombe utukumbuke.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana mkuu hii simulizi kali sana. Tupo tunaifatilia, mimi huwa sipendi sana kutoa comment simulizi ikiwa haijaisha na mara nyingi huwa sisomi ambazo hazijafika mwisho ila bidii yako ya kuweka ndo ilinishawishi niusome uzi wako.
Baada ya kuona uko kimya sana uzalendo ukanishinda ikabidi tukuombe utukumbuke.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa kiongozi shukrani.

Saa 4 naweka episodes 5 hapa.
 
Sawa, nilihisi ulisha potezewa nikausahau kabisa.....

Nimeukumbuka baada ya kuona notifications zake
Hakuna andiko lako linaweza potezewa mkuu maana yote ni 🔥🔥🔥. Tunafuatilia haswa kila sentensi na nukta
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 76

“Cersie Mhina, Cersie Mhina, Cersie Mhina” alitaja mara tatu mfululizo akiwa bado anatetemeka, alitamani hata kuupata ukichaa sio kuongea na Edison, mwanaume huyo hakujua mambo ya kupaka boda hivyo kila swali lilikuwa na athari zake kwa kuchelewa kujibiwa.
“Unamaanisha Cersie Mhina huyu mfanya biashara mkubwa wa gesi na mitandao ya simu?”
“Ndiyo, ndiyo mwenyewe. Huyo ndiyo bosi wetu”
“Huyu ndiye kiongozi wa LUNATIC SOCIETY”
“Ndiyo ni yeye”
“Una uhakika?” aliuliza kwa sauti kali ya mamlaka kama mtu ambaye anataka kuwewuka.
“Ndiyo ndiyo, nina uhakika na hilo, huwa anaishi kwenye maisha ya siri na ya kuigiza mbele za watu kiasi kwamba hakuna mtu anaweza akamhisi kwa lolote ukizingatia ni mtu ambaye anajitoa kwa jamii sana kiasi kwamba huwa anatumia nafasi hiyo kuweza kuficha mabaya yake na juzi tu hapo ametoka kuingia makubaliano mengine ya kibiashara na raisi wa Bulgaria Hristo Radoslav”
Edison alisimama akiwa anacheka, alicheka kwa sauti na nguvu kali mithili ya mtu ambaye alikuwa amechanganyikiwa. Hakucheka kwa sababu alifurahia jambo hilo, alicheka kwa uchungu mkali na hasira ambazo hakujua aziweke kwenye kitu gani kuweza kufananisha na yale maumivu ambayo alikuwa anayapitia. Aliitoa simu yake, akaingia kwenye mtandao kuweza kuangalia picha za mwanamam huyo.
Alikuwa ni mama yake mzazi wa kumzaa kabisa aisee, Edison alikuwa kwenye uchungu mkali kwa sababu mama yake ndiye ambaye alikuwa chanzo cha hayo yote. Mama yake ndiye alikuwa moja kati ya maadui zake wakubwa, alikuwa akimfahamu sana mfanya biashara huyo kwa sababu alikuwa maarufu kila kona ya nchi, sasa kugundua kwamba ndiye mama yake mzazi yule ambaye alimtelekeza kule Mbeya ilimuuma sana. Chozi lilikuwa likimshuka taratibu kwenye uso wake, kichwa chake kilikuwa kwenye wakati mgumu isivyo kawaida, hakujua afanye nini ama achukue hatua gani. Kuna nafsi ilikuwa inatamani kukutana na mwanamke huyo lakini kuna nafsi pia ilikuwa inaogopa, angeongea nini na mama yake wakati wao ni maadui wa kutupwa? Hilo huenda halikumtisha sana ila jambo ambalo lilikuwa linamuogopesha ni kwamba ni yeye ambaye alikuwa anatakiwa kumuua mama yake kwa mkono wake mwenyewe.
Aliyakumbuka maisha ambayo aliyaishi huko nyuma, alikumbuka jinsi ambavyo alikuja kubahatika kupata ndoa ambayo ingemfanya kuwa baba kwa mara ya kwanza kwenye maisha yake lakini jambo hilo lilishindikana. Sanjari na hilo, mwanaume huyo aliyaishi maisha magumu kama mkimbizi kwenye nchi yake mwenyewe aliyo zaliwa na kuifanyia kazi kwa moyo wake wote lakini hayo yote yalisababibishwa na mwanamke ambaye alim-beba yeye tumboni kwake kwa miezi tisa. Ni jambo ambalo ni dogo likisimuliwa kwenye hadithi ama kwenye tamthilia mbali mbali ila ni jambo la hatari ukiwa unaliishi kwenye maisha ya kweli.
Edison alitamani angekuwa anasimuliwa hadhithi ama iwe ndoto, alitamani kama angekuwa anaangalia ni zile thamthilia za wazungu akijua kwamba ikiisha itakuwa ni stori tu lakini sio ukweli, hisia zake hazikuweza kubadilisha ule ukweli kwamba hilo lilikuwa linamtokea yeye. Alipiga makelele makubwa akiwa anapiga ngumi ukutani, sehemu ambayo aliipigiza ngumi hiyo palibonyea, hiyo ngumi haikutakiwa kuingia kwenye mkono wa mtu kwa sababu ingekuwa hatari kwenye kiungo ambacho ingekigusa. Mwishowe alicheka sana, alicheka mpaka akakaa chini kabisa jambo ambalo lilimtisha Saimon akiwa amechakaa sana kwa mateso na maumivu kiasi kwamba hata mwili wake ulikuwa unaelekea kupoteza nguvu zote.
Kuogopa kwake kulisababishwa na sababu kubwa kamba alijua kabisa hizo hasira zilitakiwa kuishia zote kwenye mwili wake. Edison alimrudia mtu huyo akiwa anamtazama vizuri kwenye uso wake, hakuwa akicheka tena wala machozi hayakuonekana mbele yake zaidi ya mwanaume ambaye alikuwa na ghadhabu kama sio uhasama na wanadamu ambao walikua kinyume na yale matakwa yake. Alifunua ile bandegi kwenye kile kifua cha Saimon ili waendelee walipokuwa wameishia.
“Nahitaji unitajie mambo ambayo bosi wako anajihusisha nayo, biashara zake zingine, watu ambao anafanya nao kazi, udhaifu wake, uimara wake upo wapi na anakutana mara nyingi na akina nani na kwa sababu zipi” zilikuwa ni taarifa nyingi ambazo zilikuwa zinahitajika na Saimon alitakiwa kuzitolea ufafanuzi kwa sababu alikuwa anajua kile ambacho kingetokea kama asingelifanya jambo hilo.
“Biashara kubwa ambazo anazifanya zinaendeshwa pale MHINA PLAZA ambalo ndilo jengo lake kubwa. Mipango yake yote huwa inafanyika mle ndani na hata mipango yake mikubwa yote anaipanga pale. Jambao ambalo silijui mpaka leo ni mahali ambapo anaishi pamoja na watu ambao nilisikia kwamba ndio viongozi wa juu zaidi, hao niliwahi kusikia wakitajwa mara moja tu ila sijui lolote na ukikutwa unaongelea habari hizo unauawa” alimeza mate na kuendelea kuongea;
“Naweza kusema kwamba hii ndiyo jamii yenye unguvu zaidi kwa ukanda wa Afrika mashariki wote kwa sababu una viongozi wakubwa ndani yake, wanafalsafa wakubwa, maprofesa wa vyuo, wanasheria, viongozi wa ngazi za usalama nchini lakini pia hata viongozi wakubwa wa kiserikali na sio Tanzania tu bali ukanda mzima wa Afrika ya Mashariki na mpango wa sasa ni kuvuka mipaka na kwenda nje ambapo mpango umeanzia kwa raisi wa Bulgaria.”
“Hivyo naweza kusema kwamba ana watu kila sehemu ambayo unaijua wewe ndiyo maana hakuna mahakama ambayo inaweza kuhukumu kesi yake wala hakuna kiongozi mkubwa ambaye anaweza kumgusa kwa namna yoyote ile kwa sababu lazima afe, hata Ikulu ipo chini yake. Ukiachana na watu alio nao lakini pia biashara yake kubwa ambayo inampatia mabilioni ya pesa ni uibwaji wa dhahabu ambapo migodi mingi hususani ya kiserikali viongozi wanakula naye, yeye ndiye anachukua dhahabu na kwenda kuziuza kisha gawio linapita kwa wanao husika na ukienda nje na masharti yake basi anakuua hata ukiwa kiongozi wa juu kiasi gani”
“Kwa nafasi ambayo nipo nayo mimi kuna mambo mengi siyajui kuhusu yeye, kama udhaifu wake, uimara wake siujui sana kwa sababu hata kukutana huwa napewa hiyo nafasi mara moja moja tu ila kuna mtu mmoja ambaye ana taarifa zake zote na ndiye kama mkono wake wa kulia kwa sababu akitaka ifanyike shughuli ya hatari na kwa uhakika zaidi basi ni lazima amtumie yeye.” Edison alikuwa makini kusikiliza kauli hiyo kutoka kwa huyo mwanaume.
“Joeli John”
“Whaaat?”

“Jina lake huyo mtu anaitwa Joel John ila wengi huwa anawahadaa kwa jina la Yohani Mawenge. Ni binadamu hatari sana, sio mtu wa kuomba kukutana naye kwenye maisha yako kwa sababu alishatoka kwenye ubinadamu akawa mnyama” Edison alibaki ametulia tu, hiyo dunia ya michezo kama ambayo waliicheza yeye na Jack hawakuijua wao tu bali kuna watu wengine kitambo tu walikuwa ndani ya dunia hiyo.
“Unamfahamu kwa sura yake halisi?”
“Ndiyo, ni mzaliwa wa Tandale huko japo historia yake imepindishwa pindishwa “
“Unaweza kunionyesha picha yake?”
“Simu yangu kama unayo nakuonyesha”
“Simu yako haipo, kama hiyo picha yao ilikuwa kwenye simu yako unaweza kutumia simu yangu kunionyesha picha ya huyo mtu kwa sababu lazima itakuwa kwenye google drive”
“Sawa” aliulegeza mkono mmoja wa mwanaume huyo na kumpatia simu yake akiwa makini kumuangalia alichokuwa anakifanya ili asije akatoa taarifa kwa watu hao juu ya kukamatwa kwake. Ilitumika dakika moja tu kukamilisha zoezi zima, aligeuziwa simu kuonyeshwa sura ya mwanaume huyo. Kwa mara ya kwanza alikuwa anaiona sura ya binadamu ambaye alitakiwa kumpata ili kukamilisha moja kati ya mipango yake mkubwa, sasa alikuwa anampataje na aliambiwa kwamba alikuwa ni miongoni mwa vile viumbe hatari ambavyo bado vinaishi? Alijitumia picha hizo kwenye simu yake nyingine, simu ambayo ilitumika kufanyia kazi hiyo aliirushia chini na kuivunja vunja kwa mguu wake na uzuri ni kwamba haikuwa na laini bali ilikukuwa ikitumia WIFI.
“Huyu mtu unajua anapo ishi au anako patikana?”
“Hapana, huyu muda mwingi ndiye ambaye huwa anakuwa na bosi”
“Ni njia ipi ambayo huwa inatumika kuwaingiza watu kwenye jamii hii?”
“Njia kuu ni mbili, mtu akiwa ana umuhimu wa kuwepo huko basi wanatumia pesa ama nguvu. Unaahidiwa kuishi maisha mazuri na kweli unayaishi lakini ikifika wakati wa wewe kulipa pia wanachukua chochote ambacho watakihitaji kutoka kwako” Edison humo ndani, bila shaka alienda kwenye gari yake ambako alirudi akiwa na kalamu ya wino pamoja na karatasi.

UKURASA WA 76 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 77

“Nahitaji uniorodhoshee hao watu wake wa pembeni na mahali ambamo wamepatikana bila kukosea hata herufi moja” Saimon hakuwa na namna, ilikuwa ni lazima afanye hivyo. Baada ya kukamilisha hilo hakuwa na kazi naye tena, alichomoa ule upanga chini na kuusokomezea juu ya utosi wa Saimoni bila huruma, aliuzamisha mpaka ndani, Saimon alikuwa akitetemeka huku damu zikiruka juu na zingine zikimtoka mdomoni. Aliuchomoa na kuuzamisha kwenye koromeo lake ambalo alilichana chana vibaya mpaka pale ambapo Saimon alitulia kabisa na kuyapoteza maisha yake.
Alipokuwa analitekeleza tukio hilo kuna watu wengine wawili waliweza kulishuhudia, Nicola pamoja na baba yake Damasi, mzee Kazimoto mwenyewe. Alikuwa amefanikiwa kumteka mzee huyo na kufika naye hapo, huyo ndiye ambaye angemfanya ampate mtu wake kirahisi kwa sababu katika vijana ambao aliwachagua kufanya nao kazi alikuwa ni Damasi. Mzee kazimoto na utu uzima wake, aliwahi kushuhudia maiti nyingi kwa sababu alishiriki mazishi mengi na kuziaga maiti nyingi za vifo mbali mbali kama ajali, kujinyonga, kuuawa na zingine nyingi ila ya siku hiyo ilikuwa tofauti.
Aina ya kifo ambacho aliona mtu huyo anakipitia kilimtisha, hakuamini kama wanadamu walikuwa wamefikia hatua ya kuwa wakatili namna hiyo. Alikuwa anatetemeka wakati ambao Nicola alimtaka mzee huyo asogee kwenye kiti ambacho hakikuwa mbali na ile maiti, Nicola mwenyewe ni kama alikuwa ameanza kumuogopa Edison, hakuonekana kuwa mtu wa kuzoeleka kijinga kwa uhatari ambao aliuonyesha mble ya macho yake ukijumlisha na zile aibu za kuvuliwa nguo zake zote akatoa penzi, ndiyo kabisa hakuwa na ujasiri wa kumuangalia machoni mwanaume huyo.
“Karibu mzee wangu, pole kwa safari ya ghafla na ya lazima usiku huu ambao huenda ulitakiwa uwe umelala ila hakukuwa na namna kwa sababu ilikuwa lazima iwe hivi. Mimi naitwa Edison Christian, ni mtoto wa mwanasayansi wa zamani wa nchi hii Christian Edison na mwenzangu hapa anaitwa Nicola Aidan Semzaba, baba yake ni miongoni mwa wanasheria nguli zaidi kuwahi kutokea kwenye taifa hili lakini ndiyo hivyo wanadamu waliyakatisha maisha yak” Edison alijitambulisha mzee huyo akiwa anaketishwa kwenye kiti. Pembeni yake ilikuwepo ile maiti ya Saimon ambayo kiuhalisia ilikuwa ikimnyima raha kabisa akawa anageuka kila wakati.
“Nakufahamu wewe, najua historia yote ya maisha yako kwa sababu habari yako ilikuwa ndiyo habari maarufu zaidi hapa nchini kwa nyakati mbili tofauti, mara ya kwanza ulikuwa na kesi kubwa ya mauaji lakini mara ya pili ni baada ya wewe kuonekana ndiye mwanasheria ambaye ulikuwa unaishi kwenye sura nyingine tofauti na hii ya leo”
“Na wewe unaziamini hizo taarifa mzee wangu?”
“Naziamini kwa sababu zimethibitishwa mpaka na ofisi ya raisi”
“Kwahiyo raisi akithibitisha kitu basi ni cha kweli?”
“Ndiyo”
“Na vipi kuhusu mwanao? Taarifa zake kwa sababu ni za kwei juu ya kile ambacho anakifanya umewahi kuzishabikia namna hiyo?” hakujibu mzee Kazimoto, aliguswa sehemu mbaya.
“Mzee tusipoteze muda kwa sababu imekuwa siku ndefu kwangu, jambo ambalo limekuleta hapa nataka umpigie simu mwanao aweze kufika ndani ya eneo hili saivi”
“Ili umuue kama ulivyo muua huyo kijana hapo? Hapana”
“Mzee wangu nimekuita kistaraabu na natumia njia sahihi kwako kwa sababu sina uhakika kama unastahili kama ambayo ameyapitia huyo bwana mdogo ambye amekufa hapo. Mimi nimepoteza kila kitu kwenye maisha yangu ikiwemo familia yangu, mke wangu, mtoto, watu wangu wa karibu wote lakini pia nimepewa kesi isiyo yangu ambayo ilinifanya niishi kama mkimbizi ndani ya nchi ambayo nilipaswa kuilinda. Mwenzangu hapo yeye aliuliwa baba yake mzazi lakini kaka yake alikuwa ni moja ya makomando wenzangu ambao tulitakiwa kufa wote na kwa bahati mbaya yeye alikufa mimi nikiwa kiongozi wake. Naye walimlisha sumu akawa anaishi kwa kujua mimi ndiye muuaji hivyo akawa ananisaka ili kuweza kuniua lakini baadae akagundua kwamba mimi sikuwa mhusika”;
“Alipo upata ukweli ndipo alipofanya maamuzi sahihi ya kuja hapa kuungana na mimi ili kuitafuta haki yetu. Mimi nilitakiwa kuua wote ambao walihusika na hili jambo lakini kuna mtu akanishauri kwamba naweza kumtumia mwanao kulimaliza hili nikiingia naye makubaliano. Nikuhakikishie kwamba mwanao ni miongoni mwa watu ambao wanatakiwa kufa kwa namna yoyote ile ila nataka nitoe nafasi ya dhahabu kwake ambayo baada ya jambo hili kuisha yeye nitamuacha hai lakini kama itashindikana kufanyika hivyo basi mimi sitakuwa na namna nitamtafuta mwenyewe na kumuulia mbele yako. Mwenzake amenipa listi ya majina yao na mahali wanako patikana japo mwanao anaonekana ni mtu wa kuhama hama hivyo atanipotezea muda. Kwahiyo uchaguzi ni wako, umpigie simu aje haraka hapa kwa kumwambia umetekwa ili nimpe kazi ya kufanya au nimtafute mwenyewe na kumuua” Edison alikuwa siriasi sana wakati anayawasilisha maneno yake huku akiwa anampatia simu mzee huyo.
Alimsogelea Nicola
“Uko sawa mama?” Nicola hakuongea kitu, alimkimbilia Edison na kumkumbatia huku akiwa anamwaga machozi, yale maneno ambayo Edison aliyaongea pale, yalimkuna na kkumkumbushia familia yake. Alijihisi kuwa salama na mwenye amani juu ya kifua cha mjomba hicho.
“Hautakiwi kurudi tena kule kwa sababu wanajua kama umewasaliti na Saimon alikuja kukuchukua kwa nguvu ili ukawapatie wanacho kihitaji kisha wakuue” maneno ya Edison yalimshangaza kwani hakutarajia jambo kama hilo lakini wakati huo mzee Kazimoto hakuwa na namna zaidi ya kufanya kile ambacho aliagizwa kukifanya kwa kumpigia simu Damasi ili naye kwa mara ya kwanza aweze kukutana na mtu ambaye walikuwa wanamsakama huku akiwa na chaguo mwenyewe la kuishi ama kuamua kufa.

Saa tisa na dakika arobaini na tano askari polisi mmoja wa kituo cha Urafiki ambaye alikuwa anaishi Kimara Baruti alikuwa akirejea nyumbani kwake akitokea kula starehe kwa sababu ilikuwa ni ijumaa ya kuamkia wikiendi hivyo baada ya kutoka kazini alipitia Rombo kula mbuzi choma. Hakuwahi kurudi kwa sababu kesho yake haikuwa siku ya kazi hivyo aliamua kuitumia nafasi hiyo kuzila raha za dunia mpaka ulipo fika wakati huo ndipo akaamua kurudi nyumbani kwake ili akapumzike.
Hakuwa na haraka ya kurudi nyumbani hivyo alikuwa kwenye mwendo wa kawaida tu akiwa anaendelea kuimba mziki ambao ulikuwa unasikika taratibu kwenye masikio yake kupitia redio ya gari yake. Alipofika Ubungo alipita upande wa juu ambako ndiko alishangazwa na kile ambacho alikuwa anakiona mbele yake, ulikuwa ni mwili wa mtu ukiwa umetapakaa damu ambayo iligandiana ndani ya mwili huo. Alishuka na kusogea eneo hilo ambalo mwanga wa taa ulikuwa mkubwa kiasi kwamba alikuwa anaona kia kitu kwa usahihi, karibu na ukingo wa kuta moja ya barabara hiyo ndipo mwili huo ulipokuwepo.
Alipiga simu kwa wenzake kituoni kuwapa taarifa, hata ile hali ya kulewa ambayo alikuwa nayo ilipotea ghafla kwenye kichwa chake ilipotea. Baada ya kuhakikisha ameifikisha taarifa alisogea taratibu ulipokuwepo mwili na kuuangalia kwa umakini, hiyo sura aliifahamu vyema kwa sababu jana yale tu ilitoka kuwa maarufu kwenye kile kona ya nchi, kila upande watu walikuwa wakiliimba jina hilo kwa sababu alikuwa anafahamika sana. JACK THE LAWYER ndiye ambaye mwili wake ulikuwa hapo akiwa kwenye sura ambayo alijitambulisha nayo jana yake kama Edison.
Habari ya kifo cha mwanasheria huyo ilianza kusambaa kwa kasi kubwa kiasi kwamba waandishi wa habari walifika kwenye eneo hilo na kuanza kupiga picha. Taarifa hizo pia zilimfikia mlengwa ambaye alihitaji plani yake kufanya kazi kwa wakati huo Lionela Philson kama alivyokuwa amempa mpango mheshimiwa raisi. Alifika hapo na timu yake ambapo aliwaacha waandishi wa habari wachukue picha ndipo akaondoka na huo mwili huku eneo la tukio likitengenezwa kuwa CRIME SCENE na yule askari polisi ambaye alifanikisha zoezi hilo kupewa pongezi za dhati. Wakati anaondoka pale ndio muda ambao alipiga simu kwenye zile media ambazo zilikuwa zikitumika na serikali kutekeleza propaganda zao kuanza kuchapisha ile habari ambayo alimweleza raisi.
Ndani ya muda mfupi tu habari zilizagaa kila sehemu ya nchi huku watu wakiwa wanachanganywa kwani habari ambayo aliongea mwanasheria huyo ilikuwa ni tofauti na mamlaka za usalama. Maafisa usalama wa taifa walisambazwa kila sehemu wakiwemo wana usalama wa IBA, shirika ambalo llikuwa likishughulika na ule upelelezi wa ndani (Ukachero/ushushushu) lakini pia upelelezi wa nje ya nchi (Ujasusi).
Watu hao walikuwa wamepiga hatua moja kubwa ya kuanza kutatua kesi hiyo huku wakitarajia kumtafuta mhusika wa jambo hilo. Mkurugenzi aliinyanyua simu yake na kuipiga mahali, simu iliita umbali kidogo kutoka pale ambapo ilikuwepo nyumba ya Aaliyah Beka na mtu ambaye alikuwa karibu na nyumba hiyo alikuwa ni Jumapili. Alikuwa ameshika kiona mbali akiwa makini kuangaza kwenye ile nyumba kwa masaa zaidi ya matatu.

UKURASA WA 77 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 78

“Umeona chochote kipya ama kigeni?”
“Hapana bosi ila kuna muda taa zilikuwa zimezimwa lakini ilipofika saa nane kamili taa zikawashwa tena na mapazia yamezunguka kila sehemu hivyo siwezi kuona kinacho endelea ndani”
“Ondoka haraka hilo eneo kwa sababu huenda ameshajua kwamba kuna mtu anamfuatilia”
“Sawa bosi” mwanaume huyo alibeba begi lake na kuondoka kwenye hilo eneo. Bosi wake alikuwa sahihi, ndani ya nyumba hiyo Aaliyah alikuwa karibu na kumpyuta yake akiwa anamwangalia kwa mbali mwanaume huyo. Alifanya kosa kwa sababu eneo ambalo alikuwepo ndiko ambako kamera ya jengo hilo ilikuwa imeelekezewa, baada ya kuondoka Aaliyah alichungulia dirishani baada ya kuzima taa, alipoona kumekuwa shwari alienda kupumzika.

Damasi alikuwa ameelekezwa kuweza kufika eneo la tukio, kupokea taarifa ya kutekwa kwa baba yake lilikuwa ni zaidi ya pigo kwa upande wake, alikuwa akimpenda mno. Alitumia dakika arobaini tu kuweza kufika ndani ya hilo eneo, aliingia sehemu hiyo ambayo alielekezwa kuweza kufika akiwa ameshika bastola zake mbili mkononi, uso wake ulikuwa unaongea lugha nyingi ambazo zilitawaliwa na hasira ndani yake ambayo haikuwa ikielezeka.
Baada ya kuingia hapo kwanza alishtuka, kumuona Edison ambaye alidaiwa kutekwa na watu wasio julikana lilikuwa jambo la kushangaza kwake. Huyo ni binadamu ambaye walikuwa wakimsaka isivyokuwa kawaida, siku hiyo ndiye ambaye alikuwa mbele yake. Edison alikuwa ameketi kwenye kitu akiwa anamwangalia kijana huyo, bila shaka alikuwa anamkadiria kwenye mwili wake kumpima kuanzia uimara wa mifupa yake, mwili na hata uwezo wa maamuzi kichwani ili awe na uhakika kama angemfaa kwenye majukumu yake. Damasi alimuona vizuri mwanaume huyo akiwa anachezesha vidole vyake, aliwahi kupewa onyo akiwa jeshini kwamba kwenye ulimwengu wa wauaji ni watu ambao walikuwa wakidili zaidi na ishara za mwili na moja kati ya alama za hatari zaidi ni kama hizo ambazo alikuwa anazionyesha hapo Edison.
Spidi ya vidole vyake, macho yake na mwili ambao alikuwa nao ndicho kitu ambacho kilimpa mashaka kidogo Damasi, licha ya kuishi kwenye hiyo dunia ya watu wababe lakini alijua kwamba lazima kuna wale ambao wanamzidi yeye kila kitu. Hiyo haikuwa sababu ya yeye kuwa muoga kwani alikutana na watu wengi na akawaua bila shida, bastola zake alizielekezea kwa Edison wakati huo hakuwa amegeuka upande wa pili ambapo alishangaa kuuona mwili wa Saimon ukiwa kwenye kiti hauna uhai. Hakuamini kuona hali kama hiyo, Saimon alikuwa miongoni mwa watu ambao hata yeye alikuwa akiwaogopa kwa sababu alimjua kiundani mwanaume huyo alivyokuwa mtemi ila kwa wakati huo ni mwili wake tu ndio ulikuwa pale, nafsi yake ilikuwa mbali na dunia.
Namna mwili wake ulivyokuwa umefanywa, ndicho kitu ambacho kilimfanya asisimke. Aliyasogeza macho yake pembeni zaidi ndipo akamuona baba yake akiwa ameketi, alikuwa mpole kama mtu ambaye alinyeshewa mvua kwa muda mrefu halafu akaukosa moto au joto la kupunguza baridi kwenye mwili wake, aligundua kwamba baba yake alikuwa amewekewa bastola kwenye kichwa chake na mwanamke ambaye alikuwa na taarifa zake kwa sababu licha ya mwanamke huyo kuitengeneza sura yake kwa namna nyingine lakini bado alikuwa akimjua vyema kabisa. Alishangazwa na jambo la pili, kivipi mwanamke ambaye hata yeye alishiriki kumteka kule uwanja wa ndege awe hapo na mtu huyo? Swali ambalo binafsi hakuwa na majibu nalo, kufanya masiara kungemfanya ampoteze baba yake.

“Mimi nimgekuwa wewe basi ningekuwa nimetupa hizo bastola mbali mpaka sasa kwa sababu ndani ya dakika moja ijayo baba yako atakufa mbele yako na mhusika wa kifo chake utakuwa ni wewe mwenyewe” EdJr aliongea kwa sauti kavu akiwa anasimama, alitembea taratibu mpaka alipofika alipokuwa Damas, alizichukua zile bastola kwenye mikono yake kisha akatoa risasi zote na kuzitupia pembeni.
“Unathubutu vipi kumshika baba yangu mpuuzi mkubwa wewe?”
“Baba yako anajua kama wewe ni miongoni mwa watu ambao wanaua watu wasiokuwa na hatia bila sababu za msingi na kusingizia watu kesi ambazo hata hawahusiki?”
“Unataka nini?
“Kila kitu Damasi”
“Unajua kabisa hautafika popote ni suala la muda utakufa”
“Ndiyo maana nipo hapa kwa sababu ambaye anaweza kuwa na muda mfupi wa kuishi ni wewe sio mimi Damasi”
“Nimekuuliza unataka nini?”
“Nina mengi ya kuongea na wewe ila kwa sasa nahitaji uniambie, Yohani Mawenge anapatikana wapi?”
“Utakuwa unaota wewe, hakuna mtu kama huyo hapa duniani”
“Nililitegemea hilo kutoka kwako” Edison alisogea mpaka pale alipokuwepo Nicola, aliichukua ile bastola na kupiga risasi mbili katikati ya miguu ya mzee Kazimoto, risasi zilichimba chini mzee huyo akabaki anatetemeka. Ilisikika nyuma sauti ya mtu akiwa anacheka kwa nguvu, Damasi alikuwa anacheka uso wake ukiwa umeghafilika.
“Wewe sio mwanamke, wewe ni mtu mwenye jinsia ya kiume ambaye unajificha kwenye sketi za wanawake. Hakuna jambo ambalo unaweza kulifanya zaidi ya kutishia tishia wazee kama hivyo, kama wewe mwanaume kweli unatakiwa kupambana na mwanaume mwenzako. Njoo kama una huo uwezo ambao unakupa jeuri ya kumteka baba yangu halafu nikimalizana na wewe naenda kumbaka huyo malaya wako kisha namuua. Hahaha hahahahahaha” Damasi alionekana kabisa hakuwa sawa kama sio kuchanganyikiwa, alijinadi kwa dharau na matusi mazito akihitaji Edison apambane na mwanaume mwenzake sio kujificha kwenye sketi za wanawake. Yalikuwa zaidi ya matusi, Edison alimrushia Nicola bastola halafu akamsogelea Damasi tararibu pale alipokuwepo kama ambavyo alihitaji yeye, Damasi hakujua aina ya mtu ambaye alikuwa mbele yake alikuwaje.
Aliyumba kidogo na kujileta, mguu wake mmoja ulikuwa juu mithili ya paka ambaye anakwepa mgongo wake usiguse chini, mguu ulipitiliza kuelekea ulipokuwepo uso wa Edison, alipiga hewa. Aligeuka na ngumi mbili ambazo zilifuatana alibahatika kugusa shati tu na sio mwili, Edison alikuwa amelibonyezea tumbo lake kwa ndani ndiyo maana ngumi hizo hazikufika na wakati wote huo alikuwa amemkazia macho Damasi. Alibiringita kwa sarakasi ambayo ingemfanya teke lake safi litua kwenye kichogo cha Edison ila ilikuwa ni bahati mbaya kwake, ngumi ilitua kwenye tumbo lake, alirudi nyuma hatua kadhaa akiinamba, alihisi kuna vitu vinagawanyika ndani ya tumbo lake.
Alitumia staili ya chini mithili ya nge, alikuwa anazunguka kama mtu aliyechanganyikiwa na baada ya kumfikia Edison alizungusha buti lake ambalo lilidakwa, akiwa ameinama chini alisokomezewa buti la kifua, lilimbeba mpaka karibu na nguzo moja ya zege. Hakutua kijinga buti lake ndilo ambalo lilikita hapo akajigeuza na kusimama tena ila kifua kilikuwa kinamuwasha vibaya kwa maumivu. Aliichana shati yake akabaki kifua wazi ili kuonyesha umwamba wake, aliikaza mikono yake kwa mara nyingine na kudunda chini mara mbili, alijifyatua kwa kasi ya ajabu kwa double kick moja ambapo teke moja lilipanguliwa na moja lilikita kwenye shingo ambayo haikutikisika, shingo ilikuwa ngumu kama mti ikiwa imejichora mishipa ambayo ilikuwa migumu kiasi kwamba yeye mwenyewe alibaki anashangaa.
Pambano hilo hata Nicola alionekana kulihitaji mno kuweza kuliangalia kwa sababu hakuwa amepata muda sahihi zaidi wa kumuona Edison akiwa anapigana na mtu mwingine tofauti na kile ambacho alikishuhudia yeye kwenye mwili wake kutoka kwa kiumbe hicho.
“Wewe ni dhaifu sana bwana mdogo, kaa chini unisikilize sababu ya kukuitia hapa” maneno ya Edison yalikuwa kama kumpigia mbuzi gitaa, Damasi aliyapuuzia na kuhitaji kuijaribu bahati yake kwa mara nyingine tena. Aliinama na kuchomoa kisu kwenye buti lake, sasa alikuwa anajiamini zaidi kwa ajili silaha hiyo ambayo alikuwa akiizungusha kama aliitengeneza yeye. Kasi ambayo alienda nayo ilimfanya Edison kurudi nyuma kwa hatua kadhaa, alipishana na kisu karibu na shingo yake hali iliyo mfanya kumchukulia mtu huyo siriasi kwani alionekana kudhamiria kumuua.
Damasi alizidi kuongeza kasi lakini alisita baada ya kuhisi amepishana na mtu, Edison alijigeuza kwa sarakari kali ya mbele akampita juu Damasi ambaye alikuwa amelenga tumbo lake kwa kisu, Damasi aligeuka haraka ndipo kisu kilipo mponyoka kytokana na ngumi ambayo alikutana nayo kwenye bega lake la kulia. Aliyumba mara moja alihisi kichwa kizito kwa sababu ya ngumi ambayo ilitua kwenye paji lake la uso, alidakwa shingo yake, uso ulipigizwa kwenye kisigino cha buti na kupigwa kiganja cha kifua ambacho kilimtupa mbali.

UKURASA WA 78 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA79

Alikuwa mbishi, aliitumia sarakasi safi kuweza kunyanyuka kwa mara nyingine tena, alienda kwa hasira zaidi akiwa analinyoosha bega lake, aliruka sarakasi ili atue kwa miguu yake kwenye kichwa cha Edison, Edison aliinama kidogo ambapo miguu hiyo ilimkosa na kutoa chini ila wakati anatua chini Damas mguu wake ulipigwa na teke kali ambalo lilimfanya atoe ukelele, alibaki anaelea hewani kwa kukosa balansi ndilo alipo funikwa vyema na buti la mguu ulio komaa kwenye uso wake. Alijibamiza vibaya kwenye zege lakini alijikakamua na kusimama akiwa anapiga makelele kumkimbilia Edison ambaye aliudaka mkono wa Damasi na kuutegua kwa nguvu kisha akaunyoosha wakati huo huo, alimpiga viganja vingi kwenye kichwa chake na kumtwisha ngumi moja kati ya mbavu Damasi ambaye mpaka wakati huo alikuwa anatokwa na damu nying mdomoni.
Alidondoka chini kama mtu ambaye amechanganyikiwa akiwa anapiga makelele. Alisimama akiwa anayumba yumba kila upande Damasi, vile viganja vilimpotezea network kwenye kichwa chake kabisa. Udenda nao ulikuwa unamtoka kwa wingine, hakujua hata mtu ambaye anapambana naye alikuwa wapi, alizipanga ngumi akiwa anaangaliana na ukuta akihisi ndiye Edison, alipiga ngumi kadhaa kwenye ukuta kwa jaziba mithili ya kumpata mpinzani wake kiasi kwamba mikono yake ilianza kutoka damu kwa wingi kwa sababu alikuwa anajiumiza mwenyewe, hakumaliza hata sekunde ishirini, alidondoka chini na kupoteza fahamu.
Baba yake alilishuhudia lile tukio, lilimtisha isivyokuwa kawaida, kwa mara ya kwanza alimuona mtu huyo alivyo na mwanae wa kumzaa uhalisia wake. Mwanae huenda alikuwa miongoni mwa wanadamu hatari kwa aina ya mapigo ambayo alikuwa nayatumia ila Edison? Hakuamini kama naye alikuwa binadamu kama wao, Damasi hakufanikiwa kumshambulia Edison kabisa zaidi ya lile teke ambalo lilikita kwenye shingo ambayo ilikazwa, hakuona usalama wa mwanae kabisa kwa aina ya tukio ambalo alilishuhudia.
“Naomba tafadhali usije ukamuua mwanangu, nakuomba sana nitajaribu kumbadilisha awe mtu mwema” aliongea kwa uoga mzee Kazimoto.
“Mimi sina mpango wa kumuua mwanao ila hilo chaguo analo yeye atakapo amka. Kwa sasa wewe kazi yako imeisha unaweza kupelekwa nyumbani ila zingatia haya ambayo yametokea yanatakiwa kubakia baina yangu mimi na wewe tu kwa sababu kama yakifika sehemu nyingine basi mwanao nitalazimika kumuua kwa lazima” mzee huyo aliitikia kwa kichwa akiwa anamtazama mwanae pale chini, kijana wake alipigwa mpaka akapoteza kabisa akili kichwani kiasi kwamba alianza kupigana na ukuta. Lile lilikuwa ni jambo la hatari kwa mwanadamu kama mwanae.
Lile tukio hata Nicola lilimtisha, mtu kama Damasi kukutana na mapigo tena ambayo alionekana kuachiwa kabisa kwa sababu hakushambuliwa sana kiasi kwamba akafikia hatua ya kuchanganyikiwa! Halikuwa jambo la kawaida, huenda alipewa mapigo mazito ambayo ni hatari kwa mwili wa mwanadamu. Edison aliliona hilo kwenye uso wa Nicola ikabidi amsogelee pale ambapo alikuwepo;
“Kwenye hii dunia ambayo tunaiishi mimi na wewe kuna misingi ambayo inabidi uifuate ili uweze kuishi, kosa ambalo wengi huwa wanalifanya ni kutaka kumtangazia kila wanaye muona kwamba wao wana nguvu kubwa na uwezo wao haupimiki kabisa. Lakini hawaujui ukweli kwa sababu kuna muda mtu ambaye wewe unahitaji kumtambia hizo nguvu zako na uwezo wako anaweza kuwa hatari hata mara mbili yako na bado akawa kimya tu mbele za watu kama mjinga ila siku ambayo utajaribu kuingia kwenye viatu vyake basi utajuta hata kuufahamu huu ulimwengu”
“Mimi natamani ningekuwa na maisha ya kawaida Nicola, natamani ningekuwa baba kwenye familia yangu, niwe na maisha ya utulivu kama watu wengine wa kawaida lakini wanadamu wamesha nichagulia aina ya maisha ambayo natakiwa kuishi nami sina namna ya kufanya hivyo. Nimefikia hatua kiasi kwamba hata mimi mwenyewe binafsi najiogopa kwa sababu ninayo yafanya mpaka natamani atokee mtu ambaye atakuwa na uwezo wa kuniua ili nikapumzike. Kwenye yale makundi ya binadamu hatari hususani wapiganaji na waburudishaji nimeshapita huko kwa sasa nimeingia kwenye kundi wa wauaji wa hatari. Kama kuna jambo utaliona kwangu basi kama utakuwa upande wangu inakulazimu uishi nalo kwenye moyo wako siku zote kwa sababu unaenda kuushuhudia usiri wangu mwingine ambao huenda utakutisha zaidi ya huu ambao unauona” alimpa uhalisia wake akiwa anampiga piga mgongoni, alimpa ishara ya kuweza kuondoka na mzee huyo kumrudisha Mkuranga kwa sababu kazi yake ilikuwa imeisha na muda ulikuwa umekwenda, yeye angebaki na Damasi ili atakapo amka wamalizie pale ambapo walikuwa wameanzia.
Mpango ulikuwa ni kufanikisha kumteka Nicola baada ya kuonekana kwamba alianza kuufahamu ukweli na kuwafuatilia watu hao, jambo lingine ambalo liliongeza chachu ya hatua hiyo ni baada ya Saimon kumpigia simu bosi wake na kueleza kwamba walikuwa wamempata Edison, alidai kwamba alikuwa akimhitaji akiwa hai na mzima wa afanya kabisa mtoto wake wa damu huyo, bila shaka alikuwa na ya kumueleza mtoto ambaye alimtelekeza kwa miaka mingi na kuhitaji kumuua kwa gharama yoyote ile.
Muda ulizidi kwenda bila taarifa yoyote ile kutoka kwa Saimon hali ambayo ilileta kashikashi kubwa kwake na wasiwasi. Kama alikutana na adui yake maana yake alitakiwa awe kwenye mkono wake hivyo ukimya wa Saimon ulizalisha taharuki na wasiwasi kwao jambo ambalo lilimfanya Madam Kate kutuma vijana wengine kufuatilia eneo husika kwa kuidukua simu Saimon ambayo ilikuwa hewani bado. Walifika eneo la tukio ambako walikutana kwa mara ya kwanza na mtu huyo lakini hapakuwa na maiti zaidi ya miili ya vijana ambao walikuwa wa Saimon na damu ikiwa imetapakaa kila kona.
Aina ya vifo ambavyo walikufa hapo ndivyo waliwashtua ikawalazimu kwenda kwa wenye jengo hilo na kuzichukua video za CCTV kamera huku wakidai kwamba wao walikuwa ni watu wa usalama. Walipewa video ya tuki ambalo lilitokea hapo, wote walibaki wanaogopa, kwa namna watu hao walivyokuwa wameuliwa pamoja na Saimon mwenyewe alicho fanywa kama mtoto mdogo iliwafanya kuituma kwa bosi wao.
“Wanadamu tumefikia hatua ya kuwa wakatili kiasi kwamba tunaweza kuuana kwa namna hii kweli? Mbona hili taifa halikuwahi kuwa hivi kabla?” aliuliza mwanaume mmoja ambaye alikuwa anairudia rudia video hiyo mwili ukiwa unamsisimka isivyokuwa kawaida.
“Kiukweli hata mimi sijawahi kuona mtu akiuawa namna hii, hata sisi tumeyachukua maisha ya watu wengi lakini mara nyingi ni kwa kutumia risasi, hata kumchoma visu haiwezi kuwa hivi lakini wengine huwa tunawafunga kwenye viroba na kuwarushia baharini. Ila hili! Hapana, huu sio ubinadamu hata kidogo, tumefikia hatua mbaya zaidi na huenda ni jambo la muda tu huyu mtu hata sisi tutakutana naye”
“Kipindi natoka kijijini, nilimuaga babu ambaye ndiye mtu pekee aliyekuwa ananilea na kumwambia kwamba nakuja ndani ya jiji la Dar kuyasaka maisha ya ndoto zangu. Kuna kauli ambayo aliniambia mpaka leo huwa namkumbuka sana babu yangu ambaye sikuhudhuria hata mazishi yake huko Makongolosi Chunya “Mjukuu wangu unakwenda kwenye jiji ambalo limewashinda wengi, jiji ambalo lina kila kitu ndani yake, jiji ambalo lina neema ya kutosha, jiji ambalo lina kila aina ya dhambi ambayo umewahi kuisikia hapa duniani lakini kumbuka kuishi vizuri na watu ama kujifanya mjinga kwani mjinga huishi kwa muda mrefu kuliko mtu mjanja. Wanadamu wote huwa tupo sawa kipindi tunazaliwa ila huwa tunaanza kuwa tofauti pale ambapo tunaanza kukua na hiyo ni kutokana na kuyapata malezo tofauti lakini pia aina ya maisha ambayo watu wanayaishi. Kuna watu wamewahi kuwa wema sana lakini ulimwengu haukujali wema wao ukaamua kuwafunza kuwa na roho mbaya zilizo pitiliza hivyo kwenye utafutaji wako omba sana usije ukakutana na mtu wa namna hii kwa sababu utayajutia maisha ya kukutana naye. Kumbuka mjukuu wangu ulimwengu wa siri ndio umebeba hatima ya maisha ya watu wengi kwahiyo jitahidi sana huo ulimwengu usije ukakuangukia wewe, utakumbana na ambayo hata shetani hakuwahi kukumbana nayo” alikuwa akitoa somo kwa kumkumbuka babu yake kipenzi huku wenzake wakiwa wanamsikiliza kwa umakini.
“Mhhhhh unaanza kututia huzuni rafiki yangu, bosi ametoa amri kwamba mtu huyu atafutwe haraka popote alipo kwa sababu ni hatari kuwa na Saimon akiwa mzima kabisa wa afya kwani ana siri nyingi na akiteswa kuna uwezekano akaanza kutaja baadhi ya siri hizo” alimkatisha mwenzake na ujumbe wa babu yake baada ya kupata maagizo.
“Sasa tunampatia wapi na hatujui aliko mpeleka?”

UKURASA WA 79 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 80

“Mara nyingi mtu akihitaji kumhoji mtu kinguvu hawezi kwenda naye kwenye mazingira ya nyumbani kwake, huwa wanatumia magodauni, majengo yaliyo telekezwa, viwanja ambavyo havifanyi kazi na majengo kama hayo hivyo tuhakikishe anapatikana haraka Saimon na ikiwezekana kama hakutakuwa na mazingira ya kumuokoa basi auawe” ilikuwa ni amri ambayo ilitakiwa kufanyiwa kazi mara moja wakati huo.
Ulifanyika msako mkali kila sehemu ya jiji mpaka ilipotimu majira ya saa kumi na moja asubuhi ndipo ulipatikana mwili wa Saimon, mwili ambao ulikuwa umechakaa isivyo kawaida akiwa amekufa. Madam Kate alipewa taarifa ambayo ilimlazimu kuweza kufika mwenyewe eneo la tukio kuweza kumshuhudia moja ya vijana wake ambao alikuwa akiwategemea kwani alimfanyia mengi makubwa isivyo kawaida. Alishangaa kwa aina ya kifo cha kikatili ambacho alikufa nacho, kichwa kilitobolewa vibaya, shingo yake ilikuwa inatisha kuitazama hata mara mbili, hapo ndipo aliikumbuka kauli ya mwanasheria Jack kwamba siku hiyo isingepita hivi hivi lazima mtu wake mmoja angeweza kupoteza maisha. Jambo hilo lilikuwa la kweli kabisa na mpaka Saimon kuuliwa maana yake mtu huyo alikipata ambacho alikuwa anakitaka kutoka kwake, kama alikipata alichokuwa anakitaka maana yake ni kwamba baadhi ya siri zake zilikuwa uchi hivyo hakuwa salama tena, lilikuwa jambo la hari kwake.
Alitoa amri mwili huo ukazikwe porini huku kichwa chake kikiwa cha moto akiwaza jambo ambalo alitakiwa kulifanya kwa wakati huo. Hakujua kijana huyo alikuwa anamzidi wapi akili kwani kwenye maisha yake yote hakuwahi kukutana na mtu wa namna hiyo na watu wake walianza kupungua mmoja mmoja. Hofu ilimzidia alipo ikumbuka kauli nyingine ya Jack kwamba angejisikiaje siku ambayo angeuliwa kwenye mikono ya mtoto wake wa kumzaa? Alihisi kuna kitu kinamkaba shingoni hali ambayo ilimpelekea yeye kutoka hapo kwa hasira.

Aaliyah asubuhi sana kabla jua halijaroka alikuwa barabarani kuelekea Upanga. Safari yake ilikuwa ni kuelekea ilipokuwepo ofisi ya mkuu wa majeshi. Sababu kubwa ambayo ilimfanya aelekee huko ni baada ya kuyasikia yale mazungumzo kwenye simu kati ya bosi wake pamoja na mheshimiwa huyo ambaye alikuwa analalamika kutohusishwa kwenye masuala ya mhimu ya nchi. Alihisi kama raisi na mkurugenzi huyo walikuwa wanamsaliti kwa sababu alijua wana mahusiano ya kimapenzi yanayo waweka karibu kila wakati.
Akiwa ndani ya gari mawazo yalikuwa mengi, akiwa ndani ya gari ni taarifa nyingi zilikuwa zinakatiza kwenye kichwa chake akiwa anaziwazia kwa mengi. Mambo ambayo alikuwa anayaona yalikuwa yameanza kumtisha na kumpa hofu, hakujiona salama hata kwa watu wake hivyo aliona njia sahihi ni kuutumia kila udhaifu ambao aliona mbele yake. CDF alionekana kabisa kwamba alikuwa pamoja na watu hao lakini ugomvi wao wa muda mfupi yeye alihitaji kuutumia kwa manufaa yake binafsi.
Alifika kwenye ofisi hizo ambapo alikaguliwa, hakuwekewa vizuizi kwa sababu taarifa za kufika kwake hapo zilikuwa zimefika hata kabla hajawasili hivyo aliruhusiwa moja kwa moja kwenda kumuona kiongozi huyo wa juu kabisa kwenye jeshi.
“Aliyah nimeshtuka kupokea simu yako, wewe ni miongoni mwa watu wachache ambao wanaendesha vikosi vya siri na vyenye nguvu zaidi ndani ya taifa hili, unaweza ukaniambia ni sababu ipi imekuleta hapa kiasi kwamba umenisisitiza nisimwambie bosi wako kwamba tunaonana” mheshimiwa aliongea akiwa anasogeza kikombe kimoja cha kahawa kwa mrembo huyo ambayo ililetwa na katibu wake. Aaliyah aliipokea na kupiga funda moja akakirudisha kikombe mezani kwa sababu hakuwa hapo kwa ajili ya kuifurahia kahawa.
“Mimi najua kwamba wewe ni miongoni mwao ila nipo hapa kwa ajili ya kukupa nafasi ya pekee ambayo itakulinda hata kama kuna mambo yatatokea”
“Nisikilize Aaliyah, nakuheshimu sio kwa sababu upo karibu na mkurugenzi wako bali kwa sababu ya kazi yako tukuka ambayo wachache tunaojua uwepo wenu tunaitambua, nina muda mchache wa kukusikiliza hivyo fupisha maelezo yako nenda kwenye shida iliyokuleta hapa na asubuhi yote hii”
“Najua kwamba wewe ni miongoni mwa wanafamilia wa jamii ya siri ya LUNATIC SOCIETY” Mheshimiwa alikuwa mtulivu, hakuwa mtu wa papara kwa sababu papara haikuwa ikifaa maeneo kama hayo.
“Unaongelea kuhusu nini bibie?”
“Nadhani umetoka kuelezea ubora wa kazi ambayo huwa naifanya hivyo unajua kabisa kwamba nina taarifa za watu wengi kwenye taifa hili hata zako pia kwa sababu ni kazi yangu kuhakikisha nalilinda taifa kwa namna yoyote ile”
“Unataka kuniambia ulikuwa unanipeleleza mimi? Unaijua adhabu yake binti?”
“Sipo hapa kubishana na wewe, naijua nguvu yako, najua unaweza ukafanya lolote kukamilisha na kulinda mambo yako ya nyuma ya pazia lakini unatakiwa kuijua nafasi yangu mimi ni nani pia na hujui nyuma yangu kuna watu gani hivyo ukifanya jambo lolote la hovyo umma wote utajua wewe ni nani na unajishughulisha na nini nje ya kazi yako”
“Unataka nini?”
“Mimi nataka kufanya kazi na wewe”
“Umechanganyikiwa?”
“Mimi sijalewa ni asubuhi saivi. Jana ulikuwa unaongea na bosi wangu na nilimsikia vizuri mkipishana kwenye kauli hususani akionekana kukuficha taarifa nyingi za mhimu ambazo zinaweza kukusaidia wewe na jeshi lako. Mimi nataka nikusaidie wewe kukupa kila taarifa ambayo utaitaka”
“Halafu mimi natakiwa kukupa nini?”
“Ufanye kazi na mimi”
“Kivipi?”
“Kuna mpango wa kuiondosha hii jamii ya siri, najua nyuma yake kuna watu wenye nguvu ila wewe ukiwa upande wetu nina uhakika tutalikamilisha hili”
“Hahaah hahaha hahah nina uhakika haujui hata unacho kiongea”
“Kama makubaliano hayawezi kufikiwa basi naenda ila kitakacho kutokea usije ukanilaumu, kumbuka tu kwamba nina siri zako nyingi” Aaliyah alianza kutoka baada ya kuona mheshimiwa hamsikilizi.
“Subiri” alimuita kimamlaka na kumsogelea mpaka pale alipokuwepo.
“Mimi sikupenda kujiunga na hawa watu ila nafanya haya kwa sababu ya familia yangu, kama nikienda kinyume nao basi familia yangu inakufa”
“Hilo nalijua ndiyo maana nipo hapa”
“Kazi unafanya na nani?”
“Edison”
“Umekosea, huyu alitekwa baada ya kutoka Ikulu”
“Hajatekwa, yupo huru”
“Unataka kuniambia Jack hakuwa yeye?”
“Ile ni kama copy yake tu sio yeye”
“Plani yako ni ipi?”
“Nitakupa taarifa zote kwa sasa nilitaka tu nijue kama tupo upande mmoja kwa sababu hata bosi wangu amenisaliti simuamini tena” Kabla CDF hajatoa jibu lake kwenye hilo simu yake ya mezani ilianza kuita kwa fujo, simu hiyo iliyakatisha maongezi yao. Alisogea na kuipokea
“Hello!”
“Mheshimiwa, kuna tatizo kubwa” ilikuwa sauti ya upande wa pili kutoka kwa mtu ambaye alikuwa anahema na kuongea kwa sauti ya chini.
“Nani wewe?”
“Jaiwelo”
“Kuna tatizo gani?”
“Bosi ameuawa”
“Niambie kwamba unanitania”
“Huu ndio ukweli, ni mimi tu ambaye nimefanikiwa kutoka hai japo nipo kwenye hali mbaya na muda wowote naweza kupoteza maisha. Mtu ambaye amefanya hilo ni niiii!” mwanaume huyo hakumalizia maongezi yake zaidi ilisikika sauti moja kali ya kilio kukawa kimya, simu ilikuwa imekatwa.
“Jaiwelo, Jaiwelo ongea na mimi uko wapi na nini kimetokea?” sura na hali ya mkuu wa majeshi ilikuwa imebadilika kabisa. Alibaki anaongea mwenyewe mpaka akaibamiza simu hiyo na kuipasua. Alionekana kuchanganyikiwa hali iliyo anza kumpa mashaka hata Aaliyah, lilionekana ni jambo kubwa lilitokea.
“Hapana hapana, hii sio kweli” aliongea tena kwa kufoka akiwa anazunguka kila sehemu, jasho lilikuwa linamtoka kwa mbali usoni.
“Kimetokea nini?”

UKURASA WA 80 unafika mwisho.
 
duuuh.! balaa zito..na zaidi mtunzi unajua sana hapa muendelezo tusubiri hadi mwisho wa mwezi..kwa utamu wa simulizi hii ni mateso kweli kusubiri muda mrefu..respect mtunzi
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 80

“Mara nyingi mtu akihitaji kumhoji mtu kinguvu hawezi kwenda naye kwenye mazingira ya nyumbani kwake, huwa wanatumia magodauni, majengo yaliyo telekezwa, viwanja ambavyo havifanyi kazi na majengo kama hayo hivyo tuhakikishe anapatikana haraka Saimon na ikiwezekana kama hakutakuwa na mazingira ya kumuokoa basi auawe” ilikuwa ni amri ambayo ilitakiwa kufanyiwa kazi mara moja wakati huo.
Ulifanyika msako mkali kila sehemu ya jiji mpaka ilipotimu majira ya saa kumi na moja asubuhi ndipo ulipatikana mwili wa Saimon, mwili ambao ulikuwa umechakaa isivyo kawaida akiwa amekufa. Madam Kate alipewa taarifa ambayo ilimlazimu kuweza kufika mwenyewe eneo la tukio kuweza kumshuhudia moja ya vijana wake ambao alikuwa akiwategemea kwani alimfanyia mengi makubwa isivyo kawaida. Alishangaa kwa aina ya kifo cha kikatili ambacho alikufa nacho, kichwa kilitobolewa vibaya, shingo yake ilikuwa inatisha kuitazama hata mara mbili, hapo ndipo aliikumbuka kauli ya mwanasheria Jack kwamba siku hiyo isingepita hivi hivi lazima mtu wake mmoja angeweza kupoteza maisha. Jambo hilo lilikuwa la kweli kabisa na mpaka Saimon kuuliwa maana yake mtu huyo alikipata ambacho alikuwa anakitaka kutoka kwake, kama alikipata alichokuwa anakitaka maana yake ni kwamba baadhi ya siri zake zilikuwa uchi hivyo hakuwa salama tena, lilikuwa jambo la hari kwake.
Alitoa amri mwili huo ukazikwe porini huku kichwa chake kikiwa cha moto akiwaza jambo ambalo alitakiwa kulifanya kwa wakati huo. Hakujua kijana huyo alikuwa anamzidi wapi akili kwani kwenye maisha yake yote hakuwahi kukutana na mtu wa namna hiyo na watu wake walianza kupungua mmoja mmoja. Hofu ilimzidia alipo ikumbuka kauli nyingine ya Jack kwamba angejisikiaje siku ambayo angeuliwa kwenye mikono ya mtoto wake wa kumzaa? Alihisi kuna kitu kinamkaba shingoni hali ambayo ilimpelekea yeye kutoka hapo kwa hasira.

Aaliyah asubuhi sana kabla jua halijaroka alikuwa barabarani kuelekea Upanga. Safari yake ilikuwa ni kuelekea ilipokuwepo ofisi ya mkuu wa majeshi. Sababu kubwa ambayo ilimfanya aelekee huko ni baada ya kuyasikia yale mazungumzo kwenye simu kati ya bosi wake pamoja na mheshimiwa huyo ambaye alikuwa analalamika kutohusishwa kwenye masuala ya mhimu ya nchi. Alihisi kama raisi na mkurugenzi huyo walikuwa wanamsaliti kwa sababu alijua wana mahusiano ya kimapenzi yanayo waweka karibu kila wakati.
Akiwa ndani ya gari mawazo yalikuwa mengi, akiwa ndani ya gari ni taarifa nyingi zilikuwa zinakatiza kwenye kichwa chake akiwa anaziwazia kwa mengi. Mambo ambayo alikuwa anayaona yalikuwa yameanza kumtisha na kumpa hofu, hakujiona salama hata kwa watu wake hivyo aliona njia sahihi ni kuutumia kila udhaifu ambao aliona mbele yake. CDF alionekana kabisa kwamba alikuwa pamoja na watu hao lakini ugomvi wao wa muda mfupi yeye alihitaji kuutumia kwa manufaa yake binafsi.
Alifika kwenye ofisi hizo ambapo alikaguliwa, hakuwekewa vizuizi kwa sababu taarifa za kufika kwake hapo zilikuwa zimefika hata kabla hajawasili hivyo aliruhusiwa moja kwa moja kwenda kumuona kiongozi huyo wa juu kabisa kwenye jeshi.
“Aliyah nimeshtuka kupokea simu yako, wewe ni miongoni mwa watu wachache ambao wanaendesha vikosi vya siri na vyenye nguvu zaidi ndani ya taifa hili, unaweza ukaniambia ni sababu ipi imekuleta hapa kiasi kwamba umenisisitiza nisimwambie bosi wako kwamba tunaonana” mheshimiwa aliongea akiwa anasogeza kikombe kimoja cha kahawa kwa mrembo huyo ambayo ililetwa na katibu wake. Aaliyah aliipokea na kupiga funda moja akakirudisha kikombe mezani kwa sababu hakuwa hapo kwa ajili ya kuifurahia kahawa.
“Mimi najua kwamba wewe ni miongoni mwao ila nipo hapa kwa ajili ya kukupa nafasi ya pekee ambayo itakulinda hata kama kuna mambo yatatokea”
“Nisikilize Aaliyah, nakuheshimu sio kwa sababu upo karibu na mkurugenzi wako bali kwa sababu ya kazi yako tukuka ambayo wachache tunaojua uwepo wenu tunaitambua, nina muda mchache wa kukusikiliza hivyo fupisha maelezo yako nenda kwenye shida iliyokuleta hapa na asubuhi yote hii”
“Najua kwamba wewe ni miongoni mwa wanafamilia wa jamii ya siri ya LUNATIC SOCIETY” Mheshimiwa alikuwa mtulivu, hakuwa mtu wa papara kwa sababu papara haikuwa ikifaa maeneo kama hayo.
“Unaongelea kuhusu nini bibie?”
“Nadhani umetoka kuelezea ubora wa kazi ambayo huwa naifanya hivyo unajua kabisa kwamba nina taarifa za watu wengi kwenye taifa hili hata zako pia kwa sababu ni kazi yangu kuhakikisha nalilinda taifa kwa namna yoyote ile”
“Unataka kuniambia ulikuwa unanipeleleza mimi? Unaijua adhabu yake binti?”
“Sipo hapa kubishana na wewe, naijua nguvu yako, najua unaweza ukafanya lolote kukamilisha na kulinda mambo yako ya nyuma ya pazia lakini unatakiwa kuijua nafasi yangu mimi ni nani pia na hujui nyuma yangu kuna watu gani hivyo ukifanya jambo lolote la hovyo umma wote utajua wewe ni nani na unajishughulisha na nini nje ya kazi yako”
“Unataka nini?”
“Mimi nataka kufanya kazi na wewe”
“Umechanganyikiwa?”
“Mimi sijalewa ni asubuhi saivi. Jana ulikuwa unaongea na bosi wangu na nilimsikia vizuri mkipishana kwenye kauli hususani akionekana kukuficha taarifa nyingi za mhimu ambazo zinaweza kukusaidia wewe na jeshi lako. Mimi nataka nikusaidie wewe kukupa kila taarifa ambayo utaitaka”
“Halafu mimi natakiwa kukupa nini?”
“Ufanye kazi na mimi”
“Kivipi?”
“Kuna mpango wa kuiondosha hii jamii ya siri, najua nyuma yake kuna watu wenye nguvu ila wewe ukiwa upande wetu nina uhakika tutalikamilisha hili”
“Hahaah hahaha hahah nina uhakika haujui hata unacho kiongea”
“Kama makubaliano hayawezi kufikiwa basi naenda ila kitakacho kutokea usije ukanilaumu, kumbuka tu kwamba nina siri zako nyingi” Aaliyah alianza kutoka baada ya kuona mheshimiwa hamsikilizi.
“Subiri” alimuita kimamlaka na kumsogelea mpaka pale alipokuwepo.
“Mimi sikupenda kujiunga na hawa watu ila nafanya haya kwa sababu ya familia yangu, kama nikienda kinyume nao basi familia yangu inakufa”
“Hilo nalijua ndiyo maana nipo hapa”
“Kazi unafanya na nani?”
“Edison”
“Umekosea, huyu alitekwa baada ya kutoka Ikulu”
“Hajatekwa, yupo huru”
“Unataka kuniambia Jack hakuwa yeye?”
“Ile ni kama copy yake tu sio yeye”
“Plani yako ni ipi?”
“Nitakupa taarifa zote kwa sasa nilitaka tu nijue kama tupo upande mmoja kwa sababu hata bosi wangu amenisaliti simuamini tena” Kabla CDF hajatoa jibu lake kwenye hilo simu yake ya mezani ilianza kuita kwa fujo, simu hiyo iliyakatisha maongezi yao. Alisogea na kuipokea
“Hello!”
“Mheshimiwa, kuna tatizo kubwa” ilikuwa sauti ya upande wa pili kutoka kwa mtu ambaye alikuwa anahema na kuongea kwa sauti ya chini.
“Nani wewe?”
“Jaiwelo”
“Kuna tatizo gani?”
“Bosi ameuawa”
“Niambie kwamba unanitania”
“Huu ndio ukweli, ni mimi tu ambaye nimefanikiwa kutoka hai japo nipo kwenye hali mbaya na muda wowote naweza kupoteza maisha. Mtu ambaye amefanya hilo ni niiii!” mwanaume huyo hakumalizia maongezi yake zaidi ilisikika sauti moja kali ya kilio kukawa kimya, simu ilikuwa imekatwa.
“Jaiwelo, Jaiwelo ongea na mimi uko wapi na nini kimetokea?” sura na hali ya mkuu wa majeshi ilikuwa imebadilika kabisa. Alibaki anaongea mwenyewe mpaka akaibamiza simu hiyo na kuipasua. Alionekana kuchanganyikiwa hali iliyo anza kumpa mashaka hata Aaliyah, lilionekana ni jambo kubwa lilitokea.
“Hapana hapana, hii sio kweli” aliongea tena kwa kufoka akiwa anazunguka kila sehemu, jasho lilikuwa linamtoka kwa mbali usoni.
“Kimetokea nini?”

UKURASA WA 80 unafika mwisho.
Kaka una nafas yako taar katik hii Kaz 🙌🙌 usituweke sana walau once per week
 
Back
Top Bottom