Simulizi ya kijasusi: Nafsi zilizotelekezwa

Simulizi ya kijasusi: Nafsi zilizotelekezwa

HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 62

“Jambo hili halitakuwa mwisho bali utakuwa mwanzo kwa sababu zile NAFSI ZILIZO TELEKEZWA hazitaenda bure bali ile damu ambayo ilimwagika itamrudia kila mmoja na kuyaondoka maisha yake hata kama ni kwa kuchelewa. Mimi naenda kufa kwani kuendelea kuwa hai ni hatari kwao na hawawezi kuruhusu jambo hili liweze kuendelea. Kila hatua ambayo niliipiga nilikusanya ushahidi wa kutosha, kila ambalo nililiongea kuhusu kesi hizi ni la kweli na hata ambayo nayaongea hapa ni ya kweli kabisa na nina imani ipo siku kuna mtu atakuja kuthibitisha ama kuuweka ushahidi wote ambao nimeufanyia kazi hadharani”
“Mimi naenda kufa kwa sasa ila watanzania msiwe wapumbavu kwa sababu mtakuja kulipoteza taifa lenu kama msipokuwa wamoja na kuamua kulipigania kwa nguvu na jasho, nyie ndio watu pekee ambao mnaweza kuibadilisha hii nchi na kuirudisha kama ilivyokuwa mwanzo tangu waasisi walipo pigania uhuru wake. Dunia haichagui wapi wa kukupeleka bali wewe ndiye unachagua wapi pa kuipeleka dunia ambayo unaiishi. Natamani niwe na muda mwingi zaidi wa kuongea nanyi ila nimechoka, mwanasheria wenu nimechoka kuongea nahitaji nikapumzike, nina uhakika tutakuja kuonana kwa wakati mwingine tena kwenye maisha yajayo! Kwa sasa niliyo yafanya yanatosha. JACK THE LAWYER” Mwanaume huyo aliongea maneno mazito sana akiwa mubashara kila mtu anaona, hakuwa mbali wala bali alikuwa amejifungia kwenye ofisi yake ndani ya jengo lake kubwa ambalo lilikuwa na ofisi yake ya sheria.
Aliongea maneno mengi na mazito ambayo bila shaka yalikuwa yanaenda kuleta utofauti ndani ya nchi kwa sababu watu wangeandamana na kuhitaji ukweli uwekwe wazi, mtu huyo siku kadhaa aliahidi kuishtaki serikali na akadai ana ushahidi wote halafu ghafla tena anadai kwamba anaenda kufa? Hakuna mwananchi ambaye angeisaemehe wala kuielewa serikali kwa namna yoyote ile zaidi ya kuhitaji majibu yapatikane vinginevyo kungekuwa na machafuko mabaya ukizingatia alikuwa ni kipenzi cha watu mwanasheria Jack.

Vyombo vya ulinzi na usalama vilikuwa vimetumia muda mwingi wakati anaongea kuweza kuidukua website ambayo alikuwa anaitumia kurushia habari yake hiyo kwa sababu mambo ambayo alikuwa anayaongea yalikuwa ni hatari kwa usalama wa taifa, yalikuwa yanaenda kubadili mtazamo wa nchi nzima na ubaya hawakuwa na uwezo wa kuzuia habari hizo kwani kama angekuwa anatumia ni chombo cha habari chochote basi wangekizima haraka iwezekanavyo ila kutumia website ambayo aliitengeneza mwenyewe hakuna kitu wangefanya kuzuia jambo hilo.
Walifanikiwa kutambua kwamba alikuwa ndani ya ofisi yake hivyo mitaa ilichafuka gari za polisi zikiwahi huko lakini pia hata kikosi maalumu cha THE RIGHT HAND kilikuwa kipo njiani kuelekea eneo hilo wakitamani kuwa wa kwanza kufika huko kwa sababu huyo ndiyo ilikuwa silaha yao kubwa ya kuweza kukamilisha kazi zote ambazo zilikuwa mbele yao. Mwanasheria huyo baada ya kutoa taarifa hiyo maisha yake yalikuwa hatarini isivyokuwa kawaida ndiyo maana walaihitaji kuwa wa kwanza kufika hapo waondoke naye.
Mwanasheria huyo baada ya kuhakikisha kwamba amekamilisha kile ambacho kilimpeleka humo ndani alizunguka ndani ya ofisi yake akiwa anaangalia kwa umakini kila kitu ambacho kilikuwa humo ndani. Vitu ambavyo vilikuwa humo ndivyo ambavyo vilimpa jina na umaarufu mkubwa bila kusahau akili yake, jina lake lilikuwa limekolezwa kwenye kibao ambacho kilikaa vyema kwenye meza yake. Alitazama ukutani eneo ambalo lilikuwa na picha yake, aliishia kushusha chozi la furaha na uchungu kwani ilikuwa ni mara yake ya mwisho kuviona vitu hivyo kwa macho yake asingekuja kuviona tena kwenye maisha yake yote.
Baada ya kuhakikisha ameridhika, alijifuta machozi yake na kushuka mpaka chini kabisa ya jengo hilo. Alitoka mpaka nje kabisa sehemu ambayo alikuwa ameipaki gari yake, alipanda juu ya gari hiyo na kukaa kisha akaitoa Cigar kwenye mfuko wake wa koti na kuiwasha. Alikuwa anapata upepo huku akiwa anaivuta taratibu na muda mfupi tu alisikia gari moja ikipiga breki kali umbali kidogo kutoka hapo alipokuwepo yeye. Ndani ya gari hiyo aliyetangulia kushuka ni Aaliyah Beka akiwa ameongozana na wenzake wanne, Jack alitabasamu kwa sababu kwa wakati huo alikuwa ana soko zaidi hata ya zile hisa za mabenki makubwa nchini.
“Hamkutakiwa kuwepo hapa binti”
“Nataka nikupeleke eneo ambalo ni salama kwa sababu najua hapa sio salama tena kwako, tafadhali naomba tuondoke haraka” Jack aliuvuta moshi tena kwa hisia kali akaruka na kutua chini karibu na alipokuwepo mwanamke yule.
“Hili jambo lipo nje ya uwezo wako, hauna huo uwezo wa kunipelekea popote kwa sababu hakuna mahali utafika na mimi watakuja kunichukua”
“Nani atakuja kukuchukua?”
“Wenye uwezo zaidi yako”
“Hapana mimi nina uwezo wa kukulinda”
“Bibie wewe mwenyewe hapo wakiamua kukuua ni suala la dakika tu halafu unasema unaweza kunilinda mimi?” wakati huo vyombo vya habari na magari ya polisi yalikuwa yanaingia kwa kasi mno eneo hilo, lakini kabla hata Aaliyah hajajibu zilikuja gari tano nyeusi ambazo zilikuwa na namba za Ikulu na walishuka wanaume wa kutosha ambao walikuwa ndani ya suti zao nyeusi na vifaa vya mawasiliano masikioni.
“Nimekwambia mapema, nina imani hao ndio ninaondoka nao ila nisikilize kwa umakini sana Aaliyah; hii nchi inakuhitaji sana wewe. Kuna mtu ambaye atakutafuta wewe naomba kama akifanya hivyo mpe ushirikiano kwa asilimia zote, mtu huyo ndiye pekee ambaye anaweza kuleta ukombozi kwenye hii nchi lakini unahitajika na wewe uwe karibu yake kwani huko mbele atakuhitaji mno kwa sababu anaenda kupambana na jambo la hatari ambalo nadhani yeye halichukulii kwa uzito mkubwa” maneno kidogo yalimshangaza Aaliyah, mwanaume huyo alikuwa anaongea kwa kunong’ona wakati wanaume wale wakiwa wanazidi kusogea pale ambapo alikuwepo na picha nyingi zikiwa zinapigwa.
“Ni nani huyo?”
“Haina haja ya wewe kumfahamu kwa sasa ila atakutafuta mwenyewe. Jambo la kuzingatia usimwamini mtu yeyote hata hao wenzako usiwe na imani nao kabisa, bosi wako ndo kabisa usimuamini na kuna taarifa ambazo unatakiwa uanze kuzihifadhi kama siri yako mwenyewe vinginevyo wewe mwenyewe upo kwenye hatari kubwa ya kuweza kupoteza maisha. Kumbuka kauli ambazo nilikwambia siku ile na uzifanyie kazi” Aaliyah alibaki ameduwaa, alikuja kuhitaji kuondoka na mtu huyo lakini kuwahi kwake kukamfanya apewe kazi zingine za kuweza kufanya.
“Mr Jack tunakuomba uongozane na sisi wakati huu kwenda Ikulu mheshimiwa raisi anahitaji kuongea na wewe” ilisikika sauti nzito ya mamlaka kutoka kwa mwanaume mmoja ambaye alikuwa anaongea mbele ya mwanasheria huyo ambaye kwa wakati huo alikuwa na sura tofauti kabisa na ile ambayo wao waliizoea siku zote kwani mwonekano wake ulikuwa ni ule wa sura ile ya Edison. Hakuleta upinzani zaidi ya kuongoza kuelekea kwenye gari, aligeuka kabla ya kuingia akatikisa kichwa chake kwa Aaliyah kama kukubali jambo kisha akaingia na safari ya kuelekea Ikulu ikaanzia hapo.
Barabara ilikuwa na askari wa kutosha kuelekea Ikulu hali ambayo iliifanya kuwa nyeupe. Hawakuchukua muda mrefu kuweza kufika na msafara huo ambao ulienda kumchukua mwanasheria huyo nguli nchini kwa ajili ya kwenda kukutana na raisi wa Tanzania kwa mara ya kwanza ana kwa ana. Mageti yote yalifunguliwa na baada ya kushuka mwanasheria huyo alikaguliwa kwenye kila pembe ya mwili wake ambapo zilitolewa bastola mbili pamoja na kimkebe cha kuhifadhia sigara za bei ghali ambazo alionekana kuzivuta kwa mara ya kwanza kabisa kwenye maisha yake kisha baada ya hapo akaongozwa na watu hao eneo ambalo alitakiwa kufika wakati huo.
Sehemu ambayo alipelekwa ilikuwa ni kwenye nyumba moja ambayo ilikuwa inapendeza mno, ndani ya nyumba hiyo ndiyo sehemu ambayo raisi alichagua kufanyia mazungumzo na mwanaume huyo, mazungumzo ambayo kwake yalikuwa ya mhimu na aliyahitaji isivyokuwa kawaida. Raisi alikuwa kwenye kiti chake ambacho kilitengenezwa maalumu kwa ajili yake Faraji Asani, wawili hao hawakuwahi kabisa kukutana kwenye maisha yao yote zaidi ya kila mmoja kumuona mwenzake kwenye vyombo vya habari kwa wakati wake.

UKURASA WA 62 unafika mwisho.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 63

“Hatimaye tumekutana kwa mara ya kwanza bwana Jack”
“Nasikitika tumekutana wakati mbaya zaidi mheshimiwa raisi”
“Hakuna wakati mbaya ila huwa kuna wakati sahihi tu ambao ndio naamini huwa unafanya mambo kuweza kutokea”
“Nimeshangaa unahitaji kukutana na mtu kama mimi tena ukiwa umechelewa namna hii, kuna kipi ambacho unahitaji kujua kutoka kwangu?”
“Kila kitu Jack”
“Kwa bahati mbaya hilo haliwezekani kujua kila kitu kutoka kwangu”
“Nina uhakika utatueleza”
“Vipi unanitisha?”
“Mimi ni raisi wa nchi sina hiyo tabia ya kumtishia mtu kama wewe tena mwananchi wa kawaida tu”
“Mpaka nipo hapa ujue mimi sio wa kawaida kama ambavyo unaongea kirahisi tu, kama umepanga kuhitaji kunitesa ama kuniulia hapa achana na hayo mawazo kwa sababu utaonekana raisi wa hovyo zaidi kuwahi kuliongoza hili taifa, ni bora uendelee kuwandanganya wananchi kama ulivyo zoea kwani wote wanajua kwamba nipo hapa hivyo kama unahitaji kuyatekeleza hayo basi hakikisha unanitoa hapa na kunipeka kwenye moja ya magereza yako ya siri ukafanye hayo ambayo unayataka”
“Unajiamini Jack lakini haupo hapa kwa ajili ya kuuawa wala kuteswa, mimi nimekualika hapa kama raisi wa nchi ndiyo maana umekuja ukiwa haujafungwa hata pingu kwenye mikono yako zaidi ya kusindikizwa na walinzi” Jack alitabasamu kwa sababu alimjua mheshimiwa huyo kwa ubingwa wake wa propaganda.
“Unaweza ukaniambia sababu ambayo imekufanya unialike mheshimiwa?”
“Taifa siku kadhaa limeingia kwenye hali mbaya kidogo kwa sababu ya mauaji kadhaa ambayo yametokea lakini kuanzia usiku wa leo taifa limeingia kwenye hali mbaya zaidi kwa sababu ya kile ambacho wewe umekiongea. Kama jambo hili lilikuwa na uzito mkubwa kiasi hiki ulitakiwa kunishirikisha kabla ili nijue kama kuna namna ya kukusaidia wewe niweze kukusaidia hapo ingetegemea kama taarifa zako ambazo ulizitoa zilikuwa sahihi lakini umeamua kusababisha machafuko namna hii unategemea nini kinaenda kutokea?”
“Mhhh mheshimiwa mbona unajisahaulisha namna hiyo, haya matatizo yameanza kutokea leo? Jibu ni hapana ni muda mrefu sasa yanaendelea kutokea, nimekemea haya mambo mpaka nikathibitisha mbele ya umma kwamba naenda kuishtaki serikali kwa sababu ipo nyuma ya mambo machafu ambayo yanahatarisha maisha ya raia ambao wamjitoa kwa ajili ya kulilinda taifa hili, je uliwahi kujali hata mara moja juu ya mambo hayo zaidi ya kuyapuuzia? Le unaanzia wapi kuniambia kwamba nilitakiwa kukushirikisha wewe?”
“Wewe ni nani Jack?”
“Jina langu la kuzaliwa naitwa Edison Christian, mtoto wa damu wa yule mwanasayansi ambaye aliuawa nina uhakika kipindi kile ulikuwa kijana mdogo ambaye hata siasa nina uhakika hukuwa umeianza”
“Wewe hauwezi kuwa huyo kwa sababu nadharia zenu zinapishana, muda ambayo mwanaume yule aliutumia jeshini wewe ulitumia kusoma na kuingia kwenye kazi, ulikuwa makini mno kiasi kwamba mtu ambaye hatulizi akili yake kugundua hilo ni jambo gumu ila niamini mimi usingeweza kujigawa muda wote uwepo jeshini na muda huo huo uwepo kuipambania sheria!”
“Kumbe haya mambo ulikuwa unayafuatilia kwa umakini mheshimiwa?”
“Mimi ni raisi kujua mambo kama haya ni kawaida”
“Na baada ya kuyajua umefanya nini kuliokoa taifa lako?”
“Unahisi napoteza muda kukaa hapa Ikulu?”
“Hujajibu swali langu”
“Wewe ni nani?”
“Haina msaada wowote kwako kwa wakati huu, nambie unataka nini?”
“Nahitaji tuingie makubaliano ambayo yatanifanya mimi nitoe kauli ya wewe kusamehewa na urudi kwenye kazi yako kama kawaida”
“Mimi na wewe wote tunajua kabisa kwamba hilo jambo haliwezekani mheshimiwa raisi”
“Mimi ndiye raisi wa nchi lolote linawezekana. Nahitaji ufanye mahojiano mengine uweze kuyakana yale maneno ambayo umeyaongea muda mfupi ambao umepita, baada ya hapo nitaziondoa kesi zote ambazo zitakkabili kwa sasa na utapewa ruhusa ya kuendelea kufanya kazi yako kama ilivyokuwa mwanzo” Jack alicheka tena kwa sauti kubwa.
“Kwahiyo mheshimiwa unataka kuniambia kwamba unajua alipo Irina Espanovich si ndiyo?”
“Whaaaaat?”
“Mpaak unahitaji kuzificha taarifa hizi maana yake na wewe ni mmoja wao”
“Sielewi unacho kiongea bwana mdogo, nisikilize vyema na unielewe. Jambo ambalo umelisababisha ni hatari kwa upande wako na huwezi kupona, haya mengine mimi na wewe tutayaongea vizuri ila kwa sasa safisha jina lako kwa kile ambacho kimetokea”
“Siamini kama raisi wa nchi leo ananishawishi mimi leo niukatae utu wangu kwa ajili ya kulisafisha jina lake chafu na mfumo wake mbovu wa uendeshaji wa nchi”
“Kwa sasa sijali kwamba wewe ni nani na unajua nini na nini ila fanya nilicho kwambia na kama huwezi kufanya hili basi sitakuwa na nafasi nyingine ya kukubembeleza kwa mara ya pili”
“Nisikilize kwa umakini bwana Faraji, huenda unayo yafanya yanakupa ujeuri kwa sababu kuna watu wameahidi kukulinda na hicho kiti chako kinakwenda kukulinda, mimi najua kabisa maisha yangu hayana thamani tena ni suala la muda tu kabla sijafa ila mwisho wako unaenda kuwa mbaya kuliko unavyo fikiria wewe. Haujui hata sababu ya msingi ya kwamba ni kwanini nimeamua kujikamatisha makusudi na nina uhakika unajua kwamba mimi sio mjinga kiasi hicho kwahiyo kila ambacho ninakifanya najua kabisa naanzia wapi na kitaishia wapi hata nisipokuwepo mimi. Una muda mchache wa kutamba kwenye hicho kiti chako kwani muda mfupi ujao unaenda kujutia kwa kila jambo ambalo ulikuwa umelifanya”
“Mimi sikuwa na mpango wa kuongea na wewe kwa sababu ningesha kutafuta ila kuna mtu ambaye utakuwa na uhitaji mkubwa wa kuongea naye hapo baadae. Nipeleke kule ambako umepanga kunipeleka wakati huu nikapumzike kwani nimechoka siku ya leo” mwanaume hakujali kama alikuwa anaongea na raisi, alimpa ule ukweli wake ambao alistahili kiasi kwamba hata mheshimiwa mwenyewe alibaki anashangaa asiamini kile ambacho kilikuwa kinatokea. Yeye ndiye alikuwa mtu wa mhimu zaidi kwenye taifa na mtu mwenye nguvu zaidi, kuchukuliwa kawaida na mwanasheria kulimpa hasira kali moyoni mwake.
“Kwa sababu umegoma kunisikiliza kwa njia ya amani basi njia ya lazima itakufaa zaidi” aliongea kwa hasira huku akiwaita walinzi wake na kuhitaji mtu huyo asafirishwe usiku huo huo kupelekwa kwenye gereza lake la siri ambalo lilikuwa linapatikana mpakani wa Dar es salaam na Bagamoyo.
Msafara wa gari kumi ulitoweka Ikulu kuianza safari ya kumsafirisha mwanaume huyo kwenda eneo ambalo waliamini kwamba angepatiwa mateso makali na kutapika kila ambacho kilikuwa kwenye moyo wake kwa mheshimiwa. Ulikuwa ni usiku wa manane tayari wakati huo ambao gari hizo zilikuwa kwenye mwendo mkali kumsafirisha mwanaume huyo kwa siri majira hayo ya usiku. Baada ya msafara huo kufika Morocco ukiwa umenyooka na ile Bagamoyo road, gari ya mbele ilipasuliwa tairi vibaya na risasi ya mdunguaji ambaye mpaka akati huo hakujulikana alikuwa amekaa wapi maana eneo hilo lilizungukwa na majengo ambayo yalikuwa mbali mbali.

UKURASA WA 63 unafika mwisho.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 64

Gari hiyo ilidondoka vibaya na kulipuka hali ambayo ilipelekea gari zingine za nyuma kusimama ghafla na kusababisha ajali mbaya. Walishuka wanaume kutoka kwenye hayo magari lakini kila ambaye alikuwa anashuka humo alikutanishwa na risasi kutoka kwa watu ambao walianza kulizingira eneo hilo wakiwa wamezifunika nyuso zao kwa vitambaa vyeusi. Wanaume hao walizichakaza gari hizo vibaya kwa uzito wa mashine ambazo walikuwa nazo kwenye mikono yao. Alibakia mwanaume mmoja ambaye alikuwa anagala gala chini akiwa na maumivu kwenye mwili wake, mwanaume mmoja alimmiminia risasi nyingi kwenye kifua chake kikabaki kama nyama ya buchani. Mmoja aliusogelea mlango na kumtaka mtu ambaye alikuwa ndani atoke, Jack alitoka ndani ya gari akiwa wa afya tele kabisa, hakuwa na la kufanya silaha nzito zilikuwa zinamwangalia yeye hivyo alikuwa anatazamana na kifo moja kwa moja. Mwanaume mmoja alimsogelea pale alipokuwepo, akamfunga pingu na kumfunika uso wake. Walimuingiza kwenye gari na kutoweka naye hilo eneo, baada ya dakika kama tano baadae gari za polisi zilifika kwa kasi lakini zilikuwa zimechelewa kwani mtu wao alikuwa amekwenda wasijue ni nani alifanya tukio hilo na kumchukua JACK THE LAWYER.
Nicola Aidan alikuwa mmoja wa watu ambao walikuwa wanafuatilia kwa umakini kile ambacho kilikuwa kinaendelea kwa mwanasheria JACK THE LAWYER. Alikuwa makini kufuatilia taarifa hiyo tangu mtu huyo anaanza nayo mpaka anakaribia kumaliza, alihangaika kuifuatilia sehemu ambayo mtu huyo alikuwa anafanyia tukio hilo na baadae aligundua kwamba ilikuwa ni ofisini kwake hivyo alijitahidi kuwahi kufika huko ili amuwahi mwanaume huyo kwani alijua kwamba baada ya taarifa hiyo mwanasheria asingekuwa mahali salama kwa mara nyingine.
Maneno ambayo aliongea naye kule Buguruni yalikuwa bado yamemkaa kichwani kwake, ile sura ambayo aliiona kwa mtu huyo ilimchanganya. Fikra zake zilimkumbushia tukio ambalo alikutana nalo la kuelekezwa kwa Maliki na Saimon na kukuta mtu huyo amepigwa risasi muda mfupi baada ya tukio, alihisi kuna jambo halikuwa sawa hivyo mtu pekee wa kumpa ukweli halisi alikuwa ni huyo mwanasheria. Aliona kabisa kwamba alikuwa na mengi ya kuongea na mtu huyo na kwa wakati huo alimhitaji akiwa hai. Jambo la kuamini kwamba mtu huyo pia ndiye alikuwa yule komando wa KOM kwake halikumuingia akilini kabisa.
Uamuzi ambao aliufanya ni kuwahi kwenye ofisi hizo ili angalau awe mtu wa kwanza kuongea na huyo mtu, hali hiyo ilimfanya kuingia kwenye gari yake na kuitoa kwa spidi kali ili awe wa kwanza lakini hakujua wakati anao upanga yeye kuna watu waliupanga kabla yake. Wakati unatua mguu wake kwenye lile eneo ni wakati ambao Aaliyah alikuwa amewasili eneo lile kuongea na Jack huku wanaume wengine watatu wakiwa karibu na gari na wote walionekana kuwa watu wa kazi kwa mionekano yeo, jambo hilo lilimfanya asite kusogea na kuamua kubaki kwenye gari umbali kadhaa kutokea kwenye zile ofisi.
Alijisonya mwenyewe kwa kuchelewa kwani ile ndiyo ilikuwa nafasi ya pekee kabisa ya yeye kutekeleza ambacho alikuwa anakihitaji kwa wakati huo. Muda mchache gari za polisi na vyombo vya habari vilifika pale akiwa anatizama kila kitu na jambo ambalo lilimshangaza ni kuona gari za Ikulu zikiingia pale na kuondoka naye lakini kabla ya jambo hilo kufanyika aliona mwanasheria akifanya mazungumzo ambayo yalionekana kuwa ya siri na mwanamke yule ambaye Nicola hakuwahi kumfahamu. Aliichukua kamera na kumpiga picha yule mwanamke ili aweze kumfahamu kama alikuwa ni nani hasa mpaka mtu yule aonekane kufahamiana naye.
Zile gari za Ikulu ziliondoka na Jack, hakuwa na uwezo wa kuzifuatilia gari hizo kwani jambo hilo lingekuwa la hatari kwake. Jambo ambalo alililafanya na kuichukua ile picha ya Aaliyah na kuiingiza kwenye mtandao ambapo alishangazwa na taarifa ambazo aliziona kwa mwanamke huyo kwa sababu alikuwa ni moja ya maagent wa juu ndani ya shirika la kipelelezi la nchi. Alibaki amepigwa na butwaa asipate jibu kama Jack naye alikuwa mtu wa kitengo huko mpaka afahamiane na huyo mwanamke au walijuana vipi kwenye hizo kazi zao! Jambo ambalo lilimfanya ajipe ahadi ya kumtafuta huyo mrembo lakini kwa wakati huo alikuwa na jambo moja la kufanya, jambo hilo lilikuwa ni kuwahi nyumbani kwa mwanasheria huyo kwani aliamini kukamatwa kwake kungemfanya nyumba yake kuwa pweke hivyo alihitaji kwenda kufanya uchunguzi huko huenda kuna vitu vya mhimu angeweza kuvipata ambavyo vingemsaidia kumuweka nuruni.
Kwenye jumba la mwanasheria Jack, Edison alishtuka kwenye usingizi mkali, usingizi ambao ulimfanya kichwa chake kuuma isivyokuwa kawaida. Hakuwahi kukutana na hali kama hiyo kiasi kwamba alale bila kujitambua, kichwa chake kikawaka taa nyekundu na kuhisi kwamba kuna jambo halikuwa sawa. Aliwaza kwa umakini sababu ya msingi ambayo ilimfanya kuishia kwenye hali hiyo, akakumbuka mara ya mwisho alipewa juisi nzito na Jack, kwamba juisi ilikuwa na dawa? Roho yake ni kama ilisita kuamini, kama Jack alimpatia juisi ya kumfanya alale kwa muda mrefu alikuwa na lengo gani? Alishtuka kama mtu ambaye alikumbuka jambo, alisogea mbele yake na kuiwasha runinga ili kujua kama kuna jambo lolote lile.
Baada ya kuiwasha runinga ndipo alijihakikishia kwamba mtu yule alimpatia ile juisi ndani yake ikiwa na dawa kwa sababu maalumu. Edison alikuwa amekata shauri kwamba asingeruhusu kijana huyo afe, alihitaji kumsaidia na hiyo kazi ya kuwatafuta hao watu alikuwa anaenda kuifanya mwenyewe. Kuamua kwake kumsaidia JACK THE LAWYER ndiko ambako kulipelekea Jack kufanya uamuzi huo ili wakati EdJr amelala ili autumie huo muda kukamilisha hilo jambo. Kwenye runinga aliona waandishi wa habari kutoka sehemu mbalimbali wakiwa wanaripoti habari hizo taarifa zao zikiwa zimeambatanishwa na video pamoja na picha za mwanasheria huyo akiwa anachukuliwa na watu wa Ikulu ofisini kwake.
Ile ni taarifa ambayo ilimsikitisha kwa kiasi kikubwa hasa baada ya kutambua kwamba mwanaume yule aliamua kuitambulisha sura ya EdJr kama sura yake yeye binafsi jambo ambalo alijua lilikuwa linaenda kuwa na mwisho mbaya kwa kijana yule aliye jitoa sadaka kwa ajili ya kumsaidia yeye ili aweze kukamilisha mambo yake. Aliangalia kwa umakini wakati ambao Jack alikuwa anaongea na Aaliyah, alimkumbuka mwanamke yule ndiye ambaye Jack alimsisitiza kumtafuta kwani angekuwa na msaada mkubwa kwa upande wake.
Edison aliitoa simu yake moja mfukoni ambayo ilikuwa ina ulinzi wa kutosha na kuitafuta moja ya namba wakati huo, namba hiyo ilikuwa imechanganywa tarakimu kiasi kwamba mtu wa kawaida angeiona asingejua kwamba imewahi kuwepo namba ya aina hiyo. Alipiga kwenda kwenye namba hiyo, simu iliita mara ya kwanza mpaka ikakata, iliita kwa mara ya pili ikakata, mara ya tatu ndipo ilipokelewa na upande wa pili ikasikika sauti ya mwanamke mtu mzima;
“Nani wewe?”
“Hakikisha Jack The Lawyer anakuwa hai, kama kuna tatizo lolote likimpata basi mimi nitakuua kwa mkono wangu”
“Unajua unaongea na nani?”
“Ndiyo, najua kwamba naongea na mkurugenzi wa shirika la IBA Lionela Philson”
“Wewe ni nani hasa?”
“Hilo swali litunze kama hautafuata kile ambacho ninakwambia basi utaniuliza siku ambayo utaniona kwa mara ya kwanza na ya mwisho kwenye maisha yako”
“We mpuuzi una…..”
“Hakikisha Jack anakuwa salama tena kwenye mikono yako” aliongeza Edison kwa msisitizo wakati anayakatisha maongezi ya mwanamke huyo na kuikata hiyo simu. Simu hiyo aliirushia chooni na kuifrash kwa sababu haikuwa na kazi tena, kuendelea kuwa hewani ingemletea matatizo. Akiwa anawaza kujua hatua ambayo alikuwa anatakiwa kuichukua kwa wakati huo, alisikia makelele, kelele za ugomvi kutokea nje ya jumba hilo hali ambayo ilimfanya kutoka nje mara moja kujua kulikuwa na nini.
Nje ya jengo hilo kulikuwa na ugomvi mkali kati ya wale walinzi wa Jack na mtu ambaye hakujulikana zaidi ya kuificha sura yake. Kwa mwonekano tu alikuwa ni mwanamke yule, alikuwa ni mkatili mno mbele ya wale wanaume wanne hali ambayo ilimpelekea kuwaua wanaume wawili ndani ya muda mfupi. Alikuwa anajiandaa kumfanyia mauaji mwanaume wa tatu ila hakuipata hiyo nafasi baada ya kupokea maumivu ya kwenye nyonga mpaka alihisi kwamba kiuno chake kinavunjika.

UKURASA WA 64 unafika mwisho.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 65

Alidondokea mbali lakini hakuwa mnyonge, alijiviringisha kwa sarakasi na kusimama kwenye mkono wake akiwa ameshika visu viwili ambavyo vilikuwa na damu ya kutosha, kiunoni kwake alipachika bastola mbili. Alikuja akiwa anavizungusha visu vyake kuelekea kwa Edison kwa ghadhabu kali kwani alihisi kama watu hao wanamfanyia masihara kwa sababu mmoja alikuwa amekematwa muda mfupi lakini hapo mbele yake alikuwa anamuona mwingine tena. Ujio wake ulikuwa wa kasi kubwa akiwa makini kwenye urushaji wa visu vyake, kasi yake ilikuwa ndogo ukilinganisha na mtu ambaye alikuwa anamshambulia, Kisu kimoja kilimkosa Ed kwenye mbavu na kingine kilipita karibu n bega lake.
Alirudi nyuma kidogo wakati anakuja kwa mara nyingine mkono wake ulirushwa kwa nguvu kiasi kwamba ungempata mtu huyo angekuwa kwenye hali mbaya ila alifanikiwa kuukwepa, kuukwepa mkono huo ikawa hatari zaidi kwake kwa sababu Ed aligeuka na mguu wake ambao ulitua kwenye uso wa mwanamke huyo na kumfanya apige kelele ya maumivu, mguu ulikoma isivyokuwa kawaida. Akiwa anayumba yumba alifikiwa na kutulizwa na ngumi ya kifua mithili ya nyundo. Alijitahidi kusimama ngangali ila hakuweza kwani alitapika damu kutokana na maumivu ambayo aliyapata kwenye kifua chake, alivirusha visu vyake kuelekea kwa mtu huyo wakati akizitoa bastola kwenye kiuno chake lakini hakufua dafu, Edison aliinama chini kuvipisha visu hivyo kiasha akajinyanyua kwa sarakasi mithili ya mzimu uliotokea ardhini.
Sarakasi yake ilitua kwenye miguu ya mwanamke huyo ambayo ilimchota chini akabaki anaambaa ambaa mithili ya mpira wa kutengwa, alipokea goti kali la tumbo, licha ya kutoa kilio lakini hakupewa muda wa kujipanga kwani kabla ya kutua chini alidakwa na kupokea ngumi kali ya kwenye taya akadondoka chini. Hata bastola zake hakujua zimedondokea wapi, wakati anafika chini alipigwa na mguu kwenye tumbo lake kama ambavyo huwa unapigwa ule mpira wa kutengwa wa penati hali ambayo ilimfanya aburuzike na kwenda kujibamiza kwenye tairi la gari mpaka gari hiyo ikayumba yumba mara kadhaa. Alikuwa anahema kwa shida akiwa hajaingiza ngumi hata moja kwa mwanaume huyo ambaye alihisi kwamba labda alikuwa anapambana na jinamizi kwani binadamu wa kawaida asingekuwa hivyo.
Edison alisogea pale ambapo alikuwepo mwanamke yule akiwa anatweta kama mtu ambaye alikuwa anaomba msaada lakini alikuwa jeuri kutamka kwa kinywa chake, alimfunua kile kitambaa usoni na kuona namna ambavyo uso ulikuwa umeiva kwa maumivu na damu ikiwa inamtoka kwenye mdomo wake na puani. Alimwangalia kwa umakini ile sura haikuwa ngeni kwake, aliijua sura ile kwa muda na mwanasheria ndiye alimuonyesha na kupewa masharti na Jack kwamba anatakiwa kumlinda mwanamke huyo kwa gharama yoyote ile. Alikuwa ni Nicola Aidan Semzaba.
Kumuona mwanamke huyo kulimfanya akumbuke mbali, alikumbuka kipindi ambacho walikuwa wanaishi na wenzake kama ndugu kambini kwao wale makomando wenzake tisa. Mwanamke huyo alikuwa anajua kwamba yeye ndiye muuaji wa kaka yake hivyo alikuwa akimtafuta ili kuweza kumuua kwa mara ya kwanza kabisa alikuwa anakutana naye kwenye maisha yake akiwa kama adui yake lakini Nicola yeye hakuwa na hilo wazo kabisa hali iliyompa mshangao mkubwa kwa kuwa alikuja hapo kutafuta kama angepata ushahidi wa namna yoyote ile wa kumsaidia kujua ambayo alihisi hayajui ndipo akakutana na hiyo sura ambayo ilimpa maswali mengi kwa sababu muda mchache uliokuwa umepita aliishuhudia sura kama hiyo ikikamatwa.
Edison alimbeba mwanamke huyo na kumpeleka mpaka ndani kwenye chumba cha matibabu, Nicola alipokea maumivu makali tena ya kiume hivyo hali yake haikuwa sawa japo alitamani kumfahamu mtu huyo, yeye alikuwa ni nani na yule mwingine alikuwa ni nani? Je walikuwa ni mapacha? Aliamua kuupa muda nafasi kwanza, wakati huo alitakiwa kutibiwa kwanza na ndicho ambacho kilikuwa kinafanyika huku wao kila mtu akiwa kimya bila kuongea jambo lolote matibabu yakiwa yamechukua nafasi yake. Alimtibu kwa dakika kumi na tano kisha akatoka ndani ya hicho chumba kumuacha aweze kumpumzika kwani alijua mrembo huyo alikuwa na maswali mengi kwenda kwake.
Alirudi baada ya saa zima kuisha akiwa na dawa pamoja na matunda kwenye sahani, alimpatia dawa mwanamke huyo, halafu yakafuata matunda ambayo aliyafakamia utahisi ni mtu ambaye hakula kwa siku nyingi. Baada ya kujiona yupo sawa alimgeukia Edison ambaye alikuwa ameketi kwenye kiti kilichokuwa pembezoni kwa kitanda hicho kikiwa kinatazamana na kitanda
“Wewe ni nani?”
“Ni mtu ambaye unatamani kuniona nikiwa nimekufa”
“Haujajibu swali langu”
“Mimi ni muuaji wa kaka yako kama ambavyo wamekutaka wewe uamini hivyo”
“Na yule ambaye amekamatwa kule ni nani?”
“Niambie kwanini umekuja hapa na kuanza kuua watu?”
“Nimekuja kwa sababu ya kutaka kuhakiki maneno ambayo aliniambia mwanasheria ambaye sijui kama ni wewe au ni yule. Maneno yake akidai kwamba nalishwa sumu kupambana na jambo ambalo sio la kweli yalinigusa kwa namna fulani kwa sababu niliamua kufuatilia jambo hilo na kweli nikapata ukakasi. Nikiwa nahitaji kukutana naye ndipo nikaona akifanya ule mkutano hivyo nilijua ni suala la muda tu yeye kuingia matatizoni hali ambayo ilinifanya niwahi kutaka kukutana naye lakini kwa bahati mbaya wakati nafika pale nilikuwa nimechelewa. Sikuona sehemu yoyote ile ya kuweza kupata nilichokuwa nakihitaji zaidi ya kuja kufanya uchunguzi nyumbani kwake ila kwa bahati nafika hapa nakutana na mtu mwingine kama yeye”
“Ni kitu gani ambacho wewe umekuja kukitazama hapa ili kupata huo ukweli ambao unautafuta?”
“Nataka kujua muuaji halisi wa kaka yangu, je ni nyie au kuna mambo mengine ambayo siyajui?”
“Wewe imani yako inakwambia muuaji ni nani?”
“Nimeishi miaka yote hii nikimtafuta mtu kama wewe lakini kwa sasa hata sijui niyaamini vipi mawazo yangu”
“Umeisikiliza taarifa ambayo ameitoa Jack?”
“Ndiyo”
“Ule ndio ukweli halisi, hakuna sehemu hata moja ambayo amedanganya”
“Kama yule ni Jack na wewe ni nani?”
“Mimi ndiye huyo ambaye umeishi miaka yote ukihitaji kukutana naye ili uweze kulipa kisasi”
“Wewe ndiye Edison Christian?”
“Ndiyo”
“Kivipi! Mbona Jack amejitambulisha kwamba yeye ni wewe?”
“Ni hadithi ndefu ya maisha yangu mimi na yeye ila mimi mwenyewe nimekutana naye muda mfupi ambao umepita”
“Kwamba anatumia sura bandia ya kufanana na wewe?”
“Hilo linaweza kuwa jibu sahihi”
“Haiwezekani, kivipi mtu ahatarishe maisha yake kwa ajili yako wewe halafu unaniambia hata hamkuwa mnajuana?” Edison hakuongea tena bali alimpa kitabu mwanamke huyo aweze kukisoma, kitabu ambacho kilikuwa na historia nzima ya maisha ya Edison.
Muda ambao aliutumia kusoma kitabu hicho ni muda ambao aliutumia kujutia na kumwaga machozi. Walimwengu walimuaminisha kuhusu taarifa ambazo hazikuwa za kweli naye akazivaa kama zilivyokuwa, alizibeba habari za kuambiwa bila kuwa na uhakika kiasi kwamba aliutumia muda mrefu wa maisha yake kumchukia mtu ambaye hakustahili hiyo chuki huku akifanya kazi na watu ambao ndio alipaswa kuwachukia kwa maisha yake yote. Nicola alijisikia vibaya mno na kujiuliza vipi kama angemuua mtu ambaye hakuwa na hatia kabisa kwenye maisha yake, hakika hakuona namna ambayo ingefanya MUNGU amsamehe kama ageitekeleza dhambi hiyo.
Taarifa zote za mhimu juu ya historia ya mtu huyo zilikuwa kwenye kichwa chake sasa, hakuwa na maswali tena kuhusu utambulisho wa jack ilikuwa ni yeye kufanya maamuzi ya hatua ambayo ilitakiwa kufuata baada ya hapo.
“Mimi natakiwa kufanya nini?” ndiyo kauli ya kwanza ambayo aliitamka baada ya muda mrefu kupita akiwa anaupata ukweli wa kitabu hicho ambacho kiliandikwa kwa mkono wa bwana Edward Pande.

UKURASA WA 65 unafika mwisho.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 66

“Kwa sasa wewe hautakiwi kufanya jambo lolote wala kujionyesha kwamba kuna kitu unajua kwani wakifahamu hiyo basi wewe ni maiti inayo tembea”
“Ila kwa sasa mimi hawawezi kuniua”
“Kwanini?”
“Kwa sababu nina mzigo wao wa thamani kubwa”
“Mzigo upi?”
“Mzigo wa dhahabu wa Madam Kate”
“Madam Kate ndiye nani?”
“Nadhani ndiye kiongozi wa jambo hili ambalo linaendelea”
“Ni mtanzania?”
“Ndiyo”
“Maana yake sio bosi mwenyewe”
“Umejuaje hilo?”
“Kwa sababu mwanzilishi wa hili jambo sio mtanzania. Kama kweli una huo mzigo wao wa thamani kubwa kama unavyo dai basi hawawezi kuwa wanakuacha hivi hivi lazima kuna watu watakuwa wanakufuatilia kwa kila hatua ambayo unaipiga na siku ambayo watafanikiwa kujua sehemu ambayo mzigo wako upo basi watakutesa kisha kukuua” Nicola alibaki kama amechanganyikiwa, Edison alisogea kwenye kabati ambapo alitoa laptop na frash mfukoni. Alihitaji kujua yaliyokuwa kwenye ile frashi hasa yalikuwa ni yapi maana tangu aipate frash hiyo hakuwahi kuifanyia kazi wala kutazama yaliyokuwa humo ndani kiasi kwamba mpaka yaondoke na maisha ya Issa kule Jangwani.
Walicho kishuhudia humo ndani kilikuwa kinatisha, kulikuwa na mipango mikakati yote kuanzia taarifa za baba yake Edison, kuuawa kwake na makomando wenzake lakini mpaka taarifa za ndani za jamii hiyo. Baadhi ya majina ya memba wa hiyo jamii likiwemo jina la daktari Namaki Prasad bila kumsahau bosi ambaye alikuwa ni Zulpha Mazipa, jina hilo alilikumbuka vyema kabisa kwa sababu lilikuwa jina la mama yake mzazi, kupitia hilo alithibitisha kwamba mama yake alikuwa hai tena akiwa ndiye kiongozi wa umoja huo kwa taarifa ambazo zilikuwa zimeainishwa hapo ndani.
Wote walibaki wameduwaa kama watu ambao wanaulizana maswali ila hakukuwa na wa kuweza kuyajibu kwa wakati huo.
“Inawezekana Madam Kate ndiye…….!” Nicola alikatishwa na Edison
“Yeah nadhani ndiye mama yangu mzazi”
“Oohhh shiiit! Nadhani hii ni habari mbaya sana kwako”
“Yeaha haiwezi kuwa nzuri”
“Kwamba mama yako ndiye mhusika wa haya mambo yote ambayo yanafanyika?”
“Inaonekana hivyo”
“Unaweza ukamkumbuka kwa sura labda?”
“Hapana sidhani kwa sababu ilikuwa ni zamani mno”
“Kwahiyo unahisi utafanya nini?”
“Siku ambayo nitakutana naye ana kwa ana ndiyo siku ambayo nitajua kitu ambacho natakiwa kukifanya ila kwa sasa bado sijui. Najaribu kuwaza ni mama wa namna gani anaweza kuamua kumuacha mtoto wake kwa kumkimbia! Ni mama wa namna gani hajawahi hata kujihangaisha kumtafuta mtoto wake licha ya taarifa kibao kusambaa kila sehemu kuhusu uwepo wangu tena nikipewa kesi ambayo sikuhusika nayo? Nina maswali mengi ya kumuuliza”
“Kama yeye ndiye kiongozi maana yake yeye ndiye ambaye anapanga mipango yote ili wewe uweze kufa”
“Hilo ndilo jambo ambalo siwezi kuyapata majibu yake mpaka sasa mpaka siku ambayo mimi nitakutana naye”
“Mimi naweza kuwasiliana naye na kuna mtu mmoja tu peke ambaye anaweza kutusaidia sisi kukutana au kufanikiwa kuongea naye”
“Nani?”
“Anaitwa Saimon, ni kijana wake mtiifu na wa karibu kwake japo nahisi amesha anza kunishtukia na sidhani kama ananiamini tena baada ya kumuuliza baadhi ya maswali”
“Kwani wewe huyu Madam Kate haumfahamu kwa sura?”
“Hapana, wakati nafanya naye mawasiliano sura yake ilikuwa imezibwa”
“Maana yake kama anaziba sura yake basi kwenye maisha ya kawaida atakuwa ana jina lingine ambalo analitumia mbali na hilo la Madam Kate pamoja na jina lake la kuzaliwa la Zulpha Mazipa, lazima kuna jina lingine ambalo analitumia na hilo ndilo jina ambalo nalihitaji”
“Saimon ndiye mtu pekee ambaye atatusaidia kwa hilo”
“Basi wewe unatakiwa kurudi na kuendelea na maisha kama ya mwanzo kwani kama ukipotea kwa sasa lazima watakuwa na mashaka na wewe. Kwa sasa nataka kukutana na yule binti mpelelezi Aaliyah, baada ya hapo utanipeleka kwa huyo Saimon”
“Sawa, kuwa makini Edison” alitamka kinyonge Nicola, ni kama alijihisi amani na salama kuwa karibu na mtu huyo lakini muda haukuwa sahihi. Mambo ambayo waliyaona kwenye frash hiyo yalikuwa na maelezo ya mipango mingi ambayo ilikuwa imechukua maisha ya watu wengi mno lakini kulikuwa na majina ambayo mengine hawakuwahi kuyasikia popote lakini yake machache ambayo walikuwa wameyapata nayo walitakiwa kuyafanyia kazi kubwa ili kuweza kuwapata wahusika wake ambao ndio walikuwa wamiliki wa majina hayo hususani mama yake mzazi ambaye ndiye alidaiwa kuwa kiongozi wa jamii hiyo ya siri na huenda ndiyo sababu kubwa ambayo iliwafanya watu hao kuitafuta hiyo frash kwa nguvu kubwa kwa sababu ya uwepo wa jina la bosi wao ndani ya taarifa zilizokuwa ndani.

Aliamshwa na maji ya baridi kali, alishtuka kwani ubaridi wake haukuwa wa kuvumilika kirahisi hali ambayo ilimfanya ajihisi alitundikwa ndani ya friji ambayo haikuwahi kuzimwa kwa mwaka mzima. Kushtuka kwake kulipokelewa na taa zenye mwanga mkali, ilimlazimu kuyafumba macho yake kisha akayafumbua kwa mara nyingine macho yakiwa yanaona nyota nyingi mbele yake. Baada ya muda wa dakika tano macho yake yalirudisha uangavu wake, hapo ndipo akagundua kwamba alikuwa ametekwa na watu ambao hakuwafahamu na hiyo haikuwa shida kwake kwa sababu alikuwa ni mtu mwenye soko kubwa kwenye utafutwaji wake.
Kumbukumbu zake zilimpa fahamu ya kumrudisha nyuma kujua kilichokuwa kimetokea, ndipo alikumbuka jambo ambalo lilitokea kipindi ambacho walikuwa wamefika pale Morocco baada ya kutoka kufanya mazungumzo na raisi wa nchi akiwa anasafirishwa kwenda mahali ambako binafsi hakuwa akijua kwamba ni wapi. Eneo lile alilikumbuka kwa usahihi kutokana na tukio la kutisha ambalo lilitokea pale kisha yeye akabebwa na watu wasio julikana na baadae akachomwa sindano tatu kwenye mwili wake zilizo mfanya akazima na wakati anarejesha fahamu zake ndipo alijikuta akiwa ndani ya eneo hilo. Alitoa tabasamu hafifu kwa sababu hakuwa na matumaini yotote ya maisha yake tena na hilo alikuwa analitambua vizuri kwamba ana muda mchache wa kuendelea kuivuta pumzi ya dunia, hali hiyo haikumsumbua hata kidogo alijiandaa maisha yake yote kuikabili.
Chumba ambacho alikuwepo kilikuwa kikubwa, kilizungukwa na walinzi wenye silaha kali kila kona huku mwanaume mmoja mbavu ambaye alikuwa kifua wazi ndiye ambaye alikuwa anashughulika naye kwenye suala zima la kuhakikisha anaamka na kuwa macho kwa kumpatia dozi ya hayo maji ya baridi kali. Alikisa kichwa chake kukiweka vyema kwani alijua hapo asingepata nafasi ya kulala kwa mara nyingine tena. Lango la chumba hicho lilifunguliwa ndipo aligundua kwamba kulikuwa kumekucha tayari hususani baada ya kufanikiwa kuuona mwanga wa jua kwa mbali kutokana na nafasi finyu ambayo ilikuwepo wakati lango lile linafunguliwa.

UKURASA WA 66 unafika mwisho.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 66

“Kwa sasa wewe hautakiwi kufanya jambo lolote wala kujionyesha kwamba kuna kitu unajua kwani wakifahamu hiyo basi wewe ni maiti inayo tembea”
“Ila kwa sasa mimi hawawezi kuniua”
“Kwanini?”
“Kwa sababu nina mzigo wao wa thamani kubwa”
“Mzigo upi?”
“Mzigo wa dhahabu wa Madam Kate”
“Madam Kate ndiye nani?”
“Nadhani ndiye kiongozi wa jambo hili ambalo linaendelea”
“Ni mtanzania?”
“Ndiyo”
“Maana yake sio bosi mwenyewe”
“Umejuaje hilo?”
“Kwa sababu mwanzilishi wa hili jambo sio mtanzania. Kama kweli una huo mzigo wao wa thamani kubwa kama unavyo dai basi hawawezi kuwa wanakuacha hivi hivi lazima kuna watu watakuwa wanakufuatilia kwa kila hatua ambayo unaipiga na siku ambayo watafanikiwa kujua sehemu ambayo mzigo wako upo basi watakutesa kisha kukuua” Nicola alibaki kama amechanganyikiwa, Edison alisogea kwenye kabati ambapo alitoa laptop na frash mfukoni. Alihitaji kujua yaliyokuwa kwenye ile frashi hasa yalikuwa ni yapi maana tangu aipate frash hiyo hakuwahi kuifanyia kazi wala kutazama yaliyokuwa humo ndani kiasi kwamba mpaka yaondoke na maisha ya Issa kule Jangwani.
Walicho kishuhudia humo ndani kilikuwa kinatisha, kulikuwa na mipango mikakati yote kuanzia taarifa za baba yake Edison, kuuawa kwake na makomando wenzake lakini mpaka taarifa za ndani za jamii hiyo. Baadhi ya majina ya memba wa hiyo jamii likiwemo jina la daktari Namaki Prasad bila kumsahau bosi ambaye alikuwa ni Zulpha Mazipa, jina hilo alilikumbuka vyema kabisa kwa sababu lilikuwa jina la mama yake mzazi, kupitia hilo alithibitisha kwamba mama yake alikuwa hai tena akiwa ndiye kiongozi wa umoja huo kwa taarifa ambazo zilikuwa zimeainishwa hapo ndani.
Wote walibaki wameduwaa kama watu ambao wanaulizana maswali ila hakukuwa na wa kuweza kuyajibu kwa wakati huo.
“Inawezekana Madam Kate ndiye…….!” Nicola alikatishwa na Edison
“Yeah nadhani ndiye mama yangu mzazi”
“Oohhh shiiit! Nadhani hii ni habari mbaya sana kwako”
“Yeaha haiwezi kuwa nzuri”
“Kwamba mama yako ndiye mhusika wa haya mambo yote ambayo yanafanyika?”
“Inaonekana hivyo”
“Unaweza ukamkumbuka kwa sura labda?”
“Hapana sidhani kwa sababu ilikuwa ni zamani mno”
“Kwahiyo unahisi utafanya nini?”
“Siku ambayo nitakutana naye ana kwa ana ndiyo siku ambayo nitajua kitu ambacho natakiwa kukifanya ila kwa sasa bado sijui. Najaribu kuwaza ni mama wa namna gani anaweza kuamua kumuacha mtoto wake kwa kumkimbia! Ni mama wa namna gani hajawahi hata kujihangaisha kumtafuta mtoto wake licha ya taarifa kibao kusambaa kila sehemu kuhusu uwepo wangu tena nikipewa kesi ambayo sikuhusika nayo? Nina maswali mengi ya kumuuliza”
“Kama yeye ndiye kiongozi maana yake yeye ndiye ambaye anapanga mipango yote ili wewe uweze kufa”
“Hilo ndilo jambo ambalo siwezi kuyapata majibu yake mpaka sasa mpaka siku ambayo mimi nitakutana naye”
“Mimi naweza kuwasiliana naye na kuna mtu mmoja tu peke ambaye anaweza kutusaidia sisi kukutana au kufanikiwa kuongea naye”
“Nani?”
“Anaitwa Saimon, ni kijana wake mtiifu na wa karibu kwake japo nahisi amesha anza kunishtukia na sidhani kama ananiamini tena baada ya kumuuliza baadhi ya maswali”
“Kwani wewe huyu Madam Kate haumfahamu kwa sura?”
“Hapana, wakati nafanya naye mawasiliano sura yake ilikuwa imezibwa”
“Maana yake kama anaziba sura yake basi kwenye maisha ya kawaida atakuwa ana jina lingine ambalo analitumia mbali na hilo la Madam Kate pamoja na jina lake la kuzaliwa la Zulpha Mazipa, lazima kuna jina lingine ambalo analitumia na hilo ndilo jina ambalo nalihitaji”
“Saimon ndiye mtu pekee ambaye atatusaidia kwa hilo”
“Basi wewe unatakiwa kurudi na kuendelea na maisha kama ya mwanzo kwani kama ukipotea kwa sasa lazima watakuwa na mashaka na wewe. Kwa sasa nataka kukutana na yule binti mpelelezi Aaliyah, baada ya hapo utanipeleka kwa huyo Saimon”
“Sawa, kuwa makini Edison” alitamka kinyonge Nicola, ni kama alijihisi amani na salama kuwa karibu na mtu huyo lakini muda haukuwa sahihi. Mambo ambayo waliyaona kwenye frash hiyo yalikuwa na maelezo ya mipango mingi ambayo ilikuwa imechukua maisha ya watu wengi mno lakini kulikuwa na majina ambayo mengine hawakuwahi kuyasikia popote lakini yake machache ambayo walikuwa wameyapata nayo walitakiwa kuyafanyia kazi kubwa ili kuweza kuwapata wahusika wake ambao ndio walikuwa wamiliki wa majina hayo hususani mama yake mzazi ambaye ndiye alidaiwa kuwa kiongozi wa jamii hiyo ya siri na huenda ndiyo sababu kubwa ambayo iliwafanya watu hao kuitafuta hiyo frash kwa nguvu kubwa kwa sababu ya uwepo wa jina la bosi wao ndani ya taarifa zilizokuwa ndani.

Aliamshwa na maji ya baridi kali, alishtuka kwani ubaridi wake haukuwa wa kuvumilika kirahisi hali ambayo ilimfanya ajihisi alitundikwa ndani ya friji ambayo haikuwahi kuzimwa kwa mwaka mzima. Kushtuka kwake kulipokelewa na taa zenye mwanga mkali, ilimlazimu kuyafumba macho yake kisha akayafumbua kwa mara nyingine macho yakiwa yanaona nyota nyingi mbele yake. Baada ya muda wa dakika tano macho yake yalirudisha uangavu wake, hapo ndipo akagundua kwamba alikuwa ametekwa na watu ambao hakuwafahamu na hiyo haikuwa shida kwake kwa sababu alikuwa ni mtu mwenye soko kubwa kwenye utafutwaji wake.
Kumbukumbu zake zilimpa fahamu ya kumrudisha nyuma kujua kilichokuwa kimetokea, ndipo alikumbuka jambo ambalo lilitokea kipindi ambacho walikuwa wamefika pale Morocco baada ya kutoka kufanya mazungumzo na raisi wa nchi akiwa anasafirishwa kwenda mahali ambako binafsi hakuwa akijua kwamba ni wapi. Eneo lile alilikumbuka kwa usahihi kutokana na tukio la kutisha ambalo lilitokea pale kisha yeye akabebwa na watu wasio julikana na baadae akachomwa sindano tatu kwenye mwili wake zilizo mfanya akazima na wakati anarejesha fahamu zake ndipo alijikuta akiwa ndani ya eneo hilo. Alitoa tabasamu hafifu kwa sababu hakuwa na matumaini yotote ya maisha yake tena na hilo alikuwa analitambua vizuri kwamba ana muda mchache wa kuendelea kuivuta pumzi ya dunia, hali hiyo haikumsumbua hata kidogo alijiandaa maisha yake yote kuikabili.
Chumba ambacho alikuwepo kilikuwa kikubwa, kilizungukwa na walinzi wenye silaha kali kila kona huku mwanaume mmoja mbavu ambaye alikuwa kifua wazi ndiye ambaye alikuwa anashughulika naye kwenye suala zima la kuhakikisha anaamka na kuwa macho kwa kumpatia dozi ya hayo maji ya baridi kali. Alikisa kichwa chake kukiweka vyema kwani alijua hapo asingepata nafasi ya kulala kwa mara nyingine tena. Lango la chumba hicho lilifunguliwa ndipo aligundua kwamba kulikuwa kumekucha tayari hususani baada ya kufanikiwa kuuona mwanga wa jua kwa mbali kutokana na nafasi finyu ambayo ilikuwepo wakati lango lile linafunguliwa.

UKURASA WA 66 unafika mwisho.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Big up FEBIANI BABUYA
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 67

Iliingia sura ya mwanamke ambaye huenda hakuwa anategemea kumuona hapo, mwanamke ambaye alikuwa akimfahamu vizuri kwa sababu alikuwa mtu mashuhuri ndani ya taifa la Tanzania na hakuwa mashuhuri tu bali mfanya biashara mkubwa aliyekuwa na mafanikio ya kutosha mbele ya umma. Ni mwanamke ambaye alikuwa anaandikwa mpaka kwenye vitabu na watoto wakamsoma shule, alikuwa ni mwanamke ambaye alikuwa mfano mkubwa wa mapambano hususani kwa watoto wa kike, Cersie Mhina. Lilikuwa ni jambo la ajabu kwake kuweza kumuona mwanamke huyo asijue kwamba alikuwa anahusika vipi na jambo hilo ila aliamua kujipa nafasi na muda wa kujua kilichofanya akaishia kwenye mikono ya mfanya biashara huyo ambaye alikuwa anamiliki jengo kubwa la MHINA PLAZA.
Mwanamke huyo alikuwa ndani ya vazi la gharama kubwa akiwa amejifunika na koti la manyonya na mkoba wake mdogo mkononi lakini baada ya kusogea eneo alilokuwepo mwanasheria Jack, mwanaume mmoja alimvua bosi wake koti hilo na kulishika pamoja na ule mkoba aliushika kwenye mkono wake. Mwanamama huyo aliletewa sigara moja akiwa anaiwasha kwa mikogo kisha akaketi kwenye kiti safi ambacho kiliandaliwa umbali kiasi kutoka pale alipokuwepo Jack. Aliuvuta moshi wake kwa hisia kali akiwa anamwangalia Jack kwa umakini kwenye uso wake.
“Huenda hukutegemea kama ungekutana na mimi siku ya leo mwanasheria, huenda utakuwa unajiuliza mengi kwamba kwanini niwe mimi ambaye nimekuchukua kutoka kwenye mikono ye serikali!”
“Hapana hilo halinishangazi kwa sababu dunia ina mengi ya kushangaza ila kitu ambacho sikipatii jibu ni kwamba kwanini uwe wewe?”
“Nilitegemea ungeniuliza swali hilo ila nina mambo mengi ya kwenda kuyafanya kwa wakati huu hivyo nitahitaji mazungumzo yetu yawe mafupi. Mwanangu yuko wapi?” hiyo kauli ndiyo ambayo ilimfanya Jack atabasamu na kutikisa kichwa.
“Kwahiyo kumbe wewe ndiye madam Kate, wewe ndiye ambaye upo nyuma ya haya kutekeleza kile ambacho mabosi wako walikiacha kwenye mikono yako? Bila shaka wewe ndiye ambaye unajua alipo Irina Espanovich?” Jack alikuwa anazitamka hizo silabi akiwa anacheka, ungehisi kwamba alikuwa mtu mwenye furaha isivyo kawaida lakini haikuwa kweli, alikuwa anacheka kwa sababu ulimwengu ulikuwa unampa elimu ambayo asingeweza kuipata kwenye darasa lolote lile.
“Unaonekana ulikuwa unalifuatilia jambo hili kwa ukaribu, hivyo unanifahamu japo hukuwa ukijua kama ndiyo mimi. Sina haja ya kuzunguka kukuficha kwa sababu mazungumzo yetu yanatakiwa kuwa mafupi, mimi ndiye huyo ambaye unamsema na kweli mimi ndiye ambaye najua alipo Irina na mumewe Novack Nyangasa lakini hili umelijua wakati mbovu kwa sababu hautakuwa na sehemu pa kulipeleka. Nijibu nilicho kuuliza” alisikitika Jack kwani huenda alitegemea mengi ila sio hilo ambalo alikutana nalo wakati huo.
“Unathubutu vipi kujiamini mbele ya mwanao baada ya ushetani ambao uliufanya kwa miaka ambayo imepita huko nyuma?”
“Mimi ndiye nilimnyonyesha yule mtoto na kuibeba mimba yake, haijalishi imepita miaka mingapi bila kumtia machoni ila huwezi kuwa wewe, niambie Edison yuko wapi?”
“Ningejisikia vibaya sana kama ningekuwa na mama wa aina yako wewe, namskitikia Edison kwa sababu alistahili kuwa na mama bora zaidi yako. Mama ambaye unaisaka roho ya mwanao kuliko unavyo utafuta utajiri, una uhakika siku ukikutana naye ana kwa ana utakuwa na ujasiri wa kumtamkia kauli kama ambazo unanitamkia mimi?”
“Anajua kwamba mimi nipo hai?”
“Anajua hilo ila kitu ambacho hajui ni kipi ambacho atakufanya siku anakutia kwenye mkono wake. Sijui utajisikia vipi kufia kwenye mikono ya mtoto wako wa damu tena ukifa kama gaidi kwake?” mwanamama huyo alitabasamu kwa hasira kwa sababu kauli hiyo ilimuuma kwenye moyo wake na kumchoma vilivyo.
“Nahitaji unijibu Edison yuko wapi na kwanini wewe ujifanye ni yeye ili kutudanganya sisi?”
“Kwa sababu anatakiwa kuishi na kulimaliza hili ambalo mlilianza”
“Unahisi unatujua sana kijana?”
“Huenda kuliko unavyo fikiria wewe, ushahidi wote Edison anao hivyo kama mlishindwa kumuua mkiwa na nafasi kule Somalia, basi sahau hilo kwa sasa kwa sababu ni suala la muda tu kabla hajakufikia wewe hapo”
“Kumbe ndiye wewe ambaye ulimuokoa kule Somalia?”
“Mzee alikuwa sahihi kunitengeneza mimi kwa sababua lijua kwamba maisha yangu yangekuja kuwa na umuhimu siku moja kwa Edison”
“Kwahiyo ulitengenezwa ili kuyalinda maisha yake?”
“Ndiyo, alizaliwa kwa ajili ya kazi hii. Ni miaka mingi imepita huenda angekuwa amelimaliza hili lakini alitolewa kumbukumbu zake za nyuma ila kwa sasa nimemrudishia hizi kumbukumbu zake zote kwahiyo kila taarifa anayo na usiku wa leo ninavyo zungumza kuna mtu wako wa karibu lazima afe. Kuua watu kulinda siri zako, kumuua yule daktari Namaki usihisi upo salama, unahesabiwa ni siku tu za kujihisi upo salama na baada ya hapo utakumbana na aibu ambayo utatamani dunia ijivue nguo ikufunike wewe usionekane kwenye haya maisha”
“Unaonekana ni mtu mwenye jeuri na kujiamini kijana wangu lakini huenda hujui yale ambay unayazungumza, mimi niliitoa sadaka familia yangu ili niishi. Mpaka nafikia hatua ya kuwa na nafasi kubwa kama hii haikuja kwa bahati mbaya bali kwa kuipigania kwa nguvu zangu, nimeua watu wengi, nimeudhalilisha mwili wangu na kudhalilika kwa baadhi ya watu mpaka nikafika hapa halafu mpuuzi mmoja tu kama wewe unaongea kirahisi kuhusu mimi?”
“Kitu pekee ambacho nakusihi uweze kukifanya ni kutumia kila rasilimali uliyo nayo asije akaujua utambulisho wako, kwa sababu haukijui kile kiumbe, baada ya kurudishiwa kumbukumbu zake ndio wakati ambao rasmi ameufuta ule ubinadamu ambao upo kwenye nafsi yake hivyo usihangaike kumtafuta atakutafuta yeye, wewe nenda ukamsubiri unapohisi panakufaa kufanya hivyo”
“Niambie ni wapi alipo mwanangu” aliongea kwa sauti ya ukali akinyanyuka na kwenda kwa mlinzi wake mmoja kuchukua ile silaha AKA 47, Jack hakuogopa bali aliishia kucheka kwa sauti kali
“Malaya mkubwa wewe” ndiyo kauli peke ambayo aliitoa kwenda kwa mama huyo, kauli hiyo haikuvumilika kwake, alipandwa na hasira kiasi kwamba alisahau kama kijana huyo alikuwa ni mhimu zaidi kwake akiwa hai, alimmiminia risasi nyingi kifuani. Habari ya JACK THE LAWYER waweza kumuita CHRISPIN MWAMBANO ikawa inafika tamati kama ambavyo alikuwa akihitaji siku zote za maisha yake kwenda kupumzika akiwa ameitimiza kazi yake ya kuokoa maisha ya wengi duniani. Madam Kate alipiga kelele kwa hasira kali ambazo ziliuponda ponda moyo wake akiwa mwingi wa ghadhabu.”
“Mwili wake mkautupe katikati ya barabara ya Ubungo pale juu kabisa, kwa sababu anataka kujifanya dunia iamini amekufa basi acha tumwaminishe hivyo kwamba na sisi tumeamini kwamba amekufa kama anavyotaka yeye. Namhitaji huyu mpuuzi akiwa mzima wa afya kabisa kisha mimi nitakuwa na mazungumzo naye binafsi kama mama na mwana.

Habari zilikuwa za moto kwa upande wake raisi Faraji Asani, kupokea taarifa za kuvamiwa kwa msafara ambao aliuandaa kwa ajili ya kumsafirisha mtu wake lilikuwa jambo la kutisha kwa upande wake. Alifura kwa hasira akiwa anashangaa kwamba ni mtu wa aina gani huyo ambaye alikuwa na hiyo jeuri ya kufanya jambo la ajabu kama hilo? Aliinyanyua simu yake kwenda kwa mkurugenzi wa IBA usiku huo huo ambao aliipokea taarifa hiyo. Simu iliita mara moja na kupokelewa.
“Nakuhitaji Ikulu muda huu”
“Sawa bosi” yalikuwa mazungumzo mafupi mno ambapo simu ilikatwa. Baada ya saa moja kuweza kupita, gari ya mkurugenzi ilikuwa inaingia ndani ya Ikulu akiwa anaonekana kama mtu mwenye haraka, alikuwa amezipata taarifa za tukio ambalo lilitokea kule Morocco hivyo alijua kwamba lazima ndiyo ilikuwa sababu kubwa ya yeye kuweza kuitwa wakati huo. Alishuka kwenye gari na kutembea haraka haraka kuelekea kwenye ofisi ndogo ya raisi ambayo mara nyingi alikuwa akiitumia kwa ajili ya mazungumzo binafsi na watu wake wa karibu. Siku hiyo Ikulu ilikuwa tofauti na siku zingine, tangu lilipo tokea lile tukio, kulikuwa na ulinzi mkali isivyokuwa kawaida.

UKURASA WA 67 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 68

“Heshima yako bosi”
“Sina haja na salamu zako, nahitaji maelezo ya kilicho tokea huko”
“Huko sina taarifa zozote za maana mpaka sasa ila kufikia asubuhi nitakuwa na taarifa kamili ya kukupatia”
“Unajua wakati nakuteua wewe hapo kuwa mkurugenzi wa nafasi nyeti kama hii nilipokea lawama nyingi na ukosoaji mkubwa kutoka kila pande ya nchi na Afika. Wengi walidai kwamba mwanamke hawezi kuongoza nafasi kubwa kama hii kwa sababu wanawake wamezoea kuendeshwa, lakini nilikubali kukupa nafasi hii kwa sababu nilikuamini hivyo usitake kuniambia nilikupa nafasi hii kimakosa, kumbuka ninaweza kukutoa muda wowote hapo hivyo sitaki unipe maelezo ya kitoto namna hii kwenye ishu kubwa kama hii ambayo wananchi watahitaji maelezo yaliyo shiba ukizingatia mtu ambaye amepotea ni mtu wanaye mpenda sana”
“Naomba unisamehe sana mheshimiwa lakini nina imani tatizo hili limetokea nje ya mikono yangu, haukunishirikisha juu ya hatua ambazo ulikuwa unaenda kuzichukua na nina imani kama ungekuwa umenishirikisha tangu mwanzo sidhani kama lingefikia huku ambako limefikia hivyo sijioni kuwa na hatia kwenye hili. Kuhusu wananchi usijali, tunatakiwa kupika taarifa za kuwapa kwa sababu hatujui mtu ambaye amemchukua ana mipango gani na mwanasheria na huenda ni watu ambao hawakutakii mema wanaweza kumuua na kesi itakugeukia wewe hivyo tunatakiwa kucheza mchezo mapema”
“Nakusikiliza”
“Kama tutampata akiwa hai basi kesi itakuwa rahisi kwetu lakini kama tutaipata maiti yake basi tunatakiwa kumgeuzia kibao yeye mwenyewe. Inatakiwa tuue baadhi ya maaskari wetu wa serikali”
“Whaaaaat!? Yaani niue askari wangu bila sababu?”
“Ungenisikiliza kwanza kiongozi ili ujue pointi yangu iko wapi”
“Endelea”
“Tukiua askari wetu hata kumi hivi, tunatengeneza tukio halafu tunaeleza kwamba mtu huyo alikuja kuokolewa na watu wake ambao ndio walikuwa wamepanga mipango yote michafu tangu mwanzo hivyo jana aliamua kuupika uongo ambao anaujua yeye ili kujitoa nje ya hatia wananchi wamuone kama mtu mwema wakati sio kweli. Serikali ilimshikilia ili aweze kusema ukweli na kutaja wenzakea mbao amekuwa anashirikiana nao hivyo alikuja kwako hapa akakubali kwamba ni kweli taarifa zake zilikuwa za uongo na ameamua kulisaidia taifa baada ya wewe kufanya naye makubaliano ya yeye kusema ukweli ili asiliingize taifa kwenye machafuko” Mwanamama huyo alikunywa maji kidogo akaendelea;
“Kwa sababu ulimpa heshima kwa kazi kubwa ambayo alilifanyia taifa ukaamua kumpa nafasi hiyo kwa ajili ya kutumia nafasi hiyo ili kujisafisha na aweze kusamehewa kama atakubali kuisaidia nchi. Ndipo hapo ukaamua kumsafirisha ili kumpeleka kwenye safe house ya taifa kwa ajili ya kuhakikisha yupo salama lakini kumbe lilikuwa ni kosa kubwa kumuamini kwa sababu hao magaidi wenzake ambao amekuwa akishirikiana nao ndio ambao walivamia msafara na kuondoka naye baada ya kuua maaskari wengi wa Ikulu”
“Mpango wako umekaa vizuri mno na nimeupenda ila bado sijapata muunganiko wa kuuawa kwa maaskari na kesi ya mwanasheria huyu”
“Hapo baadae ndipo maaskari wanaingia, kwamba baada ya watu hao kutekeleza tukio hilo ulianza kufanyika uchunguzi mkali kujua wako wapi kwani kuwepo kwa mwanasheria huyo uraiani ilikuwa ni hatari kwa usalama wa nchi na ndipo askari mmoja alipogundua mahali ambapo walikuwepo baada ya kumuona mwanasheria huyo akishuka kwenye gari. Baada ya kuwaona aliwapigia simu wenzake na ndipo walipo anza zoezi la kurushiana risasi mpaka umauti ukampata mwanasheria huyo baada ya kupigwa risasi”
“Umenishawishi nisijutie kukuweka kwenye hiyo nafasi, kumbe unaweza kuwa na matumizi makubwa kwangu kwa hapo baadae, sasa tutajuaje kwamba kama akifa atakufa kwa risasi au mtu aliye naye atamuua kwa risasi?”
“Maana yake sisi ndio tunatakiwa kuwa watu wa kwanza kabisa kumpata kwa namna yoyote ile, wanatakiwa kusambazwa askari wa siri kila kona, wanajeshi wavae nguo za kiraia wawepo kila eneo la hadhara, kila eneo ambalo lina muunganiko wa barabara nyingi na kwenye fukwe za bahari”
“Kwanini yawe ni hayo maeneo?”
“Kwa saabbu kama muuaji akimuua mtu kama yule lazima atahitaji umma ujue na ili umma ujue anatakiwa kuwekwa kwenye maeneo ya hadhara ndiyo ambayo yatakuwa rahisi kufikika au mwili wake kuonekana” Raisi alitabasamu, alikuwa anamlaumu bure mwanamke huyo ila kilikuwa ni kichwa haswa kwenye mipango mikali kama hiyo.
“Unaamini kwamba yule ni Edison kweli?”
“Hapana bosi”
“Inanichanganya sana, kwanini haya yote yaweze kutokea na kipi kinakufanya uwe na uhakika wa moja kwa moja kwamba yule mtu siye mwenyewe bali anatuchezea akili?”
“Kwenye suala la mgawanyo wa muda hesabu zinagoma kabisa, kama angekuwa mwenyewe kuna eneo moja angekuwa anakosekana kwa urahisi. Wakati ambao Lamaeck alikuwa anahitajika kambini muda wote alikuwepo na muda huo huo mwanasheria alikuwa anaendelea na kesi zake ila alikosekana siku moja tu ile ambayo lilitokea tatizo lile Somalia hivyo yule sio yeye ila anajua alipo mtu huyu na anamlinda japo sababu ya kumlinda kwake ndiyo bado sijaijua mpaka sasa”
“Kwahiyo kuna uwezekano kwamba Edison ndiye amemteka?”
“Hiii haiingii akilini, kama alikuja kujidhihirisha wazi na kukubali kukamatwa maana yake walifikia makubaliano na watu wake, ni jambo ambalo lisingewezekana yeye kuja kumteka tena hivyo sio yeye”
“Unataka kuniambia ni LS, wakubwa wameamua kufanya haya?”
“Hapana, kama jambo hilo lingefikia huko basi ningekuwa na hizo taarifa”
“Hakikisha huo mpango wako unafanya kazi, lakini nina wasiwasi kubwa kwa zile siri ambazo huyu mpuuzi ameziweka wazi na wananchi wamezisikia. Alikuwa anaaminika mno kwa watu yule hivyo wataamini ni ukweli na jambo hili linaweza kuleta hatari kubwa huko mbeleni hususani kwenye hiki kiti changu hivyo naliacha kwenye mikono yako hakikisha haufanyi kosa hata moja na nataka kujua ambacho utakifanya kwenye hili”
“Hatua ya kwanza ni hii ya kuanza kumchafua kama nilivyo kweleza hapo mwanzo, tukimchafua tutawagawa watu, kuna wengine hawataendelea kumuamini tena na huo muda tutautumia kupika uongo mwingine ambao utawafanya wananchi kurejesha imani kwako na wakati huo mwanasheria huyu atakuwa amekufa”
“Na huyu bwana mdogo ambaye alipona huko Somalia?”
“Huyu ni suala la muda mchache umebaki tuweze kujua ni wapi alipo, kama mwanasheria amejitokeza hadharani na ndiye mtu ambaye kama tungemtesa angetupa ukweli ila hayupo tena ila naamini vijana wangu watakuwa na majibu mpaka kesho asubuhi hivyo mapema tutakuwa naye”
“Sihitaji uzembe wala kosa lolote katika hili” raisi hakumalizia sentensi yake, mdomo wake ulidakwa na mdomo wa mwanamama huyo Lionela Philson. Mwanamke huyo alikuwa ni hawala wake wa muda mrefu na ndiyo sababu kubwa ambayo ilimbeba mpaka akaweza kuipata nafasi hiyo ambayo alikuwa nayo. Hawakujali kama walikuwa kwenye ofisi kubwa na ya heshima ya nchi watu hao walicho kiangalia na kuhakikisha mioyo yao inapata kile ambacho ilikuwa inakitaka. Lionela alivua nguo zake zote kisha akamvua na mheshimiwa, walibaki uchi wa mnyama kabisa na kwa mikogo Lionela alimlaza mheshimiwa kwenye kochi kubwa ambalo lilikuwa pembeni kisha naye akapanda kwa juu, kilicho fuata ni kelele za kuudhi na kumdhihaki alitekuwa akiwasikiliza. Raha zilikuwa upande wao.
Asubuhi ya mapema, Lionela alikuwa anaingia ofisini kwake, siku hiyo hakutokea nyumbani kwake bali alitokea kwenye ile ofisi ambayo waliidhalilisha kwa mgongo wa kujifanya kwamba walikuwa wanapanga mipango mikali ya usalama wa nchi. Kabla hajaingia ofisini simu yake ya mfukoni ilikuwa inaita, baada ya kuangalia aligundua kwamba ni CDF alikuwa anapiga. Aliikadiria simu hiyo mwisho wa siku akaamua kuipokea.
“Mbona tunasumbua na asubuhi yote hii”
“Lionela, siwaelewi wewe na raisi, hili jukumu tunahitaji kulifanya pamoja, nchi kwa sasa ipo kwenye machafuko, wananchi wanauliza maswali magumu na hakuna majibu yoyote ambayo yanatolewa. Raisi yupo kimya, wewe upo kimya halafu ubaya raisi hapokei hata simu zangu, mimi ni mkuu wa majeshi wa taifa hili mnataka nijifikirie vipi labda na niwaelewe vipi kwenye jambo la mhimu kama hili ambalo mnaonekana kulichukulia poa?”

UKURASA WA 68 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 69

“Kwani wewe unataka nini?”
“Upo siriasi unanijibu mimi kama hivyo?”
“Jambo la wewe kutopokelewa simu na raisi mimi linanihusu nini? Hayo ni makubaliano yenu nyinyi wawili acha kunipa lawama za kijinga. Mimi silali kupambania hali ya usalama wa taifa langu halafu unakuja kunipa lawama za kijinga na asubuhi yote hii. CDF unatakiw akujiheshimu sana”
“Wewe ndiye ambaye unatakiwa kujiheshimu mpuuzi wewe, unanipigia makelele hapa kwamba unapambana kuweka hali ya usalama wakati unafanya umalaya na raisi wa nchi ambaye wananchi wanamhitaji. Hauna hata aibu unakwenda kumkatikia viuno vyako raisi tena kwenye ofisi ya nchi, huna haya mwanamke wewe, huu upuuzi ukiendelea nitafanya maamuzi magumu ambayo yatawashangaza wote. Mtu ameshajulikana kwamba ni mhalifu mnamtetea, leo hii anaingia kwenye mikono yenu mnajifanya amepotea mara katekwa halafu mkuu wa majeshi sipewi taarifa yoyote, mwambie huyo raisi wako anitafute kabla siku haijaisha” aliongea kwa jazba kali kisha akaikata simu hiyo. Alihisi kama watu hao walikuwa wanamuengua taratibu kwa sababu isingewezekana mambo yawe yanatokea tena ya mhimu kwa taifa halafu yeye kama mkuu wa majeshi hapewi taarifa zozote zile za maana.
Mkurugenzi alihema hata ile mood ambayo alikuwa nayo ilikata ghafla. Aliipiga simu yake muda huo huo kwenda kwa raisi.
“CDF anajua kila kitu kuhusu mimi na wewe, ametishia kufanya jambo baya hivyo mtafute. Anajua mengi hivyo anaweza kuwa tatizo kwa hapo baadae” Ulipita ukimya kidogo bila shaka alikuwa anasubiri jibu upande wa pili, alijibiwa na simu ikakatwa. Baada ya kuingia kwenye ofisi yake alishtuka, hofu ilijichora kwenye uso wake kwani alikuwa amejiachia na maongezi mlangoni asijue kwamba ndani kulikuwa na mtu. Aaliyah Beka alikuwa amesimama karibu na mlango akimsubiri bosi wake, mama huyo alionyesha kuchukizwa na jambo hilo isivyokuwa kawaida.
“Kwanini unanisimamia mlangoni kama umeniajiri?”
“Uliwahi kuniambia nisikae kwenye hivi viti kabla haujanipa ruhusa, ungejisikiaje kama ningevunja amri yako bosi?”
“Ni muda gani umenisikiliza nikiwa naongea na simu hapo nje?”
“Hakuna nilicho kisikia, nimewahi hapa kwa sababu nina mambo mhimu sana mbayo nataka kuongea na wewe bosi” Aaliyah alizuga kama hakuna kitu alisikia ila uhalisia ni kwamba alisikia mazungumzo yote, akachagua kuuchuna kwani kama angegundulika kujua lolote au kusikia basi maisha yake yangekuwa matatani kuanzia wakati huo.
“Niambie kwamba umepata taarifa zote ambazo nilikuwa nazihitaji”
“Naweza kusema taarifa zipo nusu na zingine pia nazitegemea kutoka kwako”
“Unamaanisha nini?”
“Yale maneno ambayo ameyaongea mwanasheria ni ya kweli?”
“Unaniulizaje swali kama hilo?”
“Kwa sababu nataka kujua ukweli, mimi ndiye mtu ambaye umenipa kazi hii kuifanya hivyo natakiwa kujua naanzia hapa namalizia pale lakini kuna mahali nafaika nakwamba kwa sababu ni kama napata taarifa nusu nusu”
“Huenda sijakuelewa, nenda kwenye pointi yako ya msingi”
“Kwenye kufuatilia maisha ya mwanasheria huyu na kujiita kwake Edison kuna mambo ambayo nimeyapata kutoka kwake lakini yana ukakasi. Kwanza nina uhakika hata wewe unajua kwamba yeye sio Edison japo faida kwake ni kwamba wananchi wameliamini hilo japo nao wana maswali mengi. Kesi hii imenirudisha nyuma miaka kadhaa ambayo ilikuwa imepita, kuanzia kifo cha raisi Justin Nyangasa, mwanasayansi Christian Edison, vifo vya wale makomando tisa wa KILL ON MISSION. Ukiachana na hayo imenipatia jambo jipya la agent wa zamani wa KGB Irina Espanovich ambaye ndiye anadaiwa kuwa mwanzilishi wa jamii ya siri ya LUNATIC SOCIETY ambayo tuliwahi kulipata faili lake lakini tukaamuriwa kuifunga kesi hiyo kwa sababu ilionekana kwamba ni nadharia ambazo hazipo (Conspiracy theory) na serikali ikagoma kutenga bajeti kwa ajili ya kufuatilia kesi hiyo hivyo tukaamriwa kulifunga faili hilo na mpaka sasa halijawahi kujulikana lilifichwa wapi” Aaliyah alikuwa makini kuangalia mwitikio wa uso wa bosi wake akiwa analielezea jambo hilo.
“Licha ya kuwa kama nadharia lakini imeonekana kwamba watu wengi wamekufa ili kulinda juu ya uwepo wa jamii hiyo ya siri ambayo sijui kama kweli ipo na kama ipo inajishughulisha na nini, ipo chini ya nani na mlengo wake mkubwa ni upi? Hivyo hii ndiyo kesi ambayo inaweza kunifanya nikampata Edison kwa saa ishirini na nne tu ila natakiwa kuifahamu kiundani na kila kitu chake kwa sababu majibu ambayo nitayapata hapa yatanipa mwongozo ambao utanifanya niunganishe doti na kufikia lengo langu haraka. Najua wewe ni mtu ambaye ni wa ngazi ya juu kiusalama kwenye taifa hivyo kama kuna habari kama hizi lazima utakuwa na taarifa zake za ndani kabisa, kwa vile nakuamini nahitaji kama hii jamii ipo basi unipe maelezo yake na kama haipo basi unithibitishie kwa sababu mimi nakuamini wewe” kauli ya mwisho ndiyo ilimpa ahueni mheshimiwa Lionela, alikuwa ameanza kuhema kwa shida ila aliamini kwamba hakuna alijualo la maana binti huyo.
“Hizo habari umezipatia wapi Aaliyah?”
“Nimezipata wakati nafuatilia kesi ya mwanasheria bosi”
“Nisikilize kwa umakini Aaliyah, hakuna kitu kama hicho wala hakijawahi kutokea kitu kama hicho kwenye taifa hili. Hakuna jamii yoyote ya siri, hizo ni propaganda za baadhi ya mataifa ya nje ambayo tuligundua kwamba walikuwa na mlengo wa kutumia mwanya huo kuanzisha jambo la ajabu kwenye taifa hili kwa ajili ya maslahi yao ila tulilipinga mapema na kufutilia mbali mipango hiyo. Siwezi kukwambia kila kitu kwa sababu ni taarifa za siri na za juu kimamlaka hivyo sina hiyo nafasi ya kukwambia wewe hapo. Kuhusu Christian Edison pia ni mambo ambayo ni ya siri za ulinzi za nchi hivyo siwezi kukufungikia mambo yote hapa. Jambo ambalo unataka kulielewa ni kwamba kuna watu ambao wanatumia nafasi hii kuhitaji kutuchanganya sisi ili waitumie nafasi hiyo kukamilisha mambo yao na nitafurahi zaidi kama hautakuja kuniletea hizo nadharia kwa mara nyingine tena kwenye ofisi yangu”
“Nimekuelewa bosi” alijibu kinyonge Aaliyah kwa sababu aliona bosi wake anamdanganya wazi wazi
“Bado haujaniambia ulipo fikia kwenye kazi ambayo nilikupa”
“Moja kati ya malengo ya kazi hii ilikuwa ni kumjua mwanasheria huyu kiundani. Hilo ni jambo ambalo nadhani nipo wazi hata kwako ila ni kwamba Edison yupo hai kweli na yupo mjini hapa hapa”
“Unajua ni wapi ambako anapatikana?”
“Ni mwanasheria pekee ambaye alikuwa analijua hilo”
“Na unajua ni kitu gani ambacho amepanga kukifanya kwa sasa?”
“Bado, inatakiwa tuwe makini kufuatilia tukio lolote ambalo litafanyika kuanzia sasa, kama naye atahusika kwenye tukio la namna yoyote ile basi itawezekana kumpata kirahisi”
“Hilo jambo lifanyie kazi kwa uharaka mkubwa kwa sababu raisi anauliza maswali magumu ambayo kuna muda yananipa ugumu kuweza kuyapata majibu yake”
“Sawa bosi” alitoa heshima na kutoka humo ndani moyo wake ukiwa unatetemeka. Alikuwa kwenye hali hiyo baada ya kugundua kwamba hata bosi wake alikuwa anamdanganya, asingemdanganya hivi hivi bila kuwa na sababu ya msingi lazima kuna mambo ambayo alikuwa anayafahamu kama sio kuyaficha yasiweze kumfikia binti huyo. Alizikumbuka kauli za mwanasheria kabla watu wa Ikulu hawajaondoka naye kwamba asiwaamini hata watu wake wa karibu hususani huyo mkurugenzi wake. Sasa jambo hilo lilianza kumuingia akilini, mtu pekee ambaye alikuwa ana uwezo wa kumsaidia kwenye hilo alikuwa ni Edison mwenyewe, maana yake yeye ndiye alikuwa anatakiwa kuwa wa kwanza kabisa kuweza kuonana na Edison, sasa angempatia wapi? Hakujua hivyo akatoweka ndani ya ofisi hiyo.
Mkurugenzi Lionela Philson alishangazwa mno na maswali ambayo alikuwa anaulizwa siku hiyo na kijana wake Aaliyah, alikuwa akimfahamu binti huyo kiundani kwa muda mrefu ila wakati huo alihisi kama kuna vitu vingi kwenye kichwa cha mwanamke huyo hakuwa akivijua. Isingekuwa kwa bahati mbaya kuja kumuuliza maswali kama hayo, alikuwa akichungulia dirishani kumuangalia jasusi huyo akiwa anatoka nje kabisa ya ofisi hizo akiwa na mashaka naye, hakutakiwa kumwamini tena kwa wakati huo. Aliinyanyua simu yake na kumpigia mtu ambaye alimsevu J2 ikiwa na maana ya Jumapili.

UKURASA WA 69 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 70

“Sina imani na Aaliyah, ebu mfuatilie kwa ukaribu kila hatua ambayo anaipiga kisha utakuwa unakuja kuripoti kwangu. Fuatilia ujue anajua nini, anakutana na nani, muda mwingi anashinda wapi? Ila hakikisha hajui kwamba unamfuatilia kwa sababu akikukamata sidhani kama atakusame na mimi sitaingilia kwenye hilo, kwahiyo ukikamatwa you are on your own” hakusubiri jibu upande wa pili akaikata simu hiyo.
Saa moja jioni Aaliyah alikuwa anarudi nyumbani kwake ambako alikuwa akiishi. Alikuwa anaishi eneo la Kawe karibu na vilipo viwanja wa Tanganyika Parkers, ilikuwa ni hatua ya dakika kumi tu mpaka kufika eneo hilo ukiwa unatembea kwa mguu. Nyumba yake ilikuwa ya siri, hakuna mtu ambaye aliwahi kumjua mmiliki zaidi ya kuonekana gari ikiingia eneo hilo na kutoka. Jioni hiyo alikuwa na mengi ya kuyawaza kichwani mwake hususani kwa kazi ambayo alikuwa nayo mbele yake, hakujua aanzie wapi na aishie wapi kwani watu ambao walikuwa wanamtuma ndio hao hawakuonekana kuwa waaminifu kwake hata kidogo.
Baada ya kuingiza gari yake ndani, alifungua mlango wa nyumba kubwa lakini nyumba haikuwa sawa, hisia zake ziliufanya moyo wake kwenda kwa haraka hali ambayo ilimfanya atazame vizuri kila sehemu kama kulikuwa na dalili zozote za uwepo wa mtu kwenye hilo eneo lakini hakuona hata hivyo hakutaka kukaa kijinga, aliichomoa bastola yake na kuiweka sawa huku akiwa anaelekea ghorofa ya juu taratibu. Baada ya kuingia ndani alishangaa kuona kuna mtu ndani ambaye alistarehe kama yupo kwake, mkononi mwake alikuwa na gazeti, juu ya meza akiwa anaweka juisi kwenye bilauri anainywa taratibu huku anapitia gazeti lake.
“Nyoosha mikono juu” aliongea kwa jaziba, alihisi ni dharau kwake mtu kuvamia nyumba yake kirahisi namna hiyo.
“Nina muda mchache wa kuongea na wewe hivyo weka hiyo bastola yako chini kwa sababu kuna mahali natakiwa kuwepo” ilisikika sauti nzito kwenye masikio yake mtu huyo akiwa anaachia gazeti ambalo lilimfunika uso wake, uso kwa uso alikuwa anakutana na Edison mwenyewe kwa mara ya kwanza kabisa kwenye maisha yake. Alibaki ameduwaa asiamini mtu huyo alifikaje na kuingia ndani, ni mtu ambaye alitamani kupata nafasi ya kuweza kukutana naye na kufanya naye mazungumzo na hakujua angempatia wapi kwa sababu alikuwa anaishi kwa siri ila wakati huo alikuwa amejileta mwenyewe ndani kwake. Aliangaza kila upande kuangalia kama labda kulikuwa na watu wengine ila aligundua kwamba alikuwa ni mmoja tu pekee.
“Umeingiaje humu ndani?”
“Nimepasua dirisha lako la nyuma nikaingia kirahisi tu. Tuachane na hizi habari za kitoto ambazo hazijanileta hapa, nilitakiwa nikuue wewe hapo lakini kuna mtu alinishauri unaweza kuwa msaada kwangu kwa baadae. Je hilo ni jambo la uhakika?”
“Kwanini umechagua kuishi maisha ya namna hii EDISON?”
“Acha kujifanya una uchungu na maisha yangu bibie, jikite kwenye swali ambalo nimekuuliza”
“Mimi mpaka sasa sijui nipo upande upi, miaka yote nimefanya kazi kwa kujituma lakini nakuja kugundua kwamba hata mkubwa wangu wa kazi ananidanganya! Imeniuma sana”
“Ulikuwa miongoni mwa watu ambao walikuwa wanaisaka roho yangu kwa udi na uvumba, nafikiri ni suala la muda tu kabla hawajaanza kukutengenezea kesi na kukuwinda, utaelewa aina ya maisha ambayo nimeyaishi miaka yote hii na ladha yake inakuwaje”
“Kwa sasa unahitaji kufanya kitu gani?”
“Nataka kuuteketeza hii jamii yao ya siri yote mpaka wote wafe”
“Hilo ni jambo gumu kwa sababu hujui nani yupo upande wako na nani hayupo nawe”
“Hata wewe haupo upande wangu?”
“Unahisi kirahisi tu naweza kumuamini mtu ambaye taifa zima lilikuwa linamtafuta kama gaidi kwa kuhusika na mauaji ya wenzake tisa? Unataka nimuamini mtu ambaye ameigiza kifo chake na sasa watanzania wanaenda kujua kwamba umekufa? Unataka nimuamini mtu ambaye amemtoa sadaka mwanasheria ili yeye aishi? Nitakuwa binadamu wa ajabu sana”
“Sikuja hapa kukubembeleza, nimekuja hapa kwa sababu ni maelekezo ambayo nilipewa na Jack ila nadhani mimi na wewe hatuwezi kuwa sehemu moja hivyo kuanzia sasa nakuhesabia kama adui yangu na nakuahidi huenda wakati ujao tutakutana sehemu ambayo itanilazimu kukuua” Edison alinyanyuka baada ya kuongea maneno hayo na kutaka kuondoka lakini alisikia sauti ya bastola ikikokiwa kwa mara nyingine tena, hakuogopa bali alimsogelea Aaliyah pale kwenye sofa na kumuinamia.
“Nina uhakia umelisoma faili langu vyema ila bado haujawahi kuniona kwa macho yako hadharani, mimi sio binadamu wa kuanza kujibizana na binti wa kike kama wewe na usije ukathubutu kuninyooshea hii bastola tena kwenye maisha yako yote kwa sababu nitakuua” Aaliyah hakukubaliana na huo ukweli wa kutishiwa nyau wakati alikuwa na mikono yote miwili, alimvuta Edison ghafla na kumtia kichwa cha uso akihitaji kumwekea bastola kichwani ila kitu alifanywa hata yeye alibaki anajutia.
Mkono wake ulidakwa na kuteguliwa kwenye bega, alipigwa ngumi ya taya akiwa ameshikiliwa mkono ulioteguka. Kibao kilipita kwenye shavu lake akahisi amebugia kitu kwenye mdomo wake. Wakati huo alikuwa amesimama, kupigwa kwake kulifanya ayumbe yumbe hali ambayo ilifanya apigwe na mguu wa kwenye goti akataka kudondokea mbele, alikutanishwa na kisigino cha uso ambacho kilimzoa mpaka kwenye kabati ambalo lilikuwa pembeni, kabati lilivunjika. Edison alisogea pale kwenye kabati akiwa anamwangalia mwanamke huyo mtata.
“Huwa sipendi kupiga piga wanawake ndiyo maana nimekupiga kwa kukudekeza ila hili ni onyo la mwisho. Huapo kwenye listi ya watu ambao nawahitaji labda kama nitalikuta jina lako huko mbele au kama utaingia katikati ya njia yangu kwa kigezo cha kudai kwamba unatimiza kazi yako hivyo hili liwe mwanzo na mwisho mimi sijali lolote kuhusu sheria binti” alimatamkia kwa msisitizo, aliisogelea bastola akatoa risasi zote na kuipasua. Edison akawa anatoka taratibu kwenda mlangoni lakini aliisikia sauti ya majuto ikimuita
“Stop please!” Aaliyah aliongea akiwa anajinyanyua kwa maumivu.
“Naweza kufanya kazi na wewe” alijibu akiwa anaunyoosha mkono wake mpaka ulipo kaa sawa.
“Kipi kimeyabadili mawazo yako?”
“Kwa sababu watu ambao niliwaamini wameivunja imani yangu”
“Unataka kulisaliti shirika lako?”
“Yeah kama ambavyo jeshi na serikali vilikusaliti wewe”
“Kwahiyo kwa sasa ndo umejua kwamba nilisalitiwa?”
“Ndiyo, sitaki kurudia makosa kama hayo”
“Kwahiyo unataka kufanya nini?”
“Nitaifanya hii kazi ya kuudondosha umoja huu pamoja na wewe, nitazitafuta taarifa za ndani kwa bosi na nikizipata tu basi nitakupatia kila kitu cha ndani ili tuiteketeze kuanzia ndani”
“Kazi yako kubwa kwa sasa ni kuhakikisha unajifanya upo nao bega kwa bega kwa sababu nahitaji ufuatilie nyendo za bosi wako kila mahali, ujue anafanya nini, anakutana na nani na kwa sababu zipi”
“Hilo naweza kulifanya lakini vipi kuhusu maisha ya mwanasheria?” Edison aliiangalia saa yake ya mkononi
“Atakuwa ameshakufa saivi”
“Unawajua walio mteka?”
“Ni hawa hawa ambao nawatafuta kwa sababu walijua alishakuwa hatari kwao, sikutaka hili litokee lakini aliniwekea dawa ya usingizi hivyo akanitoroka, wakati nashtuka nilikuwa nimechelewa”
“Kwahiyo unataka kuniambia kwamba hata raisi anaweza kuwa mhusika ndiyo maana amempoteza mtu huyu makusudi kwa kigezo cha kutekwa?”
“Usiwaamini viongozi wako kupitiliza. Fanya nilicho kuagiza”
“Nikiwa na taarifa za kukupa nakupata wapi?”
“Nitakutafuta mwenyewe”
“Kwahiyo na wewe haujui ni wapi alipo Irina Espanovich?” Edison alimwangalia Aaliyah kwa umakini bila kumpatia jibu, mwanamke huyo alikuwa na uhusiano wa moja kwa moja na mama yake mzazi hivyo kuliweka wazi jambo hilo ingekuwa hatari kubwa hususani kwa mama yake kwani hakutaka mwanamke huyo aingie matatizoni kabla hajakutana naye na kufanya mazungumzo. Alitamani awe mtu wa kwanza kabisa kumpata kwa sababu alikuwa na mengi ya kumuuliza mwanamama huyo ambaye hakuwahi kuonyesha kujali kuhusu uwepo wake huku yeye ndiye akiwa kinara wa kutafutwa kwake nchini.

UKURASA WA 70 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 71

SURA YA SABA
JNIA ilikuwa imefunguliwa na shuguli zote zilikuwa zinaendelea kama kawaida. Walionekana wanaume wawili wakiwa kwenye suti zao mithili ya wafanya biashara wakubwa wakiwa wanaingia ndani ya eneo hilo. Walikuwa ni majasusi kutoka ndani ya nchi ya Uganda ambao walikuwa wamekuja kwa ajili ya kufuatilia kwa ukaribu kile ambacho kilitokea kule hususani kupeleleza kuhusu uhalisia wa Yohan Mawenge na namna ya kuweza kumpata yeye na mtandao wao kwa sababu alikuwa na kesi ya kujibu.
Baada ya kukamilisha taratibu zote hapo uwanjani, hatimaye waliweza kutoka nje kabisa wakiwa wanatembea kwa mguu. Madereva wengi wa tax walijaribu kuwashawishi waweze kuingia kwenye magari yao lakini hakuna hata mmoja ambaye alijishugulisha nao zaidi ya kufuata kile ambacho walikuwa wamekipanga wao. Wanasema mjini fuata kilicho kuleta bwana! Na ndicho ambacho walikuwa wanakifanya wanaume hao wawili.
Walitokezea mpaka barabarani, barabara ambayo ilikuwa inaelekea Gongo la Mboto. Walisimama hapo na kuangaza, wote waliyavusha macho yao ng’ambo baada ya kusikia mlio wa honi kutoka kwenye gari ambayo ilikuwa imepaki kule ambako walikuwa wameyaelekezea macho yao. Alphard nyeusi ilikuwa ikiwasubiri, kwa sababu mida ya jioni barabara hiyo huwa ina foleni kubwa, walisubiri kwa dakika moja ndipo wakafanikiwa kuvuka huku watu wakiwa wanawashangaa, hawakuonekana kuwa watu wepesi hivyo waliwashangaza wapita njia kwa namna walivyokuwa wakiranda randa hapo barabarani.
Kwenye ile gari kulikuwa na wanaume wawili ambao nao hawakuwa wanyonge kwa mionekano yao, walishiba vilivyo. Wanaume hao walikuwa ni double agents, yaani ni wale wapelelezi ambao walikuwa wanakula sehemu mbili, kwa asili walikuwa ni watanzania lakini kwa muda mrefu walikuwa wakipokea bakshishi kutoka kwa serikali ya Uganda hivyo kuwa kama wauza siri za nchi kwa serikali ya uganda jambo ambalo kiuhalisia lilikuwa ni uhaini kwa nchi yao.
Walisalimia kwa dakika moja kisha gari hiyo ikaondoshwa hapo kwa mwendo mkali lakini hali hiyo haikudumu kwa sababu ya foleni kuwa kubwa hivyo ilimlazimu dereva kuwa mpole na kuendesha kistaarabu kwa sababu hakuwa na namna. Hayo mambo yote yalitokea kwa muda mfupi na kwa umakini mkubwa ila haikuwa kwa umakini kama ambavyo walihisi wao kwa sababu kuna mtu alikuwa analifuatilia jambo hilo tangu watu hao wanaingia uwanja wa ndege mpaka wanatoka nje ya uwanja huo akiwa kwenye gari yake aina ya BMWX5. Alitumia gari hiyo ya kwaida ili asije kushtukiwa, ni gari ambayo mtu yeyote angeiona angehisi kwamba alikuwa ni mtafutaji tu na asingehisiwa kuwa mtu wa kutisha au mtu hatari.
Alikuwa ni mwanaume mmoja shupavu, sura yake ilikuwa imenona kwa matunzo ambayo alionekana kuyapata, hakuonyesha dalili za shida kabisa kwake. Aliwaona watu hao tangu wanavuka barabara kwa sababu alikuwa anadili na lile gari ambalo lilikuwa limepaki, naye alipaki pembezoni wa fremu moja gari ikiwa imezimwa kabisa hivyo hakuna mtu angeweza kuhisi kwamba kuna lolote linaendelea ndani ya gari hiyo ila alikuwa makini kwa kila hatua. Alihakikisha mpaka ameshuhudia watu hao wakiwa wanaingia ndani ya hiyo gari ndipo alifungua droo na kutoa sura bandia, sura ambayo haikuwa yake, ilikuwa ni sura ya Yohani Mawenge, bila shaka alikuwa ni yeye mwenyewe.
Kwa mara ya kwanza alituthibitishia kwamba alikuwa akiitumia sura isiyo yake kwa ajili ya kufanyia kazi zake za hatari, hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya ulinzi wake binafsi. Alikuwa na uhakika kwamba ingefika siku moja ambayo watu wangehitaji kumkamata ndiyo maana alikuwa akizuga na hiyo sura huku akiwa na maisha yake mengine mbali na sura hiyo ambayo aliitengeneza kwa ajili ya kazi. Alikuwa amepewa kazi na bosi wake Madam Kate kuhakikisha hao watu wote wanakufa na kuupoteza ushahidi, jambo hilo la kufuatilia kile ambacho alikuwa amekifanya Uganda hakikutakiwa kuendelea kwa namna yoyote ile kwani lilikuwa ni hatari kwao.
Aliendelea kuwafuatilia taratibu na kwa umakini, barabara ilikuwa imejaa magari mengi isingekuwa rahisi wahusika kujua wanafuatiliwa. Walinyoosha njia iliyokuwa inakwenda mpaka Kariakoo ila baada ya kufika lilipo jengo kubwa la QUALITY CENTER walitembea kidogo kwa mbele wakakunja mkono wa kushoto na kuishika nia ya vumbi ambayo iliwafanya wakatize relini na kuingia Machinga Complex. Walinyoosha moja kwa moja mpaka kwenye mataa ya Karume na Ilala pale ambapo walisubiri kwa muda kidogo wakaendelea na safari yao moja kwa moja.
Walipita Kigogo wakiwa hawana habari kwamba wanafuatiliwa, hatimaye walitokezea Magomeni kwenye mataa. Taa zilikuwa zimeruhusu hivyo safari yao ikaendelea, walitokezea Mgomeni Kanisani ambapo dereva aliikunja gari hiyo mkono wa kushoto akaishika njia ya kwenda Tandale, hapo alitembea kidogo na kukunja kulia ambapo alitembea kwa dakika moja tu akaenda kusimama kwenye jengo moja ambalo lilionekana kuwa la zamani ila bado lilikuwa kwenye ubora. Mmoja alitoka nje na kufungua geti la hapo gari ikaingizwa ndani ila wakati wanaingia kuna mmoja alishuka akiwa makini kuangalia nyuma.
“Tito nini shida?”
“Nahisi kama kuna mtu anatifuatilia tangu tunatoka kule uwanja wa ndege”
“Tungekuwa tumeshajua kama kuna mtu anatufuatilia sisi sio wajinga namna hiyo na hakuna mtu anaweza kutufuatilia kipumbavu hivi wakati anajua kabisa anakitafuta kifo”
“Umeiona ile gari ambayo imeondoka pale?”
“Imefanyaje Tito mbona unakuwa mwoga kiasi hicho? Sijakuzoea hivyo ndugu yangu acha kuwatisha wageni”
“Ile gari nimeiona kule uwanja wa ndege ikiwa imepaki umbali kadhaa toka tulipokuwa, ni ile ile nimeiona tena kwa mara nyingine pale na ni wazi mtu huyo alikuwa anatuangalia ni sisi, haiwezi kuwa bahati mbaya” mwenzake alimsikitikia
“Jiji kubwa hili, kuna watu wengi wanamiliki gari ambazo zinafanana, acha uoga kuna kazi kubwa ya kuifanya hivyo tuwakaribishe wenzetu tukaipange mipango ya kuanza nayo kesho na unajua kabisa kwamba baadae tunakwenda kasino kuwatafutia wenzetu warembo wa kuzisuuza nyoyo zao” mwenzake hakuonekana kujali kabisa, alihisi rafiki yake alikuwa na mashaka yake binafsi ambayo alitakiwa kuyatoa ila haikuwa hivyo kwa Tito, alikuwa ana uhakika na kile ambacho alikiona ila kwa vile hakutaka makuu mbele ya wageni aliamua kukubali kishingo upande japo nafsi yake ilikuwa inamsuta.
Kosa kubwa ambalo alilifanya Tito ni kuzipuuza hisia zake, hisia zake zilikuwa na umuhimu mkubwa kwenye maisha yake ya kazi ila kwa sababu ya kutowashtua wenzake na kumridhisha rafiki yake aliamua kulichukulia poa jambo hilo. Waliingia ndani ambapo yalipita masaa mawili, ilikuwa ni saa tano usiku tayari, ilionekana gari ile aina ya Alphard ikitoka lile eneo. Waliingia barabarani kwa shangwe wakiwa wanaenda kuponda raha, wangeshindwaje kulifaidi jiji wakati mifuko ilikuwa imetuna na pesa zilikuwa nyingi? Wabongo na starehe tena, walihitaji kuwaonyesha wenzao namna Dar es salaam ilivyo. Lakini wakati wanapita, pembezoni mwa barabara kulikuwa na mwanaume mmoja ambaye alikaa kwenye kiduka ambacho kilikuwa kinauza pombe kali na sigara za kutosha.
Alikuwa makini kuangalia kila upande wa barabara mpaka pale alipo shuhudia gari ile ikitoweka, juu ya mbao ndogo ambayo iliunganishwa na dirisha la kiduka hicho karibu na alipokuwa ameketi, aliweka pombe kali pamoja na pakiti la sigara akiwa anaiteketeza moja moja bila wasi wasi, alikuwa n Yohani Mawenge mwenyewe. Aliiona ile gari ikipita ila hakuifuata, aliiangalia mpaka ilipo tokomea njia ya kwenda Kinondoni, alijua kabisa ambacho alikuwa anakifanya ndio maana hakuweza kuhangaika nayo kabisa.
Aliitazama saa yake ya mkononi, ilikuwa imetimu saa tano na nusu usiku. Mtaa ulikuwa na makelele ya kutosha watu wakiwa wanapishana kila kona, wengine walikuwa wakiendelea kumlaumu raisi kwa kuhisi ndiye chanzo cha maisha kuwa magumu kwao, wengine walipita kwa vicheko kwa sababu maisha yaliwanyookea, wapendanao nao waliendelea kuonyesha mbwembwe zao kwa kupita na mikogo mbali mbali lakini zaidi zaidi, daladala zilikuwa zikipishana huku makondakta wakijaribu kutumia lugha ya matusi yasiyo boa pamoja na misimu mbali mbali ambayo ilikuwa kama kivutia kwa wateja hao.

UKURASA WA 71 unafika mwisho.
 
Back
Top Bottom