FEBIANI BABUYA
JF-Expert Member
- Mar 5, 2022
- 1,916
- 3,850
- Thread starter
- #141
LeoHeshima kwako.
Lini tena??
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
LeoHeshima kwako.
Lini tena??
Kama ilivyo title, nafsi zilizotelekezwa, ona anko hizo nafsi ndio sisi mkuu umetutelekeza😂
🤣Kama ilivyo title, nafsi zilizotelekezwa, ona anko hizo nafsi ndio sisi mkuu umetutelekeza😂
Kazi nzuri sn.. hongeraHADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 75
Wale wawili ni kama waliingia ubaridi hivyo wakawa wanaenda kwa hofu bila mahesabu ya kueleweka, aliyekuwa mbele aliurusha mkono wake kwa nguvu ili akimkuta Edison aweze kumlainisha ila hakuwa na bahati, mkono wake ulikutanishwa na mkono wa Edison hali ambayo iliufanya mkono wake kuvunjika vibaya, alipiga kelele ila alitakiwa kujipambania yeye, Edison alimvuta na kumpigiza kwenye ukuta wa zege kichwa kikapasuka vibaya, alimrushia chini na kuikanyaga shingo ambayo ilifubaa ghafla! Hakuwa akiwaua tu bali alikuwa anawaua kikatili kiasi kwamba ambaye alikuwa anawatazama ilikuwa ni lazima amuogope na kujutia kwenye maisha yake kukutana na mtu wa namna hiyo.
Kijana mmoja alibakia, hakuwa na uwezo wa kuihimili hali hiyo, alitaka kuvunja amri ya bosi wake kutotumia silaha lakini alipo iangalia silaha yenyewe ilikuwa mbali kutoka alipokuwepo hivyo wakati Edison anamsogelea alianza kurudi nyuma. Kurudi kwake nyuma ukawa mwisho wa maisha yake kwa sababu ulikuwa udhaifu mkubwa kutaka kukimbia vitani. Upanga ulizama na kutokezea mbele ya tumbo lake, Saimon alikuwa ameuokota ule upanga wake ndio ambao aliutumia kumuulia kijana huyo kwa sababu ya upuuzi wake wa kutaka kukimbia eneo hilo hivyo kwake hakuwa akifaa tena. Aliuchomoa upanga wake kwa nguvu akaupitisha kwenye shingo ya kijana wake mithili ya mtu ambaye alikuwa anachinja kuku macho yake akiwa ameyaelekezea kwa Edison ambaye hakuwa hata na chembe chembe ya uoga, hayo ni maisha ambayo aliyazoea kwa muda mrefu.
Saimon alikuwa anauzungusha ule upanga kwa spidi ukiwa unavuja damu ya kijana wake, alienda nao mbele ya Edison, ulizungushwa kwenye kiuno chake kisha akauachia kwa kuunyoosha mkono, alimkosa Edison kwenye bega lake kwa sentimita kadhaa tu lakini hakumpata. Kumkosa kwake na upanga ikawa upenyo wa kuliachia buti lake ambalo lilikutana na ngumi ya Edison, Saimon alirudi nyuma akiwa ameunyanyua mkuu wake, buti halikufua dafu mbele ya ngumi ya kilo za kutosha, mguu wake ulikuwa unawaka moto ndani.
Aliukandamiza mguu wake chini akipiga kelele mithili ya beberu, alijaribu tena bahati yake akiwa makini zaidi ya mwanzo lakini wakati huo Edison naye alikuwa ameokota kisu chake. Ule upanga wakati unakuja kifuani kwake aliinama chini kama anataka kudondokea nyuma ila mwili ulikuwa na balansi ya kutosha, upanga ulimpita katikati ya bega la kulia na shingo, alinyanyuka kwa nguvu na kukita kisu chake kwenye bega la Saimon, kilizama ndani kiasi kwamba alikiacha hapo hapo kilichofuatia ni kushusha kiganja chake kama mtu ambaye alikuwa anahitaji kuikata shingo ya Saimon kwa kutumia kiganja. Maumivu ambayo aliyapitia Saimon yalifanya mshipa kujichora eneo hilo akiwa ameinama na upanga wake ambao wakati huo alikuwa nao yeye. Alishangazwa na tukio lile upanga ulivyo pishana na shingo ya Edison ukaenda mbali, hiyo ni nafasi ambayo Ed aliitumia kufanya huo ukatili kwani mkono wa Saimon ulikuwa sawa na usawa wa kichwa chake hivyo mpaka Saimon anataka kuurudisha ule upanga akiamini kwamba angeukita kwenye bega la Edison, ndio muda ambao alifanyiwa huo unyama kiasi kwamba hakuna na nguvu za kufanya hivyo tena.
Aliyumba mithili ya mtu ambaye alikuwa amelewa, kisu kilizama kwa kiasi kikubwa lakini shingo yake ilikuwa kama imebendi upande mmoja hivi. Hakuwa na muda wa kuanza kujitibia ilimlazimu ajikaze misuli ikiwa imejichora mpaka kwenye paji la uso, hasira zilimuendesha akawa anataka kufanya jaribio la mwisho ambapo aliurusha ule upanga wake kwa nguvu kuelekea alipokuwepo Edison, ule upanga aliukwepa ukampita lakini kabla haujafika sentimeta hata hamsini aliunyoosha mkono wake nyuma akafanikiwa kuudaka. Muda ambao aliutumia kuurusha ule upanga Saimon alijua kabisa kwamba huenda mtu huyo angefanikiwa kuukwepa na kama hesabu zake zingeenda vyema basi yeye ndiye alitakiwa kuwahi kumlegeza Edison hivyo wakati anarusha ule upanga alikuja kwa spidi nyuma yake akikichomoa kile kisu ambacho kilikita kwenye bega lake kwa nguvu kubwa kijasiri.
Zilibakia hatua kadhaa tu aweze kumfikia Edison ila alisimama mwenywe na kukiachia kisu hicho akiwa anaunguruma kama jogoo ambalo linaleta mbele ya jogoo mwenzake kugombea tetea. Alikiachia kile kisu kwenye mkono wake, Edison hakuwa hata amegeuka kuangalia tukio hilo, jambo ambalo alilifanya ni kwamba wakati Saimon anakaribia kumfikia ule upanga uligeuziwa uelekeo, ulielekezwa kule ambako alikuwa anatokea Saimon. Upanga ulikuwa mrefu kuliko kisu hivyo upanga ulizama kwenye kifua cha upande wa kulia, upanga ulizama karibia nusu nzima halafu akawa anaunyonya nyonga.
Ulimletea maumivu makali Saimon, nguvu zilikuwa zinamuishia hakuwa na la kufanya kwa wakati huo zaidi ya kumsubiri Israeli mtoa roho aweze kusema na roho yake vizuri ila kitu cha ajabu ni kama mtu wake hakuwa na mpango wa kumuua kwa wakati huo. Kama angehitaji kumuua basi upanga huo angeuzamisha upande wa kushoto ambako ndiko kuna moyo, kuukita upande wa kulia ni kwamba alikuwa anamhitaji akiwa bado yupo hai. Alikuwa na mengi ya kuyaongea na Saimon hivyo asingekubali kumpoteza kizembe namna hiyo, alimvutia kwake akamtwisha ngumi nzito kwenye shingo, alizima hapo hapo. Aliichomoa ile simu yake mfukoni akaiacha pale pale ikiwa ipo hewani, akabeba visu na upanga akamrushia navyo Saimon kwenye buti la gari yake, akatoweka hilo eneo akiwa ametumia dakika kumi tu pekee kuikamilisha kazi ambayo ilimpeleka. Alikuwa ni binadamu hatari na katili mno Edison, hakupenda kuwa hivyo ila wanadamu walimchagulia njia ya kupita. Kwenye moyo wake alikuwa anapitia machungu mazito tangu arejeshewe kumbukumbu zake, kwahiyo watu hao hakuwa na muda wa kucheka nao, alikuwa na usongo nao isivyokuwa kawaida.
Safari yake Edison ilienda kuishia Mwananchi kwenye jengo moja la zamani ambalo lilionekana kuwa kama kiwanda lakini halikuwa likifanya kazi kwa wakati huo. Alimshusha mtu wake na kwenda kumfunga vizuri kwenye kiti cha chuma ambacho kilikwa ndani ya chumba hicho pamoja na viti vingine viwili vya ziada. Edison alimwangalia mwanaume huyo kwa umakini, damu haikuwa inatoka kwa wingi kwa sababu alikuwa amemfunga bandegi kwenye maeneo ambayo yalikuwa yanavuja, alikuwa na hamu kubwa na Saimon kwa sababu alikuwa na mazungumzo naye marefu.
Alisomgelea pale kwenye kiti, akasogeza kiti kimoja akakaa naye karibu chini akiwa ameuweka upanga lakini kwenye mkono wake alikuwa ameshika kisu chake na bastola moja akiwa ameiweka kwenye karibu na buti lake la kulia. Alimtandika Saimoni kofi kali ambalo liliacha alama za mikono kwenye shavu lake, Saimon alishtuka kwa wenge na kelele, alipewa ishara ya kutulia, akiwa na wenge la kutaka kujua yupo wapi, kisu kilipenyezwa kwenye goti lake mfupa mmoja ukavunjika. Alipiga kelele kwa sababu wenge lilikuwa halijamuisha bado lakini wakati huo alikutana na dhahama hiyo nyingine, asingekuwa sawa.
Edison alinyanyuka akatoka humo ndani ambapo baada ya dakika moja alirudi akiwa na maji kwenye kikopo, maji yalikuwa ya baridi kiasi kwamba yalikuwa yanatoa mvuke. Saimon hakuwa na uwezo wa kushika chochote kwa sababu ya kufungwa vizuri hivyo EdJr ndiye ambaye alimsaidia kumnywesha maji hayo, licha ya maji kuwa ya baridi lakini aliyagida yote, alihema kwa nguvu akiwa na wasiwasi, mguu wake nao ulikuwa unamletea shida ndipo akaangalia chini na kugundua kwamba yupo peku na mtu ambaye alikuwa mbele yake alikuwa anamwangalia kwa sura ya kisasi vibaya mno.
“Bosi wako ni nani?” lilikuwa swali kwenda kwa Saimon, aliuchuna. EdJr aliinama akaiokota ile bastola ambayo alifyatua risasi moja kwenye lile eneo la goti ambalo alitoka kulibomoa na kisu muda mchache ambao ulikuwa umepita.
“Nisamehe tafadhali ndugu yangu, naweza kufanya kazi na wewe” alipiga mekelele akiwa anatia huruma, jeuri ile ilikiwa inamponza kwa sababu alibaki anaombea auawe lakini hakukuwa na mtu ambaye alipanga kumuua wakati huo ila alitakiwa kujuta, maumivu yalikuwa makali yakaanza kuishinda imani yake.
“Haujajibu swali langu” Edison aliikoki bastola kwa mara nyingine na kuwa tayari kushambulia tena.
“Madam Kate, madam Kate”
“Najua kwamba ni Madam Kate ila nahitaji jina lake la kweli”
“Siwezi kufanya hivyo kwa sababu ataniua” Edison aliona kama mtu huyo anamletea utani, yaani alikuwa naye yeye wakati huo halafu anamhofia mtu mwingine? Alifanya jambo la haraka, kisu chake kilizamishwa kwenye paja ya Saimon, paja hilo liligawanyishwa kama mtu ambaye akagawa pande mbili za nyama. Lilibaki wazi katikati, halikuachwa hivyo hivyo zilipenyezwa risasi tatu na kupelekea mguu kutoboka toboka vibaya ukawa mpaka unatisha kuuangalia.
“Nakuuliza swali mimi halafu unanijibu kwamba watakuua, unahisi nipo kucheza na wewe sio?” Saimon mwili ulikuwa unetetemeka, alishusha machozi kama mtoto mdogo mpaka alijikojolea kwenye nguo zake. Mdomo wake ulikuwa unashusha udenda kama mtoto mdogo, chozi lilikuwa linamshuka taratibu wala usingeamini kwamba alikuwa ni yule mwanaume ambaye alikuwa na tambo nyingi isivyokuwa kawaida, Saimoni alikuwa mpole. Alipokea kibao kingine ambacho kilimuweka sawa.
UKURASA WA 75 unafika mwisho.
Shukrani mkuuSalute kwako mwandishi
Shukrani sanaKazi nzuri sn.. hongera
🫡Respect Babuya
Huu uzi mpaka nilisha usahau kabisa.
fanya manuva basi tuende sawaHuu uzi mpaka nilisha usahau kabisa.
Tukumbuke mana wengine tunaufatilia kimyakimya.Huu uzi mpaka nilisha usahau kabisa.
Mkuu Sisi tunafuatiliaHuu uzi mpaka nilisha usahau kabisa.
Nadhani hauna wachangiaji huu uzi hivyo huwa nausahau mara kwa mara....fanya manuva basi tuende sawa