Simulizi ya kijasusi: Nafsi zilizotelekezwa

Simulizi ya kijasusi: Nafsi zilizotelekezwa

HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 72

Akiwa anaangalia hali ya maisha ambayo ilikuwa inaendelea hapo, ilimfanya akakumbuka mbali! Aliyakumbuka maisha ya nyuma, aliko tokea yeye. Aliwahi kuyaishi maisha hayo kwa kipindi kirefu hivyo aliyafahamu fika kwa jinsi yalivyokuwa yanaumiza, aliachia tabasamu na kutoa pesa nyingi kwenye mfuko wake, alimlipa muuzaji wa kibanda hicho mpaka yeye mwenyewe akawa anashangaa mtu kumpa pesa yote kama hiyo wakati hata hawafahamiani ila alielewa mjini hakuna cha bure bwana.
“Gari yangu nimeiweka nyuma huko, nitakuja kuifuata baadae hivyo hiyo pesa niliyokupa ni ya huo usumbufu. Nimeamua kukuamini kwa vile umesema unakesha hapa, usifanye ujinga wowote kwenye hiyo gari” sababu ya kumpa pesa nyingi hizo ilikuwa ni kumtaka amlindie gari yake hiyo, ndiyo maana wale jamaa wakati wanatoka hawakuiona, alikuwa ameipaki nyuma ya kibanda hicho sehemu ambayo ilikuwa na uwazi mdogo. Alizunguka ilipo gari hiyo, akabeba koti lake kubwa na kuvaa gloves kwenye mkono wake, akatokomea kuelekea ile sehemu ambayo wanaume wale walikuwa wametokea akisindikizwa na manyunyu ya mvua kwa mbali ambayo yalikuwa yameanza kulisumbua anga la jiji la BANDARI YA SALAMA waweza kuliita Mzizima.
Geti la ile nyumba lilikuwa fupi, aliruka juu na kujivuta kwa nguvu akafanikiwa kuudaka ule ukuta, alijivuta tena kwa mkono mmoja akatua ndani kama karatasi, alikuwa mwepesi isivyokuwa kawaida Yohani. Alichomoa bisu kubwa kwenye koti lake akavunja kitasa cha mlango akaingia ndani ambako alianza kufanya uchunguzi hatua kwa hatua mpaka pale ambapo aliona ameridhika na kile ambacho alikuwa anakifanya.
Saa nane na nusu usiku ulisikika mlio wa gari, gari ambayo ilikuwa kwenye mwendo wa taratibu lakini ndani yake kulikuwa na sauti kubwa ya mziki watu wakionekana kusherehekea maisha yao kuwa safi. Alitoka mmoja na kufungua mlango wakati huo mvua ilikuwa inashuka taratibu baada ya kupungua tofauti na ilivyokuwa mwanzo. Waliingiza gari kwa mbwembwe na kulifunga geti kwa mara nyingine tena. Walikuwa ni wale wapelelezi wanne ambapo walirudi na wanawake wanne pia, kila mtu alihitaji kujichana kwa namna ya pekee usiku huo mpaka kunakucha.
Aliyekuwa mbele alionekana kufurahia kampani ya mwanamke mrembo aliyekuwa naye, alitembea kwa maringo akiwa ameyashika matako ya mrembo huyo ambao yalikuwa yanavutia kila alipokuwa anatembea. Jambo hilo lilimfanya bwana huyo kuhisi kwamba yeye ndiye mwanaume ambaye alikuwa ameyapatia maisha hapa duniani, alitembea kwa kudunda akiwa ameongozana na huyo malaika aliyekosa pesa za kumfanya aulinde utu wake. Alipokumbana na mlango akiwa ameinyoosha funguo ili aweze kuufungua ndipo wenge lake lilikata ghafla, kwanini? Mlango ulikuwa wazi na kitasa hakikuwepo, jambo hilo lilikuwa ni hatari kubwa kwao ikamlazimu kuwageukia wenzake ambao bado walikuwa ndani ya gari wakiwa wanaendelea kuburudika na warembo wao.
Kugeuka kwake kulimfanya ahisi kama anaona kivuli kinatembea, kivuli kilikuwa kinatembeaje? Ndipo akapata wazo la kunyanyua macho yake juu, kuna mwanaume alikuwa juu ya paa la nyumba, pembeni kidogo kutoka alipokuwa yeye.
“We are under ataaack!” sentensi yake haikusikika vizuri mwisho japo aliitamka kwa sauti kubwa, sababu pekee ni kwamba umeme ulikatika ghafla lakini alikutana na kitu ambacho kiliikatisha safari yake ya kwenda kula hiyo starehe ambayo aliipanga kwa wakati huo. Kisu kilipita kuanzia lilipo sikio lake mpaka lilipo bega lake, shingo iliharibiwa kiasi kwamba mtu alikuwa anaweza kuhifadhi maji kwenye hilo eneo yasimwagike badala yake yakaingia ndani ya mwili. Mpelelezi yule alidondoka chini taratibu akiwa kama mtu ambaye alikuwa anataka kutoa ushuhuda wa jambo fulani lakini angetolea wapi nguvu maskini. Buti lilitua kwenye kichwa chake ambacho kilijibamiza chini ya sakafu ya uwanja wa ndani ya geti hilo na kupelekea kupasuka vibaya, hakutoa ushuhuda wake, malaika mtoa roho akawa ameondoka na roho yake tena akiwa anaelekea kutenda dhambi ya kuvunja amri maarufu zaidi kwenye maandiko matakatifu.
Wakati lile buti linatua kwenye kichwa chake umeme ulikuwa umerudi tayari huenda ni radi ambayo ilipiga iliwafanya wahusika waukate na kuurudisha ghafla na wale wanaume wote walikuwa wameshuka kwenye gari tayari baada ya kusikia zile kelele. Hawakuamini walichokuwa wanakiona kwa mwenzao pale chini mvua ikiendelea kuifuata taratibu damu nyingi iliyokuwa ikimwagika kutoka kwenye shingo yake na kichwa chake. Tito alikuwa miongoni mwa mashuhuda wa tukio lile, alijiona mjinga wakati ule kuzipuuzia hisia zake kwa sababu kama angezichukulia kwa ukubwa basi hayo yote huenda wangeweza kuyazuia, muda ulikuwa umekwenda, kuendelea kujutia zaidi alikuwa anaendelea kupoteza muda mwingine.
Mwanamke ambaye alitangulia na mwenzao, lile jambo ambalo lilitokea lilikuwa la ghafla hivyo lilimshtua kiasi kwamba alibaki anatetemeka akiwa anashanga asijue alitakiwa kufanya uamuzi gani kwa wakati huo. Yohani alimpa ishara ya kutoweka haraka ndani ya ile eneo, ni kama alikifungulia kilio chake ambacho alikihifadhi, alilia kwa uchungu akiwa anaelekea usawa wa ile gari ilipokuwa, aliyashuhudia mauaji ya kikatili kwenye maisha yake, huenda hakuwahi kutegemea kukutana na wanadamu wa namna ile hali ambayo ilimfanya kujichomeka kwenye ile gari, ni kama waliambizana, wenzake ambao walikuwa wamebakia mle mmoja aliigeuza gari hiyo kama amechanganyikiwa, alipita na geti likiwa halijafunguliwa ili kuyanusuru maisha yao akatokomea gari ikiwa kwenye mwendokasi.
Lile tukio ndilo ambalo lilimkumbusha Tito wakati warembo wale wanakimbia na gari ambalo halikufungwa hata milango huku wakiwa wanatoa sauti kali za kuhitaji msaada. Tito alijisachi kwenye kiuno chake hakuwa na bastola, aliwaangalia wenzake ambao nao walijisachi na kugundua kwamba bastola hazikuwepo, zilikuwa wapi? Alikumbuka kwamba njia nzima kweye gari walikuwa wanaendelea kufanya mapenzi, wasingefanya mapenzi huku bastola zikiwa zipo viunoni, starehe iliwapotezeshea umakini wa kuyalinda maisha yao maana yake ni kwamba waliziacha kwenye gari ambayo kwa wakati huo ilikuwa imeondolewa! Kilichokuwa kimebaki kwa wakati huo ni kuweza kuyatetea maisha yao wao kama wao kwa mikono yao na hilo halikuwa jambo geni kwao kwani ilikuwa ni sanaa mojawapo ambayo waliishi ila kile kifo cha mwenzao kwa namna ile na jinsi alivyokuwa kilitengeneza hofu kwenye nafsi zao, likawa kosa lingine wanalifanya.
Mbele yao alisimama mwanaume aliyekuwa amevaa koti la mvua, koti ambalo matone ya mvua yalikuwa yanamwagikia na kutelezea chini, halikuwa likipitisha maji. Mkononi mwake alikuwa na kisu ambacho kilikuwa kinachruzika damu, lile koti lake liliificha sura yake hivyo hawakufanikiwa kumfahamu kama alikuwa nani, aliivua kofia yake uso wake wote ukawa unaonekana sawia kwenye macho yao.
“Yohani Mawenge?” alitamka mwanaume mmoja, ni kati ya wale ambao walikuwa wametokea Uganda kuja kumtafuta mwanaume huyo.
“Nasikia mmesafiri kutoka Uganda kuja kunitafuta mimi huku Tanzania hivyo nimewarahisishia kazi yenu na kuamua kujileta mwenyewe ili niende na nyie huko ambako mnanihitaji”
“Mshenzi mkubwa wewe, Uganda sio taifa ambalo unaweza kufanya kile ambacho unakitaka halafu ukapona hivi hivi, muda huu tunaondoka wote kwenda huko” hakuonekana kukumbuka kilicho mkuta mwenzao, alijichomoa pake alipokuwepo, alidunda mara moja chini akajigeuza kwa sarakasi safi kuelekea alipokuwepo Yohani, hakumkwepa mwanaume huyo, mguu wake ulikita kwenye kifua ambacho kilikuwa kama kisiki. Yohani hakutikisika, alibaki amesimama vile vile, ule mguu ulizungushwa kwa mara nyingine ili uweze kutua kwenye koo lake ndipo alipo udaka kwa mkono wake mmoja, alikita kisu kwenye mguu wa mwanaume yule.
Kisu kilitoboa kiatu laini ambacho alienda nacho kwenye starehe kikapenya mpaka kwenye unyayo wake, ilisikika sauti ya kilio cha maumivu. Alimuachia akiwa anamzawadia teke safi la paja ambalo lilimrudisha mwanaume huyo nyuma kwa hatua kadhaa lakini kabla hajatua na kutulia aliyaona mateke mawili yakiwa upande wake, yalikuwa na kasi kubwa hivyo hakufanikiwa kuyakwepa, alipigwa kwenye tumbo lake na usoni akadondokea kwa wenzake ambao iliwalazimu kumdaka na kumlaza chini ili apumue, hali yake ilikuwa mbaya.
Yohani alikuwa mkatili na mtu mbaya kwenye huo uwanja wa mapambano, aliangalia saa yake na kuona anapoteza muda na tayari alikuwa amepoteza muda wa kutosha. Alikuwa na uhakika kwa namna mabinti wale walivyofanikiwa kuondoka lazima wangesababisha polisi kujongea eneo hilo, hakutaka kufikia huko kwa sababu ingekuwa hatari kwake kuweza kujulikana. Tito na mwenzake waliangalia usoni, wakapeana ishara zilizo wafanya wakimbie kwa pamoja kuelekea kule ambako alikuwepo Yohani.

UKURASA WA 72 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 73

Mpango wao ulikuwa ni kwenda pamoja, hivyo mmoja aliteleza chini na Tito akaruka kwa juu, walijua kabisa mtu huyo hatakuwa na uwezo wa kuwakwepa wote kwa wakati mmoja. Yohani alicho kifanya ni kuvua na kurusha koti lake kwa nguvu ambalo lilimfunika Tito akapoteza uelekeo, alipigwa na ngumi kali ambayo ilitua kwenye mdomo lakini hata Yohani mwenyewe alichotwa mguu wake akayumba, alikutanishwa na teke ambalo lilipiga kwenye shavu lake mpaka kisogoni.
Tito alidondokea kwenye maji na kuteleza, alifunua koti lile kwa kasi akiwa anatoa damu kwenye mdomo wake, alitema damu alishangaa kuona meno yake mawili yanadondokea chini hapo aligundua kwamba alikutanishwa na ngumi nzito kwenye mdomo wake ambao mpaka wakati huo ulikuwa umechanika vibaya. Yohani alijitikisa kichwa chake maana hata yeye alipata maumivu kiasi chake, alijiweka sawa na kusimama vizuri. Alikuwa amechukizwa kupigwa lile pigo, alikimbia kumfuata yule mwanaume ambaye alimkita na mguu huo, wakati anamsogelea aliinama chini na kuteleza na magoti yake. Mwanaume yule hakulitegemea hilo hivyo wakati anashtuka alikuwa amekumbana na mkono mzito kwenye goti lake, goti ambalo lilivunjika vibaya.
Alirudi nyuma akiwa anachechemea, kwa bahati mbaya hakuwa na huo uwezo wa kufika mbali, Yohani alinyanyuka kama mzimu akiwa amepiga maji chini, kunyanyuka kwake kulimfanya kufyatuka na teke kali lililo tua kwenye paja ya yule bwana, alipiga sauti kali ya maumivu, paja lake lilikuwa limemenyeka, yaani lilibaki lonya lonya kama nyanya iliyo sagwa, asingeweza kutembea kwa maisha yake yote. Ukelele wake ulimfanya apoteze umakini, alianza kutao ndamu kwenye mdomo wake akiwa anahema kwa shida, kisu kilikuwa kimetoboa katikati ya kifua chake, kilipasua mifupa ambayo ilikuwa hapo.
Kilichomolewa kwa nguvu, Yohani alikichomeka kwenye moyo na kuanza kukizungusha akiwa anauma meno yake, ilikuwa ni dharau kwa upande wake yeye kuweza kupigwa na mtu kama huyo ambaye alimhesabia kama dhaifu kwake. Alichomoa kisu chake kwa kumkita na kichwa kikali cha paji la uso, ilikuwa ni maiti ambayo ilidondoka hapo chini. Tito alibaki anajishauri kama akimbie au aendelee kubaki, hakuona namna ya kuweza kushindana na hilo jitu zaidi ya kutafauta nafasi ya kukimbia, angekimbiaje sasa mtu mwenyewe alikuwa mita kadhaa kutoka alipokuwepo yeye? Aliamua kujikaza kiume asionekane mwanaume wa hovyo huku akijua kabisa kwamba alikuwa anayatoa maisha yake sadaka.
Tito jambo ambalo alilifanya ni kuuzungusha mkono wake kiunoni akauchomoa mkanda wake, alizunguka nao kwa nguvu akafanikiwa kumtwisha nao Yohani mmoja kwenye kifundo cha mkono bila shaka ulimpatia maumivu. Yohani alikubali kukutana nao kwa sababu ndiyo ilikuwa njia rahisi ya kuweza kumfikia Tito. Aliirusha ngumi yake, ilimkosa Tito kwenye kichwa kwa sababu aliinama ila nafasi hiyo Yohani aliitumia kukirushia kisu chake upande wa mkono mwingine ukiwa nyuma ya Tito, alichana sehemu ya uti wa mgongo kwa kisu hicho. Tito aliachia hata ule mkanda wake, nguvu zilikuwa zinaelekea kumuishia.
Alirusha ngumi kama mtu ambaye alikata tamaa ila kiuhalisia hakuwa na namna ya kufanya, mkono wake ulidakwa, kisu kikapitishwa kwenye kwapa yake kama mtu ambaye alikuwa anakata kata paja ya kuku kwa ajili ya supu. Alishingwa shingoni, kisu kilizamishwa kati kati juu kabisa ya utosi kichwani kisha kikachomolewa na kupachiwa kwenye shingo yake. Yohani hakukitoa hicho kisu bali alimnyanyua Tito na kuuvunjia uti wa mgongo kwenye goti lake! Jambo hilo lilishuhudiwa na yule mpelelezi wa Uganda ambaye alikuwa kwenye hali mbaya, muda ule alidakwa na wenzake na kukalishwa chini, aliogopa na kujuta kumfuata mtu huyo.
Yohani alimsogelea pale alipokuwepo huku akiiwasha sigara yake kwa shida kutokana na hali ya mvua lakini hali ya mvua ambayo ilikuwepo lakini alifabikiwa kuiwasha kwa kiberiti cha gesi. Aliyavuta mafunda kadhaa akachuchumaa na kumpa yule bwana naye avute kidogo kuisindikiza safari yake.
“Kama kungekuwa na namna ya mimi kukupa nafasi ya maisha ningekupa somo juu ya haya maisha ndugu yangu ila kwa bahati mbaya hauwezi kutoka nje ya jengo hili ukiwa hai hivyo maelezo yangu yatakuwa mafupi kwako. Mimi kwa mara ya kwanza niliwahi kuishi maisha magumu, ukisikia neno magumu basi unatakiwa ulieelewe kwa kirefu kwa sababu yalikuwa ni magumu haswa lakini sikuwahi kukata tamaa kwa namna yoyote ile mpaka nikafikia hapa ambapo nipo leo”;
“Licha ya kuwa na maisha magumu lakini nilimpa imani mwanamke mmoja ambaye nilikubali kukosa kwa ajili yake ila yeye ndiye akaja kuwa chanzo ya maisha yangu kuwa kituko na kunikosesha heshima kiasi kwamba nikawa nachekwa kila kona ya mtaa. Siku ambayo nilikuwa nimekata tamaa ya maisha ndiyo siku ambayo binafsi alikuja mtu mpya kwenye maisha yangu akanipa tumaini jipya la kuwez akuishi kwa mara nyingine, alinipa kauli kubwa mbili ambazo huwa naziishi mapaka leo. Kwanza mwanaume hatakiwi kulia kwa sababu ya mapenzi, pili mwanaume analia akikosa kuitafuta nguvu ya pesa na nguvu kimamlaka. Kati ya hivyo mara nyingu huwezi kuvipata vyote bali unatakiwa kuchagua kitu kimoja ambacho utatakiwa kwenda nacho kwenye maisha yako ila kwa bahati mbaya wengi huwa wanalitambua hilo wakiwa wanasubiri dakika za kufa kama wewe hapa leo”

“Nilikuwa nahitaji kujiua kwa sababu ya uchi wa mwanamke lakini nikaipata sababu halisi ya mimi kuishi, ule ni ujinga ambao kila nikiukumbuka basi huwa unanifanya nitamani hata kujipiga risasi. Yaani mimi nilikuwa nalilia uchi? Hahaha hahaha hahah huu ni upumbavu mkubwa kuwahi kuufanya kwenye maisha yangu ila unajau baada ya mimi kukutana na yule mtu nilikuwaje? Nilikuwa binadamu wa kutisha ambaye niliitafuta nguvu na sasa nimeipata hivyo sipo tayari vijana kama wewe hapo mje kuiharibu kijinga tu eti kisa nchi yenu imetaka iwe hivyo. Nina uhakika utaikumbuka hii sura vizuri hata tukikutana kwenye maisha yajayo, jambo ambalo unatakiwa kulikumbuka kupitia sura hii ni kwamba haukutakiwa kuingia kwenye ardhi ya taifa hili kwa sababu wakati tu ndege yenu ilipo tua pale JNIA ndio muda ambao ulikuwa umeipokea barua ya kifo chako” Yohani aliongea akisimama na kuivua ile sura yake bandia na kubaki na ile sura yake halisi kama Joel John waweza kumuita Joh, yule kijana wa Tandale kwa Tumbo ambaye alikuwa akiulilia uchi wa mwanamke kiasi kwamba akahitaji kuyatoa maisha yake sadaka kwa sababu ya mwanamke huyo. Aliichomoa bastola yake kiunoni na kumpiga risasi zote mwanaume huyo ambaye alikufa akiwa na sigara yake mdomoni.

Usiku ambao Yohani alikuwa anamalizana na wapelelezi wa Uganda na wale mamluki wa Tanzania ndio usiku ambao Edison alitakiwa kukutana na Saimon kwa mara ya kwanza kwa msaada wa Nicola, kwahiyo jambo ambalo walilifanya ni kuhakikisha Nicola anafanya mawasiliano na mtu huyo kuhitaji kuonana naye. Alimtaka Saimon kufika kwenye parking kubwa ya magari ambayo ilikuwa inapatikana kwenye jengo moja kubwa ambalo lilikuwa limeletekezwa maeneo ya Mikocheni. Kwa sababu watu hao kwa wakati huo walikuwa wanafanya kazi chini ya mtu mmoja japo hawakuwa wakiaminiana ila Saimon aliukubali wito huo wa kufika ndani ya eneo husika kwa saa moja ambalo lilikuwa linafuata.
Wakati wanafanya makubaliano hayo, Ed na Nicola walikuwa wapo ndani ya gari, baada ya mazungumzo na mtu wake kutamatika walibaki wanaongea mambo ya historia za maisha yao. Historia ambazo zilikuwa zinavujisha machozi kwenye moyo wa kila mmoja wao, mazungumzo yao yalinogeshwa na lugha ya picha, mawasiliano ya miili wakajikuta wanaangaliana kwa muda mrefu. Watu hao walikuwa wapo karibu wakati kila mtu akiwa anamkadiria mwenzake moyoni akiwa anajua alichokuwa anakiwaza mwenyewe.
Ukaribu wao ulizifanya hisia zao kuwa sawa, mapigo ya moyo yakaanza kuwa sawa, midomo yao ilianza kusogezana kuelekea kila alipokuwepo mmoja wao hatimaye wakajikuta ile juisi ambayo inapatikana mdomoni inakuwa halali ya kila mtu. Hawakukumbuka kama walikuwa ni kwenye gari, hawakujali mtikisiko wa gari, hisia zao zilikuwa juu waliamua kuziridhisha nafsi zao.
Sanaa ya mikono ya Edison ilikuwa inajua namna ya kuziimba nyimbo tamu za mapenzi, aliifunua nguo ya Nicola taratibu ambaye naye alijikuta akiucheza huo mziki lipsi zikiwa zimebanana mithili ya fundi viatu na sindano yake. Furaha ilizidi kipimo wakajikuta wamezama penzini, walifanya mapenzi kwa fujo mithili ya watu ambao walikuwa wanashindania zawadi fulani maridhawa. Walishtuka baada ya nusu saa kupita Nicola akiwa na aibu nyingi, hakuwa anajiamini tena mbele ya mwanaume huyo ambaye alikuwa anajiweka sawa kwani alikuwa na kazi ya kuifanya wakati huo.

UKURASA WA 73 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 74

“Nenda kamchukue baba yake Damas, ukisha mpata nipigie simu mimi nitakuwa na Saimon” ilikuwa sauti nzito ya Edison. Hikuwa tatizo kwake kwa sababu alijua eneo ambalo alitakiwa kwenda na picha ya mhusika wake alikuwa nayo hivyo aliamua kugawa majukumu kwani walikuwa nje ya muda. Nicola alitoka ndani ya hiyo gari na kuingia kwenye gari yake ambayo ilikuwa mita kadhaa kutoka pale kila mtu akiingia kwenye majukumu yake baada ya kuagana kwa denda. Mwanamke huyo alirasimishwa kuwa sehemu ya mwili wa Edison, kufanya mapenzi ni mwanamke ni ishara kwamba unampa ruhusa ya kuingia moja kwa moja kwenye maisha yako kwa namna yoyote ile.
Edison alibaki anajiuliza maswali mengi juu ya kile ambacho alikuwa amekifanya na Nicola, hakuelewa kama alikuwa amejivunjia heshima ama alifanya kitu sahihi. Kumbukumbu zake zilimrejesha siku kadhaa nyumba ambapo alikuwa akifanya mazungumzo na Jack, alimsihi kuhakikisha anamuweka mwanamke huyo karibu ili aweze kumlinda, alimtaka asije kufanya kosa lolote kwani hatima ya maisha ya Nicola ilikuwa kwenye mikono yake hivyo jukumu la kumlinda lilikuwa kwake. Jambo hilo lilikuwa limewezekana lakini walivuka mipaka mapema, aliamini kwamba kutumia muda kujutia kile ambacho alikuwa amekifanya ulikuwa ni upotezaji wa muda mwingine bila sababu za msingi hivyo aliliondoa gari eneo hilo kuelekea ambako alitakiwa kukutana na Saimon.
Alitumia dakika ishirini tu akawa yupo eneo la tukio, alizima gari akatoka na funguo akasogea na kwenda kukaa umbali kadhaa kutoka eneo lile. Ilipita nusu saa nyingine bila dalili za uwepo wa mtu hayo maeneo hali ambayo ilimpa shaka na wasi kwa kuhisi kwamba huenda walidanganywa lakini akiwa anaelekea kukata tamaa na kujiandaa kuondoka ili akaandae mpango mwingine aliona kuna gari zinaingia hapo zikiwa mbili tena zimeongozana kwa spidi. Walishuka wanaume sita jumla huku mmoja wa mbele akiwa amevaa vest nyeusi na suruali ya jeshi huku kwenye miguu yake akia ndani ya kombati. Alilipata jibu kwamba bila shaka yule ndiye alikuwa mwenyewe.
Alimkagua vizuri kwa mbali mwanaume yule, nyuma ya kiuno chake alikuwa amepachika bastola mbili na kwa namna alivyokuwa, hakuwa mlaini bali alikuwa ni mtu ambaye alikuwa anaiweza kazi. Kwenye mkono wake alikuwa na upanga mrefu ambao ulikuwa unang’aa isivyokuwa kawaida, ni ishara kwamba maisha ya Nicola hayakuwa salama, inaonekana walikuja hapo kumfuata kwa ubaya. Waliangaza huku na huko bila kuona mtu yeyote hivyo Saimon akaitoa simu yake ili aweze kumpigia Nicola kumpa taarifa kwamba alikuwa amefika hapo, zoezi lake alilisitisha baada ya kusikia sauti kwa mbali.

Sauti ilikuwa ni ya kilio mwanaume ambaye alikuwa nyuma yao alishuka chini taratibu akiwa ameishika shingo yake. Kisu kilirushwa kutoka nyuma, kikazama kwenye shingo mpaka kikatokezea mbele yake ndiyo maana alitoa sauti ya chini akiwa anahitaji msaada wa wenzake. Licha ya jambo hilo kuwa la ghafla na la kushangaza, Saimon alimsogelea akamkata shingo yake ili atulie hapo chini huku akiwa makini kuweza kutazama na kujua ni nani ambaye alikuwa ameingia eneo hilo kwa ajili ya kufanya mauaji kwani aliamini Nicola asingeweza kufanya jambo la namna hiyo.
“Kila mtu atupe silaha yake chini haraka” ilisikika sauti nzito kutoka kwa mtu ambaye alizishika bastola mbili kwenye mikono yake. Alitokea kwenye chemba ambayo ilikuwa na giza kiasi, kwa sababu walikuwa wamegeuka hivyo waliona bastola hizo moja ikiwa imeelekezwa kwa Saimon na nyingine mwa mwanaume ambaye alikuwa na AK47 mkononi. Wote walizirushia silaha zao chini, hata Saimon aliuachia ule upanga wake akiwa makini kuhitaji kumfahamu huyo mtu ambaye alikuwa amejitoa sadaka kumfuata yeye.
Lahaula! Ni yule ambaye walikuwa wakimtafuta kwa udi na uvumba, mwanaume ambaye alijifanya mwanasheria lakini hakuwa yeye. Edison alikuwa mbele yake.
“Kumbe wewe ndiye malaya ambaye unajificha ficha kwa kuogopa kukutana na wanaume hahaha hahaha” Saimon alitamka kwa jeuri lakini wakati huo kijana wake mmoja alijichetua akili akahitaji kuokota silaha yake, alipigwa risasi ya kwenye goti, mfupa ulitokezea nje akapiga yowe lililodumu kwa sekunde moja tu na kutulia baada ya bastola moja risasi zote kuishia kichwani, kichwa kilipondeka pondeka kama nyanya. Hilo jambo lilifanya vicheko kuisha, hakuna ambaye alikuwa anaendelea kucheka wala kudhihaki tena hata Saimon mwenyewe heshima ilirudi akajua kabisa kwamba risasi haikuwa na mjanja wala fundi alilazimika kuwa watulivu kwa sababu ndani ya muda mfupi walikuwa sita lakini kwa wakati huo walikuwa wamebaki wanne tu na kama wangefanya makosa ya kipuuzi basi huenda wangeisha wote.
“Kwanini mmekuja hapa na silaha nzito namna hiyo wakati makubaliano yalikuwa ni kukutana na mtoto wa kike”
“Ninajua kwamba Nicola anatusaliti, hivyo ni lazima akalipe kwa usaliti wake”
“Kwahiyo nyie wote hapa mmekuja kwa ajili ya binti mmoja?” Majibizano yao yalikuwa ya mahesabu makali hususani kwa Saimon, alikuwa akizipigia hesabu hatua zake kali ambazo zilikuwa kwenye kichwa chake. Kipindi ambacho Edison aliuliza swali la pili, miguu ya Saimon ilikuwa makini na kila neno lilivyokuwa linatoka mdomoni mwa Edison. Aliipata sekunde moja tu pekee ambayo aliitumia kumkunja kijana wake mmoja na kumuweka mbele yake, alimsukumizia mbele hali iliyo pelekea Edison kuachia risasi ambazo zote ziliishia kwenye kifua cha kijana huyo na Saimon alikuwa amefika.
Alikunjuka kwa teke zito ambalo lilitua kwenye bega la Edison, alilipangua kwa nguvu lakini lilikuwa limemfikia. Saimon alitua chini na kujigeuza kama paka akarudi na mateke mawili tena ambayo yalimsukuma Edison mpaka kwenye nguzo ambazo zilikuwa na zege zito zikishikilia eneo hilo la upande wa chini wa jengo. Alikidondosha kisu chini kwa dharau ili isonekane kwamba alikuwa anatumia silaha mbele ya mwanaume huyo.
“No guns” Saimon alifoka kwa vijana wake ambao aliona wanainama kubeba silaha, silaha zilikuwa ni hatari kwa sababu kwenye kashikashi kama hiyo zingemletea madhara hata yeye lakini kwake ngumi ndiyo ilikuwa silaha yake kubwa hivyo hakutaka kutumia silaha nyingine mbele ya mwanadamu anayepigwa na kutoa damu kwenye mwili wake, ingekuwa dharau na kujidhalilisha kwa upande wake ndiyo maana alisimama kidete kucheza na mikono yake tu pekee.
Alicheza kama Bruce lee wakati anasogea alipo Edison, lile shambulizi la kwanza lilimpa uhakika, kwanza angepata sifa kubwa kwa wakubwa zake kuwa mtu wa kwanza ambaye angempata mtu huyo waliyekuwa wamemtafuta kwa gharama kubwa na kwa miaka mingi bila mafanikio yoyote yale. Mikono yake ilikuwa imekakamaa vilivyo, aliichanganya mikono yake akiwa anairusha kwa nguvu kubwa, hakuna mkono ambao ulimgusa Edison, EdJr aliikaza mikono yake ikawa inaitikia tu mifupa kukubali zoezi hilo. Saimon alijikuta anakubali ngumi ambayo alishindwa kuipangua, ilitua kwenye bega lake, alihisi ni tofali la chuma limetua hapo, aliurusha mkono mwingine ila ulikuwa mfupi kwa sababu chini aliguswa na mguu kwenye mhogo wake jambo ambalo lilimfanya ainame. Alikutanishwa na ngumi mbili za uso zikamfanya akawa kama ameletwa, alimaliziwa na viganja vya mikono ambavyo vilimbeba mpaka kwenye gari moja ambayo alipasua vioo vyake kwa namna ambavyo alitua kwa nguvu.
“Namhitaji akiwa hai” ilikuwa ni sauti kali ambayo aliitoa huku akiwa anajichomoa vioo ambavyo vilizama mwilini baada ya kuona vijana wake wanahitaji kushambulia kwa risasi. Alinyanyuka kwa hasira kali lakini wakati huo simu yake ilianza kuita kwenye mfuko wake, aliitoa akiwa anasonya na kupokea.
“Ndiyo bosi’
“Mmempata?”
“Hisia zangu zilikuwa sahihi, Nicola ametuuza na sasa nipo mbele ya mtu ambaye tulikuwa tunamtafuta”
“Edison?”
“Ndiyo”
“Niletee akiwa hai, hakikisha unakuja naye kwa namna yoyote ile”
“Sawa bosi” aliijibu simu hiyo ikakatwa. Wakati ambao alikuwa anayafanya hayo mazungumzo na kupewa maagizo alimuona kijana wake mmoja akiwa anamkimbilia Edison, mwanaume huyo alichomoka yeye kabla kijana huyo kufika, ni kama alimshtukiza kitu ambacho hakujiandaa nacho mapema. Yeye ndiye ambaye alipokea ngumi ya shingo, shingo ilipinda lakini hakuachiwa kirahisi Edison alizamisha mkono wake katikati ya koo la kuchomoa nyama za eneo hilo ndipo akamtupa kijana huyo ambaye bila shaka alikuwa wa saba na alibakia ndani ya gari ama alikuwa nyuma ya gari kwani hakuonekana kwenye ile hesabu ya mwanzo wakati wanashuka wale sita wote.

UKURASA WA 74 unafika mwisho.
 
HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 75

Wale wawili ni kama waliingia ubaridi hivyo wakawa wanaenda kwa hofu bila mahesabu ya kueleweka, aliyekuwa mbele aliurusha mkono wake kwa nguvu ili akimkuta Edison aweze kumlainisha ila hakuwa na bahati, mkono wake ulikutanishwa na mkono wa Edison hali ambayo iliufanya mkono wake kuvunjika vibaya, alipiga kelele ila alitakiwa kujipambania yeye, Edison alimvuta na kumpigiza kwenye ukuta wa zege kichwa kikapasuka vibaya, alimrushia chini na kuikanyaga shingo ambayo ilifubaa ghafla! Hakuwa akiwaua tu bali alikuwa anawaua kikatili kiasi kwamba ambaye alikuwa anawatazama ilikuwa ni lazima amuogope na kujutia kwenye maisha yake kukutana na mtu wa namna hiyo.
Kijana mmoja alibakia, hakuwa na uwezo wa kuihimili hali hiyo, alitaka kuvunja amri ya bosi wake kutotumia silaha lakini alipo iangalia silaha yenyewe ilikuwa mbali kutoka alipokuwepo hivyo wakati Edison anamsogelea alianza kurudi nyuma. Kurudi kwake nyuma ukawa mwisho wa maisha yake kwa sababu ulikuwa udhaifu mkubwa kutaka kukimbia vitani. Upanga ulizama na kutokezea mbele ya tumbo lake, Saimon alikuwa ameuokota ule upanga wake ndio ambao aliutumia kumuulia kijana huyo kwa sababu ya upuuzi wake wa kutaka kukimbia eneo hilo hivyo kwake hakuwa akifaa tena. Aliuchomoa upanga wake kwa nguvu akaupitisha kwenye shingo ya kijana wake mithili ya mtu ambaye alikuwa anachinja kuku macho yake akiwa ameyaelekezea kwa Edison ambaye hakuwa hata na chembe chembe ya uoga, hayo ni maisha ambayo aliyazoea kwa muda mrefu.
Saimon alikuwa anauzungusha ule upanga kwa spidi ukiwa unavuja damu ya kijana wake, alienda nao mbele ya Edison, ulizungushwa kwenye kiuno chake kisha akauachia kwa kuunyoosha mkono, alimkosa Edison kwenye bega lake kwa sentimita kadhaa tu lakini hakumpata. Kumkosa kwake na upanga ikawa upenyo wa kuliachia buti lake ambalo lilikutana na ngumi ya Edison, Saimon alirudi nyuma akiwa ameunyanyua mkuu wake, buti halikufua dafu mbele ya ngumi ya kilo za kutosha, mguu wake ulikuwa unawaka moto ndani.
Aliukandamiza mguu wake chini akipiga kelele mithili ya beberu, alijaribu tena bahati yake akiwa makini zaidi ya mwanzo lakini wakati huo Edison naye alikuwa ameokota kisu chake. Ule upanga wakati unakuja kifuani kwake aliinama chini kama anataka kudondokea nyuma ila mwili ulikuwa na balansi ya kutosha, upanga ulimpita katikati ya bega la kulia na shingo, alinyanyuka kwa nguvu na kukita kisu chake kwenye bega la Saimon, kilizama ndani kiasi kwamba alikiacha hapo hapo kilichofuatia ni kushusha kiganja chake kama mtu ambaye alikuwa anahitaji kuikata shingo ya Saimon kwa kutumia kiganja. Maumivu ambayo aliyapitia Saimon yalifanya mshipa kujichora eneo hilo akiwa ameinama na upanga wake ambao wakati huo alikuwa nao yeye. Alishangazwa na tukio lile upanga ulivyo pishana na shingo ya Edison ukaenda mbali, hiyo ni nafasi ambayo Ed aliitumia kufanya huo ukatili kwani mkono wa Saimon ulikuwa sawa na usawa wa kichwa chake hivyo mpaka Saimon anataka kuurudisha ule upanga akiamini kwamba angeukita kwenye bega la Edison, ndio muda ambao alifanyiwa huo unyama kiasi kwamba hakuna na nguvu za kufanya hivyo tena.
Aliyumba mithili ya mtu ambaye alikuwa amelewa, kisu kilizama kwa kiasi kikubwa lakini shingo yake ilikuwa kama imebendi upande mmoja hivi. Hakuwa na muda wa kuanza kujitibia ilimlazimu ajikaze misuli ikiwa imejichora mpaka kwenye paji la uso, hasira zilimuendesha akawa anataka kufanya jaribio la mwisho ambapo aliurusha ule upanga wake kwa nguvu kuelekea alipokuwepo Edison, ule upanga aliukwepa ukampita lakini kabla haujafika sentimeta hata hamsini aliunyoosha mkono wake nyuma akafanikiwa kuudaka. Muda ambao aliutumia kuurusha ule upanga Saimon alijua kabisa kwamba huenda mtu huyo angefanikiwa kuukwepa na kama hesabu zake zingeenda vyema basi yeye ndiye alitakiwa kuwahi kumlegeza Edison hivyo wakati anarusha ule upanga alikuja kwa spidi nyuma yake akikichomoa kile kisu ambacho kilikita kwenye bega lake kwa nguvu kubwa kijasiri.
Zilibakia hatua kadhaa tu aweze kumfikia Edison ila alisimama mwenywe na kukiachia kisu hicho akiwa anaunguruma kama jogoo ambalo linaleta mbele ya jogoo mwenzake kugombea tetea. Alikiachia kile kisu kwenye mkono wake, Edison hakuwa hata amegeuka kuangalia tukio hilo, jambo ambalo alilifanya ni kwamba wakati Saimon anakaribia kumfikia ule upanga uligeuziwa uelekeo, ulielekezwa kule ambako alikuwa anatokea Saimon. Upanga ulikuwa mrefu kuliko kisu hivyo upanga ulizama kwenye kifua cha upande wa kulia, upanga ulizama karibia nusu nzima halafu akawa anaunyonya nyonga.
Ulimletea maumivu makali Saimon, nguvu zilikuwa zinamuishia hakuwa na la kufanya kwa wakati huo zaidi ya kumsubiri Israeli mtoa roho aweze kusema na roho yake vizuri ila kitu cha ajabu ni kama mtu wake hakuwa na mpango wa kumuua kwa wakati huo. Kama angehitaji kumuua basi upanga huo angeuzamisha upande wa kushoto ambako ndiko kuna moyo, kuukita upande wa kulia ni kwamba alikuwa anamhitaji akiwa bado yupo hai. Alikuwa na mengi ya kuyaongea na Saimon hivyo asingekubali kumpoteza kizembe namna hiyo, alimvutia kwake akamtwisha ngumi nzito kwenye shingo, alizima hapo hapo. Aliichomoa ile simu yake mfukoni akaiacha pale pale ikiwa ipo hewani, akabeba visu na upanga akamrushia navyo Saimon kwenye buti la gari yake, akatoweka hilo eneo akiwa ametumia dakika kumi tu pekee kuikamilisha kazi ambayo ilimpeleka. Alikuwa ni binadamu hatari na katili mno Edison, hakupenda kuwa hivyo ila wanadamu walimchagulia njia ya kupita. Kwenye moyo wake alikuwa anapitia machungu mazito tangu arejeshewe kumbukumbu zake, kwahiyo watu hao hakuwa na muda wa kucheka nao, alikuwa na usongo nao isivyokuwa kawaida.
Safari yake Edison ilienda kuishia Mwananchi kwenye jengo moja la zamani ambalo lilionekana kuwa kama kiwanda lakini halikuwa likifanya kazi kwa wakati huo. Alimshusha mtu wake na kwenda kumfunga vizuri kwenye kiti cha chuma ambacho kilikwa ndani ya chumba hicho pamoja na viti vingine viwili vya ziada. Edison alimwangalia mwanaume huyo kwa umakini, damu haikuwa inatoka kwa wingi kwa sababu alikuwa amemfunga bandegi kwenye maeneo ambayo yalikuwa yanavuja, alikuwa na hamu kubwa na Saimon kwa sababu alikuwa na mazungumzo naye marefu.
Alisomgelea pale kwenye kiti, akasogeza kiti kimoja akakaa naye karibu chini akiwa ameuweka upanga lakini kwenye mkono wake alikuwa ameshika kisu chake na bastola moja akiwa ameiweka kwenye karibu na buti lake la kulia. Alimtandika Saimoni kofi kali ambalo liliacha alama za mikono kwenye shavu lake, Saimon alishtuka kwa wenge na kelele, alipewa ishara ya kutulia, akiwa na wenge la kutaka kujua yupo wapi, kisu kilipenyezwa kwenye goti lake mfupa mmoja ukavunjika. Alipiga kelele kwa sababu wenge lilikuwa halijamuisha bado lakini wakati huo alikutana na dhahama hiyo nyingine, asingekuwa sawa.
Edison alinyanyuka akatoka humo ndani ambapo baada ya dakika moja alirudi akiwa na maji kwenye kikopo, maji yalikuwa ya baridi kiasi kwamba yalikuwa yanatoa mvuke. Saimon hakuwa na uwezo wa kushika chochote kwa sababu ya kufungwa vizuri hivyo EdJr ndiye ambaye alimsaidia kumnywesha maji hayo, licha ya maji kuwa ya baridi lakini aliyagida yote, alihema kwa nguvu akiwa na wasiwasi, mguu wake nao ulikuwa unamletea shida ndipo akaangalia chini na kugundua kwamba yupo peku na mtu ambaye alikuwa mbele yake alikuwa anamwangalia kwa sura ya kisasi vibaya mno.
“Bosi wako ni nani?” lilikuwa swali kwenda kwa Saimon, aliuchuna. EdJr aliinama akaiokota ile bastola ambayo alifyatua risasi moja kwenye lile eneo la goti ambalo alitoka kulibomoa na kisu muda mchache ambao ulikuwa umepita.
“Nisamehe tafadhali ndugu yangu, naweza kufanya kazi na wewe” alipiga mekelele akiwa anatia huruma, jeuri ile ilikiwa inamponza kwa sababu alibaki anaombea auawe lakini hakukuwa na mtu ambaye alipanga kumuua wakati huo ila alitakiwa kujuta, maumivu yalikuwa makali yakaanza kuishinda imani yake.
“Haujajibu swali langu” Edison aliikoki bastola kwa mara nyingine na kuwa tayari kushambulia tena.
“Madam Kate, madam Kate”
“Najua kwamba ni Madam Kate ila nahitaji jina lake la kweli”
“Siwezi kufanya hivyo kwa sababu ataniua” Edison aliona kama mtu huyo anamletea utani, yaani alikuwa naye yeye wakati huo halafu anamhofia mtu mwingine? Alifanya jambo la haraka, kisu chake kilizamishwa kwenye paja ya Saimon, paja hilo liligawanyishwa kama mtu ambaye akagawa pande mbili za nyama. Lilibaki wazi katikati, halikuachwa hivyo hivyo zilipenyezwa risasi tatu na kupelekea mguu kutoboka toboka vibaya ukawa mpaka unatisha kuuangalia.
“Nakuuliza swali mimi halafu unanijibu kwamba watakuua, unahisi nipo kucheza na wewe sio?” Saimon mwili ulikuwa unetetemeka, alishusha machozi kama mtoto mdogo mpaka alijikojolea kwenye nguo zake. Mdomo wake ulikuwa unashusha udenda kama mtoto mdogo, chozi lilikuwa linamshuka taratibu wala usingeamini kwamba alikuwa ni yule mwanaume ambaye alikuwa na tambo nyingi isivyokuwa kawaida, Saimoni alikuwa mpole. Alipokea kibao kingine ambacho kilimuweka sawa.

UKURASA WA 75 unafika mwisho.
 
Kazi nzuri sn.. hongera
 
Back
Top Bottom