HADITHI: NAFSI ZILIZO TELEKEZWA
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
EMAIL:
thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
UKURASA WA 81
βMakamu wa raisi ameuawaβ Aaliyah alibaki ameganda
βNani mwenye uwezo wa kumvamia makamu wa raisi na kumuua? Na kwanini afanye hivyo?β
βSijui ila nimepigiwa simu na mlinzi wake mkuu ambaye bila shaka naye ameuawaβ Aaliyaha aliangalia saa yake hapo ndipo aligundua kwamba miadi yake na kiongozi huyo ndiyo iliwafanya kuwa hapo mapema namna hiyo, ilikuwa saa kumi na mbili kasoro ya asubuhi. Alishangaa inawezekanaje makamu wa raisi kuuawa tena alfajiri kabisa?
βTunatakiwa kwenda huko muda huu kabla mtu mwingine yeyote hajajua kinacho endelea huenda kuna vitu tutavijuaβ alikuwa amechanganyikiwa, alibeba kofia yake na kutoka nje ambapo Aaliyah alimfuata ili waweze kwenda huko. Hiyo ni habari mbaya ambayo ilikuwa wakati mbaya pia. Makamu wa raisi kuuawa lilikuwa ni zaidi ya tatizo hilo kwa usalama wa taifa tena akiuliwa nyumbani kwake? Wangewaeleza nini wananchi wakaelewa? Majibu huenda wangeyapata huko huko mbele ya safari.
Raisi wa Tanzania Faraji Asan alikuwa ndani ya bwana la kuogelea, kichwa kilikuwa cha moto asubuhi ya mapema kabisa hivyo aliamua kwenda kukipooza eneo hilo la bwana kwa maji safi. Akiwa ametoka na kukaa kwenye kingo ya bwawa hilo, alikuja msaidizi wake wa kazi akiwa anatembea kwa mwendo wa haraka kidogo.
βBosi unasubiriwa wewe tu kila kitu kipo tayariβ alimhitaji mlinzi wake ampatie taulo bila kujibu kitu juu ya jambo ambalo aliambiwa, alijifuta vizuri na kuvaa nguo yake nyingine ambayo aliovaa kuwahi huko ambako alikuwa anahitajika wakati huo. Ndani ya chumba kimoja ambacho kilikuwa kama maktaba ndiko ambako alielekea na baada ya kuingia huko aliwahitaji watu wengine wote wabaki nje kwani hakutaka bugdha pindi awapo huko.
Ndani ya chumba hicho ambacho kilipangwa kwa ustadi mkubwa, alikuwa amesimama mzee mmoja wa makamo ambaye umri wake ulikuwa umekwenda. Kwenye mkono wake mzee huyo alikuwa na begi jeusi ambalo lilifungwa kwa ustadi mkubwa.
βProfessor Christopher Nyemo nimepewa habari kwamba kila kitu kipo sawa kama nilivyo kuagiza!β
βNdiyo bosi, nimeandaa taarifa zote tena kwa usahihi kabisa kama ambavyo ulihitaji niziwekeβ
βUna uhakika taarifa zote zipo humo?β
βNdiyo kiongozi, zipo zote tangu ule mwaka ambao umeuainisha wakati unanipa maagizoβ
βAsante kwa kazi ambayo umeifanya kwa wakati wote huu na kwa hili, hakika sitakusahau Nyemo na hata taifa litaikumbuka kazi yako daimaβ raisi aliongea kwa masikitiko akiwa anaivuta droo ndogo ambayo ilikuwa kwenye meza ya pembeni. Aliitoa bastola na kumnyooshea mzee huyo ambaye alionyesha wasiwasi wa wazi kabisa mbele ya raisi.
βMheshimiwa tafadhali usifanye hicho ambacho unahitaji kukifanyaβ aliongea kwa sauti ya upole ila ya kumaanisha kile ambacho alikuwa anakisema ama kukihitaji, bado maisha yake alikuwa akiyapenda hivyo raisi kuhitaji kuyachukua alikuwa anakwenda kumkatili pakubwa.
βUnajua kabisa mimi sikupenda kuwa hivi, mimi sikuhitaji kuishi haya maisha ya kupangiwa. Nipo Ikulu lakini ni kama raia wa kawaida ambaye naishi kwa kupokea maagizo kutoka kwa watu ambao hata siku moja hawakuhitaji kuja kuonana na mimi. Wewe ni miongoni mwa watu ambao waliwahi kunishawishi nikubaliane na jambo hili ili kuweza kuishi lakini baadae ukaja ukaanza kunisaliti kwa kutumika nao kuuza taarifa zangu. Nyemo nilikuwa naweza kukusamehe yote lakini sio la hili kugundua kwamba unanisaliti mimi, taarifa ambazo nilikuwa nazihitaji bila shaka umeziandaa kwa usahihi ili uendelee kunihadaa na kunifanya mjinga, kumbuka mimi ni raisi wa nchiβ
βMheshimiwa tafadhali usifanye hili, wewe ni raisi lakini upo chini ya watu, wewe umewekwa hapo kama kivuli na ndiyo yalikuwa makubaliano ya mara ya kwanza kabisa wakati umepiga magoti unalia uachwe hai. Leo unaniona mimi sikufai kwa sababu unataka kubadili njia ya kupita?β
βSiku zote mimi sikupenda kuwa hivi, nimeitafuta hii nafasi ya kuweza kutoka huko muda mrefu lakini sikuipta, kwa sasa nahisi nimepata mtu ambaye naweza kumuamini hivyo nahitaji kufanya naye kazi kuwamaliza woteβ
βHahaha hahaha hahaha hahaha Asani nina uhakika kwamba wewe ni smart zaidi ya hapo, kweli unaamini kwamba unaweza kuacha mambo yakaenda kirahisi namna hii kama unavyo hitaji wewe? Makamu wa raisi kuuawa sio tatizo kwa sababu atawekwa mwingine na wananchi watadanganywa kama kawaida ila hiki ambacho unataka kukifanya wewe? Hili ni kosa ambalo litakufanya ufe ndani ya wiki hii tu, tufanye kama hakuna kitakacho tokea na taarifa hizi sizipeleki popote ila usije ukathubutu tena kuweza kuninyooshea bastola kwenye uso wangu mpuuzβ¦β¦.β Sentensi ya mzee huyo Christopher Nyemo iliishia njia baada ya risasi mbili kupenya kwenye paji la uso wake. Alidondoka chini akiwa anavuja damu hata hivyo raisi alimalizia risasi zote kwenye bastola kwenye kifua cha mzee huyo ambaye alichakaa damu kwenye shati yake safi nyeupe ambayo ilikuwa ndani ya koti ya suti ya blue.
Muda huo huo waliingia walinzi na kuubeba mwili huo huku wengine wakisafisha ile damu ili chini pabaki safi kama palivyokuwa mwanzo. Mwanaume mmoja shababi kweli kweli aliinama kuiokota ile begi akamsogezea mheshimiwa raisi na kumkabidhi.
βBosi una uhakika na hili?β
βNdiyo, nimeamua kufanya hivi hata kama nitakufa basi nitafurahi nikiwa kwa kuwa mtu mwema. Nimechoka kuua watu wasio na hatia, nimechoka kuwa kibaraka wa mtu, nimechoka kuwadanganya waananchi na kuliendesha taifa kitapeli. Nahitaji kukutana na Edison kwa gharama yoyote ileβ
βEdison amekufa bosiβ
βYupo hai, nitafutie Aaliyah Beka, hakikisha unamleta hapa Ikulu nadhani yule binti atanifaa kwa kazi hii. Nipo tayari kufa lakini nataka hawa watu wote ambao wamehusika wafe na kufutika kwa taifa hili, miaka zaidi ya ishirini ambayo wameliendesha taifa hili watakavyo wao imefika mwisho. Siwezi kuendelea kuruhusu huu ujinga uendelee kwenye taifa teule kama hiliβ Aliongea kwa kufoka ila sauti ya utulivu mheshimiwa akionekana kabisa kutofurahishwa na jambo hilo ambalo lilionekana kuwa kero kwake kwa kipindi kirefu ni kwa vile tu hakuwa na namna ya kufanya akaamua kuishi nalo kama lilivyokuwa.
Christopher Nyemo alikuwa ni mwanahistoria wa Ikulu kwa muda mrefu. Alikuwa miongoni mwa watu wachache ambao walikuwa wakiijua Ikulu kwa ukubwa kuliko watu wengi, ndiye ambaye alikuwa anatunza nyaraka za mhimu za Ikulu na kujua kila taarifa mahali inako patikana kuhusu nchi hii hususani viongozi, waliyoyafanya na awamu ambazo walidumu kwenye madaraka. Siku hiyo alikuwa amepewa kazi moja ya mhimu na raisi, kazi ya kuweza kumkusanyia taarifa zote za viongozi wa Ikulu tangu mwaka wa 1991 mpaka siku ambayo yeye alikuwa anaingia Ikulu, kuna mambo hakuona kama yapo sawa kwa upande wake hivyo alihitaji kuyajua.
Mr Nyemo alikuwa ni mtu makini kwenye kazi yake, hakuwahi kumuangusha bosi wake wala kuruhusu amhisi kwa lolote baya hivyo kila kazi ambayo alipewa alikuwa anaifanya kwa uhakiwa wa asilimia zote na raisi alilijua hilo. Aliamini kwamba mtu huyo anempa taarifa za kweli ili aendelee kumuamini ila habari hiyo ingewafikia watu ambao hakuwa akihitaji kabisa waweze kujua juu ya mpango wake mpya ambao ulichipua ghafla kwenye kichwa chake. Mwanahistoria huyo ni miongoni mwa watu ambao walichangia kwa kiasi kikubwa yeye kuweza kuingia Ikulu ila baadae aligundua kwamba mwanahistoria huyo alikuwa miongoni mwa watu na viongozi wa kuaminika ndani ya jamii ya siri ya LUNATIC SOCIETY ambayo hata yeye alikuwa mmoja wapo. Taarifa ambazo alizihitaji siku hiyo zilikuwa zinaainisha namna viongozi walivyo patikana ndani ya taifa la Tanzania na walichokuwa wanakifanya baada tu ya kuanguka kwa umoja wa nchi za Kisovieti.
Alihakikisha wamesafisha kila kitu hapo akamkonyeza mlinzi wake ambaye aliufunga mlango wa kuingilia kwenye chumba hicho, alihitaji kuwa mwenyewe. Alinyoosha mbele ambako kulikuwa na shelf kubwa ya kitabu, alitoa vitabu viwili akaviweka pembeni, mbele kulikuwa na kibox ambacho kilikuwa kinahitaji namba, aliingiza namba kadhaa shelfu la vitabu likajigeuza. Ulikuwa ni mlango wa kuingilia ndani zaidi, palifunguka akaingia huko kisha pakajifunga tena kama palivyokuwa mwanzo.
Alitulia kwenye meza na kutoa makablasha yale kisha akaanza kuyapitia moja moja huku kumbukumbu zake zikizama mbali miaka ya nyuma huko kabla hata hana hiyo ndoto ya kuja kuwa raisi wa Tanzania.
UKURASA WA 81 unafika mwisho.