SEHEMU YA 291
Moja ya sababu ambayo ilimpelekea Master Chi kumfundisha Roma mbinu ya kujiponyesha kutoka ujinini ni kutokana na ugonjwa Roma aliokuwa nao , ugonjwa wa saratani ya ubongo , ugonjwa ambao licha ya kwamba mwili wake ulifanyiwa sayansi , lakini ilishindikana kupona kabisa kwa asilimia mia moja , hivyo mara nyingi kumpelekea kushindwa kujizuia pale mwili wake unapopitia mabadiliko.
Ijapokuwa Master Chi aliweza kumfundisha mbinu hio Pamoja na levo zake , lakini hakumwambia jina la mbinu hio linaitwaje , Sasa Roma alijifunza kwa miaka mingi pasipo kujua jina lake , baada ya kifo cha Seventeen ndio aliweza kuvuka kutoka levo namba saba ya Lango na kuingia levo namba nane ya Kifo na Uhai na baada ya hapo ndipo alipoaamua kuipatia mbinu yake jina la kingereza ‘Endles Resolve restoration Scripture’ na kwa lugha ya Kiswahili ni Nguvu ya kimaandiko ya urejesho isiokuwa na kikomo.
Moja ya sababu ya kuipatia jina hilo ni kutokana na kwamba kila akitaka kuitumia mbinu hii lazima atamke baadhi ya meneno maalumu ili kuweza kupata kuitumia , unaweza kuifanananisha na ‘Spirity energy’ au kama vile ‘Albadir’ katika dini ya uislamu lakini utofauti wake ni kwamba mbinu yake Roma haikuwa ikitegemea ‘Freewill’ au Imani kuweza kuitumia , bali alikuwa akitumia kanuni za namna ambavyo ulimwengu umeumbwa.
Dunia imeumbwa kwa namna ya uwili(Duality) kwa falsasa za kichina wanaita Yin and Yang, yaani ukinyume unaoungana , kwa mfano kinyume cha mwanamke ni mwanaume , knyume cha dunia ni mbingu , kinyume cha uhai ni kifo na kinyume cha Nishati Maada(Matter Energy ) ni Nishati isio Maada(Ant-Matter Energy).
Sasa Roma ili mbinu yake kufanya kazi lazima atumie siri iliopo kati ya ‘Matter Energy’ na ‘Anti-Matter energy’ ili kupata nguvu ya kimaandiko ya urejesho isio na kikomo , mbinu hii ndio moja ya njia ambazo majini wengi hutumia kufanya mambo mengi yanayofanana na miujiza au Mazingaombwe(Magic).
Sasa Noriko Okawa na wenzake ambao waliandaa mpango wa kumuua Roma hawakuamini kama mpango wao ndio umemuwezesha Roma kupanda levo nyingine, licha ya kwamba hakuna ambaye alikuwa akifahamu ni mbinu gani hio Roma aliokuwa akiizungumzia ya kumfanya kuingia levo nyingine , lakini Noriko Okawa kwa kutumia uwezo wake aliona kabisa Roma alikuwa ni wa tofauti na alivyokuwa mwanzo.
Roma licha ya kwamba alikuwa ameamka , lakini alionekana kuwa katika mawazo , ni kama mtu ambaye alikuwa akitafakari kilichotokea siku mbili zote akiwa ndani ya jokofu.
Muda huo huo mvua na yenyewe ilianza kunyesha nje kiasi chakumfanya Roma kuzidi kuingia katika tafakuri nzito, mwili wake haukuwa kama ulivyokuwa kabla ya kuja hapa Japani na msisimko anaousikia ulikuwa wa kipekee sana na ndio uliomfanya kuanza kufikiria.
Sasa wale wawakilishi kutoka Innova baada ya kuona Hades hajafa , waliona sehemu hio sio mahali pake kubakia , walimwangalia Roma na kuona alikuwa kama mtu ambaye yuko kwenye mawazo na waliona huo ni wakati sahihi kwa wao kuondoka ndani ya hilo eneo .
Jasie na Jasoni pia waliona hapo sio mahala pake , kwani muda wowote ambao Roma atarudi kutoka kwenye hali yake ya kutafakari basi ni hakika kwamba hawawezi kupona hata kidogo.
Kwa kutumia kelele zilizokuwa zikisababishwa na mvua waliamini Roma mpaka akigeuza macho upande wao basi watakuwa wametoweka lakini jambo ambalo hawakuwa wakijua ni kwamba , licha ya Roma kuwa kwenye tafakari , lakini bado alikuwa akielewa kila kinachoendelea, ni kama alikuwa akiwasubiria wafike mlangoni kama ilivyokuwa kwa Kawanako.
“Hakuna mtu kuondoka hapa ndani bila ruhusa yangu”Aliongea Roma alieibukia mbele ya Jessie na Jassoni na mabwana hao walianza kutetemeka na kurudi nyuma kwa woga na ile wanafika kati walishangaa kitendo cha ajabu kikitokea , milango yote pamoja na madirisha yalijifunga yenyewe kwa wakati mmoja na kumfanya hata Noriko Okawa na Tanya kushangazwa na uwezo wa aina hio.
Roma aliwaangalia maadui zake kwa tabasamu la kifedhuli na akili yake ilichokuwa ikimwambia kwa wakati huo ni kuwaua wote.
“Kama nakumbuka vizuri miaka kadhaa nyuma nilitaka kuharibu makao makuu ya Innova kwa uchokozi wao usiofika mwisho , lakini kwasababu ya heshima ya Aphrodite niliwasamehe , ila kwa siku ya leo sidhani kama awamu hii nitaweza kutoa msamaha , nisipopata maelezo ya kutosha kutoka kwenu , basi viongozi wenu wakubwa watanipa maelezo baada ya vifo vyenu”Aliongea Roma huku akitembea taratibu akiwasogelea wawakilishi wale wa Innova , ambao sasa kila Roma akipiga hatua moja na wao walikuwa wakipiga hatua mbili kurudi nyuma , walionekana kuwa katika hofu isiokuwa na kifani.
“Hades tupo hapa kwa maelekezo kutoka makao makuu , hatuhusiki juu ya hili”Aliongea Bruno na Roma wala hakumzingatia bali macho yake yalimwangalia Jasoni pamoja na Jessie ambao na wao walikuwa wakimwangalia kwa wasiwasi.
“Nina maswali pia kwanin Dhoruba nyekundu wananifuatilia sana na nina mashaka hata muda huu kuna kamera za siri walizotega na wanaona kila kitu kinachoendelea hapa”Aliongea Roma.
“Hades mimi ni shabiki wako wa siku zote na sijawahi kukusudia kifo chako , mimi pamoja na Jasoni na kundi lote la Dhoruba nyekundu”Aliongea Jessie na kumfanya hata Jasoni kumshangaa mwenzake.
“Kama kweli wewe ni shabiki yangu , kwanini mpo mahali hapa mkiambatana na wahalifu na kwanini Innova wametaka muwekwe huru kwa dili alilolifanya Noriko Okawa kwa kutumia mwili wangu?”Aliuliza Roma na Jasoni alimshika mkono Jessie akionyesha ishara ya kwamba haruhusiwi kuongea na Roma aliwaangalia kwa dakika kadhaa na kisha akaachana nao na akamwangalia Kawanako , mwanadada ambaye ndio aliemwingiza mtegoni kwa kumuigizia kuwa ni Seventeen.
Roma alimwangalia mwanamke huyu aliejificha nyuma ya Noriko Okawa kwa sekunde kadhaa na akili yake ilimkumbusha miaka kadhaa nyuma , siku ambayo Seventeen alijirusha kutoka kwenye mwamba na kutua kwenye bahari na ikafuatia mlipuko ambao kwanzia siku hio alikuwa akitafuta wahusika.
Roma alijiambia kwenye moyo wake siku ya leo ndio ya kulipiza kisasi, kwanza kabisa Kawanako alikiri mwenyewe kwamba Seventeen hakujirusha kwa hiali yake , bali yeye ndio alimsukuma , hivyo moja kwa moja ikimaanisha kwamba yeye ndio aliemuua , Roma alimwagalia kwa dakika kadhaa na alijikuta tukio la Seventeen kujirudia rudia kama mkanda wa video unaopelekwa mbele na kurudishwa nyuma, na kadri alivyokuwa akishuhuduida tukio lile kwenye akili yake ndio hasira zilianza kumjaa na kufanya macho yake ambayo yalikuwa na kiini cha rangi ya kijani kubadilika na Kwenda kwenye tangi ya njano na kumfanya Jasoni na Jessie waliokuwa wakishuhudia tukio hilo kujawa na wasiwasi , kwani walikuwa wakijua maana ya rangi za macho ya Roma zinamaanisha nini.
“Jessie this time there is no way out for us to be alive”
“Jasoni ningejua hii misheni ilikuwa ya aina hii nisingeleta mguu wangu hapa , hata kama makao makuu ndio wangenipa oda ya moja kwa moja , wametuweka kwenye misheni ya kifo”Aliongea Jessie kwa wasiwasi mno.
“Jessie tumefunzwa kutii oda kutoka kwa wakubwa wetu , haijalishi misheni ni ya aina gani lakini lazima tutii kile tunachoagizwa”
“Na nini kitatokea baada ya hapa , tunakufa hapa huku makao makuu wakishuhudia vifo vyetu?”Aliuliza Jessie kwa namna ya hasira lakini kabla Jasoni hajampa jibu walijikuta wakiziba mdomo mara baada ya kushuhudia Kawanako akiwa kwenye mikono ya Roma akining’inia hewani akiwa amekabwa shingo.
Noriko Okawa ambaye alikuwa tayari kupambana na Roma hakuelewa hata Roma alipotea vipi na kuibuka nyume yake , kwani kitendo hiko kilikuwa hca haraka sana.
‘Puuh’
“Nadhani kabla ya kutekeleza kifo chako nikupe nafasi ya kuonyesha uwezo wako , naamini haujapewa jina la Mbweha wa miguu tisa bila sababu”Aliongea Roma baada ya kumtupa chini Kawanako.
“Hades ijapokuwa naweza nisikushinde lakini asante kwa kunipa nafasi ya kupambana kabla ya kuniua , sijutii kufa kwa mikono yako katika harakati za kujaribu kulipiza kisasi cha dada yangu”Aliongea Kawanako na palepale alinyanyuka haraka sana na kusimama , huku mwili wake ukainza kupitia mabadiliko na kufanya kila mmoja aliekuwa hapo ndani kuhisi msisimko usiokuwa kawaida.
Kawanako dakika ileile alipotea alipokuwa amesimama kama jini na kumfanya Roima kutabasamu kifedhuli na kufumba macho na kilikuwa ni kitendo cha nusu dakika tu Roma alisogea pembeni kwa namna ya kukwepa hewa na hapo hapo Kawanako alionekana akiwa mbele yake huku mwili wake ukiwa umebadilika na kuwa na nywele nyingi nyeupe kama vile paka , huku vidole vyake vikiwa na kucha zilizochomoza.
“Wow I like it”Aliongea Roma kwa tabasamu baada ya kuona Kawanako kabadilika na kuwa na mwonekano kama wa paka Shume.
Kawanako baada ya kuona Roma kamkwepa kwa mara ya kwanza aligeuka kwa spidi kubwa na kumsogelea Roma tena huku awamu hii akidhamiria kumpiga ngumi .lakini Roma alikuwa amemtegemea kwani ile anamfikia alimuwahi ngumi ya kifua na kumfanya kurudishwa nyuma na kudondoka chini.
“Inukaaaa…!!!”Aliongea Kawanako kwa lugha ya kijapani huku akionyesha hali kama mtu ambaye alikuwa akiita mapepo , kwani mikono yake yote miwili alipeleka mble kama vile mtu anasali.
“Inukaaa… Frujooof.. Frujoof!!!!”
“Boom! Boom!”
Hakuna mtu ambaye alitegemea lile tukio , kwani baada ya Kawanako kupandisha mashetani palepale sakafu ilipasuka na kusababisha mawe kuruka juu na kugonga ukuta , kitendo ambacho kilimfanya Roma kusogea sehemu aliosimama , kwani kidogo tu apigwe na jiwe.
“Damn it you are Demonic Cat!!?”Aliongea Roma kwa mchango baada ya kuona sehemu ambayo alikuwa amesimama kuchimbika na hapo ndipo alipogundua hakuwa akipambana na mtu mwenye nguvu mithili ya Mbweha wa vichwa tisa , bali alikuwa akipambana na Demon- Cat yaani pepo la kichawi sura ya paka.
Kawanako licha ya Roma kuongea kwa upande wake alionekana kama vile hakuwa akijielewa alichokifanya , na macho yake yalikuwa yamevilia damu mpaka alikuwa akitisha , ukijumlisha na Ngozi yake ambayo ilikuwa na vimelea vingi ilimfanya hata wale ambao hawakuwahi kukutana na hali kama hio kuwa katika mshangao mkubwa sana , akiwemo Jasoni na Jessie.
Kawanako baada ya kuona jaribio la kwanza limeshindikikana aliona atumie mwili wake kama siraha, alianza kuzungusha mikono yake juu kama vile anatafuta balansi ya kuruka sarakasi na Kumfanya Roma kutaka kujua anataka kufanya nini , lakini ghalfa palepale Kawanako aligeuka kama mpira ambao umezingiwa na miale kama radi ya rangi ya pimk na kumsogelea Roma kwa spidi kali , lakini mtaalamu Roma alikuwa amesimama palepale na ile mwili wa Kawanako unamfikia aliinua mkono wake juu na kisha akapiga ngumi mpira ule na Kawanako alirushwa na Kwenda kutua kwenye ukutana mpaka akatoka damu , lakini bado alionekana nguvu za kupigana anazo.
“Noriko unaonaje tukiunganisha nguvu kupigana kwa Pamoja , najua tulikuwa kwenye sintofahamu kati yetu lakini muda huu ni wa kifo na uhai”
“Sitaki kuichafua ‘Legacy’ ya mababu zangu kwa kuchangiana na mwanamke katika mapambanoo , wewe ukishindwa mimi nitapigana nae kwa wakati wangu”Aliongea kwa Kebehi , licha ya kwamba alijua Roma ana uwezo mkubwa , lakini aliamini kupigana kwa kusaidiana na mwanamke kwake ni matusi.
Kawanako baada ya kuona hana msaada palepale alijibadilisha mwili wake na kuwa Seventeen na kumfanya Roma kushangaa kutokana na mabadiliko hayo ya Ghalfa.
“Thirteen .. please don’t kill me anymore..”Aliongea Kawanako Seventeen feki huku akijifanyisha myonge mbele ya Roma,. Aliamini hiio ndio mbinu pekee ya kumchanganya Hades.
Roma baada ya kuona mwanamke ambaye alikuwa akifanana na Seventeen kwa kila kitu alijikuta macho yake yakitoka kwenye unjano na kurudi kuwa kawaida na jambo hilo lilimfanya hadi Noriko Okawa kutabasamu na kwa upande wa Kawanako aliona hio ndio nafasi pekee ,kwani palepale alitoka alipokuwa amesimama na ile anaibukia alikuwa juu ya shingo ya Roma , lakini pia haikuwa kwa Kawanako tu baada ya Noriko Okawa kuona Roma alikuwa amechanganyikiwa kwa dakika kadhaa na yeye alitoa upanga wake wa Masamura na kumsogelea Roma kwa nyuma na ile anamfikia tu alitumai nguvu zote kumchoma Roma mgongoni kwa panga lake , lakini alijikuta akitoa macho kwani panga lake lilipita hewani na Kwenda kumchoma Kawanako mwenye muonekano kama wa Seventeen.
“Why..!!!”Alishangaa Noriko O?kawa baada ya kugundua kuwa kilichokuwa mbele yake sio mwili wa Roma bali ni kama picha iliokuwa kwenye mfumo wa Hologam na kitendo chake cha kutumia nguvu kuchoma picha hio panga lake limeenda kumchoma kawanako.
Kawanako ambaye alikuwa akitokwa na damu mfuliulizo alimwangalia Roma aliekuwa nyuma yake kwa macho ya huzuni , alionekana alikuwa akimlaani hata akiwa kwenye kifo chake , Noriko Okawa baada ya kuvuta panga lake nje palepale Kawanako alidondoka chini na kufa hapohapo akiwa kwenye sura ya Seventeen ileile na kitendo kile kilimfanya Roma kuwa katika hali ambayo haikuwa ikielezeka kama alikuwa na fuaraha ama huzuni , ila alimwagalia Kawanako kwa namna isiokuwa ya kwaiada.
Noriko Okawa baada ya kugundua kuwa yupo kwenye hatari kubwa ilibidi awaangalie Tanya na Tanuki waliokuwa pembeni muda wote , Jesie na Jasoni pia walikuwa wamejibanza kwenye kona wakishuhudia kile ambacho kinaendelea na pia kwa upande wa Bruno na mwenzake pia walikuwa wakishuhudia kila kitu , lakini walionekana kuwa katika hali ya hofu mno .
“Kama mnataka kuishi inabidi mpambane na mimi”Aliongea Noriko Okawa kwa kuwaamrisha Tengu na Tanya kuungana kumshambulia Roma. ,lakini kwa Tengu aliona Master wake hana nafasi ya kumshinda Roma , hivyo aliamini mbinu pekee ya kuweza kuishi ni kutafuta namna ya kukimbia , aliangalia upande wa darini ambao umeharibika baada ya Kawanako kutumia nguvu zake za kichawi na alijiambia hio ndio sehemu pekee kwa yeye kukimbilia ili kuweza kutoka , lakini ni kama Roma alikuwa amemsoma mawazo yake kwani ile anapiga hatua tu Roma yuko mbele yake.
“Mara ya mwisho ulivyokuja Tanzania na kumteka mke wangu , nilitamani sana kukuua lakini nilikuacha kwasababu sikuwa kwenye nafasi nzuti , lakini leo hii ni swala tofauti”Aliongea Roma na palepale kwa kutumia mikono yake miwili alimpiga Tengu kichwani na kwasababu nguvu aliokuwa akitumia ilikuwa sio ya kwaida basi palepale Tengu alipasuka pasuka kama vile ni tikiti maji.
“Tanya anza kushambulia na mimi nitakufuatia kwa nyuma yako”Aliongea Noriko Okawa ambaye bado aikuwa ameshikilia mystical Masamura huku akionekana ni mwenye wasiwasi kweli.
“Sawa baba mlezi”Aliongea Tanya.
Ukweli ni kwamba Noriko Okwa alikuwa pia akitafuta upenyo wa kuchoropoka hapo ndani na mbinu pekee ambayo aliamini ingefanyakazi ni kumfanya Tanya kupigana na Hades na yeye kutoweka.
Sasa Noriko alikuwa amempa mgongo Tanya ambaye alikuwa ameshikilia kisu kwa namna ya kijihami , wakati Roma akishangaa uhusiano wa Tanya na Noriko , jambo la kushangaza lilitokea , kwani Tanya kwa spidi kubwa sana alimsogelea baba yake mlezi kwa nyuma , bwana Noriko Okawa na kumkita na kisu mgongoni na kikatokea mbele kifuani.
Jessie , Jassoni na Bruno na mwenzek walishangazwa na tukio hilo na hawakuelewa kwanini Tanya aliamua kufanya maamuzi ya kumshambulia Noriko Okawa ilihali ni kiongozi wake.
SEHEMU YA 292
Noriko Okawa alikuwa ni kama hakuwa akiamini kama mtu aliemdhuru alikuwa ni mtoto wake wa kike aliemlea kwa miaka mingi na kumpa cheo kikubwa ndani ya kundi la Yamata Sect.
“Usishange Noriko Okawa , hii nafasi nilikuwa nikiitafuta kwa miaka mingi”Aliongea Tanya na kisha alichomoa kisu chake na kumkita kwa mara ya pili Noriko Okawa na kumfanya panga lake la Masamura kudondoka chini.
“Tanya kama umeamua kumuua baba yako mlezi ukiamini kwamba nitakuacha hai naomba ulisahau , hilo mimi sina huruma kiasi hiko”Aliongea Roma aliekuwa amesimama mita kadhaa kutoka waliposimama.
Tanya alimwangalia Noriko Okawa uku akibubujkwa na machozi na alitumia tena nguvu zake zote kunyanya kisu alichokishikiria na kumchoma nacho Okawa eneo la moyo na pale ndio ilikuwa safari ya mwisho ya Noriko kwani alimwachia na akadondoka chini.
“Mfalme Pluto nilichotaka kwenye Maisha yangu ni kulipiza kisasi kwa huyu mwanaume kwa kuniulia familia yangu , lakini pia kunibaka tokea nikiwa mtoto mpaka sasa hivi , huku akiendeleza unafiki kwa kuniita mtoto wake”Aliongea kwa hasira huku akimwangalia Noriko Okawa mfu pasipo ya kuonyesha hali ya kiujutia hata kidogo.
Roma alisogea mpaka akalifikia panga alilokuwa akitumia Norio okawa , panga la Mystical Masamura na kisha alianza kulichunguza , lilikuwa ni panga zutri sana kwake na kwa kuliangalia tu lilimkumbusha mambo mengi ya nyuma , kipindi ambacho alikuwa akitumia panga katika kufanya mauaji, kipindi hiko akifahamika kwa jina la Thirteen , kabla ya kupata cheo cha Hades.
Roma baada ya kuangalia panga hilo kwa sekunde kadhaa alimrushia Tanya aliekuwa amepiga magoti chini akitoa kilio na Tanya baada ya kuona panga lile limerushwa kwake , ni kama alielewa nini anapaswa kufanya kwani alilichukua na kisha akaliweka kwenye shingo yake akiwa tayari kujiua kwa kujichinja.
“Sijakupa maagizo ya kujiua”Aliongea Roma kwa sauti ya kawaida.
“Kama sio hivyo hili..”
“Utakufa mpaka nitakapokupa ruhusa ya kufa , kwasasa unapaswa kuwa hai kwani utakuwa wa manufaa kwangu”Aliongea Roma
Ukumbuke pia hapo ndani walikuwepo Jasie na Jasoni Pamoja na wale wawakilishi wa Innova.
Tanya baada ya kusikia Roma anasema atakuwa wa manufaa kwake , palepale alianza kuona aibu za kike , kwake alikuwa akielewa kabisa kwamba mwanaume akimwambia mwanamke ana manufaa basi anamaanisha kumpa mwili wake kutumia.
Tanya alisimama na kisha akafungua gauni lake la kininja alilovaa kutoka kwenye mabega na likadondoka chini na kumuacha uchi na kuufanya mwili wake wa kijapani kuonekana wazi, Roma akifaidi kwa mbele uku wale wengine wakifaidi kwa nyuma kwani Tanya alikuwa amewapa mgongo.
Roma alimchunguza Tanya kwanzia juu mpaka chini na macho yake yakanasa sehemu ya katikati ya mwili wa mwanamke huyo kwa madakika kadhaa , aliangalia Tatoo iliochorwa kuzunguka sehemu ya uzazi na kumfanya kushangaa kwa sekunde kadhaa.
“Unafanya nini?”Aliuliza Roma.
“Mfalme Pluto nipo tayari kwa chochote unachotaka kwenye mwili wangu”Aliongea Tanya kwa kingereza.
Roma alimwangalia Tanya kwa macho kidogo ya huruma , aliamini Tanya yuko kama hivyo kutokana na Maisha yake aliokulia , mwanamke siku zote kuwa chombo cha starehe kwa mwanaume ndio Tanya alichokuwa amezoea na ndio maana alikuwa tayari kumhudumia Roma kwa kutumia mwili wake.
“Unafikiri nitautamani mwili wako? , nimekuacha hai kwasababu moja tu , Yamta Sect ni kubwa na siwezi kuijua yote na namna inavyojiendesha , hivyo nataka unisaidie katika hilo , panga la Masamura nadhani ndio ishara ya mamlaka kwa Ninja wote wa kundi la Yamata Sect na mimi nakupa mamlaka hayo”
“Ah .. Mfalme Pluto sikujua kama ulikuwa ukimaanisha kitu kingine , nilijua unataka …”Alisita kuongea huku akiona aibu na kuvaa gauni lake la kininja
“Mfalme Pluto kama unataka Yamta Sect kuwa chini yako , wala jambo hilo sio gumu ninaweza kulikamlisha hata kwa kutokutumia hili panga, kwasababu sasa hivi Okawa amekufa na Tengu, mimi ndio mwenye nguvu katika Ninja wote ivyo lazima waheshimu kile ninachowaambia”
Roma alijikuta akishangaa , hakujua kwamba kupata kundi lote la Yamta Sect ni rahisi namna hio, ukweli ni kwamba hakutaka kumuua Tanya kwasababu moja , aliamini kama Yamata Sect ikaachwa bila ya kuwa kiongozi basi kuna uwezekano wa watu wengine kuwa kiongozi na kuanza kumsumbua tena , jambo ambalo hakuwa akitaka litokee , hivyo aliamini akiacha kiongozi ambaye atakuwa anatii maagizo yake basi atakuwa na amani na baadhi ya mambo yake mengi yatarahisishika hata akiwa kwa Tanzania tu.
“Okey basi kwasasa Yamata Sect itakuwa chini yako , na wewe utakuwa chini yangu , sitaki ufanye kila kitu kwa maagizo yangu bali mtafanya mambo yenu kama ilivyokuwa mwanzo , lakini pale ambapo nikitaka kutumia hili kundi basi sitaki mambo ya kipumbavu yajitokeze , kuhusu mtu ambaye anaweza kuwa hatarishi na kutaka kukuondoka kwenye uongizi mimi nitadili nae mwenyewe”Aliongea Roma na kisha akawageukia watu wanne walijibanza ndani ya jengo hili wakiwa hawana tumaini tena la kuishi.
Roma mwenyewe alijishangaa kwani alikuwa hana hamu ya kuua kabisa kama ilivyokuwa mwanzo , alijiuliza huenda ni kwasababu ya kuingia levo nyingine ya Kuzaliwa Upya na ndio maana ashaanza kuwa na huruma , kwani alivyowaangalia watu hao wanne , alikuwa akishikia Roho ya huruma ikimwambia awaache hai na ilionekana kuwa na nguvu mno , kitu ambacho hakijawahi kumtokea hapo kabla.
Kwa mfano Tanya alimsamehe kirahisi sana licha ya kwamba ashawahi kumchokoza yeye na wenzake kwa kumteka mke wake , lakini akaamua kumpa msahama bila hata yakufikiria makosa yake, lakini pia muda huo alikuwa akiona kwa Jessie , Jasoni na wale wawakilishi wa Innova kutaka kuwasamehe.
“Sina mudi kabisa ya kuua leo , lakini haimaanishi kwamba nimewasamehe , kila mmoja wenu ili kupata msahamaha wangu lazima aniembie maisha yake hapa duniani ni ya thamani kiasi gani, Ofcourse kama kuna mmoja wenu anahisi maisha yake hayana thamani basi sitosita kumuua”Aliongea Roma akiwaamrisha Jasoni , Jessie na Bruno na wenzake kuongea.
Walijikuta wakiangaliana kwa kutokujua namna ya kujibu , kwani mpaka wakati huo licha ya kwamba wameishi , hawakujua Maisha yao yanathamani kiasi gani na swali la Roma kwao lilionekana kama mtego.
“Uthamani wa Maisha yangu unategemeana na wale watu wanaonipenda na kunithamini , hivyo siwezi kusema kwa hakika Maisha yangu yanathamani kiasi gani”Aliongea Bruno kwa wasiwasi na kumfanye Roma tabasamu kifedhuli.
“Okey tukiachana na wale wanaokutegemea , wewe mwenyewe unajihisi unathamani kiasi gani katika kipimio cha hela?”Aliongea Roma na sasa kuwafanya wote kuelewa swali.
“Maisha yangu yana thamanii ya Dollar milioni mia moja”Aliongea Jessie na kumfanya Roma amwangalie na kuona huenda mwanamke huyo ameji ‘overate’ sana, Jasoni na yeye alijiambia kuwa ana thamani ya Dollar milioni mia tatu , wakaja wale mabwana wawili wakasema wao wanathamani ya Dollar milioni hamsinni hamsini kila mmoja na kumfanya Roma kutabasamu kifedhuli.
“Kwahio jumla ya thamani ya Maisha yenu wote ni dollara milioni mia tano?”Aliongea Roma na wote walitingisha vichwa na Roma alimgeukia Tanya.
“Hela zilizolipwa kwa ajili ya mwili wangu ni kiasi gari?”
“Mfalme Pluto ni Dollar milioni mia tano na kumi”Aliongea Tanya na Roma alitngisha kichwa.
“Okey nitawaacha muendelee kuishi na kwakua malipo mshayatanguliza basi nitakata Dollar milioni mia tano kama malipo ya thamani ya uhai wenu na Dollar milioni kumi iliobaki nitajilipa kama sehemu ya usumbufu”Aliongea Roma na sasa kuwafanya Jassie na wenzake kuelewa alichokuwa akimaanisha Roma , kumbe alikuwa akitafuta uhalali wa kumiliki pesa ambazo zilikuwa zimeskwisha kulipwa kwa ajili ya mwili wake, lakini hakuna hata mmoja alietaka kuleta kipingamizi , wote kwa Pamoja walishukuru kutoka hai.
Roma alimpa malekezo Tanya ya kutuma hela zote ambazo zimelipwa kwa ajili ya mwili wake Kwenda kwenye akaunti yake ya Swiss na Tanya kwa haraka haraka alituma hela hizo kutoka katika Wallet ya Bitcoin Kwenda Swiss Bank.
“Mfalme Pluto kuna hizi pesa taslimu zilizobaki”Aliongea Tanya huku akimuonyesha Roma maburungutu ya pesa yaliokuwa kwenye Briefcase na alifikiria kidogo na kuona sio mbaya kama hela hizo ataziingiza kwenye akaunti yake ya kawaida.
Roma alimpa Tanya namba ya akaunti ya kawaida anayotumia akiwa Tanzania na kumpa maagizo ya kuziingiza pesa hizo kwake.
“Nadhani unajua cha kufanya juu ya kundi la Yamata Sect na taratibu zingine za kuongoza?”
“Ndio Mfalme Pluto ninalijua kundi hili nje ndani hivyo sio ngumu kiliongoza”Aliongea na Roma alitingisha kichwa na kuamini Tanya ni mtu sahihi kumuachia aongoze kundi hili la Yamata Sect ambalo mpaka muda huo ni kama la kwake.
Roma alibadili nguo zote alizokuwa amevaa kwani zilikuwa zimechafuka na Damu na sasa akili yake ilianza kurudi kwenye jambo ambalo limemleta Japani , swala la kumuokoa mrembo Amina.
Lakini bado mwili wake ni kama haukuwa sawa , sumu ambayo ilikuwa imeingizwa kwenye mwili wake bado haikuwa imeisha kabisa na kumsababishia kuhisi kizunguzungu, aliamini kama sumu hio itaendeea kuwa ndani ya mwili wake inaweza kumletea shida , hivyo aliamini kuna ulazima wa kuitafutia dawa yake , wakati akiendelea kuwaza aliamini mtu pekee ambaye anaweza kumsaidia kutoa sumu hio kwenye mwili wake ni Profesa Clark, Roma alijaribu kutoa simu yake kumpigia Profesa Clark na bahati nzuri iliita kwa dakika kama moja hivi mpaka kupokelewa.
Mwanzoni sauti ya mrembo Profesa Clark ilionekana kuwa katika furaha mara baaada ya kujua Hades ndio kampigia , lakini sekunde chache mbele sauti ya mwanamke huyo ilijawa na wasiwasi mara baada ya Roma kumwambia kwamba amewekewa sumu kwenye mwili wake na bado hajisikii vizuri na anataka ajaribu kumwangalia,
“Hades nipo Hongkong nilikuwa na semina ya siku tatu na tumemaliza leo , nitafanya safari ya dharula, niambie ni wapi tunapaswa kuonana niweze kuangalia hali ya afya yako”Aliongea Profesa Clark kwa wasiwasi mkubwa
“Tukutane Hokkaido Sapporo City”Aliongea Roma na Profesa Clark alionekana kuelewa na hapo hapo Roma alikata simu na kumwangalia Tanya aliekuwa pembeni yake akisikiliza mazungumzo yao.
“Your Majest Pluto ,do you need me to employ our private jet?”Aliulia Tanya na hio ni mara baada ya kusikia mazungumzo ya Roma Kwenda Sapporo City hivyo alijiongeza haraka haraka na kutoa pendekezo ambalo kidogo lilimshangaza Roma.
“What private jet?”Aliuliza Roma kwa mshangao.
“We have exclusive jets in every airport in Japan , its not publicly known since its secret, all of them are at your service anytime”
“Tunazo ndege binafsi kwa kila uwanja wa ndege hapa Japani ambazo hazifahamiki kwani ni za sirisa na ndege zote hizo zipo kwa ajili ya kukuhudumia”Aliongea na kumfanya Roma kushangaa , hakuwa na taarifa kwamba Yamata Sect ilikuwa na pesa kiasi gani.
“Hili kundi la Yamata Sect lina thamani ya kiasi gani in total Asset?”aliuliza Roma , alitaka kujua ni thamani kiasi gani kwa kundi lote.
Kwa maelezo ya Tanya thamani yote ya kundi la Yamata Sect ni dollar za kimarekani bilioni sita kuanzia pesa iliokuwa ndani ya benki , lakini pia baadhi ya vitu biashara ambazo zipo chini ya Yamata Sect.
Roma alitabasamu baada ya kugundua kumbe kundi hilo lina thamani kubwa kiasi hiko , alijiambia safari yake ya kuja Japani haikuwa ya kupoteza muda kwani mpaka hapo alikuwa ametengeneza kiasi kikubwa sana cha pesa ndani ya siku mbili takribani Dollar bilioni saba.