Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEHEMU YA 299.

Baada ya Fayezi kutoka ndani ya chumba cha Mke wake Mtarajiwa Amina , alitoka kabisa ndani ya hoteli hio akiwa ametangulizana na wanajeshi wawili kutoka kikosi maalumu ambao wote wamekodiwa na familia yake kwa ajili ya kumpa ulinzi, wote wakiwa wamevalia suti.

Dakika chache mbele walikuja kusimamisha magari yao mawili upande wa pili ndani ya jiji hili la Otaru ,sehemu maarufu sana iliokuwa ikisifika kwa kuwa na huduma ya masaji iliokuwa ya kiwango cha juu sana.

Fayezi alitaka kuweka mwili wake sawa kabla ya siku yake kubwa ya kesho na ndio maana alikuwa ndani ya eneo hilo kwa ajili ya kufanyiwa masaji, Alikutana na mwanaume mwingine wa kijapani ambaye alikuwa ni wa umri wa kati alievalia suti na alimuongoza kwa heshima kubwa na kwa Pamoja waliingia kwenye jengo ambalo lilikuwa na bango linalowaka taa na maandishi makubwa rangi nyekundu yaliosomoeka kwa juu ‘Clubhouse’.

Wote wawili Pamoja na bwana ambaye alimpokea walionekana wakiwa ndani ya chumba cha masaji huku wakiwa wamezungukwa na wanawake warembo sana waliovalia nusu uchi wakishikwa kwa mikono laini sana wakifanyiwa masaji , kitendo amacho kiliwafanya kujihisi kama vile wapo dunia nyingine kabisa.

Dakika takribani ishirini walikuwa wakiminywa minywa kwanzia makalioni mpaka kwenye shingo , Fayezi licha ya kutozoea huduma hio , lakini alionekana kuifurahia mno.

Wakati wakiendelea kufanyiwa masaji simu ndani ya chumba hiko ilianza kuita mfululizo ikiashria kuna dharula na mhuduu aliekuwa karibu aliichukua na kisha kuipokea baada ya kuona inatokea mapokezi.

“Sir kuna kundi la watu limeingia ndani pasipo ruhusa kutoka mapokezi na wanasema wanawatafuta”Aliongea yule mwanamke na kumfanya bwana yule wa kijapani kumwangalia kwani mhudmu aliongea kwa kijapani .

“Amesema wametokea wapi?”

“Wamesema ni kutoka kundi la Yamata Sect”Aliongea yule muhudumu na kumfanya Fayezi aliekuwa akiendelea kuburudika kuinua kichwa.

“Kama ni Yamata haija haja ya kuwahofia , nina ushirkiano nao katika maswala ya kibiashara hivyo hawana madhara kwetu kwani kila kitu kinaenda sawa”Aliongea Feyezi kwa kingeteza , lakini mara baada ya kumaliza Sentensi yake , kundi la wajapani waliovalia suti wakiwa mchanganyiko wa wanawake na wanaume waliingia ndani ya chumba hiko cha masaji huku nyuso zao zikiwa katika hali ya usiriasi mno.

Fayezi aliwaangalia watu hao na kuona hakuwa akiwatambua hata mmoja , lakini hakujali , alichokuwa akiamini ni kwamba watu hao walikuwa ni moja ya vijana wa Noriko Okawa.

“Wewe ndio unafahamika kwa jina la Fayezi kutoka kampuni ya Emaar Dubai?”Aliuliza kwa Kingereza mwanaume mmoja wa kijapani ambaye sura yote imajaa ndevu huku akiwa na sura ya kutisha.

“Ndio ni mimi , mnashida gani na mimi , kwani kila kitu nilishamalizana na boss wenu?”

“Tumepata taarifa kwamba unafanya biashara ya madawa ya kulevya ndani ya eneo letu jambo ambalo ni kinyume na makubaliano yetu ya kibiashara”

“Madawa ya kulevya!! , hapani sio kweli , boss wenu atakuwa amekosea”

“Hajakosea na ndio alietupatia maelekezo ya kuja hapa, utatoa ushirikiano wako na tutakusachi kama hauna madawa ya kulevya tutakuacha na kuendelea na mambo yako”Aliongea yule bwana ambaye alionekana kuwa ndio kiongozi wa kundi la Yamata Sect.

Lakini hata hivyo Fayezi aligoma kusachiwa na sharti lake lilikuwa ni kuongea kwanza naNoriko Okawa ambaye alikuwa akimjua kama mkuu wa kundi la Yamata na vijana wale hawakuwa na shida , simu ilipigwa kwa boss mwenyewe

“Mr Fayezi wape vijana wangu ushirikiano , tumepewa taarifa unafanya biashara ya heroin ndani ya mji wetu wa kibiashara”Ilisikika suati ya mwanamke upande wa pili na kumfanya Fayezi kutabasamu kifedhuli.

“Nataka kuongea na boss wako”

“Kwanzia leo mimi ndio boss wa Yamata Sect, kama unamuulizia Noriko Okawa basi fahamu kwamba hayupo tena hai”ilisikika sauti na kumfanya Fayezi kushangaa mno ni kama hakuwa akiamini.

“Noriko Okawa hawezi kufa haraka hivyo ,mchana wa leo niliwasiliana nae na hata hivyo mimi sifanyi biashara yoyote ya madawa ya kulevya mmekosea mtu mnaemtafuta”Aliongea Fayezi kwa namna ya kujitetea , lakini watu kumi kutoka kundi la Yamata Sect walionekana kuwa siriasi mno na walikuwa wakitaka tu kusikia amri ya boss wao wachukue hatua.

“Kama unajiamini hauna madawa ya kulevya , basi haina haja ya kuewaletea matatizo vijana wangu unachotakiwa kufanya ni kuwaruhusu kufanya kazi yao , kama alietoa taarifa kakosea basi adhabu itakuwa juu yake”Aliongea Mwanamke aliekuwa kwenye simu na mjapani aliekuwa ni msaidizi wa karibu wa Fayezi alimpa ishara ya kukubaliana na watu hao kumsachi.

“Okey mnaweza kusachi , sina haja ya kuogopa kusachiwa kwasababu najiamini sina madawa ya kulevya ya aina yoyote ile”Aliongea Fayezi na wale vijana wakiongozwa na kiongozi wao aliekuwa akifahami kwa jina la iboru , walianza kufanya ukaguzi wao ndani ya chumba hiko kwa haraka sana , hawakutaka kuchelewa kwani mteja wao alikuwa akionyesha kujiamini sana kutokuwa na madawa ndani ya chumba hiko , hivyo wlaiamini kufanya haraka ni kuokoa muda.

Walinzi wa Fayezi walitaka kuzuia jaribiio hilo , lakini vijana wa Yamata walionekana kuwa tayari kupambana, Fayezi ilibidi kuwapa ishara watulie na kuruhusu zoezi hilo kufanyika kwa dakika chache kwani alikuwa akiamni hakuwa na madawa ya kulecya na hakuwa hata na mpango wa kufanya biashara hizo haramn ndani ya Japani, yeye alikuwepo hapo ndani ya Japani kwa ajili ya kufunga ndoa na mpezni wake Amina , hivyo swala la madawa lilikuwa limemkalia kushoto.

Maninja wale wa kundi la Yamata Sect walitumia dakika kama tatu tu kusachi kwenye suti za Fayezi na yule mchina na hatimae waliweza kuibuka na vijimfuko vya nailoni vitatu vilivyokuwa na unga mweupe ndani yake , na kwa mtaalamu wa haraka haraka angegundua kuwa hayo ni madawa ya kulevya aina ya Heroin kutokana na rangi yake kuwa kama ya unga wa ngano.

“Hapana hayo madawa sihusiki nayo kabisa , sijawahi kupanga kuuza madawa ndani ya Japani na sio hivyo tu Emaar haijawahi kujihusisha na biashara haramu”Aliongea Fayezi kwa kujitetea huku akiwa kwenye mshangao kuona mfuko wake wa suti ndio uliotolewa paketi tatu za madawa hayo.

“Usitufanye sisi ni wajinga , tunaamini vipi hauhusiki, ushawahi kusikia wapi mtu anaeuza madawa ya kulevya akajitangaza, kila mtu anafanya siri na wewe pia ni mmoja ya watu wanaotunza siri katika biashara hii”

“Sio kweli labda hawa wanaofanya masaji ndio wamehusika kunibambikizia madawa hayo , ila sihusiki nayo kabisa na Mungu wangu ni shahidi”Aliongea Fayezi lakini vijana wale walionekana kutokujali kabisa , walichokifanya ni kupiga simu kwa boss wao.

“Boss tumepata kugundua Fayezi ndio muusika anaeuza madawa ndani ya jiji hili , tunapaswa kuchukua hatua gani baada ya hapa”

“Mkamateni na mleteni kambini tumuhoji vizuri”Sauti ya mwanadada Tanya ilisikika na vijana wale mara baada ya kusikika maelekezo hayo walitoa ishara kwa vijana wao kwa ajili ya kumzingira Fayezi , ili kumkamata na kumpeleka kambini kama walivyopewa maagizo na boss wao.

Fayezi alikuwa ni mwenye hasira mno , mpaka hapo aliamini huo ni mtego umeandaliwa kwa ajili ya kumkamatisha hivyo hakuwa tayari kukamatwa kizembe wakat iyeye ni mtoto wa Tajiri kutoka dubai na alikuwa na koneksheni nyingi.

“Naombeni nifanye mawasiliano”Aliongea Fayezi huku akisogelea suruali yake , lakini maninja wa Yamata Sect waliichukua nguo zake na kutoa simu na kisha wakamrushia nguo zake avae haraka na kwakua Fayezi na mwenzake alikuwa uchi , hawakuleta ubishi walivaa.

“Hatuwezi kukupa simu tena kwani mara ya kwanza ulituambia huna madawa na tukakukutan nayo , unatufanya sisi wajinga na hatuwezi kuruhusu”Aliongea yule jamma mwenye kutisha huku akimwangalia Fayezi aliekuwa akivaa mavazi yake kwa haraka.

Walinzi wa Fayezi walidhibitiwa ndani ya dakika chache tu na wale wahudumu pia na wenyewe walidhbitiwa na kwa Fayezi na msaidizi wake pia walidhibitiwa na wote kwa Pamoja walipoteza fahamu palepale na dakika kadhaa mbele walikuwa wakitolewa nje kabisa ya Clubhouse na kuingizwa kwenye gari aina ya Noah Toyota na palepale gari ile iliondolewa na Kwenda kusimama mita kadhaa mbele sehemu yenye miti ya bustani na mlango wa Gari lile ulifunguliwa kwa mara nyingine na Fayezi Pamoja na msaidizi wake walionekana wakitoka ndani ya gari lile na kuanza kupiga hatua kurudi kule walikotoka wakiwa vile vile na mavazi yao yaleyale.
 
SEHEMU YA 300.

Uwepo wa Lanlan kwenye Maisha ya Edna ni kama ulimbadilisha kwa asilimia mia moja , kwanza kabisa ratiba za Edna zilibadilika hakuwa mtu wa kufanya kazi kwa masaa mengi kama ilivyokuwa mwanzo , Edna alikuwa kila ikifika saa tisa na nusu tayari atakuwa njiani akiwa na zawadi akirudi nyumbani kwa ajili ya kumuona Lanlan.

Hisia za kuwa mama kwake zilimfanya hata baadhi ya mawazo aliokuwa nayo kumpotea kwa asilimia mia moja na sasa kila akichofikiria , Lanlan alikuwa akihusika kwa asilimia kubwa.

Upande wa ndani ya kampuni ya Edna Ernest Komwe alikuwa na urafiki wa karibu sana na Benadetha, mara nyingi wawili hao walionekana kuwa Pamoja sana na jambo kubwa Zaidi ni kwamba Komwe alikuwa kila akifka kazini lazima aingie ndani ya ofisi ya Benadetha na kumsalimia, licha ya wafanyakazi kushangazwa na ukaribu wao na hat baadhi yao kumuuliza Benadetha juu ya uhusiano wao , lakini Benadetha aliishia kukana kwamba hakuwa na mahusiano kabisa na Ernest Komwe, na mahusiano yao yalikuwa ni ya kiikazi Zaidi.

Ni muda wa saa tatu kamili ndani ya familia ya Edna , familia yote ya Roma ilionekana ikiwa eneo la Sebuleni wakiangalia runinga huku Lanlan akiwa amelala kwenye mapaja ya Edna akiwa anakoroma baada ya kula nusu ya chakula chote kilichopikwa.

“Lanlan kabadilika sana”Aliongea Qiang kwa Kingereza na kumfanya Edna kumwangalia.

“Unamaanisha nini kabadilika Qiang?”

“Mara nyingi Lanlan kulala ni mpaka saa saba ya usiku ndio anapitiwa na usingizi , lakini tokea siku hizi alivyofika hapa amekuwa akilala mapema”Aliongea na kumfanya hata Blandina kushangazwa na maneno ya Qiang, mtoto kulala saa saba za usiku ni jambo ambalo halikuwa limezoeleka ndio maana walishangaa.

Edna alimwangalia Lanlan aliekuwa akijikunja kunja kwenye mapaja yake na kujikuta akitabasamu na kumshika mashavu.

“Sister Edna unafanana kabisa na Lanaln kwa kila kitu , mtu asiemjua Lanlan historia yake basi atasema umemzaa kabisa”Aliongea Sophia na kumfanya Edna kutabasamu.

“Vipi maandalizi ya mashindano ya uimbaji?”Aliuliza Edna na Sophia alitabasamu.

“Yanaendelea vizuri sister natamani ingekuwa mchana nijaribu kuimba ili muone uwezo wangu”Aliongea Sophia.

“Kwa sauti yako inaonyesha ni hakika una uwezo mkubwa wa kuimba , kesho asubuhi inabidi tukusikie namna ulivyojaaliwa”Aliongea Blandina na kumfanya Sophia kutingisha kichwa kukubaliana nae.

Wakati Edna akijianda kumbeba Lanlan kupandisha nae juu kwa ajili ya Kwenda kumlaza kitandani kwake , mara vilisikika vishindo nje ya nyumba na kufanya watu wote kuangaliana, Blandina ndio aliekuwa wa kwanza kusoglelea mlango wa nje ili kujua ni kitu gani kimedondonda , Blandina hakuwa na wasiwasi maana kulikuwa na walinzi nje ya nyumba , lakini baada ya kufikia mlango.

“Yesuu…!!!”Alijikuta akitoa ukulele baada ya kushuhudia mtu aliekuwa mbele yake huku akiwa amemnyooshea siraha aina ya bastora na kufanya watu wote kusimama kwa woga kuangalia upande wa mlangoni na hata Lanlan aliekuwa amelala alishituka.

Jumla ya wanaume kumi waliingia ndai ya eneo la sebuleni ,mmoja ambaye alikuwa ni Salah alikuwa ameshikiria bastora huku wengine tisa wakiwa si raia wa Tanzania kwa namna walivyokuwa wakionekana , kuna wawili walionekana kama wajapani na wengine wote wlaiobakia walikuwa ni wachina , wote kwa Pamoja walikuwa wameshikilia mapanga huku wakiwa wamejifunga vitambaa usoni kwa staili flani hivi kama ile wanayopendelea Alshababu.

Edna na wanafamilia wengine walijikuta wakiwa kwenye kiwewe na kilichofanya kuwa katika kiwewe Zaidi ni kwamba watu waliokuwa mbele yao walionekana hawakua na nia nzuri kwao.

“Nyie ni wakina nani na kwanini mevamia kwenye nyumba yetu?”Aliuliza Edna baada ya kuuvaa ujasiri lakini wanaume waliokuwa mbele yao ni kama hawakuwa wakimwelewa kabisa na Edna mwenyewe aliliona hilo na kuona watu hao huenda hawakuwa wakijua lugha ya kiswalihi hivyo alitumia lugha ya kingereza kujaribu kuongea nao , lakini vilevile watu wale walionekana kutolewa kabisa , yaani walikuwa ni kama mizimu hivi.

Salah ambaye alionekana kama ndio kiongoozi alimwangalia Edna kwa madakika kadhaa huku akionekana kama mtu aliekuwa akijiuliza ni wapi amemuona huyo mrembo , lakini licha ya hivyo alionekana kutokumkumbuka vizuri.

Edna yeye alikuwa kwenye mshangao mkubwa sana , kwani Salah alikuwa akimkubuka vyema kufariki kwa kuuliwa na mume wake Roma , sasa alishangaa na kujiuliza kwanini mtu huyo yupo hapo akiwa hai, tena akiwa ameshikilia siraha , mpaka hapo alihisi kabisa kuna jambo baya ambalo linakwenda kutokea , aliamini huenda Salah alikuwa na pacha wake na ni huyo aliekuwa mbele yake na wapo hapo usku huo kwa ajili ya kulipa kisasi.

Saa kabla hawajafanya maamuzi ya kuwashambulia wanafamilia hao , muda uleule Chiara alitaengulizana na John waliingia na walianza kupambana na wanaume wawili waliokuwa nyuma ambao wameshikilia mapanga lakini kilichowakuta kilimfanya hata Edna kufumba macho , kwani wachina wale walikuwa na spidi isio ya kawaida , kwa haraka haraka walionekana kuwa na mafunzo ya Kung Fu , kwani wakati Chiara analetea pigo upande wa kulia kupangua upanga uliokuwa umeshikiliwa kwa mkono wa kulia na mchina , yule bwana alifyatua kwa nguvu upanga wake na kulenga tumbo la Chiara na kilichotokea ni kwamba Panga lile lilipita moja kwa moja na kutokezea upande wa pili mgongoni na Chiara aliishia kutoa macho huku akimwangalia Edna kwa namna ya kama mtu anaomba msamaha kwa kutokumlinda.

Upande wa John yeye baada ya kugundua mwenzake kadungwa na panga la tumbo alijikuta akikosa umakini na kilichosikika ni ‘Shwaa..’ panga lilimkata kwenye kiwikicho cha mkono na kusababisha damu kusambaa eneo lote la hapo ndani.

Sasa mpaka hapo Edna na wanafamilia wengine waliona hawapo eneo salama kabisa , kwani watu waliokuwa wakiwategemea kuwadhibiti wavamizi ndio hivyo tena, John mzungu amekatwa mkono na alikuwa amedondokea pembeni akiugulia maumivu na Chiara keshapoteza Maisha ya kudungwa na panga la tumbo.

Kwa jinsi watu hawa walivyokuwa wakifanya ni kama walikuwa hawana akili vizuri , kwani wote walifanana kiuhaiba, yaani hakukuwa na maongezi Zaidi ya kuangaliana kama maroboti na hata mchina ambaye alimdunga Chiara na panga lake alionekana kutokuwa kwenye hali ya kujutia kabisa kwa kitendo chake , alikuwani kama myama.

“Kill them all”

“Uweni wote”

Ni kama sauti za mwangwi ndio zilizokuwa zikisikika kwenye vichwa vya Wavamizi hao waliokuwa wakiongozwa na Salah aliefufuka , walikuwa wakipokea maagizo ya kuua kila kichokuwa mbele yao na Salaha ndio alieanza kupiga hatua ya kuwasogelea, ukumbuke hapa licha ya kujipanga ndani ya sebule hii kubwa , walikuwa wakiwaangalia wanafamilia hao kama vile hawakuwa na nia ya kuwaua kabisa, yaani walikuwa binadamu lakini kama misukule.

Huku nyuma Sophia , Yezi pamoja na Qiang walikimbilia upande wa jikoni kwa ajli ya kujificha , Bi Wema na Blandina wao walikuwa wamesimama huku presha ikianza kupanda kwa haraka sana na Bi Wema alikuwa akikosa pumzi na palepale alilegea na kabla hajatua chini Blandina alimuwahi na kumzuia asidondokee meza ya kioo.

Edna sasa baada ya kuona tayari yupo kwenye hatari alijikuta akimrudisha Lanlan nyuma kwa staili ya kumkinga ili kama ni kudhurika aanze yeye , kati ya wanawake wale wote yeye pekee ndio aliekuwa amesimama vilevile akionyesha kuwa tayari kukumbana na jambo lolote..

Edna alijikuta akianza kumuwaza Roma , lakini mawazo yake kabla hayajatimia Salah aliinua siraha yake na kisha kumyooshea Edna kwa nia ya kumuua , kitendo kile kilimfanya Edna kuinama na kumkumbatia Lanlan na kumpa mgongo Salah.

“Paah… Paaah!!!”.

Ni mlio wa risasi uliosikika kwenye masikio ya Edna na mpaka hapo aliamini kabisa risasi hizo zimekosa na alijikuta akinyanyua uso wake na kugeuka nyuma huku akitetemeka mno kwa woga na hapo ndipo aliposhuhudia Salah aliwa chini amepigwa risasi za mgongoni na John aliekuwa anaugulia maumivu nyuma.

John baada ya kuona risasi zile zimempata Salah macho yake yalijaa ukungu na pelapela alipoteza fahamu kwani damu ilikuwa zikimtoka kwa kasi sana kiasi kwamba nguvu zilimuishia.

Sasa kitendo cha John kupoteza fahamu kilishuhudiwa na Edna na kumfanya kukata tamaa Zaidi na kutamani muujiza utokee,kwa jinsi mrindimo wa risasi ulivyosikika aliamini kabisa watu wan je wangesikia , kwani eneo alilokuwa akiishi lina ulinzi mkali kutokana na kupakana na viongozi wa jeshi lakini pia wanasiasa wakubwa , lakini aliamini kwa watu ambao wako mbele yake , wanaoonekana kama misukule , mpaka msaada ukiwafikia basi watakuwa wote wamepoteza Maisha.

“Edna kimbilia jikoni na Lanlan “Aliongea Blandina kwa kutahadharisha huku akimpita Edna na kusimama kwa mbele.

Sasa jambo la kushangaza hapa ni kwamba licha ya matukio hayo yote ya kufa mtu kupigwa risasi na kuchomwa kwa Chiara panga la tumbo , upande wa Lanlan hakuwa na wasiwasi kama ilivyokuwa kwa wanafamilia wengine , mtoto huyu ni kama mwili wake ulikuwa umechomwa na sindano ya madawa ambayo yanaufanya mwli wake kusisimka.

“Grandmaa..!!!!, Mamaaaaa nyuma yako …!!!”

“Tuuh!!!!”

Unajua hawa wachina ni kama walikuwa wakitegeeana kufanya mashambulizo kwani walikuwa wakiacha mmoja afanye shambulizi na wao kufatia yaani walikuwa ni kama wanategeana hivi, hawakuwa kama majambazi kwamba waongee au kutahadharisha na hata kwa Edna aligundua watu hao hawakuja hapo ndani kupora bali ni kuua pekee.

Ssasa mjapani aliekuwa mita kadhaa nyuma alimsogelea Blandina kwa kasi kubwa huku akidhamirira kumfekya , lakini sasa kabla hata hajamfikia , alijjikuta akirushwa kwa nguvu isiokuwa ya kawaida na Kwenda kutua kwenye Gympsum mpaka ikapausika , kwani nguvu iliomrusha juu haikuwa ya kawaida na kitendo hiki ni mara baada ya Lanlan kuita kwa nguvu jina la Bibi yake.

Edna aliekuwa hajaelewa kilichotokea alijikuta akigeuka na kumwangalia Lanlan na hapo ndipo aliposhuhudia kitu kichokuwa cha kawaida, kwani macho ya Lanlani yalikuwa ni kama Kioo, yaani kile kiini cheusi hakikuwa kikionekana na sasa ni kiini cheupe tu ndio kilikuwa kwenye macho ya Lanlan.

Sasa wale wachina wenyewe walijikuta wakiwa katika mshangao na macho yao yote waliyaelekeza kwa ,mtoto mdogo Lanlan.

“Mpo hatarini shambulia mtoto”

Sauti kama mwangwi ilisikika katika vichwa vyao na kuwafanya wakuje vichwa vyao kwa kujizungusha na kisha palepale mmoja ya mchina aliekuwa upande wa kushotoa alifyatuka kumsogelea Edna na Blandina , lakini kabla hajawakaribia Lanlan aliekuwa amesimama aligeuka kama Mpira na Kwenda kumpiga kikumbo yule mchina na kilichotokea ni kwamba mchina yule alirushwa nyuma kwani nguvu iliomgonga haikuwa ya kawaida.

“Atakeye mgusa mama yake Lanlan na bibi yake nitamuua…”Aliongea Lanlan kwa namna ya kuwa siriasi kabisa huku macho yake yakiwa vilevile pasipo ya kubadilika na kumfanya Blandina na Edna kujawa na hofu mno.

“Mshambilieni wote kwa Pamoja , mapanga tanguliza mbele”

Sauti pia ilianza kusikika kwenye vichwa cha watu tisa sasa na palepale walisogeleana karibu na kunyoosha mapanga yao mbele kwa ajili ya kumshambulia mtoto mdogo Lanlan.

Mpaka hapo akili zao ni kwamba zilikuwa zinahisi hatari , hivyo walikuwa kwenye mfumo wa kujiokoa na pia akili zao zilikuwa zikiwapa maelekezo ya kwamba mtoto aliekuwa mbele yao alikuwa ni hatari kwao.

Salah ambaye alikuwa amepigwa risasi na kudondoka mita kadhaa kutoka aliposimama Edna alisimama tena kama vile mtu abaye dakika moja iliopita hakuwa amepigwa risasi na baada ya kusimama kitu cha kwanza alichotafuta ni siraha yake iliodondokea pembeni , aliisogelea na kisha akaichukua.

“Lanlan…” Edna na Blandina walijikuta wakitamka kwa Pamoja na kumsogelea Lanlan na kumkinga baada ya Salah kumyooshea bastora.

‘”Arrggh …!!!!”

Ni damu ya moto iliowarukia Edna na Blandina huku wakisikia miguno ya maumivu kutoka kwa wavamizi hao na walijikuta kwa pamoja wakigeuka na kuangalia ni nini kinaendelea, na hapo ndipo walipoweza kuwa katika mshangao , kwani ni kivuli pekee ndio walichoweza kuona kikiadhibru wale wachina na wajapani kwa dakika chache mno na mtu ambaye alikuwa akiwaadhibu hakuwa na huruma kabisa kwani alikuwa akitenganisha shingo moja kwa moja.

Dakika moja tu tayari majambazi yote kumi yalikuwa hayana vichwa , kwani vilishatenganishwa kwa upanga.

“Persephone… !!, naitwa Christine ni rafiki wa karibu na Hades”.

Sasa Edna alikuwa kwenye mshangao mno , kwanza kabisa mtu aliekuwa mbele yake alikuwa akimfahamu kama moja ya waigizaji na waimbaji maarufu sana , kitu cha pili Edna kilichomfanya kushangaa ni kwamba mwanamke huyo mrembo wa kutisha , alikuwa pia na uwezo wa kimapigano ambao hakuwahi kuhisi kwenye Maisha yake atakuwa nao , kwani siku zote alimuona mwanamke huyo kama mwimbaji mlaini sana ambaye alikuwa akipewa ulinzi , sasa kitendo ambacho kilitokea hapo ndani cha vichwa vya wajapani Pamoja na wachina kutenganishwa , kilimfanya Edna kumwangalia Christine Stewart mwimhaji kutoka Marekani kwa maswali mengi , juu ya yote ni jina la yeye kuitwa Persephone na mzungu huyo licha ya kutokuwa mara ya kwanza kulisikia , lakini pia urafikiwa Christine na Hades , jina hilo pia lilikuwa geni kwake.

“Upo kwenye mshangao kwa namna nilivyowafyeka hawa binadamu wapuuzi waio na nafsi, kwa majina mengine pia nafahamika kama Aphrodite nitakuwa na huzuni kama Hades hajakutajia jina langu ilihali ndio kanikaribisha Tanzania.. hata kumsaidia kulinda familia yake.”Aliongea Christine baada ya kuona bado Edna yupo kwenye mshangao.

“Aunt you are terrific…..”Aliongea Lanlan na kumfanya Edna kuangalia mbele na hapo ndipo alipoweza kumuona Lanlan akiwa ameshikilia kichwa cha Salah huku akionyesha kuridhishwa sana na kitendo cha Christine kuwafyeka watu hao, yaani alionyesha hali ya furaha mno na kwa jinsi alivyoonekana ni kama haikuwa mara yake ya kwanza kuona mtu akitenganishwa kichwa.

END OF SEASON 10.
SEASON 11 ITAENDELEA JUMAMOSI- KWA KUNISAPOTI WASILIANA NAMI KUPITIA 0687151346 ONLY WATSAPP.
 
Ubarikiwe kwa hii kazi master
 
Mpaka hapa kwakweli unahitaji support yangu. This is fantastic!
 
Ohooooo
 
Roma anatakiwa ammalize mapema kibaraka wa Athena prof. Bwan maana amedhamiria kwa kila namna kumuangamiza asisahau kumuwekea ulinzi Mama yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…