Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEHEMU YA 299.

Baada ya Fayezi kutoka ndani ya chumba cha Mke wake Mtarajiwa Amina , alitoka kabisa ndani ya hoteli hio akiwa ametangulizana na wanajeshi wawili kutoka kikosi maalumu ambao wote wamekodiwa na familia yake kwa ajili ya kumpa ulinzi, wote wakiwa wamevalia suti.

Dakika chache mbele walikuja kusimamisha magari yao mawili upande wa pili ndani ya jiji hili la Otaru ,sehemu maarufu sana iliokuwa ikisifika kwa kuwa na huduma ya masaji iliokuwa ya kiwango cha juu sana.

Fayezi alitaka kuweka mwili wake sawa kabla ya siku yake kubwa ya kesho na ndio maana alikuwa ndani ya eneo hilo kwa ajili ya kufanyiwa masaji, Alikutana na mwanaume mwingine wa kijapani ambaye alikuwa ni wa umri wa kati alievalia suti na alimuongoza kwa heshima kubwa na kwa Pamoja waliingia kwenye jengo ambalo lilikuwa na bango linalowaka taa na maandishi makubwa rangi nyekundu yaliosomoeka kwa juu ‘Clubhouse’.

Wote wawili Pamoja na bwana ambaye alimpokea walionekana wakiwa ndani ya chumba cha masaji huku wakiwa wamezungukwa na wanawake warembo sana waliovalia nusu uchi wakishikwa kwa mikono laini sana wakifanyiwa masaji , kitendo amacho kiliwafanya kujihisi kama vile wapo dunia nyingine kabisa.

Dakika takribani ishirini walikuwa wakiminywa minywa kwanzia makalioni mpaka kwenye shingo , Fayezi licha ya kutozoea huduma hio , lakini alionekana kuifurahia mno.

Wakati wakiendelea kufanyiwa masaji simu ndani ya chumba hiko ilianza kuita mfululizo ikiashria kuna dharula na mhuduu aliekuwa karibu aliichukua na kisha kuipokea baada ya kuona inatokea mapokezi.

“Sir kuna kundi la watu limeingia ndani pasipo ruhusa kutoka mapokezi na wanasema wanawatafuta”Aliongea yule mwanamke na kumfanya bwana yule wa kijapani kumwangalia kwani mhudmu aliongea kwa kijapani .

“Amesema wametokea wapi?”

“Wamesema ni kutoka kundi la Yamata Sect”Aliongea yule muhudumu na kumfanya Fayezi aliekuwa akiendelea kuburudika kuinua kichwa.

“Kama ni Yamata haija haja ya kuwahofia , nina ushirkiano nao katika maswala ya kibiashara hivyo hawana madhara kwetu kwani kila kitu kinaenda sawa”Aliongea Feyezi kwa kingeteza , lakini mara baada ya kumaliza Sentensi yake , kundi la wajapani waliovalia suti wakiwa mchanganyiko wa wanawake na wanaume waliingia ndani ya chumba hiko cha masaji huku nyuso zao zikiwa katika hali ya usiriasi mno.

Fayezi aliwaangalia watu hao na kuona hakuwa akiwatambua hata mmoja , lakini hakujali , alichokuwa akiamini ni kwamba watu hao walikuwa ni moja ya vijana wa Noriko Okawa.

“Wewe ndio unafahamika kwa jina la Fayezi kutoka kampuni ya Emaar Dubai?”Aliuliza kwa Kingereza mwanaume mmoja wa kijapani ambaye sura yote imajaa ndevu huku akiwa na sura ya kutisha.

“Ndio ni mimi , mnashida gani na mimi , kwani kila kitu nilishamalizana na boss wenu?”

“Tumepata taarifa kwamba unafanya biashara ya madawa ya kulevya ndani ya eneo letu jambo ambalo ni kinyume na makubaliano yetu ya kibiashara”

“Madawa ya kulevya!! , hapani sio kweli , boss wenu atakuwa amekosea”

“Hajakosea na ndio alietupatia maelekezo ya kuja hapa, utatoa ushirikiano wako na tutakusachi kama hauna madawa ya kulevya tutakuacha na kuendelea na mambo yako”Aliongea yule bwana ambaye alionekana kuwa ndio kiongozi wa kundi la Yamata Sect.

Lakini hata hivyo Fayezi aligoma kusachiwa na sharti lake lilikuwa ni kuongea kwanza naNoriko Okawa ambaye alikuwa akimjua kama mkuu wa kundi la Yamata na vijana wale hawakuwa na shida , simu ilipigwa kwa boss mwenyewe

“Mr Fayezi wape vijana wangu ushirikiano , tumepewa taarifa unafanya biashara ya heroin ndani ya mji wetu wa kibiashara”Ilisikika suati ya mwanamke upande wa pili na kumfanya Fayezi kutabasamu kifedhuli.

“Nataka kuongea na boss wako”

“Kwanzia leo mimi ndio boss wa Yamata Sect, kama unamuulizia Noriko Okawa basi fahamu kwamba hayupo tena hai”ilisikika sauti na kumfanya Fayezi kushangaa mno ni kama hakuwa akiamini.

“Noriko Okawa hawezi kufa haraka hivyo ,mchana wa leo niliwasiliana nae na hata hivyo mimi sifanyi biashara yoyote ya madawa ya kulevya mmekosea mtu mnaemtafuta”Aliongea Fayezi kwa namna ya kujitetea , lakini watu kumi kutoka kundi la Yamata Sect walionekana kuwa siriasi mno na walikuwa wakitaka tu kusikia amri ya boss wao wachukue hatua.

“Kama unajiamini hauna madawa ya kulevya , basi haina haja ya kuewaletea matatizo vijana wangu unachotakiwa kufanya ni kuwaruhusu kufanya kazi yao , kama alietoa taarifa kakosea basi adhabu itakuwa juu yake”Aliongea Mwanamke aliekuwa kwenye simu na mjapani aliekuwa ni msaidizi wa karibu wa Fayezi alimpa ishara ya kukubaliana na watu hao kumsachi.

“Okey mnaweza kusachi , sina haja ya kuogopa kusachiwa kwasababu najiamini sina madawa ya kulevya ya aina yoyote ile”Aliongea Fayezi na wale vijana wakiongozwa na kiongozi wao aliekuwa akifahami kwa jina la iboru , walianza kufanya ukaguzi wao ndani ya chumba hiko kwa haraka sana , hawakutaka kuchelewa kwani mteja wao alikuwa akionyesha kujiamini sana kutokuwa na madawa ndani ya chumba hiko , hivyo wlaiamini kufanya haraka ni kuokoa muda.

Walinzi wa Fayezi walitaka kuzuia jaribiio hilo , lakini vijana wa Yamata walionekana kuwa tayari kupambana, Fayezi ilibidi kuwapa ishara watulie na kuruhusu zoezi hilo kufanyika kwa dakika chache kwani alikuwa akiamni hakuwa na madawa ya kulecya na hakuwa hata na mpango wa kufanya biashara hizo haramn ndani ya Japani, yeye alikuwepo hapo ndani ya Japani kwa ajili ya kufunga ndoa na mpezni wake Amina , hivyo swala la madawa lilikuwa limemkalia kushoto.

Maninja wale wa kundi la Yamata Sect walitumia dakika kama tatu tu kusachi kwenye suti za Fayezi na yule mchina na hatimae waliweza kuibuka na vijimfuko vya nailoni vitatu vilivyokuwa na unga mweupe ndani yake , na kwa mtaalamu wa haraka haraka angegundua kuwa hayo ni madawa ya kulevya aina ya Heroin kutokana na rangi yake kuwa kama ya unga wa ngano.

“Hapana hayo madawa sihusiki nayo kabisa , sijawahi kupanga kuuza madawa ndani ya Japani na sio hivyo tu Emaar haijawahi kujihusisha na biashara haramu”Aliongea Fayezi kwa kujitetea huku akiwa kwenye mshangao kuona mfuko wake wa suti ndio uliotolewa paketi tatu za madawa hayo.

“Usitufanye sisi ni wajinga , tunaamini vipi hauhusiki, ushawahi kusikia wapi mtu anaeuza madawa ya kulevya akajitangaza, kila mtu anafanya siri na wewe pia ni mmoja ya watu wanaotunza siri katika biashara hii”

“Sio kweli labda hawa wanaofanya masaji ndio wamehusika kunibambikizia madawa hayo , ila sihusiki nayo kabisa na Mungu wangu ni shahidi”Aliongea Fayezi lakini vijana wale walionekana kutokujali kabisa , walichokifanya ni kupiga simu kwa boss wao.

“Boss tumepata kugundua Fayezi ndio muusika anaeuza madawa ndani ya jiji hili , tunapaswa kuchukua hatua gani baada ya hapa”

“Mkamateni na mleteni kambini tumuhoji vizuri”Sauti ya mwanadada Tanya ilisikika na vijana wale mara baada ya kusikika maelekezo hayo walitoa ishara kwa vijana wao kwa ajili ya kumzingira Fayezi , ili kumkamata na kumpeleka kambini kama walivyopewa maagizo na boss wao.

Fayezi alikuwa ni mwenye hasira mno , mpaka hapo aliamini huo ni mtego umeandaliwa kwa ajili ya kumkamatisha hivyo hakuwa tayari kukamatwa kizembe wakat iyeye ni mtoto wa Tajiri kutoka dubai na alikuwa na koneksheni nyingi.

“Naombeni nifanye mawasiliano”Aliongea Fayezi huku akisogelea suruali yake , lakini maninja wa Yamata Sect waliichukua nguo zake na kutoa simu na kisha wakamrushia nguo zake avae haraka na kwakua Fayezi na mwenzake alikuwa uchi , hawakuleta ubishi walivaa.

“Hatuwezi kukupa simu tena kwani mara ya kwanza ulituambia huna madawa na tukakukutan nayo , unatufanya sisi wajinga na hatuwezi kuruhusu”Aliongea yule jamma mwenye kutisha huku akimwangalia Fayezi aliekuwa akivaa mavazi yake kwa haraka.

Walinzi wa Fayezi walidhibitiwa ndani ya dakika chache tu na wale wahudumu pia na wenyewe walidhbitiwa na kwa Fayezi na msaidizi wake pia walidhibitiwa na wote kwa Pamoja walipoteza fahamu palepale na dakika kadhaa mbele walikuwa wakitolewa nje kabisa ya Clubhouse na kuingizwa kwenye gari aina ya Noah Toyota na palepale gari ile iliondolewa na Kwenda kusimama mita kadhaa mbele sehemu yenye miti ya bustani na mlango wa Gari lile ulifunguliwa kwa mara nyingine na Fayezi Pamoja na msaidizi wake walionekana wakitoka ndani ya gari lile na kuanza kupiga hatua kurudi kule walikotoka wakiwa vile vile na mavazi yao yaleyale.
 
SEHEMU YA 300.

Uwepo wa Lanlan kwenye Maisha ya Edna ni kama ulimbadilisha kwa asilimia mia moja , kwanza kabisa ratiba za Edna zilibadilika hakuwa mtu wa kufanya kazi kwa masaa mengi kama ilivyokuwa mwanzo , Edna alikuwa kila ikifika saa tisa na nusu tayari atakuwa njiani akiwa na zawadi akirudi nyumbani kwa ajili ya kumuona Lanlan.

Hisia za kuwa mama kwake zilimfanya hata baadhi ya mawazo aliokuwa nayo kumpotea kwa asilimia mia moja na sasa kila akichofikiria , Lanlan alikuwa akihusika kwa asilimia kubwa.

Upande wa ndani ya kampuni ya Edna Ernest Komwe alikuwa na urafiki wa karibu sana na Benadetha, mara nyingi wawili hao walionekana kuwa Pamoja sana na jambo kubwa Zaidi ni kwamba Komwe alikuwa kila akifka kazini lazima aingie ndani ya ofisi ya Benadetha na kumsalimia, licha ya wafanyakazi kushangazwa na ukaribu wao na hat baadhi yao kumuuliza Benadetha juu ya uhusiano wao , lakini Benadetha aliishia kukana kwamba hakuwa na mahusiano kabisa na Ernest Komwe, na mahusiano yao yalikuwa ni ya kiikazi Zaidi.

Ni muda wa saa tatu kamili ndani ya familia ya Edna , familia yote ya Roma ilionekana ikiwa eneo la Sebuleni wakiangalia runinga huku Lanlan akiwa amelala kwenye mapaja ya Edna akiwa anakoroma baada ya kula nusu ya chakula chote kilichopikwa.

“Lanlan kabadilika sana”Aliongea Qiang kwa Kingereza na kumfanya Edna kumwangalia.

“Unamaanisha nini kabadilika Qiang?”

“Mara nyingi Lanlan kulala ni mpaka saa saba ya usiku ndio anapitiwa na usingizi , lakini tokea siku hizi alivyofika hapa amekuwa akilala mapema”Aliongea na kumfanya hata Blandina kushangazwa na maneno ya Qiang, mtoto kulala saa saba za usiku ni jambo ambalo halikuwa limezoeleka ndio maana walishangaa.

Edna alimwangalia Lanlan aliekuwa akijikunja kunja kwenye mapaja yake na kujikuta akitabasamu na kumshika mashavu.

“Sister Edna unafanana kabisa na Lanaln kwa kila kitu , mtu asiemjua Lanlan historia yake basi atasema umemzaa kabisa”Aliongea Sophia na kumfanya Edna kutabasamu.

“Vipi maandalizi ya mashindano ya uimbaji?”Aliuliza Edna na Sophia alitabasamu.

“Yanaendelea vizuri sister natamani ingekuwa mchana nijaribu kuimba ili muone uwezo wangu”Aliongea Sophia.

“Kwa sauti yako inaonyesha ni hakika una uwezo mkubwa wa kuimba , kesho asubuhi inabidi tukusikie namna ulivyojaaliwa”Aliongea Blandina na kumfanya Sophia kutingisha kichwa kukubaliana nae.

Wakati Edna akijianda kumbeba Lanlan kupandisha nae juu kwa ajili ya Kwenda kumlaza kitandani kwake , mara vilisikika vishindo nje ya nyumba na kufanya watu wote kuangaliana, Blandina ndio aliekuwa wa kwanza kusoglelea mlango wa nje ili kujua ni kitu gani kimedondonda , Blandina hakuwa na wasiwasi maana kulikuwa na walinzi nje ya nyumba , lakini baada ya kufikia mlango.

“Yesuu…!!!”Alijikuta akitoa ukulele baada ya kushuhudia mtu aliekuwa mbele yake huku akiwa amemnyooshea siraha aina ya bastora na kufanya watu wote kusimama kwa woga kuangalia upande wa mlangoni na hata Lanlan aliekuwa amelala alishituka.

Jumla ya wanaume kumi waliingia ndai ya eneo la sebuleni ,mmoja ambaye alikuwa ni Salah alikuwa ameshikiria bastora huku wengine tisa wakiwa si raia wa Tanzania kwa namna walivyokuwa wakionekana , kuna wawili walionekana kama wajapani na wengine wote wlaiobakia walikuwa ni wachina , wote kwa Pamoja walikuwa wameshikilia mapanga huku wakiwa wamejifunga vitambaa usoni kwa staili flani hivi kama ile wanayopendelea Alshababu.

Edna na wanafamilia wengine walijikuta wakiwa kwenye kiwewe na kilichofanya kuwa katika kiwewe Zaidi ni kwamba watu waliokuwa mbele yao walionekana hawakua na nia nzuri kwao.

“Nyie ni wakina nani na kwanini mevamia kwenye nyumba yetu?”Aliuliza Edna baada ya kuuvaa ujasiri lakini wanaume waliokuwa mbele yao ni kama hawakuwa wakimwelewa kabisa na Edna mwenyewe aliliona hilo na kuona watu hao huenda hawakuwa wakijua lugha ya kiswalihi hivyo alitumia lugha ya kingereza kujaribu kuongea nao , lakini vilevile watu wale walionekana kutolewa kabisa , yaani walikuwa ni kama mizimu hivi.

Salah ambaye alionekana kama ndio kiongoozi alimwangalia Edna kwa madakika kadhaa huku akionekana kama mtu aliekuwa akijiuliza ni wapi amemuona huyo mrembo , lakini licha ya hivyo alionekana kutokumkumbuka vizuri.

Edna yeye alikuwa kwenye mshangao mkubwa sana , kwani Salah alikuwa akimkubuka vyema kufariki kwa kuuliwa na mume wake Roma , sasa alishangaa na kujiuliza kwanini mtu huyo yupo hapo akiwa hai, tena akiwa ameshikilia siraha , mpaka hapo alihisi kabisa kuna jambo baya ambalo linakwenda kutokea , aliamini huenda Salah alikuwa na pacha wake na ni huyo aliekuwa mbele yake na wapo hapo usku huo kwa ajili ya kulipa kisasi.

Saa kabla hawajafanya maamuzi ya kuwashambulia wanafamilia hao , muda uleule Chiara alitaengulizana na John waliingia na walianza kupambana na wanaume wawili waliokuwa nyuma ambao wameshikilia mapanga lakini kilichowakuta kilimfanya hata Edna kufumba macho , kwani wachina wale walikuwa na spidi isio ya kawaida , kwa haraka haraka walionekana kuwa na mafunzo ya Kung Fu , kwani wakati Chiara analetea pigo upande wa kulia kupangua upanga uliokuwa umeshikiliwa kwa mkono wa kulia na mchina , yule bwana alifyatua kwa nguvu upanga wake na kulenga tumbo la Chiara na kilichotokea ni kwamba Panga lile lilipita moja kwa moja na kutokezea upande wa pili mgongoni na Chiara aliishia kutoa macho huku akimwangalia Edna kwa namna ya kama mtu anaomba msamaha kwa kutokumlinda.

Upande wa John yeye baada ya kugundua mwenzake kadungwa na panga la tumbo alijikuta akikosa umakini na kilichosikika ni ‘Shwaa..’ panga lilimkata kwenye kiwikicho cha mkono na kusababisha damu kusambaa eneo lote la hapo ndani.

Sasa mpaka hapo Edna na wanafamilia wengine waliona hawapo eneo salama kabisa , kwani watu waliokuwa wakiwategemea kuwadhibiti wavamizi ndio hivyo tena, John mzungu amekatwa mkono na alikuwa amedondokea pembeni akiugulia maumivu na Chiara keshapoteza Maisha ya kudungwa na panga la tumbo.

Kwa jinsi watu hawa walivyokuwa wakifanya ni kama walikuwa hawana akili vizuri , kwani wote walifanana kiuhaiba, yaani hakukuwa na maongezi Zaidi ya kuangaliana kama maroboti na hata mchina ambaye alimdunga Chiara na panga lake alionekana kutokuwa kwenye hali ya kujutia kabisa kwa kitendo chake , alikuwani kama myama.

“Kill them all”

“Uweni wote”

Ni kama sauti za mwangwi ndio zilizokuwa zikisikika kwenye vichwa vya Wavamizi hao waliokuwa wakiongozwa na Salah aliefufuka , walikuwa wakipokea maagizo ya kuua kila kichokuwa mbele yao na Salaha ndio alieanza kupiga hatua ya kuwasogelea, ukumbuke hapa licha ya kujipanga ndani ya sebule hii kubwa , walikuwa wakiwaangalia wanafamilia hao kama vile hawakuwa na nia ya kuwaua kabisa, yaani walikuwa binadamu lakini kama misukule.

Huku nyuma Sophia , Yezi pamoja na Qiang walikimbilia upande wa jikoni kwa ajli ya kujificha , Bi Wema na Blandina wao walikuwa wamesimama huku presha ikianza kupanda kwa haraka sana na Bi Wema alikuwa akikosa pumzi na palepale alilegea na kabla hajatua chini Blandina alimuwahi na kumzuia asidondokee meza ya kioo.

Edna sasa baada ya kuona tayari yupo kwenye hatari alijikuta akimrudisha Lanlan nyuma kwa staili ya kumkinga ili kama ni kudhurika aanze yeye , kati ya wanawake wale wote yeye pekee ndio aliekuwa amesimama vilevile akionyesha kuwa tayari kukumbana na jambo lolote..

Edna alijikuta akianza kumuwaza Roma , lakini mawazo yake kabla hayajatimia Salah aliinua siraha yake na kisha kumyooshea Edna kwa nia ya kumuua , kitendo kile kilimfanya Edna kuinama na kumkumbatia Lanlan na kumpa mgongo Salah.

“Paah… Paaah!!!”.

Ni mlio wa risasi uliosikika kwenye masikio ya Edna na mpaka hapo aliamini kabisa risasi hizo zimekosa na alijikuta akinyanyua uso wake na kugeuka nyuma huku akitetemeka mno kwa woga na hapo ndipo aliposhuhudia Salah aliwa chini amepigwa risasi za mgongoni na John aliekuwa anaugulia maumivu nyuma.

John baada ya kuona risasi zile zimempata Salah macho yake yalijaa ukungu na pelapela alipoteza fahamu kwani damu ilikuwa zikimtoka kwa kasi sana kiasi kwamba nguvu zilimuishia.

Sasa kitendo cha John kupoteza fahamu kilishuhudiwa na Edna na kumfanya kukata tamaa Zaidi na kutamani muujiza utokee,kwa jinsi mrindimo wa risasi ulivyosikika aliamini kabisa watu wan je wangesikia , kwani eneo alilokuwa akiishi lina ulinzi mkali kutokana na kupakana na viongozi wa jeshi lakini pia wanasiasa wakubwa , lakini aliamini kwa watu ambao wako mbele yake , wanaoonekana kama misukule , mpaka msaada ukiwafikia basi watakuwa wote wamepoteza Maisha.

“Edna kimbilia jikoni na Lanlan “Aliongea Blandina kwa kutahadharisha huku akimpita Edna na kusimama kwa mbele.

Sasa jambo la kushangaza hapa ni kwamba licha ya matukio hayo yote ya kufa mtu kupigwa risasi na kuchomwa kwa Chiara panga la tumbo , upande wa Lanlan hakuwa na wasiwasi kama ilivyokuwa kwa wanafamilia wengine , mtoto huyu ni kama mwili wake ulikuwa umechomwa na sindano ya madawa ambayo yanaufanya mwli wake kusisimka.

“Grandmaa..!!!!, Mamaaaaa nyuma yako …!!!”

“Tuuh!!!!”

Unajua hawa wachina ni kama walikuwa wakitegeeana kufanya mashambulizo kwani walikuwa wakiacha mmoja afanye shambulizi na wao kufatia yaani walikuwa ni kama wanategeana hivi, hawakuwa kama majambazi kwamba waongee au kutahadharisha na hata kwa Edna aligundua watu hao hawakuja hapo ndani kupora bali ni kuua pekee.

Ssasa mjapani aliekuwa mita kadhaa nyuma alimsogelea Blandina kwa kasi kubwa huku akidhamirira kumfekya , lakini sasa kabla hata hajamfikia , alijjikuta akirushwa kwa nguvu isiokuwa ya kawaida na Kwenda kutua kwenye Gympsum mpaka ikapausika , kwani nguvu iliomrusha juu haikuwa ya kawaida na kitendo hiki ni mara baada ya Lanlan kuita kwa nguvu jina la Bibi yake.

Edna aliekuwa hajaelewa kilichotokea alijikuta akigeuka na kumwangalia Lanlan na hapo ndipo aliposhuhudia kitu kichokuwa cha kawaida, kwani macho ya Lanlani yalikuwa ni kama Kioo, yaani kile kiini cheusi hakikuwa kikionekana na sasa ni kiini cheupe tu ndio kilikuwa kwenye macho ya Lanlan.

Sasa wale wachina wenyewe walijikuta wakiwa katika mshangao na macho yao yote waliyaelekeza kwa ,mtoto mdogo Lanlan.

“Mpo hatarini shambulia mtoto”

Sauti kama mwangwi ilisikika katika vichwa vyao na kuwafanya wakuje vichwa vyao kwa kujizungusha na kisha palepale mmoja ya mchina aliekuwa upande wa kushotoa alifyatuka kumsogelea Edna na Blandina , lakini kabla hajawakaribia Lanlan aliekuwa amesimama aligeuka kama Mpira na Kwenda kumpiga kikumbo yule mchina na kilichotokea ni kwamba mchina yule alirushwa nyuma kwani nguvu iliomgonga haikuwa ya kawaida.

“Atakeye mgusa mama yake Lanlan na bibi yake nitamuua…”Aliongea Lanlan kwa namna ya kuwa siriasi kabisa huku macho yake yakiwa vilevile pasipo ya kubadilika na kumfanya Blandina na Edna kujawa na hofu mno.

“Mshambilieni wote kwa Pamoja , mapanga tanguliza mbele”

Sauti pia ilianza kusikika kwenye vichwa cha watu tisa sasa na palepale walisogeleana karibu na kunyoosha mapanga yao mbele kwa ajili ya kumshambulia mtoto mdogo Lanlan.

Mpaka hapo akili zao ni kwamba zilikuwa zinahisi hatari , hivyo walikuwa kwenye mfumo wa kujiokoa na pia akili zao zilikuwa zikiwapa maelekezo ya kwamba mtoto aliekuwa mbele yao alikuwa ni hatari kwao.

Salah ambaye alikuwa amepigwa risasi na kudondoka mita kadhaa kutoka aliposimama Edna alisimama tena kama vile mtu abaye dakika moja iliopita hakuwa amepigwa risasi na baada ya kusimama kitu cha kwanza alichotafuta ni siraha yake iliodondokea pembeni , aliisogelea na kisha akaichukua.

“Lanlan…” Edna na Blandina walijikuta wakitamka kwa Pamoja na kumsogelea Lanlan na kumkinga baada ya Salah kumyooshea bastora.

‘”Arrggh …!!!!”

Ni damu ya moto iliowarukia Edna na Blandina huku wakisikia miguno ya maumivu kutoka kwa wavamizi hao na walijikuta kwa pamoja wakigeuka na kuangalia ni nini kinaendelea, na hapo ndipo walipoweza kuwa katika mshangao , kwani ni kivuli pekee ndio walichoweza kuona kikiadhibru wale wachina na wajapani kwa dakika chache mno na mtu ambaye alikuwa akiwaadhibu hakuwa na huruma kabisa kwani alikuwa akitenganisha shingo moja kwa moja.

Dakika moja tu tayari majambazi yote kumi yalikuwa hayana vichwa , kwani vilishatenganishwa kwa upanga.

“Persephone… !!, naitwa Christine ni rafiki wa karibu na Hades”.

Sasa Edna alikuwa kwenye mshangao mno , kwanza kabisa mtu aliekuwa mbele yake alikuwa akimfahamu kama moja ya waigizaji na waimbaji maarufu sana , kitu cha pili Edna kilichomfanya kushangaa ni kwamba mwanamke huyo mrembo wa kutisha , alikuwa pia na uwezo wa kimapigano ambao hakuwahi kuhisi kwenye Maisha yake atakuwa nao , kwani siku zote alimuona mwanamke huyo kama mwimbaji mlaini sana ambaye alikuwa akipewa ulinzi , sasa kitendo ambacho kilitokea hapo ndani cha vichwa vya wajapani Pamoja na wachina kutenganishwa , kilimfanya Edna kumwangalia Christine Stewart mwimhaji kutoka Marekani kwa maswali mengi , juu ya yote ni jina la yeye kuitwa Persephone na mzungu huyo licha ya kutokuwa mara ya kwanza kulisikia , lakini pia urafikiwa Christine na Hades , jina hilo pia lilikuwa geni kwake.

“Upo kwenye mshangao kwa namna nilivyowafyeka hawa binadamu wapuuzi waio na nafsi, kwa majina mengine pia nafahamika kama Aphrodite nitakuwa na huzuni kama Hades hajakutajia jina langu ilihali ndio kanikaribisha Tanzania.. hata kumsaidia kulinda familia yake.”Aliongea Christine baada ya kuona bado Edna yupo kwenye mshangao.

“Aunt you are terrific…..”Aliongea Lanlan na kumfanya Edna kuangalia mbele na hapo ndipo alipoweza kumuona Lanlan akiwa ameshikilia kichwa cha Salah huku akionyesha kuridhishwa sana na kitendo cha Christine kuwafyeka watu hao, yaani alionyesha hali ya furaha mno na kwa jinsi alivyoonekana ni kama haikuwa mara yake ya kwanza kuona mtu akitenganishwa kichwa.

END OF SEASON 10.
SEASON 11 ITAENDELEA JUMAMOSI- KWA KUNISAPOTI WASILIANA NAMI KUPITIA 0687151346 ONLY WATSAPP.
 
SEHEMU YA 297

Dakika kama tano hivi zilipita tokea Salah kuondoka , Ytan buwen aliekuwa ndani ya chumba ambacho alikuwa amelazwa Salah akimfanyia matibabu , alisogelea na kushika kijichupa ambacho ndani yake kilikuwa na kimiminika cha rangi nyeusi na kukiangalia kwa namna ya kama mtu ambaye alikuwa akishangaa.

Jambo moja ambalo lilikuwa likipita katika kichwa cha Yan Buwen ni juu ya kimiminika hiko , ukweli ni kwamba hakuwa na elimu yoyote iliopo nyuma ya kimiminika hicho kutokana na kwamba yeye alikabidhiwa tu na Athena ,sasa tokea siku ambayo amekabidhiwa kimiminika hiko alikuwa akijaribu kutafuta sayansi iliopo ndani ya kimiminika hiko , lakini alishindwa kabisa kujua kanuni yake na ndio maana muda huo alikuwa akikishangaa na kujiuliza maswali mengi kwa wakati mmoja.

Salah kwake ilikuwa ni maiti ya kumi kuirudishia uhai wake tokea siku ambayo alipewa kimiminika hiko na Athena kwa ajili ya kukifanyia majaribio na kugundua kanuni yake.

Yan Buwen aliangalia kichupa hiko kwa dakika kama tano hivi akikigeuza kulia na kushoto na baada ya kuridhika kwa kiasi Fulani alikirudisha kwenye kikabatii kilichokuwa ndani ya wodi hio.

Yan Buwen mara baada ya kukiweka alitoa tena kishikwambi ambacho hakikujulikana ni cha kampuni gani na baada ya kushikilia kile kishikwambi na kukiwahsa alienda moja kwa moja mpaka sehemu iliokuwa na ‘icon’ ilioambatana na jina la NLC2P(Neural Link Chip Control Pad).

Baada ya kufungua ‘App’ hio moja kwa moja ilikonekti na satilaiti na palepale ilionekana ramani ya jiji la Dar es salaam lote juu kukiwa na kidoti cha rangi nyekundu , kidoti hiko kikionyesha kilikuwa kikisogea kwa kasi sana ndani ya barabara ya Bagamoyo Road kama ilivyokuwa ikionyesha kwenye Ramani.

Yan Buwen alijikuta akitabasamu kifedhuli mara baada ya kuona kidotii kile kilikuwa kwenye kasi sana na mpaka hapo aliamini Salah atakuwa kwenye gari.

Unachotakiwa kuelewa ni kwamba Yan Buwen licha ya kwamba alikuwa ameuamsha mwili wa Salah , lakini jambo moja tu ambalo kimiminika kile kilishindwa kufanya kazi ni kurudisha nafsi yote ya mtu aliekufa , Sasa Yan Buwen kabla hajamdunga mtu na kimiminika, kitu cha kwanza anachokifanya ni kuingiza ‘Neural Link Chip’ katika ubongo.

Chip ambayo anamuwekea mtu mara nyingi haina kumbukumbu za iana yoyote ile , yaani kwa maneno marahisi ni kwamba Salah hakuwa Salah kama alivyokuwa awali kabla ya kifo chake , bali Salah ni mtu mwenye kumbukumbu zingine kabisa ambazo alikuwa akizipata kupitia Chip iliowekwa kwenye ubongo, sasa mafaili ambayo yamewekwa kwenye ubongo ndio yanayomuongoza katika ufanyaji wa matendo yake pamoja na kufikiria.

“Ameamka na sasa yupo njiani kwenye gari na nadhani anakuja nyumbani”Aliongea Yan Buwen kwa kingereza mara baada ya kupiga namba ya simu ambayo mpaka muda huo haikuwa ikieleweka alikuwa akiongea na nani.

“Tunatakiwa kufanya nini mara baada ya kufika?”

“Mnatakiwa kumuacha na kumuona wa kawaida tu , nimejitahidi kuingiza baadhi ya taarifa zinazomuhusu lakini zoezi halikukamilika kwa asilimia mia moja , naweza kusema nimesevu asilimia hamsini ya taarifa zake alipokuwa hai , teknolojia hii bado ipo katika maboresho”Aliongea Yan buwen kwa namna ya upole.

“Okey nitawasiliana na mtu wa nyumbani na kuwapa tahadhari” Sauti ilisikika na palepale simu ilikatwa.

******

Upande mwingine ndani ya familia Mzee Maya ni kama hakuna kitu ambacho kimetokea kama baadhi ya watu walivyokuwa wakifahamu, ni kweli kwamba siku kadhaa nyuma watu walishuhudia kifo cha Salah , lakini jambo la kushangaza ni kwamba ndani ya familia hii yenye makazi yake ndani ya eneo la Mbweni , hakukuwa na aina yoyote ya kuashiria kuna msiba.

Hata Mage na Magdalana ambao walikuwa ni watu walioshihudia kifo cha Salah walionekana kuwa kwenye mshangao na kutoelewa ni kipi kinaendelea , ni kweli kwamba Mgadalena au Ajenti Flamingo alipokea maagizo kutoka kwa Afande Maeda kuhakikisha swala la kifo cha Salah hakimletei shida Roma , lakini jambo la kushangaza ni kwamba kesi ya Salah ilifutwa polisi na mwanasheria wa familia ya Mzee Maya Huberi na kuwafanya warembo hao kutoelewa kinachoendelea , lakini kwasababu jambo hilo lilikuwa heri kwao basi waliona watulie kimya , lakini licha ya hivyo kuna jambo ambalo lilikuwa likiwatekenya mno , yaani walitaka kujua nini kinachoendelea , mapacha hao wote ni wanausalama , hivyo walitaka angalau kujua ni sababu gani kwa familia ya Mzee Maya kufuta kesi ya kuuliwa kwa mtoto wao ndani ya polisi.

Upelelezi wa warembo hao wawili uliwafikisha ndani ya nyumba ambayo inaaminika ndio makazi ya mke wa Tajiri Maya Hubert kwa hapa Tanzania , ili kuangalia ni nini kinaendelea , lakini baada ya kuuliza baadhi ya majirani nje ya geti la jumba hilo ni kwamba, jambo la kushangaza hakuna ambaye alikuwa amesikia kama kuna msiba , yaani hakuna jirahi yoyote ambaye alikuwa akielewa kinachoendelea ndani ya familia hio , jambo ambalo liliwafanya maswali kuibuka katika vichwa vyao.

Wakati wakiwa ndani ya gari , Mage akiwa na Magdalena , mara simu ya Ajenti Flamingo ilitoa mwashirio kwamba inaita na kwa haraka sana Magdalena aliitoa kwenye surauali yake ya jeans na kuangalia ni mtu gani ambaye anampigia na alijikuta akijiweka sawa mara baada ya kugundua ni mkuu wake wa kazi , yaani afande Maeda.

“Jambo Afande”

“Jambo Afande! ,Ajenti Flamingo nadhani mpaka sasa unafahamu kesi ya Salah familia imeamua kuifuta , hivyo nakupigia simu hii kukupa maelekezo mengine uache kufatilia kabisa juu ya kesi hio na swala ambalo limetokea lisifahamike tena, nishawalisiana na makao ya polisi na jarada la Salah lishafungwa”

“Afande kwan…?””

“AJenti Flamingo taarifa ni hio , na kwanzia sasa endelea na kazi yako ya kuwa karibu na Hades na kuhakikisha jambo la namna hio halitokei tena , ili kupunguza maswala yasio na majibu”Na palepale simu ilikatwa na kumfanya Magdalena kumwangalia pacha wake Mage.

“Kuna nini Magdalena?”

“Nimepewa oda ya kuacha kufuatilia chochote kinachomuhusu Salah , na jambo hilo liwe kama halijatokea , hayo ndio maagizo yetu na hapa tunapaswa kuondoka”Aliongea Magdalena kwa wasiwasi na kumfanya Mage kushangaa.

“Mbona sielewi, kuna nini kinaendelea?”

“Mage tunapaswa kushukutu pia kwani tumeondolewa mzigo , najua jambo hili linamaswali mengi ila inabidi tutii tulichoambiwa”Aliongea na Magdalena hakusubilia jibu la pacha wake na palepale aliendesha gari kuelekea barabara kuu wakitoka eneo la Mbweni.

“Magdalena angalia kushoto”Aliongea Mage kabla ya Magdalena kukata kushoto karibu na kituo cha kuwekea mafuta cha Lake Oil wakati akitaka kuingia barabara kuu na Magdalena ile anaangalia kushoto alijikuta na yeye akitumbua macho ni kama wote wameona mzimu.

“Salah!!!!”Magdalena alijikuta akikanyaga breki mara baada ya kumuona mwanaume ambaye walikuwa wakimtambua , mwanaume ambaye walikuwa wakijua amekufa kwa kuuliwa na Roma , Mage alijikuta akipagawa na kufungua mlango haraka haraka na kukimbilia nyuma kumuwahi mtu ambaye aliamini ni Salah na kwa upande wa Magdalena hivyo hivyo alikimbilia nyuma kumuwahi dada yake.

“Salah!!!!”Aliita Mage kwa nguvu mara baada ya kumkaribia mwanaume ambaye anaamini ni Salah na pelapele mwanaume yule alievalia suti alisimama na kisha akageuka nyuma na kumwangalia Mage na wote kwa Pamoja wlaijikuta wakirudi hatua mbili nyuma kwa kujikokota huku wakiwa hawaamini macho yao.

Salah alimwangalia Mage na Magdalena kama mtu ambaye alikuwa akijaribu kuwakumbuka , lakini aliishia kutowatambua watu wa mbele yake , lakini pia hakuongea neno lolote Zaidi ya kugeuka na kuendelea na safari yake na kuwafanya Mage na Magdalena kuangaliana.

“Labda watakuwa mapacha”Aliongea Mage na Magdalena na yeye aliunga hoja , walikuwa wakiamini Salah amekwisha kufa hivyo hakuna uwezekano wa Salah kuwa hai na hivyo waliemuona alikuwa ni pacha wake Salah , walikubaliana kutokana na wao pia kuwa mapacha wanaofanana hivyo hoja ya kuona ina mashiko.
Ubarikiwe kwa hii kazi master
 
SEHEMU YA 300.

Uwepo wa Lanlan kwenye Maisha ya Edna ni kama ulimbadilisha kwa asilimia mia moja , kwanza kabisa ratiba za Edna zilibadilika hakuwa mtu wa kufanya kazi kwa masaa mengi kama ilivyokuwa mwanzo , Edna alikuwa kila ikifika saa tisa na nusu tayari atakuwa njiani akiwa na zawadi akirudi nyumbani kwa ajili ya kumuona Lanlan.

Hisia za kuwa mama kwake zilimfanya hata baadhi ya mawazo aliokuwa nayo kumpotea kwa asilimia mia moja na sasa kila akichofikiria , Lanlan alikuwa akihusika kwa asilimia kubwa.

Upande wa ndani ya kampuni ya Edna Ernest Komwe alikuwa na urafiki wa karibu sana na Benadetha, mara nyingi wawili hao walionekana kuwa Pamoja sana na jambo kubwa Zaidi ni kwamba Komwe alikuwa kila akifka kazini lazima aingie ndani ya ofisi ya Benadetha na kumsalimia, licha ya wafanyakazi kushangazwa na ukaribu wao na hat baadhi yao kumuuliza Benadetha juu ya uhusiano wao , lakini Benadetha aliishia kukana kwamba hakuwa na mahusiano kabisa na Ernest Komwe, na mahusiano yao yalikuwa ni ya kiikazi Zaidi.

Ni muda wa saa tatu kamili ndani ya familia ya Edna , familia yote ya Roma ilionekana ikiwa eneo la Sebuleni wakiangalia runinga huku Lanlan akiwa amelala kwenye mapaja ya Edna akiwa anakoroma baada ya kula nusu ya chakula chote kilichopikwa.

“Lanlan kabadilika sana”Aliongea Qiang kwa Kingereza na kumfanya Edna kumwangalia.

“Unamaanisha nini kabadilika Qiang?”

“Mara nyingi Lanlan kulala ni mpaka saa saba ya usiku ndio anapitiwa na usingizi , lakini tokea siku hizi alivyofika hapa amekuwa akilala mapema”Aliongea na kumfanya hata Blandina kushangazwa na maneno ya Qiang, mtoto kulala saa saba za usiku ni jambo ambalo halikuwa limezoeleka ndio maana walishangaa.

Edna alimwangalia Lanlan aliekuwa akijikunja kunja kwenye mapaja yake na kujikuta akitabasamu na kumshika mashavu.

“Sister Edna unafanana kabisa na Lanaln kwa kila kitu , mtu asiemjua Lanlan historia yake basi atasema umemzaa kabisa”Aliongea Sophia na kumfanya Edna kutabasamu.

“Vipi maandalizi ya mashindano ya uimbaji?”Aliuliza Edna na Sophia alitabasamu.

“Yanaendelea vizuri sister natamani ingekuwa mchana nijaribu kuimba ili muone uwezo wangu”Aliongea Sophia.

“Kwa sauti yako inaonyesha ni hakika una uwezo mkubwa wa kuimba , kesho asubuhi inabidi tukusikie namna ulivyojaaliwa”Aliongea Blandina na kumfanya Sophia kutingisha kichwa kukubaliana nae.

Wakati Edna akijianda kumbeba Lanlan kupandisha nae juu kwa ajili ya Kwenda kumlaza kitandani kwake , mara vilisikika vishindo nje ya nyumba na kufanya watu wote kuangaliana, Blandina ndio aliekuwa wa kwanza kusoglelea mlango wa nje ili kujua ni kitu gani kimedondonda , Blandina hakuwa na wasiwasi maana kulikuwa na walinzi nje ya nyumba , lakini baada ya kufikia mlango.

“Yesuu…!!!”Alijikuta akitoa ukulele baada ya kushuhudia mtu aliekuwa mbele yake huku akiwa amemnyooshea siraha aina ya bastora na kufanya watu wote kusimama kwa woga kuangalia upande wa mlangoni na hata Lanlan aliekuwa amelala alishituka.

Jumla ya wanaume kumi waliingia ndai ya eneo la sebuleni ,mmoja ambaye alikuwa ni Salah alikuwa ameshikiria bastora huku wengine tisa wakiwa si raia wa Tanzania kwa namna walivyokuwa wakionekana , kuna wawili walionekana kama wajapani na wengine wote wlaiobakia walikuwa ni wachina , wote kwa Pamoja walikuwa wameshikilia mapanga huku wakiwa wamejifunga vitambaa usoni kwa staili flani hivi kama ile wanayopendelea Alshababu.

Edna na wanafamilia wengine walijikuta wakiwa kwenye kiwewe na kilichofanya kuwa katika kiwewe Zaidi ni kwamba watu waliokuwa mbele yao walionekana hawakua na nia nzuri kwao.

“Nyie ni wakina nani na kwanini mevamia kwenye nyumba yetu?”Aliuliza Edna baada ya kuuvaa ujasiri lakini wanaume waliokuwa mbele yao ni kama hawakuwa wakimwelewa kabisa na Edna mwenyewe aliliona hilo na kuona watu hao huenda hawakuwa wakijua lugha ya kiswalihi hivyo alitumia lugha ya kingereza kujaribu kuongea nao , lakini vilevile watu wale walionekana kutolewa kabisa , yaani walikuwa ni kama mizimu hivi.

Salah ambaye alionekana kama ndio kiongoozi alimwangalia Edna kwa madakika kadhaa huku akionekana kama mtu aliekuwa akijiuliza ni wapi amemuona huyo mrembo , lakini licha ya hivyo alionekana kutokumkumbuka vizuri.

Edna yeye alikuwa kwenye mshangao mkubwa sana , kwani Salah alikuwa akimkubuka vyema kufariki kwa kuuliwa na mume wake Roma , sasa alishangaa na kujiuliza kwanini mtu huyo yupo hapo akiwa hai, tena akiwa ameshikilia siraha , mpaka hapo alihisi kabisa kuna jambo baya ambalo linakwenda kutokea , aliamini huenda Salah alikuwa na pacha wake na ni huyo aliekuwa mbele yake na wapo hapo usku huo kwa ajili ya kulipa kisasi.

Saa kabla hawajafanya maamuzi ya kuwashambulia wanafamilia hao , muda uleule Chiara alitaengulizana na John waliingia na walianza kupambana na wanaume wawili waliokuwa nyuma ambao wameshikilia mapanga lakini kilichowakuta kilimfanya hata Edna kufumba macho , kwani wachina wale walikuwa na spidi isio ya kawaida , kwa haraka haraka walionekana kuwa na mafunzo ya Kung Fu , kwani wakati Chiara analetea pigo upande wa kulia kupangua upanga uliokuwa umeshikiliwa kwa mkono wa kulia na mchina , yule bwana alifyatua kwa nguvu upanga wake na kulenga tumbo la Chiara na kilichotokea ni kwamba Panga lile lilipita moja kwa moja na kutokezea upande wa pili mgongoni na Chiara aliishia kutoa macho huku akimwangalia Edna kwa namna ya kama mtu anaomba msamaha kwa kutokumlinda.

Upande wa John yeye baada ya kugundua mwenzake kadungwa na panga la tumbo alijikuta akikosa umakini na kilichosikika ni ‘Shwaa..’ panga lilimkata kwenye kiwikicho cha mkono na kusababisha damu kusambaa eneo lote la hapo ndani.

Sasa mpaka hapo Edna na wanafamilia wengine waliona hawapo eneo salama kabisa , kwani watu waliokuwa wakiwategemea kuwadhibiti wavamizi ndio hivyo tena, John mzungu amekatwa mkono na alikuwa amedondokea pembeni akiugulia maumivu na Chiara keshapoteza Maisha ya kudungwa na panga la tumbo.

Kwa jinsi watu hawa walivyokuwa wakifanya ni kama walikuwa hawana akili vizuri , kwani wote walifanana kiuhaiba, yaani hakukuwa na maongezi Zaidi ya kuangaliana kama maroboti na hata mchina ambaye alimdunga Chiara na panga lake alionekana kutokuwa kwenye hali ya kujutia kabisa kwa kitendo chake , alikuwani kama myama.

“Kill them all”

“Uweni wote”

Ni kama sauti za mwangwi ndio zilizokuwa zikisikika kwenye vichwa vya Wavamizi hao waliokuwa wakiongozwa na Salah aliefufuka , walikuwa wakipokea maagizo ya kuua kila kichokuwa mbele yao na Salaha ndio alieanza kupiga hatua ya kuwasogelea, ukumbuke hapa licha ya kujipanga ndani ya sebule hii kubwa , walikuwa wakiwaangalia wanafamilia hao kama vile hawakuwa na nia ya kuwaua kabisa, yaani walikuwa binadamu lakini kama misukule.

Huku nyuma Sophia , Yezi pamoja na Qiang walikimbilia upande wa jikoni kwa ajli ya kujificha , Bi Wema na Blandina wao walikuwa wamesimama huku presha ikianza kupanda kwa haraka sana na Bi Wema alikuwa akikosa pumzi na palepale alilegea na kabla hajatua chini Blandina alimuwahi na kumzuia asidondokee meza ya kioo.

Edna sasa baada ya kuona tayari yupo kwenye hatari alijikuta akimrudisha Lanlan nyuma kwa staili ya kumkinga ili kama ni kudhurika aanze yeye , kati ya wanawake wale wote yeye pekee ndio aliekuwa amesimama vilevile akionyesha kuwa tayari kukumbana na jambo lolote..

Edna alijikuta akianza kumuwaza Roma , lakini mawazo yake kabla hayajatimia Salah aliinua siraha yake na kisha kumyooshea Edna kwa nia ya kumuua , kitendo kile kilimfanya Edna kuinama na kumkumbatia Lanlan na kumpa mgongo Salah.

“Paah… Paaah!!!”.

Ni mlio wa risasi uliosikika kwenye masikio ya Edna na mpaka hapo aliamini kabisa risasi hizo zimekosa na alijikuta akinyanyua uso wake na kugeuka nyuma huku akitetemeka mno kwa woga na hapo ndipo aliposhuhudia Salah aliwa chini amepigwa risasi za mgongoni na John aliekuwa anaugulia maumivu nyuma.

John baada ya kuona risasi zile zimempata Salah macho yake yalijaa ukungu na pelapela alipoteza fahamu kwani damu ilikuwa zikimtoka kwa kasi sana kiasi kwamba nguvu zilimuishia.

Sasa kitendo cha John kupoteza fahamu kilishuhudiwa na Edna na kumfanya kukata tamaa Zaidi na kutamani muujiza utokee,kwa jinsi mrindimo wa risasi ulivyosikika aliamini kabisa watu wan je wangesikia , kwani eneo alilokuwa akiishi lina ulinzi mkali kutokana na kupakana na viongozi wa jeshi lakini pia wanasiasa wakubwa , lakini aliamini kwa watu ambao wako mbele yake , wanaoonekana kama misukule , mpaka msaada ukiwafikia basi watakuwa wote wamepoteza Maisha.

“Edna kimbilia jikoni na Lanlan “Aliongea Blandina kwa kutahadharisha huku akimpita Edna na kusimama kwa mbele.

Sasa jambo la kushangaza hapa ni kwamba licha ya matukio hayo yote ya kufa mtu kupigwa risasi na kuchomwa kwa Chiara panga la tumbo , upande wa Lanlan hakuwa na wasiwasi kama ilivyokuwa kwa wanafamilia wengine , mtoto huyu ni kama mwili wake ulikuwa umechomwa na sindano ya madawa ambayo yanaufanya mwli wake kusisimka.

“Grandmaa..!!!!, Mamaaaaa nyuma yako …!!!”

“Tuuh!!!!”

Unajua hawa wachina ni kama walikuwa wakitegeeana kufanya mashambulizo kwani walikuwa wakiacha mmoja afanye shambulizi na wao kufatia yaani walikuwa ni kama wanategeana hivi, hawakuwa kama majambazi kwamba waongee au kutahadharisha na hata kwa Edna aligundua watu hao hawakuja hapo ndani kupora bali ni kuua pekee.

Ssasa mjapani aliekuwa mita kadhaa nyuma alimsogelea Blandina kwa kasi kubwa huku akidhamirira kumfekya , lakini sasa kabla hata hajamfikia , alijjikuta akirushwa kwa nguvu isiokuwa ya kawaida na Kwenda kutua kwenye Gympsum mpaka ikapausika , kwani nguvu iliomrusha juu haikuwa ya kawaida na kitendo hiki ni mara baada ya Lanlan kuita kwa nguvu jina la Bibi yake.

Edna aliekuwa hajaelewa kilichotokea alijikuta akigeuka na kumwangalia Lanlan na hapo ndipo aliposhuhudia kitu kichokuwa cha kawaida, kwani macho ya Lanlani yalikuwa ni kama Kioo, yaani kile kiini cheusi hakikuwa kikionekana na sasa ni kiini cheupe tu ndio kilikuwa kwenye macho ya Lanlan.

Sasa wale wachina wenyewe walijikuta wakiwa katika mshangao na macho yao yote waliyaelekeza kwa ,mtoto mdogo Lanlan.

“Mpo hatarini shambulia mtoto”

Sauti kama mwangwi ilisikika katika vichwa vyao na kuwafanya wakuje vichwa vyao kwa kujizungusha na kisha palepale mmoja ya mchina aliekuwa upande wa kushotoa alifyatuka kumsogelea Edna na Blandina , lakini kabla hajawakaribia Lanlan aliekuwa amesimama aligeuka kama Mpira na Kwenda kumpiga kikumbo yule mchina na kilichotokea ni kwamba mchina yule alirushwa nyuma kwani nguvu iliomgonga haikuwa ya kawaida.

“Atakeye mgusa mama yake Lanlan na bibi yake nitamuua…”Aliongea Lanlan kwa namna ya kuwa siriasi kabisa huku macho yake yakiwa vilevile pasipo ya kubadilika na kumfanya Blandina na Edna kujawa na hofu mno.

“Mshambilieni wote kwa Pamoja , mapanga tanguliza mbele”

Sauti pia ilianza kusikika kwenye vichwa cha watu tisa sasa na palepale walisogeleana karibu na kunyoosha mapanga yao mbele kwa ajili ya kumshambulia mtoto mdogo Lanlan.

Mpaka hapo akili zao ni kwamba zilikuwa zinahisi hatari , hivyo walikuwa kwenye mfumo wa kujiokoa na pia akili zao zilikuwa zikiwapa maelekezo ya kwamba mtoto aliekuwa mbele yao alikuwa ni hatari kwao.

Salah ambaye alikuwa amepigwa risasi na kudondoka mita kadhaa kutoka aliposimama Edna alisimama tena kama vile mtu abaye dakika moja iliopita hakuwa amepigwa risasi na baada ya kusimama kitu cha kwanza alichotafuta ni siraha yake iliodondokea pembeni , aliisogelea na kisha akaichukua.

“Lanlan…” Edna na Blandina walijikuta wakitamka kwa Pamoja na kumsogelea Lanlan na kumkinga baada ya Salah kumyooshea bastora.

‘”Arrggh …!!!!”

Ni damu ya moto iliowarukia Edna na Blandina huku wakisikia miguno ya maumivu kutoka kwa wavamizi hao na walijikuta kwa pamoja wakigeuka na kuangalia ni nini kinaendelea, na hapo ndipo walipoweza kuwa katika mshangao , kwani ni kivuli pekee ndio walichoweza kuona kikiadhibru wale wachina na wajapani kwa dakika chache mno na mtu ambaye alikuwa akiwaadhibu hakuwa na huruma kabisa kwani alikuwa akitenganisha shingo moja kwa moja.

Dakika moja tu tayari majambazi yote kumi yalikuwa hayana vichwa , kwani vilishatenganishwa kwa upanga.

“Persephone… !!, naitwa Christine ni rafiki wa karibu na Hades”.

Sasa Edna alikuwa kwenye mshangao mno , kwanza kabisa mtu aliekuwa mbele yake alikuwa akimfahamu kama moja ya waigizaji na waimbaji maarufu sana , kitu cha pili Edna kilichomfanya kushangaa ni kwamba mwanamke huyo mrembo wa kutisha , alikuwa pia na uwezo wa kimapigano ambao hakuwahi kuhisi kwenye Maisha yake atakuwa nao , kwani siku zote alimuona mwanamke huyo kama mwimbaji mlaini sana ambaye alikuwa akipewa ulinzi , sasa kitendo ambacho kilitokea hapo ndani cha vichwa vya wajapani Pamoja na wachina kutenganishwa , kilimfanya Edna kumwangalia Christine Stewart mwimhaji kutoka Marekani kwa maswali mengi , juu ya yote ni jina la yeye kuitwa Persephone na mzungu huyo licha ya kutokuwa mara ya kwanza kulisikia , lakini pia urafikiwa Christine na Hades , jina hilo pia lilikuwa geni kwake.

“Upo kwenye mshangao kwa namna nilivyowafyeka hawa binadamu wapuuzi waio na nafsi, kwa majina mengine pia nafahamika kama Aphrodite nitakuwa na huzuni kama Hades hajakutajia jina langu ilihali ndio kanikaribisha Tanzania.. hata kumsaidia kulinda familia yake.”Aliongea Christine baada ya kuona bado Edna yupo kwenye mshangao.

“Aunt you are terrific…..”Aliongea Lanlan na kumfanya Edna kuangalia mbele na hapo ndipo alipoweza kumuona Lanlan akiwa ameshikilia kichwa cha Salah huku akionyesha kuridhishwa sana na kitendo cha Christine kuwafyeka watu hao, yaani alionyesha hali ya furaha mno na kwa jinsi alivyoonekana ni kama haikuwa mara yake ya kwanza kuona mtu akitenganishwa kichwa.

END OF SEASON 10.
SEASON 11 ITAENDELEA JUMAMOSI- KWA KUNISAPOTI WASILIANA NAMI KUPITIA 0687151346 ONLY WATSAPP.
Mpaka hapa kwakweli unahitaji support yangu. This is fantastic!
 
SEHEMU YA 294

Roma ilibidi kwanza ambembeleze mrembo Clark kwanza ili kufahamu ni kitu gani kapata kwenye majaribio ya damu yake, lakini licha ya kumbembeleza ,mrembo huyo bado alionekana kuwa na wasiwasi sana.

“Roma niambie , imekuwaje ukalishwa kitu cha ajabu namna hii?”Aliuliza Clark huku akimwangalia kwa macho yenye wasiwasi.

Roma ilibidi aanze kumueleza kila kitu kwanzia sababu ya kuja Japani lakini pia namna ambavyo amekutana na Seventeen feki na kumlisha sumu , mpaka anamaliza stori yake Clark alishangaa na kusikitishwa na jambo hilo

“Roma huyu Seventeen ni muhimu kwako mpaka unashindwa kujua mtego wa wa namna hio, kwanini hutaki kukubaliana na ukweli kwamba alishakufa na huwezi kumuona tena , Roma kwanini hubadiliki?”Aliuliza Clark kwa hasira mno na kwa jinsi alivyo, alionekana kuwa mtu ambaye alikuwa akimjali sana Roma Ramoni na ndio maana alikuwa amekasiika mno , mrembo huyu alikuwa akikumbuka mengi ya nyuma , Roma alikuwa akifanya mambo mengi ya kijinga mara baada tu ya Seventeen kufariki na ndio maana alilalamika na kuona licha ya kwamba tukio la Seventeen kufa lilitokea miaka mingi iliopita , lakini kwa upande wa Roma alionekana kama mtu ambaye hakuwa tayari kukubali ukweli kama Seveteen ashakufa , kuna muda Profesa aliamini uwepo wa Edna utamfanya Roma kumsahau Seventeen , lakini kwa namna ambavyo Roma alikamatika kwenye mtego wa kijinga namna hio aliamini bado Roma alikuwa na kumbukumbu za Seventeen.

“Roma unafikiria nini kitatutokea mara baada ya wewe kufariki, ni maadui wangapi watatuandama siku wakisikia kifo chako , sisi tunaishi kwa amani na maadui zetu wanatuogopa kwa ajili ya uwepo wako , lakini siku wakisikia kifo chako ni Habari nyingine…”Mrembo Clark alionekana kulalamika sana.

Ni kweli kabisa anachoongea Clark ,kwa mfano siku ikatokea Roma akafariki maadui wengi wa familia ya kifalme ya Wales watapata nafasi sasa ya kuwashambulia , kwani siku zote hawakuweza kufanya hivyo kutokana na uwepo wa Hades na jeshhi lake la The Eagles, na ndio maana Clark alikuwa akiogopa sana Roma akipatwa na matatizo na alitaka sana kumlinda , lakini tabia za Roma za kibinafsi za kumfikiria Seventeen mpaka kujiingiza kwenye matatizo zilimuumiza sana moyo wake.

Roma mwenyewe aliona kuna ukweli juu ya maneno ya Clark , kwa mfano sumu ya Polonium ilioingia kwenye mwili wake , kama angetemegea uwezo wa mwili wake tu pasipo kuwa na mbinu za kijini kujiponyesha huenda ingekuwa ni habari nyingine kuhusu yeye.

“Roma Do you know its real possible for you to die?”Aliuliza Clark huku akimwagalia Roma

“Is it very serious?”Aliuliza Roma kwani alikuwa kwenye sintofahamu kwani mrembo huyu badala ya kumueleza hali yake analia.

“Right now ,every single drop of the blood in you body is mixed with countless amount of lethal toxins , including heavy metal and radioactives ones , if all the element in your body combined can be used to develop nuclear bomb”

“Kwasasa damu yako kila tone limechanganyika na kiasi kisichohesabika cha sumu kali ukijumlisha na madini mazito kama elementi ndani ya mwili wako zikaambatanishwa basi zinao uwezo wa kuzalisha bomb la nuklia”Aliongea Jane na kumfanya Roma kutoa macho ni kweli alikuwa akifahamu sumu ya Polonium ni kali sana , lakini hakuamini kama inaweza kuwa na hatari kubwa namna hio.

Radioactives element maana yake ni aina flani ya madini ambayo yanadharisha mionzi mikali sana , mionzi ambayo kama itagusana na mwili wa binadamu athari zake ni kuua seli za mwili , mfano wa madini hayo ni Polonium , Uranium , sasa madini hayo ndio yanayotumika kutegenezea mabomu ya nyuklia.

Sasa ilishangaza sana kwa mwili wa Roma kuweza kuhimili sumu aina ya Polonium.

“Unauhakika kwamba chembe za sumu ambazo zipo kwenye mwili wangu zinaweza kutegeneza bomu?”Aliuliza Roma akiwa katika mshangao wa kutokuamini maneno ya Profesa Clark.

“Unafikiri natania , unahisi nimelia vyote hivi kwasababu uko sawa, nipo hapa mwenyewe nikishangaa umewezaje kuishi Zaidi ya siku mbili ukiwa na sumu mwilini”Aliongea

Roma mpaka hapo aliamini kwamba mbinu ambayo Master Chi aliomfundisha inauwezo mkubwa sana.

“Okey , niambie kama nitaweza kupona?”Aliongea Roma

“Inawezekana kuua dutu zote ambazo zipo kwenye mwili wako , ijapokuwa teknolijia ya sumu ulioingiziwa inatoka ndani ya kundi la Dhoruba nyekundu,lakini siwezi kushindwa kuiyeyusha sumu yote , lakini shida moja ni kwamba ijapokuwa ninaweza kutengeneza ‘Antidote’ lakini mwili wako kwasasa wote unasumu , jambo ambalo linanifanya kuona itakuwa ngumu sana kumaliza sumu yote mwilini”Roma alifikiria kidogo baada ya kusikia maelezo hayo.

“Vipi kama nitatumia uwezo wangu kuikusanya sumu yote mwilini na kuiweka sehemu moja?”Aliongea Roma na kumfanya Clark kushangaa.

“Can you really do it , there is no scientific theories at all that make it possible”Aliongea akimaanisha kwamba hakuna nadharia yoyote ya kisayansi ambayo inawezekana kwa mtu kukusanya sumu mwilini na kuiweka sehemu moja , Profesa Clark alionekana kuwa katika mshangao.

“Ninachokifanya sio kama Sayansi”Aliongea Roma

“Unazungumzia mbinu ya mazingaombwe ambayo uliniambia ulijifunzia Mongolia?”Aliuliza na Roma alitingisha kichwa , kwani katika stori yake hakumueleza Clark kwamba ameshafika levo ya juu kabisa , levo ya kuzaliwa upya, sasa Roma kipindi alipokuwa anaishsi Uingereza ashawahi kumwambia kuwa alikuwa akijifunza mafunzo ya kijini , ambayo yalikuwa yakimsaidia katika uongojjwa wake wa kuwa kichaa , ugonjwa ambao ulikuwa ukisababishwa na Saratani iliokuwa kwenye ubongo wake.

“Kama unaweza kufanya hivyo basi itakuwa rahisi , nitategeneza dawa haraka haraka , wanasayansi wengi ambao wapo ndani ya Dhoruba nyekundu ni wanafunzi wangu”Aliongea Clark.

Unachotakiwa kuelewa ni kwamba Redstorm au Dhoruba nyekundu ipo chini ya Zeros Organisation, lakini sasa misheni nyingi sio kama zilikuwa zikiongozwa na Zeros Organisation moja kwa moja bali ni kupitia kundi hili la Dhoruba Nyekundu , ni kwa mfano uchukulie Marekani kama Zeros halafu C?IA kama Dhoruba nyekundu.

Sasa Zeros ni Secret international Organisation ambayo imeundwa na mataifa makubwa duniani , lakini hio haimaanishi kwamba mataifa mengine madogo hayapo ndani ya Zeros , ukweli ni kwamba mataifa yote yapo ndani ya Zeros lakini sio wahusikaji wa moja kwa moja.

“Naona wanafunzi wako ndio wanataka kuniua?”Aliongea Roma akimwangalia Profesa Clark.

“Unatakiwa ujione kama mtu mwenye bahati , kwani wanasayansi wengi duniani hawaamini katika maswala ya mbinu za kijini unazotumia, mim mwenyewe kuna muda nilijaribu kufanya utafiti juu ya sayansi za kijini lakini mwisho wa siku kichwa kiliniuma kwani mambo mengi yanakosa Nadharia ya kufanyia Practical Experiment.”Aliongea Clark.

Unachotakiwa kuelewa ni kwamba katika ulimwengu wa Sayansi vitu havitokei bahati mbaya , au wanasayansi hawafanyi gunduzi kwa bahati mbaya , kinachokamilisha gunduzi kwa mwanasayansi ni Nadharia(Theories) ambayo ina Thesis ndani yake , Sasa usichanganyikiwe sana katika sayansi kunaanza ‘hypothesis’ halafu ndio inafuatia Nadharia, unaweza kuwa na ‘Thesis’ halafu ukakosa nadharia(Failed Thesis) , lakini huwezi kuwa na nadharia halafu ukakosa ‘Thesis’.

Ijapokuwa Clark hakuwa na uelewa na mbinu za kijini ambazo Roma alikuwa akitumia lakini alizipenda kwani zilikuwa na manufaa makubwa kwa Roma kuliko hasara , kwa mfano Roma kama isingekuwa mbinu hizo angekuwa sio binadamu Zaidi ya kuwa mnyama ambaye mara zote matamanio yake yatakuwa ni kuua pekee yaani asingeweza kuiongoza akili yake.

Roma kabla ya kupitia project LADO saratani yake ilikuwa ikisambaa mwilini kwa kiasi kikubwa sana na kipindi hiko alikuwa na miezi michache sana ya kuishi , lakini mara baada ya kupitia project hio faida kubwa aliopata ni kwaba ile saratasi ilibadilika kutoka malignant(Kansa inayosambaa kwa kasi) Kwenda ‘Benign’(Kansa ambayo haisambai inakuwa kama uvimbe),sasa kutokana na uvimbe huo kuwa katika ubongo inanamfanya muda mwingine kutoweza kujiongoza , Sasa mafunzo ambayo alifundishwa na Master Chi , yalimuongezea uwezo mkubwa sana wa kuongoza akili yake , yaani ilikuwa ni mara chache sana kwa yeye kupitia mabadiliko halafu akashindwa kurudi katikahali ya kawaida.

Roma baada ya kusikia maelezi ya Clark lakini pia namna mrembo huyo alivyokuwa akilia mbele yake , alijikuta pia akianza kumkumbuka mke wake kauzu , alitoa simu yake na kujaribu kupiga Kwenda Tanzania kwa kutumia namba yake iliozoeleka , lakini simu haikuweza kuunganishwa , ikimaanisha kwamba mtandao wa kitanzania haukuwa na huduma ya kupiga simu kimataifa.

Roma baada ya kuachwa na Clark ambaye alienda kutegeneza Dawa ya kumaliza sumu katika mwili wake , aliona awasiliane na Tanya .

“Contact the telecomunication Company immediately , ensure my number will be able to make and receaive call from Tanzania”Aliongea Roma akimpa maelekezo Tanya kwama ahakikisha namba yake inauwezo wa kupokea simu na kupiga ndani ya Japani Kwenda Tanzania.

Tanya upande wa pili ni kama alikuwa amepewa kazi anayoipenda kwani alipokea maagizo hayo kwa furaha kubwa na zilipita nusu saa tu namba ya Roma ilisoma mtandao na palepale alitafuta namba ya mke wake Edna na kupiga Kwenda Tanzania.

Na simu iliita kwa madakika kadhaa na kupokelewa .

SEHEMU YA 295

“Babe Wifey , mnaendeleaje huko Tanzania, nimekumiss sana mke wangu kipenzi”Aliongea Roma , lakini hakukuwa na jibu upande wa pili na kumfanya kutoa simu sikioni na kuangalia kama imekatwa , lakini aligundua simu haijakatwa.

“Wife muda si mrefu nitarudi Tanzania , nipo Hokkaido huku , niambie unataka nikuletee zawadi gani wewe na Lanlan , Unataka pete ya Almasi yanye ukubwa kama jicho , vipi kuhusu mkufu wa dhahabu wa thamani kubwa , vyote hivyo nitanunua nimeingiza pesa ndefu mumeo”Alijiongelesha Roma mwenyewe , lakini hakukuwa na jibu kabisa.

Upande wa Tanzania ilikuwa ni usiku kama wa saa saba za usiku na mrembo Edna alionekana mpaka muda huo hakuwa amelala kabisa, alikuwa na wasiwasi pia kwani zilipita takribani siku mbili tokea Roma atoke Tanzania Kwenda Japani lakini hakupokea hata simu ya kujulishwa kama alifika salama , mwanzoni hakuwa na tatizo , kwani alikuwa akiamini uwezo wa Roma , lakini bado alikuwa na wasiwasi , lakini pia mrembo huyo alikuwa na mawazo , maswala ambayo ameongea na Amiri juu ya dokta Sheba , yalikuwa yakizunguka kwenye kichwa chake , kuna hisia ambazo zilikuwa zikimwambia kwamba kifo cha mama yake hakikuwa cha kuitwa na Mungu bali kilikuwa cha kusababishwa na binadamu.

Ijapokuwa uchugugzi wa Amiri haukuwa umekamilika lakini kifo cha Dokta huyo siku mbili baada ya kuthibitisha kifo cha mama yake kilimfanya kuwa na wasiwasi sana na kuamini kuna jambo ambalo lilikuwa likiendelea ambalo yeye mwenyewe hakuwa akilifahamu , aliamini huenda kisasi ambacho alikuwa akizungumzia mama yake kilikuwa kikihusiana na kifo chake.

Sasa Edna akiwa kwenye wakati mgumu kama huo, ndio alijikuta akiwa na mawazo mno na hata kuanza kumkumbuka Roma , ijapokuwa ni kweli licha ya kwamba hawakua wa kukaa Pamoja mara nyingi , lakini Edna kwenye moyo wake aliona miezi mitano ambayo aliishi na Roma ilikuwa ni kama miaka miwili na aliamini uwepo wake karibu yake ulikuwa ukifaa Zaidi na kumfanya kutokujihisi mpweke.

Sasa baada ya siku nzima kuangalia simu yake huku akimtukana Roma kimoyo moyo kwa kutokumtaarifu kama amefika salama huko Japani , lakini pia kutowajulia hali , alijikuta akiwa na wasiwasi na hasira juu yake , muda wa saa saba hata alipoona simu ya Roma hakutaka kusikiliza pumba zake kabisa , alikuwa na hasira mno na alichokifanya ni kupokea na kuweka simu sikioni pasipo kujibu chochote mpaka pale Roma alipokata simu.

Edna aliamini kutokuongea ilikuwa ni adhabu nzuri kwa Roma , ndio alifurahi kwamba Roma amemkumbuka , lakini wakati huo alikuwa na hasira nae hivyo alimkalia kimya.

Baada ya kusikia sauti ya Roma , alirudi kitandani na kisha aakamwangalia Lanlan aliekuwa amelala Fofo na kumbusu kwenye maji la uso na kisha akajifunika shuka na usingizi ulimchukua dakika kadhaa mbele.

Asubuhi kulivyokucha Edna alimfikishia Blandina juu ya Roma kupiga simu usiku.

“Edna kasema yuko salama , anaendeleaje na kasema anarudi lini?”Aliuliza Blandina mfululizo huku akiwa ameshikilia ‘Cleaner’na alikuwa akisafisha eneo la sebuleni.

“Yuko salama mama , hupaswi kuwa na wasiwasi tena”Aliongea Edna lakini alijikuta akigeuka nyuma mara baada ya kukumbatiwa kwa nyuma na aligundua aliemkubatia alikuwa ni Lanlan aliekuwa akifikicha macho akionesha ndio kwanza anaamka.

“Mama Lanlan ananjaa…”Aliongea Lanlan na kumfanya Edna kutabasamu kwa uchungu , yaani ndio kwanza anaamka na kitu pekee ambacho anaulizia ni chakula hata salamu hakutoa.

“Lanlan msalimie kwanza bibi na unisalimie na mimi ndio nitakuandalia chakula”Aliongea Edna akimfundisha Lanlan.

“Goodmorning Grandma , Goodmorning Mom “Aliongea Lanlan na Blandina alitabasamu na kuitikia salamu ukweli kila alipokuwa akimuona Lanlan alitamani awe mtoto wa damu wa Roma , aliamini angejisikia vizuri kwa Roma kuwa na mtoto wake wa kumzaa ambae asubuhi angemuita bibi.

Upande wa Qian Xi Maisha yake ndani ya familia ya Edna aliyafurahia , rafiki yake mkubwa alikuwani Yezi na moja ya sababu kubwa ya kujiweka karibu na Yezi ni kutokana na kwamba wote walikuwa na asili ya bara moja , yaani Yezi alikuwa ni Mkorea upande wa baba na Mtanzania upande wa Mama.

Yezi licha ya kwamba alikuwa akipata kila kitu ndani ya familia ya Edna , lakini hakubweteka , mrembo huyo alikuwa amepata kazi kwenye moja ya mgahawa wa Kikorea hapohapo Osterbay , hivyo mara nyingi kila akitoka chuo anaunga moja kwa moja kufanya kazi , licha ya kwamba Edna alikuwa na pesa , ila hakupenda kabisa kumuomba na alitamani kushika hela alioitolea jasho yeye mwenyewe, Blandina ambaye alimchukulia Yezi kama mtoto wake hakupenda kabisa kwa Yezi kufanya kazi , lakini pia hakupenda kumuingilia kwani Yezi alikuwa mtu mzima.

Blandina sasa akili yake ilitulia baada ya kupewa taarifa na Edna kama Roma yupo salama , ule wasiwasi aliokuwa nao uliisha na hali ya furaha ilirudi kwa mara nyingine na hilo Edna aliliona na kumfanya hata kumkumbuka mama yake mzazi Rahel.

*******

Ni siku ya tarehe 25 jioni , yaani siku moja kabla ya ndoa ya Amina na Fayezi ndani ya taasisi ya utafifi wa kibaiolojia , Profesa Clark alionyesha kuridhishwa na dawa yake ilivyofanya kazi ndani ya mwili wa Roma , licha ya kwamba ilikuwa jambo la kushangaza kwa Roma kukusanya sumu yote mwilini mwake na kuisukuma mpaka kwenye mikono yake , lakini alijikuta akifaurahi baada ya kuona Roma kapona.

Upande wa Roma baada ya sumu ile kuisha kwenye mwili wake , hatimae aliweza kujisikia hali ambayo hakuwahi kuisiikia hapo kabla , ni kama mwili wake ulikuwa ukipitia mabadiliko ya hali ya juu sana , kwanza kabisa alijihisi kuwa mwepesi mno na alikuwa ni kama mtu ambaye amepoteza kumbukumbu na sasa akili yake ilikuwa ikianza upya kuhifadhi mafaili , alijikuta mara baada ya kunyanyuka kwenye kitanda akitabasamu huku akimwangalia Profesa Clark.

“Kipi kinakufanya kutabasamu?”

“Mwili wangu ni mwepesi sana , sijawahi kujisikia hivi hapo kabla”Aliongea Roma kwa furaha na kujiona sasa ile levo namba tisa ya kuzaliwa upya ndio anaihisi kikwelikweli.

Profesa Clark baada ya kuona Roma ni mwenye furaha , alishindwa kujizuia na kumsogelea Roma na kumbusu kwenye paji la uso huku akiwa ni mwenye hisia kali , kitendo ambacho kilimshangaza Roma , lakini pia kumfanya kuwa na aibu kwa mara ya kwanza kwenye Maisha yake , kwani kitendo cha mwanamke kumbusu kwenye paji la uso haikuwa cha kawaida hata kidogo na yeye ndio alipaswa kumfanyia mwanamke hivyo.

“Mwili wako ushakuwaa sawa kwa sasa”Aliongea Profesa Clark huku akipotezea tukio alilolifanya kwa kuangalia data zilizokuwa zikionekana kwenye Skrini.

“Thank you , you are always the one who can solve my biggest Troubles”

“Asante sana , siku zote umekuwa mtu wa kutatusha matatizo yangu makubwa”Aliongea Roma kwa namna ya shukrani kwa moyo msafi kabisa , ni kweli mrembo Clark alikuwa ni moja ya msaada mkubwa sana kwake, kwa mfano tu tokea jana yake hakulala alikesha ndanni ya maabara akitengeneza dawa ya kumtibu Roma.

Ukweli ni kwamba moja ya sababu ya Profesa Clark kusoma mambo ya biolojia ni kutokana na matatizo ya ubongo aliokuwa nayo Roma , tokea siku ambayo alifahamu kwamba Roma alikuwa na shida , alitumia muda mwingi sana kuangalia namna ya kumsaidia na mrembo huyo alikuwa ameweka nadhiri zake kwa Roma kwamba ipo siku lazima agundue dawa ya kuponya kansa, hivyo kumhudumia Roma ilikuwa ni jambo ambalo alikuwa akilipenda sana , na juu ya yote ni kwamba membo huyo alikuwa akimpenda sana Roma kwa mapenzi ya dhati kabisa tokea alivyokuwa mtoto hakujali kabisa Roma alikuwa akijihusisha kimapenzi na mama yake mzazi , kwake alitii hisia zake na aliamini Roma siku moja atakuwa wake na mpaka umri aliokuwa nao huo wa kuitwa Profesa hakuwahi kuguswa na mwanaume , alikuwa ni kama anamtunzia Roma.

Ukumbuke Roma wakati anamuokoa Catherine kwenye mikono ya maadui zake , Clark alikuwa ni wa umti wa miaka kumi na moja , lakini kutokana na kujaaliwa kwake uwezo mkubwa wa akili Clark alipofikisha umri wa miaka kumi na tano alikuwa ashafanya vitu vikubwa sana katika ulimwengu wa Sayansi , vitu ambavyo wanasayansi wa kawaida wangechukua miaka Zaidi ya arobaini katika ‘Carear’ zao.

“Kama unapenda nipokee sukrani zako , usiwe unafanya mambo ya kijinga na kujiweka katika hali hatarishi, ukumbuke wewe ni Pluto”Aliongea Clark.

“Hilo ni jina tu , lakini mimi pia ni binadamu , tukio la juzi limetokea kwasababu kumbukumbu za Maisha yangu ya nyuma ni za kuumiza sana na siwezi kuzifuta mara moja , hayo ni makosa ya kibinadamu tu , lakini nina uhakika swala hili haliwezi kujitokeza tena”Aliongea Roma.

“Hujaniambia una mpango gani na Kundi la Dhoruba nyekundu Pamoja na Takamagahara na Innova?”

“Kwasasa sina mpango wa kudili nao , nimeaachia vijana wao kwakua nina mpango wangu kichwani , miaka iliopita niliharibu makao makuu yote ya Zeros , lakini mpaka sasa naamini wamejikusanya upya mahali na wanaendeleza ushetani wao , nimeachia vijana wangu waendelee kufatilia taarifa zote za Zeros , siku wakijichanganya sitosita kuua mmoja mmoja nihakikishe nimeondoa mzizi wote”Aliongea Roma kwa ukawaida kabisa

“Umebadilika sana Roma , nimependezwa sana na mabadiliko yako”Aliongea na kisha akaweka baadhi ya mambo yake vizuri na kisha wote kwa Pamoja walitoka kwenye hio maabara , kazi ya Clark ilikuwa ishaisha hata hivyo kwahio kubaki hapo ndani ya maabara ilikuwa ni kama kupoteza muda.

Roma jana usiku wake alikuwa amewapa kazi kundi la Yamata Sect kuangalia nini kinaendelea sehemu ambayo Amina alikuwa amezuiliwa na taarifa zilionyesha kwamba licha ya mrembo huyo kuzuiwa kutotoka , lakini alikuwa akipata huduma zote kama vile malkia na Roma aliona haina haja ya Kwenda haraka , kwanza kabisa mpango wake haukuwa kumuokoa Amina tu , alikuwa na mpango mwingine kichwani , alijiambia kama kilichomleta Japani ni kuzia ndoa ya Amina basi angeagiza vijana wake tu kufanya kazi hio.

Upande mwingine ndani ya hoteli ya hadhi ya nyota tano ndani ya jiji la Otaru Hoteli iliofahamika kwa jina la El-Fadh, anaonekana mheshimiwa kigombola akiwa ndani ya eneo la VIP akiongea na Dodi Fayez.

“Mheshimiwa nadhani kwasasa unaweza kuwa na amani kabisa , nilikuambia kwamba ninao uwezo kumzimisha yule mpumbavu”Aliongea Fayezi kwa lugha ya kingereza na kumfanya mheshimiwa Kigombola asijue nazungumzia nini.

Kigombola alikuwa ndani ya Japani kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya harusi ya Amina na Fayezi , yeye akiwa kama rafiki wa karibu wa Familia ya Tajiri Khalifa hakuwa na mpango wa kukosa kabisa sherehe hio kwani pia alikuwa na mwaliko maalumu.

“Mr Fayezi sijui unachomaanisha “Aliongea Mheshimiwa Kigombola alievalia suti yake huku akiwa ameshikilia Glass ya wine .

Fayezi alitabasamu na kisha alitoa simu yake kampuni ya Apple na kisha akaenda upande wa picha na kumpatia mheshimiwa Kigombola na mheshimiwa alijikuta ni kama mtu ambaye hakuwa akiamini kile alichokuwa akiangalia kwani kwenye simu hio kulikuwa kukionekana picha ya Roma Ramoni akiwa amelala kwenye kitanda cha kusukuma kwa mataili.

“Mheshimiwa nadhani sasa ushaelewa ninachomaanisha”

“Unataka kusema Roma…. no I mean Hades amekufa?”Aliuliza mheshimiwa kwa namna ya kubabaika.

“Ndio amekufa , kama unavyoona picha yake hapo , mtego ambao aliwekewa ilikuwa ni ngumu sana kuukwepa”Aliongea Fayezi kwa furahsa sana na aliminimna Mvinyo kwenye glass zote mbili na kisha akampa ishara mheshimiwa kugongesha ‘Cheers’ kusherehekea.

Mheshimiwa Kigombola licha ya kuangalia picha hizo hakuwa akiamini kabisa maneno ya Fayezi , aliamini huenda mtu aliekuwa kwenye picha sio Roma mwenyewe , maana tokea siku ambayo amepata kusikia mambo ya kisaynasi kutoka kwa Yan Buwen , alikuwa na wasiwasi sana na kila mtu mwenye uwezo wa ajabu , aliamini huenda huko duniani kuna watu wawili wawili , yaani Clone za watu wengi sana na hata yeye mwenyewe alikuwa akitamani kutengeneza kopi yake.

“Hongera sana Fayezi kwa kufanikisha jambo ambalo nilishindwa kulikamilisha , hakika baba yako amekuwa mwenye maamuzi sahihi sana kukurithisha mali za familia”Aliongea Mheshimiwa Kigombola , ukweli hakutaka hata kusikia ni kwa namna gani ambavyo aliweza kumdhibiti Roma.

Baada ya mheshimiwa raisi kuachana na Fayez na yeye kuingia kwenye chumba chake ndani ya hoteli hio ya El Fadhi , alitoa simu yake haraka haraka na kisha akatafuta namba ya mtu Tanzania na ndani ya dakika kadhaa tu simu ilipokelewa.

“Mr Yan Buwen ninayotaarifa ambayo bado haina uthibitisho”Aliongea Mheshimiwa huku akisikiliza kwa umakini kwenye simu yake.

“Ni uzushi gani huo mheshimiwa unataka kuniambia ukiwa Japani?”Ilisikika sauti tulivu upande wa pili.

“Ni juu ya Hades, nimepata taarifa kutoka kwa mtoto wa Khalifa kutoka Dubai kwamba amekufa”Aliongea.

“Hahaha.. Hahahaha” kilisikika kicheko upande wa pili.

“Mr Yan Buwen mbona unacheka”

“Kigombola mimi pekee ndio mwenye nafasi ya kumuua Hades , hakuna binadamu ambaye ataweza kumuua Hades na mtu yoyote mwenye mpango wa kumuua tofauti na mimi mwenyewe ni adui yangu”

“Mr Yan Buwen lakini nimeona picha yake kabisa kwa macho yangu, na ni yeye kabisa”

“Mheshimiwa unaonaje ukiweka akili yako kwenye mpango wetu, wa kupata damu ya Hades tofauti na kuongea mambo yasio na maana usiku wote huu?”Sauti ilisikika upande wa pili na kumfanya mheshimiwa Kigombola kutulia kwa dakika kadhaa na kisha akavuta pumzi na kuzishusha.

“Sawa Mr Yan , naamini maneno yako Zaidi kuliko ya Fayezi , Hades hajafa bado”

“Safi mheshimiwa … mtu pekee ambaye unaweza kumuamini akikuambia kama Hades amekufa ni mimi peke yangu mheshimiwa , wengine wote wanazungumza uzushi , lakini hata hivyo taarifa yako inanifanya nitake kufanya jambo kabla ya Hades hajafufuka ….”

“Unataka kufanya nini?”

“Utapata matokeo mheshimiwa”Aliongea Yan Buwen na kisha akakata simu.
Ohooooo
 
Roma anatakiwa ammalize mapema kibaraka wa Athena prof. Bwan maana amedhamiria kwa kila namna kumuangamiza asisahau kumuwekea ulinzi Mama yake.
 
Back
Top Bottom