Mzee wa Chai
JF-Expert Member
- Sep 20, 2022
- 684
- 1,202
Imeisha ili nisome au niachane nayo tu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndio kweli kabisa huko watsapp mambo ni moto sanaWakuu hii kitu ni kali na haijaisha yaani ukitaka kuifaidi kama una nguvu ya kiuchumi ifate what's up.
Mkuu Singano jr big up
Si utani unatisha juzi nimekesha kumaliza kusoma file ulizonitumia yaani kila nikisema nilale ndo uhondo unakolea.Ndio kweli kabisa huko watsapp mambo ni moto sana
SafiSEHEMU YA 90
Roma alikuwa tayari ashawasiliana na Neema luwazo sehemu ya makutano yao, licha ya kwamba Roma alishangazwa na umbali wa eneo ambalo Neema alikuwa amechagua , eneo la Mbezi Beach ila aliona haina tabu
Roma hakujali sana, alichukulia kama fursa ya kuendesha gari umbali mrefu, kwanza sio kama alikuwa na shida ya mafuta , hakuwa nayo ,kwani pesa ya mafuta ilikuwa ni ya mke wake Edna.
Dakika kama arobaini hivi alikuja kukutana na Neema Luwazo karibu na kanisa la KKKT Mbezi beach ,Neema usiku huu alikuwa pia yupo kwenye gari yake kubwa aina ya Range Rover Spot , alishusha kioo.
“Nifuatishe nyuma kuna sehemu nataka twende”Alionea Neema na Roma alitingisha kichwa huku Neema akipandisha kioo cha gari yake na kuanza kulitoa taratibu kulekea upande wa Tegeta ,dakika chache mbele baada ya kutoka barabara kuu hatimae waliweza kuingia sehemu ambayo Roma hakuwa akiifahamu , yeye alichofanya nikufatisha tu gari ya Neema , walikuja kuegesha gari zao na kisha wakatoka.
Neema usiku huu alikuwa amependeza kweli , alikuwa amevalia gauni na kijikoti cha suti rangi ya Bluu na raba nyeupe.
“Umependeza”Aliongea Roma huku akimwangalia Neema , mbaye kwa usiku huu hakuonekana yule mwanamke ambaye alikuwa akiwahenyesha wenzake bungeni kwa maswali yake wakati wa kuachangia hoja.
Neema alitabasamu huku akimwangalia Roma , alionekana alikuwa akimwangalia kwa maswali mengi .
“Unapajua hapa au ushawahi kufika?”Aliuliza Neema
“Sijawahi kufika hapa , kwanza ningeweeza vipi kufika wakati nilianza kutembea na matajiri juzi tu baada ya kumuoa Edna mwanamke tajiri”aliongea Roma, huku wakisogea sehemu ambayo kulikuwa na viti , hii sehemu ilikuwa nzuri sana , ilikuwa ni Fukwe yenye upepo wa hali ya juu , lakini pia iliojengwa vizuri sana kwa watu kupumzika na hata pia kulala , palikuwa na hoteli kubwa tu sehemu hii.
“Hapa ni Upepo Beach Garden , nimewekeza hapa, hio hoteli ni ya kwangu”aliongea Neema na kumfanya Roma aangalie lijihoteli la nyota tano lililokuwa mbele yake.
“Kuna muda najiulizaga kwanini kila mwanamke ambaye nimetokea kujuana nae ana hela kuliko mimi”Aliongea Roma.
“Na hilo pia unajali Roma?”
“Wewe unaonaje?”Aliuliza Roma mara baada ya wao kuketi ndani ya eneo hili ambalo usiku huu palionekana kutokuwa na watu wengi , licha ya kwamba baadhi ya watu wapo, tena wakiwa na wapenzi.
“Unaonekana kama usiekuwa ni mwenye kujali watu wenyepesa na hili naweza kusema limenifanya nikuone wa tofauti na vijana wengi”aliongea Neema huku akitabasamu na muda huohuo alisogea mzee mmoja.
“Neema naona leo umekuja hapa na mgeni kwa mara ya kwanza?”Alikuwa ni mzee hivi mwenye Mvi japo sio nyingi , alikuwa amevalia mavazi ya uhudumu ndani ya hili eneo na kumfanya Roma ashangae inakuwaje mzee kama huyu akafanya kazi kama hio.
“Ndio Mzee Chino , huyu ni Roma ni rafiki yangu”Aliongea Neema akimtambulisha Roma na mzee akatabasamu.
“Roma huyu ni Mzee Chino ni mmiliki wa hili eneo lakini pia anaweza kua kama baba yangu baada ya mama na baba kufariki”Aliongea Neema na kumfanya Roma ashangazwe na mambo mawili, kwanza juu ya Mzee huyu kumiliki eneo hili la fukwe na wakati huhuo akifanya kazi za uhudumu hakuonesha kabisa kama mmiliki , lakini pia Juu ya Wazazi wa Neema kufariki.
“Kijana unabahati sana , unaonekana kuwa ‘Special’ kwa Neema hajawahi kuja na mwanaume hapa ni mara ya kwanza, Zaidi ya kuja na mtoto wake pekee”Aliongea Mzee Chino na kumfanya Neema aone aibu kidogo na Roma alitabasamu.
“Sasa Mzee unaonekana unapesa lakini imenishangaza unaonekana kuwa muhudumu au ndio swaga za kuwavutia warembo”alitania Roma na kumfanya Neema kucheka.
“Kijana una maneno sana , ninachokifanya ni kitu ninachokipenda , licha ya Eneo hili Neema kujenga hoteli yake , lakini huu mgahawa ni wa kwangu na ninapenda kufanyakazi ya kuhudumia watu kwani inanikutanisha na watu tofauti tofauti , lakini pia ndio kazi ninayopenda , nimeanza kufanya kazi hii wakati nikiwa namfukuzia mama yake Neema”Aliongea Mzee Chino Bila aibu na kumfanya Roma ashangae.
“Kwahio ilikuwaje sasa Mzee Chino , ulimpata Mama yake Neema?”
“Nimpate wapi alinipa sharti la kuacha kazi yangu ya uhudumu niwe nae , nikakataa , akaniacha akaenda kwa mwanaume mwingine mwenye pesa Zaidi yangu”aliongea Mzee chino
“Mzee Chino tuletee supu yako ile unayotengezaga na chapatti pembeni”Aliongea Neema kukatisha maongezi na Mzee chino alitii na kwenda kuleta , ila kwa Roma alishangazwa inakuwaje Waziri akaagiza Chapati na supu usiku wote huu.
“Unashangaa ! kila ninapokuja hapa mara nyingi napenda kunywa supu ya Samaki”Aliongea Neema na Roma alimwelewa ,ukweli ni kwamba hata yeye alikuwa amemisi sana aina hio ya chakula.
‘Seafood’ ni vyakula ambavyo Roma alikuwa na muda mrefu tokea afike Tanzania hajavigusa kabisa , na aliona sio mbaya kwa usiku huo kupata aina hio ya chakula , Roma aliona kwa jinsi walivyokuwa wanaonekana walikuwa kwenye ‘Date’.
“Nilijua Mkeo atakukataza kuja kuonana na mimi?”.
“Na amenikataza , ila sikutaka kumtii kwasababu nilishaweka ahadi ya kuonana na wewe”.
“Nijikuwa sina jinsi Zaidi ya kumuomba namba yako Roma , sikutaka kujificha mbele yake , kama angenikatalia namba yako nisingelazimisha hata tuonane , lakini alivyonipatia nikaona hakuwa na shida ya mimi na wewe kuonana”Aliongea Neema kwa sauti ya kawaida na wakati huohuo Chino alileta kile Neema alichoagiza mabakuli mawili , Roma baada ya kuona mifupa ya samaki na nyama nyama alipandwa na hamu ya kushughulikia msosi huo.
“Neema inabidi unitambulishe vizuri , siamini kama kuna urafiki unaoendelea hapa”Aliongea Mzee Chino huku akindoka akiwa na tabasamu na Neema aliishia kutabasamu.
“Unajua kwanini nimechagua hii sehemu?”Aliuliza Neema.
“Mimi najuaje wewe ndio umenileta hapa”
“Nilivyokuwa mdogo Mama alikuwa akipendelea kunileta sana hapa, ni kama kumbukumbu pekee ambayo ameniachia , kila ninapokuwa sina Amani nakuja hapa, nakaa natulia then kesho nitaondoka nikiwa mpya, na nilijiambia siku nikipata mwanaume ambaye nitatokea kumpenda kwa dhati nitamleta hii sehemu”Aliongea Neema kwa hisia na wakaangaliana na Roma.
“Lakini mwanaume ambaye nilikuwa nikimuota amechelewa sana kuja kwenye maisha yangu mpaka nikiwa na umri huu”
“Neema mbona unaonekana kama ndio unanifungukia sasa”Aliongea Roma na Neema akatabasamu baada ya kuona namna Roma anavyonyoosha maneno.
“Unajua Roma unaonekana muhuni sana wakucheza na wanawake na bado nikashangaa kwanini mwanamke kama Dorisi akakupenda na pia Edna kuwa mke wako na mimi mwenyewe pia kukupenda kiasi hiki”
“Sasa kwanini unaonekana ni mwenye kunipenda , mimi mwenywe najua sijatulia na udhaifu wangu mkubwa ni wanawake , kwanini licha ya kulijua hilo unaonekana kunipenda?”
“Kwasababu sisi wanawake ni tofauti na nyie wanaume , nyie ili mumpende mwanamke mnaangalia vitu vingi ,kama vile uzuri . upole na vigezo kibao , ila kwetu sisi hatuna sababu ya kumpenda mwanaume, ukimkuta mwanamke kapenda kweli na ukamuuliza kwanini kapenda atashindwa kukupa jibu , ila kwa mwanaume ni rahisi kukupa jibu kwanini kampenda mwanamke wake”Aliongea na Roma licha ya kwamba alikuwa akisikiliza lakini alikuwa bize na chakula chake , alikunwa akitafuna yaani, hakuwa ni mwenye kuchanganywa na mwanamke kama waziri kumfungukia yeye kwake aliona ni kawaida,ingekuwa ni vijana wengine wakakutana na hali kama hio huenda wangekuwa wapo tofauti sana na Roma.
“Kwahio huna sababu nyingine ambayo inakufanya kunipenda , yaani huwezi eleza kwanini unanipenda?”
“Licha ya kwamba unaonekana mwanaume ambaye huwezi kutulizwa na mwanamke mmoja ,ila ninashauku ya kukujua Roma , najua kabisa haupo wa kawaida , kila siku ambayo tumekutana mimi na wewe lazima unishangaze ,ni mwanaume ambaye hautabiriki na hii imenipa shauku Zaidi ya kuwa na ukaribu na wewe ili kukujua”
Aliongea Neema na Roma akamwangalia mrembo huyu ambaye kwake ki umri walikuwa wamepishana sana , licha ya kwamba Neema kuonekana mdogo lakini umri ulikuwa umeenda na hakuna mtu wa kukataa hilo ni vile tu kwamba alikuwa ni mwanamke wa kujitunza na pesa pia ilikuwa imemfanya kuonekana mdogo.
Roma alimalizia supiu yake lakini kwa Neema alionekana hata hamu ya kuendelea kula hakuwa nayo.
“Lakini Neema unajua kabisa mimi nina mke ,na nisiwe muongo hapa hata kama nikikubalia ujue sitoweza kucheza kwenye matarajio yako kama mwanamke ambaye ana mwanaume anaempenda”Aliongea Roma na Neema alitabasamu na kisha akanyanyuka.
“Unaonaje tukitembea tembeatembea mpaka kule”Aliongea na Roma hakubisha, alinawa mikono na kisha akanyanyuka .
“Nishazeeka tayari kwasasa Roma ,ki ufupi mimi sipo kama wasichana wa miiaka ishirini ambao watatamani vitu vikubwa kwa mwanaume , kwasasa nina kila kitu pesa na pia nina mtoto ,ninajua una mke na hilo nitaenda kuliheshimu na pia na mheshimu Edna , lakini ukweli ni kwamba licha ya kwamba unaonekana kuwa kijana mdogo , lakini nimetokea kukupenda sitaki unifanyie kikubwa , ila nitapenda kama utakuwa na mimi wakati nitakapokuhitaji”Aliongea Neema kwa hisia huku akisimama mbele ya Roma akiangalia upande wa baharini.
Na Roma hakujua cha kujibu kwa wakati huu , siku zote alikuwa ni mwenye kuanza wanawake lakini leo hii , yeye ndio kaanzwa na pia mwanamke aliembele yake alikuwa tayari ashaonja utamu wake.
Roma alimsogelea Neema kwa nyuma na kumkumbatia na kumfanya mwanamama huyu atabasamu na ajisikie vizuri sana , upande wa Roma hakutaka kuuliza sana juu ya Edna kumtahadharisha kuachana na Neema ,kwanza hakuwa akiogopa kiumbe chochote kwenye hii dunia kwanini aogope kuwa na mwanamke aliekuwa mbele yake ambaye anataka kuweka kumbukumbu kabla ya kuingia kwenye uzee wake.
Kadri sekunde na dakika zilizvyokuuwa zikisogea miili yao ilipata Joto la mapenzi na Neema ndio wa kwanza kugeuka na kugusisha midomo na Roma na kuanza kunyonyana kimahaba , huku Roma na yeye ekipitisha mikono kwenye mwinuko wa Mrembo Neema Luwazo.
“Cling .. Cling …Cling”
Ni simu ya Neema ndio iliowakatishia utamu na Neema hakutaka kupuuzia simu iliokuwa inaita alijitoa kwa Roma na kisha akaangalia ninani anapiga na jina lilisomeka ‘My daughter’.
Roma hakujua Neema alikuwa akiongea nini na simu kwani Neema alisogea mbali kidogo ,baada ya dakika kama moja za Neema kuongea na Simu , alimsogelea Roma.
“Naona jambo letu leo litaishia hapa nina dharula tutapanga siku nyingine ya kuonana”Aliongea Neema na kumfanya Roma atoe macho , yaani hakuamini hii pisi leo inamuacha hivihivi pasipo kumpa kidogo ukizingatia joto lake limepanda kwa kiwango kikubwa.
“Unaniachaje hivi sasa Neema?”Aliuliza Roma .
“Ni jambo muhimu sana , ni juu ya mtoto wangu naomba niondoke nitakutafuta siku nyingine”Aliongea Neema na alionekana hakuwa tayari kusubiri jibu kutoka kwa Roma alianza kupiga hatua kuondoka.
Wakati Roma akijiuliza cha kufanya kwa wakati huo , kwani hali yake haikuwa sawa kabisa na alihitaji kampani ya mwanamke kwa usiku huo , mara simu yake ilianza kuita , aliitoa na kuangalia jina na aliona aliekuwa akipiga ni Nasra , Roma alijikuta akimkumbuka huyu mrembo maana tokea arudi Japani hawajaonana.
“Bebi Nasra naona umenikumbuka leo,halafu unaonekana kuwa sehemu yenye makelele upo nyumbani kweli?”
“Sipo nyumbani nifuate , nipo Kidimbwi”aliongea Nasra upande wa pili na kumfanya Roma ashangae , kwanza hakuwa akipajua Kidimbwi ni wapi.
“Kidimbwi ndio wapi Nasra?”
“Ni ufukweni Kidimbwini nifuate”Aliongea Nasra na kukata simu , alionekana alikuwa amelewa , Roma hakutaka kubaki hapo , alitembea kuitafuta gari yake.
Baada ya dakika chache tu alikuwa ashaifikia na kutafuta Kidimbwi ilipo maana Gari lake lilikuwa na uwezo wa kuonyesha ramani , na alitabasamu baada ya kuona hakuwa mbali na sehemu yenyewe ni kilomita kama moja tu hivi kutoka alipo.
Nasra alionekana kujiinamia chini kwenye Meza , haikueleweka alikuwa na nani hapo ndani kwani muda huu ,alikuwa peke yake na jambo hili lilimshangaza Roma.
“Mbona upo peke yako na unafamya nini hapa ?”Aliongea Roma.
“Nilikuja na marafiki zangu niliomaliza nao chuo ndio wameondoka na kuniacha na siwezi kuendesha gari nikiwa mlevi hivi”aliongea Nasra huku akijinyanyua kilevi na Roma alimshikilia.
Roma hakuona haja ya kumrudisha Nasra Mikocheni , kwani asingeweza kuacha gari yake hapo , alichoona ni kuchukua chumba ili waweze kuondoka asubuhi.
*****
Ilikuwa ni muda wa asubuhi , Roma aliamshwa na simu akiwa ndani ya hoteli na Nasra ambaye alikuwa amejilaza vibaya kweli , na hii ni baada ya wao wawili kumaliza kufanya mapenzi usiku kucha na staili yao ambayo Roma alimwambia Nasra inaitwa ‘Facing The Ocean’.
“Diego kuna nini ?”Aliuliza Roma baada ya kuona jina la mpigaji ni Diego na alijua lazima kutakuwa na tatizo.
“Your Majesty ! nadhani usiku wa leo haujalala nyumbani”
“Ndio”
“Chiara na John walifika nyumbani kwako kwa ajili ya jukumu lao la kazi , lakini hali walioikuta haikuwa shwari , geti walikuta lipo wazi na pia vijana wanaotoa ulinzi hawana fahamu ”Aliongea Diego na hapa Roma aliona kweli kuna tatizo.
Alikurupuka harakaharaka na kisha akavaa nguo zake .
“Diego hebu jaribuni kufatilia nin kimetokea ninafika nyumbani mara moja kuona tatizo ni nini”Aliongea Roma haraka haraka na kisha akakata simu , na akamuamsha na Nasra na kumwambia kuna dharula na ataondoka wa kwanza na hata hakusubiria jibu , alifungua mlango na kutoweka ndani ya eneo hilo.
Ndani ya kama nusu saa tu hivi ,Roma alikuwa akiingia Kigamboni nyumbani kwake , na ni kweli ile anafika geti lilikuwa wazi na hata mlango wa mbele wa nyumba yao ulikuwa wazi pia , alikimbilia ndani mpaka sebuleni huku akiita jina la Edna na hakukuwa na majibu , lakini ile amesimama ,alivyoangalia kwenye meza ya kioo aliona kikaratasi cha rangi ya njano kilichokuwa kimebandikwa kwenye Meza ba gundi.
“Your Majest Pluto ,Jumba unalokaa ni kubwa sana na tumeshangazwa , Tupo na mkeo pamoja na Mama wa nyumbani , ukiwataka wakiwa hai tuletee jiwe la Kimungu(Godstone),Sehemu ni Mabwepande , uje peke yako…Cc Froma Yamata Sect”Kilikuwa ni kikratasi ambacho kimeandikwa kwa lugha ya kijapani.
END OF SEASON 3 HAVE NICE WEEKEND
ITAENDELEA SIKU YOYOTE
ACHA KUTESEKA NA AROSTO CHANGIA 2000 KUENDELEA HALAFU NICHEKI WATSAPP 0687151346 UUNGANISHWE NA GURPU , AU KAMA HUPENDI GRUPU NITAKUTUMIA INBOX, KILA SIKU VIPANDE VITAT , KWA SASA TUPO SEASON 5 KIPANDE CHA 130
NAMBA ZA KULIPA NI 0687151346 AIRTEL AU 0743015453 M-PESA AU 0657195492 TIGO PESA AU 0623367345 HALOPESA JINAA ISSAI SINGANO
UKILIPA TUMA MESEII YA MUAMALA WATSAPP NAMBA NI 0687151346
Sasa hawa walinzi wa kizungu wana kazi gani hadi Edna na bi wema wametekwa?SEHEMU YA 90

Wamewahiwa kijanjaSasa hawa walinzi wa kizungu wana kazi gani hadi Edna na bi wema wametekwa?