SEHEMU YA 96
Roma baada ya kumaliza kuongea na simu alishuka mpaka chini sebuleni kwa ajili ya kujipatia kifungua kinywa ili aelekee kazini.
Edna tayari alikuwa ameketi kwenye meza na Bi Wema wakijipatia kifungua kinywa ,Edna alimwangalia Edna na kisha kumtingishia kichwa kama salamau na Roma alitabasamu na kisha akavuta kiti na kuketi.
Saa tatu kamili Roma aliingiza gari lake kwenye maegesho ya kambuni na akaingia kwenye lift kuelekea kwenye ofisi ambayo alikuwa akifanyia kazi.
Wafanyakazi wenzake leo hii walikuwa bize na majukumu yake , na Roma hakutaka kuwabughuzi , alichokifanya ni kusalimia kila mmoja na kisha akakaa kwenye meza yake na kuwasha tarakishi yake kuangalia ni gemu gani ambalo leo atacheza.
Recho aliekuwa bize alimwangalia Roma na kisha akatabasamu , mrembo huyu alionekana alikuwa akikumbuka kitendo ambacho alikuwa amefanyiwa na Roma siku chache nyuma , na Roma alimuona Recho ambaye alikuwa akimwangalia na kumkonyeza.
Saa sita kamili Roma alikuwa ashachoka muda mrefu kucheza gemu na sasa alikuwa ameegamia kwenye kiti chake akiwa ameuchapa usingizi.
“Romaa..!!”Ilikuwa ni sauti ya mwanadada Benadetha iliomshitua kutoka kwenye usingizi wake na aligeuza shingo na kumwangalia.
“Kuna sehemu naomba unisindikize “Alionea Benadetha huku akimwangalia Roma.
“Unaonaje ukiniambia ni wapi tunaenda”
“Naelekea Site , nimeona huna kazi , hivyo sio mbaya kama utanisindikiza”Aliongea Benadetha na Roma hakuona shida kumsindikiza , kwanza alikuwa ashachoka kukaa sehemu moja na alitaka kidogo anyooshe miguu.
Roma na Benadetha waliingia kwenye gari moja ya Benadetha huku Roma akiwa ndio dereva ,Benadetha alimpa Roma maelekezo kama anaelekea Mbagala eneo ambalo Barabara ya mwendokasi ilikuwa ikijengwa kwa ushirikiano wa kampuni mbili yaani JR na Vexto grupu.
“Benadetha nadhani cheo chako cha ukuu wa Idara ya ‘Public Relation’ hakikutoshi”Aliongea Roma.
“kwanini unasema hivyo?”
“Katika wanawake ambao ni wachapakazi kwenye kampuni ni wewe”
“Mh!,Sio kweli wapo ambao wanafanyakazi Zaidi kuliko mimi , kwa mfano CEO Edna nadhani ndio anaefanya kazi kuzidi wafanyakazi wote wa kampuni,licha yakampuni kuwa yak wake”Aliongea Benadetha na Roma aliona ni kweli Edna alikuwa akifanya sana kazi ,kwani alikuwa akikumbuka kuna siku alikuwa akilala ofisini.
“Nadhani , lakini kwenye idara yetu wewe ndio mfanyakazi unaewajibika muda wote , sijawahi kuona hata ukipiga umbea na wafanyakazi wenzako , inabidi CEO akupandishe cheo”Aliongea Roma na kumfanya Benadetha ajisikie vizuri, hakuna mtu ambaye hakupenda kusifiwa , lakini pia ilikuwa kweli Benadetha alikuwa ni moja ya wafanyakazi wa Vexto ambao muda wote walikuwa bize.
Na kuna muda Roma alimuona Benadetha kama mfanyakazi ambaye huenda kwao Maisha hayakuwa mazuri sana ndio maana anafanya kazi sana ili apandishwe cheo na mshahara uongoezeke.
“Sema Roma ulitushangaza wewe na Dorisi baada ya kufanikiwa kufanikisha Saini ya dili nono na kampuni ya Yamakuza , hakuna ambaye alitegemea mafanikio yale,unaonekana kuwa mtu ambaye hujali sana maswala ya kazi , lakini ukiwa siriasi utafanya mambo makubwa”Aliongea Benadetha na kumfanya Roma atoe tabasamu.
Dakika chache walikuwa washafika Mbagala Rangi tatu na Roma alisimamisha gari upande wa kulia na kisha akatoka.
Benadetha licha ya kwamba hakuwa mzuri sana kama Edna , lakini alikuwa ni moja ya wanawake ambao unaweza kusema kwamba ni mazuri kiasi kwamba kila mwanaume atakae mwangalia lazima avutiwe nae ,Roma aliongozana na Benadetha mpaka upande wa pili wa Barabara.
Sehemu ilikuwa na wafanyakazi wengi ambao walikuwa wakifannya kazi ya kuchimba mashimo na kumwaga Zege,Roma hakuelewa ni jambo gani ambalo limemleta Benadetha ndani ya haya maeneo ambalo lilikuwa likihusiana na Idara yao.
“Romaa!”Ilikuwa ni sauti ya kiume ambayo ilimfanya Roma ageuze macho upande wa kushoto na kumwangalia ni nani aliekuwa akimwita.
“Yusuph!”Aliita Roma mara baada ya kugundua aliekuwa akiliita jina lake alikuwa ni Yusuph ,Roma tokea atoke Mbagala hakuwahi kupata wasaa wakuja kuwatembelea marafiki zake,aliokuwa akibeba nao mizigo.
Yusuph alikuwa amevalia kijikoti cha rangi ya kijani na kofia ngumu kichwani,Roma alishangazwa na Yusuph kuwa ndani ya hilo eneo , kwani kazi ambayo alionekana alikuwa akifanya ilikuwa ikihusisha wahandisi.
“Ni muda Man hatujaonana tokea uoe,Maisha yako yamekuwa Super sana siku hizi”Aliongea Yusuph baada ya kuwasogelea Roma na Benadetha.
“Ndio ni kama mwezi sasa , ila sijawahi kujua kuwa wewe ni injinia”
“Haha…nadhani haujawahi kuniuliza kuhusu levo ya Elimu yangu Roma”Roma alitingisha kichwa na kuona ni kweli , kwani licha ya kwamba alikuwa akifanya kazi na baadhi ya watu pale Soko la Mbagala , lakini hakuwa akijua kuhusu elimu zao , alichokuwa akijua Roma ni kwamba ni wabeba mizigo kama yeye alivyokuwa mbeba mizigo.
“Kwahio unaniambia ulikuwa msomi wa injinia?”
“Ndio , ile kazi ilikuwa ni kusogeza tu siku, si unajua mwenyewe kazi siku hizi ni ngumu sana kupata na ndio maana nilikuwa nimejishikiza pale, ila kwasasa namshukuru Mungu nimefanikiwa kupata kazi hapa”Aliongea Yusuph na kumfanya Roma atingishe kichwa.
“Benadetha huyu ni rafiki yangu , kabla sijapata kazi Vexto nilikuwa nikifanya kazi Soko la Mbagala kama Mbeba mizigo”aliongea Roma na kumshangaza Benadetha hakuwa na hio taarifa
“Daah ! Roma kumbe unafanya kazi Vexto hii ambayo ndio wanajenga hapa?”
“Roma unaweza kuongea kwanza na Rafiki yako , ngoja nikaonene na Injinia mkuu nitarudi baada ya nusu saa”Aliongea Benadetha na Roma alitingisha kichwa kukubaliana nae.
“Ndio Yusuph,Mbona unaonekana kushangaa?”
“Nimeshangaa Man , kama ninejua mapema ningekuja kwako unifanyie koneksheni haraka niweze kupata nafasi ya kazi hapa”
“Ndio , ila ni vileile tu , bahati ililuwa upande wako ushapata kazi”
“Ndio sema mshikaji wangu Mhando yule hakupata na mpaka sasa yupo palepale sokoni anafanya kazi , amejitahidi kuomba sehemu mbalimbali ila bahati haijawa yake”
“Unamaanisha yule jamaa mpole sana?”
“Ndio man , nimejaribu kuongea na Director hapa ampe nafasi ila kasema pashajaa na hapokei injinia mwingine na jamaa namuonea huruma maana Bi mkubwa wake ni mgonjwa wa kisukari na pesa anayopata anamtumia lakini bado kiasi ambacho anatuma hakitoshi”Aliongea Yusuph na kumfanya Roma amuonee huruma , alikuwa akimjua Mhando hakuwa muongeaji sana ,ila hakujua kuwa alikuwa pia yeye ni mhandisi wa ngazi ya shahada kama ilivyokuwa kwa Yusuph.
“Sasa Roma kama una konekesheni unaonaje ukimuunganisha mshikaji, namuonea sana huruma najitahidi ninachopata hapa kumsevu na kiasi lakini bado”
Aliongea na Roma aliguswa kumsaidia Mhando , aliona ni jukumu lake kuwasaidia washikaji zake ambao alikuwa akifanya nao kazi kwa takribani miezi sita alipoingia ndani ya jiji la Dar na ni hao ambao walimpokea kwa ukarimu , hivyo aliona kuwasadia ilikuwa jukumu lake.
“Okey! Nitamsaidia mshikaji mpigie simu tuonane hapa”Aliongea Roma na Yusuph alitoa tabasamu la Furaha , alitoa simu yake ndogo mfukoni na kupiga.
“Anasema yupo maeneo hayahaya na anakuja saivi”
“Vyeti vyake je?”
“Haha..Jamaa anatembeaga navyo kila anapoenda”Aliongea Yusuph na kumfanya Roma tabasamu.
Zilipita kama dakika kumi na tano tu hivi Mhando alifika , alikuwa amechafuka mno kiasi cha kumfanya Roma aone kweli taifa la Tanzania lina tatizo kubwa la Ajira , kwani msomi wa Uhanidisi hakuwa na utofauti na watu ambao hawajasoma.
Mhando alisalimiana na Roma kwa shauku kubwa iliokuwa imemvaa kwenye uso wake.
“Oya Mhando mwenetu Roma hapa atakusaidia juu ya kazi , anafanya kazi Vexto na anakonekesheni”Aliongea Yusuph na kumfanya Mhando atoe tabasamu.
“Nitashukuru sana kama utanisaidia Roma”Aliongea na kumfanya Roma atabasamu na wakati uleule Benadetha alifika ndani ya eneo ambalo Roma alikuwa amesimama na marafiki zake , alionekana kumaliza kile ambacho kilikuwa kimemleta ndani ya hili eneo.
“Benadetha kuna huyu Rafiki yangu nataka nimsaidie kupata kazi hapa , ni injinia na hivi ni vyeti vyake”Aliongea Roma huku akimkabidhi Benadetha vile vyeti na kuanza kuvikagua pamoja na CV yake na mwanadada huyu alijikuta akishangaa kwani Mhando alikuwa na ufaulu mkubwa sana wa GPA.
“Unaonekana kuwa na ufaulu mkubwa , kwanini wameshindwa kuchukua mhandisi kama wewe”Aliongea Benadetha huku akiendelea kusoma karatasi zile , licha ya Mhando kuwa na GPA ya 4.7 ya Civil Engeneering lakini pia alikuwa na uzoefu wa kufanya kazi sehemu tofauti tofauti na hili ndio jambo ambalo lilimshangaza Benadetha kwanini mtu ambaye ana ufalu mkubwa kama huu hajapata nafasi.
“Sister hata mimi nimeshangaa ,GPA yangu ni 3.0 lakini nimepata ajira na Mhando kakosa licha ya kwamba tumeleta maombi wakati mmoja”Aliongea Yusuph.
Roma kwa maelezo hayo aliona ukakasi kwa watu ambao walikuwa wakihusika na maswala ya uajili.
“Sema swala la ajira na usimamizi wote wa waajiriwa hapa unasimamiwa na JR , sisi tunahusika na kuleta malighafi tu”Aliongea Benadetha lakini Roma hakuridhika.
“Hata kama Benadetha,kulitumika kigezo gani kwa Mhando hapa kukosa kazi,lazima kuna ufisadi unafanyika”Aliongea Roma.
“Kwahio Roma unataka kufanya nini?”
“Mhando nitumie hizi CV na vyeti vyako kupitia Email yangu nitaangalia namna ya kukusaidia kupata kazi , kesho nitakupa jibu”Aliongea Roma na kumfanya Mhando macho kumtoka maana kwa jinsi alivyomuona Roma ni kama alikuwa na uhakika wa kupata kazi , kwani Roma aliongea kwa kujiamini.
Roma baada ya kumtajia Mhando Emaili yake waliondoka ndani ya hilo eneo na kurejea walipo acha gari yao.
“Benadetha unaonaje tukipata kabisa chakula hukuhuku kabla ya kurudi”
“Yeah! Itakuwa vizuri hata mimi nilikuwa nikifikiria hivyo”Aliongea Benadetha huku akitabasamu.
Roma alikuwa akiyajua sana haya maneneo ya Mbagala hivyo kuchagua mgahawa wa wao kukaa kwa ajili ya kupata chakula halikumpa shida.
Walikuja kusimamamisha gari Zakhem barabara ya kwenda Kijichi kwenye mgahawa moja maarufu ndani ya eneo hili.
Roma alimuongoza Benadetha ambaye alionekana kuwa mgeni kwenye haya maeneo.
“Sio pabaya sana”Aliongea Benadetha baada ya kupenda mpangilio na usafi wa hapa ndani , licha ya kwamba ni sehemu ambayo ilikuwa na watu wengi.
Roma aliagiza ugali na samaki pamoja na juisi na Benadetha pilau na nyama ya kukaanga.
Wakati Roma akianza kula mara macho yake yalitua kwenye watu waliokuwa wakiingia ndani ya hili eneo , na sehemu ambayo Roma na Benadetha walichagua kukaa ilikuwa ni rahisi kwao kuona mlangoni na hii ilimfanya Roma kutambua watu haraka.
Roma alimuona Najma aliekuwa ameambatana na watu wanne , wa kwanza kutambua ni Juma, wa pili yake alikuwa ni mama ambaye kwa harakaharaka ukimwangalia ni mtu wa miaka kama arobaini hivi kwenda juu mweupe mnene alievalia ushungi na dela rangi nyeusi , halafu pia mtu wanne alikuwa ni mwanaume hivi msomali mwenye kitambi saizi ya kati ambaye Roma alishindwa kumtambua.
Najma alijikuta akikutanisha macho na Roma na kumfanya Juma aliekuwa akiangalia sehemu ya kukaa ,huku akiongea na bwana mwenye kitambi kugeuka upande ambao Najma alikuwa akiangalia na hapo ndipo na Juma aliokutanisha macho na Roma.
SEHEMU YA 97.
Juma licha ya kwamba alikuwa amemuona Roma lakini hakuonyesha hali yoyote ile ya kutaka kumsalimia, Roma aliekuwa amekaa na Benadetha alishindwa kujua ni kwanini watu hao wanne wapo hapa ndani ya mgahawa , kwani kwa muonekano wao hawakuonekana kama watu ambao wamekuja kwa ajili ya kula tu , bali walionekana kama kuna jambo muhimu ambalo walikuja kulizungumza.
Juma alinyooshea kidole Meza iliokuwa tupu pembeni kidogo na walipokuwa wameketi Roma na Benadetha na waliisogelea japo kwa Najma ni kama hakupenda hio sehemu.
Najma alimwangalia tu Roma na alishindwa hata kumpa salamu na kwa Juma hivyohivyo kitendo ambacho kilimfanya Roma kujiuliza kuna nini kinaendelea , ila hakutaka kufuatilia , alijiambia kwenye akili yake kwakua wamekuja kukaa karibiu na yeye basi atajua ni kwanini kuna mabadiliko hayo kwa upande wa Najma , kiwani alikuwa akimjua sana mwanadada huyu hata kama kaka yake asingesalimia ila kwa Najma asingempita Rma bila salamu.
Benadetha alimwangalia Roma na alionekana na yeye kuna kitu alikigundua ila hakutaka kuongea , aliendelea kuwa bize na chakula chake.
“Baba hili tushalimaliza kabisa na mimi kama Shangazi yake Najma unabaraka zote na unachopaswa ni kuleta barua ya posa na taratibu zingine zitafuatia”Roma alipata kusikia maneno hayo kutoka kwa mwannamke ambaye sasa aligundua ni Shangazi yake na Najma.
“Ninashukuru sana mama kwa kutupa Baraka zako mimi na Najma, niseme tu nampenda sana Najma na nipo tayari kumuoa hata kesho”Roma aliweza kusikia mwanaume mwenye kitambi akiongea,
“Hahaha..Unaonekana kumpenda sana Najma, ila niseme Shangazi yangu kwakweli ni mrembo , hapa umepata mke”Aliongea Shangazi na hakujali kuongea kwa sauti ya chini na watu waliokuwa pembeni walijua kinachoongelewa hapo ni ndoa , Najma muda wote alionesha hali ya kutokuwa na utulivu , licha ya kwamba Roma alikuwa amempa kisogo ila kwa sauti ya Shangazi yake alijua kabisa atakuwa amesikia kila kitu.
“Bro Ahmedi Mdogo wangu ni Chombo , wewe fanya chapu kama shangazi alivyosema ili ndoa isichelewe”Aliongea Juma na yeye kwa sauti kubwa kidogo kuliko ya shangazi yake.
Roma hata ile hamu ya kula ilikuwa imemuishia na Benadetha aligundua mabadiliko ya Roma ila alipanga kukaa kwanza kimya kwa wakati huo na pia Roma alishukuru kwa Benadetha kutouliza kwani aliona angemfanya asisikie ni kitu gani Najma na kaka yake kilikuwa kimewaleta hapo ndani.
Roma baada ya kumaliza kula chakula , alilipia na kutembea kuelekea barabarani na kuingia kwenye gari yao na safari ya kuridi kazini ikaanza.
“Alikuwa ni mpenzi wako?”Benadetha alivunja ukimya .
“Siiwezi kusema alikuwa mpenzi , ila tulifikia hatua nzuri ya kuwa wapenzi , ila kuna changamoto zilikuwepo katikati yetu ndio maana”
“Lakini Roma Wewe si unmake?”
“Ndio ninae na naweza kusema na hio ni moja ya changamoto”Alijibu Roma na kiukweli ni kwamba moyo wake ulikuwa mzito sana kumuachia Najma awe na mwanaume mwingine ni hali ambayo hakuwahi kujihisi kwenye maisha yake.
Roma baada ya kufika ndani ya kampuni alinyoosha moja kwa moja kwenda kwenye ofisi ya mke wake Edna.
Alimkuta Miss Airport aliekuwa bize na tarakishi yake na Roma alimpungia tu mkono na kupita moja kwa moja , jambo ambalo lilimfanya mwanadada huyu akasirike.
Roma baada ya kuingia ndani ya ofisi hii , alimkuta Edna akiwa anaongea na Simu , jambo ambalo kwa Roma kwa kumuangalia tu mke wake alijua kabisa simu hio ilionekana kuwa muhimu kutokana na muonekano wake.
“Hahaha..Chibu! Acha kunichekesha , haujaacha mambo yako tu mpaka sasa hivi”
“Sawa.. Usijali Chibu,Nitajitahidi kufanikisha ombi lako”
Edna alikuwa akiongea kwa kifaransa jambo ambalo lilimshangaza Roma , hakujua mke wake alikuwa akijua kuongea kifaransa tena ‘Fluently’,lakini licha ya Roma kushangazwa na namna ambavyo mke wake alikuwa akiongea kifaransa ila jina la ‘Chibu’ ndio lililomfanya afikirie ni uhusiano gani Chibu anao na mke wake kiasi cha wawili hao kuongea kwa furaha mpaka kuwekeana ahadi.
“Vipi Roma kuna shida?”Aliuliza Edna baada ya kumuona Roma anamwangalia tu bila ya kuongea lolote.
“Wife sikujua kama unaweza kuongea kifaransa”
“Mh! Ulifikiri ni wewe tu ambae unajua kuongea lugha tofauti tofauti?”
“Sijamaanisha kama hupaswi kujua kuongea kifaransa , nimeshangaa kwani unaonekana kujua kuongea Kiswahili na Kingereza pekee”Aliongea Roma.
“Haya niambie ni jambo gani limekuleta kwenye ofisi yangu?”
“ Nimekumiss mke wangu”Aliongea Roma na kumfanya Edna akose utulivu lakini wakati huohuo kujisikia vizuri hajawahi kuambiwa maneno ya moja kwa moja hivyo.
“Niambie umekuja kufanya nini kuwa siriasi”Aliongea Edna.
“Kuna rafiki yangu nataka apatiwe ajira ana CV nzuri na GPA kubwa ya uhandisi wa majengo , ila sina koneksheni ya kumsaidia , Wife unaonaje ukimsaidia mumeo kwenye hili”Aliongea Roma na kumfanya Edna amwangalie na kisha akafikiria kidogo.
“Siwezi kukusaidia bure”Aliongea Edna na kumfanya Roma ashangae , alijikuta akitabasamu na kuona mke wake sasa hivi anakuwa mjanja sasa.
“Bebi wife unataka nifanye nini ili unisaidie”
“Ninapanga kufungua kampuni mpya ya Burudani na Habari na mtu wa kuisimamia kampuni hio napanga uwe wewe”Aliongea Edna na kumfanya Roma atoe macho.
Ukweli Edna alikuwa amepanga baada ya kufanikisha swala la mkataba wa Yamakuza,faida atakayopata kupitia Malighafi mpya atumie kufungua kampuni nyingine mpya itakayohusika na maswala ya habari na Burudani , kampuni ambayo itakuwa na kituo cha Television ,nia na madhumuni ya kutaka kufungua kwa kampuni hii , alitaka kupunguza Gharama za matangazo , kwani Vexto ilikuwa ikitumia Zaidi ya bilioni tano kwa mwaka kwa ajili ya matangazo lakini pia kulipa mabalozi wa bidhaa zao, hivyo aliamini akifungua kampuni ambayo itakuwa inahusisha maswala ya habari na burudani ni rahisi kwake kupromote bidhaa zake, pasipo kutumia kiasi kikubwa cha pesa , lakini pia mrembo huyu alipanga pia kampuni hio ampe Roma aiendeshe ili kukuza hadhi yake , hakupenda ije kufahamika mume wake ni mfanyakazi wa kawaida ndani ya Vexto.
“Wifey hilo swala la kuongoza kampuni siliafiki hata kidogo”Aliongea Roma na kumfanya Edna amwangalia kwa maswali, ni kama alitegemea upinzani kutoka kwa Roma.
“Kama hutaki basi sahau kuhusu rafiki yako kupata ajira”Aliongea Edna huku akirudisha macho yake kwenye tarakishi yake,Roma alimwangalia Edna.
Ukweli sio kama Roma hakupenda kuongoza kampuni, ila hakutaka kazi ambazo zitamfanya kufikiria, na hii ni kutokana na ugonjwa wake,Profesa Clark alimpa ushauri Roma wa kutofanya kazi ambayo itakuwa inaumiza kichwa.
“Wife hakuna namna nyingine ya kumsaidia rafiki yangu?”
“Roma mimi msimamo wangu ndio huo, ukikubali kuwa Director wa kampuni ambayo nitaifungua rafiki yako nitampa mkataba wa kazi wa kudumu na mshahara mzuri”Aliongea Edna na kwa namna ambavyo Roma alimuona mke wake ni kwamba alikuwa siriasi.
“Kuongoza kampuni sio jambo gumu sana Roma , kuna wataalamu ambao watakusaidia kufanya majukumu yote , wewe itaiuwa ni kutia sahihi tu na kutoa baadhi ya maagizo”Aliendelekea kuongea Edna na alionekana kumshawishi Roma.
“Okey !,Wife tufanye umeshinda , utampa rafiki yangu mkataba wa kazi wa kudumu na mshahara mzuri na mimi nitaongoza kampuni”Edna alijikuta akitabasamu , hakudhania jambo lake litaenda kirahisi hivyo,kwani usiku wote alikuwa akifikiria namna ya kumshawishi Roma juu ya jambo hilo.
“Hii ndio mbinu nzuri ya kumfanya awe siriasi na maisha,Anaweza kuona nafanya haya yote kwa faidia yangu ila ni kwa ajili yake”Aliwaza Edna.
Ni muda wa saa moja za jioni Roma alimuaga Edna na Bi Wema kama anatoka ila atarudi , na baada ya kutoka moja kwa moja alielekea Mbutu kwenye makazi ya The Eagles , alikuwa na mchecheto kweli wa kujua ni jambo gani The Eagles wameweza kulifanikisha kuligundua katika kazi aliowapaitia , kazi ambayo ilikuwa ni juu ya kumfatilia mtu aliekuwa akifahamika kwa jina la The Don ,lakini pia kujua muunganiko uliokuwepo kati ya Edna na Seventeen.
Dakika chache mbele alikuwa akiingia ndani ya kambi hii na leo ilikuwa tofauti kidogo , kwani alikuwepo Deigo pekee na Bram ndani ya jumba hili.
“Mfalme Pluto habari za wakati huu?”
“Salama Diego , naona vijana wengine siwaoni?”Aliongea Roma na kumfanya Diego kutabasamu kidogo
“Vijana wameenda kukutana na wapenzi wao”Aliongea Deigo na kumfanya Roma kushangaa.
“Usiniambie wote nane wamepata wapenzi?”
“Hahaha..Ndio mfalme Pluto ni mimi na Bram ambaye mpaka sasa tupo Single”
“Diego na ujanja wako wote umeshindwa kupata mchumba hapa Tanzania au hawakuvutii”.
“Mfalme Pluto wanawake wa Tanzania ni warembo sana na nimejaribu bahati yangu na kupata mmoja , tatizo limekuja anaonekana kupenda sana hela kuliko mapenzi”Aliongea Diego na kumfanya Roma acheke hakujua Diego ni mbahiri kiasi hiko.
“Nimeijia Ripoti Diego naomba usinipe nisome , nataka unielezee ili iwe rahisi kuelewa”Aliongea Roma na kuegamia kwenye sofa na Diego alichukua kishikwambi kilichokuwa kwenye meza na kupapasa kwa dakika kadhaa na kisha akakohoa kidogo alionekana kuwa na mzuka kweli.
“Mfalme Pluto nitaomba kuanza na taarifa ya The Don”Aliongea Diego na Roma alimpa ishara ya kuendelea.
“Kwa namna ambayo vijana wetu wameweza kukusanya taarifa , lakini pia kwa namna ambavyo marafiki zetu walio ndani ya MOSSAD walivyotusadia tumegundua yafuatayo”Alipozi kidogo.
Diego alieonekana kuwa na mchecheto juu ya taarifa hio na kwa Roma pia alijikuta akipata msisimko kwani hakudhania kama ripoti ya The Don imewafanya The Eagles mpaka kutumia mashushu(The Eagles wanaita mashushu marafiki) wao walio ndani ya kitengo cha kijasusi cha Taifa la Israeli cha MOSSAD.
“Kwanza kabisa mfalme Pluto tumegundua The Don ni jina tu la utambulisho ambalo halina muunganiko na mfanyabiashara yoyote wa madawa ya kulevya hapa nchini”
“Unamaanisha nini Diego?”
“Mfalme Pluto katika hatua zetu za kuchimba Zaidi Tumegundua The Don hahusiki moja kwa moja na biashara inayohusu madawa ya kulevya”Aliongea Diego na kumfanya Roma kushangaa.
“Wafanyabiashara wote wa madawa ya kulevya hapa Tanziania hakuna hata mmoja ambaye ashawahi kumuona huyu mtu ambaye anafahamika kwa jina la The Don, wakati tunafatilia taarifa tulikisia huenda Mheshimiwa Kigombola ndio mtu anaejiita The Don, lakini tulichogundua nikwmaba Mheshimiwa Kigombola sio The Don na hata yeye mwenyewe hamfahamu huyu mtu”
“Kwahio unamaanisha kwamba ndani ya Tanzania hakuna mtu ambaye anamfahamu The Don?”Aliuliza Roma.
“Ndio Your Majesty Pluto , ndani ya Tanzania hakuna anaemfahamu mtu anaefahamika kwa jina la The Doni licha ya kwamba wafanyabiashara wote wa madawa ya kulevya na wale wakufanya biashara ambazo sio halali ,kama vile kusafirisha viungo vya binadamu wanalipa kamisheni ya mapato yao kwenda kwa The Don”
“Diego hapo umenichanganya , umesema huyu mtu hawamjui , kwanini wanalipa mapato kwenda kwake?”Aliuliza Roma na Diego alitabasamu.
“Mfalme Pluto hilo ndio swala ambalo limetufanya tufuatilie kwanini wafanyabiashara wakubwa wa biashara ambazo sio halali wanalipa kamisheni kwa mtu ambaye hawamfahamu”
“Kwahio mmegundua nini?”
“Kwanza kabisa kutokana na kwamba tulikosa taarifa ambazo zinahusiana na huyu The Don kutokana na kwamba watu wengi hawamfahamu hapa Tanzania, tukafanya maamuzi ya kufuatilia usajili wa akaunti ya benki ambayo wafanyabiashara hawa hulipia Kamisheni , na tulichogungua ndio kilichotufanya kuwasiliana na marafiki zetu waliondani ya MOSSAD”Aliongea Diego na kupapasa kishikwambi chake kwa dakika moja.
“Kwanza kabisa baada ya kufuatilia kuhusu hii akaunti ya Benki, tuligundua ni Akaunti iliosajiliwa mwaka 1990 ndani ya Swiss Bank na Nyaraka ya vidhibiti vilivyoambatanisha jina la HEGEMONI , lakini licha ya jina hili pia tuliweza kugundua jambo ambalo sio la kawaida, tumegundua akaunti hii hupokea miamala ya fedha kila kona ya dunia na kila muamala unahusisha biashara ambazo sio halali”
“Hegemoni?”
“Ndio mfalme Pluto na baada ya sisi kufatilia kuhusu hili jina la Hegemoni tulishindwa kupata taarifa na hapo ndipo tulipowatafuta marafiki zetu kutoka MOSSAD na walitupatia taarifa ya kushitusha kidogo , ambayo wote hapa ndani imetushangaza kidogo”
“Taarifa gani?”
“HEGEMONI is uknown person”
“HEGEMONI hafahamiki”Roma alishangaa inawezekana vipi watu waweke fedha kwenye akaunti ambayo mtu anaeimiliki hio akaunti hafahamiki.
SEHEMU YA 98
Hegemony katika Ugiriki ya kale ni neno lenye maana ya kikundi au nchi yenye nguvu ya kutawala wengine aidha kwa njia ya utamaduni , Dini ,Kijeshi au kiuchumi.
“Mfalme Pluto kwa maelezo marahisi ni kwamba The Doni wa Kenya ndio huyu huyu wa Tanzania na The Doni wa Mexico ni huyu huyu wa kitanzania”Aliongea Diego na kumfanya Roma atafakari , kama kweli maneno ya Deigo ni kweli basi huyu mtu anaejiiita The Doni ni mtu ambaye ana nguvu kubwa sana, lakini pia hata kama mtu huyo ana nguvu ni kwa namna ipi ameweza kuwa’control’ wafanyabiashara wakubwa mpaka kumtii na kumlipa , hilo ndio swali ambalo liliibuka kwenye kichwa cha Roma.
“Mfalme Pluto tumeweza pia kugundua The Doni kwa kila taifa ana mwakilishi wake”
“Kwa hapa Tanzania mwakilishi ni nani?’
“Kwa hapa Tanzania tumegundua mwakilishi mkuu wa The Doni ni mheshimiwa Kigombola”
“Unamaanisha Raisi Mstaafu ndio anamwakilisha The doni?”
“Ndio Mfalme Pluto”
“Kama ni kweli , ni kwa njia gani Kigombola ameweza kukutana na huyu The Doni , kwani haiwezekani awe mwakilishi pasipo ya wao kukutana”
“Ndio mfalme Pluto, na sisi mpaka sasa tunafanyia swala hilo kazi kujua ni kwa namna gani hawa wawili wanafanya mawasiliano , lakini pia ni kwa namna ipi The Doni kawa na nguvu ya kumfanya Mheshimiwa Kigombola kumtii ,na sio kwa Tanzania tu kwa kila taifa , tunajitahidi kuweza kujua ni kwa namna gani na kwa nguvu ipi the Doni ameweza kuwafanya wawakilishi wake kumtii ”Aliongea Diego.
“Ndio ripoti imeisha hivyo Diego?”
“Hapana Mafalme Pluto Ripoti inaendelea”alipozi kidogo na kupangusa upande kishikwambi chake kwa dakika kadhaa.
“Mfalme tumeweza pia kugundua licha ya akaunti hii inayomilikiwa na Hegemoni kuingiziwa pesa kila kona ya dunia , tumegundua pia jambo ambalo limetushangaza kidogo”.
“Lipi hilo Diego?”
“Tumeweza kugundua pia kuna miamala ambayo imetoka kwenye hii akaunti tofauti na ile ambayo inaingia”Roma alishangaa.
“Kwahio unamaanisha kuna watu wanatoa pesa kwenye hii akaunti ,kama ni hivyo hao watu ni nani?”
“Mfalme Pluto kwa tulivyowezakufuatilia benki ya Swiss imetoa kadi mbili tu za aina ya ‘Black Card’ kwa watu wawili na hao watu wawili ndio ambao wanatoa hela kwenye hii akaunti, kutokana na msaada wa MOSSAD kupata taarifa haikuwa ngumu kwetu ,na kwa taarifa yao wametupatia majina mawili ambayo ndio wanatoa pesa kwenye hii akaunti na jina la kwanza ni la Yan Buwen na jina la Pili ni Dorisi Alex”.
“Na taarifa za hao watu zipoje”Aliuliza Roma na Diego alitabasamu na kisha alipangusa kwa dakika kadhaa na kisha akampatia kishikwambi kile Roma.
Roma macho yalimtoka ni kama taarifa ambayo alikuwa akiisoma haikua ya ukweli , kwani aliweza kuona taarifa za Dorisi Alex ambaye alikuwa akimjua kabisa na sio kumjua tu lakini pia alikuwa mpenzi wake , jambo hili lilimshangaza na hakuelewa hili linawezekana vipi.
Kwa maelezo ya Diego The Doni alikuwa ni kama mtawala wa biashara haramu zote, kutokana na kwamba The Doni wa Tanzania ndio The Doni pia ambaye yupo kwenye mataifa mengine na hii ni kutokana na kwamba pesa zote za kamisheni kwa wafanyabiashara wa Madawa ya kulevya na zile ambazo ni haramu nyingine pesa yao ilikuwa ikienda kwenye akaunti moja inayotambulika kwa jina la Hegemoni.
“Diego kuna uhakika wa huyu Dorisi kumiliki kadi ambayo inatoa pesa kwenye hio akaunti?”
“Ndio mfalme Pluto na tuliweza kuihakiki kabisa hii kadi baada ya vijana kuingia ndani ya nyumba anayoishi Dorisi na hizi ni picha za kadi ambayo anamiliki Dorisi”Roma alizinagalia picha hizo na ni kweli ni kadi ya yenye jina la ‘Platinum’ ya rangi nyeusi.
“Kwahio mnahisi ni uhusiano gani ambao Dorisi anao na The Doni mpaka kumiliki hii kadi?”
“Mheshimiwa Pluto hilo hatujaweza kulipatia ufumbuzi , ila tumeweza kufatilia taarifa za Dorisi kwanzia wazazi wake na asili yake kwa ujumla”
“Na mkagundua nini?”
“Wazazi wa Dorisi walipotea kwenye mazingira ya kutatanisha mwaka 2010 hio ni kwa taarifa ya jeshi la Polisi la Tanzania na mpaka sasa ‘They are Declared Dead”Roma aliona hii ripoti inaanza kuumiza kichwa chake , maana kila kitu kilikuwa kipya kwake.
“Kuna sababu zozote za hao wawili kupotea kwao , na walikuwa na kazi gani hapa Tanzania?”
“Walikuwani wamiliki wa mgodi wa Almasi huko Mwadui”
“Vipi kuhusu Yan Buwen?”
“Yan Buwen ni mwanasayansi ngazi ya PhD na jambo la kushangaza Zaidi ni kwamba Profesa aliesimamia masomo yake ya ngazi ya juu ni Profesa Clark”Roma aliendelea kushangaa.
“Vipi kuhusu wazazi wake, kuna taarifa yoyote ambayo inamuunganisha huyu Yan Buwen na Dorisi?”
“Yan Buwen wazazi wake wote wapo hai na ni raia wa China na mpaka sasa wapo hai na ni familia yenye nguvu ndani ya Beijing na hakuna muunganiko wa aina yoyote na Dorisi Zaidi ya kuwa na kadi za Black Card”
“Okey! Diego nipatie hio Ripoti ya The Doni nitaipitia mwenyewe taratibu , lakini nadhani kuna kazi kubwa Zaidi ya hii kuhusu huyu the Doni nataka muendelee kuchimba taarifa zake mpaka tupate kujua ni nguvu gani anayo huyu mtu na pia tufahamu ni nani”
“Sawa Mfalme Pluto”
“Nielezee na taarifa ya Edna na Seventeen , kwanini wanafanana kama mapacha na muunganiko wao , nadhani mnataarifa ya kutosha”
“Mfalme Pluto kwanza kabisa niende moja kwa moja kwenye hitimisho la uchunguzi wetu, kwanza mpaka sasa tuna makisio ya juu ya Madam Edna na Seventeen kuwa mapacha”
“Ushahidi uliowapelekea kuwa katika hayo makisio ni upi?”
“Kwanza tumegundua Edna baba yake halisi ni Raisi wa Rwanda Mheshimiwa Jeremy ”Roma alitoa macho.
“Na huu ndio ushahidi wa kuonyesha Rahel mama yake Edna na Mheshimiwa Jeremy walikuwa na mahusiano ya muda mrefu tu ambayo yalikuwa ni ya siri”alimpa Picha Roma na ni kweli kwenye picha Rahel na Mheshimiwa Jeremy walikuwa wakionekana kwenye ufukwe wakiwa wamekumbatiana kimahaba , fukwe ambayo Roma kwa kuangalia tu aliweza kuijua.
“Mmeweza kupata vipi hizi picha?”
“Bram aliweza kufanikisha kuhack Emaili ya Mheshimiwa Jeremy na tuliweza kusoma baadhi ya jumbe na viambatanisho ambavyo vimetoka kwa Jeremy kwenda kwa Raheli kwa muda tofauti tofauti na hapa ndipo tulipoweza kufungua kodi na kujua wawili hawa walikuwa na mawasiliano , lakini licha ya kujua jambo hili kuna meseji tatu ambazo kidogo zimetushangaza na ndio zilizotupelekea kujua Edna na Seventeen wanaweza kuwa ndugu wa damu”
“Meseji gani?”
“Hizi hapa Mfalme Pluto”Alimpatia tena kishikwambi na Roma aliweza kusoma jumbe hizo.
1.“Najutia maamuzi yangu Jeremy ya kukukabidhi loraine ,huenda maka sasa ningekuwa na watoto wangu wote mapacha”
2.”Raheli najua ni namna gani unaumia , lakini hili swala naomba liwe siri kwa Edna kama amezaliwa na dada yake”
3.”Raheli kabla sijafa nitahakikisha nalipiza kisasi kwa wote na nitahakikisha naujua ukweli juu ya kilichonyuma ya ajali ya ndege ya M Airline”.
Hizo ndio jumbe ambazo Roma aliweza kuzisoma na kumshangaza kwa wakati mmoja na kwa meseji hizo ni kweli Edna alionekana kuzaliwa na pacha wake anaefahamika kwa jina la Lorraine, lakini bado haikumthibitishia kama Seventeen ni Lorraine anaetajwa kwenye hizo jumbe na yeye swala hilo likabaki kwenye makisio.
“Kama kweli Lorraine ni Seventeen ilikuwaje mimi na yeye tukawa ndani ya kile kisiwa”Aliwaza Roma.
Ukweli ni kwamba Roma hakuwa na kumbukumbu zozote za maisha yake ya nyuma , kwani kumbukumbu alizokuwa nazo ni za Sehemu ambayo yeye mwenyewe anaita kisiwa , lakini kuhusu kumbukumbu ni kwa namna gani aliweza kuingia kwenye hiko kisiwa akiwa pamoja na Seventeen haikueleweka.
Sasa Roma anatambua kuwa baba yake Edna ni Raisi wa Rwanda , swali bado linabaki kwenye kichwa chake , kama baba yake Edna ni Raisi wa Rwanda yeye baba yake ni nani na mama yake ni nani , asili yake ni ipi?”.
Hakukua na kubwa sana kutoka kwenye Ripoti ya Diego dhidi ya Edna na Seventeen Zaidi ya kujua kuwa mama yake Edna alikuwa na mahusiano na Jeremy Raisi wa Rwanda.
Roma aliingia kwenye gari yake kuianza safari ya kurejea nyumbani , hakuwa na jambo lingiine la kumfanya kuwa ndani ya hio kambi , aliona atapitia ripoti hio kwa umakini akiwa nyumbani.
Roma akiwa njiani bado mawazo hayakumuacha salama , alikuwa akiwaza hili na kurukia jambo lingine.
“Kwanini Dorisi amiliki kadi inayotoka kwa The doni , wana uhusiano gani , au yeye anamfahamu huyu The Doni , Huyu Yan Buwen ana uhusiano gani na The Doni na yeye kumilikishwa kadi ya kitajiri , wazazi wa Dorisi kwanini wapotee”Roma aliwaza Zaidi mpaka kupelekea kichwa chake kuwa kizito na alihisi kitampasuka , alijiambia kwa sasa hatakiwi kuwaza Zaidi , kazi hio ya kuwaza viijana wake wataifanyia kazi , yeye jambo la kufanya kwa wakati huo ni kutuliza kichwa.
Ilikuwa ni saa nne za usiku , Roma hakujisikia kabisa kurudi moja kwa moja nyumbani , alitamani atembe tembee ili kupata hewa safai ndani ya eneo hili la Kigamboni.
Roma alikuja kusimamisha gari yake pembeni mwa barabara kuu , mita kadhaa kutoka Pongoni Beach.
Alishuka kwenye gari na kuanza kutembea taratibu kuelekea upande wa ilipo hii Beach na siku hii ndani ya hili eneo kulionekana kuna burudani iliokuwa ikiendelea ndani ya hayo maeneo kwani watu aliokuwa akipishana nao walikuwa ni wengi licha ya muda kwenda , lakini pia alikuwa akisikia Mziki uliokuwa mbele yake , alitembea taratibu huku akifurahia upepo wa fukwe.
Baada ya kutembea kama mita mia moja hivi alijikuta akisimama sehemu ambayo ilikuwa na kibanda kama kiosk , ambacho kwa haraka haraka aligundua kibanda hiki kilikuwa ni cha chips , haikueleweka alivutiwa na nini lakini alikisogelea na wakati uleule walionekana watu wawili msichana na Mvulana wakisogelea kile kibanda.
“Tufungie Chips na mishikaki minne”Aliongea yule mvulana.
“Sawa”Sasa Sauti hii kidogo ilimshangaza Roma ilikuwa ni ya kike na hili ndio jambo ambalo lilimvutia na mtu aliekuwa akiuza kwenye hilo eneo ni kama ashawahi kumuona , alisogea mpaka karibu na hapa ndipo alipogundua hisia zake zilikuwa ni za kweli , alikuwa ni mwanadada aliemchomolea waleti kwenye Mwendokasi.
“Anko!”Aliita yule msichana ambaye aliikuwa na ushombe ushombe ambao Roma alishindwa kuujua ni wa muunganiko mtu mweusi na mtu gani.
Roma alikaa kwenye benchi lililokuwa pembeni bila ya kuongea neno huku akimwangalia bidada huyu alivyokuwa akihangaika kuwahudumia wateja wake.
SEHEMU YA 99
BOLIVIA –AMAZONI 1990
Ni ndani ya mwaka 1990 miezi minne tu baada ya kijana Levente pamoja na Profesa Banosi kupigwa Risasi nchini Hungaria ndani ya mji mkuu wa Budapest .
Ndani ya sehemu moja iliokuwa katikati ya Msitu wa Amazon kilomita kadhaa kutoka mji mkuu wa La Paz , ilionekana Chopa iliokuwa ikiambaa ambaa angani ndani ya msitu huu , huku ikiwa na nembo ya Jeshi.
Ndani ya chopa hii walionekana wanaume wawili waliokuwa kwenye mavazi ya suti na miwani usoni pamoja na marubani wawili ambao walikuwa na umakini wa hali ya juu sana kuendesha ndani ya eneo hili la huu msitu , wanaume wote wawili ambao walikuwa wamevalia suti walikuwa ni wazungu , kwa haraka haraka wanaume hawa wawili walikuwa kati ya umri wa miaka arobaini hivi , kwa aliekuwa ameketi upande wa kushoto alionekana kuwa mkubwa Zaidi kuliko wa upande wa kulia.
Baada ya Chopa hii kutembea kwa umbali wa kilomita kama moja hivi mbele upande wa chini lilionekana jengo ambalo lilikuwa limejengwa kwa mabati magumu sana kwa muuno wa mshale , lakini pia kwa duara.
“We are Landing Sir”aliongea Rubani upande wa kushoto akiwaangalia wanaume waliovalia suti na hawa wanaume walipeana ishara ya kukubali.
Dakika chache mbele Chopa hii ilianza kushuka chini taratibu ikilikaribia jengo hilo ambalo kadri mabwana hawa walivyokuwa wakilikaribia lilikuwa likiongezeka ukubwa , huku upande wa chini wakionekana baadhi ya wanajeshi ambao walikuwa wakilinda, na wanajeshi hawa kwa mavazi yao haikueleweka walikuwa ni wa jeshi gani kwani mavazi yao hayakuwa na nembo yoyote licha ya kushikiria siraha nzito kwa kuzunguka eneo hilo lote ambalo pia limezungushiwa waya.
“Mr Anderson I am happy to see you again”Aliongea mwanamama mmoja hivi alievalia suti ya Zambarau mrefu kidogo aliekuwa rika la ujana.
“Me Too Mellissa”aliongea Mr Anderson ambaye alikuwa ni yule mzee kidogo na Mellisa alimgeukia yule mwanaume mwingine ambaye alionekana mtu mzima lakini mdogo kwa Andersson.
“Mellisa kutana na Mr Cohen ni Mafadhili mpya wa Project yetu,Mr Cohen huyu ni Mellisa Luiz ndio Meneja ndani ya hii kambi ya Pro Human”Aliongea Anderson na Mellisa alimpa mkono Coheni kusalimiana nae na walianza kupiga hatua kuelekea ndani ya jengo hili ambalo lilionekana kuwa kubwa kwa muonekano wa chini kuliko ilivyokuwa juu, lilikuwa limejengwa na mabati magumu na muonekano wake ulikuwa ni kama kiwanda , na pia kulikuwa na sauti ya mvumo wa Sauti ya majenereta ndani ya hili eneo.
“Banosi was Real Amaizing Anderson , This is Beyond my Expectations”Aliongea Coheni huku wakiangalia kupitia kioo vitoto vichanga ambavyo vinaonekana kwenye makabati ya vioo , na kilichomfanya mzee huyu ashangae ni namna ambavyo ubongo wa vichanga hivyo ulivyokuwa ukionekana kwenye Screen.
“Your Gradfather was Great Scientist Cohen and with this Discovery we are going To Create the God`s hahaha..”Aliongea Anderson na kutoa cheko na kumfanya Mellisa kutabasamu.
Kwa jinsi sehemu hii ilivyokuwa ikionekana , ilionyesha kama maabara ya kisasa kabisa , kwani kulikuwa na machine za kisasa zilizofungwa.
Wakati mabwana hawa wakiendelea kushangazwa na maendeleo ya Projekti yao , mara aliingia mwanajeshi mmoja aliekuwa ameshikilia bunduki lake na kumfanya Mellisa ageuke na kumwangalia Mlinzi huyu.
“What is it Carlos?”
“There is Problem Mellisa. which need your attention”
“What! , Which Problem”Aliongea mwanamama huyu huku akiongoza njia nakuacha mabosi hawa ndani na Carlos alifuatisha nyuma na walikuja kusimama kwenye mlango ambalo ulikuwa na bango kwa juu ‘CCTV control And Monitoring Room’.
Wakati Mellisa anaingia kwenye chumba hiki ,Alarm ya jengo hili ilianza kutoa mlio wa kuashiria kuna uhatari uliokuwa ukitaka kutokea na kufanya wanajeshi wote waliokuwa wakilinda wajiandae kukabiliana na tatizo , lakini ilikuwa ni jambo la Ghafla sana , kwani ile Mellisa anakimbilia nje kwa spidi ulisikika mlio ‘Vuuum’.
“Boom” ‘Boom’
Ulikuwa ni mlipuko ambao haukuwa wa kawaida ambao uliacha eneo lote kuwaka moto , kwa haraka haraka mlipuko huu ulisababishwa na mabomu ambayo ,yalionekana kutegwa na mtu ndani ya eneo lote la hapa ndani.
Haikueleweka kuna mtu ambaye aliweza kusalia ndani ya hili eneo kwani moto ulikuwa ni mwingi sana na ulikuwa umezingira karibia eneo lote.
Baada ya kama nusu saa hivi kupita kilometa kadhaa kutoka lilipo hili eneo , alionekana bwana ambaye alikuwa kwenye mavazi ya suti akikimbia huku akionekana kubeba mtoto ambae amemviringisha kwenye mavazi ya bluu ambayo ni kama ya hospitalini , huyu bwana alikuwa ndie alietambulishwa kwa jina la Cohen.
Alikuwa akihema kama mbwa huku akizidi kusonga mbele na baada ya dakika chache za mwanaume huyu kukimbia hatimae aliweza kufika eneo ambalo lilikuwa na uwazi na kupunguza mwendo huku akigeuza shingo kulia na kushoto , kama mtu ambaye alikuwa akitafuta mtu, hili eneo halikuwa hata na aina yoyote ya kuonesha kama lilikuwa na mtu , kwani Zaidi ya keleleza ndege pamoja na wanyama , hakukua na sauti yoyote ya kuashiria kuna binadamu anaeishi ndani ya haya maeneo.
“Ryan.!!”Ilikuwa ni sauti ya mwanamke, ilisikika katikati ya huu msitu na kumfanya bwana huyu asimame na kugeuza macho kulia na kumuona mwanadada wa kizungu akimkimbilia kwa spidi , huku akionesha hali ya shauku kwenye uso wake.
“You did it, Our Plan worked”Aliongea huyu mwanadada huku akimsogelea Ryan kwa mwendo hafifu ni kama hakuwa akiamini.
“Epholia we got our Daughter Back!, We did it”Aliongea yule bwana huku akionesha furaha na hamasa kwenye macho yake huku akimfunua taratibu yule mtoto.
Kwa jinsi walivyokuwa wakionekana hawa wawili ni Dhahiri kabisa aliekuwa kwenye mikono ya Ryani ni mtoto wao wa kike , walionesha hali ya hamasa na furaha kwenye macho yao.
Ryani alimpa Epholia yule mtoto na baada ya kumpa alivua suti na shati alilokuwa amevaa na kujifinya kifuani na kuvuta ngozi kwa juu na palepale alionekana kama mpira ukijitengenisha na ngozi, alitumia mkono wa kushoto na kuingiza kidole kwa chini na kikapita kwenye ngozi na akavuta kwa juu na hapa ndipo ilipoonekana akijivua gamba la Juu na kila kitu kikabadilika , bwana huyu alikuwa mtu mwingine kabisa tena lika la ujana , hakuwa Cohen tena.
Wakati wakiwa wamesimama kwenye hili eneo , mara walianza kusikia sauti za mvumo wa Chopa kutoka mbali ikija uelekeo wao na kuwafanya waangaliane na kukimbilia ndani kabisa ya msitu.
Hii ilikuwa ni miaka ya Tisini, tukio hili linahusiana vipi na hii simulizi , utaelewa mbele.
****
“Unaitwa nani?”Aliuliza Roma mara baada ya wale vijana ambao walikuja hapo kwa ajili ya kununua chipsi kuondoka.
“Yezi”Alijibu huku akigeuza geuza viazi vilivyokuwa vikichemka na mafuta na Roma alishangazwa na hilo jina.
“Sasa Yezi huogopi kufanya kazi usiku wote huu?”
“Hakuna wakunigusa , ndio maana”Aliongea Yezi na kumfanya Roma atabasamu , alifurahishwa na namna ambavyo Yezi alikuwa akijiamini.
“Anko kama umekuja kuniuliza maswali naona tu uondoke maana nipo kazini”Aliongea Yezi.
“Unapaswa kunishukuru kwa kukuachia salama baada ya kuniibia waleti yangu”Aliongea Roma lakini muda huo zilikuja pikipiki nne ambazo zilikuwa zikitokea barabra kuu na Roma macho yake ya haraka haraka aliweza kutambua watu waliokuwa wakiendesha hizi pikipiki ni vijana wadogo na Wote walikuwa ni mashombe shombe kama ilivyo kwa Yezi, ila hawa Roma aliweza kuwatambua kama mchanganyiko wa Arab na Mbongo.
“Yezi unajifanya sana mjanja na leo tumekukamata , lazima ulipe hela yetu”Aliongea kijana mmoja hivi kwa rafudhi ambayo ilidhihirisha sio mzawa.
“Abdull yule jamaa nilidhani anatudanganya kumbe ni kweli huyu choko kahamia huku”Aliongea kijana mwingine na Roma aliendelea kuwaangalia tu hawa vijana , hakuelewa ni kipi kinaendelea , lakini alitaka kuona mwisho wake.
“Sharif tulishamalizana , kwanini mnaendelea kunighasi na maisha yangu”
“Hahaha,,acha kujifanya mjanga Yezi nani kakuambia unaweza kufanya kama unavyotaka, hatukukulazimisha kujiunga na kundi letu lakini hauwezi kutoka kwa hiari , lazima ulipie”Kwa jinsi ambavyo vijana hawa walivyokuwa wakiongea Roma aliona kama wavuta bangi tu , ila alitulia kwenye benchi huku akimwangalia Yezi aliekuwa bize pasipo kuwazingatia hawa vijana.
“Sharif unamuona alivyonadharau , mnaonaje tukichukua kila kitu na tujajilipizia , japo naamini pesa tunayomdai haiwezi kutoka kwenye hiki kibiashara”Aliongea Dogo Abduli na walisogea upande wa karai lililokuwa likichemka na dogo mmoja ambaye alikuwa mkimya muda wote alisukuma kalai lililokuwa likichemka na mafuta yake chini kwa kutumia Helmeti na kumfanya Yezi amwangalia na kupandwa na hasira.
“Sharif mnataka nini kwangu , si tulishamalizana mbona mnanifanyia hivi kila siku hamtaki kunipa Amani”
“Unaongea sana Yezi”Aliongea Sherif na kuvuta kabati la chipsi na likatua chini na kumfanya Yezi akasirike na kumpiga na chujio la kuepulia chipsi.
“Arrghh”alitoa mguno wa maumivu na baada ya wenzao kuona mwenzao kajeruhiwa walimzunguka Yezi na kumshika mikono na Abduli alimsogelea na kumsindilia ngumi ya tumbo na kumfanya Yezi agugumie kwa maumivu , walimpiga na mtama wakamuweka chini kwenye mchanga na dogo ambaye hakuwa muongeaji sana alichukua sahani ambayo ilikuwa ikitumika kupimia Chipsi na kuchota mchanga ambao ulikuwa umechanganika na mafuta ya moto yaliomwagika na kumsogelea Yezi.
Roma aliona sasa hawa madogo wanazidi manyanyaso , alimsogelea yule dogo na kumvuta kwa juma na kumpiga kibao na kudondoka pembeni.
“Haya ondokeni”Aliongea Roma kuamrisha wale vijana lakini walionekana kukasirika maradufu kwani Sherif alichukua chujio lile la kuepulia na kumsogelea Roma kwa dhamira ya kumpiga nalo , lakini ni kama Roma alikuwa ametegemea kwani kabla hata hajamfikia alimfyeka mtama na kudondoka chini.
“Anko nyuma yako”Aliongea Yezi ambaye aliachiliwa sasa na hawa vijana na kuona wamdhibiti Roma , na kuna mmoja aliekuwa kwa nyuma alieshikilia jiwe kwa ajili ya kumpiga Roma na kabla hata ya Yezi hajamtahadharisha , yule Dogo alirusha , lakini Roma ni kama masikio yake yalikuwa na macho kwani alikwepa kidogo na likaenda kumpata Abduli ambaye alikuwa akinyanyuka huku akijifuta mchanga.
“Mamaaa….!!!”Alitoa ukulele , lakini sasa muda huo huo ilikuja gari ya Doria iliokuwa na polisi na kuwazingira , ilikuwa ni ghafla sana
SEHEMU YA 100
Vijana ni kama hawakuwa wametegemea polisi kuja eneo hilo , kwani walishindwa hata kujitetea, polisi wale waliwashika mmoja mmoja na kuwafunga pingu hawakukata maelezo
“Nyie ndio Mnaofanya wananchi wanalamikia polisi kwa kutofanya kazi yake kwa weredi na leo mtatutambua”Aliongea polisi mmoja mwembamba huku akimfunga Yezi pingu mikononi, walionekana hawakutaka kujua kabisa ni nini kilikuwa kikiendelea hapa kwenye hili eneo na waliona kila mmoja alikuwa ni mhalifu , hata Roma mwenyewe walimuona kama mhalifu tu.
“Gondwee mfunge huyo mpuuzi ,ndio litukutu likubwa hilo”Aliongea polisi ambaye alionekana kiongozi na kumpiga Roma bao la mgongoni.
“Aaah ! Maafande namna gani sasa hii ya kupigana na usiku wote huu”
“Tulia Ngederec wewe , unajifanya mjanja ngoja tukakushikishe adabu na hiki kiburi lazima kitaisha”Aliongea huku akimfunga Roma pingu na Roma hakutaka kuleta ubishi alikubali kufungwa pingu.
Watu waliokuwa wanapita walishangaa kile kilichokuwa kikiendelea kwa polisi hao , ila hakuna ambaye alijaribu kuuliza , kila mtu aliendelea na mambo yake , lakini pia na wenyewe waliogopa kujumrishwa.
Dakika kama kumi tu hivi Roma na wale vijana watukutu walisweka kwenye difenda na ikaondolewa hapo kwa kasi kuelekea kituoni, Roma alishangazwa na aina hii ya utaratibu wa polisi ila hakutaka kuleta ubishi , alitaka kuona mwisho wake.
Vijana walionekana kuwa na wasiwasi ila kwa Roma hakuwa na wasiwasi na baada ya dakika kama nane hivi waliingizwa ndani ya kituo cha polisi.
“Wamefanyaje hawa tena?”Aliongea mwanamama mmoja ambaye amevaa mavazi ya kipolisi , ni kama alikuwa akiwafahamu hao vijana.
“Walikuwa wanaleta vurugu Afande , watalala leo hapa kituoni”.
“Afande huyu Anko hana kosa alikuwa akinisaidia tu”
“Kimya wewe mbuzi”
“Oya Afande hebu niachieni nataka niondoke”Aliongea Roma ambaye alikuwa amekarishwa kwenye benchi na yule mama alimwangalia Roma.
“Hawatatuachia hawa mpaka asubuhi”Aliongea Yezi.
“Nilale hapa polisi kwa kosa lipi?”Aliongea Roma kwa sauti na kusogelewa na polisi na kupigwa buti mguuni.
“Tukisema tulia tulia wewe nguruwe”Aliongea polisi mwembamba huku akimwangalia Roma kwa hasira.
“Hawa watoto kila siku sio wenye kusikia , kila siku ni wenye kufanya fujo tu ,Wewe Sherif umesahau onyo la baba yako wiki iliopita , kwanini unapenda kuleta fujo”aliongea yule mama huku akimwangalia Sherif lakini kijana huyu hakuongea lolote Zaidi ya kununa na kuzika kichwa chake chini.
“Afande Mnene , unaonaje kwanza ukiuliza nini kimetokea , maana nipo hapa kimakosa” Aliongea Roma lakini mwanamama alionekana kutomzingaria na kumfanya Roma apandwe na hasira.
“Anko usiwe hivyo , watatuachia asubuhi”Aliongea Yezi lakini Roma hakutaka kubaki ndani ya hili eneo, lakini pia hakutaka kutumia mabavu kutoka , alitaka atii sheria ilia toke lakini polisi walionesha kutomsikiliza.
“Chief!!”Ilikuwa ni sauti ya afande Mnene akisimama wima baada ya mwanamke mmoja ambaye pia alikuwa kwenye mavazi ya kipolisi kuingia , Roma aliinua macho yake na kumwangalia huyo alieitwa chifu na kuona huenda huyo anaweza kumsikiliza , lakini baada ya kumwangalia tu alimfahamu , kwani alikuwa ni Mage.
“Okey! Afande Mage Bora hata umekuja nadhani nitawahi kwenda nyumbani”Aliongea Roma na kumfanya Mage ambaye hakuwa amemuona Roma ageuke na kumwangalia.
“Mr Roma unafanya nini hapa?”
“Waulize hao polisi”Aliongea Roma na Mage aliwageukia polisi akitaka maelezo.
“Afande walikuwa wakifanya fujo Pongoni Beach” Aliongea polisi mwembamba na Mage aligeuza macho kuangalia wale vijana ambao wote baada ya Mage kuingia hapa ndani waliinamisha vichwa vyao chini , ni kama hawakutaka Mage awaone na hata kwa Yezi pia , Mage alisogea na kuinua kichwa cha Sherifu.
“Ni nyie wajinga”Aliongea Mage na alionesha kuwafahamu hao vijana, alisogea kwa kila mmoja na kumwangalia na akamalizia kwa Yezi na kujikuta akitabasamu.
“Afande unaweza ukamuachia Mr Roma pale , nitadili na hawa vijana”Aliongea Mage na wale polisi walijikuta wakishangaa , lakini hawakutaka kubisha , alichukua ufunguo na kumfungulia Roma na kutoa zile pingu.
“Afande Mage mimi sijaleta fujo ni Sherifu na wenzake ndio waliokuja kunianza kwenye eneo langu la biashara”Aliongea Yezi na alionesha kumfahamu Mage na kumfanya Roma ashangae.
“Yezi kaa kimya ,Sherifu unakumbuka nilikupiga mpaka ukazimia Osterbay , mpaka ukanifanya nipewe adhabu ya kuwa trafiki na kutolewa kwenye cheo changu sasa nasema hivi, mimi Mage kwakua umenifuata tena nitahakikisha mkitoka hapa akili zimewakaaa sawa”Aliongea Mage na hapa hakujali tena uwepo wa Roma hapo ndani na Roma ambaye alikuwa ameruhusiwa kuondoka , alibakia hapo hapo ndai kuona ni nini kinaendelea, hakutaka kuondoka akimuacha Yezi ilihali hakuwa na makosa.
“Afande Mage!,Unaonaje ukiuliza kwanza nini kimetokea kuliko kuanza kuwatishia”Aliongea Roma kwa sauti ya kawaida na kumfanya Mage amwangalie.
“Mr Roma usharuhusiwa , unaweza kuondoka , hawa vijana nawajua sana tu ni waharifu wa kupindukia na wanahistoria ya kukamatwa na polisi Zaidi ya mara tano”
“Lakini Yezi hahusiki, hawa madogo ndio wamekuja kumfanyia fujo mwenzao”Aliongea Roma na kumfanya Yezi amwangalie Roma alijisikia vizuri kwani ni mara yake ya kwanza kupata mtu wa kumtetea.
“Ndio Afande Mage mimi sihusiki , walikuja kunifanyia fujo , nilishaachana na kundi la Sherif na ndio maana nikahamia hapa Kigamboni kuanza maisha upya”Aliongea Yezi na alionesha hali ya kuogopa mara baada ya kuingia Mage.
“Anachoongea ni kweli Koplo?”Aliuliza Mage.
“Afande …”
“Hauna haja ya kuwauliza hao wapuuzi , wamekuja eneo la tukio na wakatusweka mpaka hapa pasipo ya kujua sababu , hawaelewi chochote hata tukio lilivyokuwa”Aliongea Roma .
“Chunga kauli yako , upo polisi hapa Mr Roma usijifanye kwasababu unafahamina na Chief unaweza kututukana , aliongea Koplo akimsogelea Roma na Roma alijikuta jaziba ikimpanda na alisimama haraka sana na kumpiga mtama Koplo na alitua chini kama furushi na Roma hakuishia hapo tu alimkanyaga kwenye vidole vya mikono na kumfanya bwana huyu atoe ukulele wa muamivu.
Yezi na vijana watukutu walijikuta wakishangazwa na namna ya Roma kujiamini , ilikuwa ni mara yao ya kwanza kushuhudia Polisi akipigwa ndani ya kituo cha polisi.
“Polisi mnakosaje utimamu wa akili , mnaweza vipi kulinda raia kwa staili hii”Aliongea Roma na kumwachia na kisha akamsogelea Sherifu na kunnyanyua juu.
“Wewe ndio utaelezea tukio zima na ole wako udanganye”Aliongea Roma kwa sauti ya kuamrisha , lakini Sherif hakutaka kuongea , aliangalia chini kwa jeuri na Roma hakutaka kumchelewesha alimning`iniza hewani na mkono mmoja na kumfanya aanze kukohoa huku akitapatapa.
Sio Mage tu hata polisi wenzake walishangazwa na nguvu alizokuwa nazo Roma lakini pia ujasiri wake.
“Utaongea huongei?Au ni kuvunje shingo?”.
“Roma muachie utamuua”Aliongea Mage kwa wasiwasi , lakini Roma ni kama hamsikii alizidi kumminya Sherif mpaka pale alipokata moto ,alimtupia chini, na kufanya polisi hawa wamsogelee Sherif kwa wasiwasi.
“Mmoja wenu ajitolee kuongea la sivyo mtafuatia mmoja mmoja”Aliongea Roma na vijana hawa watatu waliobaki , walianza kuangaliana kwa wasiwasi.
“Mnajifanya mabubu sio , Nitaanza na wewee”
“Nitaongea…”Alinyanyuka Abduli kwa pupa .
Abduli alianza kuelezea tukio kiuwoga woga , kwenye maisha yake hakuwahi kukutana na mtu wa aina ya Roma na ndio maana aligopa.
“Afande nadhani mpaka hapo Yezi hana kosa”Aliongea Roma.
“Yezi unaweza kwenda ila nakutahadharisha tu kama umebadili tabia yako iwe kweli , siku ukiletwa polisi ninakupeleka gerezanni moja kwa moja”Aliongea Mage
“Afande Mage , nimebadilika kweli nishaachana na kuwa mtoto mtukutu”
“Maneno yako yawe kweli”Aliongea Mage na kisha akamgeukia Roma , alishindwa kwanza kuelewa kwanini Roma alikuwa nje muda huu wa saa nne mpaka kukamatwa na polisi wakati ameoa na anatakiwa kuwa na mke wake nyumbani.
“Afande Mage kazi njema”Aliongea Roma huku akimshika Yezi bega wakitaka kutoka.
“Roma tunaweza kuongea kidogo”Aliongea Mage na kufanya Askari hawa washangae ni ukaribu gani Mrembo Mage na Roma wanao.
“Sawa”aliitikita Roma na Mage alitoka na Roma mpaka kwenye kijibaraza.
“Unasemaje ?”
“Mbona unauliza kwa usiriasi hivyo Roma kama hatufahamiani , au ushasahau sisi ni marafiki”Aliongea M,age na kumfanya Roma atabasamu.
“Haya ongea Mage”
“Kwanza nina shida na namba yako ya simu”Aliongea Mage pasipo kupepesa macho na kumfanya Roma ashangae , hakuwahi kuombwa namba ya simu na mwanamke kwa namna hio,Mage alimpa simu Roma aandike na Roma alitabasamu na kisha akachukua simu na kuandika.
“Kwahio shida ilikuwa namba yangu tu?”
“Hapana !, hilo ni la kwanza la pili nilikuwa nikitaka tuonane kesho jioni kama utakuwa na muda”Yaani Roma alimuona Mage kama mwanamke mbabe kwani licha ya kwamba alikuwa akiomba lakini sauti yake ilikuwa ni kama amri.
“Usifikirie sana Roma kuna jambo tu ambalo nataka kukushirikisha”
Roma hakuona haja ya kumkatalia Mage , kwanza alikuwa na shauku ya kutaka kujua kwanini Mage alikuwa akitaka kuonana nae , na kwa jinsi ambavyo Roma alimuona Mage , hakumuona kama mwanamke ambaye alikuwa akitaka kuongea nae habari za mapenzi hivyo alikubali moja kwa moja na kurudi ndani.
“Anko!”Ilikuwa ni sauti iliomfanya Roma ageuze shingo mara baada ya kutoka getini la hiki kituo na kumuona Yezi aliejibana kwenye kona ya ukuta.
“Hujaondoka tu , unasubiri nini , au ndio unaogopa giza?”
“Hapana nilikuwa nakusubiria”
“Mh!, haya twende nikusindikize urudi ulipoacha vitu vyako”
“Sidhani kama nitavikuta pale ,na kwa jinsi Sherifu na wenzake walivyovitupa tupa sidhani”
“Twende tukaangalie acha kudhanna”aliongea Roma na hata wazo la kuwahi nyumbani limepotea katika kichwa chake na sasa ilikuwa ni Zaidi ya saa tano.
“Ilikuwaje mpaka ukajiunga kwenye kundi la watoto watukutu kama wale tena ukiwa msichana?”Aliuliza Roma wakati wakitembea taratibu.
“Ni Stori ndefu sana Anko , walikuwa ndio marafiki zangu wa kwanza kukutana nao baada ya kutoroka kituo cha kulelea watoto yatima”Aliongea na kumshangaza Roma.
“Kwahio na wewe ni yatima?”
“Yeah! Nahisi hivyo , niliambiwa na walezi wangu niliokotwa kwenye geti la kituo”
“Ukiwa na miaka mingapi?”
“Nadhani mwaka mmoja , hawakuwa na uhakika pia ,hakukua na taarifa zozote kuhusu mimi au wazazi wangu Zaidi ya jina langu pekee”Roma alishangazwa na historia hio .
“Sasa kwanini ulitoroka?”
“Ni Stori ndefu , ila kikubwa sikupenda maisha ya kituoni, na baada ya kutoka ndio nikakutana na Sherifu ndio wakanishawishi kuingia kwenye kundi lao na kutokana na kwamba sikuwa na pesa hata ya kula nililazimika kufanya hivyo”Roma hakutaka kuuliza maswali mengi sana alimuonea tu huruma kwani maswala kama hayo yalikuwa ni kawaida pia hata kwa baadhi ya nchi ambazo zimeendelea.
Walivyofika eneo kwenye kile kibanda ni kama ilivyokuwa mategemeo ya Yezi , hakukuwa na chombo cha aina yoyote, kila kitu kilikuwa kishachukuliwa , jambo ambalo lilimfanya Yezi kutoa machozi , licha ya kwamba taa za hapa ni hafifu , lakini Roma alishuhudia machozi ya Yezi.
“Anko asante kwa wema wako leo wa kunitetea kule polisi , lakini pia kunisindikiza mpaka hapa , unaweza sasa kuondoka nisikucheleweshe”Aliongea Yez huku akimpa mgongo Roma.
“Sasa unaficha hayo machozi ya nini wakati nishakuona unalia?”
“Anko naomba uondoke” Roma aliangalia eneo hili kwa nmna ya kukagua
“Kwahio unalipa wema wangu kwa kunifukuza?”Yezi aligeuka.
“Kwahio unataka nikulipe nini, wakati unaona kila kitu nilichopigania kwa zaidi ya miezi minne kimepotea na sasa nakwenda kuanza upya naomba uondoke?”Aliongea kwa sauti ya kukasirika.
Roma alijipapasa mfukoni na kuibuka na noti za dola mbili , Dola mia mia , haikueleweka alikuwa ameziweka mfukoni muda gani.
“Kama unataka niondoke , nitaondoka ila chukua hii pesa itakusaidia”
Yezi aliangalia pesa iliokuwa kwenye mikono ya Roma kwa dakika kama moja, huku akionesha kufikiria na bila ya kuongea lolote alimpita Roma na kuelekea barabarani na jambo hili lilimshangaza Roma, ila alimfuata.
“Yaani nakusaidia unanikimbia au ndio unanidharau”
“Anko sikia mpaka hapa uliponisaidia panatosha , sitaki msaada wako Zaidi”
“Kama hutaki msaada wangu , unaonaje ukinipa kitu chochote cha Thamani ulichonacho na ukachukua hii pesa kama mkopo na siku ukifanikiwa unanirudishia pesa yangu,”aliongea Roma hivyo kwani alikuwa ashamfahamu Yezi ni msichana wa aina gani , aliona ni wale wasichana ambao walikuwa wakiogopa kufanyiwa wema ambao umezidi.
“Unahisi kwa umasikini huu nitakuwa na kitu gani cha Thamani?”
“Wewe ndio ufikirie kama una kitu cha thamani unipatie kama huna nitaondoka”
“Sina”
Alijibu Yezi kwa sauti na kufanya watu waliokuwa kwenye mgahawa mita kadhaa kutoka waliposimama , ndani ya eneo hili wawaangalie, na kwa haraka haraka walitafsiri Roma anabembeleza akalale na Yezi, na Roma aliona watu walivyokuwa wanawaangalia ila hakujali.
“Okey Yezi kwakua huna kitu cha Thamani naondoka”Aliongea Roma na kweli akaanza kuondoka huku akimuacha Yezi aliesimama.
“Anko!,Subiri”aliognea Yezi na kumkimbilia Roma huku akijishika shingoni.
“Nitakupa hii cheni yangu , ndio kitu pekee ambacho nimeokotwa nacho kama utambulisho , ila imepita miaka mingi nimewasubiri wazazi wangu na sidhani kama watakuwa hai, unaweza ukanitunzia, ndio kitu cha thamani nilicho nacho kwenye maisha yangu”Aliongea Yezi na kutoa cheni ambayo alikuwa ameiweka mfukoni kwenye suruali yake ya Jeans.
Roma macho yalimtoka mara baada ya kuangalia ,ilikuwa ni Necklace(Mkufu) ulioambatana na Pendant(kidani)
Baada ya Roma kuiangalia macho yalimtoka kutokana na aina ya pendant hio.
“Inakuwaje mtoto kama huyu akamiliki kitu kama hiki?”Aliwaza Roma huku akigeuza kidani hiko nyuma na mbele ni kama alikuwa akitafuta hitilafu , alitoa simu yake na kumulika
“Ni ya uhakika”Aliongea na kisha akainua macho yake na kumwangalia Yezi na wakakutanisha macho.