Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEASON 04

SEHEMU YA 91

Roma baada ya kusoma kikaratasi kilichokuwa kimeachwa na kundi la Kijapani lililokuwa likifahamika kama Yamata Sect , alin`gata meno kwa hasira.

Alietembea uelekeo wa chumba cha mazoezi na baada tu ya kufika alifungua sehemu ambayo alikuwa ameficha kiboksi alichokuwa ametoka nacho kutoka Mbagala na baada ya kukitoa , alikifungua ndani na akatoa kijiwe flani hivi ambacho kilikuwa na ukubwa wa Goroli , ni jiwe ambalo kwa kuliangalia tu halikuwa lakawaida kabisa , kwani mara baada ya Roma analitoa kwenye kile kiboksi na kupigwa na mwanga wa jua lililotoa mg`ao Flani wa bluu , mg`ao ambao ulikuwa ukiumiza macho.

Roma aliweka kile kijiwe mfukoni na akatoka ndani ya nyumba hii baada ya kufunga vizuri na alianza safari ya kutafuta Mabwepande kama alivyokuwa ameelekezwa ,kutokana na spidi yake ya kuendesha alitumia Zaidi ya dakika arobaini hivi , aliingia ndani ya msitu wa Mabwepande.

Aliegesha gari yake na kisha akasonga mbele kwa mguu kutokana na kwamba barabara ilikuwa imefikia ukomo , alipita nyumba kadhaa chache zilizokuwa ndani ya haya maneo na kutokomea juu kabisa msituni na ile anatembea kwa dakika kama kumi hivi aliweza kuwaoona watu aliokuwa akiwatafuta, walikuwa wapo watatu na wote walikuwa wajapani , wakwanza alikuwa ni Tanya , kulikuwa na Tanuki ambaye Roma alikuwa akimfahamu na mwingine alikuwa akifahamika kwa jina la Tengu,Tanya alionekana akiwa ameketi kwenye gogo huku akiangalia kucha zake.

“Yuko wapi Edna na Bi Wema?”Aliuliza Roma mara baada ya kuwafikia kwa mita kadhaa.

““Your Majesty Pluto, don’t get impatient. If you want to see them, we have to see God’s Stone.”

“God’s Stone is in the pocket of my pants, but I want to ensure the safety of the hostages”(Jiwe la Kimungu lipo kwenye mfuko wangu , nataka kuwaona kwanza ili kuhakiki kama wako salama)

“Hehe”Alicheka Tanuki

“The mighty ‘Beheading of Ten Thousand People’ is indeed worthy of its title. The Death God Hades who has slain countless lives unexpectedly came to negotiate for the life of an ordinary woman using God’s Stone.”

“Mtu mwenye uwezo wa kuua watu Zaidi ya elfu moja,Mungu wa wafu ambaye amechinja na kuua watu wasiohesabika leo hii amekuja kumuokoa mwanamke wa kawaida kwa kutumia Jiwe la kimungu”Aliongea Tanuki kwa kejeli. Na leo alikuwa akitumia kingereza tu.

“Your Majesty Pluto, I really got a bit jealous as a woman myself”

“Mfalme Pluto najukuta mwenyewe kuona wivu kama mwanamke”Aliongea Tanya huku akitabasamu

“Acheni kuongea upuuzi , sijaja kuokoa maisha ya mtu mmoja , mmeteka watu wawili,halafu sio mwanamke wa kawaida kama mnavyodhania”Aliongea Roma huku hasira zikionekana kwenye macho yake

“Usiwe na wasiwasi kama utatupatia Jiwe la kimungu tutakurudishia mwanamke yule mzee, na baada ya kuturuhusu kukimbia kwa umbali wa kilomita moja bila ya kutufukuzia tutakuambia ni wapi mkeo alipo kwa kutumia njia zetu maalumu za kuwasiliana , na usije ukathubutu kutudanganya au kufanya jambo lolote la kijinga , ukifanya hivyo tutahakikisha humuoni mkeo mrembo”Aliongea Tanuki.

“Kwahio mnanitishia?”Aliuliza Roma kwa hasira.

“Mfalme Pluto tunajua kwamba hupendi kutishiwa kwenye maisha yako , tunachokuambia ni jambo jepesi sana , tupatie jiwe umpate mkeo na mpaka sasa muda unaenda na zikipita dakika chache huenda mkeo akapatwa na shida”

Roma alijikuta akipandwa na jaziba sana , aliingiza mkono wake kwenye mfuko , aliona hakuwa na jinsi Zaidi ya kuwapatia kile walichokuwa wanataka , ili amuokoe mke wake

Baada ya kutoa kile kijiwe alichokuja nacho , Tanya , Tengu na Tanuki walijikua wakitoa macho kwa furaha , ukweli ni kwamba licha ya kwamba walikuwa wakisikia kuhusu jiwe la kimungu , lakini hawakuwahi kuliona laivu.

“Mfalme Pluto umekuja nalo kweli .. hahaha tupatie sasa chapu”

“Nataka kumuona kwanza Bi Wema kama yupo salama ndio niwapatie”

“We swear upon the dignity of the warriors in Japan, as long as you give us God’s Stone, we’ll definitely give the two hostages back to you safely”

Tunaapia kwa hadhi ya miungu ya kivita ya kijapani , kama utatupatia hilo jiwe ni uhakika lazima tukurudishie familia yako ikiwa salama”aliongea Tengu.

“Huna haja ya kutaja hadhi ya Miungu ya Japani , sidhani kama mnaijua hata maana ya hio hadhi”Aliongea Roma huku akijiandaa kuwarushia jiwe upande wa Tanuki, lakini wakati ule ule uliskika mvumo wa visu kumpita Roma kwa spidi kuelekea upande wa wale wajapani na , wale wajapani wakavikwepa.

“Wewe ni nani?”Aliongea Tanya kwa sauti na kufanya sauti yake ijirudie rudie kwenye huu msitu na muda huo huo alitokea Ajenti flamingo aliekuwa akihema , alionekana amekuja hapo kwa spidi kweli.

“Ajenti flamingo umekuja kufanya nini?”Aliuliza Roma.

“Nimekuja kukupatia taarifa , Jenerali wa jeshi ameniagiza , usije ukatoa hilo jiwe”

“Wewe na huyo Jenerali wenu hamuwezi kunifanyia maamuzi , jiwe ni la kwangu na nina uhuru wa kufanya maamuzi ninayotaka”Aliongea Roma.

“Ndio Ajenti Flamingo , tunakujua sana kabla ya kuja hapa Tanzania ,na unatakiwa kufikiria vizuri , tunachoongea hapa ni dili la Maisha ya mke wake Hades na Jiwe la Kimungu ni bora ukakaa kimya”Aliongea Tanuki.

“Acha kuongea , unatakiwa uelewe hapa ni Tanzania na sio kama hatuna uwezo wa kuwafanya chochote, Mpo kwenye ardhi yetu msijifanye vijogoo”aliongea Magdalena huku hasira ikionekana kwenye macho yake.

“Unaongea sana mrembo , lakini sidhani kama wewe unamaamuzi , sisi tunaongea na Pluto hapa na yeye ndio atafanya maamuzi ya kuacha familia yake ife au atupatie jiwe la kimungu”Aliongea Tanya na Flamingo akaachana nao na kumuangalia Roma kwa macho ya huruma.

“Hades tulikuwa tunataarifa ya juu ya uwepo wa hilo jiwe hapa nchini na uhatari wake likifikiwa watu mashetani kama hao na tulikuwa tukiamini kwamba hautowapa watu wabaya ,hivyo tunaomba usifanye hivyo , jeshi la Tanzania lina jukumu la kulinda hilo jiwe”

“Magdalena licha ya wewe kuwa mwanajeshi , Edna ni rafiki yako , kwanini unaweka maslahi mbele zidi ya maisha ya mtu”Aliongea Roma

“Naelewa na pia najisikia vibaya , lakini naheshimu sheria za jeshi, na jambo unalotaka kulifanya linahatarisha usalama wa dunia kwa wakati mmoja,Na pia Jenerali Mstaafu Athumani kaniagiza jiwe hilo lisitolewe kwa namna yoyote ile”

Unajua baada ya General Yang kuja Tanzania na kuomba kuundwe kikosi ambacho kitakuwa na kazi ya kulinda jiwe la kimungu ambalo lilikuwa kwenye mikono ya Roma , kikundi hiko kiliundwa na mkuu wa kikundi hiko alikuwa ni jenerali mstaafu Athumani babu yake Edna.

“Hahahaha…Acha kunichekesha ,huyo mzee kwa maelezo ya Edna ni kwamba anataka Edna amuite babu , lakini leo hii anasahau kuwa Edna ni mjukuu wake na anataka kumuacha afe kwa ajili ya kijwe kama hiki ambacho kwanza sio cha kwake na hata hajui kilipotoka”

“Hades Jenerali anafanya haya mambo kwa ajili ya usalama wa raia wa dunia yote , kwanini unashindwa kuona hili , mtu yupo tayari kutoa mjukuu wake kwa ajili ya usalama wa watu wengi”

“Hayo ni juu yenu , mimi Hades siwezi kutoa kafara familia yangu kwa kajiwe kama haka , tena mke wangu , hapana yaani nina uwezo hata kwa kuuza dunia nzima kwa ajili ya kuokoa familia yangu , nyie mnaojiita jeshi kama mnaona ni sawa kwa kutoa familia zenu kwa ajili ya kulinda taifa na usalama wa raia ,sidhani mpaka miaka ijayo mtakuwa na familia, huwezi ukajiita unalinda nchi huku ukishindwa kulinda familia yako , nchi inaanzia kwenye familia , ukiwa na mtu unaempenda utapata hamasa ya kulinda taifa, kwani usalama wa raia unahusisha na familia yako , sasa mnachoongea ninyi ni upuuzi”

“Vyovyote vile Hades nimetuwa hapa kuhakikisha hilo jiwe haulitoi , wanajeshi wetu wanakuja na hawa watu hawatafanikiwa kuondoka”

“A living entrepreneur is far more useless than a dead person to the country,I can’t afford to risk Edna life. I won’t complain to trade this stone for my wife’s life.”Aliongea Roma na kisha akarusha jiwe kwenda kwa Tanuki.

“Hahaha ..Hades wewe unabusara sana”Aliongea Tanuki kwa furaha baada ya jiwe la kimungu kutua kwenye mikono yake.

Ajenti flamingo machozi yalianza kumtoka hakuelewa ni kipi anaenda kueleza wakuu wake juu ya jambo ambalo Roma alikuwa amelifanya.

“Roma kwanini umefanya jambo la kijinga namna hio , ni kweli umewapa hilo jiwe?”

“Magdalena tafahdari naomba usinipigie kelele juu ya hilo jiwe mimi kwangu halina thamani”

“Kwa hio unamaanisha Edna ni muhimu kwako kuliko maisha ya watu wa dunia hii?”Aliongea huku machozi yakimtoka ,alionekana kuwa mwanamke ambaye alikuwa na machozi ya karibu.

“Magdalena ngoja nikwambie , sio Edna tu mwanamke wangu yoyote yule ambaye unamjua wewe ana umuhimu mkubwa kuliko hako kajiwe”

“Hehe….Sikujua Mfalme Pluto unapenda warembo kiasi hiki,Watu unaowatafuta wapo kwenye hii karatasi”Aliongea Tanuki huku akitoa karatasi na kuipuliza na mdomo wake na ikamsogelea Roma na kuidaka.

Na palepale Tanya na Wenzake walitoweka , Magdalena alitaka awkimnbize lakini alishindwa kabisa , aliishia kumwangalia Roma kwa hasira.

Roma baada ya kuangalia ile karatasi alijikuta akitoa matusi , watu ambao alikuwa akiwatafuta walikuwa wapo kulekule kigamboni.

“Hades jenaral atasikitishwa sana na hili jambo , nasema kwamba kwenye jambo la kijinga ulilolifanya ni hii leo , sijui kwanini hata unaitwa Pluto”aliongea Magdalena.

“Acha kunipigia kelele Magdalena na ukiendelea kunisumbua nitakwenda kumuua huyo Jeneral unaenipigia nae kelele”Aliongea Roma na kuondoka.

Roma aliamua kupiga simu kwa The Eagles na kuwapa maelekezo ya sehemu ambapo Edna na Bi Wema walipo ,maana alijua hatopata muda wa kuwafikia kama atataka kuwaokoa yeye mwenyewe.

Chiara na John baada ya kupata maekekezo kutoka kwa Mfalme Pluto waliondoka haraka sana kwenda eneo husika.

Ilikuwa sio mbali sana na eneo la Mbutu , wale wajapani walionekana kukodi kabisa nyumba na walioekana walikuwa hapo kwa muda mrefu kidogo , kwani ndio sehemu ambayo walikuwa wamewaweka Edna na Bi Wema na jambo la kusikitisha ni kwamba walikuwa wamewafunga kwenye Swimming Pool , ambayo haikuwa na maji na wakaachia maji yanayoingia kidogokidogo na kujaa , na kama Roma angechelewa kidogo kuwaifikia Yamata Sect , basi huenda Edna na Bi Wema wangezama kwani mpaka The Eagles wanafika maji yalikuwa yamewafikia kwenye kifua.

Edna baada ya kumuona Mzungu mwanadada, alijikuta moyo wake ukitulia sasa kwani alikuwa na wasiwasi mwingi na mtu aliekuwa akimuonea huruma ni Bi Wema , kwani miguu ishaanza kumvimba tayari kwa ubaridi wa maji.

“Malkia Persephone , Tusamehe kwa kufanya haya yakufikie ni uzembe wetu katika kazi , Mfalme Pluto katuagiza tuje kukuokoa”

Aliongea Chiara kwa heshima na kumchanganya Edna hakujua kwanini anamwita Malkia na hakuelewa huyo mfalme ni nani , na pia hakutaka kuuliza , licha ya kwamba hakuwa na maelezo ya kutosha juu ya Roma kuwa na hawa wazungu ambao walionekana kumfanyia kazi , kwa muda huo alihitaji kutolewa kwenye maji kwanza.
 
SEHEMU YA 92

Roma alitumia dakika chache tu kufika Kigamboni , aliingia haraka haraka mara baada ya kuegesha gari yake na kukimbilia ndani , kumwangalia Edna na Bi Wema.

Edna alikuwa amekaa sebuleni akiwa na Bi Wema na mtu wa tatu ambaye alimshangaza Roma kuwepo hapa ndani , mtu huyu hakuwa mwingine bali alikuwa ni Mage, tena leo hii hakuwa kwenye mavazi ya kitrafiki bali ya kipolisi.

Roma alijiuliza huyu mwanamke kaja hapo nyumbani kufanya nini , kwani kwa kumbukumbu zake hakuwa na kosa lolote alilolifanya.

“Wife pole kwa yaliokukuta , Bi Wema pole kwa yaliowakuta wewe na Edna , mnisamehe kwa kutowapa ulinzi wa kutosha”Aliongea Roma

“Mr Roma usijisikie vibaya , yaliotukuka sio kwa sababu yako , ni majambazi tu waliokuwa wakihitaji pesa na kututeka”Aliongea Bi Wema na Roma alimgeukia Edna.

“Unabahati haukulala nyumbani huenda ungetekwa na sisi”Aliongea Edna na Roma alitoa tabasamu la uchungu na kwa jinsi alivyomuona Edna ni kama hakuwa akijua ni watu gani walikuwa wamemteka.

Roma aliinua macho yake kumwangalia Mage ni kama alitaka kujua ni kwanini mwanamke huyu alikuwepo hapa ndani, na Edna alimuona Rma alivokuwa akimwangalia Mage.

“Mage kaja baada ya mimi kuwasiliana na kituo cha polisi juu ya tukio lililotupata , sikujua kama kwasasa ni mkuu wa kituo cha polisi cha Kigamboni”Aliongea Roma.

“Ahaa,,niliogopa nikajua amekuja kunivalisha pingu”aliongea Roma na kumfanya Mage ajisikie vibaya kutokana na maneno yake.

“Edna nitarufi kituoni , naona hali yenu kwa sasa imekuwa sawa, nina majukumu mengine”

“Sawa Mage nadhani tutaonana mara kwa mara”

“Ndio nitakuwa nakuja kukutembelea”Aliongea Mage na kisha akamwangalia Roma.

“Roma naomba tuongee hapo nje mara moja”Aliongea Mage kibabe na hakusubiria jibu , alitoka na Roma alikosa namna , na yeye alitoka huku Edna akijiuliza ni kitu gani Mage anataka kuongea na Roma.

“Niambie Afande Mage ni jambo gani unataka kuongea na mimi”

“Roma najua tunahistoria mbaya baina yetu , lakini haimaniishi kama sisi ni maadui , nataka tusahau yaliopita na tuanze upya”Aliongea Mage na kumfanya Roma atoe macho , hakuelewa ni nini Mage alikuwa akimaanisha.

“Afande Mage mimi wala sina tatizo na wewe , ulikuwa kwenye majukumu yako ya kazi , hivyo sioni kama ni jambo baya kwa kile ulichofanya”

“Okey! Kama unaelewa , unaonaje tukiwa marafiki?”Aliongea Mage na kumfanya Roma ashange , hakuelewa kwanini ghafla afande Mage anataka kuwa na urafiki na yeye.

“Mimi sina tatizo”aliongea Roma.

“So you mean…?”

“I mean yes Friend we are”Aliongea Roma na kumfanya Mage kwa mara ya kwanza atabasamu mbele ya Roma na kuudhihirisha urembo wake.

“Okey Bye”Aliaga Mage na Roma alitabasamu na kuingia ndani , Edna alikuwa akimwangalia Roma muda wote , haikueleweka alikuwa akifikiria nini.

“Siiii..chaaaaa..!!!”Ilikuwa ni chafya kutoka kwa Edna , alionekana na yeye alikuwa ameathiriwa na maji , kwani Roma alipewa taarifa zote na Chiara jinsi alivyowakuta Edna na Bi Wema.

“My Darling wife pole,Bi Wema ngoja nikawatafutie dawa, nikirudi nitaandaa kifungua kinywa”Aliongea Roma na kumfanya Edna amwangalie Roma nikama alikuwa hajamsikia vizuri,ilaRoma hakujali , alitoka kwa ajili ya kwenda kutafuta dawa

*****

Upande wa Ajenti flamingo baada ya Roma kuondoka , Ajenti flamingo alibonyeza kifaa kilichokuwa karibu na sikio lake.

“Afande Roma Keshaondoka na Jiwe kalikabidhi”Aliongea

“Ajenti flamingo , Rudi kikosini na ongoza wanajeshi kuwafukuzia hao wajapani , nitawasiliana na wanajeshi walio mipakani kwa ajili ya kuwasaidia”ilisikika sauti upande wa pili.

“Sawa Afande”

“Vipi huyo Hades kaelekea wapi, au ndio anawafatilia hao wajapani”

“Hapana Afande anaonekana kuelekea nyumbani Afande”

“Okey! Fanya kama nilivyokuelekeza”

Ajenti Flamingo alirudi alipokua amekiacha kikosi kwa ajli ya kuendelea akuwafukuzia Yamata Sect.

“Upande mwingine ndani ya msitu uliokuwa ukipatikana Tanga na Kenya , walionekana wale wajapani wakitembea kwa spidi , walionekana walikuwa wakitaka kuwahi kutoka nje ya Tanzania , ili wasije wakakamatwa na wanajeshi wa kitanzania.

“We got it… Finally hahaha… we got it! We can become gods… become gods!”

““Lord Tanuki, let me take a look. Is this rock really that impressive?”

“Lord Tanuki naomba na mimi nilione hilo jiwe”Aliongea Tengu.

“Tengu , kaa kwa kutulia , hili jiwe tumefanikiwa kulipata kutokana na mpango wangu niliopanga mwenyewe , sitompatia mtu mpaka nimkabidhi Master”Aliongea Tanuki akiwa siriasi

“Mbona unaongea kama vile haujiamini , ulidhani mimi na Tanya tutakuibia Crediti zako tukilishika Tanuki, kwanini unataka kulishika wewe mwenyewe au una mpango wako kichwani?”

“Tengu acha kuongea ujinga ,mimi ni muaminifu sana kwa Master ,usiongee vitu ambavyo havipo”Aliongea Tanuki kwa hasira na alionekana kitendo chake cha kushika jiwe la Kimungu limemuongezea hali ya kujiamini.

“Tanuki kabla hatujaja hapa Tanzania , mimi ndio niliokabidhiwa uongozi wa hili kundi letu , haijalishi kwamba mpango wako ulifanikiwa , lakini mimi ndio kiongozi na ukinidharau mimi ni kumdharau Master”Aliongea Tanya.

“Hahah..Tanya japokuwa nakupenda , lakini jiwe nitamkabidhi mimi Master na nitakubali kupokea adhabu yoyote na baada ya hapo nitaomba Master tufunge ndoa”aliongea Tanuki kifedhuli.

“Tanuki mimi kama kiongozi wako na kuamrisha mpe Tengu hilo jiwe alishike yeye”Aliongea Tanya akiwa na hasira.

“Achenni kuongea upumbavu , siwezi kutoa hili jiwe , mimi ndio niliolichukua kwenye mikono ya Hades , siwezi kupatia watu msio na maana kama nyie”

“Hehe..jigambe tu , hujui hapo ulipo unakufa”Aliongea Tengu na kumshangaza Tanuki.

“Umamaanisha nini?”Aliongea Tanuki kwa hasira

Lakini wakati uleule Tanya alipotea alipokuwa amesimaa na ile anatokea alikuwa mbele ya Tanuki , lakini Tanuki ni kama alimtegemea , na yeye alitoa panga lake kiunoni na kumkinga Tanya, lakini wakati huo huo Tengi na yeye hakuwa nyuma alirusha Daga, na ikamchana Tanuki kwenye mkono kiasi cha kumtoa Damu.

Tanuki hakutaka kufa kizembe, alijua alikuwa na mbinu nyingi Zaidi ya hawa wawili aliokuwa akipigana nao, alijitoa kwa sarakasi karibu na Tanya na kurudi nyuma , lakini Tanya alimzidi akili kwani ile anarudi alirudisha upanga kwa spidi na ile Tanuki anakuja kutua , upanga ulipita kwenye koo lake , na aliishia kutoa macho kwa namna ambavyo alidhibitiwa na ukawa mwisho wake.

‘Huna thamani kwetu”Aliongea Tanya na kisha aliingiza mkono kwenye mfuko wa Tanuki na kutoa jiwe linalowakawaka na kisha akamrushia Tengu alishike , alitoa kichupa kidogo na akamnywesha Tanuki aliekuwa akitapatapa kushindana na kifo.

Na pale pale wakapeana ishara na wakapotea eneo la msituni.

*****

Roma alitembea kwenye maduka yaliokuwa yapo wazi kwa ajjili ya kununua dawa za kuwasaidia Edna na Bi Wema , ilikuwa ni muda wa asubuhi hivyo hakukuwa na shida sana , kwani maduka mengi yalikuwa yamefunguliwa , tatizo kwa Roma nikwamba hakujua ni dawa ipi inafaa kwa ajili ya kutibu.

Wakati akikaribia na duka la dawa mara alisogelewa na bwana mmoja ambaye alikuwa amevalia suti , mrefu mweupe.

“Naitwa Faridi ni mlinzi wa karibu wa Jenerali Athumani”

“Ndio bwana Faridi kwanini upo hapa?”Aliuliza Roma akimkagua huyu bwana ambaye kwa kumwangalia tu Roma alijua kuwa mtu aliekuwa mbele yake alikuwa na mafunzo ya Kung Fu.

“Nimekuletea dawa niliopewa na Afande Athumani kwa ajili ya Edna”aliongea Faridi.

“Roma alipokea zile dawa na kuzingalia , ilikuwa ni mizizi ambayo haukuezielewa , alichojua tu ni kwamba ni dawa za asili”

“Hizi ni dawa gani?”

“Ni za Asili kutoka China , Zinaweza kutibu magonjwa Zaidi ya hamsini m unachotakiwa ni kuchemsha na kumpatia Edna na Bi Wema”Aliongea Faridi na kwa jinsi alivyokuwa akiongea ni Dhahiri alikuwa akiwajua sana Edna na Bi Wema.
 
SEHEMU YA 93

Roma hakujali sana juu ya Babu yake katoa dawa hizo , alizipokea na kutembea taratibu kuelekea uelekeo wa nyumbani , kwani hakuwa amekuja na gari , wakati akiwa njiani alikutana na mama mmoja aliekuwa anauza vijikeki flani hivi.

“Baba nunua Kashata”Aliongea mwana mama huyu baada ya kumsimamisha Roma.

“Ndio vitu gani?”Aliuliza Roma kwani hakuwahi kusikia hilo jina la Kashata.

“Ni keki za Karanga zilizochanganywa na sukari , ngoja nikuonjeshe”Aliongea huyu Mama huku akitua kindoo chake kidogo na kufungua ufuniko na hapa Roma aliweza kuona vijikeki vidogo vilivyokuwa vimekatwa kwa pembe nne rangi ya Brown.

“Ni Vitamu mama sijawahi kula hivi”aliongea Roma mara baada ya kuonja kikeki kimoja.

“Ndio baba ni vitamu sana , ukiwapelekea watoto wako watavipenda”Aliongea mama huyu aliekuwa mnene kidogo na mweupe.

“Okey ! Mama ngoja nikuungishe na biashara yako , na kwa hiki kindoo kilivyojaa naonekana kuwa mteja wako wa kwanza , nadhani utaniongezea”aliongea Roma na Mama akatasamu , alionekana ni wale wamama wa Pwani waliokuwa wakijua kumshawishi mteja.

Roma alipewa Vishata vyake na kufungiwa kwenye karatasi na kisha akapiga mwendo na kuondoka taratibu kurudi nyumbani.

Bi Wema na Edna hawakuonekana eneo la sebuleni , walionekana wapo kwenye vyumba vyao wamejipumzisha na Roma hakutaka kuwasumbua sana , aliingia jikoni na kutoa ile mizizi na kuweka kwenye sufuria , akaweka na maji na kisha akafungua jiko la gesi na kuanza kuchemsha.

Dawa ilikuwa na harufu kweli na ilifanya jiko lote kujaa harufu ya mizizi , wakati Roma anachemsha Bi Wema aliingia .

“Mr Roma hio dawa ya asili umeipatia wapi?”Aliuliza bi Wema ni kama alikuwa akiijua hio harufu.

“Nimekutana na mzee anauza na kaniambia ni nzuri”Alionea Roma kwa kudanganya , hakutaka kutaja kama alikuwa amepewa na babu yake Edna kupitia Faridi.

“Ni dawa ambayo Bibi yake Edna alikuwa akiitumia sana kumtibu nayo Edna wakati akiwa mdogo na ndio maana nimeshangazwa na harufu yake ,Mr Roma unaonekana una uwelewa na dawa za asili”aliongea.

Huku Bi Wema akisogea karibu na meza ya jiko na kuona karatasi ambayo ilimvutia , alijiuliza ni nini Roma kanunua.

“Mh !Mr Roma na hizi Kashata umetoa wapi?”

“Nimenunua , kuna mama alinisamamisha na nilishindwa kukataa kununua”Bi Wema alishangaa.

“Mr Roma hivi unajua kuwa Bibi yake Edna kabla hajafungua kampuni ya Vexto alianza na biashara za Kashata”Aliongea Bi Wema na kumshangaza.

“Bi Wema mbona na wewe unaonngea kama wale’ Motivational Speaker’”

“Ni kweli ninachokuambia, kabla bibi yake Edna hajapata mtaji wa kuanza kufanya biashara kubwa kubwa alikuwa akiuza hizi Kashata shuleni, na hata Edna analifahamu hili, na Edna alivyokuwa mdogo alikuwa akitengenezewa na bibi yake hizi Kashata na alikuwa akizipenda kweli”.

“Kumbe…!!!”

“Ndio Mr Roma , umenishangaza leo , kila kitu ulicholeta leo kimenikumbusha miaka yangu ya nyuma wakati naanza kuja kufanya kazi ndani ya familia ya Edna”

“Kwahio Bi Wema ulianza kufanya kazi ndani ya familia ya Edna kwa miaka mingapi?”

“Miaka mingi kabla ya Edna ya Edna kuzaliwa tuseme mwaka mmoja kabla , kipindi hiko natokea kwetu Bukoba huko , nilikutana na Marium njiani ndio nikamweleza mkasa wangu ndio akanisaidia na kunileta Dar Es salaam”

“Bi Wema kumbe na wewe unawakwako mkasa , unahusu nini?”

“Mr Roma ni jambo ambalo sitaki kulikumbuka mpaka leo hii ni lenye kuniumiza kila siku”Aliongea Bi Wema na kumfanya Roma aache kuuliza Zaidi, alimuwekea Bi Wema mchuzi wa dawa kwenye kikombe na kumpatia anywe na Bi Wema alishukuru.

Roma aliweka pia dawa nyingine kwenye kikombe na kuchukua Kashata na kupandisha ngazi kwenda kwenye chumba cha Edna kwa ajili ya kumpatia Dawa , aligonga mlango na Edna alifungua.

“My Wife Mrembo nimekuletea Dawa ya Asili , kunywa itakusaidia na hii ni zawadi yako”Aliongea Roma akiwa ni mwenye kutabasamu kama kawaida yake , Edna aliangalia Vikashata vilivyokuwa kwenye sahani kwenye mikono ya Roma kwa dakika.

“Sijisikii kunywa dawa”Aliongea Edna na kufunga mlango na kumfanya Roma ashangae , yaani amemletea dawa , lakini yeye anaikataa , Roma hakutaka kubembeleza alishuka chini.

“Mnona unarudi nayo?”

“Amekataa ,Bi Wema una uhakika Edna anapenda Kashata?”Aliuliza Roma alieshikilia kikombe chake akiwa amesimama uelekeo wa kwenda jikoni na Bi Wema akatabasamu.

“Mr Roma , unasafari ndefu ya kumjua mkeo , kwa jinsi ulivyompelekea ni lazima umemkumbusha miaka ya nyuma”.Roma alishangaa na kujiona amekosea huenda amemkumbusha majonzi Edna ya kufiwa na wapendwa wake , alijongea upande wa jikoni na kuweka kikombe kwenye kabati na kuanza kusuuza vyombo alivyotumia na alipanga pia aandae Chai.

“Hio Dawa iko wapi Roma?”Aliuliza Edna ambaye alikuwa amesimama mlangoni akiwa na tisheti lake lenye maandishi ya “Fair Girl” huku chini akiwa amevalia kijikaptula kilichoishia Magoti , alionekana kujiachia leo.

“Hii hapa wife”Aliongea Roma na kumpatia kikombe.

“Na hizo Kashata ulizokuwa umebeba ziko wapi nitolee uchungu wa hii dawa”Aliongea Edna kwa sauti yake kama vile alikuwa mtoto.

“Hehe..Wife unajua umekuwa Mcute ghafla tu”Aliongea Roma huku akimpatia Edna kashata na Roma akaendelea na kazi ya kuandaa kifungua kinywa , licha ya kwamba muda ulikuwa umeenda.

Sasa wakati Roma yupo Bize hakujua kama Edna yupo tu anamwangalia Muda wote , Edna alikuwa amesimama huku akiangalia namna ambavyo Roma yuko bize , kwake ni picha ambayo hakuwa akiitegemea kuiona kwa Roma na ilimfanya ajisikie utamu kwenye moyo wake.

“Wife mbona unaniangalia sana”Aliongea Roma na kumfanya Edna aone aibu kwa kukamatwa.

“Nilitaka nikuambie baadae kuna sehemu nataka unisindikize”Aliongea Edna kwa sauti ya chini.

“Wapi Wife,Mbona unaongea kama mtoto anaeomba ruhusa Wazazi wake aende Disco?”

“Kuna familia moja ni washirika wetu wa kibiashara kwa miaka mingi na ni moja ya familia pia yenye nguvu sana ndani ya Tanzania ,wameomba tuhudhurie pamoja”Aliongea Edna na Roma alitabasamu.

“Usijali Wife tutaenda”

“ Nakukumbusha tu ni watu wazito ndani ya hili taifa , hivyo jitahidi kuwa makini na utumie hio fursa vizuri kwa faida yako ya baadae”

“Wife usiniambie ndio ushaanza kunitengenezea watu wa kukutana na mimi kwa ajili ya kutengeneza koneksheni”

“Ndio nataka uache tabia yako ya kucheza magemu na kulala tu kazini, nataka angalau unisaidie kwenye baadhi ya mambo na ndio maana nataka ukutane na watu wakubwa ndani ya taifa hili ambao watakusiadia baadae”Roma alitabasamu huku akimwangalia Edna alivyokuwa siriasi na maneno yake .

“Wife usijali , najua majukumu ya kuongoza kampuni yanakushosha hivyo nitakuwa na kusaidia pale utakapo taka msaada wangu”.

“Kumbe unajua nachoka , uwe unanisadia sasa , ulifikiri napenda kila saa kuwa kwenye kampuni bila kupumzika , ni kwasababu familia nyingi zinanitegemea ,nakosa tu mtu sahihi wa kunisaidia, Simaanishi kwamba hauko vizuri, ninachomaanisha angalau unisaidie najua una uwez mkubwa ila hutaki kuutumia”Aliongea Edna leo kwa mara ya kwanza kwa namna ya kufunguka na kumshangaza Roma kidogo , ila hakutaka kuweka kila kitu kwake, aliona huenda Edna ashaanza kuona umuhimu wake na anaanza kumkubali kama mume wake.

Roma na Edna hawakuenda kazini kabisa waliishia kupumzika , Roma alikaa chumbani kwake na kuangalia a Runinga kwa muda, baada ya kuchoka alilala mpaka muda wa jioni alipokuja kushituliwa na simu yake iliokuwa ikiita mfululizo , aliangalia jina la mpigaji nakuona ni namba mpya tena ambayo sio ya kitanzania.

“Hello!!”

“Hades ni mimi Balozi hapa”

“Ndio Balozi”

“Nimekupigia kukueleza kuwa wiki ya keshokutwa Sophia anakuja Tanzania na ameniambia hataki kukaa kwa babu yake , anataka aje akae unapoishi”Aliongea Balozi na kumchanganya Roma.

“Balozi hakuna ulazima wa Sophia kukaa nyumbani kwangu , kwanza kabisa sina mpango wa kumfanya mke kama unavyotaka”

“Hades ninachokuomba sio kumfanya Sophia kuwa mkeo , nataka akae kwa muda kidogo hapo kwako”

“Unafikiri hilo swala linawezekana vipi balozi ,Sophia na Edna ni ndugu, na unajua kuwa Edna na familia yako hampatani”

“Hilo lisikupe shida Hades,Edna hamjui Sophia kabisa , Hehe..Hades unaonaje ukimwambia mkeo Sophia ni mdogo wako na unaomba akae hapo nyumbani kwako kwa muda”

“Balozi unaongea vitu ambavyo haviwezemi na simuhitaji Sophia mimi”Aliongea Roma huku akionesha hasira waziwazi na kukata simu na kuitupia pembeni.

Muda wa saa moja kamili Edna na Roma walitoka kwenye gari ya pamoja kwa ajili ya kuelekea sehemu ambavyo Edna alimwambia Roma kuwa ni kwenda kuonana na familia yenye nguvu ndani ya taifa la Tanzania.
 
SEHEMU YA 94.

Roma ndio aliekuwa dereva usiku huu huku mke wake Edna aliekuwa amependeza akiwa amekaa pembeni ,Edna akiwa amevalia gauni la rangi nyeupe lenye maua kama michirizi huku kiunoni akafunga na mkanda wa rangi nyekundu, alikuwa amependeza , Roma nae mavazi yake yalikuwa ni suti kama kawaida na shati rangi ya bluu bila tai.

Roma aliendesha kwa maelekezo ya Edna mpaka wakaja kusimama kwenye jumba moja la Kifahari kubwa tu , na kwa kuangalia tu ndani ya eneo hili la Masaki huenda hilo jumba ndio ambalo ni kubwa sana kuliko nyumba zote ambazo wanaishi matajiri ndani ya huu mtaa.

Wakati Roma anasubiria geti la jumba hili kufunguliwa baada ya kupiga honi , nyuma yake aliona gari nyingine ya kifahari na ilionekana na yenyewe ilikuwa ikitaka kuingia ndani ya jumba hili , ilikuwa ni gari aina ya Porsche.

Geti lilifunguliwa taratibu na Roma aliingiza gari ndani ya jumba hili ambalo lilimshangaza sana Roma kwa madhanri ya hapo ndani , alipaki gari baada ya kuonyeshwa sehemu na mfanyakazi ambaye alionekana kama mlinzi na akaegesha gari yake , sehemu hii ilikuwa na magari mengi ambayo yapo ndani ya hili eneo , na jambo hili kwa harakaharaka lilimfanya Roma kugundua leo ndani ya hili jumba huenda kuna sherehe inayoendelea na sio kama alivyosema Edna kama anakuja tu kuonana na familia yenye nguvu ndani ya Tanzania.

Baada ya kugesha alishuka na kumfungulia Edna mlango na wakati huo huo ile gari iliokuwa nyuma yake pia ilikuwa eneo hilo la Maegesho na ile Roma na Edna wanapiga hatua kama mbili ,Dereva aliekuwa akiendesha gari hio alitoka na Wote Roma na Edna walimtambua , alikuwa ni Nadia Alfonso.

“Nadia alilazimisha tabasamu baada ya kuwaona Edna na Roma ambao kwa jinsi walivyokuwa wakionekana walidhihirisha uhusiano wao , yaani mume na mke.

“Mmependezana Edna”Aliongea Nadia baada ya kuwasogela na Edna alitabasamu na kumangalia Roma.

“Asante Nadia na wewe umependeza”Aliongea Edna huku Roma akimwangalia Nadia bila ya kuongea na Nadia alimwangalia Roma usoni ni kama alikuwa akisubiria Roma amsifie ila Roma hakufanya hivyo , alionekena akikumbuka baadhi ya mambo.

“Mr Roma hatujaonana tokea urudi Japani Hongera kwa kukamilisha jambo kubwa kwa kampuni”

“Asante sana Nadia , yote nimefanya tu kwa ajili ya mke wangu kipenzi”aliongea Roma huku akitabasamu na kumkonyeza Edna alietabasamu , ila kwa Nadia hakuonesha kufurahi kwa namna Roma anavyomwangalia Edna Zaidi ya kuweka abasamu bandia usoni.

Waliongozwa na mfanyakazi wa kike na kuzunguka upande wa pili wa jumba hili , hawakuingia ndani kama Roma alivyotegemea , Roma aliendelea kuangalia mandhari yakuvutia ya jumba hili.

“Nadia ,Edna karibuni”Aliongea mwanamama mmoja hivi maji ya kunde mtu mzima , makadirio ya miaka kama Arobaini na tano hivi , mwanamama huyu baada ya kuwasogelea macho yote yalikuwa kwa Roma , alimwangalia Roma kama vile alikuwa akimfananisha nah aa Roma alitambua hilo.

“Asante Mrs Mohamed”Alijibu Nadia na wakapeana mikono , alikuwa ni mwanamama ambaye alionekana mkarimu kwa jinsi alivyokuwa ameweka tabasamu usoni mwake.

“Mrs Mohamed huyu ni ndio mume wangu , anafahamika kwa jina la Roma Ramonni ,Roma huyu ni Mke wa Mohamedi tulikutana nae kwenye kusanyiko”Aliongea Edna akimtambulisha Roma.

“Unamaaisha huyu ndio mke wa yule tajiri Azizi?”

“Ndio Mr Roma naitwa Mama Nusra ,hongera kwa kupata mke mzuri kama Edna , Edna hongera nimefurahi kukutana na Mr Roma, Azizi alikuwa akiniambia kuhusu mumeo na nilitamani sana kumuona”Aliongea Mama huyu kwa furaha na kumfanya Nadia aliekuwa pembeni kuchukizwa na sifa za Mama Nusra.

“Nafurahi pia kukufahamu mama Nusra unaonekana kuwa mkarimu kweli na sikudhania Azizi atakuwa na mke kama wewe”Aliongea na kumfanya mwanamama huyu amwangalie usonni na kutabasamu.

“Ulidhania atakuwa na mke wa aina gani?”.

“Hehe..kwa anavyonekana ana hela ila Swaga hana hata mimi nimemzidi, kwanza anacheka kichafu na nilijua hatokuwa na mwanamke mrembo kama wewe ,Eti Mama Nusra umempendea nini yule mzee au ni kwasababu anapesa,”

Aliongea Roma na kumfanya Edna amfinye, maana aliona Roma anaanza kuongea ujinga lakini kwa Mama Nusra alijikuta akicheka , alionekana kujisikia vizuri sana kusifiwa kwa aina ya tofauti na Roma

Basi Edna na Roma waliongozwa mpaka upande wa Swimming Pooll , sehemu ambayo ilikuwa imepambwa , kulionekana kulikuwa na sherehe iliokuwa ikiendelea hapa ndani , kwani pia kulikuwepo na wageni japo hawakua wengi sana.

“Mr Roma.. hahahaha..tunaonana tena”Aliongea Tajiri Mohamedi , alionekana kufurahi sana kama kawaida yake na cheko lake.

“Sema Mzee unajua kucheka kichafu ,Mkeo anaweza kuingia kwenye kumi bora ya wanawake wenye huruma ndani ya Tanzania .. Anyway mimi na mke wangu tunafurahi kukutana kwa mara nyingine”Aliongea Roma na Tajiri huyu alichukulia maneno ya Roma kama sifa na alicheka tena.

“Edna kwa jinsi ulivyomzuri nilikuwa nikitegemea ,utatafuta mwanaume matawi ya juu , sikudhania utakuja kuangukia kwa mwanaume mbeba mizigo,Asie na pesa”Aliongea Tajiri Azizi na Roma alitabasamu aliona huyu mzee anamlipizia.

Wakati wakiwa wanaongea na Tajiri Azizi mara kuna mwanamke mremfu mrembo mno, mtu mzima aliwasogelea, Roma na uwezo wake wa kujua watu alijua kabisa mwanamke huyu hakuwa mtanzania.Edna alionesha kutomfahamu huyu mwanamke.

“Edna kutana na ‘First Lady’ kutoka Rwanda , Mke wa mheshimiwa Jeremy”aliongea Azizi na mwanamama huyu akaachia tabasamu na kumwangalia Edna huku akimpa mkono wa salamu.

“Nafurahi kukufahamu hakika ni kama watu wanavyokusigia , umrembo sana”Aliongea mwanamama huyu kwa kingereza na Edna alitabasamu.

“Nimefurahi pia kukutana na First lady kutoka Rwanda”Aliuongea Edna huku akiwa ametabasamu ,ila kwa Roma kuna kitu alikuwa akikiangalia kwenye uso wa huyu mwanamke , kitu ambacho mtu ambaye ni wa kawaida hawezi kukigundua , Roma aligundua huyu mwanamke anaefahamika kwa jina la ‘First lady’ hakuwa na tabasamu la dhati ni kama alikuwa akifosi na haikueleweka ni kwa namna gani aligundua.

Roma aligundua sherehe hii ilikuwa ni ya kumpongeza mtoto wa kiume wa tajiri Azizi aliekuwa amemaliza masomo yake ya ngazi ya Uzamili kutoka chuo cha Cambridge maana kulikuwa na maandishi juu ya jukwaa yalionakshiwa kwa maneno ya pongezi.

Baada ya kusalimiana na baadhi ya watu ambao wamealikwa hapa ndani , walionyeshwa meza yao ya kuketi huku wakiletewa vinywaji.

Meza aliokuwa amekaa Roma ilikuwa na jumla ya watu watatu , yaani yeye na Edna pamoja na Nadia, Edna na Nadia walionekana kuongea huku Roma akikagua mandhari ya hili eneo ni kama alikuwa akichunguza kila mtu aliekuwepo na ambaye alikuwa akiingia hapa ndani.

“Edna habari za siku”Ilikuw ani sauti iliowafanya Edna na Nadia waliokuwa wakiongea wainue macho yao na kumwangalia ni nani aliekuwa akiwasalimia na hata kwa Roma pia aligeuza shingo yake na kuangalia upande wa mtu aliesalimia.

“Denisi..!! ,Ni nzuri habari”Aliongea Edna , alikuwa ni Denisi mtoto wa raisi Senga, hata Roma alimkumbuka huyu bwana na tena alikumbuka kipindi wanaenda ikulu na Edna kuna jambo aliweza kuligundua kwenye uso wa Denisi.

“Salama kabisa , Umezidi kuwa mrembo Edna”Aliongea Denisi na leo hii alionekana kuchangamka kuliko ilivyokuwa kipindi c ha nyuma wakati Edna na Roma wapo ikulu.

Nadia alikuwa akimwangalia Denisi na Edna ni kama kuna jambo alikuwa akitafuta baina ya wawili hao , aliona wawili hawa walionekana kufahamiana kwa muda mrefu kidogo japo hakujua ni kivipi , hata kwa Roma alijua mke wake anaonekana kufahamiana na Denisi kwa muda mrefu.

Denisi p alionekana kufanya makusudi yaani licha ya kwamba Roma alikuwepo hapo kwenye Meza ila hakumsalimia na Roma hakujali ila alikerwa na namna ambavyo Denisi alikuwa akimwangalia Edna na pia namna ambavyo amemsifia ,Denisi alimwangalia Edna kwa macho ya kumtamani kabisa , licha ya kwamba wawili hawa wanaonekana kupishana umri kwani Denisi bado alikuwa mdogo kwa Edna.

Wakati Roma akiangalia namna ambayo Denisi akiongea na Edna mara alijikuta akizibwa uso na mikono laini na harakaharaka aligundua aliemziba ni mwanamke , ila alishindwa kung`amua mwanamke huyo ni nani.

“Ukinifahamu nakuachia”Ilimnong`oneza sauti masikioni na Roma alijikuta akikumbuka sauti hio lakini alishindwa kujua ni wapi aliisikia.

“Kwahio nisipokukumbuika utaendelea kuniziba hivihivi mpaka sherehe iishe”Aliongea Roma na aliemziba macho alimwachia na Roma hapo ndipo alipogeuka na kumuona msichana mrembo mwenye haiba ya utoto aliekuwa amemziba macho yake , alikuwa ni Donyi.

“Mungu wako hajajibu maombi yako tumekutana tena”Aliongea Donyi huku akivuta kiti na kuketi , alikuwa amependeza mno usiku huu.

Edna aliekuwa akiongea na Denisi alishuhudia tukio lote ,Roma kuzibwa macho na mwanamke mrembo ambaye alikuwa akimkumbuka vyema kwa kitendo cha kumkubatia Roma wakati wakiwa ndani ya jengo la My World Fashion Mall.

“Donyi Donyi unafanya nini hapa?”Aliuliza Roma.

“Na wewe unafanya nini hapa?”

“Wakubwa zako wakiuliza maswali jibu ,acha kuuliza maswali”Aliongea Roma akimfinya Donyi puani na kumfanya mwanadada huyu ampige Roma na kijibegi chake alionesha kutopenda Roma alichomfanyia.

“Unaniona kama mtoto?”

“Sio nakuoan kama mtoto , wewe ni mtoto na nikikukadiria unamiaka kumi na nane na umevunja ungo juzi tu”

“Looohh! Umekosea babu ,nina kumi na tisa”Aliongea Donyi na alionekana kumzoea kweli Roma kwa haraka , jambo ambalo lilimshangaza hata Nadia aliekuwa akiwaangalia.

“Hivi Anko jina lako unaitwa nani?”

“Naitwa Anko”Wakati Roma na Donyi wakiendelea kujibizana Sherehe ilianza na ni kama Roma alivyodhania , ilikuwa ni sherehe ya kumpongeza kijana wa kiume mkubwa wa Tajiri Azizi aliekuwa akifahamika kwa jina la Kassimu, lakini pia kulikuwa na tukio lingine la kumpongeza Mzee Atanasi, ambaye ametimiza miaka mia moja , Roma alishangazwa na jambo hili , licha ya kwamba Babu ambaye alipandihswa kwenye steji kuonekana mzee , lakini alikuwa ni mwenye afya yake nzuri..

Mzee Azizi alimpongeza kijana wake huku akiweka wazi kama mrithi wa mali zake, watu walimpongeza Atanasi na kwa jinsi kijana huyu alivyoonekana, alikuwa ni vijjana ambao walionekana kujiamini.

Kuna jambo ambalo Roma hakuelewa ila alipanga kumuuliza Edna wakati wa kurejea nyumbani.

Roma kwenye sherehe hii alipenda tukio moja tu na hilo lilikuwa ni muda wa chakula , yeye mambo mengine kwake hayakumvutia tofauti na Edna alieonekana kufurahi kuongea na baadhi ya wageni ambao walikuwa ni wafanya biashara wenzake.

Roma alikuwa ni kama mlinzi muda wote alikuwa akiangalia usalama wa Edna , licha ya kwamba alikuwa mita kadhaa tokea alipokuwa amesimama mke wake , lakini aliweza kugundua ni nani aliekuwa akimwangalia kwa macho mabaya Edna na aliweza kupata watu wawili ambao walikuwa wakimwangalia Edna kwa macho ambayo hakuyaelewa , wa kwanza alikuwa ni Denisi , huyu alionesha hali flani ya kimatamanio kwa Edna na kwa Roma alimuona Denisi kama mtu ambaye alikuwa ana mpango na Edna na hakuonesha kuheshimu Edna kama mwanamke ambaye ana mume , jambo ambalo kwake sio kama hakupenda wanaume kumwangalia Edna kwa macho ya kumtamani , alikua akijuwa mke wake ni mrembo hivyo kukodolewa macho na wanaume ni jambo la kawaida , ila macho ya Denisi yalizidi ila hakutaka kufanya lolote kwea wakati huo, aliona kuna siku lazima ambananishe tu.

Mtu mwingine aliekuwa akimwangalia Edna alikuwa ni mke wa Raisi Jeremy , alietambulishwa kwake kama First Lady huyu mwanamama Roma alimuona kama mtu ambaye hakuwa akimwangalia Edna kwa namna ya kumtakia mema , alimuangalia kwa namna flani hivi ambayo mwenyewe alitafsiri kama mtu mwenye kinyongo.

Wakati Roma akiwa ameshikilia wine yake, mara alikuja kushituliwa na mke wa Tajiri Azizi yaani Mama Nusra.

“Mr Roma kuna mtu nataka uonane nae ,nadhani hautojali nikikuiba kwa dakika”Aliongea mwanamama huyu na Roma alitingisha kichwa na kuongozana na Mama Nusra.

Waliingia ndani ya jumba hili kubwa ambalo kwa ndani lilikuwa likipendeza Zaidi ya nje ,kutokana na thamani za hali ya juu zilizokuwa zimetumika kama mapambo.

Aliongozwa mpaka kwenye chumba ambacho Roma aligundua kuwa chumba hiki sio sebule bali ni kama chumba cha kulala.

“Karibu Mr Roma”Roma alikaribishwa na Mama Nusra ndani ya chumba hiki ambacho kilikuwa ni Chumba kilichokuwa kinajitegemea , kwani kilikuwa na sebule kwa ndani ndogo na meza ya kusomea iliokuwa na tarakishi ya kampuni ya Dell, Roma macho yake yalipita harakaharaka kukagua chumba kizima na hapa ndipo alipoweza kuona picha kubwa iliotundikwa ukutani , picha hii ilikuwa ni ya Mzee Atanasi na Raisi wa kwanza wa Tanzania Julius Kambarage nyerere na wanaume wawili ambao Roma hakuwafahamu , ilikuwa ni picha ya pamoja mabayo kwa kuiangalia tu, ungegundua watu waliokuwa kwenye picha hio walionekana kuwa marafiki kutokana na mkao wao , walikuwa wameangaliana huku wakicheka.

NITARUDI WIKIEND JMOSI SAA 3 KAMILI USIKU

SIMULIZI INAENDELEA GRUPU NA WATSAPP INBOX KWA SPIDI YA 4G UNACHOPASWA KUFANYA NI KUCHIGIA KIASI KISICHOPUNGUA 2500 ILI NIKUUNGE A GRUPU , UKITAKA INBOX TU SPECIL BILA KUUNGWA GRUPU NI 3000.

NAMBA ZA KULIPA NI 0687151346 AIRTEL AU 0743015453 M-PESA AU 0657195492 TIGO PESA AU 0623367345 HALOPESA JINAA ISSAI SINGANO
UKILIPA TUMA MESEII YA MUAMALA WATSAPP NAMBA NI 0687151346
 
Pamoja Sana Mkuu hauna baya
singanojr

Sent from my SM-J700H using JamiiForums mobile app
 
hii 3000 inakuwa kwa kila nikihitaji muendelezo ama nikilipa nimelipa!?ama napata katika namna gani muendelezo wa hii hadithi!?
 
lete story.

halafu mnaoquote uzi mzima hebu acheni ujinga watu tukiona vichwa tu tunadhani katupia kumbe Kuna nyie wehu mmequote.

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] tunakoelekea Mwigulu atatuua na matozo yake haya[emoji23][emoji23][emoji23]

Yote haya ni makasiriko ya tozo[emoji3][emoji3][emoji3] japo kiukweli hawafanyi fresh ila njia iliyofikisha ujumbe sasa[emoji23][emoji23][emoji23]

Mkuu ujumbe umefika kwa walengwa mwenyewe wananikera kinyama sema ndo hivyo tunamtafuta msemaji
 
SEHEMU YA 95

Wakati Roma akiwa anachunguza chumba hiki , mara mlango ulifunguliwa tena, na akaingia Tajiri Mohamedi aliekuwa akisukuma baiskeli ya mataili manne ambayo ilikuwa imembeba Mzee Atanasi mpaka upande wa kulia kwake.

“Baba huyu ndio mume wa Edna”Aliongea Mama Nusra akimtambulisha Roma , wakati huu tajiri Mohamedi akiwa amekaa chini na yeye.

“Ninafurahi kukufahamu Mr Roma,Naitwa MR Atanasi , nadhani haujawahi kunisikia popote”Aliongea Mzee huyu na alionekana bado akili zake zilikuwa zikifanya kazi , jambo ambalo pia lilimshangaza Roma na macho yake pia yalionesha kuwa vyema.

“Ndio Babu Atanasi sijawahi kukusikia popote”aliongea Roma, na hata Edna hajawahi kutamka jina lako.

“Ndio inawezekana sana , ila mimi na bibi yake Edna tulisoma wote,hivyo Edna ni kama mjukuu wangu kutokana na ukaribu wangu na bibi yake”Aliongea Mzee huyu na kumfanya Roma atingishe kichwa kuelewa.

“Mr Roma utanisamehe kama nitavuka mipaka, lakini nataka kujua asili yako , nikimaanisha sehemu ulioazaliwa na baadhi ya ndugu zako”aliongea Mzee huyu kwa sauti yake ya hafifu na Roma alifikiria kidogo.

Upande wa Tajiri Azizi alionekana kuwa mtulivu hapa ndani na alionesha heshima kubwa kwa huyu babu.

“Kuhusu familia yangu hapa Tanzania siijui , ila ninachojua ni kwamba nimezaliwa Tanzania , mimi nimekulia nchini Marekani nilikolelewa na kama utaniuliza ni kwa namna gani niliweza kuelelwa nchini Marekani nitakuambia sijui”Aliongea Roma na kumfanya Mama Nusra atoe macho.

“Kwa hio Mr Roma hapa Tanzania hauna ndugu kwa maneno marahisi?’Aliuliza Mama huyu.

“Ni kama nilivyojibu”

“Okey! Mr Roma utusamehe kwa kuuliza maswali binafsi sana kuhusu maisha yako , ujio wako Tanzania ni mwanzo wa kutengeneza ndugu na tunakukaribisha sana kwenye familia yetu”Aliongea mzee huyu na hakukuwa na maongezi mengi , na Roma mwenyewe alishangaa , kwani ni nje ya mategemeo yake.

“Mr Roma nitakusindikiza mpaka nje”Aliongea Mohamedi na Roma na Azizi walitoka wakimuacha Mama Nusra na Mzee Atanasi.

“Baba unasemaje , wanaonekana kufanana?”

“Ndio japo kwa uzee wangu huu nimegundua kitu, na nadhani rafiki yangu angekuwepo hai mpaka leo angekubaliana na wewe Jestina”Aliongea Mzee huyu akimjibu mama Nusra.

“Ila baba nimemkumbuka sana Dada , natamani angekuwepo hai mpaka leo”

“Unawaza mambo ambayo hayawezekani Jestina ,inapaswa usahau yaliopita,mimi muda sio mrefu nitawafuata marafiki zangu na familia hii itakuwa chini yako ukisaidiwa na Mohamedi , unatakiwa kuwa imara”Aliongea Mzee huyu.

“Kasimu kutana na Anko Roma”Aliongea Donyi mara baada ya Roma kurudi nje na kukutana na Donyi aliekuwa na Mtoto wa Azizi aliekuwa akifahamika kwa jina la Kasimu ambaye ndio aliekuwa akifanyiwa sherehe.

“Donyi nadhani sijakutajia jina langu , umefahamu vipi?”

“Nimemuuliza mkeo”Aliongea Donyi na kumfanya Roma ageuke amwangalie Edna aliekuwa akiongea na wanawake wenzie, na Roma alimwangalia Donyi, yaani alijiambia haka katoto kanaonekana kuwa kajanja kuliko isivyokawaida.

“Nafurahi sana kukuona Mr Roma naitwa Kasimu ni Rafiki wa Donyi,nimesikia taarifa zako kutoka kwa Donyi”Alijitambulisha Kasimu na Roma kuna kitu aligundua kwenye macho ya Kasimu , aligundua mapenzi , alimuona Kasiimu alikuwa na mapenzi mazito kwa mwanadada Donyi.

“Amekuambia nini huyu mtoto?”

“Anko Roma nakutahadharisha mimi sio mtoto ,na manyonyo yote haya unaniitaje mtoto”Roma alijikuta akicheka.

“Donyi hebu tulia bwana”Aliongea Kasimu ambaye hajapendezwa na tabia ya Donyi.

“Kanihadhitia namna ulivyodhibiri majambazi ambayo yalitaka kumdhuru, Mr Roma naomba nikushukuru kwa kunilindia huyu mrembo”Aliongea Kasimu na kumfanya Roma atabasamu.

“Unaonekana unampenda ,ila unajua ni jambo gani lingine ambalo aliniahidi”Aliongea Roma na kumfanya Donyi amwangalie Roma kwa hasira huku akimpa ishara ya kumwambia asiseme.

“Hajaniambia Mr Roma”Aliongea Kasimu huku akimwangalia Donyi.

“Basi kaa nae chini umuulize,halafu pia mwambie apunguze utoto kwa staili hii atakusumbua ukioa”

“Nani kasema naolewa na Kassimu”Aliongea Donyi kwa hasira , ila Roma hakujali aliachana nao na kumsogelea Edna ambaye alikuwa akimwangalia ni kama alikuwa akiwasiliana nae jambo.

“Roma tuondoke sherehe ishaisha hii , ninataka kwenda kupumzika nimechoka nina kwenda kazini kesho”Aliongea Edna na Roma kweli aliona muda umeenda na giza limezidi kuongezeka

“Ulikuwa umeenda wapi? , nilikuwa sikuoni kwa dakika kadhaa”Aliuliza Edna wakati wakiingia Feri kwa ajli ya kutumia kivuko kuvuka upande wa pili.

“Mzee Atanasi alitaka kuonana na mimi”Aliongea Edna na kumfanya Edna ashangae .

“Alikuambia nini?”

“Kaniuliza juu ya ndugu zangu hapa Tanzania”Aliongea Roma na kumfanya Edna atamani kujua jibu ambalo Roma kajibu maana ukweli ni kwamba licha ya kuaona na Roma, hakuwa akiwafahamu ndugu zake na hata asili yake hakuwa akiijua na hii pia ilimshangaza kwani hakuwa kuwaza juu ya ndugu wa Roma na anapotokea.

“Na ulimjibu nini?”Aliuliza Edna na Roma alijua Mke wake anataka kujua leo ni wapi ametokea .

“Nimemjibu kuwa sina ndugu Tanzania na nimelelewa nchini Marekani”Alijibu Roma na kumfanya Edna ashangae.

“Kumbe umekulia Marekani , nilikuwa sijui”

“Ndio Wife nimeishi sana Marekani na hapa Tanzania nipo kwa miezi sita pekee mpaka siku tunakutana”Aliongea Roma na kumshangaza Edna tena.

“Mbona sasa unaonekana kama umeishi Tanzania muda mrefu?”

“Hehe..Wife kwannini unauliza hivyo?’

“Unavyoongea , unaonekana kuwa kama Mswahili”

“Wife mimi niko hivihivi ,ukinipeleka Marekani ninaweza kuishi kama Mmarekani mweusi na hutoweza kugundua tofauti , ukinipeleka Korea Kusini nitaishi kama Mkorea na nitaongea Kikorea kama Mzawa na kitakachonitofuatisha na Wakorea labda rangi yangu tu”aliongea Roma na kumfanya Edna ashangae , alijiuliza kuna siri gani ipo nyuma ya meneno ya Roma, lakini aliona aulize maswali ambayo ni muhimu kwake.

“Kwa hio kwanini umerudi Tanzania , ikiwa huna ndugu?”

“Nimekuja kutafuta asili yangu Edna, ndio misheni kubwa ilionileta Tanzania , walionilea waliniambia wazazi wangu wanaweza wakawa hai na ndio maana nipo hapa Tanzania”Aliongea Roma kwa kifupi , kiukweli ni kwamba alikuwa akichagua jibu la kumpa Edna.

Edna alijikuta akijisikia huzuni , hakujua mume wake alikuwa na historia ya aina hio kwenye maisha yake na pia alijilaumu kwa kutolijua hilo mapema na kwa haraka aliona huenda mpaka sasa Roma anawachukulia Bi Wema na yeye kama ndugu zake wa pekee hapa Tanzania.

Nitajitahidi kuishi nae vizuri”Aliwaza Edna huku akimwangalia Roma aliekuwa bize akitoa gari kwenye pantoni.

Ningemwambia nimeishi Zaidi ya mataifa 100 kwa muda rofauti tofauti asingeniamini”Aliwaza Roma huku akiongeza mwendo baada ya kuingia barabarani.

“Wife Mzee Atanasi ni nani haswa , na kwanini umesema ndio familia yenye nguvu ndani ya taifa la Tanzania?”.

“Mzee Atanasi ni watu wachache sana wanamfahamu ndani ya taifa hili, naweza kusema ndio mzee tajiri sana ndani ya Tanzania”Aliongea Edna na kumfanya Roma ashangae

“Unamaanisha nini wife kusema ndio mzee Tajiri?”

“Utajiri wa Azizi Moihamedi umetokana na Mzee Atanasi na hii ni Baada ya mtoto mkubwa wa Mzee Atanasi Mama Nusra kuolewa na Mohamedi , kwa historia ambayo siijui vizuri ni kwamba tajiri Azizi hakuwa na pesa kabisa wakati akimuo Mama Nusra”

“Kwahio Wife unamaanisha kwamba Mzee Atanasi ndio tajiri na Mohamedi ni mwakilishi tu”

“Siwezi kusema ndio , kwani Mzee Atanasi anampenda sana Mzee Azizi na anamchukulia kama sehemu yake ya familia, licha ya kwamba ni kitu na mkwe wake , Mzee Atanasi hakubahatika kupata mtoto wakiume kwenye ujana wake ndio maana”Aliongea Edna.

“Kama ni hivyo kwanini ajifiche kwenye mgongo wa Mohamedi?”

“Hilo sijui ila kwa maelezo alionipa Bibi ni kwamba Mzee Atanasi na Raisi wa kwanza wa Tanzania walikuwa ni marafiki wakubwa sana na walisoma wote chuo kimoja kipindi cha ukoloni na mzee Atanasi alikuwa ni mshauri mkuu kwa Raisi Nyerere juu ya maswala ya uchumi Enzi hizo na nasikia ndio aliemshauri Raisi Nyerere Ujamaa Tanzania haufai kwa maendeleo ya taifa”

“Kwahio unamaanisha utajiri wa Mzee Atanasi unaweza kuwa ni kutokana na kuwa na urafiki na Raisi kipindi hiko na hakutaka kuonekana kama fisadi?”

“Inaweza kuwa sababu, japo sina uhakika kwa asilimia kubwa , lakini mpaka sasa kati ya wazee ambao walikuwa wakifanya kazi karibu na raisi wa kwanza wa Tanzania aliebaki hai ni Atanasi peke yake , na familia yake inanguvu sana kutokana na kumiliki uchumi wa Tanzania kwa sehemu kubwa , nikuambie tu utajiri wa Azizi sio kamili, kuna mali nyingi ambazo zinamilikiwa na familia ya Atanasi ndani ya taifa hili na hili lipowazi kabisa kwa viongozi wote wa juu wa kiserikali, ni rahisi kusema kwamba ile familia haigusiki Afrika Mashariki yote , kwani mpaka Rwanda huko ndio wawekezaji wakubwa , huku mali zote zikisimamiwa na Mohamed pamoja na vitukuu”

Alijibu Edna na kuzidi kumshangaza Roma na kwa haraka haraka katika akili ya Roma alijua ndio maana akaona picha ya Raisi nyerere na alijua lazima kuna sababu kubwa kwa Mzee Atanasi kujificha kwenye mgongo wa Mohamedi Azizi , lakini Roma bado alikuwa na maswali mengi na alishindwa kuyapatia ufumbuzi kwani Edna alionekana kuchoka na pia walikuwa washafika nyumbani.

Ilikuwa ni asubuhi Roma baada ya kumaliza taratibu zake zote kabla ya kwenda kazini , wakati akijiandaa kushuka chini kwa ajili ya chai ya asubuhi simu yake iliita na jina lilikuwa ni Diego.

“Habari za asubuhi Mheshimiwa Mfalme Pluto?’

“Salama Diego , kuna habari gani?

“Mfalme Pluto nimekupigia kukueleza ile ripoti imekamilika na nataka kukupatia siku ya leo”Roma alijikuta akipata mushikeli ila alijituliza kwanza

“Okey!,Diego nitapitia jioni ya leo naamini kuna mengi kwenye hio ripoti”

“Ndio mfalme Pluto yapo mengi ambayo tumegundua , ni hakika utashangaa”Aliongea Diego na Roma alipatwa na hamu yakujua ni kipi kipo kwenye hio Ripoti.

Sawa Diego nitapitia jioni ya leo”

“Sawa Mafme Pluto nikutakie kazi njema”Aliongea Diego na kukata simu

SEHEMU YA 96​

Roma baada ya kumaliza kuongea na simu alishuka mpaka chini sebuleni kwa ajili ya kujipatia kifungua kinywa ili aelekee kazini.

Edna tayari alikuwa ameketi kwenye meza na Bi Wema wakijipatia kifungua kinywa ,Edna alimwangalia Edna na kisha kumtingishia kichwa kama salamau na Roma alitabasamu na kisha akavuta kiti na kuketi.

Saa tatu kamili Roma aliingiza gari lake kwenye maegesho ya kambuni na akaingia kwenye lift kuelekea kwenye ofisi ambayo alikuwa akifanyia kazi.

Wafanyakazi wenzake leo hii walikuwa bize na majukumu yake , na Roma hakutaka kuwabughuzi , alichokifanya ni kusalimia kila mmoja na kisha akakaa kwenye meza yake na kuwasha tarakishi yake kuangalia ni gemu gani ambalo leo atacheza.

Recho aliekuwa bize alimwangalia Roma na kisha akatabasamu , mrembo huyu alionekana alikuwa akikumbuka kitendo ambacho alikuwa amefanyiwa na Roma siku chache nyuma , na Roma alimuona Recho ambaye alikuwa akimwangalia na kumkonyeza.

Saa sita kamili Roma alikuwa ashachoka muda mrefu kucheza gemu na sasa alikuwa ameegamia kwenye kiti chake akiwa ameuchapa usingizi.

“Romaa..!!”Ilikuwa ni sauti ya mwanadada Benadetha iliomshitua kutoka kwenye usingizi wake na aligeuza shingo na kumwangalia.

“Kuna sehemu naomba unisindikize “Alionea Benadetha huku akimwangalia Roma.

“Unaonaje ukiniambia ni wapi tunaenda”

“Naelekea Site , nimeona huna kazi , hivyo sio mbaya kama utanisindikiza”Aliongea Benadetha na Roma hakuona shida kumsindikiza , kwanza alikuwa ashachoka kukaa sehemu moja na alitaka kidogo anyooshe miguu.

Roma na Benadetha waliingia kwenye gari moja ya Benadetha huku Roma akiwa ndio dereva ,Benadetha alimpa Roma maelekezo kama anaelekea Mbagala eneo ambalo Barabara ya mwendokasi ilikuwa ikijengwa kwa ushirikiano wa kampuni mbili yaani JR na Vexto grupu.

“Benadetha nadhani cheo chako cha ukuu wa Idara ya ‘Public Relation’ hakikutoshi”Aliongea Roma.

“kwanini unasema hivyo?”

“Katika wanawake ambao ni wachapakazi kwenye kampuni ni wewe”

“Mh!,Sio kweli wapo ambao wanafanyakazi Zaidi kuliko mimi , kwa mfano CEO Edna nadhani ndio anaefanya kazi kuzidi wafanyakazi wote wa kampuni,licha yakampuni kuwa yak wake”Aliongea Benadetha na Roma aliona ni kweli Edna alikuwa akifanya sana kazi ,kwani alikuwa akikumbuka kuna siku alikuwa akilala ofisini.

“Nadhani , lakini kwenye idara yetu wewe ndio mfanyakazi unaewajibika muda wote , sijawahi kuona hata ukipiga umbea na wafanyakazi wenzako , inabidi CEO akupandishe cheo”Aliongea Roma na kumfanya Benadetha ajisikie vizuri, hakuna mtu ambaye hakupenda kusifiwa , lakini pia ilikuwa kweli Benadetha alikuwa ni moja ya wafanyakazi wa Vexto ambao muda wote walikuwa bize.

Na kuna muda Roma alimuona Benadetha kama mfanyakazi ambaye huenda kwao Maisha hayakuwa mazuri sana ndio maana anafanya kazi sana ili apandishwe cheo na mshahara uongoezeke.

“Sema Roma ulitushangaza wewe na Dorisi baada ya kufanikiwa kufanikisha Saini ya dili nono na kampuni ya Yamakuza , hakuna ambaye alitegemea mafanikio yale,unaonekana kuwa mtu ambaye hujali sana maswala ya kazi , lakini ukiwa siriasi utafanya mambo makubwa”Aliongea Benadetha na kumfanya Roma atoe tabasamu.

Dakika chache walikuwa washafika Mbagala Rangi tatu na Roma alisimamisha gari upande wa kulia na kisha akatoka.

Benadetha licha ya kwamba hakuwa mzuri sana kama Edna , lakini alikuwa ni moja ya wanawake ambao unaweza kusema kwamba ni mazuri kiasi kwamba kila mwanaume atakae mwangalia lazima avutiwe nae ,Roma aliongozana na Benadetha mpaka upande wa pili wa Barabara.

Sehemu ilikuwa na wafanyakazi wengi ambao walikuwa wakifannya kazi ya kuchimba mashimo na kumwaga Zege,Roma hakuelewa ni jambo gani ambalo limemleta Benadetha ndani ya haya maeneo ambalo lilikuwa likihusiana na Idara yao.

“Romaa!”Ilikuwa ni sauti ya kiume ambayo ilimfanya Roma ageuze macho upande wa kushoto na kumwangalia ni nani aliekuwa akimwita.

“Yusuph!”Aliita Roma mara baada ya kugundua aliekuwa akiliita jina lake alikuwa ni Yusuph ,Roma tokea atoke Mbagala hakuwahi kupata wasaa wakuja kuwatembelea marafiki zake,aliokuwa akibeba nao mizigo.

Yusuph alikuwa amevalia kijikoti cha rangi ya kijani na kofia ngumu kichwani,Roma alishangazwa na Yusuph kuwa ndani ya hilo eneo , kwani kazi ambayo alionekana alikuwa akifanya ilikuwa ikihusisha wahandisi.

“Ni muda Man hatujaonana tokea uoe,Maisha yako yamekuwa Super sana siku hizi”Aliongea Yusuph baada ya kuwasogelea Roma na Benadetha.

“Ndio ni kama mwezi sasa , ila sijawahi kujua kuwa wewe ni injinia”

“Haha…nadhani haujawahi kuniuliza kuhusu levo ya Elimu yangu Roma”Roma alitingisha kichwa na kuona ni kweli , kwani licha ya kwamba alikuwa akifanya kazi na baadhi ya watu pale Soko la Mbagala , lakini hakuwa akijua kuhusu elimu zao , alichokuwa akijua Roma ni kwamba ni wabeba mizigo kama yeye alivyokuwa mbeba mizigo.

“Kwahio unaniambia ulikuwa msomi wa injinia?”

“Ndio , ile kazi ilikuwa ni kusogeza tu siku, si unajua mwenyewe kazi siku hizi ni ngumu sana kupata na ndio maana nilikuwa nimejishikiza pale, ila kwasasa namshukuru Mungu nimefanikiwa kupata kazi hapa”Aliongea Yusuph na kumfanya Roma atingishe kichwa.

“Benadetha huyu ni rafiki yangu , kabla sijapata kazi Vexto nilikuwa nikifanya kazi Soko la Mbagala kama Mbeba mizigo”aliongea Roma na kumshangaza Benadetha hakuwa na hio taarifa

“Daah ! Roma kumbe unafanya kazi Vexto hii ambayo ndio wanajenga hapa?”

“Roma unaweza kuongea kwanza na Rafiki yako , ngoja nikaonene na Injinia mkuu nitarudi baada ya nusu saa”Aliongea Benadetha na Roma alitingisha kichwa kukubaliana nae.

“Ndio Yusuph,Mbona unaonekana kushangaa?”

“Nimeshangaa Man , kama ninejua mapema ningekuja kwako unifanyie koneksheni haraka niweze kupata nafasi ya kazi hapa”

“Ndio , ila ni vileile tu , bahati ililuwa upande wako ushapata kazi”

“Ndio sema mshikaji wangu Mhando yule hakupata na mpaka sasa yupo palepale sokoni anafanya kazi , amejitahidi kuomba sehemu mbalimbali ila bahati haijawa yake”

“Unamaanisha yule jamaa mpole sana?”

“Ndio man , nimejaribu kuongea na Director hapa ampe nafasi ila kasema pashajaa na hapokei injinia mwingine na jamaa namuonea huruma maana Bi mkubwa wake ni mgonjwa wa kisukari na pesa anayopata anamtumia lakini bado kiasi ambacho anatuma hakitoshi”Aliongea Yusuph na kumfanya Roma amuonee huruma , alikuwa akimjua Mhando hakuwa muongeaji sana ,ila hakujua kuwa alikuwa pia yeye ni mhandisi wa ngazi ya shahada kama ilivyokuwa kwa Yusuph.

“Sasa Roma kama una konekesheni unaonaje ukimuunganisha mshikaji, namuonea sana huruma najitahidi ninachopata hapa kumsevu na kiasi lakini bado”

Aliongea na Roma aliguswa kumsaidia Mhando , aliona ni jukumu lake kuwasaidia washikaji zake ambao alikuwa akifanya nao kazi kwa takribani miezi sita alipoingia ndani ya jiji la Dar na ni hao ambao walimpokea kwa ukarimu , hivyo aliona kuwasadia ilikuwa jukumu lake.

“Okey! Nitamsaidia mshikaji mpigie simu tuonane hapa”Aliongea Roma na Yusuph alitoa tabasamu la Furaha , alitoa simu yake ndogo mfukoni na kupiga.

“Anasema yupo maeneo hayahaya na anakuja saivi”

“Vyeti vyake je?”

“Haha..Jamaa anatembeaga navyo kila anapoenda”Aliongea Yusuph na kumfanya Roma tabasamu.

Zilipita kama dakika kumi na tano tu hivi Mhando alifika , alikuwa amechafuka mno kiasi cha kumfanya Roma aone kweli taifa la Tanzania lina tatizo kubwa la Ajira , kwani msomi wa Uhanidisi hakuwa na utofauti na watu ambao hawajasoma.

Mhando alisalimiana na Roma kwa shauku kubwa iliokuwa imemvaa kwenye uso wake.

“Oya Mhando mwenetu Roma hapa atakusaidia juu ya kazi , anafanya kazi Vexto na anakonekesheni”Aliongea Yusuph na kumfanya Mhando atoe tabasamu.

“Nitashukuru sana kama utanisaidia Roma”Aliongea na kumfanya Roma atabasamu na wakati uleule Benadetha alifika ndani ya eneo ambalo Roma alikuwa amesimama na marafiki zake , alionekana kumaliza kile ambacho kilikuwa kimemleta ndani ya hili eneo.

“Benadetha kuna huyu Rafiki yangu nataka nimsaidie kupata kazi hapa , ni injinia na hivi ni vyeti vyake”Aliongea Roma huku akimkabidhi Benadetha vile vyeti na kuanza kuvikagua pamoja na CV yake na mwanadada huyu alijikuta akishangaa kwani Mhando alikuwa na ufaulu mkubwa sana wa GPA.

“Unaonekana kuwa na ufaulu mkubwa , kwanini wameshindwa kuchukua mhandisi kama wewe”Aliongea Benadetha huku akiendelea kusoma karatasi zile , licha ya Mhando kuwa na GPA ya 4.7 ya Civil Engeneering lakini pia alikuwa na uzoefu wa kufanya kazi sehemu tofauti tofauti na hili ndio jambo ambalo lilimshangaza Benadetha kwanini mtu ambaye ana ufalu mkubwa kama huu hajapata nafasi.

“Sister hata mimi nimeshangaa ,GPA yangu ni 3.0 lakini nimepata ajira na Mhando kakosa licha ya kwamba tumeleta maombi wakati mmoja”Aliongea Yusuph.

Roma kwa maelezo hayo aliona ukakasi kwa watu ambao walikuwa wakihusika na maswala ya uajili.

“Sema swala la ajira na usimamizi wote wa waajiriwa hapa unasimamiwa na JR , sisi tunahusika na kuleta malighafi tu”Aliongea Benadetha lakini Roma hakuridhika.

“Hata kama Benadetha,kulitumika kigezo gani kwa Mhando hapa kukosa kazi,lazima kuna ufisadi unafanyika”Aliongea Roma.

“Kwahio Roma unataka kufanya nini?”

“Mhando nitumie hizi CV na vyeti vyako kupitia Email yangu nitaangalia namna ya kukusaidia kupata kazi , kesho nitakupa jibu”Aliongea Roma na kumfanya Mhando macho kumtoka maana kwa jinsi alivyomuona Roma ni kama alikuwa na uhakika wa kupata kazi , kwani Roma aliongea kwa kujiamini.

Roma baada ya kumtajia Mhando Emaili yake waliondoka ndani ya hilo eneo na kurejea walipo acha gari yao.

“Benadetha unaonaje tukipata kabisa chakula hukuhuku kabla ya kurudi”

“Yeah! Itakuwa vizuri hata mimi nilikuwa nikifikiria hivyo”Aliongea Benadetha huku akitabasamu.

Roma alikuwa akiyajua sana haya maneneo ya Mbagala hivyo kuchagua mgahawa wa wao kukaa kwa ajili ya kupata chakula halikumpa shida.

Walikuja kusimamamisha gari Zakhem barabara ya kwenda Kijichi kwenye mgahawa moja maarufu ndani ya eneo hili.

Roma alimuongoza Benadetha ambaye alionekana kuwa mgeni kwenye haya maeneo.

“Sio pabaya sana”Aliongea Benadetha baada ya kupenda mpangilio na usafi wa hapa ndani , licha ya kwamba ni sehemu ambayo ilikuwa na watu wengi.

Roma aliagiza ugali na samaki pamoja na juisi na Benadetha pilau na nyama ya kukaanga.

Wakati Roma akianza kula mara macho yake yalitua kwenye watu waliokuwa wakiingia ndani ya hili eneo , na sehemu ambayo Roma na Benadetha walichagua kukaa ilikuwa ni rahisi kwao kuona mlangoni na hii ilimfanya Roma kutambua watu haraka.

Roma alimuona Najma aliekuwa ameambatana na watu wanne , wa kwanza kutambua ni Juma, wa pili yake alikuwa ni mama ambaye kwa harakaharaka ukimwangalia ni mtu wa miaka kama arobaini hivi kwenda juu mweupe mnene alievalia ushungi na dela rangi nyeusi , halafu pia mtu wanne alikuwa ni mwanaume hivi msomali mwenye kitambi saizi ya kati ambaye Roma alishindwa kumtambua.

Najma alijikuta akikutanisha macho na Roma na kumfanya Juma aliekuwa akiangalia sehemu ya kukaa ,huku akiongea na bwana mwenye kitambi kugeuka upande ambao Najma alikuwa akiangalia na hapo ndipo na Juma aliokutanisha macho na Roma.

SEHEMU YA 97.

Juma licha ya kwamba alikuwa amemuona Roma lakini hakuonyesha hali yoyote ile ya kutaka kumsalimia, Roma aliekuwa amekaa na Benadetha alishindwa kujua ni kwanini watu hao wanne wapo hapa ndani ya mgahawa , kwani kwa muonekano wao hawakuonekana kama watu ambao wamekuja kwa ajili ya kula tu , bali walionekana kama kuna jambo muhimu ambalo walikuja kulizungumza.

Juma alinyooshea kidole Meza iliokuwa tupu pembeni kidogo na walipokuwa wameketi Roma na Benadetha na waliisogelea japo kwa Najma ni kama hakupenda hio sehemu.

Najma alimwangalia tu Roma na alishindwa hata kumpa salamu na kwa Juma hivyohivyo kitendo ambacho kilimfanya Roma kujiuliza kuna nini kinaendelea , ila hakutaka kufuatilia , alijiambia kwenye akili yake kwakua wamekuja kukaa karibiu na yeye basi atajua ni kwanini kuna mabadiliko hayo kwa upande wa Najma , kiwani alikuwa akimjua sana mwanadada huyu hata kama kaka yake asingesalimia ila kwa Najma asingempita Rma bila salamu.

Benadetha alimwangalia Roma na alionekana na yeye kuna kitu alikigundua ila hakutaka kuongea , aliendelea kuwa bize na chakula chake.

“Baba hili tushalimaliza kabisa na mimi kama Shangazi yake Najma unabaraka zote na unachopaswa ni kuleta barua ya posa na taratibu zingine zitafuatia”Roma alipata kusikia maneno hayo kutoka kwa mwannamke ambaye sasa aligundua ni Shangazi yake na Najma.

“Ninashukuru sana mama kwa kutupa Baraka zako mimi na Najma, niseme tu nampenda sana Najma na nipo tayari kumuoa hata kesho”Roma aliweza kusikia mwanaume mwenye kitambi akiongea,

“Hahaha..Unaonekana kumpenda sana Najma, ila niseme Shangazi yangu kwakweli ni mrembo , hapa umepata mke”Aliongea Shangazi na hakujali kuongea kwa sauti ya chini na watu waliokuwa pembeni walijua kinachoongelewa hapo ni ndoa , Najma muda wote alionesha hali ya kutokuwa na utulivu , licha ya kwamba Roma alikuwa amempa kisogo ila kwa sauti ya Shangazi yake alijua kabisa atakuwa amesikia kila kitu.

“Bro Ahmedi Mdogo wangu ni Chombo , wewe fanya chapu kama shangazi alivyosema ili ndoa isichelewe”Aliongea Juma na yeye kwa sauti kubwa kidogo kuliko ya shangazi yake.

Roma hata ile hamu ya kula ilikuwa imemuishia na Benadetha aligundua mabadiliko ya Roma ila alipanga kukaa kwanza kimya kwa wakati huo na pia Roma alishukuru kwa Benadetha kutouliza kwani aliona angemfanya asisikie ni kitu gani Najma na kaka yake kilikuwa kimewaleta hapo ndani.

Roma baada ya kumaliza kula chakula , alilipia na kutembea kuelekea barabarani na kuingia kwenye gari yao na safari ya kuridi kazini ikaanza.

“Alikuwa ni mpenzi wako?”Benadetha alivunja ukimya .

“Siiwezi kusema alikuwa mpenzi , ila tulifikia hatua nzuri ya kuwa wapenzi , ila kuna changamoto zilikuwepo katikati yetu ndio maana”

“Lakini Roma Wewe si unmake?”

“Ndio ninae na naweza kusema na hio ni moja ya changamoto”Alijibu Roma na kiukweli ni kwamba moyo wake ulikuwa mzito sana kumuachia Najma awe na mwanaume mwingine ni hali ambayo hakuwahi kujihisi kwenye maisha yake.

Roma baada ya kufika ndani ya kampuni alinyoosha moja kwa moja kwenda kwenye ofisi ya mke wake Edna.

Alimkuta Miss Airport aliekuwa bize na tarakishi yake na Roma alimpungia tu mkono na kupita moja kwa moja , jambo ambalo lilimfanya mwanadada huyu akasirike.

Roma baada ya kuingia ndani ya ofisi hii , alimkuta Edna akiwa anaongea na Simu , jambo ambalo kwa Roma kwa kumuangalia tu mke wake alijua kabisa simu hio ilionekana kuwa muhimu kutokana na muonekano wake.

“Hahaha..Chibu! Acha kunichekesha , haujaacha mambo yako tu mpaka sasa hivi”

“Sawa.. Usijali Chibu,Nitajitahidi kufanikisha ombi lako”

Edna alikuwa akiongea kwa kifaransa jambo ambalo lilimshangaza Roma , hakujua mke wake alikuwa akijua kuongea kifaransa tena ‘Fluently’,lakini licha ya Roma kushangazwa na namna ambavyo mke wake alikuwa akiongea kifaransa ila jina la ‘Chibu’ ndio lililomfanya afikirie ni uhusiano gani Chibu anao na mke wake kiasi cha wawili hao kuongea kwa furaha mpaka kuwekeana ahadi.

“Vipi Roma kuna shida?”Aliuliza Edna baada ya kumuona Roma anamwangalia tu bila ya kuongea lolote.

“Wife sikujua kama unaweza kuongea kifaransa”

“Mh! Ulifikiri ni wewe tu ambae unajua kuongea lugha tofauti tofauti?”

“Sijamaanisha kama hupaswi kujua kuongea kifaransa , nimeshangaa kwani unaonekana kujua kuongea Kiswahili na Kingereza pekee”Aliongea Roma.

“Haya niambie ni jambo gani limekuleta kwenye ofisi yangu?”

“ Nimekumiss mke wangu”Aliongea Roma na kumfanya Edna akose utulivu lakini wakati huohuo kujisikia vizuri hajawahi kuambiwa maneno ya moja kwa moja hivyo.

“Niambie umekuja kufanya nini kuwa siriasi”Aliongea Edna.

“Kuna rafiki yangu nataka apatiwe ajira ana CV nzuri na GPA kubwa ya uhandisi wa majengo , ila sina koneksheni ya kumsaidia , Wife unaonaje ukimsaidia mumeo kwenye hili”Aliongea Roma na kumfanya Edna amwangalie na kisha akafikiria kidogo.

“Siwezi kukusaidia bure”Aliongea Edna na kumfanya Roma ashangae , alijikuta akitabasamu na kuona mke wake sasa hivi anakuwa mjanja sasa.

“Bebi wife unataka nifanye nini ili unisaidie”

“Ninapanga kufungua kampuni mpya ya Burudani na Habari na mtu wa kuisimamia kampuni hio napanga uwe wewe”Aliongea Edna na kumfanya Roma atoe macho.

Ukweli Edna alikuwa amepanga baada ya kufanikisha swala la mkataba wa Yamakuza,faida atakayopata kupitia Malighafi mpya atumie kufungua kampuni nyingine mpya itakayohusika na maswala ya habari na Burudani , kampuni ambayo itakuwa na kituo cha Television ,nia na madhumuni ya kutaka kufungua kwa kampuni hii , alitaka kupunguza Gharama za matangazo , kwani Vexto ilikuwa ikitumia Zaidi ya bilioni tano kwa mwaka kwa ajili ya matangazo lakini pia kulipa mabalozi wa bidhaa zao, hivyo aliamini akifungua kampuni ambayo itakuwa inahusisha maswala ya habari na burudani ni rahisi kwake kupromote bidhaa zake, pasipo kutumia kiasi kikubwa cha pesa , lakini pia mrembo huyu alipanga pia kampuni hio ampe Roma aiendeshe ili kukuza hadhi yake , hakupenda ije kufahamika mume wake ni mfanyakazi wa kawaida ndani ya Vexto.

“Wifey hilo swala la kuongoza kampuni siliafiki hata kidogo”Aliongea Roma na kumfanya Edna amwangalia kwa maswali, ni kama alitegemea upinzani kutoka kwa Roma.

“Kama hutaki basi sahau kuhusu rafiki yako kupata ajira”Aliongea Edna huku akirudisha macho yake kwenye tarakishi yake,Roma alimwangalia Edna.

Ukweli sio kama Roma hakupenda kuongoza kampuni, ila hakutaka kazi ambazo zitamfanya kufikiria, na hii ni kutokana na ugonjwa wake,Profesa Clark alimpa ushauri Roma wa kutofanya kazi ambayo itakuwa inaumiza kichwa.

“Wife hakuna namna nyingine ya kumsaidia rafiki yangu?”

“Roma mimi msimamo wangu ndio huo, ukikubali kuwa Director wa kampuni ambayo nitaifungua rafiki yako nitampa mkataba wa kazi wa kudumu na mshahara mzuri”Aliongea Edna na kwa namna ambavyo Roma alimuona mke wake ni kwamba alikuwa siriasi.

“Kuongoza kampuni sio jambo gumu sana Roma , kuna wataalamu ambao watakusaidia kufanya majukumu yote , wewe itaiuwa ni kutia sahihi tu na kutoa baadhi ya maagizo”Aliendelekea kuongea Edna na alionekana kumshawishi Roma.

“Okey !,Wife tufanye umeshinda , utampa rafiki yangu mkataba wa kazi wa kudumu na mshahara mzuri na mimi nitaongoza kampuni”Edna alijikuta akitabasamu , hakudhania jambo lake litaenda kirahisi hivyo,kwani usiku wote alikuwa akifikiria namna ya kumshawishi Roma juu ya jambo hilo.

“Hii ndio mbinu nzuri ya kumfanya awe siriasi na maisha,Anaweza kuona nafanya haya yote kwa faidia yangu ila ni kwa ajili yake”Aliwaza Edna.

Ni muda wa saa moja za jioni Roma alimuaga Edna na Bi Wema kama anatoka ila atarudi , na baada ya kutoka moja kwa moja alielekea Mbutu kwenye makazi ya The Eagles , alikuwa na mchecheto kweli wa kujua ni jambo gani The Eagles wameweza kulifanikisha kuligundua katika kazi aliowapaitia , kazi ambayo ilikuwa ni juu ya kumfatilia mtu aliekuwa akifahamika kwa jina la The Don ,lakini pia kujua muunganiko uliokuwepo kati ya Edna na Seventeen.

Dakika chache mbele alikuwa akiingia ndani ya kambi hii na leo ilikuwa tofauti kidogo , kwani alikuwepo Deigo pekee na Bram ndani ya jumba hili.

“Mfalme Pluto habari za wakati huu?”

“Salama Diego , naona vijana wengine siwaoni?”Aliongea Roma na kumfanya Diego kutabasamu kidogo

“Vijana wameenda kukutana na wapenzi wao”Aliongea Deigo na kumfanya Roma kushangaa.

“Usiniambie wote nane wamepata wapenzi?”

“Hahaha..Ndio mfalme Pluto ni mimi na Bram ambaye mpaka sasa tupo Single”

“Diego na ujanja wako wote umeshindwa kupata mchumba hapa Tanzania au hawakuvutii”.

“Mfalme Pluto wanawake wa Tanzania ni warembo sana na nimejaribu bahati yangu na kupata mmoja , tatizo limekuja anaonekana kupenda sana hela kuliko mapenzi”Aliongea Diego na kumfanya Roma acheke hakujua Diego ni mbahiri kiasi hiko.

“Nimeijia Ripoti Diego naomba usinipe nisome , nataka unielezee ili iwe rahisi kuelewa”Aliongea Roma na kuegamia kwenye sofa na Diego alichukua kishikwambi kilichokuwa kwenye meza na kupapasa kwa dakika kadhaa na kisha akakohoa kidogo alionekana kuwa na mzuka kweli.

“Mfalme Pluto nitaomba kuanza na taarifa ya The Don”Aliongea Diego na Roma alimpa ishara ya kuendelea.

“Kwa namna ambayo vijana wetu wameweza kukusanya taarifa , lakini pia kwa namna ambavyo marafiki zetu walio ndani ya MOSSAD walivyotusadia tumegundua yafuatayo”Alipozi kidogo.

Diego alieonekana kuwa na mchecheto juu ya taarifa hio na kwa Roma pia alijikuta akipata msisimko kwani hakudhania kama ripoti ya The Don imewafanya The Eagles mpaka kutumia mashushu(The Eagles wanaita mashushu marafiki) wao walio ndani ya kitengo cha kijasusi cha Taifa la Israeli cha MOSSAD.

“Kwanza kabisa mfalme Pluto tumegundua The Don ni jina tu la utambulisho ambalo halina muunganiko na mfanyabiashara yoyote wa madawa ya kulevya hapa nchini”

“Unamaanisha nini Diego?”

“Mfalme Pluto katika hatua zetu za kuchimba Zaidi Tumegundua The Don hahusiki moja kwa moja na biashara inayohusu madawa ya kulevya”Aliongea Diego na kumfanya Roma kushangaa.

“Wafanyabiashara wote wa madawa ya kulevya hapa Tanziania hakuna hata mmoja ambaye ashawahi kumuona huyu mtu ambaye anafahamika kwa jina la The Don, wakati tunafatilia taarifa tulikisia huenda Mheshimiwa Kigombola ndio mtu anaejiita The Don, lakini tulichogundua nikwmaba Mheshimiwa Kigombola sio The Don na hata yeye mwenyewe hamfahamu huyu mtu”

“Kwahio unamaanisha kwamba ndani ya Tanzania hakuna mtu ambaye anamfahamu The Don?”Aliuliza Roma.

“Ndio Your Majesty Pluto , ndani ya Tanzania hakuna anaemfahamu mtu anaefahamika kwa jina la The Doni licha ya kwamba wafanyabiashara wote wa madawa ya kulevya na wale wakufanya biashara ambazo sio halali ,kama vile kusafirisha viungo vya binadamu wanalipa kamisheni ya mapato yao kwenda kwa The Don”

“Diego hapo umenichanganya , umesema huyu mtu hawamjui , kwanini wanalipa mapato kwenda kwake?”Aliuliza Roma na Diego alitabasamu.

“Mfalme Pluto hilo ndio swala ambalo limetufanya tufuatilie kwanini wafanyabiashara wakubwa wa biashara ambazo sio halali wanalipa kamisheni kwa mtu ambaye hawamfahamu”

“Kwahio mmegundua nini?”

“Kwanza kabisa kutokana na kwamba tulikosa taarifa ambazo zinahusiana na huyu The Don kutokana na kwamba watu wengi hawamfahamu hapa Tanzania, tukafanya maamuzi ya kufuatilia usajili wa akaunti ya benki ambayo wafanyabiashara hawa hulipia Kamisheni , na tulichogungua ndio kilichotufanya kuwasiliana na marafiki zetu waliondani ya MOSSAD”Aliongea Diego na kupapasa kishikwambi chake kwa dakika moja.

“Kwanza kabisa baada ya kufuatilia kuhusu hii akaunti ya Benki, tuligundua ni Akaunti iliosajiliwa mwaka 1990 ndani ya Swiss Bank na Nyaraka ya vidhibiti vilivyoambatanisha jina la HEGEMONI , lakini licha ya jina hili pia tuliweza kugundua jambo ambalo sio la kawaida, tumegundua akaunti hii hupokea miamala ya fedha kila kona ya dunia na kila muamala unahusisha biashara ambazo sio halali”

“Hegemoni?”

“Ndio mfalme Pluto na baada ya sisi kufatilia kuhusu hili jina la Hegemoni tulishindwa kupata taarifa na hapo ndipo tulipowatafuta marafiki zetu kutoka MOSSAD na walitupatia taarifa ya kushitusha kidogo , ambayo wote hapa ndani imetushangaza kidogo”

“Taarifa gani?”

“HEGEMONI is uknown person”

“HEGEMONI hafahamiki”Roma alishangaa inawezekana vipi watu waweke fedha kwenye akaunti ambayo mtu anaeimiliki hio akaunti hafahamiki.

SEHEMU YA 98

Hegemony katika Ugiriki ya kale ni neno lenye maana ya kikundi au nchi yenye nguvu ya kutawala wengine aidha kwa njia ya utamaduni , Dini ,Kijeshi au kiuchumi.

“Mfalme Pluto kwa maelezo marahisi ni kwamba The Doni wa Kenya ndio huyu huyu wa Tanzania na The Doni wa Mexico ni huyu huyu wa kitanzania”Aliongea Diego na kumfanya Roma atafakari , kama kweli maneno ya Deigo ni kweli basi huyu mtu anaejiiita The Doni ni mtu ambaye ana nguvu kubwa sana, lakini pia hata kama mtu huyo ana nguvu ni kwa namna ipi ameweza kuwa’control’ wafanyabiashara wakubwa mpaka kumtii na kumlipa , hilo ndio swali ambalo liliibuka kwenye kichwa cha Roma.

“Mfalme Pluto tumeweza pia kugundua The Doni kwa kila taifa ana mwakilishi wake”

“Kwa hapa Tanzania mwakilishi ni nani?’

“Kwa hapa Tanzania tumegundua mwakilishi mkuu wa The Doni ni mheshimiwa Kigombola”

“Unamaanisha Raisi Mstaafu ndio anamwakilisha The doni?”

“Ndio Mfalme Pluto”

“Kama ni kweli , ni kwa njia gani Kigombola ameweza kukutana na huyu The Doni , kwani haiwezekani awe mwakilishi pasipo ya wao kukutana”

“Ndio mfalme Pluto, na sisi mpaka sasa tunafanyia swala hilo kazi kujua ni kwa namna gani hawa wawili wanafanya mawasiliano , lakini pia ni kwa namna ipi The Doni kawa na nguvu ya kumfanya Mheshimiwa Kigombola kumtii ,na sio kwa Tanzania tu kwa kila taifa , tunajitahidi kuweza kujua ni kwa namna gani na kwa nguvu ipi the Doni ameweza kuwafanya wawakilishi wake kumtii ”Aliongea Diego.

“Ndio ripoti imeisha hivyo Diego?”

“Hapana Mafalme Pluto Ripoti inaendelea”alipozi kidogo na kupangusa upande kishikwambi chake kwa dakika kadhaa.

“Mfalme tumeweza pia kugundua licha ya akaunti hii inayomilikiwa na Hegemoni kuingiziwa pesa kila kona ya dunia , tumegundua pia jambo ambalo limetushangaza kidogo”.

“Lipi hilo Diego?”

“Tumeweza kugundua pia kuna miamala ambayo imetoka kwenye hii akaunti tofauti na ile ambayo inaingia”Roma alishangaa.

“Kwahio unamaanisha kuna watu wanatoa pesa kwenye hii akaunti ,kama ni hivyo hao watu ni nani?”

“Mfalme Pluto kwa tulivyowezakufuatilia benki ya Swiss imetoa kadi mbili tu za aina ya ‘Black Card’ kwa watu wawili na hao watu wawili ndio ambao wanatoa hela kwenye hii akaunti, kutokana na msaada wa MOSSAD kupata taarifa haikuwa ngumu kwetu ,na kwa taarifa yao wametupatia majina mawili ambayo ndio wanatoa pesa kwenye hii akaunti na jina la kwanza ni la Yan Buwen na jina la Pili ni Dorisi Alex”.

“Na taarifa za hao watu zipoje”Aliuliza Roma na Diego alitabasamu na kisha alipangusa kwa dakika kadhaa na kisha akampatia kishikwambi kile Roma.

Roma macho yalimtoka ni kama taarifa ambayo alikuwa akiisoma haikua ya ukweli , kwani aliweza kuona taarifa za Dorisi Alex ambaye alikuwa akimjua kabisa na sio kumjua tu lakini pia alikuwa mpenzi wake , jambo hili lilimshangaza na hakuelewa hili linawezekana vipi.

Kwa maelezo ya Diego The Doni alikuwa ni kama mtawala wa biashara haramu zote, kutokana na kwamba The Doni wa Tanzania ndio The Doni pia ambaye yupo kwenye mataifa mengine na hii ni kutokana na kwamba pesa zote za kamisheni kwa wafanyabiashara wa Madawa ya kulevya na zile ambazo ni haramu nyingine pesa yao ilikuwa ikienda kwenye akaunti moja inayotambulika kwa jina la Hegemoni.

“Diego kuna uhakika wa huyu Dorisi kumiliki kadi ambayo inatoa pesa kwenye hio akaunti?”

“Ndio mfalme Pluto na tuliweza kuihakiki kabisa hii kadi baada ya vijana kuingia ndani ya nyumba anayoishi Dorisi na hizi ni picha za kadi ambayo anamiliki Dorisi”Roma alizinagalia picha hizo na ni kweli ni kadi ya yenye jina la ‘Platinum’ ya rangi nyeusi.

“Kwahio mnahisi ni uhusiano gani ambao Dorisi anao na The Doni mpaka kumiliki hii kadi?”

“Mheshimiwa Pluto hilo hatujaweza kulipatia ufumbuzi , ila tumeweza kufatilia taarifa za Dorisi kwanzia wazazi wake na asili yake kwa ujumla”

“Na mkagundua nini?”

“Wazazi wa Dorisi walipotea kwenye mazingira ya kutatanisha mwaka 2010 hio ni kwa taarifa ya jeshi la Polisi la Tanzania na mpaka sasa ‘They are Declared Dead”Roma aliona hii ripoti inaanza kuumiza kichwa chake , maana kila kitu kilikuwa kipya kwake.

“Kuna sababu zozote za hao wawili kupotea kwao , na walikuwa na kazi gani hapa Tanzania?”

“Walikuwani wamiliki wa mgodi wa Almasi huko Mwadui”

“Vipi kuhusu Yan Buwen?”

“Yan Buwen ni mwanasayansi ngazi ya PhD na jambo la kushangaza Zaidi ni kwamba Profesa aliesimamia masomo yake ya ngazi ya juu ni Profesa Clark”Roma aliendelea kushangaa.

“Vipi kuhusu wazazi wake, kuna taarifa yoyote ambayo inamuunganisha huyu Yan Buwen na Dorisi?”

“Yan Buwen wazazi wake wote wapo hai na ni raia wa China na mpaka sasa wapo hai na ni familia yenye nguvu ndani ya Beijing na hakuna muunganiko wa aina yoyote na Dorisi Zaidi ya kuwa na kadi za Black Card”

“Okey! Diego nipatie hio Ripoti ya The Doni nitaipitia mwenyewe taratibu , lakini nadhani kuna kazi kubwa Zaidi ya hii kuhusu huyu the Doni nataka muendelee kuchimba taarifa zake mpaka tupate kujua ni nguvu gani anayo huyu mtu na pia tufahamu ni nani”

“Sawa Mfalme Pluto”

“Nielezee na taarifa ya Edna na Seventeen , kwanini wanafanana kama mapacha na muunganiko wao , nadhani mnataarifa ya kutosha”

“Mfalme Pluto kwanza kabisa niende moja kwa moja kwenye hitimisho la uchunguzi wetu, kwanza mpaka sasa tuna makisio ya juu ya Madam Edna na Seventeen kuwa mapacha”

“Ushahidi uliowapelekea kuwa katika hayo makisio ni upi?”

“Kwanza tumegundua Edna baba yake halisi ni Raisi wa Rwanda Mheshimiwa Jeremy ”Roma alitoa macho.

“Na huu ndio ushahidi wa kuonyesha Rahel mama yake Edna na Mheshimiwa Jeremy walikuwa na mahusiano ya muda mrefu tu ambayo yalikuwa ni ya siri”alimpa Picha Roma na ni kweli kwenye picha Rahel na Mheshimiwa Jeremy walikuwa wakionekana kwenye ufukwe wakiwa wamekumbatiana kimahaba , fukwe ambayo Roma kwa kuangalia tu aliweza kuijua.

“Mmeweza kupata vipi hizi picha?”

“Bram aliweza kufanikisha kuhack Emaili ya Mheshimiwa Jeremy na tuliweza kusoma baadhi ya jumbe na viambatanisho ambavyo vimetoka kwa Jeremy kwenda kwa Raheli kwa muda tofauti tofauti na hapa ndipo tulipoweza kufungua kodi na kujua wawili hawa walikuwa na mawasiliano , lakini licha ya kujua jambo hili kuna meseji tatu ambazo kidogo zimetushangaza na ndio zilizotupelekea kujua Edna na Seventeen wanaweza kuwa ndugu wa damu”

“Meseji gani?”

“Hizi hapa Mfalme Pluto”Alimpatia tena kishikwambi na Roma aliweza kusoma jumbe hizo.

1.“Najutia maamuzi yangu Jeremy ya kukukabidhi loraine ,huenda maka sasa ningekuwa na watoto wangu wote mapacha”

2.”Raheli najua ni namna gani unaumia , lakini hili swala naomba liwe siri kwa Edna kama amezaliwa na dada yake”

3.”Raheli kabla sijafa nitahakikisha nalipiza kisasi kwa wote na nitahakikisha naujua ukweli juu ya kilichonyuma ya ajali ya ndege ya M Airline”.

Hizo ndio jumbe ambazo Roma aliweza kuzisoma na kumshangaza kwa wakati mmoja na kwa meseji hizo ni kweli Edna alionekana kuzaliwa na pacha wake anaefahamika kwa jina la Lorraine, lakini bado haikumthibitishia kama Seventeen ni Lorraine anaetajwa kwenye hizo jumbe na yeye swala hilo likabaki kwenye makisio.

“Kama kweli Lorraine ni Seventeen ilikuwaje mimi na yeye tukawa ndani ya kile kisiwa”Aliwaza Roma.

Ukweli ni kwamba Roma hakuwa na kumbukumbu zozote za maisha yake ya nyuma , kwani kumbukumbu alizokuwa nazo ni za Sehemu ambayo yeye mwenyewe anaita kisiwa , lakini kuhusu kumbukumbu ni kwa namna gani aliweza kuingia kwenye hiko kisiwa akiwa pamoja na Seventeen haikueleweka.

Sasa Roma anatambua kuwa baba yake Edna ni Raisi wa Rwanda , swali bado linabaki kwenye kichwa chake , kama baba yake Edna ni Raisi wa Rwanda yeye baba yake ni nani na mama yake ni nani , asili yake ni ipi?”.

Hakukua na kubwa sana kutoka kwenye Ripoti ya Diego dhidi ya Edna na Seventeen Zaidi ya kujua kuwa mama yake Edna alikuwa na mahusiano na Jeremy Raisi wa Rwanda.

Roma aliingia kwenye gari yake kuianza safari ya kurejea nyumbani , hakuwa na jambo lingiine la kumfanya kuwa ndani ya hio kambi , aliona atapitia ripoti hio kwa umakini akiwa nyumbani.

Roma akiwa njiani bado mawazo hayakumuacha salama , alikuwa akiwaza hili na kurukia jambo lingine.

“Kwanini Dorisi amiliki kadi inayotoka kwa The doni , wana uhusiano gani , au yeye anamfahamu huyu The Doni , Huyu Yan Buwen ana uhusiano gani na The Doni na yeye kumilikishwa kadi ya kitajiri , wazazi wa Dorisi kwanini wapotee”Roma aliwaza Zaidi mpaka kupelekea kichwa chake kuwa kizito na alihisi kitampasuka , alijiambia kwa sasa hatakiwi kuwaza Zaidi , kazi hio ya kuwaza viijana wake wataifanyia kazi , yeye jambo la kufanya kwa wakati huo ni kutuliza kichwa.

Ilikuwa ni saa nne za usiku , Roma hakujisikia kabisa kurudi moja kwa moja nyumbani , alitamani atembe tembee ili kupata hewa safai ndani ya eneo hili la Kigamboni.

Roma alikuja kusimamisha gari yake pembeni mwa barabara kuu , mita kadhaa kutoka Pongoni Beach.

Alishuka kwenye gari na kuanza kutembea taratibu kuelekea upande wa ilipo hii Beach na siku hii ndani ya hili eneo kulionekana kuna burudani iliokuwa ikiendelea ndani ya hayo maeneo kwani watu aliokuwa akipishana nao walikuwa ni wengi licha ya muda kwenda , lakini pia alikuwa akisikia Mziki uliokuwa mbele yake , alitembea taratibu huku akifurahia upepo wa fukwe.

Baada ya kutembea kama mita mia moja hivi alijikuta akisimama sehemu ambayo ilikuwa na kibanda kama kiosk , ambacho kwa haraka haraka aligundua kibanda hiki kilikuwa ni cha chips , haikueleweka alivutiwa na nini lakini alikisogelea na wakati uleule walionekana watu wawili msichana na Mvulana wakisogelea kile kibanda.

“Tufungie Chips na mishikaki minne”Aliongea yule mvulana.

“Sawa”Sasa Sauti hii kidogo ilimshangaza Roma ilikuwa ni ya kike na hili ndio jambo ambalo lilimvutia na mtu aliekuwa akiuza kwenye hilo eneo ni kama ashawahi kumuona , alisogea mpaka karibu na hapa ndipo alipogundua hisia zake zilikuwa ni za kweli , alikuwa ni mwanadada aliemchomolea waleti kwenye Mwendokasi.

“Anko!”Aliita yule msichana ambaye aliikuwa na ushombe ushombe ambao Roma alishindwa kuujua ni wa muunganiko mtu mweusi na mtu gani.

Roma alikaa kwenye benchi lililokuwa pembeni bila ya kuongea neno huku akimwangalia bidada huyu alivyokuwa akihangaika kuwahudumia wateja wake.

SEHEMU YA 99

BOLIVIA –AMAZONI 1990

Ni ndani ya mwaka 1990 miezi minne tu baada ya kijana Levente pamoja na Profesa Banosi kupigwa Risasi nchini Hungaria ndani ya mji mkuu wa Budapest .

Ndani ya sehemu moja iliokuwa katikati ya Msitu wa Amazon kilomita kadhaa kutoka mji mkuu wa La Paz , ilionekana Chopa iliokuwa ikiambaa ambaa angani ndani ya msitu huu , huku ikiwa na nembo ya Jeshi.

Ndani ya chopa hii walionekana wanaume wawili waliokuwa kwenye mavazi ya suti na miwani usoni pamoja na marubani wawili ambao walikuwa na umakini wa hali ya juu sana kuendesha ndani ya eneo hili la huu msitu , wanaume wote wawili ambao walikuwa wamevalia suti walikuwa ni wazungu , kwa haraka haraka wanaume hawa wawili walikuwa kati ya umri wa miaka arobaini hivi , kwa aliekuwa ameketi upande wa kushoto alionekana kuwa mkubwa Zaidi kuliko wa upande wa kulia.

Baada ya Chopa hii kutembea kwa umbali wa kilomita kama moja hivi mbele upande wa chini lilionekana jengo ambalo lilikuwa limejengwa kwa mabati magumu sana kwa muuno wa mshale , lakini pia kwa duara.

“We are Landing Sir”aliongea Rubani upande wa kushoto akiwaangalia wanaume waliovalia suti na hawa wanaume walipeana ishara ya kukubali.

Dakika chache mbele Chopa hii ilianza kushuka chini taratibu ikilikaribia jengo hilo ambalo kadri mabwana hawa walivyokuwa wakilikaribia lilikuwa likiongezeka ukubwa , huku upande wa chini wakionekana baadhi ya wanajeshi ambao walikuwa wakilinda, na wanajeshi hawa kwa mavazi yao haikueleweka walikuwa ni wa jeshi gani kwani mavazi yao hayakuwa na nembo yoyote licha ya kushikiria siraha nzito kwa kuzunguka eneo hilo lote ambalo pia limezungushiwa waya.

“Mr Anderson I am happy to see you again”Aliongea mwanamama mmoja hivi alievalia suti ya Zambarau mrefu kidogo aliekuwa rika la ujana.

“Me Too Mellissa”aliongea Mr Anderson ambaye alikuwa ni yule mzee kidogo na Mellisa alimgeukia yule mwanaume mwingine ambaye alionekana mtu mzima lakini mdogo kwa Andersson.

“Mellisa kutana na Mr Cohen ni Mafadhili mpya wa Project yetu,Mr Cohen huyu ni Mellisa Luiz ndio Meneja ndani ya hii kambi ya Pro Human”Aliongea Anderson na Mellisa alimpa mkono Coheni kusalimiana nae na walianza kupiga hatua kuelekea ndani ya jengo hili ambalo lilionekana kuwa kubwa kwa muonekano wa chini kuliko ilivyokuwa juu, lilikuwa limejengwa na mabati magumu na muonekano wake ulikuwa ni kama kiwanda , na pia kulikuwa na sauti ya mvumo wa Sauti ya majenereta ndani ya hili eneo.

“Banosi was Real Amaizing Anderson , This is Beyond my Expectations”Aliongea Coheni huku wakiangalia kupitia kioo vitoto vichanga ambavyo vinaonekana kwenye makabati ya vioo , na kilichomfanya mzee huyu ashangae ni namna ambavyo ubongo wa vichanga hivyo ulivyokuwa ukionekana kwenye Screen.

“Your Gradfather was Great Scientist Cohen and with this Discovery we are going To Create the God`s hahaha..”Aliongea Anderson na kutoa cheko na kumfanya Mellisa kutabasamu.

Kwa jinsi sehemu hii ilivyokuwa ikionekana , ilionyesha kama maabara ya kisasa kabisa , kwani kulikuwa na machine za kisasa zilizofungwa.

Wakati mabwana hawa wakiendelea kushangazwa na maendeleo ya Projekti yao , mara aliingia mwanajeshi mmoja aliekuwa ameshikilia bunduki lake na kumfanya Mellisa ageuke na kumwangalia Mlinzi huyu.

“What is it Carlos?”

“There is Problem Mellisa. which need your attention”

“What! , Which Problem”Aliongea mwanamama huyu huku akiongoza njia nakuacha mabosi hawa ndani na Carlos alifuatisha nyuma na walikuja kusimama kwenye mlango ambalo ulikuwa na bango kwa juu ‘CCTV control And Monitoring Room’.

Wakati Mellisa anaingia kwenye chumba hiki ,Alarm ya jengo hili ilianza kutoa mlio wa kuashiria kuna uhatari uliokuwa ukitaka kutokea na kufanya wanajeshi wote waliokuwa wakilinda wajiandae kukabiliana na tatizo , lakini ilikuwa ni jambo la Ghafla sana , kwani ile Mellisa anakimbilia nje kwa spidi ulisikika mlio ‘Vuuum’.

“Boom” ‘Boom’

Ulikuwa ni mlipuko ambao haukuwa wa kawaida ambao uliacha eneo lote kuwaka moto , kwa haraka haraka mlipuko huu ulisababishwa na mabomu ambayo ,yalionekana kutegwa na mtu ndani ya eneo lote la hapa ndani.

Haikueleweka kuna mtu ambaye aliweza kusalia ndani ya hili eneo kwani moto ulikuwa ni mwingi sana na ulikuwa umezingira karibia eneo lote.

Baada ya kama nusu saa hivi kupita kilometa kadhaa kutoka lilipo hili eneo , alionekana bwana ambaye alikuwa kwenye mavazi ya suti akikimbia huku akionekana kubeba mtoto ambae amemviringisha kwenye mavazi ya bluu ambayo ni kama ya hospitalini , huyu bwana alikuwa ndie alietambulishwa kwa jina la Cohen.

Alikuwa akihema kama mbwa huku akizidi kusonga mbele na baada ya dakika chache za mwanaume huyu kukimbia hatimae aliweza kufika eneo ambalo lilikuwa na uwazi na kupunguza mwendo huku akigeuza shingo kulia na kushoto , kama mtu ambaye alikuwa akitafuta mtu, hili eneo halikuwa hata na aina yoyote ya kuonesha kama lilikuwa na mtu , kwani Zaidi ya keleleza ndege pamoja na wanyama , hakukua na sauti yoyote ya kuashiria kuna binadamu anaeishi ndani ya haya maeneo.

“Ryan.!!”Ilikuwa ni sauti ya mwanamke, ilisikika katikati ya huu msitu na kumfanya bwana huyu asimame na kugeuza macho kulia na kumuona mwanadada wa kizungu akimkimbilia kwa spidi , huku akionesha hali ya shauku kwenye uso wake.

“You did it, Our Plan worked”Aliongea huyu mwanadada huku akimsogelea Ryan kwa mwendo hafifu ni kama hakuwa akiamini.

“Epholia we got our Daughter Back!, We did it”Aliongea yule bwana huku akionesha furaha na hamasa kwenye macho yake huku akimfunua taratibu yule mtoto.

Kwa jinsi walivyokuwa wakionekana hawa wawili ni Dhahiri kabisa aliekuwa kwenye mikono ya Ryani ni mtoto wao wa kike , walionesha hali ya hamasa na furaha kwenye macho yao.

Ryani alimpa Epholia yule mtoto na baada ya kumpa alivua suti na shati alilokuwa amevaa na kujifinya kifuani na kuvuta ngozi kwa juu na palepale alionekana kama mpira ukijitengenisha na ngozi, alitumia mkono wa kushoto na kuingiza kidole kwa chini na kikapita kwenye ngozi na akavuta kwa juu na hapa ndipo ilipoonekana akijivua gamba la Juu na kila kitu kikabadilika , bwana huyu alikuwa mtu mwingine kabisa tena lika la ujana , hakuwa Cohen tena.

Wakati wakiwa wamesimama kwenye hili eneo , mara walianza kusikia sauti za mvumo wa Chopa kutoka mbali ikija uelekeo wao na kuwafanya waangaliane na kukimbilia ndani kabisa ya msitu.

Hii ilikuwa ni miaka ya Tisini, tukio hili linahusiana vipi na hii simulizi , utaelewa mbele.

****

“Unaitwa nani?”Aliuliza Roma mara baada ya wale vijana ambao walikuja hapo kwa ajili ya kununua chipsi kuondoka.

“Yezi”Alijibu huku akigeuza geuza viazi vilivyokuwa vikichemka na mafuta na Roma alishangazwa na hilo jina.

“Sasa Yezi huogopi kufanya kazi usiku wote huu?”

“Hakuna wakunigusa , ndio maana”Aliongea Yezi na kumfanya Roma atabasamu , alifurahishwa na namna ambavyo Yezi alikuwa akijiamini.

“Anko kama umekuja kuniuliza maswali naona tu uondoke maana nipo kazini”Aliongea Yezi.

“Unapaswa kunishukuru kwa kukuachia salama baada ya kuniibia waleti yangu”Aliongea Roma lakini muda huo zilikuja pikipiki nne ambazo zilikuwa zikitokea barabra kuu na Roma macho yake ya haraka haraka aliweza kutambua watu waliokuwa wakiendesha hizi pikipiki ni vijana wadogo na Wote walikuwa ni mashombe shombe kama ilivyo kwa Yezi, ila hawa Roma aliweza kuwatambua kama mchanganyiko wa Arab na Mbongo.

“Yezi unajifanya sana mjanja na leo tumekukamata , lazima ulipe hela yetu”Aliongea kijana mmoja hivi kwa rafudhi ambayo ilidhihirisha sio mzawa.

“Abdull yule jamaa nilidhani anatudanganya kumbe ni kweli huyu choko kahamia huku”Aliongea kijana mwingine na Roma aliendelea kuwaangalia tu hawa vijana , hakuelewa ni kipi kinaendelea , lakini alitaka kuona mwisho wake.

“Sharif tulishamalizana , kwanini mnaendelea kunighasi na maisha yangu”

“Hahaha,,acha kujifanya mjanga Yezi nani kakuambia unaweza kufanya kama unavyotaka, hatukukulazimisha kujiunga na kundi letu lakini hauwezi kutoka kwa hiari , lazima ulipie”Kwa jinsi ambavyo vijana hawa walivyokuwa wakiongea Roma aliona kama wavuta bangi tu , ila alitulia kwenye benchi huku akimwangalia Yezi aliekuwa bize pasipo kuwazingatia hawa vijana.

“Sharif unamuona alivyonadharau , mnaonaje tukichukua kila kitu na tujajilipizia , japo naamini pesa tunayomdai haiwezi kutoka kwenye hiki kibiashara”Aliongea Dogo Abduli na walisogea upande wa karai lililokuwa likichemka na dogo mmoja ambaye alikuwa mkimya muda wote alisukuma kalai lililokuwa likichemka na mafuta yake chini kwa kutumia Helmeti na kumfanya Yezi amwangalia na kupandwa na hasira.

“Sharif mnataka nini kwangu , si tulishamalizana mbona mnanifanyia hivi kila siku hamtaki kunipa Amani”

“Unaongea sana Yezi”Aliongea Sherif na kuvuta kabati la chipsi na likatua chini na kumfanya Yezi akasirike na kumpiga na chujio la kuepulia chipsi.

“Arrghh”alitoa mguno wa maumivu na baada ya wenzao kuona mwenzao kajeruhiwa walimzunguka Yezi na kumshika mikono na Abduli alimsogelea na kumsindilia ngumi ya tumbo na kumfanya Yezi agugumie kwa maumivu , walimpiga na mtama wakamuweka chini kwenye mchanga na dogo ambaye hakuwa muongeaji sana alichukua sahani ambayo ilikuwa ikitumika kupimia Chipsi na kuchota mchanga ambao ulikuwa umechanganika na mafuta ya moto yaliomwagika na kumsogelea Yezi.

Roma aliona sasa hawa madogo wanazidi manyanyaso , alimsogelea yule dogo na kumvuta kwa juma na kumpiga kibao na kudondoka pembeni.

“Haya ondokeni”Aliongea Roma kuamrisha wale vijana lakini walionekana kukasirika maradufu kwani Sherif alichukua chujio lile la kuepulia na kumsogelea Roma kwa dhamira ya kumpiga nalo , lakini ni kama Roma alikuwa ametegemea kwani kabla hata hajamfikia alimfyeka mtama na kudondoka chini.

“Anko nyuma yako”Aliongea Yezi ambaye aliachiliwa sasa na hawa vijana na kuona wamdhibiti Roma , na kuna mmoja aliekuwa kwa nyuma alieshikilia jiwe kwa ajili ya kumpiga Roma na kabla hata ya Yezi hajamtahadharisha , yule Dogo alirusha , lakini Roma ni kama masikio yake yalikuwa na macho kwani alikwepa kidogo na likaenda kumpata Abduli ambaye alikuwa akinyanyuka huku akijifuta mchanga.

“Mamaaa….!!!”Alitoa ukulele , lakini sasa muda huo huo ilikuja gari ya Doria iliokuwa na polisi na kuwazingira , ilikuwa ni ghafla sana

SEHEMU YA 100​

Vijana ni kama hawakuwa wametegemea polisi kuja eneo hilo , kwani walishindwa hata kujitetea, polisi wale waliwashika mmoja mmoja na kuwafunga pingu hawakukata maelezo

“Nyie ndio Mnaofanya wananchi wanalamikia polisi kwa kutofanya kazi yake kwa weredi na leo mtatutambua”Aliongea polisi mmoja mwembamba huku akimfunga Yezi pingu mikononi, walionekana hawakutaka kujua kabisa ni nini kilikuwa kikiendelea hapa kwenye hili eneo na waliona kila mmoja alikuwa ni mhalifu , hata Roma mwenyewe walimuona kama mhalifu tu.

“Gondwee mfunge huyo mpuuzi ,ndio litukutu likubwa hilo”Aliongea polisi ambaye alionekana kiongozi na kumpiga Roma bao la mgongoni.

“Aaah ! Maafande namna gani sasa hii ya kupigana na usiku wote huu”

“Tulia Ngederec wewe , unajifanya mjanja ngoja tukakushikishe adabu na hiki kiburi lazima kitaisha”Aliongea huku akimfunga Roma pingu na Roma hakutaka kuleta ubishi alikubali kufungwa pingu.

Watu waliokuwa wanapita walishangaa kile kilichokuwa kikiendelea kwa polisi hao , ila hakuna ambaye alijaribu kuuliza , kila mtu aliendelea na mambo yake , lakini pia na wenyewe waliogopa kujumrishwa.

Dakika kama kumi tu hivi Roma na wale vijana watukutu walisweka kwenye difenda na ikaondolewa hapo kwa kasi kuelekea kituoni, Roma alishangazwa na aina hii ya utaratibu wa polisi ila hakutaka kuleta ubishi , alitaka kuona mwisho wake.

Vijana walionekana kuwa na wasiwasi ila kwa Roma hakuwa na wasiwasi na baada ya dakika kama nane hivi waliingizwa ndani ya kituo cha polisi.

“Wamefanyaje hawa tena?”Aliongea mwanamama mmoja ambaye amevaa mavazi ya kipolisi , ni kama alikuwa akiwafahamu hao vijana.

“Walikuwa wanaleta vurugu Afande , watalala leo hapa kituoni”.

“Afande huyu Anko hana kosa alikuwa akinisaidia tu”

“Kimya wewe mbuzi”

“Oya Afande hebu niachieni nataka niondoke”Aliongea Roma ambaye alikuwa amekarishwa kwenye benchi na yule mama alimwangalia Roma.

“Hawatatuachia hawa mpaka asubuhi”Aliongea Yezi.

“Nilale hapa polisi kwa kosa lipi?”Aliongea Roma kwa sauti na kusogelewa na polisi na kupigwa buti mguuni.

“Tukisema tulia tulia wewe nguruwe”Aliongea polisi mwembamba huku akimwangalia Roma kwa hasira.

“Hawa watoto kila siku sio wenye kusikia , kila siku ni wenye kufanya fujo tu ,Wewe Sherif umesahau onyo la baba yako wiki iliopita , kwanini unapenda kuleta fujo”aliongea yule mama huku akimwangalia Sherif lakini kijana huyu hakuongea lolote Zaidi ya kununa na kuzika kichwa chake chini.

“Afande Mnene , unaonaje kwanza ukiuliza nini kimetokea , maana nipo hapa kimakosa” Aliongea Roma lakini mwanamama alionekana kutomzingaria na kumfanya Roma apandwe na hasira.

“Anko usiwe hivyo , watatuachia asubuhi”Aliongea Yezi lakini Roma hakutaka kubaki ndani ya hili eneo, lakini pia hakutaka kutumia mabavu kutoka , alitaka atii sheria ilia toke lakini polisi walionesha kutomsikiliza.

“Chief!!”Ilikuwa ni sauti ya afande Mnene akisimama wima baada ya mwanamke mmoja ambaye pia alikuwa kwenye mavazi ya kipolisi kuingia , Roma aliinua macho yake na kumwangalia huyo alieitwa chifu na kuona huenda huyo anaweza kumsikiliza , lakini baada ya kumwangalia tu alimfahamu , kwani alikuwa ni Mage.

“Okey! Afande Mage Bora hata umekuja nadhani nitawahi kwenda nyumbani”Aliongea Roma na kumfanya Mage ambaye hakuwa amemuona Roma ageuke na kumwangalia.

“Mr Roma unafanya nini hapa?”

“Waulize hao polisi”Aliongea Roma na Mage aliwageukia polisi akitaka maelezo.

“Afande walikuwa wakifanya fujo Pongoni Beach” Aliongea polisi mwembamba na Mage aligeuza macho kuangalia wale vijana ambao wote baada ya Mage kuingia hapa ndani waliinamisha vichwa vyao chini , ni kama hawakutaka Mage awaone na hata kwa Yezi pia , Mage alisogea na kuinua kichwa cha Sherifu.

“Ni nyie wajinga”Aliongea Mage na alionesha kuwafahamu hao vijana, alisogea kwa kila mmoja na kumwangalia na akamalizia kwa Yezi na kujikuta akitabasamu.

“Afande unaweza ukamuachia Mr Roma pale , nitadili na hawa vijana”Aliongea Mage na wale polisi walijikuta wakishangaa , lakini hawakutaka kubisha , alichukua ufunguo na kumfungulia Roma na kutoa zile pingu.

“Afande Mage mimi sijaleta fujo ni Sherifu na wenzake ndio waliokuja kunianza kwenye eneo langu la biashara”Aliongea Yezi na alionesha kumfahamu Mage na kumfanya Roma ashangae.

“Yezi kaa kimya ,Sherifu unakumbuka nilikupiga mpaka ukazimia Osterbay , mpaka ukanifanya nipewe adhabu ya kuwa trafiki na kutolewa kwenye cheo changu sasa nasema hivi, mimi Mage kwakua umenifuata tena nitahakikisha mkitoka hapa akili zimewakaaa sawa”Aliongea Mage na hapa hakujali tena uwepo wa Roma hapo ndani na Roma ambaye alikuwa ameruhusiwa kuondoka , alibakia hapo hapo ndai kuona ni nini kinaendelea, hakutaka kuondoka akimuacha Yezi ilihali hakuwa na makosa.

“Afande Mage!,Unaonaje ukiuliza kwanza nini kimetokea kuliko kuanza kuwatishia”Aliongea Roma kwa sauti ya kawaida na kumfanya Mage amwangalie.

“Mr Roma usharuhusiwa , unaweza kuondoka , hawa vijana nawajua sana tu ni waharifu wa kupindukia na wanahistoria ya kukamatwa na polisi Zaidi ya mara tano”

“Lakini Yezi hahusiki, hawa madogo ndio wamekuja kumfanyia fujo mwenzao”Aliongea Roma na kumfanya Yezi amwangalie Roma alijisikia vizuri kwani ni mara yake ya kwanza kupata mtu wa kumtetea.

“Ndio Afande Mage mimi sihusiki , walikuja kunifanyia fujo , nilishaachana na kundi la Sherif na ndio maana nikahamia hapa Kigamboni kuanza maisha upya”Aliongea Yezi na alionesha hali ya kuogopa mara baada ya kuingia Mage.

“Anachoongea ni kweli Koplo?”Aliuliza Mage.

“Afande …”

“Hauna haja ya kuwauliza hao wapuuzi , wamekuja eneo la tukio na wakatusweka mpaka hapa pasipo ya kujua sababu , hawaelewi chochote hata tukio lilivyokuwa”Aliongea Roma .

“Chunga kauli yako , upo polisi hapa Mr Roma usijifanye kwasababu unafahamina na Chief unaweza kututukana , aliongea Koplo akimsogelea Roma na Roma alijikuta jaziba ikimpanda na alisimama haraka sana na kumpiga mtama Koplo na alitua chini kama furushi na Roma hakuishia hapo tu alimkanyaga kwenye vidole vya mikono na kumfanya bwana huyu atoe ukulele wa muamivu.

Yezi na vijana watukutu walijikuta wakishangazwa na namna ya Roma kujiamini , ilikuwa ni mara yao ya kwanza kushuhudia Polisi akipigwa ndani ya kituo cha polisi.

“Polisi mnakosaje utimamu wa akili , mnaweza vipi kulinda raia kwa staili hii”Aliongea Roma na kumwachia na kisha akamsogelea Sherifu na kunnyanyua juu.

“Wewe ndio utaelezea tukio zima na ole wako udanganye”Aliongea Roma kwa sauti ya kuamrisha , lakini Sherif hakutaka kuongea , aliangalia chini kwa jeuri na Roma hakutaka kumchelewesha alimning`iniza hewani na mkono mmoja na kumfanya aanze kukohoa huku akitapatapa.

Sio Mage tu hata polisi wenzake walishangazwa na nguvu alizokuwa nazo Roma lakini pia ujasiri wake.

“Utaongea huongei?Au ni kuvunje shingo?”.

“Roma muachie utamuua”Aliongea Mage kwa wasiwasi , lakini Roma ni kama hamsikii alizidi kumminya Sherif mpaka pale alipokata moto ,alimtupia chini, na kufanya polisi hawa wamsogelee Sherif kwa wasiwasi.

“Mmoja wenu ajitolee kuongea la sivyo mtafuatia mmoja mmoja”Aliongea Roma na vijana hawa watatu waliobaki , walianza kuangaliana kwa wasiwasi.

“Mnajifanya mabubu sio , Nitaanza na wewee”

“Nitaongea…”Alinyanyuka Abduli kwa pupa .

Abduli alianza kuelezea tukio kiuwoga woga , kwenye maisha yake hakuwahi kukutana na mtu wa aina ya Roma na ndio maana aligopa.

“Afande nadhani mpaka hapo Yezi hana kosa”Aliongea Roma.

“Yezi unaweza kwenda ila nakutahadharisha tu kama umebadili tabia yako iwe kweli , siku ukiletwa polisi ninakupeleka gerezanni moja kwa moja”Aliongea Mage

“Afande Mage , nimebadilika kweli nishaachana na kuwa mtoto mtukutu”

“Maneno yako yawe kweli”Aliongea Mage na kisha akamgeukia Roma , alishindwa kwanza kuelewa kwanini Roma alikuwa nje muda huu wa saa nne mpaka kukamatwa na polisi wakati ameoa na anatakiwa kuwa na mke wake nyumbani.

“Afande Mage kazi njema”Aliongea Roma huku akimshika Yezi bega wakitaka kutoka.

“Roma tunaweza kuongea kidogo”Aliongea Mage na kufanya Askari hawa washangae ni ukaribu gani Mrembo Mage na Roma wanao.

“Sawa”aliitikita Roma na Mage alitoka na Roma mpaka kwenye kijibaraza.

“Unasemaje ?”

“Mbona unauliza kwa usiriasi hivyo Roma kama hatufahamiani , au ushasahau sisi ni marafiki”Aliongea M,age na kumfanya Roma atabasamu.

“Haya ongea Mage”

“Kwanza nina shida na namba yako ya simu”Aliongea Mage pasipo kupepesa macho na kumfanya Roma ashangae , hakuwahi kuombwa namba ya simu na mwanamke kwa namna hio,Mage alimpa simu Roma aandike na Roma alitabasamu na kisha akachukua simu na kuandika.

“Kwahio shida ilikuwa namba yangu tu?”

“Hapana !, hilo ni la kwanza la pili nilikuwa nikitaka tuonane kesho jioni kama utakuwa na muda”Yaani Roma alimuona Mage kama mwanamke mbabe kwani licha ya kwamba alikuwa akiomba lakini sauti yake ilikuwa ni kama amri.

“Usifikirie sana Roma kuna jambo tu ambalo nataka kukushirikisha”

Roma hakuona haja ya kumkatalia Mage , kwanza alikuwa na shauku ya kutaka kujua kwanini Mage alikuwa akitaka kuonana nae , na kwa jinsi ambavyo Roma alimuona Mage , hakumuona kama mwanamke ambaye alikuwa akitaka kuongea nae habari za mapenzi hivyo alikubali moja kwa moja na kurudi ndani.

“Anko!”Ilikuwa ni sauti iliomfanya Roma ageuze shingo mara baada ya kutoka getini la hiki kituo na kumuona Yezi aliejibana kwenye kona ya ukuta.

“Hujaondoka tu , unasubiri nini , au ndio unaogopa giza?”

“Hapana nilikuwa nakusubiria”

“Mh!, haya twende nikusindikize urudi ulipoacha vitu vyako”

“Sidhani kama nitavikuta pale ,na kwa jinsi Sherifu na wenzake walivyovitupa tupa sidhani”

“Twende tukaangalie acha kudhanna”aliongea Roma na hata wazo la kuwahi nyumbani limepotea katika kichwa chake na sasa ilikuwa ni Zaidi ya saa tano.

“Ilikuwaje mpaka ukajiunga kwenye kundi la watoto watukutu kama wale tena ukiwa msichana?”Aliuliza Roma wakati wakitembea taratibu.

“Ni Stori ndefu sana Anko , walikuwa ndio marafiki zangu wa kwanza kukutana nao baada ya kutoroka kituo cha kulelea watoto yatima”Aliongea na kumshangaza Roma.

“Kwahio na wewe ni yatima?”

“Yeah! Nahisi hivyo , niliambiwa na walezi wangu niliokotwa kwenye geti la kituo”

“Ukiwa na miaka mingapi?”

“Nadhani mwaka mmoja , hawakuwa na uhakika pia ,hakukua na taarifa zozote kuhusu mimi au wazazi wangu Zaidi ya jina langu pekee”Roma alishangazwa na historia hio .

“Sasa kwanini ulitoroka?”

“Ni Stori ndefu , ila kikubwa sikupenda maisha ya kituoni, na baada ya kutoka ndio nikakutana na Sherifu ndio wakanishawishi kuingia kwenye kundi lao na kutokana na kwamba sikuwa na pesa hata ya kula nililazimika kufanya hivyo”Roma hakutaka kuuliza maswali mengi sana alimuonea tu huruma kwani maswala kama hayo yalikuwa ni kawaida pia hata kwa baadhi ya nchi ambazo zimeendelea.

Walivyofika eneo kwenye kile kibanda ni kama ilivyokuwa mategemeo ya Yezi , hakukuwa na chombo cha aina yoyote, kila kitu kilikuwa kishachukuliwa , jambo ambalo lilimfanya Yezi kutoa machozi , licha ya kwamba taa za hapa ni hafifu , lakini Roma alishuhudia machozi ya Yezi.

“Anko asante kwa wema wako leo wa kunitetea kule polisi , lakini pia kunisindikiza mpaka hapa , unaweza sasa kuondoka nisikucheleweshe”Aliongea Yez huku akimpa mgongo Roma.

“Sasa unaficha hayo machozi ya nini wakati nishakuona unalia?”

“Anko naomba uondoke” Roma aliangalia eneo hili kwa nmna ya kukagua

“Kwahio unalipa wema wangu kwa kunifukuza?”Yezi aligeuka.

“Kwahio unataka nikulipe nini, wakati unaona kila kitu nilichopigania kwa zaidi ya miezi minne kimepotea na sasa nakwenda kuanza upya naomba uondoke?”Aliongea kwa sauti ya kukasirika.

Roma alijipapasa mfukoni na kuibuka na noti za dola mbili , Dola mia mia , haikueleweka alikuwa ameziweka mfukoni muda gani.

“Kama unataka niondoke , nitaondoka ila chukua hii pesa itakusaidia”

Yezi aliangalia pesa iliokuwa kwenye mikono ya Roma kwa dakika kama moja, huku akionesha kufikiria na bila ya kuongea lolote alimpita Roma na kuelekea barabarani na jambo hili lilimshangaza Roma, ila alimfuata.

“Yaani nakusaidia unanikimbia au ndio unanidharau”

“Anko sikia mpaka hapa uliponisaidia panatosha , sitaki msaada wako Zaidi”

“Kama hutaki msaada wangu , unaonaje ukinipa kitu chochote cha Thamani ulichonacho na ukachukua hii pesa kama mkopo na siku ukifanikiwa unanirudishia pesa yangu,”aliongea Roma hivyo kwani alikuwa ashamfahamu Yezi ni msichana wa aina gani , aliona ni wale wasichana ambao walikuwa wakiogopa kufanyiwa wema ambao umezidi.

“Unahisi kwa umasikini huu nitakuwa na kitu gani cha Thamani?”

“Wewe ndio ufikirie kama una kitu cha thamani unipatie kama huna nitaondoka”

“Sina”

Alijibu Yezi kwa sauti na kufanya watu waliokuwa kwenye mgahawa mita kadhaa kutoka waliposimama , ndani ya eneo hili wawaangalie, na kwa haraka haraka walitafsiri Roma anabembeleza akalale na Yezi, na Roma aliona watu walivyokuwa wanawaangalia ila hakujali.

“Okey Yezi kwakua huna kitu cha Thamani naondoka”Aliongea Roma na kweli akaanza kuondoka huku akimuacha Yezi aliesimama.

“Anko!,Subiri”aliognea Yezi na kumkimbilia Roma huku akijishika shingoni.

“Nitakupa hii cheni yangu , ndio kitu pekee ambacho nimeokotwa nacho kama utambulisho , ila imepita miaka mingi nimewasubiri wazazi wangu na sidhani kama watakuwa hai, unaweza ukanitunzia, ndio kitu cha thamani nilicho nacho kwenye maisha yangu”Aliongea Yezi na kutoa cheni ambayo alikuwa ameiweka mfukoni kwenye suruali yake ya Jeans.

Roma macho yalimtoka mara baada ya kuangalia ,ilikuwa ni Necklace(Mkufu) ulioambatana na Pendant(kidani)

Baada ya Roma kuiangalia macho yalimtoka kutokana na aina ya pendant hio.

“Inakuwaje mtoto kama huyu akamiliki kitu kama hiki?”Aliwaza Roma huku akigeuza kidani hiko nyuma na mbele ni kama alikuwa akitafuta hitilafu , alitoa simu yake na kumulika

“Ni ya uhakika”Aliongea na kisha akainua macho yake na kumwangalia Yezi na wakakutanisha macho.
 
NITARUDI WIKIEND JUMATANO SAA 3 KAMILI USIKU

Back
Top Bottom