Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

SEHEMU YA 318

Roma aliweza kufika nyumbani kwa Afande Kweka na ilionekana walikuwa wakisubiriwa kwa hamu , kwani hapo ndani ilikuwa ni kama sherehe ambayo ilikuwa ikiendelea kwa jinsi mpangilio ulivyo.

Mzee Kweka mwenywe ndio aliweza kutoka mpaka nje kwa ajili ya kumpokea mjuukuu wake Denisi ambaye alimtoa kafara kwa ajili ya ugonjwa wake miaka mingi iliopita , sasa anarejea nyumbani kama mwana mpotevu.

Afande Kweka alikuwa akisubiria kwa hamu sana siku ambayo Roma atakanyaga mguu ndani ya familia yake.

Edna kwa mapokezi aliopokewa nayo , lakini pia namna ulinzi ulivyoimarishwa ndani ya hili eneo ndio aliweza kujua nguvu aliokuwa nayo Mzee Kweka.

Unachopaswa kujua familia ya Mzee Kweka ndio ambayo ina nguvu namba mja ndani ya taifa la Tanzania , na hio sio kwasababu Raisi Senga alikuwa raisi, Hapana, bali ni ushawishi mkubwa aliokuwa nao Afande kweka kwenye majeshi ya Tanzania.

Ma afande wengi waliokuwa ndani ya jeshi walikuwa wakimuheshimu sana Afande Kweka na mara nyingi kwenye mambo mengi walikuwa wakihitaji busara zake .

Hivyo hata kwa wanasiasa wanaotaka kuwa maraisi ,walikuwa wakihitaji sana sapoti kutoka kwa Afande Kweka , lakini hata hivyo sio familia ya Mzee Kweka pekee ambayo ilikuwa na nguvu Zaidi , familia ya Mheshimiwa Kigombola pia ni moja ya familia zenye nguvu kisiasa ndani ya taifa la Tanzania , Raisi Kigombola alikuwa na vijana wengi ambao amewaingiza ndani ya serikali wakiwa kama viongozi wakubwa kipindi alivyokuwa raisi na mpaka alipostaafu.

Unaweza kusema kwamba moja ya viongozi ambao walijijengea mazingira ya kuwa na nguvu ndani ya Tanzania basi ni Familia ya Kigombola ikiongozwa na mheshimiwa Kigombola mwenyewe, hio ndio famulia yenye nguvu kisiasa nchini , lakini familia pia nyingine ambayo ilikuwa na nguvu sana ndani ya Tanzania ni familia ya Mzee Atanasi anakozaliwa Blandina , Familia ya Mzee Atanasi ukubwa wake ni kwenye uchumi, familia hii ilikuwa imeteka kwa kiasi kikubwa uchumi wa Tanzania , kwani imewekeza kwa kila Nyanja ,huku ikiongozwa na Tajiri Mohamedi Azizi, hivyo unaweza kusema uchumi wa Tanzania kwa asilimia kubwa ulikuwa umeshikiliwa na familia hii ya Mzee Atanasi , Familia nyingine ya nne ambayo ilikuwa na ushawishi pande zote ni familia ya Nyerere , familia hii licha ya kwamba hawakuwa wakionekana sana hadharani , lakini ndio familia ambayo ilikuwa na ushawishi pande zote yaani kuanzia kwenye uchumi , siasa na jeshi na hii familia inafanana kwa kiasi kikubwa na familia ya Karume kutoka Visiwani , licha ya familia ya karume kuwa na nguvu sana Visiwani lakini pia ilikuwa na ushawishi mkubwa upande wa bara na inasemekana kati ya familia ya Nyerere na Karume ndio wanaoshikilia siri kubwa iliopo chini ya muungano, ssajambo moja ambalo unatakiwa kuelewa ni kwamba familia ya hii kutoka visiwani ndio inashikilia asilimia Zaidi ya therathini ya makampuni yote ya Maya hapa Tanzania.

“Edna karibuni sana nyumbani , Roma karibu sana nyumbani”Ilikuwa ni sauti ya ukarimu ya mwanamama Damasi mke wa Raisi Senga , ilishangaza sana kuwepo ndani ya familia hio kwa siku hio kuwapokea Roma na Edna .

Roma alikuwa akimfahamu mke wa raisi Senga , kwani walishakutana Zaidi ya mara mbili , mara ya kwanza alivyoenda ikulu na mara ya pili mwanamama huyo alivyompigia magoti kwa ajili ya kumsaidia Denisi.

“Asante sana mama, Lanlan msalimie Bibi”Aliongea Edna kwa Kingereza akimtaka Lanlan kumsalimia bibi yake.

“Goodmorning Grandma”Aliongea Lanlan.

“Wow! , jamani katoto kazuri kweli, hajui kuongea Kiswahili?””

“Ndio, Anajua kingereza pekee”

“Mr Roma karibu sana nyumbani baada ya miaka mingi”Aliongea Mzee Kweka baada ya kuwasogea na kukatisha maongezi kati ya Damasi na Edna.

“Mzee Kwani nilishawahi kufika hapa?”

“Unaweza ukawa hujawahi kufika hapa, lakini hapa ndio makao makuu ya ukoo wa Kweka na wewe ni mwanaukoo kabla ya kupotea , hivyo wewe sio mgeni bali ni mwenyeji unaerudi , karibu sana nyumbani”Aliongea Mzee Kweka. Kwa bashasha kubwa.

“Edna karibu sana nyumbani kwako , huyu bwana kakuoa lakini hajawahi kukuleta nyumbani , karibu sana kwa mara ya kwanza kwenye familia yetu”Aliongea na kumfanya Edna amwangalie Roma kwanza na Roma alimkonyeza.

“:Asante sana babu , nimekaribia”Aliongea Edna na mzee Kweka alitingisha kichwa huku macho yake akiyageuzia kwa Lanlan na kuanza kumtathimini kwa dakika kadhaa.

“Lanlan msalimie babu”Aliongea Edna na Lanlan alimsogelea Mzee Kweka na kushika mkono wake na kuuweka kichwani.

“Goodmorning Grandpa”Aliongea Lanlan na kumfanya Mzee KWeka kuachia tabasamu la kizee huku akimshika mkono Lanlan.

Muda huo wote walisogea mpaka eneo maalimu ambalo limeandaliwa nje ya jumba hili la Mzee Kweka kwa ajili ya kukaa.

Macho ya Roma hayakuwa yameridhika kabisa , kwani alikuwa akimtafuta Zenzhei na hiko ndio ambacho kilimleta hapo nyumbani , kama sio Zenzhei asingekanyaga mguu wake hapo ,kwanza hakuwa akipenda sana mambo ya ukoo kwani aliyatafsini kama mambo yaliopitwa na wakati na yeye hakuwa akihitaji ukoo kuwa na nguvu.

Mzee Kweka alionekana kuzoeana haraka na Lanlan na kumfanya hata Edna kushangazwa na Lanlan kuweza kuzoea watu wapya haraka, tofauti na Watoto wengine.

“Hahahaha….Kwahio Lanlan anapenda kula , kuangalia Wanyama na kufanya nini?”

“Na kuendesha Farasi na Tembo”Aliongea Lanlan na kumfanya Mzee Kweka kucheka Zaidi na kushangazwa na Lanlan.

“Lanlan ushawahi kuendesha tembo?”Aliuliza Roma.

“Mama yake Lanlan amenifundisha kuendesha Tembo na farasi , Lanlan anapenda Wanyama, Grandpa nataka kuona Wanyama”

“Grandpa atampeleka Lanlan kuona Wanyama”

“Grandpa promise me!”

“Grandpa anaahidi atampeleka Lanlan kuona Wanyama”Aliongea Mzee Kwek ana kumfanya Lanla kuripukwa na furaha , huku watu wote wakishindwa kuongea wakiwaangalia Lanlan na mzee Kweka, ndio waliteka mazungumzo na hata ule ukaribisho ulizidiwa na maongezi ya Lanlan, uzuri pia ni kwambwa wanafamilia karibia wote walikuwa wakielewa lugha ya kingereza.

Zilipita dakika kadhaa tu , alionekana na Denisi akiingia ndani ya jumba hili la Mzee Kweka akiwa anatumia gari yake aina ya Audi, alipokelewa vyema na wafanyakazi na kuelekezwa upande wa nyuma sehemu ambayo watu wote wameketi.

“Grandpa nimeitikia wito”Aliongea Denisi mara baada ya kukaribia eneo hilo ambalo limetegenezwa kwa hema.

Roma alimwangalia Dnisi na kujikuta akikunja sura na Denisi alimwangalia Roma na kisha kukunja sura kidogo kabla yakuachia tabasamu.

“Karibu sana Denisi nyumbani”

“Asante sana babu , jambo uliloniitia ni muhimu , nimeona nitakuwa sio muungwana kama nitakosa siku hii ya kumkaribisha kaka yangu na mke wake nyumbani, Roma karibu sana kwenye ukoo wetu”Aliongea Denisi na alisogea upande wa Roma na kumnyooshea mkono kama ishara ya salamu.

“Sipendi kukaribishwa kinafiki , unaweza tafuta sehemu ukakaa ila iwe mbali na mimi”Aliongea Roma pasipo ya kupokea mkono wa Denisi na jambo lile kidogo lilifanya hali ya hewa kuwa ngumu kidogo.

“Shemeji Edna karibu sana kwenye familia yetu ya Kweka , chaguo lako la kuolewa na Bro wangu hapa halikuwa baya, inaonesha unaona sana mbali”Aliongea Denisi na maneno yake licha ya kwamba yalinyooka , lakini yalikuwa na chembe za unafiki ndani yake.

“Denisi tafuta sehemu ya kukaa ukae, tuna mambo mengi ya kuongea leo kama wanafamilia ndio maana nimewaita wote muwe hapa”

“Lakini babu vipi kuhusu baba , yeye hayupo , familia bado haijakamilika”

“Denisi acha kuongea upuuzi , unafikiri ukoo wa Kweka umejengwa na mimi tu Pamoja na baba yako ,wapo wanaukoo wengine ambao hawajafika na siku ikiwadia wote nitawaita kwa ajili ya kumtambulisha Roma ”Aliongea Afande Kweka.

“Naamini hio siku ndio ya kumtambulisha Roma kama kiongozi wa ukoo akirithi nafasi yako?”Aliongea Denisi na kufanya watu wote hapo kushangaa.

“Denisi nifuate”Aliongea Damasi akimwashiria mwanae amfaute ndani na Denisi hakutaka kubisha alifuata nyuma akimuacha Mzee Kweka akiwa kwenye ‘jazba licha ya maneno alioongea Denisi kuwa ya kweli.

“Denisi ndio alivyo , amejaa tabia za kisiasa siasa na na maneno mengi ya mzunguko , msijali sana .. Ooh yeah nilisikia ulimwadabisha inaonekana hajatia adabu”Aliongea Afande Kweka kupoza hali.

“Afande mimi nimekuja kwa ajili ya Zenzhei lakini simuoni hapa”Aliongea Roma akiulizia uwepo wa Zenzhei.

“Zenzhei kaenda kukutana na kaka yake na kaahidii atawahi kurudi na mtaonana”Aliongea Afande Kweka na kumfanya Roma kushangaa Zenzhei kuwa na kaka.

“Usishangae kuna mambo mengi ambayo unapaswa kuyasikia kutoka kwa Zenzhei”

Upande mwingine asubuhi hio , upande wa Bagamyo baharini , wanaonekana watu wawili ambao kwa kuwaangalia hawakuwa wazawa kutokana na Ngozi zao , watu hawa hawakuwa wengine bali ,mmoja alikuwa ni Zenzhei na mwingine alikuwani Gumila.

Walikuwa wameketi kwenye mchanga huku macho yao yote wakiyaelekezea upande wa baharani , sehemu ambayo mitumbwi mingi ya kufanyia uvuvi ikiwa inaelea , Pamoja na wavuvi waliokuwa wakilanda landa kupokea wenzao ambao ndio kwanza wanrudi kutoka kwenye shughuli za uvuvi asubuhi hio.

“Zenzhei , ulifikaje Tanzania?”Aliuliza Gumila na kumfanya Zenzhei aliekuwa akiangalia baharini kuvuta pumzi.

“Ujio wangu hapa Tanzania zilikua ni harakati za kukutafuta”Aliongea na kumfanya Gumila kushangaa kidogo.

“Ulifahamu vipi nitakuwa ukanda wa Afrika mashariki, usiniambie ulinipeleleza ndani ya kundi la Yamaguchi?”Aliongea Gumila japani huyu , huku leo hii akiwa tofauti na mara ya mwisho tulivyomuona.

“Ni Stori ndefu sana ambayo napaswa kukueleza tokea mara ya mwisho wewe kuondoka lakini pia hata familia yangu kuwa ‘Demoted’”

“Unamaanisha nini kuwa Demoted?”
 
SEHEMU YA 320

“Unapaswa kutoa sadaka ya kitu unachopenda sana kwenye Maisha yako?”Aliongea Balozi na kumfanya Raisi Kamau kushangaa.

“Kitu ninachokipenda?”

“Ndio mheshimiwa Kamau Kamau”Alijibu balozi aliemtembelea raisi Kamau na kumfanya ndugu balozi kutabasamu huku Mheshimiwa kamau akijiuliza ni kitu gani anakipenda sana kwenye Maisha yake , lakini wakati huo huo upande wa Tanzania na Raisi Senga kufikiria ni kitu gani anakipenda Zaidi.

“Tunamuhitaji mkeo kama sehemu ya sadaka”Aliongea ndugu balozi upande wa Kenya.

“Tunamuhitaji mkeo Blandina kama sehemu ya sadaka”Aliongea ndugu balozi upande wa Tanzania, Raisi Senga na Raisi Kamau wote kwa wakati mmoja wakapigwa na butwaa.

“Hapana Blandina sio mke wangu”Alijibu Raisi Senga akimaanisha kwamba Blandina alietajwa sio mke wake, na ndugu balozi akatabasamu.

“Hapana Blandina sio mke wangu tena na ashakufa”Alijibu Raisi Kamau na kumfanya ndugu Balozi kutabasamu.

“Kwa macho ya kawaida ni kweli kabisa Blandina sio mke wako , lakini katika ulimwengu wa Roho ndoa yenu wewe na Blandina ilishakwisha kfungwa na ni yenye kukubalika”Aliongea ndugu balozi akimueleza Raisi Senga.

“Blandina ndio mkeo na mimi na wewe tunajua hajakufa kama wengi wa taifa hili wanavyojua”Aliongea ndugu balozi upande wa Kenya.

“Vipi kuhusu mke wangu Damasi , ndio mke wangu wa halali”

“Mheshimiwa nasikikita kukuambia kwamba Damasi ni mwanamke unaeishi nae na sio mke wako , angalau kwa macho ya kibinadamu ni mke wako , lakini katika ulimwengu wa roho mkeo bado ni Blandina na ndoa yako na yeye haikuwahi kubatilishwa , jambo la kufurahisha Zaidi mheshimiwa unampenda sana Blandina , ni ukweli ambao hutaki tu kuukubali”Aliongea Balozi upande wa Tanzania na kumfanya Raisi Senga kushindwa kuongea neno tena.

“Mheshimiwa haya ndio maandalizi unayotakiwa kufanya kwa ajili ya sadaka kabla ya siku ya ibada, nikutakie utekelezajia mwema”Aliongea ndugu balozi na kisha akanyanyuka , huku akiacha karatasi mezani kwa mheshimiwa Senga.

Sasa upande wa Kenya ilikuwa hivyo hivyo, kila mmoja alipokea nyaraka iliokuwa ikielezea maandalizi ya Sadaka takatifu au kafara.

Sasa katika maelezo ambayo aliachiwa raisi Kamau ni kwamba sheria namba moja alitakiwa kumrudisha Blandina nchini Kenya na kuwa mke wake tena kihalali kabisa , lakini wakati huo huo akimaliza tofauti zake na Raisi Senga kutokaTanzania , huku karatasi ikielezea namna sahihi ya kumrudisha Blandina ,yaani kwa maneno marahisi ni kwamba kila kitu kilikuwa kimeandaliwa na ilikuwa ni kwa Kamau tu kutekeleza , upande pia wa Tanzania Raisi Senga alipata kusoma karatasi iliochwa na yenyewe ilikuwa na maelezo ambayo yanamtaka kwanza kabisa kuhakikisha kunakuwa na amaini kati yake na Kamau , lakini pia wakati huo huo akimsaidia Raisi mwenzake kuhakikisha Blandina anarudi Kenya , huku maelezo namna ya kufanya zoezi hilo yakiwa yanaendelea.

Sasa kwa jinsi kila kitu kilivvyoandikwa ndani ya karatasi hio , ilionyesha kabisa jamii hio ya siri ilikuwa ikimfahamu vyema Blandina kwa kila alichokuwa akikifanya na walikuwa wakimfuatilia kwa ukaribu sana.

Sasa maelezo hayo yote yanaonyesha kwamba Blandina ameweza kufunga ndoa na wanaume wawili kwa wakati mmoja ndani ya ulimwengu wa Kiroho na ndoa yake na wanaume hao kuwa katika kumbukumbu na kukubaliwa moja kwa moja ,sasa swala hili halikueleweka linawezekana vipi, lakini utaelewa hivi punde.

Ni kweli kabisa baada ya Raisi Senga kujiuliza kwenye moyo wake aligundua kabisa alikuwa akimpenda sana Blandina bado na jambo hili liliibuka upya mara baada ya kuambiwa amtoe kafara , moyo wake ni kama umetibuliwa upya.

Upande wa Raisi kamau alikuwa hivyo hivyo , alikuwa akiumia sana mara baada ya kupewa sharti la kumtoa Blandina mwanamke wake kipenzi sadaka.

Sasa jambo ambalo unatakiwa ulifahamu ni kwamba raisi Kamau licha ya kwamba alikuwa amemuoa Blandina kimagumashi , lakini kuna historia kubwa ilikuwa chini yao , upande huo huo Blandina akiwa na historia kubwa sana ilionyuma yake na Senga, halafu jambo la kufutahisha Zaidi kuna historia kubwa iliokuwepo kati ya Raisi Kamau na Raisi Senga.

Sasa hawa mabwana wote wawili ni marafiki na wakatokea kumpenda sana mwanamke mmoja kiasi kwamba kila mtu kwa wakti wake akafunga na mwanamke huyo ndoa ,na ndoa hio ikakubalika katika ulimwengu wa kiroho , yaani kwa maneno marahisi katika mafaili ya ndoa huko kwenye ulimwengu wa kiroho Blandina anatambulika kama mke halali wa Raisi Senga , lakini wakati huo akitambulika kama mke halali wa Raisi Kamau. Huku Damasi na Raisi Senga wakionekana mwanaume na mwanamke wanaoishi pamoj , yaani walionekana walikuwa wakizini tu sio kufanya tendo la ndoa.

Sasa mabwana hawa kutokana na mapenzi yao kwa mwanamke mmoja na mwanamke huyo kuwa sehemu ya kitu wanachopenda sana ndani ya dunia hii wanajikuta wakiwa kwenye mtego wa kutakiwa kumtoa mwanamke huyo kafara.

Sasa unachotakiwa kuelewa hapa ni kwamba Imani za hawa watu wote wawili zilikuwa zipo kwenye majaribio na muda ambao watakubali ni ishara kwamba wapo tayari kuwa wanachama wa Freemason watiifu.

Sasa kwa kile ambacho kimetokea ndani ya kituo cha Son and daughter Ophanage, itoshe kusema kwamba wote kwa Pamoja wameamua kukubaliana na matakwa ya kumtoa Blandina kafara, na hatua ya kwanza ilikuwa ni hatua ya kumrudisha Blandina nchini Kenya, yaani blandina anatakiwa atolewa kafara akiwa tena mke wa raisi Kamau Kamau , huku raisi Senga akitoa baraka zake zote za kumwachia Raisi Kamau Blandina wake.

********

“Blandina utafanya nini juu ya hili, upo kwenye wakati mgumu kweli rafiki yangu , kwanini haya yote yanakupata wewe tu?”Aliongea Mama Issa kwa huzuni na muda huu ni mara baada ya raisi Senga na Kamau kuondoka na kuwaacha Blandina na Mama Issa.

Sasa Blandina aliweza kumueleza Mama Issa kile ambacho kinatokea, kwa maelezo ya Blandina ni kwamba karatasi ambayo amepewa na maraisi hao ilikuwa ikionyesha kwamba vituo vyake vyoote alivyovijenga kwa jasho na damu kwa ajili ya Watoto yatima vitabomolewa , sasa ile karatasi ilikuwa na sahihi za maraisi katika kila nchi ambazo vituo hivi vipo , yaani kulikuwepo na sahihi ya raisi wa Congo tayari, kulikuwa na sahihi ya Raisi wa Sudani tayari.

Lakini haikuwa hivyo tu , kulikuwa na sahihi kutoka umoja wa mataifa inayosimamaia maswala ya Watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu , yote hii ilikuwa ni kumfanya Blandina kukubali kurudi Kenya ili kuwa mke wa Raisi kamau na kama atakataa basi vituo hivyo vitabomolewa.

Kwa maneno marahisi ni kwamba nguvu ambayo inamtaka Blandina kurudi Kenya kuwa mke wa Raisi Kamau kwa mara nyingine ilikuwa ni kubwa mno kiasi kwamba hana nguvu ya kulinda vituo hivyo hata kama ataenda kushitaki , kwanza atashitaki wapi kwani watu wanaolinda hizo sheria ndio waliaoamua kuzivunja.

Blandina anazo siku tano tu kuamua cha kufanya , aidha akubaliane na masharti na arudi Kenya au akubali kuishi Tanzania na vituo vyote mpaka cha Son and daughter orphanage kubobolewa.

Blandina aliangalia Watoto waliokuwa wakicheza na Yezi na alijikuta akizidi kuwa kwenye wakati mgumu Zaidi , Watoto waliokuwa mbele yake walionekana kuwa na furaha na walichukulia eneo hilo kama nyumbani kwao , sasa ataanzaje kubomoa kwa ajili ya kitu kidogo kama ndoa.

Asichokijua Blandina ni kwamba alikuwa akiandaliwa kama sadaka kwa ajili ya Imani ya wanaume ambao walitokea kumpenda sana kwenye Maisha yake , Raisi Senga na Kamau.

“Sijui cha kufanya Mama Issa , nitatumia siku mbili hizi kufikiria na niamini mimi nitafanya maamuzi sahihi, Tabea kwa vyovyote vile siwezi kuruhusu Watoto hawa kuteseka tena kwa sababu yangu , Imani yangu ipo kwa hawa Watoto kuliko kitu kingine chochote ndani ya dunia hii na ndio sadaka pekee ambayo naweza kutoa kwa Mungu”Aliongea Blandina na kumfanya Mama Issa Chozi la kiutu uzima kumtoka.

********

Ikawa jioni ikawa asubuhi, hatimae ikawa jioni tena siku ya Jumatatu.

“Mama unaonekana kutokuwa sawa kwa siku hizi mbili”Aliongea Roma marabaada ya kumkuta mama yake akiwa ameketi eneo la nje akiwa amekodolea macho maji ya bwawa la kuogelea.

Ukweli ni kwamba Edna ndio aliekuwa wa kwanza kuona mama mke wake alikuwa kwenye mawazo na ugunduzi huo ndio ulimpelekea Edna kumfauta Roma chumbani kwake kwa ajili ya Kwenda kuongea na mama yake.

“Kumbe hata wewe mke wangu umelishudia hilo , wife unaonekana kumjali sana mama mkwe wako”Aliongea Roma akimwangalia Edna aliesimama mbele yake Roma muda huo mwenyewe alikuwa amevalia bukta tu na kumfanya nyoka yake kuonekana Zaidi kwenye macho ya Edna.

“Acha utani ,vaa ukaongee nae, yupo kule nje bustanini kakaaa ,wewe ni mtu gani hata haujali hali aliokuwa nayo mama yako”Aliongea Edna na Roma alisimama na kumsogelea Edna , sasa kitendo cha kusimama ndio kilizidisha dudu ya Roma kujionyesha wazi , ukijumlisha pia na ukubwa wake ilifanya kudhihirika.

Sasa macho ya Edna yalipotua kwenye Jongoo la Roma , mwili wake ulishikwa na ubaridi mkali mno na kabla hata ya Roma hajamfikia alitoka nduki na kumuacha Roma kutabasamu kifedhuli , alijua ni sababu gani ilimfanya Edna kumkimbia.

Kwa hio Roma aliweza kumsogelea mama yake kumuuliza nini kinamsibu kwani alikuwa kwenye mawazo.

Blandina baada ya kumuona Roma kaketi upande wa kulia kwake , alijikuta akitabasamu na kumwangalia Roma usoni na palepale machozi yalionekana yakitawala mboni za macho yake.

“Roma mwanangu asante sana”Aliongea Blandina na kumfanya Roma kushangaa , kwanini mama yake analia halafu wakati huo huo anamwambia asante , jambo hili la kuona machozi ya mama yake hakuwa ni mwenye kulipenda.

ITAENDELEA

NJOO WATSAPP UTUMIWE VIPANDE VYA MBELE NA KUUNGANISHWA NA GRUPU 0687151346
 
Unaweza pata PDF ya hii simulizi kutoka episode ya 1 mpaka 300 kwa wale mnao anza kusoma na mnaona ugumu kupitia kila post nitafute watsap 0687151346
 
SEASON 2
SEHEMU YA 31

Ilikuwa ni Jumapili tulivu , kwa wale wakristo waliokuwa wakienda kanisani walikuwa wakienda na kwa wale ambao walikuwa ni wa dini nyingine walikuwa na pilipilika za mambo mengine za Maisha yao.

Roma kama kawaida yake aliamka asubuhi asubuhi na kwenda kufanya mazoezi ya hapa na pale ili kuweka mwili wake katika hali nzuri , kwa upande wa Bi wema alikuwa bize na kuandaa kifungua kinywa kwa siku hio na kwa upande wa Edna alikuwa bize na kusoma kama ilivyokuwa kawaida yake , aliamini matatizo yake yote yanaweza kutatuliwa na kusoma na ndio maana aliamini katika kusoma sana.

Alijitahidi kusoma kwa muda , lakini akili yake haikuwa ni yenye kutulia , alionekana kuna jambo lilikuwa likimuumiza kichwa kwani alikosa utulivu , baada ya kuona haelewi kile alichokuwa anakisoma alisogelea tarakishi yake ya mapakato na kuingia kwenye mtandao maarifu wa Google na kuanza kutafuta taarifa zinazohusiana na macho ya mtu kubadilika Rangi , lakini kila majibu yaliokuwa yamekuja yalionekana kutokumridhisha kabisa na kukosa jibu alilokuwa analitaka.

“Au nimuulize mimi mwenywe kwanini macho yake yanabadilika Rangi?” Aliwaza mrembo huyu huku akiwa amevalia kigauni chake kilichoufanya mwili wake mnene kiasi kupendeza.

“Ila naamini siku moja ataniambia mwenyewe kwanini yuko vile , sitakiwi kumuuliza”Alijijibu mwanamke huyu huku akiona hayupo kwenye nafasi ya kumuuliza mume wake Roma kwanini macho yake yanabadilika rangi anapokuwa na hasira kali.

Saa mbili kamili za asubuhi Edna alishuka chini kwa ajili ya kupata kifungua kinywa baada ya kuitwa na Bi Wema , Roma alikuwa tayari yupo mezani , na alikuwa anamsubiria mke wake waanze , baada ya Edna kuketi wanafamilia hawa watatu ndani ya jumba hili kubwa la kifahari walianza kupata kifungua kinywa chao ambacho kwa familia za Maisha ya chini wangedhania moja kwa moja aina hio ya chukula ni kwa ajili ya sherehe.

“Miss unaonaje ukienda na Mr Roma leo kituoni?”Aliongea Bi Wema na kupendekeza .

“Bi Wema kituo gani?”Aliuliza Roma

“Kuna kituo cha kulelea yatima kipo Mkoa wa pwani Bagamoyo Kiwangwa, Ni kituo ambacho kampuni inakifadhili na imekuwa utamaduni kila jumapili Miss Edna kwenda huko kuwatembelea Watoto hao na kuwapelekea baadhi ya mahitaji muhimu”Roma alishangaa.

Edna alimwangalia Roma , hakuwa akipinga swala hilo la kwenda nae , kwanza kabisa mrembo huyu alipanga kujiweka kidogo karibu na Roma ili kuweza kujua ni kwanini macho yake yanabadilika Rangi , aliamini kama watakuwa marafiki Roma anaweza kumfungukia.

“Bi Wema kama mke wangu anapenda kuongozana na mimi nipo tayari , isitoshe leo sina pakwenda na sijazoea kukaa ndani”Aliongea Roma.

“Roma itakuwa vizuri kama tutaenda wote , unisaidie kwenye kubeba mizigo ya kwenda nayo”Aliongea Edna na Roma aliitikia kwa kichwa.

Baada ya nusu saa Roma alikuwa ashajiandaa kwa ajili ya kuianza safari ya kuelekea Bagamoyo , alikuwa sebuleni akimsubiria Edna ambaye kama ilivyokuwa tabia ya wanawake kujiandaa muda mrefu Edna alichukua lisaa mpaka kuonekana akiwa anashuka.

Roma siku zote alikuwa akijivunia hata kuitwa mume wa Edna , kwani mwanamke huyu hata avae nini , alikuwa akipendeza sana na kuvutia,Edna alikuwa amevaa leo Suruali ya jeans rangi ya Bluu iliomfanya umbo lake kuonekana vyema, na kishati flani kitambaa mtelezo mikono mirefu , na akakikunJa hadi kwenye kiwiko cha mikono , chini akiwa amevalia viatu vyeupe kama Raba Rangi ya pink.

Edna alimpa Roma ufunguo na Roma alitangulia mpaka sehemu ya kuegeshea magari na kubonyeza Rimoti na Pickup aina ya Cadillac Escalade EX ili Tweak na kuwasha taa ,Roma alitabasamu na ufahari wa hii gari , aliitoa na kuleta mpaka katikati na Edna aliingia.

Bi Wema aliekuwa juu ya Gorofa alikuwa akitabasamu kwa furaha baada ya kuona Edna na Roma wakitoka , alijiambia ni mwenye akili sana kushauri waende pamoja.

“Kuanzia sasa misheni yangu ni kuhakikisha wanafanya mambo kwa pamoja , hii itawaongezea kuwa karibu” Aliwaza Bi Wema huku akijiona jasusi mbobezi likija swala la mapenzi.

Safari ya wanandoa hawa iliishia Mliman City , Watu waliokuwa ndani ya eneo hili waliwaangalia kwa macho ya tofauti kabisa huku kila mtu akiwa na mawazo yake ,Edna alikuwa amevalia miwani ambayo ilimfanya apendeze lakini yeye hakuvaa kwa ajili ya kupendeza , alikuwa amevaa kwa ajili ya kufanya watu wasimtambue.

Roma alievalia jeans lake Rangi nyeusi na koti la Ugolo alijongea upande upande na mke wake , huku akijisikia fahari namna ambavyo wanaume wa eneo hili walivyokuwa wanamwangalia kwa macho ya wivu.

Walinunua mahitaji mengi ndani maduka ya vyakula , baadhi ya nguo , taulo za kike na makolo koloo mengi sana ambayo yalikwa ni sehemu ya mahitaji ya Watoto , walichukua na baadhi ya zawadi kwa Watoto hao ikiwemo biskuti pipi na vitu vingine.

Baada ya kumaliza kufanya manunuzi , Roma kusaidiana na baadhi wafanya kazi walipakia huku Edna akiwa bize kulipia.

Wakati Roma akiwa bize kupandisha vitu , mara alisikia sauti iliokuwa ikimuita nyuma yake , sauti ya kike ambayo alikuwa akifahamu vyema, alikuwa ni mrembo Doris ambaye alikuwa akiegesha gari yake , akiwa yupo peke yake aliependeza kama kawaida.

“Doris !”Aliongea Roma kwa kushangaa baada ya kumuona mrembo huyu mbele yake.. wakati Doris anamwangalia Roma kwa mshangao mara alikuja Edna na kwenda kusimama karibu na Roma.

“Edna!”Macho yalimtoka Doris , hakuelewa ni kwanini wawili hao wako pamoja .

“Vipi Doris umekuja kufanya Shopping?”Aliuliza Edna wa kwanza baada ya kuona Dorisi yupo kwenye mshangao pasipo kuongea neno.

“Ndio Edna , lakini kwanini upo na Roma?”

“Nisamehe Dorisi rafiki yangu , nadhani unakumbuka nilikuambia nina mume?”

“Usiniambie Edna huyu ndio mumeo na siku zote huniambii?”.

“Ndio Dorisi huyu ni mke wangu,Tunaelekea Bagamoyo na muda unaenda tutaongea Zaidi”Aliongea Roma akikata mazungumzo hayo , hakutaka waendeleee kusimama ndani ya eneo hilo la maegeisho ya magari

“Nitakupigia simu Doris , tutaongea”Aliongea Edna na Roma alimshika bega Edna na kumsukumizia ndani na kufunga mlango na kisha akazunguka upande wa dereva na kuingia ndani na kuliwasha huku wakimwangalia Doris aliekuwa amesimama akiangalia gari yao ikitokomea.

“F**ck you Roma , siku zote unanichora tu kumbe mkeo ni Edna , halafu kwanini Edna hajaniambia”Alijiongelesha mwenyewe na kusahau kuwa baadhi ya watu walikuwa wakimshangaa , alifuta machozi kwa mkono ambayo yalikuwa yashaanza kujitengeneza ndani ya mboni za macho yake na kufungua mlango wa gari na kuingia na kisha akatoa gari ndani ya eneo hilo , alionekana kughairi , alichokuwa amefata hapo.

“Doris atakuwa amekasirika”Alianzisha maongezi Edna wakati wakipita Lugalo.

“Kwanini unasema hivyo?”

“Doris ni Rafiki yangu wa muda mrefu na niseme ni Zaidi ya Rafiki yangu , tumekuwa pamoja kwa muda mrefu kidogo , nilimwambia nimeolewa na kumuhaidi nitakutambulisha kwake lakini sikufanya hivyo na leo ametuona pamoja , kama marafiki atakasirika na kujisikia vibaya”.

“Mke wangu usiwe ni mwenye wasiwasi , Doris ni Rafiki yako na wewe ulikuwa pia na sababu za kutonitambulisha kwake mapema , hivyo atakuelewa , isitoshe hatuna muda mrefu tokea tumesajili ndoa yetu”.Edna aliitikia kwa kichwa.

“Kila jumapili unakujaga huku kutembelea kituo?”Aliuliza Roma kwa makusudi a ya kubadilisha stori.

“Ndio , imekuwa utamaduni , kila jumapili lazima nitembelee , napenda Watoto na najisikia faraja ninapokuwa nao karibu”.

“Mke wangu nilijua wewe ni kauzu kila sekta , kumbe una upande wako mwingine ambao sikuwa nikiufahamu”.

“Mimi sio kauzu ila napenda kuwa siriasi kwenye maeneo yanayonitaka kuwa hivyo , sipo kama wewe kila eneo haupo siriasi”.

“Kwa hio mke wangu wewe unataka niwe vipi?”Edna hakujibu aliendelea kukaza macho barabarani na Roma hakutaka kuongea Zaidi.

Ni masaa machache tu walikuwa washafika ndani ya kituo hiki , kilikuwa ni kituo kikubwa sana, kilikuwa na majengo makubwa kama chuo , jambo ambalo lilimshangaza Roma.

“Mke wangu hiki kituo ni kikubwa ni shirika gani limejenga hiki kituo?”

“Sio shirika ni mke wa raisi wa Kenya ndio amejenga hapa Tanzania”Roma alishangaa ,yaani mke wa raisi atoke Kenya kwao ambako kuna Watoto wengi waliozagaa mtaani aje ajenge Tanzania , alishangazwa na jambo hilo.

“Kwanini ajenge Tanzania sio Kwao Kenya?”

“Hata Kenya kajenga vituo vingi tu na sio Kenya wala Tanzania ,Uganda , Rwanda na Kongo kajenga vituo vinavyofanana hivi hivi, ni mwanamke ambaye ana moyo mzuri sana na anasifika sana ndani ya Afrika kwa kuisadia jamii.

Roma alitingisha kichwa baada ya kupewa jibu hilo na mke wake , aliona huyo mwanamama anapaswa kupewa tuzo kwa msaada mkubwa ambao anaufanya kwa jamii zenye uhitaji.

Kitendo cha kumaliza kuegesha Gari Tu ni kama Watoto waliokuwa ndani ya hili eneo walikuwa wakimsubiria Edna kwani kundi lote lilimkimbilia na kumzingira huku wakionyesha furaha yake na Edna na yeye hakuwa nyuma , alionekana kufurahi kweli uwepo wa Watoto na kwa mara ya kwanza Roma anamshuhudia Edna akiwa na furaha sana.

“Sikujua mke wangu kumbe mzuri hivi akicheka , halafu anaonekana kuwa na moyo mzuri sana , kanaigiza tu kuwa siriasi”Aliwaza Roma huku Watoto hao wakiwa hawana habari nae.

“Edna karibu” Aliongea mwanamama mmoja hivi mnene mwili wa kibonge mwenye umri si chini ya hamsini hivi alikuwa wa maji ya kunde.

“Asante Mama Issa ”Alijibu Edna aliekuwa akiwaangalia Watoto hawa , lakini kwa upande wa yule mama alimwangalia Roma na hapa ndipo Edna aliekuwa amemshau Roma akainuka.

“Mama Issa Watoto wamenifanya nisahau kukutambulisha , huyu ni mume wangu anaitwa Roma Ramoni” Mama huyu macho yalimtoka kwa mshangao huku Roma akiwa ni mwenye kutabasamu , alijiuliza huyu mwanaume ana nini mpaka kupata nafasi katika maisha ya Edna.

“Sikujua.. kumbe umepata mume Edna .. jamanii.. karibu baba mimi naitwa Tabea Singano ni mkuu wa hiki kituo”Aliongea mama huyu huku akionyesha furaha yake waziwazi , alionekana pia ni mtu ambaye alitamani siku moja Edna kumtambulisha mume wake kwake.

“Nashukuru sana kukufahamu Mama”.

“Karibu sana , unabahati sana kumpata Edna katika Maisha yako , umchunge sana”Aliongea mwanamama huyu huku Edna hata hakuwa akiwasikia , kwani alikuwa bize na Watoto aliokuwa akiwabeba mmoja mmoja juu.

Walishusha mizigo kwa kusaidiana na wafanya kazi wa hapa ndani , na Roma pia alisaidia katika kazi hio na baada ya zoezi hilo dogo kuisha Edna na Roma walichukua zawaidi walizokuwa wamekuja nazo na kuanza kuzigawa kwa Watoto hao .

Roma alimkubali sana aliejenga hiki kituo kutokana na wingi wa Watoto hao , kilikuwa mpaka na shule kubwa ya msingi mpaka sekondari , ni kituo ambacho kilionesha kujitosheleza sana kwa kila kitu.

Mama Issa alimchukua Roma na kuanza kumtembeza ndani ya kituo hichi , kwa kumuonesha baadhi ya huduma ambazo wanatoa kwa Watoto hawa ya kimalezi , mama huyu alionekana kuwa mkarimu sana.

“Edna ni msichana wa kipekee sana ,nimemuona akikua kwanzia alivyokuwa mdogo”Roma alishanga

“Mlikuwa maishi majirani?”.aliuliza Roma na mwanamama huyu alitabasamu.

“Hapana , wakati wa utoto wake alikuwa akija na bibi yake hapa mara kwa mara kucheza na Watoto na naweza kusema Muda wake wa utoto mwingi alicheza na Watoto ambao walikuwa kwenye hiki kituo”Aliongea mama huyu na kumfanya Roma ashangae , na wakati huu walikuwa wakiingia ndani ya mejengo ya ofisi hizi za kituo hiki kilichokuwa kinafahamika kwa jina la Son and Daughter Orphanage(SDO)..

Roma baada ya kuingia ndani ya hii ofisi kubwa ya mama Issa alijikuta akishangaa picha iliokuwa juu ya ukuta ,ilikuwa ni picha ya mwanamama mmoja maji ya kunde aliekuwa kwenye pozi la kutabasamu, kichwa chake kilianza kuuma na kupiga kama Radi na picha picha za matukio zikianza kupita .. macho yake yalianza kubadilika palepale na kuwa ya kijani.

SEHEMU YA 32

Roma alishindwa kuvumilia , alikuwa akishindana na hali iliokuwa ikiendelea kwenye mwili wake , alifumba macho yake haraka sana , ili Mama Issa asimuone akibadilika na kisha akageuka, Uzuri ni kwamba mwanamama huyu alikuwa amempa mgongo Roma na hakuwa akijua kilichokuwa kikiendelea kwenye kichwa chake.

Roma alikimbilia nje , lakini ile anatoka kwenye ofisi alijikuta akikumbana na Edna ambaye aliona hali yake ya macho Alitaka kumwepa lakini Edna hakufanya hivyo , alimshika mkono.

“Roma Calm Down”Aliongea Edna na Roma ni kama ameshituka kwani macho yake yaligeuka na kurudi katika hali yake ya kawaida na kumwangalia Edna.

“Am Sorry Edna”.

“Sorry ya nini?”

“Sijui …”Kabla Roma hajaibu walishitushwa na sauti ya Bi Tabea.

“Nilishangaa umeenda wapi kumbe umemfata mkeo”Aliongea Bi Tabea na Edna alitabasamu.

“Edna niseme tu hongera sana kwa kupata mume , Roma anaonekana kuwa kijana mzuri naamini mama yako na bibi yako watakuwa na furaha na wanaweza kupumzika kwa amani maana wewe..”

“Mama Issa Maana nini…”aliongea huku akicheka.

“Umekuwa mgumu sana , nakumbuka yule nani yule .. ee Elvice alikuwa akitoka jeshini lazima aje hapa kulalamika..”Mama huyu alijikuta akiishia njiani kuongea na kujiona ameropoka ila kwa Roma alikuwa amesikia kila kitu na akajiuliza kuna historia gani kati ya Elvice na Edna ambayo hakuwa akiijua , ila hakutaka kuuliza.

Saa moja kamili za jioni ndio muda ambao wawili hawa walitoka ndani ya kituo hiki kurudi nyumbani , Edna alionekana kuchoka kweli kutokana na kucheza na Watoto , kwa upande wa Roma yeye hakuwa amechoka , kwanza hakucheza kabisa na Watoto kwani sio mtu wakupenda sana kama ilivyokuwa kwa Edna.

Alimwangalia mke wake aliekuwa amesinzia pembeni na kujikuta moyo wake ukiwa wa moto , alitamani Maisha yake yawe kama hivyo kila siku ,awe anapendana na mke wake , watembee hapa na pale kurefresh mind, alitamani kufurahi na kuendeleza Maisha ya ukawaida , lakini Roma Maisha ya aina hio yalikuwa kwake ni ndoto.

“Hapana lazima nifanye juu chini nina kamilisha yote yalionileta Tanzania , nikishachimba swala hili kwa undani na kujua kwanini nilikuwa kwenye kile kisiwa cha mateso mimi na Seventeen na kuifahamu familia yangu nadhani nitatulia na mke wangu, Edna licha ya kwamba hatujaoana kimapenzi , lakini sidhani kama itakuja siku nitakuacha hata pale mkataba utakapoisha”Roma aliwaza mawazo hayo mchanganyiko huku akizidi kukanyaga pedeli kuelekea jijini Dar es salaam.

Wakati akiendelea kuendesha gari alikumbuka kauli ya Bi Issa kumuuliza hali ya kimaendeleao ya Nasra , alijiuliza kwanini mwanamama yule kauliza juu ya maendeleo ya Nasra ila alikosa majibu kwa wakati mmoja , alijiambia kuwa atafahamu kadri atakavyokuwa karibu na Nasra.

****

Doris alijikuta ni mwenye hasira sana , baada ya kujua kuwa Edna na Roma ni mume na mke , alikasirika sana , lakini na kuumizwa kwa wakati mmoja.

Alianza kukumbuka tukio ambalo Roma alimuomba hela ya nauli wakati akiwa anarudi nyumbani na kumpatia , alikumbuka usiku wao waliotumia na kufanya mapenzi na mwanadada huyu alizidi kutokwa na machozi ,alihisi moyo wake ulikuwa ukimuuma sana kiasi cha kwamba mwenyewe alishindwa kuelewa kwamba moyo wake ulikuwa ukimuuma kutokana na kwamba Edna na Roma walimficha na kumuona mjinga siku zote , au ni kwasababu alijua kuwa Roma mke wake ni Edna mwanamke mrembo na kilichokuwa kikimliza ni wivu wa kimapenzi.

Alisimama kukodolea maji ya baharini muda huu wa jioni huku machozi yakiwa yanamtoka , lakini kila alipokuwa akiangalia baadhi ya wapenzi waliokwa ndani ya fukwe hii ya Coco walivyokuwa wakifurahi na kuonyesheana mapenzi , aliijikuta akizidi kutoa machozi.

“Ninaonekana kutokuwa na bahati katika Maisha yangu , Edna nifanye nini mimi nahisi kumpenda sana mumeo , najiona kabisa siwezi kumuacha hata kidogo , kwanini iwe wewe rafiki yangu”Aliwaza mwanadada huyu na kuwazua huku akionekana ni mwenye kukosa jibu , alionekana alikuwa akishindana na hisia zake.

Doris licha ya kwamba alikuwa sio mwenye kuonyesha waziwazi mapenzi yake kwa Roma alikuwa ashampenda tokea siku ya kwanza wanaonana ,Roma alivyomuomba kiasi cha pesa , tokea siku ile alikuwa alikuwa ni mwenye kumkumbuka Roma , hakujua ni kwanini alikuwa akimkiumbuka mwanaume huyo , lakini picha yake haikuwa ni yenye kutoka kwenye kichwa chake.

Siku ambayo anamuona Roma kwa mara nyingine ndani ya kampuni yake , akija kufanya usaili , alijiambia kabisa ni Mungu ndie aliekuwa amewakutanisha kwa mara nyingine na hivyo hapaswi kuzarau kile Mungu alichompatia na ndio maana siku ile ile aliona atumie nafasi ile kumtambulisha Roma kwa mwanaume mzee aliekuwa akimsumbua , mwanaume aliekuwa akimfahamu kama Mr Kijembe .

Hakujali kabisa katika moyo wake kwamba Roma ameoa , alichokuwa akiamini ni Kwamba Roma alikuwa amepangiwa kuwa nae katika Maisha yao yote na mke aliemua ni makosa ambayo Roma alikuwa amefanya , hayo ndio yalikuwa mawazo ya mwanadada huyu mrembo , aliamini mke wa Roma sio mtu sahihi kwa Roma na yeye ndio alikuwa sahihi , kwani matukio yao ya kukutana ni kama Mungu aliwakutanisha.

Hata pale alipopata taarifa ya Roma kulala na mwanamke Neema Luwazo Mwanamke ambaye alikuwa akimjua sana tu, kwa kuwa na mahusiano na Raisi mstaafu , alijiambia kuwa ni mihemko tu ya Roma ya kukosa mtu sahihi wa kumtuliza na kama atampata basi Roma angetulia kwake na kuachana na mambo ya wanawake , kwani angempa kile kitu ambacho anakitafuta nje , kitu ambacho aliamini ni kwamba alikuwa akikikosa kwa mke wake.

Siku ya Jumapili ndio siku ambayo alipanga kutimiza jambo lake la kuanza kuweka ukaribu na Roma , aliamini anapaswa kufanikisha swala la yeye kuwa karibu kabla ya kwenda safari ya kikazi Japani , alitaka katika safari hio waitumie kama sehemu yao ya matembezi kama wapenzi , na ili kukamilisha swala hilo anachotakiwa kufanya ni kuhakikisha Roma anakuwa karibu yake anamzoea na hatimae kumpenda.

Baada ya kuwaza hayo , hatua ya kwanza aliofikiria ni kwenda kutafuta zawadi yoyote ambayo aliamini itamfurahisha Roma na eneo pekee alipoona panafaa kupata zawadi hio kwa siko hio ya jumapili ni Mlimani City.

Nwanadada huyu alijiandaa , alichukua kadi yake ya benki aina ya ‘Black Card’ kadi ambayo ilikuwa ikimruhusu kutoa kiasi chochote kile cha pesa na kuiweka katika mkoba wake , na kisha akachukua ufunguo wa gari yake na kutoka ndani ya jumba hili la kifahari alilokuwa akiishi mwenywe na wafanya kazi.,Jumba ambalo alikuwa amenunuliwa kama zawaidi na baba yake .

Lakini baada ya kufanya safari yake na kufika Mlimani anajikuta akishuhudia kitu ambacho moyo wake haukutarajia kukiona , alimuona mwanamke ambaye aliamini sio sahihi kwa Roma akiwa ni Edna , Rafiki yake kipenzi , bosi wake kazini, moyo wake ulipigwa na ganzi.

“Doris!!”Ilikuwa ni sauti ya mwanaume iliosikika nyuma yake na kumfanya mwanadada huyu ageuke ni nani anamuita , lakini ile anageika alikutana na uso wa Abu.

“Abu vipi , kwanini uko hapa ?”Aliuliza Doris kwa namna ya kushangaa.

“Nimekuja kupunga upepo kama wengine Doris , wewe vipi , kwanini uko hapa?”.

“Namini nipo kwa ajili ya kupunga upepo “Abu alijikuta akitabasamu .

“Doris najua unaonekana kuwa katika hali ya mawazo , lakini nimekuwa nikisubiria sana jibu lako”

Doris alishangaa na kuanza kuvuta pumzi kwa nguvu na kumgeukia Abuu….

Ni jibu gani ??

SEHEMU YA 33

2010 -KIGALI STATE HOUSE

Ni mwaka 2010 muda wa saa tano za Asubuhi mheshimiwa Jeremy alionekana ndani ya ofisi yake akifanya kazi kama kawaida, katika kuwatumikia wananchi wa Rwanda, lakini siku hii kwa mheshimiwa huyu hali yake ilionekana kuwa sio ya kawaida , kwani alionekana kuwa ni mwenye wasiwasi sana kuliko siku zote hali ambayo ilimfanya kukosa utulivu , kila saa alionekana kuangalia saa ya ukutani kama mtu ambae alikuwa na jambo ambalo alikuwa akilisubiria.Ilivyofika saa sita na nusu aliingia Linda mlinzi wa karibu wa Mheshimiwa Jeremy.

“Mheshimiwa Ashafika”Aliongea Linda na kumfanya mheshimiwa Jeremy avute pumzi .

“Mruhusu aingie”Aliongea mheshimiwa na kisha akatoka kwenye meza yake na kwenda kwenye masofa na hapo hapo mlango ulifunguliwa na aliingia mwanaume mmoja wa kizungu alievalia shati la Blue bahari na suruali ya kadeti , muonekano wa huyu jamaa ni kama vile hakuwa akiingia kuonana na mheshimiwa , kwani alivaa kikawaida sana kama muhuni flani hivi.

“Welcome Mr Viladkov”Aliongea mheshimiwa kwa kingereza.

“Asante sana mheshimiwa”Aliongea na kisha alitoa karamu nyeusi flani hivi pana kidogo lakini ya kawaida , kama zile za rangi na kisha alianza kuifungua kama mtu ambae anatoa ule mrija wa wino, na akatoa kifaa Fulani hivi kama kile kichwa cha kuchomekea kwenye Earphone lakini hiki kwa juu mwisho kina kitu kama kigoroli.

“Hili ndio faili mheshimiwa”Aliongea na kisha alimpatia Jeremy kile kidude na mheshimiwa alishangaa m inakuwaje kadude kama hako kawe ndio faili ambalo alikuwa akilisubiria kwa hamu.

‘”Usishangae mheshimiwa Hata Urusi sasa imeendelea kwenye teknolojia , na hio ni mbinu yetu mpya kuficha taarifa wakati wa kuzisafirisha” ’Mheshimiwa Jeremy hapa alishangaa na akachukua Tablet iliokuwa kwenye meza yake na kuchomeka kale kadude na baada ya tablet ile kusoma kama Earphone ilisoma kama memori , alishangaa na Viladkov akatabasamu.

“Ni taarifa nyeti sana hio , na serikali ya Urusi imelipa kiasi kikubwa kuinunua kwa mtu aliekuwa akiuza”Aliongea bwana huyu na mheshimiwa Jeremy aliifungua na ajabu ni kwamba alikutana na picha.

“Mbona ni picha sio kama faili nilivyokuwa nikitegemea?”

“Angalia kwanza hizo picha mheshimiwa kwa umakini na uniambie umegundua nini?”

Alianza kuangalia hizo picha kwa kuzizoom na katika picha hizo kulionekana meli kubwa ya mizigo ikiwa inashusha mavyuma , lakini baada ya mheshimiwa kuangalia kwa ukaribu Zaidi aligundua ni bawa la Ndege.

“Linaonekana kama bawa la Ndege”

“Angalia na hio nyingine” Aliangalia na pia yenyewe ilionekana kama baadhi ya vipandevvipande vya mabaki ya ndege.

“Hio meli inamilikiwa na kampuni Neptune , kampuni ambayo ni sehemu ya kampuni kubwa ya kuzalisha ndege ya kimarekani inayofahamika kwa jina la Ngebo Aeronautical”Mheshimiwa alionekana kushangaa , lakini pia alizidi kuongeza umakini.

“Hizo picha zilipigwa Tarehe saba March 1998”Aliongea na mheshimiwa huyu alishangaa sana.

“Unataka kumaanisha kwamba ni siku moja kabla ya ndege ya Malaysia kupotea?”

“Ndio kutoka sehemu ambayo meli hio ilipo na sehemu ambavyo ndege ya shirika M ilipotea ni umbali wa kilomita ishirini tu , kwa maana hio hayo ni mahesabu ambayo yamepigwa kabisa na hio meli ilitupa mabaki hayo unayoyaona kwenye hizo picha eneo hilo”Mheshimiwa Raisi alijikuta akitetemeka maana anacho ambiwa hapo ni taarifa nzito sana , tena nzito kweli kweli.

“Mheshimiwa hii ni siri ninayokupatia ambayo ni siri kubwa ndani ya taifa la Urusi na ni kama Asset kwetu , hivyo taarifa hii inapaswa kuwa siri , mheshimiwa Raisi Viladmn karuhusu upatiwe taarifa hio ili kwa ajili ya kushawishi mataifa ya Afrika kuingia kwenye Mpango TASAC”Mheshimiwa alishangaa Zaidi.

:Mheshimiwa chomoa hio flash na uichomeke tena” aliongea Viladkov na mheshimiwa alichomoa na kuichomeka tena na ikasoma tena kama memori , aligusa ten ana zile picha zikawa zimefutika ils sasa kulionekana faili lililokuwa kwa mfumo wa ‘Xml’ , mheshimiwa alilifungua na kuanza kusoma na hapa ndipo aliposhangaa.

“Hio ni barua ya wito iliotumwa kwa mashirika ya kijasusi makubwa yote duniani na katika hio barua inaonesha kulikuwa na makubaliano ambayo yalikuwa yanatakiwa kufanyika juu ya mpango ambao ulipewa jina la LADO ambapo sisi tulishindwa kung`amua kirefu cha neno hilo , na shirika letu pekee ndiio halikutuma muwakilishi kwenda kuhudhuria kikao hiko ambacho kilifanyikia nchini Italy”Mheshimiwa jasho lilimtoka maana kadiri anavyoambiwa ndio anavyoona siri hii kuzidi kuwa nzito na kuhofia Maisha yake.

“Kwa hio unamaanisha kwamba LADO na kupotea kwa ndege ya shirika la M ni swala ambalo lina muunganiko na limeratibiwa kwa makubaliano ya mashirika makubwa ya kijasusi duniani?” Aliuliza na jamaa alitingisha kichwa kukubaliana nae.

“Kwanini mmeamua kunipa hii taarifa?”

“Mpango TASAC ni mpango ambao unahusisha serikali ya Urusi kurudisha umoja wa Kisoviet , lakini hili ili liweze kufanikiwa , tunahitaji sapoti kutoka Afrika , tunahitaji udhaifu kutoka kwa mataifa makubwa ambao utatusaidia pale itakapobidi serikali yetu kuingia vitani , mataifa haya hayatoi msaada , lakini nyie wa mataifa ya Afrika mnapaswa kutuunga mkono kwa kukaa kimya.”

“Na ili swala hili lifanikiwe unapaswa kuhakikisha asiliamia sabini ya mataifa ya Afrika yanakuwa kwenye huu mpango TASAC na mheshimiwa Raisi wa Urusi amekuchagua wewe kutokana na uzoefu wako katika uongozi, ukifanikisha mpango huu basi serikali ya Urusi itafanya juu chini kubaini ni nini kipo ndani ya operesheni iliopewa jina la LADO”.

“Natakiwa kukubali swala hili hapa hapa?”

“Hapana mheshimiwa , swala hili lina umuhimu sana kwa nchi yetu na mheshimiwa Raisi atakupigia simu na mimi nipo hapa kwa ajili ya kukueleza haya , kwani tunajua kuwa wewe ni mmoja ya wahanga wa AJali ya ndege na unataka kulipiza kisasi , lakini kutokana na ukubwa wa tukio lenyewe na udogo wa taifa lako, hautoweza kupata hio nafasi ya kuujua ukweli”Aliongea bwana huyu na heshimiwa Jeremy alikubali kuwa kiongozi wa juu wa mpango TASAC.

****

“Sauron habari za muda huu?”

“Salama kabisa mfalme Pluto, habari za Tanzania?”

“Hapa ni kwema kabisa Sauron , nimekupigia kupata ripori ya yale tilioongea jana”

“Mfalme Pluto , nimeshayakamilisha yote na nimepanga vijana kumi wenye uwezo wa hali ya juu kwa ajili ya kuja nchini Tanzania, lakini kuna jambo moja nimeona nitoe pendekezo”

“Edelea kuongea Sauron nakusikiliza”

“Nimeona makomandoo hawa wakiingia nchini kama watalii hawatapata kibali cha muda mrefu cha kukaa hapo Tanzania , hivyo nimejaribu kuwasiliana na balozi ya Sweeden nchini Tanzania na kuwaomba watufanyie mpango wa kuwaingiza wanajeshi wetu kama wafanya kazi wao”Roma Alitabasamu.

“Sauron wewe unakili sana , hili sikulifikiria , ni kweli watapaswa kukaa nchini muda mrefu kidogo kwani pia nataka wamlinde mke wangu”Sauron alishangaa.

“Mfalme Pluto usiniambie umepata mke?”

“Ndio Sauron , sio muda mrefu sana nimefanikiwa kupata mke”

“Hongera sana mfalme Pluto , ila kwa hatua hio sidhani kama utarudi huku kisiwani”

“Yanayotokea kesho hatuyajui Sauonoi hivyo siwezi kuongea lolote juu ya hili”.

“Ni kweli Mheshimiwa Pluto , ila nitatamani kumuona malkia wetu”Roma alitabasamu

“Utamuona Sauron nitakuja nae siku moja , Sauron kuna jipya lolote kutoka The Zeros?”

“Mfalme Pluto vijana bado wanaendelea kufuatilia na naamini muda si mrefu watatupatia taarifa “

“Sawa Sauron , nadhani tutawasiliana baada ya vijana kufika Tanzania”Baada ya hapo waliagana na Roma akakata simu .

Muda huu Roma anawasiliana na Sauron ilikuwa ni saa moja kwenda saa mbili hivi , hivyo baada ya kumaliza tu aliitwa na Bi wema kwa ajili ya chakula cha usiku.

Baada ya kufika tu chini na Edna alikuwa akishuka alievalia kigauni kilichokuwa kikipeperuka kiasi kwamba kilimfanya Roma aliekuwa chini ya ngazi aone mapaja ya malaini ya Edna na alijikuta hisia za mapenzi zikimuandama.

“Kukaa na mwanamke kama Edna halafu hupati kitumbua chake ni swala ambalo nina uhakika madaktari wataniambia ni sumu kwa Afya yangu , nikimaliza hapa nduki kwa Rose nikapunguze kichupa”Aliwaza Roma huku akivuta kiti na kuketi.

Edna na yeye alijikuta akitabasamu baada ya kumuona Roma leo hajatoka kabakia nyumbani , kwani mara nyingi hakuwa akipenda sana Roma a tabia yake ya kutoka na kurudi asubuhi yeye kama mke aliona sio vizuri.

Wanafamilia hawa walikula wakashiba na baada ya hapo Edna aliungana na Bi wema kusafisha vyombo , lakini wakati Edna akiwa bize na vyombo upande wa jikoni Roma alimchungulia kwenye mlango.

“Bebi ndio natoka hivyo , hapa hadi kesho”Aliongea Roma na Edna ambaye alikuwa ameweka mikono yake kwenye Sink alijikuta akikunja ngumi kwenye maji na kung`ata meno , kwani kila ambacho kilikuwa kikimfurahisha dakika chache nyuma kimegeuka ndivyo sivyo,Edna aliishia kutingisha kichwa na Roma hakujali aliondoka.

“Yaani huyu mwanaume hatulii nyumbani”Aliongea Edna kwasauti pasipo kujua nyuma yake kasimama jasusi mbobezi wa mapenzi Bi Wema.

“Miss ulifikiri sasa atafanyaje , mmeoana lakini hamlali chumba kimoja , yule ni mwanaume na wanaume tendo la nndoa ni kama hitaji lao la msingi hawezi kukaa na mtoto mrembo kama wewe halafu akuangalie kama picha ya ukutani”Edna alifikiria kidogo.

“Bi Wema nitafanyaje , bado sina hisia nae na wewe unaelewa tumeoana kimkataba”.

“Naelewa ndio , lakini miss angalau jaribu kuufungua moyo kwa Roma , huenda ukampenda na mkawa Mume na mke kimapenzi sio kimkataba”Edna alitingisha kichwa kuelewa

Baada ya kufika chumbani kwake alionekana kuwaza maneno ya Bi Wema na kuona kidogo yana maana.

“Au nijaribu kumpa?”Aliwaza Edna akimaanisha ajaribu kumpa Roma kitumbua.
Unafikiri nini mwisho wa yote ....??
WIKIEND NJEMA TUONANE JUMATATU

CHANGIA KAZI HII KWA KULIPIA KUANZIA 2000 KUENDELEA NIKUUNGANISHE NA GRUPU UIFATILIE KWA VIPANDE VITATU KILA SIKU TUPO SEASON 2 KWENYE GRUPU

GRUPU NI KWA AJILI YA SIMULIZI HAKUNA KUCHAT

LIPIA NAMBA 0687151346 AIRTEL AU 0623367345 HALOPESA AU 0657195492 TIGOPESA JINA ISSAI SINGANO UKILIPA TUMA MESEJI YA MUAMALA NAMBA 0687151346 WATSAPP


View attachment 2336156
[emoji119]
 
jioni ya leo
Naaam hili dude imebidi jana nilipige saa 6 usk mpaka saa 8. Yaani ukiliweka tu tunalo...hadithi nzuri sana na ni unpredictable. kama inaisha vile kumbe ndio inaanza...SinganoJr wewe ni Mwamba kabisa. Big up mzee.
 
Back
Top Bottom