SEHEMU YA 327
Kwa jinsi Roma alivyoshangaa ilimfanya Nasra kuamini Roma hakuwa na taarifa za Edna kumfadhili Najma Kwenda masomoni nchini Marekani.
Na hio ilikuwa kweli kabisa , baada ya Roma siku ile kufahamu matibabu ya Juma yalifadhiliwa na mke wake hakuendelea kufatilia kabisa maendeleo ya Juma lakini pia kwa Najma vile vile , moja ya sababu ambayo ilimfanya kutotaka kuwa na ukaribu wa mara kwa mara na Najma ni juu ya hisia zake , aliamini kukaa mbali na msichana huyo ndio kumsaidia.
Sasa Roma hakufahamu kama Najma alikuwa amekwisha Kwenda masomini nchini Marekani, jambo hili lilimshangaza sana mara baada ya kufahamu mke wake ndio aliefanikisha hilo.
“Unataka kuniambia Edna mke wangu kafadhili masomo ya Najma bila sababu?”Aliuliza Roma.
“Siwezi kufahamu , ila ninachohisia nadhani kuna makubaliano yaliofanyika kati ya Najma na Edna , maana kutokana na yaliotokea ni ngumu kwa Edna kutoa kiasi cha pesa kwa ajili ya matibabu ya Juma na wakati huo huo kumepekea Nasra masomoni”Aliongea Nasra na Roma aliona ni kweli huenda kuna jambo ambalo mke wake alikubaliana na Najma na alijiambia atakuja kufahamu tu , aliamini sana katika kumtendea mtu wema , lakinisiku zote wema ukizidu huibua mashaka na ndicho ambacho alihisi.
Roma baada ya kumfikisha Nasra nyumbani kwake, moja kwa moja alichukua uelekeo wa Kwenda nyumbani na ndani ya nusu saa tu alikuwa ashafika na kuingiza gari ndani mara baada ya kufunguliwa na Derick.s
Nyumba ilionekana kutulia kuliko isivyokuwa kawaida na muda ambao Roma alikuwa akiingia hapo ndani ilikuwa imetimia saa kumi na moja za jioni.
Roma baada ya kuingia ndani , eneo la Sebuleni aliweza kukutana na Bi Wema , ambaye alionekana alishatambua uijio wake kwani alimlaki kusalimiana nae.
“Bi Wema Lanlan yupo wapi?”.
“Miss Mage , alikuja na kumchukua na kumpeleka kuangalia Wanyama , wametoka tokea asubuhi pamoja na Qiang”
Roma baada ya kusikia jina la Mage , alikumbuka hakuwa ameonana na huyo mrembo Polisi kwa siku kadhaa tokea mara ya mwisho kukutana kutokana na tukio la Salah, licha ya kwamba waliishi wakiwa majirani.
Ukweli Roma muda mwingine alijihisi ni kama mkatili kwani alikuwa na wanawake wengi lakini hakuwahi hata mara moja kuanza kuwatafuta hata kwa kuwatumia jumbe za meseji.
Roma alinyoosha moja kwa moja mpaka ndani kwake na kuweka mwili wake sawa kwa kuoga na kubadili nguo na alivyomaliza alichukua simu yake na kutafuta namba ya Tanya , huku dhumuni lake lilikuwa ni kuafahamu kile kilichokuwa kikiendelea ndani ya Hongkong.
Roma baada ya kuongea na simu kwa madakika kadhaa na kupewa taariufa ambazo zilimridhisha alijitupia kitandani na muda aliokuja kushituka ilikuwa ni usiku wa saa moja , alipiga mswaki na baada tu ya kumaliza alishuka mpaka sebuleni.
“Ankoo.!!”Aliita Lanlan na kumkimbilia, Roma alitabasamu na kumbeba Lanlan juu juu.
“Chubi umeshinda wapi siku nzima?”
“Aunt Mage alinipeleka kuona Wanyama, nimeona Simba , Twiga na na Manyani”Aliongea na kumfanya Roma kutabasamu na kushindwa kuelewa kwanini Lanlan alikuwa akipenda kuona Wanyama kwa kiasi kikubwa , Roma alimwangalia Mage aliekuwa ameketi kwenye sofa akimwangalia kwa macho yenye kuonyesha alikuwa na mambo mengi yanapita kichwani kwake.
“Baba na mwana”Aliongea Mage na Roma alitabasamu huku akimkagua mrembo huyo.
“Tumependezana sio?”
“Hakika, ukiwa na mtoto kama hivyo unaonekana kuwa mtu mzima Zaidi na upo siriasis na Maisha.”Aliongea Mage na Bi Wema alichangia na yeye, lakini Roma kwa namna flani hivi aliona Mage amemtupia na dongo. Hasa hapo kwenye kuwa siriasi na Maisha.
Kwa jinsi ilivyoonekana ni kama Mage alisuburia Edna asafiri, kwani Roma baada ya kuketi kwenye masofa Mage alisema anaenda kusaidiana na Bi Wema kuandaa chakula.
“Bi Wema halafu sijamuona Mama”Aliongea Roma,ukweli aliamini mama yake atakuwa yupo nyumbani kwa baba yake , kwani hapakuwa mbali , lakini aliona aulize.
“Kaenda nyumbani kusalimia ila ameahidi anarudi kabla ya chakula cha usiku”Aliongea Bi Wema na Roma alitingisha kichwa kuelewa.
Mage aliekuwa jikoni alijitahidi sana kujipikisha, alitaka kuchukua pointi mbele ya mwanaume anaempenda, yaani Roma na ndio maana wakati anafika hapo asubuhi yake alikuwa amebeba mahitaji maalumu ya kupikia na hata Bi Wema alipofika jikoni alisaidia vitu vichache tu na kumuacha Mage kuendelea mwenyewe.
Saa moja kama na nusu alianza kurudi Yezi . akafuatia Sophia ambaye alitoka kumsalimia babu yake na kabla hata ya wanafamilia hao hawajakaa mezani aliingia Blandina ambaye alionekana kuchoka mno licha ya kwamba ametoka nyumbani kwao ,Roma kwajinsi alivyomuona mama yake , alimuonea huruma.
Juhudi za Mage zilionekana kuzaa matunda kwani kila mmoja alifurahia chakula mno , akiwemo Lanlan na Roma ambao walikua Zaidi ya robo tatu ya chakula chote.
Baada ya kumaliza kula Roma ndio aliechuua jukumu la kumsindikiza Mage , sasa wakati Mage anatoka hapo ndani, huku nyuma Blandina alikuwa na wasiwasi mno , aliona kila dalili ya Mage kuwa na ukaribu wa Zaidi , kiasi ambacho kwa umri wake huo aliamini wawili hao walikuwa kwenye mapenzi , sasa mama huyu jambo hilo lilimchanganya na kujiuliza Roma alikuwa akielewa anachokifanya au tamaa zimemzidi kupitiliza , maana alishindwa kuelewa mwisho wake utakuaje na kuna muda aliona huenda yote hayo yanatokea kutokana na mazingira ambayo Roma amekulia.
Baada kama nusu saa kupita hatimae Roma aliweza kurudi nyumbani na ile anakaribia kuingia mlango mkubwa , Mama yake Blandina aliekuwa ameketi eneo la bustanini alimwita.
Kwasababu Roma ndio kwanza alikuwa amerudi kutoka safarini , ilibidi kumuelezea mama yake juu ya safari yake ya Kwenda kijijini na Roma alimuelezea namna ambavyo amepokelewa.
“Roma mwanangu unataka kuoa mke wa pili? , maana bado sijaelewa mpaka sasa mipango yako”
“Mke wa pili siwezi kuoa mama , tayari Edna ni mke wangu”
“Sasa kama hutaki kuoa mke wa pili imekuwaje ukaenda kujitambulisha nyumbani kwa Nasra ,kama huna nia ya kumuoa?”
“Nasra atabakia kuwa mwanamke wangu tu mama , ila kuhusu ndoa Hapana na uzuri licha ya kwamba sitaki kumpoteza mwanamke yoyote ambaye nipo nae kwenye mahusiano , lakini kama kuna atakae fanya maamuzi ya kuniacha kwa hiari yake basi siwezi kumng’ang’ania abaki kwangu ilihali siwezi kumtimizia kile anachotaka, ila kama wataendelea na mimi kwa mapenzi yao basi siwezi kuwaacha”Aliongea Roma na kumfanya Blandina kuvuta pumzi kwa nguvu na kuzishusha maana mpaka hapo aliona kuna kazi kubwa sana, kwanza hakukuwa na mapenzi ya karibu kati ya Roma na Edna , lakini baada ya mwanae kutatua tatizo la umbali uliokuwepo na mke wake yeye anaongeza wanawake mpaka Kwenda kujitambulisha , lakini licha ya hivyo alishindwa kabisa kuingizia neno.
“Na huyu Mage pia una mahusiano nae?” Roma alijikuta akikuna kichwa kutokana na swali hilo la mama yake , ukweli alikuwa akijionea aibu muda mwingine.
“Naweza pia kusema hivyo mama”.
“Roma mimi naamini unaelewa unachokifanya na sitaki sana kukuingilia kwenye maswala yako ya kimahusiano , lakini wasiwasi wangu upo kwa Edna”
“Mama kuhusu Edna , hilo lisikuumize kichwa sana , Edna ni mke wangu na siku zote atabakia kuwa mke wangu na naamini kuna sababu kubwa ya Edna kuwa mke wangu , mpaka sasa tumefikia hatua ambayo siamini kama Edna anaweza kunikatia tamaa na kuniacha”Aliongea na kumfanya Blandina kumwangalia Roma na kisha aligeuza uso wake na kuangalia maji.
“Ni Vyema kama anagalau unamjua mkeo, ila unachopaswa pia kuelewa sisi wanawake tunazo tabia ambazo tunafaana kwa asilimia kubwa , unaweza ukamuona Edna katulia lakini itafikia kipindi anaweza kuchoka na kuchukua maamuzi magumu”Aliongea Blandina na Roma aliona mama yake ana pointi ya msingi , lakini hata hivyo hakuwa na chakufanya , kama kweli Edna atachukua hayo maamuzi magumu kwa sababu ya wanawake aliokuwa nao basi aliona atakuwa kwenye hali ambayo hataweza kuwa na chaguzi ya aidha kumuacha Edna au kuwaacha wanawake wengine.
“Mama nadhani ni muda sasa wa kunieleza kile ambacho kinakusumbua , unaonekana kupauka kwa mawazo mama yangu”Aliongea Roma.
“Jumapili iliopita nilivyoenda kituoni niliweza kukutana na Raisi Kamau pamoja na Raisi Jeremy”Aliongea Blandina kwa unyonge na kumfanya Roma kushangaa.
“Wote wawili kwa pamoja , walikuwa wakihitaji nini?”Aliuliza Roma na Blandina alivuta pumzi nyingi akijiandaa kuongea.
********
“Miss Edna nitoe shuktani zangu za dhati kabisa kwa kuweza kufanya swala hili ambalo lilikuwa likituumiza kichwa kumalizika kwa urahisi , kama sio wewe huenda kungekuwa na mvutano mkubwa sana”Aliongea Tikayi mara baada ya kikao cha pamoja kumalizika na kufikia kwenye makubaliano , huku katika maongezi hayo Edna akionekana ndio aliekuwa kinara kusuluhisha swala hili la mgogoro ya kimaslahi na kampuni ya Aba.
Ukweli licha ya kwamba Edna aliweza kumaliza mgogoro huo , lakini aliona ni kama hakuwa amefanya kitu kabisa , kwani kila kitu kimetokea kutokana na yeye kuwa na cheo cha Persephone yaani mke wa Hades
Swala la mgogoro huo kama sio konekesheni , basi lingechukua sura mpya na kupelekea mauzo ya hisa za kampuni yake kushuka kwa kiasi kikubwa jambo ambalo hakuwa tayari kabisa kuona likitokea hata kidogo , kwani alikuwa na mipango mingi sana na kampuni yake, hivyo vikwazo vikubwa kama hivyo hakutaka kabisa vimkwamishe kufikia malengo aliojiwekea.
Kilichofanyika ilikuwa rahisi sana , Edward aliweza kutumia ushawishi wake kumtumia Mr Kelphin kumaliza swala hilo , Kelphin alishindwa kukataa na hio ni kutokana na kwamba , licha ya Ye Chen na Morri kushirikiana kugundua hio teknolojia ya material mapya , lakini kutokana na mkataba ambao walisaini wanasayansi hayo na taasisi ya utafiti ya Yamakuza , ulikuwa ikionyesha asilimia arobaini ya umiliki wa teknolojia huo upo chini ya kampuni huku wagunduzi wakiwa na aslimia therathini kwa kila mmoja, hivyo kitendo cha Ye Chen Kwenda kuuza teknolojia hio kwa kampuni ya Aba , lilikuwa ni swala la ukiukwaji wa vipengele vya kimkataba , licha ya kwamba Ye Chen alishavunja mkataba na tasisi ya Yamakuza kabla ya kuhamia Aba.
Sasa kilchofanyika sio kwamba Yamakuza wangeshindwa kesi kutokana na Ushahidi uliokuwepo , lakini ambacho hawakutaka kama kampuni ni uchelewashwaji wa uzinduzi wa material hayo ,kwani terehe ilikwisha tolewa tayari na mikataba mingi na makampuni ilikwisha kusainiwa , hivyo kama kesi hio ingeendelea kusikilizwa katika mahakama ya kimataifa Usuluhishi , ingechukua Zaidi ya miezi sita mpaka kukamilika, jambo ambalo lingepelekea hasara Zaidi, na ndio maana hatua ya kuyamaliza maswala hayo kibiashara ilikuwa busara kuyamaliza chini kwa chini.
Edna akibakia na asilimia zake zilezile za faida kama awali ,lakini upande wa kampuni ya Yamakuza wakipata hasara ya asilimia kumi kama fidia ya Kwenda kwa Ye chen ambaye alishikiri katika ugunduzi , lakini wakati huo huo na Mori akiingia hasara ya kutoa fidia ya asilimia kumi Kwenda kwa Ye Chen kwa makubaliano yaliofkiwa.
Kilicho msaidia Edna pamoja na kampuni ya Maple kutoingia hasara ni kutokana na kwamba mkataba wao ulikuwa ni wa usambazaji na Marketing pekee , bali sio wa umiliki wa teknolojia, hivyo mgogoro ulikuwa ukiwagusa Yamakuza moja kwa moja , huku yeye na kampuni yake wakiguswa kwa njia isiokuwa ya moja kwa moja.
Ni muda wa usiku sasa ,Edna alikuwa ndani ya chumba chake akiwa amesimama akiangalia upande wa nje wa jiji hili la Hongkong huku mkononi akiwa ameshikilia bangiri ambayo alipatiwa siku mbili zilizopita na babu yake Roma.
Edna alionekana kuwaza mambo mengi kwa wakati mmoja , lakini kubwa Zaidi ni juu ya yeye pamoja na Roma, mawazo yake yalimfanya mpaka kugeuka na kuangalia chupa ya Mvinyo ambayo alikuwa ameiweka Mezani, Chupa ambayo alikuwa amepewa kama zawadi na Mr Kelphin , zawadi ambayo gharama yake kwa haraka haraka ni Zaidi ya milioni mia nne za kitanzania, sasa Edna hakuwa mjinga kwa mtu mzito kama Kelphin mwenye hadhi yake kwenye jamii kumpa zawadi kubwa ya namna hio , aliamini urafiki uliokuwepo baina ya Roma na Mr Kelphin ulikuwa mkubwa mno na hilo ndio lilimfikirisha , lakini pia pamoja na maswala yake ya kibiashara yalivvyokuwa rahisi kwa msaada wa familia ya Rothchild.
Alitoka dirishani na kutembea mpaka kwenye meza ya kioo na kisha kunyanyua ile chupa ya mvinyo na kuiangalia kama mtu ambaye alikuwa akiishangaa, lakini katika hali ya kushangaza , ghafla Edna alijikuta akirudisha ile chupa chini haraka sana kama vile ilikuwa ya moto huku akianza kutetemeka akiwa ameshikilia kichwa , hali ile iliendelea kwa dakika kama nne hivi ..
“Aarrggg….!!!”Edna alijikuta akishika kichwa huku akionekana kupitia maumivu makali sana ya kichwa lakini wakati huo huo matukio ambayo hayakueleweka kwenye kichwa chake kuanza kupita kwa kasi , alikuwa kama mtu ambaye alipoteza kumbukumbu na sasa zinaanza kurejea upya na katika picha hizo mchanganyiko za matukio moja wapo ni mwanaume anaefanana na Mr Kelphin kumpatia chupa ya Mvinyo hio hivo iliokuwepo hapo ndani kwake ,yaani tukio la siku hio ni kama lilishawahi kumtokea katika Maisha yake na siku hio limejirudia upya , sasa kumbukumbu hizo zinamfanya kupitia maumivu makali mno ya kichwa.
“Mamaaa…!!!!”
“Puuus!!!”Edna alijikuta akidondoka chini palepale na kutua kwenye zuria na kupoteza fahamu