SEHEMU YA 390.
Kilichotokea kwa Edna kuamka mapema nje ya muda Roma alioukadilia ni kama kile kile kilichotokea Ufaransa, wakati Roma akipambana na Depney , sasa haikueleweka kwanini Edna kuathiriwa kidogo sana na nguvu zao miungu , kwani ufaransa aliemlaza kwenye usingizi alikuwa ni Apollo..
Edna aliamka ndani ya lisaa limoja tu , yaani wakati Roma alivyokuwa usingizini ndio muda ambao Edna aliamka na kuanza kuomboleza.
Edna tokea siku ambayo aliweza kujua siri ya mama yake , siri aliopata kupitia flash Disk aliopewa na raisi Kigombola , alikuwa akitegemea siku moja atakuja kugundua kitu ambacho kitakuja kumuumiza sana kihisia.
Ikumbukwe katika flash ambayo Raisi Senga alimpatia Edna , hakukuwa na maelezo mengi , alichokigundua Edna ni kwamba mama yake alikuwa na kisasi alichokuwa akikiendeleza, lakini pia akampa kazi hio ya kisasi yeye kuikamilisha , huku akiacha orodha ya kampuni ambazo hakukuwa na maelezo yoyote kwamba alichokuwa akitakiwa kufanya ni nini mpaka alipokuja kugundua uwepo wa ‘Deposit Box’ ndani ya Swiss In, ambapo ndani yake ilikuwa imebeba bahasha iliokuwa na taarifa ambayo ndio inamfanya kuwa kwenye hali ya huzuni na majonzi.
Raheli Adebayo katika stori yake ya kimaisha mara baada ya kujua ukweli kwamba mtoto wake Lorraine, pacha wake na Edna anaishi kwa jina la Agent 17, ndio kisasi chake kilianza rasmi , lakini kutokana na kwamba watu ambao walikuwa na mtoto wake kuwa wakubwa serikalini, aliamini pesa pekee ndio zitakazo muwezesha kutimiza azma yake, Azma ya kumrudisha mtoto wake huyo ili kutoendelea kujutia kosa alilolifanya miaka mingi nyuma , kosa la kukubali kumuachia Lorraine Kwenda kulelewa na Raisi Jeremy jambo ambalo lilipelekea kadhia ambayo mtoto wake amekutana nayo mpaka kubadilishwa jina , lakini bahati mbaya mpaka anakufa hakuwa ametimiza Azma yake.
Kwahio ni rahisi kusema kwamba Edna sasa anajua kifo cha mama yake ni cha kutengenezwa , lakini hafahamu kama kuna Zaidi ya kile anachokifahamu ambacho kilikuwa kikiendelea kwenye Maisha ya mama yake, anajua tu kwamba mama yake alikuwa mjamzito wa Watoto mapacha lakini hakuwa akielewa pacha mwenzake yupo wapi.
Edna alikaa kitandani akiwa peke yake huku machozi yakiwa yanamtiririka , kila akijaribu kuyafikiria maisha magumu ambayo mama yake alikuwa akiishi moyo wake ulimuuma na alijidharau mno kwa kutogundua kama mama yake alikuwa akipitia kipindi kigumu , yeye kama mtoto alijihisi alikuwa na haki ya kuwa karibu na mama yake lakini kutokana na ubize wa masomo akashindwa kujua kile kinachoendelea.
Baada ya kuwaza na kuwazua alijikuta akifuta machozi yake na kisha akachukua picha ya mama yake iliokuwa pembeni kwenye kijimeza na kisha akaishika kwa kuikodolea macho , lakini kadri alivyokuwa akiangalia alijikuta machozi yakizidi kumtoka kwa mara nyingine , mrembo Edna alionekana kuwa katika hali ya huzuni mno.
“Mom naomba unisamehe , sikuwepo karibu yako wakati ulipokuwa unapitia kipindi kigumu , I am so so….”Alijikuta akishindwa kuendelea na kuanza kulia kwa kwikwi awamu hii kwa takribani nusu saa nzima alizitumia kuomboleza , mpaka aliponyamaza mwenyewe.
“Nitautafuta ukweli wote na nitahakikisha nalipa kisasi kwa ajili yako mama yangu , ndio njia pekee ambayo naamini utanisamehe kwa kutokufahamu kama ulikuwa ukipitia magumu mengi”Aliwaza Edna huku hali yake ikirejea upya , ijapkuwa hakuonyesha furaha , lakini alionekana kuacha kulia na kuwa na sura iliojaa usiriasi.
Saa moja za jioni ndio alishuka kutoka chini huku akiwa ashaongea na halmashauri ya kichwa chake , alishajiambia kwenye akili yake kwamba vita ndio inaanza , vita ya kulipa wale waliohusika kumfanyia mama yake majaribio ya kisayansi mpaka kupelekea kifo chake , alikuwa ashafanya maamuzi tayari , maamuzi ambayo ili kuyakamilisha alitakiwa kuwa na nguvu na sio kukaa kitandani kuomboleza , alitakiwa kuwa jasiri ambaye muda wowote yupo tayari kukabiliana na maumivu ili kutimiza malengo yake.
Muda ambao alikuwa akishuka kutoka juu ndio muda ambao Afande Kweka alipiga simu kumwambia kwamba ataondoka na Lanlan Kwenda nae Iringa kwenye mashamba yake na Edna jibu alilotoa ni kwamba mpaka amshirikishe mume wake Roma kwanza ,lakini Afande Kweka alimwambia atampigia mwenyewe simu kumjulisha.
Roma alienda kukaa karibu na mke wake na kisha kumshika mkono , Blandina aliekuwa amesimama alijiua kuna kinachoendelea , lakini hakutaka kuingilia na alitembea mpaka jikoni kwa ajili ya kuandaa chakula.
Edna alimwangalia Roma alieshika mkono wake , huku akiwa na sura isio jaa furaha wala huzuni , ilikuwa ni sura yake ile ile ya kikauzi ambayo imezoeleka.
“Edna mke wangu , najua unapitia kipindi kigumu kwa sasa na sijui namna ya kurudisha furaha yako, jana nilikuambia nitakuwa bega kwa bega na wewe kwa nyakati zote za furaha na huzuni hilo ndio nilaloweza kukuahidi”Aliongea Roma na Edna alimwangalia Roma kwa dakika kama moja huku vitu vingi vikipita kwenye kichwa chake , haikueleweka alikuwa akifikiria nini lakini alionekana kuwa na hisia mchanganyiko , hisia za kumlaumu Roma kwanini alimficha juu ya Suzzane , kwanini alimficha mara baada ya kujua ukweli juu ya mama yake lakini wakati huo huo aliamini Roma alikuwa na sababu ya kumficha na huenda hata yeye angekuwa kwenye nafasi yake angeweza kufanya hivyo lakini wakati huo huo akiwa na hisia kwamba mambo yote yameanza kuwa hadharani kwasababu ya uwepo wa Roma kwenye Maisha yake.
Edna alijikuta akitoa machozi na kisha alimsogelea Roma na kumkumbatia na kuanza kulia kwa kwikwi , kitendo ambacho kiliwafanya Bi Wena na Blandina waliokuwa wakiandaa chakula kutoka kuangalia kuna nini kinaendelea.
“Roma kwanini Edna yuko hivi umemfanya nini?”Aliongea Blandina kwa wasiwasi huku akimsogelea Edna na kumshika mikono kwa namna ya upendo na Bi Wema na yeye alimsogelea na kukaa mbele yake , huku upande wa Yezi aliekuwa juu chumbani kwake pia akishuka chini aliona jambo hilo na kumsogelea dada yake wa hiari pia.
Wanafamilia wote walionekana kuwa na wasiwasi na Edna na walitaka majibu, kitendo cha Edna kuona kila mwanafamilia alikuwa na wasiwasi juu yake alijikuta akiinua macho yake na kumwangalia Roma kwa huzuni.
“Edna nisikilize kuna hisia mbaya zinaniambia kilichopo kwenye hii bahasha kinaweza kukutoa machozi, nataka uangalie ukiwa nyumbani na watu wote wanaokupenda wakiwa pembeni yako”Edna alijikuta akikumbuka maneno ya Roma na sasa anaelewa alikuwa akimaanisha nini.
Maisha yake yalikuwa yamebadilika sana , alikuwa na watu wengi waliokuwa wakimpenda tofauti na kipindi cha Maisha yake ya nyuma , sasa alikuwa na familia kubwa ambayo yote inamjali sana.
Edna ilibidi awaelezee kile alichogundua , stori yake iliwafanya kila mmoja kushangazwa na jambo hilo na kuhuzunika kwa wakati mmoja na wote walijikuta wakimfariji.
Roma alipendezwa sana na jambo hilo , swala la kuwa na familia iliokuwa inakujali kwa kila kitu , yalikuwa ni Maisha ya kipekee na alijua nini maana yakuwa na familia Maisha yake ya nyuma alikosa kujua radha halisi ya kuwa na familia na hapo yeye mwenyewe ni kama alikuwa katika hatua za kujifunza nini maana ya familia.
Wakati akiendelea kuwaangalia wanafamilia wake , simu yake iliokuwa kwenye mfuko ilianza kuita mfululizo aliitoa na kuangalia jina la mpigaji na alijikuta akishanga, kwani alikuwa ni rafiki yake Makedoni kutoka Mossad.
Roma alinyanyuka na kisha alipandisha juu kwa ajili ya kuongea na Makedoni , kwani aliamini ikitokea Makedoni akianza kumtafuta yeye basi kuna jambo kubwa ambalo limetokea.
“Your Majesty Pluto were you too bored after not killing anyone for two years , why did you destroy the American Fleet entirely” Ilisikika sauti ya kitetemeshi kutoka kwa Makedoni akimuuliza Roma kwamba amechoshwa na kutoua mtu kwa miaka miwili ndio maana akaharibu meli ya kivita ya Kimarekani.
Roma macho yalimtoka , hakuelewa Makedoni alikuwa akimaanisha nini , Meli ya Kimarekani , mtu yupo Tanzania kwanini aharibu Meli ya kivita ya kimarekani ,
“Makedon , What is this nonsense ? what did I do which even I am not privy to?”Aliuliza Roma kwamba ni ujinga gani Makedoni anaongea juu ya kufanya jambo ambalo hata yeye mwenyewe hakuwa na uelewa nalo.
*******
Ni siku nyingine kabisa alionekana Raisi Jeremy akiwa ndani ya ofisi yake , huku mkononi akiwa ameshikilia picha ndogo , picha ambayo ambayo alikuwa akionekana yeye na mke wake Kizwe wakiwa kwenye pozi la tabasamu huku Kizwe akiwa amevalia gauni la harusi.
Raisi Jeremy picha hio alikuwa akiangalia tokea jana yake usiku alipompa maagizo Linda kwa ajili ya kuandaa mpango wa kumuua Kizwe , mheshimiwa huyu licha ya kufanya maamuzi ya kumuua Kizwe lakini haikumaanisha kwamba hakuwa akiumia ndani kwa ndani, ukweli alikuwa kwenye majonzi makubwa , Kizwe ni mwanamke ambaye alitoka nae mbali sana tokea kabla hata hajawa raisi wa nchi hio ya Rwanda , walipitia nyakati tofauti tofauti , za furaha na zile za huzuni..
Lakini licha ya histora yao, aliamini Kizwe hakuwa na mapenzi kwake tena na kumuweka hai karibu yake ni hatari zaidi, kitendo cha kuweza kuishi kwa kumuigizia kilimfanya hata yeye mwenyewe kumuogapa na kujiuliza ni mangapi Kizwe amemficha , ni mangapi ambayo amefanya pasipo yeye kujua, ndio alikuwa ni mke wake lakini alimuona kama vile amemfahamu juzi na sio miaka mingi iliopita..
Mheshimiwa Jeremy na mke wake Kizwe walibahatika kupata Watoto wawili pekee ,mmoja akiwa ni Desmond ambaye ndio aliekuwa wa kwanza na wa pili alikuwa ni msichana anaefahamika kwa jina la Kyler.
Kyler alikuwa ni marehemu baada ya kupata ajali kwenye mashindano ya magari nchini Marekani wakati alipokuwa masomoni , hivyo unaweza kusema ni Desmond pekee ambaye alibakia kwenye uzao wake ambaye anaweza kumfanya kama mrithi.
“Forgive me Kizwe Mke wangu?”Aliongea Raisi Jeremy kwa huzuni na kisha ile picha ambayo ilikuwa kwenye mikono yake aliichana vipande vinne na kisha akatupia kwenye dastibin.
Muda huo huo mlango ulifunguliwa na akaingia Linda ambaye amevalia suti ya rangi nyeusi iliomkaa vyema mwilini pamoja na shati rangi ya ugoro ndani yake.
“Mheshimiwa hili ni faili la taarifa za mwanaume aliekuwa na Madam”Aliongea Linda na kisha akampatia raisi Jeremy lile faili na kuanza kulisoma na kadri alivyokuwa akiendelea kusoma alijikuta akishangaa.
“Hii taarifa ni sahihi?”
“Ni sahihi mheshimiwa hata ndugu zake wapo hapa nchini , jimbo la Mashariki”Aliongea na kumfanya Jeremy kufikiria kidogo na kisha akaliweka chini.
“Vipi kuhusu maagizo mengine niliokupatia”
“Kila kitu kipo tayari mheshimiwa, tutampa dawa ambayo itamfanya moyo wake kufeli , ni njia nzuri zaidi ambayo itafanya watu wasitilie mashaka kifo chake”Aliongea Linda kwa huzuni kidogo.
“Okey , nitaelekea State Area D , nikishamaliza mazungumzo ,mpango huo utafuatia”
“Mheshimiwa una uhakika na hili?”
“Linda nishafanya maamuzi tayari na hakuna wa kunizuia tena”Aliongea Raisi Jeremy na kisha alisimama kwa ajili ya kuondoka.
State Area D ni moja ya maeneo maarufu ndani ya Rwanda, eneo hili umaarufu wake ulitokana na kwamba yalikuwa makazi maalumu ya raisi Jeremy.
Sasa muda huo wa asubuhi ulinzi ndani ya hili eneo ulikuwa umeimarishwa mno tokea jana usiku , sabababu kubwa ya kuimarishwa kwa ulinzi ndani ya eneo hilo na makachero wa serikali ni kutokana na maagizo ya raisi mwenyewe mara baada ya Kizwe na Lelcha kufikishwa kwa siri sana nchini kwa ndege binafsi ya kijeshi.
Kwenye watu ambao walikuwa kwenye maswali mengi ni Lekcha tokea siku ya jana anapandishwa ndege mpaka kufikishwa nchini Rwanda kwake kila kitu ilikuwa ni mshangao , hakuwa akijua ni kipi kinaendelea na alishindwa kuuliza pia , kwani alitenganishwa na Kizwe.
Sasa baada ya kutolewa kwenye ndege na kuingizwa kwenye gari ya pamoja na walinzi ndio alipata nafasi ya kuongea na Kizwe.
“Hey nini kinaendelea , hawa watu walitotuleta hapa ni wakina nani?”Aliuliza Lekcha.
“Vipi una wasiwasi?”
“Wasiwasi , mimi niwe na wasiwasi nishakuwa kwenye hali hatarishi kuliko hata hii , kwanini niwe na wasiwasi, unafikiri kwanini nina mguu bandia , yote haya ni Maisha magumu niliopitia kama nilikuwa tayari kushindana na wanyama wakali kwanini niogope binadamu wachache wanaotaka kunidhuru?”
“Wanyama ni rahisi kuwafukuza kwa hila , lakini kuhusu binadamu ni Habari nyingine , binadamu ni kiumbe kisichotabilika na hatari Zaidi”Aliongea Kizwe na tabasamu la uchungu mno.
“Hey hupaswi kuwa na huzuni kiasi hiki kama vile familia yako yote imekufa , wewe ndio ulitendwa kwanini unaonekana kama mwenye kuogopa kama vile kuna mtu kakuwekea siraha kwenye kichwa chako?”Aliuliza Lekcha lakini kabla hajajibiwa gari ilisimama ndani ya eneo hilo la Area D na geti lilifunguliwa na kuingizwa ndani.
……..
Saa tano kamili za asubuhi ndio muda ambao raisi Jeremy aliweza kufika ndani ya eneo hili la Area D, safari yake ambayo ilikuwa ya kimya kimya akiwa ametangulizana na Linda pamoja na walinzi wachache.
Baada ya kufika tu aliongozwa na wanajeshi wawili waliokuwa wana siraha za moto kuzunguka upande wa nyuma na kuingia kwenye moja ya jengo kati ya matatu yaliokuwa ndani ya eneo hilo la makazi maalumu ya raisi Jeremy.
Baada ya kuingia ndani ya chumba aliweza kukutana na sura mbili , ya kwanza ikiwa ni ya mke wake Kizwe na ya pili ilikuwa ni ya Lekcha , wote wakiwa wameketi kwenye masofa wakiwa chini ya ulinzi mkali.
“Nafikiri unanichukia kwa staili niliokurudisha nchini Rwanda?”Aliuliza Raisi Jeremy bila salamu mara baada ya kumwangalia Kizwe kwa dakika kadhaa.
“Kitendo cha kuja mpaka hapa kwa ajili ya kukutana na mimi licha ya yote , nadhani napaswa kushukuru”Aliongea Kizwe. Na kumfanya kuvuta pumzi nyingi na kuzishusha.
“Kwanini uliamua kumchokoza Roma?”Aliuliza kwa kifaransa awamu hii.
“Hindsitght is real bitch , you know that ? You might as well say that I shouldn’t have taken action against that little bitch”
“Nyuma ya pazia ndio kuna mbwa halisi na ndio alietoa maagizo na unafahamu hilo? , unaweza pia kusema sikupaswa kuchukua hatua kwa mbwa huyo mdogo”Aliongea kwa namna ya kimafumbo hapo alikuwa akimlenga Edna na alijibu kwa Kingereza.
“Kaa kimya , kwanini unamwita kwa jina la kukera namna hio , unapaswa kufahamu sasa ni mtoto wangu na pia ni mdogo wake Desmond”Aliongea kwa hasira.
“Mtoto wako.. hahaha… hio mimi inanihusu nini? , Edna ni matokeo ya usaliti wako ulionifanyia , kama sio Afande Athumani babu yake kumlinda ningekuwa nishamuua mpaka wakati huu”Aliongea kwa hasira.
“Sijakuleta hata kwa ajili ya ngonjera zako?”Aliongea Raisi Jeremy
“Uko sahihi kabisa , kama nisiposema ninachotaka nani anajua kama naweza kutopata nafasi tena?”
“Ni bora kama ungeendelea kuniigizia kwa Maisha yako yote na kufanya mambo yako kwa umakini, sisi ni wanandoa lakini kudanganyana ingekuwa bora Zaidi kuliko kilichokutokea kama mke wa raisi, Kizwe nilitamani sana siku utakayogundua juu ya Edna ndio mwanzo wetu mpya na kuzika yaliopita , lakini kwa hili linaloendelea najikuta sina chaguo lingine”Aliongea huku uso wake ukibadilika.
“Unaogopa Jeremy ninaweza kukufanyia jambo baya Zaidi kwa kuweza kukuigizia miaka mingi , unaogopa naweza pia kukutoa kwenye nafasi yak kutokana na nguvu yangu ndani ya taifa hili , hivyo unahisi mimi kuwa hai ni hatari Zaidi kwako”
“Unaweza kuwa sahihi , umepotea siku chache tu lakini mabaraza yote yanataka kujua taarifa zako na serikali kwasasa haiko na utulivu , hata kama nikikuua sasa hivi maswali mengi yataibuka”Aliongea Jeremy.
“Kwahio unataka kunifanya nini?”
“Nina mtu tayari ashaandaa sindano ya kimiminika , ambayo itakuwa na uwezo wa kukufanya kama mgonjwa ambaye moyo wake umefeli , nitaelezea uma baada ya kifo chako kama mke wa raisi lakini mwanaharakati wa taifa hili kwamba baada ya kuwa nje ya nchi ulipatwa na tatizo ambalo lilipelekea tatizo la moyo na kutokuonekana kwako hadharani kwa siku hizi chache ni kutokana na kwamba ulikuwa chini ya uangalizi wa madaktari wakijaribu kuokoa afya yako , lakini mwisho wa siku hakuna kilichowezekana kwani hali yako ilikuwa kwenye hatua ya mwisho kabisa”Aliongea Jeremy bila ya kuwa na huzuni kabisa , alionekana ashavunja ndoa yake na kizwe moyoni mwake pekee na hakuna chochote ambacho anajutia.
Kizwe alijikuta akishangazwa kabisa na maneno ya mume wake yakimtoka bila wasiwasi kabisa.
“Sikuweza hata siku moja kufikiria kama itakuja siku mume wangu ndio anaagiza kifo changu , maneno yanakutoka kana kwamba hatukuwahi kupendana hapo kabla , hakika wewe ni raisi wa taifa hili ambaye unapambana kwa maendeleo makubwa Zaidi , Hahahaha… haha,, mbinu yako Jeremy ni nzuri sana na haiwezi kabisa kuacha maswali kama kweli nitakufa kwa shida ya moyo ni mbinu nzuri sana umefikiria”Aliongea na kumfanya Raisi Jeremy kufumba macho kwa hisia na kisha akayafumbua.
“Dawa utakayopewa itakuletea maumivu katika mchakato mzima wa kuathiri moyo wako , nilitamani kufanya kifo chako kisiwe cha maumivu lakini hakuna mbinu mbadala Zaidi ya hii , Kizwe nakuhakikishia baada ya kifo chako mwanao Desmond atarithi kila kitu changu nakuahidi”Aliongea
“Hakika utamrithisha kila kitu , sio kwasababu unampenda bali ni kwasababu hauna mbadala hahahaha.., kuna muda nishawahi kufikiria kama Edna angekuwa mwanaume agekuwa na nafasi sawa na Desmond? , kinachoniumiza siku zote kila nilivyojitahidi kujitoa kwa ajili ya Desmond lakini hukukubali msaada wangu na kunipenda kama mkeo bali mawazo yako yalikuwa kwa mpuuzi Raheli na mtoto wake muda wote”Alifoka lakini Jeremy alishindwa kumjibu alimwacha aongee kwani ndio siku yake ya mwisho ya uhai hata hivyo.
“Kwasababu nitakufa muda wowote naomba nikuambie siri ambayo niliificha kwa miaka mingi , ili kukuonysha ni kwa kiasi gani wewe ni mbumbumbu “
“Siri gani?”
“Miaka iliopita sio kweli kwamba Raheli alikufa kwa kansa ya damu iliompelekea moyo wake kufeli”
“Unataka kumaanisha nini?”Aliongea Jeremy kwa wasiwasi.
“Namaanisha kama unavyofikiria , najua hakuwahi kufikiria lakini daktari Hubery aliekuwa akimhudumia Raheli alikuwa chini yangu na vipimo vyake vya kimatibabu vilivyotolewa hospitalini vyote vilikuwa ni feki, hakuna ugonjwa uliomuua bali nilimuua mimi kwa mikono yangu”Aliongea na kumfanya Raisi Jeremy kuanza kutetemeka kwa hasira.
“Wewe mwanamke ni shetani wa aina gani , hivi unajua ni kwa kiasi ganri Raheli alikuwa akikujali , ni kweli nilikuwa na uhusiano nae lakini hakutaka uhusiano wake na mimi kukuathiri hata kidogo , ndio maana akaamua kuolewa na mwanaume asiekuwa na mapenzi nae , aliishi bila ya kunitafuta na siku zote mimi ndio niliekuwa nikimsumbua ,kwanini hukujali yote hayo na alikuwa rafiki yako?”Aliongea kwa hasira mno , huku macho yake yakiwa mekundu.
“Niite shetani na majina mengine ,lakini siku zote nilikuwa mwenye kupta ninachokitaka”Aliongea bila ya hatia.
“Sawa ulichokifanya kishakwisha kufanyika , ni wakati wa kulipwa kwa makosa yako , jitafakari kwa matendo yako yote kabla ya sumu ya kifo haijaletwa kwako na kuchomwa”Aliongea na kisha alimwangalia Lekcha.
“Kwasababu huyu bwana wako ndio aliekuokoa lakini pia ameweza kusikiliza kila kitu, tulichoongea hapa angalau safari yako haitakuwa ya kinyonge mnaweza kuendelza mapenzi yenu mbele ya safari huko kuzimu”Aliongea na kisha akaondoka kwenye chumba hicho na kuwaacha marehemu watarajiwa.
MWISHO WA SEASON 13
Unafikiri ni nani alieharibu meli ya kivita ya Marekani , je ni Hades kama alivyosema Makedoni.
Yan Buwen na teknolojia yake ya Growth acceleration kama ni kutengeneza Clone ya Roma basi atahitaji angalau miezi minne , swali je amefanikiwa nje ya miezi minne.
Je kifo cha Kizwe ndio mwanzo wa Jeremy kumtangaza Edna kama mtoto wake , unafikiria Desmond atakuwa na hali gani akijua baba yake ndio aliemuua mama yake.
Yajayo yanafurahisha sanaaaaaa…..
OYA ACHA UBAHILI BWANA NI BUKU TATU TU KUJIUNGA GRUPU TUPO SEHEMU YA 460 , NICHEKI NAMBA 0687151346 ONLY WATSAPP
SEE YOU SOON