singanojr
JF-Expert Member
- Sep 24, 2020
- 1,974
- 10,361
- Thread starter
- #2,341
SEHEMU YA 433.
Je ni hofu gani ambayo binadamu anayo , huenda ni swali ambalo kila binadamu atacheza kwenye majibu yanayofanana , hofu ya kifo , hofu ya kufeli , hofu ya kukataliwa na hofu ya nini kinatungojea mbele ya muda.
Lakini je binadamu ashawahi kukaa chini na kujiuliza katika historia ya binadamu hapa duniani ni kitu gani muhimu kilishawahi kutokea ambacho binadamu amesahau au kutokuzingatia.
Athena anakuwa hatari kutokana na kujua mambo mengi , lakini kwanini kati ya vitu vyote akaweka tumaini lake kwenye picha ama mchoro wa mwanamke mwenye tabasamu ambalo linatafsiri kuu ya kishetani , je inamaanisha kwamba anchowazia alishawahi kukiona?.
Kuna uwezekano kila kinachoendelea kwenye ulimwengu wa sasa kishawahi kufanyika hapo kabla na binadamu tupo kwenye marudio.
“Mpaka sasa ili kuhakikisha mwanamke huyu anaendelea kutabasamu nimesimamia ma elfu ya misheni na asilimia tisini na nane ya misheni zote zimefanikiwa, maisha yangu ni kusimamia mafanikio ya misheni zote, Naira unaweza kuniona kichaa na labda siku moja ukataka kunizuia nisiendeelee na kile nilichokianzisha , lakini nikuambia kuna misheni zaidi ya elfu moja zinaendelea duniani kote ambazo dhumuni kubwa ni kuhakikisha tabasamu la huyu mwanamke linaendelea kudumu, hivi ndipo nitakapoendelea kuamini kinachomsubiria binadamu hakijabadilika na hata kama itatokea mtu kunizidi akili hakuna mtu wa kuzuia kile kinachoendelea kwasasa?”Aliongea Athena akiwa kawaida huku macho yote yakiangalia ile picha.
“Nafikiria binadamu tunapaswa kuogopa zaidi kile ambacho hatukioni kuliko kile tunachokiona”Aliongea Naira kwa sauti ndogo na maneno yake yalikuwa na mantiki kubwa.
“Hahaha… upo sahihi binadamu anapaswa kuogopa kile ambacho haoni kuliko anachoona , lakini hio kwangu ni tofauti kwasababu naona kila kitu”Aliongea huku akimwangalia Naira kwa tabasamu lakini Naira alionekana kuwa na mshangao na alijikuta akinyamaza na kuangalia mchoro ule.
Zilipita dakika kama therathini mbele Athena alionekana tena akiwa kwenye chumba ambacho kina teknolojia ya Cryosleep , chumba ambacho mwili wa Seventeen umehifadhiwa.
Athena awamu hii hakuonekana mwenye furaha hata kidogo kwenye macho yake , alionekana kuwa na huzuni na haikueleweka ni kwanini , aliweka mkono wake juu ya kabati la cryo na palepale ukungu uliokuwa umezingira kioo kwa juu uliondoka na sura ya Seventeen ilionekana ikiwa kwenye hali ya usingizi , Athena alionekana kumuangalia Seventeen kwa kumpapasa kana kwamba alikuwa akigusa sura yake.
“What is my biggest fear?”Alijiuliza yeye mwenyewe huku akimwangalia Seventeen akijiuliza kwamba ni ipi hofu yake kubwa.
“Hofu yangu kubwa kwenye maisha yangu ni pale niliposhuhudia ukiutoa uhai wako mwenyewe , kosa langu kubwa ni kuruhusu Roho yako iuche mwili wako, nilihitaji roho yako pamoja na mwili wako lakini ulionekana kuwa mjanja kwa kutoniruhusu kuipata roho yako ,lakini haimaanishi mpango wangu umefeli kadri tabasamu litakapoendelea kudumu , sina cha kuogopa”Aliongea mwenyewe kama kuna aliekuwa akimuongelesha na kumjibu.
Baada ya kukaa kwa muda alitoka kwenye chumba hicho cha kisasa ambacho kimejaa ukungu wa baridi na kurudi alipokuwa amemuacha Naira.
“Una swali la kuuliza kabla sijaondoka?”Aliuliza Athena huku akimwangalia Naira ambaye bado macho yake yalikodolea ile picha.
“Yes nina swali la mwisho?”.
“Uliza”
“Kati ya misheni zote unazofanya ili kuhakikisha tabasamu la huyu mwanamke linadumu , je kuna misheni kubwa tofauti na ya Mpango LADO?”Aliuliza Naira.
“Kama nitaamua kuandaa kumi bora ya misheni ambazo zinaendelea mpaka sasa, mpango LADO ni misheni ambayo inaingia kwenye ishirini bora yenyewe ikichukua nafasi ya kumi na mbili lakini hata hivyo misheni zote kwangu ni muhimu”Aliongea na kumfanya Naira kutoa macho.
“Unamaanisha kuna misheni kumi na moja ambazo zipo zinaendelea kubwa zaidi kuliko ya mpango LADO?”Aliuliza Naira kwa mshangao
“Hahaha… tutaonana ndani ya siku mia moja zijazo huenda nikakueleza moja wapo ya misheni kubwa ambayo inaendele”Aliongea na palepale akapotea kwenye macho ya Naira , huku hata ile picha kwenye ubao ikifutika , Naira alijikuta akishika kichwa na kujibwaga chini kwenye sofa.
Huenda ni zaidi ya dakika au sekunde ndani ya jiji la Cologne huko Ujerumani gari aina ya Porche ilionekana ikisimama kwenye jengo moja refu kwenda hewani lililojengwa kwa usanifu wa kigothia.
Ni sehemu ambayo ina ulinzi mkali sana , ijapokuwa ilikuwa ni usiku lakini eneo lote lilionyesha hali ya kupendeza sana kutokana na wazungu tabia yao ya kutunza mazingira.
Gari ile ilifunguliwa mlango na mwanaume alievalia suti na gloves nyeupe mkononi na kuruhusu aliekuwa kwenye siti ya abiria kutoka, na hapo ndipo mwanamke mrembo sana alitoka kwenye gari hio huku akitoa tabasamu na kuangalia eneo lote.
Lakini muda ule ule kutoka ndani ya jengo hilo alitoka mwanaume alievalia suti lakini ukimwangalia haraka utaona bwana huyu aidha ni mchungaji kutokana na kuvalia ‘Clerical collar’ kwenye shingo au ni Padri , bwana yule wa mwonekano wa kizungu hakuwa mzee sana , alikuwa na mwonekao wa kijana kiasi kwamba ni ngumu kumchukulia kama mtumishi wa mungu kutokana na miondoko yake.
Yule bwana mara baada ya kusogeleana na yule mwanamke alietoka kwenye gari walikumbatiana kwa bashasha.
“My brother”Aliongea yule mwanamke huku akuonyesha hali ya furaha.
“Welcome home my half sister”
“Karibu nyumbani dada yangu”Aliongea kwa lugha ya kijerumani na yule mwanamke mrembo aliitikia kwa lugha hio hio huku wakishikana mikono na kutembea kuingia kwenye jengo hilo takatifu.
Naam mwanamke ambaye ni mrembo akiwa amevalia vali la gauni na kusalimiana na mwanaume anaeonekana kuwa kama mchungaji wa kanisa mwanamke huyu alikuwa ni Athena alievalia mwili wa Clelia Allisanto.
************
Upande mwigine ndani ikulu jijini Dar es salaam , alionekaa mheshmiwa Senga Kweka ndani ya makazi yake na familia ni muda wa saa kumi na moja hivyo iliashiria alishatoka ofisini na sasa alikuwa ameketi eneo la sebuleni akiwa ana angalia runinga kwa kubadilisha badilisha vituo mbali mbali ambavyo vilikuwa vikionyesha habari.
Muda huo huo alifika Damasi mke wake na kukaa pembani yake na kumwangalia mume wake kwa dakika moja kama vile anajaribu kumsoma mawazo , lakini hata hivyo Raisi Senga alionekana kuendelea kubadilisha chaneli na mwishowe aliishia kuweka chaneli ya kitaifa iliokuwa ikionyesha kipindi cha makala maalumu na taarifa hio ilionyesha kumfurahisha Raisi Senga kwani ilikuwa ni tukio la jana yake la ufunguzi wa maabra ya kisasa ndani ya jengo la Bima ya Taifa.
“Sijawahi kusikia kama kulikuwa na mradi wa aina hii unaendelea hapa nchini”Alivunja ukimya mke wa raisi na Raisi Senga alimwangalia mke wake na kisha akatabasamu.
“Huo mradi ni wa miaka mingi na ulianzishwa na Raisi wa Marekani aliekuja kufanya ziara yake hapa nchini kipindi cha mstaafu Kigombola”Aliongea Raisi Senga na kumfanya Damasi kushangaa.
“Unamaanisha kwamba ulikamilika miaka mingi ila ulikuwa haujawekwa wazi?”Aliuliza lakini Raisi Senga hakujibu zaidi ya kuangalia Runinga .
“Kama mradi huu ulikuwa siri ndani ya taifa kwanini ukaamua kuuweka wazi?”
“Unaweza kusema huo mradi ni wa serikali ya Marekani kwani ulifadhiliwa kwa kila kitu ,unakumbuka kipindi unanilalamikia kuhusu mabadiliko ya rafiki yako Rahel?”Aliuliza Raisi Senga na kumfanya Damasi kushangaa.
“Ndio nakumbuka , si jengo hili lilijengwa na kampuni yake mpaka lilipofikia katikati ya kumalizikia ,nakumbuka hakuna siku nilizomuona Raheli kuwa na stress kama kipindi kile , umenifanya nikumbuke mambo mengi yaliopita mume wangu”Aliongea Damasi huku akionyesha hali ya huzuni kidogo.
“Sasa sababu ya kutolewa kwa kampuni ya Vexto kutoendeleza ujenzi wa jengo la Bima ni kwasababu ya huu mradi , kama unakumbuka vizuri utagundua ni siku chache tu baada ya Raisi Barrack Mabo kutembelea Tanzania ndipo kampuni ya Raheli ilipotolewa kwenye mradi na kupewa kampuni ya Innova”Aliongea Raisi Senga na sasa kumfanya Raheli kuelewa.
“Kumbe hiki ndio kilichokuwa kikifanyika mume wangu , sikuwahi kufahamu”
“Huwezi kufahamu kwani kipindi kile nilikuwa waziri tu”Aliongea na kumfanya Damasi kucheka.
“Vipi mbona huulizi ni kwanini ukawa siri huu mradi?”Aliuliza Raisi Senga
“Kila kitu kipo wazi , kilichokuwa kikifanyika humo kinaonekana kilikuwa ni siri”
“Upo sahihi , lakini siku chache nyuma balozi wa Marekani hapa nchini aliponitaka kuuweka mradi huu wazi kuna maswali mengi nilijiuliza sana”
“Mume wangu mbona kama unanitisha , ni mambo gani ulijiuliza?”
“Well! nilijiuliza huenda kilichokuwa kikiendelea ndani ya maabara hii ndio kilichomuua Raheli rafiki yako , swali linalonifanya nijiulize haya ni kwasabau kwenye miasha ya Raheli kuna mambo mengi ambayo yalikuwa yakiendelea, unajua ni kauli gani ya mwisho ambayo Raheli aliniambia?”Aliuliza na kumfanya Damasi kukaa vizuri.
“Alinipa flash disk ambayo nilipaswa kumkabidhi Edna mtoto wake akishaolewa , huku akiniusia nihakikishe uwepo wa flash Diski hio haumfikiia Raisi Jeremy, kwa namna alivyokuwa akiongea ile siku ni kama alikuwa ashakiona kifo chake , lakini la kushangaza zaidi alikuwa ni kama ana uhakika Edna mtoto wake angeolewa na mwanaume mwenye nguvu kubwa”Aliongea Raisi Senga.
“Inashangaza mume wangu lakini ni kweli mume wake Edna sio wa kawaida”Aliongea Damasi.
“Hahaha.. upo sahihi na hili ndio linanifanya nisimpende Roma kama mwanangu , naona sio Denisi kabisa ni kama mtu ambaye hajazaliwa hapa Tanzania , ukiachana na kufanana kwa damu zetu hakuna muunganiko wowoe wa kihisia mimi na Roma, Damasi akili yangu inaniambia kabisa Roma sio Denisi , ijapokuwa baba amenificha mambo mengi lakini nina uhakika kuna jambo kubwa zaidi na yale ninayoyajua lilitokea , huenda ni kosa langu kumchukia Roma na Blandina lakini jambo ambalo nina uhakika Denisi niliemzaa mimi sio Roma , Denisi alishakufa muda tu baada ya kutangazwa kupotea kwa ndege ya M- Airline.”Aliongea kwa hisia kweli na kumfanya Damasi kumsogleea mume wake na kumshika mabega , lakini muda ule ule simu ya Raisi Senga ilianza kuita na kisha akaipokea ,aliongea na simu kwa dakika kadhaa na kisha alionekana akisimama na kuondoka eneo la sebuleni.
………..
Ni saa tatu kamili za usiku alionekana mheshimiwa raisi Senga akiingia ndani ya hoteli moja iliokuwa pembezoni mwa bahari ndani ya jiji la Dar es salaam akiwa amevalia suti.
Tofauti ya siku ya leo na siku zote ndani ya hii hoteli ni kwamba palikuwa pametulia sana , lakini pia hata walinzi aliokuja nao mheshimiwa walikuwa ni wachache sana , ni kama safari ya mheshimiwa ndani ya hoteli hio alitaka ibakie isiri kwani ni itifaki nyingi sana zimezingatiwa.
Mheshimiwa mara baada ya kuingia ndani ya lift ya jengo hilo alienda kutokezea floor ya juu kabisa ambayo inahudumia watu muhimu sana , alitembea na kwenda kusimama kwenye mlango namba XXX kwa dakika kadhaa na mlango ulifunguliwa na kuingia ndani.
Sasa haikueleweka ni jambo gani ambalo mheshimiwa alikuwa akifanya ndani ya chumba hicho , lakini saa sita kamili alionekana kutoka kwenye chumba hicho huku mkononi akiwa ameshikilia kijiboksi kama ambacho Edna alipatiwa na Clelia Allisanto , kiboksi ambacho ndani yake kina ua la langi ya bluu , ua maarufu ambalo linafahamika kwa jina la Ghost orchids.
Sasa mwonekano wa Raisi Senga anaotoka nao na ule alioingia nao ni tofauti sana , muda huo alionekana kuwa mchomvu sana hata kwa tembea yake tu ungeweza kumtambua.
******
Suzzane na Edna walimwangalia Roma aliekuwa akichunguza kijiboksi ambacho alipatiwa na mrembo Clelia Allisanto kwa dakika n kisha akamgeukia Edna akitaka ampe maelezo ya kile kilichotokea.
Na Edna alielezea kila kitu ambacho kimetokea kwanzia namna ambavyo Chriss aliweza kuwasiliana na Suzzane na jinsi walivyolutana na kuongea maswala yanayohusiana na Dr Elvice Daniel.
Sehemu iliomsisimua Roma kwenye maelezo ni mara baada ya Edna kumwambia aliewaokoa ni mwanamke ambaye anafamika kwa jina la Clelia Allisanto, kilichomchanganya zaidi Roma ni pale Edna aliposema kwamba mwanamke huyo alipinga yeye kuwa sio Clelia Allisanto wanaemfahamu , yaani akimaanisha kwamba sio Clelia Allisanto katibu wa umoja wa mataifa.
Roma aliangalia kwa mara ya pili kiboksi ambacho Edna amepatiwa kama zawadi na alijikuta kumbukumbbu zikimpeleka mbali sana, kipindi flani alipokuwa Agent 13 chini ya kundi lake la kininja la New Zero alishawahi kupokea oda za kuua baadhi ya watu mashuhuri kwenye mataifa ya Amerika na Ulaya lakini katika misheni alizowahi kupatiwa alitakiwa kuacha ua hilo la Blue-Ghost Orchid kama ushahidi.
Lakini kubwa zaidi mara baada ya kukutana na Hades wa zamani aliweza kumbiwa akae mbali na watu wanaotumia ua hilo kama nembo ya misheni wanazofanya , Roma hakuwahi kuelewa kuhusu kauli hio mpaka leo hii na ilimshangaza kuona Edna kukutana na mtu ambaye alimwokoa na kisha kumpatia hilo ua.
“Hili linafahamika kwa jina la Blue Orchids au Ghost Orhids ni aina ya ua adimu sana ndani ya dunia ya sasa na hata kuna baadhi ya watu mpaka leo hii wanaamini kwamba uwepo wa haya maua ni hadithi tu , nishawahi kukutana na jamii ya siri duniani ambayo inatumia ua hili kama ishara ya ukaribisho, nembo au kifo”Aliongea Roma na kumfanya Edna kushangaa.
“Nini?”Akiwa kama haamini maneno ya mume wake.
“Ukaribisho wa kuwa mwanachama wa jamii hio, au ishara ya kuuliwa na jamii hio au nembo ya kuwa mwanachama”Aliongea Roma kwa ufupi na Edna alionekana kugopa , hata hivyo yule mwanamke alivyowatokea na kuondoka ilikuwa ikiogofya sana , ni hivyo tu alikuwa amejaaliwa ugumu wa moyo lakini pia kujua mambo mengi yaiokuwa sio ya kawaida , lakini huenda angekuwa mtu wa kawaida angepoteza fahamu kama Suzzae tu.
“Wife usifikirie sana , hili ua nitakusaidia kuliharibu kama hutaki kujiunga na jamii hizo”
“Sipo tayari kujiunga liharibu tu”Aliongea Edna huku akiwa na wasiwasi na kumfanya Roma atabasamu.
“Edna najua unashauku ya kujua mengi ambayo mama yako hajakuambia lakini kwanzia sasa nataka uniachie kazi hio mimi na kama kuna swala lolote au mtu yoyote kuzungumzia kitu chochote kuhusu mama yako unapaswa kuniambia , Kwako Suzzane pia nadhani umeona hatari ya leo sitaki Edna kukutwa na hatari yoyote kwani sitoweza kujisamehe kama jambo baya litamkuta hivyo pia sitoruhusu kumuona mtu anamwingiza mke wangu kwenye hatari”Aliongea akiwa siriasi na Suzzane alitingisha kichwa kumuelewa Roma hata hivyo lilikuwa kosa lake kumuamini Chriss hata kumuingiza Edna matatizoni.
Roma aliweza kuondoka na Edna kurejea nyumbani huku ua lile ambalo Edna alipatiwa kama zawadi aliliharibu, Roma akili yake ilikuwa ikimfikiria mwanamke anaeitwa jina la Clelia Allisanto.
Alikumbuka maneno ya Christen alivyogusia kuhusu katibu wa umoja wa mataifa kuwa mwanamke wakati wanaongea ndani ya hoteli ya Maple , kauli ya Christen ilionekana kuwa na mshaka na hilo ndio lilimjaza shauku sana Roma kuhusu Clelia Allisanto..
“Nitalifuatilia hili kujua ni nini kinaendelea na huyu Clelia ni nani haswa?”Aliwaza Roma kwenye kichwa chake.
“Vipi umeweza kukutana na Clone yako?”Aliuliza Edna na Roma alitingisha kichwa na kumfanya Edna kumwangalia Roma kwa macho ya kutaka maelezo zaidi.
“Ni kweli?”
“Ni kweli nini?”
“Kuna mtu anafanana na wewe kila kitu?”
“Ndio!, Amina atakuhadithia kwa kila kitu , yupo nyumbani kwa Nasra”Aliongea Roma , ukweli Roma hakujisikia vizuri kabisa kuelezea jambo hilo kwani kwake ni kama alihisi ni matusi.
“Nitaelekea China tena”Aliongea Roma.
“Kumtafuta Yan Buwen?”
“Ndio , swala hili nataka nidili nalo moja kwa moja , sipendi kuishi kwa mashaka kwa kufikiria kuna mtu ametengeneza kopi yangu , naamini kuna Clone nyingi zaidi zinazofanana na mimi, nisiposhughulikia hili mapema huenda akafanya mambo ya ajabu makubwa”Aliongea Roma na Edna aliona Roma kaongea pointi , hata hivyo hakuwa na namna ya kumzuia.
“Nilijua yupo hapa hapa Tanzania lakini asubuhi nilipo ona ile habari ya Raisi Senga kuweka ile maabara nilishafahamu Yan Buwen kakimbia”.
“Kumbe uliona? Ndio maana nilivyokuambia naelekea China moja kwa moja ulijua namfuata Yan Buwen , babe unaonekana upo vizuri kichwani”
“Kwahio unasema sipo vizuri kichwani”Aliongea Edna huku akikunja sura .
“Haha.. nimekutania ninachomaanisha nimeoa mwanamke sio mrembo was ura tu , lakini pia mwenye kichwa chepesi cha kuelewa mambo , nadhani napaswa kujivunia”Aliongea na kumfanya Edna kukunja mdomo huku akijiegamiza kwenye kiti cha gari lakini hata hivyo alijisikia vizuri kusifiwa.
Dakika chache tu Roma aliweza kufika nyumbani na Edna ndio aliekuwa wa kwanza kuingia ndani lakini alijikuta akishangaa baada ya kukuta kundi la wanawake wakiongea huku Amina akiwa msemaji mkuu , alijikuta akikunja sura.
Amina mara baada ya kukutana na Roma feki hakutaka jambo hilo limkae moyoni peke yake na ndio maana alifika nyumbani kwa mama yake Roma na kuhadithia kila kitu na kuwafanya watu wote kumsikiliza kwa umakini kama vile hawakuwa wakiamini.
Ilibidi Edna ajiunge na yeye na kuelezea yale ambayo yalimkuta huko Kibaha na mpaka anamaliza kuelezea kila kitu Blandina alijihisi akili yake haifanyi kazi na imesimama kwa muda.
Upande wa Roma hakutaka kukaa sana hapo , alienda hadi kwenye chumba chake na aliweza kumpigia Makedoni simu ili amsaidie kupata taarifa zinazohusiana na Clelia Allisanto lakini ilionekanaalikuwa na taarifa zote , hata hivyo ni jambo ambalo linawezekana kwani mwanamke huyo alikuwa na cheo kikubwa.
Kwa maelezo ya Makedoni Clelia Allisanto ni mzaliwa wa Italy katika mji wa Florence , baba yake Clelia Mzee Allisanto alikuwa ni mwalimu huku mama yake Clellia ni mganga wa maswala ya ngozi(Dematologist).
“Makedoni kwa tukio lililotokea leo kuna hisia zilizoniambia huenda Clelia akawa Athena”Aliongea Roma.
“Mfalme Pluto hilo haliwezekani na kama kweli Clelia Allisanto angekuwa sehemu ya miungu tungeweza kufahamu”
“Lakini kwa maelezo ya mke wangu , Clellia aliekutana na mke wangu anafanana kwa kila kitu na Clelia ambaye ni katibu mkuu wa umoja wa mataifa”Aliongea Roma.
“Mfalme Pluto nashindwa kuamini kabisa , lakini hata hivyo siwezi pia kuyakataa maneno yako moja kwa moja kwani ni wachache sana wanaomfahamu Athena kwa sura yake”Aliongea Makedoni na kumfanya Roma kufikiri.
“Okey nitajaribu kumwangalia huyu Clelia kwenye mtandao nione kama kuna chochote mbacho hakipo sawa , ila utanielezea kama kuna jambo jipya utagundua”Aliongea Roma na kisha aliagana na Makeodn na kukata simu
Roma alijiambia Makedon anaweza kukataa lakini linaweza kuwa jambo linalowezekana kabisa , kwa mfano Christen alikuwa ni Aphrodite lakini dunia inamjua Christen alizaliwa na mkulima wa machungwa huko jimbo la Arizona Marekani, lakini pia kwa mfano Poseidon ambaye alikuwa na vyeo vingi lakini dunia ilikuwa ikimtambua kama mpishi wa kimataifa hivyo ilikuwa jambo la kuwezekana kabisa kwa mwanamke mrembo kama Clelia Allisanto kuwa katibu mkuu wa kimataifa.
Wakati Roma akiwa chumbani kwake aliweza kupokea ujumbe kwenye simu yake na alipoangalia ulikuwa ukitoka kwa Dorisi , ambaye alionyesha uhitaji wa kuonana nae , Roma alimjibu angefika nyumbani kwao.
Muda ambao Dorisi alikuwa akimtafuta Roma ndio walikuwa wakiondoka kurejea kwao kila mmoja , huku Amina akiambatana na Nasra.
Nyumba ya Amina iliharibiwa , hivyo Roma hakuona itakuwa jambo zuri kwa Amina kuendelea kuishi kwenye nyumba hio , ndio maana alimfanya kuishi na Nasra kwa muda huku nyumba yao ikifanyiwa ukarabati.
Saa tano za usiku Roma alichomoka na kwenda nyumbani kwa Dorisi na Rose ili kuona mrembo huyo alikuwa akitaka kumuelezea nini, alifika na aliwakuta wote wakiwa sebuleni wakiangalia runinga.
Na Roma alimbusu mmoja mmoja na kisha akakaa katikati akiungana nao kuangalia Runinga.
“Dorisi ulitaka kuniambia nini?”aliuliza Roma na Dorisi alimwangalia Rose kwa dakika na kisha akamgeukia Roma.
“Nishawahi kukutana na Clelia Allisanto”Aliongea Dorisi na kumfanya Roma kumwangalia Dorisi kwa mshangao..
Unafikiri Yan Buwen atamuweza Roma , unafikiri Clelia allisanto ni Athena mambo mengi sana
itaendelea jumamosi unaweza kujiunga na grupu la watsapp kupata mwendelezo nitafute watsapp 0687151346