SEHEMU YA 512.
Blandina mara baada ya kusikia gari likitoka na wao walitoka haraka akiwa yeye na Bi Wema.
“Roma unafanya nini?, nini kimetokea?”Aliuliza Blandina mara baada ya kumuona Roma akiwa anazunguka zunguka kama kichaa.
“Mama rudi tu ndani?”Aliongea huku kidogo akionyesha amekasirika ila alijitahidi kutoonyesha mbele ya mama yake.
“Nimefanya nini mimi … nisingeingilia?”Aliongea huku akiona kabisa amekosea kile ambacho amefanya na kuona kheri kama angekaa kimya.
“Sio kosa lako kwani haya yote yanatokea kwasababu yangu , hivyo usijilaumu”Aliongea Roma
“Mr Roma nadhani itakuwa vizuri kama ukimfatilia mkeo , kwani muda huu ni hatari akiwa peke yake huko nje”Aliongea Bi Wema ambaye alikuwa na wasiwasi mno.
Roma hata yeye aliona alichoongea Bi Wema ni sahihi , hakupaswa kumwacha Edna akawa peke yake katika mazingira hatarishi ukizingatia alikuwa na maadui wengi na hapo hapo hakutaka kusubiri muda mrefu kwani alirudi ndani na kuchukua ufungo wa gari na kisha akaondoka.
Upande Wa Edna mara baada ya kutoka hapo , hakuwa hata akijua ni wapi aelekee , kwani akili yake haikuwa sawa kabisa.
Alijikuta akiendesha gari umbali mrefu na kuja kuliingiza katika moja ya mgahawa ulioungana na Bar uliopo ndani ya eneo la Tegeta.
Edna aliingia kwenye mgahawa huo huku akikodolewa macho na baadhi ya wanaume waliokuwepo hapo ndani , lakini kwa upande wake yeye hakujali kabisa.
Baada ya kutafuta sehemu ambayo aliona inafaa , aliketi chini na muda uleule na mhudmu hakucheza mbali , kwani alimsogelea Edna akihitaji kuchukua oda yake.
Upande wa Roma alimuona Edna akiingia ndani ya mgahawa huo ambao una bar ndani yake, hakutaka kumzuia Edna kwa muda huo kwani alijua ana hasira na kwa upande wake hakuna chochote ambacho anaweza kufanya , hivyo baada ya kumuona Edna amechagua meza na kukaa na yeye alitafuta meza ya pembeni na kukaa huku akihakikisha Edna hamuoni,
Ijapokuwa hakupendezwa na macho ya wanaume wakola namna ambavyo wanamwangalia mke wake kwa macho ya matamanio lakini alijtahidi kujizuia.
Baada ya muda mchache tu Edna kutoa oda , mhudumu alifika na chupa ya mvinyo ambao una kiwango cha juu cha kilevi na Roma licha ya kwamba alikuwa mbali lakini aliweza kuona jina la mvinyo ule na aliamini Edna kaagiza aina hio ya mvinyo ili kulewa kidogo kupunguza mawazo.
Dakika kumi na tano zilipita , hatimae dakika kumi na tano nyingine zilipita na Edna aifanikisha kumaliza chupa mbili ya mvinyo na kilichomshangaza Roma ni kwamba Edna hakuwa akilewa haraka kama alivyotarajia , alikuwa akimsubiri alewe ili iwe rahisi kumbeba na kumrudisha nyumbani.
Ukweli Roma sio kwamba alihisi kuna kitu kimetokea kati yake na Hanson , lakini kilichomchanganya ni pale Edna alipodanganya kwamba hakukutana na Hanson siku hio wakati ushahidi ulionyesha kabisa walikutana.
Baada ya kama dakika arobaini na tano hatimae kilevi kilimkolea Edna na sasa kuanza kupendeza na kuwafanya wanaume waliokuwa ndani ya eneo hilo wakiburudika waone sasa ni wakati mzuri wa kumsogelea mrembo huyo ili kujaribu kurusha ndoano zao.
Kilichowafanya wasimsogelee mapema ni kutokana na ile hali ya kukosa ujasiri wa kumsogelea kutokana namna alivyoingia , isitoshe ndani ya hilo eneo kuna wale ambao walikuwa wakimfahamu na ambao pia hawakuwa wakimfahamu.
Katika watu ambao hawakuwa wakimfahamu ni mfanyabiashara mmoja wa madini kutoka nje ya nchi , ambaye alikuwa kwenye meza moja na wapambe wake.
Mwanaume yule mwenye kitambi mara baada ya kuona hakuna mwanaume hapo ndani mwenye ujasiri wa kumsogelea mrembo alieingia hapo ndani, alifanya maamuzi ya kusogea wewe ili kuonyesha umwamba wake.
Hata hivyo historia yake na wanawake ilikuwa nzuri sana , hakuwahi kukataliwa na mwanamke mrembo wa aina yoyote, hivyo aliamini kwa mrembo Edna mambo yangekuwa marahisi pia, alikuwa akijiamini kutokana na kwamba alikuwa na hela za kuhonga.
“Mrembo unaonyesha kuwa mpweke leo , je naweza kuungana na wewe?”Mwanaume mwenye kitambi aliongea huku akilegeza sauti kidogo na kumfanya Edna ainue kichwa chake kivivu na kumwangalia.
“Kwenda zako”Aliongea, licha ya kwamba alishaanza kulewa lakini akili yake ilikuwa ikifanya kazi vizuri tu, lakini kwa yule mwanaume wala hakukata tamaa, alishazoea kukutana na changamoto za aina hio kwa warembo mwanzo mwanzo.
“Maisha yana changamoto nyingi, Biashara kutoenda vizuri, mahusiano kuvunjika, na mambo mengi ya kukatisha tamaa ,nina shauku ya kujua upande wako wewe kipi kinakusumbua bibie”.Aliongea lakini Edna kwasababu hakuwa kwenye mudi ya kumjjibu , alijikuta palepale akiona huo ni muda wa kuondoka m hivyo alisimama lakini baada ya kusimama alijihisi kichwa kuwa kizito mno na kushindwa kabisa hata kupiga hatua kwenda mbele na kuanza kulega lega.
“Kuwa makini , ngoja nikusaidie?”Aliongea yule mwanaume akitaka kumshika Edna lakini palepale alijikuta akivutwa na nguvu ya ajabu kwenye shingo na kumfanya adondoke chini na baada ya kugeuka nyuma ndio alikutana na Sura ya mwanaume ambaye hakuwa akimfahamu.
“Kaa mbali, unaetaka kumshika ni mwanamke wangu”Aliongea Roma kibabe na kufanya watu wote macho kuwa upande wao, kwani hawakutgemea tukio lile.
Edna mara baada ya kusikia sauti ya Roma aliinua kichwa chake na kumwangalia na kisha akatoa tabasamu ambalo halikueleweka ni la furaha au la huzuni.
“Nani mwanamke wako , wewe kaka tunafahamiana?”Aliongea huku akijitahidi kutaka kupiga hatua lakini bado alishindwa kufanya hivyo kwani kichwa kilikuwa kinazunguka zunguka.
“Bro kisingizio chako kinachekesha , unajifanyisha kufahamika mbele ya huyu mrembo , ngoja nikwambie katika eneo kama hili fursa ni kuwahi, kama ni mwanamke wako kweli ondoka nae bila kumlazimisha”Aliongea mwanaume mwenye kitambi lakini Roma aliona ampotezee kwani hata yeye alionekana kwanza ashaanza kulewa.
“Kama unashindwa kuhimili kilevi hivi kwanini unalewa , nimekufuata turudi nyumbani t”ongea Roma akimshika Edna.
“Niachie bwana , wewe ni nani kwanza?”Aliongea Edna huku akijitoa kwa Roma na kitendo kile cha Roma kumlazimisha Edna mwanaume mwenye kitambi aliona hio ni nafasi nzuri ya kujichukulia pointi.
“Mwachie bwana , mtu hata hakufahamu wewe unalazimisha?”Aliongea na kumfanya Roma amwangalie asijue hata amfanye nini kuingilia mambo yake , huenda ingekuwa zamani tayari ashamuadhibu lakini kwa kipindi hiko alipenda sana kufikiria kabla ya kutenda.
“Mimi ni mume wake na kama utaendelea kulazimisha mambo ya kijinga nitakuchukulia hatua”
“Mume wake haha.. , unaongea upuuzi gani?”Roma alianza kupandwa na jazba, alielewa hakuna ambaye angemuamini kwa muda huo kwani ukweli siku zote huja mwisho.
Hivyo alimshika yule mwanaume tai na kisha akamsukumia mbele yake na kutua kama zigo,licha ya Roma kutumia nguvu kidogo lakini yule mwanaume mwenye kitambi alirushwa mbali sana na kwenda kuvaa viti ndani ya hilo eneo na kuzua taharki.
Roma hakutaka kuendelea kubaki ndani ya hilo eneo , kwani alimbeba Edna palepale na kuondoka nae.
“You asshole! Damn you Roma ,,nimekuambia niache kabla sijakupasua pasua”Edna alianza kufurukuta huku akiongea kilevi mara aweke kingereza mara kiswahili lakini haikumpa sababu Roma ya kumwacha na hata hakujali pia macho ya watu waliokuwa wakimwangalia.
Roma alikuwa ameegesha gari lake upande wa pili hivyo alichukua muda kulifikia na ile anataka kumwigiza ndani kwenye gari, alianza kumwona akijinyoga.
‘Edna una tatizo gani?”
“Mkojo!”Aliongea na kumfanya Roma kushangazwa na kauli hio na alielewa ni sawa kuongea hivyo kwani alikunywa kiasi kikubwa cha kilevi.
“Tupo mjini hapa na hakuna choo cha kulipia karibu, vumilia tufike nyumbani”
“Mimi siwezi kujizuia tena , umenibana”Aliongea na palepale alikimbia kivivu upande wa pili wa nyuma ya duka na kumfanya Roma amsogelee huko huko.
“Edna huwezi jisaidia hapa , watu wanakuangalia”Aliongea lakini Edna akili yake imetawaliwa na pombe hivyo hakutaka kujali , Roma baada ya kuona hivyo alimshika na kumpeleka sehemu salama zaidi nyuma ya ukuta wa kiwanda na kumwonyesha sehemu nzuri huku yeye akilinda kwa mbele watu wapita njia wasione na alichoweza kusikia ni mlio wa ‘chwaaa..’ na kumfanya kushindwa kujizuia na kuanza kucheka.
Hakuwahi kufikiria kwenye maisha yake angemzibia mwanamke kama hivyo ili ajisaidie tena mwanamke huyo akiwa Edna mke wake , ilikuwa ni picha ya kudmu kwenye akili yake.
Edna baada ya kumaliza alijikuta akianza kutoa kilio kama mtoto huku akiwa ameshikilia ukuta na kumfanya Roma kumwangalia kwa huzuni.
“Edna ni..”
“Hebu angalia hali niliokuwa nayo , nimesingiziwa na mama , mume wangu ananishuku na wote mnanidharau, nimefanya kosa gani mpaka nikafikia hapa, nipo uje usiku huu nikiogopa hata kurudi nyumbani na kuishia kulewa mpaka kujisaidia mtaani….
Tokea tuanze kuishi pamoja nilijihisi kama mwanamke kichaa ambaye hajui nini maana ya kuwa mke , nilijiona mpumbavu nisiekuwa na thamani katika maisha yako , lakini upande mwingine kila siku nakuwa ni mwenye wasiwasi juu yako . najihisi kama vile maisha yangu siku hizi yanaendeshwa na watu wengine.
Huenda hata alichoongea Nasra ni sahihi , mimi sio Edna tena na hata sijifahamu mimi mwenyewe ni nani .. Roma siwezi kuendelea kuishi hivi kama mjinga , mimi ndio Edna……, na kama hali hii ya kukosa utulivu wa moyo itaendelea nitafikia hatua siwezi kuendelea tena”Aliongea na kumfanya Roma ashindwe kabisa kuongea lolote na hata kumsogelea alishindwa, aliishia kumuonea huruma kwani alijua anayopiia yeye ndio msababishaji.
“Hubby…!!”Aliita Edna mara baada ya muda kupita bila ya Roma kuongea lolote.
“Nipo hapa”Aliongea Roma na Edna alifuta machozi na kupiga hatuua moja mbele na kumsogelea Roma.
“Nakuambia sasa kilichotokea , ni kweli nilikutana na Hanson , lakini yeye ndio alienifuata na alikuwa akijaribu kunibembeleza kwa ajili ya ombi lake la ubia wa kibiashara , alikuwa akiomba sana kiasi cha kufikia hatua ya kunishika mkono …, najua una wasiwasi kwasababu tulifahamuna chuoni na ashawahi kunitongoza lakini hayo yote yalikuwa ni ya zamani na sio sasa.
Wewe ndio mwanaume wangu wa kwanza kukupenda kwa moyo wangu wote , najua siwezi kukumiliki mwenyewe lakini nilijiambia naweza kuvumilia wanawake wako wengine , wewe ndio ambaye ulibadilisha mtazamo wangu na kunifanya nianze kufikiria maisha tofauti na biashara, nakupenda sana mpaka nahisi uchizi…
Najua naweza kuonekana mchoyo kwa kutaka uwe wangu peke yangu lakini naamini hayo ni makosa yangu ambayo yalipita na nimeamua kupotezea mawazo yote ambayo yananifanya nisiwe na furaha, lakini kwanini kama kweli unanipenda unashindwa hata kuniamini?”Aliongea huku akianza kulega lega na kutaka kudondoka lakini Roma alimuwahi na kumshikiria.
‘Nakuamini saa ni makosa yangu..I am sorry…”Aliongea Roma lakini palepale Edna aliishia kujilaza kwenye kifua na kuonekana kama mtu ambae yupo kwenye usingizi mzito na kumfanya Roma avute pumzi na kumbeba tena kulisogelea gari lake.
Ni baada ya dakika kama ishirini hatimae Roma aliweza kurudi nyumbani na kupokelewa na Bi Wema pamoja na Blandina ambao bado walikuwa wapo macho wakiwa wanawasubiri.
“Roma kwanini yupo hivyo jamani, yaani mtu kakosea anakimbilia kulewa”Aliongea Blandina mara baada ya kumuona Edna akiwa amelewa.
“Mama hebu acha kumsema , kashachoka na mambo ya kusingiziwa na hana sehemu yoyote ya kutolea hasira ndio maana kakimbia kulewa , unaonaje asubuhi ukamwomba msamaha yaishe , najua sio vizuri kufanya hivyo lakini pia umekosea”Aliongea Roma na kumfanya Blandina kushangaa.
“Siwezi kufanya hivyo,kwani hata mimi nishawahi kuwa katika rika lake najua sisi wanawake ni wapi tunakosea na isitoshe nia yangu haikuwa mbaya , kama asingekutana na yule mwaname sidhani yote haya yangekuwa yametokea , naweza nikawa nimekosea kweli lakini nikimwomba msahama ni kujishushia heshima kama mama yako”
“Mama , tupo karne ya ishirini na moja sasa na sio tatizo mzazi kuomba msamaha pale anapomkosea mtoto”
“Sawa nitajirahidi kumuomba msamaha lakini nitafanya hivyo sio kwa ajili yake bali kwa ajili yako , mimi sio mzee kihivyo kushindwa kuelewa wapi nimekosea”Aliongea Blandina huku akionyesha hapendezwi na namna Roma anavyomkingia kifua mke wake , alikuwa ni kama anataka Roma ndio awe upande wake , lakini kwa Roma mke wake ndio kila kitu kwani ndio mtu anaekwenda kuishi nae maisha yake yote.
“Blandina ni sawa na wew alichoongea , kama mzazi huwezi kushinda kila mazungumzo, najua unahisi upo sahihi juu ya hili lakini kwa ajili ya familia ni kheri ukaamua kujishusha tu ili amani irudi”Alishauri Bi Wema na kumfanya Blandina akubalikwa kichwa.
“Huenda ndio maana tamthilia za siku hizi lazima ziwe na mama mkwe kigeugeu , kama sijaelimika huenda ningekuwa kama watu wa kwenye tamthilia kwa kumtaka mwanangu kuwa upande wangu tofuati na upande wa mke wake”aliongea Blandina na kumfanya Bi Wema kucheka.
Roma mara baada ya kumwingiza Edna kwenye chumba chake , aligundua Lanlan hakuwepo hapo ndani na alijua huenda kalala na Qiang xi.
Baada ya kumuweka kitandani alipunguza nguo alizovaa na kisha akamfunika ili alale , Edna muda huo alionekana hakuwa akijua kabisa kinachoendelea zaidi ya kutafuna tafuna na alipowekwa kwenye kitanda ni kama ambeambiwa ndio alale.
Roma hakuondoka baada ya kumuweka Edna kitandani , alionekana kuongea maneno mengi kwa hisia sana kwa zaidi ya dakika kama tano na kisha alimwinamia Edna na kumbusu usoni na kisha akazima taa na kuondoka.
Ilikuwa ni siku nyingine Roma akiwa usingizini , mlango uligongwa kwa nguvu mno kiasi kwamba Roma ilimshangaza kwani hakuwahi kugongewa kwa nguvu kiasi hicho na isitoshe mlango ulikuwa wazi, ilikuwa ni kama anegona ana hasira.
Muda uleule mlango ulifunguliwa na baada ya kuangalia aliekuwa akigonga aligundua alikuwa ni Lanlan.
“Lanlan mlango upo wazi kwanini unagonga kwa nguvu?”
“Mama ameniambia nigonge mlango kabla ya kuingia”
“Kwahio hajakufundisha kugonga taratibu?”
“Hapana?”Alijibu na kumfanya Roma kumwangalia kwa kumchunguza.
“Bad Dady, Bibi kasema uamke, kwani hatuwezi kupata kifungua kinywa mpaka uwepo na Lanlan ananjaa sana”Aliongea Lanlan na kisha kwa hasira alisogelea shuka ambalo Roma amejifunika na kulivuta kwa nguvu na kumfanya Roma abakie kifua wazi na mpaka hapo alijuwa kwanini Lanlan alikuwa akigonga kwa nguvu.
“Lanlan nipe shuka langu?”Aliongea Roma huku akijaribu kujifunika na mto.
“Bad Daddy unakifua kidogo kuliko cha mama”Aliongea Lanlan kwa kingereza na kisha alikimbia kutoka nje na Roma alicheka na kisha akavuta tena shuka kulala kidogo , lakini muda ule ule na mlango ulifunguliwa na Edna ambaye alionekana kushikilia nguo mkononi zilizokunjwa.
Alimwangalia Roma alielala kwenye kitanda na kisha alienda moja kwa moja mpaka kwenye makabati na kuanza kupanga nguo katika sehemu husika , zilionekana kuwa nguo za Roma ambazo zimetoka kusafishwa na kukaushwa na mashine.
“Wife bado umekasirika?”
“Ndio bado nimekasirika , lakini licha ya yote bado wewe ni mume wangu”Aliongea kwa sauti ndogo na kumfanya Roma kushangazwa na kuguswa na kauli yake na palepale alitoka kama mshale kitandani na kumsogelea kisha akampakua na kwenda kumlaza kitandani.
“Nilijua tu mke wangu ushanisamehe tokea jana ile ile”Aliongea Roma huku akionyesha furaha na Edna alimwangalia na kuanza kuona aibu kwani kuna kitu kizito kilichokuwa kikimgusa upande wa chini mapajani.
Ukweli ni kwamba Edna wala hakuwa amelewa kiasi cha kutojitambua , wakati Roma anamrudisha nyumbani alikuwa akisikia kila kitu lakini alijifanyisha kuwa katika hali ya ulevi wa kupindukia.
Uwezo wake wa kijini ambao alianza kujifunza ulikuwa umemsaidia sana kuweza kuhimili kiasi kikubwa cha pombe , hivyo hata wakati Roma anamlanza kitandani na kuanza kuongea ngonjera zake za kimapenzi aliweza kumsikia na maneno yake yalimgusa mno na ndio maana hata alivyoamka alikuwa na mudi nzuri.
Baada ya kama nusu saa waliweza kushuka sebuleni wakiwa pamoja kwa ajili ya kifungua kinywa , Blandina licha ya kwamba Edna alionekana kuwa katika mudi nzuri na kuonyesha kupatana na Roma lakini bado kwenye moyo wake alikuwa na kiwingu , lakini alijitahidi kutoonyesha tofauti yoyote.
Bi Wema baada ya kuona kuna ukimya mkubwa kwenye meza ilibidi awwashe Tv ili kuchangamsha hali.
Wakati wakiendelea kupata kifungua kinywa Roma alikuwa ndio wa kwanza kuangalia moja wapo ya taarifa ya habari iliokuwa ikitolewa na mojawapo ya chaneli maarufu nchini.
Ilikuwa ni habari inayohusiana na kifo cha Hanson , habari hio haikumshangaza Roma tu lakini hata Blandina ambaye aliweza kumjua siku ya jana Hanson , sura yake iliokuwa ikionyeshwa kweny runinga ilimfanya aifahamu palepale, upande wa Edna hakushitushwa kabisa na habari hio na aliishia kutoa tabasamu la kebehi ni kama mtu alietangazwa kufariki alikuwa adui yake.
Kwa maelezo ya taarifa hio inasemekana kwamba Hanson alikutwa hotelini akiwa amekufa huku uchunguzi ukionyesha kwamba amekunywa sumu, taarifa za awali zilionyesha huenda kilichomuua mtoto wa tajiri huyo kutoka Norway ni msongo wa mawazo ambao umesababishwa na kile kilichosemwa ni kushindwa kufikia makubaliano na kampuni ya Vexto.
Katika maelezo ya waandishi wa habari wanasema Hanson alifika nchini akiwakilisha kampni ya Hanson enterprises na BMW ukanda wa Afrika na alipaswa kuingia kwenye makubaliano ya kibiashara na kampuni ya Vexto , makubaliambayo hayakufanikiwa.
Sasa taarifa ya pili yake ndio ilimshngaza sana Roma na kumfanya amwangalie Edna kwa mshangao na sio yeye tu hata Blandina pia alimwangalia Edna huku wote wakionekana kuhitaji maelezo.
SEHEMU YA 513.
Ilikuwa ngumu sana kwa mwanamke mfanyabiashara kama Edna kuacha mkataba wa kibiashara mnono na kampunni kubwa duniani ya BMW , Edna mshindani wake mkuu kibiashara ilikuwa ni kampuni ya Maple Group ambao walikuwa na mkataba wakibiashara na kampuni ya Toyota, hivyo Edna ili kuwa katika levo sawa na kampuni ya Maple upande wa biashara za magari alihitaji kampuni ya BMW.
Siku chache zilizopita kipindi Edna aliporudi kutoka Mediterranian aliweza kupokea proposal’s mbili za kibiashara kutoka kwa kampuni ya Hanson enterprises yenye makao yake makuu jijini Oslo Norway , pendekezo la kwanza liliwakilishwa kwake na Hanson kupitia kampuni yao Hanson Enteprises na pendekezo la pili lilitumwa kwake kwa kupitia barua pepe na mkurugenzi msaidizi wa kampuni ya Hanson afahamikae kwa jina la Asam Scott Hanson.
Mapendekezo yote mawili yalikuwa yakifanana , kilichotofautiana ni kwamba wawasilishaji walikuwa ni watu wawili tofauti , yaani kulikuwa na Hanson halafu kuna mwingine aliejitambulisha kama mkuruguezi msaidizi wa kampuni ya Hanson enterprises afahamike kwa jina la Asam Hanson.
Ikumbukwe Hanson Enterprises yenye makao yake makuu nchini Norway ndio walikuwa wanatakiwa kuwa kama daraja la biashara kati ya BMW na kampuni ya Vexto ili kukuza soko la magari yao katika soko la Afrika mashariki na kati kwa ujumla., haikueleweka sababu kwanini BWM waliichagua moja kwa moja kampuni ya Vexto iliopo nchini Tanzania lakini masharti ambayo kampuni ya Hanson ilipewa ni kuhakikisha kampuni ya Vexto inahusishwa katika ubia kwa lazima.
Edna mara baada ya kupata mapendekezo mawili ya kibiashara kwa wakati mmoja ilimfanya kuingiwa na wasiwasi kidogo na wasiwasi wake ndio uliompelekea kuwapa kazi Athena kumfatilia Asam Hanson ni nani na kwanini na yeye akamtumia ombili la kibiashara wakati kuna mwakilishi tayari amekwisha kutumwa.
Hanson ilikuwa ni kampuni kubwa hivyo taarifa hazikuwa ngumu kupatikana , Athena waliweza kugundua Asam ni kaka yake Hanson(Half brother), na ilionyesha Hanson ndio alipewa kazi ya kusimamia mkataba wa kibishara na kampuni ya Vexto nchini Tanzania kupimwa uwezo wake lakini kaka yake alionyesha kumzunguka mdogo wake na kuanza mchakato wa kukamilisha dili yeye mwenyewe na kampuni ya Vexto.
Edna mara baada ya kupata taarifa aliona inaleta mantiki kwani Asam katika mkataba wake aliweka kiasi kikubwa cha faida ambacho kampuni ya Vexti ugeweza kupata kama tu itasaini mkataba wa ubia na yeye , ilikuwa ni kama Asam alikuwa akijua ni kiasi gani ambacho Hanson angeweka katika mkataba , hivyo alichokifanya ni kuoneza namba tu na kumpiku Hanson.
Lakini vilevile Edna alishindwa kuelewa kwanini kampuni kubwa ya Hanson ikang’ang’ania kampni yake nchini Tanzania kutaka kufanya nae kibiashara lakini hakutaka kuuliza swali kama hilo kwani ni kama angeishusha thamani ya kampuni yake hivyo alijiambia tu anapaswa kuwa makini.
Mwanzoni Edna alitaka kusaini mkataba ulioletwa na Hanson kwake na kuachana na wa kaka yake kutokana na kwamba walisoma pamoja,lakini ugomvi wa Hanson na Roma lakini pia yeye mwenyewe kuwa na wasiwasi na nia halisi ya Hanson ndio iliomsukuma kuchagua kusaini mkataba wa kibiashara uliotumwa na Asam na isitoshe hakuona ni hasara kufanya hivyo kwani mkataba wa Asam ulioonyesha kuwa na faida kubwa kuliko iliowekwa katika mkataba wa Hanson.
Hivyo wakati siku ya jana kikao kinaendelea ndani ya kampuni ya Vexto, upande wa Nairobi alikuwep Benadetha ambaye alienda kumwakilisha Edna katika maongezi ya kibiashara na Asam, ambaye aligoma kufika nchini Tanzania kutokana na sababu hakutaka kuzitaja, Edna alielewa ndio maana akamwagiza Benadetha kwenda kusimamia.
Hivyo polisi wanaamini kifo cha Hanson ni kwasababu ya msongo wa mawazo baada ya kugundua kwamba mkataba ambao alipaswa kuufanikisha yeye Kaka yake Asam tayari ashaufanikisha na rasmi kampuni ya Vexto ikawa na ubia wa kibiashara na kampuni ya BMW na yeye kukosa sifa kutokana na kwamba kazi hio ilikuwa kama majaribio kwake.
Sasa haikueleweka kulikuwa na sababu nyingine ipi ambayo moja kw moja ilipelekea Hanson kujiua kwa kutumia sumu , kwani kusema alikufa kwasababu ya mkataba ni jambo lenye ukakasi kidogo na hili huenda ndio linaelezea ni kwanini Hanson alikuwa akimbembeleza sana Edna kumkubalia kusaini nae ubia huo wa biashara.
Hivyo hata Nasra ambaye ni CEO msaidizi hakuwa akifahamu mpango wa Edna ni upi na alijua kabisa Edna alikuwa ameacha dili hilo nono kwasababu ya Roma , lakini ukweli Edna hakuwa na mpango wa kuachana na dili hilo kwani alikuwa ni mfanyabiashara na siku zote mfanyabiasha haachi fursa impite kirahisi bila sababu ya msingi na Edna amelelewa katika misingi ya kibiashara.
“Mwanzoni nilitaka kabisa kuachana na Projekti hio na kumfanya Hanson kwenda kutafuta kampuni nyingine , lakini alinikasirisha ndio maana nikaamua kumkomesha , lakini sikudhania kama anaweza kuchukua maauzi ya kujua yeye mwenyewe”Aliongea Edna baada kuelezea kile kilichotokea.
Mpaka Edna anamaliza kuelezea mlolongo mzima wa tukio la siku ya jana ndipo sasa Blandina anaelewa ni kweli alikosea kwa kumfikiria vibaya.
“Jana baada ya kikao kuisha sikutaka Hanson anikute ofisini na kuanza kunibembeleza ndio maana nikatoka bila hata ya kumwambia Recho ni wpai naenda , lakini nilishangaa aliweza kujua mahali nilipo kwa urahisi na akili yangu iliniambia moja kwa moja ndani ya kampuni kuna watu aliowapandikiza kufatilia nyendo zangu”Aliongea Edna na kumfanya Roma kuelewa , lakini kwa wakati mmoja aliona kabisa uhai wa Hanson ulikuwa mikononi mwa Edna na muda na saa aliokubali kusaini mkataba na kaka yake alikuwa ndio anammaliza, lakini kwakuwa yeye pia hakuwa mtu wa huruma sana hakuona shida ukatili wa Edna.
“Kama ungesema siku ya jana juu ya mpango wako , mama asingekushuku”Aliongea Roma.
“Ni kweli ungeniambia kila kitu ningekuelewa na nisingekufikiria vibaya , kwanini ukaamua kuficha kila kitu?”
“Haikuwa mpango wangu kumsaliti Hanson na kuamua kuchagua pendekezo aliloleta kaka yake na kama habari hii isingetokea kwenye vyombo vya habari nisingeenda nayo kaburini”Aliongea Edna.
Upande wa Roma hakutaka kushangaa zaidi kwani haikuwa mara ya kwanza kwa Edna kufanya hivyo tokea akutane nae, alikuwa ni mtu wakucheza na akili za watu sana.
Ilikuwa siku ya sikukuu na siku pia ya kumbukumbu ya kifo cha bibi yake Edna hivyo hakuna ambaye alienda kazini siku hio, hata Roma alibakia nyumbani na muda wa mchana ndio alimfuata Rufi ili kuja kujuamuika na familia yake kama makubaliano yalivyokuwa.
Rufi haikuwa mara yake ya kwanza kufika nyumbani kwa Roma , lakini likuwa ni mara yake ya kwanza kukutana na Blandina mama yake Roma.
Baada ya Roma kumfikisha nyumbani alipokelewa kwa ukarimu mkubwa na hata Edna ambaye alikuwa na wasiwasi na Rufi kuingia katika mahusiano na Roma alimchangamkia ili ajisikie yupo nyumbani
Ilikuwa rahisi zaidi kwa Rufi kuzoena na Lanlan , huenda ni kutokana na wote kuongea lugha moja, hivyo baada ya kufika hapo ndani walianza kucheza m pamoja jambo ambalo lilimfurahisha Roma kwani alimuona Lanlan akiwa kwenye furaha ya kiwango cha juu.
Baada ya chakula kuiva wote walijumuika mezani na kuanza kupata chakula cha pamoja na Rufi alipendezwa sana na namna maisha yalivyokuwa hapo ndani , ilikuwa mara yake ya kwanza kushuhudia familia inaishi kwa upendo namna hio, huenda ni kwasababu hakuwahi kuwa na familia ambayo inamjali na kumpenda.
******
Ni baada ya chakula wakati wanafamilia hao wakiwa wameketi eneo la sebuleni , Blandina alitumia nafasi hio kumuuliza maswali kuhusu Rufi ili kumfahamu zaidi , maana kitendo chake cha kujtolea kumsaidia Roma ilimfanya amuone wa kipekee, lakini kilichomshangaza Blandina ni mara baada ya kuona Rufi amechanganya rangi yaani akiwa mchanganyiko wa mafrika na mchina.
Bi Wema alikuwa amekaa sebuleni na yeye macho yake yote yalikuwa kwenye runginga kwani hakuwa akielewa lugha ya kingereza vizuri hivyo hakuelewa kile kilichokuwa kikiongelewa.
Upande wa Blandina alishangazwa na stori ya maisha ya Rufi kwanzia alipokuwa mdogo mpaka kufikia umri huo , historia yake ilionyesha kuwa ya maumivu na aijikuta akimwonea huruma na kumpa pole kwa yale aliopiitia .
“Umesema mama mzazi wako ametokea Afrika mashariki?”Aliuliza Blandina na Riufi alitingisha kichwa kukubali.
“Ingeleta faraja kama ungeweza kukutana na mama yako mara baada ya kutoka kwenye hayo mateso, una njia yoyote ambayo inaweza kusaidia kuweza kumpata mama yako mzazi, niikimanisha picha au mahali alipoishi?”
“Kuhusu mama sina taarifa zozote kuhusu yeye, lakini mlezi wangu aliniambia njia pekee ya mama yangu mzazi kunitambua ni alama niliozaliwa nayo”Aliongea Rufi na kumfanya hata Edna kushangazwa na kauli hio.
“Alama gani?”aliuliza Blandina kwa shauku na palepale Rufi alivua blazia yake upande mmoja na kuacha bega lake la kushoto kuwa wazi na hapo ndipo walipoweza kuona alama ambavo Rufi anazungumzia.
Ilikuwa ni kama tatoo ya rangi nyeusi katika bega la Rufi , alikuwa ni mweupe mwili mzima lakini hio sehemu ya bega ilikuwa nyeusi mno huku ikiwa imekaa kama michirizi ya ngozi nyeusi.
Bi Wema baada ya kuona tukio lile na kumwangalia Rufi , alijikuta macho yakimtoka na kusimama kiwasiwasi na kusogea karibu zaidi na alipokaa , kiendo kile kilimfanya Edna na Roma kumwangalia Bi Wema kwa shauku.
Kitendo cha Rufi kuzaliwa na mama mwafrika na baba mchina ni stori ambayo ilikuwa ikifanana kwa kiasi kikubwa na ya Bi Eema na ndio maana walitaka kumpa nafasi ya kuweza kumwangalia Rufi kama hana uhusiano wowote na yeye.
‘Hii Alama..!!!!’Bi Wema alijikuta akimwangalia Rufi kwa namba isioelezeka na kuanza kutetemeka.
“Wema unaifaham hii alama?”Aliuliza Blandina baada ya kumuona Bi Wema akiwa amebung’aa.
“Mtoto wangu nakumbuka kabisa alikuwa na alama ya kuzaliwa kama hii eneo hili hili”Aliongea na kuwafanya wote kuanza kujawa na msisimko.
Upande wa Rufi hakuelewa alichoongea Bi wema na alishangazwa na mshituko wake na aliishia kumwangalia Roma ili amtafsirie kile ambacho kinaendelea na ilibidi afanye hivyo na Rufi alishangazwa.
“Bi Wema si una picha ya baba mtoto wako?”Aliuliza Edna na palepale Bi Wema alikumbuka jambo hilo na kutoka nduki kupandisha juu kwa ajili ya kuleta picha hio na ndani ya sekunde chache tu alirudi akiwa na picha moja iliochakaa kutokana na kuishi muda mrefu , lakini sura ya mtu aliekuwa kwenye picha ilikuwa ikionekana vyema.
“Rufi umeweza kumtambua mtu wa kwenye hio picha?”Aliuliza Edna na Rufi aliishia kutingisha kichwa huku machozi yakianza kujitengeneza kwenye mboni za macho yake.
“Huyu ni baba yangu”
Aliongea na Bi wema aliweza kusikikia ile kauli na kumfanya amwangalie Rufi akiwa kama haamini, haikuwa kwake tu hata kwa Blandina na wengine wote walishangazwa kuona Rufi ameweza kumpata mama yake kiahisi sana.
Ilikuwa ni jambo ambalo lilileta msisimko wa mshangao , lakini pia na furaha ndani yake , nani angeweza kugundua kwamba Rufi mama yake alikuwa ni Bi Wema , hata Roma mwenyewe alishangaa.
Bi Wema alijikuta akianza kutoa kilio mara baada ya kugundua Rufi alikuwa ni mtoto wake , mateso alioshi nayo muda mrefu pasipo ya kumuona mtoto wae yalimuumiza sana na muda huo furaha yake ilikuwa ya juu sana kiasi kwamba alijihisi ni kama yupo ndotoni na muda wowote angeamka lakini kila kitu kilikuwa halisia , aliekuwa mbele yake ni mtoto wake ambaye alimsurubiria kwa muda mrefu sana kukutana nae.
Baada ya kama nusu saa kupita ndio muda ambao sasa kila mmoja alitulia na ilibidi Bi Wema achukuea nafasi ya kumwelezea Rufi kuhusu stori ya maisha yake na baba yake namna walivyokutana mpaka wakatokea kupata mtoto na namna ambavyo aliishia mara baada ya kumpoteza mtoto wake.
Stori yake ilimhuzunisha sana Rufi na kumuona baba yake alikuwa moja ya watu wakatili sana kuwahi kutokea.
Alimtenganisha na mama yake lakini baada ya kumpeleka katika miliki za kijini na kwenyewe hakuonyesha kumjali na kumchukulia kama kifaa cha majaribio.
Upande wa Bi Wema alishangazwa kusikia kwamba mwanaume wa kichina ambaye alitokea kumpenda hakuwa mtu wa kawaida , bali ni kutoka katika jamii za kijini.
Blandina alijikuta akimwangalia Roma na kumuona kama amefanya jambo la maana kumkutanisha Rufi na mama yake , mpaka hapo waliamini Bi Wema sasa angeishi kwa furaha na sio mwenye mawazo tena na kuendelea kuwa mwanamke mwenye upweke.
“Nadhani naweza kufa sasa kwa amani”Aliongea Bi Wema kwa furaha.
“Mama usiongee hivyo”Aliongea Rufi kana kwamba alielewa kauli ya mama yake na kumfanya Bi Wema kuanza kutoa kilio tena cha furaha kuitwa mama.
Edna na yeye alimpongeza Bi Wema kwa kumpata mtoto wake na pia akampongeza Rufi kwa kumpata mama yake , huenda yale maisha ya upweke ambayo Rufi aliishi nayo yanakwenda kuisha.
Rufi alifurahi sana na kuona kama asingemsogelea Roma siku ile kule marekani huenda asingeweza kumuona mama yake na maisha yake kuchukua sura mpya..
Baada ya maongezi yaliodumu muda mrefu kuisha Roma alimchukua Rufi na Bi Wema kuwasikikiza kwenda Kerege kwenye nyumba ya Bi Wema ili akamuonyeshe namna ambavyo aliishi kwa kukadiria umri wake kwa kununua viatu kila inapofikia siku yake ya kuzaliwa.
Nama ikawa ndio namna ambavyo Bi Wema aliweza kukutana na mtoto wake wa kike aliempoteza kwa zaidi ya miaka ishirini, Bi Wema alijiambia kwa siku ambazo ataishi atahakikisha anafidia kila kitu ambacho Rufi alikosa katika makuzi yake.
“Mr Roma sijui namna gani nikushukuru , umekuja kwenye hii familia na ukamsaidia miss Edna na sasa umenisaidia na mimi kuweza kukutana na mtoto wangu”Aliongea Bi Wema mara baada ya kufika ndani ya jumba lake eneo la kerege.
“Hehe.. Bi Wema huna haja ya kuwa hivyo kwani muda si mrefu unakwendada kuwa mama mkwe wangu , ijapokuwa sisi ni familia lakini uwepo wa Rufi utatufanya kuwa ndugu zaidi”Aliongea Roma bila aibu na kumfanya Bi Wema kumwangalia Rufi na kutabasamu.
Edna alipendekeza Rufi kuishi nyumba moja , lakini kutokana na uhusiano uliokuwepo baina yake na Roma Bi Wema aligoma.
Ilikuwa ni sahihi Edna kumjali Rufi mpaka hatua hio kwani alikuwa ni mtoto wa Bi wema na yeye Bi Wema alikuwa kama mzazi kwake , lakini isingeleta picha nzuri na Edna mwisho wa siku asingejisikia vizuri.
Hivyo Bi Wema na yeye akawa na mipango ya aina mbili , wa kwanza ni aidha Rufi akaishi Kerege kwenye nyumba ya mama yake au Bi Wema anunnue nyumba nyingine karibu na mtaa huo ili iwe rahisi kuhudumia familia zote mbili na mpango uliokubalika na Bi Wema kununua nyumba eneo hilo hilo la karibu..
Ijapokuwa Edna alitaka kunnua yeye kwa hela zake lakini Bi Wema aligoma na kutaka kununua na hela zake kabisa na jambo hilo lilimshangaza Blandina mama yake Roma , kwani ilionyesha Bi Wema alikuwa na mapesa mengi na hata Qiang Xi aliekuwa kama mfanyakazi tu alishangazwa.
“Wema kumbe na wewe ni tajiri usiependa makuu na hatuambiani?”Aliongea Blandina kiutani na kumfanya Bi Wema kucheka.
“Bi Wema mshahara wake ni mkubwa kuliko hata wa kwangu?”
“Haiwezekani?”Aliongea Qiang xi na kumfanya Edna aelezee namna ambavyo Bi Wema analipwa.
Kwa maelezo ya Edna Bi Wema alikuwa akilipwa kwa mwaka sio kwa mwezi na hela zake hazikuingia moja kwa moja kwenye akaunti yake ili asikatwe kodi bali zilikuwa zikiingia kwenye hadhina ya kampuni, ilikuwa ni rahisi kusema kila mshahara wake wote alikuwa akiwekeza katika kampuni ya Vexto.
“Kimahesabu Bi Wema hela zake mpaka sasa naweza kusema sio chini ya bilioni therathini za kitanzania”Aliongea Edna na kufawafanya watu wote kushangazwa na taarifa hio, Bilioni ishirini sio hela ndogo kwa mtu anaefanya kazi za ndani, lakini ilieleweka , Edna hakuwa na mzazi wa kumlea hivyo wazazi wake walihakikisha Bi Wema analipwa pesa nyingi ili kumhudumia Edna vizuri.
********
Baada ya siku mbili kupita Bi Wema aliweza kupata nyumba ya bilioni moja na nusu eneo la ununnio na kuinunua na rasmi ikawa anaishi yeye na mtoto wake Rufi na Edna ndio alisimamia utaratibu wa Rufi kuthibtishwa kuwa raia wa Tanzania kwa kuzaliwa
Bi Wema sasa hakulala tena nyumbani kwa Roma bali alifika nyumbani hapo kwa ajili ya majukumu ya kazi na kila jioni angerudi nyumbani kwa mtoto wake Rufi na kulala pamoja.
Hata ule uzee ambao ulikuwa ukianza kumnnyemelea ulianza kumpotea na sasa alionekana kuwa na furaha.
***************
Siku nazo hazikuganda kabisa na zilienda kwa kasi , katika kipindi chote hicho Roma aliendelea kuwafuatilia wanawake wake kwa ukaribu kabisa juu ya kuangalia mafunzo yao kila giza linapoingia na kitendo cha Lanlan kugangania kulala na mama yake aliona ni jambo zuri mno kwani lilimpunguzia migogoro.
Na kutumia vile vidonge ambacho alitengeneza , hakika mafanikio yalikuwa makubwa mno na hata Neema ambaye uwezo wake ulikuwa wa taratibu sana aliweza kufika kwa haraka katika levo ya nusu mzunguko.
Mage na Rose ndio ambao waliweza kupanda levo kwa haraka mno na kuingia mwishoni mwa levo ya mzunguko kamili na Roma alikuwa akihesabu tu siku mpaka wakatapo ingia katika levo ya Nafsi, yalikuwa ni mafanikio ambayo yalimfurahisha sana.
Upande wa Edna licha ya kwamba alikuwa ndio kwanza anaanza kuingia levo ya nusu mzunguko lakini bado mwili wake haukuwa na mabadiliko makubwa sana , kilichomsaidia sana ni kwamba mafunzo hayo yalimpunguzia uchomvu na alikuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa urahisi zaidi bila ya kuchoka na kichwa chake kuwa chepesi katika kufanya maamuzi.
Baada ya wiki moja kubakia kabla ya safari ya kuelekea Korea kusini haijaanza Roma alienda kwanza kazini kuangalia kinachoendelea na alifurahi kuona Tanya alikuwa akijitahidi kufanya kazi kubwa, lakini hata hivyo aliona kumwachia Tanya majukumu makubwa kama hayo ni kumchosha , hivyo alijiambia atakaporudi Korea atatafuta mtu wa kukaimu nafasi yake kwani yeye alikuwa na mambo mengi.
Upande wa Sophia rasmi sasa mkataba wake wa kuigiza filamu ulisainiwa na kampuni ya Vexto Media na taratibu za kushoot zilikuwa zikiendelea kwa usimamizi wa kampuni ya Penguin Production na ni zaidi ya mwezi tokea aelekee nchini Afrika ya kusini kwa maandalizi.
Mashabiki zake wengi walikuwa wakitarajia sana kuona namna ambavyo Movie hio itakuwa , kwani walikuwa wakimpenda sana Sophia sio kwa sauti yake tu lakini pia kwa namna ambavyo alijaliwa uzuri.