Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

𝕄𝕜𝕦𝕦 𝕞𝕓𝕠𝕟𝕒 𝕙𝕒𝕦𝕡𝕒𝕥𝕚𝕜𝕒𝕟𝕚 𝕦𝕫𝕚𝕞𝕒 𝕦𝕡𝕠𝕠
 
SHETANI RUDISHA NAFSI ZETU.

MTUNZI:SINGANOJR.

SEHEMU YA 166.
Kimulimuli Gizani.
Hamza alianza kumfukuzia Mzee Farook , huku akimpotezea Nyakasura na moto wake . Alijiambia hata kama akifa lazima amuue kwanza Master Farook.
Lakini hata hivyo kabla hata hajamfikia , Mzee Farook alitupiwa moto na Nyakasura kwa spidi ya juu kiasi kwamba ulitoboa tumbo lake na kilichoweza kusikika ni ‘puch’.
Mzee Farook aliishia kugeuza uso wake kumwangalia Nyakasura na alijikuta akitoa ukulele wa kutotaka kufa na palepale alidondoka chini na kuanza kuungua.
Mwili wake wote uliunguzwa na moto wa Nyakasura kiasi kwamba ni kama amemwagiwa petroli na ndani ya sekunde kadhaa aligeuka majivu.
“Nilikuambia usiondoke , ina maana hukuyachukulia maneno yangu kwa uzito . sasa ni zamu yako kuungua na wewe”Aliongea Nyakasura.
Hamza aliishia kuachama kiasi . Ingawa aliweza kuhisi kitu kikija kutoka nyuma yake , lakini hakuhisi hatari ikimaanisha yeye ndio hakulengwa, lakini alishangaa kuona Nyakasura ndio amemuua Mzee Farook.
Ilishangaza kwasababu Nyakasura ndie aliekuwa akimzuia kutokumuuwa mzee huyo lakini muda huo ni kama amebadilika na hakujali tena kuhusu sheria . Alichokuwa akitaka muda huo ni kupigana basi.
Kuwa na nguvu kubwa hutengeneza ukiburi na hilo ndio alionyesha Nyakasura kiumbe Foeniksi.
“Nyakasura kuna ulazima wa sisi kuendelea? Farook amekufa hivyo mimi naondoka”Aliongea Hamza huku akijiambia kuhusu Fabi hana haja ya kuwa na wasiwasi , kwasababu bila ya baba yake maana yake hakuwa na nguvu yoyote.
“Usijifanye sijui hujapigana na mimi ukiwa siriasi wakati mimi nikikuonyesha nia yangu ya dhati. Ukikimbia wewe sio mwanaume”Aliongea Nyakasura kwa kejeli huku akiinua kichwa chake , moto uliokuwa umezingira mwili wake ulikuwa ukitisha na haikueleweka alikuwa akiwezaje kuudhibiti.
Sehemu tu aliokuwa amekaa kila kitu kumzunguka kilikuwa kikiungua m alikuwa ni kama jua linalotembea , kama mfalme wa ndege wote.
Hamza alishindwa kujizuia na kuishia kutetemeka mwili mzima , hisia za kuwa na mwili kama wake mbele ya kiumbe huyo ilimfanya damu kuchemka na vinyweleo kusimama.
Mpaka hapo busara aliona ni kukimbia na ndio anaweza kupona katika hali hio. Aliona hakuwa na haja ya kuhatarisha uhai wake kudili na kiumbe ambae hakuwa binadamu , maana aliona ili mradi akiwa karibu na moto hawezi kufa.
Lakini licha ya hofu hio aliokuwa nayo , lakini ndani kabisa katika moyo wake asingeweza kukimbia , hadhi yake na utu wake kama mtaalamu wa mapigano ilikuwa imeguswa haswa . ile hali ya kutaka kuendelea kulinda hadhi yake hakutaka kuipoteza kwasababu tu ya miaka mitatu ya kuwa nje ya ulingo.
“Kwasababu umesema mwenyewe basi sina budi zaidi ya kupambana na wewe”Aliongea Hamza na palepale aliinama na kuangalia mwili wake. Nguo zake zote zilikuwa zimeungua na kubakia uchi lakini kwa Nyakasura hakuona tashwishwi ya aina yoyote . Alionekana alikuwa mzoefu wa kuona watu wakiwa uchi.
Ilikuwa ni bahati tu kwamba wao pekee ndio walikuwa juu ya mlima la sivyo ingekuwa kadhia ya mwanaume ambae yupo uchi anapambana na kiumbe mrembo.
Hamza aliishia kutingisha kichwa chake akipotezea mawazo hayo na kisha palepale alivuta pumzi nyingi na kuzishusha mara kadhaa na kadri alivyokuwa akifanya hivyo mpangilio wa pumzi yake ulianza kubadilika , mwanzoni alianza kupumua kwa haraka kama binadamu lakini muda huo alikuwa akitumia muda mrefu kupumua na kushusha pumzi.
Muda ule mwili wa Hamza misuli yake ilianza kutanuka kwa kasi na viungio vya mifupa katika mwili wake vilipiga kelele. Dakika ambayo Hamza aliyafumbua macho , yalikuwa yameingia ndani kwa kuwa siriasi na alipiga hatua moja na kukanyaga chini kwa nguvu.
Boom!
Kitendo cha kukanyaga chini kulitokea kishindo kizito na ardhi ilibonyea kwenda ndani na kutengeneza shimo.
Misuli yake ya kiuno ilionekana kuunganika moja kwa moja na mapaja yake , miguu na hata vidole na kumtengenezea muunganiko mkubwa wenye nguvu.Kila wakia(ounce) ya nguvu ya msuli wake ilikuwa imeungana pamoja na kutengeneza mkusanyiko wa nguvu ya juu.
Kuona vile Nyakasura macho yake yalisinyaa na alijikuta akitingisha kichwa huku akimwemwesa maneno.
“This is very interesting…”Aliongea.
Hamza hakuongea neno , kwa hatua moja alimsogelea Nyakasura bila ya kujali moto wake.
Kwa mbali ilikuwa ni kama vile jua halitaki kupatwa. Miale ya moto ya Nyakasura ilimfunika Hamza na kuunguza kila kitu . Lakini spidi ya Hamza ilikuwa sio kidogo , alikuwa kama mwanga na kumfanya Nyakasura kushindwa kuendana nae kutokana na miale yake ya moto ilitembea katika spidi ya mkondo wa hewa.
Hamza alikuwa akitumia uwezo wake wa kujongea kwa spidi kukwepa miale ya Nyakasura.
Nyakasura upande wake alionekana ni kama ashajua tatizo hilo na hakumfukuzia Hamza na badala yake alisimama katika eneo moja huku akisambaza miale pande zote.
“Ah!
Hamza alinguruma akiamua kuikaribisha baadhi ya miale ambayo aliona hawezi kuikwepa na muda huo huo alisogea kwa spidi kubwa kumshambulia Nyakasura na teke , akilenga maeneo dhaifu ya mwili wake.
Nyakasura mara baada ya kuona Hamza amefanikiwa kupita katika moto wake na sasa anamsogelea , alijikuta akishituka lakini hakutaka kusubiria kizembe.
“Mbawa mbayumbayu!”
Mara baada ya kuongea hivyo ghafla tu moto wake wote ulimfunika na kugeuka mbawa ambazo zilimpaisha kukwepeshwa na shambulizi la Hamza.
Hamza kuona hivyo alijikuta akishikwa na mshituko . Alijikuta akimwangalia Nyakasura akipaa kwenda angani na mbawa zake kwa spidi kubwa kiasi kwamba ndani ya sekunde tu alikuwa mita kadhaa mbali, na kumfanya aonekane kama malaika wa moto.
“Damn.. unaweza hata kupaa!!”
Hamza alijikuta akiamini uwezo wa damu ya kifoeniksi haukuwa wa kawaida kabisa . Ilikuwa kheri kama damu hio ingekuwa na nguvu pekee lakini ilikuwa na nguvu za kimitego nyingi za siri. Hamza yeye hakuwa na uwezo wa kupaa bali alikuwa na uwezo wa kuruka na kama Nyakasura anao uwezo wa kupaa watawezaje kuendelea kupigana.
Nyakasura akiwa hewani alikusanya donge kubwa la moto na mara baada ya kulichezesha kwa sekunde tu liligeuka na kuwa mkuki na kurushia sehemu alipo Hamza , mkuki huo kwa namna ulivyokuwa ukikata hewa ulikuwa ukitoa mlio kama wa ndege Mwewe , lakini sauti yenye kuumiza masikio.
Hamza mara baada ya kuona siraha hio hakuthubutu kabisa kuisogelea karibu na haraka sana alikimbia mbali.
Sekunde mluki ule wa moto ulivyochoma ardhi ulitengeneza wimbi kubwa la moto na kuyeyusha kila jiwe lililokuwa pembeni na kutengeneza shimo.
Nguvu hio ya uharibifu binadamu angeweza kuishuhudia angezimia hapo hapo. Lakini kwa Hamza hakuwa na muda wa kujali sana kuhusu maajabu hayo kwasababu Nyakasura alikuwa akimsogelea kwa kasi na mbawa zake za mbayumbayu.
Hamza aliamini kama akikutana moja kwa moja na nguvu hio ya mbawa inayomsogelea anaweza akawa katika hali mbaya. Kwa macho yake makali aliona kisima cha kuhifadhia maji nyuma ya nyumba za kambi hio zilizoharibika na bila ya kujiuliza mara mbilimbili alitimua mbio kukisogelea.
Nyakasura mara baada ya kuona Hamza anakimbia , alimfukuzia kwa nyuma kwa spidi kubwa huku akirefusha moto wake na kugeuza kuwa mkuki wa mita kadhaa.
Ile Nyakasura anataka kumkaribia Hamza kumchoma na ule mkuki mgongoni, Hamza aliwahi na kama mshale alitumbukia ndani ya kile kisima ‘chubwii’ na kula mbizi na kukoswa koswa na shambulizi.
“Unadhani utakuwa salama ukiingia kwenye maji?”Aliongea Nyakasura na palepale alinyoosha mkono wake na kushika ukuta wa kisima kile huku akisambaza moto mkali na ndani ya sekunde tu kisima kile mawe yake yalianza kuyeyuka huku maji yakianza kushika mvuke.
Muda huo huo Hamza alifyatuka kutoka kwenye kisima hicho kama Samaki na ile anafika nje alimtemea Nyakasura maji mengi kama Kiboko.
Hamza baada ya kufanya vile hakujua acheke ama alie, alidhania akimtemea maji Nyakasura angeuzima moto wake na kumfanya kuwa dhaifu lakini alijisumbua tu . Kwa alivyoona hata kama ingekuwa ni bahari pengine asingezimika.
Hamza palepale aliachana na mbinu ya kufikiria namna ya kuzima moto wake na badala yake aliona namna ya kushinda ni kupigana nae moja kwa moja na hapo ndipo vita ya mvutano ilipoanza.
Hamza alitumia uwezo wake wa kukimbia kumuacha mbali adui yake na wakati huo Nyakasura aliendelea kumfukuzia Hamza huku akimtupia moto na kukwepa mashambulizi yake ya kushitukiza.
Yalikuwa ni mapigano ya kwenda mbele na kurudi nyuma na hakuna alionekana kushinda ama kupoteza pambano.
Baada ya dakika kumi za mvutano , Hamza alikuwa na majeraha mengi ya moto katika mwili wake , huku upande wa Nyakasura akiwa amepigwa mara kadhaa na ilikuwa bahati hakupokea shambulizi la moja kwa moja.
Hamza ili kumshambulia Nyakasura ilibidi ajitoe muhanga wa kuunguzwa na moto lakini wakati huo huo akihakikisha shambulizi lake linamfikia kisawa sawa.
Hamza mara baada ya kutua chini baada ya kufanya shambulizi aliishia kuangalia mikono yake iliogeuka na kuwa mieusi kwa kuungua na alijikuta akipata msongo wa mawazo.
Nyakasura nguvu zilikuwa zimempugnua pia na alikuwa akihema kwa kuitafuta hewa , mbawa za moto alizokuwa nazo zilikuwa zimepotea pia.
“Nyakasura ni muda wa kuacha sasa , tukiendelea hivi tutakufa”Aliongea Hamza.
“Bado mshindi hajapatikana” Aliongea Nyakasura na palepale alivamia jengo la nyumba iliokuwa ikiwaka moto na kwenda kuoga moto.
Hamza mara baada ya kuona hivyo machozi yalitaka kumtoka . Alijiuliza huyu mwanamke anajaribu kufanya nini , wamepigana muda mchache tu lakini bado anataka kujirudisha katika hali yake ya kawaida.
“Hey! Kwa staili hio unadhani utachukua muda gani kumaliza kupigana?”Aliuliza Hamza na Nyakasura hakujali zaidi ya kuvuta pumzi ya moto na ndani ya dakika alitoka akiwa na ari mpya kwa ajili ya kuendelea kupigana.
“Usiwe na wasiwasi maana haitochukua muda mrefu nitakuwa nishakupiga”Aliongea Nyakasura akiwa katika hali ya kujiamini.
“Sidhani kama itawezekana ..”Aliongea Hamza.
“Nini! Usiniambie una mbinu ambayo hujaitumia bado?”Aliuliza Nyuakasura huku akionyesha ishara ya kutokuamini lakini bado aliamini kwa wakati mmoja.
Kwa mtazamo wake , mpaka Hamza kumlazimisha kuoga mara mbili katika moto haikuwa kawaida, ilikuwa mara yake ya kwanza kukutana na binadamu wa daraja la uwezo huo.
Hamza alifanya maamuzi katika moyo wake , uwezo wa kukimbia alikuwa nao , lakini hakutaka kufanya hivyo na njia pekee ya kushinda pambano hilo ni kutumia uwezo wake wa juu sana kumshikisha adabu vinginevyo licha ya kwamba alikuwa na mwili wa kuvumilia maumivu ya kuungua lakini isingekuwa vizuri kuendelea kuunguzwa.
“Ni mara yangu ya kwanza nakwenda kutumia hii mbinu ambayo nimeielewa kwa ufupi sana zidi yako kiumbe Phoenix ,. Sipo tayari kudhalilika nadhani pia hutojilaumu mwishoni”Aliongea Hamza.
Muda uleule mwili wake ulifunikwa na kivuli cha ajabn huku hewa kuzunguka ilianza kutingishika kama vile ni gesi inasambaa angani.
Hamza mwili wake ulianza kudunda kama vile misuli imegeuka na kuwa moyo, ilionekana ni dhahiri ni kama kuna kitu ambacho kipo ndani yake na kinataka kutoka.
Nyakasura alijikuta akikunja ndita . Alijikuta akihisi kuna kitu hakipo sawa kuhusu Hamza licha ya kuwa mbali,mapigo yake ya moyo yalibadilika.
Aliona Hamza ni kama alikuwa amefanana na anga linalomzunguka . Na sehemu aliosimama ni kama vile anga lake linadondoka chini.
“Decompose!”
Aliongea Hamza isieleweke anamaanisha nini na palepale alianza kutingishika kama vile anacheza kibwebwe huku akitamka maneno. Maneno ambayo alikuwa akitamka ni yale ambayo Yonesi alimpatia akimwambia kwamba aliokota maandishi yale jangwani katika misheni ya kijeshi.
Hamza hakuwahi kutumia maandiko yale tokea mara ya mwisho alivyojaribu kujifunza na kumuona mwanamke katika ndoto , sababu ya kuhisi muda huo ni wakati wa kutumia sio kwamba alikuwa na uhakika ila alipanga kujaribu akiwa katika hali ya juu sana ya uwezo wa mwili wake , kwani siku ile hisia alizopata ni kama akili yake ilitawaliwa na mdudu. Moja ya kanuni ya mafunzo ambayo yanajumlisha na nguvu ya kiroho , ili kupata majibu unayoyataka ni lazima kwanza consciosness yako iwe katika hali ya uamko(Active) ili kunyonya nguvu yoyote bila kuathiri nafsi yako. Mbinu hio wataalamu wa mafnnzo hayo wanaita Mgawanyiko wa nafsi na Roho (Soul and Spirit Disintergration).
Mbinu hio hata hivyo ilikuwa na hasara zake , kwasababu inatengeneza mlipuko wa nguvu ya ndani kutokana na kwamba nafsi na roho kiungo chake kikuu ni damu.
Hamza hakujali chochote, muda huo alitaka kuamsha uwezo wake wote wa damu kwa kuichanisha nafsi yake na damu ili kutengeneza mwili ulio huru. Mtego wa nguvu ya miili yetu upo katika nafsi zetu na roho , kuishinda nafsi maana yake ni kujiweka huru.
“Ah!”
Hamza alijikuta akipiga makelele huku akiangalia hewani , macho yake ni kama hayakuwa yake bali yameshikiliwa na kiumbe kingine na lile eneo alilokuwa amesimama lilianza kutitia na kufanya mawe kuporomoka.
Jambo lile lilimshangaza Nyakasura na alisogea mbali huku akijiuliza Hamza anafanya kitu gani. Licha ya kujiuiliza hivyo , ilikuwa ni wazi kabisa mbinu hio Hamza aliotumia imemuongezea nguvu zake maradufu.
Hamza mara baada ya kusimama juu wima , umbo lake ni kama vile lilikuwa limeongezeka maradufu , lakini haikuwa hivyo alikuwa kawaida lakini kivuli chake ndio kilimfanya kuonekana kama vile ameongezeka urefu na upana wa mwili. Ajabu ni kwamba yale majeraha yake yote yalipona mara moja.
Muda huo Hamza alikuwa kama sanamu la Shujaa wa Ugiriki ya kale na alihisi kabisa misuli yake ilikuwa na nguvu isiokuwa ya kawaida . Mwenyewe hakudhania mbinu hio ingemletea hali hio na kumtengenezea pia hali ya kupona.
Mara baada ya kuhisia joto la Nyakasura aliona halikuwa likiunguza kama ilivyokuwa mwanzo , cha kushangaza ni kwamba alijihisi kuwa mwepesi kama unyoya.
Palepale akili yake yote ilikuwa katika mwili wake na ile alivyokanyaga chini ni kama aliinuliwa na upepo na kusogea kwa spidi uelekeo wa Nyakasura alipo huku akiwa ametanguliza ngumi mbele na hakuhofia miale ya moto wake.
Nyakasura upande wake alikuwa amejiandaa pia kwa shambulizi hilo na palepale aliugeuza moto wake kuwa siraha na kushambulia ngumi ile ya Hamza , lakni ilivyogusana na ngumi ile ilisambaratisha na kumfanya ashikwe na mshituko mkubwa na kujiuliza amekuwa shetani wa aina gani. Mara baada ya kuona mkuki wake haukuwa na madhara kwa Hamza aliona akimbie kwa kurudi nyuma lakini muda ule bado ngumi nyingine ya Hamza ilikuwa ikimsogelea.
“Ngao!!”Aliita
Palepale mkono wake wa kushoto uliibuka na ngao ya moto wa Zambarau na kusambaa hewani kama sahani kubwa ya kumfunika mtu asionekane upande wa pili.
Boom!!
Ngumi ya Hamza ilienda kugongana na ile ngao na kutengeneza sauti kubwa yenye kishindo.
Lakini haikuwa mwisho . Hamza mabega yake . misuli ya mikono yake na vidole vilikuwa vikisambaza wimbi la nguvu kiasi kwamba ile ngumi ilimfanya Nyakasura kushindwa kuidhibiti na kufanya ngao itawanyike huku yeye mwenyewe mwili wake ukipepesuka na kumfanya aende kudondokea mwamba chini ya mlima.
Shambulizi la ngumi ambalo Nyakasura alipokea lilimretea majeraha makubwa sana. Pigo lile lilimfanya moto uliokuwa umemzingira mwili wake kupotea mara moja na nywele zake kurudi katika hali ya kawaida.
Nyakasura alijishika kifua huku viashiria vya kutoka damu vilionekana katika mdomo wake . Aliinua kichwa chake na kumwangalia Hamza katika hali ya mkanganyiko huku akijishangaa alikuwa amepata majeraha ya ndani na kujiuliza inawezekana vipi ilihali yeye sio binadamu.
“Wewe kiumbe .. nadhani mpaka sasa hakuna haja ya kuendelea kupigana”Sauti ya besi ilisikika kutoka juu
Nyakasura aliishia kung’ata meno yake kwa hasira na alipiga kibao ardhini kwa hasira na kusimama.
“Bado hujanishinda , pigo moja huwezi kusema shindano limeisha”Aliongea na palepale aliita moto na mbawa kwa mara nyingine na kupanda juu hewani.
Licha ya kwamba alikuwa ameumia , lakini haikutosha kumfanya aache kupambana . Alikuwa akipanga kupanda juu ya mlima ili kwenda kuoga katika moto kujiponyesha.
Hamza hakuwa mzembe , alikuwa akijua huyo msichana anataka kwenda kujirudisha upya katika moto na majivu. Kwasababu alishachoka kupambana nae kusikoisha , hakutaka kumpa nafasi hio. Hivyo alianza kumfukuzia huku akiwa ameshatengeneza ngumi yenye ujazo.
Aliamini ngumi hio ikipata , hata kama hatomuuwa lakini atahakikisha amemjeruhi kiasi cha kutoweza kupaa angani.
Hamza alikuwa ni kama Kombola namna alivyokuwa akimsogelea Nyakasura na ile anafikia miale ya moto hakujali na alipita kwa kasi kiasi cha kusababisha mlipuko mkubwa.
Nyakasura mara baada ya kuhisi mlipuko ule , palepale aligeuka na alijikuta akiwa katika hali ya mshituko kumuona Hamza akimkaribia.
Hamza hakutaka kupoteza muda , baada ya kumsogelea karibu aliiongezea ujazo wa kutosha ngumi yake akinuia kumaliza pambano hilo kwa ngumi moja tu kabla mwanamke huyo hajaingia katika lindi la moto na kujiponyesha.
Lakini sasa dakika hio anataka kushambulia sauti kama ya ngurumo ilisikika kutoka chini ya mlima . Ilionyesha ni dhahiri kuna mtu ambae ametumia nishati ya mbingu na ardhi kusafirisha sauti hio
“Hamza utamuuwa. Acha!!”
Hamza mara baada ya kusikia sauti hio imetoka kwa nani , palepale aliacha kumshambulia. Nyakasura alikuwa amefumba macho mara baada ya kuona hakuna namna ya kuwekepa shambulizi la Hamza na jasho lilimtoka lakini alishangaa baada ya kusikia sauti ya Hamza kuzuiwa kutokuendelea.
Dakika hio hio vivuli vya watu wawili vilitua katika mlima huo . Alikuwa ni Afande Simba na Afande Himidu.
Afande Simba mara baada ya kuona uharibifu uliotokea katika kambi hio na kuzunguka kilele hicho cha mlima aliishia kutingisha kichwa kwa masikitiko na mshangao kwa wakati mmoja.
“Nyakasura nimekutuma kwa ajili ya kuisadia kambi ya nyoka , lakini kwanini umeinguza ?”Aliuliza Afande Simba kwa sauti.
“Mimi nilisema nakuja tu kuangalia ila sikuahidi kama sitoiunguza na moto”Aliongea.
“Wewe…” Fande Simba alijikuta aking’ata meno kwa hasira , “Inaonekana nimekuharibu kwa hiki ulichokifanya , hivi unadhani wafuasi wake watakuchukuliaje? Na hii hasara uliosababisha unadhani nani atailipia? Ni hela za kodi za wananchi na unajua hilo”Aliongea.
“Ubaya ubwela, kama ni hela zipotee tu. Na usinizuie maana bado sijamaliza kupigana”Aliongea kwa kiburi.
“Kupigana! Kama nisingemzuia Hamza ungeweza kukwepa shambulizi lake?” Afande Simba alifoka na kumfanya Nyakasura kung’ata meno kwa hasira.
“Ningekubali anishambulie na kisha kujiponyesha na moto . Wewe jali mambo yako mimi nataka kuendelea kupigana”Aliongea kwa kiburi na kumfanya Afande Simba kushindwa kuongea na kutingisha tu kichwa na palepale aligeuza sura yake na kumwangalia Hamza aliekuwa na mwili uliotuna na misuli kuonekana nje na kumfanya kuoekana mgumu kama mti.Nguvu ya Hamza alioshuhudia ilimtisha mno.
Afande Himidu aliekuwa hapo alimwangalia bosi wake na kumwonyeshea kidole gumba cha kumkubali. Aliona fika bosi wake ambae ameachana na maswala ya kuvuna nishati bado hakuwa mdhaifu.
Mwanzoni alidhani kutokana na Hamza kupoteza uwezo wake wote basi atakuwa hayupo katika levo ileile kama Nyakasura lakini muda huo aliona alikuwa amekosea kuidharau mbinu binafsi ambayo Hamza alikuwa akijifunza.
Hamza aliona hana haja ya kuendelea kupigana tena , hivyo palepale aliachilia nguvu ile nafsi mgawanyo na kurudi katika mwonekano wa kawaida.
“Himidu hebu acha kuniangalia nikiwa uchi na fanya mpango nipate nguo za kuvaa”Aliongea Hamza .
“Hahaha.. sawa bosi , ngoja nimpigie mtu alete nguo haraka sana”Aliongea Himidu huku akiwa na furaha.
“Nani kakuambia tunaacha? Bado sijamalizana na wewe”Aliongea Nyakasura kwa hasira
Hamza aliishia kuona mwanamke huyo ni king’ang’anizi mno , kama wakiendelea kupigana itakuwa ni aidha amuue au auliwe,. Kitu ambacho hakuona kama kitakuwa na maana kutokana na kutokuwa na uadui kati yao.
“Nyaka ukiendelea hivi . nitawasiliana na baba yako kumwambia”Aliongea Afande Simba akionya.
“Wewe ni Simba mshenzi , Simba unaenuka , unaona ni vizuri hivi unavyonifanyia?”Aliongea huku akikanyaga miguu yake chini kwa hasira.
Hamza mara baada ya kuona hivyo alijikuta akifurahi , alijiambia kumbe Nyakasura anae baba ambae anaweza kumkontrol? Tukio hilo alifananisha na namna mwalimu anavyomtishia mwanafunzi kuita wazazi wake.
“Nipo tayari kutokuiambia familia yako juu ya kuunguza kambi ya Nyoka! Kama unataka wafahamu kila kitu ni kheri ukaishia hapa la sivyo utakosa uhuru wako”Aliongea na kumfanya Nyakasura kusaga meno yake kwa hasira huku akimwangalia Hamza.
“Mimi na wewe hatujamalizana , nitakuacha kwasababu ya Simba , ila usiombe tukutane tena!”Aliongea kwa kulalamika.
Hamza hakuwa na muda wa kuendelea kubishana na mwanamke huyo na aliishia kutingisha mabega yake kumpa ishara ya kumkaribisha muda wowote.
Haikuchukua muda mrefu Hamza aliletewa mavazi ya kuvaa na baada ya kuyachukua hatimae Himidu alimsogelea bosi wake.
“Bosi wewe ni hatari . Hii ni mara yangu ya kwanza kumuona Nyakasura kuwa katika hali ya kutaka kulia..”Aliongea Himidu kwa sauti ya chini lakini alisikiwa vizuri tu na Nyakasura na kumfanya azidi kupandwa na hasira.
“Himidu endelea kuropoka tu ukidhani siwezi kukuunguza na mtoto nikuue”Aliongea na Himidu alinywea huku akicheka chinichini.
“Hey! hebu acha kumtishia rafiki yangu na moto wako , kwanza nina njaa maana umenisumbua sana”Aliongea Hamza huku akishika tumbo lake.
“Bosi hio mbinu uliokuwa ukitumia mwisho mwisho , inaitwaje?”
“Unadhani naweza kukuambia kirahisi namna hio , Hio mbinu inaitwa Siri”Aliongea Hamza na kumfanya Afande Himidu kukosa neno la kuongea. Hata hivyo alijua Hamza hawezi kumwambia.
Muda huo huo kundi la wazee wa kambi ya nyoka walipandisha mlima na kusogea wakiongozwa na Mjomba ambae jina lake ni Mzee Sembe.
Walisikitika sana kuona msingi wote wa kambi yao ulikuwa umeungua kwa moto na macho yao yote yalimwangalia mkuu wa majeshi wakimtaka achukue hatua.
“Mzee Farook yupo wapi ?”Aliuliza Afande Simba huku akimwangalia Hamza na Hamza baada ya kuulizwa hivyo alimnyooshea kidole Nyakasura.
“Ameshakufa.. kauliwa na huyo mrembo”
“Nini!?” Mkuu huyo ndita ilijikunja huku akimwangalia Nyakasura kwa mshangao ,”Kwanini umemuua mzee Farook ikiwa nimekutuma kuja kumsaidia?”





















SEHEMU YA 167.
Wafuasi wa Nyoka mara baada ya kusikia kufa kwa Mzee Farook kumesababishwa na Nyakasura walijikuta wakiwa katika hali ya kumshangaa. Walikuwa wakiokoa maisha yao muda ule na hawakuweza kuona tukio hilo.
“Alikataa kusikiliza nilichomwambia na kukimbia akijifanya anataka kuokoa maisha yake ilihali yalikuwa mkononi mwangu. Mtu kalegea legea mnafanya kiongozi, nimemuuwa mimi”Aliongea Nyakasura kwa kejeli akionyesha hajutii kabisa alichokifanya.
Afande Simba aliishia kuvuta pumzi na kuzishusha huku akimwangalia Mzee Sembe kwa masikitiko.
“Jeshi litasimamia ujenzi upya wa kambi ya nyoka , ni bahati tu mnahifadhi nyaraka zenu muhimu ndani ya pango , hivyo tofauti na hasara ya majengo hakuna hasara kubwa. Kuhusu suala la Farook kutuma wanafunzi wake kwenda kufanya vurugu na kuhatarisha usalama wa raia wa kawaida lilikuwa kosa kisheria hivyo tutaishia hapa”Aliongea
“Asante sana Simba! Ingawa kambi yetu ya nyoka sio tajiri kuzidi taifa lakini tuna kiasi cha kutosha kuijenga upya . Hela na utajiri ni kitu cha kupita ila tunajali sana hadhi na taswira ya kambi yetu. Hatuwezi kumuwajibisha Nyakasura lakini kuhusu huyu Hamza, je hana kosa?”Aliuliza Sembe, alikuwa tayari kumsamehe Nyakasura kutokana na kutokuwa kiumbe wa kawaida lakini kuhusu Hamza hakutaka lipite kirahisi kwa kuwadhalilisha.
Afande Simba alikuwa katika hali ya mkanganyiko , aliishia kumwangalia Hamza na kisha wazee hao wa kambi pamoja na wanafunzi wao wakiwa na hamu kusikiliza maamuzi yake. Baada ya kufikiria kidogo aligeuzia kichwa chake kwa Afande Himidu.
“Mshauri mkuu , unamjua Hamza vizuri . Unadhani tunapaswa kudili nae vipi?”Aliuliza na kumfanya Himidu kuanza kumtukana mkuu huyo ndani kwa ndani baada ya kuona anamtupia mpira . Ila hata hivyo hakuongea na badala yake alikunja mikono yake nyuma na kutembea mpaka mbele ya wazee wa kambi.
“Wazee kuna mambo ni vigumu kuyaongea mbele ya watu wengi. Kwanini tusiende sehemu tulivu na kuongea kidogo ?”Aliongea na Mzee Sembe na wenzake walitingisha kichwa na kukubali na walishuka kuelekea chini ya mlima.
Nyakasura aliishia kumwangalia Hamza kwa macho ya chuki na kisha alimpa ishara ya heshima Afande Simba.
“Mimi natangulia kuondoka . Wewe,nitakutafuta turudie upya”Aliongea akimwashiria Hamza na kisha palepale aliyeyuka na Hamza alipumua kwa ahueni na kisha alimsogelea Afande Simba.
“Simba katika vitu vitatu ambavyo ulihitaji kutoka kwangu vimebakia vitu viwili tu”Aliongea.
“Unasemaje?”, Afande Simba alishikwa na mshangao, “Kwanini?”
“Usiniambie unataka kuwa kinyume na maneno yako , Si ndio wewe ulieniambia nimuache na nikaacha. Unadhani Nyakasura amepona ponaje?”Aliongea Hamza huku akicheka kiuovu.
“Na hio inahesabika? Hivi unajua ungejiingiza katika matatizo ya namna gani kama nisingekuzuia na ukamjeruhi Nyakasura?”
“Mimi sijali kuhusu hilo , vyovvyote vile wewe ndio ulieniambia nimuache , Hivyo ni sawa na mimi kukubaliana na hitajio moja katika yale matatu . Wewe ni mkuu wa jeshi hivyo sidhani utaenda kinyume na maneno yako”Aliongea lakini mkuu huyo uso wake ulionyesha kutokuwa tayari kukubaliana nae. Lakini hata hivyo alikosa njia ya kukataa. Alijiambia akienda kuelezea mbele ya mkuu wake atasema Hamza alimfanyia hila..
“Sijawahi kudhania mtawala wa ulimwengu wa giza mwenye uwezo wa kutingisha ulimwengu anapenda michezo ya hila”Aliongea
“Hakuna cha hila hapo , najaribu kupata haki yangu , kuna tatizo kwani mtu kudai haki yake?”Aliuliza Hamza.
“Basi sawa , tuseme umeshinda katika hili, lakini kwasababu yako kambi ya nyoka imeingia hasara kubwa . Ni ngumu sana kwenda kuelezea kilichotokea hapa kwa viongozi wa kiserikali. Kama hutaki kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria ni vizuri ukionyesha uaminifu wako”
“Uaminifu? Ni uaminifu wa namna gani unahitaji kutoka kwangu ? Ni wafuasi wa Nyoka ndio walifika katika kampuni ya mke wangu na kufanya fujo na nimefika hapa kwa ajili ya kulipa kisasi kulingana na sheria ya ulimwengu wa mapigano . Kuna kosa gani hapo?”
“Ndani ya nchi yetu ya Tanzania kuna sheria moja na hakuna sheria za kimapigano zinazoongoza nchi. Kama unataka kuendelea kuishi kwa amani ndani ya nchi yetu unapaswa kutii sheria bila shuruti”Aliongea na Hamza hakutaka kumjibu na kutaka kujua ni ombi gani anahitaji kutoka kwake.
“Niambie unataka nini kutoka kwangu ili niishi kwa amni?” Aliuliza na kumfanya Afande Simba kutoa tabasamu.
“Mwezi ujao Ulaya kutakuwa na kusanyiko la SETH Great . Nadhani hujasau?”
“Unazungumzia Sytor rating Assembly?”Aliongea Hamza huku akihesabu siku kupitia vidole vyake , “Ni kweli aisee , kama usingenikumbusha ningeshasahau mimi , miaka mitano imepita tayari”.
Seth Association ni jumuiya ambayo inashirikiana na mataifa makubwa ulimwenguni katika kutoa maksi na kupembua mashirika na jamii za siri ulimwengoni kote . Kila baada ya miaka mitano huitishwa kusanyiko la siri ambalo huitwa SETH Great Assembly au maarufu kama Set Rating Assembly.
Sababu ya kusanyiko hilo ni kwa ajili ya kugawa maksi kimadaraja kwa makundi ambayo yamepanda na kushuka katika ulimwengu wa siri.
Ilikuwa ni kama sherehe za ugawaji tuzo kwa wahalifu, tofauti tu ni kwamba sherehe hizo hufanyika kwa siri sana japo zinahudhuriwa na viongozi wakubwa duniani na wanachama wa mashirika ya siri na yale ya giza kama Freemason , Illuminat na mengineyo , haikuwa hivyo tu hata baadhi ya vitengo vya siri vya kiserikali kutoka mataifa mbalimbali hushindanishwa na kukwapua tuzo mfano Malibu pia wanayo haki ya kushiriki wakitaka.
Dunia ina jamii nyingi za siri za milengo ya kulia na kushoto ambazo zinachipua na kupotea na ndio maana wakaweka kipimo cha kutambua jamii ambazo zimeimarika zaidi katika muda huo ili kutambuliwa dunani kote.
Haikujalisha kundi ama kitengo kilikuwa cha ulimwengu wa giza ama ulimwengu wa haki , walipaswa kuweka unafiki pembeni na kisha kufanyiwa evaluation na jumuiya hio ya watoa maksi. Kwa ufupi ni kwamba hata wale wahalifu wa daraja la kwanza Duniani hupewa tuzo na wakati wa kusanyiko hilo wanakuwa nje ya sheria ya taifa husika na badala yake wanakuwa chini ya Sheria ya Seth Association. Kwa mfano wewe ni Jambazi wa kimataifa na Ulaya inakutafuta na ukataka kuhudhuria kusanyiko utaruhusiwa kuhudhuria chini ya ulinzi wa sheria za Seth na baada ya kusanyiko kuisha unapewa muda wa kwenda mafichoni kama kawaida na sheria za ulimwengu wa haki zitaanza kukutafuta upya . Ndio kipindi ambacho majambazi na magaidi hupata fursa ya likizo bila ya hofu ya kukamatwa mpaka kusanyiko liishe.
“Kama unataka serikali isiendelee kufuatilia hili swala basi unapaswa kushiriki chini ya kitengo chetu cha Malibu”
“Afande Simba unatania au? Wewe unajua nishaachana na hayo mambo ya ulimwengu wa giza muda mrefu halafu bado unataka nikashiriki kama mwakilishi wa kitengo chenu cha Malibu?”
“Kwa nafasi yako katika ulimwengu wa siri hata jumuia ya watoa maksi wakisikia sidhani kama watakuwa na furaha . ila sisi kuhusu hilo hatujali maana lipo juu yako”Aliongea
“Kama nikishiriki nitakutana na watu ambao nimepotezana nao kitambo na maadui zangu pia na nikishiriki chini ya kitengo chako ni sawa na kuwatangazia naishi Tanzania , wewe unadhani nitapata amani?”
“Usipokubali pia huwezi kuwa na amani hapa nchini , Unadhani Amiri jeshi mkuu atakubali hivi hivi umemuua ndugu yake . Amini usiamini ndani ya saa moja tu amri ikitoka watu wote ambao una uhusiano nao ikiwemo mkeo watakuwa chini ya ulinzi”Aliongea.
“Afande Simba unanitishia?”
“Sikutishii nakuonyesha njia ya kupita . Haupo peke yako , hata kama isiwe ni kwa ajili yako , kumbuka kuhusu familia yako. Au nakosea?”Aliongea na kisha alitembea na kumshika Hamza bega.
“Kijana wewe ni hatari sana , una nguvu kiasi kwamba nakuonea wivu. Sidhani tokea kale mpaka sasa kuna binadamu ashafikia uwezo wako bila ya kuwa na nishati za mbingu na ardhi. Lakini kumbuka haijalishi mwanaume ana nguvu kiasi gani lazima awe na udhaifu wake . Wapendwa wako na ndugu zako ndio udhaifu ambao unauwa watu wengi wenye nguvu , Hivyo hata kama una nguvu unapaswa kuwa na watu katika mfumo kukulinda. Vinginevyo unadhani hawa wazee ni kipi wanajali , unadhani wanaogopa kwasababu hawawezi kupigana na wewe ana kwa ana . Kama madaraka huna basi kuwa na koneksheni na wenye madaraka . Vinginevyo maadui zako hawatakuangalia uimara wako ulipo bali wataangalia ni wapi udhaifu wako ulipo”Aliongea mkuu wa majeshi.
Hamza licha ya kwamba hakufurahiswa na maneno hayo , lakini vilevile ilikuwa ni kweli. Ijapokuwa alikuwa na uwezo wa kufanya vitu vingi lakini wengi ni wengi ,wakiamua lao asingeweza kufanya chochote.
“Endelea..”Aliongea Hamza na kumfanya Afande Simba kucheka.
“Nikiongelea koneksheni , unapaswa kujua kabisa inaweza kukusaidia kutatua matatizo yako mengi , lakini je unajua ni koneksheni gani ngumu mtu kuwa nayo?”Aliuliza.
“Usiniambie ni Kitengo cha Malibu?”
“Hapana! Ni kuwa na koneksheni na raia elfu arobaini wenye nguvu ambao wapo chini ya kamandi. Ili mradi upo ndani ya mipaka ya Tanzania , haijalishi upo angani , ardhini au baharini hakuna mahali ambapo jeshi letu halifiki”Aliongea na kumfanya Hamza aliekuwa katika hali ya umakini akili yake sasa kufanya kazi. Alimwangalia Afande Simba akiwa katika hali ya tabasamu ambalo sio tabasamu.
Aliona ndio maana maneno ya bwana huyo yalikuwa yakishangaza siku hio , kumbe zunguka yote anataka kumungiza jeshini?.
“Niseme ukweli , Simba uwezo wako wa kulobby ni mkubwa mno”Alitania Hamza na kumfanya Afande Simba kucheka.
“Viongozi wanakukubali sana , sizungumzii viongozi wa kisiasa namaanisha viongozi wa jeshi wa juu kabisa wanapagawa sana na mafanikio yako. Ili mradi ukisema ndio jeshi lipo tayari kukupatia cheo cha kuanzia cha Meja Jenerali na kama ukifanya vizuri haitokuwa ngumu kufikia cheo cha Luteni Jenerali ndani ya umri wa miaka therathini tu na kuvunja historia ya kuwa mkuu wa majeshi mwenye umri mdogo zaidi . Kubwa zaidi utakuwa mwenzetu sasa, ndani ya mipaka ya Tanzania hakuna ambae atathubutu kukugusa wewe wala watu wako wa karibu . Vinginevyo utakuwa ni mwenye kuhangaika tu na kulipa visasi” Mara baada ya kuongea hivyo Afande Simba alimwangalia Hamza kwa shauku.
“Vipi unaonaje kuhusu pendekezo langu?”
“Niseme ukweli maneno yako yamefanya damu yangu ichemke , kunipa cheo cha Meja Jenerali kama zawadi itamfanya mtu yoyote moyo kusukuma damu kwa shida .. lakini kwa heshima na taadhima nakataa”Aliongea Hamza.
“Kwanini?” Afande Simba alikunja ndita , “Au umeridhika na kuwa msaidizi ndani ya kampuni ya mke wako?"Aliuliza na Hamza alitingisha kichwa kukataa.
“Ulichopendekeza kinavutia , unanifanya niwe Jenerali na kisha jeshi linakuwa ndio koneksheni yangu . lakini kwa lugha nyepesi nikishakubali maana yake lazima pia nikitumikie cheo changu na kuhusu mimi nimechoka kupigana , ninachotaka ni maisha marahisi. Sitaki usumbufu labda tu nichokozwe. Hao mabosi nawashukuru kwa kunikubali . Lakini nimeishi maisha ya mbwa mwitu na kama nikiingia katika mfumo kuna kitu lazima kitatokea , tena kikubwa tu”Aliongea.
“Una uhakika huhitaji muda wa kufikiria kuhusu hili?”
“Tubadilishe tu masharti , sijioni nikikaa chini na kufikiria kuhusu hili”Aliongea Hamza na kumfanya Afande Simba kuona utayari wa Hamza katika macho yake na aliishia kukubali kinyonge.
“Basi sawa , ila hata kama haupo tayari kujiunga na jeshi letu bado utapaswa kusafiri na timu yetu ya vikosi vya Malibu kwenda Ulaya . Bila hivyo awamu hii swala la kuharibu kambi ya Nyoka kuwajibika kutakuwa juu yako”
“Kwani kuna haja ya kushiriki katika hilo kusanyiko , kama mnahisi hamna nguvu ya kutosha sioni haja ya kushiriki”
“Upo sahihi hakuna faida ya sisi kushiriki ama kutokushiriki , lakini mwaka huu kwasababu ya kugundulika kwa Earth Axis kuwa chini ya jeshi letu . Ikitokea tumewekewa vikwazo na mataifa ya nje moja kwa moja lawama za wananchi zitaenda kwa serikali na kwa jeshi. Mpaka sasa Serikali ya Marekani kupitia viongozi wao wameshaanza kuiongelea vibaya nchi yetu na ni swala la muda tu kuchukua hatua kwa siri ama kwa njia ya wazi”
“Nyakasura pia atashiriki . Ijapokuwa anahesabika kuwa mtaalamu wa juu katika ulimwengu wa mapigano kama ilivyo lakini asili yake inaweza kuleta sintofahamu nje ya nchi na vilevile hata kama akishiriki uzoefu hana na isitoshe kuna wataalamu wengi ambao bado hajakutana nao . Kwenda kwetu kushiriki ni kwa ajili ya kukuza hadhi ya jeshi vinginevyo kusingekuwa na haja ya kushiriki na kuwapa kazi wanasiasa kutuliza hali , lakini kama mabeberu wataamua kutushambulia iwe moja kwa moja ama kwa njia isio ya moja kwa moja tutakuwa kichekesho kwa dunia kwa nchi ndogo kama yetu kujaribu kutunishiana misuli na taifa kubwa. Ndio maana tunachotaka ni kujijengea hadhi kwanza katika ulimwengu usionekana , ili kam wakitaka kuchukua hatua wajifikirie mara mbilimbili.”Aliongea kwa kirefu.
“Kule Dodoma nilikuambia utupatie teknolojia ya Barham na Baffold ila haukuwa tayari , basi kubali katika hili, kama unajihisi wewe mweneywe kutoshiriki nadhani haitokuwa ngumu kutumia watu wako . Si ndio?”Aliongea na kumfanya Hamza macho yake kuchanua katika hali ya uovu.
“Simba unaenda mbali sasa , ile mara ya mwisho uliniomba teknolojia ya Barham na Baffold , kwahio yote ilikuwa ni kwa ajili ya kujiandaa na hili kusanyiko la wagawa maksi?”
“Haha.. nadhani unajua Tanzania bado ni nchi ndogo sana na mapungufu mengi kulinganisha na mataifa ya ulimwengu wa kwanza . Tunaweza kuimiliki Earth Axis lakini bado tupo dhaifu kuilinda na ndio maana tumekuomba vile. Ijapokuwa unaweza usijichukulie kama raia wa Tanzania , lakini wewe ni Mtanzania , au nakosea?”Aliongea na kumfanya Hamza kufikiria.
Muda ule alikumbuka Regina alikuwa pia na mpango wa kusafiri kwenda Ulaya mwezi ujao na kwasababu alihitaji kumsindikiza aliona sio mbaya kama atachukua muda wake kwenda kuhudhuria hilo kusanyiko.
Hamza aliona nchi ya Amerika haikuwa na utani kwenye kupigania maslahi yake na kama kweli wakichukua hatua watakaoathirika sio yeye bali wanawake waliokuwa karibu yake, ikiwemo biashara za Regina kwa ujumla.
“Basi kama ni hivyo utanitaarifu muda ukiwadia . Namaanisha nimekubali lakini sina uhakika nitakuwa salama..”Aliongea Hamza.
“Ili mradi ukijitahidi . Naamini hakutakuwa na tatizo kabisa . Hii ni msiheni ndogo sana ukilinganisha na misheni ulizofanya , ikiwemo ile ya Vita takatifu”Aliongea Afande Simba huku akiwa na tabasamu pana usoni na Hamza alipotaka kuongea Afande Simba aliingilia haraka.
“Kuhusu hili ombi letu usije ukasema lipo ndani ya mahitajio mawili mawili yaliobaki , hii ni ziada na usije kwenda kinyume na maneno yako”Aliongea na kumfanya Hamza kukuna kichwa na kujiambia hilo lizee kweli lina akili.
Muda huo Afande Himidu alirudi akiwa na wale wazee wafuasi wa Nyoka.
“Afande Simba , Bosi ! Kwanzia sasa hili swala limeisha . Mzee Sembe na wenzake hawana pingamizi tena”Aliongea Himidu.
“Oh! Mzee Sembe kweli umekubali hili lipite?”Aliuliza na Mzee Sembe na wenzake walimwangalai Hamza na macho ya heshima na wasiwasi kwa wakati mmoja.
“Bila shaka tumekubali yaishe lakini shukrani zetu zimwendee Mshauri mkuu kwa kuwa hiari kutuambia kuhusu Hamza … Kitendo cha kuwa maarufu kama alivyo Nyakasura nadhani ni swala la shukrani zetu kumuacha kwa ajili ya maslahi ya taifa . Lawama ni kwa Farook kwa kwenda kinyume na sheria na kusababisha kambi yetu kupata hasara kubwa”
Hamza mara baada ya kusikia maelezo hayo , palepale alimpiga Afande Himidu teke la makalio kwa kuwa mbeya.
“Himidu kwahio umewaambia kuhusu siri yangu sio?”
“Bosi sikuwa na namna ya kumaliza hili swala ndio maana . Lakini hata hivyo wameahidi hawatotoa taarifa ya chochote nilichowaambia . Lakini bosi wewe ni kama Kimulimuli gizani , huwezi kujificha kirahisi”Aliongea.
ITAENDELEA.
 
Thanks
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…