Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

Chimera.


Mvua ilikuwa ni kubwa mno ndani ya jiji la Paris chini ya anga jeusi, minunurisho ya mwanga wa taa katika maji ilikuwa imesambaa kila mahali. Jiji hilo la kimitindo na la mapenzi lilibadilika ghafla.


Pembezoni mwa Bar moja ambayo inauza vinywaji kama bia na mvinyo alionekana mwanaume alievalia nguo nyeusi akiwa amesimama na mwanvuli wa rangi nyeusi.


Alikuwa amevalia koti refu lililovuka magotini( Trench Coat) la rangi nyeusi na kofia ya hat rangi nyeusi pia. Ukiachana na mwamvuli alikuwa ameshikilia kibegi kidogo cha leather rangi nyeusi , na muda ule alonekana kufungua kibegi kile na alitoa kitu kama mfuko wa nailoni hivi ambao umetuna na kuutupia kwenye ndoo ya takataka.


Baada ya kufanya vile , palepale hakujali mvua iliokuwa ikinyesha kwani na mwamvuli wake alitokomea katikati ya nyumba mbele yake.


Dakika moja mbele alionekana kijana mzungu mwenye nywele zilizojikunja kunja akitoka katika ile Bar akiwa amevalia Aproni.


Alisogelea ndoo ile ya takataka bila wasiwasi na kisha alichukua ule mfuko na kuingia nao ndani ya Bar ile.


Zoezi hilo lilifanyika ndani ya dakika mbili tu na kwa giza na mvua iliokuwa ikinyesha , ilionyesha hakuna mtu ambae ameshitukia.


Lakini upande wa mbele katika jengo refu kulikuwa na mtu alieshikilia darubini akiangalia jambo lile kwa umakini mkubwa bila ya kutoa sauti yoyote.


*****


Nusu saa mbele katika makao ya muda ya kikosi cha Malibu ndani ya hoteli.


Mkurugenzi wa kikosi cha Malibu kwa masuala ya kigeni , Balozi Rajabu , alionekana akiwa ameketi mbele ya tarakishi mpakato, alikuwa akivuta sigara lakini umakini wake wote ulikuwa ni kwenye monita ya tarakishi hio na alionekana kufikiria kwa kina pia juu ya kile anachoangalia.


Balozi Rajabu alikuwa mlevi wa sigara ndio maana alichagua chumba cha peke yake ambacho kingemruhusu kufanya kazi huku akiwa anavuta sigara


“Ding Dong!


Mara baada ya Balozi Rajabu kusikia kengere ya mlango haraka sana alifunga laptop yake.


“Nani?” Aliuliza


“Balozi , nimekuletea chakula”Alikuwa ni Rehema sekretari na msaidizi wake, na baada ya kumtambua Rajabu alisimama na kwenda kufungua mlango.


Rehema alionekana kuchoka kwa namna alivyokuwa akitembea na mkononi alikuwa ameshikilia mfuko ambao ulionekana kuwa na vyakula.


“Pole Rehema kwa kutembea na mvua na asante”Aliongea Balozi Rajabu huku akipokea mfuko ule na tabasamu.


Rehema aliishia kufuta maji ya mvua usoni mwake na kutingisha kichwa na tabasamu hafifu.


“Usijali balozi , hata mimi nilikuwa na njaa”Aliongea huku akimuonyesha mfuko wake wa chakula pia.


Wawili hao hawakupenda chakula cha kifaransa hivyo walienda kwenye duka ambalo lilikuwa likiuza vyakula ambavyo vinaendana na radha ya kibongo.





“Basi sawa, kwasasa unaweza kwenda kupumzika maana hakuna kingine cha kufanya , tutaonana asubuhi”


“Sawa! Usiku mwema Balozi”Aliongea Rehema na kugeuka.


“Hebu subiri kwanza!”Aliongea Balozi mara baada ya kuona Rehema anatokomea nje.


“Kuna tatizo mheshimiwa!?”


“Hebu nenda kaangalie kama Mboma yupo kwenye hii hoteli , nipe taarifa baada ya kuhakikisha”


“Okey!”


Mara baada ya Rehema kutoka , Balozi aliweka chakula mezani na kuanza kula taratibu na dakika tatu mbele alipokea simu kutoka kwa Rehema.


“Vipi Rehema , yupo?”


“Chief Mboma hayupo , msaidizi wake Juma anasema ametoka tokea saa kumi na mbili kwenda kukutana na marafiki zake”


“Okey! Asante kwa taarifa , nenda kampumzike sasa”


“Sawa Balozi”


Mara baada ya simu ile kukatwa , Balozi alifungua tarakishi ile ya mapakato na kisha aliangalia kilichokuwa kikionekana na palepale alionekana kuingia katika fikra nzito.


******


Ndani ya chumba cha hadhi ya raisi katika hoteli ya Four Season , Regina mara baada ya kusikiliza mapigo ya moyo ya Hamza kwa muda , sura ilimjaa aibu.


‘Sitaki tena kusikia , unaongea sana ila sikuamini”Aliongea Regina


“Wife nilichoongea ni kweli , mimi ni mpiganaji na ni kawaida kuweza kudhibiti mapigo yangu ya moyo. Hata wakati ninapopambana na jeshi kubwa mapigo yangu hayabadiliki namna hii . labda tu iwe nimefanya mazoezi makali sana . Lakini nikikukumbatia na kukukiss nashindwa kabisa kudhibiti mapigo yangu ya moyo. Ni aina ya hisia ambazo zijawahi kuzipata tokea niwajue wanawake”


“Wewe umejuaje! Maana sio kama umekutana na wanawake wote kwenye dunia hii . Unajuaje pengine siku moja utakutana na mwanamke mwingine ambae anafanya mapigo yako yaende mbio”


“Ah! Unataka nikutane na kila mwanamke dunia nzima , ili kujihakikishia nani anayabadilisha mapigo yangu ya moyo . Si itakuwa ni kupoteza muda na kama ingekuwa hivyo basi watu wasingeoa na kuolewa”


“Ila mimi sijawahi kupenda hapo kabla , sijui hata mapenzi yakoje… najuaje kama unanipenda kweli?”Aliongea Regina na kumfanya Hamza kuishia kunusa harufu ya marashi ya nywele ya Regina.


“Hata mimi sijawahi, likija swala la hisia hakuna kipimo maalumu, hata mtu aseme mapenzi ni sawa na kujumlisha moja na moja na kisha kupata mbili, ukiuliza kanuni ya kuja na hesabu hio hutopata majibu . Kitu pekee ninachojua ni kwamba nikiwa na wewe hata kama unifokee , uwe na hasira za haraka na kununa siwezi kukuchukia , haijalishi upoje bado nakupenda. Unajua kumpata mtu unaempenda na anaekupenda ni kazi ngumu sana , kwanini unafikiria sana?”


“Jiangalie sasa ulivyokosa aibu , una wanawake kibao lakini unasema unanipenda , unaniona mjinga eh! Mimi najua umenioa kwasababu unajua mimi ni mjinga kati ya wanawake wote uliokuwa nao na ni rahisi kukubali kila unachofanya. Unajua fika kama ungewaoa wengine wasingekuvumilia”


“Wife wewe sio mjinga, una busara kubwa na IQ yako ni kubwa vilevile , kwanini uwe mjinga?”


“Mh! Lazima utakuwa unaniona mimi mjinga mtu rahisi kudanganyika na kukubali kila kitu”


“Wife kwanini unafikiria mbali hivyo , kama ni kweli kulikuwa na haja gani ya mimi kukuoa sasa?”


“Mimi sijui , lazima uliona kwasababu ya ujinga wangu sitokusumbua na kujihisi ni kama upo bachela tu”


“Unachofikiria sio sahihi mke wangu”


“Utajua mwenyewe , muda umeenda na nataka kuosha uso kuondoa makeup”Aliongea Regina akijiondoa kwa Hamza.


“Wife kwani umepaka make up! Mbona haionekani?”


“Wewe ni mjinga! Unadhani kwa sherehe ya leo ningeenda bila ya kujipodoa , huwezi kuona ndio lakini nilijipaka foundation kidogo ili macho yangu yaonekane vizuri. Macho yamenikauka sana , nitaenda kununua lensi nyingine nzuri ili yawe mazuri”Aliongea huku akifikicha macho yake na muda huol Hamza aliishia kucheka baada ya kuona Regina anataka kupendeza macho na lenzi.


“Wife unajua una macho mazuri sana, ni kama umechanganya damu ya mzungu na mwafrika kama mimi”


“Wewe mshenzi huaminiki! Unasema unanipenda lakini umeshindwa kujua nimepaka makeup. Hujali mwonekano wangu kabisa wewe , hebu toka chumbani kwangu kwanza”


“Wife ni kwasababu ya uzuri wako ndio maana sizingatii kabisa mabadiliko madogo”


“Kamdanganye mtoto wa darasa la tatu ndio atakuamini sio mimi”


“Kweli mke wangu , umejaliwa uzuri na silika nzuri, ukiachana na uzuri wako wa sura namna ulivyo tu inatosha kuwapiku wanawake wengi”


“Nilivyo kivipi?”aliuliza Regina.


“Mwonekano wako umegawanyika katika matabaka kadhaa ,yaani kawaida sio kawaida , ni kama upo katikati ya kila aina ya uzuri , ukivaa vizuri ndio unabadilika kabisa , Aura unayosambaza ni kama vile ni malkia kutoka falme ya kufikirika”


“Kadri unavyoongea ndio unavyoonekana muongo , unanisifia kama vile umekula asali, kwa taarifa yako siwezi kulainika kwa kuzidisha kunisifia,hebu toka kwanza nataka nioshe uso”


Hamza aliishia kujiambia moyoni , kwani amemzuia kuosha uso au ndio hivyo tu hataki kukaa uchi mbele yake , lakini alijua fika Regina hakutaka kutengeneza mazingira ya kugawa kitumbua chake.


“Wife usiku mwema , mimi naenda”.Aliongea Hamza huku akipiga hatua na Regina aliishia kumwangalia tu huku kwa namna flani akijisikia vibaya.


“Kesho sitoenda kazini” Aliongea Regina baada ya Hamza kufikia mlango na baada ya kusikia sauti hio aligeuka.


“Basi nitakutoa out kesho tukatembee!”


“Sawa! Asubuhi tutaongea vizuri. Uwe na usiku mwema”


“Na wewe pia mke wangu”


Hamza aliongea akiwa na furaha na kisha alitoka na kufunga mlango.


Hamza mara baada ya kutoka nje alijikuta akihema kwa nguvu , ukweli ni kwamba kipindi cha nyuma hakufikiria sana namna ya kuongea anapokuwa na mrembo , lakini ilikuwa tofauti na alipokuwa na Regina , alijitahidi akili yake ifanye kazi kwa kiwango kikubwa , Lakini hata hivyo aliridhika na namna alivyomsifia.


Hamza alijihisi ni kama amegeuka kichaa ambae anayafurahia maumivu Regina anayomsababishia, maana kadri Regina anavyomwekea ngumu na kumfanya ajisikie vibaya ndio alivyozidi kumpenda.


Hamza hakuwahi kuyafurahia mapenzi na ndio kwa mara ya kwanza alijihisi kupenda kweli, alijua alikuwa amependa kweli maana alivyokuwa akijisikia akiwa na Eliza na Dina ni tofauti sana alivyokuwa na Regina.


Ijapokuwa aliona sio haki kwa wanawake wengine kuchanganywa na mwanamke mmoja , lakini hakuweza kujizuia kufurahia hisia hizo.


“Haha.. nahisi huu ni ujinga ila napenda radha yake”Aliongea Hamza mwenyewe huku akijicheka.


Hamza alijiambia njia rahisi ya kumega tunda ni kuharakisha zoezi la kumchumbia Regina , lakini aliona zoezi hilo lazima lifanyike kitaalamu zaidi. Vinginevyo matokeo yanaweza kuwa tofauti kwa mrembo huyo.


Wakati akiendelea kufikira , bila kujijua alikuwa ashafika kwenye mlango wa chumba chake na kabla ya kupitisha kadi alihisi kuna mtu alikuwa amefika kumtembelea na aliishia kutoa tabasamu la kifedhuli na kisha bila kujali chochote alipitisha kadi na kufungua mlango na kuingia ndani.


Mara baada ya kuingia ndani aliweza kuona kivuli cha mtu kikiwa kimekaa kwenye kiti dirishani. Mtu huyo nywele zake ndefu zilikuwa zimefunika uso wake na mavazi yake machafu yalionekana kuloa na maji ya mvua.


“Aah! Mchafu ya nini kuja kwenye chumba changu usiku wote huu kuniogopesha”Aliongea Hamza akijifanyisha kushituka baada ya kuwasha taa.


Alikuwa ni Asmuntis , kama ninja namba moja duniani kuingia katika chumba kama hicho bila ya kuwa na ufunguo ilikuwa ni rahisi sana kwake.


“Bosi , uko sawa!”Aliuliza Asmuntis huku akiruka kutoka kwenye kiti.


Hamza aliishia kutoa tabasamu na alisogea mpaka kwenye kimeza na kutoa sigara kwenye pakti na kumpatia Asmuntis na kisha alimsaidia kuiwasha.


“Naona umenitembelea usiku usiku?”Aliongea Hamza muda huo akiwasha ya kwake sigara na kufungua mlango wa kutokea kwenye balkoni na wote waliangalia upande wa nje ya jiji.


“Nani mwingine kajua kuhusu mimi?”Aliuliza Hamza , haikuwa na haja ya kuuliza kwanini Asmuntis amefika hapo.


“Ni watu wa Metal Tide. Inaonekana Gonzalez amekosa uvumilivu wa kutaka kupata cheo cha Ugwiji. Isitoshe vikao vya magwiji ni adimu sana kama hivi , nadhani anataka kutumia nafasi hii kuthibitisha mbele ya watu wote kwamba ana hadhi ya kuwa katika orodha ya magiwji kumi wa dunia”


“Kama ana shida sana na cheo hicho ningemwachia tu , kulikuwa na haja ya kutuma watu kunijaribu?”


“Bosi hatuwezi kuruhusu Gonzalez kuchukua cheo cha hadhi yako . Hata kama umepoteza uwezo wako wa nishati , sisi tupo . Inferno ni jamii iliokamilika, wewe ndio uliotutoa kutoka kuwa Clubs na kuwa umoja. Nimekwisha kuwasiliana na Azzle, tutakusindikiza kwenda kuhudhuria kilele cha magwiji . Muda ukiwadia tutakuwa chini ya maagizo yako na kupigana kwa ajili yako. Hatuwezi kumruhusu Gonzalez kushinda”Aliongea Asmuntis akiwa sirasi mno.


“Pepo mchafu , nashukuru sana kwa kunijali . Kwa muda mrefu nilikuwa nikidharau sana hiki cheo , ila kama ndio hivyo basi nipo tayari kuwakaribisha wakibisha hodi. Ukweli mpango wangu ni kustaafu moja kwa moja katika ulimwengu wa siri na kuishi kama binadamu wa kawaida anaeonekana na mke wangu na wapenzi wangu na mengine yatajidhihirisha yenyewe. Malengo yangu mengine ya kimaisha ni kumuamsha malaika , kuhusu mengine yote sitaki kuyazungumzia”


“Bosi bado tu hujamkatia tamaa Malaika?”Aliuliza Asmuntis akiwa amekunja sura.


“Ndio! Ni swala ambalo siwezi tu kuliacha. Nimekuja kugndua kupitia Earth Axis ambayo serikali ya Tanzania imeshikiria , kuna tumaini kubwa la kumuamsha malaika na hata kumfahamu mzee. Ndio maana nimekuwa na ukaribu na kitengo cha Malibu”


“Bosi Kama kweli Malaika ataamka , ataweza kukulinda kwa hakika na unaweza kupata majibu ya maswali yako mengi” Aliongea na Hamza alitingisha kichwa.


“Angalau leo mchafu umeongea vizuri. Halafu vipi kuhusu huyu msichana wetu.. nini kimetokea juu ya hii mbinu ya Hundred Shadow?” Asmuntis mara baada ya kusikia kauli ile macho yake yaliwaka.


“Ametumia hundred Shadows?”


“Usiwe na wasiwasi , kaniambia nisikwambie lakini mimi na wewe hatuna haja ya kufichana ndio maana nasema sasa hivi mbele yako. Yule ni kama mdogo wangu wa kike hivyo nataka kumsaidia , hivyo kabla sijachukua hatua nataka kusikia kutoka kwako na mtazamo wako juu ya mbinu hii ya hundred Shadows”.


“Bosi ukweli mimi niliishia kumfundisha tu , lakini kuhusu uwezo aliopata sina uhakika kama unatokana na mbinu yenyewe , ni kama vile ni kitu ambacho amezaliwa nacho”


“Duh! Unataka kumaanisha nini? Mbona hata mimi sijui . Hundred Shadows ni mbinu ya kumuwezesha mtu asionekane katika macho ya kawaida , lakini alichopata kupitia hii mbinu ni spidi kubwa kitu ambacho ni ngumu wewe kumfundisha. Hebu niambie unachojua kuhusu chimbuko la Rhoda kwa ujumla”Aliongea Hamza.


“Wakati nilivyomuokota na kuamua kumlea . hakuwa akikumbuka wala kuelewa chochote zaidi ya jina lake tu. Miaka kadhaa iliopita baada ya kufikia daraja la juu la mafunzo nilimpa ruhusa ya kufuatilia chimbuko lake. Baadae alikuja kujua ufunuo aliopata baada ya kufika levo ya nafsi, ilikuwa ni asili ya ufunuo uliokuwa ukifundishwa katika shule moja iliofahamika kwa jina la Night Shadows. Ajabu ni kwamba watu ambao walikuwa wakivuna nishati kwa ajili ya kugeuka vivuli, kambi yao imeteketezwa yote na mtu ambae alitumia shambulizi la radi na inaonekana katika shambulizi hilo ni Rhoda peke yake alisalimika mpaka mimi kuja kumuokota na kumwasili”


“Unasema wanafunzi wote wa mafunzo ya Black Shadows waliuliwa?”


“Ndio na muuaji alitokea nyakati za usiku wa mvua kubwa kama hivi na hakujulikana ni nani. Mama yake Rhoda pengine alikuwa ni ninja na pengine ni yeye aliemuokoa”


“Lakini bado mpaka sasa nina swali , kwa nilichosikia kutoka kwa Rhoda ana asili ya ki Afrika na Ugiriki , ilikuwaje ukamuokota Japani?”Aliuliza Hamza.


“Hata mimi nilijiuliza hivyo mwanzo! Ila baada ya kufuatilia kwa umakini niliweza kupata habari za biashara ya viungo iliokuwa ikiendelea kutoka bara la Asia na Afrika , wanawake wengi kutoka Afrika walikuwa wakisafirishwa kwenda Asia. Pengine mama yake alikuwa ni moja ya Wa afrika waliongizwa Japani”


Hamza hatimae aliweza kuelewa mbili tatu , ndio maana Rhoda alikuwa akikwepa kuongea kuhusu chimbuko lake.


“Inawezekana , ndio maana wakati unamuokota alikuwa mdogo sana, lakini spidi yake ya kuvuna nishati ni kubwa sana kiasi cha kunishangaza”


“Bosi kuna swala lingine pia sikukuweka wazi, pengine ndio linalochochoa uwezo wake wa kuvuna nishati”


“Swala gani?”


“Rhoda ni Chimera”


“Chimera! Unamaanisha ana wazazi watatu?”Aliuliza Hamza kwa mshangao. Kama mtu mwenye mafunzo ya utabibu alikuwa akijua nini maana ya Chimera au Chimerism , mtoto ambae anakuwa na baba wawili kwa wakati mmoja , ni binadamu adimu sana wa namna hio ambae hutokea baada ya mwanamke akiwa katika siku za hatari kuzalisha mayai mawili kwa wakati mmoja kutoka katika ovari zake na hayo mayai hutungishwa na mbegu za wanaume wawili tofauti na baadae ya hapo mayai hayo huungana na kutengeneza mtoto mmoja na kumfanya mtoto kuwa na vina saba vya wanaume wawili kwa wakati mmoja , ukijumlisha na Mama anakuwa mtoto mwenye wazazi watatu. Mtoto wa aina hio huitwa Chimera.


Kwa lugha nyepesi unaweza kumpima Rhoda vinasaba vya damu kwa kulinganisha na vya Hamza akafanana kwa asilimia kubwa na ukapima damu yake tena kwa kulinganisha na Asmuntis pia ikaonyesha ni baba yake, japo pia inategemea na aina ya kipimo.


“Ninachomaanisha bosi ana chimbuko la watu wa damu ya Aikido , pengine ndio maana spidi yake ya kuvuna nishati ni ya juu sana”Aliongea Asmuntis.


“Inawezekana pia , ukijumlisha na changamoto alizopita , moyo wake umejaa moto , pengine ni wa kisasi ya juu kilichotokea.”Aliongea Hamza.


“Nadhani pia linaweza kutokuwa swala zuri , kuna hisia zinaniambia pengine mtu ambae alihusika na kuimaliza kambi hio , sio mtu wa kawaida kudili nae”


“Haha , mara nyingi ikifikia hatua kama hii , wewe kama mwalimu huna chakufanya zaidi ya kumwelekeza mwanafunzi wako nini chakufanya”


‘Sidhani kama anaweza kupokea maelekezo yangu , mimi namjua vizuri”


“Basi sawa , tutaongelea kuhusu hili vizuri . Vipi kuhusu taarifa juu ya watu tuliowaweka kufuatilia wanajeshi wa kitengo cha Malibu?”Aliuliza Hamza.


“Ni kama ulivyotea bosi , mtu ambae ulimshuku anaonekana kuwa tatizo lakini kuna zaidi ya watu wawili ndani ya Malibu ambao wana matatizo”


“Ni hivyo , basi napaswa kukusikiliza kwa umakini ..”


*****


Katika anga moja , kulikuwa na jengo kubwa lenye bango kubwa la chuma ambalo limebandikwa juu kabisa ya jengo hilo.


Bango hilo la chuma lilionekana kama la pembe sita lenye mchoro wa ishara ya dhoruba.


Sehemu hio ndio yalikuwa makao makuu ya kundi la kimasenari kwa nchi ya Mafuvu maarufu kama Metal Tide. Katika Command Room alionekana jitu kubwa la miraba minne na urefu wa mita mbili akiwa amesimama mbele ya dirisha akiwa amevalia koti.


Ingawa ngozi ya nguo zake ilikuwa imefunika mwili wake vyema , lakini haikutosha kuficha namna misuli ya mwili wake ilivyotuna.


Mtu huyo ndio mwanzilishi wa kundi hilo la kimasenari la Metal Tide. Alikuwa pia ni mtaalamu wa kimapigano ambae alikuwa akikaribia kuingia katika daraja la Ugwiji, Aliitwa Jitu Chuma au Gonzalez.


“Kwahio unasema mwanzo mwisho mtu aliezuia mashambulizi ya kumuua Lucifer ni Black Fog?”Aliuliza mtu huyo kwa sauti ya chini.


Nyuma yake alikuwa amesimama mwanaume na mwanamke. Walikuwa ndio viongozi wakubwa wa kundi hilo , watu ambao Hamza alikutana nao yaani Helena na Gray.


“Ndio, Kapteni. Nadhani sio suala la kawaida kwasababu kwa kile nilichoona Lucifer hakushituka kabisa”


“Halafu pia tumeweza kugundua maninja kutoka Baffodil wameingia mjini . Makisio yetu ni kwamba wapo kwa ajili ya kumpa ulinzi Lucifer”Aliongea Gray.


Gonzalez aligeuka na misuli mingi ilionekana katika uso wake kama vile ni mizizi ya mti uliozeeka.


“Kipindi kile baada ya Lucifer kuondoka , nilijua tu kuna kitu hakipo sawa . Kimsingi baada ya kumuua Mr Black angejitokeza hadharai kupata sifa zake , lakini akaamua kwenda kujificha , ili nichanganya na kuona ni mtu gani ambae ana sifa nyingi namna hii kuamua kwenda kuishi maisha ya kawaida? Lakini naona yote haya ni kwasababu hana nguvu yoyote iliobakia katika mwili wake. Sasa mtu hana nguvu na anajaribu kutaka kushiriki katika Baraza la maksi. Hizi ni dharau na sisi Metal Tides hatuwezi kuchukulia hili kiwepesi .


Nataka kuona nani atasogelea kundi letu baada ya kuwatia uvilema mashetani wote wa Inferno! Natamani kuona namna watu watakavyoniangalia baada ya pambano”


“Hongera sana Master , hatimae ndoto yako ya kubeba cheo cha hadhi ya nyota kumi , inakwenda kutimia”Aliongea Helena na Gray huku wakiwa na msisimko wa hali ya juu sana kwa kiongozi wao.


Muda ule mwanga wa radi ulitokea na kufanya sura ya Gonzalezi iliofunikwa na giza kuonekana , alikuwa katika tabasamu la uovu na halikumlenga mtu mwingine bali Hamza.


******


Saa tatu kamili za asubuhi Hamza na Regina walimaliza kupata kifungua kinywa na kuanza safari ya matembezi kuzunguka jiji hilo la Paris.


Hamza alikuwa mzoefu wa jiji na alikuwa akijua historia ya maeneo mengi , hivyo alikuwa kama tour guide kwa siku hio na uwezo wake wa kuongea kifaransa ulimpa maksi nyingine.


Mara baada ya kufika katika Eiffel Tower , waliweza kuona wapenzi wengi wakipiga picha , hivyo na yeye alitoa simu akitaka kupiga picha na Regina.


“Wife ngoja tuweke kumbukumbu”Aliongea Hamza huku akimshika Regina bega na kuanza kupiga selfie , lakini Regina alionekana hataki.


“Wewe hujui kupiga picha vizuri, unanifanya naonekana mbaya”


“Mke wangu kwa uzuri wako huo , unaogopaje kupiga picha? Vipi kufanananisha na hawa wengine ambao ni wakawaida lakini wanajitahidi kuonekana wazuri?”


Hamza hakujali ubishi wa Regina na alimshika kwa nguvu na kuanza kupiga selfie za kutosha.


Muda huo , mwanaume alievalia katika mavazi ya mtindo wa mpiga picha aliwasogelea , akiwa na tabasamu pana usoni.


“Excuse me, may I bother you two for a few minutes?”Aliongea yule mwanaume kwa lugha ya kingereza , huku akiwaangalia Regina na Hamza.
 
Hamza alishangaa kidogo baada ya bwana huyo kuwasogelea.


“Ndio mkuu , kuna tatizo?”Aliuliza.


“Mimi ni mpiga picha wa jarida maarufu la mitindo hapa Paris. Jarida letu linahusisha utoaji wa ripoti juu ya watu waliopendeza zaidi kwa wiki ndani ya Paris. Nimeona huyu mwanadada mrembo mbele ya Eifell tower na kudhania macho yangu yananidanganya kwani ni kama kiumbe kilichoshushwa ghafla , hivyo nauliza kama naweza kuchukua picha zake kadhaa. Msiwe na wasiwasi picha hizi hazitotumika kwa ajili ya matangazo ya kibiashara na pia jina lako litafichwa ili tusivunje faragha yako”


Regina mara baada ya kusikia maelezo hayo alishindwa kujizuia aibu kumshika . Ingawa ameitwa sana mrembo tokea akiwa mdogo lakini sio kama kiumbe alieshushwa kutoka angani tena katika ardhi ya ugenini.


“Ni wapi picha hizi zitatumika katika jarida lenu?”Aliuliza Hamza


“Ni mbele ya jarida , lakini vilevile katika mitandao yetu ya kijamii na ofisi za maonyesho”


“Sasa kama mkichukua picha ya mke wangu si itawavutia watu wengi na maana yake mtapata trafiki kubwa , ambayo huleta hela , kuna utofauti gani na kufanya biashara?”Aliuliza Hamza akiwa hajaridhika.


“Sir kwa kusema hivyo hatuwezi kupinga pia . Lakini jarida letu linadili zaidi na wanawake warembo na hatuwezi kuchukulia swala hili kwa namna ya kujinufaisha”Aliongea na Hamza aliishia kumwangalia Regina.


“Wife , vipi unataka kupigwa picha na kuonekana kwenye jarida lao?”


Regina alikuwa na aibu sana kupiga picha ndio maana hata mtandaoni hakufahamika sana , sasa inawezekanaje apigwe picha kwa malengo ya fasheni kwa ajili ya kuonekana katika jarida.


Lakini Regina aliona kama angekubali kupigwa picha katika mazingira kama hayo itakuwa ngumu kusahaulika na pia ingekuwa nzuri zaidi.


“Sioni shida kupiga”Aliongea Regina baada ya kusita kidogo na Hamza alitingisha kichwa kukubaliana nae.


“Vipi utampatia mke wangu hela , namaanisha hela za umiliki wa picha yake?”


“Sire , tunachokifanya ni kama interview ya mtaani , itakuwa ngumu kuweza kulipa hela kila tunaeomba kumpiga picha. Kama dada atakataa kupigwa picha hatuwezi kumlazimisha pia”


“Yaani hamtaki kunipa hata shilingi , halafu mnataka kumiliki picha ya mke wangu ? Mnaniona mjinga , kwanini niwagawie mke wangu bila sababu?”


Regina alijikuta akichizishwa na maneno yake na kujiuliza huyu mtu anaongea nini ? Alishindwa kujizuia na kumfinya Hamza kiunoni.


“Wewe unaongea ujinga gani? Kupiga picha kunafanana vipi na kunigawa?”Aliongea na kumfanya Hamza kucheka.


“Ndio hivyo , sitaki mtu mwingine akuone kila siku , mimi peke yangu ndio mwenye kigezo cha kukuona wewe kila siku”Aliongea.


“Wewe , mbona unakuwa kama mtoto” Regina hakujua anune au afurahi, lakini moyo wake ulijaa utamu.


Cameraman yule aliishia kutingisha kichwa chake kwa masikitiko na kisha aliaga na tabasamu baada ya kukataliwa.


“Ipo hivyo , wewe ni wa kwangu na nitakuwa kichaa kuacha wanaume wengine waangalie picha yako kila siku”


“Yule ni msanii wa picha tu , kwanini unafikiria mbali. Jitu kubwa lakini una mawazo ya kitoto”Aliongea Regina akitingisha kichwa kama kujutia kukosa nafasi ya kupigwa picha.


“Nilitaka kupata picha moja nzuri , angalia ulizopiga zilivyo mbaya”


“Basi kama ni hivyo nitaenda kutafuta mtaalamu wa hali ya juu wa kupiga picha. Lakini mke wangu picha yako itawekwa nyumbani tu ili mimi niwe naingalia mwenyewe vinginevyo nitashikwa na wivu eti” Regina alishindwa kujizuia na kucheka.


“Wewe umekuwa mtoto kweli na vituko vyako.. nishakata tamaa sitaki picha tena”


“Haha.. mke wangu labda utakuwa hujasikia tu , Mwanaume siku zote ni kama mtoto mbele ya mwanamke anaempenda. Mwanaume akiwa hakupendi mbingo zake zitakuwa ni za kibaba baba tu. Hivyo mke wangu nipo hivi kwasababu nakupenda kutoka uvungu wa moyo wangu”


“Lione, sitaki kukusikia tena . ninunulie basi kitu chochote kitamu cha kula”


“Sawa mke wangu , ngoja nikupeleke ukale kitu utakachopenda”


Hamza alimchukua mrembo wake na kununua vitu na kisha walienda kupanda kwenye Ferris Wheel. Ijapokuwa hawakuwa na mengi ya kufanya pamoja , lakini kuwa kama hivyo , kama wapenzi wa kawaida iliwafanya ukaribu wao kuzidi kuongezeka.


Baada ya kutumia siku nzima kutembea na kucheza kama wapenzi Hamza alimuaga Regina kwamba siku tatu zitakazofuatia kuna vitu anaenda kufanya hivyo hatoweza kuwa nae.


Regina hakuhitaji maelezo mengi kujua Hamza anaenda kufanya nini , alikuwa na vitu vingi ambavyo hakuwa akijua kuhusu Hamza hivyo aliishia kumkubalia. Walikubaliana tu akisharudi huko anakoenda wataanza safari ya kurudi Tanzania.


Hamza upande wake alijua hatokuwa na muda wa kununua zawadi , hivyo aliingia mtandaoni na kuchagua vitu vingi kama zawadi na kumtumia Mzee Pino kuviandaaa kwa ajili ya Eliza, Yulia na Dina.


Wanawake hao watatu walikuwa ni warembo wake , kuhusu Prisila alimchukulia kama mdogo wake na Irene kutokana na bado kuwa mwanafunzi aliona asimpatie zawadi maana atamfanya azidi kuchizika.


Muda huo Hamza alishindwa kujizuia na ghafla tu mawazo juu ya Yonesi yalimvaa palepale. Kama bado angekuwa na mawasiliano na mrembo huyo angemnunulia pia zawadi.


*****


Ni ndani ya mji mdogo unaofahamika kwa jina la Limours , uliokuwa kusini Magharibi mwa jiji la Paris , uliozungukwa na vilima vidogo vidogo vyenye msitu.


Ni sehemu ambayo ilikuwa na utulivu mkubwa na mahali ambapo ni rahisi kuficha siri kwa watu wa ulimwengu wa nje. Hivyo Baraza la maksi lilipangwa kufanyikia katika mji huo.


Eneo la uwanja wa ndani wa mpira wa miguu , ndio mahali ambapo paligeuzwa kuwa Venue kwa ajili ya Set Conference.


Katika siku hizo , kwa watu wote ambao walifika nchini Ufaransa kwa ajili ya kushiriki baraza hilo la maksi walikuwa wamejazana katika mji huo wa Limour , karibia katika kila hoteli na gesti zote.


Kulikuwa na wanajeshi wengi pamoja na polisi ambao wametumwa na serikali kwa ajili ya kutoa ulinzi ili kuepusha machafuko.


Hamza sasa alifika ndani ya mji huo akiwa ametangulizana na Asmuntis na Black Fog kupitia gari aina ya Hummer.


Watu wa kawaida walipangiwa kuishi katika hoteli kwa kipindi chote cha baraza hilo lakini ilikuwa tofauti kwa Hamza. Watu wake wasingemruhusu kukaa hotelini na watu wa kawaida hivyo walikodisha nyumba nzima kando ya shamba.


Ukweli ni kwamba Magwiji wakubwa kama wangejitokeza ama kufahamika mbele ya watu wa kawaida ingeleta msisimko na aina flani ya ukinzani. Hivyo hoteli haikuwa maeneo sahihi kwao kuishi.


Mara baada ya kufika katika nyumba iliozungukwa na shamba kubwa la Farasi , ijapokuwa eneo lilikuwa limejitenga lakini lilikuwa limeboreshwa ulinzi wake kwa teknolojia ya hali ya juu na kulikuwa na vyanzo mbalimbali vya starehe.


Ndani ya uzio wa shamba hilo kulikuwa na magari kadhaa ya kifahari yaliokuwa yameegeshwa. Ikionyesha mtu ambae sio wakawaida alikuwa ametangulia kufika.


“Bosi nasikia sauti ya kugongelea chuma”Aliongea Asmuntis wakati akitoka nje ya gari.


“Hata mimi pia , ngoja tukajionee huyu mhunzi ni kitu gani anatengeneza tena”Aliongea Hamza.


Mara baada ya kuzunguka nyuma ya banda la Farasi , waliweza kuona mwanaume akiwa ndani akigongelea chuma na nyundo kubwa.


Kipande cha juu cha mwili wa mwanaume huyo kilikuwa cha rangi ya kahawia na misuli mikubwa iliotuna iliweza kuonekana. Kila msuli ulionekana kuwa mgumu kama jiwe.


Alikuwa na nywele fupi zilizojikunja kunja, alikuwa ametoboa masikio na kuvalia heleni kubwa za dhahabu.


Dang , Dong , Clang!


Sauti hio ya kugongelea chuma , ilikuwa ni kama inatoka kwa mpangilio maalumu wa kutengeneza mziki.


Mara baada ya kumuona mwanaume huyo wa mita moja na nukta tisa , midomo ya Hamza na Asmuntis ilicheza kwa kuonyesha tabasamu.


“Uncle Azzle , kwanini kufika tu unaanza kugongelea chuma?”Aliongea Black Fog


Mwanaume huyo wa rangi ya zambarau alikuwa ni Azzle mkuu wa kundi la Kimasenari la Barhams, Maarufu kama Ares of Arabian Peninsula.


Azzle mara baada ya kugeuka na kumuona Hamza , haraka sana aliweka kile chuma kwenye dimbwi la maji.


Siziiiii! Mvuke wa maji ulipanda ukipoza chuma kile na palepale aliweka nyundo yake chini na kisha alishuka chini na goti moja huku akiweka mkono kifuani.


“My Prince!”


Alimsalimia Hamza kwa mbali na kisha akasimama na kumwangalia Asmuntis kwa macho makali.


“Wewe Mtu mchafu kwanini umechelewa kumleta bosi hapa?”


“Kwahio kama nimechelewa inakuhusu nini? Bosi alipaswa kuwa na shemeji yetu kwanza”Aliongea Asmuntis.


“Oh Tena nimekumbuka , bosi mbona simuoni shemeji?”Aliuliza Azzle.


“Wewe mzee wa Stroke , unavyoongea tu ni kama mzimu uliofufuka , halafu unataka nije na mke wangu, Unataka umtishe? Ni muda mrefu tokea tuonane mara ya mwisho nipokee hata kwa kicheko basi”Aliongea na kumfanya Azzle kutabasamu.


“Bosi nilijizuia tu , ila jana nilitaka kuja Paris kukutafuta , lakini baada ya kufikiria nikaona nije hapa mapema kuona maandalizi yakoje. Ni Berrly alieagiza hii sehemu iwe wazi kwa ajili yako , si unajua alivyo mvivu ndio maana nikaona nijihakikishie. Unapenda kuendesha Farasi ndio maana na kutengenezea viatu hapa”Aliongea.


“Ni lini nilikuambia napenda kuendesha farasi. Nakumbuka ilikuwa ni miaka sita iliopita tukiwa Argentina Pampas Height, kipindi kile niliendesha farasi sio kwasababu napaenda bali ni kwasababu nilikuwa nikifukuzia mtu nilietaka kumuua”


“Ni kwasababu bosi wewer ni tajiri tayari hivyo sijui ni kipi naweza kukupatia kama zawadi , nimeona kutengeneza horseshoes itakuwa na maana zaidi” Hamza mara baada ya kuona jitu siriasi namna hio linataka kumfurahisha aliguswa.


Washikaji zake ambao alikuwa nao kwa muda mrefu , wengi wao wanaishi kwa kuamini wana deni kubwa kwake na kila siku wanajribu kutafuta namna ya kumlipa.Lakini ukweli ni kwamba kuweza kuishi katika ulimwengu wa giza na kufanikiwa ni swala la kutegemeana.


Hivyo Hamza hakuwahi kuwaza mafanikio yake yametokana na uwezo wake pekee bali ni kwasababu ya kuwa na marafiki wengi. Hivyo hata baada ya kustaafu na kuachia maeneo aliokuwa akiongoza wayasimamie wao hakujutia wala kujisikia vibaya.


“Wewe Mhunzi nashukuru sana unaonekana kunijali lakini haijalishi kama napenda kuendesha farasi au lah . Ila kwasasa nataka tukae chini na tupate kinywaji pamoja na kupiga stori . Naamini umekuja na mvinyo mzuri , maana mpaka kuwa Mshauri mkuu wa mfalme naamini wanatumia hela zao za mafuta kukulipa vizuri”


“Bosi niseme tu ukweli sijaja na mvinyo wowote , Berly pia ni mbahiri mno sijaona mvinyo wowote hapa , ngoja nimpigie mtu simu atuletee..”Mara baada ya kuongea , sauti nyingine ilisikika kutoka chini.


“Pumbavu zako Azzle , ushaanza kunisnitch tayari kwa bosi.Mimi Berly naweza nisikupe wewe wine lakini mimi ni mtiifu kwa bosi wangu na nimemuandalia kitu roho inapenda. Huko ardhini nina chumba kizima cha mapipa ya wine kama haya, sikutaka kukuonyesha mlevi kama wewe”Aliongea huku akiwa ana kohoa mfululizo , akiwa anatoka ndani ya eneo la chini kama shimo, ilionekana eneo hilo lilikuwa na vumbi mpaka kumfanya kukohoa.


Berly alikuwa ndio mwanaume mtanashati kuliko wenzake wote , alikuwa amevalia shati la maua maua na cheni shingoni , huku nywele zake akiwa amezisuka. Muda huo alikuwa amebeba pipa la kuozeshea mvinyo na haraka sana alilitua chini na kumsogelea Hamza na kumkumbatia.


“Bosi , hatimae umefika. Nilikumisi sana. Katika miaka mitatu yote nilikuwa nikikuota wewe tu . Hatimae nimekuona tena”Aliongea huku akiwa amemkumbatia lakini Hamza aliimshia kumsukuma


“Hebu acha kuniganda kama mwanamke”Aliongea Hamza.


Berly alikuwa tofauti sana , ilikuwa ngumu kuamini alikuwa akijihusisha na ulimwengu wa giza, katika ulimwengu wa nje alikuwa ni msanii , DJ na Playboy ambae maisha bila kuzungukwa na wanawake hayaendi. Alijua sana kuhonga na kila jiji alilopita aliacha alama.


Kubwa zaidi ni kwamba alikuwa na ushawishi mkubwa sana katika tasnia ya mziki , watu wengi alikuwa akifahamiana nao na alikuwa hata na ushaiwshi wa nani apewe tuzo na nani asipewe na hio ilimfanya kuwa maarufu sana.


Ukiachana na kuimba hakuwa na kazi maalumu , alichofanya siku nzima ni kula bata kwenye mayatcht ya kifahari na kupiga milegezo. Hakujali kabisa swala la mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi na ilikuwa ngumu kuamini mtu kama huyo alikuwa na ukaribu na Hamza.


Lakini alikuwa mtu muhimu sana kwa Hamza , anaweza asiwe na nguvu ama na uwezo kama Asmuntis , lakini kipindi alipokuwa na Hamza alikuwa ndio mtu pekee aliekuwa akiongoza kwenye vita ya maneno , alikuwa na kipaji cha kuongea na mtu yoyote na akakubali kile anachomwambia , hivyo alifanikisha mambo mengi kwa ajili ya Hamza.Lakini mbaya zaidi aliatumia uwezo wake wa ushawishi kuwakopa wenzake.Alikuwa anakula bata kwa kukopa marafiki zake.


“Bosi usinilaumu wakati wewe ndio uliniacha mwenyewe , nina picha yako nyumbani na muda wote naingalia kila nikikukumbuka . Kuna muda mwingine hadi nalia’


“Tangu lini ukawa na nyumba ya kuamkia kila siku wewe, Si unaamkia mahotelini na kwenye maboti wewe. Imepita miaka mingi lakini tabia yako ya kudanganya hujaacha tu”Aliongea Hamza huku asijue acheke ama alie.


“Bosi nilipomuambia atukodishe hili shamba , aliniambia tumlipe Euro milioni mbili. Jamaa ni mbahiri sana kwa sisi washikaji zake ila mbele ya mbususu anakuwa kama chizi kwa kuhonga tena kwa hela zetu”


“Azzle acha kunisnitch , ndio maana muda wote unanuka mafuta ya taa na petroli. Niliemkodisha shamba kaniuzia na mvinyo , kuomba Euro milioni mbili unaona nyingi sana?”


“Nakudai Dollar milioni mia moja zangu , ulizonunulia private Jet. Nakupa mwaka mmoja , usiponilipa nitayafanya maisha yako kuwa magumu”Aliongea Azzle.


“Wewe Mhunzi , kwanini unashindwa kujali ushikaji wetu. Bosi ashawahi kusema upendo na haki ni zaidi ya thamani ya dhahabu. Hela kidogo hio ila makelele meengi”Aliongea Berly kwa sauti


“Berly hata mimi nimekumbuka nakudai dolla milioni moja na hamsini, mimi nirudishie tu milioni mia , zinazobaki nimekupunguzia”Aliongea Hamza.


“Bosi mimi ni shabiki wako namba moja , kwanini unanikandia? Nyie wote naona hamtaki niwe na amani . Yaani nimewatafutia eneo zuri kama hili kwa ajili ya kukutania baada ya kunipa shukrani mnaanza kunidai madeni. Hela zote hizo natoa wapi , sijui kupigana , sijui kuuza siraha , sijui kuua watu , ninachojua ni kuwakopa tu bila kujua namna ya kulipa”Aliongea huku akijitilisha huruma na kuigiza alikuwa akilia huku amekaa chini kama mtoto.


Baada ya kuona anachokifanya Berly iliwaacha midomo wazi na walishindwa kujizuia na kucheka.


“Mnanifanya hata binamu yangu Roda ananidharau . Kuna haja gani ya mimi kuendelea kuishi , sina thamani kabisa hata ya kuwa mbele yenu na bosi ..”Aliongea kama mkiwa.


“Bosi mbona kuna makelele mengi huko ndani , mnamfanya nini huyo mwehu. Hebu tokeni kwanza huko ndani mje tucheze raundi boja la sivyo Leviathani ataniua kwa kipigo”


Mara baada ya kusikia sauti hio , kila mmoja alijua ni nani na palepale waligeuka na ndio muda walioweza kumuona mwanaume bonge kama Rickross akiingia


Boss!


Mwanaume huyo mwenye mwili mweusi alitembea huku akitawanya upepo na kwenda kumkumbatia Hamza.


Kama Hamza asingekuwa na nguvu angedondoka nae chini maana sio kwa uzito huo.


“Mameni kila ulipo unawaza kucheza kamari tu , utaacha lini?”Aliongea Hamza huku akicheka.


Mameni ukiachana na kuwa Taikuni wa kuuza siraha , lakini vilevile alikuwa ni mlevi mkubwa wa michezo ya kamari na kubeti.


“Ndio kitu kinachonipa furaha, hili eneo lilivyokauka kamari ndio starehe pekee iliobaki”aliongea huku akicheka


“Twendeni zetu tukacheze , Azzle huna haja ya kuendelea kutengeneza hicho chuma”Aliongea Hamza na Azzle alikubali.


Mara baada ya kuona kila mtu anaondoka bila kujali huzuni yake , Berly aliekaa chini alianza kulia tena.


“Bosi vipi kuhusu mimi! Unanitelekeza masikini kama mimi”


“Njoo na hio pombe”Aliongea Hamza na kumfanya Berlly furaha kumvaa na haraka haraka aliinuka na kubeba pipa lile.


Wote walitembea na kwenda kuingia katika nyumba iliokuwa katikati ya shamba hilo , kwa nje haikuwa nzuri sana , ila ndani ilikuwa imepambwa vizuri tu na kupendeza.


Katika eneo la Dining kwenye meza ndefu alionekana Leviathani akiwa amekodolea macho kararata.


Mara baada ya kumuona Hamza akiingia Leviathani haraka haraka alisimama na kumpa Hamza heshima yake.


“Wewe ngiri kwanini unang’ang’ania kucheza na Mameni! Unaishi baharini halafu unataka kumfunga?”


“Sikutaka kukubali ndio maana nikampiga, kwanini kila saa yeye ndio anashinda tu” Hamza muda ule aliweza kuona Leviathani alikuwa amenyoa kipara na alishangaa.


“Wewe Ngiri hicho kipara umekitoa wapi kwanza?”


“Haha.. binti yangu anasema rasta zangu zinamuumiza kila ninapomkumbatia ndio maana nikaamua kunyoa kipara”


“Kumbe hata shetani mkubwa wa baharini ana upande mwingine mlaini , Ajabu iliooje hii”Aliongea Berry na kauli y ake ile ilimfanya Leviathani haraka haraka amsogelee na kumkwida tai.


“Wewe takataka ni lini utanilipa milioni zangu therathini ninazokudai na dhahabu ulizochukua?”Aliongea akiwa siriasi.


“Ngisi hebu acha kuwa hivi basi , ijapokuwa tunalingana umri lakini nimekuzidi mwezi mmoja , hivyo mimi ni kaka yako na uache kuniabisha, kama ni hela nitalipa tu nikipata..”


Mara baada ya kusikia hivyo watu wote walijikua wakianza kucheka , huku Leviatahni akishangaa , maana hakujua ni kipi kimewafanya kucheka.


Mara baada ya kuongea kidogo , kila mmoja alikaa kwenye nafasi yake . Hamza alikaa katika kiti cha heshima na kumfanya awe anawaangalia kupitia pande zote mbili. Ndani hapo karibia marafiki zake wakubwa wote walikuwepo , akiwemo Azzle , Asmuntis , Mammeni, Livotani , Berly na wengine. Black Fog hakuthubutu kukaa , aliishia kuwamiminia mvinyo huku akiwa amesimama nyuma ya Asmuntis.


Muda huo wote walitulia na Hamza hakuongea neno wala Berly muongeaji sana hakuongea neno . Kila mmoja alikuwa na mwonekano mzito , wakiwa katika takafakari ya kukumbukia mambo yote yaliopita.


Mpaka dakika kumi kupita hatimae Hamza aliwaangalia mmoja baada ya mwingine na kisha akaongea.


Kunani huko kwenye Baraza la maksi?
 
Jitu la Chuma.


The long Table au Meza ndefu ndio kikao cha daraja la juu katika jamii ya siri ya Inferno tokea kuanzishwa kwake. Inferno ilitokea katika Clubs mbalimbali za kishetani ambazo zilianzishwa hapo mwanzo katika miaka ya 70, club hizi zilipewa jina la Hellfire Clubs. Watu wa Hellfire club walijaribu kuvumisha jamii yao hii kwa kuingiza katika filamu kubwa za kimataifa kama Marvel Comics , Stranger Thing na baadhi ya nyingine nyingi wakijaribu kuonyesha ushawishi wao katika kila sekta ndani ya dunia hii kwanzia katika maswala ya uchumi , jamii na hata tamaduni.


Hellfire Club walifahamika kama watu wanaomzihaki Mungu nchini Ireland katika miaka hio. Hii jamii ilikuwa ikifanana sana na Freemason au Iluminat na iliongozwa na Black Emperor au Mr Black.


Baada ya kufa kwa jamii hii kupitia vita takatifu ndio ikaibuka jamii nyingine ambayo ndio hii ya Inferno.


Waasisi wakuu walikuwa ni watu kumi na mbili ambao walitengeneza kikao cha hadhi ya Meza Ndefu ya siti kumi na mbili.


Maana yake ni kwamba vikao vya juu havikuzidi watu hao kumi na mbili tokea kuanzishwa kwake.


Iliwachukuwa miaka miwili tu kuingia katika daraja S katika ulimwengu wa giza ambapo ndio kipindi chote cha Vita takatifu , vita ambayo sio tu kumpa Hamza umaarufu lakini ilimpa ushawishi mkubwa.


“Mephistopheles hajafanikiwa kufika”Aliongea Azzle


“Sallisbury hajasafiri kwa ajili ya kulinda kisiwa cha Toharani”Aliongea Asmuntis na Hamza palepale aliinua juu kikombe cha mvinyo.


“Kikombe cha kwanza cha mvinyo huu ni kwa ajili ya kuwaenzi wale waliotuacha , Belzebuli , Abtoni , Samuel na Roffe , Jamaa zetu hawa wa nne licha ya kutokuwepo na sisi leo hii lakini nafasi zao zitaendelea kuwa wazi katika vikao vyote vya Long Table milele”Aliongea Hamza.


Katika meza hio kila mmoja aliinua glasi ya mvinyo wake na kisha alikunywa yote kwa ajii ya kuwaenzi washikaji zao wengine.


Hali ile ya huzuni na kutafakari ilipita baada ya awamu hio ya kwanza ya mvinyo. Hamza alitaka kunywa na washikaji zake mpaka kesho , kunywa kujigalagaza kabla ya kwenda kushiriki katika baraza la maksi. Lakini muda ule simu ya Azzle ilianza kuita.


“Kuna nini na naongea na nani?” Aliuliza Azzle huku akiwa amekunja sura.


“Kapteni! Sitaki kuwasumbua katika kikao chenu na Mkuu wetu , lakini kuna kitu kimetokea hapa , watu wetu wanashambuliwa na watu wa Wimbi la chuma”


“Metal tide!” Azzle alijikuta akishangazwa na habari ile huku akiinua macho yake na kumwangalia Asmuntis


Asmuntis hata yeye uso wake ulibadilika mara moja baada ya kusikia mwenzake anataja Metal tide na aliishia kumwangalia Hamza kwa wasiwasi.


“Nimesikia vibaya?”Aliongea Mameni kwa sauti kubwa.


“Metal tide wanathubutu vipi kushambulia watu wetu , hawajui mtu ambae yupo nyuma ya Barhamu ni bosi “Aliendelea kuongea Mameni.


“Mhh! Bosi inaonekana kutoonekana kwako kwa miaka mingi , hawa watu washaanza kujihisi wapo juu. Kwanini tusiwaonyeshe kile wanachohitaji”Aliongea Leviathani na kisha akaendelea “Sasa hivi tumezidi kuwa na nguvu , tukiungana mimi , Mhunzi hapo na Mchafu na watu wake ni swala la kufumba na kufumbua tushalizima kundi lote la watu wa Wimbi La Chuma”Aliendelea kuongea Leviathani akiwa katika hamasa kubwa sana.


Hamza alijikuta akiishiwa na usemi , aliishia kunyoosha mkono wake kwa ishara ya kuzuia pendekezo la Leviathani.


“Msiniingize mimi huko tena , nilishawaondolea wasumbufu wote lakini bado tu mnataka kunichosha?”Aliongea Hamza.


Upande wa Azzle na Asmuntis walikuwa na hali zisizoelezeka katika nyuso zao , walifikiria kuona Leviathani na wenzake hawakuwa na taarifa ya Hamza kupoteza uwezo wake wa nishati za mbingu na ardhi.


Ukweli ilikuwa tofauti kwa wenzao , walikuwa wakifahamu Hamza hakuwa na tatizo lolote kuhusu uwezo wake maana alishawasiliana nao na hata kukutana nao siku kadhaa zilizopita.


“Bosi timu yetu ya Barham inaonekana kupambana na watu wa Wimbi la Chuma hapa Limour . Mimi nitaelekea huko nikadili na hili suala,sitoungana na nyie kuendelea kunywa”Aliongea Azzle na kusimama.


“Hey! Mhunzi , hili swala limeamsha shauku yangu. Kwanini tusiende wote kuangalia. Nataka kumuona Jitu Chuma uwezo wake ni mkubwa kiasi gani”Aliongea Mameni huku na yeye akisimama.


“Ndio bosi , hujaonekana kwa muda mrefu na hawajakukaribisha kwenye kikao cha kilele cha Magwiji . Ukijionyesha sasa hivi asilimia kubwa ya watu watakuwa mashabiki zako”Aliongea Berlly.


“Mashabiki wa nini? Unadhani nimekuwa msanii?”Aliongea Hamza.


“Kwa mtazamo wangu haina haja. Bosi huna haja ya kwenda ,kama bosi akienda si kama tunawaheshimu sana ? Mimi na Mhunzi peke yetu tunatosha kudili na hii hali”Aliongea Asmuntis.


Hamza aliishia kusinyaza macho baada ya kuona Azzle na Mchafu wanamtetea asiende kwasababu wanadhani hana uwezo wowote. Hamza alifikiria kidogo na palepale aliona haina haja ya kuwaambia ukweli kwanza, kwasababu alijua anachofanya Gonzalez ni kutaka kumtega yeye. Gonzalez alikuwa akitafuta tu ugomvi , lakini ukweli ni kwamba makundi yote mawili yaani Barham na Wimbi la Chuma walikuwa ni daraja A hivyo wasingeenda mbali.


Alipanga pale ambapo Gonzalez atakuja moja kwa moja kwake ndio atadili nae na atatumia nafasi hio kumkamata na kumshikisha adabu.


“Tutaenda wote , ila sitojitokeza. Ijapokuwa Barham kwasasa ipo chini yako lakini bado nina hisia na jina lake , nisipoonekana itawavunja moyo vijana wetu”Aliongea Hamza.


“Bosi kwasababu umeongea hivyo , basi twendeni pamoja”Aliongea Azzle


Asmuntis alishindwa kufanya lolote mpaka hapo lakini maneno ya Hamza yalikuwa na mantiki. Kama kila mtu yupo ndani ya Limuour na kitu kibaya kikatokea vijana wao na Hamza hajajitokeza itawafanya kuvunjika moyo na pia ingeibua minong’ono.


“Twendeni , sitaki kuchelewa tena , ni bora Gonzalez akajitokeza mwenyewe nimpasue kichwa chake”Aliongea Leviathani huku akisimama.


“Haha.. Ngisi huna haja ya kuwa na wasiwasi juu ya hilo , tupo nchi kavu na huwezi tumia matamvua yako kirahisi. Ni kheri ukawaacha Mchafu na Mhunzi kudili na hili swala”Aliongea Mameni.


Wakati wakiwa wanaongea walitoka ma kwenda moja kwa moja mjini Limour kupitia magari yao ya kifahari.


Nje ya Bar moja mjini Limour, kulikuwa kumejazana watu. Walikuwa ni wanaume na wanawake , wazee na vijana na karibia kila mmoja amevaa staili yake. Ndani ya eneo hilo kulikuwa na taasisi mbalimbali kutoka pande karibia zote za ulimwengu ambazo zimetuma wawakilishi kwa ajili ya kushiriki katika baraza la Maksi.


Sasa ndani ya hii Bar, ndio vurugu ilipokuwa imetokea baina ya watu wa Wimbi la Chumba na masenari wa kundi la Barham. Ilikuwa ni pata shika.


Kitendo cha kufanya watu wengi kusimama nje kuangalia mapigano hayo, ilifanya watu wengi kusogelea eneo hilo.Licha ya kwamba vita ilikaribia kuisha lakini hali ya Bar hio haikuwa ikitamanika tena , kwani meza na viti vilikuwa vimeharibika na kusambaa kila sehemu huku chupa nyingi zikiwa zimepasuka chini.


Upande mmoja katika Bar hio lilionekana kundi ambalo lilikuwa limevalia mavazi ya kijeshi ya rangi ya kijivu na isignia za mchoro wa mawimbi kwenye vifua vyao na mabegani.


Upande mwingine lilikuwa ni kundi lililovaa mavazi ya kijeshi rangi ya jangwa wakiwa na isignia za nembo ya nyota kifuani na mabegani.


Masenari hao wote walikuwa katika mavazi yao ambayo yalikuwa yamechafuka kwa damu. Na walikuwa wamesimama pande zote mbili wakiangaliana huku wakihema kwa nguvu.


“Nini kinaendelea hapa?”


Muda huo mwanaume na mwanamke alieongozana na kundi la wanajeshi wa kimasenari walijipenyeza katika kundi la watu waliosimama nje ya bar na kuingia ndani.


Baada ya kusikia sauti hio watu wa upande wa kundi la Wimbi la chuma walikakamaa miili yao.


“Ripoti kwa Afande Gray. Ni hili kundi la Barham limejaribu kutuletea vurugu. Kwa ajili ya kulinda hadhi ya kundi letu tukaamua kupigana nao”Aliongea.


Mwanaume na mwanamke alieingia hapo alikuwa ni Gray na Helena. Baada ya ripoti hio Gray aliwaangalia Masenari saba wa kundi la pili na kisha akatabasamu.


“Marafiki , Mnaweza kuwa watawala katika peninsula ya Uarabuni , lakini hapa ni Ufaransa”


“Mh ! Kama sio watu wako kutuchokoza tusingekuwa na muda na nyie”Aliongea mwanajeshi wa Kimasenari wa kundi la Barham huku akitema mate chini.


“Oh! Walimuongelea vibaya Lucifer nini?”Aliongea Gray huku akiwaangalai watu wa kundi lake.


“Sir tulikuwa tukiongelea kuhusu Lucifer kupotea baada ya kupigana na Black Emperor . Je tumekosea wapi?”


“Mshenzi! Mlikuwa mkimuongelea vibaya bosi wetu na kusema baada ya vita alipotea baada ya kupoteza uwezo wake ndio maana mpaka leo anaoagopa kujitokeza. Dunia nzima inajua ni Prince aliemuua Black Empor kwa ajili ya amani ya dunia. Kwa ajili ya kuifungua katika minyororo ya giza aliamua kupigana vita takatifu na kuwaachia huru waliofungwa gizani na Mahakama takatifu. Master ni mtu wa haki ndio maana hata baada ya kushinda aliamua kutawanyisha watu wa Inferno ili wasijikusanyie umaarufu na ushawishi kuingilia mambo ya ulimwengu wa kawaida. Hata viongozi wetu wa Barham ni watu wa haki. Unatoa wapi ujasiri wa kumuongelea Master vibaya?”Aliongea Mwarabu huyo na kumfanya Helena kucheka.


“Nyie watu wa Barhams, siku hizi mpo sensitive sana. Tunajua mnamwabudu bosi wenu lakini kuna haja ya kupaniki baada ya kusemwa kidogo tu?”Aliongea Helena.


Kati ya Masenari hao , kuna mmoja ambae alikuwa amekaa , mwanajeshi aliekuwa na nyota kwenye bega lake. Alikuwa ndio kiongozi wa kundi hilo la Barham. Mara baada ya kuona Helena anacheka kwa dharau alisimama na kusogea mbele.


“Wewe Gray na Helena watu wa kundi la Wimbi la Chuma nimeyasikia sana majina yenu lakini sijawahi kudhania watu wa sifa zenu mtakuwa kichefuchefu namna hii. Ijapokuwa mimi Kent ni Kiongozi wa kikosi tu najua heshima za msingi zidi ya watalaamu wa daraja la Ugwiji , nje na ndani ya kundi letu. Bosi wetu sio mtu wa kuongelewa na mtu mwenye mdomo mchafu kama wewe. Hata kama alituacha kwa muda mfupi , yeye ndio kiongozi wetu , mtu wa imani pekee tuliekuwa nae . Kama ujasiri unao , tangaza vita na kundi letu hapa hapa. Nyie kumi na mbili mtashambuliana na sisi saba na hamtoweza kutushinda. Kwa uwezo wenu mdogo hata mwanajeshi wetu wa daraja la chini hamuwezi kumshinda”


“Haha.. Majigambo meengi. Kama tusingewaonea huruma mnadhani mngeendelea kusimama?”Aliongea mwanaume wa upande wa Metal Tide.


“Eti mmetuonea huruma. Kama mmetuonea huruma mngekuwa na nundu usoni?”Aliongea Kent.


“Nyie , mmeshinda si kwasababu mlitutega , mlikuwa na siraha na sisi hatukuwa nazo’


“Kuna chupa kibao haba ambazo mngeweza kutumia kama siraha lakini mkashindwa , msilaumu kwa uzembe wenu. Haishangazi ndio maana kwa miaka mingi mmebakia kuwa kundi la daraja A. Moja ya mafunzo ya mkuu wetu anatusisitizia; kufanikiwa zaidi ni kukubali kushindwa na kuyatambua mapufungu yako”Aliongea Kent.


“Damn it! Sir Gray wanaendelea kutudhalilisha tu”


“Jina lako ni Kent sio? Maneno yako uliongea yametukosea sana. Piga magoti chini na uombe msamaha , la sivyo usije kutulaumu kumdhalilisha Master wako Azzle”Aliongea Gray.


“Nipige magoti!?” Kundi lote la Barham walitunisha vifua huku wakikamamaa miili kwa kujiamini, “Hata mkuu wetu Azzle hawezi kutuambia tupige magoti. Sisi Barham ni watiifu kwa Mfalme wa kuzimu pekee” Mara baada ya kuongea hivyo aliwapa ishara vijana wake na kuanza kupiga hatua kutoka katika Bar hio lakini Gray alisogea na kusimama mbele ya Kent.


“Usipopiga magoti na kuomba msamaha , usifikirie kabisa kuondoka hapa kirahisi”


“Pisha njia” Kent alikuwa na hasira mno. Palepale alikusanya nishati ya mbingu na ardhi na kumsukuma Gray.


Ingawa hakukuwa na mabadiliko sana , lakini katika vita halisi , tena vita mchanganyiko kama hivyo utofauti wa nishati ya mbingu na ardhi ulikuwa na faida kubwa. Ilikuwa ni vita ya kifo , unapigana ukiwa na nafasi ya kushinda na kama hakuna njia rahisi ni kuondoka ndio maana Kent aliongoza watu wa kundi lake kuondoka.


Gray mara baada ya kuona Kent anajitutumua haraka sana alikunja ngumi yake na kumrushia Kent.


“Bang!


Gray alikuwa ni mpiganaji ambae pia alifikia katika daraja la Ukaidi wa asili na mwanzo wa ufunuo wa mwili mpya , hivyo kwa namna flani alichukuliwa kama mbobezi.


Ngumi yake ambayo ilikuwa imeambatana na nishati ya mbingu na ardhi ilikuwa nzito kiasi kwamba ilimfanya Kent kutetemeka mwili.


Arghhhh!


Mfupa katika mkono wake ulipinda mara baada ya kujaribu kupangua ngumi ya Gray, uliumia na kumfanya ashindwe hata kukunja ngumi tena.


Kundi la nje ambalo walikuwa wakiangalia waliona Kent alikuwa akijikadiria kwa viwango vya juu kutaka kupigana na mtu kama Gray ambae hakuwa katika daraja sawa la uwezo.


“Unadhani sisi watu wa kundi la Metal Tide hatuna uwezo? Piga magoti na omba msamaha kabla ya kufikiria kuondoka”


Kent aliishia kusaidiwa na wenzake wawili kusimama juu na hakuonekana kukubali kushindwa kirahisi.


“Mwanajeshi wa daraja la ukaidi wa asili , kushambulia mtu kama mimi ambae ni kiongozi wa kikosi ni sawa na kujidhalilisha. Lakini hata kama tutakufa hapa hapa sisi Barham hatuwezi kupiga goti na kuomba msamaha kwa watu washenzi kama nyie”


“Umeongea vyema!”Sauti ilisikika kutoka nje ikiambatana na makofi.


Muda huo kundi lilitawanyika baada ya wanajeshi waliojazia miili wa Barhampton Empire kutengeneza njia kwa ajili ya Azzle alievalia kombati za kijeshi na Asmuntis alievalia jacketi la kijani kibichi kupita.


Watu baada ya kuona wanajeshi hao wawili , walijihisi ni kama miili yao imetawaliwa na presha kubwa na kufanya wahisi woga.


“Oneni sana , yule ndio Bwana wa Vita. Marshall wa kundi la Barham, Kapteni Azzle mwenyewe”


“Msisimko anao toa ni wa ajabu mno. Inafanya watu kuwa na wasiwasi kwa kuangaliana nae usoni tu. Kama ilivyokuwa inasemekana moja kati ya mashetani kumi na mbili wa Inferno waliosalimika katika vita takatifu hawa ni moja wapo”


“Hey! Achana na Azzle , angalia alieambatana nae , yule ndio Asmuntis mwenyewe, Assassin namba moja duniani! Bosi na mmiliki wa kundi la wauaji la Baffodil DayDreamers! Ni adimu sana kujianika hadharani”


“Mungu wangu! Inamaana umoja wa Inferno unajikusanya upya, wanapanga kushiriki katika Baraza la Maksi au?”


“Inawezekana , Lucifer hajulikani alipo , hivyo ni kawaida kwa Baffodil na Barhampton kuja kushiriki”


Kundi lote la washiriki wa Baraza la maksi waliokuwa katika eneo hilo walikuwa wakiongea wao kwa wao kwa kile walichokuwa wakifahamu , lakini Azzle na Asmuntis wala hawakujali kabisa


Azzle aliwapita Gray na Helena na kwenda kusimama mbele ya Kent akimwangalia.


“Vipi umeumia?”


Kent na wenzake mara baada ya kuona kiongozi wao amefika , walijikuta wakipatwa na ahueni na kufarijika kwa wakati mmoja.


“Report kwa Kapteni! Ni majeraha madogo tu”Aliongea akijikakamua na Azzle alitingisha kichwa na kisha aliwageukia Gray na Helena.


“Umemuumiza mtu wangu. Ni mkono upi ulioutumia , uvunje mwenyewe kabla sijachukua hatua”


Kauli hio ni kama vile Gray alikuwa amekuhukumiwa kifo , hakuweza kuleta ukinzani tena.


“Kiongozi Azzle nakuheshimu sana. Wewe ni mwanajeshi mwenye nguvu na hadhi kubwa , lakini huna mamlaka ya kuniamrisha kufanya chochote. Kundi letu ni la daraja sawa na la kwako. Kwanini usianze kwanza kujua nini kimesababisha haya yote?”


“Haina haja kwani vijana wangu hawawezi kufanya kosa kwasababu wanajua matokeo yake ni nini ikiwa wamekosea”


“Hapa sio Uarabuni. Wewe ni maarufu tu kama Ares wa Peninsula ya Uarabuni , lakini huwezi kuziba anga lote na mkono. Gray tuondoke , Kapteni anatusubiria”Aliongea Helena na Gray alitingisha kichwa kukubali


“Tuondokeni”Aliongea Gray akiwapa ishara vijana wake.


Mara baada ya agizo hilo , wanajeshi wa kundi la Metal Tide walianza kutembea kutaka kutoka , lakini Azzle na mwili wake kama wa tembo alienda kusimama mbele ya Gray na Helena kuwazuia.


“Kubali kupoteza mkono au ufie hapa hapa . chagua moja”Aliongea Azzle akiwa siriasi kiasi kwamba macho yake ni kama yamejaa moto wa kuzimu, kusudio lake la kuua lilikuwa limetawala Bar nzima.


Gray na Helena waliishia kuangaliana na bila kupenda walijikuta wakipiga hatua mbili kurudi nyuma. Na muda ule ghafla tu walisogea kwa spidi katika pande mbili tofauti na kuanza kumshambulia Azzle kushoto na kulia.


Ukweli ni kwamba walikuwa wakijua ni ndoto ya mchana kuweza kumshinda mtu wa daraja la Azzle kwa kupambana mmoja mmoja , hivyo waliona angalau wakishambulia kwa wakati mmoja wanaweza kufanikisha.


Hawakutaka kukimbia pia kwani ingewafanya watu kuwadharau. Lakini bado mtu wanaepambana nae alikuwa ni hatari mno , mtu kuwa moja ya sehemu ya watu wa karibu wa Hamza halikuwa swala rahisi hata kidogo.


Azzle hakuonyesha mabadiliko kabisa , mara baada ya kuona shambulizi la Helena na Gray limekaribia shingo yake , palepale alifyatua mikono yake yote miwili kwa wakati mmoja na kupangua mashambulizi yale.


Bang Bang!


Kwa wepesi kabisa aliweza kuyapangua na kwa wakati mmoja alinyoosha mikono yake akijaribu kuwakamata wote wawili . Lakini Gray na Helena haraka sana walifyatuka wakimkwepa baada ya kuona mashambulizi yao hayakuzaa matunda.


Baada ya hapo wote wawili walikuwa wakishambulia kitahadhari wakimkwepa Azzle asiwakamate.


Azzle alikuwa amesimama katika eneo moja , hakuwa amesogea hata kidogo na ni mikono yake tu ndio iliokuwa ikicheza , alikuwa na nguvu za mikono kiasi kwamba alionekana kama sio binadamuwa kawaida. Licha ya kushambuliwa, Gray na Helena ni kama walikuwa wakigusana na chuma kwani hawakumwathiri hata kidogo.


Asmuntis upande wake aliishia kusimama tu akiangalia , huku akiwa hana nia ya kusaidia.


Kundi lote nje lilijawa na hamasa na shauku katika kuangalia pambano hilo , asilimia kubwa ni wanajeshi waliokuwa katika daraja la chini kabisa katika mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi hivyo waliokosa ujuzi na ufunuo, hivyo kwa pambano kama hilo wasingeweza kulimudu.


Mara baada ya kumshambulia kwa dakika kadhaa , Azzle ni kama alikuwa akiwasoma muda wote na alionekana kugundua udhaifu wao . Ghafla tu Azzle alipiga hatua kubwa mbele na kumshika Gray mkono wake mmoja. Gray ambae alikuwa akitaka kushambulia alijikuta akigutushwa na shambulizi hilo na kutaka kusogea lakini sasa kabla haja sogea Azzle alikuwa tayari asharusha ngumi kwa kulenga bega lake.


Kwa namna alivyofyatuliwa ni kama alikuwa mpira , kwani alipaa hewani na kwenda kutua mbele ya Helena , na mwanamke huyo hakuwa na jinsi zaidi ya kumkwepa Gray na ile alipotua kilichosikika ni Kwacha.


“Arghhhhh!!


Gray alitoa ukulele mkubwa baada ya mkono wake mmoja kuvunjika


“Nilikuambia vunja mkono wako au kufa ila hukunisikiliza”Aliongea Azzle.


Shambulizi lile liliwafanya watu wengi kushangaa baada ya kuona licha ya Azzle kushambuliwa na watu wawili , lakini hakupata jeraha hata moja


“Muue . haina haja ya kumuacha akiendelea kuishi”Aliongea Asmuntis aliekuwa pembeni.


Gray na Helena walijikuta akiwa katika mshituko mkubwa , hata Gray ambae alikuwa katika maumivu alijikuta yakipotea kutokana na kauli ya Asmuntis.


“Ngoja niwaache , kesho ni ufunguzi wa baraza la maksi . Haina haja ya kulikuza hili swala . Sitaki kuona sura zenu hapa tena , waambie watu wako wakae mbali na sisi”Aliongea Azzle akimuonya Helena.


“Mhunzi , wapo hapa kutafuta ugomvi tu , kuwaacha hai ni kuwapa kiburi cha kutuchokoza zaidi”


Azzle alikuwa sio mjinga , mara nyingi katika tukio kama hilo ilikuwa ni mtego umewekwa . Metal tide wametuma watu dhaifu ili kuibua ugomvi ili baadae Gonzalez akiingilia mwenyewe na hata Hamza kujitokeza na kupigana , watu wa baraza wasingemhukumu kwa kusema anajitafutia sifa.


Sasa kwasababu walijua Hamza ni dhaifu kama kweli atapigwa na Gonzalez basi moja kwa moja ingekuwa rahisi sana kwa bwana huyo kupata hadhi ya Ugwiji.


Ki ufupi ni kwamba mtego huo alikuwa amewekewa Hamza ili aingie kati na Gonzalez achukue hatua.


“Kama unataka kutuua tuue tu. Sisi ni wanajeshi sio Maninja”Aliongea Gray.


“Mhunzi!” Aliita Asmuntis huku akijua kwa tabia ya kizamani ya Azzle asingechukua hatua ya kuwaua. Lakini Asmuntis yeye kama muuaji hakujali watu watamfikiria nini kama atawaua hivyo alipiga hatua kusogea.


Gray na Helena mara baada ya kuona kweli Asmuntis anasogea walijikuta wakianza kupaniki.


Watu waliokuwa nje walijikuta pia wakishangaa , wakiwa hawaamni kama kweli Asmuntis kiongozi wa wauaji wa kundi la Bafodili anakwenda kuua wanajeshi wa kundi la kimasenari la Metal tide.


Kama angefanya hivyo maana yake ni kwamba kabla hata ya baraza , Baffodil ingejiingiza katika ugomvi na Metal Tide .


“Inasemekana aina ya mauaji ya King of killers , Asmuntis hayajawahi kukosa sababu ..Na kama akichukua hatua huwezi hata kujua namna unavyokufa”Watu walianza kuongea wao kwa wao.


“Kwa uwezo huo si hao watu wameisha tayari”


“Lakini mkumbuke huyu ni muuaji wa siri, yaani Assassin , lakini hapa si hadharani, Sidhani kama atamuua Gray na Helena kirahisi”


Wakati maneno yakiibuka kati ya kundi hilo la watu waliokuwa wakiangalia , upande wa Gray na Helena ulikuwa ni wa kutia huruma. Hisia zao zilisimama pia kwa presha kubwa iliokuwa ikiwasogelea kutoka kwa Muuaji namba moja duniani.


Asmuntis aliishia kusimama mara baada ya kutembea kwa hatua kadhaa huku akiwaangalia , hakuwa mrefu sana wala hakuwa na mwonekano wa kupendeza , lakini msisimko aliokuwa akitoa ulikuwa ni wa baridi na kufanya wahisi ni kama wanachomwa na vichomi vya baridi mwilini.


“Uchokozi wenu ni wa kijinga sana”Aliongea Asmuntis.


Kabla ya Gray na Helena kujibu ghafla tu walishuhudia Asmuntis akipotea mbele yao na ile anatokea kwa mara nyingine kilichosikika ni;


‘Clang!!’


“Haaa !”


Kundi lote la watu lilipiga kelele ya mshangao , waliweza kuona Asmuntis alikuwa amekwisha kumfikia Gray alipokuwa akitaka kumchinja na kisu, lakini matokeo yake hakufanikisha baada ya mkono uliokuwa mgumu kama chuma kuzuia shambulizi lile.
 
Kwa ukubwa na misuli ya mkono ile ilitosha kuogopesha kila mtu aliekuwa karibu.


“Jitu chuma ! Gonzalez!”


Watu waliongea kwa nguvu katika hali ya kushangaa, mara baada ya kuona mtu goliati alievalia vazi la ngozi akiwa amezuia shambulizi la Asmuntis kwa mkono wake tu.


Mbele ya mtu huyo ilikuwa ni kama simulizi ya Daudi na Goliathi katika biblia. Gonzalez alikuwa mrefu kwenda juu na alimwangalia Asmuntis kwa chini.


Kapteni!” Gray , Helena na wanajeshi wote wa Metal Tide waliita kwa shangwe kubwa.


Asmuntiss mara baada ya kuona shambulizi lake limefeli kwa spidi ya juu sana aliruka sarakasi ya kurudi nyuma na kwenda kutua ardhini huku akimwangalia Gonzalez kama chui ambae yupo tayari kumrukia.


Ukisikia jitu la chuma , halikuwa jina la bahati mbaya ni mtu ambae alikuwa na mwili mkubwa ambao ulimpa faida kuu katika uwanja wa mapambano , kwanza alikuwa na uwezo wa kushambulia kwa nguvu kubwa na pili alikuwa na uwezo wa kukinga shambulizi kwa mwili wake bila ya kuumia.


Gonzalez alikuwa ni binadamu wa ajabu kuwepo katika uso wa dunia , mwanachama wa umoja wa wasio wa kawaida(Adept Race or Adept Associations). Elementi za chuma ambazo zilikuwa ndani ya mwili wake zilipita hali ya kawaida ya ubinadamu. Alikuwa na uwezo wa hali ya juu wa kukusanya elementi zote za chuma zilizojihifadhi katika mwili wake na kutengeneza misuli na ngozi ambayo inakuwa ni kama chuma kwa kusaidiwa na nishati za mbingu na ardhi.


Kabla ya kuanzishwa kwa kundi la kimasenari la Wimbi la Chuma , Gonzalez alikuwa ni mwanachama hai wa Adept Associaton(Umoja wa Binadamu wasio wa kawaida). Serikali ya Mafuvu ili kutengeneza kundi hili la kimasenari walitumia gharama kubwa sana kumwajiri Gonzalez.


“Asmuntis kama wewe ni Assassin huenda ningekuhofia lakini hii ni kunidharau sana kutaka kuuwa watu wangu mchana kweupe”Aliongea Gonzalez huku akimwangalia Asmuntis kwa kejeli.


“Kapteni aliemuumiza Gray ni Azzle”Aliongea Helena na kumfanya Gonzalez kumwangalia Azzle.


“Oh! Naona leo Barhams na Baffodil mmeamua kuunganisha nguvu kushambuliana na Kundi langu la Wimbi la chuma”Aliongea na palepale Azzle alipiga hatua moja mbele.


“Sisi Barhams , hatujawahi kuwa na uadui na yoyote , katika ulimwengu wetu usipokuwa rafiki yetu basi wewe ni adui yetu. Kama unataka kuwa adui yetu tunakukaribisha”Aliongea na kumfanya Gonzalez kuchezesha vidole vyake kama vile kuna kitu anafikiria.


“Kwa muda mrefu sana imekuwa ikifahamika Barhams ni kundi kubwa lenye nguvu la kimasenari duniani, lakini mimi sijawahi kukubali kuhusu hili. Kwasababu tumefikia hatua hii sina jinsi zaidi ya kuwaruhusu vijana wangu kufanya kile wanachotaka. Kapteni Azzle nitakupa nafasi wewe na ndugu yako Asmuntis kupigana na mimi , kama mtashinda nitakubali , ila mkishindwa msije kufikiria kuondoka hapa . Sisi Wimbi La Chuma , hatujawahi kukubali hasara , mnapaswa kupiga goti na kutuomba msamaha”


“Unaongea ujinga , unadhani wewe peke yako unaweza kumfanya Kapteni wetu na Mkuu Asmuntis kukupigia magoti?”Wanajeshi wa Barham waliongea kwa hasira”


“Mnapaswa kujivunia kwa Master wetu kutaka kupigana na wakuu wenu, mnaijua hadhi yake kwanza? Hapa mtu aliepaswa kushindana nae ni bosi wenu Prince of hell lakini ameamua kuwapa heshima kwa kutaka kupigana na hawa wawili”


“Helena usiongee hivyo , Asmuntis na Azzle ni wanajeshi wakubwa sana katika umoja wa muungano wa Inferno na pia ni watu wa karibu wa Lucifer . Nishawahi kupambana nao na sio watu wepesi wa kudharau”


Watu mara baada ya kusikia kauli hio walihisi matumbo kuanza kuchemka kwa msisimko mkubwa.


Hakuna hata mmoja aliedhania kutatokea jambo kama hilo kubwa kabla ya kuanza kwa Baraza la maksi.


Makundi mawili ya kimasenari duniani na kiongozi wa kundi kubwa la kimauaji duniani waliokuwa chini ya umoja ya Ki-inferno , wanaenda kupambana na Jitu chuma kiongozi mkuu wa kundi la kimasenari la Metal tide , mtaalamu wa mapigano ambaye alikuwa akiwania nyota ya Ugwiji.


Tukio kama hilo mara nyingi ni adimu sana kutokea na hakuna namna linaweza kuwachosha watu , kila mmoja alishikwa na hamu ya kutaka kuona kile kitakachotokea, huku watu wengi zaidi wakisogea katika eneo hilo.


Kutokana na umati mkubwa wa watu , Asmuntis na Azzle walihisi ni kama jambo hilo limeandaliwa na kama wataondoka bila ya kupambana ni kama kutengeneza ushahidi kupitia watu hao kwamba wameshindwa pambano kwa kumkimbia Gonzalez.


Lakini sasa bado hawakuwa katika hali ya kujiamini kama wangeweza kupigana na Gonzalenz na kushinda.


“Inaonekana hili eneo lishakuwa dogo na ni ngumu kupigania hapa , mnaonaje tukienda kwenye jukwaa la ngazi na kushindania kule”Aliongea Gonzalez akiwa na utulivu wa hali ya juu.


“Kama ni hivyo nakubali , ila nitashindana na wewe mimi peke yangu”Aliongea Azzle na kumfanya Asmuntis macho kumsinyaa lakini hakuongea neno.


Ukweli ni kwamba , ilikuwa rahisi kumuelewa Azzle , kwasababu kama wangepambana wote kumshambulia Gonzalez hata kama wakishinda ni rahisi watu kusema hakukuwa na usawa. Hivyo kwa ajili ya kulinda heshima ya Barhams na heshima ya Hamza , Azzle aliona ashindane yeye peke yake.


“Interesting! Kama ni hivyo basi leo hii nataka kushuhudia maajabu ya Kamanda namba moja wa jeshi la kujitegemea , Mfalme Azzle kutoka jeshi la jangwa”Aliongea Gonzalez na palepale aliongozwa na watu wake kutoka katika hilo eneo na kwenda eneo la juu kwa ajili ya pambano.


Azzle kabla ya kupiga hatua kumfuata , alimgeukia Asmuntis na kumnong’oneza.


“Mwambie bosi asije kutokea hata kama nishindwe”


“Nimekuelewa” Aliongea Asmuntis huku akiwa na wasiwasi katika macho yake.


Upande wa Hamza , Berly , Leviathani , Mamoni na wengine walikuwa wakinywa bia juu ya balkoni katika floor ya tatu ya jengo la hoteli pembeni ya jukwaa la wazi.


“Bosi hili pambano linakwenda kuwa la aina yake , Gonzalez naona anajitafutia kifo”Aliongea Mameni huku akicheka.


“Anakufaje sasa kwa kujiamini vile?”Aliuliza Hamza aliekuwa ameshikilia chupa ya bia akipiga mdogo mdogo.


“Bosi kuna haja ya kuuliza , kwa uwepo wako hapa kama akitaka kumuua Azzle si utaenda kumshughulikia tu mara moja”


“Ndio bosi! Halafu kwanini tusishuke chini bosi kumpa sapoti Azzle , pengine Gonzalez akikuona ataacha kupigana na Azzle”Aliongea Leviathani


“Haina haja , ngoja tuangalie kwanza . Ili mradi hatuoni hatari kwa Azzle , ni shindano la kawaida la kutambua nani mshindi na nani kashindwa. Kingine mimi nishastaafu mwenzenu. Kama hakuna tatizo kubwa sioni haja ya kuingilia”aliongea Hamza.


“Ni kweli kabisa bosi , kwa hadhi yako haina haja ya kujisumbua sana kwa mtu kama Gonzalez. Kama ni kupigana nae inapaswa kuwa mbele ya watu wa Baraza la maksi ili kuonekana dunia nzima ni kwa namna gani Gonzalez ni dhaifu na ni mwili tu unaombeba”Aliongea Berrly.


Ukweli ni kwamba Hamza alikuwa ashachoka kuendelea kujifanya ni mdhaifu. Alijiambia kama angeona Azzle yupo hatarini asingejiuliza mara mbilimbili na angeenda kumsaidia. Ila kama swala hilo sio hatari sana hakuona haja ya kujidhihirisha mapema namna hio. Isitoshe mshindani ambae alikuwa akitaka kushindana nae sio mtu wa levo za Gonzalezi yaani ni zaidi ya Gonzalez.


Unachopaswa kujua ni kwamba , kutokana na kuitishwa kikao cha kilele cha magwiji maana yake wale Magwiji wa dunia lazima wangekuwepo, hivyo maana yake ni kwamba lazima vurugu ingetokea tu baina yao na pengine kati ya umati huo wa watu moja ya magwiji hao wapo kama ilivyo kwa Hamza anavyoangalia kwa mbali , Hivyo kama angejitokeza na kuonyesha uwezo wake ingekuwa ni sawa na kujiuza na kuwafanya maadui zake kujipanga vizuri na ingekuwa na athari mbaya kwake.


Wakati wakiwa wanaongea , Gonzalez na Azzle walikuwa washapandisha juu ya eneo la wazi kabisa kama jukwaa lililotengenezwa kwa ngazi kuzunguka.


Licha ya Azzle kuwa mrefu , lakini bado alionekana kama mtoto mbele ya Gonzalez mwenye mwili mkubwa.


Muda ule walianza kuangaliana kama mapaka na upepo mkali ulianza kuvuma na yote hio ni kutokana na kudhibiti pumzi yao na kuruhusu nishati ya mbingu na ardhi kuvaa miili yao.


Kutokana na hilo kundi lote la waangaliaji , lilijikuta likikamaaa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.


Gonzalez alitoa tabasamu jepesi lakini kwa Azzle alikuwa na uso uliojaa usiriasi mno , ilikuwa ngumu kujua kama alikuwa na wasiwasi au yupo katika hali ya kujiamini.


Waliangaliana upande kwa upande , kila mmoja akimsoma mwenzake, hakuna aliekuwa na haraka za kushambulia.


Ilionyesha kutokana na mkusanyiko mkubwa wa watu ulivutia watu wa kila aina, Hivyo hata baadhi ya wanajeshi wa kitanzania waliofika kushiriki walivutiwa.


“Mnaangalia nini! Nipisheni mimi nataka kuona pia”


Sauti ya kibabe ya mwanamke ilisikika kutoka nyuma ya kundi. Alikuwa ni mwanamke alievalia koti la manyora ya rangi nyekundu na suruali nyesi na soksi za mikono , alikuwa na nywele zilizojikunja kidogo lakini ziliozompendeza na kumfanya kuonekana mwanamke wa kisasa zaidi. Alijichomeka katika kundi la watu mpaka alipoweza kujipenyeza na kufika eneo la ndani zaidi.


Mwanamke huyo mrembo mkononi alikuwa ameshikilia Ice Cream na alikuwa akiilinda isiharibike kadri alivyokuwa akijipenyeza katika kundi hilo la watu, na ile baada ya kupata nafasi nzuri ya kuangalia , aliendelea kulamba lamba akiwa katika mudi nzuri kabisa.


Haikuchukua dakika chache wanaume weusi walienda kusimama nyuma yake. Walioneakan kuwa wakubwa kuliko yeye na muda wote walikuwa wakimfuata nyuma nyuma kama wasaidizi.


“Madam Nyakasura , hatuwezi kuendelea kuwa hapa , tunapaswa kuwa hotelini kwa ajili ya kuendelea na kikao cha maandalizi ya kesho”Alikuwa ni moja ya mwanajeshi wa kitengo cha Malibu.


Ukweli ni kwamba hata wao ndio kwanza walikuwa wamefika mjini Limour, lakini wakati wakitaka kwenda hotelini kwa ajili ya kuanza maandalizi , matokeo yake Nyakasura alikataa kwenda nao hotelini na kukimbilia mtaani , ambako alipita kila palipomvutia na kununua vitu na kula kama mtoto . Sasa mara baada ya kuona kundi la watu limekusanyika ndani ya mtaa alishikwa na shauku ya kutaka kujua nini kinaendelea.


“Kama mnataka kwenda kwenye kikao sijawazuia , nyie nendeni tu . Mimi nataka kuangalia wanavyopigana”Aliongea Nyakasura akiwa ameshikwa na hamu pia ya kuona pambano hilo.


“Nyakasura wewe ni mtu muhimu sana kwenye timu yetu na pia unapaswa kushiriki katika kilele cha kikao cha magwiji . Tanaanzishaje kikao bila ya uwepo wako , tunapaswa pia kukuandalia hotuba utakayotoa mbele ya watu wa baraza katika kikao”Aliongea Mboma.


“Hebu acheni kunichosha na mambo yenu ya vikao , sijali nitakachoenda kuongea kwenye kikao na mniache, kaendeleeni na mambo yenu”


“Madam hili ni muhimu zaidi” Aliongea Juma msaidizi wa Mboma.


“Hamna mnachojua? Hili pambano ndio muhimu , pale yupo Mkuu wa kundi la Kimasenari Gonzalez na mwiingine pia ni mkuu wa kundi la Kimasenari , unadhani hili ni shindano la kawaida. Ni bora mkatulia mwangalie na muache kunisumbua”


“Ndio tunajua hili ni pigano zuri , lakini halituhusu na lipo nje ya malengo yetu yaliotuleta”


“Acha malelele na ujinga wako , huna utaalamu wa mapigano ndio maana unachukulia vitu kirahisi rahisi. Mkiendelea kunisumbua msinilaumu nikiwachoma moto”Aliwakodolea macho kuwaogopesha na kisha aliendelea kulamba icecream yake kwa raha zake.


Watu wa kundi la Malibu waliishia kukosa cha kufanya. Mwanamke huyo tofauti na Afande Simba hakuna mtu mwingine anaeweza kumwamrisha na akakubali jambo kirahisi.


Sasa tukio hilo Hamza aliekuwa amechill zake juu na bia yake aliweza kumuona Nyakasura katika kundi hilo la watu . Alishindwa kujizuia na kutabasamu na kwa namna alivyokuwa akizongwa zongwa na wanaume wale alijua lazima alikuwa amevutiwa na pambano hilo na anakataa kuondoka.


Ilikuwa ndio muda huo huo katikati ya jukwaa la ngazi , Azzle alijitutua kupandisha uwezo wake wote na upepo mkali ulianza kumzunguka katika miguu yake na palepale alifyatuka na kumsogelea Gonzalez kwa spidi.


Nishati ya Nafsi ya kweli iliokuwa imemzingira Azzle ilikuwa ni ya juu kabisa na kila hatua aliokuwa akipiga kumsogelea Gonzalezi ilikuwa ni kama vile ni gari la kusindilia barabara linatembea.


Mara baada ya kurusha ngumi yake kumlenga , ilionekana kuwa na nguvu kubwa mno , kama vile ulikuwa ni mtalimbo wa chuma uliorushwa kumlenga Gonzalezi kichwani.


Gonzalez macho yake yalichanua , huku akiinua mkono wake mmoja kupokea shambulizi lile.


Bam!!


Eneo alilokuwa amekanyanga lilititia , lakini hakuonekana kupata madhara yoyote na badala yake tabasamu la uovu lilimvaa palepale na alikunja ngumi na kisha aliirusha kumlenga Azzle kifuani.


Azzle alikuwa mwepesi mno kwani kabla ngumi ile haijamfikia kifuani haraka sana alidaka na mkono wake wa kushoto na kisha alipiga hatua moja kurudi nyuma na kujaribu kuvuta mkono wa Gonzalez ili kuuweka kwenye bega lake na kuubonda.


‘Ah!’


Ilikuwa maajabu , licha ya Gonzalez kuwa na mwili mkubwa lakini Azzle kama vile ni mcheza mieleka kwani aliweza kuurusha mwili wa Gonzalez chini kama furushi.


Boom!!


Shindo kubwa iliweza kusikika na kufanya watu wote waliokuwa wakiangalia kushikwa na hofu baada ya kuhisi mtetemeko mkubwa wa ardhi.


Spidi ya shambulizi lile iliwafanya hata watu wa Metal Tide kushikwa na hofu, Hawakudhania Azzle angekuwa wa kwanza kufanya shambulizi.


Sekunde ambayo mwili wa Gonzalez ulitua chini , ulitengeneza shimo. Mpiganaji wa kawaida kama angepatwa na shambulizi la namna hio pengine angekuwa katika maumivu makali sana kama sio kushindwa kuamka kabisa.


Lakini sasa licha ya kuangushwa chini, Gonzalez hakuonyesha kuumia kabisa na alienda mbali na kumshika Azzle mkono kwa nguvu asimtoroke


“Good Kung fu ,Nimesikia mbinu za mashambulizi uliozokuwa nazo ni nzuri sana. Hakika unaishi ndani ya sifa zako , ila ni muda wangu sasa wa kukuonyesha mimi ni nani”Aliongea Gonzalez huku akianza kucheka kwa sauti na muda uleule alimshika Azzle na kumuinua juu hewani kama kifurushi na kama vile anadunda mpira chini, kwa nguvu aliutua mwili wa Azzle kwa kuupigisha kwenye sakafu. Songa nayo hapa bure kabisa:- SEHEMU YA 196
 
Kwa ukubwa na misuli ya mkono ile ilitosha kuogopesha kila mtu aliekuwa karibu.


“Jitu chuma ! Gonzalez!”


Watu waliongea kwa nguvu katika hali ya kushangaa, mara baada ya kuona mtu goliati alievalia vazi la ngozi akiwa amezuia shambulizi la Asmuntis kwa mkono wake tu.


Mbele ya mtu huyo ilikuwa ni kama simulizi ya Daudi na Goliathi katika biblia. Gonzalez alikuwa mrefu kwenda juu na alimwangalia Asmuntis kwa chini.


Kapteni!” Gray , Helena na wanajeshi wote wa Metal Tide waliita kwa shangwe kubwa.


Asmuntiss mara baada ya kuona shambulizi lake limefeli kwa spidi ya juu sana aliruka sarakasi ya kurudi nyuma na kwenda kutua ardhini huku akimwangalia Gonzalez kama chui ambae yupo tayari kumrukia.


Ukisikia jitu la chuma , halikuwa jina la bahati mbaya ni mtu ambae alikuwa na mwili mkubwa ambao ulimpa faida kuu katika uwanja wa mapambano , kwanza alikuwa na uwezo wa kushambulia kwa nguvu kubwa na pili alikuwa na uwezo wa kukinga shambulizi kwa mwili wake bila ya kuumia.


Gonzalez alikuwa ni binadamu wa ajabu kuwepo katika uso wa dunia , mwanachama wa umoja wa wasio wa kawaida(Adept Race or Adept Associations). Elementi za chuma ambazo zilikuwa ndani ya mwili wake zilipita hali ya kawaida ya ubinadamu. Alikuwa na uwezo wa hali ya juu wa kukusanya elementi zote za chuma zilizojihifadhi katika mwili wake na kutengeneza misuli na ngozi ambayo inakuwa ni kama chuma kwa kusaidiwa na nishati za mbingu na ardhi.


Kabla ya kuanzishwa kwa kundi la kimasenari la Wimbi la Chuma , Gonzalez alikuwa ni mwanachama hai wa Adept Associaton(Umoja wa Binadamu wasio wa kawaida). Serikali ya Mafuvu ili kutengeneza kundi hili la kimasenari walitumia gharama kubwa sana kumwajiri Gonzalez.


“Asmuntis kama wewe ni Assassin huenda ningekuhofia lakini hii ni kunidharau sana kutaka kuuwa watu wangu mchana kweupe”Aliongea Gonzalez huku akimwangalia Asmuntis kwa kejeli.


“Kapteni aliemuumiza Gray ni Azzle”Aliongea Helena na kumfanya Gonzalez kumwangalia Azzle.


“Oh! Naona leo Barhams na Baffodil mmeamua kuunganisha nguvu kushambuliana na Kundi langu la Wimbi la chuma”Aliongea na palepale Azzle alipiga hatua moja mbele.


“Sisi Barhams , hatujawahi kuwa na uadui na yoyote , katika ulimwengu wetu usipokuwa rafiki yetu basi wewe ni adui yetu. Kama unataka kuwa adui yetu tunakukaribisha”Aliongea na kumfanya Gonzalez kuchezesha vidole vyake kama vile kuna kitu anafikiria.


“Kwa muda mrefu sana imekuwa ikifahamika Barhams ni kundi kubwa lenye nguvu la kimasenari duniani, lakini mimi sijawahi kukubali kuhusu hili. Kwasababu tumefikia hatua hii sina jinsi zaidi ya kuwaruhusu vijana wangu kufanya kile wanachotaka. Kapteni Azzle nitakupa nafasi wewe na ndugu yako Asmuntis kupigana na mimi , kama mtashinda nitakubali , ila mkishindwa msije kufikiria kuondoka hapa . Sisi Wimbi La Chuma , hatujawahi kukubali hasara , mnapaswa kupiga goti na kutuomba msamaha”


“Unaongea ujinga , unadhani wewe peke yako unaweza kumfanya Kapteni wetu na Mkuu Asmuntis kukupigia magoti?”Wanajeshi wa Barham waliongea kwa hasira”


“Mnapaswa kujivunia kwa Master wetu kutaka kupigana na wakuu wenu, mnaijua hadhi yake kwanza? Hapa mtu aliepaswa kushindana nae ni bosi wenu Prince of hell lakini ameamua kuwapa heshima kwa kutaka kupigana na hawa wawili”


“Helena usiongee hivyo , Asmuntis na Azzle ni wanajeshi wakubwa sana katika umoja wa muungano wa Inferno na pia ni watu wa karibu wa Lucifer . Nishawahi kupambana nao na sio watu wepesi wa kudharau”


Watu mara baada ya kusikia kauli hio walihisi matumbo kuanza kuchemka kwa msisimko mkubwa.


Hakuna hata mmoja aliedhania kutatokea jambo kama hilo kubwa kabla ya kuanza kwa Baraza la maksi.


Makundi mawili ya kimasenari duniani na kiongozi wa kundi kubwa la kimauaji duniani waliokuwa chini ya umoja ya Ki-inferno , wanaenda kupambana na Jitu chuma kiongozi mkuu wa kundi la kimasenari la Metal tide , mtaalamu wa mapigano ambaye alikuwa akiwania nyota ya Ugwiji.


Tukio kama hilo mara nyingi ni adimu sana kutokea na hakuna namna linaweza kuwachosha watu , kila mmoja alishikwa na hamu ya kutaka kuona kile kitakachotokea, huku watu wengi zaidi wakisogea katika eneo hilo.


Kutokana na umati mkubwa wa watu , Asmuntis na Azzle walihisi ni kama jambo hilo limeandaliwa na kama wataondoka bila ya kupambana ni kama kutengeneza ushahidi kupitia watu hao kwamba wameshindwa pambano kwa kumkimbia Gonzalez.


Lakini sasa bado hawakuwa katika hali ya kujiamini kama wangeweza kupigana na Gonzalenz na kushinda.


“Inaonekana hili eneo lishakuwa dogo na ni ngumu kupigania hapa , mnaonaje tukienda kwenye jukwaa la ngazi na kushindania kule”Aliongea Gonzalez akiwa na utulivu wa hali ya juu.


“Kama ni hivyo nakubali , ila nitashindana na wewe mimi peke yangu”Aliongea Azzle na kumfanya Asmuntis macho kumsinyaa lakini hakuongea neno.


Ukweli ni kwamba , ilikuwa rahisi kumuelewa Azzle , kwasababu kama wangepambana wote kumshambulia Gonzalez hata kama wakishinda ni rahisi watu kusema hakukuwa na usawa. Hivyo kwa ajili ya kulinda heshima ya Barhams na heshima ya Hamza , Azzle aliona ashindane yeye peke yake.


“Interesting! Kama ni hivyo basi leo hii nataka kushuhudia maajabu ya Kamanda namba moja wa jeshi la kujitegemea , Mfalme Azzle kutoka jeshi la jangwa”Aliongea Gonzalez na palepale aliongozwa na watu wake kutoka katika hilo eneo na kwenda eneo la juu kwa ajili ya pambano.


Azzle kabla ya kupiga hatua kumfuata , alimgeukia Asmuntis na kumnong’oneza.


“Mwambie bosi asije kutokea hata kama nishindwe”


“Nimekuelewa” Aliongea Asmuntis huku akiwa na wasiwasi katika macho yake.


Upande wa Hamza , Berly , Leviathani , Mamoni na wengine walikuwa wakinywa bia juu ya balkoni katika floor ya tatu ya jengo la hoteli pembeni ya jukwaa la wazi.


“Bosi hili pambano linakwenda kuwa la aina yake , Gonzalez naona anajitafutia kifo”Aliongea Mameni huku akicheka.


“Anakufaje sasa kwa kujiamini vile?”Aliuliza Hamza aliekuwa ameshikilia chupa ya bia akipiga mdogo mdogo.


“Bosi kuna haja ya kuuliza , kwa uwepo wako hapa kama akitaka kumuua Azzle si utaenda kumshughulikia tu mara moja”


“Ndio bosi! Halafu kwanini tusishuke chini bosi kumpa sapoti Azzle , pengine Gonzalez akikuona ataacha kupigana na Azzle”Aliongea Leviathani


“Haina haja , ngoja tuangalie kwanza . Ili mradi hatuoni hatari kwa Azzle , ni shindano la kawaida la kutambua nani mshindi na nani kashindwa. Kingine mimi nishastaafu mwenzenu. Kama hakuna tatizo kubwa sioni haja ya kuingilia”aliongea Hamza.


“Ni kweli kabisa bosi , kwa hadhi yako haina haja ya kujisumbua sana kwa mtu kama Gonzalez. Kama ni kupigana nae inapaswa kuwa mbele ya watu wa Baraza la maksi ili kuonekana dunia nzima ni kwa namna gani Gonzalez ni dhaifu na ni mwili tu unaombeba”Aliongea Berrly.


Ukweli ni kwamba Hamza alikuwa ashachoka kuendelea kujifanya ni mdhaifu. Alijiambia kama angeona Azzle yupo hatarini asingejiuliza mara mbilimbili na angeenda kumsaidia. Ila kama swala hilo sio hatari sana hakuona haja ya kujidhihirisha mapema namna hio. Isitoshe mshindani ambae alikuwa akitaka kushindana nae sio mtu wa levo za Gonzalezi yaani ni zaidi ya Gonzalez.


Unachopaswa kujua ni kwamba , kutokana na kuitishwa kikao cha kilele cha magwiji maana yake wale Magwiji wa dunia lazima wangekuwepo, hivyo maana yake ni kwamba lazima vurugu ingetokea tu baina yao na pengine kati ya umati huo wa watu moja ya magwiji hao wapo kama ilivyo kwa Hamza anavyoangalia kwa mbali , Hivyo kama angejitokeza na kuonyesha uwezo wake ingekuwa ni sawa na kujiuza na kuwafanya maadui zake kujipanga vizuri na ingekuwa na athari mbaya kwake.


Wakati wakiwa wanaongea , Gonzalez na Azzle walikuwa washapandisha juu ya eneo la wazi kabisa kama jukwaa lililotengenezwa kwa ngazi kuzunguka.


Licha ya Azzle kuwa mrefu , lakini bado alionekana kama mtoto mbele ya Gonzalez mwenye mwili mkubwa.


Muda ule walianza kuangaliana kama mapaka na upepo mkali ulianza kuvuma na yote hio ni kutokana na kudhibiti pumzi yao na kuruhusu nishati ya mbingu na ardhi kuvaa miili yao.


Kutokana na hilo kundi lote la waangaliaji , lilijikuta likikamaaa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.


Gonzalez alitoa tabasamu jepesi lakini kwa Azzle alikuwa na uso uliojaa usiriasi mno , ilikuwa ngumu kujua kama alikuwa na wasiwasi au yupo katika hali ya kujiamini.


Waliangaliana upande kwa upande , kila mmoja akimsoma mwenzake, hakuna aliekuwa na haraka za kushambulia.


Ilionyesha kutokana na mkusanyiko mkubwa wa watu ulivutia watu wa kila aina, Hivyo hata baadhi ya wanajeshi wa kitanzania waliofika kushiriki walivutiwa.


“Mnaangalia nini! Nipisheni mimi nataka kuona pia”


Sauti ya kibabe ya mwanamke ilisikika kutoka nyuma ya kundi. Alikuwa ni mwanamke alievalia koti la manyora ya rangi nyekundu na suruali nyesi na soksi za mikono , alikuwa na nywele zilizojikunja kidogo lakini ziliozompendeza na kumfanya kuonekana mwanamke wa kisasa zaidi. Alijichomeka katika kundi la watu mpaka alipoweza kujipenyeza na kufika eneo la ndani zaidi.


Mwanamke huyo mrembo mkononi alikuwa ameshikilia Ice Cream na alikuwa akiilinda isiharibike kadri alivyokuwa akijipenyeza katika kundi hilo la watu, na ile baada ya kupata nafasi nzuri ya kuangalia , aliendelea kulamba lamba akiwa katika mudi nzuri kabisa.


Haikuchukua dakika chache wanaume weusi walienda kusimama nyuma yake. Walioneakan kuwa wakubwa kuliko yeye na muda wote walikuwa wakimfuata nyuma nyuma kama wasaidizi.


“Madam Nyakasura , hatuwezi kuendelea kuwa hapa , tunapaswa kuwa hotelini kwa ajili ya kuendelea na kikao cha maandalizi ya kesho”Alikuwa ni moja ya mwanajeshi wa kitengo cha Malibu.


Ukweli ni kwamba hata wao ndio kwanza walikuwa wamefika mjini Limour, lakini wakati wakitaka kwenda hotelini kwa ajili ya kuanza maandalizi , matokeo yake Nyakasura alikataa kwenda nao hotelini na kukimbilia mtaani , ambako alipita kila palipomvutia na kununua vitu na kula kama mtoto . Sasa mara baada ya kuona kundi la watu limekusanyika ndani ya mtaa alishikwa na shauku ya kutaka kujua nini kinaendelea.


“Kama mnataka kwenda kwenye kikao sijawazuia , nyie nendeni tu . Mimi nataka kuangalia wanavyopigana”Aliongea Nyakasura akiwa ameshikwa na hamu pia ya kuona pambano hilo.


“Nyakasura wewe ni mtu muhimu sana kwenye timu yetu na pia unapaswa kushiriki katika kilele cha kikao cha magwiji . Tanaanzishaje kikao bila ya uwepo wako , tunapaswa pia kukuandalia hotuba utakayotoa mbele ya watu wa baraza katika kikao”Aliongea Mboma.


“Hebu acheni kunichosha na mambo yenu ya vikao , sijali nitakachoenda kuongea kwenye kikao na mniache, kaendeleeni na mambo yenu”


“Madam hili ni muhimu zaidi” Aliongea Juma msaidizi wa Mboma.


“Hamna mnachojua? Hili pambano ndio muhimu , pale yupo Mkuu wa kundi la Kimasenari Gonzalez na mwiingine pia ni mkuu wa kundi la Kimasenari , unadhani hili ni shindano la kawaida. Ni bora mkatulia mwangalie na muache kunisumbua”


“Ndio tunajua hili ni pigano zuri , lakini halituhusu na lipo nje ya malengo yetu yaliotuleta”


“Acha malelele na ujinga wako , huna utaalamu wa mapigano ndio maana unachukulia vitu kirahisi rahisi. Mkiendelea kunisumbua msinilaumu nikiwachoma moto”Aliwakodolea macho kuwaogopesha na kisha aliendelea kulamba icecream yake kwa raha zake.


Watu wa kundi la Malibu waliishia kukosa cha kufanya. Mwanamke huyo tofauti na Afande Simba hakuna mtu mwingine anaeweza kumwamrisha na akakubali jambo kirahisi.


Sasa tukio hilo Hamza aliekuwa amechill zake juu na bia yake aliweza kumuona Nyakasura katika kundi hilo la watu . Alishindwa kujizuia na kutabasamu na kwa namna alivyokuwa akizongwa zongwa na wanaume wale alijua lazima alikuwa amevutiwa na pambano hilo na anakataa kuondoka.


Ilikuwa ndio muda huo huo katikati ya jukwaa la ngazi , Azzle alijitutua kupandisha uwezo wake wote na upepo mkali ulianza kumzunguka katika miguu yake na palepale alifyatuka na kumsogelea Gonzalez kwa spidi.


Nishati ya Nafsi ya kweli iliokuwa imemzingira Azzle ilikuwa ni ya juu kabisa na kila hatua aliokuwa akipiga kumsogelea Gonzalezi ilikuwa ni kama vile ni gari la kusindilia barabara linatembea.


Mara baada ya kurusha ngumi yake kumlenga , ilionekana kuwa na nguvu kubwa mno , kama vile ulikuwa ni mtalimbo wa chuma uliorushwa kumlenga Gonzalezi kichwani.


Gonzalez macho yake yalichanua , huku akiinua mkono wake mmoja kupokea shambulizi lile.


Bam!!


Eneo alilokuwa amekanyanga lilititia , lakini hakuonekana kupata madhara yoyote na badala yake tabasamu la uovu lilimvaa palepale na alikunja ngumi na kisha aliirusha kumlenga Azzle kifuani.


Azzle alikuwa mwepesi mno kwani kabla ngumi ile haijamfikia kifuani haraka sana alidaka na mkono wake wa kushoto na kisha alipiga hatua moja kurudi nyuma na kujaribu kuvuta mkono wa Gonzalez ili kuuweka kwenye bega lake na kuubonda.


‘Ah!’


Ilikuwa maajabu , licha ya Gonzalez kuwa na mwili mkubwa lakini Azzle kama vile ni mcheza mieleka kwani aliweza kuurusha mwili wa Gonzalez chini kama furushi.


Boom!!


Shindo kubwa iliweza kusikika na kufanya watu wote waliokuwa wakiangalia kushikwa na hofu baada ya kuhisi mtetemeko mkubwa wa ardhi.


Spidi ya shambulizi lile iliwafanya hata watu wa Metal Tide kushikwa na hofu, Hawakudhania Azzle angekuwa wa kwanza kufanya shambulizi.


Sekunde ambayo mwili wa Gonzalez ulitua chini , ulitengeneza shimo. Mpiganaji wa kawaida kama angepatwa na shambulizi la namna hio pengine angekuwa katika maumivu makali sana kama sio kushindwa kuamka kabisa.


Lakini sasa licha ya kuangushwa chini, Gonzalez hakuonyesha kuumia kabisa na alienda mbali na kumshika Azzle mkono kwa nguvu asimtoroke


“Good Kung fu ,Nimesikia mbinu za mashambulizi uliozokuwa nazo ni nzuri sana. Hakika unaishi ndani ya sifa zako , ila ni muda wangu sasa wa kukuonyesha mimi ni nani”Aliongea Gonzalez huku akianza kucheka kwa sauti na muda uleule alimshika Azzle na kumuinua juu hewani kama kifurushi na kama vile anadunda mpira chini, kwa nguvu aliutua mwili wa Azzle kwa kuupigisha kwenye sakafu. Songa nayo hapa bure kabisa:- SEHEMU YA 196
Unatukosea sana tunaolipia kule kwa kutokuweka muendelezo kwa wakati.
 
SEHEMU YA 196.


Malkia Nyakasura.





Watu waliokuwa na moyo mwepesi hawakuweza kuangalia shambulizi lile kwani lilikuwa sio la kiubinadamu kabisa. Eneo ambalo Azzle alitupiwa palitengeneza shimo huku matofauti yakiporomoka.


Kama sio mbinu ya Azzle kuzunguka na kuruhusu mguu mmoja kutua chini kabla ya mwili angekuwa ameumia sana , pengine angeshindwa kuamka. Lakini hata hivyo licha ya kuhimili shambulizi hilo, alikuwa katika hali ya maumivu makubwa na kumfanya ahisi ni kama mwili wake umekufa ganzi.


Kabla ya Gonzalez kumsogelea kumshambulia tena, haraka sana alisimama kwa shambulizi kumlenga Gonzalezi kwenye kiganja cha mkono ili asimshike na kisha alipiga sarakasi na kurudi nyuma ya Gonzalezi na hakuchelewa palepale alimgeukia na kumpiga ngumi kisogo.


Bam!


Spidi ya Gonzalez ya kugeuka haikuwa kubwa kama ilivyokuwa kwa Azzle ndio maana alishindwa kukwepa shambulizi la ngumi.


Lakini hata hivyo Gonzalez kichwa chake ni kama kilikuwa kimevalishwa helmeti la chuma. Hakuhisi maumivu hata kidogo na badala yake Gonzalezi aliishia kucheka huku akimpiga Azzle teke na kumfyatua hewani.


Azzle alidondoka chini kwa kujizuia na mguu na mkono na kisha alifanikiwa kupata balansi na kusimama tena,. Aliishia kusugua tumbo lake ambalo lilikuwa katika maumivu makali na palepale uso wake ulizidi kuwa siriasi.


Ndani ya jengo Hamza alikuwa akiangalia yote hayo na mara baada ya kuona pambanno limefikia hatua hio aliishia kuhema kwa nguvu na kisha aliwaangalia wenzake.


“Tushukeni chini”Aliongea.


“Bosi si tuendelee tu kuangalia , sidhani Azzle anaweza kupoteza pambano kirahisi namna hio , bado hajatumia uwezo wake wote”


“Ameshapoteza pambano tayari. Hata kama Azzle na Mchafu waungane hawawezi kumshinda Gonzalez, asilimia kubwa ya binadamu jamii ya Gonzalez wanategemea nguvu zao za kimwili kujilinda na hawana uwezo mkubwa wa kimapgiano . Lakini Gonzalezi ni tofauti ana mwili wa kujilinda lakini vilevile uwezo wake wa kimapigano ni wa juu , hivyo ni ngumu kwa Azzle kushinda”


“Bosi unaongea kwa kututisha mbona , sidhani kama kuna utofauti mkubwa kati yao”Aliongea Mameni akiwa katika hali ya kushangaa na kabla ya Hamza kuelezea , waliweza kusikia sauti ya mwanamke ikipaza kwa nguvu kutoka chini.


“Wewe Azo hebu tumia nguvu zako bwana , kama huwezi kuchana ngozi yake kuna haja gani ya kuendelea kupigana!”Alikuwa ni Nyakasura aliekuwa akiongea kwa sauti kubwa ya kingereza akilalamika.


Watu waliomsikia walijikuta wakishikwa na ubaridi na kujiuliza mwanamke huyo ametokea wapi na ukichaa wake.


Nyakasura alikuwa si mshiriki sana katika mapigano nje ya nchi , ki ufupi hakusafiri sana kuja katika nchi za nje na ndio maana wengi hawakuwa wakimfahamu, hivyo maneno yake alioongea yalizarauliwa na watu.


Lakini hata hivyo Nyakasura hakujali sura za kumkejeli zilizokuwa zikimwangalia na aliendelea kuongea kwa nguvu;


“Kama unamshindwa muite ndugu yako huyo Asmuntis, si nasikia mna nguvu sana nyie , mnashindwa vipi kulipiga hilo furushi la chuma. Mnamtia tu aibu bosi wenu”


Hamza mara baada ya kusikia maneno ya Nyakasura alishindwa kujua alie ama acheke.


“Hehe bosi yule mrembo naona anakukubali sana , kwanini usimchukue?”Aliongea Berlly.


“Unadhani ni kuchukua tu kama unachukua nguo?”Aliongea Hamza.


“Bosi ni mrembo sana , kama humtaki ngoja mimi niende nikaingize voko mbili tatu”Aliongea na kumfanya Hamza kutabasamu kifedhuli.


“Mimi sina shida , kama umemkubali baadae mfuate urushe ndoano zako , ninakusapoti kwa asilimia mia”


“Bosi umeongea mwenyewe , usije tu kunigeuka . Kusema ukweli yule mwanamke ni mrembo kuliko hata wasaniii niliotembea nao”Aliongea Berrly huku mwili ukiwa mchangamfu.


Hakuwa akimjua mwanamke yule ni Nyakasura , hivyo alitaka kujaribu bahati yake.


Ijapokuwa maneno ya Nyakasura yaliingilia hali ya mapigano yale , lakini hakuwafanya waache kupigana.


Haikuchukua muda mrefu Azzle aliachia shambulizi lingine kwa Gonzalez.


Wote wawili walikuwa wakishambuliana kwa uwezo wao wote . Ngumi na mateke ya Azzle yalilenga maeneo dhaifu tu katika mwili wa Gonzalez.


Lakini mwili wa Gonzalez ulikuwa mgumu kuliko isivyokawaida na licha ya kushambuliwa kwa kasi hakuonyesha kama alikuwa akipata madhara kabisa.


Hamza na washikaji zake hatimae waliweza kufika chini , lakini hawakusogelea kundi hilo la watu haraka haraka , aliamua kukaa karibu na pambano ili akiona Azzle yupo hatarini awe na uwezo wa kumsaidia kwa urahisi.


Mara baada ya kumuona Hamza ameshuka chini , Asmuntis alijawa na wasiwasi katika sura yake.


Wakati huo huo Nyakasura alionekana kugundua jambo na palepale aligeuza kichwa chake na alifanikiwa kumuona Hamza.


Kama mtoto mara baada ya kumuona Hamza macho yalimtoka na kisha alianza kukimbia katikati ya kusanyiko hilo la watu kumsogelea Hamza.


“Hamza! Nilikuwa nikikikutafuta kule Paris, kumbe uliniacha na kuja mwenyewe”Aliongea huku akimwangalia kwa kutoridhishwa na tabia ya Hamza.


“Unamaanisha nini kukuacha. Hakuna mahali niliposema nitakuja na nyie huku mimi. Kwanza yule mkuu wako Mboma anaonekana kutonipenda”Aliongea Hamza akitingisha mabega.


“Kwanini unajisumbua na hao watu , kwanza na mimi nawachukia , hawana msaada wowote zaidi ya kuwa ving’ang’anizi”Aliongea Nyakasura kwa hasira.


“Bosi , kumbe unafahamiana na huyu mrembo?”Aliuliza Berlly.


“Kuna tatizo nikifahamiana nae?”


“Hamna , tena ni vizuri”Aliongea Berrly huku akijiweka mwili vizuri na nywele zake na kisha aliweka tabasamu la swaga na kunyoosha mkono wake kumpatia Nyakasura.


“Mrembo naitwa Berrly. Je tunaweza kufahamiana ?”.


“Sikujui kwanini nifahamiane na wewe ?”Aliongea Nyakasura akikunja sura, lakini haikumfanya Berrly kupoa kwenye kutupia mistari.


“Unajua dakika niliokuona tayari ushauteka moyo wangu. Unaonaje ukiurudisha?”


“Huna aibu kutumia mistari iliopitwa na wakati. Wewe ni babu? Hayo mashairi si ya miaka elfu ishirini iliopita?”Aliongea Nyakasura kwa kejeli na kumfanya Berrly mwili wake kukakamaa. Nyakasura baada ya kuongea hivyo alimsogelea Hamza kwa kujibana kwake.


“Hamza najua hukai hotelini, utaishi wapi kwenye siku hizi mbili zote?”


“Kwani unataka nini?”


“Sitaki kukaa hotelini mimi kushanichosha. Nataka nikakae unapoishi nikacheze, watu wako wa Inferno ni maarufu sana , nataka kuwaona wote”Aliongea na kumfanya Hamza asijue namna ya kujibu. Kung’ang’aniwa na mwanamke kama hivyo halikuwa swala jepesi.


“Wewe unahisi tupoje mpaka utake kutuona , unadhani ni watu wenye vichwa vitatu na mapembe?”Aliongea Hamza na Berrly mara baada ya kusikia mrembo huyo anachoomba aliona ajichukulie pointi.


“Mrembo tunaishi kwenye shamba la Farasi. Mimi ndio nimelikodisha. Kama hutojali tunaweza kwenda pamoja , utapata fursa ya kuendesha farasi , kula nyama choma na kunywa mvinyo wenye radha tamu isiokinaisha. Karibu sana..”


“Kumbe kuna farasi! Hamza nataka kwenda na mimi, niandalie chumba basi”


Hamza muda huo alitamani kumpiga Berrly kibao aache kuongea upuuzi. Maana hakutaka kuambatana na Nyakasura lakini Berrly kaharibu kila kitu.


Wakati huo katika jukwaa Azzle na Gonzalez walikuwa wameshambuliana kwa staili zisizopungua hamsini , ingawa mshindi hakupatikana bado , lakini Gonzalez alioneana kuwa na nafasi kubwa ya kushinda , upande wa Azzle licha ya kwamba hakuwa na uwezo wa kimwili kama aliokuwa nao Gonzalez , lakini katika mafunzo ya nishati walikuwa wakilingana kimadaraja. Hivyo pia hakukuwa na dalili ya kuonyesha pia alikuwa ameshindwa pambano.


Watu waliokuwa wakiangalia pambano hilo walikuwa wakipiga makelele ya kushangilia huku wengine wakimpongeza Azzle kwa kufanikisha kuhimili mashambulizi ya Gonzalez kwa muda mrefu.


“Azzle yuko vizuri sana , yaani ameweza kusumbuana na Gonzalez kwa muda mrefu hivi?”


“Sioni kama inashangaza sana , huyu ni mtu ambae alipigana vita takatifu, uwezo wake sio wa kubezwa”


“Ndio maana watu wanamuita mungu wa vita ya peninsula ni hivyo tu hana nguvu za ziada kama alivyo Gonzalez, vinginevyo angeweza kushinda hili pambano”


Kutokana na maneno mengi ya kumpongeza Azzle , Gonzalez uvumilivu ulianza kumshinda . Malengo yake yalikuwa ni kupata cheo cha hadhi ya Ugwiji , hivyo kusumbuana kwa muda mrefu na mtu wa Hamza ni kama alikuwa akijishushia hadhi yake.


Hivyo palepale aliona ni muda wa kumaliza pambano, na kufanya hivyo alivua koti lake la ngozi alilokuwa amevalia na kufanya misuuli yake kuonekana huku ikizidi kutuna.


“Graaaagh!


Gonzalez alivuma kama simba na kufanya misuli yake ya mwili kuonekana ni kama inaanza kushikwa na kutu huku ikizidi kupanuka na ndani ya sekunde tu mwili wake ulibadilika na kuwa jitu la chuma kamili la rangi ya silver iliojaa kutu.


“Kula chumaa!!”


Gonzalezi alikunja ngumi yake kwa nguvu na kisha kwa spidi alimsogelea Azzle na kumrushia ngumi ile kwa uwezo wake wote. Azzle na yeye kabla ngumi ile haijamfikia alirusha ya kwake kupangua ngumi ile ya Gonzalez lakini uzito wa ngumi ile ulimfanya kuhisi maumivu makali ya mifupa na kutoa ukulele wa maumivu huku akirudishwa hatua chache nyuma.


Aliishia kuangalia mkono wake wa kulia na palepale aligundua ulikuwa umemvimba mno kiasi kwamba hata nishati ya mbingu na ardhi ilishindwa kupooza uvimbe na maumivu.


Kwa namna mkono wake ulivyoumia , ingemchukua mwezi au miezi mwili mpaka kupona kabisa.


Masenari wa kundi la Metal Tide walishangilia kwa nguvu mara baada ya kuona kilichomtokea Azzle , wakati huo Masenari wa kundi la Barhams wakiwa katika wasiwasi mkubwa.


Ijapokuwa Masenari hao hawakutaka kupokea matokeo hayo , lakini waliamini kushinda kwa Gonzalez ni kwasababu ya mwili wake na sio uwezo. Lakini katika ulimwengu wa giza hakukuwa na sheria maalumu ya mapigano hivyo jibu la mwisho ni ameshinda na sio ameshinda vipi.


“Hakika anastahili kuingia katika hadhi ya Ugwiji , sidhani kama kuna mtu anaweza kushindana nae”


“Kweli kabisa , nadhani huu mwaka Gonzalezi anaweza kuchukua nafasi ya Lucifer ambae amestaafu na kushika cheo cha Nyota kumi”


“Inferno kukosa kiongozi wao , hakuna namna wanaweza kuendelea kubakia katika utukufu wao”


Watu walianza kujadiliana wao kwa wao wakilinganisha kundi la Inferno na la Gonzalezi. Wengi waliamini utawala mpya wa ulimwengu wa giza unakwenda kuwa chini ya Gonzalez na Inferno kubakia kuwa katika kumbukumbu tu.


Gonzalez mara baada ya kusikia makelele hayo ya sifa furaha yake iliongezeka na alikunja vidole huku akimwangalia Azzle kwa tabasamu la kejeli.


“Azzle sikutegemea kama utaweza kuvumilia pambano kwa muda mrefu kama hivi? Kwanini usiungane na Asmuntis kama nilivyopendekeza mwanzo mnichangie?”aliongea Gonzalez na kumfanya Azzle kumwangalia Asmuntis.


Wote walikuwa na wasiwasi , kwasababu mpaka kufikia hatua hio hali haikuwa shwali hata kidogo. Waliona hata kama wakiungana itakuwa ngumu kumshambulia na akaumia kutokana na ulinzi wa mwili wake. Lakini pia waliona hata kama hawawezi kushinda kama wangekubali kushindwa na kuondoka basi wangewapa Metal tide ushindi wa mezani kupitia hila zao.


Muda huo mara baada ya kuona wanajishauri , Gonzalezi aligeuka na kisha aliangalia upande aliosimama Hamza , alionekana kumuona licha ya kuwa mbali kidogo.


“Lucifer! Wewe ndio unaeshikilia hadhi ya cheo cha Ugwiji wa nyota kumi mpaka sasa , kwanini unaangalia watu wako wakiumia tu bila kuchukau hatua yoyote?”Aliongea kwa sauti kubwa iliojaa uchokozi.


Mara baada ya maneno yake hayo kusikika watu wote walijawa na mshangao mkubwa na kugeuka upande aliokuwa akiangalia Gonzalez.


“Nini! Yule ndio Lucifer!”


“Mungu wangu! Inamaana hakustaafu?”


“Nimesikia hakualikwa katika kilele cha kikao cha magwiji mwaka huu! Ila siamini kama rolemodel wangu karudi”


“Ni yeye kweli hebu angalieni pale yupo pia Mameni na Leviathani”


“Leo ni siku ya bahati sana! Sijawahi kudhania Gwiji ambae ameshinda vita takatifu na kuangusha jamii nyingi za siri akawa mdogo namna ile?”


Watu wote waligeuka na kumwangalia Hamza kama vile alikuwa ni jiwe la madini ya kung’aa , kila mtu alikuwa na mwonekno wa fanaka , heshima , mapenzi , woga na husuda.


Asilimia kubwa ya waliokuwa wakimwangalia walikuwa ni kama mashabiki ambao walitamani kumsogelea na kuomba sahihi yake.Lakini kutokana na umbali wa ki uwezo hakuna aliethubutu kusogea.


Hamza kuwa Gwiji namba moja mwenye hadhi ya nyota kumi , kiongozi mkuu wa Inferno alikuwa na mvuto wa juu sana wa kumuathiri mtu yoyote moyoni.


Kundi lote la Masenari la Barhams , mara baada ya kujua bosi wao amefika , haraka haraka walikimbia na kwenda kupiga magoti mbele yake.


MY- PRINCE!!


Wakiwa wamepiga magoti na mguu mmoja waliongea kwa nguvu kwa kuliita jina lake , huku macho yao yakiwa na viashiria vya machozi na msisimko wa hali ya juu.Hamza aliishia kutoa tabasamu tu na kisha aliwapa ishara ya kusimama;


“Azzle ndio kapteni wenu kwasasa, mimi na nyie tunafanana maana sio kapteni tena , hivyo hamna haja ya kuwa hivi”Aliongea Hamza.


“Wewe sio kapteni bali ni bosi wetu wa kiroho”Aliongea Kent kwa nguvu na kufanya wenzake warudie maneno yale.


Nyakasura mara baada ya kuona tukio lile aliishia kununa na kumwangalia Hamza bila furaha;


“Kwanini hawa washenzi wanakuabudu , una kitu gani cha maana cha kuwafanya wawe hivi?”


“Nyakasura chukulia mimi ni kama msanii maarufu na hawa ni mashabiki zangu , huna haja ya kuwa siriasi hivyo”


“Hawana wanachokijua kuhusu ulimwengu ndio maana wamekuwa wepesi kudanganywa na mtu kama wewe. Kuna watu katika dunia hii wana nguvu na madaraka makubwa kuliko wewe , kwanini wakusujudie wewe kama sio wajinga?”Aliongea Nyakasura.


Black Fog ambae alikuwa kimya muda wote hakuonekana kumpenda Nyakasura hata kidogo na alikasirika zaidi baada ya kuona mwanamke huyo anamzihaki Hamza wake.


“Unajua nini wewe! Unajua ni kitu gani Bro amekifanya kwa miaka yote iliopita , unajua ni watu wangapi walinufaika kupitia ushindi wake wa vita takatifu?”


“Wewe ni nani kwanza! Kama unamkubali kiasi hicho si umwambie akuoe na uwe mke wake?”


“Wewe..”Rhoda alikuwa amekasirika kiasi kwamba alitamani kushambulia palepale lakini Hamza alimuzia.


“Achana nae Rhoda”Aliongea na Rhoda aliekuwa hana furaha alisikiliza maneno ya Hamza, lakini Nyakasura uchokozi ulikuwa haumwishii kwani alimtolea Rhoda ulimi kumbeza.


“Kama unao uwezo nisogelee, unadhani nakuogopa?”Aliongea.


“Nyakasura mbona unapenda sana ugomvi , kuna haja ya kwenda hivi kisa tu mimi kuonyeshewa heshima?”


“Sijali na sikupendi. Kwaninii uwe maarufu?”


Upande mwingine mara baada ya Gonzalez kuona Hamza yupo bize kuongea na mwanamke badala ya kumjibu yeye alizidi kukasirika.


“Lucifer , unajifanya hunisikii sio au uwezo wako ni kama wa hawa watu wako tu?”


“Bosi , yule jamaa anashida kwenye akili yake! Ana uwezo wa kupigana na wewe au majigambo tu?”Aliongea Berly.


“Gonzalez huna akili! Kama sio huo mwili wako wa chuma unadhani ungeweza kumshinda Azzle , harafu unataka kushindana na bosi wetu, kipindi cha vita takatifu usingeweza kushindana hata na adui mmoja wa mahakama takatifu , lakini sasa hivi unadhani unalingana na bosi ki uwezo!”


“Ushasema wakati wa vita takatifu iliotokea miaka iliopita , unadhani dunia haizunguki. Uwezo wa Kapteni wetu ni kitu ambacho huwezi kufikiria kwa akili za kawaida”Aliongea Helena.


“Nachukia sana watu wanaojua kujisifia tu, Kwasababu hamtaki kukubali juu ya uwezo wangu leo nitawafanya mnikubali. Mnaonaje tukifanya hivi, Lucifer njoo tupigane?.”


Hamza pia alikuwa na furaha , miaka mitano iliopita baada ya vita takatifu kuisha , ili mradi watu walisikia jina lake wasingethubutu kumchokoza. Umaarufu na hadhi yake ilikuwa ya juu sana , hivyo kwa mtu wa daraja la Gonzalez kutafuta uchokozi na yeye aliona ni kama kichekesho.


Aliona akipigana na akashinda atalipa gharama na akishindwa vilevile hatopata manufaa hata kidogo. Ndio maana Hamza siku zote hakutaka kushindana na mtu ambae ana mchokoza makusudi.


Matendo ya Gonzalez yalimkumbusha kipindi cha nyuma , alikuwa akikutana sana na watu ambao walikuwa wakitaka kupigana nae , kiasi kwamba hata alipokuwa amelala aliogopa angeshambuliwa kwa kushitukizwa.


Black Fog , alikuwa na wasiwasi baada ya kuona pengine Gonzalez alishajua Hamza ni dhaifu , haraka sana alisogea kuingilia.


“Gonzalez kama unataka kupigana wewe pigana , haina haja ya watu kuonyesha uwezo wao kupitia wewe, Ukifanikiwa kuingia katika hadhi ya Magwiji pengine unaweza kuwa na haki ya kuongea maneno hayo”Aliongea Black Fog na watu waliona alikuwa na mantiki , walianza kumuona Gonzalez ni kama mtu mjivuni ambae anatafuta umaarufu kwa kulazimisha. Kwani kwa sheria na vigezo vya ulimwengu wa siri alikuwa dhaifu sana.


“Mh! Wewe kama mtu wa hadhi ya nyota kumi , unaogopaje kushindana kidogo na mtu kama mimi?,” Aliongea na kisha alianza kuwaangalia watu hao kwa kuzunguka na kisha akaendelea , “Mimi Gonzalez sijawahi kupenda wala kulazimisha kuwa maarufu. Ni kwamba tu awamu hii watu wangu wa Metal Tide walidhalilishwa hivyo lazima haki ipatikane, vinginevyo nitawaangalia vipi watu wangu usoni. Mimi kama kiongozi napaswa kusimama mbele na kutetea heshima ya watu wangu bila kupepesa macho”


Mara baada ya kuongea hivyo Azzle alitembea mpaka mbele ya Hamza na kisha akaongea kwa sauti ya chini ;


“Bosi haina haja ya kujishusha katika levo yake. Hastahili kupigana na mtu kama wewe”


“Ni kweli kabisa bosi , kwanza ushastaafu hivyo mpotezee”Aliongea Asmuntis na kumfanya Hamza kuangalia mkono wa Azzle uliovimba.


“Kama amesimama kwa ajili ya watu wake , nadhani sio mbaya na mimi kuweka juhudi kwa ajili ya mkono wako uliovunjika..”


“Lakini bosi..”Asmuntis alitaka kuongea lakini aliishia katikati.


“Hey Mchafu mbona unang’ata ng’ata meno , unaogopa bosi atamuua yule mshenzi? Hata akifa afe tu nini cha kuogopa bwana”Aliongea Mameni.


Hamza alitabasamu na kisha alipiga hatua moja kusogea mbele. Alipanga kuchukua fursa hio kuwaambia ukweli Aziz na wenzake juu ya uwezo wake.Lakini kabla hajapiga hatua kusogea jukwaani alizuiwa na Nyakasura.


“Niachie hili furushi la chuma nitadili nalo, usijusumbue kushindana nae”Hamza mara baada ya kusikia kauli hio alijikuta akishangaaa na hata washikaji zake pia walishikwa na hali ya kuchanganyikiwa.


“Wewe! Kwanini unataka kupigana na Gonzalez kwa ajili yangu?”Aliuliza Hamza kwa mshangao.


“Nani kakuambia naenda kupigana nae kwa ajili yako , kwa hawa watu wengi hivi lazima unataka kuichukulia kama fursa kwa ajili ya kujionyesha na kujibebea umaarufu zaidi na mimi siwezi kuruhusu”


Nyakasura alikuwa akimchukia Hamza kwa kujiaminisha kwamba kama walikuwa na uwezo sawa , kwanini yeye ndio anaabudiwa na watu wengi tena wazungu , alijiambia hio ni fursa ya yeye pia kujichukulia umaarufu. Katika kipindi chote hakuwahi kujionyesha hadharani na hio yote ni kutokana na watu wengi wa Kitanzania kuwa wa kawaida sana ambao kama angeonyesha uwezo wake tofauti na kupata mashabiki watu wangemuogopa. Lakini asilimia kubwa ya watu waliokusanyika hapo walikuwa ni wauaji , wanajeshi na wapiganaji wa kila aina hivyo wasingemuogopa na badale yake wangemshabikia.


Kuona namna watu walivyokuwa wakimtukuza Hamza na kufahamiana na watu maaarufu , aliitaka nafasi hio , alijihisi atakuwa na furaha sana kama kila anapopita watu watapiga magoti na kumsujudia kwa kuliita jina lake la Malkia Nyakasura. Hayo ndio yalikuwa mawazo ya mwanamke huyo, alitaka na yeye kuitwa Malkia Nyakasura.


Watu walivyosikia kauli ya Nyakasura waliishia kucheka , hawakumjua kama hakuwa binadamu wa kawaida pia , hivyo waliona ni msichana ambae anajitafutia kifo.


“Mrembo hebu acha kufikiria kujiingiza kwenye hatari. Siwezi kuona mwanamkie mrembo kama wewe ukiumia”Aliongea Berly huku akisogea mbele na akaendelea, “Mwanamke mzuri kama wewe unapaswa kulindwa”


“Hebu sogea huko!”Aliongea Nyakasura akiwa amemkazia macho Berly , bwana huyo alijikuta akijihisi maumivu na kujiuliza kwani amekosea nini ilihali anaonyesha kumjali.


“Sitaki kushindana na mwanamke , Lucifer usiniambie unataka mwanamke ndio akusaidie?”Aliongea Gonzalez na kufanya watu wa kundi la Meta Tide kucheka kwa nguvu na jambo lile lilimfanya Nyakasura kupandwa na hasira.


“Wewe furushi la chuma? Sisi wanawake tuna nini kwani? Unadhani unaweza kunipiga kwasababu tu mimi ni mwanamke?” Mara baada ya kuongea hivyo aligeuka na kumwangalia Hamza.


“Ole wako na wewe usogee hapo , nitakuunguza mpaka ufe , ngoja nilifundishe kuheshimu wanawake hili jitu”Aliongea akiwa siriasi na kumfanya Hamza asiongee tena , aliona ni kheri kumuacha tu mwanamke huyo achukue nafasi la sivyo , mchumba huyo wakishafika huko shambani anaweza kumuunguza akiwa amelala kwa hasira.


“Haya sawa Madam Nyakasura , kama unataka kwenda wewe nenda , leo nitakuwa shabiki wako”Aliongea Hamza huku akitoa tabasamu.


“Boss! Kwa uwezo wa Gonzalez nadhani sio vizuri kumruhusu huyu msichana kwenda..”Aliongea Asmuntis kwa wasiwasi na kauli yake iliungwa mkono na washikaji zake wengine wote. Waliona pengine Nyakasura ni mpenzi wa Hamza na kama atapata majeraha halitokuwa jambo zuri.


“Kama anataka kupigwa mwache aende. Master kwanini unamzuia?”Aliongea Black Fog ambae hakuwa akimpenda kabisa Nyakasura.


Nyakasura alihisi kudharauliwa kwa mara nyingine na alijikuta moyo wake ukifurukuta kwa hasira zidi ya Black Fog.


“Wewe mshenzi unanichukiza mno , ila ngoja nitayafungua macho yako”


Mara baada ya kuongea vile , chini ya kundi hilo la watu Nyakasura aliruka na kwenda kutua kwenye jukwaa huku mkononi kukiwa na miale ya moto.
 
“Hey Furushi la chuma anza kushambulia sasa nimekuja”Aliongea Nyakasura.


Kundi lote la watu waliokuwa wakiangalia walishikwa na butwaa.


“Huyu mwanamke nae ni Adept?” Adept maana yake Wasiowakawaida.


“Sidhani kama ni hivyo , anaonekana kama mtu mwenye mafunzo ya juu ya nishati za mbingu na ardhl”


“Ule moto wake ni wa maajabu ya aina gani , licha ya kuwa mbali hivi lakini unafanya mapigo ya moyo kwenda mbio?”


Watu ambao hawakuwa na uzoefu juu ya mambo yaliokuywa yakiendelea katika ulimwengu wa siri au wa Giza ilikuwa sahihi kupaniki na kushindwa kuelewa chimbuko la Nyakasura. Lakini wataalamu wengi waliokuwa katika eneo hilo wenye uzoefu hamasa ziliwavaa na kuona hatimae mapigano yanakwenda kuchukua sura mpya.


“Bosi! Usiniambie ndio mwanamke wa kifoeniksi tuliekuwa tukisikia jina lake?”Aliuliza Azzle kwa mshangao mkubwa , alikuwa ashasikia sana kuhusu Phoenix Girl na uwezo wake ila hakuwahi kumuona ana kwa ana.


“Nadhani sasa mmejua kwanini sipendi kubishana nae”Aliongea Hamza akiwa na tabasamu.


Washikaji wote walitingisha vichwa kumuelewa huku Berrly ambae alikuwa akimuwazia msichana huyo akiwa uchi juu ya kitanda cha sita kwa sita alijihisi kutetemeka mwili mzima na mawazo yake ya kishenzi kumpotea mara moja.


“Daah bosi! Ulitaka kuniona nikifa , yaani uliniacha tu nikijaribu kumtupia mistari mwanamke hatari kama huyu?”Alilalamika.


“Bosi anastahili kuitwa bosi siku zote, yaani kwenda Tanzania tu miaka michache ashajuana na mrembo wa kifoeniksi. Siamini tutatembeaje kama kati ya mashemeji zetu hapo baadae mmoja wapo akawa ni huyu mrembo haha..”Aliongea Big.


“Hebu kaa kimya asije kukusikia na ukaunguzwa na moto wake”Aliongea Leviathani akimwangalia Mameni kwa macho ya kuonya kama vile anamwangalia mdogo wake.


Black Fog aliishia kushangaa sana , baada ya hatua ya huzuni kupita hatimae alijua kulikua na gepu kubwa la uwezo kati yake na huyo mwanamke.


Hatimae sasa alijua msichana huyo alikuwa ni moja ya magwiji kumi wa dunia ambae anakweda kupambana na Gonzalez. Watu wote wa Hamza walijikuta wakiwa katika hali ya shauku kubwa mno.


Ikumbukwe kwamba kuna magwiji kumi tu ambao wamepewa vyeo na Baraza la maksi na kati ya hao kumi na Nyakasura alikuwepo na ndio maana watu kama Leviathani na wenzake wamelisikia jina lake , lakini sio hivyo tu ndio maana nchi kubwa hazikujaribu kushurutishana moja ka moja na serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuipata Earth Axis. Kama isingekuwa uwepo wa Nyakasura katika kitengo cha Malibu serikali kubwa kama ya Amerika na jeshi lake wasingesita kuishambulia Tanzania na kuinyakua Earth Axis kama walivyofanya katika mataifa ambayo walikataa kutoa rasilimali zao.


Gonzalez hakuamini mwanamke ambae aliongea kwa kumkejeli alikuwa ni hatari namna hio.


“Sikutarajia utakuwa ndio wewe msichana maarufu wa damu ya Phoenix. Mimi kinyongo changu ni zidi ya Lucifer , sina ugomvi wowote na wewe”Aliongea Gonzalez.


“Kimya na ujinga wako , unatudharau sana sisi wanawake na nachukia watu ambao mpo sexist kama wewe, Kwa niaba ya wanawake wote kama usipofanya chochote usinilaumu nikikugeuza uji wa chuma”Aliongea Nyakasura kwa ukauzu na kujivunia.


Watu wa kitengo cha Malibu walihisi ukichaa ulikuwa ukienda kuwavaa . Walijiuliza imekuwaje ghafla tu Nyakasura akaununua ugomvi huo?.


“Madam Nyakasura , tunaomba usinunue ugomvi , tupo hapa kwa malengo tofatui”Aliongea Mboma kwa masikitiko lakini Nyakasura hakujali meneno yao.


Gonzalez alijikuta akiwa katika mgogoro wa nafsi , hakuwa na uhakika kama akipigana na huyo mwanamke angeshinda na aliona pia kama angeacha basi mpango wake wote ungekuwa ni bure tu.


Palepale alijiambia kwasababu alikuwa akitaka kuingia katika daraja la Magwiji basi hana namna zaidi ya kushindana na magwiji.Hivyo kwa kukosa namna aliona ni kheri kujiandaa tu na lolote.


“Kama ni hivyo nipo tayari kuona uwezo wa damu ya Phoenix” Mara baada ya kuongea hivyo palepale alianza kukusanya elementi za chuma na kuzielekeza katika ngozi yake na kufanya misuli yake kuanzia mikononi mpaka miguuni kuwa kama chuma.


“Mwili wa chuma!!”


Aliongea Gonzalez kwa nguvu na pale umbo lake lilibadilika na kuwa kubwa zaidi na misuli yake ilizidi kuwa ya kung’aa kama upanga.Ilikuwa ni kama vile mwili wake wote umevalishwa mavazi ya chuma kilichong’ariswa vizuri.


Dakika ambayo alinyanyua mguu wake na kupiga hatua , alikuwa ni kama transfoma kwani alifanya matofali kubondeka bondeka na kutengeneza shimo.


Msisimko aliokuwa akitoa ulifanya baadhi ya watu kushindwa kupumua vizuri.


“Ndio lenyewe sasa ,hili ndio jitu chuma halisi. Hakika natisha sana”


“Kwa mara ya kwanza tumebahatika kuona magwiji wawili na kuona mwili halisi wa chuma Gonzalez katika uwezo wake wote”


Waangaliaji wa pambano walikuwa katika hamasa ya juu sana . Pambano hilo lililokwenda kuanza lilikuwa kubwa zaidi kuliko la mwanzo na Azzle.


Nyakasura alikuwa na mwonekano wa kawaida sana wakati huo mikono yake ni kama vile ilikuwa ikiungua na moto na alionekana kukosa uvumilivu wa Gonzalez kumaliza kujibadilisha.


“Hujamaliza tu! Kwanini unapiga makelele sana kuita uwezo wako?”


“Apologies!” Gonzalez alinguruma kama roboti na palepale alimsogelea Nyakasura kama kiboko na ngumi yake iliobeba upepo mwingi akiilengesha.


Moto uliokuwa katika mikono ya Nyakasura ulitawanyika na kugeuka kama mapovu ya moto na kumsogelea Gonzalezi kwa spidi.


“Mvua ya moto!!”


Mapovu yale ya moto palepale yakiwa hewani ni kama yalisikia agizo la Nyakasura na palepale kwa kasi ya ajabu yalimvaa Gonzalez na kufanya sauti kama ya kuchomelea chuma ianze kusikika , ilikuwa ni ‘ Siziiii!’ isiokuwa na mwisho.


Kundi la watu wote lilijikuta likirudi nyuma kukaa mbali zaidi kwa hofu.


Ingawa Gonzalez alikuwa na uwezo wa kuvumilia maumivu ya kuungua kwa chuma chake katika mwili lakini asingeumia mara moja na kushindwa , lakini kuendelea kuungua namna hio haikuwa nzuri kwake.


Licha ya kuunguzwa na moto wa Nyakasura alivumilia na kumsogelea mwanamke huyo na kutaka kumpiga ngumi , lakini ngumi ile kabla haijamfikia, moto uliokuwa katika mikono ya Nyakasura uligeuka na kuwa mjeledi kama kamba na kujiviringisha katika mikono yake


“Ziiii.si…. ziiii!!”


Tabaka la juu la ngozi ya chuma liliyeyuyka na kwa haraka sana mkono wake ulionekana kuungua.


Wakati huo Nyakasura alitumia nishati za mbingu na ardhi na kuelewa angani na kufanya shambulizi lile la Gonzalez kutomgusa kabisa.


“Wepesi wa juu sana , hakika ana stahili kuitwa Phoenix girl”


“Upo sahihi , nilijua uwezo wake upo katika moto , lakini anaonekana kuwa na mafunzo ya hali ya juu ya kimapigano pia”


Wachambuzi kadhaa wa mchongo walifanyia uchambuzi wa haraka haraka shambulizi la kwanza.


Watu wa kundi la Wimbi la Chuma walikuwa katika wasiwasi mkubwa mno hasa baada ya kuona namna pambano lilivyomgeukia bosi wao na kuwa gumu. Upande mwingine wa Barhams walimshangilia Nyakasura.


“Moto wa Nyakasura ni mkali mno , yaani unaweza kuyeyusha mwili wa Gonzalez!!?”Aliongea Asmuntis aliekuwa pembeni ya Hamza.


Hamza aliishia kutabasamu tu na kujisemea kimoyo moyo kwamba pale ilikuwa mwanzo tu na ni kama shambulizi la kitoto , kipindi alichokuwa akipambana na Nyakasura ni kama alikuwa katika jehanamu ya moto. Nyakasura hakuwa amefikia uwezo wake wote bado, na mbinu alizotumia zilikuwa zile nyepesi nyepesi.


Hamza alikadiria Nyakasura anaweza kushinda hilo pambano pengine bila ya kutumia uwezo wake wote wa andiko la mbingu tisa za moto. Alijua kama akitumia uwezo wake wote wa juu basi hata watu waliokuwa hapo wanaweza wasivumilie , kwani moto wake haukuwa ukishambulia kwa joto tu bali uliunguza hata nafsi kabla ya kugusa mwili.


Gonzalez aliona mwili wake bado haukuwa na nguvu za kutosha kuhimili moto wa Nyakasura , hivyo aliacha kushambulia na badala yake macho yalitua katika moja ya nguzo ya taa(Lamppost) karibu yake na haraka sana aliishikilia na ajabu yake ni kwamba nguzo ile ni kama ilianza kugeuka mchanga kwani elementi zake zote za chuma zilimwingia Gonzalez huku elementi nyingine kama kutu na rangi zikidondoka chini kama vumbi na sekunde tu nguzo ile ilipotea.


Baada ya vile mwili wake ulirejea katika utukufu wake na elementi za ziada katika mwili wake ziligeuka na kuwa ngao.


“Uwezo wa kusharabu chuma na kukipindisha ni uwezo wa juu sana , mtu kama huyu kama angekuwa karibu na machimbo ya chuma ni ngumu kumshinda”Aliongea Leviathani.


“Ndio maana kudili na mtu wa aina yake ni kumshambulia na pigo moja tu na kumuua”Aliongea Asmuntis.


“Sidhani kama ni hivyo , kwa uwezo wa moto wa Phoenix haijalishi Gonzalez atasharabu mara ngapi chuma , ataishia kuyeyushwa tu mpaka vyuma vya kusharabu viishe”


Wakati kila mtu akifanya uchambuzi wake juu ya mapigano hayo , Gonzalez kwa mara nyingine alifunikwa na moto wa Nyakasura. Alijaribu kumshambulia Nyakasura na elementi za ziada za chuma kupitia ngao yake , lakini alizidwa ujanja kwa mara nyingine kwani Nyakasura hakuishia kumchapa na mjeledi wa moto wa mikono tu na badala yake aliigawanya kwa wingi ile mijeledi ya moto na kumfunga miguuni na mikononi na kuanza kuyeyuka kwa mara nyingine


“Arghhhhhhh!!”


Gonzalez alijikuta akipiga goti bila ya kupenda huku akitoa ukulele mkali wa maumivu. Ijapokuwa aliunguzwa kwa sekunde tu na kuruudi katika hali yake ya kawaida lakini akili ilimuwehuka.


Nyakasura mara baada ya kuona vile , haraka sana alifanya shambulizi lingine kwa kumrushia boriti ya moto na Gonzalez aliweza kukwepa boriti ile lakini bado aliunguzwa mkononi lakini ajabu yake hakuungua wala kuyeyuka kama mwanzo.


“Nini kimeotokea , mbona hayeyuki tena ?”Aliongea Mameni kwa mshango.


“Gonzalez anaonekana kutumia akili , inaonekana amesharabu elementi za chuma cha pua na kujifunika nazo kama ngao na ili kuyeyuka inahitajika zaidi ya digrii elfu tatu za joto mara mbili ya chuma cha kawaida. Ijapokuwa kinaweza kuwa kiasi kidogo cha elementi za chuma cha pua alizosharabu lakini inatosha kugeuza kuwa ngao”Aliongea Hamza.


Muda huo Gonzalez ambae alifanikiwa kuhimili joto la Nyakasura palepale alisimama juu na kuruka juu na kufyatua ngumi huku kwa wakati mmoja akiwa amenyoosha kidole kimoja ambacho kadri alivyokuwa akimsogelea Nyakasura kiliongezeka urefu na kuwa kama mkuki wa chuma.


Nyakasura hata yeye hakutemegea Gonzalez angeweza kugeuza mwili wake kutoka kuwa chuma cha kawaida na kuwa aina nyingine ya chuma kigumu.


Mara baada ya kuona kidole chake kimeguka na kuwa mkuki wa chuma hakupaniki na badala yake aliikutanisha viganja vyake vya mikono pamoja na palepale miale ya moto wake ilijigeuza na kuwa kama nyuzi nyuzi za umeme wa bluu na ndani ya sekunde tu alivyofungua viganja vile kulionekana kitu kama puto kubwa la moto wa bluu.


“Pigo la radi!!”


Dakika ambayo puto lile la moto lilivyogusana na mkono wa Gonzalez mlipuko wa moto wa bluu ulitokea na kutoa sauti kama vile ni radi,wakati huo Nyakasura alitumia nishati za mbingu na ardhi kuendeleza kusafirisha moto katika puto lile licha ya kuwa mita kadhaa mbali.


Gonzalez na yeye alijikuta akihangaika kiasi cha kurudi hatua moja nyuma , mkono wake uliokuwa ukipambana na msukumo wa puto lile la moto ulianza kugeuka na kuwa mwekundu.


Ijapokuwa ilikuwa ngumu kujua nani angeshinda lakini Nyakasura alionekana kuwa katika utulivu zaidi kuliko Gonzalez ambae alikuwa na hali ya kupaniki.


“Wewe jitu , huna mbinu nyingine ya mashambulizi tofauti na kujigeuza chuma , kwa spidi yako ndogo inanifanya niboreke hata kupigana na wewe”Aliongea Nyakasura ambae alijihisi ni kama anapigana na ukuta wa chuma na kumfanya aboreke maana hakukuwa na ubunifu wowote kutoka kwa Gonzalez.


Gonzalez alijikuta akishangaa kisirisiri , ijapokuwa alishawahi kusikia kuhusu uwezo wa damu ya foeniksi lakini hakutegemea kuona mwanamke huyo haingiliki hata kidogo.


Ni kweli alipanga kuingia katika orodha ya magwiji lakini hakutaka kuingia kwa kuweka rehani uhai wake na kuendelea kupigana na Phoenix. Mpango wake ulikuwa ni kumdhalilisha Hamza ambae hana uwezo wowote wa nishati za mbingu na ardhi na kisha kuchukua hadhi yake.


“Kesho ni siku ya Baraza la maksi , kama unataka tupigane kwa uwezo wa juu basi tupigane hio siku. Sioni haja ya kupoteza nguvu zetu hapa. Mbele ya Baraza la maksi tutaweza kuonekana mbele ya wapiganaji wakubwa duniani. Unaonaje tukifanya leo iwe sare?”


“Unaongea kama vile nataka sana kupigana na wewe , unaweza kujiona mshindani wangu lakini mimi sikufirikii kama mshindani. Sitaki kuendelea na pambano linaniboa tu”


Mara baada ya kuongea hivyo alitembea na kwenda kusimama mbele ya wanajeshi wa kitengo cha Malibu:


“Nitandoka na Hamza na marafiki zake nikacheze , nyie mnaweza kwenda hotelini tu tutaonana kesho”


Mboma na wenzake waliishia kuwa na sura zilizokuwa zimejikunja lakini hawakutaka kupinga.


Ukweli ni kwamba ndio sasa wamefahamu Hamza ndio mtu ambae anasifika katika ulimwengu wa siri kwa kuitwa Prince of hell ambae aliongoza jamii ya siri ya Inferno.


Mboma alijilaumu kwa kutolijua hilo mapema , alikumbuka namna alivyomdharau Hamza mwanzo na hali ya kujiamini iliisha palepale , hivyo hakutaka kuongea neno lolote. Lakini kwa wakati mmoja waliomba Hamza bado aendelee kuwa upande wao.


Hamza mara baada ya kuona Nyakasura anataka kwenda na yeye Shamba alijikuta akikosa namna ya kumkaatalia , hivyo aliishia tu kujilazimisha na kutabasamu.


Upande mwingine Asmuntis na wenzake walijikuta wakiwa na furaha mno. Waliona kuwa karibu na mwanamke mwenye nguvu namna hio ingewapandisha hadhi zaidi na zaidi.


Gonzalez mara baada ya kurudi katika hali yake ya kawaida , alichukuana na watu wake na kwa kujiamini alisogea mpaka mbele ya Hamza.


“Lucifer ni bahati mbaya sijapata nafasi ya kupigana na wewe leo hii kwasbabu ya huyu mwanamke wa kifoeniksi kuingilia , ila kundi letu la wimbi la chuma na la kwako la Barhams , bato hatujamalizana. Kesho siku ya Baraza usipotoa maelezo ya kutosha basi nitaomba pambano rasmi kupigana na wewe kwa ajili ya watu wangu”Mara baada ya kuongea hivyo kwa jeuri aligeuka na kuondoka na wafuasi wake.


Watu waliosikia walishangaa kwa kuona ni Gonzalez ni mwamba kutaka kushindana na mtu kama Hamza.


“Kwanini anang’ang’ania kupambana na wewe sana?”Aliuliza Nyakasura.


“Mimi najuaje sasa , hebu achana nae na turudini shamba nikapumzike”Aliongea Hamza , hakumchukulia kabisa Gonzalez siriasi.


Watu waliokuwa katika eneo hilo wakiangalia hawakufurahi kuona pambano halijaisha vizuri , lakini isingewezekana kuendelea kupigana hivyo walianza kutawanyika huku wakisubiria kwa hamu kitakachojili siku ya kesho yake katika Baraza la maksi.Huku wengi wakijiuliza je kweli Hamza atakubali kupambana na Gonzalez?.


****


Muda mchache mbele , alionekana Gonzalez akiwa ameketi kwenye sofa ndani ya jumba la kifahari ndani ya Limour huku akiangalia mkono wake.


Hakuwa na majeraha tena katika mkono huo, ukweli ni kwamba hata kama mkono wake wote uyeyuke , ili mradi yupo katika hali ya mwili wa chuma unaweza kupona na kurudi upya.


Yalikuwa yamepita masaa kadhaa tokea pambano liishe , lakini moyo wake ulikuwa ukidunda kwa nguvu.


“Phoenix Girl .. Mtaalamu daraja la Ugwiji ..”Aliongea mwenyewe na muda ule Helena akiwa na makada kadhaa waliingia ndani ya eneo hilo na kumpigia Gonzalez saluti.


“Kapteni , hakuna tatizo kubwa kuhusu majeraha ya Gray , dokta wa jeshi amesema anaweza kutibiwa na kupona”


“Vizuri! Kwasasa nendeni mkaandae mpango wa kesho , hakikisheni hamfanyi makosa”


“Sawa Kapteni!”Waliitikia na baadhi ya wale makada wakati wakitoka Helena alibaki na kumwangalia Kapteni wake.


“Kapteni umeutingisha ulimwengu leo. Yule kiongozi wa Inferno hana aibu kabisa kuruhusu mwanamke amsaidie. Nina uhakika kesho ukishindana nae lazima upande cheo”


“Phoenix girl ni gwiji wa daraja la juu , kama ikitokea kesho nikapangiwa nae kupigana sipaswi kumdharau kabla ya kutumia uwezo wangu wote. Lakini bado nina mashaka , Lucifer licha ya kuona Azzle ameumia hakuchukua hatua , ni kweli hana uwezo wowote”Aliongea.


“Master sababu ya Phoenix kukuhangaisha ni kwasababu ya sifa yake ya kutengeneza moto , ila kama ni mtaalamu mwingine asingeweza kushindana nae hata kidogo kama wewe ulivyofanya. Kapteni usidharau uwezo wako ni mkubwa mno”


“Upo sahihi! Kwasababu kesho ndio siku ya ufunguzi wa Baraza la Maksi ni muda sahihi wa kuonyesha ulimwengu ni nguvu kiasi gani tupo nayo sisi Metal Tide”Aliongea.


******


Upande wa Shamba mara baada ya kufika , kila mtu alimkaribisha Nyakasura kwa ukarimu mkubwa.


Berrly kama kawaida alichangamka na kuita kundi la watu na ng’ombe mzima alichinjwa na kuchomwa moto na kufanya watu wafurahie nyama tamu pamoja na bia huku wakiangalai jua likizama.


“Mrembo Nyakasura . nimesikia sana kuhusu sifa za jina lako lakini sikutarajia mwonekano wako utakuwa ni wa kupagawisha kuliko hata uwezo wako. Can I, Beryl, be lucky enough to invite you to taste the steak that I've roasted?”


Aliongea Berrly kiswaga mbele ya Nyakasura akiwa ameshikilia na uma steki ya nyama.


“Nataka ilioiva vizuri, kwanini unanipa ya hivyo mimi?”


“Oh! Kumbe unataka ilioungua kwa asilimia mia moja , ngoja niichome tena”


“Hebu acha tu maana upo slow sana , nitaiivisha mweyenye vizuri”Aliongea na palepale aliachia moto. Kitendo kile kilimfanya Berry apige yowe la mauvimu kutokana na kuungua kwa mkono wake.


“Unalia nini sasa , nenda kaniletee ilioiva vizuri”Aliongea kwa kuamrisha na Hamza aliekuwa akitoka ndani alisogea na kumpiga piga Berly begani.


“Berly unapaswa kukaa mbali , Nyakasura sio mwanamke ambae unaweza kuongea nae kama unavyofanya kwa wanawake wengine”Aliongea.


Unadhani kitajili nini kwenye Baraza la Maksi.Usikose
 
SEHEMU YA 198.


The White Queen.


Nyakasura mara baada ya kumuona Hamza amefika , alifuta midomo palepale na kumwangalia:


“Nimesikia hapa kuna farasi , nipeleke basi nikaendeshe?”Aliongea na Hamza kabla ya kumijibu aligida pafu la bia kwanza;


“Farasi wapo upande ule kwenye zizi. Unaweza kwenda na kuchagua mmoja na kumtoa nje , kwanini unataka nikupeleke?”


“Mimi ni mgeni hapa, si sahihi kwa mwenyeji kunipeleka?”Aliongea Nyakasura akiwa hajaridhika.


Hamza alijiambia ni mgeni gani anajikaribisha mwenyewe , lakini kutokana na kuhofia tabia yake aliamua tu kumkubalia.


“Sawa nitakupeleka ukaendeshe”


Nyakasura kusikia hivyo , furaha ilimvaa palepale na kuchukua mhindi wa kuchemsha na kumnyooshea achukue.


“Hivyo ndio inavyotakiwa , malizia na huu muhindi kwanza”


Hamza aliangalia mhindi huo , ingekuwa afadhali ulikuwa haujaguswa ila mwanamke huyo alikuwa amekula nusu na kuubakisha na kibaya zaidi ulikuwa na mate ya kutosha.


“Asante ila nimeshiba sana”


“Mh! Nilikuwa nakujaribu tu , siwezi kuruhusu mtu wa kawaida kama wewe kumalizia nilichoanza kula”Aliongea.


Pembeni Leviathani , Mameni na wengine mara baada ya kuona tukio hilo waliishia kutingisha vichwa vyao tu , waliona ni msichana huyo pekee ndio anaeweza kumuendesha Hamza atakavyo ila sio wao.


Ilibidi wawaache wengine kumalizia kutafuna nyama huku wao wakiongozana mpaka kwenye zizi la farasi


“Mbona wote ni weusi tu , hakuna mweupe?”Aliuliza Nyakasura huku akionekana kutoridhishwa na farasi hao.


“Hawa weusi ndio wazuri sasa, wana damu ya kifalme na ni ghali zaidi kuliko farasi wa kawaida. Wewe ni Nyakasura hivyo unapaswa kuendesha wa hivi , kwanini unataka kuendesha kulingana na rangi yake?”


Nyakasura mara baada ya kusikia hivyo , aliona ni kweli na aliridhika na maelezo ya Hamza.


“Upo sahihi , mimi pia nina damu ya kifalme hivyo napaswa kuendesha farasi yenye damu ya kifalme. Leo umejua kuniridhisha na maneno yako”


Hamza aliishia kufurahi kisirisiri , ni kama sasa alijua namna ya kudili na mrembo huyo , ili kumfanya akubali ni kuongea kile ambacho anataka kusikia.


Hamza alimtoa farasi mmoja mpaka nje ya zizi na kisha kumpa ishara ya kupanda.


Nyakasura mwili wake ulikuwa mwepesi mno kwani aliruka na kutua katika mgongo wa farasi juu ya tandiko lake na kisha alishikilia hatamu. Farasi ile ilionekana kutishika na kuanza kupandisha miguu yake ya mbele hewani ikitaka kumtupia Nyakasura chini.


“Ahh! Inafanya nini hii ?”


Nyakasura yalimshinda na alijikuta akiruka kutoka kwenye Farasi na Hamza haraka haraka alisogelea ile farasi na kuishikilia.


“Wewe umefanya kuirukia ulifikiria ni bindamu huyu , kwanini usingepanda kawaida tu?”


“Sasa si ungesema , au ulitaka kuona nikidondoka?”Aliongea huku akiwa ameweka mikono yake kiunonni.


“Sasa mimi ningejuaje kama inaogopa kurukiwa?”Aliongea Hamza akijitetea na kumfanya Nyakasura kumwangalia kwa macho ya mashaka na kisha alipanga kujaribu tena.


“Wewe Farasi ole wako utake kunidondosha tena , nitakugeuza nyama”Aliongea Nyakasura bila ya kujali farasi hio ilikuwa ikielewa maneno yake au lah.


Mara baada ya kupanda , hatimae alifanikiwa kukaa bila ya farasi ile kuleta ukinzani


“Haha.. Hamza umeona hii farasi inaniogopa?”


“Ni kweli kabisa. Inaonekana kuogopa nguvu zako za kifoeniksi”Aliongea Hamza kumridhisha.


“Tembea”


Nyakasura alitingisha ile hatamu ya farasi lakini farasi ile haikusogea hata kidogo zaidi ya kutingisha kichwa chake kulia na kushoto.


“Hii farasi mbona imekaa kivivu vivu , kwanini haitembei?”Nyakasura alijikuta akikasirika baada ya kuona farasi hio inakataa kumtii, “Wewe farasi kimbia”


Hamza alitamani kucheka kuona mwanamke huyo anataka kuendesha farasi kwa kuiamrisha na maneno.


“Hebu fanya kukandamiza miguu yako kwa pamoja kwenye tumbo lake uone”Aliongea Hamza.


Nyakasura alifanya kama Hamza alivyoongea na kweli farasi ile ilianza kutembea kwenda mbele.


“Wow! Inatembea. Vipi nikitaka itembee kwa kasi?”Aliuliza na Hamza alifikiria kidogo.


“Unaonaje tukiendesha pamoja , nitakufundisha kidogo , ijapokuwa hio kamba ni kwa ajili ya kuongoza lakini mwili wako ndio unaoweza kuiongoza farasi kwa haraka”


“Sasa unabwabwaja nini , panda haraka unifundishe”Aliongea Nyakasura, muda huo hakufikiria sana alichotaka ni kujua kuendesha basi.


Hamza palepale alipanda juu ya farasi na kwenda kukaa nyuma ya Nyakasura. Awamu hio wawili hao walikuwa wamekaribiana mno na Hamza aliweza kuhisi ulaini wa mwili wa mrembo huyo.


Upande wa Nyakasura pia aliweza kuhisi kitu cha tofauti na kufanya uso wake kukakamaa na mara baada ya kukandamiza lipsi zake aliishia kukaa kimya.


“Inama kidogo kwa usawa wa mwili , kisha shikilia hio hatamu vizuri. Hizi lijamu zote zinatumika kuongoza farasi na pia ni kama breki unapotaka kupunguza na kuongeza mwendo. Ukiona spidi yake ni ndogo tumia mjeledi kuichapa kwa upole kuihimiza iongeze mwendo”


Hamza alimwelekeza kwa vitendo Nyakasura huku akiwa ameshikilia mikono yake namna ya kushikilia hatamu na kisha alimshika kiuno na kuweka sawa mwili wake.


Ni muda huo sasa Hamza aligundua ndani ya koti jekundu alilovalia ndani alikuwa amevalia nguo nyeusi ambayo ilikuwa imebanana na mwili wake kutokana na wepesi wake , aliweza kuona kutokana na kikoti kile kupandisha juu na kuacha kiuno wazi.


Mara baada ya farasi kuanza kutembea , miili yao ilianza kucheza kwa kupanda na kushuka na kufanya Hamza mwili wake kuzidi kujisugua katika ngozi laini ya mrembo Nyakasura. Hisia alizokuwa akipata zilikuwa za ajabu kabisa.


Hamza mara baada ya kuona eneo lake la mbele limemkaribia sana Nyakasura ilibidi atumie magoti yake kukandamiza makalio ya Nyakasura ili kugosea nyuma , lakini sasa mkandamizo huo ulimwongezea msisimko na kumfanya ashindwe kujizuia na kukandamiza tena.


Upande wa Nyakasura hakuwa akijua kinachoendelea , alikuwa akifurahia hisia za kuendesha farasi kwa spidi. Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuendesha farasi.


“Hamza angalia inavyoenda kwa spidi.. hahaha.. kumbe kuendesha ni raha mno , nikirudi nyumbani lazima ninue farasi”Aliongea Nyakasura kwa fuaha huku akiona ashagundua namna nyingine ya kupoteza muda.


Lakini Hamza aliekuwa nyuma alikuwa akifurahia hisia nyingine. Alichokuwa akifikiria muda huo ni kama mrembo anaemkandamiza makalio yake ni mrembo maarufu anaefahamika kama Phoenix Girl.


Nyakasura muda huo aliweza kugundua kuna kitu kigumu kama mti kinachomkandamiza eneo la karibu na kiuno chake na bila kuwaza sana alipeleka mkono kugusa ili kujua ni nin.


“Ah!”


Hamza aliekuwa kwenye fantasy zake alijikuta akishituka mara baada ya mwanamke huyo kushika naniliu yake.


“Ni nini hichi ndani ya suruali yako?”


“Nyakasura hakugundua mara moja na alikuja kujua mara baada ya kuminya na kuhisi joto lake.


Haraka sana alitoa mkono wake kama vile ameshika kitu cha moto huku sura yake ikipatwa na moto. Alishikwa na aibu kiasi kwamba hata pumzi ilimkata.


Kubwa zaidi ni kwamba baada ya kushika hicho kitu, kilibadilika na kuwa kikubwa zaidi na kwasababu farasi ilikuwa mbio kitu kile kilizidi kujisugua katika eneo la kiuno mpaka kwenye mgongo wake na kumfanya ajihisi hali ya ajabu mno.


Tokea awe mdogo , Nyakasura hakuwahi kukutana na tukio la namna hio kwenye maisha yake na ndio maana alishindwa kujua ajiweke vipi katika hali ya ajabu iliojitokeza kama hio.


Upande wa Hamza aliishia kutabasamu kifedhuli huku akizidi kusikia raha namna msuguano ulivyokuwa ukiendelea na alisogea karibu zaidi.


“Wewe.. mshenzi usinisogelee..”Nyakasura alijikuta akishindwa kujizuia na kuongea kwa nguvu.


“Sio kama nakusogelea , ni kwasababu Farasi inatembea kwa kasi na kunitingisha”


“Basi , iambie isimame”


“Sawa!” Hamza palepale alishikilia kamba ya Farasi na kisha akapunguza mwendo.


Nyakasura muda huo alijihisi ni kama amegeuka na kuwa mtiifu ghafla na kujikuta akipandwa na hasira.


“Wewe mwanaharamu , kwanini unanishika?”


“Sijakushika , mimi nilikuwa nikijaribu kuzuia farasi isije kutudondosha”Aliongea Hamza akiwa na mwonekano wa kizembe.


“Na vipi kuhusu hapo chini , ulikuwa unafanya nini?”


“Hii ni hali ya kawaida kwa mwanaume. Nisipokuwa hivi kwa mwanamke mrembo kama wewe inabidi niende hospitalini nikapimwe”


Nyakasura mara baada ya kusikia neno mwanamke mrembo hasira iliokuwa kwenye moyo wake ilipotea palepale na alijikuta akipepesa macho na kushikilia hatamu ya Farasi na kuifanya isimame moja kwa moja na kisha aligeuka na kumwangalia Hamza.


“Unahisi mimi ni mrembo?”


“Ndio”


Hamza hakuongea uongo , mwanamke huyo alikuwa mzuri mno ambae alikuwa na ile hadhi ya uanamke Clasic na ukisasa.


“Upo sahihi , kwa mwanamke mrembo kama mimi ni ngumu kujizuia.Lakini naomba uelewa kitu kimoja nilipohisi hicho kitu chako mgongoni nilikigusa bila kujua , huruhusiwi kunitania kwa kusema nimegusa makusudi la sivyo nitakachokufanya hutosahau”


Hamza aliona mwanamke huyo alikuwa mwepesi kutegeka kuliko hata Regina , hivyo haraka haraka alitingisha kichwa kukubali.


Hakuna shida kabisa, siwezi kuongea. Halafu kwa mwanamke mrembo na hatari kama wewe naanzaje kwa mfano?”Aliongea Hamza na Nyakasura aliruka kutoka kwenye farasi na kutua chini.


“Huna haja ya kujitetea , najua kabisa mwanaume kama wewe huna damu ya kifalme na hadhi ya familia yako ni ya kawaida , hivyo ni kawaida kujiona wa hadhi ya chini kuliko mimi. Lakini angalau unajitahidi , kuna vitu vichache tu unapaswa kuvifanyia kazi hasa kuboresha silika yako na kujiamini kidogo , ukifanikiwa unaweza kujaribu pengine naweza kukupa nafasi”


Hamza mara baada ya kusikia hivyo hakujua acheke ama alie na kujiuliza anaongea nini , mbona imegeuka ni kama anamfukuzia?.


“Madam Nyakasura kwa hadhi yako ilivyo kubwa natoa wapi ujasiri wa kujaribu kukukaribia? Isitoshe nimekwisha oa tayari , siwezi kuwa na wazo hilo zidi yako”Aliongea Hamza huku akicheka na muda huo Nyakasura alikumbuka Hamza alikuwa amekwisha kuoa.


“Oh tena nimekumbuka kumbe umeoa , kama ni hivyo basi kazi unayo. Lakini najua mke wako hawezi kunizidi uzuri hivyo huwezi kuacha kunifikiria. Nikushauri ukijihisi umeshaanza kunipenda ili kunipata unapaswa kwanza kumtaliki mkeo , vinginevyo siwezi kukubali”Hamza mara baada ya kusikia hivyo kidogo tu atapike.


“Nyakasura usinielewe vibaya ,ni kweli sina mawazo hayo kabisa na wewe. Tuwe tu marafiki na nipo hapa kukufndisha kuendesha farasi na kilichotokea ni bahati mbaya tu kama mwanaume”Hamza aliona ni vizuri kujielezea.


“Unakataa nini? Si wewe ulieniita mrembo sasa hivi na hata kupandisha midadi yako kwasababu yangu?”


“Hamna bwana ni..” Hamza alishindwa kujua namna ya kujielezea , aliona ni kama stori nyingine sana ambayo ingekuwa na mwisho mwingine.


“Nadhani nishaanza kukuelewa sasa , unaonekana kwenye moyo wako unanitamani , lakini unaogopa nitakukataa. Kama mwanaume sioni ni ajabu kuvutiwa na mwanamke mrembo kama mimi , hivyo usiwe na wasiwasi , siwezi kukucheka” Mara baada ya kuongea hivyo alijishika kiunoni kuonyesha umbo lake vizuri.


“Sittaki kuendesha tena , narudi zangu kwenye nyumba kule , Berlly amesema atanipa mvinyo mtamu , naenda kunywa”


Hamza hata yeye hakutaka kuendelea kujielezea mbele ya mwanamke huyo , maana aliona kabla atakavyoongea ndio namna atakavyoharibu.


Mara baada ya kurudi , Hamza alimpeleka farasi yule kwenye zizi na muda huo aliweza kuhisi kuna mtu aliekuwa akiingia katika zizi hilo. Hamza hakuwa hata na haja ya kugeuka kujua ni nani kwali alishamjua kupitia hisia zake ni Asmuntis.


“Boss!!”Aliita Asmuntis huku akiwa na uso uliosawijika.


“Nini tatizo mchafu? Mbona unaonekana kuwa na huzuni namna hio, unapaswa kuwa na furaha kwa kukutana kwetu mara nyingine”Aliongea Hamza na kumfanya Asmuntis kushusha pumzi.


“Nilikuwa na mazungumzo na Azzle na tumeona itakuwa vizuri kutowaambia wengine kuhusu hali yako ili tusije kuwapanikisha , nadhani unajua Berrly na Leviathani walivyo. Lakini kesho hata kama usipoenda kwenye Baraza , lazima Gonzalez atataka kukuchallenge. Amekuwa akiwazia nafasi yako kwa muda mrefu. Hivyo tumeona ni vizuri kukaa chini na kupata suluhisho”


“Suluhisho? Nyie mnadhani ni kipi kifanyike?”


“Tumeona kwasababu huwezi kupigana , basi itakuwa ni vizuri ukiwaruhusu wanachama wa INFERNO kupigana , hii ndio njia pekee ya kulinda heshima yetu. Hivyo itakuwa vizuri kama tukimruhusu Sally kufanya safari ya kuja hapa haraka. Kwa uwepo wake ndio njia rahisi ya kuweza kushinda”Aliongea Asmuntis na maneno yake yalimfanya Hamza uso wake kuongeza usiriasi.


“Roho Mchafu nadhani utakuwa umesahau? Nilishawahi kusema mwanzo ili mradi ninapumua nitamlinda Sally kwa uwezo wangu wote na kutoruhusu mikono yake kujichafua na damu. Ukimwambia Sally aje ni kweli atakuja lakini unajua nini kitatokea akiwa uwanja wa mapambano na kushindwa kujidhibiti, nini matokeo yake?”


Asmuntis aliishia kupanua mdomo wake tu akitaka kuongea kitu lakini alishindwa na kuishia kutingisha kichwa.


“Bosi , upo sahihi , kumuita Sally kuja ni hatari zaidi”


“Usiwe na waswasi Asmuntis , nakuahidi kesho hakuna kitakachotokea”Aliongea Hamza na kisha alitembea na kumshika bega kwa kuligonga gonga kumtuliza aondoe wasiwasi na kisha alitoka nje ya zizi.


Dakika ambayo alitembea mpaka nje ya nyumba aliweza kuona magari kadhaa ya Mercedenz Benz rangi nyeusi yakisogelea ueleko wa shamba yakiwa yamewasha taa za mbele kutokana na giza.


Kila mtu ndani ya nyumba hio aliweza kugundua kuna mgeni aliekuwa akifika hapo shambani na kufanya watoke , akiwemo Nyakasura aliekuwa ameshikilia glasi ya Blood Mary.


“Bosi ni nani? Au ni Metal Tide wameamua kuja mpaka huku?”Aliuliza Mameni.


“Hapana , kwa spidi ya gari zao, inaonyesha sio watu waliokuja kwa ajili ya kutafuta ugomvi”Aliongea Hamza.


Haikuchukua muda mrefu gari zile zilisimama katika eneo la kuingilia katika upande wa nyumba hio na kundi la watu lilishuka. Watu wote walikuwa wamevalia mavazi ya suti na mashati ya rangi nyeupe na tai. Kulikuwa na wazungu na watu weusi na wote walionekana kuwa walinzi wenye mafunzo.


Muda ule kundi lile lilitengeneza safu mbili na kumuongoza mwanaume wa makamo hivi, mzungu ambae nyewele zake alikuwa amezichana vizuri. Mkononi alikuwa ameshikilia Briefcase, na kabla ya kupiga hatua alionekana akitingisha kichwa uelekeo wa Hamza na kisha alianza kutembea kusogea na jumla ya walinzi nane.


Ijapokuwa ilikuwa ni usiku lakini kila mtu aliweza kuona bango lililokuwa katika eneo la kifua chake karibu na mfuko wa suti , ni bango ambalo lilikuwa na nembo ya siraha na ngao na chini yake kulikuwa na maandihi ya ‘SETH’.


“Ni mtu kutoka Set Association”Aliongea Asmuntis.


“Inaonekana wapo hapa kwa ajili ya bosi”Aliongea Azzle.


Sekunde chache tu watu wale waliweza kufika mbele ya Hamza na wale walinzi walimuonyeshea heshima Hamza na Nyakasura.


“Honorable Prince of Hell and Phoenix Lady, I am a member of the Sytry Council. My name is Hewitt. Please forgive us for intruding and disturbing you.”Aliongea akimpa heshima Hamza kwa kumuita mtukufu Prince wa kuzimu na Bi Phoenix na kujitambulisha kwamba ni mwanachama wa Baraza la maksi akifahamika kwa jina la Hewitt. Na anaomba radhi kwa kuwavamia usiku usiku.


Bwana huyo Hewitt alisaliamaiana na Hamza na Nyakasura tu , wakati akiwapa tabasamu wengine , ilikuwa ni ishara ya kutoa heshima kwa wataalamu wa mapigano wa hadhi ya Ugwiji.


“Kwanini mwanachama wa Baraza la maksi kufika usiku usiku hapa kunitafuta?”Aliuliza Hamza na bwana yule palepale alifungua ile Briefcase na kisha alitoa bahasha iliokuwa ikimeta meta kwa kumwagiwa madini ya almasi na madini ya dhahabu na kisha alifungua.


“Sir Lucifer , tuwie radhi sana , ukweli tulikuwa tukikutafuta sana kwa kipindi cha miaka miwili iliopita , lakini hatukuweza kukupata. Tumetunza hii barua yako ya mwaliko kwa ajili ya kilele cha magwiji mwaka huu , mpaka tuliposikia kuonekana kwako leo hii, ijapokuwa tumechelewa , ila ni matumaini yetu utaupokea mwaliko kwa ajili ya kuhudhuria katika Baraza la maksi mwaka huu”


Hamza aliishia kuangalia bahasha hio ambayo ilionekana kutumia hela nyingi kwa ajili ya kuiandaa na kisha alitoa tabasamu.


“Ni mwaliko tu kwani kuna haja ya kuyakuza namna hii?”


“Kumbe hukupata mwaliko , mimi nilipewa mwaliko mwaka jana”Aliongea Nyakasura.


“Haha.. bosi nilikuambia mimi , haiwezekani hawa watu wakakusahau? Kama usipoenda haiwezi kuwa kikao tena”Aliongea Berlly lakini mwonekano wa Azzle na Asmuntis ulizidi kuwa siriasi. Kwasababu waliona kukubali kwa Hamza kupokea mwaliko huo maana yake aangeenda kuhudhuria.


Hamza licha ya kuona mabwana hao walivyo na wasiwasi , lakini alipokea mwaliko ule.


“Hii bahasha mmeijua kupamba vizuri mno , nadhani itakuwa vizuri kumpatia mke wangu”


Mara baada ya kusikia hamza akuongea hivyo , wenzake walishangaa kiasi cha kuzimia.


Hewitt mara baada ya kuona mwaliko huo Hamza ameupokea , palepale alitingisha kichwa kwa ishara ya heshima.


“Wa kuheshimiwa , Prince of hell na Phoenix Girl , barua zetu zimepokelewa vyema na tunatarajia ujio wenu siku ya kesho. Tumewaandalia siti maalumu katika eneo la VIP kwa ajili ya Magwiji wakati wa Baraza likiendelea na pia kutakuwa na siti hizo hizo maalumu katika kikao kikuu . Kama mtakuwa na maswali yoyote mnaweza kuwasiliana na bodi ya wakurugenzi moja kwa moja. Nafasi zenu zitapatikana ndani ya masaa ishirini na nne”


“Naona watu wa Set siku hizi mnazidi kuwa profesheno na kufanya baraza la mwaka huu kuwa kama sherehe ya kifahari , sio mbaya”Aliongea Hamza huku akihisi kusanyiko la mwaka huu litakuwa la kiheshima zaidi kuliko la miaka mitano iliopita.


“Your encouragement is our motivation to move forward.”Aliongea Hewwit na kisha aliwapungia mkono kila mmoja na kisha aliongozana na kundi lake kuondoka ndani ya eneo hilo.


Mara baada ya watu wale kuondoka , Black Fog alimsogelea Hamza akiwa na wasiwasi.


“Bro , una uhakika unataka kwenda? Hata kama usiende hawawezi kusema chochote”Aliongea na muda ule Nyakasura aliingilia.


“Wewe mtoto unajua nini? Kushiriki katika Baraza kuu la maksi ni raha sana pia ni mahali ambapo utaweza kukutana na watu wengi wazito. Au unaogopa watakuchokoza kwasababu unaonekana mdhaifu . Usiwe na wasiwasi , kwanzia sasa hivi niite dada na nitahakikisha nakulinda”


“Miss Nyakasura , ijapokuwa una cheo cha Ugwiji , tafadhari naomba uniheshimu , mimi sio mtoto”


“Haijalishi unavyojiona , ila wewe ni mdogo sana kwangu .”Aliongea huku akimkagua na kisha akaendelea , “Naona una umbo matata sana , hakika umejua kujitunza”


“Wewe..” Black Fog hasira zilimjaa na palepale alipeleka mkoo wake kiunoni na kutoa visu.


“Ah!” Asmuntis alikuwa fasta sana kumzuia Roda kufanya alichokusidia.


“Black Fog , umekuwa kichaa! Hebu acha kuwa mkorofi mbele ya Miss Nyakasura, kwa uwezo wako mdogo hustahili hata kupigana nae”


Black Fog aliishia kupumua kwa nguvu kudhibiti hasira zake na aliishia kupiga piga miguu chini na kisha alikimbilia ueleko wa porini kwenye shamba la chakula cha farasi. Huku Nyakasura aliishia kumtolea ulimi kwa kumuweza.


“Kwanini unamchokoza , anaonyesha wasiwasi wake juu yangu,. Kama wewe ni mtu mzima kwanini usiwe kama mdogo wake kweli?”Aliongea Hamza.”


“Sio mdogo wangu, Kama ni kuwa na mdogo wangu yupo ila sio yeye”Aliongea Nyakasura.


“Oh! Niambie huyo mdogo wako ni nani?”


“Wewe jua tu hivyo na ni mtiifu kuliko yeye, ni ..”Nyakasura alitaka kuongea lakini aligundua ni kitu ambacho hapaswi kuongea hivyo aliishia kumwangalia tu Hamza.


“Kwani lazima nikwambie kuhusu mdogo wangu? Naenda zangu kunywa , kwaheri”


Hamza aliishia kufosi tabasamu , alitaka kumfanya aongee kidogo ili amjue zaidi lakini alionekana kuwa makini.


“Amekasirika kwa namna ulivyomfokea , itakuwa vizuri ukienda kumtafuta”Aliongea Hamza akimwambia Asmuntis.


“Usiwe na wasiwasi bosi , hawezi kufanya chochote , Amefunzwa kuwa ngangari tokea akiwa mdogo”Aliongea Asmuntis na palepale aliona aingize kitu kingine, ‘Lakini bosi tunapaswa kufikiria mara mbili kuhusu hili suala la kesho”


“Najua unachotaka kusema ni mimi kutokwenda , ila nishakuambia usiwe na wasiwasi. Ngoja nikamtafute mdogo wangu nimbembeleze”


Hamza mara baada ya kuongea alitembea kuingia katika shamba la majani kumtafuta Chimera na aliweza kumuona akiwa amekaa juu ya kifusi cha majani yaliokauka akiwa anaangalia juu angani.


Hamza aliishia kusimama kwa mbali akimwangalia huku akionekana kufikiria na ni muda huo Black Fog aliweza kugundua kuna mtu aliekuwa akimwangalia.
199 mpaka 200 ni free kabisa , gusa link hapa:- SEHEMU YA 199
 
Back
Top Bottom