Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

SEHEMU YA 199.


“Bro unafanya nini hapa?”Aliuliza Black Fog huku akionekana kuwa na furaha kiana hivi.


Hamza alimwangalia kidogo na kisha alitembea kumsogelea akiwa na tabasamu , na kupandisha katika kifusi hicho cha majani.


“Una hasira na Master wako?”Aliuliza Hamza na tabasamu la Nyakasura lilipotea palepale na aliishia kuokota majani makavu ya nyasi na kuaza kuyakunja kunja.


“Hapana , tokea nikiwa mdogo nishazoea kufokewa. Hii sio mara ya kwanza”


“Sasa kwanini umenuna hivyo?”Aliongea Hamza akimzodoa na kidole.


“Sina hasira nae , ni kwamba simpendi Nyakasura ana majivuno kisa tu ana damu ya kifoeniksi. Kama ningekuwa na damu yake ningekuwa na uwezo mkubwa kuliko wake. Anachojua ni kula , kunywa na kucheza na kuonyesha ubishi wake na hachukulii mambo siriasi kwasababu hajawahi kupitia magumu”


“Unamchukulia Nyakasura kirahisi kwasababu ya alivyo?”Aliuliza Hamza.


“Bro kwanini unasema hivyo?”


“Sikiliza , katika huu ulimwengu hakuna mtu yoyote ambae anaweza kupata anachokitaka bila ya kufanya kazi kwa bidii. Hakuna watu wengi ambao wanaweza kufanikiwa kirahisi tu . Ni kweli Nyakasura sio wa kawaida kutokana na damu yake lakini presha iliowekwa tokea akiwa mdogo kuutambua na kuelewa uwezo wake ni kubwa kuliko mtu wa kawaida. Kitendo cha watu kujua ana damu isio ya kawaida , watu waliweka matarajio makubwa kwake kuliko kwa wengine wote. Wengine wanaweza kufeli na watu asifikirie sana lakini yeye hawezi kufeli kwasababu ya utofauti wake. Sio bahati mbaya kwa mtu kama yeye kuhimili presha aliopitia tokea akiwa mdogo na kisha kukua na kutambulika kama Gwiji katika mapigano. Mfano rahisi angalia watu wengi ndani ya chama cha Adept Association , licha ya kuzaliwa kuwa na uwezo usio wa kawaida , lakini ukiachana na kiongozi wao hakuna mwingine yoyote ameingia katika orodha ya magwiji kumi. Hii maana yake ni nini ? Kuzaliwa na uwezo wa ziada kuliko binadamu wengine hakuwezi kukufanya kuwa hatari kama usipofanya kazi kwa bidii. Pengine Nyakasura uliemuona leo ni mtu anaejua kufurahia maisha , lakini nyuma ya pazia anaweka juhudi kubwa mno. Hata mimi pia namuona Nyakasura ni mtu wa kukurupuka , muda mwingine ni kama kichaa , kuna muda ni mwenye majivuno na muda mwingine anakasirisha sana. Lakini faida anayoipata sasa hivi imetokana na juhudi zake alizowekeza na sio kitu ambacho amepata bila ya kufanya kazi . Umeelewa?”


Rhoda aliishia kupanua macho yake huku akipepesa kidogo na kisha mara baada ya kuyasharabu maneno ya Hamza alitingisha kichwa kuashiria ameelewa.


“Nimekuelewa Bro , ni kama mimi tu , kama nitafanya kazi kwa juhudi na kufanikisha kupandisha levo ya mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi , pengine naweza kuhimili mbinu ya Hundred shadows”


“Hakika wewe ni mdogo wangu , upo sahihi ., Ukweli ni kwamba ninaamini na wewe pia una uwezo ambao sio wa kawaida na haujaufahamu tu. Vinginevyo kwanini tunashindwa kupata maelezo sahihi ya kuelezea uwezo ulioonyesha kupitia mbinu ya Hundred Shadows. Nina uhakika kadri utakavyoendelea kupanda levo itafikia hatua utaelewa ni karama gani imejificha katika mwili wako”


Black Fog mara baada ya kusikia maneno hayo hamasa ya kupambana ilimvaa palepale. Alijikuta akijirusha katika mikono ya Hamza na kumkumbatia kwa kupitisha mikono yake shingoni.


“Kaka upo vizuri sana , Master hajawahi kuniambia hivi . Anachojua ni kunifokea tu , naamini ungekuwa mwalimu wangu , ningekuwa zaidi ya nilivyo sasa.”


Kumbatio hilo halikuwa muhimu sana , kubwa ni kwamba kifua cha Rhoda kilikuwa kimekandamiza kwa nguvu eneo la mbele la kifua cha Hamza na kumfanya bwana huyo ahisi vichomi na alishindwa kujizuia na kuhisi ni dhambi ya kinachotokea.


“Ni kweli , Mchafu ni mtu mkali sana , hawezi kuwa mkamilifu. Unaonaje kwanza tukirudi”Hamza alijikuta akijitahidi kuongea.


Rhoda aliishia kumwachia Hamza na kisha kumwangalia usoni kwa umakini.


“Bro hakikisha kesho unakuwa makini , usije ukaruhusu kuingia katika mtego wa maneno ya Gonzalez. Kama utajikuta katika hali ambayo inahitaji ufanye vitendo ni vyema ukiwaacha Master na wengine kuchukua hatua. Isitoshe pia yupo Sister Sally kutoka kiswani Toharani”


“Sawa nimekuelewa , usiwe na wasiwasi na hakuna kibaya kitakachotokea”


Hamza aliona amfariji mwanamke huyo , lakini maneno yake yalisafirishwa na upepo.


Mita ishirini kutoka walipokuwepo , kulikuwa na kivuli cha mtu kilichovalia nguo nyekundu na Cocktail mkononi na alikuwa akisikilza kwa umakini kila sentensi Hamza aliokuwa akiongea kwa kutumia uwezo wake.Hata Hamza hakujua kama walikuwa wakifuatiliwa.


Baada ya kufuatisha maelezo ya Hamza , mwanamke huyo alionekana kutoa tabasamu.


******


Siku iliofuata watu kutoka pande mbalimbali za dunia walikusanyika katika mji wa Limour.


Ingawa watu wengi hawakuwa na vigezo vya kuingia ndani ya Convention center , walikuwa na hamu ya kujua kitakachoendelea chini ya baraza la uchambuzi la Set.


Watu wengi walitamani kuingia na kupata kujua wataalamu wengi ambao ilikuwa ni ngumu kufahamika katika macho ya kawaida.


Asubuhi maafisa wa juu kutoka nchi tofauti tofauti pamoja na maafisa wa Set Association walifanya kikao cha mapema kukamilisha baadhi ya mambo ambayo hayakuwa sawa kulingana na ufunguzi rasmi wa baraza.


Wakati hio taasisi mbalimbali , zile zinazofahamika katika ulimwentgu wa kawaida na zile ambazo zilikuwa ni za siri ziliwahi kufika kwa ajili ya mapokezi.


Nyakasura ndio aliekuwa wa kwanza kuondoka. Alikuwa ni mlinzi wa kitendo cha Malibu hivyo isingekuwa sahihi kutokea akiwa ametangulizana na watu wa jamii ya INFERNO.


Hamza hakutegemea Nyakasura angeondoka kimya kimya bila hata ya kuaga , maana alimzoea kuwa mtu wa vurugu na jambo hilo lilimfanya kujisikia vibaya kidogo bila ya kujua ni kwannini.


Kuhusu kushiriki kwa Hamza kila mtu alipanga kuhakikisha Hamza anatokea akiwa katika hali inayoendana na hadhi yake.


Ijapokuwa Hamza aliwaeleza itakuwa vizuri akienda kimya kimya lakini hawakuwa tayari kumsikiliza.


Mchana kabla ya kuondoka Azzle alikuwa ameshaandaa gari ya kifahari ya Lykan- hyepersport. Kama mshauri mkuu wa Falme ya Daebia haikuwa ngumu kuweza kuandaa gari ya kifahari namna hio.


Uelewe Lykan Hypersport yapo saba tu duniani na gari moja iligharimu zaidi ya Bilioni nane za kitanzania. Licha ya thamani yake kubwa ni aina ya gari ambayo huwezi tu kununua kwasababu una hela.


Taa zake za mbele zilizungushiwa mkanda mwembamba wa madini ya almasi , siti zake zilitengenezwa kwa nyuzi nyembamba za madini ya dhahabu.Licha ya gari hio kuwa na uwezo mkubwa kwenye spidi lakini hakikuwa kigezo kikubwa , muhimu ni kwamba ni gari ambayo ilielezea hadhi ya mtu kama Hamza.


Hamza mara baada ya kuona gari hio imeengeshwa kwa ajili ya yeye kupanda alishangaa.


“Mhunzi! Hii gari ni kwa ajili yangu?”


“Ndio bosi , nimeiazima kwa Mfalme wa Daebia”


“Basi mwambie kwanzia leo ni ya kwangu na itapelekwa kisiwani”Aliongea Hamza akiwa na tabasamu.


“Haha..Bosi kwasababu umesema hivyo , sidhani kama Mfalme atakataa”Aliongea Azzle .


Hamza aliacha kuongea ujinga na kisha aliingia upande wa Dereva na kuipasha moto , kitendo cha kuiwasha ilinguruma kama mnyama mkali na kisha aliondosha kwa spidi ya juu sana.


“Bosiiiiii.. Tusubiri” Mameni na wenzake waliita huku haraka haraka wakiingia kwenye magari mengine na kisha wakawasha moto na kulifukuzia gari la Hamza ueleko wa mjini.


Hamza mara baada ya kufika katikati kufikia mjini Limour na gari yake ya Lykan, kulikuwa na watu wengi mbele ya barabara hivyo alilazimika kupunguza mwendo.


Watu wengi walianglia gari hio kwa macho ya mshangao , lakini kutokana na vioo vya gari hio hawakuweza kuona nani alikuwa akiendesha.


Wakati muda huo Hamza akipanga kusogeza gari hio mpaka nje ya ukumbi, aliweza kuona kundi la watu likiwa limeziba njia na ilionekana kuna vurugu iliokuwa ikiendelea. Yalikuwa ni makundi mawili yalioonekana kushambuliana.


Kulikuwa na magari kadhaa ya kifahari yaliokuwa yamesimama kwa kukwama kama vile Bentley , Aston Martin na hata Rolls Royce , yote yalionekana kushindwa kupita kutokana na vurugu hio.


Kundi hilo lilionekana kushikilia baadhi ya watu na kuna wengine waliokuwa wakipigana kwa ngumi. Wengi walionekana kuwa na mafunzo ya mapigano na kuna baadhi walikuwa na mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi nusu mzunguko mpaka Mzunguko kamili.


“What the heck…”Aliongea Hamza huku akijiuliza watu hao watachukua muda gani mpaka kumaliza kupigana kama itaendelea kwa staili hio.


Alijikuta akiwa hana jinsi na kufungua mlango na kisha kutoka nje ya gari akipanga kuwaondoa njiani hao watu. Ile tu anatoka katika gari ile mtu mmoja alisikika akipaza sauti;


“Angalieni ni Lucifer , Prince of hell”


“My God! My idol is here. Is inferno going to regroup?”


Kutokana na Hamza kutokea kwake hadharani jana watu wengi walionekana kuikariri sura yake na sasa baada ya kumuona tena walimjua kwa uharaka.


Ijapokuwa hawakumsogelea karibu , lakini watu wengi walishikwa na hamasa na msisimko wa juu.


Hamza muda ule alijua muda mwingine kuwa Star sio jambo zuri kwani namna watu walivyokuwa wakimwangalia hakupenda.


“Nini kinaendelea?”Aliuliza watu waliokuwa karibu yake.


“Ripoti kwa Master Lucifer! Mbele ni kundi la kimasenari la Mchwa Wa Moto na kundi la Kimasenari la Kisigino Cha Chuma. Wameanza kupigana kwa zaidi ya saa moja mpaka sasa kwasababu ya kubishana juu ya madaraja yao”


“Ni makundi gani yenye majina ya kipuuzi , sijawahi hata kuyasikia ..”Hamza alijikuta akiongea chini chini huku akitingisha kichwa.


Makundi mengi mapya ya Kimasenari yalikuwa yakikua kwa haraka kufikia daraja C na B , hivyo ni rahisi kwa muda aliokuwa nje ya ulimwengu wa siri kutoyafahamu. Hamza aliishia kusogea mbele huku akiwaongelesha kwa sauti baadhi ya watu walionekana wengi wao kuwa katika umri wa miaka arobaini hivi wakipigana.


“Hey , nyie kama mnataka kupigana , nendeni kando ya barabara. Kwanini mnazuia njia?”


Licha ya kuongea makundi hayo yalikuwa katika munkari ya juu kabisa ya kupigana na hawakumsikiliza kabisa Hamza.


“Mnathubutu kumdharau Lord Lucifer , nadhani mmechoka kuishi”


“Hey nyie Mchwa Wa Moto na Kisigino Cha Chuma , je mnakiuka maneno ya Mfalme wa Kuzimu?” Kundi la watu lililokuwa karibu zaidi lilipaza sauti.


Hatimae moja ya wapiganaji alionekana kusikia na aligeuza kichwa na kumuona Hamza akiwa amesimama na hasira na haraka sana alianza kuwaongeleza wenzake waache.


Hatimae watu kadhaa walishituka kutoka katika hisia zao za kimapiugano na kumwangalia Hamza na haraka sana walianza kusogea. Huku wakihema , wengine wakivuja damu na kujificha kando ya barabara.


“Samahani Master! Sio makusudi yetu kukuzuia”


Makundi yote mawili ya Mchwa Wa Moto na Kisigino Cha Chuma waliongea kwa sauti wakiomba kusamehewa.


Kila mmoja alidhania Hamza angewachukulia hatua lakini matokeo yake Hamza aliishia kuwapa ishara tu ya mkono.


“Sawa, ila siku nyingine ni sawa tu kupigana na hata kuuana ila hakikisheni hamzuii njia wengine kupita. Ijapokuwa tunafuata sheria za ulimwengu wa giza lakini tunaishi katika mazingira ambayo yanaendeshwa kwa kanuni za watu wa ulimwengu wa kawaida. Sio vizuri kuchelewesha wasio na hatia kwenda kwenye shughuli zao, ni sawa?”Aliongea Hamza na kundi lote la masenari hao walitingisha cichwa kuitikia.


Watu waliokuwa pembeni waliishia kushangaa , na hio ni kwasababu hawakutegemea mtu ambae aliwaondoa watu hao kando ya barabara baada ya kuwakasirikia, aliishia kuwapa ushauri.


Hamza mara baada ya kuongea hivyo muda ule aliona ni sahihi kurudi kwenye gari yake na kuendelea na safari , lakini sasa muda huo kutoka kwenye gari ya kifahari ya Roll Royce ya rangi nyeupe ilifunguliwa, na mwanamke mrembo alievalia gauni la rangi nyeupe alishuka.


Lilikuwa gauni la kitambaa mtelezo , mkanda wa rangi ya bluu uliofungwa kiunoni na viatu vya kisigino kirefu , Wazungu wanaita Mediteranian Charm style uvaaji wake.


Alikuwa mrefu wa mita kama moja na nukta nane hivi , mzungu mwenye nywele ndefu za rangi ya dhahabu zilizofungwa kwa nyuma. Macho mazuri ya bluu na kidevu mchongoko ilimfanya aonekane kama mwanamke mrembo kutoka katika hadithi za kusadikika.


Dakika ambayo mwanamke huyo alijitokeza , watu wote walitoa macho na kuzuia pumzi zao. Wote waliogopeshwa na urembo wake na msisimko aliokuwa akisambaza.


Hamza macho yake yalisinyaa huku mboni za macho yake zikicheza kwa haraka na sio hivyo tu moyo wake ulidunda kwa nguvu na alijikuta bila ya kupenda akitoa tabasamu lililojaa majuto.


“Selafi , Long time no see , you’ve changed a lot”


Mwanamke huyo aliongea , alionekana kuwa katika makadirio ya umri wa miaka therathini hivi na aliongea huku akiwa na tabasamu la upole akionekana kumfahamu Hamza kwa muda mrefu.


“That's right. It's been a long time since we last met, but you haven't changed at all … Mistress.”Aliongea Hamza akikubali kwamba ni muda mrefu hawajaonana , lakini hakuwa amebadilika tokea mara ya mwisho waonane , huku akimalizia kumuita jina la Mistress yaani Mchepuko au hawala , licha ya kwamba aliita kwa kusita.


Sekunde ambayo maneno hayo yalimtoka Hamza , kundi la watu lilishangaa


“Mistress!? Inamaana huyu ni hawala wa Lucifer , White Queen” Mtu mmoja alisikika akiongea.


“Itakuwa lazima , kwa msisimko anaotoa na urembo wake lazima atakuwa ni mtawala wa the OD- Ones . Madam Silvia Somerset”


“Oh sasa nimeelewa , nikajua mnamaanisha ni mchepuko wa Lucifer wa sasa , kumbe mnamaanisha ni aliekuwa hawala wa Black Emperor”Aliongea mmoja.


“Sijategemeea Lucifer angemwita Mchepuko licha ya kumuua mpenzi wake Mr Black”


“Black Emperor na White Queen … kwa nilivyosikia ni kwamba wote wana uwezo wa juu sana wa mapigano , pengine uwezo wao unalingana. Ila Silvia hakumsaidia Mr Black wakati akipambana na Lucifer . Vinginevyo kama wangeunganisha nguvu ingekuwa ngumu kwa lucifer kushinda”


“Unaongea ujinga , kwa hadhi aliokuwa nayo Master Lucifer hata kama wangeunana lazima angeshinda”


“Sidhani ipo hivyo wewe , nasikia Silvia alikuwa na mipango yake , alitaka Mr Black kufa kwa ajili ya kupata utawala kamili wa The OD-Ones , ndio maana alimsaliti na kumsaidia Lucifer na kushinda vita”


Watu walianza kuongea wao kwa wao , wakiwa katika majibizano yasio na uhakika juu ya Mchepuko wa mke wa Mr Black.


“Selaf.. Oh sasa umerithi cheo cha Ucifer , mfalme mpya wa kuzimu , nadhani siwezi kutumia jina lako lililozoeleka kukuita” Aliongea Silvia akiwa si mwenye kujali minong’ono ya watu.


“Ukweli sijali kabisa ni majina gani watu wananiita , ukweli juu ya mimi ni nani ninaeujua ni mimi mwenyewe. Sasa hivi napenda kutambulika kwa jina jipya la Hamza Mzee”Aliongea Hamza.


Ukweli ni kwamba siku zote mwanamke huyo mrembo alikuwa akimtia wasiwasi sana , alikuwa mwanamke ambae sio mwepesi kudili nae kama ilivyokuwa kwa mume wake Mr Black.


Kwa tukio la kumuangalia bila kufanya chochote yeye akimuua mume wake na hakuchukua kisasi chochote na sasa wamekutana na kuanza kukumbushia yaliopita bila kuonyesha chuki ilimfanya aonekane sio wa kawaida.


“Oh sawa , basi kwanzia sasa nitakuita Hamza”Aliongea na kisha alionekana kumpiga jichoHamza kwa namna ya kumchunguza.


“Lakini kwanini unaonekana kama vile hakuna ishara yoyote…”
 
SEHEMU YA 200.


Mpango wa Dharula


Silvia uwezo wake ulikuwa ulikaribiana na aliekuwa mume wake Mr Black , hivyo ilikuwa ni rahisi kwake kuweza kuona Hamza hakuwa na msisimko wowote wa nishati za mbingu na ardhi.


Lakini kwa mtu kama Silvia , licha ya kugundua hilo hakutaka kuongea kwa sauti.


“Binadamu ndio hubadilika , lakini dunia ipo vilevile”Aliongea Hamza akiwa katika hali ya utulivu na kumfanya Silvia kucheka.


“Upo sahihi, spidi ya kubadilika kwa binadamu imefanya dunia kuonekana inabadilika kwa spidi. Mtu kama mimi wa miaka mitano iliopita sijawahi kudhania nitapata nafasi ya kushiriki katika baraza la Maksi kama kiongozi wa The Odd Ones. Lakini ukiachana na hayo nina furaha kubwa kukutana na wewe kwa mara nyingine , Hamza , Rafiki yangu wa kitambo”


Mara baada ya kuongea hivyo aligeuka na kuangalia nyuma kuangalia watu waliokuwa wakitoka kwenye magari.


Azzle , Asmuntis , Mamen na baadhi ya wanachama wa Inferno waliokuwa wakimfukuzia Hamza kwa nyuma ndio waliokuwa wakifika na kumuona White Queen.


Kila mmoja muonekano wake ulikuwa wa umakini mkubwa sana , kama kwamba wamekutana na adui mkubwa. Lakini mara baada ya kuona Hamza hakuchukua hatua yoyote na wanaongea kirafiki waliishia kusubiri.


“Madam Silvia , vita yetu ya kipindi kile ilikuwa ni ya kufa na kupona na sidhani kwasababu bosi wetu alishinda zidi ya mume wako unataka kulipa kisasi?”Aliongea Azzle kwa tahadhari.


“Hehe.. Azzle ni saa ngapi nimesema nataka kulipa kisasi . kama kweli ningekuwa na mpango wa kisasi kwanini nisubiri mpaka sasa? Mume wangu aliua ndugu zenu makusudi na kisha akachagua kupigana na Hamza mpaka mauti yakamkuta. Aliamua kunitelekeza yeye mwenyewe kwa tamaa zake kwanini nilimlipie kisasi?”


“Basi kama ni hivyo sawa , nadhani ni muda wa kurudi kwenye gari na kuondoka , muda unatupa mkono”Aliongea Mameni na kumfanya Silvia kutingisha kichwa.


“Huna haja ya kuwa na wasiwasi . Ijapokuwa ulituacha mimi na mume wangu, ila mpaka leo hii bado tunakuchukulia kama msaliti. Sitarajii kukuona ukinichukulia kama rafiki lakini vilevile sitaki unione kama adui yako”Aliongea Silvia akimwambia Mameni.


Palepale alisogea upande aliokuwepo Hamza na kusimama kidogo karibu yake na kuzuia pumzi kwa dakika kama moja hivi na kisha akapita, na wakati anapita mbele ya kundi la wanajeshi mwili wake ni kama ulianza kubadilika na kutoa miale safi ya rangi nyeupe ya kuumiza macho.


Silvia aliinua mkono wake juu hewani na kwenye mkono kulionekana kuwepo kwa kitu kama tufe la kung’aa kama jua.


“Illumination of Holy Light!”


Aliongea kwa nguvu kwa namna kama wale wachungaji wanavyoongea wakati wa maombezi na lile donge kama la mpira kwenye mkono wake lilipasuka na kugeuka matone mengi ya mwanga ambayo yalidondokea wale Masenari waliokuwa wakipigana na kuumizana vibaya.


Matone yale yalipogusana na miili yao ajabu majeraha yaliokuwa katika miili yao yalianza kupona kimiujiza kwa haraka sana.


“Nini kinaendeleas!”


“Damu imeacha kunitoka”


“Nahisi nguvu zangu kunirudia”


Ilikuwa kawaida kwa wale wanaoangalia kuona kinachoendelea na walishangazwa na jambo lile.


“Uwezo wa kimiujiza wa White Queen unafanya kazi yake sasa”


“Huna haja ya kushangaa sana , huyu ndio mwakilishi wa Wavuna nishati wa Ufunuo wa Nuru, Kwa levo aliofikia uwezo wake wa kuponya ni mkubwa mno ,Vinginevyo unadhani kwanini anaitwa Malkia wa nuru?”


“Nimesikia kwamba Silvia na Black Emperor walijifunza kutoka kwa master mmoja. Najiuliza kama yeye ana uwezo mkubwa namna hii vipi kuhusu mwalimu wao ?”


“Sidhani! Inawezekanaje kukawa na mwalimu wa kufundisha mtaalamu wa hadhi ya Ugwiji?”


“Labda utakuwa tu hujui wewe, ila kuna watalaamu ambao ni zaidi ya Magwiji na naamini hao ndio watakuwa walimu wao”


“Hizo ni hadithi tu za kuongea kitu ambacho huna uhakika nacho. Kama kweli wapo ushawahi kusikia majina yao au hata kuwaona?”


“Sijawahi kuwasikia wala kuwajua lakini hio haimaanishi kwamba hakuna watu wenye uwezo zaidi ya Magwiji”


Hayo yalikuwa ni maneno ya watu waliokuwa wamezunguka katika eneo hilo , kila mmoja akijaribu kuongea kile alichohisi ni ukweli kulingana na uzoefu na uelewa waliokuwa nao.


Masenari ambao walikuwa nusu wafu walijikuta wakirudiwa na hali zao mara baada ya kupokea muujiza kutoka kwa Malkia Mweupe , Silvia Somerset, na haraka sana walipiga magoti kando ya barabara na kuanza kumshukuru kwa kumsujudia.


“Hamna haja ya kunishukuru mimi, kama mnataka kutoa shukrani zenu basi mshukuruni yule maana kama angewaua nisingepata nafasi ya kuwaponya. Kumbukeni tu siku nyingine msizibe njia”Aliongea Silvia na kundi la watu hao walianza kumshukuru Hamza kwa kuinamisha vichwa vyao chini.


Upande wa Hamza aliishia kudhibiti mapigo ya moyo wake yaliokuwa yakidunda kwa kasi. Aliona shukrani hizo ni kama hazikuwa zikimuhusu kabisa kwasababu sio kichaa ambae angeanza kuua watu kwasababu ya swala dogo kama hilo. Lakini, hata hivyo alishawahi kuona Silvia akitumia muujiza wake wa nuru mara kadhaa ila hakujua ni kwanini awamu hio alivyotumia alihisi kuna kitu hakipo sawa.


Ni kitu ambacho Hamza pekee aliweza kugundua lakini hakutaka kuongea hivyo yaliishia ndani ya moyo wake pekee. Alihisi pia pengine alihisi tofauti kutokana yeye kubadili mbinu zake za mafunzo na kuachana na mafunzo ya nishati za mbingu na Ardhi, hakujisumbua sana kufikiria kuhusu suala hilo kichwani mwake.


“Silvia gari lako liko mbele , anza kutangulia”Aliongea Hamza na Silvia alitabasamu.


“Okey , tutaonana ukumbini basi”


Mara baada ya kuongea hivyo , Silvia aliingia katika gari yake ya kifahari maalumu na kisha kutoweka katika eneo hilo.


Hamza upande wake alisogelea katika gari yake ya Lykan huku akiwapungia mkono washikaji zake akiwaambia wasiwe na wasiwasi na kisha aliwasha gari na kuondoka.


Hatimae msongamano wa magari ya kifahari ulianza safari ya kuingia mjini Limour kusogelea katika eneo maalumu kwa ajili ya Baraza la Maksi.


****


Katika chumba cha kulala cha Gonzalez , bwana huyo alionekana kuwa katika mavazi ya kijeshi huku mkononi akiwa amevalia saa ya bei ghali na vito mbalimbavli vya thamani katika vidole vyake. Alionekana kuwa jitu ambalo linamiliki utajiri mkubwa.


Mara baada ya kujiangalia kwenye kioo alionekana kutoa tabasamu kwa namna ya kujikubali huku akiongea chini chini.


“Hatimae siku ambayo nimeisubiria kwa muda mrefu imewadia”Aliongea na kisha palepale alipanga kutoka kwa ajili ya kuelekea ukumbini , ila alisimama baada ya kusikia hodi kutoka mlangoni.


“Kapteni nataka kutoa ripoti” Alikuwa ni Helena ambae kauli yake ilimfanya Gonzalez kukunja sura huku akifungua mlango.


“Wote tunaondoka , kuna nini tena kimebakia?”


“Shushu wetu ametuma ripoti sasa hivi na kusema Lucifer amekutana na White Queen , Silvia!”


“Nini! Kwahio wanapigana?”


“Hapana , anasema Silvia alionekana kuwa katika hali ya urafiki na hakukuwepo na mtafaruku wowote. Pia ametumia Ufunuo wake wa nuru kuponyesha makundi mawili ya kimasenari yaliojeruhiana. Nimeambiwa pia ameongea na Lucifer kwa muda huku akimwambia ni matarajio yake hawatokuwa maadui bali watakuwa marafiki”


“Inawezekanaje! Alikuwa ni mke wa Black Emperor, kwanini…”Aliongea Gonzalez akiwa na mwonekano wa kufikiria.


“Tokea mwanzo mpango wa Silvia ulikuwa ni kufanya umoja wake wa The Odd ones kuwa mkubwa zaidi kuliko wa Inferno, moja kwa moja hili linawafanya kuwa washindani hivyo ni ngumu kusema wanataka kuwa marafiki”Aliongea Gonzalez.


“Hata mimi pia hiko ndio nilichofikiria lakini imeshangaza kuona Silvia kuwa katika mwonekano wa kawaida na wa kirafiki zidi ya lucifer. Master au ni kwasababu Lucifer hajapoteza uwezo wake ndio maana Silvia ameogopa kushambuliana nae?”Aliongea Helena.


“Haiwezekani. Kama kweli anao uwezo kama alivyokuwa mwanzo kwanini jana wakati nawashambulia watu wake aliamua kuangalia tu. Kingine alikuwa slow kwenye kushitukia shambulizi la kutaka kumuua ile juzi”


“Kapteni nadhani itakuwa vizuri tukichukua tahadhari. Sidhani kama utakuwa tayari…”


“Oh! Kuna wazo upo nalo?”Aliuliza huku akimwangalia kwa shauku.


“Kulingana na watu wetu walivyosema , Lucifer amefika hapa Paris akiongozana na mke wake. Ni mmiliki wa kampuni moja kubwa kutoka Afrika, kwa taarifa tulizonazo inaonekana huyu mwanamke ni muhimu sana kwa Lucifer na pia hana mafunzo yoyote ya nishati za mbingu na ardhi, kama tutaweza kumkamata..”


“Shut up! Unanichukuliaje? Yaani unataka nimteke mwanamke kwa ajili ya kumtishia mshindani wangu?”Aliongea kwa kufoka na kumfanya Helena kutetema.


“Samahani kapteni. Ni kwasababu nahisi labda kuna njama ambayo Lucifer kapanga zidi yako .."


Gonzalez alionekana kufikiria kwa sekunde kadhaa na palepale macho yake yalionekana kuchanua kidogo.


“Ingawa sitaki kutumia mbinu ya namna hii ya kuteka na kutishia lakini kama ni kweli Lucifer ameniwekewa mtego siwezi kuingia tu kizembe na kusubiri kifo changu. Kama kweli hana uwezo wowote basi tutaachana na wazo hilo ila kama anao basi endelea nao.”Aliongea na kumfanya Helena kucheka kicheko cha kishetani.


“Nimekuelewa kiongozi , tutaufanya kuwa mpango wa dharula”


“Leo lazima nipate nyota ya hadhi ya cheo cha Ugwiji. Kundi letu la Metal Tide pia litaingia katika daraja S rasmi. Hakutakiwi kuwa na makosa na kupoteza hii fursa”


“Yes sir!”


*****


Nje ya kuingilia katika ukumbi wa Set Great Assembly mambo yalikuwa yamepamba moto. Wawakilishi mbalimbali kutoka katika ulimwengu wa siri , kuanzia jamii maarufu duniani kama vile Freemason , Illuminat , Templar knight, Binamu na kuendelea walikuwa wamekusanyika nje ya mlango wa kuingilia wakifuata taratibu za kuruhusiwa kuingia ndani.


Eneo la ukumbi mwanzoni ulikuwa ni uwanja wa mpira ambao ulikuwa na uwezo wa kubeba zaidi ya mashabiki elfu therathini , lakini Watu wa Baraza la Maksi waliugeuza na kuwa ukumbi maalumu kwa ajili ya kufanyikia kwa kusanyiko hilo.


Ndani ya ukumbi kulikuwa na mizunguko mitatu ya siti na kila siti kulikuwa na jina la muhusika wa siti hio.


Watu ambao walipaswa kukaa katika siti za mzunguko wa kati walikuwa ni wanachama muhimu zaidi wa Baraza la maksi na washiriki, na hao wote wengi wao walikuwa ni wawakilishi kutoka nchi mbalimbali na pia wengine walikuwa ni kutoka mashirika mbalimbali ya daraja B na kuendelea ya ulimwengu wa giza.


Kuhusu watu waliokuwa katika madaraja ya chini zaidi wao walikaa katika siti za mzunguko wa mwisho kabisa na asilimia kubwa hao walikuwa ni kama mashabiki tu.


Kilichowavutia wengi zaidi katika ukumbi huo ni eneo la katikati.


Katika eneo hilo la katikati kulikuwa na jukwaa ambalo limejengwa kwa namna ya kipekee sana ya duara.


Steji hio ilikuwa imejengwa na nguzo ngumu na kubwa za chuma kwenda hewani. Juu ya jukwaa hilo kulikuwa na siti kumi zilizotengenezwa kwa ngozi na madini ya dhahabu. Jukwaa hilo na siti hizo zilikuwa ni kwa ajili ya Magwiji kumi wa dunia.


Viti hivyo kumi vilipangiliwa katika mfumo wa duara na katikati kulikuwa na meza kubwa ambayo ilikuwa imejaa kila aina ya vinywaji. Kubwa zaidi ni kwamba katika ngazi za kupandia katika jukwaa hilo kulikuwa kumetandazwa zuria jekundu na juu kabisa chini ya siti kulikuwa pia na mazuria mengine ya rangi tofauti tofauti ambayo juu yake yalikuwa na majina ya magwiji , kwa lugha nyepesi ni kwamba kapeti hizo zilikuwa zikionyesha ni kiti gani kila gwiji alipaswa kukaa.


Kupitia runinga ambazo zimefungwa kuzunguka katika ukumbi huo , kila mtu alikuwa na uwezo wa kuweza kuona majina ya siti hizo na mpangilio wote wa eneo la jukwaa hilo.


Katika ulimwengu wa siri Set Great Assembly au Baraza la maksi ilikuwa ni sawa na mashindano ya Olympic au Kombe la dunia na Magwiji ni wageni rasmi na wajuu zaidi. Hata hivyo umuhimu wa Baraza la maksi ulikuwa mkubwa zaidi kuliko mashindano hayo ya michezo , kwasababu kila kinachoendelea hapo kilikuwa ni kwa ajili ya kudumisha usalama wa dunia, kadri ulimwengu wa giza ulivyokuwa katika hali tulivu ndio namna ambavyo ulimwengu wa kawaida ulikuwa salama pia.


Kadri watu walivyokuwa wakiingia ndani ya Arena , kila mmoja alijawa na matarajio makubwa ya Baraza hilo.


Macho ya maelfu ya watu yalikuwa katikati ya jukwaa ndani ya ukumbi hu. Ukiachana na wawakilishi wakubwa kutoka katika mataifa mbalimbali na jamii nyingi za siri , wengi walikuwa na shauku zaidi na Magwiji kumi wa dunia ni muda gani watawasili.


Wakati huo huo upande wa nje Hamza alifuata maelekezo yaliokuwa katika kadi ya mwaliko na alikabidhi gari yake kwa mhudumu wa baraza na kisha alielekezwa katika njia maalumu ya watu mashuhuri(VIP) na ile anasogea upande huo aliweza kumuona Hewitt bwana ambae alimletea kadi ya mwaliko jana usiku akiwa anamsubiri.


“Mtukufu Prince of hell , asante kwa kutumia muda wako kushiriki katika mkutano mkuu wa Baraza la maksi mwaka huu. Ufunguzi utaanza ndani ya lisaa limoja kuanzia sasa , tafadhari nenda mpaka VIP Lounge na usubiri. Kutakuwa na mtu ambae atawakaribia kwa ajili ya kuwaelezea mchakato mzima wa kikao cha leo”Aliongea Hewitt kwa kifaransa huku akiwa na tabasamu.


“Nipo peke yangu kwenye hio lounge?”Aliuliza Hamza.


“Soryy Prince, kwasababu ya uwepo wa VIP lounge tano ,mmepangiwa kukaa wawili wawili ili kutosha. Ila kama hukubali tunaweza kubadilisha utaratibu kwa ajili yako haraka”Aliongea Hewitt.


“Usiwe na wasiwasi, naona itakuwa ni usumbufu tu na mnaonekana kuwa bize pia”Aliongea Hamza akionekana sio mwenyee kujali sana , alijiambia ili mradi aliepangiwa nae kukaa katika lounge moja sio Silvia basi hana haja ya kuwa na wasiwasi.


“Thank you for your tolerance, this way please …”Aliongea na kisha alimwelekeza.


Haikuchukua muda Hamza aliweza kufikishwa katika chumba cha mapumziko na ile anaingia tu pua zake ziliweza kunasa harufu ya kuvutia kutoka ndani.


Ndani ya chumba hicho katika meza , alionekana mwanaume alievalia joho la rangi nyeupe na Stole(Kashida au mharuma), lilikuwa ni aina ya vazi ambalo alionekana kama vile ni shekhe lakini kwa wakati mmoja alionekana pia kama mchungaji au askofu. Alikuwa na mwonekano wa kuchanganya , mzungu sio mzungu na Mwarabu sio Mwarabu, nywele zake zilikuwa ndefu na alizifunga kwa juu. Mkononi alikuwa ameshikilia kitabu ambacho kwa kukiangalia kwa haraka haraka kilionekana ni kitabu cha kale sana na maandishi yake yalionekana kuwa katika aina ya lugha ambayo haielezeki , ilikuwa ni lugha ya maumbo kama Runes hivi.


Alikuwa na muonekano wa utanashati mno na kwa haraka haraka ungekadiria umri wake kuwa katika miaka therathini hivi. Kilichokuwa kimejaza harufu nzuri ndani ya eneo hilo ni kifaa kidogo cha chuma muonekano wa kopa kama kichomea ubani na ndio kilichokuwa kikitoa moshi wa harufu ya kuvutia.


Hamza alijikuta akishituka kidogo baada ya kumuona mwanaume huyo lakini alirudi katika hali yake ya kawaida baada ya kuvuta pumzi ndefu na palepale alianza kuongea maneno ambayo hayakuwa yakieleweka kama ni lugha gani na kisha akatulia kidogo na kisha akaendelea kwa kubadilisha lugha.


“Na kitu kingine ni…”Alionekana kufikiria na yule mwanaume aliekuwa akisoma aliinua kichwa chake na kutoa tabasamu hafifu na kisha akaongea;


“Na kingine ni Forsythia”


“Ahahaha.. ni kweli ni Forsythia”Aliongea Hamza akicheka na kisha alitembea na kuchukua kikombe cha chai kilichokuwa mbele ya yule mwanaume na alikunywa kidogo.


“Mh , chai nzuri sana hii , inanukia..”


“Kumfanya mtu kama wewe kupenda kitu sio jambo rahisi”Aliongea yule mwanaume akionekana kutojali Hamza kunywa chai yake.


“Huge nakumbuka katika Baraza lililopita tuliwekwa katika chumba kimoja cha mapumziko. Kwanini na awamu hii nimewekwa katika chumba kimoja na wewe? Niambie tu ukweli umewaambia watupangie kuwa katika chumba kimoja makusudi si ndio?”.


Watu ambao hawajawahi kumuona ana kwa ana Mathiasi Huge, kiongozi mkuu wa Binamu , shirika la siri la daraja la juu zaidi la watu kutoka Bondeni, moja kwa moja angedhania bwana huyo ni mtu mzima na mzee, hakuna ambae angekubali kumuona ni kijana mdogo namna hio.


Lakini ukweli kwa viongozi wakubwa ambao wanaongoza mashirika makubwa ya kiitelijensia kama binamu walikuwa na maisha na mwonekano wa kawaida sana.


Ikumbukwe bwana huyo hakuwa tu kiongozi wa Binamu , lakini vilevile alikuwa akimiliki mtandao mkubwa wa kiitelijensia ufahamikao kama jicho la Anga, mtandao ambao humuwezesha kujua kila aina ya siri ya dunia.


“Kama nikisema ni kama bahati kuwekwa katika chumba kimoja , je utaniamini?”Aliuliza Huge huku akifunga kila kitabu.


“Siwezi kukuamini”


“Kama ni hivyo sidhani ni muhimu kuelezea ukweli , maana hakutokuwa na utofauti wowote”


“Kulikuwa na haja ya kwenda mbali hivyo? Najua bila hata ya kumiliki pete umeweza kuwa kiongozi mkuu wa Binamu na Bondeni kwa miaka mingi. Nikwambie tu pete niliokuwa nayo ni ya mke wangu na naitunza kwa ajili yake, hata kama uniambie nikupatie sasa hivi siwezi kufanya hivyo”Aliongea Hamza.


“Napenda watu watu wa aina yako Bro, watu wa lugha ya moja kwa moja kwenye pointi”


“Sijaona haja ya kuznguka kwasababu najua kwa mtandao mliokuwa nao lazima mmefanya uchunguzi na mnajua pete ninayo mimi. Kwanini niigize kutokuwa nayo?”Aliongea Hamza na Huge alitingisha kichwa.


“Ukweli ni kwamba sina uadui wowote zidi yako wala juu ya mke wako, vinginevyo kama ningetaka asingekuwa hai mpaka sasa hivi. Lakini kuhusu hio pete ina uhusiano mkubwa na jamii yetu ya watu wa Bondeni kwa kubeba siri nyingi . Ijapokuwa siihitaji kwa ajili ya kuonyesha cheo changu, lakini ina umuhimu wake mkubwa”Aliongea na kumfanya Hamza kucheka.


“Kama ni hivyo unaonaje tukifanya hivi , kwanini msiniache nikaa kwanza na hii pete kwa muda na baada ya muda nitaongea na mke wangu na kama akikubali nitawarudishia”Aliongea Hamza.


“Bro kama utanipatia hii pete sasa hivi nitakuambia taarifa muhimu na nyeti sana”Aliongea.


“Taarifa gani?”


“Nyeti maana yake ni ya siri. Ninachoweza kukuambia ni kwamba ukichelewa kuijua , unaweza kujutia maisha yako yote” Mara baada ya kuognea hivyo alinyoosha mkono wake kuelekea kwa Hamza.


“Nipatie hio pete na nitakuambia inahusu nini. Unapaswa kujua mimi Mathias Huge sijawahi kuongea ujinga”


Hamza alihisi fukuto katika moyo wake. Alijua ni kweli Huge hakuwa akitania, lakini bado aliona itakuwa sio vizuri kumpatia hio pete. Mara baada ya kufikiria kwa muda aliishia kutingisha kichwa chake kukataa.


“Kwa hiari yangu siwezi kukabidhi pete , labda ujaribu kuichukua kwa nguvu”Aliongea Ha,mza.


“Siwezi kuichukua kutoka kwako kwa nguvu maana najua gharama yake ni kubwa. Lakini je hutaki kujua ni taarifa gani muhimu nataka kukujuza?”


“Kuna siri nyingi sana kuhusu ulimwengu na kuna vitu vingi ambavyo vinaweza kunifanya nijutie maisha yangu yote. Hata kama ukiniambia siri moja haimaanishi utaniambia kila siku juu ya siri itakayojitokeza inayonihusu. Hivyo ni suala la muda tu nitakuja kukutana na kitu ambacho kitanifanya nijutie. Kama ni hivyo kwanini nikupatie pete kwa ajili ya kuepuka kujutia mara moja? Mimi ni binadamu na kama binadamu siwezi kutabili kitakachonitokea , kama ningekuwa na uwezo huo kuna maana gani ya kuishi sasa?”.


“Kama huo ndio mtazamo wako basi siwezi kukupinga , wala kukulazimisha kuichukua pete kutoka kwako, ila sisi watu wa Binamu na teknolojia yetu ya jicho la Anga , hatuwezi kutoa taarifa yoyote kwa watu wa jamii ya INFERNO mpaka pale tutakapoipata Pete”


“Kama unanibania hivyo basi sina jinsi zaidi ya kutegemea mfumo wa intalijensia yangu mwenyewe”Aliongea Hamza na muda huo waliweza kusikia mtu akigonga mlango na Hamza alimkaribisha kuingia.


Baada ya mlango kusukumwa aliingia mwanaume mweusi alievalia suti nyeusi na miwani yenye fremu za rangi ya nyeusi.


“Master kutoka Bondeni na Master Lucifer, naitwa Khalid Seid katibu muhtasi wa baraza la Set na nipo hapa chini ya maagizo ya viongozi kwa ajili ya kuwaelezea utaratibu wote wa mkutano”Aliongea.


“Nini kinaendelea! Kikao si kikao tu cha pamoja?”Aliuliza Hamza.


“Sir, kwasababu ya baraza la mwaka huu kuambatana na mkutano mkuu wa Magwiji na wote kumi mmewasili , uwepo wenu ni tumaini kwa watu wa daraja la chini kama sisi. Hivyo tumeweka utaratibu kwa ajili ya kutoa tuzo kwa taasisi ambazo zimepanda madaraja. Katika miaka mitano iliopita zipo jumuiya kumi na tatu ambazo zimepanda kutoka daraja C mpaka daraja B na kuna jumuia tatu ambazo zimepata kutoka Daraja B kwenda Daraja A.”


“Mheshimiwa Lucifer , wewe ni mtu muhimu na wa kipekee zaidi hivyo tunaomba ushiriki katika utoaji wa tuzo katika makundi yaliopanda daraja kutoka B kwenda A”


“Makundi matatu ambayo yamepanda kutoka Daraja B kwenda Daraja A ndio Barham , Bafodill na Sea Demons?”Aliuliza Hamza.


“Ndio , haya ni makundi yote ambayo uliwahi kuhudumu, yote yamepanda madaraja na kuingia katika orodha ya makundi ya hadhi ya daraja A”


Ijapokuwa makundi haya tokea mwanzo yalikuwa katika daraja A , lakini bado hayakuwa yamepokea cheti rasmi kutokana na kwamba kipindi ambacho walingia katika daraja A Baraza la Maksi bado halikuitishwa.


“Tumeona kama mwanzilishi wa haya makundi , itakuwa vizuri kama utawakabidhi cheti na tuzo”


Hamza alishangaa , hakutegemea kutakuwa na tukio la shangwe la namna hio , ila ilikuwa kweli , kipindi cha nyuma ili kuunganisha makundi ya wapiganaji katika ulimwengu wa siri ili kujitegemea alitengeneza makundi matatu na kazi tofauti , la kwanza alitengeneza Barhams ambalo hili lilikuwa kundi la Kimasenarti , akatengeneza Bafodil ambalo hili lilikuwa kundi ambalo kazi yake ni kuua , Kuhusu kundi la kiharamia la Sea Demosn liliundwa na Leviathani na wengine. Mwanzoni kundi hili halikuwa na ushirikiano kabisa na Hamza lakini baadae ukaribu ulitokea kutokana na Mameni kulisaidia sana hili kundi katika biashara ya kusambaza na kuuza siraha ma kutokana na mchango mkubwa wa Hamza ilibidi Leviathan na wenzake kulisalimisha kwa Hamza.


Sasa makundi haya Hamza hakujihusisha nayo sana baada ya kustaafu na badala yake aliwaacha washikaji zake wayaendeleze na kipindi anayaacha na wakati uliopo hayakuwa kawaida , yalikuwa yamepiga hatua.


Hamza mara baada ya kufikiria kuhusu kwenda kuwapa tuzo washikaji zake kwa mafanikio yao alijihisi kujivunia..


“Hamza hongera sana , watu wako kumi na mbiili wa jumuia ya Inferno hakika wanayaishi majina yao . Wamekuletea heshima kubwa”Aliongea Huge ambae alikuwa akijua kuhusu hilo kwa muda mrefu tu.


“Haha.. ndio , hawa ni ndugu zangu wakubwa. Kwasababu ndio wameyakuza na kuyapandisha kimadaraja na mimi sikuchangia chochote basi itakuwa sawa kuwapatia tuzo.”


“Asante sana Sir Lucifer kwa kukubali utaratibu tulioweka . Mimi kama mwafrika mwenzako najivunia sana juu ya mafanikio yako”Aliongea yule bwana na kumfanya Hamza kutabasamu.
 
SEHEMU YA 201.


Baada ya Khalidi kuondoka, Mathias Huge alionyesha tabasamu la kutanabahika huku akimwangalia Hamza.


“Hamza unapanga kweli kutojihusisha na makundi yako ya Barhams, Bafodil na Sea Demons?”


“Kwanini nijihusishe wakati Washikaji zangu wanafanya kazi nzuri , wanastahili kuongoza na isitoshe ikitokea ninahitaji msaada wao naweza kuwaomba tu”


“Hata kama ni marafiki zao wa kufa na kuzikana lakini hawawezi kukufuata kila mahali. Lakini kwa msingi uliowajengea sidhani kama wangechukia kushiriki kwako kama ungetaka, maisha yako yangekuwa mepesi zaidi kuliko kustaafu”Aliongea.


“Nimekusikia Msomi, lakini kwanini nahisi maneno yako yana zaidi ya maana. Kwa unavyoongea ni kama vile unahisi kuna vita inayokuja mbele yangu na nahitaji kuwa na kikosi cha kunilinda”


“Kuhusu hilo siwezi kuongea sana , hususani taarifa muhimu ambayo nilipaswa kukuambia kama ungekidhi matakwa yangu”


“Hey! Msomi kama nisingekuwa katika mudi nzuri , ningekuwa nishachana kitabu chako kama ungeniendelezea haya maigizo yako”Aliongea Hamza huku akitoa sigara kwa ajili ya kuvuta.


“Bro hii sio sehemu ya kuvutia sigara na isitoshe nishafukiza dawa hiki chumba”Aliongea Huge huku akiwa amekunja sura .


“Una masharti mengi sana , yaani umefukiza dawa ila hutaki mimi nivute sigara?”Aliongea Hamza na kuwasha sigara yake bila kujali.


“Kwa leo unaweza kufanya unavyotaka , ila kwanzia kesho nitafanya ninavyotaka mimi”Aliongea.


“Wewe msomi maneno yako yamejaa ukakasi muda wote ila hayanitishi”Aliongea Hamza akimwangalia huyo bwana.


Mathiasi Zuge hakujali sana maneno yake na alikaa kwenye zuria na kisha alikunja miguu na kuanza kufanya tahajudi kama vile anasali.


“Nina shukuru kwa umoja wa Inferno kusitishwa. Vinginevyo kwa ninavyojua lingeshanikuta jambo muda huu”Aliongea akiwa amefumba macho na Hamza hakujali zaidi ya kuendelea kuvuta sigara yake , huku akichukua rimoti na kuwasha TV na kuweka chaneli inayoosha marudio ya mpira na kuanza kuangalia kupoteza muda.


*****


Muda wa saa tisa za mchana katika gari aina ya Chevrolet SUV , Regina alijikuta akishituka kutoka usingizini huku akiwa katika hali ya kuhamaki.


Regina hakukumbuka hata ni kitu gani kilimtokea. Kutokana na Hamza kumuaga kwamba hatokuwa nae kwa kipindi cha siku mbili , siku ya jana yake alishinda kazini na siku ya pili hivyo hivyo alienda kazini kwa ajili ya kuendelea na vikao na kusaini baadhi ya makubaliano.


Lakini sasa wakati alipoenda msalani akiwa ndani ya jengo la kampuni , alikutana na mwanamke wa kizungu na ile anamaliza tu kujinawisha mikono alijikuta macho yake yakiingiwa na ukungu na kupoteza fahamu hapo hapo.


“Hello my dear Miss Regina”


Regina aliinua kichwa chake kuangalia pembeni na aliweza kumuona yule mwanamke akiwa pembeni yake na kufanya mapigo yake ya moyo kudunda kwa nguvu.


“Ilikuwa ni wewe..! Wewe ni nani na hapa tupo wapi?”Regina alijikuta akiongea kwa kingereza huku akibabaika.


“Acha kupaniki , jina langu naitwa Helena . Hapa ni mji mdogo nje ya Paris”Aliongea yule mwanamke.


“Kwanini umeniteka? Unataka hela?”Aliuliza Regina ambae alijikaza kujituliza.


“Hehe.. Regina najua wewe ni tajiri lakini kwetu sisi hela haina matumizi sana”Aliongea Helena kwa tabaasmu lakini macho yake yalionyesha ni kwa jinsi gani alikuwa siriasi.


“Kama ni hivyo unataka nini?”


“Hilo swali litakuwa gumu kujibu. Miss Regina unachopaswa kufanya ni kutoa ushirikiano wako kwetu na kutimiza kila tunachokwambia na mwishowe utaelewa maswali mengi uliokuwa nayo”


“Unataka nifanye nini?”Aliuliza Regina akiwa katika hali ya kuchanganyikiwa na Helena alinyoosha mkono kuelekea uwanja wa mpira wa miguu.


“Kuna tukio linalohusisha ulimwengu wa siri , linaloendelea ndani ya huo uwanja. Tunachotaka ni wewe kuingia na sisi kama mwanachama wa kundi letu la kimasenari”.Aliongea Helena na kumfanya Regina mapigo yake kwenda mbio.


“Nyie watu , mna ugomvi na Hamza?”


“Miss Regina , una maswali mengi sana”


“Kama usiponielewesha , siwezi kutoa ushirikiano”


Aliongea Regina lakini dakika ile ghafla tu kwenye mikono ya Helena kilionekana kisu ambacho kilienda kuwekwa katika shingo ya Regina.


“Darling, I only need less than a second to kill you. Are you sure you want to play with fire?”Aliongea Helena kwa sauti ya kunong’oneza lakini alionekana kuwa sirasi mno.


Regina aliishia kuchanua macho yake tu bila ya kufanya chochote , alijihisi kukosewa mno . Lakini kutokana na kuogopa kufanyiwa kitu kibaya aliishia kutingisha kichwa kukubali.


“Niambie unataka nifanye nini?”





“Ni rahisi sana , unachopaswa kufanya ni kunifuata na kuingia ndani ya huo uwanja pamoja na utakaa pembeni yangu na kila kitu kitakuwa sawa”


Regina alijikuta akitamani kumuona Hamza akitokea na kumsaidia lakini alijua ni kitu ambacho hakiwezekani hivyo aliishia kukubali tu.


Helena alivuta kombati ya kijeshi ya kundi la Metal Tide na kumpatia Regina.


“Kipenzi kabla ya kutoka nje ya hili gari unapaswa kwanza kubadilisha katika hayo mavazi”


Regina aliishia kuangalia mavazi hayo ya kijeshi na kisha alivuta pumzi nyingi na kuzishusha na kisha aliyachukua na kuanza kubadilisha.


Mara tu baada ya kutoka nje ya gari , wanajeshi wa kiume kama nane hivi waliwasogelea.


“Comb na Sean kila kitu kipo tayari?”Aliuliza Helena akiwaangalia wanaume wa kizungu waliokuwa mbele.


“Usiwe na wasiwasi Helena , kila kitu tayari , tushawahonga watu wa getini na watamruhusu huyu mrembo kuingia, Mpangilio wa siti pia ushafanyiwa marekebisho na jina lake kuongezwa” Aliongea yule mwanajeshi na kumfanya Helena kutingisha kichwa na kisha kumwangalia Regina ambae hakuwa akielewa wanachoongea kutokana na kutumia lugha ya kifaransa .


“Kipenzi tangulia mbele yangu na fuata hao wanaume kwa nyuma. Usije kujifanya mjanja la sivyo kisu changu hakitokuwa na huruma kutoboa moyo wako”


Regina aliishia kung’ata meno yake kwa hasira na hakuongea neno zaidi ya kutingisha kichwa chake kukubali.


Mapema tu kundi lile la watu lilifika katika geti la kuingilia uwanjani. Watu wa getini hawakuonekana kumjali Regina kabisa zaidi ya kumruhusu kuingia ndani haraka.


Muda huo Regina alikuwa amekwisha kusahau woga wake kabisa na badala yake alijikuta akishitushwa na mabandiko mengi katika njia ya kuingilia yaliokuwa na slogani mbalimbali.


Tokea aachane na Hamza alikuwa bize sana kutafuta taarifa mtandaoni kuhusiana na ulimwengu wa siri lakini pia aliweza kutumiwa faili kuhusiana na taarifa za ulimwengu huo , hivyo alielewa mara moja eneo hilo ndio mahali ambapo Baraza kuu la Maksi katika ulimwengu wa siri ndio linapofanyikia.


Muda ule ni kama sasa akili yake ilifunguka na kujiuliza au Hamza alivyoaga kuna sehemu anaenda , amekuja hapo kwa ajili ya kushiriki?.


Regina alishindwa kujizuia na kuhisi wasiwasi. Alikuwa na wasiwasi uwepo wake unaweza kutumiwa kwa ajili ya kumdhuru Hamza na kama ni hivyo si inamaana watu waliomleta hapo ni hatari zaidi kwake?.


Mara baada ya kufikiria kuhusu hilo , Regina palepale mawazo ya kukimbia yalimwingia na ile anageuka nyuma na kukutanisha na macho ya ukauzu ya Helena alijikuta akinywea na kuishia kutembea kimya kimya.


Hatimae kundi la watu hao akiwemo Regina waliweza kufika katika siti zao. Regina alionyeshwa pakukaa na Helena alikaa pembeni yake.


Regina alijikuta akianza kukagua mazingira ya eneo hilo na hakuacha kushangazwa na jukwaa mbele yake lenye viti vya muonekano wa dhahabu na kupambwa na mazuria makubwa.


“Vipi! Una shauku ya kutaka kujua nani anakaa pale?” Helena alikuwa ashamaliza kazi yake aliopewa na Gonzalez hivyo aliona aongee na Regina kwa upole kidogo.


“Kuna jina la Mkuu wa Bondeni katika hizo kapeti?”Aliuliza Regina.


“Ndio , si unaona kabisa pale jina lilioambatana na nembo ya jicho la anga kuashiria jamii ya siri ya daraja S ya watu wa Binamu. Kwanini unaiuliza?”Aliongea


Regina mara baada ya kuona nembo ya Binamu ambayo iliashiria watu wa bondeni alijikuta akishikwa na shauku juu ya chimbuko lake.


“Vipi kuhusu majina mengine?”


“Unachoona hapa ni Baraza la maksi la Set Evaluation. Zile siti ni kwa ajili ya magwiji wa dunia mbao wamealikwa kwa ajili ya kushiriki mkutano mkuu. Miaka mitano iliopita magwiji wengi wameshuka madaraja , huku wengine wakistaafu. Hivyo ili kuhakikisha hakutokei mgogoro wa nani wa kuziba mapengo ,ndio maana magwiji wote mpaka wale waliostaafu wameitwa kushiriki”


“Kwa kukurahisishia ni kwamba Mkutano wa Magwiji ni kwa ajili ya kuwapa changamoto watu ambao hawajaridhika na uwezo wa magwiji ambao wameteuliwa na wakishinda maana yake wataweza kupanda daraja na kurithi nafasi zao”


Regina pia alikuwa na uelewa japo ni hafifu kuhusu wataalamu wa mapigano wa daraja la Ugwiji ni nini.


“Lakini je hawa magwiji wote watafika? Kwanini wakubali kujaribiwa upya kama washafikia katika hatua hio ya ugwiji? Kuna haja ya kuthibitishia uwezo wao kwa watu tena?”


“Kipenzi changu Regina unaonekana huna unalolijua. Unadhani ukishafikia katika Daraja la Ugwiji ndio mwisho ? Watu wanajifunza na wanapanda levo vilevile na kila mtu ndoto yake ni kuwa katika orodha ya magwiji kumi. Je unadhani watawezaje kuingia katika hilo daraja bila ya kuwapa changamoto na kuwashinda waliopo ili kuwaangusha. Isitoshe pia hata hao magwiji wenyewe wanajali heshima yao , ikitokea mtu akibeza uwezo wao kwa kujigamba kuwa na uwezo kuwazidi unadhani ni kipi kitafanyika kama sio kupigana nao na kuwazimisha? Asilimia kubwa ya Magwiji wote kumi wana makundi yao , iwe ni ya kimasenari au ni makundi ya kifamilia ambayo wanataka kulinda , ikitokea gwiji akakosa heshima mbele ya wapiganaji wadogo maana yake na makundi yake pia yatadharaulika, ila wakishinda na kuzima wale ambao wanawachokoza mbele ya umati huu maana yake ni kujitengenezea mazingira ya heshima na kutochokozwa. Unaelewa?”Aliongea Helena.


Regina alionekana kuwa katika hali ya kuwaza lakini kwa maneno hayo alijikuta akishindwa kujizuia na kumfikiria Hamza. Alijiuliza ni nafasi gani ambayo Hamza anayo katika ulimwengu huo wa giza, alijikuta akiangaza macho yake kulia na kushoto na kujiambia lazima na yeye atakuwa na nafasi yake vilevile japo hakujua ni nafasi gani.


Lakini kwa wakati mmoja swali liliingia katika kichwa chake , kama Hamza amepambana na kujitafutia umaarufu kupitia mapigano je alikuwa akijaribu kulinda nini?.


Wakati Regina akiwa katika dimbi la mawazo ghafla aliweza kusikia sauti nzuri ya kiume kupitia spika ikiongea kwa lugha ya kingereza;


“Friends from the global underground world! Delegates from different countries! And representatives from various major organizations! This event is hosted by the SETH Association, supported by the five main members and eighteen non-permanent ones. The 21st International SETH Rating Conference is officially starting now!”


“Marafiki kutoka kila pande ya dunia ya ulimwengu wa siri! Vikosi kutoka nchi mbalimbali na wawakilishi kutoka mashirika makubwa tofauti. Tukio hili limeandaliwa na Seth Association na kuungwa mkono na wanachama wakuu watano na wanachama kumi na nane wasio wa kudumu. Mkutano wa 21 wa Baraza la maksi hatimae umeanza rasmiiii….”


“Na sasa nachukua nafasi hii ya heshima kumkaribisha Mr Maxim , Mwenyekiti wa Baraza la Maksi la Sytor Asscociation , kwa ajili ya kutoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano”


Mara baada ya kuongea hivyo makofi mengi yaliweza kusikika kila pande za uwanja huo, kwa wakati mmoja alionekana mzee wa kizungu akitembea kupandisha katika jukwaa maalumu.


Hakupokea maiki lakini dakika ambayo alianza kuongea sauti yake ilikuwa ni kama ngurumo ya radi , kwani ilisikika kwa kila mtu.


“Habari kwenu wote , mimi ni Paul Stephan Maxim ….”


Regina alijikuta akipigwa na butwaa mara baada ya kuona mzee yule akiongea na sauti yake kusafiri uwanja mzima bila ya kutumia kifaa chochote , lilikuwa ni jambo la maajabu kwake.


“Anawezaje kuongea bila kifaa na sauti yake kusikika kote?”Aliongea Regina kwa mshangao na kumfanya Helena kutoa kicheko.


“Raisi Maxim kabla ya kuwa mwenyekiti wa Set Association alishawahi kuwa kiongozi wa juu wa jamii ya binadamu wasio wa kawaida inayofahamika kama Adept Association. Ana uwezo wa ajabu wa sauti hivyo hata asitumie maiki anaweza kusikika kwa zaidi ya maili kadhaa. Baada ya kustaafu kama raisi wa Adept association ndio alijiunga na Set Associaton. Anachukuliwa kama moja ya watu wa heshima sana wenye uwezo usio wa kawaida , ijapokuwa hajawahi kuingia katika orodha kumi ya magwiji lakini ni mtu wa kuheshimiwa na watu wa mataifa mengi na hata mashirika makubwa duniani ya siri”Aliongea Helena.


Regina kusikia hivyo alikuwa makini mno na alikuwa amekwisha kusahau kama alikuwa ametekwa na sasa aliweka umakini wake katika kusikiliza hotuba ya Maxim.


Dakika kumi mbele hotuba fupi ya Maxim ilikaribia kufika mwisho na alimalizia kwa kutoa tabasamu na kuangalia pande zote za majukwaa kwa kuzunguka huku akiwa na tabasamu pana usoni na kisha akaendelea kuongea;


“Kwa namna ulimwengu wa giza unavyozidi kustawi na kukua , mimi mzee wenu najiona ni mwenye furaha kubwa . Katika mkutano huu ndani ya hili eneo ni matarajio yangu kwa kila mmoja wenu kusahau kinyongo alichokuwa nacho na kisha tukae chini na tuongee na kufanya maamuzi juu ya maendeleo ya ulimwengu wa siri. Sina haja ya kusema mengi lakini niwaambie tu Baraza hili la ishirini na moja litakwenda kuwa la aina yake. Baada ya vikao vitatu vya kawaida tutaingia katika hatua ya mwisho ya kikao kikuu cha magwiji. Nimwachie sasa steji muongozaji wetu wa mkutano kwa ajili ya kuwakaribisha Magwiji kumi wa dunia”


Mara baada ya kumalizia na sentensi hio , eneo lote lilipuka shangwe kubwa kutoka kwa watu. Sauti ya mtikisiso wa uwanja ulisambaa kila kona.


Rais Maxim aliishia kupiga makofi na kisha kupungia watu pande zote na akatoka nje ya steji.


“Hatimae ni muda wa kuwaona magwiji kumi wa dunia wa hadhi ya juu kabisa. Wataitwa mmoja mmoja kwa kuzingatia alfabeti za majina yao halisi. Piga makofi mengi kwa ajili ya kumkaribisha Gwiji namba moja wa dunia”


Palepale mziki mlaini lakini wa kuchangamsha akili ulisikika ukiambatana na tukio la kufurahisha lililoonekana katika skrini zote za TV zilizofungwa juu ya steji na kufanya watu wote kukaa kimya na kutoa macho yao juu ya runinga hizo.
 
SEHEMU YA 202.


Karibu kuzimu.


Katika zile Skrini kubwa zilizokuwa zimezungushwa kwenye jukwaa kulionekana kitabu kikubwa kilichokuwa kina maandishi kikifunguliwa kurasa zake huku yakionekana maandishi yalioambatana na picha. Katika kitabu hicho ulionekana wasifu wa Gwiji namba moja na yule mshereheshaji palepale alianza kusoma maandishi yale kwa namna ya kuvutia;


“Amebeba wasifu wa jina sawa na la mfalme mkuu wa mithiolojia za Kiarmenia, ambae alifunga elementi nne za mhimili wa dunia. Uwezo wake uliibua wivu mkubwa kwa watu wote wanaotumia nguvu za ziada kwa kuwa na uwezo uliomruhusu kuzitumia elementi kwa faida yake pekee. Hakuna anaejua jina lake halisi ni nani , mwonekano wake ni wenye kubadilika badilika milele. Ana uwezo wa kubadilika na kuwa hewa na ndio maana watu wa ulimwengu wa siri wakaamua kumbatiza jina la Air . Makofi mengi kwa ajili ya kumkaribisha Raisi wa Adept Association, Mr Air”


Mara baada ya mshereheshaji kuongea watu wote walipiga makofi na kisha walitulia kwa ajili ya kumuona gwiji namba moja akiingia. Lakini sasa, hakuna mtu yoyote alieweza kumuona akiingia katika njia maalumu iliotandazwa zuria na badala yake watu walishangaa tu mtu kuwa tayari amekwisha kukaa katika siti iliokuwa na jina la Air ndani ya jukwaa la Magwiji.


Alikuwa amevaa vazi la kikale mfano wa joho lililofungwa na kamba kiunoni. Licha ya mwili wake kuonekana lakini sura yake haikuweza kuonekana moja kwa moja na kujua alikuwa ni mtu wa rangi gani. Kwa namna ambavyo alifika katika jukwaa hilo ni kama vile aliteleport na kuibukia moja kwa moja kwenye siti yake.


Kitendo kile cha ajabu kilifanya watu ndani ya uwanja huo kupiga makofi mengi sana na kupiga makelele ya kumshangilia, hususani kwa binadamu ambao ni wanachama wa umoja huo wa watu wenye vipawa maalumu.


Mr Air alisimama na mkono wake ulionekana kupungia watu na kisha alirudi na kukaa kwenye kiti chake.


Regina ambae alikuwa akiangalia mlolongo wa matukio hayo alijikuta akifikicha macho yake kwa nguvu akiwa haamini kile ambacho anaona.


“Inawezekanaje , amewezaje kufika pale bila ya kuonekana au ni kwa mazingaombwe?”


“Hapana ule ni uwezo wake, anaitwa hewa kwasababu anaweza kujifananisha na hewa na asiweze kuonekana kwa macho. Hajawahi kujulikana kwa sura moja kwasababu kila anapotokea ana sura tofauti na sauti tofauti , hivyo hakuna anaemfahamu ni sura ipi ni ya kwake halisi au kama alishawahi kuonyesha sura yake kabisa. Kwa lugha nyepesi ni mtu ambae haonekani , na kwasababu hajawahi kuwa na ugomvi na mtu yoyote haijawahi kufahamika uwezo wake halisi ni upi .”


Regina kama binadamu wa kawaida ilikuwa ngumu kwake kuamini mtu anaweza kuwa translucent na asionekane hewani , kitu ambacho kilikuwa nje ya mantiki za kisayansi.


Maajabu ya ulimwengu wa siri yalikuwa ni zaidi ya kile alichowahi kufikiria. Regina alijikuta akisahau kabisa kama ametekwa na kumuona Helena ni kama mtu ambae amemleta hapo kwa ajili ya matembezi.


“Kwahio unasema kuna watu aina ya Mr Air kwenye Chama cha Adept?”Aliuliza Regina.


“Usifikirie sana, umoja wa Adept una watu wasiopungua mia moja , licha ya kuwa na uwezo wa ajabu ila hawana uwezo mkubwa wa mapigano. Mr Air anaaminika sio kiumbe wa sayari ya dunia, Asilimia kubwa ya watu wa jumuia ya Adept wana vina saba vya damu ya wanyama”





“Damu ya Wanyama !” Regina aliishia kutingisha kichwa kwa mshangao, “Ila inawezekana kwa namna alivyo haonekani kuwa binadamu wa kawaida”Aliongea Regina na kumfanya Helena kucheka.


“Miss Regina hata wewe pia unaonekana kushangaza? Yaani nimekuteka kukuleta hapa lakini naona umeshanigeuza kuwa Tour Guide wako. Huogopi nitakuuwa na kisu changu?”


“Nitafanyaje sasa? Kwamba nikuogope mpaka kufa. Nimeona kwasababu siwezi kujiokoa ni bora nikachukulia kama fursa ya kujifunza zaidi”Aliongea Regina na Helena alitaka kuongea neno lakini aliacha baada ya kusikia mshereheshaji akimtangaza Gwiji mwingine.


“Kutokana na uadilifu wake wa kiimani , aliogelea katika utukufu mkuu wa Bwana mtakatifu na kuishi katika baraka za mbingu na ardhi. Alipofikisha miaka ishirini na moja alielekeza mikono yake juu na kupokea upanga wa kiapo, alipofikisha miaka ishirini na tanu akaelekeza mikono yake juu na kupokea mkuki wa kulinda mbingu na ardhi. Hata baada ya miongo kadhaa kupita bado alisimama kileleni kama shujaa juu ya Jumba takatifu. Tunamkaribisha kwenu Malaika Mkuu Mika kutoka Madhabahu takatifu ya kifalme”


Akiwa amevalia joho refu lililonakishiwa na nyuzi za dhahabu alionekana. Alikuwa amevaa mkanda kiunoni wa rangi ya dhahabu kama shujaa. Huku akiwa ameshikilia mkuki mrefu kwenda hewani kuzidi kimo chake uliokuwa umenakishiwa na vito vingi vya thamani


Alikuwa na nywele za kahawia , na masharubu mengi katika uso wake. Alikuwa akitembea huku kichwa chake akiwa amekiinua juu bila ya kukipindisha kama mwanajeshi. Mwanaume huyo aliaminika kuwa na umri zaidi ya karne moja. Hakuwa mwingine bali ni Malaika ama kiongozi mkuu wa Mahakama takatifu Mikaeli.


Mika mara baada ya kwenda kusimama juu ya jukwaa wafuasi wake kutoka Falme ya Mahakama takatifu walisimama na tofauti na kushangilia walianza kusali huku macho yao yakiwa yameng’azwa na nuru ya imani.


Lakini hata hivyo kulikuwa na kundi la watu ambao walikuwa wamekunja sura kama wamebanwa na mlango huku sura zao zikiwa zimejaa dharau , walikuwa ni wafuasi wa shetani wakiwakejeli wafuasi hao kwa sala zao.


Mikaeli aliinua mkuki wake juu angani na kufanya utoe mwanga wa kuumiza macho na kisha ukazima na haukuonekana kwenye mikono yake bali ulionekana kusimikwa katika mkono wa kulia wa kiti chake.Akiwa na mwonekano wa kujiamini alikaa chini.


Mapema tu kabla ya mshereheshaji kutangaza Gwiji mwingine kujitokeza mwanaume mwenye mwili mkubwa sana kama kiboko alitokea katika njia ya kutokea uwanjani.


Mtu huyo alikuwa na kimo zaidi ya mita mbili kwenda hewani na alikuwa amevalia Vest ya ngozi ya mamba bila shati na kufanya mikono minene sana kuonekana , nywele zake zilikiwa ni nyeupe kama mvi na masharubu yake pia.


Alikuwa amevalia kofia ya kijeshi kichwani ilionekana kuwa ya zamani mno na mkononi alikuwa ameshikilia kiko na alitembea huku akivuta sigara kutoka katika kiko kile.


Kiunoni mwake kulikuwa na Kitara au sime ndefu na pana, mpini wa Sime ile ulitengenezwa kwa madini ya Silver na dhahabu na vito vingine vya kuvutia. Ilionekana haikuwa Sime ambayo unaweza kuikadiria bei yake.


Bwana huyo alionekana kujikaribisha mwenyewe huku akipunga mkono hewani kwa kucheka.


“Nadhani sina haja ya kumtambulisha tena , kila mmoja wenu amemuona na kumfahamu”


Alikuwa ndio mkuu wa kundi la kiharamia namba moja duniani. Inasemekana ushujaa na ujasiri wake alirithi kutoka kwa watangulizi wak, yaani mababu zake maarufu kama The Vikings !. Kundi lake la kharamia lilikuwa la Daraja A lililofahamika kama Nyangumi wa Barafu(Ice Whaler).


“Ni kapteni Phantom Oleg” Sauti za maharamia wa Ice Whaler zilisikika zikishangilia.


Leviathani aliekuwa amekaa, alimpigia makofi Oleg . Ingawa walikuwa washindani lakini Oleg alikuwa mkubwa kwake katika kazi ya uharamia, kwa Lugha nyepesi ni kwamba Leviathani alimkuta Oleg kazini.


“Maharamia pia wanaruhusiwa kushiriki katika huu mkutano , si wanawinda na serikali nyingi duniani?”Aliuliza Regina .


“Haha.. kwa nguvu waliokuwa nao hao maharamia inaweza kutishia usalama wa nchi yoyote ile wakijaribu kumkamata , kingine katika Mkutano mkuu wa Baraza la Maksi hakuna mtu mzuri wala mbaya , au mhalifu na asie mhalifu. Ukisikia sehemu ambayo wafuasi wa mungu na shetani hupeana mkono wa amani, basi ni hapa”


“Hili jitu Midevu linaonekana kuwa na msisimko mkubwa kuliko Mr Air na Mika licha ya kuonekana uwezo wake ni mdogo”Aliongea Regina.


“Regina usimchukulie poa Phantom. Ingawa anaonekana wa kawaida lakini ni maarufu mno katika mbinu za kivita baharini. Ana miliki meli ya kivita yenye upanga maarufu kama Sea God Blade, unaovumishwa kuwa na uwezo wa kukata meli yoyote mara mbili.


“Sea God Blade!” Regina licha ya kutokujua tamathali za kijeshi hakutaka kuamini kama kuna meli ya kivita ambayo ina uwezo wa kutenganisha meli nyingine mara mbili kupitia upanga.


“Ndio. Meli yake ya kivita imefungwa upanga mkubwa mbele wenye nguvu kubwa. Phantom anajitambulisha kutokea katika kizazi cha Vikings, yaani waliobarikiwa juu ya bahari. Anaweza asiwe na uwezo wa kupigana mkubwa akiwa nchi kavu lakini katika bahari ni mtu mwinginge kabisa.Anao uwezo wa kuponya majeraha yake yote kwa kugusana na maji ya bahari”


“Kweli!?”Regina aliuliza kwa kushangaa.


“Hakuna uthibitisho , ila inasemekana anao uwezo wa kuwasiliana na viumbe wanaoishi chini ya bahari, ikiwemo Majini bahari na Nguva na ndio wanaomsaidia kuzamisha meli na kuiba mali. Inasemekana uwezo wake aliupata baada kufariki akiwa baharini na nafsi ya kiumbe wa ajabu ilimvaa na akafufuka. Kama isingekuwa uwezo wake mkubwa wa kupambana akiwa majini unadhani angeweza kulipa umaarufu kundi lake la kiharamia la Ice Whalrer? Yote ni kwasababu sio mtu wa kawaida”


Regina mara baada ya kusikia maelezo hayo aliihsi ubaridi wa mgongoni ukimpitia, kwasababu alichosikia ni kama Oleg hakuwa binadamu. Alijikuta akitoka mawazoni mara baada ya kumsikia mshereshaji akiongea tena;


“It is said that the real Dragon Knights will not be harmed by the dragon flames. They can bathe in the dragon flames and dance with the dragon …”


Mara baada ya kuongea hivyo sauti zilianza kupiga mayowe ya shangwe huku wakiimba kwa shangwe kwa kutamna neno; we’re burning.


“Nichukue nafasi hii kumkaribisha kwenu Aulando- Saint Rodriguez, kiongozi mkuu wa Holy Knight na mlinzi mkuu wa DSS(Dragon Slaying Sword)”


Mara baada ya kuongea hivyo palepale alitokeza mwanajeshi alievalia vazi la kijeshi la chuma kuanzia miguuni mpaka kichwani huku akiwa na upanga mrefu kiunoni.


Vazi lake lote la chuma cha silver lilikuwa na nakshi za ajabu zilizochongwa na kubandikiwa madini ya dhahabu ya michoro ya nyoka. Eneo la kifa chake kulikuwa na picha kubwa ya Dragoni akitema moto.


Kilichovutia zaidi ni helmeti la kiroma alilovalia katika kichwa chake katika eneo la macho. Kulikuwa kumetengeneza kama vile ni miwani kubwa ya madini ya kung’aa na kumfanya aonekane kutisha mno.


Ala ya upanga wake ilikuwa imenakshiwa na chata la Wyvern na kuangalia tu mpini wa upanga huo unaweza kugundua haikuwa siraha yenye uzito wa kawaida.


“Wanaongea nini?”Aliuuliza Regina.


“Ni Creed. Tafsiri yake ni ‘We’re Burning’ maana yake ni kuwaamrisha waendesha madragoni kuwabatiza kwa moto wa Dragoni bila woga. Kwa lugha nyepesi ni kama kauli ambazo dini huwaamrisha wafuasi kuongea kama njia ya kukubali kuwa muumini kwa kubatizwa. Holy Dragon Knight ni umoja wa kiimani wa wanajeshi katika majeshi ambao wanaamini wana nguvu kubwa sana , si tu kiroho lakini kimwili pia . Ingawa Auland ndio mwanajeshi pekee alieweza kuingia katika hadhi ya Ugwiji lakini inaamnika kuna zaidi ya wanajeshi wenye uwezo kupita hata wa Auland , lakini yeye ametangulizwa machoni mwa watu kama mwakilishi pekee..”


Regina muda huo aliweza kukumbuka kauli ya Hamza kuhusu madaraja ya jamii za siri na daraja la juu zaidi ni S Class.


Ikumbukwe hata watu wa dini kubwa duniani pia wanachukuliwa kama jamii au jumuia na huingia katika Daraja S , hivyo wote hao walikuwa na misemo yao maalumu ya kutamka ukitaka kujiunga nao.


Auland hakuvua helmeti lake hata baada ya kukaa , ilionyesha ni dhahiri hakutaka kuonyesha sura yake.


“Najua wote mmekuwa na hamu ya kumuona Auland ambae ni mara chache sana kuonyesha sura yake. Lakini mtu anaefuatia ndio mzito zaidi” Mshereheshaji alitulia kidogo na kisha palepale akaongea.


“Kila kiza kinapoingia yeye ndio huamka na hakuna la kumshinda kufanya . Namkaribisha kwenu mwanachama wa kudumu wa Madhabahu ya Giza , Mwanachama pekee wa damu ya kifalme ya Strigoi . Prince Sebastianii!!”


Mara baada ya kuongea watu hawakushangilia kama ilivyokuwa kawaida, japo kwa mbali yalisikika makofi , ilionyesha watu wengi walikuwa na shauku ya kumuona pekee na hawakuwa na ushabiki nae.


Muda ule aliweza kuonekana mwanaume mzungu mwenye ngozi iliopauka , na nywele za kiblonde, aliekuwa katika makadirio ya umri wa miaka arobaini hivi akitembea kwa kujiamini kusogelea jukwaa, alikuwa amevaa Tuxedo na viatu vyeusi vya ngozi.


Sebastiani mara baada ya kupungia mkono watu kidogo , alisogea kwenye jukwaa na kuketi kwenye nafasi yake. Lakini sasa bwana huyo aligeuza uso na kumwangalia Mikaeli na wawakilishi hao wa Madhabahu ya Nuru na Madhabahu ya Giza walionekana kukasirikiana kiasi cha kufanya macho yao kuwaka.


“Regina je unaweza kuamini Prince Sebastiani umri wake ni miaka elfu tatu?”Aliongea Helena akimwongelesha Regina.


‘Nini! Miaka elfu tatu?”


“Ndio , ijapokuwa Strigoi wanakufa kama binadamu tu , lakini wanaishi muda mrefu sana, lakini hata hivyo ni wachache sana wa kufikisha zaidi ya miaka elfu moja , kutokana na kwamba wengi wao hutegemea zaidi vipawa vyao vya kulala muda mrefu ili kurefusha maisha. Mfano Prince Sebastiani mpaka kufikisha umri aliokuwa nao ni kutokana na kuwa na uwezo mkubwa sana wa kulala muda mrefu na kupigana pale anapoamka ili kujilinda , la sivyo isingekuwa rahisi kuwa hai mpaka leo hii”


Regina aliishia kumeza mate mengi na kujihisi mambo ambayo alikuwa akisikia muda huo yalikuwa ni ngumu sana kuamini. Hakuamini Vampire kama huyo ameweza kuishi miaka yote hio kwa kutegemea usingizi tu.


Ikumbukwe Strigoi wanachukuliwa kama wafu , lakini uhalisia sio wafu bali wanakuwa katika hali ya usingizi tu kwa muda mrefu. Mfano Prince Sebastiani anaweza kweli kuwa na umri wa miaka zaidi ya elfu moja lakini asilimia themanini ya umri wake ameutumia kulala usingizi mzito.


“Hakuna asie na mwisho , nadhani nikiongea kauli hii wengi wataelewa ninachomaanisha. Hatua inayofuata nakwenda kumkaribisha mwanamke ambae ameachiwa majukumu makubwa na mume wake na kujisimika katika hadhira ya watu wengi kupitia uwezo wake. Kiongozi mkuu wa The Odd ones na mwakilishi mkuu wa mamajusi wa nuru. The White Queen, Madam Silvia Somerset”


Hatimae muda huo alionekana mwanamke mrembo sana alievalia mavazi ya rangi nyeupe akipandisha kwenye jukwaa. Umbo lake na uzuri wake ulivutia wengi mno.


“Yule mwanamke ni mrembo mno. Mume wake amefariki?”Aliuliza Regina ambae alishindwa kujizuia kushangazwa na uzuri wake.


“Ms Regina huyu mwanamke kwa namna moja ama nyingine mna ukaribu..”Aliongea Helena akiwa na tabasamu la uchokozi.


“Unamaanisha nini?”


“Utakuja kujua baadae ukipata nafasi”Aliongea Helena akiacha kumuweka wazi Regina. Ukweli moja ya sababu ya kuitishwa kwa mkutano mkuu wa Magwiji ni huyo mwanamke pia.


Ijapokuwa Silvia alikuwa na uwezo mkubwa wa mapigano na kuwa maarufu lakini siku zote hakuwa akionyesha uwezo wake zaidi ya kujificha nyuma ya aliekuwa mume wake. Kwasababu ndio kwa mara ya kwanza anasimama kama kiongozi wa The Odd ones watu wengi walitaka kuona uwezo wake halisi.


Silvia mara baada ya kufika kwenye steji aliishia kuwatingishia vichwa wenzake waliotangulia na kisha alienda kukaa katika nafasi yake.


“Gwiji anaefuatia anatokea ndani kabisa ya Amerika ya Kusini , gwiji mwenye uwezo wa kuicha nafsi yake kuzurura kuzunguka msitu wote wa Amazon. Gwiji anaejitanabahisha kutokufa milele. Nawaletea kwenu Mr Skeleton kutoka Amazoni.Jeshi la mtu mmoja”Aliongea Mshereheshaji.


Palepale alionekana mtu alievalia mavazi ya kitamaduni ya asili ya Red Indiani huku kila kiungio cha mwili wake alikuwa amejifunga kwa kuning’iniza mifupa, ya aina mbalimabli kuanzia ya watoto mpaka wazee na pia ya wanyama na ndege mbalimbali. Mwonekano wake hakika ulitisha sana.


Haikuonekana sura yake kutokana na rangi alizopaka usoni na pia ngozi yake haikuwa ya kawaida , ilikuwa ni kama vile inaelekea kuoza. Regina mara baada ya kumuona mtu huyo sura yake ilikunjamana.


“Usiwe na wasiwasi, yule anafahamika kama Mchawi wa msitu wa Amazoni, ile mifupa haijatoka katika miili ya binadamu hai bali kutoka katika maiti zao”Aliongea Helena.


“Mshereheshaji kasema mtu huyu ni jeshi la mtu mmoja. Anamaanisha nini?”


“Ni rahisi sana , inamaanika kupitia uchawi wake kupitia ile mifupa anaweza kuamsha wafu na wanyama waliokufa na kupigana kwa ajili yake. Akiwa eneo la vita kadri watu wanavyokufa ndio namna anavyozidi kuwa na nguvu”.


“Unamaanisha kama White Walker wa GOT?” GOT ni filamu ya Game of throne.


“Haha.. kumbe unaangalia filamu! Ndio ni kama ulivyokisia”


“Kwanini hawa Magwiji kila mtu ana stori ya kuogopesha?”Aliuliza Regina.


“Anaefuatia sio wa kuogopesha na kubwa zaidi anatokea ukanda wa Afrika ya mashariki mathalani nchi unayotokea”Aliongea Helena na kumfanya Regina kushikwa na shauku akitaka kujua ni nani


“Mabibi na mabwana. Kabla ya White Queen kuingia katika orodha ya magwiji kumi , anaefuatia alikuwa ni mwanamke pekee kushikilia hadhi ya ugwiji. Anamiliki damu ya kifalme yenye maajabu ya moto. Anaweza kuunguza chochote. Moto ni wa kuogopwa na binadamuy wa kawaida lakini kwake ndio chanzo cha uhai. Namkaribisha kwenu binti mdogo kutoka Afrika mashariki . Nyakasura ,Miss Phoenix Girll”


Mara baada ya kuongea , palepale alionekana Nyakasura aliekuwa katika mavazi yake ya aina moja ya rangi nyekundu, hadhira haikuwa nyuma kumpokea kwa makofi mengi na vifijo.


Nyakasura siku hio licha ya kwamba hakubadilisha rangi , lakini alikuwa amevalia gauni refu lenye chata la ndege wa maajabu. Huku akiwa ameachia nywele zake ndefu.


Regina alishangazwa na mwonekano wa Nyakasura kwa kiasi kikubwa.


“Huyu msichana ni mdogo mno na yeye pia ni Gwiji?”


“Kwani humjui! Huyu ndio mlinzi mkubwa wa nchi yenu chini ya kitengo cha Malibu. Regina unaonekana kuna mambo mengi sana ya siri ambayo huyafahamu”


Regina alijihisi kuwa mjinga , aliishia kuzungusha macho yake kuangalia watu namna walivyokuwa katika majadiliano makali.


Ukweli kama sio uwepo wa Helena karibu yake asingewewza kufahamu lolote.


Walikaribisha jumla ya Magwiji nane na ni wawili tu ambao walikuwa wamebakia kutambulishwa.


Mshereshaji, ilikuwa ni kama makusudi kwani aliacha kuongea kwa nusu dakika hivi huku akiiangalia hadhira kabla ya kumtaja mtu wa tisa. Na muda uleule aliweka maiki na kuongea.


“Mtu anaefuatia kutambulishwa , jina lake halisi watu wengi hamlifahamu , lakini kulingana na mtiririko wa Alfabeti anashika nafasi ya tisa. Ni mtu wa pekee sana kulingana na sifa zake , kwasababu kwa kipindi cha miaka mitano ameacha doa kubwa la wino mzito ndani ya ulimwengu wa giza.


Kuonekana kwake kumebadili muundo wa zaidi ya miaka mia moja ya ulimwengu wa siri. Kutokana na kughairishwa kwa Mkutano mkuu wa Magwiji katika baraza la maksi lililopita chini ya maombi ya wanachama wa jumuia, nitachukua nafasi hii kuelezea kwa kina utambulisho wake kama njia ya kuonyesha heshima juu ya huyu Gwiji mwenye umri mdogo kabisa!”


Mara baada ya maneno hayo kusikika , asilimia kubwa ya wahudhuriaji wa mkutano huo walishamjua ni nani. Watu wengi hususani wale ambao ni binadamu wa kawaida katika ulimwengu wa giza walijawa na machozi katika macho yao na hamasa ya juu mno. Wote macho yao yalikuwa ni katika mlango wa kutokea kwenye juktwaa kwa hamu kubwa ya kumuona huku wakijiandaa kumshangilia.


“Alikuwa na miaka sita pekee alipoletwa na kuingizwa katika kundi la The Odd one. Alithaminiwa sana na mtawala mkuu Mr Black na hatimae kukidhi vigezo na kuwa mwanafunzi wa Black Emperor wa kwanza…Aliweza kupata hadhi ya Selafi akiwa na umri wa miaka kumi na tatu huku akiwa katika daraja la juu sana la mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi. Katika kipindi chake cha mafunzo ya nishati alifanikisha kuishambulia kambi ya kundi la kimauaji la Kichwa cha Faru na kumuua kiongozi wao. Alipofikisha umri wa miaka kumi na sita alivunja rekodi ya ufanisi mkubwa wa kuua na wingi wa watu aliowaua katika vita. Katika umri wa miaka kumi na saba alivunja rekodi ya kuwa Bounty Hunter aliefanikisha kuwinda watu wengi duniani na kuwapata. Watu wengi walimuona kama mwiba katika harakati zao na kumtegea kila aina ya njama lakini hawakuweza kumzuia. Baada ya kutimiza miaka kumi na nane aliachana na Uanajeshi pamoja na uninja na katika hali isiotegemewa akavunja tena rekodi ya kuokoa raia wengi katika maeneo ya vita . Mwaka huo huo kwa ajili ya kupata uhuru wake alimuua Gabriel, Mkuu wa Mahakama takatifu na kuamua kujitegemea kutoka kwa Mtawala wake.


Ndani ya mwaka mmoja na nusu wa kujitegemea aliweza kukusanya wafuasi na kuingia katika vita kali na mahakama takatifu. Mapigano yalikuwa makali na yaliosambaa dunia nzima ya ukubwa tofauti tofauti bila ya kushindwa. Mwaka mmoja baadae Mahakama ya Baraza la giza wakaamua kumuunga mkono na kulazimisha watu wa Holy Court kukimbia. Kwa nguvu zake aliweza kufufua makundi ya Baffodil na Barhams na kuzima makundi mengi ya daraja A na B ili kukuza hadhi ya makundi yake….”


Wakati wote mshereheshaji akiwa anaongea , Azzle , Asmuntis , Mameni, Berly, Leviathani na wengine waliokuwa wamekaa katika siti chini ya jukwaa pamoja na wanachama wa Barhams, Baffodil na Seas Demons, macho yao yaligeuka na kuwa mekundu kwa furaha kubwa.


Upande wa Regina ambae alikuwa akifuatilia tukio hilo kwa ukaribu kabisa alijikuta akitetemeka kwa sifa hizo. Ijapokuwa hakujua zaidi ya maneno yaliokuwa yakiongelezwa yalikuwa yakimaanisha nini . lakini maelezo hayo yalitosha kumuonyesha huyo Gwiji mwenye sifa hizo alikuwa ni hatari kiasi gani.


Alijikuta akiwa na shauku na kutaka kumjua ni Gwiji gani mwenye sifa nyingi namna hio.


Upande wa jukwaa, Mika, Silvia na wengine walikuwa na mwonekano usioelezeka katika nyuso zao. Wanachama wa mahakama takatifu na watawala wa zama zile walionekana kutofurahia . Lakini walijua hata kama MC asingetaja sifa hizo watu walikuwa wakizijua.


Mshindi ni mfalme na alieshindwa ni mhalifu, hio ndio ilikuwa sheria ya ulimwengu wa siri bila kujalisha ulikuwa ukipigania nini. Mwenye nguvu ndio mwenye haki ya kuongea. Hivyo kwa watu wenye madaraka makubwa kama hao waliishia kuinamisha vichwa vyao chini huku wakijiambia kushindwa kwao ni kwa muda mfupi tu, kisasi kinakuja.


“Katika miaka miwili yeye na wafuasi wake walitembea sehemu mbalimbali ulimwenguni na kuwakomboa watu walionyimwa haki na uhuru wao wa kuishi. Aliharibu mashirika mengi ya giza na kupandisha mengi, Ari yake ya kutokukubali kujisalimisha imewapa watu wengi motisha ya kupambania haki zao na kuathiri mpangilio mzima wa utendaji wa ulimwengu wa giza. Vita hii iliodumu kwa miaka miwili imebatizwa jina la Vita takatifu ya ukombozi na kufanya watu wengi kumkubali lakini yeye mwenyewe anajihisi ni mtu aliwaasi binadamu na anapostahili ni kuzimu pekee na kupitia msimamo huo,Nuru ilimpotea katika uso wake na Giza likamwangukia na kumfanya adondokee kuzimu na hatimae jamii ya watu kumi na mbili wenye dhambi zisizosameheka ikazaliwa. Jamii ya watu wa Karibu Kuzimu ya daraja S ikazaliwa na kubatizwa jina la INFERNO. Nichukue nafasi hii kumkaribisha kwenu. Lucifer, kiongozi wa Karibu Kuzimu(Inferno) ambae amerudi tena. Anaefahamika kwa jina lake maarufu na la siri,Devin-rth” endelea hapa - SEHEMU YA 203
 
Back
Top Bottom