Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

Inayofuata alisema weekend ambayo ndio Leo na kesho, but hakutaja weekend ya wiki gani
 
Singano jr sawa kama umeamua hivyo tutakuwa ni wenye kusubiri nadhani unatuona
 
SHETANI RUDISHA AKILI ZETU



MTUNZI:SINGANOJR



SEHEMU YA 50

Kitendo cha Chekani kuletewa Yonesi kupigana nae aliona ni kama dharau.

“Kwahio mnadhani nimejifunza sanaa ya mapigano kwajili ya kushindana na kila mtu hata kama hana vigezo?”

“Acha visingizio , tutaongea hili baada ya kuweza kunishinda”Aliongea Yonesi akiwa ameshakaa pozi la kupigana.

Kechani aliishia kutingisha kichwa na kuingia ndani ya ulingo huku akipiga hatua moja kumsogelea Yonesi , wakati huo kidole chake gumba kilinyooka na kisha kikajikunja huku vile vinne , viwili vilitokezea kwa mbele huku viwili vikisambaa na kufanya mkono wale uonekane kama vile ni mguu wa Mwewe.

Baada ya kuona mbwebewe za adui yake, Yonesi hakutaka kuchelewa na alianzisha mashambulizi kwa kumrushia ngumi Chekani akimlenga kifuani, lakini mara bada ya kurusha ngumi ile Chekani alisogeza mkono wake wa kushoto uliokuwa katika umbo la kucha za tai akinuia kuikamata ile ngumi , lakini upande wa Yonesi aliinama kwa mbele na kisha kunyanyua mguu kwa mzunguko , alionekana kumzubaisha adui yake kwa kumuonyesha anataka kumpiga ngumi lakini shambulio halisi alikuwa amepanga litokee katika mguu wake.

“Bamm!!

Chekani alijikuta akishituka na alijitahidi kwa uwezo wake wote kuzia shambulizi lile.

Upande wa Yonesi mara baada ya kufyatua mguu na kwenda hewani alipiga sarakasi na kwenda kusimama tena lakini hakuzubaa alirudi na teke staili ya roundhouse ambayo ilimpiga Chekani mgongoni na kumfanya kujikota kwenda mbele.

Tukio lile la Yonesi kufanikiwa kumpiga Chekani lilimfanya Mzee Konki na wenzake kushangazwa mno , maana ni kitu ambacho hawakuwa wametegemea kabisa.

Chekani alijikuta akigusa eneo alilopokea shambulizi na uso wake ulizidi kujaa usiriasi , ni kama ile dharau aliokuwa nayo juu ya Yonesi ilipotea.

“Mbona unashangaa , unadhani kujua kwako sanaa za kimapiugano zilizopitwa na wakati unaweza kunipiga kirahisi?”AliongeaYonesi.

“Safiii,,, nimekudharau ndio maana , hebu angalia hii kwanza”Aliongea Chekani kwa kingereza na palepale alisogea kwa haraka kwa staili flani kama vile ni Sungura anaekimbia na kisha kumrukia Yonesi huku kucha zake zilikuwa zimeleekezewa upande wa kiganja cha mkono cha Yonesi.

Lakini Yonesi hakuwa na mpango wa kumshambulia na mara baada ya Chekani kumfikia alimkwepa kwa kuinama huku akiweka mikono yake nyuma kujisapoti vizuri na kisha palepale alifyatua mguu wake kumlenga Chekani usoni.

Chekani kwa wepesi aliweza kukwepa shambulizi lile , alijua fika kama litampata usoni basi litategua taya lake.

Yonesi mara baada ya kuona amezimisha shambulizi la adui yake palepale hakutaka kuchelewa na aliannzisha shambulizi lingine la teke la mzinguko na kumfanya Chekani kuweka mikono yake kifuani kwa ajili ya kupangua teke lile.

Yonesi hakuonekana mzembe, stamina yake ya kurusha mateke pamoja na nguvu ya miguu ilionyesha ni kwa kiasi gani alikuwa na mazoezi makali na ujuzi wa kimapigano.

Upande wa Chekani ni kama alikuwa akisoma mashambulizi ya Yonesi kwa kujilinda asipatwe na pigo lingine.

Hamza mara baada ya kuona tukio lile aliona kabisa mambo hayo hakutagemea yangetoka kwa Yonesi, alimuona ameimarika mno.

Ijapokuwa mbinu ya Kucha za tai ilikuwa na nguvu zaidi katika mbinu ya mapigano ya ana kwa ana katika ulingo lakini bado Yonesi aliweza kuonyesha wepesi zaidi, lakini hata hivyo Hamza aliona kabisa mbinu ya Yonesi katika kupambana na mtaalamu kama Chekani hawezi kumzidi zaidi ya kujichosha, isitoshe Chekani alionekana kuwa mzoefu zaidi ya Mzee Konki.

Kitendo cha Yonesi kupambana mara ya kwanza na Mzee Konki ni kama ilimpa nafasi ya kwenda kufanya utafiti ya udhaifu wa mbinu ya kucha za Tai ndio maana alitumia nguvu ya miguu zaidi kushambulia maeneo ambayo yataifanya mbinu hio ya kimapigano kukosa nguvu.

Kwa wasiomjua Yonesi wanaweza kumuona ni msichana wa kawaida lakini ni mwanamke ambae ameanza jeshi akiwa na umri mdogo na alikuwa katika kitengo cha makomandoo na likija swala la mapigano alikuwa na uzoefu pengine zaidi ya Chekani.

Walinzi wa kampuni ya Dosam walijikuta wakifurahi mara baada ya kuona Chekani alikuwa akishindwa kumshambulia Yonesi.

Lakini upande wa Hamza aliona sio muda wa kushangilia bado ni ngumu sana kwa Chekani kushindwa bila ya kushambulia kisawa sawa la sivyo Mzee Konki asingemsafirisha kutoka Thailland mpaka Tanzania.

Sasa upande wa Chekani alionekana kushindwa kuvumilia zaidi na alianza kuonyesha uwezo wake wote.

Ghafla tu alipiga kelele kama vile ni chui na misuli ya mwili wake ilianza kutuna na akawa mgumu kama chuma.

Miondoko ya miguu yake ilibadilika ghafla na kuanza kucheza kwa kasi mno , licha Hamza kuwa mita kadhaa mbali lakini aliweza kuhisi kuna kitu kimebadilika kuhusu Chekani.



“Inner force!!!”

Yonesi alijikuta akipagwa , mwanzoni alijua ataweza kumdhibiti Chekani kwa kumshambulia kwa haraka haraka lakini hakutegemea Chekani amejifunza mbinu ya ajabu kuamsha nguvu kutoka ndani ya mwili.

Yonesi palepale alijikuta akikumbuka mafunzo ya mkufunzi wake wakati akiwa nchini China chini ya usimamizi wa serikali.

“Wanajeshi wanatofautiana katika madaraja mengi , mnaweza kuwa na mafunzo sawa na kutii kila maelekezo mnayopatiwa lakini haimaanishi kama wewe unaweza kuwa mwanajeshi bora , kwasababu mafunzo haya haya hata adui yako anaweza kufunzwa na akayamudu kwa asilimia kubwa, kinachomtofautisha mwanajeshi na mwanajeshi licha ya kuwa na uwezo sawa ni namna ambavyo anauwezo wa kuvuna nguvu za asili ambazo zimejificha katika mwili wake , mwingine ataweza kuwa imara kwa kuweza kuamsha uwezo wake wa kumuotea adui , mwingine anaweza kuamsha uwezo wake wa asili kutokana na namna ubongo wake unavyofanya kazi kwa haraka , katika mbinu hizi zote ni wanajeshi wachache sana ambao wamefanikiwa kujifunza mbinu ya kuamsha nguvu yao ya ndani , ukifanikiwa kutumia viungo vyako vya ndani kama chanzo cha nguvu zako za mikono na miguu basi utahesabika kuwa mwanajeshi mwenye nguvu sana katika sanaa ya mapigano, Nguvu ya ndani ni kama chanzo cha umeme wakati wa kupigana, mbinu hii inakuwa bora kwasababu msingi wake ni kuzungusha nishati ya mwili katika kila kiungo cha mwili na kufanya uwezo wako wa kufanya maamuzi kuwa mkubwa sana na spidi yako ya kivitendo kuongezeka , unaweza kupata majeraha ya nje ambayo kiuhalisia huwezi kuendelea kupigana lakini ukafanikiwa kushindana nae”Yonesi alikuwa akikumbuka mafunzo hayo vyema alikumbuka na mkufunzi wao aliwapa mfano wa mtu ambae hana uwezo wowote wa kuruka ukuta na mara hatari ikawa mbele yake na kutokana na njia pekee ya kujiokoa ni kuruka ukuta akafanikiwa kruuka ule ukuta licha ya kwamba ukimrudisha akiwa katika hali ya kawaida ukimwambia aruke hata ajitahidi vipi hatoweza kabisa , huo ndio mfano wa nguvu ya ndani iliojificha.

Upande wa Hamza aliona ni sahihi kabisa na ukweli ni kwamba hakushangaa kumuona Chekani kuwa na uwezo wa kuamsha nguvu yake ya ndani , kama ndio makamu wa Shirka yote ya Mwewe mweusi lazima awe na kitu kinachomtofautisha na wenzake wote na ndio mbinu hio ya ndani.

Kwa lugha nyepesi nguvu ya ndani ni uwezo ambao binadamua anakuwa nao lakini umejificha na uwezo huu hudhihirika mara moja moja wakati mtu akiwa katika hatari , sasa kuna mafunzo maalumu ambayo hufanyika ili kuweza kuuamsha huu uwezo muda wowote unaotaka hata kama haupo kwenye hatari.

“Mwanamke mjinga sana wewe , kwasababu unaonekana kupenda sana kupiga mateke ninakwenda kukuvunja miguu yako”Aliongea Chekani ambae alimwangalia Yonesi kama kiumbe cha hatari.

Alikuwa amekasirika mno , aliona ni dharau kwake kuona mwanajeshi kama yeye anweza kupigwa mateke na mwanamke mara nyingi kiasi hicho.

Muda huo hasira zilikuwa zimemvaa na hakujali ni nguvu kiasi gani atatumia kumshambulia Yonesi lakini mpango wake ni kumvunja vunja na kidole kimoja tu cha Tai.

Ilikuwa ni kwa uwezo mkubwa Chekani alikuwa ashamfikia Yonesi na kutokana na kujua kabisa Chekani sio saizi yake tena Yonesi alijikuta akirudi nyuma na kusababisha mpaka kiatu kumtoka mguuni lakini Chekani alimshika bega la mkono wa kulia kwa spidi kubwa ambayo ilikuwa ngumu kwa Yonesi kumkwepa, kitu cha pakee alichoweza kufanya ni kusogea kidogo ili kuepuka kuguswa maeneo ambayo yanaweza kumsababishi kifo.

“Arhhhhhhhhhhhh..!!”

Yonesi alijikuta akipiga yowe la maumivu, eneo la bega nguo yake ilichanika palepale huku matobo ya midole ya Chekani ikionekana

“Yonesi!!!”

Regina alijikuta akishindwa kujiuzia na kuomba waache kupigana mara moja.

Hamza hata yeye aliona hana muda wa kupoteza kwani Yonesi anaweza kufanywa kiwete na aliruka na kuingia kwenye ulingo mara moja, hakujali swala hilo litamfanya Yonesi kujihisi mnyonge au nini.

“Mtu uliemfuata kupigana nae ni mimi”Aliongea Hamza.

“Subiri kwanza!!”

Yonesi aliongea huku akionekana kuvumilia maumivu eneo la bega lake na alitembea mpaka mbele ya Hamza.

“Bado sijashindwa”Aliiongea Yonesi kibabe huku aking’ata meno kwa nguvu , kitendo cha ukiburi na hasira alizokuwa nazo Yonesi na hali ya kutokata tamaa ilimfanya Hamza kumkubali kutoka ndani ya moyo wake, aliona ni wanawake wachache sana ambao wanaweza kuwa kama Yonesi.

“Kapteni nadhani mwili wako ni muhimu zaidi”Aliongea Hamza , alijua hata kama Yonesi ana nia ya namna gani ya kupigana na Chekani haiwezi kutosha kushinda.

“Unanidharau sio?”

“Sijamaanisha hivyo”

“Yonesi nakuagiza mara moja acha na uende ukatibiwe”Aliongea Regina kibabe lakini licha ya hivyo Yonesi bado hakutaka kukubali na aligeuka na kumwangalia Chekani.

“Ukiendelea kushindana na mini nitahakikisha unabakia uchi kwa kuchana chana nguo zako zote , bado tu unataka kuendelea?”Aliongea Chekani kwa dharau.

Yonesi alishindwa kusema lolote huku jasho jingi likimtoka kiasi cha kudondoka chini, aliishia kukunja ngumi yake kwa nguvu huku mwili wake ukianza kumtetemeka na kitendo kile kilimfanya Hamza kuhisi nguvu kubwa ambayo inamtoka Yonesi , ilikuwa ni kubwa mno kuliko hata ya Chekani.

Sasa muda ule Hamza aliona pengine amemdhania vibaya Yonesi na kuna uwezo ambao ameuficha alijikuta akishangazwa na kilichotokea. Yonesi alijikuta akitapika damu na dakika ileile mwili wake ulilegea na alidongoka chini.

“Yonesi!”

“Kaptenni!”

Kila mtu ambae alikuwa akimjua Yonesi alijikuta akipiga kelele za kuogopa maana ilikuwa ni damu nyingi aliotapika.

Hamza dakika ileile alichuchumaa na kushika mkono wa Yonesi ili kupima mzunguko wake wa damu.

“Huyu mwanamke ni mkurupukaji sana , angalia sasa alichojisababishia”Aliwaza Hamza

"Hahaha.,.. ndio umeamua kujitapisha damu , kama umekubali kushindwa sema acha maigizo”Aliongea Chekani lakini Hamza alipotezea kauli yake.

“Mkurugenzi nampeleka Yonesi hospitalini”Aliongea Hamza mara baada ya kuona akichelewa kidogo tu Yonesi anaweza kupatwa na shida kubwa.

Regina alitaka kuita gari ya wagonjwa lakini aliona itakuwa rahisi zaidi kama Hamza atamuwahisha kwa gari.

Hamza muda uleule alimpakata Yonesi na kuanza kuondoka na kitendo kile kilimfanya Chekani kukasirika.

“Wewe mwanaharamu nani kasema unaweza kuondoka , isije ukawa unadharau uwezo wangu?”

Mzee Konki pia hakutaka Hamza kuondoka kabla ya pambano hivyo wale watu aliokuja nao walimzuia kwa mbele.

“Muweke huyo mwanamke chini na uonje kipigo cha mkuu wetu”Aliongea.

“Unataka kufa?”Aliuliza Hamza akiwa amemgeukia Chekani.

“Wewe ndio unakimbia halafu unaniuliza nataka kufa?”

“Kupigana na wewe sihitaji hata kutumia mikono yangu”Aliongea Hamza kwa hasira

“Unaongea sana , kama unajiamini njoo ujaribu nikuonjeshe nini maana ya nguvu ya ndani yenye muunganiko na kucha za Tai”Aliongea Chekani huku akiwa na hasira zaidi mara baada ya kuona ni kama anadharauliwa na Hamza na alitooka alipokuwa amesimama na kumsogelea Hamza kwa nguvu akidhamiria kumshambulia.

“Hamza kuwa makini”Aliongea Regina mara baada ya kuona kitendo kile cha Chekani kutaka kumshambulia Hamza.

Kwasababu Hamza alikuwa amempakata Yonesi hakuna aliejua kama ataweza kufanya chochote.

Kutokana na spidi aliokuwa nayo Chekani aliweza kumfikia Hamza na kilichosikika ni sehemu ya nguo mgongoni kuchanika lakini ilikuwa ni mchanikoo huo mdogo tu , lwani wakati kila mmoja akijua Hamza anakwenda kuumizwa na shambulizi lile upande wake Hamza alikuwa amesimama katika eneo moja bila ya kusogea huku akimwangalia Chekanni kwa macho yaliojaa ukauzu.

Macho ya Hamza yalikuwa ya hatari kama vile ni ya mnyama Chui.

Chekani alijikuta akiwa mjinga mbele ya Hamza , shambulizi lake ambalo alimfanyia Hamza aliliunganisha na nguvu yake yote ya ndani lakini ajabu hakumletea madhara yoyote Hamza hata kumsukuma tu.

Kwa jinsi Hamza alivyokuwa amesimama ni kama vile hakuwa amemshambulia kabisa.

“Hili limeweekana vipi..”

Muda huo Hamza aligeuka na kuinua nguu wake wa kulia na kumpiga Chekani teke kwenye paja lake la mguu wa kushoto kama vile anapiga mpira.

“Crack!!!”

Watu walichoweza kusikia ni kama mshindo wa kitu kudondoka , upande wa Chekani hakuwa hata na muda wa kukwepa teke lile na alichoweza kusikia ni mvunjiko wa ndani kwa ndani wa mfupa wa paja lake.

“Arghhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh!!!, Mguu wanguuuuu!”

Lilikuwa teke la kawaida tu lakini kwa Chekani ni kama paja ake limepigwa na bomu.

Aliishia kupiga magoti na mkuu mmoja huku machozi ya maumivu yakimtoka na ilionekana anaweza kuzimia , ukulele wake ulifanwa watu wote waliokuwa wakiangalia ikiwemo Regina kushikwa na butwaa.

Chekani ambae alionekana mbabe dakika chache zilizopita na kumfanya Yonesi kutapika damu alikuwa ameshikishwa ardhi na kupiga mayowe kwa teke moja tu kutoka kwa Hamza.

Hamza alijifanya ni kama hakuna kilichotokea na hakurudia hata kumwangalia aligeuka na kisha akiwa amempakata Yonesi aliondoka, Mzee Konki na wale watu wake aliokuja nao walimpisha njia huku wakimwangalia kwa maswali mengi , kama isingekuwa eneo hilo ni la kazi Hamza alijiambia angewageuza viwete kila mmoja.

Mzee Konki alikuwa katika majuto , kama angejua hilo litatokea asingemsafirisha mtoto wa mkuu wake kuja nchini Tanzania , hakujua Shirka yao itaonekana vipi kwa mtu ambae ametumia maisha yake kufunzwa kupigana kushindwa kwa pigo moja tu , ki ufupi aliona ni fedheha kwa wakufunzi wake.

Regina aliishia kumwangalia Hamza akiondoka na Yonesi bila kuongea neno loloe lakini wakati huo kichwa chake hakikuwa sawa kwa kile alichokuwa akiwaza.

Hamza mara baada ya kumwingiza Yonesi kwenye gari alimpeleka moja kwa moja moja katika hospitali binafsi iliokuwa mita kadhaa kutoka yalipo makao makuu ya kampuni yao.

Mara baada ya kumtambulisha Yonesi kama mfanyakazi wa Dosam haraka sana alipokelewa na kuanza kufanyiwa tiba ya kiuchunguzi.

Baada ya vipimo kutoka ilionekana Yonesi hakuwa ameumia sana na ni kwamba alikuwa katika hali ya uchomvu sana

Hamza mara baada ya kupewa majibu hayo moja kwa moja alimpeleka Yonesi mpaka wodini na baada ya hapo alimtaarifu Regina hali ya Yonesi.

“Vipi Yonesi anaendeleaje , imeonekana hajaumia?, kwanini ametapika damu?”Aliuliza Regina akiwa na shauku mara baada ya Hamza kumwambia kuwa hakuwa na shida kubwa , lakini upande wa Regina hakukubali maana aliona kabisa Yonesi akitapika damu.




“Yonesi alipata majeraha ya viungo vya ndani lakini kwa vifaa vya kawaida haviwezi kuona hili tatizo , wanachoweza kuona ni uchomvu tu, ki ufupi ni kwamba damu aliotema ilivuja kidogo tu na kuacha na ndio aliitapika yote”

“Kwahio unamaanisha ni kitu cha kweli hicho kinachoitwa inner force?”Aliuliza Regina na kumfanya Hamza kufikiria huku akijiambia kitendo cha Yonesi kutema damu sio kutokana na shambulio la Chekani bali alijisababishia mwenyewe, lakini Hamza hakutaka kuongea sana hivyo alilipotezea swali la Regina , isitoshe hata yeye alikuwa na maswali kwa Yonesi imekuwaje akajitapisha damu.

“Kwanza nini kinaendelea huko kwenye kampuni?”Aliuliza Hamza.

“Umemvunja yule mbaba wa watu mguu unadhani wangeendelea kukaa?, halafu familia ya James imepiga simu na kusema kwamba hawahusiki na Mzee Konk tena na alichokifanya ni kisasi chake mwenyewe”Aliongea Regina.

“Wamekupigia simu na kuongea hivyo?”

“Ndio walivyosema hawahusiki na ni maamuzi ya Mzee Konki pekee”Aliongea Regina na kumfanya Hamza kuhisi kuna kitu hakipo sawa lakini hata hivyo hakutaka kuuliza zaidi.

“Hebbu tuachane na hayo kwasasa , kwasababu wamekupigia na kusema hawahusiki nadhani hawatoleta matatizo ndani ya kampuni tena”

“Sawa , huna haja ya kuja kazini unaweza kuendelea kukaa hospitalini mpaka hali ya Yonesi ikiwa sawa”Aliongea Regina na Hamza alikubali.

******

Upande mwingine alionekana James akiwa nyumbani kwao sebuleni mbele yake kulikuwa na mwanaume alievalia suruali ya Jeans na tishirt iliombana mikono , alikuwa na miwani ya juu alioitundika kwenye kifua chake huku mkononi akiwa ameshikilia sigara.

“Nadhani kwa staili hii itakuwa ni rahisi kudili na Regina , ataona kabisa kumwambia hatuhusiki na swala la Mzee Konki lazima ataanza kuishi bila tahadhari na ndio itakuwa rahisi kumuua”Aliongea yule bwana huku akitoa moshi.

“Unadhani ni sawa kumuua sasa hivi , nazungumzia ushirikiano wa baba yako zidi ya mgombea wa uraisi?”Aliuliza yule bwana.

“Kuhusu hili baba pia alinipa msisitizo , lakini tusipomuua sasa hivi na Hamza wake tutajikuta tunachelewa”

“Ninachomaanisha kumuua kwa staili ya wazi wazi kama hivi , kwa mfano leo imeonekana Mzee Konki akiingia ndani ya kampuni ya Dosam na kuleta vurugu kama ikitokea Regina akikumbwa na kitu kikubwa zaidi basi moja kwa moja tukio hili litaunganishwa na familia yenu , isitoshe ndio wanufaika wakubwa”Aliongea Yule bwana.

“Kwahio Gonji unamaanisha kipi kifanyike?,”

“Kuna njia nyingi za kumuua mtu bila ya kifo chake kuonekana cha kupangwa”Aliiongea na kumfanya James macho kuchanua.

“Unadhani inaweza kuwa rahisi , MzeeKonki na kundi lake wameenda kumshambulia Hamza lakini wameambulia maumivu , hawa vijana wako ambao unawasifia unadhani wanaweza kuwa na uwezo wa juu kumzidi Hamza?”

“Kama nilivyosema kuna njia nyingi za kumuua mtu lakini njia hizo sio lazima ziwe kupigana ana kwa ana , kama huwezi kumuua mtu kwa kushindana nae ulingoni basi unatumia mtego, mfano kusababisha ajali , kutega bomu katika gari yake na kadhalika”Aliongea Gonji na kumfanya James sasa kuelewa.

“Hapo kwenye ajali nakubaliana na wewe lakini vipi kuhusu bomu , sio rahisi kupata bomu”

“Hilo lisikupe shida , kwasasa vigogo wengi wanahitaji kuona Hamza akifariki kutokana na kuzuia mipango yao, ni rahisi kushawishi makomandoo kutupa siraha yoyote ile”

“Kama hili unadhani linawezekana basi naliacha katika mikono yako , lakini nikukumbushe linapaswa kufanyika kwa haraka maana hatuna muda wa kupoteza”Aliongea James na kumfanya Gonji kutoa tabasamu.

“Ili mradi malipo ni ya kueleweka nitahakikisha wiki mbili hazipiti unaipata taarinfa nzuri”Aliongea kwa kujiamini huku akizima ile sigara kwa kuiminya katika kisahani cha majivu.

********

Yonesi alijikuta akifumbua macho yake taratibu na kitu cha kwanza alichoweza kuhisia ni radha ya damu iliokuwa kwenye midomo yake.

Baada ya akili kumkaa sawa ndio sasa aliweza kujua alikuwa hospitalini katika wodi na hio ni mara baada ya kupatwa na harufu ya dawa za kuzuia maambukizi ya vinyemelea.

“Fyaaaa…Fyaaa…sio mbaya , sio mbaya hii juisi ni tamu”

Ilikuwa ni sauti ya mwanaume iliomfanya kugeuza shingo yake na aliweza kumuona Hamza akifyonza juisi kwa kutumia mrija na kufanya chupa ile itoe sauti kwa ndani ikionyesha imeishiwa na juisi na anavuta hewa.

Hamza alikuwa amemaliza chakula chote ambacho kililetwa kwa ajili ya mgonjwa na muda huo alikuwa akimalizia juisi.

Upande wa Yonesi ilikuwa mara ya kwanza kuona mtu akifurahia chakula namna hio mpaka kujilamba midomo akiwa katika mazingira ya hospitalini.

“Ah! Kapteni umeamka sasa?”Aliuliza Hamza mara baada ya kumuona Yonesi anamwangalia.

“Kwanini upo hapa?”

“Mkurugenzi kaniambia nibaki na wewe , kazi yangu leo ni kukaa na wewe na kukuhudumia kwa kila unachotaka”

“Mkurugenzi… nini kiliendelea kwenye kampuni?”

“Yashaisha yale , wale watu wote wamekwisha ondoka”Aliongea Hamza na kumfanya Yonesi kuvuta pumzi ya ahueni.,

“Vipi ulifanikiwa kumshinda yule Kechani?”Aliuliza na kumfanya Hamza kutingisha kichwa huku akicheka.

“Unacheka nini sasa , kama unasema sema tu, usinidharau ukidhani mimi dhaifu kiasi hicho”

“Lakini sijasema nakudharau”

“Lazima utakuwa unajiambia kwenye moyo wako nina kiburi na sijui kukubali kushindwa na najikweza sana hata kwa watu ambao sina uwezo wa kupambana nao na mwisho wa siku nikaishia kujiumiza mwenyewe”Aiongea Yonesi kwa sauti ya kulalamika na kumshangaza kiasi Hamza.

“Kapteni nikupe maji kidogo?”

“Sitaki maji , unaweza kwenda huna haja ya kunisaidia”Aliongea Yonesi huku akijitahidi kusimama lakini alijikuta akigugumia maumivu makali ya tumbo.

“Majeraha uliopata kwa ndani hayajapona bado , hivyo kuwa makini usijilazimishe la sivyo utajiumiza zaidi”

“Sihitaji ushauri wako”Aliongea Yonesi huku akionyesha hasira waziwazi.

“Sikia Yonesi sio kwamba nakudharau , unaweza kuniamini au usiniamini hio ni juu yako lakini ukweli sijawahi kudharau uwezo wako”

“Huna haja ya kunifariji kwa kujitia upole”

“Ninachomaanisha sio kwamba huna uwezo wa kupigana na yyule Kechani , kama umeweza hadi kufanya utafiti wa namna ya kudili na mbinu za Kucha za tai basi unaonyesha ni kwa kiasi gani una juhudi ya kujifunza na kuhusu hili nimekukubali na kama ni ushindi pale ulishinda , kosa lako ni kwamba hukujua mwenzako ana mafunzo ya kuamsha nguvu za ndani hivyo ni halali kukuzidi”Aliongea Hamza na maneno yale kidogo yalionesha kumlainisha Yonesi.

“Ndio uivyoona pia?”

“Kapteni kwanini nikudanganye , umeonyesha ni kiasi gani una nia ya kutimiza wajibu wako , nadhani kupitia hili Mkurugenzi anapaswa kukuongeea mshahara”Aliongea na kumfanya Yonesi bado kutoyaamini maneno ya Hamza.

“Unaongea maneno ya kijinga ili kunifariji tu ila ndani kwa ndani utakuwa unachekelea”Aliongea lakini Hamza alipotezea alijua asingeweza kushinda mbele ya ukiburi wa Yonesi.

“Vipi una njaa?, Dokta amesema unapaswa kula vyakula vya ujiuji kwa siku tatu , ngoja nikuagizie uji”

“Sina nja… “Kabla hata hajamaliza sentensi yake tumbo lake lilianza kunguruma kama jenereta.

Muda ulikuwa umeenda tokea aletwe hapo na pia alitoka kwenye pambano kali hivyo ilikuwa ni halali kushikwa na njaa.

Hamza aliishia kutoa tabasamu na alipiga simu uji uletwe mpaka kwenye wodi yao , Hospitali hio ilikuwa ni binafsi na ilikuwa na huduma ya mgonjwa kuagiza chakula kabisa na kuletewa kutoka jikoni.

Dakika chache mbele uji uliletwa na Hamza aliumimina kwenye bakuli na kuchukua kijiko kwa ajili ya kumlisha Yonesi , lakini alikataa.

“Nina mikono nitakunywa mwenyewe”Aliongea na Hamza hakutaka kulazimisha na kumpatia Yonesi lile bakuli.

Muda huo Yonesi aliweza kugundua sasa mavazi yake yote mwililini yalikuwa yamebadilishwa na amevaa mavazi maalumu ya hospitalini.

“Nguo zangu ziko wapi?”.

*******

Saa nane za mchana alionekana Frida akiingia ndani ya majengo ya taasisi ya Haliz, mwendo wake siku hio ulionekana kuwa ni ule wa kujiamini zaidi kuliko siku nyingine zote.

Baadhi ya wafanyakazi aliopishana nao baadhi yao walimkaribisha kazini kwa mara nyingine huku wengine wakimpa ishara ya salamu tu ambapo Frida alizipokea kwa kutabasamu.

Mara baada ya kuzikaribia Lift alibonyeza kitufe na dakika chache Lift ilifunguka na akaingia ndani na alibonyeza kitufe cha floor ya 24 juu kabisa ya jengo hilo.

Na ilimchukua dakika tu lift ilimfikisha katika floor ya uongozi wa taasisi hio na alitembea kwa kujiamini katika Koridio hio huku akipokewa na marashi mazuri yaliotokana na AC.

“Naima nipo hapa kwa ajili ya kuonana na Mkurugenzi”Aliongea Frida mara baada ya kufika katika dawati la mapokezi na kukutana na mwanadada alievalia sare za rangi ya bluu iliokolea pamoja na Hijab huku akiwa na tabasamu.

“Karibu sana Dokta , Mkurugenzi anakusubiri”Aliongea yule mwanadada kwa tabasamu kwa kingereza na Frida alimrudishia tabasamu la ukarimu na kupiga hatua kuingia katika ofisi ya Mkurugenzi.

Frida hakusumbuka hata kugonga kutokana na kuona taarifa za ujio wake zishamfikia bosi wake , hivyo aligonga kidogo na kisha akasukuma mlango na kuingia ndani.

“Karibu tena kazini Dokta Frida”

Sauti ya mwanamama iliweza kusikika na kumfanya Frida kutoa tabasamu huku akimwangalia mwanamke ambae amevalia Hijab.

Alikuwa ni Dokta Maya Thema na ndio mkurugenzi mkuu wa taasisi ya maswala ya fahamu ya Haliz Foundation.

“Asante sana Dokta Maya”Alijibu Frida na Sister yule alitoka katika meza yake ya kufanyia kazi na kuja kuketi katika masofa.

Ilikuwa ni ofisi kubwa mno , ilikuwa na kila sifa ya kuitwa Ofisi ya Mkurugenzi mkuu wa taasisi hio kubwa , licha ya kwamba vitu vingi vilionekana kawaida lakini kwa macho ya tathimini lazima ujue samani na mapambo ni ya bei ghali , ki ufupi kila kitu kiliendana na hadhi ya mtu wa dini.

“Inaonekana taarifa za kurudi kwangu zimefika mapema kuliko nilivyotarajia”Aliongea Frida akiwa na tabasamu.

“Ndio, Frida wewe ni mwanasayansi mkubwa sana ndani ya taasis ya Haliz na viongozi wanajua hilo , licha ya kwamba nimekutangulia ki uzoefu lakini umenizidi vitu vingi, Askofu alinipigia simu juu ya kurudi kwako tena , Karibu sana”

“Unaonekana kuwa na furaha sana juu ya ujio wangu pia Professor , licha ya kujua kilichotokea”Aliongea na kumfanya Sister kutabasamu na alisimama kutoka kwenye sofa na kumimina maji kwenye glasi kutoka kwenye Dispenser

“Utapendelea maji?”Aliuliza.

“Asante sister , ila sina kitu”Aliongea na kumfanya Sister Maya kutingisha kichwa na kurudi kwenye sofa na kukaa.

“ Faiths!, to me all faiths are admonitions that there is something we cannot understand , something to which we are accountable. It doesn’t matter what we believe personally , as long as there is sometting that we cannot understand about someone’s faith , then we have no reason to judge”Aliongea Sister akimaanisha kwamba hatuna uwezo wa kumhukumu mtu kutokana na dini yake kwasababu katika hio imani mtu anayokuwa nayo lazima kuna kitu ambacho mtu mwingine huwezi kuelewa.

Kauli ile ilimfanya Frida kutoa tabasamu hafifu akionekana kukubaliana na Profesa wake.

“Frida unajua sababu kubwa ya kuanzishwa kwa kanisa la Wasinagogi?”Aliuliza na kumfanya Nadia kutingisha kichwa kwamba haelewi.

“Mwasisi wa kanisa la Sinagogu alikuwa ni muumini mkubwa kutoka kanisa kuu mpaka siku ambayo Dokta Genesha alitoka hadharani na kusema kwamba ana uwezo wa kuthibitisha uwepo wa nguvu ya kiroho kwa kutumia sayansi, mpaka leo hatukujua ni ushahidi gani ambayo Dokta Genesha alimuonyesha mwasisi wetu lakini ni kitu ambacho kilimbadilisha mawazo mno na kugeuka mara moja kutoka Kanisa kuu na kuanza kufikiria kama mtu ambae hajawahi kusoma biblia”

“Kama wanasinagogu hawakuona ushahidi ambao Dokta Genesha aliongelea na mwasisi hakuwaambia kwanini alipata wafuasi , lazima kuna sababu ambayo iliwashawishi wengine kumfuata na kuja kuwa jumuia tishio na yenye ushawishi mkubwa duniani?”



































SEHEMU YA 51.

Sister Maya mara baada ya kuulizwa swali lile alionekana kuwaza kidogo na kisha akamwangalia Frida.

“Hakuna sababu yoyote , wote tunaamini katika siri ambazo hatujaambiwa”Aliongea Sister.

“Siri ambazo hamjaambiwa!, unamaanisha nini kusema hivyo?”

“Ndio, licha ya kwamba umekuwa chini ya Sinagogu kwa muda mrefu lakini je imani yako inakuambia nini kuhusu siri , je unaamini kuna uwezekano wa uwepo wa siri kubwa sana ambayo hujaambiwa katika maisha yako kuhusu ulimwengu ulivyo?”Aliuliza na kumfanya Frida kutingisha kichwa.

“Naamini zipo siri nyingi ambazo sijaambiwa mpaka sasa”

“Hio ndio sababu yetu binafsi , kila mwanasinagogi anaamini katika siri ambazo hajaambiwa na sio ukweli ambao tunaaminishwa, wala sababu ambazo tunapewa ili kuamini”Aliongea na kumfanya Frida kufikiria sentensi yake.

“Kama ni hivyo basi kila mtu anaweza kuwa Mwanasinagogi , siamini katika ulimwengu huu hakuna asieamini uwepo wa siri juu ya vitu mbalimbali”

“Huo sio msingi pekee wa imani yetu , tunachoamini zaidi ni ile siri ambayo tuna malengo nayo, unaweza kuamini kuwepo kwa siri lakini huna juhudi yoyote ya kuzitambua hizo siri basi wewe sio Mwanasigiogi, kwa lugha nyepesi Sinagogi ni jamii ya watu wanaoamini katika kweli ambayo haijasemwa lakini inaonyesha dalili”

“Dalili!, naweza kufahamu zaidi?”Aliuliza Frida kwake ndio mara ya kwanza kufahau kuhusu kauli hio , isitoshe katika jamii ya wanasinagogu kuna madaraja ya uanachama ndio unaweza kujua baadhi ya vitu.

“Kuhusu hili nadhani una majibu tayari , kama sio hivyo usingerudi katika taasisi ya Feliz na usingefanikiwa kumshawishi Askofu Alfonso kukurudisha licha ya kwamba kwake unaonekana mtu hatari”Aliongea Sister na kumfanya Frida kutulia na kuanza kutafakari maneno ya Sister.

“Unamaanisha kuhusu wimbi la watu wenye zaidi ya nafsi moja!!?”Aliongea na kumfanya Sister Maya kutingisha kichwa.

****

Huna haja ya kuwa na wasiwasi , ni nesi ndio kakubadilisha”Aliongea Hamza mara baada ya kuona Yonesi alikuwa na wasiwasi kama yeye ndio amembadilisha.

“Nimeuliza nguo zangu ziko wapi na sio nani kanibadilisha”Aliongea Yonesi huku kidogo akihisi ahueni.

Hamza hakutaka kubishana nae hivyo alimpatia bakuli lile la uji lakini sasa kitendo cha Yonesi kuchota kwenye kijiko na kupeleka mdomoni alijikuta akishindwa baada ya kuhisi maumivu makali ya viungo vya ndani.

“Ngoja nikusaidie acha ubishi unakuwa mjinga sasa kuzidi kujiumiza kwa ujeuri wako”Aliongea Hamza na kumfanya Yonesi kukosa sababu ya kukataa.

Hamza alianza kumlisha Yonesi taratibu lakini kitendo hicho ni kama kimempa nafasi ya kumwangalia zaidi usoni kwa ukaribu zaidi , sasa harufu ya kimwili ya Yonesi pamoja na ya hospitalini ilimfanya pua zake kuburudika.

Kitendo cha Hamza kumlisha akiwa kimya ilimfanya Yonesi kujihisi hali isio ya kawaida.

“Mbona huongei?”

“Kapteni leo Nimegundua ngozi yako ni laini mno bila hata ya kuigusa”Aliongea Hamza.

“Acha kuongea”

“Unatakiwa kuniacha nimalize kwanza kuongea na kisha ndio uniambie ninyamaze”

“Sitaki kusikia ujinga wako”

“Nimekusifia unaita ujinga”

“Haina haja ya kunisifia hivyo kwangu ni ujinga”Aliongea Yonesi lakini mapigo yake ya moyo yalikuwa yakienda kasi mno na kuanza kujiuliza nini kinaendelea kwanini anakosa utulivu mbele ya Hamza.

“Labda ni kwasababu tupo katika chumba kimoja wenyewe”Aliwaza Yonesi akijaribu kujipa sababu.

Upande wa Hamza wakati akiendelea kumlishaYonesi macho yake yalikuwa yamegota katika kifua cha mrembo huyo , ilionekana nesi ambae alimvalisha hakufanya kazi nzuri kiasi kwamba kwa juu kila kitu kilionekana kwa ndani.

Yonesi mara baada ya kumwangalia Hamza usoni aligundua ni wapi alipokuwa akiangalia na alitamani kumpiga lakini kwasababu hakuwa na uwezo huo kutokana na maumivu aliishia kung’ata macho kwa hasira.

“Endelea kuangalia tu kama sijayatoboa hayo macho yako”

“Umenidhania vibaya Kapteni , nilikuwa nikijiuliza nikusaidie kukufunga hicho kifungo vizuri , naona nesi hajafanya kazi nzuri kwenye kukuvalisha”

“Haina shida wewe jua mambo yako tu “Aliongea Yonesi huku akivumilia maumivu na kujiweka vizuri.,

Mara baada ya kushiba Hamza alimsaidia kuegamia kwenye kitanda lakini ni muda ule Yonesi alianza kukunja sura.

“Naomba uniitie nesi”Aliongea.

“Nesi wa nini , kuna shida yoyote?”

“Nenda niitie nesi maswali mengi ya nini?”Aliongea na kumfanya Hamza kutoka nje kwenda kumuita nesi.

“Mgonjwa kuna chochote unachohitaji nikusaidie?”Aliuliza Yule nesi.

“Nataka kwenda bafuni”Aliongea Yonesi na sasa kumfanya Hamza ajue shida ya Yonesi ni nini na kutamani kucheka.

Ilikuwa ni sahihi kuhisi mkojo maana tokea asubuhi alikuwa amelala na muda huo amepewa madawa pamoja na kunywa uji.

Yule nesi alimwangalia Hamza kwa maswali kadhaa , ni kama alimuona Yonesi na Hamza ni wapenzi lakini hata hivyo alikubali.

“Sawa ngoja nikusaidie , shuka taratibu taratibu ukiona unahisi maumivu niambie”Aliongea yule nesi hakuwa mrefu sana alikuwa na mita kama moja na nusu lakini Yonesi alikuwa na zaidi ya mita moja nukta saba.

Yonesi alipiga hatua kuelekea chooni lakini mwili wake wote ulikuwa umemlemea yule Nesi na kuonesha ni kwa namna gani alikuwa akipata shida kwani alianza kutetemeka.

“Arggh,,!”

Yonesi alijikuta akihisi maumivu na kuguna na yule nesi kutokana na kuchoka alijikuta akishindwa kumsaidia zaidi Yonesi na kumuombaHamza amsaidie.

“Kaka itakuwa vizuri ukimsaidia wewe , sina nguvu za kutosha na itakuwa hatari kama nikidondoka”

“Haina shida nitaweza mwenyewe”

“Dada huna haja ya kujilazimisha sana ni hatari kwako , ngoja mpenzi wako akusaidie , mtu yoyote anaweza kuwa mgonjwa na kuhitaji mtu wa kumsaidia , haina haja ya kuona aibu”

Upande wa nesi aliamini kama Hamza sio mpenzi wa Yonesi basi ni mume wake maana ndio amemleta hospitalini na hata chakula ndio amemsaidia kumlisha na amekaa wodini tokea asubuhi.

Yonesi alitamani kumwelezea yule nesi kwamba sio vizuri kwasababu ni jinsia tofauti na hana mahusiano yoyote na Hamza lakini Hamza alikubali haraka.

“Ngoja nitamsaidia mimi”Aliongea Hamza na kumpokea yule nesi na ni kama alipata nafuu , alionekana kuwa bize hivyo aliondoka mara moja.

“Kapteni usiwe na wasiwasi naahidi sitokuchungulia kabisa “Aliongea Hamza akiwa siriasi.

Yonesi kwasababu mkojo ulikuwa umembana sana hakutaka kujizuia tena hivyo alikubali kusaidiwa.

“Sijasema chochote , nisaidie niingie”Aliongea na Hamza alikubali na alimsaidia mpaka ndani lakini mara baada ya kuingia ndani kulikuwa na tatizo lingine , alishindwa kuinama ili kushusha suruali chini kwani angejisababishia maumivu.

Alijikuta akikakamaa akishindwa kujua afanye nini , aliogopa kujikojolea pia kwa kuogopa aibu atakayoipata.

“Kapteni nitageuka nyuma halafu nitakusaidia kushusha suruali, nadhani hapo hutojisikia vibaya”

“Sawa”Aliongea Yonesi maana hakuwa na jinsi.

Hamza alijikuta akigeuka nyuma huku mkono ukiendelea taratibu kushusha suruali ya Yonesi pamoja na nguo yake ya ndani kwa wakait mmoja.

“Taratibu usiniguse”

“Sawa”

“Huko unakogusa ni wapi wewe?”

“Sioni vizuri sasa , basi ngoja niangalie tu”

“Unajitakia kifo sio , ole wako ugeuke”

Mara baada ya kuteseka kwa sekunde kadhaa hatimae alifanikisha misheni ya kuishusha.

Yonesi alijiegamiza katika mwili wa Hamza huku akijitahidi kukaa katika choo , lakini bado alikuwa na wasiwasi Hamza atageuka na kumwangalia

“Usiwe na wasiwasi , kama nilivyosema siwezi kufanya chochote ni bora ujiachie hayo maji yakutoke haraka haraka kuliko kujikaza usitoe sauti”Aliongea Hamza na kumfanya Yonesi kumwemwesa lips zake alitamani kumwambia Hamza atoke.

“Halafu Kapteni ushawahi kuwa mwanajeshi inakuwaje unapata wasiwasi na jambo la kawaida kama hili”

“Kwahio kuwa mwanajeshi ndio nini?”

Aliuliza Yonesi huku akiona asijikaze tena na kuachia kojo limtoke , lilikuwa na presha kama vile bomba la maji limepasuka, isitoshe wote walikuwa kimya hakukua na alieongea.

Yonesi alikuwa na aibu mno ilikuwa afadhali Hamza hakuongea chochote mpaka anamaliza.

“Unaweza kuondoka tu”Aliongea Yonesi mara baada ya kufanikiwa kurudi kitandani.

“Usiwe na wasiwasi , isitoshe bado ni muda wa kazi na hata nirudi kwenye kampuni sitokuwa na chakufanya, kwa maelekezo ya Dokta unapaswa kupumzika kwa siku mbili”

“Siku mbili?”

“Umejiumiza sana na hutakiwi kujiingiza katika matatizo tena , halafu tena umenikumbusha imekuwaje mpaka ukajiumiza ni mbinu gani ambayo umeitumia?”Aliuliza Hamza.

Ukweli ni kwamba alikuwa ashashuhudia mbinu nyingi za mapigano lakini hakuwahi kuona mbinu ambayo mtu anajiumiza mwenyewe kiasi cha kutema damu , alijua lazima mbinu ya Yonesi sio ya kawaida, lakini licha ya kuuliza Yonesi aliendelea kubakia kimya.

“Niwie radhi , huna haja ya kujibu kama ni siri yako?”

“Ukweli ni kwamba hata sijui ni mbinu gani, siwezi pia kusema ni mbinu ya kuamsha nguvu ya ndani?”

“Kwanini unasema hivyo?”

“Kuna kipindi wakati nikiwa chini ya kitengo kama mwanajeshi katika misheni maalumu katika Jangwa la Sahara niliweza kupata hii mbinu imeandikwa katika Notebook , mtu ambae aliandika nilimkuta akikaribia kupoteza maisha na alinikabidhi , nilimpatia Kapteni hio notebook lakini alisema haina maana yoyote , wakati nikiwa mafunzoni China nilimpa mkufunzi hio notebook na alitafsiri maandishi yale na kusema ni mbinu ya mafunzo ya kichawi ya kuamsha nguvu ya asili ya mwili lakini haijakamilika”

“Kwahio uliamua kujifunza bila ya kukamilika kwake?”

“Mwanzoni sikupanga kujifunza ila niliamua kuhifadhi tafsiri yake kama ilivyo , lakini kutokana na maelezo yake yalivyo yalinipa shauku na kuanza kuitumia na wakati nikifanya hivo mwili wangu huwa najihisi ni kama vile unaungua na presha kupanda juu mno huku nikijihisi mwenye nguvu lakini viungo vya mwili huwa ndio vinauma mno, nilikuwa na wasiwasi ni mbinu ya nguvu za giza hivyo sikuendelea nayo sana , lakini mara baada ya kumuona yule Chekani na kutamani kumshinda kwa mbinu yoyote ile nilianza kufuata maelekezo ya hio mbinu na matokeo yake ndio kama ulivyoona”

“Yaani kitu hakikukamilika lakini ukaamua kujifunza?”

“Ndio, mwanzoni nilifanya kutokana na shauku lakini mara baada ya kujaribu yale mabadiliko yalinijengea shauku ya kutaka kujua zaidi , Master alikuwa sahihi kabisa hii mbinu sio nzuri”Aliongea na kumfanya Hamza kumwangalia kwa mshangao kidogo.

“Kwanini unaniangalia hivyo?”

“Kapteni nimekusaidia kwenda chooni , vipi mimi unaweza kunisaidia kitu?”

“Niondokee hapa , kuna haja gani ya kurudish kumbukumbu za matikio yaliopita”

“Kukusaidia kwenda chooni inamaanisha wewe ni rafiki yangu mpaka hatua hii ndio maana naomba msaada kama rafiki pia”

“Kama unataka kujamba wewe jamba , huna haja ya kuongea sana”Aliongea Yonesi lakini Hamza alibadilika na kuwa siriasi zaidi.

“Unaweza kuniambia hio mbinu ilivyo?”

“Unataka kujaribu pia , inaweza kukusabishia matatizo?”

“Nataka kuijua tu , usiwe na wasiwasi siwezi kwenda mbali zaidi”

“Basi nitakuambia maana sio kama ni hazina ya maana mpaka nikufiche”

Yonesi mara baada ya kuona namna ambavyo Hamza alikuwa siriasi aliona amwelekeze tu maana ni kama ndio mara ya kwanza anamuona akiwa siriasi.

“Fumba macho kisha tengeneza hisia za kusikiliza mapigo ya moyo wako yanavyodunda , iliruhusu nafsi yako kuitawala akili yako , endelea hivo hivyo mpaka uone giza katika macho yako linapotea , litafute jua katika nafsi yako mpaka liwe katika uhalisia wa macho yako kisha lipotezee , utafute mwezi katika nafsi yako na kisha upotezee na kwanzia hapo kila kitu kitajielezea chenyewe kwa kadri unavyoona ….”Yonesi aliendelea kuongea lakini baadhi ya maneno yake hayakueleweka kwani yalikuwa na rahaja ya mafunzo ya kimapigano ambayo mtu wa kawaida hawezi kuelewa.

Hamza aliendelea kuwekeza akili yake katika kile alichoona lakini ghafla alijihisi mapigo yake ya moyo yakizidi kwenda mbio kwa kile alichoona na alijikuta akitoka mara moja katika mawazo yale na kufumbua macho.

Na muda huo huo mlango wa wodi uifunguliwa na msichana mdogo ambae Hamza alimfahamu ni moja ya mlinzi katika idara ya Yonesi aliefahamika kwa jina la Joyce.

“Kapteni vipi hali yako , unaendeleaje?”

“Joy unafanya nini hapa muda wa kazi?”Aliuliza Yonesi.

“Mkurugenzi kaniambia nije kumpokea Hamza , maana mimi ni mwanamke mwenzako hivyo ni rahisi kukusaidia”

Yonesi alijikuta akiona aibu kidogo lakini kwa wakati mmoja alijikuta akikasirika alitamani Joy angekuja mapema kabla ya kuaibika mbele ya Hamza.

“Mr Hamza Mkurugenzi anasema urudi makao makuu haraka haraka kuna vitu anataka kukuuliza”Aliongea Joyce na kumfanya Hamza kushangaa kidogo maana aliona kama ni kuuliza si angepiga tu simu, lakini hata hivyo hakuuliza zaidi na aliaga na kuondoka.

Hamza mara baada ya kuingia kwenye gari alijikuta akifikiria kile alichoona wakati wa kujaribu kufuatisha ile mbinu , alijiuliza kwanini aliona sura ya yule mwanamke aliekuwa akichomwa moto kwenye ile ndoto na ni kama alikuwa akimsubiria.

Hamza aliamua kupotezea kwanza swala hilo na palepale aliondoa gari mpaka katika makao makuu ya kampuni na mara baada ya kuegesha gari na kwenda moja kwa moja katika ofisi ya Regina , alishangaa kumkuta Bibi Mirium akiwa ndani ya ofisi katika kiti chake cha Magurudumu.

Pembeni yake alikuwepo Regina alieismama kiadabu kabisa , hakuwa kabisa na ile hali ya kuwa bosi wa kampuni.

“Kwanini bibi amekuja mpaka huku , shangazi hayupo nyumbani?”Aliuliza Hamza mara baada tu ya kuingia ndani ya ofisi hio na kumfanya Bibi yake Regina kugeuka na kumwangalia Hamza.

“Nasikia umevunja mtu mguu alietumwa na familia ya Benjamini kwa teke moja tu licha ya kuwa na mafunzo ya hali ya juu , nikama nilivyoambiwa unaonekana sio mwepesi mwepesi nadhani ndio maana Regina anakupenda”Aliongea.

“Bibi, Simpendi mimi”Aliongea Regina kwa haraka akikataa.

“Bibi ngoja nikuambie ukweli , yaani tokea nijiunge na hii kampuni nimekuwa na mchango mkubwa sana , siku nyingine ukija utazisikia sifa zangu tu”Aliongea Hamza

“Hehe,, nimekuja angalau kwa mara ya mwisho katika hii ofisi ili niweze kuliangalia jiji la Dar kupitia hili dirisha , sidhani kama nitaweza kuja tena kwenye maisha haya. Ila uzee una mambo mengi sana nakumbuka kipindi na babu yako wakati tunasimama hii sehemu baada ya jengo kukamilika mandhari hayakuwa ni ya kuvutia kama ninavyoyaona leo, naona kama uzuri wake umezidi kuongezeka mara tatu zaidi”Aliongea huku akionekana kama vile ni mwenye kujutia.

“Bibi kwanini kila saa unapenda kuongea maneno ya kujikatia tamaa”

“Wewe mtoto sisi wote ni wafanyabiashara na ili ufanikiwe kama mfanyabiashara unapaswa kujifunza namna ya kuukabili uhalisia , haina haja ya kufikiria mambo yasiowezekana kwasababu tu uhalisia ni mgumu , mimi bibi yako siku zangu zinahesabika na nashukuru hata kuweza kufika hapa juu nikiwa katika kiti cha magurudumu , pengie inaweza hata kunisahaulisha kile ambacho nataka kuona kikitokea kabla ya kuondoka”Aliongea na kumfanya Hamza kumkubali huyo bibi aliona ni kama umri wake umemfanya kuzidi kuwa na busara.

“Bibi unaonaje tukienda kupata chakula cha usiku katika hoteli kubwa ya kifahari , inaweza kuwa sehemu ya matamanio yako ya mwisho mwisho kutaka kufanya”

“Kuhusu hilo .. nadhani sio mbaya chagua hoteli nzuri kabisa tutaagiza mvinyo wa bei ghali kuliko yote inayopatikana nchini na kusherehekea”Aliongea kinyonge na kumfanya Regina macho yake kuanza kuwa mekundu.

“Nitamwambia Linda aweke utaratibu , vipi nialike na wazee wa kampuni”

“Washaondoka kuna haja gani ya kuonana nao , malizana nao kabisa ndio nitapata nafasi ya kwenda kuwaona , kwasasa sitaki kuwaona maana sidhani kama wana maana yoyote kwangu”Aliongea kikauzu na kumfanya Hamza kuishia kupumua tu kwa masikito aliona kabisa kuna uwezekano Regina karithi kila kitu kwa huyo mzee.

Muda huo huo mwanaume mzee wa miaka kama sabini na kitu hivi mwenye dalili ya mvi aliweza kuingia katika ofisi hio na kumfanya Regina kushangaa.

“Mzee Kibatala kwanini upo hapa?”Aliuliza Regina , Mzee Kibatala ndio aliekuwa mwanasheria mwenye umri mkubwa sana ndani ya kampuni yao na alisimamia maswala mengi tokea kipindi cha babu yake.

Ni moja ya wanasheria ambao walikuwa wakiheshimika mno ndani ya Tanzania nzima.

Kutokana na umri mkubwa aliokuwa nao alijichukulia kama vile amestaafu hivyo kazi nyingi za kampuni zilikuwa zikiwakilishwa na vijana waliokuwa katika ulingo wa sheria na yeye alionekana mara chache sana kwenye maswala ya kisheria ya kampuni.

“Mkurugenzi nipo hapa kwa maombi ya Madam , nimeleta wosia na nyaraka nyingine za kisheria”Aliongea.

“Wosia!!”

“Ndio”Aliongea na muda uleule alianza kutoa nyaraka katika mkoba wake wa Briefcase aliokuja nao , ilikuwa ni ile mikoba ya zamani kabisa na ilionekana ulitumika kwa kipindi kirefu mno.

“Kwasababu Madam hawezi kusaini na karamu basi tutatumia alama ya vidole vyake , pia nitarekodi tukio zima kwa ajili ya ushahidi”Aliongea.

“Mzee Kibatala amefikiria vya kutosha na ameona huu ndio muda”Aliongea Bibi Mirium.

Muda uleule yule mzee alianza kusambaza nyaraka katika meza ya kioo iliokuwepo katika ofisi hio na kumpa nafasi ya Mirium kuweka kidole gumba katika kila nyaraka

Regina ambae alikuwa pembeni aliweza kuona kila kitu na mara baada ya kuona mwisho wa nyaraka hio alijikuta akishangaa.

“Bibi , unataka kunipa hisa zote?”

“Ndio lakini kama nilivyosema kuna masharti”Aliongea huku akinyooshea mkono karatasi ya mwisho.

“Sharti langu ni wewe kuolewa , nikifariki bila ya kuona hujaolewa basi hisa zote kisheria zitaenda kwa baba yako”Aliongea na kumfanya Hamza kukunja sura na kujiambia huyu mzee ni mkatili mno kwa kutumia sababu hio kumfosi Regina kuolewa.

Lakini kwa upande mwingine aliona kama hisa hizo zitaenda kwa baba yake Regina basi kampuni inaweza kuwa ndio mwisho wake maana moja kwa moja hisa zote zitakuwa zinamilikiwa na Lamla.

Sasa kama Regina amefanya kazi kwa juhudi kubwa kuifikisha kampuni ilipo ataweza kuruhusu kuona kampuni inaangukia katika mikono ya watu wenye nia ovu.

Upande wa Regina aliona ni kama bibi yake anamuonea na kabla hajaweka kidole gumba katika karatasi yenye masharti alianza kulalamika.

“Lakini bibi mimi sitaki kuolewa nae”Aliongea na kumfanya Hamza midomo yake kucheza na kujiambia kwani amemkosea nini huyo mwanamke mpaka kumkataa waziwazi.

“Mimi sina shida , sio lazima uolewe na Hamza , mimi ninachotaka ni ndoa hivyo sijali nani unaoana nae”Aliongea na kumfanya Regina kuona wazo hilo ni baya zaidi.

“Bibi kwani lazima niolewe , ninao uwezo wa kuendesha kampuni bila ya kuolewa , sitaki mwanaume kabisa”

“Huu ni wosia wa baba yako na wa kwangu pia na sifanyi hivi kwasababu sina sababu haya yote ni kwa ajili yako , na nishaweka alama tayari hivyo kama unataka kuilinda kampuni isiende kwa mwingine hakikisha unaolewa haraka iwezekanavyo”Aliongea na kisha alimwangalia Hamza.

“Ila kwa upande wangu nimetokea kumkubali Hamza zaidi kama utaolewa nae una baraka zangu zote”Aliongea na kumfanya mzee Kibatala kutabasamu.

“Madam mimi ninawaacha kazi yangu ishamalizika hapa”

“Asante sana na pole kwa usumfufu matumaini yangu hili swala utalifanya kuwa siri kwa muda”

“Usiwe na wasiwasi Madam”Aliongea na Bibi Mirium alitingisha kichwa kumuaga.

Muda ule hali ya Bibi ilianza kubadilika na kumfanya Regina kumpeleka mpaka chumba cha kupumzikia , ofisi ya Regina ilikuwa na chumba cha kulala na sebule kabisa , ilikuwa ni kama ofisi ndani ya Apartment.

Upande wa Hamza wakati akiwa akimsubiria Regina kutoka ujumbe kwenye simu yake uliingia na alipoangalia namba ni mpya na aliufungua ule ujumbe na alikuta sentensi ya neno’ I am Back – From 2F .

Hamza palepale alijua aliekuwa ametuma ujumbe huo ni Frida na alijikuta akishangaa kidogo na alitaka kuipiga ile namba palepale lakini simu yake ilianza kuita na aliekuwa akipiga ni Eliza.

“Babe naona unanipigia muda wa kazi , utakuwa umenimisi sana nini?”

“Hata sijakumisi , nimesikia Yonesi kalazwa ndio maana nimepiga kujua maendeleo yake”

“Kwahio unachojali ni Kapteni Yonesi tu na sio mimi?”

“Hamna bwana.. ukweli nimepiga kwa ajili yako , nataka kujua kama una ratiba usiku , kama huna unaonaje ukija nyumbani nikupikie chakula kitamu kama ishara ya shukrani kwa ajili ya matibabu ya mama yangu?”

“Kwa leo haiwezekani , nishakubali kwenda kupata chakula cha usiku na bibi yake Regina”

“Oh… basi hata siku nyingine tu”Aliongea Eliza kinyonge.

“Babe ila usiwe na wasiwasi naweza kuja hata baada ya chakula”

“Sikufungulii mlango”

“Napitia dirishani”

“Halafu wewe .. sitaki kuongea na wewe”Aliongea na muda uleule simu ilikatwa.

Hamza mara baada ya kusikia sauti tamu ya Eliza moyo wake ulianza kuhisi majuto , na kuanza kujiuliza au baada ya chakula aende kwake kumfanyia surprise , pengine anaweza kupewa tunda.

Hamza mara baada ya kurudi katika ofisi yake ili kupoteza poteza muda ghafla tu mlango wa ofisi yake ulifunguliwa bila hodi na aliengia alikuwa ni Linda.

“Hamza”

“Kuna nini?”

“Bibi kazidiwa , wahi ukawashe gari tunamshusha”Aliongea Linda na kumfanya Hamza muonekano wake kubadilika mara moja na kitendo cha kutoka aliweza kusikia sauti ya kilio cha Regina akimwita bibi yake aamke.
 
SHETANI RUDISHA NAFSI ZETU

MTUNZI: SINGANOJR





SEHEMU YA 53/52

Tuliishia Bibi yake Regina ametembelea makao makuu ya kampuni na kuzidiwa Ghafla.

Endelea sasa.

Licha ya kwamba Mirium kuonekana amepoteza fahamu lakini ilionyesha ni kiasi gani alikuwa katika maumivu makali , uso ulipoteza nuru kabisa na ulikuwa umejikunja kana kwamba alikuwa akisikia maumivu makali.

Hamza mara baada ya kumuona mzee huyo alijua moja kwa moja ni vipindi vya mwisho mwisho vya ugonjwa huo na muda wowote anaweza kuondoka.

Lakini namna ambavo Regina alikuwa akilia na alivyowekewana ahadi na bibi yake kwa ajili ya kutoka nae Out , aliona kama akifa mapema Regina atakumbwa na majuto na huzuni kubwa , hivyo mara baada ya kuingia garini aliliendesha kama kichaa na ilimchukua dakika ishirini kufika hospitalini.

Mara baada ya Manesi kumchukua upande wa Regina alikuwa ni kama mpira ulioisha upepo wakati akikaa kwenye benchi.

Hamza alijua hata aongee neno la kumfariji halitokuwa na maana kwa muda huo hivyo na yeye alikaa pembeni yake kimya akimpa kampani.

Muda nao haukusimama,sekunde baada ya sekunde dakika zilisogea na hatimae usiku ukaingia.

Regina aliejichokea aliinua uso wake na kuangalia saa na hakuweza hata kujua muda umesogea vipi kwa kasi namna hio , kwani ilikuwa imetimia saa mbili kamili za usiku tayari.

Aligeuza uso wake na kumwangalia Hamza na alimuona kuwa na utulivu huku mikono akiwa ameikunja kifuani.

Hamza muda huo alikuwa ni kama sanamu kutokana na mkao wake , ilikuwa ni kama anaogopa kupiga kelele.

“Unaweza kutangulia ili uwahi chakula cha usiku kabla ya muda haujapitiliza”Aliongea Regina kwa upole huku macho yake yakiwa na majimaji kama mtu anaetaka kutoa machozi.

“Hata wewe hujakula chakula cha usiku bado”

“Sijisikii kula , huna haja ya kuendelea kubaki na mimi hapa , ninaweza kubakia mwenyewe tu”

Aliongea na kumfanya Hamza kuvuta pumzi nyingi na kuzishusha na kisha alishika bega lake.

“Kama umechoka unaweza kuegamia hapa , niwe feki au halisi bado cheo changu ni mpenzi wako”

“Haina haja , sijachoka hata hivyo”Aliongea huku akigeuka na kuangalia pembeni na kumfanya Hamza kuishia kutoa tabasamu kuonyesha kumwelewa na kisha aliegamia ukuta.

“Japo sina kumbukumbu za kutosha wakati nikiwa mtoto , lakini napata nusu nusu ya kumbukumbu za maisha yangu nikiwa mdogo , nakumbuka nikimuona mama yangu akiwa katika hali ya maumivu makali.. natamani kukumbuka kila kitu lakini bado nashindwa kuona kila kitu lakini licha ya kumbukumbu kidogo nilizokuwa nazo nahisi maumivu makali ambayo hayavumiliki kila dakika na saa ninapojiwa na kumbukumbu kuhusu mama yangu”Aliongea Hamza na kumfanya Regina kumwangalia Hamza kwa shauku.

“Huna kumbukumbu zote za utoto wako?”Aliuliza Regina na Hamza alitingisha kichwa kukubali.

“Mama yako amekufaje , pia hukumbuki?”

“Sikumbuki kabisa ninachokumbuka ni hisia nilizopata na kumbukumbu chache za mama yangu kuwa katika maumivu makali mpaka kukata roho, sikumbuki zaidi”.

Regina alijikuta akishindwa kujizuia na kushikilia sketi yake , ijapokuwa alimuona Hamza akiongea katika hali ya utulivu lakini alijisikia vibaya katika moyo wake kusikia maneno hayo.

“Ninachomaanisha ni kwamba najua ni hisia gani unazopita muda huu na nataka kukupunguzia mzigo”

Regina aliishia kuinamisha kichwa chake tu na hakuongea neno , upande wa Hamza pia hakuongea neno zaidi na alifunika macho yake akiwa ameegamia ukutani akisubiri.

Dakika kumi mbele aliweza kuhisi kitu kikiyagusa mabega yake na kumfanya afungue macho na kuangalia na hakuweza kujizuia kutabasamu mara baada ya kuona ni Regina aliejiegamiza kwake.

Regina alionekana kuwa na waswasi kana kwamba hakutaka Hamza kumwelewa vibaya.

“Usinifikirie vibaya , nimechoka kidogo tu”

“Ndio najua”

Baada ya hapo hakuna alieongea na walisubiria kwa namna hio mpaka lisaa lingine likapita na hatimae mlango wa cha ICU ulifunguliwa na bibi yake Regina alitolewa

“Dokta vipi hali ya bibi?”Aliuliza Regina mara baada ya kumkimbilia dokta na manesi waliokuwa wakimtoa bibi yake.

“Tumejitahidi kadri ya uwezo wetu lakini niseme tu hali yake ya inazidi kudhoofu kadri dakika zinavyosogea na muda wowote anaweza kuondoka, mnapaswa kujiandaa”Aliongea Dokta huyo wa kike wa makamo na kisha aliungana na kundi lake na kuendelea na safari

Regina aliishia kumwangalia bibi yake kwa huzuni wakati akitolewa ICU kwenda wodi za VIP.

Haikuchukua dakika nyingi na Shangazi alifika kutokea nyumbani na mara baada ya kusikia Mirium hana muda mrefu alijikuta akishikwa na huzuni.

“Baba bado tu hajafika?”Aliuliza Regina.

“Yupo mkoani kwa wakwe zake”Aliongea Shangazi akiwa katika hali ya huzuni kidogo.

“Oh..!

Regina alijikuta akikosa neno , ni kama alitegemea kitu kama hicho hivyo hakutaka kuwaza zaidi na kujipa matumaini hewa.

“Regina nitakaa hapa hospitalini kwa siku kadhaa na madam , inabidi mteseka kwa siku kadhaa wenyewe nyumbani”Aliongea.

Regina hakuwa na pingamizi , isitoshe alikuwa na majukumu makubwa sana ya kuendesha kampuni hivyo muda wa kukaa hospitalini ulikuwa ni mdogo mno.

Wakati huo Bibi Mirium ambae amewekewa Oksijeni aliweza kufumbua macho yake taratibu kivivu na kwa ukungu wa macho aliweza kuwaangalia watu hao watatu waliokuwa mbele yake.

“Regina …!”Aliita.

“Bibii!!”

Regina mara baada ya kusikia jina lake linaitwa alikimbilia kitandani kwa haraka na kwenda kushikilia mikono ya bibi yake huku akiwa ameinama.

“Bibi mimi hapa”Aliongea Regina huku akitabasamu.

“Mjukuu wangu nataka uniahidi kitu kimmoja…”Aliongea huku mikono yake ikionekana kumtetemeka na kauli yake ilimfanya Shangazi na Hamza kukunja sura kiasi maana ilionekana kabisa ni maneno ya mwisho mwisho.

“Bibi nakusikiliza , niambie tu.”

“Niahidi kwanza utafanya ninachokuambia”

“Bibi sijawahi kwenda kinyume na ahadi , bibi usiwe na wasiwasi nakuahidi”

“Hapo sawa .. nataka ufunge ndoa na Hamza hata kama ni ya serikali”Aliongea hatimae.

Dakika ambayo Regina aliyasikia maneno hayo macho yake yalichanua kwa mshagao huku uso wake ukiwa katika hali ya kutokuamini , ilikuwa ni kama vile nafsi imeuacha mwili wake.

Upande waShangazi alionekana kuwa katika tafakari ya kina huku akimwangalia Hamza.

Ijapokuwa Hamza aliikuwa ametegemea hilo lakini hakuamini bibi huyo atatumia dakika zake za mwisho kumtaka Regina kufanya jambo hilo.

Ukweli ni kwamba katika hali aliokuwa nao ilikuwa ni jambo lisilokuwa la kawaida kuongea , lakini ilionekana kutokana na uzoefu na ugumu mzee huyo aliopitia ndio maana akaongea hivyo.

Alionekana akijua hakuwa na muda wa kusubiri Regina aamue mwenyewe kuolewa na Hamza ndio maana alitaka kitendo hiko kifanyike kabla hajakata roho.

Upande wa Hamza na yeye alikuwa akimwangalia Shangazi na kwa jinsi alivyokuwa akimuona alijiambia tu lazima kuna maneno ambayo Shangazi ameongea kwenda kwa Bibi Mirium, isitoshe licha ya kumuonaShangazi kuwa kama mama wa nyumbani lakini siku ya kwanza tu kumuona alijua sio mtu wa kawaida.

“Bibi unapaswa kupumzika , unajichosha zaidi ukiongea”Aliongea Regina akitaka kuingilia anachotaka kusema bibi yake kwa mara ya pii.

Lakini Mzee huyo alimshikilia Regina kwa nguvu zake zote huku akijitahidi kumkazia macho, alionekana kuwa siriasi mno kile ambacho anataka Regina kufanya.

“Niahidi hapa hapa kama utakubali ninachokuambia”

Regina alijikuta akiingiwa na hisia mchanganyiko , ilikuwa ni hisia za maumivu , majonzi , kuchanganyikiwa, aibu na uoga.

Baada ya dakika moja ya ukimya aliishia kutoa tabasamu la kukubal.

“Nakuahidi nitafanya hivyo lakini swala la ndoa ni la makubalianyo ya watu wawili , Hamza anaweza asikubali”Aliongea Regina na kisha alimgeukia Hamza na kumpa ishara ya kukataa.

Hamza alimwangalia Regina namna alivyokuwa siriasi akimpa ishara za kukataa na alijikuta akisita kidogo.

“Mimi sina tatizo , nakubali ndoas”Aliongea

“Wewe..!!”

Regina alijikuta akifoka katika hali ya aibu na hasira kwa wakati mmoja huku akijimbia Hamza anawaza nini.

Bibi Mirium mara baada ya kusikia kauli hio kutoka kwa Hamza alijikuta akipandisha kifua na kukishusha kwa nguvu na kumwachia Regina, ilikuwa ni kama kila anavyovuta pumzi na kupumua ameongeza mwaka mmoja wa kupumua.

“Vizuri …nyie wote ni watoto wazuri na nataka kuwaona mkiwa pamoja kwa kifungo cha ndoa”

Hamza aliishia kuvuta pumzi huku akimwangalia Regina kwa kumuonea huruma , kumbukumbu za kile ambacho Yulia alimwambia kilimjia na aliona pengine ndio maana bibi yake Regina anafosi wafunge ndoa.

“Naenda kupunga kidogo upepo hapo nje , kama unataka tuongee utanikuta”Aliongea Hamza na kisha bila ya kujali alitoka nje mpaka eneo la maegesho ya magari na kwenda kuegamia kwenye mtende na kukodolea macho mwezi huku akionekana kuwa katika mawazo.

Alijikuta akiingiza mkono kwenye mfuko na kutoa simu yake na alienda upande wa namba za simu na alijikuta akiiangalia namba ya Eliza kwa muda na kisha alienda katika namba ya Dina na kuiangalia na alijikuta akirudisha simu mfukoni.

Swali lilikuwa moja tu , vipi kama kweli atafunga ndoa na Regina , Eliza atachukuliaje swala hilo? , si ataumia mno , vipi atakubali kuendelea nae , vipi kuhusu Dina.

Lakini jibu lilikuwa ni ndio, akimuoa Regina atamuumiza mno mpenzi wake Eliza , ni kweli hakuwa akimpenda Regina kiviile na pengine ni kutokana na kutokumjua kwake kwa muda mrefu , lakini mahesabu yake ni kama yalikuwa yakimwambia alimuona Regina kwanza kabla ya kumuona Eliza , pili Regina alionekana kuhitaji ulinzi mno kulingana na maadui zake pamoja na kile alichokifahamu kuhusu Regina kuwa na ugonjwa wa akili , haya yote ndio yaliomsababishia kusema ndio , lakini bado moyo wake ulikuwa mzito mno kila alipokuwa akimfikiria mpenzi wake Eliza.

Hamza alionekana kuwa na wasiwasi pia kwa wakati mmoja , hakufika Tanzania kwa ajili ya kufunga ndoa bali alifika Tanzania kwa ajili ya kumfahamu Mzee ni nani, wasiwasi wake hakujua katika misheni yake hio ni hatari za aina ngapi ataweza kupitia maana Mzee hakuonekana kuwa mtu wa kawaida.

“Kwanini umekubaliana na alichosema bibi?”Aliuliza Regina ambae alionekana kuwa katika hasira na kumfanya Hamza kumwangalia Regina kwa muda bila ya kutoa jibu , ni kama aikuwa akimchunguza lakini upande wa Regina alionekana alikuwa akitaka majibu.

“Kuna sababu gani ipi nyingine , nimeamua kujipandisha cheo kutoka kuwa Boyfriend mpaka kuwa Mume , naamini mshahara wangu utaongezeka mara mbili”Aliongea Hamza.

“Hebu geukia huko kwanza , sipo hapa kutaniana na wewe”Aliongea Regina huku akiona aibu kidogo.

“Hebu ingia kwenye gari tutafute eneo lolote tule chakula , hata kama njaa huna mimi njaa ninayo , tutaongea huku tunakula, sitanii”Aliongea Hamza akiwa siriasi na kumfahya Regina kuingia ndani ya gari kihasira hasira .

Hamza hakujali ubora wa Mgahawa kwa muda huo alijali kushibisha tumbo lake tu hivyo aliendesha gari na kwenda kupaki katika Mgahawa mdogo tu lakini ulionekana kuwa na mazingira safi na ilikuwa bahati Regina hakuwa na pingamizi.

Mmiliki wa mgahawa huo pamoja na wafanyakazi wake mara baada ya kuona gari hio ya Lexus ambayo imekaa kama zile zinazoendeshwa na wanasiasia waliishia kumkazia macho Regina na mmoja ya wafanyakazi hao ni kama alimfahamu Regina.

Walishangaa maana mgahawa wao ulikuwa ni wa hadhi ya wateja wa kawaida na sio matajiri, isitoshe hawakuwa na vyakula vya aina nyingi.

Hamza mara baada ya kukaa aliuliza ni chakula gani kinapatikana na mhudumu alimwambia.

“Vipi unaonaje tukiagiza Tambi na rosti ya mainu , unapenda?”

“Kwanini sipendi , dada niwekee hizo tambi na maini tu ila usiweke mchuzi mchuzi wenye vitunguu naomba na pilipili, pia utaniletea juisi ya embe ya Cereals”Aliongea Regina na kumfanya bosi wa mgahawa huo kutingisha kichwa huku akitoa tabasamu ni kama vile anaifurahia sauti ya Regina kama sio kumuonea wivu kutokana na uzuri wake.

Hamza alijikuta akinyamaza kimya, kwa jinsi Regina alivyochangamka ni kama alikuwa mzoefu wa migahawa ya namna hio na ilimfanya kumwangalia kwa tabasamu.

“Unaniangalia nini?”

“Sijakuangalia , ila kuna muda nakuona kama malaika uliemuasi Mungu”

“Unaongea upuuzi”Aliongea Regina huku akiona uvivu wa kujibishana na Hamza.

Dakika kadhaa waliletewa chakula na kutokana na njaa kila mtu alijikuta akiwa bize na chakula , muda huo Regina aliona midomo yake ilikuwa imejaa mafuta na kabla hata hajatafuta namna ya kujifuta Hamza alikuwa ashamchomolea tishu na kumpatia.

Regina aliishia kumwangalia Hamza kwa macho makavu kwa sekunde na kisha aliichukua ile tishu na kujifuta midomo.

“Ongea sasa kwanini umemkubalia bibi ilihali mimi sitaki”Aliongea Regina.

“Niongee nini tena , wakati kama huu bibi akiwa katika hali nzuri kidogo tunapaswa kwenda kujisajili na kupata cheti cha ndoa , isitoshe babe siwezi kubadili dini kwa ajili yako hehe”

“Acha kujipelekesha kimawazo , siwezi kuolewa na wewe”

“Lakini ushamuahidi bibi yako tayari na nimekubali mbele yake”

“Lakini wewe si una mpenzi wako?”

“Upo sahihi nina mpenzi na tupo hatua nzuri lakini hili lisikupe shida nitadili nalo mwenyewe”Aliongea Hamza na kumfanya Regina kuvuta pumzi nyingi na kuzishusha na muonekano wake ulizidi kuwa wa kikauzu.

“Ngoja nikuambie tu , mimi sijawahi kuamini maswala ya ndoa kabisa na tokea nikiwa mdogo nilijiapiza sitokuja kuolewa”

“Kwanini unasema hivyo , usiniambie ni kwasabqabu ya baba yako?”Aliuliza Hamza na Regina aliishia kuwa kimya kuonyesha ndio sababu.

Hamza alihisi kumwelewa Regina , isitoshe alikuwa ni mtoto wa nje ya ndoa.

“Sio kwasababu ya baba tu , ila nyie wanaume hamuaminiki kabisa , angalia kama wewe sasa hivi una mpenzi tayari na anaonekana kukupenda lakini bado unataka tufunge ndoa , unadhani ni kitu kizuri kwa mpenzi wako?”Aliongea Regina na kauli ile ilimfanya Hamza kutingisha kichwa kukubaliana nae.

“Nadhani sasa ushanielewa ninachomaanisha , hivyo achana na hayo mawazo kabisa , sina mpango wa kuolewa, kwangu mimi kuzikamilisha ndoto zangu naona kuna maana zaidi kuliko kuingia katika ndoa zilizojaa mateso”

“Unadanganya?”Aliongea Hamza.

“Kwanini nikudanganye?”

“Namaanisha hunidanganyi mimi ila unajidanganya mwenyewe”Aliongea na kumfanya Regina kukosa neno lakini kushangaa zaidi kutaka kujua Hamza anachomaanisha.

“Kama kweli huamini swala la ndoa basi unao uwezo wa kuolewa na yoyote yule, sio mimi tu hata awe James , kuna msemo wa kingereza wanasema ‘The more you care the more you will resist’ , kwa lugha nyepesi kama kweli ungekubali kuolewa na mtu yoyote ili kumridhisha bibi yako basi ni kweli hujali na huamini swala la ndoa”

“Sio kweli”Regina alikataa na kumfanya Hamza kumwangalia Regina na macho ya ki uchunguzi kana kwamba anajairbu kuangalia kilichopo ndani ya moyo wake.

“Basi ngoja nikuulize swali?, kwanini siku hizi umeanza kujilemba , kwanini umekuwa makini sana na mavazi yako na kwanini muda mwingine unakua mchangamfu na muda mwingine unakuwa kauzu mbele yangu?”Aliuliza Hamza na kumfanya Regina uso wake kuwa mwekundu.

“Unadhani nafanya hayo yote kwa ajili yako?, nafanya kila ninachotaka”

“Kama ni hivyo kwanini ulikasirika mimi kutokurudi nyumbani usiku na ukakasirika zaidi kutokana na kutorudi na nguo ulizonipa , kwanini umenisamehe kirahisi vile baada ya kukupiga vibao , kwanini unaonyesha hali ya kunitegemea katika baadhi ya vitu?”

“Sija.. umenielewa vibaya Hamza”

Regina alijikuta akishindwa kuwa na neno sahihi la kuongea na alijikuta akikwepesha macho yake na Hamza , mapigo ya moyo yalikuwa yakimwenda mbio mno na kauli za Hamza kusema ukweli zimemfanya kuhisi hali ya kupaniki.

“Regina!”Aliita Hamza na kumfanya Regina kumwangalia.

“Sikia kama kweli hujali ndoa basi hupaswi kuweka matarajio yoyote yae katika ndoa , kwasababu ndoa ni neno tu na hata cheti cha ndoa siku zote ni ushahidi tu wa kimaandishi , usidhanie kwasababu watu wanatambulika kama mke na mume na wanatambulika furaha wanayo au wanapendana, chukulia mfano baba yako na mama yako wa kambo, hivi unadhani wanafuraha kwasababu ni wanandoa?”

“Mama yako hakuwa ameolewa lakini alikuwa tayari kukuzaa ikimaanisha hakujutia kuzaaa na baba yako licha ya kutokuwa ndani ya ndoa , unadhani kama angekuwepo hai sasa hivi akikuangalia angejiona ni mwanamke mwenye laana kukuzaa nje ya ndoa?”

Maneno ya Hamza yalimfanya Regina machozi kuanza kujitengeneza katika mboni za macho yake.

“Tokea dakika ambayo mtoto anaanza kulia baada ya kuzaliwa moyo wake hupevuka palepale na hauna tofauti yoyote na wa mtu mzima , ili mradi una moyo na ni binadamu basi uwe ndani ya ndoa au nje ya ndoa haimaanishi kwamba huwezi kupenda, ndoa kama ndoa sio tatizo , tatizo ni watu , au nasema uongo?”

“Kupenda… kupenda… kwahio kwa mawazo yako unadhani nakupenda, hebu acha ukichaa wako”Aliongea Regina kwa hasira.

“Sawa unaweza kuniona kama kichaa na kunichukulia kama kichaa lakini kwa niaba ya kile anachopenda kuona bibi yako katika nyakati za mwisho wa uhai wake na kwa ajili ya wafanyakazi wote wa kampuni ya Dosam , tunapaswa kujiandikisha ili kupata cheti cha ndoa , kulingana na mtazamo wako hujali kabisa maswala ya ndoa na kwa mantiki hio kujisajili kama wanandoa haiwezi kukuathiri isitoshe utakuwa umepiga ndege wawii kwa jiwe moja , utamfurahisha bibi yako na utaikoa kampuni isiende kwenye mikono ya watu wasio na nia nzuri”

“Sitaki maswala ya ndoa fullstop”Aliongea Regina huku akigonga meza kabisa kutilia mkazo na kufanya baadhi ya wateja kumwangalia mrembo huyo na kujiuliza kuna nini mpaka kuonekana kuwa na hasria.

Regina hakuendelea kubakia ndani ya mgahawa huo , aliichukua mkoba wake na kuondoka haraka haraka

Hamza hakujali gharama ya chakula alitoa noti tatu za elfu kumi na kuziweka mezani na kumkimbilia Regina ambae alikuwa akilisogelea gari.

“Regina nitaendesha mimi?”Aliongea Hamza lakini Regina alimsukuma na kisha alifungua mlango wa dereva na kuingia.

“Sitaki kukuona tena , ondoka”

Regina alijihisi kuchanganyikiwa sio kwasababu Hamza alikosea ni kwasababu kila alichoongea Hamza ulikuwa ukweli ambao alikuwa katika vita nao.

“Bosi umesahau funguo za gari ninazo mimi?”

“Nipe funguo”Aliongea Regina mara baada ya kugundua hakuwa na funguo na anataka kuwa dereva.

Hamza mara baada ya kuona namna alivyokuwa siriasi aliishia kuzunguka upande mwingine na kuingia kwenye gari na kisha alimkabidhi ufunguo.

“Toka kwenye gari”

“Sitoki, kama nilivyosema kesho naenda kuaga ubachela”

“Wewe endelea tu kunichokoza”

“Nitakuchokoza mpaka uwe mke wangu”Aliongea Hamza.

Ukweli ni kwamba sio kama alikuwa akitaka sana kumuoa Regina bali aliona ndio njia pekee ya kumsaidia kwa wakati huo , ki ufupi hakuwa na jinsi na ili kufanya hivyo alitaka angalau kuonekana siriasi,ijapokuwa Regina anakataa lakini yeye ndio njia ya kutatua tatizo.

Regina aliishia kumwangalia Hamza kwa dakika kadhaa huku akijiuliza ni mkosi gani amejiingiza mpaka kukutana na Hamza, licha ya kwamba mwanzoni mpango wake ni kumridhisha bibi yake angalau kuwa na boyfriend feki lakini muda huo alijihisi kukosa amani kabisa, aliishia kuwasha gari na kulitoa ndani ya eneo hilo kurudi nyumbani.

“Regina mimi sio mtu mbaya ki hivyo , ukifikiria vizuri utaona nimekuokoa ulivyotekwa , hebu fikiria stori inavyonoga mtu akisikia namna shujaa Hamza alivyomuokoa mwanamke mrembo katika mikono ya watekaji , hili kitalaamu tunasema ni Penzi la papo kwa papo”

“Tunalikaribia daraja la Kigamboni , unadhani nashindwa kulitumbukiza gari baharini na wote kupotea, wewe endelea kuongea”

Damn .. acha kuniogopesha namna hio .. siongei tena”

Regina hakuwa mkataa ndoa bali alikuwa anaiogopa ndoa , ki ufupi wengi wanaosema ni wakataa ndoa mara nyingi wanaona aibu kusema wanaogopa ndoa.

“Usinikodolee macho angalia pembeni”Regina hakuweza kuhimili macho makali ya Hamza

Muda ambao Hamza anaangalia pembeni kama alivyoambiwa hisia mbaya zilimvaa muda uleule mara baada ya kuona pikipiki ambayo ilikuwa nyuma yao kwa muda mrefu.

Ilikuwa ni Ducat 1299 igales inayovuma kwa uwezo wake wa mbio na kusafiri kilomita nyingi, thamani yake ilikuwa sawa tu na BMW X3 au zaidi , sasa juu ya pikipiki hio kulikuwa na wanaume wawili ambao wamevalia helmeti nyeusi na kufanya sura zao zisionekane.

Kilichomfanya Hamza kuhisi hali isiokawaida ni kutokana na msisimko wa nia ovu ya kimauji iliowavaa watu wale ni hisia ambazo mtu wa kawaida hawezi kuzipata.

“Regina simamisha gari”Aliongea Hamza mara baada ya kuona usalama wao ndani ya gari ni mdogo.

“Unataka nini tena?”

“Kuna watu wanatufuatilia , haraka simamisha gari pembeni”Aliongea Hamza.

“Tunafuatiliwa…!”Regina palepale akili yake iliamka na kukanyaga breki lakini mara baada ya kuikanyaga uso wake ulifubaa.

Hamza palepale aligundua kuna kitu hakipo sawa na alimgeukia na kumwangalia.

“Nini tatizo?”

“Breki hazifanyi kazi”Aliongea Regina na kumfanya Hamza kukunja ndita na palepale alijua watu ambao wapo kwenye pikipiki mmoja wao ameshikilia kifaa kinachofanana na simu kwenye mkono wake.

“Wanatumia kifaa maalumu kudhibiti mfumo wa kielektroniki wa gari , naona wanatumia mbinu hii kutusababishia ajali ili ionekane ni ajali ya kawaida kabisa baada ya uchunguzi”











SEHEMU YA 34.

Regina mara baada ya kusikia kauli hio mikono yake iliokuwa imeshikilia usukani wa gari ilianza kutetemeka , isitoshe alikuwa msichana na ni ngumu kwake kuhimili mshituko wa namna hio

“Kwahio tunafanya nini , gari halipunguzi mwendo na tunakaribia mataa mbele yetu?”

Hamza alijikuta akiinua macho mbele na kugundua kweli mbele yao wanazikaribia Traffic light na magari ambayo yalikuwa yakitoka Kariako kwenda Mbagala yalikuwa mengi mno na pili katika lane yao kulikuwa na magari mbele yao ambayo pia yanapunguza mwendo , kama wakiendelea hivyo hivyo basi ni hakika watayagonga magari yaliokuwa mbele yao.

“Achia usukani , nitaendesha mimi rudi nyuma”

“Lakini siwezi kutoka hapa kirahisi”Aliongea Regina lakini Hamza bila ya kuchelewa kwa mkono mmoja alimnyanyua kutoka katika siti ya udereva na kumrushia katika viti vya nyuma ya gari , bahati nzuri gari yao iliikuwa SUV hivyo Regina hakujigonga na Hamza alimshika Regina makalio na kumsukumizia mpaka kwenye siti.

“Aiyaaa… umenigusa wapi!!?”

Regina licha ya kujua yupo hatarini alishindwa kujizuia kwa namna Hamza alivyomsukumiza kwa kumshika kalio.

Hamza hakutaka kujali zaidi na alishika sterling kwa mikono yake miwili na kuweka umakini kwenye kuendesha.

Gari ilikuwa ikiserereka kwa spidi kubwa mno na Hamza alijitahidi kadri ya uwezo wake kuyakwepa magari na kwenda mbele zaidi kiasi ambacho alifanya madereva kuanza kupaniki, ilikuwa ni upepo tu aliokuwa akiacha kila alivyopokuwa akipita gari.

Jambo zuri aliweza kulikunja gari vizuri na kuingia katika barabara ya dharula na bahati ilikuwa yake maana aliweza kupita mataa bila ya kugongana na gari.

Kitendo cha kupita tu Hamza aling’ata meno kwa hasira na kisha alikanyaqga pedeli na kuongeza mwendo zaidi.

“Wewe umekuwa kichaa , kwanini unakanyaga mafuta?”Aliuliza Regina kwa kupaniki asijue Hamza anafanya nini

“Wale watu kwenye pikipiki wameshikilia rimoti na inafanya kazi kwa umbali wa mita ishirini mpaka arobaini hivi, hivyo najaribu kuwaacha kwa zaidi ya huo umbali ili isifanye kazi ndio maana nimeongeza spidi zaidi”

“Kumbe! , wewe umejuaje sasa?”

“Wewe unadhani kama sina uwezo kwanini bibi yako analazimisha nikuoe?”Aliuliza Hamza na kumfanya Regina kugeuka yai.

“Ongeza umakini barabarani”

Kitendo cha kumaliza sentensi hio alichoweza kusikia ni sauti ya Ziii.. ziii..Ziii , gari ilikuwa imebadilika mngurumo wake na sasa ni kama ni mnyama aliekuwa akinguruma huku tairi zikisuguana na barabara.

“Argghh..!!”

Regina katika maisha yake hakuwahi kuwa katika hali kama hio , gari kwenda katika spidi ya hali ya juu mno na hakutaka kuangalia mbele zaidi ya kukizika kichwa chake

Uwezo wa Hamza wa kuendesha ulikuwa ni wa viwango va juu, baada ya kuingia katika daraja la Kigamboni aliongeza spidi zaidi kwa nguvu kabisa na gari ilichomoka kama mshale, mara baada ya kuangalia kwenye kioo alitoa tabasamu na palepale kwa nguvu alikanyaga breki na zilikubali.

“Creeek!!!”

Mataili ya magari yaliishia kuacha michirizi katika barabara ilioambatana na moshi , ilikuwa ni kama vile ndege inatua na hatimae aliweza kwenda kupaki gari pembeni mita kadhaa na daraja hilo katika stairi ya mshazari.

Kitendo cha gari kukanyaga breki na Hamza alivyoisimamisha gari katika mzunguko ilimfanya Regina kushikwa na kichefuchefu kikali , ijapokuwa mchakato wote ulifanyika kwa sekunde tu lakini ulikuwa sio wa kawaida kwake.

Wale watu kwenye pikipiki waliona hali sio nzuri na mpango wao ni kama umefeli hivyo kwa haraka waligeuza pikipiki wakidhamiria kukimbia.

Lakini Hamza hakuwa na mpango wa kuwaacha kabisa na alifungua mlango haraka na kutoka na kisha alianza kuikimbiza ile pikipiki na kadri alivyokuwa akikimbia mwili wake ulianza kubadilika.

Dereva wa ile pilipiki haikueeweka alikumbwa na nini lakini alijikuta akiyumba na kuisababisha pikipiki ile kuteleza na ikamshinda uzito na wote pamoja na aliempakia walidondoka chini na kabla hata hawajanyanyuka Hamza alikuwa ashawafikia tayari.

Muda huo hata Regina aliweza kutoka nje ya gari na kumkimbilia Hamza na kwenda kujificha nyuma yake.

“Nani kawatuma?”Aliuliza Hamza akiwa siriasi lakini yule dereva kwa utalamu alipiga sarakasi na kusimama na muda huo huo alichomoa Bunduki zile za kuwachomea sindano wanyama(Trangulizer gun) na kutaka kumfyatulia Hamza lakini Hamza alikuwa mwepesi mno kwani aliruka na teke na kumpiga kwenye mikono yake na kuifanya idondokee pembeni.

“Kama hamtaki kuongea nitawafanya muongee wenyewe”Aliongea.

Yule mwingine alionekana kuumia na alishindwa kusimama na Hamza aliamua kudili na yule aliesimama na kwa haraka alimsogelea na kumshika na kisha aliondoa ile helmeti na sasa aliweza kuona sura yake,alikuwa ni muafrika mwenye asili ya kisomali na alikuwa amevalia Heleni nyeusi.

Hamza alishangazwa na kitendo kile na kwa haraka haraka alimsogelea na yule mwingine aliekuwa akigulia maumivu na kutoa helmeti yake na wote kwa pamoja walikuwa wamevalia heleni japo yule mwingine alikuwa ni Mwafrika asilia.

“Nyie ni maninja kutoka kundi la Black Eared Snake!, inaonekana kuna watu kweli wamedhamiria kutuua”Aliongea Hamza akimaanisha watu hao ni kundi la maninja la Nyoka mwenye masikio meusi.

Kitendo cha Hamza kuongea neno hilo wale watu walijikuta wakishituka na kushangaa hawakuamini Hamza angeweza kuwatambua.

“Black Eared Snake ndio nini?”Aliuliza Regina.

“Ni kundi la maninja kutoka nchi ya CAR , ni kundi daraja C , ijapokuwa uwezo wa maninja wao hauwezi kuhesabika wa juu lakini wana mbinu nyingi za kusababisha mauaji , ndio kundi la kininja namba moja Afrika”Aliongea Hamza akimwelezea Regina kwa lugha nyepesi kwamba kundi hilo linatokea Afrika ya Kati.

Japo Regina hakuelewa maana ya kundi daraja C lakini alichojua muda huo hali ilikuwa ni ya hatari mno.

“Mmetumwa na familia ya Mzee Benjamini?”Aliuliza Regina.

“Usiulize maswali , ijapokuwa ni kundi daraja C lakini wanaongozwa na sheria kali za kininja , sheria kubwa ya ninja yoyote ni kutomtaja mwajiri wake”

“Kwahio tunafanyaje, tunawaacha waende?”

Hamza alifikiria kidogo na aliona asingeweza kuwaua wakati huo ambao Regina alikuwa mbele yake , alikuwa na uwezo wa kuwaua na kupoteza miili yao kimazingara lakini hakutaka maswali kutoka kwa Regina.

“Pigia simu polisi watakuja kudili nao”Aliongea Hamza na Regina alikubali lakini kabla simu haijapokelewa wale manijja walionekana kutafuna vitu huku wakiwa wamekaza sura.

Hamza hakutaka hata kuwazuia kwani aliona pia ni moja ya njia ya kutatua tatizo.

Dakika mbili tu wale manijja walitema damu nyeusi na kufariki palepale mbele ya Regina.

“Mamaaaa..!!!”

Regina alijikuta akipiga ukulele na pasipo ya kujua upande wa pili polisi alikuwa ashapokea simu yake.

“Hello , nini tatizo!!?”Hamza mara baada ya kuona Regina ameshikwa na mshituko alichukua simu na kutoa maelekezo kwa poilisi, upande wa pili wa polisi walionekana kushangaa maana ni kama hawakuwa wakiamini walichoambiwa , lakini hata hivyo walisema wanafika muda si mrefu.

Regina aijikuta akichuchumaa pembeni ya barabara huku akionekana ni kama ameshikwa na kichefu chefu.

Ilibidi Hamza kumsogelea na kisha alimshika bega kwa namna ya kumtuliza , mwanamke huyo ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuona mtu akijiua kwa staili hio hivyo ilikuwa haki yake kushituka.

Dakika chache baadae Polisi waliweza kufika eneo la tukio na kutokana na muda ulikuwa umeenda sana Hamza alimchukua Regina na kuingia ndani ya gari na kuanza safari ya kuelekea nyumbani .

Lakini sasa kitendo cha dakika chache tu za kuendesha sikio la tatu la Hamza liliweza kunasa sauti ya kitu kubip ndani ya gari , kama hakuwa mtu mzoefu asingeweza kugundua kitu hicho.

Ilikuwa ni bomu , ilionekana ndani ya gari lao kulikuwa kumetegwa bomu kama mpango B.

Hamza hakuwa hata na muda wa kumwambia Regina nini kinachoendelea na haraka sana alijifyatua kutoka katika siti yake na kuelekea upande wa Regina alipo na kumbeba juu juu akimtanguliza mbele yake , kitengo cha kufyatuka kwenye gari walisukumizwa na presha ya msukumo wa bomu na kwenda kutua kwenye majani upande wa pili wa barabara huku gari yao ikiteketea kwa moto mkubwa.

Kiikuwa kitendo cha sekunde chache mno kufanyika kuanzia kufunguliwa mkanda mpaka kutolewa nje ya gari na mlipuko kutokea na kuja kutua chini akiwa hajaumia.

Mlipuko ule uliyafanya masikio ya Regina kupatwa na ukiziwi wa ghafla na kengele za masikio kugonga , ilimchukua dakika kadhaa mpaka akili yake kurudi katika uhalisia.

Regina hakuamini alikuwa ameokoka katika mlipuko huo wa gari , Hamza angechelewa kidogo tu wangekuwa tayari ni maiti.

“Hamza… Hamza..!!”

Regina alijikuta akiita kwa nguvu mara baada ya kuzidi kulemewa na uzito wa mwili wa Hamza uliomlalia kwa juu , lakini licha ya kuita hakukuwa na majibu na alijikuta akimeza mate mengi na kujitoa katika mwili wake kwa kumsukuma pembeni..

Mara baada ya kuona mgongo wa Hamza machozi yalianza kumtoka bila ya kujua , aliweza kujua Hamza alitumia mwili wake kumkinga na presha ya mlipuko.

Regina alikuwa ameshikwa naBumbuwazi na maswali mengi yalipita katika kichwa chake na kujiuliza inamaana yeye ni wa muhimu mno kwa Hamza mpaka kujitoa kwa namna hio kumlinda.

Alijikuta akipotezea mawazo yale na kwa haraka sana alimtingisha Hamza kuamka.

“Hamza amka , nakuomba usife , fungua macho yako..”Regina alijikuta akipaliwa mpaka na mate na alijikuta akianza kutafuta simu yake ili kupiga simu lakini simu hakuwa nayo na alijikuta ni kama kuchanganyikiwa kumemvaa.

Dakika hio hio watu ni kama walisikia mlipuko huo na walianza kusogelea eneo hilo kwa kasi na Regina alianza kupiga kelele kuomba msaada.

“Regina..!!”

Alijikuta mwili wake ukimtetemeka mara baada ya kushikiliwa mkono wakati akitaka kuamka kwenda kuomba msaada lakini Hamza alionekana kuamka.

“Nipo hapa , unaendelea , hali yako ikoje?”

“Mbaya sama nadhani siwezi kuishi tena”Aliongea kinyonge.

“Uisongee hivyo huwezi kufa , ngoja niombe msaada tukupeleke hospitalini”Aliongea huku akisimama.

“Haina haja , mpaka nikifika hospitalini nitakuwa nishakufa”

“Acha kuongea kuniogopesha, huwezi kufa”

“Namuona Israeli mtoa roho mbele yangu , Regina nisamehe siwezi kukuoa kama bibi yako alivyosema”Aliongea Hamza

“Hapana usife , umesema mwenyewe unataka unioe, huwezi kufa leo, kesho tunatakkiwa kwenda kusajili ndoa yetu , naomba usife jamani”

Regina hakujua hata maneno yanatokea wapi lakini aliona ndio mbinu ya kumbembeleza Hamza asipoteze uha.

“Upo tayari tuandikishe ndoa yetu?”

“Ndio nipo tayari .. please Hamza naomba usiniache..”Aliongea na alijikuta akianza kulia kwa kwikwi.

“Kwakuwa umekubali mwenyewe , basi nimeghairi kufa mpaka siku nyingine”Aliongea Hamza huku akimwangalia Regina na tabasamu la uchokozi.

Regina mara baada ya kusikia kauli hio alijikuta akimwangalia Hamza na kumkuta hakuwa na dalili yoyote ya kuonyesha yupo kwenye maumivu.

Hamza alikaa kitako huku akipangusa mikono yake na kumwangalia Regina huku akimcheka.

“Kwahio Regina kesho ndio siku yetu ya kuuaga ubachela sio?”

Regina alijikuta akiwa haamini alikuwa akichezewa akili na Hamza muda wote , kadri alivyokuwa akimwangalia ile huzuni aliokuwa nayo ilianza kubadilika na kuwa na hasira kali, alijikuta akiona kipande cha zege pembeni na bila ya kujiuliza mara mbilimbili alikichukua na kumlenga nacho Hamza kichwani.

“Holly shit!!!”

Hamza alijikuta akifyatuka kama mshale akikwepa kipande kile ambacho kilienda kutua mtaroni.

“Hamza nitakuua …!!!”Aliongea huku akirusha ngumi za kike kwa hasira lakini Hamza aliishia kuidaka mikono yake na kumkumbatia kwa nyuma.

Shida halikuwa kumbatio tatizo ni mikono ya Hamza iliposhikilia katika eneo la kifua la mrembo huyo.

Hamza aliweza kuhisi kitu kilaini katika mikono yake na hakuweza kujizuia na kuuliza.

“Regina kumbe upo vizuri kiasi hichi”

“Wewe mpuuzi niachie”

Regina uso wake ulikuwa umeshika moto alitamani kujirusha kwenye mtaro.

“Sawa ila sijafanya makusudi”Aliongea Hamza huku akimuachia.

“Halafu kingine kwanzia kesho unakwenda kuwa mke wangu hivyo haijalishi wapi nina gusa”

“Kafie mbali huko , siwezi kuwa mke wako”

“Umeahidi mwenyewe zaidi ya mara mbili kama nikiendelea kuishi tutaenda kujiandikisha , kama bosi wa kampuni kubwa sidhani ni vizuri kwenda kinyume na ahadi yako unatoa mfano mbaya kwa wafanyakazi wako”

“Umenitega kwa kunidanganya , niliongea vile nikajua unakufa kweli”

“Kama upo tayari kuoana na mimi wakati nakaribia kufa si vizuri zaidi nikiwa hai maana utafurahia zaidi matunda ya ndoa , hata hivyo tuachane na hayo kwanza hata nikikuelezea huwezi kuelewa nini maana ya Matunda ya ndoa”

“Wewe..!!”

Regina alijikuta akipiga miguu chini kwa hasira na kuanza kupiga hatua kurudi barabarani.

Ukweli ni kwamba alishasahau kabisa kama walipata ajali ya gari lao kulipuka , ilionekana makusudi ya Hamza kumchezea akili yamemshushia presha kabisa ya swala zima la ajali.

“Mke unaenda wapi tena?”

“Naenda nyumbani”Aliongea Regina alijua hawezi kumfanya chochote Hamza hivyo hakuona haja ya kuendelea kujibishana nae , kuhusu maswala ya gari yao kulipuka aliona awaachie polisi wafanye kazi yao.

Dakika kadhaa tu wote waliweza kufika nyumbani na Regina mara baada ya kuingia ndani na kukumbuka Shangazi hayupo aliona ni kama kuna hali ambayo sio ya kawaida na alijikuta akigeuka na kumwangalia Hamza lakini alishangaa kumuona amekaa kwenye ngazi akionekana kufikiria.

“Wewe unafikiria nini?”

“Nawaza namna ya kudili na hawa watu ambao wanatusababishia ajali kila siku , sidhani kama nisiposhughulika nao mapema wanaweza kuacha”Aliongea Hamza na kumfanya Regina kumshangaa , dakika kadhaa zilizopita mwanaume huyo alionekana kuwa kama kichaa lakini sasa hivi amegeuka na kuwa siriasi.

“Kama unatengeneza hela nyingi jua kuna ambao hawana uwezo wa kutengeneza hizo hela , hivyo ni kawaida kuwa na maadui, nimejiandaa kwa vitu kama hivi ndio maana sipati shida hata vikitokea”

“Wewe unapaswa kuzingatia kufanya biashara na mimi nitazingatia namna ya kukulinda”

“Kwahio unapanga kufanya nini?”

“Regina hivi unadhani wale wajinga wametumwa na familia ya Mzee Benjamini au kuna maadui wengine ambao hatuwajui, sidhani ni swala la kawaida kukodi maninja hatari kama wale nje ya nchi kwa ajili yetu”

“Siwezi kujua ila familia ya James ndio maadui zangu wakubwa”

“Mpaka wameenda mbali kukodi majina kutoka Afrika ya kati!!?”

“Siwezi kujua kama kuna adui mwingine au lah”Aliongea Regina na kumfanya Hamza kutingisha kichwa.

“Usikurupuke kutaka kulipa kisasi , haijalishi una nguvu kiasi gani ni ngumu kushinda watu wengi”

Regina aliona swala la kuweza kuokoka katika ule mlipuko ilikuwa bahati lakini upande wa Hamza haikuwa swala la bahati.

“Naona ushaanza kuchukua cheo cha mke kwa namna unavyotoa ushauri”Aliongea Hamza akitabasamu kizembe na kumfanya Regina kugeuka na kuelekea juu chumbani kwake

Hamza mara baada ya kukaa sebuleni kwa dakika kadhaa hakuelekea tena ndani bali alitoka nje na kufunga mlango na kisha kuondoka

*******

UHALISIA NDANI YA NDOTO 04:30am

Licha ya mwanamke yule kuungua na ule moto wa maajabu na kufariki lakini kicheko chake na laana alizokuwa akiongea wakati wa kuungua zilikuwa bado zikisikika kama vile ni mwangwi unaojirudia rudia katika masikio ya watu.

Watu wale waliokuwa wakishangilia yule mwanamke mchawi kuchomwa moto walijikuta wakipatwa na woga kutokana na kitendo kile cha kuendelea kuzisikia zile sauti licha ya kwamba tayari amekwisha kuungua na kufariki.

Kusanyiko lile baada ya yule Askofu aliehusika kumuunguza yule mwanamke na moto wa nuru kuondoka walimfuata nyuma na kuingia katika kanisa kubwa na kuanza kusali kwa kutubu.

Licha ya kila mtu kutawanyika Hamza alijikuta akiwa amesimama katika eneo lilelile bila ya kupiga hatua , kilichokuwa kikimshangaza ni kwamba bado akili yake ni kama ilikuwa ikiyaona macho ya yule mwanamke yakimwangalia , haikuwa hivyo tu ule moto ambao ulimuunguza yule mwanamke bado alikuwa akihisi nguvu yake.

Alikuwa katika mshituko mkubwa mno kwa kile kilichotokea , kiasi cha kusahau kabisa nafsi yake na akili yake ipo katika mwili ambao sio wake

“Hii nguvu ni ya kimaajabu mno”Aliwaza Hamza.

Tofauti na kuogopa kama ilivyokuwa kwa watu wale ambao hakuwa akiwajua lakini yeye alikuwa ameshikwa na tamaa kubwa ya nguvu ile alioweza kuiona na kujiuliza anawezaje kujifunza uwezo ule.

Muda huo alijikuta akishikwa mkono kitendo kilichomshitua na kumwangalia aliemshika.

“Jamani Luther , Asante Mungu wa nuru , Asante Mungu wa nuru kwa kumuokoa na mateso kama ya baba yake , kijana mdogo kama huyu anastahili rehema za Mungu”

Hamza alijikuta akivutwa kutolewa katika eneo lile na yule mwanamke huku akiongea kila aina ya maneno ya shukrani kwa Mungu wa Nuru.

Alikuwa Mzungu , ukweli ni kwamba kila mtu aliekuwa akimuona kwake alikuwa ni Mzungu.

Hamza alijaribu kunyanyua mdomo ili kuongea lakini mdomo ulikuwa mzito mno na bado alikuwa katika mshangao wa kuitwa Luther, alitaka kuuliza yeye ni nani na kwanini ana mwili wa kizungu.

Hamza aliendelea kushangaa zaidi mara baada ya kuingizwa katika nyumba ndogo na mwanamke wa makamo wa kizungu ambae alikuwa akitaja kila aina ya shukrani kwenda kwa Mungu.

Kitendo cha kushangaa na kujishangaa kilimfanya yule mwanamke kumwangalia Hamza na kuendelea kutokwa na machozi.

“Luther ugonjwa wa akili umekutesa mno , hebu jiangalie ulivyokonda..”Aliongea yule mwanamke huku akimwangalia Hamza.

Hamza bado alikuwa na maswali , hakujua kilichokuwa kikiendelea ni nini lakini alijua kitu kimoja hakuwa ni Hamza bali alikuwa ni Luther, aliogopa pia kuongea kwa kuonekana labda watamjua yeye ni Hamza katika mwili wa Luther.

“Alisa usiongee sana na Luther, ndio kwanza amepona na lazima atakuwa na uchomvu , Ivani msaidie mama yako twende nyumbani”

Hamza aligeuza macho yake na kumwangalia mwanaume wa kizungu mwenye nywele nyeupe akiongea , alikuwa na kama miaka hamsini hivi kwenda sitini hivi , licha ya kuwa na ndevu nyingi lakini ilionyesha katika ujana wake alikuwa na mwonekano mzuri.

“Asante Shangazi , nipo sawa bado tu najihisi kizunguzungu”Hamza aliongea lakini aliongea nje ya hiari yake , ilikuwa ni kama kuna kitu ambacho kilikuwa kikimsukuma kuongea hivyo.

Yule kijana ambae alikuwa amemleta Hamza kuangalia mchawi akichomwa moto alikuwa amemshikilia mwanamke huyo wa kizungu aliefahamika kwa jina la Alisa.

“Luther nimefurahi sana kukuona hali yako inatengemaa yule mchawi amestahili , amekutesa sana”

“Wakati ule anahamia na kuwa jirani yako alionekana kama mwanamke mrembo sana mstaarabu mpaka nilipatwa hadi na wazo la kuhakikisha John anakuwa mke wake lakini alikuwa ni mchawi, tulimshuhudia mara kadhaa akifukua miili ya watu kutoka makaburini ili kufanyia majaribio ya kichawi , Asante sana Mungu kwa kumfanya akamatawe na ushahidi wakati akifukua mwili kaburini , nashindwa hata kufikiria kama angefanikiwa katika uchawi wake ni watu wangapi wangeathirika”

Hamza aliendelea kusikiliza yale maneno ya Alisa kwa umakini na sasa ni kama anapata mwanga , yule mwanamke alikuwa mchawi na alikamatwa na ushahidi akiroga kwa kufukua maiti makaburini ndio maana akachomwa moto.

Kutokana na mwanamke yule kuwa jirani yake na yeye pia alichukuliwa kama mshirika wa uchawi na yule mwanamke na kuanza kuhojiwa na ilionekana mahojiano hayakuwa ya kawada , kuna nguvu za ziada ambazo zilikuwa zikitumika na ndio kilichomfanya Luther kupoteza fahamu, ilimfanya Hamza kudhania pengine Luther alikuwa akishirikiana katika maswala ya ulozi na yule mwanamke ndio maana alikuwa akimwangalia sana.

Yule mwanamke Alisa alionekana kuongea mfululizo kana kwamba alikuwa akisimulia tukio zima la namna mwanamke yule alivyokamatwa na namna ambavyo pia Luther alihusishwa katika swala hilo mpaka kuachiliwa.

Yule mwanaume mwenye nywele nyeupe alimwangalia Hamza na muda uleule alionekana kutabasamu na kumshika bega.

“Yupo hivyo , unapaswa kumzoea”Aliongea na kumfanya Hamza kutingisha kichwa.

“Alisa alikuwa mwanamke mrembo sana wakati wa ujana wake lakini mara baada ya kumzaa John alibadilika sana na kuwa kama hivi , mpaka sasa naweza kusema amekuwa sio mshindani wangu tena likija swala la kuongea”Aliongea yule mzee kwa kingereza.

Upande wa Hamza bado hakuzingatia mazungumzo yao ni kama alikuwa akiwaza kutaka kujua alikuwa wapi na kwanini nafsi yake ipo katika mwili ambao sio wake.

“Joeli mwanaume aliekuwa na nguvu na hamasa ya juu ya kutimiza ndoto zake za kuwa msanii mkubwa sasa hivi amegeuka na kuwa mlevi”Aliongea Alisa

“Aalto ni jiji ndani ya nchi ya Zaburi , watu wasiohesabika wanafika kwa ajili ya kutimiza ndoto zao lakini je ni wangapi ambao wamefanikiwa , isitoshe Alisa nimeacha kuwa mlevi tokea siku John aliopata kazi”

“Asante Mungu , nadhani unajua namna tulivyoweka matumaini yetu kwa John na Ivan , John amekuwa mtoto mzuri kwetu ameweka juhudi kubwa na sasa ameweza kuchaguliwa na kujiunga na jeshi , kama ataweza kuamsha karama ya damu yake na kutambulika ataweza kupewa cheo cha Ubwana na wengi watamheshimu”Hamza alimsikia yule mwanake Alisa akiongea na upande wa yule mwanaume aliefahamika kwa jina la Joeli alitingisha mabega na yule mwanamke aliefahamika kwa jina la Alisa alionekana kujishtukia na kumwangalia Hamza.

“Luther nisamehe , sijamaanisha kwamba wewe huna uwezo , ulitakiwa kupitia mafunzo kidogo wakati ulipokuwa mdogo”Aliongea yule Alisa lakini ni kama radhi yake haikuwafanya kazi.

“Luther hana shida na naamini ataweza kuibeba ndoto yangu na kuwa msanii mkubwa”Aliongea yule Joeli.

“Ndio nataka kuwa msanii mwanamuziki mkubwa”

Hamza alijikuta akisema bila ya kufikiria huku akicheka na kumfanya yule mwanamke kuvuta pumzi ya ahueni na kuanza kuongea tena kila neno ambalo lilimjia mdomoni na ilimfanya Hamza kuelewa mji huo na ulimwengu huo kitu alichojua ni kwamba yupo katika jiji lililofahamika kwa jina la Aalto ndani ya nchi ya Zaburi.

Hamza muda huo licha ya kujua nafsi yake ipo katika mwili ambao sio wa kwake lakini ukweli alijikuta ni kama alikuwa akiangalia TV kwa kupitia VR na kumfanya awe katika mazingira yale matukio yanapotokea.

Nafsi yake muda huo ilikuwa ikimwambia lazima afahamu yupo wapi , kama yupo kwenye ulimwengu mwingine lazima ajue yupo ulimwengu gani , kama ni kumbukumbu za maisha lazima azifahamu ni kumbukummbu gani ambazo zimemleta katika mazingira ya namna hio , mazingira ambayo ni ya kale kabisa lakini yenye kujaa maajabu na hata kama ni ndoto lazima ajue kwanini anaota ndoto ya namna hio.

Hamza alijikuta akishituka mara baada ya kutingishwa kwa nguvu na akiwa katika hali ya kuhema alijikuta akifumbua macho yake na pembeni yake alikuwa amesimama Regina.

“Amka wewe , nenda kaoge na kisha badilisha mavazi yako”Aliongea Regina aliekuwa amesimama akimwangalia Hamza namna alivyojiachia bila ya kujifunika shuka kutoka kiunoni na kufanya kifua chake kuwa wazi pamoja na mwili uliovimba kutokana na mazoezi , alijikuta akishindwa kujizuia na kuanza kuona aibu za kike.

Alijiambia ndio maana Hamza anaonekana kuwa na maamuzi ya haraka kutokana na kuwa na mwili wenye mazoezi.

Aliona mwili wa Hamza haukuwa wa kawaida kabisa na aliushangaa kana kwamba hakuwahi kuona mwili wa mwanaume.

Hamza upande wake ni kama hakupenda kutoka ndotoni , ukweli ni kwamba siku kadhaa nyuma alihofia ile ndoto lakini mara baada ya kuota zaidi ya mara nne ni kama alianza kupata shauku ya kuendelea kuota , kwake ni kama alikuwa akiangalia tamthilia akiwa ndotoni , kiichomfurahisha ni kwamba ndoto hio ni kama ilikuwa ikijua wapi aliishia kuota kwani ilianza palepale na kuendelea lakini sasa mara baada ya kuona kumekucha ilimshangaza, aligeuza macho upande wa eneo la swichi kuangalia labda ule mshumaa wa nuru umechomekwa kwenye umeme lakini hakukuwa na mshumaa na aliona kabisa ameota bila ya msaada wa kitu.

“Regina kwanini umeingia chumbani kwangu bila ya kugonga?”Aliuliza Hamza.

“Nimegonga mara kibao hufungui ndio maana nikaingia , fanya haraka nataka tukachukue cheti cha ndoa”Aliongea Regina na kumfanya Hamza kufunua shuka bila ya kujali alikuwa amevalia boksa tu.

Regina hakutegemea Hamza alikuwa na boksa tu na baada ya shuka lile kumtoka mwilini kilichoonekana ni eneo la mbele la Hamza kuwa na hamasa kubwa ya mapambano.

“Ah!!.. unafanya nini ?”Regina alijikuta akigeuka na kuangalia pembeni huku mapigo ya moyo wake yakienda kasi mno.

“Hii ni swala la kibaiolojia , kuna haya gani ya kushituka wakati ni ishara nzuri kuonyesha nina afya nzuri”Aliongea Hamza

“Huoni aibu?”

“Nione aibu ya nini ndani ya chumba changu , Regina unaonekana kuwa na mchecheto mno kwenda kuchukua cheti cha ndoa asubiuhi asubuhi, hukulala nini?”

“Sitaki bibi kuwa na wasiwasi kabla ya kuondoka , usifikirie mbali ni cheti tu ila maisha yetu yatabakia vilevile, nimekaa chini na kufikiria na nimegundua bibi anachotaka ni kuona cheti tu na hajasema hatuwezi kuachana hapo baadae , baada ya mkataba wako wa kazi kuisha tunaweza kuachana na kila mtu akaendelea na mambo yake”

“Kuna haja ya kwenda mbali hivyo , kuna haja ya kuichukia ndoa kiasi hicho?”

“Sijasema naichukia ndoa nachukia kufunga ndoa na mtu kama wewe”Aliongea na kumfanya Hamza kuvuta pumzi ya masikitiko huku akimwangalia mwanamke huyo akizipiga hatua kutoka chumbani kwake.

“Regina kwasababu umekuja kuniamsha chumbani kwangu , unaonaje na mimi nikiwa nakuja chumbani kwako kukuamsha , itakuwa ni kuamshana kwa zamu”

“Ole wako uingie chumbani kwangu”Aliongea Regina na kutoka nje.

Upande wa Hamza wakati akijiandaa kwenda kuoga simu ilimfanya aghairi kwa dakika kadhaa na kisha kuchukua kujua nani anampigia asubuhi asubuhi hio , baada ya kuangalia na kuona jina ni la Dina alijikuta akitoa tabasamu la uovu na moja kwa moja alikumbuka ukatili aliofanya usiku.

“Mrembo nini maana ya kupiga simu asubuhi yote hii”

“Unaniuliza nini , umefanya nini wakati nikiwa nimelala?”Sauti upande wa pili ilionekana kuwa na hasira mno.

INAENDELEA GRUPU WATSAPP 0687161346.
 
Back
Top Bottom