Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

Story nzuri sana na uko vzuri kwenye uandishi katika mafanikio yoyote audience wako ni muhimu kuliko chochote kile inawezekana wasikulipe pesa lakini wakakusimulia kuna mwandishi anaitwa singano hvo ikakuza jina zaidi na zaidi ushauri ni kuwa mwaminifu katika muda ni heri uhaid baada ya mwezi itaendelea watu watasubr si ndo ahad ila ukisema jumatatu alafu ukapost ijumaa amin kuna watu watachoka kukufwatilia hata kama hawakupi pesa
 
Story nzuri sana na uko vzuri kwenye uandishi katika mafanikio yoyote audience wako ni muhimu kuliko chochote kile inawezekana wasikulipe pesa lakini wakakusimulia kuna mwandishi anaitwa singano hvo ikakuza jina zaidi na zaidi ushauri ni kuwa mwaminifu katika muda ni heri uhaid baada ya mwezi itaendelea watu watasubr si ndo ahad ila ukisema jumatatu alafu ukapost ijumaa amin kuna watu watachoka kukufwatilia hata kama hawakupi pesa
Enyewe kuna ks ukweli fulani,mimi mwenyewe kuna siku nisha sema hapa ila ni kama mwenyewe ana jiamini zaidi, kuna waandishi wengi mtandaoni wengne hata hawa mufikii yeye ila wana wafuasi wengi ajabu juu wana ishi ndani ya ahadi zao. Wakisema jumatatu ni jumatatu na mfaano kama haiezekani muandishi anajitokeza anasema leo kuni radhi wapendwa zangu kwa sababu zisizo epukika leo haita wezekana
 
Enyewe kuna ks ukweli fulani,mimi mwenyewe kuna siku nisha sema hapa ila ni kama mwenyewe ana jiamini zaidi, kuna waandishi wengi mtandaoni wengne hata hawa mufikii yeye ila wana wafuasi wengi ajabu juu wana ishi ndani ya ahadi zao. Wakisema jumatatu ni jumatatu na mfaano kama haiezekani muandishi anajitokeza anasema leo kuni radhi wapendwa zangu kwa sababu zisizo epukika leo haita wezekana
Hapo wala kunakua hakuna ubaya maana inakua inajulikana kuwa mwenzetu anachangamoto hivyo hakuna atayelaumu
Wazungu wanatuzidi maendeleo si kwakua wao ni bora kutuzidi hapana ila wanaheshimu muda na makubaliano
 
Aisee Nimesoma story nyingi ila jamaa unapswa kujiangalia tena sokoni.Kama ni muvi basi ni Hollywood status.
Nilikua nakuchukulia poa mwanzoni ila duh 👏👏.

Fanya upango wa kuiuza hii kitu.
 
Story nzuri sana na uko vzuri kwenye uandishi katika mafanikio yoyote audience wako ni muhimu kuliko chochote kile inawezekana wasikulipe pesa lakini wakakusimulia kuna mwandishi anaitwa singano hvo ikakuza jina zaidi na zaidi ushauri ni kuwa mwaminifu katika muda ni heri uhaid baada ya mwezi itaendelea watu watasubr si ndo ahad ila ukisema jumatatu alafu ukapost ijumaa amin kuna watu watachoka kukufwatilia hata kama hawakupi pesa
Ahsante.mkuu naendelea kupambana kuimarika zaidi ili twende kwa ahadi. Writer' s block bado ni changamoto kubwa kwangu hususani aina hii ya simulizi ambayo inakuwa ndefu na yenye scripted word nyingi na wahusika.Ila napambana. THANK YOU
 
Aisee Nimesoma story nyingi ila jamaa unapswa kujiangalia tena sokoni.Kama ni muvi basi ni Hollywood status.
Nilikua nakuchukulia poa mwanzoni ila duh [emoji122][emoji122].

Fanya upango wa kuiuza hii kitu.
Asante mkuu for feedback
 
To be Honest bro tafuta soko la hii story kunakoeleweka.

Najua kuna vipande vitawapa tabu waigizaji hasa wa Bongo ila itauza,Hapa unaweza pata series zaidi ya Huba
Ni kweli ila changamoto yake ni kubwa sana kwa kweli,ila ikiweza itauza vizuri tu. Hii inataka camera yenye ina worth 1.5 million Kenyan money ndio itoke kwa ubora uwake lasivyo itakosa ladha yake.
 
Ahsante.mkuu naendelea kupambana kuimarika zaidi ili twende kwa ahadi. Writer' s block bado ni changamoto kubwa kwangu hususani aina hii ya simulizi ambayo inakuwa ndefu na yenye scripted word nyingi na wahusika.Ila napambana. THANK YOU
Stay blessed
 
Kuna episodes ni kama JF wameifuta humu hata sielewi na sijapewa maelekezo, Naanza kutuma sehemu ya 95
 
SHETANI RUDISHA AKLII ZETU.



MTUNZI:SINGANOJR.



SEHEMU YA 95.

The Pandora Box.

Mwanaume aliekuwa mbele yao alikuwa ni Robert Eliasi Mbilu mtoto wa mheshimiwa rais anaemaliza muda wake.

Amosi na Dastani wote walikuwa wakifahamiana vizuri na Robert , kitu pekee ambacho hawakukijua ndio maana walishikwa na mshangao wa kumuona ndani ya eneo hilo ni kuhusu Robert kumpenda sana Dina , lakini hata hivyo akaishia kumpoteza mara baada ya kubeti na Hamza

“Kanali na wewe ni mhudhuriaji wa huu mgahawa?”Aliuliza Robert huku akimwangalia Kanali kwa shauku.

“Leo ni mara yangu ya kwanza kuingia ndani ya huu mgahawa,Sijategemea kukuona wewe pia mheshimiwa hapa”Aliongea Kanali.

Robert licha ya kuwa mtoto wa raisi lakini vilevile alikuwa ni mbunge.

“Nipo hapa kwa niaba ya baba na mazungumzo yangu na bosi Dina yameshaisha hivyo ngoja niwaachie uwanja , Kanali usisahau kuonja chai inayotengenezwa na huyu mrembo hapa , pengine unaweza kuwa mhudhuriaji wa mara kwa mara kama mimi”Aliongea na kisha alimgeukia Dina.

“Dina nadhani ujumbe wangu umeweza kufika na matarajio yangu ni makubwa kwako”

“Usiwe na wasiwasi Mheshimiwa , nitakupa majibu nikishafanya maamuzi”Aliongea na kisha Mheshimiwa Robert alisimama na kuaga na kuondoka na kuwaacha Kanali na Amosi ambao bado walikuwa na hali ya wasiwasi kwenye macho yao.

Dina alikuwa akimfahamu Amosi lakini hakuwa akimfahamu vizuri Kanali Dastani.

“Bosi Dina huyu ni Afande Dastani ana mazungumzo na wewe ndio maana nimemsindikiza leo kuja hapa”Aliongea Amosi.

“Amosi nilijua ni jeshi la polisi tu ambalo lipo mfukoni mwako kumbe hata watu wa vitengo?”Aliongea Dina kwa kutania na kauli ile ilimfanya Kanali kumwangalia Dina kwa macho ya mshangao kidogo.

“Kipi knakufanya uamini mimi ni wa kitengo , kama alivyonitambulisha Amosi mim ni mwanajeshi cheo cha Kanali”

“Kama ni mwanajeshi cheo cha Kanali sidhani kuna sababu ya kuwa hapa , tena ukitangulizana na Amosi, nadhani tuache maigizo na twende moja kwa moja juu ya sababu ya kutaka kuonana na mimi”Aliongea Dina na kumfanya Kanali kuvuta pumzi.

“Sababu ya sisi kuja ni juu ya Marehemu Mchuku , kwa taarifa ambazo tumeweza kukusanya tumegundua Marehemu alikuwa moja ya watu wanaofanya kazi chini yako”Aliongea Amosi na kumfanya Dina kutoa tabasamu hafifu.

“Mchuku alikuwa sehemu ya watu wangu ndio na kwasasa ni marehemu na stori yake imeisha , kuna sababu nyingne ya kumuunganisha Mchuku na mimi?”

“Ndio , uchunguzi uliofanyika juu ya kifo cha Mchuku unaonyesha sio kifo cha kawaida kutokana na ugonjwa wake bali aliuwawa”Aliongea Kanali.

“Kama kauwawa unataka kumaanisha nini kwangu?”Aliuliza.

“Ninachomaanisha ushahidi unaonyesha kifo chake sio cha asili na kama sio cha asili maana yake kuna sababu ya yeye kuuwawa, siku moja kabla ya Mchuku kupoteza maisha tumeweza kugundua kuna kiasi kikubwa cha pesa kilichoingia katika akaunti yake ya benki na baada ya kufuatlia kiasi hiki cha pesa kimetoka wapi tumegundua kimetoka katika akaunti yako binafsi, nilikuwa na mawasiliano na Mchuku saa chache kabla ya kifo chake na kuna biashara ambayo tulipaswa kufanya siku inayofuata , lakni baada ya kuwasliana alipoteza maisha ndani ya saa chache tu”

“Nenda moja kwa moja kwenye pointi yako ya msingi Kanali , haina haja ya kuelezea hayo yote?”

“Okey , kilichotuleta hapa ni kupata faili ambalo Mchuku alikuachia , kitendo cha kumwingizia hela kwenye kaunti yake kwa njia ambazo zimeturahisia kujua wewe ndio umeingizia maana yake ulitaka tukufikie na ndio tupo hapa”Aliongea Kanali.

“Mna uhakika gani hela niliomwingizia Mchuku inahusiana na hiko mnachotafuta , kama mmefuatilia vizuri basi mmeona Mchuku amekuwa kwenye payroll yangu kwa miaka mingi, ikimaanisha kwamba yupo kwenye mtandao wangu”

“Kama yupo chini yako basi moja kwa moja inaniaminisha amekuachia mzigo wangu kwasababu ya kukuamini”Aliongea Kanali na kumfanya Dina kutabasamu kidogo.

“Tuseme ni kweli Mchuku kaniachia Mzigo wako , kwahio unamaanisha kiasi cha pesa nilichoingiza kwake kinahusiana na huo mzigo?”Aliuliza na Kanali alitingisha kichwa.

“Kama kweli mnaamini hivyo basi moja kwa moja inaonekana kitu mnachofuatilia thamani yake ni kubwa , sisemi kwamba Mchuku kuna alichoniachia , ninachotaka kujua ni nyie kunipa sababu ya kukumbuka kama kweli kuna kitu Mchuku kaniachia”Aliongea Dina na kauli ile ilimfanya Kanali kukunja ndita na kujiambia mwanamke ni mhuni huyo , ndio maana alikuwa mkuu wa genge la kihalifu licha ya urembo wake.

“Nimekuja nikiamini ingekuwa ngumu kukushawishi na kutupatia bla maongezi , isitoshe umeulipia huo mzigo?”

“Ndio nakusikiliza ndugu Kanali?”

“Dina nadhani ni vizuri kama ukituelezea unachohitaji kwa ajili ya kutupatia huo mzigo, tunajua lazima Mchuku alikukabidhi hivyo haina haja ya kuzungushana , wewe elezea unachotaka na tutajua cha kufanya”Aliongea Amosi.

“Mna uhakika mnaweza kunipa ninachotaka?”Aliuliza Dina.

“Inategemea na ukubwa wa hitajio lako, isitoshe licha tunautaka huo mzigo lakini hatuna uhakika kama unaweza kuwa na thamani kwetu”Aliongea na Dina alifikiria kwa dakika kadhaa na kisha alionekana kutabasamu.

“Alichoniachia Mzigo kina taarifa ya kutosha kwenu , ni mazungumzo baina ya watu wawili na inaonekana wanazungumzia juu ya alichogundua mtu anaefahamika kwa jina la Sedekia , wametumia lugha ya Spanish lakini nimeweza kutafsiri mazungumzo yote”Aliongea Dina huku akiangalia sura za wanaume hao wawili kwa macho ya matarajio.

Muda ule Dastani mwili ulimsisimka kwani kitendo cha Dina kutamka neno Sedekia moja kwa moja alijua alichorekodi Mchuku kina taarifa ya kutosha anayoitaka.

“Unataka kiasi gani tukukabidhi hio rekodi?”Aliuliza Kanali akionyesha hali ya tamaa.

“Sihitaji pesa , hela nilizokuwa nazo zinanitosheleza”

“Kipi unataka tofauti na hela?”

“Mahitajio yangu ni mawili , la kwanza nataka mnitafutie mbadala wa Mchuku ambae ataendeleza kile alichokuwa akifanya na pili nahitaji kumjua mheshmiwa Abubakari nje ndani hususani yale ambayo hayaonekani , najua atashinda uchaguzi ujao ila kabla ya kuingia Ikulu nataka kujua uhusiano wake na familia ya Wanyika”Aliongea Dina akiwa siriasi na mahtajio yake yalionekana kumshangaza Dastani.

“Bosi Dina maombi yako yote yapo nje ya uwezo wangu , sina cheo cha kumteua mkuu wa Gereza na vilevile kuhusu Mheshimiwa Abubakari Kassimu ombi lako ni gumu kufanyika mapema kabla ya uchaguzi , linahitaji muda isitoshe kuna familia ya Wanyika”Aliiongea Kanali lakini hata hivyo Dina hakujali na alichukua mkoba wake uliokuwa pembeni na kisha alitoa flashi na kumpatia Dastani.

“Kasikilizeni kilichomo humo na pengine tutaweza kuongea zaidi baada ya hapo”Aliongea Dina na Kanali na Dastani waliishia kuangaliana kwa mshangao huku wakipokea ile Flashi, wote walijiuliza ni kipi ambacho kimo humo.

******

Hamza alipokea simu ile haraka haraka maana hakuwa amewasiliana na rafiki yake Amiri kwa muda mrefu kidogo.

“Niambie Bro?”Sauti upande wa pili ilisikika , alikuwa ni Amiri na hakukuwa na utofauti wa sauti na siku zote.

“Shwari kabisa , mambo vipi?”Aliongea Hamza huku akijitahidi kuwa kawaida kwa kujihusha kadri awezavyo ili kuendana na Amiri.

“Mambo yako shwari kabisa , hatujawasiliana kwa muda tokea tulivyo achana , nilikuwa nje ya nchi ndio nimengia nchini jana”

“Oh safi”

“Sasa Bro nilitaka kujua ulifikia wapi kwenye lile swala?”

“Ngoja nitakupa majibu muda si mrefu , vipi kuna mabadiliko yoyote kwa Mellisa?”

“Kaka sijui hata nikueleze vipi , ila kuna mabadiliko makubwa kwa Mellisa na hali yake inanitia mashaka”

“Nambie kinachoendelea?”

“Nilikuwa nae nje ya nchi likizo hivyo nilipata nafasi ya kumchunguza na nimeweza kuona kila siku anakuwa ni mwenye kuota ndoto huku akiongea maneno yasioeleweka , muda mwingine ni kama anaongea lugha ambayo simwelewi na akishaota anakosa kabisa usingizi , siku tulizokuwa pamoja ametokea kukonda sana tofauti na alivyokuwa hapa nchini”Aliongea Amiri huku sauti yake ikonekana kuwa na hali ya kusikitika na huruma.

Hamza alifikiria kidogo na kuona anapaswa kuwasiliana na Sally ili kujua amefikia wapi kutafuta maana ya zile lugha.

“Hujajaribu kukaa nae chini na kumuuliza shida yake ni nini?”Aliuliza Hamza.

“Nimefanya hivyo kaka na ndio maana nimekupigia simu , nataka tuonane ana kwa ana nadhani ndio utaweza kunelewa vizuri zaidi alichoniambia”Aliongea Amiri.

“Sawa Bro , kwasasa nipo nje ya mkoa nikirud nitakupgia simu tuonane”Aliongea Hamza .

“Sawa Bro”

Hamza mara baada ya kukata simu aliangalia muda na aliiona usiku ushaingia tayari , hivyo alianza safari ya kurudi nyumbani.

Wakati akiwa njiani ujumbe uliingia kwenye simu yake na mara baada ya kusoma aliishia kutoa tabasamu lililojaa uchungu , hakujua acheke ama alie maana aliemtafuta alikuwa ni Anitha mwanachuo mwenzake.

Hamza licha ya hivyo hakutaka kujibu ujumbe ule aliupotezea na kisha alianza kuzipiga hatua kurudi.

Ilimchukua nusu saa tu kutembea mpaka kufika nyumbani na mara baada ya kufika aligundua kuna ugeni nyumbani hapo kwani kulikuwa na gari iliokuwa imegeshwa katika eneo la dharula , gari aina ya Prado.

Hamza mara baada ya kuingia ndani aliweza kukutana na sura za watu wawili ambao hakuwa akiwajua, mmoja alikuwa ni mwanaume mzee hivi miaka kama hamsini na mwingine alikuwa ni kijana mdogo wa rika lake ila mtanashati zaidi.

Regina pia alikuwa ndani ya eneo hilo akionekana kuongea na wageni hao.

Yule Mzee na kijana mara baada ya kumuona Hamza hawakumfahamu mara moja kama ni nani, lakini dakika hio hio Regina alichukua jukumu la kumtambulisha Hamza.

“Mzee Sheiza huyu ni mume wangu , anaitwa Hamza”Aliongea Regina na mara baada ya Mzee yule alieitwa Sheiza kusikia hivyo alishangaa huku akisimama haraka na kusalimiana na Hamza na hata pia yule kijana aliekuwa nae alisimama na kuonyesha mshangao wa kutoridhika.

“Hamza huyu ni Mbunge wa hapa Lushoto lakini pia ni mfanyabashara , huyo pembeni yake ni mtoto wake Jose, Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Usambara Group”Aliongea Regina na Hamza alitingisha kichwa kuelewa , huku akijisikia vizuri mara baada ya Regina kumtambua kwa cheo chake cha mume.

“Mr Hamza nimefurahi kukuona , sikuwa na taarifa Mkurugenzi na mwenyekiti wa makampuni ya Dosam amekwisha kuolewa , hakika una bahati sana”Aliongea yule Mzee akiungana na kijana wake.

“Nimefurahi kukufahamu pia Mzee Sheiza na bwana Jose hapo karibuni sana”Aliongea Hamza na Mzee alitngisha kichwa akikubali ukaribisho na baada ya hapo Hamza alimwangalia Regina kujua kinachoendelea.

“Wapo hapa kwa ajili ya kutoa salamu za pole , Mzee Sheiza alikuwa rafiki yake baba kwa muda mrefu, lakini pia wamekuja kwa ajili ya kuzungumzia maswala ya kibiashara ambayo waliongea na Bibi”

“Bibi aliongea nao maswala ya kibiashara?”

“Ndio, ilikuwa ni ndoto ya Bibi Mirium kuendeleza hii Wilaya ki uwekezaji kama namna ya kuenzi sehemu ambayo biashara zake zilianzia , kulikuwa na mpango unaondelea wa kuinunua kampuni ya Usambara kama hatua ya kwanza ya kufanikisha hilo”Aliongea Regina.

“Mkurugenzi ukweli ni kwamba nilikuwa na makubaliano na Marehemu kuuza kampuni yangu kwenda Dosam huku akinipa msaada wa kutosha kwenye harakati zangu za siasa lakini wazo hilo nimeghaili na nipo hapa kwa ajili ya majadiliano mengine”

“Unamaanisha nini kughaili .nakumbuka bibi alianiambia mliongea kila kitu na mkakubaliana na kilichobaki ni hatua ya mwisho ya makabidhiano”

“Ni kweli niliongea nae kila kitu na tukakubaliana na hata malipo ni makubwa na ya kuridhisha lakini bado nimeona tunaweza kufanya kazi pamoja tofauti na kutununua kabisa”

“Ulikubaliana na bibi kiasi gani?”Aluliza Regina.

“Alikubali kununua kapuni yote kwa bilioni kumi na nusu, ahadi hi ipo kwenye maandishi kabisa”Aliongea na Regina alifikiria kidogo.

“Nitaichukua kwa blioni ishirini kamili”Aliongea Regina na kauki yake ilimfanya mtoto wake Jose kutoa macho na kumwangalia baba yake kwa macho ya kumtaka akubali.

“Baba usikatae hii ni zaidi ya thamani ya kampuni yetu yote”Aliongea Jose, lakini Mzee wake bado alionekana kusita sita kukubali ofa ho,zilikuwa ni pesa nyingi mno tofauti na ukubwa wa kampuni yake.

“Mkurugenzi nipo tayari kuuza asilimia hamsini na tano ya hisa zote za kampuni kwa bei halisi ya soko , lakini vilevile sitoingilia katika maamuzi ya utendaji mpya wa kampuni na mabadiliko yatakayofanyika, nitabakia kuwa mwanahisa pekee na nipo tayari kuweka ahadi yangu katika maandishi”

“Baba..!!”Jose hakuamini maneno ya baba yake , ilikuwa ni kama hakumsikia vizuri.

Upande wa Regina alionekana kufikiria kidogo na kisha akatabasamu kuonyesha ishara ya kuridhika.

“Nakuheshimu sana Mzee Sheiza katika harakati zako za siasa, maamuzi haya nadhani maana yake ni kwamba kipaumbele chako kwa sasa sio pesa”Aliongea Regina.

“Mkurugenzi Marehemu alikuwa mtu wa kuheshimika sana ndani ya mji wote huu, amesaidia watu wengi kwa kipindi chote alichokuwepo hai, mimi kama mwanasiasa ni kazi yangu kutambua mchango wake kwa jamii ili Legacy yake isipotee, pengine na wengine waige kutoka kwake”

“Maana yake unataka kutumia jina la bibi kujinufaisha kisiasa?”

“Siwezi kukataa juu ya hilo, lakini vilevile nikiwa Mbunge wa jimbo hili maana yake pia kutakuwa na faida ya kurahisisha ndoto za bibi yako kufanikiwa”Aliongea na Regina alifikiria kidogo na kisha kutingisha kichwa kukubali.

“Nipo tayari kuinunua kampuni yako kwa asilimia ambazo utaniuzia kwa sharti la kukubali kampuni yako kuwa chini ya sheria moja ya usimamizi ya makampuni yote ya Dosam”Aliongea Regina Mzee Sheiza hakufikiria mara mbilimbili bali alikubali mara moja.

Masaa machache baada ya mazungumzo hayo Mzee Sheiza na mwanae Jose walikuwa kwenye gari yao wakielekea nyumbani , huku Sheiza akionekana kuwa na furaha mara baada ya kuona mazungumzo yake yamefanikiwa lakini upande wa Jose alionekana hajaridhishwa kabisa na maamuzi ya baba yake.

“Baba kampuni yetu haina hata thamani ya bilioni saba kujumlisha na madeni tuliokuwa nayo , tumepewa ofa kubwa ya dola bilioni ishirini kwanini uliikata?”

“Jose katika dunia hii hela sio kila kitu kama una ndoto unataka kukamilisha”

“Unamaanisha nini Mzee?”

“Unajua kwanini Regina alitaka kutoa kiasi kikubwa cha pesa?”Aliuliza na Jose alitingisha kichwa kutokujua.

“Maana yake alitaka kumalizana na sisi moja kwa moja baada ya malipo, lakini kitendo cha kuuza hisa kadhaa hata kama sitoendelea kubakia kama mmiliki mkubwa lakini bado nitaendelea kuwa na ushirikiano wa karibu na Regina pamoja na mume wake , thamani yangu itaonekana katika siasa kwenye kurahisisha mipango yao lakini wakati huo huo nitautumia ukubwa wao kwenye kutumiza malengo yangu yote ya kisiasa”

“Lakini Mzee hii ni familia ya kitajiri tu na siku zote inafahamika kwa kutokufungamana na siasa”

“Dosam ni kweli na kampuni ambayo haifungamani na upande wowote wa kisiasa , lakini swali muhimu je ikitaka kuingiza ushawishi wake wa kiuchumi katika siasa nini kitatokea?”

“Kutatokea power dynamic kubwa sana”Aliongea Jose na Mzee huyo alitingisha kichwa.

“Binadamu wanaogopa nguvu wasioielewa na huo ndio ushawishi waliokuwa nao kampuni ya Dosam , kitendo cha kushikiria uchumi wa Tanzania kuptia biashara zao na wakati huo huo kutokufungaana na upande wowote wa kisiasa , imetengeneza hofu kwa wanasiasa ndio maana miaka na miaka majaribio mengi ya kuiangusha kampuni ya Dosam yanafanyika lakini hakuna mafanikio , chukulia mfano swala la kampuni ya Zena kufirisika na kuhusishwa na kampuni ya Dosam , ule haukuwa mchezo wa kibiashara ulikuwa ni mchezo wa kisiasa na Mgweno kaitoa kafara familia ya Mzee Benjamini”Aliongea na Jose alikuwa akijua sakata zima la kampuni ya Zena kufa.

“Kwahio Mzee unachojaribu kufanya ni kujiweka karibu na kampuni ya Dosam ili hata kama ikionekana kwa nje uhusiano wenu ni wa kibiashara lakini siku ikatokea Dosam ikachukua upande wowote wa kisiasa na wewe unafaidika?”

“Jose wewe ndio kijana wangu mwenye akili nyingi kuliko kaka zako ndio maana vikao vyangu vingi tunaenda pamoja , ili ufanikiwe kwenye maisha yako elewa vitu hivi viwili, kwanza kabla ya kuyatafuta mafanikio elewa kwamba mafanikio pia yanatafuta watu , kwenye mafanikio kuna utofauti mkubwa kati ya aliejenga nyumba karibu na barabara na yule aliejenga mbali na barabara , hivyo kuwa karibu na kampuni ya Dosam kwangu ni sawa na kujenga nyumba karibu na barabara ili nionekane wa kwanza pale ninapohitajika , pili jifunze kuelewa yaliojificha kupitia yale yanayoonekana”

“Baba unamaanisha nini kusema nijifunze kuelewa yaliojificha kupitia yale yanayoonekana?”

“Wakati Regina anamtambulisha yule Hamza kama mume wake niliona mabadiliko yako kana kwamba hujaridhika kwa bosi mkubwa kama yule kuolewa na kijana kama Hamza, kitendo cha kuonyesha dalili ya kumdharau maana yake ni kwamba umeshindwa kuelewa yaliojificha kupitia yanayoonekana”.

“Baba unataka kusema yule Hamza ni mtu mzito kuliko anavyoonekana?”Aliuliza na Mzee alitingisha kichwa.

“Ukweli ni kwamba wakati tunaelekea kwenye kikao nilikuwa na mpango wa kupokea kiasi chochote nitakachopata na kuuza kampuni , lakini mara baada ya Regina kumtambulisha yule Hamza kama mume wake moja kwa moja maamuzi yangu yalibadilika kabisa na wazo la kuuza kampuni lilipotea”

“Baba unaongea kimafumbo sana , kwanini usiniweke wazi?”

“Haina haja kwasasa , ila kumbuka nilichokuambia kwanzia sasa hisa zote ambazo zitakuwa za kwetu nitakupa nguvu ya kisheria ili kupata nafasi kubwa ndani ya kampuni , ukinisikiliza ninachokuambia ndoto zako za kupata zaidi ya bilioni ishirini zinaweza kutimia, pili hakikisha unajenga uhusiano mzuri na Hamza , hio ndio misheni yako kwanzia sasa”Aliongea na Jose alitingisha kichwa kuelewa.

Upande mwingine Hamza muda wote alikuwa akitabasamu kama vile ameingiwa na ukichaa wa ghafla mara baada ya wageni kuondoka.

“Mbona unatabasamu hivyo , kuna kilichotokea huko ulikotoka?”Aliuliza Regina aliekuwa bize na tablet yake.

“Kilichotokea ni hili la sasa hivi kunitambulisha kama mume wako?”Aliongea Hamza na kauli yake ilimfanya Regina kushangaa kidogo na kisha kushikwa na aibu za kike.

“Ulitaka nikutambulishe vipi , sioni tatizo maana ni kweli sisi ni wanandoa kisheria?”

“Najua lakini namna ulivyonitambulisha ulikuwa na uhakika kabisa mimi ndio mume wako”

“Umefurahi?”

“Wewe unanionaje, Regina ukiendelea hivi hivi unajua nitashindwa kujizuia?”Aliongea Hamza huku akiweka tabasamu la uovu.

“Kujizuia kufanya nini?”

“Kuwa mume anaepata haki zote”

Kauli ile ilimfanya Regina kujua anakoelekea Hamza na ilimfanya kuanza kufkiria kitakachotokea na mwili wake ulimsisimka na kuona aibu.

“Nitabakia huku kwa siku kadhaa kukamilisha yale bibi alioacha, kama una haraka unaweza kutangulia”

“Tumekuja wote na tutaondoka wote , ni vizuri kuendelea kupata faida kwa kunitammbulisha kwa watu kama mumeo, huoni Mzee Sheiza kabadili mawazo mara baada ya kuniona na wewe umefaidika”

“Ni kweli kwa jicho la kibiashara sikuwa na mpango wa kutoa zaidi ya bilioni kumi na nusu kuinunua kampuni yake kama bibi alivyoniagiza, lakini niliweza kumsoma mawazo Mzee Sheiza dakika ambayo ameingia hapa nyumbani , ni mtu ambae kwake hela sio kipaumbele , ni mtu mwenye busara naweza sema”

“Hivi kuna watu ndani ya dunia hii ambao hela sio kipaumbele?”

“Unauliza swali ambalo majibu unayo , unadhani kwa hela nilizokuwa nazo tayari hela kwangu inaweza kuwa kipaumbele tena, mtu ambae hajazaliwa familia yenye utajiei ni kweli ataona hela ndio mafanikio lakini ukishazipata hela utaona hela sio mafanikio kwasababu bado hujaridhika, malengo ya kampuni ya Dosam sio tu kwa ajili ya kunipandisha katika swala la utajili bali ni namna inavyotoa mchango wake kwa jamii , ndio maana umaarufu wa kampuni yetu ni kutoa huduma ya viwango vya juu kwa bei nafuu huku tukijipatia faida kutokana na wingi wa wateja wetu”

“Lakini yule Mzee Sheiza hakutaka kuuza kampuni kwasababu alitaka ukaribu na wewe , licha ya kujua hilo kwanini bado ukamkubalia?, zipo njia nyingi sana za kukamilisha ndoto yako bila ya kufungamana nae”

“Licha ya sera ya kampuni yetu kwa miaka mingi ni kutoingiza katika maswala ya kisiasa na kuendeshwa na sheria za ushindani wa soko , lakini si kweli kwamba imepiga hatua kwa njia za kawaida za kibiashara , maswala mlionielezea na Shangazi nimegundua kuna zaidi ya kile ninachoelewa na kuona , Sipangi kujifungamanisha na wanasiasa ila napanga kuweka wanasiasa karibu ili ikitokea nikawahitaji nisitumie nguvu kubwa, licha ya kampuni ya Zena kufirisika haimaanishi kwamba ndio mwisho wa ushindani , najua ni swala la muda tu kwa kampuni nyingine itaibukia na hizi ni kampuni ambazo haziendeswhi kwa sheria za kibiashara tu, siasa pia hutumika na siku zote namna nzuri ya kushindana na siasa ni kupitia siasa yenyewe”

“Kwahio unataka kudili na maswala ya kisiasa bila kundoa kampuni katika sera yake ya muda mrefu?”Aliongea na Regina alitingisha kichwa na Hamza aliishia kutabasamu huku akijiamba Regina anakichwa kidogo lakini kinafikiria vitu vingi kwa mpigo .

Hata hivyo ilionekana ni sahihi kufikiria mbeleya muda , kumiliki kampuni ambayo ina zaidi ya wafanyakzi laki moja halikuwa jambo jepesi hata kidogo kwa msichana mdogo kama Regina , lakini uwezo wake wa akili na wa ki uongozi alionekana anaweza kushinda jambo lolote hivyo hakuwa na wasiwasi.

*****

Siku iliofuata wakati wanamaliza kupata kifungua kinywa uliingia ugeni ambao ulimshangaza Regina na kujiuliza Hamza kafanya nini mpaka asubuhi yote hio kutembelewa na polisi.

Alikuwa ni Kamishina wa upepelezi Afande Maningi aliembatana na polisi wawili na mzee mmoja msomali alievalia suti, ambae Regina alimtambua mara moja kama Mkurugenzi wa makampuni ya Salahi.

“Afande imekuwaje ukafika asubuhi yote hii mpaka huku?”Aliuliza Hamza mara baada ya kuwakaribisha.

“Mr Hamza mambo sio mazuri ndio maana nipo hapa?”

“Unamaanisha nini?”

“Hamza wewe ni muuaji?”Sauti ya yule mwanaume ambae Regina alimtambua ilisikika , huku bwana yule akionekaana kuwa na hasira mno za kutaka kumshambulia Hamza lakini alizuiwa na wale polisi.

“Mzee Mohamed , umesema mwenyewe utakuwa mtulivu tukifika hapa ndio maana tumekuja na wewe, ukiendelea hivi hatuwezi kupiga hatua kwenye huu uchunguzi”Aliongea Kamishina.

“Kuna haja gani ya kuongea Kamishina , huyu mtu ni muuaji alieuwa watu wengi ndani ya jiji hili kwa kuwadhalilisha , yupo hivi hivi katika ile Vidio hakuna tofauti hata kidogo”Aliongea Mzee Yule kwa kufoka na kauli yake ilizidi kumshangaza Hamza maana hakuwa akielewa kinachoendelea.

“Mzee Mohamedi nini kimetokea?”Aliingilia Regina.

“Regina unamjua huyu Mzee?”Aliuliza Hamza.

“Ndio, ni Mohamed Sallahi mkuregenzi wa makampuni yote ya Sallahi , ni baba yake yule Salma uliekutana nae kipindi kile”Aliongea Regina.

“Regina mume wako kamuaa binti yangu Salma, kuna uwezekano na wewe unahusika”Aliongea yule Mzee mwenye muonekano wa kisomali.

“Mzee Mohamed , unasema Salma kafariki?”Aliongea Regina kwa mshangao mkubwa na hata Hamza alionekana kuchanganyikiwa pia.

“Afande nini kimetokea , hebu elezea vizuri niweze kuelewa”Aliongea na Afande Maningi alivuta pumzi huku akijitahdi kumtuliza mzee Mohamedi.

“Hamna utaratibu wa kuangalia taarifa ya habari?, yule muaaji maarufu wa wanawake amemuua mtu mwingine juzi”Aliongea kamishina.

“Niliona jana ila sikuitilia sana maanani hio taarifa , ila nimesikia amemkata mwanamke mdomo , kwahio alieuliwa ni Salma?”Aliuliza Hamza.

“Ndio, ni kwasababu tu hakukuwa na picha wala jina halikutajwa ndio maana hamkufahamu ni Salma”Aliongea na kauli ya Afande ilimfanya yule mzee kuanza kutoka machozi ya kiutu uzima huku akitaja jina la binti yake.

Hamza na Regina mara baada ya kuona namna mzee huyo alivyojawa na huzuni iliwafanya wote kushikwa na huzuni pia , shangazi aliekuwa pembeni alishindwa kujizuia na kutoa machozi.

“Kamishina unaonaje kwanza mkikaa chini na kuongea hili vizuri , nina uhakika asilimia mia moja Hamza hahusiki katika hili , tulikuwa wote hapa kwa siku zaidi ya nne , inawezekana vipi awe pia Dar es salaam na kumuua mtu?”Aliongea Regina.

Tokea wakiwa wadogo Salma hakuwahi kuwa mwepesi mbele ya Regina , siku zote alikuwa ni mwanamke wa mashindano akijitahidi kuonyesha alikuwa mzuri na akili nyingi kuliko yeye , lakni kifo chake cha ghafla hivyo kilimhuzunisha.

Lakini hata hivyo Regina alikuwa na uhakika aslimia mia moja Hamza sio muuaji kwani walikuwa wote.

Baada ya wote chini kukaa mazungumzo yalianza mara moja.

“Hamza nimekuja na mzee Mohamedi kwasababu hii kesi kidogo ina uzito wake na wewe pia una uzito wako ambao hatuwezi kuuweka wazi moja kwa moja , hata baada ya kuona kilichotokea mimi na timu yangu hatukuweza kuamini kama wewe ndio mhusika , lakini hii Vidio imetushangaza sana”

“Vidio gani unazungumzia?”Aliuliza Hamza kwa kusahngaa lakini palepale alikabidhiwa kishikwambi kwa ajili ya kuangalia kile wanachozungumzia na hata Regina na shangazi wote walijawa na shauku na walitaka kuona nini kinaendelea.

Sasa kitendo cha kuangalia Vidio hio Shangazi na Regina wenyewe walijikuta wakishikwa na mshangao mkubwa.

Alionekana Salma akitoka kwenye gari katika maegesho ndani ya jengo na mara baada ya kushuka mwanaume alimsogelea kwa nyuma na alionekana kumkumbatia huku akimgusa shingoni kwa wakati mmoja na akapoteza fahamu, baada ya pale alimbeba Salma na kumuingiza kwenye gari na kuondoka.

“Huyu mtu anafanana kabisa na mimi”Aliongea Hamza huku akionyesha hali ya kuchanganyikiwa , mtu huyo alikuwa na muonekano sawa na wa Hamza, lakini alijua sio yeye maana hakuwa eneo hilo na hajafanya kitendo hicho

“Nini kinaendelea , hili tukio limetokea lini?”Aliuliza Regina ambae mapigo ya moyo yalikuwa yakidunda kwa kasi mno.

“Ni juzi siku hio hio ambayo aliuliwa kikatili , haya maegesho ni ndani ya hoteli ya Dar international na baada ya kutolewa hapa alipatikana katika Lodge moja Tegeta akiwa amekwisha kuuliwa, majina yaliotumika kuandikisha chumba cha lodge hio ni ya kwako Hamza”Aliongea Kamishina na Hamza alizima Vidio ile na kisha alimwangalia mzee Mohamed ambae alikuwa na chuki kubwa mno.

“Nitaongea vitu viwili hapa kuhusu hili tukio , kwanza kabisa huyu mtu sio mimi licha ya kwamba anaonekana kufanana na mimi , pili nitamtafuta huyu mtu na nitahakikisha anakufa kifo cha kikatili kuliko binti yako”Aliongea na muda huo monekano wake ulikuwa umebadilika mno na kuwa wa kikauzu , kilichotokea kilimuudhi mno na kuona ni kheri mtu huyo angekuja kumuua yeye na sio kumchezea mchezo huo.

“Mzee Mohamedi , ni kweli kabisa Hamza hadanganyi , hii siku tulienda wote makaburini na tulirudi usiku , ukizingatia na muda tukio hili lilivyotokea haiwezekani akawa yeye”

“Mimi najuaje ni yeye ama sio yeye , nimejaribu kuulizia na nimeambiwa ni kweli Salma alikuwa na migogoro na huyu mtu , naona kabisa ana sababu ya kumua Salma”

“Kama kweli mimi ndio muuaji kwanini nitumie jina langu kwenye kujiandikisha Lodge na pia kwanini nichague sehemu ambayo naonekana kwenye kamera , hivi hamjawahi kujiuliza huyu muaaji Salma sio mtu wa kwanza kuua na katika mauaji yote hamkuweza kupata nyayo zake na ndio maana mkashindwa kumkamata lakini kwenye mauji haya akaacha viashiria vya wazi , hamuoni kuna walakini?”Aliongea Hamza na Mzee huyo hata yeye aliona ina mantiki lakini hakuongea chochote.

“Ni kweli kabisa anachoongea Hamza , hii kesi haikuwa ya miezi miachche imaenza muda mrefu sana na tulikuwa tukimfuatilia huyu muuaji bila majibu , kwa hichi kilichoendelea inaonekana kabisa Hamza anajaribiwa kutengenezewa mtego”Alionea Kamishina.

“Basi na tuseme ninaamini Hamza sio muuaji , hivyo niambieni nani kamuua binti yangu, nyie polisi mnatakiwa kuwa na majibu sio kutoa kauli za kumtetea mshukiwa”Aliuliza.

“Kuhusu hilo Mzee ni mpaka tufanye uchunguzi wa kina kumbaini muhusika”Aliongea Afande.

“Naomba nikuulize , hii siku wakati binti yako anaonekana katika maegesho ya hii hoteli , alikuwa na nani au alikuwa akienda kukutana na nani?”Aliuliza Hamza.

“Mimi nitajuaje hayo yote , Salma ni mtu mzima na sina tabia ya kumfuatilia anachofanya”

“Afande umeangalia watu ambao wana ukaribu na Salma ambao anaweza kuonana nao ndani ya hoteli hio?”

“Tumeangalia lakini hakukuwa na mtu yoyote ambae ana uhusiano na Salma?”Aliongea Afande.

“Kama ni hivyo ni mtu gani wa mwisho aliwasiliana nae?”Aliuliza na Afande huyo alifikiria kwa muda na kisha alifungua notebook yake na kuonekana kusoma..

“Kulingana na uchunguzi uliofanyika mtu wa mwisho kuwasiliana nae ni Rose Meneja wa duka la vito na urembo , na baada ya kumhoji Meneja Rosa amesema Salma alikuwa akiulizia kuhusu pete yake ya uchumba kufika nchini”

“Pete!, Salma alikuwa akiolewa mpaka kuhitaji pete?”

“Ndio , Salma na mpenzi wake Saidi walikuwa wakitarajia kufunga ndoa mwezi ujao”Aliongea Afande na kauli ile ilimfanya Hamza kukunja sura na palepale aliona kuna kitu hakipo sawa.















SEHEMU YA 96.

Kilichomfanya Hamza kuona kuna kitu ambacho hakipo sawa ni kwamba ile simu ya tukio la ufunguzi wa Albamu alimshuhudia Saidi akimfukuza Salma waziwazi na kumwambia wamemalizana , sasa alijiuliza imekuwaje tena wakataka kufunga ndoa mwezi ujao.

“Inamaana Salma na Saidi wamerudiana mpaka kufikia maamuzi ya kufunga ndoa?”Aliuliza Hamza.

“Ni kawaida kwa wapenzi kugombana na kupatana , usije ukasema Saidi ndio amehusika katika hili , Saidi ni kijana mpambanaji na mjasiriamali anaechipukia unadhani anaweza kufanya kitu cha namna hii kwa mtu kama Salma?”Aliongea Mzee Mohamed.

“Kila kitu kinawezekana , nilishawahi kumuona akigombana na Salma na sio mara moja tu ni zaidi ya mara mbili , kwanza huyo Saidi sasa hivi yupo wapi , hamjamchunguza?”Aliuliza Hamza.

“Hatukuona haja kwasababu hii siku ya tukio Saidi alikuwa katika ufunguzi wa maonyesho ya teknolojia chuo kikuu cha Dar es salaam na alialikwa kama mgeni rasmi , aliweza pia kuonekana kwenye redcapert siku hio akifanya mahojiano na waandishi wa habari”Aliongea Afande na kumfanya Hamza kuegamia kwenye sofa huku akifikiria kwa sekunde kadhaa.

“Mna picha ya Saidii wakati akitembea kwenye Redcarpet?”Aliuliza Hamza.

“Acha uvivu unaweza kutumia simu yako kuangalia mtandaoni huwezi kosa”Aliongea Regina huku akichukua kishikwambi chake na kuunganisha na internet na kuingia Youtube na ndani ya dakika tu alipata vidio hio.

Na kweli siku ya usiku huo Side alionekana kwenye ufunguzi wa tukio hilo na alifanya mahojiano mpaka na waandishi wa habari , alikuwa amevalia suti ambayo ilimfanya kuonekana mwanaume mtanashati mno.

“Nadhani umeona Saidi amehudhuria , hivyo mpaka sasa tuna uhakika sio yeye”Aliongezea Afande Maningi lakini muda huo tabasamu lilijitokeza katika sura ya Hamza.

“Huyu mtu … sio Saidi huyu”Aliongea akitingisha kichwa kukataa.

“Nini?” Wote walishangaa maana hawakuelewa alichokuwa akimaanisha.

“Macho yako nadhani yanakudanganya , huyu ni Saidi kabisa,unasemaje sio yeye , unatuona wajinga?”Aliuliza kwa hasira Mzee Mohamed.

“Kama Vidio inanionyesha nikiwa eneo la maegesho ya magari nikimteka Salma ilihali sio mimi , kwanini isiwezekane kwa Saidi kuwa tofauti na huyu?”Aliuliza Hamza na kuangalia sura za watu wote ambazo hawakumwelewa hata kidogo.

“Najua ni ngumu kuniamini ninachoongea hapa , lakini huyu mtu kitu pekee anachofanana na Saidi ni muonekano pekee lakini sio Saidi”

“Una sababu ya kusema hivyo Mr Hamza?”Aliuliza Afande Maningi.

“Sababu ni moja tu Saidi sio mtu wa kawaida na anaficha aonekane ni wa kawaida , lakini muonekano wa huyu mtu ni wa kawaida sana”Aliongea Hamza

“Unataka kumaanisha Saidi na yeye ana mafunzo ya mapigano au unamaansha nini?”Aliongea Afande huyo huku akionyesha kushangaa kama ni jambo ambalo haliwezekani.

“Mara ya mwisho kukutana na Saidi nilipatwa na hisia za ajabu sana , ninachojua tu sio mtu wa kawaida na anayo mafunzo ila sijui ni mafunzo ya aina gani, tukishampata tutapata majibu kamili”aliongea.

“Tuseme ni kweli haikuwa wewe , lakini bado ushahidi unaonyesha wewe ndio ulijiandikisha katika Lodge , unazungumzia vipi kuhusu hili, maana kwa maelezo mhudumu wa hio Lodge hawapokei wateja wasiokuwa na vitambulisho vya kura ama vya taifa?”Aliuliza Kamishna.

“Kamishina , kama mtu anao uwezo wa kubadli muonekano anashindwa vipi kudanganya jina na kitambulisho?”Aliuliza na Afande Maniingi alijiona kama mjinga kuuliza swali la namna hio.

“Kwahio machomaanisha huyu Saidi anaweza kuwa ndio muuaji wa watu wote hao?”Aliuliza Regina , alikuwa akimfahamu Saidi vizuri maana alikuwa mkurugenzi wa shirika kubwa la mtandao na hata kampuni yake ishawahi kufanya ushirikiano mara kadhaa.

Upande wa Mzee Mohamedi uso wake uliishia kujikunja huku akihisi kutetemeka , aliijiambia anaomba isiwe kweli la sivyo atakuwa yeye ndio aliemsababishia mtoto wake kuuliwa kwa kumlazimisha kuolewa na Saidi , lakini hata hivyo haikuingia akilini kabisa Saidi kuhusika.

“Kamishina nadhani hatuna muda wa kupoteza , nisaidie nipate kujua Saidi yupo wapi sasa hivi , mimi nitaenda kuonana nae”Aliongea.

Kwasababu ni swala ambalo lilikuwa likimhusu Hamza mwenyewe hakutaka kuchelewa kuondoka , hivyo aliwaaga Regina na Shangaz na kisha kwa kutumia gari ya kipolisi aliondoka kurejea jijini.

Saa tisa kama na nusu za mchana ndio waliweza kufika na walinyoosha moja kwa moja mpaka makao maku ya Vodocum , huku pia jeshi la polisi likifuatilia kwa ukaribu nyumba anayoishi Saidi pamoja na kampuni yake binafsi.

Ukiachana na Saidi kuwa Mkurugenzi wa kampuni kubwa ya mtandao wa simu lakini vilevile alikuwa ni mwanzilishi wa kampuni yake mwenyewe ya maswala ya kitafiti.

Walinzi wa eneo hilo mara baada ya kuona ni polisi wanaoingia hawakuwazuia.

Hamza na polisi wote waliingia kwenye lift moja kwa moja kuelekea katika ofisi ya Saidi.

Mara baada ya kufika nje ya mlango huo wa Mkurugenzi waligonga na sauti ya kuitikiwa kutoka ndani ilisikika.

Mara baada ya kuingia ndani waliweza kumuona Saidi akiwa amekalia kiti chake cha kibosi na alimwangalia Hamza na polisi hao kwa macho ya mshangao.

“Hamza , Kamishina , Baba… mbona mmekuja mpaka huku ofisini bila taarifa au ni juu ya kesi ya Salma?”Aliongea kwa mshangao lakini muda huo Mzee Mohamed peke yake ndio alieshikwa na hatia kumsingizia Saidi aliekuwa mkwe wake mtarajiwa.

“Saidi kuna kitu tunataka kukuuliza ndio maana nipo hapa na hawa polisi ni maswala ya ki uchunguzi hivyo wape majibu wanayotaka”

“Mzee wangu mimi sina tatizo , mnaweza kuuliza tu nitatoa ishirikiano wote”Aliongea Saidi.

“Ukweli ni kwamba kilichotuleta ni juu ya huyu Hamza , kasema wewe ndio muhusika, mim nimemkatalia maana nakuamini sana kijana wangu”Aliongea Mohamed.

“Hamza unanishuku mimi kwa mauaji! , wakati Salma anapitia ukatili huo mimi nilikuwa kwenye maonyesho ya wiki ya teknolojia , sidhani kuna hata haja ya kuuliza nilikuwa wapi maana kila kitu kipo mtandaoni”

“Hebu tuachane na maswala ya maonyesho kwanza , maana naona huna huzuni yoyote licha ya kuondokewa na mpenzi wako”

“Amekufa na hawezi kufufuka , nina stress ndio maana mpaka muda huu nimejiweka bize , ninachotaka ni kujua nani kahusika kumuua mpenzi wangu”

“Eti nataka kujua nani kamuua mpenzi wangu , kwa ninachokiona hapa ni kujifanyisha ulimpenda wakati hajawahi kuwa mpenzi wako kihisia, unadhani sijui kilichokuwa kikiendelea kati yako na Rehema?”Aliuliza Hamza.

“Rehema!?, mimi na Rehema kuna kipi kinaendelea kati yetu hebu acha kuongea ujinga?”

“Kwahio unasema humfahamu Rehema wakati mimi nina ushahidi wa picha?”Aliongea Hamza.

“Pumbavu!, hebu acha kunisingizia bwana , Salma nilimpenda tokea siku niliokunana nae nchini Canada na sikumpenda tu hata yeye alinpenda pia na kuthibitisha hili hata nilivyorudi nchini aliacha kila kitu China na kuja Tanzania kuendeleza penzi letu, sijawah kumsaliti hivyo hebu acha kuniletea habari za Rehema hapa”Aliongea.

Upande wa Mzee Mohamedi mara baada ya kusikia jina la Rehema mara moja alijikuta akiingiwa na shauku na kumuuliza Hamza.

“Rehema ni nani?”Aliuliza na Hamza aliishia kutoa tabasamu lililojaa kejeli kwa Saidi.

“Kuhusu Rehema hata mimi simjui , ni jina nimeamua kulitunga tu hapa kunogesha haya maongezi”Aliongea.

“Eeh!?”Mzee huyo hakujua Hamza alikuwa akikusudia nini lakini Afande Maningi aliekuwa akisikia kila kitu palepale aliweza kugundua maana ya Hamza kutaja jina la kubuni la Rehema ilionekana ilikuwa mtego.

“Upo sahihi huyu sio Saidi ndio maana amekubali kumjua Rehema ili hali umetunga”Aliongea

“Huyu sio Saidi kivipi?”Aliuliza Mzee Mohamedi huku akisogea karibu kuthibitsha lakini upande wa Saidi feki alionekana kuanza kupaniki.

“Vipi tena mkuu Side , umeshaishiwa na maigizo yako si ndio , mimi nimeamua kutumia jina la mtu yoyote lililonijia kichwani, au unataka kusema ni kweli una mahusiano na mtu anaeitwa Rehema?”Aliongea Hamza lakini upande wa Said feki hakuonekana kutaka kujibu.

Muda uleule Hamza alimsogelea Saidi na kisha akamkaba kolla ya shati lake kwa nguvu.

“Ongea wapi alipo Saidi na wewe ni nani na kwanini unafannaa nae?”Aliuliza na mkabo ule ulimfanya yule bwana feki kuanza kutetemeka.

“Hebu niachie , nitalipuka, niachie nakwenda kulipuka”Aliognea kwa nguvu

“Mlipuko?”

Hamza mara baada ya kufikiriia kwa sekunde alijua anachomaanisha ni nini.

“Laleni chini haraka?”Alongea kwa kuamrisha lakini sekunde ambayo kauli yake inamalizika yule Saidi Feki alilipuka kama bomu na kufanya moto kusambaa.

Boom!!

Mlipuko ule licha ya kwamba haukuwa mkubwa sana lakini uliharibu na kuungnza kila kitu kilichokuwa ndani ya ofisi hio na kufanya jengo kutikiska kwa nguvu.

******

Upande mwingine muda huo huo nje ya geti ya nyumba ya Prisila kulikuwa na utulivu mkubwa kutokana na asilimia kubwa ya wakazi wa eneo hilo walikuwa makazini na pia nyumba karibia zote zilikuwa na ukuta.

Muda huo alionekana Prisla ambae alikuwa ameshiklia mfuko akitembea usawa wa kusogelea geti lao , ilionekana ametokea dukani kwani alikuwa amevaa kinyubani zaidi.

Wakati akisogelea geti la nyumba yao gari ya kifahari aina ya Aston Martin Bd12 Convertible ilisimama na kufunguliwa mlango na palepale alionekana kijana mtanashati akishuka kutoka kwenye gari hio.

Kitendo cha Prisla kumtambua alieshuka kutoka kwenye ile gari alishangaa kidogo na kisha bila muonekano wake kubadilika alimsogelea.

“Saidi kwa kubadilisha magari ya kifahari tu hujambo, ndio maana watu wanakuita bosi wa magari”Aliongea Prisila

“Ndio kimeingia jana hiki chombo , ipo moja tu Tanzania nzima , hebu ingia kwanza ujaribishe uzuri wake”Aliongea Saidi huku akimfungulia Prisila mlango.

“Nina kazi nimeacha ndani nataka kwenda kuimalizia, Asante ila kwa leo hapana labda siku nyingine”Aliongea Prisila.

“Hebu ingia kwanza Prisila , kuna kitu muhmu pia nataka kukuambia , yaani hata kuingia tu kwenye gari yangu unaona nongwa?”Aliongea Saidi kwa sauti ya kubembeleza na upole wake mbele ya mwanamke huyo ulionekana kufanya kazi kwani mara baada ya Prisila kusita kidogo aliishia kungia

Mara baada ya mrembo huyo kuingia ndani ya gari na milango kufungwa Saidi palepale alitoa kiboksi kdogo cha rangi nyekundu cha kuhifadhia pete na kisha kumpatia Prisila.

“Hii ni kwa ajili yako Prisila”Aliongea huku akiweka tabasamu usoni.

Prisila aliishia kusita kidogo lakini alipokea kiboksi kile na kufungua ndani na macho yake yalichanua mara baada ya kukutana na pete ya karati tatu za madini iliotengenezwa na kampuni ya Tiffanny.

Ilikuwa pete nzuri mno na haikuhtaji maelezo mengi kuielezea kwani ni utaalamu wa hali ya juu uliotumika katika kutengeneza.

“Vipi umeipenda?”Aliuliza Saidi na dakika ile Prsila kwa haraka sana alimrudishia.

“Hiki ni kitu cha thamani kubwa mno , sistahli kupokea”Aliongea Prsila.

“Prisila maana ya kukupa pete hii nataka tufunge ndoa , nimekupenda kwa muda mrefu mno kuliko unavyodhani, kukupenda kwangu hakujaanza juzi na wala hakutaisha kesho , wewe ni malaika kwenye moyo wangu…”

Prisila hakutaka kuendelea kusikiliza na ghafla alimzuia asiendelee kuongea huku akionekana ashaanza kukasirika.

“Side naenda ndani nina kazi zinanisubiri”Aliongea huku akitaka kufungua mlango na kutoka lakini Saidi muda uleule alimzua kwa kumshika mkono.

“Unataka kwenda wapi , inamaana unanikataa kwasababu ya yule mpuuzi Hamza , Prisila najua unampenda yule mjinga lakini hakupendi na atakuchezea tu , mimi ndio mwanaume ninaekupenda, hebu achana na yule mpuuzi aliekosa aibu”Aliongea na muda ambao Prisila alitaka kujitetea alijikuta akiacha mara baada ya kumuona Said akiwa na sura yenye ukauzu ambao hakuwah kumona nao.

Prisila alijikuta akianza kutetemeka kwani Saidi alikuwa akitisha mno kana kwamba kuna nafsi imemtawala ndani yake.

“Saidi una matatizo gani?”

“Matatizo yangu ni kukupenda Prisila”

“Hata kama unanipenda , mimi sikupendi Saidi naomba uniachie niondoke”Aliongea huku akijitahidi kuutoa mkono wake ulioshikwa barabara lakini kadri alivyokuwa akihangaika alianza kuhisi kizungu zungu na aijikuta akigeukia kile kiboksi cha pete.

“Hayo marashi kwenye hiko kiboksi yalikuwa ni dawa?”Aliuliza kwa kulewalewa na Saidi alitoa tabasamu.

“Upo sahihi , ukisikia Pandora Box ndio hii sasa , kitendo cha kuifungua umejiingiza kwenye ndoto , haijalishi unakubali kuolewa na mmi au hutaki ila tunaondoka wote hapa na hakuna mtu atakae kuona tena”Aliongea akiwa siriasi lakini Prisila hakumsikia tena kwani alilegea na kupotelea usingizini.
 
Back
Top Bottom