SHETABI RUDISHA AKILI ZETU.
MTUNZI: SINGANOJR.
SEHEMU YA 147
Ijapokuwa Tresha alikuwa vizuri kwenye mapigano, alikuwa mdogo sana mbele ya Kanali Dastani ambaye alikuwa na mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi ya kuamsha pepo kwa kutumia mbinu ya Uwili kutoka umoja wa siri wa Black Trinity. Hivyo, kitendo cha kutaka kumkimbia alishindwa na kuishia kukandamizwa chini ya kitanda.
"Dastani, una nini wewe?" Aliongea Tresha akilalamika, akiwa hafurukuti kwa namna ambavyo Dastani alikuwa amemkaba.
“Nina nini! Wewe ndio unapaswa kujibu hilo swali?” Aliongea Kanali huku akimwangalia Tresha bila ya ishara ya utani hata kidogo.
“Niachie basi, nitakujibu. Unaniumiza ujue?”
“Ni mpaka useme. Kwanini unataka kuleta ujanja mbele yanguTresha? Unaniona dhaifu kwa sababu unadhani namuogopa hawala wako Eliasi, eh!?” Aliongea huku akizidi kumkandamiza na kumfanya mrembo huyo kuwa mwekundu na kuanza kukohoa mfululizo.
Kanali, mara baada ya kuona dawa imemwingia, alimwachia Tresha na kushuka chini ya kitanda. Kisha akasogelea mlango na kuulock kwa ndani. Tresha aliishia kushika shingo yake huku akikohoa kwa nguvu, akimwangalia Dastani kwa mshangao mkubwa.
“Anza kuongea Tresha. Una dakika tatu tu, la sivyo unatoka hapa ukiwa mfu. Sipo tayari kuona mipango yangu ikipata dosari kwa sababu yako.”
“Sio mipango yako, ni mipango yetu. Usisahau hilo.” Aliongea Tresha akiwa siriasi, alishuka chini akiwa uchi na kuchukua maji kunywa kidogo.
“Unasema ni yetu, ilihali unanisaliti na maadui zangu?”
“Sio kweli.”
“Eti sio kweli? Kwahiyo ile picha ni feki?” Aliuliza akiwa siriasi.
“Ile picha ni ya kweli ndio, lakini Dastani, hivi kwa akili zako, unadhani naweza kuwa na mahusiano na mtu kama Bakari kweli?”
“Nakusikiliza.” Aliongea huku akimwangalia.
“Ile picha ilipigwa mara baada tu ya kurudi kutokea Malaysia. Bakari Mgweno mwenyewe ndiye alinitafuta,” Aliongea na kisha alimwangalia Dastani kama alikuwa akiamini maneno yake.
“Kwanini alikuwa akikuhitaji?”
“Alikuwa akitaka taarifa ya mtu fulani kupitia koneksheni ya mtandao wa Binamu.”
“Taarifa ya mtu gani?”
“Dastani, nadhani unajua mishenzi zangu zote zinazohusisha watu wa Binamu sipaswi kukuambia, kama ambavyo siwezi kukuuliza mambo yanayoendelea chini ya kitengo cha Malibu.”
“Tresha, mpaka sasa nina mashaka na wewe. Na njia pekee ya kunifanya nirudishe imani yangu kwako ni kuniambia kitu cha kuniridhisha. Kwa muda mrefu tokea nipewe hii taarifa nimekuwa nikijiuliza sana, nikuulize au nianze kukufuatilia kimya kimya.”
“Kwanza, nani kanipiga picha na kukupatia?”
“Hilo sio muhimu. Unachopaswa kufanya ni kuongea, Tresha. Hili linagusa mipango yetu. Ila kama unataka kujitoa, mlango upo wazi! Wewe acha kuongea,” Aliongea Dastani na kisha alianza kurudia kutengeneza tai yake na kulitafuta koti kwa ajili ya kutoka.
“Alihitaji taarifa ya Edward Braxter Alonzo,” Aliongea na kumfanya Kanali macho yake kuchanua.
“Ndio nani huyo?”
“Mwanzoni sikuwa nikimfahamu na hata mimi ilinishangaza. Ila Bakari alihitaji kuingia kwenye mtandao wa Binamu kumfahamu huyu mtu, jambo ambalo nilimfanikishia,” Aliongea.
“Nadhani unajua juu ya uwepo wa Kanisa la Wabrazili hapa chini. Edward Braxter Alonzo ni ajenti chini ya kanisa hili,” Aliongea Tresha na palepale Kanali macho yake yalichanuna na kumkumbuka Amosi.
“Kama ni hivyo, kwanini Bakari akataka taarifa za Alonzo?” Aliuliza, na Tresha alitingisha mabega.
“Sijajua, lakini nilifanikiwa kumhoji Bakari. Hakutaka kuongea kirahisi, lakini kitu alichoniambia ni kwamba Alonzo yupo hapa nchini na kuna misheni anafanya. Pengine hiyo misheni ndiyo iliyomwibua Bakari. Sina uhakika, lakini baada ya kupata picha yake niliweka vijana kumtafuta Alonzo na nilifanikiwa kumpata,” Aliongea Tresha na palepale alichukua simu yake kutoka kwenye chaji na kisha alienda upande wa picha na kumuonyesha Kanali.
“Huyo unaemuona katika picha ndiyo ajenti Alonzo wa Kanisa la Wabrazili. Pembeni yake ni Amiri. Angalia, kuna picha nyingi sana ambazo vijana wangu wamezipiga kwa utaalamu wa juu bila yeye mwenyewe kujua,” Aliongea, na Kanali alianza kuangalia zile picha kwa kwenda mbele.
“Hebert, Amiri, Mellisa ni watu wachache sana ambao aliwaona katika picha hizo na wengine hakuwajua, na aliishia kukunja ndimi.”
“Unataka kusema nini? Maana naona hapa hata Bakari ni moja ya watu ambao wapo katika picha ya pamoja na huyu Alonzo. Kwanini akataka kujua taarifa zake?”
“Hilo sio swali sahihi. Unapaswa kuniuliza, uliza ni kwa sababu gani hawa wote walionekana nao katika picha?”
“Nakusikiliza.”
“Hawa wote ni wateja wa vyungu vinavyouzwa na kampuni tanzu ya Elix,” Aliongea Tresha, na kumfanya Amosi kumwangalia Tresha kwa umakini.
“Hili swala la vyungu ni swala ambalo lilikuwa likifanyiwa utafiti lakini baadaye ukaja kusitishwa. Na kwa ninavyojua, Binamu wanahusika na kinachosambazwa kupitia hivi vyungu,” Aliongea.
“Ni kweli unachomaanisha, lakini unajua Binamu ilivyo hasa namna uendeshaji wake katika kutunza siri na kuzifanyia uchunguzi. Mimi ni mtu wa pembeni sana, mimi ni kama wakala tu, na muda wowote naweza kufa au kupotezwa na Binamu,” Aliongea, na Dastani alikuwa akielewa kuhusu hilo.
“Na ndio maana kwa muda mrefu nimekuwa na wewe pamoja katika mpango ulioanzisha na ukakubali niwe mwenza wako. Licha ya kwamba ni kweli kinachosambazwa kupitia vyungu hatukijui, lakini kuna swala muhimu sana limejificha katika hivi vyungu.”
“Swala gani?”
“Night Shadows!” Aliongea Tresha akiwa na tabasamu, na kisha alienda kukaa mbele ya kioo akimwacha Kanali akiwa katika hali ya mshangao.
“Unataka kumaanisha nini, Tresha?”
“Niambie, bado unasema huu mpango ni wako mwenyewe au ni wa kwetu?” Alouliza huku akimwangalia Kanali kwa kejeli.
“Tresha, unajua fika nipo kwenye uchunguzi wa Night Shadows kwa muda mrefu sana. Kwanza, kwanini hukuniambia taarifa hii muhimu? Nishakuelezea kuna uwezekano Night Shadows na kupotea kwa Sedekia kukawa na uhusiano mkubwa lakini umeamua kukaa kimya. Tukiendelea hivi, unadhani naweza vipi kukuaminini kama wewe mwenyewe ndio unatengeneza mazingira ya mimi kutokukuamini?” Aliongea na Tresha alitoa tabasamu.
“Kuhusu Night Shadows kuwa na uhusiano na kupotea kwa Sedekia, sidhani kama lina uhusiano.”
“Nipe sababu ya kuamini maneno yako.”
“Nenda kwanza kaongee na Madam, na ukirudi majibu utakayoyapata nitakuelezea na cha kwangu. Pengine tunaweza kuwa na mwafaka mzuri zaidi,” Aliongea.
“Uko siriasi?”
“Unachelewa Dastani,” Aliongea, na kumfanya Kanali kukuna kichwa chake na kuangalia saa.
“Usije kuleta ujanja, Tresha, katika hili. Nadhani unanijua nilivyo?” Aliongea.
“Kama nilivyo na faida kwako, ndivyo ulivyo na faida kwangu. Kama nikikuacha, angalau niwe nishaingia kwenye levo ya kuinuka kwa nafsi,” Aliongea Tresha akiwa na tabasamu, na kauli hiyo ilimridhisha Dastani na kujiambia, ni kweli Tresha anaweza kuwa mjanjua lakini hawezi kumkimbia kama anataka kupata faida za mafunzo ya kuvuna nishati ya Uwili.
Mafunzo ya kuvuna nishati kupitia Uwili ni aina ya mfaunzo ambayo yanafanyika kwa mshabihiano au kunyonya. Ni aina ya mafunzo ambayo kiungu kikuu cha mafunzo hayo ni ngono.
*****
Hamza, mara baada ya kufika ofisini, hakuwa na utulivu kabisa na hakuwa na mpango wa kufanya chochote. Baada ya kuzungumza kwa dakika chache na Irene, ambaye alimuomba hela ya mafuta, alimtumia na kisha aliingia mtandaoni kupoteza muda.
Muda wa mchana, alishuka chini kwa ajili ya chakula cha mchana, lakini alishangazwa kutokumuona Yonesi. Alikuwa ameshazoea kula naye mara nyingi, hivyo alipomkosa alijisikia vibaya; isitoshe, alihitaji mtu wa kumchokoza.
Mwanzoni alidhani pengine Yonesi alikuwa ameshafika na kula na kuondoka, lakini alipokuwa akianza kula, alimuona Yonesi alievalia sare za ulinzi akiingia kwenye eneo hilo. Mrembo huyo mwanajeshi alichukua chakula na kisha aligeuka na kumwangalia Hamza. Alimwangalia kidogo kama mtu aliye na wasiwasi, kisha alitembea na kwenda kukaa pembeni yake.
Uhusiano wa Hamza na Yonesi haukuwa wazi bado. Hamza alikuwa akimtamani Yonesi, mwanamke mwenye umbo tata na rangi nzuri, lakini hakuwa na haraka.
“Yonesi, sikuhizi umebadilika. Nilidhani hutokuja kukaa hapa mwenyewe?” Aliongea Hamza na kumfanya Yonesi kupindisha midomo kidogo.
“Vipi huko ulikoenda, mambo yalienda sawa?” Aliuliza Hamza.
“Yalienda vizuri. Vipi huku kuna kilichotokea?” Aliuliza na kumfanya Yonesi kumwangalia Hamza kwa mashaka, kisha alitingisha kichwa kuonyesha hakukuwa na shida.
“Mbona ni kama una mawazo?”
“Hamna, ni swala dogo la kawaida tu linanisumbua,” Aliongea Yonesi.
“Swala gani? Niambie nikusaidie,” Aliongea Hamza akiwa siriasi, na kumfanya Yonesi kula kidogo, vijiko viwili vya pilau, kisha aliinua macho yake na kumwangalia Hamza. Alipokutana na macho ya Hamza, ujasiri ulionekana kama ulimpotea.
“Yonesi, niambie. Usiponiambia nitajua vipi kukusaidia?” Aliongea Hamza.
“Naolewa mwenzio,” Aliongea Yonesi akionekana kuwa na ujasiri wa kuweka wazi maamuzi yake.
Hamza alijikuta akinywea kama amemwagiwa maji ya barafu.
“Unaolewa na nani?” Aliuliza Hamza kwa mshangao.
Yonesi alitazama mwonekano wa Hamza, mapigo yake ya moyo yalianza kudunda haraka, na palepale aliangalia chini.
“Ni Mdudu, mchumba wangu wa zamani. Nadhani unamkumbuka,” Aliongea Yonesi.
Hamza alijikuta akikunja uso. Alimkumbuka vizuri Mdudu, Afande kutoka kikosi cha Malibu.
“Umelazimishwa na familia yako kuolewa au ni familia ya Mdudu iliyokulazimisha?” Aliuliza Hamza.
“Hakuna aliyenilazimisha. Naweza kusema sina hisia zozote mbaya juu ya hili,” Aliongea Yonesi.
“Kwahiyo unamaanisha una mpenda Mdudu au vipi?” Aliuliza Hamza, na Yonesi alitingisha kichwa kukataa.
“Unamjua vizuri Mdudu?” Aliuliza Hamza.
“Sijamjua vizuri,” Alijibu Yonesi.
“Kwahiyo unataka kuolewa na mtu ambaye humpendi wala humjui vizuri au unataka tu kuolewa katika familia ya Mdudu?”
“Sio kwamba napenda kuwa katika familia yao. Sitaki kuwa mwanamke chombo cha starehe. Nataka kuendeleza kizazi cha familia yetu na kupata watoto.”
“Sasa kama unataka watoto, lazima iwe Mdudu?” Aliuliza Hamza na kumfanya Yonesi kukunja uso kidogo.
“Wewe huelewi kitu ndio tatizo lako.”
“Sielewi nini?”
“Mimi ni mwanamke, nina miaka 28 tayari. Siwezi kuendelea kuwa bachela na kuishi bila ndoa na kuendelea kujitenga mbali na familia yangu,” Aliongea Yonesi, na kauli hiyo ilimshangaza Hamza.
Hamza hakuwahi kuona uhalisia wa mambo katika mtazamo wa Yonesi. Siku zote alikuwa akiangalia vitu katika mtazamo wake, aliona ni sahihi kwa mwanamke ambaye tayari amefikisha umri huo kuwa na ndoa na familia, kama ilivyo kwa wasichana wengi wa rika lake.
“Kesho naelekea nyumbani Dodoma. Kesho kutwa ni sherehe ya babu ya kuzaliwa na ya kutimiza miaka tisini. Nataka pia nikasalimie ndugu zangu. Nimekuwa mbali na nyumbani kwa zaidi ya miaka mitatu. Mama yangu analalamika hali yake ya afya sio nzuri siku hizi na mvi zinazidi kukivamia kichwa chake. Kaka zangu wote watatu wameshaoa na wanafamilia zao. Ni mimi peke yangu ambaye sina mwelekeo,” Aliongea Yonesi.
“Nilivyomuona mama yangu kupitia video call, alivyokunjamana uso, nimejikuta nikishikwa na hatia mno. Ukweli ni kwamba najua mimi na Mdudu tunaweza tusieandane sana, lakini angalau namjua ni mtu wa namna gani. Ni heri yeye namjua na naweza kuendelea kumjua tukiwa pamoja kuliko wazazi wangu wakinitafutia mtu mwingine ambaye simjui kabisa,” Aliongea Yonesi kwa sauti ya chini.
Hamza alijikuta akibakia kimya. Hakujua hata aongee nini, kwa sababu kila kitu alichoongea Yonesi kilikuwa sahihi. Alikuwa mtoto wa familia kubwa, na kuolewa na mtu yoyote wa kawaida ni kitu ambacho hakiwezekani. Familia ya Mdudu ni kati ya familia kubwa nchini kisiasa na kijeshi ambazo pia zina heshima. Hata kama Yonesi aolewe katika familia hiyo, haimaanishi ataenda kuteseka.
“Hamza!!”
Yonesi aliita huku akitabasamu kidogo. Wakati huo hakuwa tena kiongozi wa ulinzi ndani ya kampuni, bali alikuwa msichana au mchumba wa mtu.
“Ukweli ile siku Mwanza wakati tukihakikisha ulinzi wa Mkurugenzi na baadae wewe kuja kumchukua, ghafla nilihisi kwamba licha ya kwamba kunaweza kuwa na kitu kinachoendelea kati yetu, lakini bado utabakia kuwa mume wa mtu. Kuna msemo unasema ‘hata kiwe kizuri vipi kama sio chako ni bure’. Wewe unaonaje?”
“Sikudhania bado unaukumbuka ule usiku, samahani siku ile nilikupotezea,” aliongea Hamza huku akilazimisha tabasamu.
“Huna haja ya kuniomba msamaha na hukunifanyia lolote baya pale. Wewe sio mtu wangu na kipaumbele chako ilikuwa ni usalama wa bosi wetu.”
Ijapokuwa mwanamke huyo aliongea akiwa na tabasamu, bado ilimfanya Hamza kukosa amani katika moyo wake.
Hamza alijikuta akikumbuka siku ya kwanza aliokutana na Yonesi katika eneo hilo, namna watu walivyokuwa wakiwaangalia, namna walivyogombana mpaka kupatana na kuwa na ukaribu mkubwa. Ijapokuwa hawezi kuchukuliwa kama uongo, lakini kwa muda waliokuwa pamoja ilikuwa ngumu kusema hawakuwa na hisia kati yao za kimapenzi.
“Chakula kinapoa, ngoja nile haraka maana kuna kazi napaswa kwenda kufanya, pia nitaenda kumuaga Regina baadae kama sio kuacha kazi kabisa,” aliongea Yonesi na palepale aliendelea kula.
Hamza, upande wake, hamu yake ya kula ilimpotea kabisa. Mara baada ya kula, waliondoka wote pamoja. Mara baada ya kuingia kwenye lift, Yonesi palepale aligeuka na kumwangalia Hamza.
“Vipi ulinipenda?” aliuliza Yonesi na swali lile lilimshitua mno Hamza. Hakujua hata namna ya kujibu. Kama angesema ndiyo, maana yake swali lingine lingekuja; je, utanioa? Je, utanifanya niwe na familia? Alitaka kusema hapana lakini bado kuna kitu kilikuwa kinamzuia. Mpaka lift inafunguka hakuwa ametoa jibu na Yonesi bila kuangalia nyuma alitoka haraka haraka na kupotea kwenye macho yake.
Hamza alijikuta akibakia mdomo wazi, akimwangalia Yonesi akitokomea kwenye korido na palepale wazo la hatomuona tena lilichipuka katika akili yake.
Hamza mara baada ya kupoteza muda ofisini saa kumi na moja kama na nusu hivi, alichukua funguo za gari na kutaka kwenda kwenye ofisini ya Regina lakini alikumbuka mwanamke huyo alishajitenga nae na kutumia gari yake.
Kufikiria hivyo hata hamu ya kurudi nyumbani ilipotea na palepale aliona ni vizuri akienda sehemu kupoteza muda. Baada ya kufikiria cha kufanya, wazo la kumpigia rafiki yake Amiri liliibuka na alifanya hivyo mara moja.
Simu ilipokelewa haraka haraka na Amiri na kusalimiana, Hamza alimwambia hayupo kwenye mood nzuri kama vipi wakutane sehemu wapoteze muda na Amiri alimwambia itakuwa vizuri kama watakutana Karambezi kwanza waongee na baadae ataungana na mpenzi wake Mellisa.
Hamza mara baada ya kusikia baadae Mellisa atakuwepo aliona pia atafute mtu wa kuwa nae muda huo ili asijisikie mpweke na mtu aliemjia akilini muda huo alikuwa ni Eliza.
“Unaonaje tukikutana kabisa na wapenzi wetu kuliko kuwasubiri?” aliongea Hamza.
“Itakuwa vizuri Bro! Kwahio saa ngapi itakuwa muda mzuri?”
“Kwanzia saa moja moja hivi, itakuwa vizuri,” aliongea Hamza na Amiri alikubali palepale.
Hamza baada ya kumaliza maongezi yake na Amiri alikata simu na palepale alimpigia Eliza. Wakati anapiga Eliza, alikuwa akijiandaa kutoka kurudi nyumbani na mara baada ya kupata mwaliko kutoka kwa Hamza alijikuta akisikia furaha, lakini kidogo alishangaa maana Hamza alikuwa tofauti na alivyomzoea. Ili kupunguza watu kuwagundua waliamua wakutane nyumbani kwa Eliza kila mtu kwa wakati wake ndio watoke pamoja.
Hamza mara baada ya kufika, Eliza alikuwa amekwisha kufika tayari na alikuwa bize akifanyau usafi. Licha ya kuishi kwenye nyumba kubwa aliyopewa na kampuni, lakini hakuwa na mfanyakazi na aliishi peke yake. Kitendo cha kuingia na kukutwa akiwa bize na Hamza, alijikuta akishikwa na aibu za kike.
“Subiri kidogo naweka mazingira sawa, jana nilikuwa na marafiki zangu ndio maana unaona kumechanguka,” aliongea.
“Hata sijali,” aliongea Hamza akiwa ametabasamu lakini kwa namna moja aliguswa na namna mwanamke huyo alivyokuwa akimchukulia siriasi. Kwa kawaida, Eliza anapokuwa nyumbani alikuwa akiishi kibachela zaidi.
Eliza alikuwa ametoa koti lake na kutoa kibanio cha nywele na kufanya ziachie. Kutokana na mavazi yake na alivyokuwa akihangaika ilitosha kumfanya Hamza kupatwa na mzuka, lakini siku hiyo alikuwa amepoa mno na kumfanya akae kimya akimsubiria.
Eliza mpaka anamaliza kuweka mpangilio sawa aliishia kugeuka na kumwona Hamza ambaye alikuwa bize akimwangalia na alishindwa kujizuia na kuona aibu za kike lakini akishangazwa na mwonekano wake kwa wakati mmoja.
“Una tatizo gani leo wewe? Mbona nahisi kama haupo sawa?”
“Sipo sawa kivipi?”
“Nashindwa kujua, lakini naona kama sio wa siku zote.”
Hamza aliishia kusinyaza macho yake tu. Ilionekana Eliza anamjua sana mpaka kuona hayupo sawa. Kila siku ambayo anapokuwa karibu na mrembo huyo alikuwa akimwingia moyoni sawa, hususani upole wake.
Hamza aliishia kusimama na kisha alimsogelea na kumkumbatia. Aliinamisha kichwa chake na kumbusu shavuni na kwenye lipsi kisha akamshika mabega na kumwangalia usoni.
“Lizzy, vipi sio ngumu kuwa katika mahusiano na mimi?” aliongea Hamza na kumfanya mrembo huyo ambaye hisia zake ziliamshwa na joto la Hamza kushangazwa na swali lake.
“Kwanini unauliza hivyo? Sioni shida yoyote, una nini lakini wewe leo?”
“Ni stori ndefu, hata hivyo nimeboreka sana leo nataka tuongee kidogo.”
“Si umesema tunatoka, unaonaje tukienda kuongea huko huko wakati tukipata chakula cha usiku?”
“Itakuwa vizuri kuna rafiki yangu pia nina miadi naye Karambezi, anakuja na mpenzi wake sio mbaya tukiungana nao,” aliongea na Eliza hakuuliza sana na kuishia kutingisha kichwa.
“Nisubiri nibadilishe,” aliongea akitabasamu na kukimbilia chumbani kwake.
Hamza alitaka kukaa chini kusubiri lakini aligundua baada ya Eliza kuingia ndani hakuwasha taa.
“Eliza, mbona huwashi taa au unaogopa nikikuchungulia?”
“Hamna, bulb imeuungua na sijapata muda wa kutafuta mtu kunisaidia kuibadilisha.”
“Oh! Kubadilisha bulb mpaka umwite fundi, bulb mpya iko wapi nikusaidie kubadilisha?”
“Sijanunua bado, sijui ni bulb ya aina gani napaswa kununua, labda uangalie kwanza ndio nikanunue,” aliongea.
Taa za nyumba hiyo zilikuwa zile za kufitishwa kwenye kifaa maalumu ndani na kisha kufunikwa na kioo kwa nje.
Hamza aliingia ndani ya chumba cha Eliza na kumwangalia namna alivyokuwa bize akibadilisha. Mrembo huyo alikuwa bize akivua suruali na kumfanya abakie na nguo nyeupe ya ndani na mara baada ya kumuona Hamza ameingia, alianza kushikwa na wasiwasi.
“Hamza! Una nini wewe?”
Aliuliza Eliza si kwa sababu Hamza alikuwa akimwangalia, bali utofauti wa Hamza kukimbilia kuangalia taa ilioungua, tofauti na siku zote kama angeingia hapo angemrukia kwanza kwa namna alivyokuwa uchi.
“Nishajua ni taa ya aina gani, ngoja nikanunue kwanza niiweke kabla ya kutoka,” aliongea Hamza.
Eliza aliishia kumshangaa tu Hamza namna alivyo siriasi na joto la moyo lilimvaa palepale na kuishia kutingisha kichwa.
“Kuna kitu kingine cha kurekebisha, usisahau tulikutana mara ya kwanza kwa sababu ya ufundi?” Aliongea Hamza akiwa na tabasamu na kumfanya Eliza kucheka.
“Hamna, ni bulb tu. Ila unaonaje tukienda kununua na kuikweka kwenye gari na kisha tutoke na ukirudi ndio unaibadilisha?” Aliongea Eliza, na Hamza aliona ni wazo zuri zaidi na alitabasamu baada ya kuona limekaa kimtego.
Baada ya Eliza kujiandaa na kubadilisha, walitoka mkono kwa mkono na kuingia kwenye gari ya Hamza na kisha wakapitia dukani na wakaondoka kuelekea Karambezi.
Ilikuwa ni saa moja kasoro robo hivi wakati wanafika na kwa sababu Hamza ameahidi kukutana na Amiri saa moja kamili, ilibidi wamsubiri.
Wanaume wachache waliokuwa hapo waliishia kumkodolea Eliza macho; kama kawaida, mrembo huyo alikuwa na mvuto wa ajabu mno licha ya kutokuwa mzuri sana kumzidi Regina.
Mara baada ya kukaa, Eliza aliagiza keki ndogo na kula na Hamza huku Hamza akiagiza wine. Hamza alichukua muda huo kumwambia Eliza kile kilichotokea kati yake na Regina, pia taarifa ya Yonesi kwenda Dodoma kuolewa. Eliza alisikiliza bila kumwingilia Hamza huku muda mwingine akitingisha kichwa na mwingine akikunja sura. Mara baada ya kumaliza, Eliza alikunywa kidogo wine na kumwangalia Hamza kwa umakini.
“Hamza, unachukiza kweli, yaani tupo out lakini unachoniambia ni mambo yalivyokuendea vibaya na wanawake wengine,” Aliongea Eliza akilalamika.
“Lizzy, tatizo sina kingine cha kuongea, leo siku nzima nimekaa nakufikiria na kuona pengine siwatoshelezi kabisa. Siku familia yako ikiwa katika tatizo unapaswa kuniambia; ukijiona mpweke, nitafute muda wowote,” Aliongea Hamza kwa sauti ya chini lakini yenye uzito.
“Ukweli kwangu ni sawa tu hata tukiwa kama hivi kwa wiki mara moja. Isitoshe, nina mambo mengi pia ya kufanya. Kuhusu wewe na bosi, sina haki ya kuongea chochote. Isitoshe mimi ni sehemu ya matatizo yenu. Lakini nimefikiria na kuona mwonekano wako wa sasa unakosa kujiamini kabisa. Yaani upo kama vile unajishuku kwamba huwezi kumfanya Regina kuwa na furaha. Sasa usipojiamini, unadhani anaweza kukuamini vipi?”
“Kujiamini?”
Hamza alijikuta akiwa kimya kwa sekunde kadhaa na ni kama Eliza amemkumbusha kitu. Mchana yote alijihisi moyo wake ni kama umekuwa mtupu huku akishindwa kujua nini kimekosekana, lakini muda huo ni kama sasa amejua nini amekosa. Tokea mwanzo mpaka dakika hiyo, iwe ni Regina, Eliza, Yonesi au Yulia, ukweli ni kwamba wanawake hao wote wanaishi maisha yao na wanafanya wanachotaka.
Kutoka mwanzo mpaka mwisho, mtu ambaye alihisi amepotea ni yeye mwenyewe.
“Ndio, kujiamini. Unajua kitu ambacho kinanivutia kutoka kwako muda mwingi ni pale unavyofanya vitu bila kufikiria kwa matakwa yako mwenyewe na sio kulazimishwa. Ijapokuwa mambo yako muda mwingine yanakarahisha, lakini ndio inakufanya kuwa tofauti na wanaume wengine.”
Mara baada ya kuongea hivyo, sura ilianza kuiva kwa aibu. Aliishia na kukumbuka ile siku Hamza alivyovamia ofisini kwake na kumfanya juu ya meza.
“Mimi sio wewe, hivyo ni ngumu kujua unachofikiria. Lakini ilimradi utaendelea kuwa wewe bila kuigiza kuwa mtu mwingine ,hiko ndio kila kitu na kitakachobakia ni upande wetu kuchagua tuondoke au tubakie”Aliendelea kuongea Eliza.
SEHEMU YA 148.
Hamza alishindwa kujizuia na kuvuta pumzi nyingi sana huku akimwangalia mwanamke huyo kwa hisia kali. Ghafla tu palepale aliamka alipokuwa amekaa na kwenda kumkumbatia Eliza kwa nyuma na kuinamisha kichwa chake na kumkisi kwenye lipsi. Tukio lile sio tu kwamba lilimuogopesha Eliza, lakini pia liliogopesha wateja wengine na wahudumu ndani ya mgahawa huo.
“Unafanya nini, kuna watu wengi hapa,” aliongea Eliza huku akiwa ameiva na kumsukuma Hamza mbali.
“Si umesema kinachokuvutia kwangu ni kutokujali wengine wananiangaliaje? Tatizo unavutia sana nimeshindwa kujizuia kutokukukiss.”
“Nimesema ndiyo, lakini kuna mazingira,” aliongea Eliza.
“Bora tumekuja hapa maana umerudisha hali yangu katika hali ya kawaida, asante kwa ushauri wako na tukitoka hapa mumeo nitakwenda kununulia zawadi.”
“Mume?” Eliza alishindwa kujua namna ya kupokea kauli hiyo.
“Ndio, si lazima muda wote kuniita Hamza. Kuanzia sasa niite Husband, na mimi nitakuitwa Wife Lizzy, sawa?”
“Akuu! Sitaki,” Eliza moyo ulimjaa utamu lakini mdomo wake ulikataa kutamka. Hamza hakujali na aliendelea kumwita Wife Lizzy kwa sauti mpaka watu waliokuwa ndani ya eneo hilo kuwaangalia na kuishia kucheka wakiona Hamza alikuwa amechanganyikiwa na mapenzi ya mrembo Eliza. Hata hivyo, waliona anayo haki ya kuchanganyikiwa maana Eliza alikuwa akivutia mno. Japokuwa Hamza alikuwa kama kichaa, waliokuwa na wenza wao walitamani kuwa na mtu kichaa kama Hamza.
“Sawa, nitakuita Husband acha makelele. Yaani huna aibu wewe. Halafu hujanioa huoni sio vizuri mimi kukuita mume?” Aliongea Eliza, akimziba Hamza mdomo maana alijua ataendelea.
“Ndio, ijapokuwa hatuwezi kufunga ndoa rasmi, lakini hakuna tatizo mimi kukuita mke. Tuna uhusiano mzuri, kuna haja gani ya kufunga ndoa ndio tuitane mke na mume?” Aliongea Hamza na kumfanya Eliza kucheka hata asijue anacheka nini.
“Dakika chache zilizopita ulikuwa mpole, lakini sasa hivi naona usharudi kwenye hali yako na unaanza kuniongopea na maneno ya kunifariji.”
“Haha...Lizzy wife ukiendelea kuongea hivyo nitaendelea kupiga makelele ujue?” Aliongea Hamza na kumfanya Eliza kutabasamu na alimshika mkono Hamza huku akimwangalia kwa kurembua.
“Hubby ni zawadi gani umesema unataka kuninulia?”
“Nitakununulia kitu chochote ghali unachotaka, mfano mkoba wowote wa kampuni maarufu duniani unaotaka,” aliongea Hamza huku akijiwazia kwamba angetumia koneksheni yake kuweza kupata bidhaa ya bei ghali kama zawadi.
“Kuna mikoba maarufu ya Prada imeingia sokoni na ni habari ya mjini kwasasa, unaonaje ukinunulia huo?”
“Ushasema ishakuwa maarufu, maana yake ipo mingi mtaani. Kwanini nisikuchukulie Herms, mikoba adimu na ghali ?”
“Hiyo ni ghali sana na staili yake hainipendezi na nitashindwa kutoka nayo. Napenda zawadi ninayochagua bwana, utaninunulia au vipi?” Aliongea kwa pua na kumfanya Hamza ashindwe kuongeza eneo, ilionekana mrembo huyo hakujali bei bali kinachomvutia.
“Nitakununulia, nionyeshe staili yake iwe rahisi kuagiza uletewe,” aliongea Hamza na Eliza alitabasamu kama mtoto na kumuonyesha haraka haraka mkoba anaotaka.
Muda huo simu ya Hamza ilianza kuita, na alipoangalia anayepiga ni Amiri, na ndipo anakumbuka alikuwa na miadi naye eneo hilo hilo. Kutokana na kuwa bize na Eliza alikuwa amemsahau kwa muda.
“Bro, ushafika, sisi tunakaribia?”
“Tupo hapa muda mrefu tu, njoo utatukuta,” aliongea Amiri na kukata simu.
“Ni nani huyo? Ndio rafiki yako uliyekuwa ukisema unakutana naye hapa?”
“Ndio,” aliongea Hamza na ndani ya dakika chache tu Amiri aliingia ndani ya eneo hilo akiwa ametangulizana na mwanamke mrembo mno. Hamza alikuwa akimjua ni Mellisa, mwanamke aliyetokea kupendwa sana na Amiri.
“Braza!” Aliita Amiri akiwa na tabasamu kama lote na Hamza aliamka na kukumbatiana naye kishikaji na kisha akawakaribisha.
“Mellisa!” Aliita Eliza kwa mshangao kidogo baada ya kukutananisha macho na mrembo huyo aliyekuja na Amiri.
“Mnafahamiana?” aliuliza Amiri huku akimwangalia Eliza kwa macho ya mshangao na kisha alimwangalia Hamza, ilikuwa ni kama hajategemea Hamza angekuja na mwanamke mwingine tofauti na Dina ambaye amemzoea. Ila alishangaa baada ya kuona ni mrembo mwingine.
“Ni bosi wangu,” aliongea Mellisa kwa wasiwasi kidogo na Eliza alitabasamu.
“Ah! Nakumbuka Amiri uliniambia mpenzi wako ni mfanyakazi wa benki ya Dosam Commercial Bank?”
“Ndio, Mellisa ni Meneja tawi la Ubungo. Mellisa huyu ni Hamza, rafiki yangu niliyekuwa nikikuambia.”
“Namjua vizuri tu,” aliongea Mellisa akitabasamu na kumfanya Hamza amwangalie.
“Shemeji, umenijulia vipi?”
"Mashindano ya Basketball na pia nilisikia wewe ndio uliehusika kuwaokoa wafanyakazi wengi wakati wa Tour, wafanyakazi wengi wanakufahamu kama PA wa Mkurugenzi," aliongea Mellisa kwa uchangamfu, akimfanya Hamza kukuna kichwa huku akitambua umaarufu wake.
Asichokijua Hamza alikuwa maarufu sana sio tu kwa ujasiri wake na uwezo wake wa kucheza basketball lakini vilevile utanashati wake , uliwakolea sana warembo wengi na kumtamani lakini kulikuwa na minong’ono ya chini chini ya Hamza kuwa na uhusiano na Regina bosi wa kampuni ila hakukuwa na uhakika na kufanya wakae mbali.
"Anyway, Amiri na Mellisa, huyu mrembo hapa ndio mpenzi wangu. Mellisa, kuwa huru, hapa hayupo kama bosi wako, ila kama mpenzi wangu na shemeji yako," aliongea Hamza, huku Eliza akiwa ameiva kwa hisia kutokana na utambulisho huo na aliishia kuangalia na Mellisa na kutoa tabasamu.
Mellisa alikuwa mfanyakazi wa kwanza wa Dosam kufahamu rasmi kuhusu mahusiano ya Hamza, ukimtoa Yonesi.
"Kaka una bahati," aliongea Amiri kwa sauti ya utani, na wote walijikuta wakicheka. Lakini Amiri alijua undani wa maneno yake, akishangazwa na Hamza, ambaye alikuwa na mahusiano na mrembo Dina, na sasa tena anaonekana na Eliza.
Kujiamini kwa Mellisa na Eliza kulirudisha hali ya utulivu ndani ya dakika chache, na mazungumzo ya hapa na pale yaliendelea.
"Bro, nimeshangaa kusikia umeacha chuo?" aliuliza Amiri baada ya kutoa oda yake pamoja na Mellisa.
"Umezipataje taarifa?" Hamza alijibu kwa shauku.
"Kuna watu walikuja kunihoji juzi na kuniuliza maswali kuhusu wewe. Ndio walioniambia umeghairisha masomo. Nilishangaa, bado miezi miwili tu kumaliza," aliongea Amiri, na kauli hiyo ya kuhojiwa ilimfanya Hamza kukunja sura.
"Unasema kuna watu walikuja kukuhoji, ni watu gani?" aliuliza Hamza, akiwa amekaza macho.
"Walijitambulisha kama wafanyakazi wa kampuni ya BTX. Waliongea wanajua mimi na wewe ni marafiki. Eh, tena wameniuliza kama najua wewe ni daktari, swali ambalo lilinishangaza," aliongea Amiri, huku Mellisa akimwangalia Hamza kwa mshangao.
Hamza alihisi kuna kitu hakipo sawa. Kufuatiliwa hadi chuoni kulimaanisha watu hao wamedanganya, na hakuwa na uhakika kama kweli walikuwa wafanyakazi wa kampuni. Lakini ni watu gani waliokuwa wanamtafuta?
"Ndio, mimi ni Cardio-thoracic Surgeon," aliongea Hamza bila kubadilisha mwonekano wake.
"Bro, una siri nyingi sana! Ila hiyo fani ni ya watu wachache sana waliobobea hapa nchini. Kwa nini ukaingia chuo kusomea uchumi?" aliuliza Amiri, akiwa na mshangao.
"Nilijiunga kuongeza maarifa tu. Kwa muda mrefu, ukiachana na maswala ya matibabu, nilivutiwa sana na maswala ya uchumi, ndio maana nikachukua kama Side Course," alijibu Hamza, huku Amiri akitingisha kichwa, ingawa bado alionekana hajashawishika kabisa na maelezo hayo. Hata hivyo, alisoma mazingira na kugundua Hamza hakutaka kuzungumzia sana kuhusu hayo.
"Anyway, kwa sasa sina vielelezo vya kunitambulisha kama daktari hapa nchini, ndio maana nipo kila mahali ili kusurvive," aliongea Hamza, na Mellisa ndio alikuwa wa kwanza kutingisha kichwa, akionyesha kuelewa.
"Ndio maana unafanya kazi kama PA, Kuwa msaidizi wa bosi Regina ni nafasi kubwa sana.." Mellisa aliongea, lakini Hamza alitabasamu bila kuongezea neno.
Walikaa ndani ya eneo hilo kwa muda mfupi sana na kisha walitoka na kwenda kuangalia Sinema kwa kutumia VR na mpaka wanakuja kutoka ilikuwa ni usiku wa saa sita kwenda saa saba hivi na waliagana na kila mtu alichukua njia yake.
Hamza na Eliza baada ya kufika kazi ya kwanza ilikuwa ni kubadili taa , kazi amabyo Hamza aliifanya kwa dakika chache tu mpaka kumaliza.
“Lizzy , tukaoge basi”Aliongea Hamza baada ya kumaliza.
“Hurudi nyumbani leol?”Aliuliza Eliza akiwa katika hali ya kumshangaa Hamza.
“Muda umeenda sana haina haja ya kurudi . Isitoshe itakuwa vizuri kama tutalala wote”Aliongea Hamza akimkonyeza.
“Lakini bosi Regina bado amekukasirikia , usiborudi si itakuwa unachochea zaidi moto?”Aliongea Eliza kwa wasiwasi , lakini Hamza alimsogelea na kisha alimshika kiuno kwa mkono mmoja huku mwingine akishika eneo la shavu lake karibu na sikio.
“Tuachane nae kwasasa , nikimnyenyekea sana nitawezaje kuendesha maisha yangu baadae? Kwa vyovyote vile hakuna mtu pia wa kushindana na mimi likija swala la mwanamke , siku chache zijazo nitafikiria namna ya kumbembeleza”Aliongea Hamza.
“Unaongea kama bandidu sasa , ngoja akusikie uone kitakachokutokea”Aliongea Eliza huku akicheka.
“Hehe . ni siri yetu hii”Aliongea Hamza na kisha akaanza kumkisi kuanzia kichwani na kushuka chini.
Dakika chache mbele kilichosikika ni miguno ya kimahaba kutoka kwa Eliza.
*****
Siku iliofuata katika kituo cha treni ya mwendokasi ndani ya jiji la Dar es salaam, alionekana Yonesi akiwa amesimama pembeni pamoja na abiria wengine waliokuwa wakisubiria kuingia kwenye treni akiwa ameshikilia begi lake kubwa.
Alikuwa akigeuza geuza macho kuangalia upande aliotokea , ijapokuwa kwenye kampuni aliaga kama anaenda likizo kwa muda lakini hakuwa na uhakika kama angeweza kurudi tena kama mfanyakazi
Ingekuwa ni mwaka mmoja nyumba mtu pekee ambae angemmisi ndani ya hili jiji ni Regina pekee , lakini siku hio wakati wa kujiandaa kurudi nyumbani kwao kulikuwa na kitu kingine kwenye moyo wake kilichomfanya kutotamani kusafiri.
Alijikuta akivuta pumzi nyingi na kutingisha kichwa chake kama mtu ambae anapotezea kile anachokiwaza na kisha alishika begi lake na kuliburuza kusogelea mlango wa treni ambayo ilikuwa ikianza kupakia abiria.
Mara baada ya kuingia aliitafuta siti yake na kukaa , licha ya kwamba hela alikuwa nazo lakini hakukata tiketi ya daraja la kwanza wala nini , alikaa katika siti za kawaida tu kama abiria wengine.
Lakini licha ya hivyo abiria hawakuwa wengi siku hio kama siku nyingine.
Baada ya kuangalia mazingira kwa dakika chache na treni kuanza kuondoka , alivaa Earphone zake na kuweka mziki wa taratibu na kisha alijiegamiza kwenye kiti na kuuchapa usingizi.
Kutokana na kwamba ilikuwa ni zaidi ya miaka mitatu tokea atoke nyumbani kwao, lile wazo la kesho anarudi nyumbani ilimfanya siweze kupata usingizi usiku kucha.
Haikuchukua muda alihisi katika siti yake kuongezeka mtu , lakini hakufungua macho na kuendelea zake kulala
Lakini sasa baada ya dakika kadhaa baada ya treni kushika kasi , alisikia akiitwa jina lake.
“Yonesi huna njaa , kuna juisi na vitafungwa hapa”Sauti ilisikika katika masikio yake na kumfanya afumbue macho kwa pupa , huku akijiuliza ni muda gani earphone zake zilikuwa zimetolewa , huku akijiuliza kwanini pia sauti inayomwita anaijua.
Mara baada ya kugeuza macho yake pembeni na kujua mtu aliekuwa akimwongelesha alijikuta akishikwa na mshituko.
“Ulipata Breakfast ulipotoka , kuna bite hapa na juisi”Aliongea Hamza huku akiwa na tabasamu.
“Wewe.. Unafanya nini hapa?”Aliongea Yonesi huku akifikicha macho yake kuona kama hakuwa akiota.
“Nimekuja kukupa jibu la swali uliloniuliza ile jana”Aliongea Hamza
“Jibu!”
Yonesi alijikuta akifikiria swali la jana alilomuuliza Hamza na palepale uso ulimuiva . Hakujua ni kipi kilimfanya kumuuliza Hamza swali lile ambalo muda huo linamfanya kujionea aibu mwenyewe.
Ukweli ni kwamba alitamani kuweka kila anachojisikia moyoni mwake na hakujua nini kilimtokea jana mpaka kupeleekea kuuliza swali lile.
Lakini kitendo cha Hamza kukaa kimya baada ya kumuuliza swali lile ilimfanya afunge moyo wake moja kwa moja , kwa uwezo wake wa kufikriia aliokuwa nao aliona kabisa kimya kile lilikuwa ni jibu tosha kwake na Hamza hakutaka kuongea ili kuonekana mkatili na sababu hio ndio iliomfanya kuamua moja kwa moja kurudi nyumbani.
“Sikukupa jibu jana kwasababu ushasema unarudi nyumbani na nilichofanya baada ya pale ni kutafuta ni muda gani utaanza safari na mimi nilikata tiketi ili nikusindikize kwenda nyumbani kwenu”
“Nini!!? Unataka kwenda nyumbani kwetu? Kwanini?”
“Kuna hajam ya kuuliza sasa , nitaachaje mwanamke ninaempenda aoelewe na mwanaume mwingine? Naenda kwenu kujitambulisha?”