Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

Simulizi ya kijasusi: Shetani Rudisha akili zetu na mke wangu

SHETANI RUDISHA AKILI ZETU

MTUNZIlSINGANOJR


SEHEM,U YA 160.
Mpigie simu Nyakasura.
Regina alijikuta akivuta pumzi nyingi na kuzishusha, na alionekana kama mtu ambaye alikuwa akifikiria.
"Madam Wadeni, nadhani nishajua sasa. Asante sana kwa zawadi ya mchoro, kuna kazi naendelea kufanya, naomba niage."
Mara baada ya kuongea hivyo, palepale alimpotezea Wadeni yule na kutembea kisha kuingia kwenye lifti.
Madam yule alionekana kuwa katika hali ya wasiwasi na alimwangalia Eliza kwa wasiwasi.
"Nimefanya makosa kuja? Isije ikawa nimemuongezea Hamza matatizo?"
Eliza hata yeye mwenyewe hakujua namna ya kujibu, ukweli ni kwamba hakujua ni nini Regina anafikiria.
"Madam, huna haja ya kuwa na wasiwasi, nadhani mkurugenzi atafikiria kwa umakini juu ya hili, vinginevyo asingekusikiliza kabisa," aliongea Eliza akijaribu kumtuliza, na maneno yake yalionekana kumwondolea wasiwasi.
"Mwenyewe sikujua ni namna gani ya kumsaidia Hamza, ndiyo maana nimefanya maamuzi ya kuja na hawa watoto hapa, lakini sasa nahisi kujilaumu."
"Usiongee hivyo, naamini Hamza akisikia umekuja mpaka huku kwa ajili ya kumsaidia ataguswa mno," aliongea Eliza, na maneno yale yalionekana kumtuliza kiasi. Palepale waliaga, na Eliza aliwasindikiza mpaka kupanda kwenye gari walilokuja nalo.
*****
Mpaka ilipotimia saa kumi na mbili za jioni, Hamza alikuwa na Yulia tu. Walizunguka kila sehemu ambayo Yulia alitaka kwenda, na kumfanya Hamza kushangazwa na tabia hiyo ya mwanamke ya kumsumbua makusudi.
"Yulia, tuondoke sasa, muda umeenda sana," aliongea Hamza.
"Mbona mapema? Mpaka tupate chakula cha usiku kabisa."
"Hapana, chakula cha usiku utakula mwenyewe. Nina miadi na mke wangu," aliongea na kumfanya Yulia kuvuta mdomo huku akionekana kufikiria.
"Kwahiyo yote hayo ni kwa sababu ya Regina tu?"
"Vipi, ulipanga tulale pamoja?" aliuliza Hamza.
"Hapana, nilitaka unipe kampani na chakula cha usiku."
"Vyovyote vile, nishakusindikiza siku nzima na siwezi kuwa na wewe usiku, isitoshe nishamwahidi mke wangu muda mrefu."
"Inanihusu nini mimi? Siwezi kukuruhusu uondoke," aliongea huku akivuta mdomo.
"Hebu acha hizo, kwahiyo unadhani ukisema nisiende nitakusikiliza?Muda wangu wa kuendelea kubakia na wewe umeisha, naondoka mimi," aliongea Hamza, kisha alitembea kuelekea upande wa maegesho ya magari.
Yulia aliishia kung’ata meno kwa hasira, kisha akamfuata kwa hasira hasira.
Hamza, mara baada ya kuingia kwenye gari, alimuona Yulia kitiifu akiingia ndani ya gari na alishindwa kujizuia kutoa tabasamu huku akiliwasha.
Wakiwa njiani, Yulia alionekana kununa na hakumwongelesha Hamza, na hata hivyo hakujali na aliendelea kuendesha gari kimya kimya.
Kutokana na foleni kubwa barabarani, walitumia zaidi ya saa moja mpaka kufika hoteli ya Cloud. Mara baada ya kusimamisha gari, Hamza alishuka na kuzunguka upande wa kiti kufungua mlango.
"Mrembo, tushafika shuka sasa," aliongea.
Yulia hakuongea neno na kwa maringo alitoka nje ya gari kisha alimwangalia Hamza kwa macho ya chuki.
"Nawatakia usiku wa mahaba mazito."
Hamza alipokuwa anataka kusema "Asante," alisikia sauti ya mvumo mara mbili, na baada ya kugeuka kuangalia nini kimetokea, aliona tairi za gari yake zimebonyea.
Hamza, mara baada ya kugeuka kuangalia juu, alijikuta akitoa tusi baada ya kuona wadunguaji wawili wakimalizia kuficha bunduki zao.
Hakuhitaji D mbili kujua nani kapanga wadunguaji hao kuharibu tairi za gari yake. Yote ilikuwa ni mipango ya mwanamke kichaa, Yulia.
Ukweli ni kwamba kama wangekuwa wakimlenga yeye, angeweza kuwanasa, lakini kwa sababu walilenga gari yake, iliwaondolea ile nia ya mauaji ambayo ndiyo hisia kuu ya kumfanya mtu kama Hamza kugundua hatari.
Hamza aliishia kuangalia gari yake ilivyobonyea tairi na kujikuta akishika kiuno.
"Yulia, isingekuwa leo sina miadi ya lazima, ningekufanya kitu cha kukushikisha adabu."
"Kitu gani ungenifanya?" aliuliza Yulia akimwangalia Hamza kwa kebehi.
Hamza aliishia kukosa neno la kuongea. Aliona haina haja ya kuendelea kujibishana naye, maana muda ulikuwa umemtupa mkono, hivyo haraka haraka bila kusema chochote alikimbilia upande wa nje akipanga kuchukua taksi ya kumuwahisha.
Mara baada ya kuona Hamza akikimbilia nje, Yulia sura yake iligeuka ya ukauzu na palepale alitoa sonyo, kisha akageuka na kuingia hotelini kwake huku meneja wa hoteli hiyo akimpokea mizigo aliyoinunua.
"Bosi, hivi vitu nivilete kwenye chumba chako?" aliuliza meneja.
"Vigawe kwa wafanyakazi, chukulieni kama zawadi ya sikukuu ya Iddi," aliongea na kufanya meneja kuwaangalia wadada waliokuwa eneo la mapokezi wakionyesha kuwa na shauku juu ya kupata mgao wa vitu hivyo.
*****
Saa mbili na dakika kumi na tano, Hamza aliweza kufika nje ya ukumbi wa Le Grande. Kuona taa za rangi rangi zinawaka nje ya eneo la ukumbi huo, Hamza alijikuta akivuta pumzi huku, kwa wakati mmoja, akihisi njaa.
Aliona ni bora, kabla ya kukutana na Regina na kuingia ukumbini kwa ajili ya show, apate chochote cha kula kwanza, maana ile kuzungushwa na Yulia siku nzima imemfanya chakula kumuishia tumboni.
Palepale, aliweza kuona eneo la pembeni kuna ka-mgahawa, na alinunua mishikaki ya kutosha pamoja na ndizi, akaanza kula mpaka aliposhiba.
Saa mbili na nusu, alisogea mpaka karibu na mlango wa kuingilia ndani ya ukumbi huo, na watu wengi tangu alipofika walikuwa wakiingia kimakundi makundi, lakini upande wa Regina hakuonekana kufika.
Hamza, muda ule wakati akisubiri, aliweza kusikia simu yake ikilia, na haraka sana aliitoa kuangalia nani anapiga. Aliona ni Regina, lakini ile tu anapokea, simu yake ilijizima palepale kuashiria ilikuwa imeishiwa na chaji.
Hamza alijikuta akikakamaa mwili, alitumia simu yake kuingia mtandaoni wakati Yulia akiwa saloon, na alikuwa amebakisha chaji kidogo lakini akasahau kuzima data.
Hata hivyo, hakuwaza sana, baada ya kuona Regina amempigia, aliamini lazima atakuwa anakuja, ndiyo maana akaamua akae asubiri.
****
Upande mwingine, ndani ya makao makuu ya kampuni, Regina bado alikuwa ofisini na hakuwa na mpango wa kuondoka kurudi nyumbani. Muda huo alikuwa ameshikilia simu mkononi, na hiyo ni baada ya Hamza kupokea simu lakini ikajikata palepale. Aliishia kukunja sura, akishindwa kutafsiri hali hiyo.
“Bwana eh, kama amezima simu, haina haja ya kumwambia sitoenda, kwanza sio lazima na niko bize,” aliongea, na palepale alishika kalamu na kuanza kuzungushia baadhi ya maneno kwenye nyaraka.
Hata hivyo, kadri alivyokuwa akijitahidi kujiweka bize, akili yake ilikosa utulivu. Hakuacha kufikiria maneno ya Wadeni na ombi la wale watoto kumtaka amsamehe Hamza.
"Lazima atakuwa ametengeneza mbinu ya kukusanya wale watoto kuja ili tu nimhurumie... anadhani mimi ni mjinga," aliongea mwenyewe, akijaribu kujishawishi, kisha akaongeza umakini kwenye kile alichokuwa akikifanya.
Lakini sasa, aliishia tu kukodolea macho nyaraka alizoshika mkononi. Ilikuwa ni kama kuna kitu kilikuwa kinamshikilia akili, na kumfanya ashindwe kuelewa nyaraka hizo zilimaanisha nini.
Muda nao ulipita haraka, na alipokuja kuangalia saa, aligundua ilikuwa tayari saa tatu na nusu usiku, lakini bado hakuwa amefanya chochote cha maana. Alikuwa amebung'aa tu kama sanamu.
Baada ya dakika chache, aliona bora ampigie shangazi simu ili kujua kinachoendelea nyumbani.
“Regina, mna matatizo gani? Kwanini wote mpaka sasa hamjarudi nyumbani?” aliuliza shangazi ambaye alikuwa katika hali ya wasiwasi mkubwa.
"Hamza hajarudi bado?"
"Hajarudi, ndiyo," aliongea shangazi.
“Oh, basi sawa. Narudi ila nitachelewa kidogo,” aliongea.
“Sawa, nimekuandalia supu. Ukirudi, hata kama umechelewa, hakikisha unainywa kwanza kabla ya kulala,” aliongea shangazi, kisha palepale akakata simu.
"Inamaana hajarudi bado... yupo wapi?" aliongea Regina huku kivivu akifungua droo na kutoa ule mchoro aliopatiwa na watoto mchana wa siku hiyo. Baada ya kuangalia mchoro huo, aligundua juhudi kubwa iliyowekwa na watoto hao katika kuchora, na alishindwa kujizuia kutabasamu.
Muda ule, wakati akiwa ndani ya ofisi hiyo yenye mwanga hafifu, ni kama sauti ya Hamza ilianza kumwongelesha.
“Uje ama usije, lakini nitakusubiri.”
"Huyu mwanaume, isije ikawa ananisubiri mpaka..."
Regina alijikuta akishtuka kama mtu aliyerudia kwenye ufahamu, na palepale alichukua mkoba wake na kutembea haraka kutoka nje.
Lakini ile anatoka nje, alikumbuka kitu alichosahau. Haraka alirudi ndani, akasogeza nyaraka pembeni, na palepale aliweza kuona zile tiketi na kuzichukua kabla ya kuendelea na safari.
Saa nne hatimaye aliweza kukanyaga breki mbele ya ukumbi wa Le Grande, Posta, na mara baada ya kushuka, eneo hilo lilikuwa na utulivu mkubwa. Hapakuwa na watu kabisa, pengine ni kutokana na maduka kuwahi kufungwa. Kulikuwa na upepo wa baridi kali uliokuwa ukitokea baharini, na kumfanya atoe mtandio kwenye mkoba wake na kujifunga shingoni.
Baada ya kutembea karibu na mlango huo, aliweza kumuona mwanaume aliyekuwa amekaa kwenye ngazi, akiangalia upande wa baharini huku akivuta sigara.
Regina alijikuta akishangaa alipoona kuwa mwanaume aliyekuwa akivuta sigara nje ya ukumbi wa Le Grande ni Hamza. Kwa upande wa Hamza, hakujua ni muda gani alikuwa amekaa hapo. Mwanzoni, hakuwa hata na sigara, alizipata tu kutoka kwa mlinzi. Hakujua kama alikuwa akimsubiria Regina au alikuwa tu akipunga upepo na kutafakari mambo, lakini alijikuta akibaki hapo bila kuchukua hatua ya kuondoka. Mara tu aliposikia harufu ya marashi anayoyafahamu, aligeuka na kutabasamu akiwa na mshangao kumwona Regina.

Regina, mara baada ya kuona Hamza anatabasamu, alihisi joto kali likimfanya macho yake kuwa na ukungu na mafua ya ghafla na kushika pua zake.
"Wife, show ilishaanza, tuingie," Hamza aliongea huku akisimama na kumshika Regina mkono, lakini Regina alirudi nyuma.
"Sipo hapa kwa ajili ya kuangalia show na wewe. Nimekuja kukuletea tiketi zako na kukuambia sitokuja," alijibu Regina kwa sauti ya kukata tamaa.
Hamza alishangaa kusikia hayo na alijisikia vibaya, lakini alihisi kuwa kuna kitu hakipo sawa. Kama Regina hakuwa na mpango wa kumsamehe, kwanini alifika hapo? Zaidi ya hayo, show ilikuwa karibu kuisha, lakini bado Regina alikuwa amekuja. Aliamini lazima alikuwa amekuja ili kujiridhisha kama kweli Hamza alikuwa akimsubiri. Wakati huo, wasiwasi wa Hamza uligeuka kuwa furaha.
Bila kujali kitu kingine, alimkumbatia Regina ghafla.
"Unafanya nini?" Regina aliuliza kwa sauti ya kushangaa huku akijaribu kujitoa kwenye kumbatio hilo.
"Ni sawa tu kama hutaki kuangalia show hii na mimi, lakini nitakukumbatia hapa hapa angalau hata nje, ili kumaliza siku hii ya sikukuu pamoja," aliongea Hamza kwa upole.
"Una nini wewe lakini? Kwanini ulikaa hapa kwenye upepo mkali badala ya kutafuta sehemu nzuri ya kusubiria?" Regina aliongea kwa hasira, lakini kabla hajamaliza, Hamza alimpiga busu la mdomoni ghafla tu.
Baada ya busu hilo la takribani dakika nne, Hamza alimwachia Regina na kumshika uso kwa namna ya kubembeleza.
"Tuingie ndani, hata kama show imeanza muda mrefu, bado tutapata kuona mwisho wake," aliongea.

Regina alikuwa bado hajapata ufahamu wa maneno ya Hamza baada ya busu hilo. Alijikuta akimfuata kimyakimya na kuingia ndani. Walichelewa, lakini walibahatika kuona kipande cha mwisho cha bendi maarufu ya The Cast.
Baada ya show kumalizika na watu kutawanyika, Hamza alitaka kumuuliza Regina kama amemsamehe, lakini ghafla alisikia tumbo la Regina likigurumisha njaa.
"Wife, tumbo lako linaguruma," aliongea Hamza akitabasamu.
"Umesikia vibaya," Regina alijibu huku akiwa na aibu.
"Hukula chakula cha usiku?" Hamza aliuliza, na Regina, akiwa mkweli, alitikisa kichwa kukubali.
"Twende tukale, hata mimi nina njaa. Kuna sehemu najua kuna nyama choma nzuri sana," Hamza aliongeza.
"Kula nyama saa hizi ni kujitafutia kitambi. Ukila sasa hivi, mwili unajisafisha saa ngapi?" Regina alihoji.
"Kwahiyo utakula nini sasa?"
"Chochote cha kuchemsha kisicho na mafuta mengi," Regina alijibu, na Hamza alifikiria kwa muda mfupi kabla ya kumshika mkono na kuelekea hotelini.
Baada ya kukaa mgahawani na chakula kuletwa, harufu tu ya chakula ilimfanya Regina hamu ya kula kujaa. Ukweli ni kwamba, mchana alikuwa amekunywa tu juisi ya virutubisho na hakuwa amekula kabisa.
"Vipi, ni kitamu?" Hamza aliuliza akimwangalia mke wake aliyekuwa akifurahia supu ya samaki.
Regina alitingisha kichwa tu huku akishindwa kuongea kutokana na kutafuna.
"Wife, kwa utajiri wako unaweza kula vitu vya kitajiri kama Caviar, Kobe beef au Pine Dew kila siku, au unaweza hata kuajiri mpishi mwenye hadhi ya Michelin Star. Kwanini unajishindisha na njaa kila siku?" Hamza aliuliza kwa mshangao.
"Ulivyovitaja vyote, hakuna ninachopenda," Regina alijibu huku akiendelea kula bila kutaka kusumbuliwa.
"Kwahiyo unapenda vyakula vya bei rahisi?" Hamza alihoji tena.
"Chakula ni ladha yake, sio thamani ya hela. My taste is not cheap, okay?" Regina aliongea, na kumfanya Hamza acheke.
"Shida yako ni kwamba unajitesa na njaa. Unaweza kuugua ugonjwa wa tumbo," Hamza aliongeza kwa wasiwasi.
"Huwezi kuamini, kila nikirudi nyumbani, shangazi ameshaniandalia chakula cha kunitibu mwili wangu," Regina aliongea.
"Lakini yule ni mzee, utamwacha afanye hivyo mpaka lini?" Hamza aliuliza.
"Wewe si upo?" Regina alihoji kwa utani.
"Usiniambie unataka nianze kuwa mpishi wako?" Hamza aliongea kwa mshangao.
"Mbona unajua kupika? Usipopika utaacha na kupoteza kipaji chako," Regina alijibu.
Hamza alikubaliana naye kwa kicheko kidogo, lakini kabla ya kuendelea na mazungumzo, Regina alimwangalia kwa huzuni kidogo.
"Unajua, najua mambo mengi kuhusu biashara, lakini je kupika ndio sifa ya muhimu kwa mwanamke mbele ya mwanaume?" Regina aliuliza kwa sauti ya chini.
Hamza alishindwa kujibu mara moja, huku akijiuliza kwanini swali hilo dogo lilimletea hisia za huruma.
“Hivi kuna mwanamke asiejua kupika siku hizi , inawezekanaje?”Aliongea Hamza kumtania huku akicheka.
“Hata kupika vitu vyepesi kunanishinda , inabidi nianze kujifunza”
“Haina haja hata ya kujifunza , hata kama hujui unadhani kuna mtu atakae mdharau bosi mkubwa kama wewe kwasababu hio?”
“Hapana hata kama nisipojua sana , ila angalau chakula cha kawaida nijue”
“Basi sawa”Aliongea Hamza akimkubalia kivivu.
Wakati wakiwa wanamalizia kula ,Hamza muda ule alikumbuka kitu na kwa kuchagua maneno aliuliza;
“Wife vipi umeguswa na nia yangu ya dhati ndio maana umenisamehe?”Aliuliza na Regina alimwangalia.
“Kamshukuru madam Wadeni wa kituo cha kulelea watoto , kama asingewaleta wale watoto na kukuombea msahama nisingejisumbua”
“Madam Wadeni! Madam Neema alikuja kazini kwako?”Aliuliza Hamza kwa mshangao mkubwa .
Regina mara baada ya kuona mshangao wa Hamza aliona kweli hakuwa akijua chochote , hivyo alimwelezea kile kilichotokea.
Ijapokuwa alikuwa ameishi sana nje ya nchi na kupitia mambo mengi makubwa na madogo mpaka kufikia hatua ya kutaka kupoteza maisha , lakini siku ambayo alirudi Tanzania na kufika kituoni hapo alijikuta tu akiguswa kutaka kusaidia watoto hao na ndio alichofanya , licha ya kwamba hela alikuwa nazo lakini hakutaka kutumia hela hizo kuwasaidia bali zile ambazo alitolea jasho , hela ambazo hazikuwa na makando kando .
“Sikujua kama wangefanya hivi ..”
“Huna haja ya kuelezea , nimemuamini yule mama , hawezi kunidanganya”Aliongea Regina.
“Ukweli bado nasita , ninao uwezo wa kuwasaidia kwa mkupuko mmoja tu na kubadilisha maisha yao kabisa , lakini nimeona sio vizuri kuchukua hela chafu na kuwapa watoto Yatima ,bado sijajua kama ni kitu sahihi”
“Kwani hela zako ni chafu?”Aliuliza Regina kwa mshagao na kumfanya Hamza kuwa na wasiwasi kwenye kujibu swali hilo.
“Kwasababu hela zangu hazijapatikana kwa njia za kawaida , naweza kusema zina damu”
Ijapokuwa jibu hilo lilikuwa halijaeleweka vizuri katika kichwa cha Regina lakini hakutaka kuongea neno.
“Malizia kula tuondoke, nishaanza kushikwa na usingizi”Aliongea na Hamza alitngisha kichwa.
“Wife halafu sijakuuliza kuhusu maendeleo ya kujifunza mafunzo ya tafsiri ya lugha za kimalaika , vipi bado hujapata ufunuo wa maneno yake?”aliuliza Hamza kwa shauku.
“Hapana , sijapata muda , nina mambo mengi ya kuandaa kabla ya mwisho wa mwaka”
“Jitahidi , maandiko yale ni adimu sana , ukifanikiwa kuelewa hata kidogo mwili wako utaimarika , hata kama usipande levo ya juu kwenye kuyaelewa lakini itakusaidia kutokupata ugonjwa au kuondoa kabisa kama unao”Aliongea Hamza na kumfanya Regina kumwangalia.
“Unadhani nikijifunza na kuelewa sitoweza kubadilika kiakili?”Aliuliza na swali hilo lilimfanya Hamza kumwangalia kwa shauku , maana ni kama hakutegemea Regina kuuliza hivyo.
Ukweli ni kwamba licha ya kwamba anajua kuhusu Regina kuwa na shida hio ya akili lakini siku zote hakutaka kuuliza , alitaka Regina mwenyewe ndio awe mwenyew ekuanzisha mada.
“Sijamaanisha hivyo .. ninachomaanisha inawezekana”
“Kama sio hivyo acha porojo zako za matumaini hewa ,zinachukiza”
“Haha.. sawa mke wangu usikasirike , kama hutaki kujifunza usijilazimishe”Aliongea Hamza lakini hata hivyo Regina hakuwa na hasira,ukweli alijiambia akiendelea kuwa mpole mbele ya Hamza ataanza utundu wake na mwisho wa siku watagombana tena , hivyo hakutaka kuwa mwepesi.
Regina mara baada ya kurudi nyumbani alikumbuka ,Shangazi alimwambia anywe alichomwandalia lakini kutokana na kushiba hakunywa na kumlazimisha Hamza ndio ainywe yeye ili Shangazi akiamka asubuhi asije kujisikia vibaya.
Hamza alishiia kucheka kwa uchungu kwa adhabu ya chakula anayopewa .Ijapokuwa alikuwa amefanikiwa kumrudisha mke wake katika hali ya furaha lakini bado aliona alikuwa na safari ndefu
Lakini hata hivyo amani yake ilirudi mno na kujisikia kuwa na furaha kubwa kuliko mwanzo.
Ugomvi wao ki ufupi uliisha kabisa na hata siku iliofuata Regina aliwahi kuamka na kuanza kujifunza kupika.
Chakula alichopika, Hamza ndio alitakiwa kula, licha ya kwamba Hamza alihisi alikuwa akila sumu lakini macho ya Shangazi yalimwambia asijekuthubutu kusema chakula ni kibaya na ale hivyo hivyo na Hamza alielewa na kujikaza huku machozi yakimtoka.
Regina alivyoona Hamza macho yake yamejaa unyevunyevu alimuuliza Hamza kwanini yupo hivyo na Hamza alimjibu ni kwasababu pishi lake ni tamu mno , pishi ambalo hajawahi kuonja tokea azaliwe.
Regina ambae alipika tu bila ya kuonja baada ya kusikia hivyo alijikuta akijisikia vizuri na kuanza kujisifia namna alivyofuatisha mapishi kupitia mtandaoni.
Hamza aliishia kusifia tu ili kufanya nyumba iwe na amani . Baada ya kifungua kinywa, Regina ilikuwa ndio anaanza wikiend ya sikukuu kwake hivyo alimuomba Hamza ampeleke kituoni kwa wale watoto na Hamza hakupinga.
Walinunua kila walichoona kinafaa na kisha safari ilianza , walivyofika mke wa mkuu wa chuo hicho, Wadeni na mume wake Mzee Hizza walifurahi kumuona Regina akiwa ameongozana na Hamza tena wakiwa katika hali ya furaha.
Madam Neema aliishia kufurahi , kwa kuona kile ambacho lakifanya jana yake , hakuwa amekosea bali kilileta matokeo mazuri kwa Hamza na mke wake.
Waliweza kumpokea vizuri Regina katika kituo hicho na haikuwa kwao tu , hata kwa watoto hao waliweza kumpokea vizuri na ndani ya dakika chache tu walijikuta wakawa wamemzoea Sana.
Kwa ufupi Regina siku hio alijiachia sana mbele ya watoto na kusahau ulimwengu wake wa ubize kwa muda wa saa kadhaa , hata wakati wa kuondoka , watoto hao walionekana kutamani kumuona tena, na Regina aliwaahidi angerudi ili mradi ashafika siku ya kwanza.
Upande wa walezi wa vituo walionekana kushangazwa na upande mwingine wa Regina , ukweli walijua kwa mfanyabiashara mkubwa kama huyo angekuwa na mipaka mingi katika mazingira ambayo anaonekana mbele za watu , lakini matokeo yake ilikuwa ni tofauti na vile ambavyo walimfikiria.
Mzee Hizza na mke wake walijua ni kwanini Hamza na Regina walikuwa wameoana.
Ukweli ni kwamba hawakujua kama Hamza na Regina kukutana kwao na namna ndoa yao ilivyoanza ni tofauti na vile ambavyo walikuwa wakifikiria wenza wengi huanza, hawakujua kama wawili hao walikuwa katika hatua ya kuzoeana na kufahamiana.
Saa kumi za jioni wakati Hamza na Regina wakikaribia kuingia jijini Dar es Salaam simu ya Regina ilianza kuita na mara baada ya kuangalia anaepiga alishangaa kuona alikuwa ni Linda.
Regina mara baada ya kuona namba hio , aliona kabisa kuna kitu kimetokea , maana ni ngumu sana kwa Linda kupiga simu wakati akiwa mapumzikoni.
“Linda habari yako , kuna tatizo?” aliongea Regina mara tu baada ya kupokea.
“Mkurugenzi kuna tatizo limetokea”Aliongea Linda na sauti yake ilionekana kuwa na wasiwasi mno, kama ya mtu aliekuwa katika hali ya kupaniki.
“Nini kimetokea?”Aliongea Regina huku sura yake ikigeuka na kuwa ya ukauzu.
“Kuna kundi la watu wanafanya fujo hapa makao makuu na kuingia mpaka ndani ya ofisi yako na kuharibu vitu ,Anna na wenzake wamejitahidi kuwazuia kwa kupigana nao lakini wameshindwa kuwahimili”Aliongea na kauli ile ilimshangaza mno .
“Ni wakina nani?”Aliuliza Regina.









EHEMU YA 162.
“Siwajui bosi , wamesema tu wanataka kuonana na wewe”Aliongea Linda na Regina alimwambia anakuja hapo muda si mrefu.
Baada ya kukata simu alimwambia Hamza aendeshe haraka kuelekea makao makuu ya kampuni kuna tatizo.
Hamza hakutaka hata kuambiwa maana alishayasikiliza maongezi yao yote na alishindwa kuacha kujiuliza ni nani huyo ambae anajaribu kufanya vurugu katika mali za kampuni tena mchana kweupe.
Kwasababu hawakuwa mbali sana na makao makuu ndani ya nusu saa tu waliweza kufika ndani ya jengo hilo.
Muda ambao Hamza aliingiza gari ndani ya eneo hio mara baada ya kuangalia juu , sura yake ilijikunja palepele.
Hata Regina alionekana kugundua kitu na mara baada ya kuangalia floor za juu za jengo hilo alijikuta akikunja sura kwa ukauzu mkubwa.
Haikuwa hivyo tu baadhi ya watu waliokuwa wakipita nje ya jengo hilo walikuwa na wenyewe wanaangalia kilichokuwa kikiendelea , maana ilikuwa ni kama sinema kwao , ijapokuwa watu wengi walikuwa na uelewa na aina ya watu hao wenye mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi.
Juu ya jengo hilo kulikuwa na wanaume wawili ambao walikuwa wakishuka kutoka juu kwenda chini kwa kuruka na kisha kupanda , ilikuwa ni kama wanacheza mchezo wa kupanda jengo hilo kwa nje kwa kushindana kwa kutumia nishati za mbingu na ardhi.
Baadhi ya madirisha pia yalionekana kupasuka kutokana na nguvu yao ya kujigonga gonga kwenye kuta za jengo.
Lilikuwa ni jengo refu , lakini watu kucheza nje ya jengo hilo ilishangaza na kukasirisha kwa wakati mmoja kutokana na kwamba walikuwa wakiharibu usanifu wake.
“Nyie ni wakina nani , hebu acheni mnachokifanya”Aliongea Regina kwa sauti baada tu ya kushuka kwenye gari , lakini watu wale hawakumjali , ukweli ni kwamba haikueleweka kama wanamsikia.
Muda huo , kundi la walinzi walitoka kutokea ndani , wakiongozwa na Anna na Linda na baadhi ya wafanyakazi wengine.
“Mkurugenzi imekuwa ngumu kuzuia watu kama wale , wote wapo katika mafunzo ya juu ya nishati za mbingu na ardhi”Aliongea Anna ambae alionekana kuwa na dalili za kutoka damu mdomoni ikionyesha alikuwa amejeruhiwa.
“Mkurugenzi tunafanyaje , wanaonekana kutokuwa watu wa kawaida?”Aliongea Linda aliekuwa katika hali ya wasiwasi mkubwa kuliko hata walinzi na hio yote ni kutokana na kutisha kwa vitendo watu hao walivyokuwa wakifanya.
Regina hata yeye hakuwa akijua nini cha kufanya , maana watu hao walikuwa ni wa mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi na kitu pekee alichofanya ni kumwangalia Hamza.
“Ni wapiganaji wa kambi ya Nyoka hawa , inaonekana ndugu zake Fabiani wamekuja kunitafuta”Aliongea Hamza na kumfanya Regina kushangaa.
“Nini! Una uhakika?”Aliuliza na Hamza aliishia kutingisha kichwa kukubali.
“Hili swala mimi ndie msababishaji mkuu . ngoja nitamalizana nao”
“Utamalizana nao kivipi , nilikuambia mimi acha kumpiga siku ile mpaka kumuumiza , unadhani watakubali liishe kirahisi?”
“Majuto pkeee niliokuwa nayo sasa hivi ni kutokumuua Fabiani , ila kumtia ukilema wala sijutii”Aliongea Hamza na palepale alikimbia kuingia ndani ya jengo hilo
Anna aliekuwa pembeni aliweza kujua sasa kinachoendelea na baada ya kumuona Hamza ameondoka alimsogelea Regina.
“Mkurugenzi ni vizuri kumuacha Hamza kudili na hili mwenyewe?”aliuliza
“Atadili nalo mwenyewe maana ndio alielianzisha”Aliongea akionekana kuwa na hasira mno , hakuamini jengo lake la kampuni liliharibiwa na watu hao bila ya kuongea nae kwanza.
Muda huo hasira zake alizielekezea kwa Fabiani na kung’ata meno kwa hasira na kutamani kama angekuwepo angemchoma na kisu. Lakini hata hivyo upande mwingine alielewa hisia zake kwa kile ambacho alifanyiwa na Hamza.
Regina hakujua uwezo halisi wa Hamza , lakini aliamini hawezi kufanya vitu ambavyo vipo nje ya uwezo wake, hivyo kwasababu amesema mwenyewe atadili nalo , aliona haina haja ya kuendelea kuwaza na kuishia kumwamini.
“Pigia simu wahandishi waje warekebishe sehemu zilizoharibika , kazi ifanyike mapema kabla ya kesho saa tano”Aliongea Regina akimpatia maagizo hayo Linda.
Upande mwingine Hamza alikuwa ashafika floo za juu kabisa za jengo hilo kwa kutumia lift.
Mara baada ya kuingia ndani ya ofisi ya Regina , aligundua hali ilikuwa mbaya kuliko alivyotegemea , kulikuwa na uchafu wa kuvunjika kwa vitu kila mahala , kwa mahesabu ya haraka haraka hasara iliotokea hapo ni zaidi ya milioni kadhaa.
Ndani ya ofisi hio alikuwepo mwanaume alievalia shati la kijani na suruali nyeusi akiwa amekaa kwenye sofa , alikuwa na umri makadilio ya miaka therathini kwenda arobaini hivi , nyuma yake kulikuwa na wanaume wawili waliokuwa na mili iliotuna waliovalia mavazi ya suti na wote walikuwa na mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi kutokea kambi ya nyoka.
Ilikuwa wazi mwanaume alievalia shati la kijani ndie aliekuwa kiongozi wa kundi hilo la wavamizi.
Mkononi alikuwa ameshikilia upanga mrefu wenye kung’aa na alikuwa akiufuta futa na kipande cha hariri , huku akiwa na umakini kama vile kuna kitu anachosubiria kitokee.
Mara baada ya kumuona Hamza akiwa ameingia ndani ya ofisi hio , palepale aligeuka na kumwangalia na midomo yake ilicheza kuonyesha tabasamu la kebehi.
“Hatimae mhusika amejitokeza , Sikutaka kutumia nguvu kukutafuta nilijua nikiharibu hili jengo lazima utajileta mwenyewe”Aliongea yule mzee wa kijani.
“Ni nyie tu hakuna wengine?”Aliuliza Hamza na muda uleule yule mzee wa makamo alipiga mluzi na dakika chache tu waliingia wanaume wengine wawili ambao walikuwa wakifanya uharibifu kwa nje na hatimae jumla yao ikatimia watu watano.
“Mbona huulizi kujua sisi ni wakina nani?”Aliongea.
“Sina haja ya kujua nyie ni wakina nani , ninachotaka kujua ni kitu kimoja pekee , ni nani kutoka katika kambi yenu ya Nyoka amewatuma kuja hapa?”
“Oh , unaonekana kuwa na macho ya mbali , kwahio ushajua tunatokea kambi ya Nyoka? Mimi hapa naitwa Kambona , Afande Fabiani ni ndugu yangu ambae umemuua. Nipo hapa kwa maagizo ya mkuu wangu kukuletea machafuko”
“Ndio maana nimesikia uvumi wa Fabiani kuwa mtoto wa nje ya ndoa wa Mkuu wa kambi yenu , inaonekana ni kweli maana kwa hii hasara mliosababisha mngekuwa na wasiwasi wa kuchukuliwa. Anyway mtoto mwenyewe nimemgeuza joka la kibisa naelewa hiki alichofanya baba yake”Aliongea Hamza.
“Hamza , unajiona wewe ni nani? Master ni mtu anaeheshimika , cheo chake hakitokani na kuwa na undugu na mheshimiwa Raisi bali kinatokana na juhudi zake mwenyewe , kwanini unamdharau waziwazi?”Aliongea yule bwana.
“Mambo ya juhudi na kukosa busara kwangu naona ni bure tu , isitoshe nakwenda kuitokomeza kambi yenu yote”Aliongea na kauli ile ilimfanya yule bwana kubadilika palepale na kwa hasira alimsogelea Hamza kwa spidi
“Elementi tano za muundo wa kisiraha tafadhari!”Aliongea na palepale wote watano walijipanga katika mkao maalumu wakimzunguka Hamza.
Muundo wa Elementi tano za siraha msingi wake ni ule ule wa muunganiko wa elementi kuu tano za dunia , zikizingatia kanuni ya hasi na chanya , mara nyingi wanajeshi wa mafunzo ya nishati wakikuzunguka katika mfumo huo ni ngumu kujua nani anaanza kushambulia.
“Wadogo zangu ni muda wa kumtemea sumu ya nyoka kwa fomesheni yetu ya elementi tano”Aliongea yule Kambona.
Muda ule wale watu ni kama walikuwa wakitokwa na upepo wa baridi kali uliokuwa ukisogea kati alipo Hamza.
Hamza dakika ile alinguruma na misuli yake ya mwili ilituna na kuwa kama jiwe na palepale alifyatua mikono yake kutoka kifuani na kupangua shambulizi lile la muunganiko wa elementi tano za uchawi wa nyoka na wale mabwana walijikuta wakisukumwa mbali.
Jambo lile liliwashangaza mno , hawakuamini Hamza ameweza kuhimili muunganiko wa nguvu zao zote tano.
Hamza aliishia kuwaangalia tu namna walivyokuwa wakimshangaa na aliwaonyesha ishara ya dharau.
“Kwa nguvu yenu mmoja mmoja msije mkadhani mnaweza kunizuru kwa kuunganisha nguvu zenu zote , hata kama mngetumia mbinu ya maangamizo msingeweza kunigusa hata nywele”
Kambona na wenzake mara baada ya kusikia kauli hio , jasho lilianza kuwatoka na kusambaa mgongoni kutokana na presha ya ajabu ambayo ilikuwa ikimtoka Hamza.
Kwenye macho yao waliona mwili wa Hamza ni kama umetuna lakini ki uhalisia alikuwa vilevile , ilikuwa ni kama vile amefunikwa na gamba la kivuli cha ajabu na kuonekana kama jitu kubwa.
Hamza aliishia kutingisha kichwa chake akiwapotezea namna walivyokuwa wakimwangalia kwa hofu.
Kati yao ni Kambona peke yake ambae alikuwa amefikia mwishoni mwa levo ya Mzunguko kamili au levo ya mwanzo mwa ukaidi wa asili.Pengine ndio maana mkuu wake alimtuma kuja na wenzake ili kudili nae.
Pia aliona ilileta maintiki , isitoshe Kambona alikuwa na nguvu mara mbili zaidi ya Fabiani kwa kufanikisha kuweza kuwa kitomvu cha mbinu ya muundo wa elementi tano za mapigano.
Kwa lugha nyepesi ni kwamba Fabiani anaweza kuwa katika levo sawa na Kambona lakini Kambona amemzidi kutokana na kwamba yeye ndio aliekuwa na uwezo wa kutengeneza msingi wa mbinu ya elementi tano.
Lakini kwa bahati mbaya watu hao walikuwa wamekosea mahesabu , wakati Hamza akimwadhibu Fabiani hakuwa ametumia uwezo wake kabisa.
“Pumbavu , wewe ni nani?’Waliuliza huku wakishikwa na hofu baada ya kuona Hamza anawasogelea.
“Mhona mmesimama na kuanza kutetemeka , endeleeni?”Aliongea Hamza akiwa siriasi.
“Bro huyu hatumuwezi sio saizi yetu”Aliongea moja ya kijana kati yao na palepale waliangaliana na bila ya kujiuliza mara mbilimbili walipeana ishara na palepale walifyatuka na kukimbia wakimuacha Kambona peke yake.
“Washenzi nyie , msije kurudi kambini nyie wasaliti”Aliongea Kambona kwa hasira baada ya wenzake kukimbia
“Hamza unapaswa kufikiria mara mbili , la sivyo utageuza kambi nzima kuwa maadui labda ni kama hutaki kuendelea kuishi hapa nchini”Aliongea kwa tahadhari.
“Wewe ni m,jinga , kama ningekuwa naiogopa kambi yenu nisingemtia ukilema Fabi mbele za watu”Aliongea Hamza na hakujisumbua kuongea tena kwani palepale alimsogelea Kambona na kumpiga teke la kiuno.
Kambona mara baada ya kuona shambulizi lile , aliona hio ni fursa hivyo haraka sana kwa kutumia ule upanga wake alidhamiria kumkata Hamza mguu, lakini kabla hata upanga wake haujaufikia mguu wa Hamza alishapigwa na teke la tani na kilichosikika ni kishindo kikubwa.
Teke lile lilimfyatua na alienda moja kwa moja kujigonga kwenye dirisha la kioo na kufanya kipasuke palepale na ile anataka kudondokea nje alijikuta akishikilia ukingo wa dirisha akihofia kudondoka kutoka ghorofa ya ishirini mpaka chini, lakini hata hivyo alikuwa katika maumivu makali , kutokana na uzito wa teke la Hamza na alihisi viungo vyake vya ndani vilikuwa vimehama katika nafasi zake na alijikuta akitema damu nyingi.
“Naomba usiniue .. nisamehe tafadhari!”Aliongea kwa kujitetea mara baada ya kuona Master wake alikuwa amekosea , Uwezo wa Hamza ulikuwa ni nje ya fikra zao.
Lakini Hamza alikuwa ameshasogea tayari na bila ya huruma aliukanganya ule mkono uliokuwa umening’inia kwenye kioo .
“Arghhhh!
Kambona alijikuta akipiga yowe kubwa , alishindwa kuendela kushikilia na palepale aliachia na kuanza kuporomoka kwenda chini kama furushi.
Watu waliokuwa nje waliweza kuona mtu akidondoka kuja chini kwa spidi kubwa sana na ile anatua aligeuka kutoka kuwa binadamu na kuwa kifusi.
Watu ambao hawakuwa na moyo mgumu walijikuta wakitapika palepale . Upande wa Regina mwili ulimfubaa lakini alijitahidi kujituliza kadri awezavyo na haraka sana aliwaamrisha Anna na wenzake kusafisha.
Anna alikuwa ni ninja mstaafu na mambo kama hayo hayakumwogopesha , hivyo haraka sana alitii.
“Mkurugenzi nadhani itakuwa vizuri kuwahusisha polisi na vyombo vya habari katika hili ili kuwatuliza”Aliongea Anna.
“Nitampigia simu Kamishina”Aliongea Regina.
Muda huo Hamza aliweza kutoka nje ya jengo hilo , hakuwa na mpango wa kufukuzia wale wanne waliokimbia kwasababu walichokuwa wakifanya ni kufuata maagizo pekee na pia pengine wasingeweza kuwa na ujaisri wa kurudi kambini tena. Alitembea mpaka mbele ya Regina na kisha aliongea;
“Kuna safari naenda hivyo nitakuacha”Aliongea Hamza.
“Unaenda wapi?”
“Napanga kwenda kulimaliza kabisa hili swala”Aliongea Hamza na hakujielezea zaidi kwani palepale aliingia kwenye gari na kupotea.
Regina aliishia kuwa katika hali ya wasiwasi lakini asingeweza kumzuia kile anachopanga kwenda kufanya .
Mara baada ya kazi ya kusafisha kumalizika alijitahidi kutulia na kupanga majukumu ili mpaka kesho siku ya kazi watu wasione tofauti.
*****
Upande mwingine mkoani Iringa katika kambi kuu ya jeshi alionekana Afande Simba akiweka simu chini huku akiwa ni mwenye kuonyesha wasiwasi uliochanganyika na hasira.
“Tatizo la Faruku ni mtu wa kukurupuka sana , ametoa wapi ujasiri wa kutopata kibali kutoka kwetu na kutuma watu moja kwa moja kwenda Dar es salaam kulipiza kisasi”Aliongea .
Alikuwa ndio kwanza amepokea taarifa ya kikosi cha kambi ya Nyoka kutibua hewa katika makao makuu ya kampuni ya Dosam na jeshi la polisi limeshindwa kuingilia na kutaka kitengo cha Malibu kutuma wanajeshi wao kutuliza hali.
Ukweli ni kwamba mara nyingi matatizo ambayo yanahusisha wanajeshi wenye mafunzo ya nishati za mbingu na Ardhi , jeshi la polisi halikujihusisha kabisa.
“Kuna kitu kibaya kinakwenda kumpata Master Faruku, kosa moja ni kutokumjua Bosi wangu ni nani haswa la sivyo asingefanya alichofanya”Aliongea Afande Himidu.
“Hata kama tungemwambia kuhusu Hamza angetuelewa! Ashajiingiza kwenye matatizo tayari huyu. Himidu mpigie simu Hamza na kumwambia asifanye mambo kwa kukurupuka . Tutafanya kila liwezekanalo kumaliza hili swala kwa amani”Aliongea Afande Simba.
“Lakini Afande walichokosea ni kupeleka kisasi chao katika eneo la kazi la shemeji yangu , unadhani bosi anaweza kunisikiliza?”
“Tunapaswa kujaribu Himidu , unajua fika nini kitatokea endapo kaka yake Mheshimiwa Rais akifia katika mikono ya Hamza, mpaka sasa kuna kambi zaidi ya sita ambazo wanafunzi wake wote wapo nje ya nchi kwenye mafunzo na hawajala kiapo bado , kambi hizi zipo chini ya ofisi ya Rais , unadhani nini kitatokea kama akiamua kutumia ushawishi wake wote kuzifanya zimuone Hamza kama adui , maana yake si tu kwamba itakuwa hatari kwa usalama wa taifa lakini vilevile tutapoteza watu wengi ambao wangepaswa kujiunga na kitengo chetu”
Mara nyingi ikitokea raia akajifunza nishati za mbingu na ardhi na akafanikiwa kufika levo ya juu, moja kwa moja kitengo cha Malibu ndio kinamfuata mwanafunzo huyo na kumpa pendekezo la kujiunga na jeshi, hivyo kulikuwa na watu wengi wenye mafunzo ambao bado hawakuwa wamekula kiapo na jeshi na watu hao ikitokea wakitumiwa vibaya ni tishio kwa usalama wa nchi.
Hofu kubwa ambayo Afande Simba alikuwa nayo ni kwamba asilimia kubwa za kambi zote ikiwemo Kambi ya nyoka zilikuwa ni kama matawi tu ndani ya Tanzania lakini msingi wake wa mafunzo ulitokea kambi kuu za nje ya nchi, sasa ikitokea wao wenyewe kama nchi wakishindwa kuzilinda hizi kambi maana yake kambi kubwa za mafunzo kutoka nje watataka kujua maelezo na ikionekana Hamza ndio chanzo watataka kulipa kisasi na pengine pia kuondoa kambi hizo nchini.
“Lakini Afande unadhani hata kama Hamza akifanya anavyojisikia na Mheshimiwa akachukua hatua anayoona inafaa watamuweza..”
“Himidu inamaana unashindwa kuelewa au unataka tu kumsifia bosi wako mbele yangu”Aliongea kwa sauti kavu.
“Usiwe na wasiwasi Afande Simba , nitafanya kama ulivyoagiza ila sina uhakika kama nitaweza kumtuliza bosi , njia rahisi ya kudili na hili swala nadhani ni kumpa kazi Nyakasura na aache kucheza huko Dar”Aliongea Afande Himidu na kumfanya Afande Simba kukuna kichwa akionekana kusita.
“Japo sikutaka kumuingiza Nyakasura katika kudili na Hamza mapema , ila nadhani sina namna , ngoja niwasiliane nae alimalize hili”Aliongea.
Unadhani Nyakasura atamweza Hamza? Usikose.
 
SHETANI RUDISHA AKILI ZETU.

MTUNZI:SINGANOJR.


SEHEMU YA 162.
Damu ya Phoenix.
Ni muda wa saa saba za mchana alionekana Prisila ndani ya jengo la shule ya lugha Maarufu kama Mikocheni language Academy.
Moja ya vitu ambavyo Prisila alikuwa akifanya tokea apate likizo ni kujiandiskisha na kituo hicho cha mafunzo ya lugha , huku kwa upande wake akijifunza namna ya kuongea kifaransa.
Sasa saa saba ya mchana ndio muda ambao alikuwa amemaliza ratiba ya kipindi kwa siku hio na asilimia kubwa ya wanafunzi waliokuwa wakihudhuria vipindi walikuwa wamekwisha kutoka na kumfanya yeye kuwa wa mwisho.
Licha ya kwamba alikuwa amechelewa kutoka lakini njaa ilikuwa ikimuuma sana ni kwamba tu kuna kitu ambacho alikuwa akifanya ndio maana hakutoka haraka haraka kama ilivyokuwa kwa wengine.Hivyo mara baada ya kujiweka vizuri haraka alichukua mkoba wake na kusimama kuanza kutoka.
Lakini sasa ile anageuka kuhakiki hakuna alichokuwa amesahau alijikuta akishituka mno kiasi cha kupiga makelele.
Alikuwa na uhakika asilimia mia moja yeye pekee ndio aliekuwa amebakia ndani ya darasa hilo, lakini anashituka kuona kuna mwanamke alievalia nguo nyekundu akiwa nyuma yake , mbaya zaidi ni kwamba alimjua fika hakuwa mwanafunzi wa hio shule na hata kama alikuwa mwalimu asingeshindwa kumfahamu , kwa ufupi ni kwamba alikuwa akifahamiana na walimu wote.
Mwanamke yule alimuona alikuwa mrembo sana ,hususani pozi lake lilivyoendana na mavazi yake na kitu kikubwa alikuwa akivutia macho mno , ilikuwa ni kama kuna sababu ambayo haikuelezeka inayokufanya utamani kuendelea kumwangalia.
Mwanamke yule alimtisha Prisila sio tu kwasababu ya kusimama nyuma yake , lakini vilevile kwa muda mrefu alionekana alikuwa akimwangalia.
“Dada kuna kitu unataka kuongea?”Aliuliza Prisila kwa kusita , alikosa kujiamini kutokana na kwamba mwanamke huyo alikuwa amemzidi uzuri.
Yule mwanamke katika mavazi mekundu aliishia kuguna kwa namna ya kuitikia.
“Ulikuwa na shida gani?”Aliuliza Prisila na kumfanya yule mdada kufikiria kidogo.
“Hakuna tu , nilitaka kukuona basi”Aliongea na kauli ile ilimfanya Prisila kuwa katika hali ya kuchanganyikiwa na kujiuliza inakuwaje mtu hafahamiani nae na anasema anataka kumuona tu.
“Kuniona tu! Kwanini au tushawahi kukutana?”
“Hapana”Alijibu
“Sasa kwanini unasema ulitaka kuniona tu?”
“Hakuna sababu”
Jibu lile lilimfanya Prisila kujihisi ni kama anaingiwa na ukichaa na kujiuliza nini kinaendelea siku hio?. Kubwa zaidi ni kwamba mwanamke huyo alikuwa akimwangalia kwa namna ambavyo ni kama vile alikuwa akimchunguza kuanzia chini mpaka juu na kitendo kile kilimfanya kuwa katika hofu.
“Dada kama huna cha kuongea naondoka”Aliongea Prisila na kisha alishika mkoba wake vizuri na kuanza kuzipiga hatua.
Lakini sasa haikuchukua muda mrefu Prisila wasiwasi kuzidi kumvaa na hio ni baada ya kugundua huyo dada bado alikuwa akimfuata kwa nyuma wakati akichukua uelekeo wa kuingia mgahawani.
Mwanamke huyo hakika alikuwa mrembo , licha ya kwamba Prisila alikuwa mrembo lakini hakuwa akimzidi huyo mwanamke hasa katika mapozi yake.Mtu anaweza kusema ni binti kutoka falme fulani kwa mvuto wake.
Prisila licha ya kuwa na wasiwasi aliishia kuingia ndani ya mgahawa akifuatiwa na yule mrembo. Kwasasabu ilikuwa ni mchana na eneo hilo limechangamka kulikuwa na watu wengi waliokuwa wakipata chakula cha mchana na wengi baada ya kumuona Prisila na mwanamke mrembo aliekuwa nyuma yake kuingia, walijikuta wakikodoa macho.
Prisila uvumilivu ulimshinda mara baada ya kuona yule mwanadada kamfuata mpaka katika meza aliotaka kukaa na kumwangalia. Kuna hisia zilizokuwa zikimwambia labda mwanadada huyo hakuwa na akili nzuri kichwani , isitoshe kuna muda watu wasiokuwa na akili wanaweza kumpenda mtu ghafla na kuanza kumfuata nyuma nyuma , hizo ndio zilizokuwa hisia za Prisila kwa wakati huo.
“Dada kwanini unaendelea kunifuata?”
“Nataka nikuone ukila”Aliongea bila wasiwasi na kauli ile ilimfanya Prisila kutaka kungea neno lakini aliishia katikati , licha ya kuhisi hasira lakini alijitahidi kujizuia na kuishia kukaa tu huku na yule mrembo na yeye akikaa.
Muda si mrefu mhudumu wa pale alikuja na alionekana alikuwa akifahamiana na Prisila.
“Oh! Prisila naona leo umetuletea mteja mrembo kuliko wewe , ni ndugu yako au rafiki yako?”Aliuliza yule mhudumu mwanamama hivi.
Prisila aliishia tu kutoa tabasamu , ukweli hakujua hata namna ya kujibu swali hilo maana mlengwa alikuwa akimfuata fuata tu akiwa hamfahamu.
“Yeye ndio mrembo kuliko mimi”Yule mwanadada aliongea kwa sauti nyororo akimjibu yule muhudumu na kauli yake iliwafanya wote kumwangalia kwa mshangao kidogo.
“Usishangae ni kweli ni mrembo kuliko mimi , shida tu hajui mavazi sahihi ya kuvaa”Aliendelea kuongea yule mwanamke .
Prisila aliishia kumwangalia tu bila kusema neno , ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuona mtu anabeza mavazi yake.
Yule muhudumu aliishia kucheka tu na kisha aliomba kuchukua oda zao na Prisila ndio aliekuwa wa kwanza kuagiza na yule mwanadada aliagiza pia kilekile Prisila alichoagiza.
Dakika chache mbele chakula kililetwa na utaratibu wa mgahawa ule unalipia palepale baada ya kupewa chakula na Prisila alifanya hivyo kutoa hela kwa ajili ya kulipia cha kwake tu na muhudumu mara baada ya kupokea hela ile alimgeukia na yule mwanadada ili kulipa na alionekana kutokuwa na cash kwani alitoa kadi ya benki na kumpatia.
“Samahani dada hatuna huduma ya malipo ya kadi”Aliongea
“Nitatumia njia ya LIPA na M-pesa?”
“Hata hio huduma hatuna kwasasa”Aliongea na kumfanya yule mrembo kuangalia kile chakula na kisha akaegamia kiti.
“Kama ni hivyo basi sitokula..”
Kabla hajamaliza kuongea Prisila alitoa noti nyingine za elfu tano tano na kumpatia yule muhudumu na akaondoka.
“Kwanini umenilipia?”
“Kwasababu nimejisikia , kama hutaki kula unaweza kuacha”Aliongea Prisila na kisha palepale alijiweka bize na chakula.
Ishara ya mshangao ilionekana katika macho ya yule mwanamke na alikunja lipsi zake kwa namna ya kutabasamu na kisha aliweka sahani yake vizuri na kula.
“Dada bado hujanijibu swali langu , kwanini umenifuata mpaka huku?”Aliuliza tena Prisila.
“Kwasababu nataka kukuona”
“Kuniona! Ukishamaliza kuniona ili upate nini?”
“Nataka kujua wewe ni mtu wa namna gani?”Aliongea yule mwanamke
“Kwanini unataka kujua mimi ni mtu wa namna gani wakati hunijui, ni serikali iliokutuma kuja kunijaribu?” Aliuliza Prisila akikumbuka moja ya rafiki yake kabla ya kuingizwa kitengoni kuna watu waloanza kumfuatilia.
Yule mwanadada aliishia kutingisha kukataa na waliendelea kula wote , huku kila baada ya dakika kadhaa angeinua macho yake na kumwangalia Prisila huku akitabasamu kama vile amekuwa mpenzi wake wa ghafla.
Prisila alijikuta akianza kukosa uvumilivu na hio baada ya kuona yule mwanadada ameenda mbali mpaka kuanza kugiza namna yake ya kula na kutafuna , aliona ni ajabu mno.
“Niambie wewe ni nani hasa”Aliuliza.
“Naitwa Nyakasura”Alijibu yule mwanadada
“Nyakasura!?” Prisila alijikuta akilifikiria hilo jina na aligundua hajawahi kukutana na mtu anaefahamika kwa jina hilo.
“Mimi naitwa Prisila Singano. Eti dada Nyakasura kwanini ulikuwa unanifuata? Lazima utakuwa na sababu zako unaweza kuniambia?”
“Najua unaitwa Prisila Singano”
“Bado hujanijibu swali langu”
“Sitaki kujibu”Aliongea Nyakasura
“Wewe.. unanichokoza sio?”
“Ndio”
“Unamaanisha nini au unanidharau na kuona mimi ni rahisi kuchokozwa eh?”Aliongea Prisila kwa kukasirika lakini yule mrembo aliishia kutoa tabasamu.
Prisila alijikuta akikosa cha kufanya , alijiambia hakika huyo dada alikuwa ni chizi.
“Prisila sisi tunafanana sana , wewe hujui tu”Aliongea.
“Tunafanana kivipi?”
“Vipi kuhusu hio cheni yako shingoni?”Aliuliza yule mwanadada.
“Cheni yangu una nini?”
“Nataka kuona kidani chake”Prisila alitaka kukataa , lakini mara baada ya kumwangalia huyo Nyakasura namna ambavyo alikuwa siriasi alijikuta akikosa jinsi , ukweli ni kwamba kulikuwa na sababu kubwa ya yeye kuvaa kidani hicho kila mahali , alikuwa shabadilisha mkufu wake lakini kidani hakuwahi kukibadilisha na hio yote ni kutokana na baba yake kumsisitizia asikivue kidani hicho. Kuna muda alijihisi labda kina uhusiano na yeye ndio maana baba yake alikuwa akimwambia hivyo.
“Nitakupa ukione lakini hakikisha unanirudishia”Aliongea Prisila huku akijiuliza kwanini anashindwa kusema hapana.
Nyakasura alikichukua kile kidani haraka haraka na kukiweka kwenye mkono wake na mara baada ya kukichunguza macho yake yalionekana kuchanua.
“Vipi unakijua? Unaonekana kubadilika?”
“Nani alikupatia hiki kidani?”
“Ni baba ndio alienipatia , ila alisema kilikuwa cha mama, nimekuwa wa kukivaa kutokana na kitu pekee kinachoniunganisha na mama yangu”Aliongea na kumfanya Nyakasura kuonekana katika hali ya kufikiria na aliishia kukifumbata kwa sekunde kadhaa na kisha akamrudishia Prisila.
“Nyakasura umeshawahi kukiona hiki kidani! Unajua maana yake?”Aliuliza Prisila
“Hapana”Alijibu.
“Oh! Nikajua unafahamu maana yake . Baba alisema licha ya ubora wake lakini ni cha zamani sana na kinaitwa Ciro pendant jina la ishara ya ndege wa kufikirika jamii ya Phoenix”
“Umekosea kinaitwa Sorala maana yake ni ishara ya phoenix jike , Ciro ni ishara ya ndege dume bwana”Aliongea Nyakausra.
“Kwanini? Kuna phoenix wa kike na wa kiume?”
“Ndio ukisikia majina haya , Salaphina , Solara , Emberlyn , Ignisara , Famira au Aurelia ni majina ya kike yenye kuhimidi kiumbe Phoenix, ndege wa kufikirika”
“Unataka kusea nini kuhusu kidani changu , kuna uwezekano wa mtu mwingine kuwa nacho? Nilijaribu kutafuta mtandaoni ila sijaona cha aina yake”Aliongea Prisila
Kauli ile ilimfanya Nyakasura kumwangalia Prisila bila ya kusema neno huku akiendelea kula , alionyesha ishara kama kuna kitu ambacho anajua lakini hakutaka kukiweka wazi.
“Mbona hujanijibu?”Aliuliza.
“Kuna uwezekano kukawa na kingine cha aina yake? Unapanga kumtafuta mama yako mzazi?”Aliuliza.
‘Ndio natamani kumjua mama yangu alivyo”
“Lakini inaweza ikawa sio jambo zuri”
“Najua, anaweza akawa hanipendi ndio maana alinitelekeza , lakini kwasasa nishakuwa mtu mzima nashindwa kuzuia shauku ya kumfahamu mama yangu”
“Njia rahisi ni kumuuliza baba yako”
“Baba anasema na yeye pia hajui alipo”Aliongea Prisila kinyonge na Nyakasura alishia kumwangalia kwa sekunde kadhaa bila ya kuongea neno na kuendelea kula.
Baada ya kumaliza kula , Prisila alivyosimama na Nyakasura alifanya hivyo hivyo na kumfuata mpaka nje na kuchukua uelekeo mwingine ambao unapita katika kiwanja cha Basketball
“Bado tu unaendelea kunifuata?”Aliuliza Prisila na ile Nyakasura alivyotaka kujibu simu yake ilianza kuita
Baada ya kupokea alidumu kwa dakika kama moja akisikiliza na palepale macho yake yalionekana kuchanua.
“Hatimae umenipatia kitu cha kufanya maana nimeboreka mno .. sawa usiwe na wasiwasi nitalifanyia kazi”Mara baada ya kumaliza kuongea alimwangalia Prisila.
“Prisila naondoka ,nitakuja kukutafuta siku nyingine”
“Haina haja ya kuja kunitafuta maana sikujui”
“Nitakuja tu nikitaka”Aliongea na kisha palepale alitembea kupita kando ya kiwanja cha basketi na kulikuwa na wanafunzi waliokuwa wakirusha mpira na mmoja wapo alimrushia mpira kumlenga makusudi.
Prisila mara baada ya kuona vile aliita akitaka kumwambia angalia kuna mpira unakusogelea lakini kilichotokea baada ya hapo kilimshangaza mno ule mpira kabla hata haujamgusa ulipasuka na kuanza kuteketea kwa moto.
Ni tukio ambalo lilitokea haraka sana na watu ambao walikuwa pembeni hawakuweza kuona vizuri lakini Prisila aliweza kuona na yule mtoto piaambae aliogopa na kukimbia.
Jambo lile lilimfanya Prisila kuwa katika hali ya mshituko na kujiambia kabisa kilichotokea kimesababishwa na Nyakasura , kwa wakati mmoja ajabu lile lilimfanya kuanza kukumbuka siku aliofunikwa na moto mwili mzima.
Palepale aliamini moja kwa moja haikuwa bahati mbaya kwa Nyakasura kuja kumtafuta lazima atakuwa anajua pia kuhusu uwezo wake ule wa maajabu. Palepale aliangalia upande alipo Nyakasura akihitaji kumuuliza maswali lakini hakuweza kumuona tena , ilikuwa ni kama amepotea.
*****
Ndani ya safu za milima ya Uluguru ndio inapopatikana kambi ya mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi maarufu kama Kambi ya Nyoka juu kabisa katika vilele vyake zaidi ya mita 2630 kutoka ysawa wa bahari.
Majengo ya kambi hio mengi yalikuwa hayana muda mrefu sana , ki ufupi ni eneo ambalo liligeuzwa na kuwa la kitalii sana , hususani wale ambao walipenda kujaribu kuvuna nishati za mbingu na ardhi kwa kuzingatia elementi za mchanga na miti.
Tokea kuanzishwa kwake kwa kambi hio maeneo vijiji vingi kuzunguka milima hio vilikuwa vimeendelea sana , kutokana na utalii kukua pia.
Sasa siku hio mchana ghafla tu alionekana mtu akijongea uelekeo wa kambi hio akiwa katika pikipiki , huku mdomoni akiwa na sigara , pikipiki yake ilikuwa ikinguruma kiasi cha kufanya baadhi ya watu waliokuwa karibu na barabara kuchungulia.
Pikipiki ile ilikwenda kufunga breki katika geti la kuingia katika kambi hio na alizuiliwa na wanaume wawili ambao ni wafuasi wa mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi kambi ya Nyoka.
“Kiongozi geti la upande huu sio kwa ajili ya watalii , kama unataka kupita upande wa pili rudi kwenye ile kona na kunja kushoto”Aliongea bwana mmoja.
“Sijaja hapa kama mtalii.”Aliongea yule bwana huu akitema ile sigara pembeni na kisha akaendelea kuongea.
“Nimekuja kuua mtu”Aliongea bila wasiwasi kabisa na kauli ile ilifanya wale wanafunzi kushituka. Palepale walihisi kitu na sura zao zilibadilika mara moja.
“Wewe ni Hamza!?”
Hawakuwa wametarajia Hamza atakuja mpaka hapo tena kwa kujiamini namna hio tena wakati wa mchana kweupe.
“Inaonekana mmekwisha kuzipokea taarifa tayari. Vipi mkuu wenu wa kambi ametoroka tayari?”Aliuliza Hamza.
“Unathubutu vipi kuja kwenye kambi yetu ya Nyoka kuleta fujo? Unadhani mkuu wetu anakuogopa mpaka akukimbie?”.
Bila ya kuongea palepale bwana yule alitoa kifaa kama vile ni kibunduki na kupiga hewani na palepale kilitoa moshi wa fataki ambao Hamza alijua fika ni moshi wa ishara.
Hamza wala hakumzuia , ukweli ni kwamba hakuona kama ana haja ya kujali juu ya swala hilo kwasababu alifahamu fika lazima Faruku mkuu wa kambi hio alikuwa akitarajia ujio wake na alishatega mtego na kusubiria aingie.
Wale vijana wawili mara baada ya kutoa ishara ile,hawakujisumbua kupigana kabisa na Hamza na badala yake walikimbia na kupandisha juu mlimani wakiliacha geti wazi.
Hamza alishindwa kujizuia na kuangua kicheko kwa namna ambavyo walitimua , ilionekana washafahamu fika hawamuwezi.
Hamza hata hivyo hakujali , mpango wake kufika hapo ilikuwa ni kwa ajili ya kupigana na kambi yote m hivyo kuua wachache aliona haifai,
Hakuanza kuingia ndani ya geti hilo badala yake alichukua mfuko aliokuwa nao na kisha alifungua ndani na kutoa viazi vitamu vya kuchemsha ambavyo havikuwa vimemenywa na kuanza kuvitoa maganda mdogo mdogo na kutafuna huku akishushia na maji.
Alikuwa amepewa chakula hicho na wanakijiji huko njiani alikopita na aliona atumie kama chakula chake .
Baada ya kuhisi ameshashiba vya kutosha aliegesha pikipiki yake pembeni na kisha alizipiga hatua ndefu kuingia ndani ya eneo hilo kama vile hakuwa amekuja kifujo bali kutalii.
*****
Juu kabisa ya mlima huo katika jengo la makazi lililojengwa kwa usanifu mzuri , alionekana Fabiani aliekuwa amelela kitandani huku akiwa na uso uliopauka.
“Master ni kweli Kaka Kambona amefariki?”Aliuliza Fabiani akilenga swali hilo kwa mwanaume wa miaka kama hamsini hivi aliekuwa ameketi pembeni , alikuwa na sura ya kitanashati mno na alikuwa amevalia vazi mfano wa kanzu, lakini yenye kuachia upande wa chini kama joho.
Mzee huyo ndio aliitwa Master Farook, mkuu wa kambi ya Nyoka.Inasemekana kabla ya kuwa mkuu wa kambi hio alikuwa ni mganga wa kienyeji na ndio aliekuwa mwanzilishi wa mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi ya kinyoka.
“Kulingana na maelezo ya vijana , uwezo wa Hamza ni mkubwa mno kuliko tulivyomkadiria, nimejaribu kuulizia kuhusu namna ya mafunzo yake kutoka sehemu nyingi duniani na wanasema pengine ni aina ya mafunzo ya mnyororo maarufu kama Kifunika Tumbo, mbinu ambayo ni ngumu sana kuhimili”
“Mimi ndio msababishaji wa haya .Isingekuwa mimi Kambona asingeweza kufa mapema”
“Fabiani , hili suala sio la kwako peke yako , linahusisha hadhi ya kambi yetu ya Nyoka. Kambona hajajitoa kafara bure”Aliongea Farook.
“Kaka Kambona alikuwa mwanzoni mwa levo ya Ukaidi wa asili lakini amekufa kama hivyo…”Aliongea Master huku akionekana kuwa na hasira mno.
Bado walikuwa na hofu mno na Hamza , wakiogopa kama akija hapo na kuiangusha kambi yao , wataonekanaje mbele ya kambi zingine.Isitoshe kuwepo kwa kambi hio kulikuwa kukimpatia fedha nyingi sana , mafanikio ya kambi yake maana yake sio tu kitengo cha Malibu ambacho kitaingia ubia na yeye kuendeleza mafunzo , bali vitengo vingi nje ya nchi vingetuma wanajeshi kwa ajili ya kujifunza mbinu yao maana yake hela zingeendelea kumiminika.
Kambi nyingi changa ambazo ndio zinaanza kuweka mizizi yake nchini walimu wake ambao ndio wakuu wa kambi hizo walikuwa wakipambana usiku na mchana kuhakikisha wanafunzi wake wanapanda levo na kufikia juu ili kujijengea hadhi ya kuaminiwa na taasisi kubwa na kupewa ubia wa mafunzo.
Mfano Master Farook hakuwa mwanajeshi hapo kabla , iliaminika alikuwa mganga wa kienyeji ila baadae ndio akaja kuamini alipata ufunuo wa Nyoka katika mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi ndio maana akaja kuanzisha kambi kijijini kwao na baada ya mafanikio alipewa cheo maalumu cha Uanajeshi na Kitengo cha Malibu , cheo cha ukufunzi wa jeshi.
“Fabiani ni sahihi kwako kuwa na wasiwasi , isitoshe wewe ni kapteni wa kitengo cha kudhibiti uvamizi , ulikuwa ni kongozi tarajiwa wa kambi yetu , lakini kufanya kilema namna hii imesababishia aibu kubwa kambi yetu. Hata kama huyu mtoto Hamza anao uwezo hana watu wa kumkingia kifua hapa nchini .Akijifanya jeuri na kuvamia hapa hawezi kuwa salama..”Aliongea Farook.
“Master kwanini tusitumie mbinu yetu ya Ndimi 36 za nyoka kumzingira kisha kumuua .Hata kama Hamza yupo levo ya Ukamilifu Mkuu hawezi kuwa na uwezo wa kuhimili nguvu ya shina la ulimi wa Nyoka”
“Nimefikiria pia kuhusu hilo lakini huyu Hamza bado sijakutana nae na bila kukadiria uwezo wake mbinu yetu inaweza isifanye kazi”Aliongea Master Farook
“Haiwezekani tukamshindwa! Master au unahisi huyu Hamza amefikia levo ya Maono ya Mbingu. Hilo ni daraja la juu sana na mpiganaji yoyote wa kufikia hatua hio anahesabika kama mpiganaji namba moja dunia nzima”
Kawaida Daraja la Ukaidi wa asili au mbingu inafuatia hatua ya levo ya Nafsi, katika levo hii mara nyingi mtu anakuwa kama amezaliwa upya maana yake nafsi yake ipo nje ya vishawishi vya kiasili na mwili wake haufungwi na asili au mazingira , katika daraja hili mtu anakuwa na nguvu kubwa ya kiroho matokeo yake anaweza kunyonya sana nishati ya mbingu na ardhi ndio maana wengine wanaita hatua hii kama daraja la Nafsi Mkandamizo , kadri mtu anavyonyonya nishati za mbingu na ardhi ndio uwezo wake wa akili hupanuka na jicho la tafu hufunguka na kushuhudia maajabu ya ulimwengu.
Kwa ufupi ni kwamba kabla ya Nafsi Mkandamizo mtu anakuwa hana tofauti kubwa na binadamu , faida kubwa ni kwamba kama amefikia levo ya Mzunguko kamili mwili wake unakuwa na nguvu kubwa sana na anaweza kuhimili kifo cha mapema.
Kwa mfano mtu yoyote ambae hana mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi huyu daraja lake anaitwa Binadamu katika asili , akianza mafunzo anaitwa binadamu mwenye mafunzo katika daraja la nusu Mzunguko , faida kubwa katika daraja hili ni kwamba mtu anakuwa na bahati sana na bahati yake ndio inayomvusha na kuingia daraja la Mzunguko kamili na hatimae kabla na baada ya Ukaidi wa sili . Sasa levo zote kwanzia Binadamu katika asili mpaka daraja la Ukaidi wa asili watu wote hujumuishwa katika kundi moja linaloitwa Binadamu Kabla ya Mbingu ambapo kila binadamu anakuwa ni mwenye Kutafakari.
Ukiingia daraja la Baada ya Mbingu kwanzia levo ya Nafsi Mkandamizo na kuendelea wanafunzi wake hawana haja ya kukaa chini na kutafakari au kufanya tahajudi au kusali sana, mambo yanajipa yenyewe kulingana na uzoefu unaopitia.Kwa lugha nyepesi unakuwa Binadamu katika Ufunuo.




















SEHEMU YA 163
“Haiwezekani akawa juu ya levo ya ukamilifu! Mpaka sasa mtu pekee ambae amefikia levo ya Ukamilifu na Maono chini ya miaka therathini ni Nyakasura peke yake na ameweza kwa msaada wa damu yake ya moto wa asili ya jini ndege. Huyu Hamza kwa umri wake hata kama awe na uwezo wa juu hawezi kumzidi binadamu mwenye damu ya Phoenix. Ninachoona lazima mwili wake umepitia maboresho makubwa. Lakini hata hivyo mtu kuwa na uwezo wa aina yake inatisha mno , akiruhusiwa kujiendeleza kwa miaka kadhaa atakuwa amenizidi mbali sana”Aliongea Master Farook na mara baada ya Fabiani kusikia hivyo alijikuta akishikwa na ahueni.
“Naunga mkono hoja Master , kama angekuwa katika levo ya Nafsi Mkandamizo kitengo cha Malibu wasingelala , lakini mkuu wa majeshi hakuwahi hata kumwongelea hii inatuaminisha bado yupo chini ya levo hio”Aliongea Fabiani.
“Tena kuhusu Afande Simba wewe ni kapteni wa jeshi lakini umeumizwa na Hamza bado hakufanya chochote , inaonekana kabisa amekupotezea na anataka kumwingiza Hamza jeshini”Aliongea Master akiwa na mwonekano uliojaa kejeli kwa Afande Simba.
“Kwasababu ameonyesha kudharau ustawi wako asije kunilaumu kabisa. Hamza akitia mguu hapa nitahakikisha anarudi akiwa marehemu”Aliongea akipiga mkwala wa kibabe kabisa akijiamini alikuwa na uwezo mkubwa kumzidi Hamza.
Lakini muda huo wakati akiongea sauti ya ajabu iliweza kusikika na kumfanya achungulie.
“Ni ishara yetu! Naona kweli kajileta, Afande Simba ameniambia nisifanye kitu ila nadhani sina namna tena ya kumfundisha adabu huyu mtoto”Aliongea.
“Master kuwa tu makini , Hamza sio mwepesi sana kudili nae”
“Usiwe na wasiwasi Fabiani , mimi Master wako nitakusaidia kulipa kisasi”
Mara baada ya kuongea palepale alitoka nje kwa spidi kwa kutumia mbinu yao maarufu ya Mtambao Nyoka na kadri ambavyo aliongeza spidi ya kutambaa kwa kuinamisha mgongo ni kama ndege inayojiandaa kupaa kwani spidi yake iliongezeka mno na ndani ya dakika tu alikuwa chini ya mlima katika nusu kilele chake.
****
Hamza kutokana na kushiba viazi vitamu alitembea mdogo mdogo ili chakula kikae sawa na mara baada ya kutembea mpaka kufikia nusu kilele aliweza kufika eneo ambalo lilikuwa kama vile ni kiwanja cha mpira , sehemu ambayo imezungushiwa uzio na kuonekana kama vile ni ulingo huku mbele ya eneo hilo kulikuwa na geti lenye maandishi makubwa Gamba la Nyoka.
Lilikuwa ni eneo maalumu takatifu kwa Kambi hio, mahali maalumu kwa ajili ya Ibada ya kujivua Gamba, kulikuwa na utaratibu maalumu kulingana na levo ya wanafunzi kuhudhuria eneo hilo kwa ajili ya kujivua Gamba kama sehemu ya mafunzo, kadili unavyokuwa katika levo ya juu ndio muda wa kujivua Gamba unavyokuwa mrefu , ila kwa wale wanaoanza mara nyingi ni kila baada ya wiki mbili mpaka nne. Aunaweza kufananisha ibada hio na toba.
Sekunde ambayo Hamza alitaka kupita katika eneo hilo kusonga juu kileleni , wanafunzi kibao waliokuwa wamevaa rubega walishuka kutoka juu huku wakiwa wameshikilia mikuki.
Hamza aliona kambi hio sio dhaifu sana , maana karibia ya wanafunzi wote waliokuwa wameshikilia mikuki walikuwa katika levo ya Nusu Mzunguko.
“Mkunjo wa Nyoka! Jipangeni katika staili ya mviringo wa nyoka”Aliongea bwana mmoja kwa sauti na palepale wapiganaji wale saba wa mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi walimzingira Hamza katika muundo wa kushangaza mno, walikaa staili ileile kama vile ni nyoka anaejiandaa kung’ata , ukiangalia utadhani ni maonyesho ya sarakasi kwa jinsi walivyopandiana.
Hamza mara baada ya kuona fomesheni hio alijikuta macho yake yakisinyaa , alishawahi kusikia juu ya watu wanaojifunza nishati za mbingu na ardhi kwa msingi wa asili ya Nyoka walikuwa na staili yao maarufu ambayo inaitwa Kifo bila wasiwasi.
Mbinu hio aliwahi kuisikia tu lakini hajawahi kudili nayo wala kupata uzoefu wa kupigana na wapiganaji waliokuwa katika mkao wa namna hio.
Aliona ili kushindana na mbinu ya namna hio , kitu pekee ambacho anaweza kufanya ni kutegemea mwili wake na kuwapunguza nguvu , vinginevyo atajikuta katika hali tatanishi.
“Hamza tumeshakuzingira na mbinu yetu ya Kipigo Cha Milele, onyesha utii kwa kupiga magoti na sujudu mara nane kisha kubali makosa yako na tuachie sisi tutamshawishi Master akusamehe”Aliongea askari mmoja aliekuwa katika levo ya Ukaidi.
Muda ule Hamza aliinua macho yake na kuangalia juu na aliweza kumwona mzee ambae alikuwa amesimama katika jabari akiwa amekunja mikono yake kwa nyuma.
“Mzee Farook una kambi kubwa namna hii lakini kwasababu tu ya kulipiza kisasi cha mtoto wako wa nje ya ndoa , umeamua kutuma watu wako kwenda kwenye kampuni ya mke wangu kusababisha vurugu bila ya kujali hadhi yako. Hata ulimwengu wa giza una kanuni zake za kutohusisha watu ambao hawajakuchokoza , kwa ulichofanya unatosha kweli kuwa kiongozi wewe?”Aliongea Hamza, hakuhitaji mtu kumtambulisha kumfahamu Mzee Farook maana uwezo wake tu ulionyesha.
“Unaongea upuuzi! Fabiani ni mwanafunzi wangu na mwanafunzi wangu pendwa amejeruhiwa na mhalifu mkubwa kama wewe ni swala la kawaida kwa kambi yetu kukuchukulia hatua”
“Roja haina haja ya kupoteza maneno yetu , kama hayupo tayari kutii masharti muueni”
“Sawa Master!”
Mara baada ya kuongea hivyo haraka sana wale wanafunzi therathini na sita walianza kulipua nishati zao za mbingu na ardhi kuzizungusha na kufanya lile eneo Hamza alipo simama kutengeneza kimbunga cha nishati ya mbingu na ardhi.
“Enyi wafuasi wote wa Nyoka na mnisikilize ! Huyu mtu anao ujuzi wa kujilinda hivyo tutalenga maeneo dhaifu ya mwili wake”Aliongea Roja ambae alikuwa amejiandaa muda mrefu sana na mara baada ya kutoa maagizo hayo palepale alitoa ishara ya mzunguko wa kwanza kushambulia.
Dakika ile Hamza alianza kuhisi hali ya ubaridi mkali mno sana ulioambatana na mkandamizo wa nishati za mbingu na ardhi na kumfanya ni kama vile sumu inasambaa katika mwili wake.
Siraha ya baridi , ilikuwa ni kama sumu ya nyoka inavyoanza kusambaa katika mwili na kumfanya mtu kuwa wa baridi na kuhisi vichomi , ilikuwa ni mbinu rahisi lakini yenye shambulizi la moja kwa moja la kusababisha maumivu.
Hamza palepale aliweza kujua ni katika mzunguko upi wa mashambulizi unakotokea na alipanga kuvunja pigo lile lakini palepale aligundua kuna kitu hakipo sawa kwani askari waliokuwa katika mzunguko wa pili walishambulia pia kama vile wanatengeneza wimbi lingine ili kuongeza nguvu lile la kwanza.
Hamza alijua pigo la kwanza ilikuwa ni la kuulegeza mwili wake ili kuruhusu mzunguko wa pili kushambulia maeneo muhimu ya mwili , ijapokuwa mwili wake ulikuwa vizuri lakini kwa shambulizi la namna hio aliona ni nguvu kushindana nalo.
Kitu pekee alichoona hapo ni kukwepa mashambulizi yote. kama mmasasi aliruka mara moja chini na mara ya pili alikuwa juu angani lakini ni kama walishategemea angefanya hivyo.
“Unadhani unaenda wapi?”Waliongea askari waliokuwa katika mzunguko wa mwisho kabisa na ilikuwa ni kama mzunguko wao ulijikunja zaidi kwa kuwa mwembamba kwa kutumia mbinu yao ya Mtambao wa Nyoka wakitaka kumzuia Hamza asipite kwenda angani.
Hamza mpaka hapo alijua hakuna namna ya kuepuka na aliishia kujisemea Safu hio ya mashambulizi ilikuwa nzuri mno.
Mpaka hapo aliona hana uwezo wa kujikinga na mashambulizi yale tena , hivyo kitu alichofanya ni kutumia mikono yake na miguu kujikinga sehemu muhimu za mwili wake.
Baada ya kupokea shambulizi lile kilichoweza kusikika ni kuchanika kwa shati alilokuwa amevaa na kumfanya atie huruma.
Kitendo cha kutua chini na sarakasi mzunguko wa chini walikuwa wameachia shambulizi na kumchoma na mashambulizi ya nishati za ubaridi , kibaya zaidi wale waliokuwa juu walimwangushia shambulizi kulenga mabega yake.
Mashambulizi yale yalimfanya Hamza kuonekana kama vile ni kitu kilichotolewa kwenye friji la kugandisha na kufuka mvuke wa ubaridi.
Hamza alihisi mwili wake wote kufa ganzi kwa maumivu makali , hakika aliweza kuona mbinu hio ilikuwa na ukali ambao sio wa kawaida hata kidogo . Kama sio uzoefu wake wa kupitia vita vingi angeweza kuogopa kufa.
Lakini kwa mtu kama Hamza maumivu kama hayo aliyachukulia kama kionjo katika uwanja wa vita , hisia za kuwa katika mazingira ya kifo na uhai ndio kitu ambacho alikuwa akitafuta.
Bila ya kupata uzoefu wa kifo na uhai huwezi kukua na kustawi katika swala zima la mapigano.
“Endeleeni!”Aliongea Hamza huku akicheka
“Bado unaonyesha kiburi”Aliongea Roja huku akimwangalia Hamza kwa macho ya kumheshimu.
Palepale alitoa ishara ya kuundwa kwa safu ya ndimi therathini na sita na kutengeneza Siraha maalumu wanayoita Mkuki ndani ya pango la kifo.
Hamza palepale aliweza kuona katika mzunguko kuna upenyo kutoka kwa mmoja ambae alionekana kutokuwa katika levo sawa na wenzake ya mafunzo na palepale kwa spidi kubwa alijifyatua kwa kujiviringisha akikwepa lile shambulizi la mkuki wa kifo kwenda hewani.
Miguu yake ilikuwa ni kama mtalimbo wa chuma kwa namna ilivyosogea na kufyeka wafuasi kadhaa.
Miguu ya wafuasi wale ilishindwa kuhimili nguvu ya shambulizi lile na wote walijikuta wakidondoka chini na kuharibu uwiano wa safu ile .
Kama wangekuwa kivyao wangekuwa na uwezo wa kukwepa shambulizi lile , lakini muda huo walikuwa katika safu ya mashambulizi hivyo kuishia kukubali kupigwa na Hamza.
Wafuasi wale walijikuta wakipiga makelele ya maumivu bada ya miguu yao kuvunjwa na Hamza.
Hamza aliishia kuangalia namna kipande cha ule mzunguko wa kimashambulizi ukidondoka chini.
Roja na wenzake walijikuta wakishikwa na mshituko mkubwa.Hawakuwahi kuona mtu ambae ana mbinu ya ajabu kudili na mbinu yao ya mapigo bila ukomo.
Ukweli ni kwamba walishindwa kutafisiri mbinu ya Hamza ilikuwa ni ya mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi au ilikuwa ni mapigo ya kikale , alikuwa akionyesha kitu ambacho kipo nje ya mafunzo ya kawaida ya sanaa ya mapigano na kufanya aweze kuharibu safu ile ya shambulizi la mzunguko wa nyoka kwa shambulizi moja tu.
Safu yao ya mshambulizi ilihitaji watu kamili , kitendo cha Hamza kuvunja miguu kadhaa , maana yake alikuwa ameharibu kabisa mbinu ile na wasingeweza kufanya chochote labda waongezeke wengine na jambo hilo lilimfanya Roja na wenzake kushikwa na hasira mno.
Ilikuwa ni mara yao ya kwanza kukutana na mtu ambae amefanikisha kuharibu safu yao ya mshambulizi ndani ya dakika chache tu tena bila ya kumtengenezea madhara.
Mzee Farook ambae alikuwa amesimama juu ya jiwe akiangalia mashambulizi hayo alijikuta akiwa na mwonekano usioelezeka. Karibia wapiganaji wote katika makambi yote makubwa nchini na hata yale makubwa nje ya nchi walikuwa na mifumo yao ya pamoja ya kimashambulizi lakini hakuwahi kuwaza kama Hamza kuja tu ataweza kuharibu mfumo wao.
Haikuwa na shaka Hamza spidi yake ya kurusha mashambulizi , uwezo wake wa kimwili na uzoefu wa kivita pengine ndio kitu ambacho hawakuweza kukiweka katika mahesabu ndio maana wameweza kudhibitiwa ndani ya muda .
“Jibadilisheni!!”Mzee Farook aliishia kung’ata meno yake kwa hasira akipiga kelele.
Roja mara baada ya kusikia maneno hayo kutoka kwa Master wake palepale alitoa maelekezo meingine.
“Nyota Ndau za Kaskazini , Mtutumuko wa Joka!”
Mara baada ya kuongea hivyo palepale wale wafuasi walijigawa katika timu tatu na kutengeneza umbo la nyota na kuanza kusogea kwa namna ya kututumuka uelekeo wa Hamza.
Wakati huo huo Roja na wenzake watatu waliokuwa katika levo ya ukaidi walipita katika kona zile tatu za nyota na kuanza kushambulia
Muundo huo ulionekana kuwa mzuri kwenye kurahisisha mashambulizi lakini hakuwa mkali zaidi kama ule wa mwanzo.
Hamza hakuamini kama wangekuja na mbinu nyingine licha ya baadhi ya wenzao kuumia . Alijikuta akizidi kuvutiwa na pambano hilo na mara baada ya kuona watatu wanamshambulia kama vile ni wawindaji palepale aliruka kwa ustadi na kuwekwepa mashambulizi yale na kufanya yakutane kati na Hamza alikanyaga katika kile kiungio cha mashambulizi yao na kupangua.
Staili ile ya kuruka na pili mashambulizi yao kukutana katika eneo moja iliwashangaza sana Roja na wenzake . Hawakuamini Hamza sio tu kuweza kukwepa mashambulizi yao lakini aliweza kuyasambatarisha.
Roja hakutaka kuzubaa baada ya kuona shambulizi lao la pili limefeli palepale alitoa maagizo ya muundo mwingine.
“Shambulieni kwa mtindo wa Siraha Mkondo upepo”
Mbinu ya Siraha Mkondo upepo ndio mbinu ya juu kabisa katika kambi hio , mbinu hio ilikuwa ikitumia siraha kamili za chuma ambazo zilikuwa kama visu , siraha hizi ni ndogo hivyo mara nyingi ili kushambulia zinadhibitiwa na nguvu ya kinishati mkondo wa upepo.
Kutokana na staili yao waliokuwa wamekaa , ilifanya mashambulizi yale kuonekana kama bahari tatu zinakutanaisha mawimbi yao katikati na kumfanya Hamza kuchanwa na visu vile kila upande.
Mbaya zaidi visu vile havikudondoka chini vilivyokuwa vikitoka kulia vilihama upande mwingine na kuzibitiwa na wengine huku vya upande mwingine kudhibitiwa na upande mwingine na kadri mashambulizi yalivyokuwa yakiendelea ilipelekea eneo lile la kati Hamza alipo kuwa kama kiumbunga.
Hamza alipokea mikwaruzo kibao ya visu vile , alichoshukuru vilikuwa spidi sana hivyo havikuweza kumkata kwa kwenda ndani na kutokana na ugumu wa ngozi yake ilisaidia sana , lakini suruali yake ilikuwa haivaliki tena.
Hamza baada ya kuona mashambulizi yamekuwa mengi , aliona ni upuuzi kusubiri waishiwe nguvu na badala yake palepale alipotezea kuchomwa na visu na alisogelea wafuasi waliokuwa kushoto kwake kwa spidi kubwa
“Arghhhhhhhh…!
Hamza alibweka kama mbwa wakati akikatwa na visu vile lakini wakati mmoja akitoa shambulizi la tani kadhaa kutoka kwa kundi moja na hakuhitaji kushambulia mara mbili kwani askari wale walijikuta wakiwa chini wengine wakiwa wamevunjika miguu wengine wakiwa na majeraha ya siraha zao wenyewe.
Hamza angetaka kuwaua palepale , lakini hakutaka kufanya hivyo ,alikuwa na mpango mwingine kichwani.
“Huyu mtu ni shetani nini!”
Roja alijikuta akiwa katika hali ya mshituko mkubwa . hawakuwahi kuona mtu asiejali kushambuliwa kama Hamza , kwa namna alivyovamia visu bila ya hofu ili tu kufanya shambulizi ilishangaza.
Yote hayo ilikuwa ni kutokana na utimamu wake wa mwili na nguvu kubwa.
Wafuasi hao wa kambi ya Nyoka walijikuta wakikata tamaa , waliona hawakuwa wakipigana na mpiganaji bali walikuwa wakipigana na jitu ambalo haliogopi maumivu.
Dakika chache mbele Hamza alikuwa ashafanikisha kuwashinda wafuasi wote therathini na sita na kubakia Roja na wenzake wanne.
Mzee Farook akiwa amesimama katika jiwe alijikuta akiwa katika hali ya kutoamini kile anachoona . Tokea mwanzo mpaka mwisho alishindwa kujua ni aina gani ya mbinu Hamza anatumia kwenye kushambulia.
Hamza alijikuta akijifuta damu zilizokuwa zikitoka katika mgongo wake na kisha alimwangalia Roja na wenzake.
“Ninachotaka ni kumuua Master wenu tu , kama na nyie mnataka kufa sogeeni”Aliongea Hamza.
“Acha majigambo , humuwezi Master wetu”
“Kweli , kutuweza sisi usidhani utamuweza na Master”
Wafuasi wale wa Mzee Farook walianza kumtetea Master wao lakini maneno yao yalikuwa yamejaa hatia , hakuna aliekuwa na ujasiri kumsogelea Hamza tena , uwezo wake ulikuwa haupimiki.

ITAENDELEA- Watsapp me 0687151346
 

SHETANI RUDISHA NAFSI ZETU​

MTUNZI:SINGANOJR​





SEHEMU YA 165.

Fire and Ashes rebirth.

(Nyakasura).

Hamza alijikuta akijifuta damu zilizokuwa zikitoka katika mgongo wake na kisha alimwangalia Roja na wenzake.

“Ninachotaka ni kumuua Master wenu tu , kama na nyie mnataka kufa sogeeni”Aliongea Hamza.

“Acha majigambo , humuwezi Master wetu”

“Kweli , kutuweza sisi usidhani utamuweza na Master”

Wafuasi wale wa Mzee Farook walianza kumtetea Master wao lakini maneno yao yalikuwa yamejaa hatia , hakuna aliekuwa na ujasiri kumsogelea Hamza tena , uwezo wake ulikuwa haupimiki.



“Kama mmeamua kuwa mashabiki endeleeni”Aliongea Hamza mara baada ya kuona wale wafuasi wa Master Farook wakianza kumpa sifa ambazo aliamini hakuwa nazo.

Mara baada ya kuongea maneno hayo , aliruka mara moja chini kuazima nguvu za miguu na ile anaruka mara ya pili aligeuka kuwa kama mshale akiruka uelekeo wa alipo Master Farook.

Mzee Farook mwanzoni alidhania kama Hamza angetaka kumfikia mahali alipo angekimbia kwa kuzunguka mlima huo baada ya kuona hakuwa na ishara yoyote ya kuwa na nishati za mbingu na ardhi lakini hakutegemea Hamza angeruka kama kombora kwa kutegemea nguvu ya miguu yake pekee.

Hamza alikanyaga kwenye jabari moja tu kuongeza nguvu na kisha alifyatuka kwa mara nyingine na kufikia katika jiwe kubwa ambalo alikuwa amekanyaga Master Farook.

Mzee Farook alikuwa katika mshituko mkubwa kwa ndani lakini bado alikuwa kiongozi wa kambi yake hivyo haraka sana alikusanya nguvu zake zote za mbingu na ardhi huku mkono wake ukifikia siraha iliokuwa katika kiuno chake.

“Nadhani hujawahi kutoa machozi mbele ya jeneza. Unadhani kambi yetu ni kama kambi zingine tu kuvamia unavyotaka?”Aliongea Mzee Farook kwa sauti ya chini.

“Ongea yako haiendani na wasiwasi uliokuwa nao . Kama nimeweza kuvunja mbinu yenu ya mizinguko theratini na sita kwanini nikuogope”Aliongea Hamza

“Acha majigambo , umepata bahati kufanikiwa kuepuka safu yetu ya ulinzi . Wewe sio mtu wa kwanza kufanikiwa kutoka katika mtego wa safu yetu, acha kujiona mwamba”

“Kumbe! Sijawahi kuwaza kuna mwingine zaidi yangu. Wewe na mtoto wako ndio watu pekee mnaodhani mna nguvu ya kutosha kwenda mjini na kutibua kampuni ya mke wangu mnavyojisikia kwasababu ya koneksheni zenu. Mambo ya wanaume yalipaswa kumalizwa kiume , haikuwa na haja ya kuingiza watu wa nje”Aliongea Hamza.

“Hahaha! Wewe mtoto haijalishi utasema nini , kwangu mimi nakuona kama kichaa aliejaaliwa mwili wenye utimamu. Hivi unadhani nimesimama kihasra katika huu mlima?”Aliuliza na kauli ile ilimshangaza Hamza na kujiuliza kwanini aanaongea hivyo au ameweka mtego.

Lakini sasa dakika hio hio Mzee Farook mara baada ya kuona Hamza akishangaa alichukulia hio kama nafasi na alifyatuka kumsogelea Hamza huku akinyoosha siraha yake ya upanga mbele.

“Nishati safi , Hasira ya upanga butu!”

Mara baada ya kuongea hivyo upanga wake usio na makali ambao ulitoka katika Alla iliokuwa na umbo la nyoka ulikuwa ukimeremeta mno kiasi cha kuumiza macho baada ya kutawaliwa na nishati ya mbingu na ardhi.

Hamza kuangalia upanga ule alihisi ni kama tayari ushamfikia machoni na kumfanya aongeze umakini na ile anaukwepa kilichosikika ni ‘ siii’ upanga ule ulimpitia kwenye shavu lake na kumfanya kutokwa na damu kiasi.

Hamza alijikuta akigusa shavu lake na kugundua alishatengenezewa kidonda usoni. Alijikuta akishindwa kujizuia na kushikwa na ubaridi mgongoni kwa shambulizi lile.

Nishati safi hasira ya upanga butu ilikuwa ni mbinu nyingine kambi hio ilikuwa ikitumia , mara nyingi upanga unakuwa butu kabisa kiasi kwamba hata kukata mgomba inaweza kuwa ngumu lakini wakati wa kushambulia makali yake hutengenezwa na nishati za mbingu na ardhi. Moja ya sababu ya upanga huo kuachwa butu ni kutokana na aina ya matumizi yake kwenye kushambulia ikiwa mikononi mwa mvuna nishati.

Hamza mara baada ya kukatwa alishangaa, hakutegemea upanga kama huo unaweza kumkata na kumtengenezea kidonda tena ndani ya shambulizi moja.

Hamza sio kwamba hakuwa akiijua mbinu hio ya nishati safi hasira ya upanga butu , ukweli alikuwa akiijua sana lakini ni watu wachache sana waliokuwa wakijifunza kutokana na ugumu wake. Si rahisi kuufanya upanga ambao ni butu kuwa na makali zaidi ya makali ya kiwembe.

Hamza aliona sio haba , Master huyo alistahili jina lake , alitumia mbinu ya kumchanganya kidogo na kisha kumshambulia na aliona kama isingekuwa uzoefu wake wa mapigano angeweza kudhibitiwa na shambulizi moja tu.

Master Farook mara baada ya kuona shambulizi lake la mwanzo limefeli , palepale alibadilisha mbinu yake kwa kuchezesha upanga hewani kwa namna ya kufyeka huku kila akifanya mkato Hamza ni kama alikuwa akihisi vitu kama vinyota vikimchoma mwilini bila kuguswa na upanga ule.

Hamza hakutaka aendelee kumshambulia kwa kutumia upanga huo kumsambabishia maumivu bila ya kumgusa , hivyo aliangalia staili ile ya upanga inavyofyeka hewani na kisha na yeye angeruka kukwepa shambulizi. Isitoshe alijua mbinu ya kutumia upanga butu sio rahisi pia kwa Master Farook maana alihitajika kuunganisha nishati za mbingu na ardhi na upanga huo kabla ya kushambulia kuutengezea Aura ya makali.

“Nadhani ndio maana wanakuita Master na Fabiani kuwa mtoto wako , mbinu ya matumizi ya Upanga butu imekwisha kupitwa na wakati lakini umeweza kuifufua. Hakika kuwa Mkuu wa kambi sio swala jepesi”Aliongea Hamza.

“Acha kuongea ujinga , kama uwezo unao shindana na upanga wangu acha kukwepa”

“Hakuna shida , twende kazi”Aliongea Hamza na palepale alisogea mbele na ile Mzee Farook anataka kutumia upanga wake Hamza alishaushika tayari na mikono yote miwili.

“Arghhhhhhhhhhhhh!

Hamza alinguruma kwa sauti kubwa sana huku akiwa ameushikilia ule upanga na sekunde chache mbele kilichoweza kusikika ni ‘Clang’ na ule upanga kuvunjika vipande viwili.

Kitendo kile cha Hamza kuukata upanga wake ilimfanya Master Farook kurudi hatua nyuma akimwangalia Hamza kwa hofu.

Sifa nyingine ya kufanya upanga huo kuitwa butu ilikuwa ni ule ugumu wake , lakini Hamza kwa kutumia tu nguvu za mikono yake amefanikiwa kuuvunja , ilikuwa ni kutu cha kutisha mno kutoka kwa binadamu.

Hamza aliishia kutupa vipande vya ule upanga na kujiangalia mikononi na aliweza kuona kuvilia kwa damu kwenye mikono yake lakini hakujali.

“Mbinu ya Upanga butu kwangu ni kama kichekesho , kama una siraha nyingine, toa tuone”Aliongea Hamza huku akitoa tabasamu la uovu.

Chini ya kijimlima hicho kulikuwa na wafuasi wa kambi hio na walishangaa baada ya kuona Master wao ameweza kupokonywa mpaka siraha yake na ikavunjwa.

Mzee Farook mara baada ya kuona ameweza kupokonywa upanga wake alijikuta akikasirika sana na aliamua kutumia nishati zake za mbingu na ardhi kumshambulia Hamza.

Muda ule alibadilika na kuanza kutumia mbinu ya mneso wa nyoka na kadri alivyokuwa akitumia mbinu ile miondoko yake iliongezeka spidi kiasi cha mwili wake kuonekana kama kivuli akimshambulia Hamza.

“Kani mtungo!”

Mzee Farook mara baada ya kugundua Hamza mwili wake ulikuwa mgumu sana kushambulia aliona atumie mbinu ya Kani Mtungo kwa ajili ya kushambulia katika maeneo dhaifu ya mwili wake kwa kutumia vidole kwa namna ya kudunga.

Lakini Hamza macho yake yalikuwa ni kama ya mashine kwani sekunde ambayo Master Farook anataka kumshambulia na mkono wake aliruka na teke na kuupiga ule mkono.

“Arghhh!” Mzee Farook alitoa ukulele mkali wa maumivu kutokana na mkono wake kuvunjika.

“Master!!”

Wanafunzi wake walipiga makelele , hawakuweza kuona hata Hamza amempigaje.

Mzee Farook aliishia kujishikiza kwenye mti wa mkaratusi asidondoke chini na bila ya kuongea neno paleplae alitafuta upenyo wa kukimbia kwenda chini baada ya kuhisi hatomuweza Hamza.

Hamza mara baada ya kuona anataka kukimbia hakutaka kumruhusu kirahisi hivyo alimsogelea kwa spidi.

Mzee Farook alikuwa ametumia takribani uwezo wake wote na wakati wa kukimbia hakujali kama wanafunzi wake walikuwa wakimuona , aliishia kupiga kelele akiita jina la Mjomba.

“Mjombaa! Mjombaa kambi ipo matatizoni”Aliongea hivyo huku akiendelea kuomba mjomba huyo kuijitokeza ili kumdhibiti Hamza.

Muda ule Hamza sasa alielewa nini kinachoendelea , aliona Farook ameona uwezo wa kushindana nae hana, na kukimbia huko ni kwa ajili ya kuita msaada zaidi , ilionekana kuna watu wengine ambao walikuwa ndani ya eneo hilo ambao hakuwa amewaona.Alihisi hivyo ila hakuwa na uhakika na alisubiria kumuona huyo mjomba.

Ukweli ni kwamba katika kila kambi ilikuwa na wazee , licha ya Farook kuwa kiongozi haikumaanisha alikuwa peke yake wa kuongoza kambi , kulikuwa na wazee wengine waliokuwa na mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi na hawakujihusisha moja kwa moja katika shughuli za kambi wao walikuwa tu kama waangalizi.

Licha ya Mzee Farook kuita sana lakini hakuna Mjomba aliejitokeza na kumfanya kuzidi kushikwa na wasiwasi na pia Hamza alikuwa nyuma yake akimkaribia.

Hamza mara baada ya kuona amemkaribia Mzee huyo palepale alijiandaa kufanya shambulizi la kumuua moja kwa moja lakini kabla hajafanya hivyo alihisi joto la ajabu kutoka nyuma yake , joto lililofanya mwili wake kusisimka kwa kuhisi hatari na hakutaka kuchelewa palepale aliruka kwa sarakasi kusogea upande wa kushoto kwa kutumia utashi wake wa akili.

Ile anasogea tu kitu kilichoonekana kama moto kilipita na kwenda kutua chini kusababisha kishindo kama vile lilikuwa ni bomu.

Moto ule ulikuwa na joto kali mno kiasi cha kuyeyusha mawe jambo lililomshangaza mno Hamza na kujikuta akihisi ubaridi wa hofu.

“Wewe ni nani!?”Aliongea Hamza kwa nguvu huku akijihisi moyo wake ulikuwa ukitetemeka.

Mara baada ya kugeuza macho yake kuangalia upande wa juu aliweza kuona kivuli cha mtu juu ya paa la jengo la kambi pembeni ya Sanamu la Nyoka ishara ya kambi hio.

Kila mfuasi wa kambi hio ukimjumlisha na Mzee Farook aliekuwa akikimbia walijikuta wakisimama na kuangalia kwa shauku kubwa uelekeo wa shambulizi lile lilikotokea.

Mara baada ya kuangalai kwa umakini palepale aligundua ni mwanamke mrembo sana alievalia mavazi mekundu ya mtindo wa kileo kama vile anaenda matembezini huku nywele zake zikipeperushwa na upepo.

“Ni wewe!”

Hamza aliweza kumfahamu msichana yule haikuwa mara yake ya kwanza kumuona , alikumbuka mara ya mwisho alimuona club.Hakika ni yule mwanamke mrembo aliekuwa akimwangalia sana lakini muda huo alitoa msisimko na kumfanya asionekane kuwa binadamu licha ya kuwa katika mwonekano wa kibinadamu.

Yule mrembo aliona namna Hamza anavyomshangaa na alimtingishia mabega kwa kumuonyesha ishara ya madoido kama vile anamwambia Hamza amemfananisha.

Muda ule Hamza alivyotaka kuongea kumuuliza kwanini amemshambulia aliweza kusikia sauti ya Mzee Farook kutoka nyuma yake.

“Ewe Nyakasura je ni Afande Simba aliekutuma kuja kuisaidia kambi yetu kudili na huyu kichaa?”Aliuliza kwa nguvu.

Hamza mara baada ya kusikia jina hilo palepale alielewa nini kinaendelea, alijiambia kumbe huyo ndio Nyakasura mwanamke ambae aliaminika kuwa mwanajeshi hatari ndani ya kitengo cha Malibu , ambae pia alitunukiwa cheo cha Askari wa taifa!. Ndio mara yake ya kwanza kumuona Nyakasura katika uhalisia wake, hakuonekana kuwa binadamu kama alivyowaza bali alitoa msisimko wa kiumbe ambacho hakuwahi kukutana nacho, pengine wafuasi hao walimwona kama binadamu lakini kwa Hamza ilikuwa tofauti.

Wafuasi wote wa kambi hio walijikuta wakiwa katika hali ya furaha baada ya kuona mwokozi wao amefika . licha ya kwamba karibia wote hawakuwa wakimfahamu kwa sura lakini wamezisikia sifa zake.

Nyakasura hakujibu swali la mzee Farook , alionekana kumdharau kuongea nae hivyo palepale alitoka juu ya paa na kushuka chini taratibu mithili ya malaika au jini na kwenda kukanyaga ardhi usawa na Hamza alipo.

“Ingawa huyo binadamu hana uwezo mkubwa na amekosa busara lakini bado ni kiongozi wa kambi ya Nyoka na ulinzi wake upo chini ya jeshi.Nimechelewa kidogo tu kufika lakini naona umefanya uharibifu mkubwa, nakushauri ni kheri uache mara moja..”Aliongea Nyakasura.

Hamza macho yake yaliishia kusinyaa , katika kukutana na mshindani wa daraja kubwa namna hio asiemjua asili yake hakutaka kufanya mambo kwa kukurupuka.

Alitaka kujua kwanza mpango wa Nyakasura kuja eneo hilo ni kumzuia tu au kushindana nae ndio achukue hatua.

“Nishawahi kusikia kuhusu jina la Nyakasura na kuambiwa ni msichana mdogo sana lakini sikutegemea ni kiumbe mrembo mno”Aliongea Hamza akiwa na tabasamu akijaribu kutuliza hali.

“Hilo la mimi kuwa kiumbe mrembo halina ubishi , lakini hata hivyo siwezi kukurhusu kuendelea kufanya uharibifu hapa kwa gia yako ya kunisifia”Aliongea na jibu lake lilimfanya Hamza kucheka kisha akamjibu:

“Lakini pia unapaswa kujua kama nikiamua kumuua Farook hamtoweza kunifanya chochote”.

“Pengine inawezekana lakini ni mpaka utakapojaribu kufanya hivyo, wewe unajuaje kama siwezi kufanya chochote?”Aliuliza Nyakasura.

Hamza alianza kuhisi kadiri alivyokuwa akiongea na huyo mwanamke kivuli chake kilikuwa kikibadilika na kusababisha msisimko wa ajabu. Ilikuwa ni dhahiri alikuwa akiashiria hajafika hapo kwa ajili ya amani.

“Imani yangu inaniambia mimi na wewe hatujawahi kuwa maadui?”Aliuliza Hamza.

“Imani yako inakuambia kweli” Alijibu Nyakasura.

“Kama ni hivyo kwanini ulikuja Dar na kunifuata mpaka kwenye ile club na kuanza kunikodolea macho? Halafu sasa hivi upo mbele yangu ukiwa na nia ya uadui na mimi, Kwanini?” Aliuliza Hamza . Ukweli hakujua ni kitu gani ambacho mkuu wa majeshi Afande Simba alikuwa akimjulisha kumtuma kiumbe kama huyo kuja kuingilia mipango yake.

“Nakuuliza kwasababu kwa uwezo wako sidhani kama Simba anao uthubutu wa kukuagiza..”

Licha ya kuongea, mrembo Nyakasura alishia kupepesa macho yake tu , ijapokuwa yalikuwa yakivutia sana lakini hayakuwa yakiashiria chochote, ki-ufupi alikuwa katika mwonekano wa hali ya kawaida wa ubinadamu.

“Ninachotaka kufanya sihitaji ruhusa kutoka kwa Simba, nimekuja kujionea je ni kama watu wanavyokusifia”Aliongea

“Kwahio Himidu amekuambia kuhusu mimi?”Aliuliza Hamza.

“Ndio, ameongea sana kuhusu wewe ila sijawahi kumuamini”

“Kwanini?”Aliuliza Hamza.

“Kwasababu katika ulimwengu huu na umri niliokuwa nao hakuna binadamu wa kunizidi ki uwezo”Aliongea Nyakasura kwa kujisifia.

Hamza aliona licha ya mwanamke huyo kuwa mrembo ila vilevile alionekana kuwa kama chizi.

Ni kweli alijua msichana huyo hakuwa na asili ya kibinadamu bali asili yake ni ya damu ya ndege phoenix sifa inayompa kila kigezo cha kujiongelea hivyo lakini bado aliona anajipimia kwa vipimo vya juu sana, kitendo cha kutowahi kukutana maana yake bado hakuwa amekutana na wataalamu wengi zaidi duniani.

“Mimi na wewe hakuna uadui kati yetu , lakini kwanini unaniangalia hivyo, naona ni kama kwa muda mrefu sana ulipanga kupigana na mimi”Aliongea Hamza na kumfanya Nyakasura kupindisha mdomo kama wanawake wa kiswahili.

“Nakuangalia vibaya kwasababu nimeboreka”

“Umeboreka!?”

“Ndio! Mpaka sasa sijapata mshindani sahihi wa kupigana nae , hisia za namna hii zinachosha mno. Kwasababu Himidu amekusifia kwa kusema una uwezo mkubwa sana nimejikuta nikipata hamu ya kukutana na wewe ili tupimane”

“Kwahio kunifuata kote kwanzia kule club mpaka huku ilikuwa ni kwa ajili ya kukidhi haja zako za kupigana na mimi , tena nadhani si sawa kusema kupigana , ulikuwa ukitafuta kucheza na mimi?”Aliongea Hamza.

“Vipi haiwezekani sisi kucheza pamoja kwani?”

“Labda baadae tunaweza kucheza , kuna michezo mingi tunaweza kucheza pamoja ninayopenda, kama vile magemu na nk”

“Hio michezo mingi siitaki , ninachotaka ni mchezo wa mapigano basi”Aliongea na kumfanya Hamza kukosa neno la kuongea.

Upande wa wale wafuasi wa kambi hio walijikuta wakiwa katika bumubwazi , ukweli ni kwamba walijua Nyakasura amekuja hapo kwa ajili ya kumuua Hamza lakini ilikuwa tofauti , mwanamke huyo kaja kutafuta wa kupigana nae sio kutoa msaada.

“Nyakasura sina pingamizi kwa wewe kutaka kupigana na mimi , lakini kwasasa nina kazi , ngoja nimalize kumuua kwamza mzee Farook ndio tuanze huo mchezo”Aliongea Hamza na palepale aligeukia upande wa Mzee Farook alipo.

Nyakasura mara baada ya kuona vile palepale mkono wake ni kama ulianza kuwaka moto na ghafla tu donge la moto lilionekana katika viganja vyake na akalirusha kumlenga Hamza.

Hamza mara baada ya kuona shambulizi lile la moto palepale alifyatuka kulia na kukwepa, moto ule uliopotua chini ulitokea mlipuko uliosababisha mawe kuruka juu na miti kuanza kuungua.

“Nimekuambia nataka kumuua huyo mzee kwanza ndio tupigane , lakini mbona unaingilia? Si umesema umakuja kwa ajili ya mapigano”Aliongea Hamza.

“Mzee Farook tutamfanya kuwa tuzo kwa ajili ya pambano letu , nikikupiga na kukushinda atabakia kuwa hai ila ukinishinda unaweza kumua”Aliongea Nyakasura.

Kauli ile iliwafanya wafuasi wa kambi hio kuwa katika mshangao ,hawakuamini Nyakasura angemgeuza master wao kuwa kombe.

Mzee Farook mara bada ya kusikia hivyo alijikuta akisimama tu,hakutubutu kukimbia maana alijua anaweza kumkasirisha Nyakasura na kuishia kutupiwa moto.

Hamza mara baada ya kusikia kauli hio alijikuta akighairi kwanza kuhusu Mzee Farook na usiriasi wake katika macho uliongezeka zaidi. Mwanzoni alikuwa na mpango wa kupigana na Nyakasura japo mara moja lakini hakudhania pambano lao litawahi namna hio.

“Nimekubali! Na mimi pia nina shauku ya kuona nguvu ya damu ya kiumbe Phoenix”

“Kama kweli unataka kuona nguvu ya damu ya kiphoenix itategemea kama unavyo vigezo vya kunifanya nitumie uwezo wangu wote”Aliongea Nyakasura.

Hamza palepale mwonekano wake uligeuka na kuwa wenye usiriasi baada ya kuona mwanamke huyo anamdhihaki kwa kumwambia hawezi kuonyesha uwezo wake wote . Lakini hata hivyo aliona ana haki maana moto aliokuwa akitengeneza ulikuwa mkali kiasi kwamba ulikuwa ukiyeyusha chuma.

Hamza na Nyakasura hatimae walikuwa sasa peke yao katika uwanja wa vita , kila mmoja akiangalia mbinu za mpinzani wake kitalaamu zaidi.

Mabadiliko ya miili yao hayakujificha kwa wale waliokuwa karibu lakini ukimya wao wa kutokushambuliana uliwafanya wafuasi wa kambi hio kushikwa na wasiwasi kubwa wasijue nini kinakwenda kutokea.

Mkandamizo wa hewa uliokuwa ukitokea katika mazingira hayo uliwafanya kujihisi ni kama vile vifua vyao vimebeba mzigo mzito ambao wanashindwa kuuhimili.

Hatimae hatua ya kwanza ya kusomana msisimko iliisha baina yao na wote kwa pamoja walijiandaa kwa kuanza kushambuliana.

Hamza alipiga hatua ya kwanza ya kuonekana na hatua ya pili spidi yake ilikuwa kubvwa mno kiasi kwamba hakuweza kuonekana vizuri huku akipanga kumshambulia Nyakasura na teke zito.

Nyakasura alisimama katika eneo moja wakati huo akiinua mkono wake wa kushoto uliokuwa ukitoa mwanga wa ajabu wa rangi ya dhahabu na kumfanya aonekane ni kama ameshikilia ngao ya mwanga.

Muda huo Hamza alihisi joto kali sana likisogelea mguu wake , lakini licha ya hivyo hakutaka kuacha kushambulia, tena aliongeza spidi maradufu na kwenda kuvaana na ile ngao ya moto ya Nyakasura.

Hamza aliamini ilimradi shambnulizi lake lina nguvu ya kutosha anaweza kusambaratisha kinga yake ile ya moto.

Nyakasura pia ni kama alikuwa ashajua kwamba ngao yake hio nyepesi isingetosha kumzuia Hamza kumpiga teke , hivyo alihepa kulia akinuia kukwepa shambulizi lile na wakati huo huo akitumia mkono wake wa kulia kumshambulia Hamza na donge la moto.

“Ungua…!!” Nyakasura aliongea kwa sauti ya chini na hapo hapo donge la moto lilimlipuka kutoka mkono wake wa kulia kama uwa la alizeti

Joto alilokuwa akizalisha mwanamke huyo ilifanya hata wale waliokuwa umbali mrefu wahisi ni kama wanaunguzwa na jua la utosi.

“Bam!

Hamza aliuvaa mkono wa Nyakasura na teke na kufanya kiatu chake na suruali kuungua.

Nyakasura baada ya kupigwa teke na kusukumbwa mbali na nguvu ile, alijihisi hali ya ganzi na nyusi zake zilitingishika ikionyesha dhahiri hakuwa akijisikia vizuri. Hamza mara baada ya kukanyaga chini baada ya kufanya shambulio hilo alijikuta akivuta pumzi nyingi sana huku akiangalia mguu wake ambao ulikuwa umeiva na kuwa mwekundu mno kama nyama ya punda kwa kuungua kwa ndani.

Ilikuwa bahati ana spidi kubwa la sivyo mguu wake ungegeuka rosti ya nyama.

“Umewezaje!” Nyakasura aliongea huku akiangalia mguu wa Hamza kutokea mbali na alishindwa kujizuia na kuonyesha hali ya mshangao.

“Unao uwezo wa kuhimili ‘phoenix flames?”Aliongea kwa mshangao.

“Kumbe ndio unaitwa Phonenix flames.. Hehe nilichokifanya ni kushambulia kwa spidi kabla sijaungua”Aliongea Hamza huku aking’ata meno akivumilia maumivu

Hamza aliona akiendelea kupigana kwa staili hio itakuwa ngumu sana kushinda hivyo anapaswa kuongeza spidi na kushambulia kwa kushitukiza.

Lakini tatizo moja ni kwamba Nyakasura alikuwa na uwezo wa kuhimili mateke yake ya tani ikimaanisha kwamba sio tu kwamba alikuwa na uwezo huo wa kimoto lakini vilevile mwili wake ulikuwa timamu.

Hivyo Hamza hakujua mapigo ya kushitukiza yanaweza kuwa na faida.

“Ukiachana na watu wa jamii yetu , wewe ni binadamu wa kwanza ambae umegusana na moto wangu bila ya kuungua . Hakika mwili wako sio wa kawaida kama binadamu wengine”Aliongea Nyakasura huku akionyesha mzuka sana wa kuendelea na pambano hilo.

Hamza mara baada ya kusikia maneno hayo alijihisi ubaridi na kujiambia kwanini mwanamke huyo ni kama anataka kumgeuza mdoli wa kuchezea.

“Ni zamu yangu kushambulia; Mijeledi miwili ya ngoma ya kifoeniksi!”

Sekunde ambayo Nyakasura alitamka hayo maneno alikuwa asharuka hewani huku mkononi akiwa ameshikilia mijeledi ya moto iliokuwa ikinesa nesa.

Kwa chini ilionekana ni kama Kamba ndefu zikidondoka kutoka juu angani.

Hamza alikuwa na kiatu mguu mmoja tu na mara baada ya kuona mijeledi ile ya moto inamsogelea alianza kuikwepa kwa spidi kubwa.

Lakini sasa ardhi ilikuwa ikiunguza mno kiasi kwamba baadhi ya mawe yalianza kuyeyuka na kufanya katika eneo hilo iwe ngumu kukanyaga.

Watu waliokuwa wakiangalia pambano hilo waliona ni kama vile pambano kati ya malaika na binadamu na kufanya wawe katika hali ya shauku mno kuona nani angeshinda pambano hilo.

Muda huo Nyakasura alikuwa akichezesha mijeledi ile ya moto huku akihama hama kwa kuruka na kumfanya aonekane kama kivuli chenye mikia.

Baada ya kuona Hamza anakwepa mashambulizi yake na hakuna namna ya kumfikia , alitua ardhini na kisha alichanua mikono yake kutoka chini kwenda juu huku akitoa sauti kubwa yenye mwangwi.

“Ngoma ya Wafoeniksi na Mvua ya moto!”

Mara baada ya kuongea hivyo palepale anga lilibadilika na kushusha mvua ya moto kama dhoruba ikimsogelea Hamza.

Hamza mara baada ya kuona vile aligundua hapo hana ujanja wa kukwepa shambulizi la aina hio na palepale alikimbia uelekeo wa majengo ya kambi hio na kuingia ndani ya jengo moja karibu yake. Nyakasura hakujali alimfukuzia huko huko huku akishusha mvua katika jengo aliloingia.

Hamza akiwa ndani alisikia harufu nzito sana ya bati kuungua na ndani ya sekunde chache tu alihisi uji uji ukimwangukia huku jengo lote likishika moto.

Mzee Farook mara baada ya kuona tukio hilo , alijikut akishikwa na furaha , palepale aliamini Hamza hachomoki , hakujali kuhusu jengo hilo kuungua ili mradi atakuwa hai maboresho ya kambi hio yataboreshwa. Isitoshe majengo hayo yalikuwa ya serikali.

Lakini upande wa Nyakasura bado aliamini Hamza yupo hai na palepale hakujali moto uliokuwa ukiunguza nyumba hio kwani alikimbia na kuingia ndani.

Moto ule haukuwa na madhara kabisa kwake , ni kama ulikuwa ukimuogopa na kumpisha apite.

“Hebu acha kujificha na toka nje!”Aliongea Nyakasura kwa nguvu na wafuasi wa kambi ile mara baada ya kusikia maneno hayo walishangaa na kujiuliza inamaana Hamza licha ya moto wote huo bado yupo hai.

Baada ya kuongea hivyo Hamza alifyatuka kwenye ziwa la moto ule kwa spidi kubwa akimlenga Nyakasura, miale hio ya moto ilionekana kutokuwa na athari yoyote katika mwili wake . licha ya kuonyesha ishara za kuungua lakini alionekana kutokuhisi maumivu.

Hamza hakutoka kizembe , alichomoka na shambulizi zito la ngumi ambalo alimpiga kiumbe huyo katika eneo la mbavu na kumrusha nje.

Nyakasura baada ya pigo lile la kushitukiza alipepesuka na kwenda kukanyaga kwa nguvu ardhini huku akimfyatulia Hamza moto kwa miguu yake lakini mwamba Hamza alikwepa kwa sarakasi, hata hivyo alishangazwa na wepesi wa Nyakasura kutoa moto kwa wepesi kupitia miguu.

“Unawezaje kutoa kwa urahisi namna hio?”Aliuliza.



SEHEMU YA 165

Hii mbinu tunaita nguzo ya moto, ndio msingi wa jamii yetu , ila naona sio haba kwako pia , unao uwezo wa kutembea juu ya moto”Aliongea.

Hamza huku akikunja sura , ijapokuwa aneo lote lilikuwa limezingirwa na moto lakini moto huo haukuwa wa kawaida lakini licha ya hivyo moto huo haukuwa tishio kwake.

“Nyakasura nadhani tuishie hapa . maana naona nashindwa kukusogelea kukushambulia, na mbinu zako pia haziniletei madhara , kama tukiendelea kwa staili hii ni ngumu kumpata mshindi”Aliongea Hamza.

“Sijatumia hata nusu ya uwezo wangu, nani kasema mshindi hawezi patikana?”

“Kwasababu hata mimi sijatumia nusu ya uwezo wangu”aliongea Hamza.

“Pumbavu!” Aliongea Nyakasura kwa kejeli.

“Kama huamini unaonaje ukitumia uwezo wako wote , kwanini unapoteza muda”

“Kwasababu naweza kukuua”

“Watu wengi washanitamkia hilo neno la kuniua lakini mpaka leo bado nipo hai”

“Kama ni hivyo basi nionyeshe sababu nijue kama kweli unastahili mimi kutumia uwezo wangu wote”

Mara baada ya kuongea hivyo , palepale Nyakasura alifyatuka kumsogelea Hamza kwa spidi huku akiwa amefunikwa na miale ya moto ,wakati huo huo akiwa ameshikilia mijeledi ya moto akipanga kumtandika nayo Hamza.

Hamza alikwepa mijeledi ile ya moto na haraka sana na kisha aliokota jiwe na akamrushia Nyakasura kumponda nalo.

Jiwe lile halikuwa dogo hata kidogo , lakini licha ya kumlenga nalo Nyakasura halikumfikia badala yake lilifunikwa na moto na kuanza kumeguka , ingawa halikumeguka lote kutokana na kuwa kubwa.

Mjeledi ule wa moto aliokuwa ameshikilia Nyakasura uligeuka na kuwa kama mkuki na kuligonga lile jiwe na kudondoka chini na kugeuka vipande vipande.

Hamza palepale alitumia nafasi hio kwa mara nyingine na kuchukua jabali lingine na kumrushia Nyakasura.

“Ngoma ya Wafoeniksi Pigo la radi!!

Nyakasura mara baada ya kuongea vile palepale mijeledi ile ya moto iliokuwa katika mikono yake iliungana kwa kusuguana na kuanza kutengeneza cheche za nishati ya ajabu kama ya umeme . kila kitu kilitokea ndani ya sekunde tu.

Mara baada ya kugeuza moto wake na kuwa kama radi alilenga lile jiwe na mara baada ya kugusana ulitokea mlipuko mkubwa wa bomu.

Boom!!

Jabari lile lilisambaratishwa na kuwa vipande vipande . Shambulizi la Hamza likawa limefeli na aliishia kuruka kujitenga mbali na mlipuko ule. Nyakasura pia jasho lilianza kumtoka na macho yake yalipepesa kwa haraka wakati akimwangalia Hamza.

Kawaida hakupaswa kutumia mbinu hio ya pigo la radi kwa mtu kama Hamza kutokana na nguvu yake ya uharibifu,ukweli ni kwamba hakuwahi kutumia pigo hilo kwa binadamu lakini kutokana na Hamza kuwa na mwili usioumia alijikuta akilazimika kufanya hivyo.

“Nyakasura naona kukusogelea imekuwa ngumu kabisa”Aliongea Hamza huku akitingisha kichwa.

Hatimae alikuwa ameielewa nguvu ya Wafoeniksi, Kiumbe huyo katika ubinadamu, ukiachana na kuwa na mwili ulioimara na kuwa na spidi kubwa ya kujibu mashambulizi, kubwa zaidi ni kwamba hakuonyesha udhaifu kabisa katika mbinu yake ya kucheza na moto.

Uwezo wake wa kucheza na moto , ulikuwa ni muunganiko wa mbinu ya kushambulia na kujilinda kwa wakati mmoja . Kuhusu mbinu yake ya Phoenix Dance, kulikuwa na mengi yenye kubadilika , ilikuwa ni mbinu hatari sana ambayo inamfanya kuwa na uwezo wa kushambulia kwa mbali.

Hamza yeye uwezo wake wa kushambulia ulikuwa ni wa kibinadamu zaidi , alitegemea nguvu zake za mwili katika kushambulia hivyo ili afanikishe alihitaji kumsogelea karibu Nyakasura jambo ambalo lilionekana kuwa gumu.

Kibaya zaidi ni kwamba, Nyakasura mbinu zote alizoonyesha zilikuwa ni za kawaida sana . Bado hajatumia uwezo wake halisi katika mashambulizi .

“Ni ngumu sana pia kukushambulia , ingawa umekosa mafunzo ya nishati za mbingu na ardhi lakini umebarikiwa miguu yenye nguvu kubwa sana kiasi kwamba spidi yako ya kukimbia nashindwa kuhimana nayo. Unakimbia kama Jini Pepo”Aliongea Nyakasura.

“Unamaanisha nini kusema nakimbia kama Jini pepo, kwani hakuna namna nzuri ya kufananisha kukimbia kwangu . Kusema nakimbia kama pepo kwanini nahisi kama unanitukana”Hamza alilalamika.

“Una spidi kama Jini pepo”Aliongea Nyakasura akimpotezea .

“Sasa kama unajua huniwezi kunikamata likija swala la spidi , kwanini bado unataka tuendelee kupigana ilihali hakutokuwa na matokeo. Kwanini tusiishie hapa?”Aliuliza Hamza akiwa na tabasamu.

“Ijapokuwa siwezi kukukamata kwa spidi yako , huwezi kuondoka hapa kama bado unapanga kumuua Mzee Farook. Hivyo huna namna zaidi ya kuendelea kupigana na mimi mpaka nishinde”.

“Tufanye makubaliano mengine , nipo tayari kukubali siku nyingine turudie kupigana na tutaweka tuzo nyingine”Aliongea Hamza.

“Hapana ! Sitaki”Aliongea huku uso wake ukigeuka na kuwa wa kikauzu zaidi.

“Bila kukuunguza mimi na wewe kupigana hakujaisha”Aliongea

“Kuniunguza , ukiniunguza si utaniua?”

“Hata ukifa sijali. Leo ni mpaka mshindi apatikane”

“Wewe kwaninii unang’ang’ania iwe leo , tunaweza kupanga siku nyingine, nyie wanawake mna nini kwani?”Aliongea Hamza maana alikuwa amechoka kweli kushindana na Nyakasura , haikueleweka alikuwa akimugogopa au vipi.

“Sisi wanawake ndio tulivyo, lazima leo ajulikane mshindi hata kama tutakesha hapa”Aliongea na palepale kwa mara nyingine alimsogelea Hamza kwa ajili ya kuanza mashambulizi.

Nyakasura alifyatuka kwa sakari mzunguko kama mara tatu hivi na kisha alitengeneza mpira wa moto, kama vile ni mchezaji alipiga teke mpira ule wa moto kumwendea Hamza.

Wakati huo huo akiongea maneno ambayo hayakueleweka na ghafla tu ule mpira wa moto ulibadilika na kuwa kimbunga cha moto ambacho kilizidi kukua kadri kilivyokuwa kikikusanya upepo.

Hamza mara baada ya kuona jambo hilo aliishia kung’ata meno huku akijiambia haamini kama maajabu hayo ya moto kutoka kwa huyo mwanamke yana mwisho wake.

Hamza mara baada ya kuona vile hakutaka kusubiri moto ule wa ajabu kumvaa na palepale alitimua nduki kuelekea ndani ya majengo ya kambi hio.

“Acha kukimbia wewe mshenzi muoga sana”Aliongea Nyakasura kwa hasira huku na yeye akianza kumfukuza.

Mwili wake wote ulikuwa umefunikwa na moto na kuwa kama jua na kumfanya kadri alivyokuwa akimfukuza Hamza ndio alivyozidi kutengerneza machafuko ya moto ndani ya kambi hio.

Kitendo cha kufukuzana katika mejengo ya kambi alipelekea kuharibu mazingira yake kwa kuyaunguza , kama sio majengo mengi kujengwa kwa mawe yangeshabomoka kabisa.

Mzee Farook na wenzake kuona namna kambi yao inavyoteketea kwa moto walijikuta wakitamani kutoa kilio . Uvumilivu uliwashinda na kujikuta wakipiga magoti na kuanza kumuomba Kiumbe Nyakasura aache anachokifanya kwani anazidi kuharibu eneo hilo.

“Ee Nyakasura tunaomba usitishe…!!” Waliongea lakini sasa Nyakasura hakuwasikiliza.

Baada ya kukimbizana kwa nusu saa hatimae kambi karibia yote ilikuwa ikiteteketea kwa moto na kufanya ionekane ni kama mlima wote ulikuwa ukiungua .

Mpaka kufikia hapo wafuasi wa kambi hio wasingeweza kuendelea kukaa hapo tena , hivyo walikimbilia chini ya mlima.

Nyakasura baada ya kuona anashindwa kumkamata Hamza zaidi ya kusababisha moto aliishia kusimama katika sehemu moja huku akihema kwa nguvu na kung’ata meno kwa hasira huku akimwangalia Hamza kwa chuki.

“Kiumbe Mrembo nadhani hii inatosha sasa , kwa uwezo wangu wa kukimbia hata kama wewe sio binadamu utaishia kuchoka tu. Unaonaje ukirudi nyumbani uoge utakate kisha ulale kidogo na usipoteze muda juu ya jambo hili dogo”Aliongea Hamza kwa kubembeleza.

Mara baada ya wafuasi wa kambi hio kusikia Hamza akiongea hivyo walimuunga mkono palepale.

“Ni kweli Ee Nyakasura , tupo tayari kumtoa Mzee Farook kuchukuliwa na Hamza . hatuwezi kuendelea kuona unauguza kambi yote”Sauti ilisikika.

“Mjomba!!”Aliita Mzee Farook akionekana mwanaume mtu mzima mwenye mvi kichwani akiwa amesimama. Mzee huyo alikuwepo hapo muda mrefu ila kutokana na watu kuwa bize kuangalia pambano hawakuwa wamemuona. Ndio mzee ambae Master Farook alimwita kwa ajili ya kuomba msaada.

Mjomba huyo alishukuru hajapigana na Hamza maana kwa show aliokuwa akiangalia licha ya kuwa na uwezo kumzidi Farook lakini bado aliona Hamza sio saizi yake.

Sasa muda huo huyo mzee baada ya kuona namna kambi hio ilivyokuwa ikiteketea kwa moto aliona msababishaji mkubwa ni Farook kwa kuwa na maamuzi ya kukurupuka, ndio maana alisema kama Nyakasura angekubali kuacha Hamza angepatiwa Farook amuue tu.

Hamza mara baada ya kusikia kauli hio licha ya kutokumjua huyo mzee , alijikuta akisikia furaha, hakuona haja ya kuendeleza mapigano hayo kama kambi hio ipo tayari kumpatia Mzee Farook na mwanae Fabiani.

“Nani kawaambia nimechoka?”Aliuliza Nyakasura huku sauti yake ikitoa mlio flani wa kuumiza masikio kama vile ni maiki mbovu.

“Subirini muone”Aliongea na palepale alifyatuka na kwenda kutumbukia kwenye lindi la moto katika nyumba zile za kambi.

Mara baada ya kuingia katika ule moto cha kushangaza nguo zake nyekundu hazikuungua kabisa , kinyume chake ile miale ya moto iligeuka na kuwa kama vile ni roho na kuanza kumwingia Nyakasura kupitia macho, pua na mdomo. Kadri alivyokuwa akihema moto ule ulizidi kuingia na kumfanya aonekane kiumbe wa ajabu mno, alidhihirisha kabisa hakuwa binadamu.

Baada ya kutoka katika moto ule , ile hali ya uchomvu aliokuwa nayo ilimpotea kabisa na kuonekana kama kazaliwa upya . Tukio lile liliwashitua wafuasi wote akiwemo Hamza.

“Huo nii… ni kama inavyohadithiwa..!”Aliongea Hamza kwa mshangao.

“Usishangae,hii ndio asili ya damu yetu , tumeumbwa kwa moto na majivu na tunazaliwa upya kupitia moto na majivu, ‘Fire and Ashes Rebirth’” Aliongea Nyakasura.

“Sikutegemea ni kweli .. hakika ina tisha”Aliongea Hamza huku akikumbuka stori kadhaa kuhusu kiumbe Foeniksi(Phoenix), inasemekana kwamba kiumbe huyo hata kama awe amekufa akiweka karibu na moto au majivu anapona mara moja na kuwa mpya ili mradi nafsi yake iwe haijapotea.Ukweli ni kwamba hakuna anaejua kama njia hio ni kufufuka ama ndio kuzaliwa upya lakini katika simulizi zao kiumbe Phoenix hakuwahi kufa.

Ili mradi kuwe na moto au majivu ya kutosha anao uwezo wa kurudisha uwezo wake wote au uhai,chakula cha viumbe hao si hiki cha kibinadamu bali ni moto na majivu.

Nyakasura sasa baada ya kutoka katika huo moto alikuwa mpya kabisa na msisimko katika mwili wake uliongezeka maradufu huku akizidi kuonekana kujiamini.

“Enhe umesema bado unajihisi kuwa na nguvu za kutosha ? Ni muda wa kuona nani ataanza kuchoka”Aliongea Nyakasura na kumfanya Hamza kutoa tabasamu lililojaa uchungu.

“Kushindana kwa namna hio sio haki , kwahio kila ukichoka utaingia kwenye moto na kurudiwa na nguvu zako? Kufanya hivyo haitoletea maana tena”Aliongea Hamza akilalama kama vile anaonewa.

“Usiwe na wasiwasi , nitakuambia namna ya kunishinda , kwanza hakikisha unanizuia nisiingie katika moto na sitoweza kupona , pili niue kwa pigo moja tu na hakikisha nafsi yangu haigusani na moto wala majivu na kupelekea kuzaliwa upya. Nadhani utaweza kufanya hivyo?”Aliongea

Hamza alijikuta akishika kiuno. Ukweli ni kwamba hakuwa kabisa na uhakika wa kumshinda Nyakasura, vipi kuhusu kuua mwili wake na nafsi kwa wakati mmoja na kumzuia asigusane na jivu wala moto, inawezekana vipi?.

Kuhusu pia kumzuia asigusane na moto ni swala ambalo haliwezekani maana muda huo ni kama amejitengenezea bahari ya moto kwani kila mahali kuzunguka, moto ulikuwa ukiwaka na kama wataendelea kupigana katika mazingira hayo wanaweza kupigana mwezi mzima.

Ijapokuwa Hamza mwili wake ulikuwa umepita asili ya ubinadamu lakini asingeweza kupigana na kiumbe huyo kwa zaidi ya mwezi , hivyo ni hakika angekufa wa kwanza.

“Hakuna namna nyingine tukazungumza?’Aliuliza Hamza kinyonge huku akijishika paji la uso.

Kwasababu alisafiri mpaka kuja ndani ya hio kambi hakutaka kuondoka bila kumshughulikia Mzee Farook na mtoto wake. Aliogopa kama angewaacha hai kuna uwezekano wakalipiza kisasi kupitia watu wake wa karibu.

“Hakuna namna , umenikasirisha sana hivyo ninachotaka ni kukuunguza tu basi”Aliongea.

“Nikiamua kukimbia huwezi kunikamata , kwanini unahisi naweza kuendelea kupigana na wewe?”

“Nitahakikisha hupati hio nafasi ya kukimbia”Aliongea na palepale mwonekano wake ule wa kibinadamu ulimpotea na sasa kudhihirisha ukuu wake na macho yake yalibadilika kutoka kuwa ya kawaida na kuwa ni yenye kuwaka moto.

Muda uleule alionekana kuwa na kitu kama kisu kidogo mkononi cha madini ya jedi na alishika kidole gumba na kisha alikata eneo la juu la kidole na kufanya tone la damu ambayo sio nyekundu lilitoka , ilikuwa ni damu ya rangi ya njano.

“Damu ya Kifoeniksi!” Hamza alipaniki huku akihisi utosi wa kichwa chake kuwasha, “Usiniambie unapanga kutumia uwezo wako wote kushindana na mimi?”Aliuliza Hamza na Nyakasura hakujibu badala yake alidondoshea tone la damu ile katika kiganja cha mkono wake na alianza kuongea lugha isioeleweka na maneno ya mwisho pekee ndio yaliwezekana kutafisirika.

“Hati takatifu ya mbingu tisa, Damu inayoungua!” Aliongea hivyo akionekana kama vile anasali lakini haikuwa hivyo.

Ngoma takatifu ya Wafoeniksi ya mbingu tisa ndio daraja la juu sana la mapigano ambalo Nyakasura alipata kujifunza chini ya umiliki wa damu yake hio ya kifoeniksi. Ukilinganisha mbinu hio na Hati ya mbingu tisa, maajabu yanazidi kiasi kwamba ni ngumu kuukadiria uwezo wake wote kupitia hati hio ya mbingu tisa kwani kila ujazo wa mbingu moja una uwezo wake tofauti.

Sasa mara baada ya Nyakasura kuongea maneno yale mwonekano wake ulibadilika na kuwa wa tofauti kabisa kuliko mwanzo . Joto la miale ya moto wake liliongezeka mara tatu zaidi na mara baada ya lile tone la damu kuungua lilibadilika na kuwa moto uliosambaa mwili mzima kama vile alikuwa akijiogesha.

Nywele zake na weusi wake wa kibindamu ulipotea na alionekana mweupe wa kumeta meta , ikiwa ngumu kuelezea ndio uhalisia wake au ni kwasababu ya ule moto. Hata sauti yake ilibadilika kabisa na kila neno lake lilitingisha moyo.

“Unapaswa kujivunia kwa hadhi yangu kuamua kupigana na wewe kwa uwezo wangu wote”Aliongea huku sauti yake ikijirudia tudia masikioni.

Palepale moto ulifuka katika mkono wake na kisha aliurushia kuelekea katika nyumba ambazo hazikuwa zimeungua bado. Baada ya wale wafuasi wa kambi hio kuona jambo hilo palepale walishikwa na kiwewe.

Hawakuamini Nyakasura anaweza kuwa na huruma juu yao tena , kwani alibadilika kabisa. Haikuwa hofu tu hata kupumua kwao ilikuwa shida . Hata yule Mjomba ambae alikuwa na uwezo kumzidi Farook alianza kukohoa kwa kushindwa kupumua.

Mtu pekee ambae hakuteswa na mazingira yale ni Hamza pekee ambae alikuwa akimwangalia Nyakasura sio kwa hofu bali kwa shauku kubwa , alishindwa kujizuia kuukubali uwezo wa kiumbe huyo mwenye mwonekano wa ubinadamu na kujiuliza imekuwaje akawa katika mazingira ya Tanzania tena sehemu ya jeshi.

“Enyi Wafuasi wa ufunuo wa Nyoka nisikilizeni , kimbieni kutoka katika hili eneo! Haya mapigano sio ya levo za ubinadamu na tunaweza kufia hapa hapa”Aliongea Mjomba kwa sauti na kauli yake ilitikiwa na wafuasi wote walioanza kutimua nduki kushuka mlima huo.

Mzee Farook mara baada ya kuona hivyo , aliishia kumwangalia Hamza kwa macho makali. Alifikiria nafsini mwake kwamba Hamza anapaswa kuunguzwa na moto wa kiumbe huyo na ndio itakuwa halali yake na mara baada ya kuwaza vile aligeuka kwa ajili ya kukimbia na yeye.

Lakini angejuaje kama Hamza bado hakuwa amemsahau . Baada ya kumuona anataka kukimbia aligeuka haraka.

“Mzee Farook unakimbia kwenda wapi?” Aliuliza.

Nyakasura ni kiumbe wa aina gani kama sio binadamu vipi kuhusu Prisila?

Hamza hana nishati za mbingu na ardhi kama ilivyokuwa Roma , anategemea ubinadamu kushindana. Unadhani atapona?Naziona nyama kwa mbali.

ITAENDELEA Alhamisi
U*na maoni yoyote , unahitaji kuendelea , nitafute watsapp 0687151346.
 
Back
Top Bottom