FEBIANI BABUYA
JF-Expert Member
- Mar 5, 2022
- 1,916
- 3,850
- Thread starter
- #221
Pamoja mkuuAsante sana mwandishi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pamoja mkuuAsante sana mwandishi
🪑HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
Episode 65
“Nitawalinda kwa gharama yoyote ile” aliongea akiwa anamuacha mkewe apumzike baada ya kupitiwa na usingizi na ndipo akarudi kwa James.
“Kwa muda gani ulijua kwamba watarudi?”
“Siku mbili”
“Kwanini haukuniambia?”
“Alinisisitiza sana kwamba kama ningekwambia basi asingenisamehe kamwe kwenye maisha yangu maana ningekuwa nahatarisha hali ya mtoto”
“James unajua mpaka hivi ninavyozungumza kuna watu huenda wana picha za mwanangu na mke wangu?”
“Unahisi wanaweza wakawa wamehisi kwamba kuna mtu mgeni amefika ndani ya nchi?”
“Denis Kijazo kila taarifa za nchi hii anaweza kuzipata kwa dakika kumi tu pekee unahisi mke wangu wakati anaingia pale uwanja wa ndege hakuna kitu ambacho watakipata kutoka kwake?”
“Niliangalia sana usalama wa kamera pale sidhani kama inawezekana kuna tatizo lolote”
“Mimi nilifanya kazi ndani ya shirika letu la kijasusi, najua una uwezo mkubwa sana kwenye mitandao ila ninacho kizungumzia hapa ni kitu tofauti kabisa. Sehemu kama zile huwa zina kamera za siri sana ambazo ili kuzifungia ni mpaka ujue kwamba zipo na najua haukuwa ukijua kuhusu jambo hilo je una imani bado kwamba kutakuwa na uhakika wa usalama wao na wako pia?”
“Nisamehe sana kiongozi”
“Huu sio muda wa kuombana msamaha ila ni muda wa kujua kwamba ni kitu gani tunatakiwa kukifanya baada ya hapa. Nina imani kwamba picha zao, mke wangu na mwanangu mpaka sasa kuna watu wanazo kitu ambacho litakuwa suala la muda tu kufanikiwa kutufikia hivyo tunatakiwa kuifanya kazi hii kabla ya wao hawajafanya lolote lakini kuna ombi moja ambalo ninalo kwako”
“Nahitaji kuimaliza kazi hii na nashukuru sana kwa mchango wako mkubwa mpaka sasa tupo wote ila kwa sasa naomba uilinde familia yangu.”
“Hii tayari ishakuwa familia yangu hivyo hakuna mtu hata mmoja ambaye atafanikiwa kuigusa kama mimi bado nipo hai na kama mtu huyo atataka kufanya hivyo basi anatakiwa kuhakikisha kwamba mimi nakufa kwanza” wanaume hao walikumbatiana kisha kila mtu akaingia kwenye majukumu yake ya kawaida japo Max alikuwa ni mtu mwenye wasiwasi sana.
Kurudi kwa Max ilikuwa ni habari mbaya sana kwa Denis Kijazo lakini habari mbaya zaidi ni kwamba kijana wake alipoteza mzigo wa mhimu sana ambao kwa maelezo yake alidai kwamba ungeweza ukampoteza kabisa duniani. Nyaraka ambazo ziliibiwa zilikuwa ni mhimu sana kwake na ndiyo maana alimpa Dax masaa ishirini na manne tu awe amefanikiwa kuzipata vinginevyo angedili naye mwenyewe. Alikuwa yupo kwenye gari yake anaelekea Ikulu ambako alionekana kuwa na mazungumzo ya mhimu sana na mheshimiwa raisi wa taifa la Tanzania.
Akiwa kwenye gari aliichukua simu yake na kujiweka sawa kisha akaipiga kwa kijana wake ambaye alikuwa anamwamini sana. Simu hiyo ilikuwa inaelekea Ngarenaro ya chini Jengo la saba sehemu ambako ilikuwepo ngome yake ya siri ambayo ilikuwa inamuingizia mabilioni ya fedha. Simu ilimkuta Ted akiwa amekaa na vijana wake wakiwa wanafunga mahesabu ya pesa, aliipokea haraka sana na kusogea pembeni ili kuweza kumsikiliza bosi wake.
“Mzigo ambao Max alienda kuuchukua kwa yule mzee umepotea na upo kwenye mikono ya Max”
“Hilo haliwezekani bosi, huyo mtu alikufa miaka kumi na mbili iliyopita”
“Hata mimi nilijua hivyo ila kwa sasa kinachotakiwa ni mzigo kupatikana kisha ndo tuanze kujua kwamba huyu mtu aliponaje wakati alizikwa. Nadhani unajua ni kipi ambacho unatakiwa kukifanya lakini kabla haujafanya jambo lolote pitia kamera zote za uwanja mkubwa wa ndege ambao unapokea watu kutoka pande zote za dunia kisha kama kutakuwa na kitu utakipata utanipa taarifa”
“Sawa mkuu” Ted alikata simu na kuhema kwa nguvu sana, hiyo kazi haikuonekana kwamba itakuwa nyepesi sana japo haikuwa inampa mashaka maana alizoea sana kufanya kazi za namna hiyo. Alirudi kwa vijana wake na kumuita Kenedy pembeni ambaye naye alikuwa akimwamini sana.
“Mimi leo natakiwa kwenda Dar es salaam kuna tatizo kubwa sana limetokea. Nyaraka za mhimu sana za bosi ambazo zinaweza kumpoteza zimepotea hivyo natakiwa kwenda kuhakikisha zinapatikana na hii sehemu naiacha kwenye mikono yako ila na wewe unatakiwa kuja Dar es salaama haraka sana hesabu zikikamilika”
“Unajua ni nani amezichukua?”
“Yeap, ni Max”
“Unamaanisha yule mlinzi wa zamani wa raisi Teodensia Mpanzi ambaye alizikwa”
“Kuhusu kuzikwa unasema wewe ila yupo hai na tunatakiwa kujua kwamba ni wapi yupo, anataka kufanya nini na alikuwa wapi mpaka ajitokeze baada ya miaka hii kumi na miwili?” Maelezo ya Ted yalimchanganya sana Kenedy, ni kama alikuwa anasimuliwa simulizi za zamani ambazo zisingekuwa kweli ila kwa bahati mbaya sana alitakiwa kukubaliana na huo ukweli ambao alikuwa anapewa wakati huo.
“Kwahiyo ni kipi kinafuata kwa sasa?”
“Tunatakiwa kuangalia marejeo ya video za pale uwanja wa ndege kwa miezi kadhaa nyuma ila nataka za kuanzia leo kisha zingine zifuate” ilikuwa ni amri ambayo mara moja ilianza kutekelezwa hapo. Walisogea kwenye chumba cha kazi ambacho kilikuwa na komputa nyingi sana na kuna vijana ambao walikuwa hapo wakiwa makini sana kucheza na komputa hizo.
Walikuwa makini sana kwenye kukagua kila hatua na kila mtu ambaye alikuwa anapita eneo hilo taarifa zake zote zilikuwa zinajitokeza kwenye komputa hizo kitu ambacho kiliwarahisishia sana kazi wanaume hao. Walizipitia kwa muda mrefu sana na mara ghafla walimuona mwanamke mmoja mrembo sana akiwa na mtoto.
Ted ambaye alikuwa ameanza kusinzia kutokana na kukaa muda mrefu alishtuka sana baada ya kumuona mwanamke huyo akahitaji watu hao wasimamishe hapo kwanza.
“Stop” aliongea akimpa ishara mwanaume mmoja kuweza kuirudia video hiyo na kuikuza picha ya mwanamke huyo pamoja na mwanae. Jina lake lilikuwa linasoma mrs Howartson kutokea ndani ya nchi ya Marekani, kwake jina halikuwa na shida sana ila kitu ambacho kilimshtua ni mtoto ambaye alikuwa na mwanamke huyo, mtoto alikuwa anafanana sana na mtu ambaye aliamini kwamba alikuwa anamfahamu sana.
Mwanaume alisogea mwenyewe kwenye komputa nyingine ambayo ilikuwa pembeni yake na kuandika jina la Max. zilikuja taarifa za mtu huyo kwa sababu alikuwa maarufu sana na alidaiwa kuwa ndiye gaidi hatari zaidi wa taifa la Tanzania kwa kumuua raisi miaka kadhaa ambayo ilipita. Aliikuza picha ya mwanaume huyo akaikuza na ya mtoto kisha akawa anaangalia kwa zamu zamu kama kufananisha kitu. Baba na mtoto walikuwa wanafanana vitu vingi sana kama ungewaangalia kwa umakini mkubwa na ndiyo sababu ambayo ilimshtua sana baada ya kumuona mtoto huyo akiwa na mama yake.
“Yes, nimekupata Max”
“Mkuu unamaanisha nini?”
“Hii ni familia yake, huyo mwanamke mrembo ni mkewe na huyo binti mrembo ni mwanae wa damu. Mchezo huu unaenda kuwa mrahisi sana na mimi siku zote ndiye huwa nazichanga karata kwenye huu mchezo”
“Unataka kufanya nini?”
“Binadamu yeyote yule duniani hata kama atakuwa mgumu au katili kiasi gani, udhaifu wake mkubwa huwa ni familia. Mbele ya familia hata watu wa kutisha huwa wanapiga magoti wakiomba watu wao wanao wapenda waachiwe. Kama tukiipata familia yake basi niamini mimi atakuja yeye mwenyewe popote ambapo nitahitaji aje na kwa sasa nataka nishuhudie anavyokuja kufufuka tena kwenye mikono yangu” Ted aliongea kwa furaha sana akiwa anaangalia mpaka mwanamke huyo anavyotoka ambapo alienda kupokelewa na mwanaume mmoja ambaye alikuwa anamsubiria kwenye gari moja ya kifahari sana.
Alimpokea mwanamke huyo kwa heshima na kumpandisha kwenye gari hiyo na mtoto kisha akaondoka eneo hilo akionekana kuwa makini sana huku mbele yake kukiwa na gari moja na nyuma yake kukiwa na gari nyingine na hao wote walikuwa ni walinzi ambao walitakiwa kumlinda mwanamke huyo na mtoto.
Ted alibaki anamtazama huyo mwanaume kwa umakini mkubwa sana ambaye alikuwa anamlinda mke wa max akifahamaika kwa jina la mrs Howartson. Aliikuza na picha ya mwanaume huyo akiwa kama anaifananisha pia na alikuwa ana uhakika kwamba aliwahi kuiona mahali japo ni zamani sana. Kumbukumbu zake zilimrejesha ule usiku ambao walikuwa kwenye nyumba ya Madilu Mpagazi walipokutana na DRAGON BOYS, huyo ndiye pekee ambaye alifanikiwa kuishi na alimdharau sana kwa kipindi kile lakini ndiye alikuwa chanzo cha mambo yaote hayo kutokea.
“Ooooh shiiit! Nilifanya kosa kubwa sana kumuacha hai huyu mjinga na nahisi kwamba yeye ndiye ambaye alimsaidia Max kutoka kwenye kifo hivyo natakiwa kurudi Dar es salaam haraka sana na kama kuna kitu mtagundua basi mtatakiwa kunitaarifu haraka sana hawa watu natakiwa kuwaweka kwenye mkono wangu kwa muda mchache sana ujao”
“Sawa mkuu” wate waliitikia wakati huo mwanaume huyo alikuwa anatoka ndani humo na vijana kadhaa ili kuweza kusafiri mpaka ndani ya jiji la Dar kwenda kuikamilisha kazi ambayo alikuwa ameianza na bosi wake alihitaji yeye aimalize mapema sana.
IKULU
Bado ilikuwa ipo chini ya Justin Mtadei, mwanaume ambaye aliingizwa hapo baada ya kifo cha Teo akiwa kama ameikaimu nafasi yake na miaka ile ya kwanza haikuhesabika kama yake ndiyo maana mpaka wakati huo alikuwa kwenye hicho kiti akiwa anaimalizia miaka yake ya kula mema ya nchi. Siku hiyo alitembelewa na bosi wake ambaye ndiye alimuweka kwenye hicho kiti ili kuweza kulinda maslahi yao kwa ujumla na kuhakikisha kwamba mambo yao yanaenda vyema na kuhusu watanzania hawakuona kama ni biashara ambayo ilikuwa inawahusu.
“Karibu sana kiongozi, imekuwa ni muda mrefu sana tangu uweze kunitembelea hapa”
“Huwa sioni sababu ya msingi kuzunguka kwenye hili eneo kama mambo yangu yanaenda vizuri hivyo ukiniona nakuja hapa basi ujue kwamba kuna sehemu mambo hayapo sawa”
“Nini shida kiongozi?”
“Max bado anaishi”
“Nambie unanitania bosi” raisi aliongea kwa wasiwasi hata lile tabasamu lake lilipotea kabisa kwenye uso wake.
65 inafika mwisho.
Karibu
Nasubiri mtiririkoKaribu
hivi whatsup ndo na helaa?Karibu
Mkuu tupatie mwendelezoPamoja mkuu
Altogether bro..!! [emoji1534]Poleni sana kwa ukimya wa kupotea hizi siku mbili. Baadae tunaendelea
See you all.
👍Poleni sana kwa ukimya wa kupotea hizi siku mbili. Baadae tunaendelea
See you all.
Thanks ur Bro...!![emoji1545]HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
Episode 70
Hakujali hata uwepo wa walinzi wake hilo eneo aliendelea kumimina risasi kwa hasira sana na alipokuja kushtuka alikuwa ameua walinzi wake wawili tayari huku mlinzi wake mmoja akiwa anazunguka zunguka na bastola mkononi asijue ashambulie wapi au amshambulie nani. Umeme ulirudi ghafla sana, Max alikuwa amesimama nyuma ya yule mlinzi ambaye alikuwa amebakia, alimgusa begani mwanaume huyo akageuka kwa pupa sana alikutanishwa na kisu cha shingo ambapo shingo hiyo ilichanwa chanwa vibaya sana. Alishuka chini akiwa amekufa muda mrefu tu sasa wakawa wamebaki wawili tu wakiwa wanaangaliana.
Dax alijaribu kupiga risasi lakini aligundua kwamba zilikuwa zimeisha na alikuwa amebakiwa na kisu tu pekee. Kazi ya kuweza kukata umeme ilikuwa inafanywa na James ambaye alikuwa kwenye gari ambayo haikuwa mbali sana na eneo hilo akiwa anaangalia kila kinacho endelea kwenye kamera na alikuwa hapo kutoa msaada pale ambapo angehitajika. Dax hakuwa na namna nyingine zaidi ya kuyapambania maisha yake mwenyewe maana msaada wake walikuwa ni walinzi ambao walikuwa hawapo tena hivyo alikuwa ni yeye wa kuyatetea maisha yake kwa mara ya pili tena akiwa anakutana na mtu huyo ambaye alipotea miaka kumi na miwili.
Alijigusa kwenye kiuno akiwa anahesabu hatua zake kwa kasi ya ajabu, alichomoa bisu kubwa sana ambalo alikuwa amelilenga kwenye shingo ya Max. alimfikia lakini kisu hicho kilipita pembeni kidogo baada ya Max kukikwepa hata hivyo Dax alijigeuza kwa mateke matano mfululizo ambapo matatu yalizama kwenye kifua cha Max na baada ya kumpata alisogea nyuma kidogo ambapo alikuwa anajibamiza ukutani lakini alichomEka shoka ukutani likampa balansi ya kuweza kusimama vyema kisha akajiweka sawa wakati huo Dax alikuwa amekirusha kisu hicho kwa nguvu sana kuja kwa mwanaume huyo akiwa bado yupo ukutani.
Kisu kilienda kuchimba kwenye ukuta baada ya Max kuinama lakini hata wakati yeye mwenyewe anainama aliliachia shoka lake ambalo Dax alishtuka linaikaribia shingo yake hivyo aliruka sarakasi kwenda pembeni, alihEma kwa nguvu sana kwani lilikuwa linaondoka na shingo yake moja kwa moja. Wakati anasimama hapo alipokuwa amedondokea alishangaa buti linakuja kwenye uso wake hivyo alijivuta nyuma na kujigeuza kwa sarakasi kwa mkono mmoja na kusimama.
Buti lile ambalo lilimkosa, lilichimba chimba chini vibaya sana kiasi kwamba zege ilipasuka kiasi fulani, alimeza sana mate kwani kama lingetua kwenye mwili wake basi hali ingekuwa mbaya sana. Wanaume walikutana kwa mikono yao sasa ambapo ngumi zilikuwa zinarushwa kwa nguvu na kwa spidi ya ajabu sana ambapo kasi yao haikuwa ya kawaida. Dax alikuwa anajilinda zaidi maana mwenzake alikuwa anarusha ngumi kwa kasi na nguvu ya ajabu sana, ngumi zake mbili aliziachia kwa pamoja kama anapiga pushup, Max aliziacha ngumi hizo zipenye kwake lakini yeye mwenyewe wakati huo huo aliziachia zake na wote ngumi zilitua kwenye vifua vyao.
Max ngumi zake ziliwahi kufika kwenye kifua cha Dax hali ambayo ilifanya zake zifike zikiwa zina kasi ndogo sana maana alipunguzwa kasi kwa kiasi kikubwa sana na ngumi mithili ya chuma ambazo zilikuwa zimekita kwenye kifua chake. Dax alirudi nyuma akiwa anakohoa damu, kifua kilikuwa kinawaka moto sana lakini alikuwa kwenye vita hakukuwa na mtu wa kumbembeleza alijikaza na kuikaza mifupa yake lakini kwa maumivu makali mno maana mwili ulikuwa unawaka moto sana.
Alimkimbilia Max na kuhitaji kumzoa lakini mwanaume huyo aliinama kwa kasi sana na kuachia kisigino chake ambacho kilienda kukita kwenye paji la uso la Dax hali iliyo mfanya kuyumba yumba sana na kurudi nyuma. Wakati anayumba yumba Max alimjia kwa kasi na kumgonga na viganja kwa nguvu sana kwenye masikio yake na kumfanya kusikia sauti za milio mikali sana kama mtu anapiga mluzi kisha alivutwa kwa kasi na kupigwa na ngumi sita za haraka tumboni na kifuani.
Zilimpeleka mbali sana lakini haikuwa sababu ya yeye kuachwa Max alijibetua na kutua kwenye mguu wa Dax ambao ulivunjwa hapo hapo akawa anashuka chini akiwa anaguna kwa maumivu ila kushuka kwake alikutanishwa na buti la uso ambalo lilimbamiza vibaya sana ukutani na kumfanya akae kinyonge akiwa ameegamia ukuta anatokwa damu sehemu nyingi sana za mwili wake. Max alisogea lilipokuwa shoka lake akaliokota na kuichomoa bastola yake kisha akaenda kukaa mbele ya Dax wakawa wanaangaliana.
"Kuna watu wataanza kuniogopa sana kama wakijua historia nzima ya maisha yangu, kuna muda unafika hata mimi najiogopa sana ndugu yangu. Sio rahisi mtu unazikwa halafu baada ya miaka kadhaa unarudi ukiwa hai tena, inahitaji moyo wa kipekee sana mtu kuamini na kukubali tena kuwa karibu na mtu kama mimi. Kwenye maisha yangu sikuwahi kukata tamaa kabla lakini siku ile ukiwa unanifukia kwenye lile shimo la futi sita nilijikuta naanza kuogopa sana, niliiona hofu halisi ya mwanadamu na mimi nikajua kabisa kwamba sikuwahi kuwa roboti bali ni mwanadamu wa kawaida tu ambaye naye anakufa pia"
"Kabla ya siku ile kuna namna sikuwahi kuwaza kuhusu kifo hali ambayo ilinifanya nikawa nampotezea sana Mungu ila siku ile niliamini kwamba wanadamu huwa tunakuwa na jeuri pale ambapo tuna kila kitu kwenye maisha na furaha ipo upande wetu ila hayo mambo yanapokuwa nje ya uwezo wako na hauna ulicho bakia nacho kwenye maisha yako basi niamini mimi utaamini kwamba Mungu yupo na huenda utalia sana na kujuta ukiwa unaomba Mungu akusamehe sana huku ukiwa hujui kwamba ukifa utaenda wapi kwake au kwa wale ambao inadaiwa wapo motoni. Hii ni hofu ambayo naiona kwako saivi pia ukiwa unahema kwa kukosa matumaini hapo, basi hiyo hofu mimi siku ile niliipata kutoka kwa mtu ambaye mara ya kwanza niliwahi kuamini kwamba ni mtu wangu wa karibu sana ila nilikuwa najidanganya sana mwanzo."
"Ujue Karistus, kwenye maisha yangu mimi sikuwahi kuwa na furaha kabisa, mimi sikuwahi kuwa mmoja wa wale watu ambao waliishi kwa tabasamu hata siku moja ila nikushukuru wewe kwa kuwa sababu ya mimi kupata tabasamu upya tena kwenye maisha yangu. Kunifanyia lile jambo siku ile kulinifanya nikawa karibu na mwanamke ambaye amekuwa kila kitu kwangu kwa sasa, mwanamke ambaye amenipatia familia bora sana na kwa upande wangu naweza kusema kwamba hilo ndilo jambo ambalo linanipa furaha sana kila ninapo waona wale wawili wakiwa wanacheka" mwanaume alisikitika sana akiwa anampa mwenzake huyo hisia zake ambazo alikuwa nazo kwenye moyo wake.
"Uliponaje siku ile Donald?"
"Hilo ni swali ambalo hata mimi baada ya kuamka nilikuwa nahitaji sana majibu yake, swali ambalo lilikuwa ni gumu sana kulijibu kwa sababu kwa mara ya mwisho nilijiona kabisa kwamba mimi nakufa lakini nimekuja kushtuka nipo kitandani tena watu wakifurahia mimi kuamka tena. Nadhani kuna mkosa makubwa sana ambayo yalifanyika siku ile wakati DRAGON BOYS wanauawa kwa sababu mmoja wao aliishi na kufanikiwa kutoroka na wewe hapo na wenzako mlifanya kosa la kipumbavu sana kushindwa kunikagua kwenye mwili wangu ambapo mngeikuta simu ambayo nilikuwa naitumia kuweza kuwasiliana na wale watu"
"Uzembe wako ndio umefanya mpaka leo nipo hapa kwa sababu kupitia simu ile alifanikiwa kunipata na wakati ule ambao wewe ulkuwa unaenda kunizika nikiwa hai mwanaume yule alikuwa anaufuatilia msafara wako na kila ambacho ulikuwa unakifanya alikuwa anakiona ndiyo maana ikawa rahisi sana kuweza kunifikua pale baada ya nyie kuondoka japo hakuwa na matumaini kama anaweza kunikuta nikiwa bado hai lakini Mungu ametenda miujiza yake baada ya miaka mingi sana ya kulala kitandani leo nipo tena hapa na tumeweza kukutana kwa mara nyingine Karistus" mwanaume alikuwa anampa mipango ambayo ilifanyika mpaka yeye kuweza kupona na wakati wanaongea wakati huo walikuwa wanayatumia majina ya halisi kabisa.
"Hahaha hahaha kwahiyo na mimi nilifanya kosa la kipumbavu kama ulivyofanya wewe"
"Hapana, kosa lako lilikuwa dogo sana ukifananisha na langu, ujinga wangu wa kumwamini yule malaya umeliingiza taifa hili kwenye tatizo kubwa sana. Nina imani kama sio kumwamini Brandina mpaka leo hii basi huenda haya yote yangeisha wakati ule ule lakini ujinga wangu uliyaondoa maisha ya raisi, uliyaondoka maisha ya Bilali na kijana wake lakini watu wengi walibaki wanateseka kwa sababu ya kosa langu moja tu ndiyo maana nimerudi kuhakikisha kwamba kosa langu ambalo nililifanya haliji kujirudia tena"
"Huenda upo sahihi Donald lakini kumbuka kwa sasa unaweza usifanye kosa ila tayari una udhaifu, kuwa karibu na familia ni kosa kubwa sana unapo ingia kwenye vita na watu kama hawa hivyo bado huenda mchezo huu utakuwa mgumu sana kwa upande wako. Yule mtu ana pesa sana, ana watu wa hatari sana bado unahisi kwamba unaweza kushinda vita hii ambayo ipo mbele yako?"
"Unawaza kuhusu pesa? nina pesa nyingi sana ambazo hata nikisema nichukue watu miamoja nianze kuwaleta wasifanye kazi kwa miaka mingine miamoja ijayo hawatazimaliza, sidhani kama suala la mhimu ni pesa kwa sasa ila suala la mhimu ni uhai"
"Umezipata wapi hizo pesa?"
"Nadhani unakumbuka kwamba niliwahi kuwa na gavana kwenye mkono wangu, sidhani kama kuna haja ya kuendelea kuuliza kwamba nilizipataje pesa"
"Max una uhakika na hili unalo lifanya kwamba utashinda?"
"Unatakiwa kuyahofia kwanza maisha yako kabla ya kuanza kuwawazia watu wengine Karistus. Nina maswali machache sana ambayo nataka unijibu hapa saivi maana hatutakuwa na namna tena ya kuweza kuja kuongea tena baada ya leo. Ni kipi kilikufanya ukaisaliti nchi yako?"
"Pesa"
"Pesa tu?"
"Yeah, maisha haya ni mafupi sana kuna muda unajito sana kupigania maslahi ya wengi lakini hakuna anaye ona wala hakuna anayejali kabisa sasa kuna maana gani kuweza kuendelea kuwapigania watu ambao hawawezi hata kuona thamani ya unacho kifanya? siku zote nilikuwa nataka kuwepo sehemu ambayo nitakuwa naheshimiwa, sehemu ambayo nitakuwa napewa kile ambacho nastahili na hicho ndicho nilikifanya kwa sasa. Hii miaka kumi na miwili nimeishi maisha mazuri sana, maisha ya kifahari sana kwa kadri nilivyokuwa nataka mwenyewe na hakukuwa na mtu hata mmoja ambaye alikuwa anaweza kuja mbele yangu na kuwa kama tishio kwangu na hiki ndicho ambacho mimi nilikuwa nakihitaji kwa miaka ambayo nilikuwa naishi duniani"
"Lakini bado ulikuwa mtumwa"
"Hiyo sio biashara yangu kwa sababu hainihusu kikubwa nimeishi vile nilivyotaka mimi"
"Sawa, kuna neno lolote lile la mwisho kwa familia yako?"
"Whaaat?"
"Sio muda umetoka kutishia kuhusu kuwa na udhaifu wangu ambao ni familia yangu lakini wewe upande wako mbona unashtuka sana? Najua kwamba baada ya lile kutokea ulikuwa umempa mimba yule mwanamke ambaye alikuwa katibu wa raisi na baadae ukawa unaishi naye lakini ukaamua kukaa naye mbali baada ya yeye kupata mtoto ukihofia kwamba watu wakijua wanaweza kuja kumvamia na kumuua mwanao"
"Max usije ukathu......"
"Naona unaogopa sana, mtoto siwezi kumuua kwa sababu hahusiki kwa lolote na hajui kama baba yake ni mtu wa hovyo sana namna hii hivyo ataishi lakini vipi kuhusu mama yake karistus? mtu ambaye alihusika kumteketeza raisi wa nchi unataka naye aendelee kuishi au kuwa hai? huoni kama nitakuwa nawakosea heshima Watanzania na wapiganaji wenzangu ambao wametangulia kaburini?"
70 inafika mwisho.
🔥Thank you sana man
Umekula kwanza kijana, una kazi??Thanks ur Bro...!![emoji1545]
Daaah!! "huoni kama nitakuwa nawakosea heshima Watanzania na wapiganaji wenzangu ambao wametangulia kaburini?" Script hatarHADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)