Kb Ulayaulaya
JF-Expert Member
- Jan 5, 2023
- 727
- 1,059
Kigongo mulua kabisa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Uzi mapya contribution will be done for you our bossGood evening fellas. Nimepotea kama siku mbili nikiwa kupigania tumbo ila kama kawaida nilisema nikipotea nafidia hivyo leo nitaweka episodes tano.
NB
Acheni mambo yenu nunueni simulizi, mnatukata maini waandishi kuendelea kuandika [emoji28]
NoumaHADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
Episode 78
"Niliwahi kufanya hayo yote kwa sababu kabla ya kuwa na maisha mazuri kwenye akili yangu niliwahi kuhisi kwamba pesa ndiyo kila kitu kwenye haya maisha, niliwahi kuamini kwamba watu wenye pesa ndio watu ambao wanaishia maisha mazuri kuliko mtu yeyote yule hapa duniani lakini nilikuja kugundua kwamba nilikuwa na mawazo ya kipumbavu sana baada ya kuwa na hizo pesa ambazo nilitaka kuwa nazo na tangu siku hiyo nilijue hilo niliacha kabisa kuhangaika na pesa na hata zile pesa nyingi ambazo nilikuwa nataka niwe nazipata kila siku sikuona umuhimu wake na ndipo nilikuja hata kukukatalia kuweza kuanza kutakatisha pesa za watu. Unajua ni kipi kilinibadilisha Denis?" mzee huyo alitulia tena na kumwangalia Denis Kijazo kwa macho yaliyo choka sana kisha akaendelea;
"Familia, familia ndicho kitu bora zaidi kwenye haya maisha ya mwanadamu. Anayekwambia kwamba pesa inaleta furaha au inanunua furaha basi huyo ni mtu muongo sana au atakuwa hajui nini maana ya neno furaha. Furaha ni nyakati tu ambazo zinakuja na kupotea haijalishi una pesa na hauna, unaweza kuwa na furaha muda huu lakini dakika tano baadae ukawa na huzuni mpaka ukataka kujiua bila kujalisha kama una pesa au hauna kama wewe hapa sasa hivi. Una mabilioni ya pesa lakini hauna raha, si unaamini pesa inakupa furaha sasa kwanini unatia huruma na kuwa mnyonge namna hiyo? Pesa haileti furaha bali inasaidia sana kwenye kutatua matatizo mengi ambayo yanaleta mawazo kichwani na hapo ndipo ambapo watu huwa wanachanganya na furaha. Pesa unapaswa kuwa nayo kwa sababu ina msaada mkubwa sana na zaidi ya asilimia sabini ya maisha ya mwanadamu kutimiza mahitaji yake kunamtaka kwanza atumie pesa hilo hakuna anayebisha ila pesa sio chanzo cha furaha"
"Ukiacha familia nimejifunza kwamba amani ni bora kuliko kuwa na huu utajiri ambao watu wengi wanakuwa wanaulilia kwa sababu kuna wakati ili kuupata huo utajiri kunakulazimu kufanya mambo ya ajabu na ya kutisha sana ambayo yanakuja kukuletea mwisho mbaya ambao hata wewe haukuwahi kabisa kuufikiria kwenye maisha yako na mambo haya hayajawahi kuwa na mwisho mzuri hata siku moja, unaweza ukaishia pabaya na pesa ambazo ulikuwa unazipigia kelele zisikusaidie lolote lile" mzee huyo alitema mate chini kuuweka mdomo wake sawa akiwa anamwangalia Denis Kijazo ambaye alikuwa mbele yake anamsikiliza.
"Umenipa maelezo mengi sana ambayo yamekaa kama unanipa wosia, unamanisha nini?"
"Una chaguo moja tu Denis, ni labda mtu huyo umuue haraka au kama sio hivyo basi wewe ndiye unakwenda kufa na kuteketea vibaya sana"
"Unahisi bwana mdogo kama yule anaweza kuniua?"
"Swali lako linapaswa kuwa kwanini amerudi na kuruhusu wewe ujue kwamba amerudi? kwa sababu alikuwa ana uwezo wa kupotea moja kwa moja maana ulijua ameshakufa hivyo kama amerudi na akataka kujua, maana yake ni kwamba anajua ataanziwa wapi kudili na wewe na atakuja kumalizia wapi kitu ambacho kinakuweka kwenye hatari kubwa sana"
"Hilo nalijua ndiyo maana nimeamua kubeba familia yake na kwenda kuihifadhi mahali ambapo atakuja yeye mwenyewe na huko nadhani napaswa kumuua moja kwa moja japo nilikuwa nina mpango wa kumhifadhi ateseke kwa miaka mingi sana"
"Hivi Denis wewe umewahi kujiuliza kwamba ingekuwaje kama kuna mtu angekuja kuiteka familia yako?"
"Hakuna mtu ambaye anaweza kuja kufanya hilo"
"Wapo ila huenda huwa wanatanguliza utu kwanza kwa sababu wanafamilia wengine wanakuwa hawahusiki kabisa hivyo inaweza kuwa ni kuwaonea tu kuwaingiza kwenye hayo mambo kitu ambacho kinaweza kuwa hatari kubwa sana kama watu ambao unatishia familia zao siku wakiamua kuijia yako"
"Ni kama unanitisha sio?"
"Sipo hapa kukutisha ila nakuona kabisa ukiwa na mwisho mbaya sana. Chaguo ni lako Denis muue mapema au uishie kwenye futi sita kama ulivyo wapeleka wengi na kama unaweza kuvumilia aibu basi kajisalimishe mwenyewe hiyo inaweza kuwa njia ya kujiweka hai tena ili ufungwe tu na usiuawe" Denis Kijazo alicheka sana baada ya mzee huyo kutamka hayo maneno ya kusema kwamba akajisalimishe, alicheka sana huku akiwa anaondoka kisha akasimama baada ya kufika kwenye mlango wa chumba hicho.
"Panapo majaliwa nitakuletea kichwa chake ukae nacho kwa wiki nzima humu ndani, nimejua kwenye ushauri wako ni kipi nikichukue na kipi nisikichukue. Kwaheri profesa" alitabasamu na kutoweka humo ndani.
Max safari yake ilienda kuishia nyumbani kwa James, komando ambaye alipoteza maisha akiwa analipambania taifa lake. Baada ya kufika sehemu hiyo aligonga geti kwa nguvu sana kaisi kwamba mlinzi alifungua kwa hasira sana akiwa na silaha mkononi lakini aliguswa shingoni akatulia na kulazwa pembeni. Mwanaume alitembea akiwa anaangalia mandhari ya eneo hilo na kumsifu sana James licha ya kuishi mbali lakini alihakikisha kwamba familia hiyo inaishi maisha mazuri sana.
Aligonga mlango wa nyumba kubwa na kusogea pembeni ambapo alisikia kwa ndani hatua za mtu zikija mlangoni. Mlango ulifunguliwa na aliyefungua alikuwa ni mwanamke ambaye umri wake alikuwa anaonekana sio chini ya miaka thelathini na mitano mpaka arobaini. Mwanamke huyo baada ya kumuona mtu ambaye hakuwa akimfahamu alishtuka sana na kuangalia getini kwake ambako alishangaa kuona mlinzi yupo chini, alipiga kelele na kutaka kukimbia lakini mwanaume alimdaka na kumuwekea alama ya kidole kwenye mdomo wake kumtaka atulie.
"Mlinzi hajafa, nimemzimisha tu na usipige kelele utamshtua mwanao. Sijaja hapa kwa ubaya na kama ningekuja kufanya hilo basi nigeshakuua muda mrefu tangu unatoka hapa"
"Wewe ni nani?"
"James unamfahamu?"
"Ni mume wangu"
"Mimi ndiye yule mwanaume ambaye aliamua kuishi mbali na familia yake ili aweze kunisaidia"
"Unamaanisha wewe ndiye yule ambaye ulipandishwa kwenye ndege siku ile usiku miaka kumi na mbili iliyopita?"
"Ndiye mimi mwenyewe na niseme tu kwamba asante sana kwa msaada wako mkubwa. Kila siku James amekuwa akiwaongelea sana wewe na mwanae na ni mtu ambaye anawapenda sana isivyo kawaida"
"Mume wangu yuko wapi?"
"Unaniruhusu niingie ndani nikae?" mwanamke huyo hakuwa na namna zaidi ya kumkaribisha ndani mwanaume akaketi kwenye sofa la bei ghali sana.
"Bila shaka huyo ndiye mtoto wenu" Max aliongea akiwa anaiangalia picha kubwa ambayo ilikuwa ukutani.
"Uko sahihi kabisa lakini bado haujanijibu swali langu"
"Mumeo amepoteza maisha usiku wa leo"
"Whaaaaaat?"
"Nasitahili sana kubeba hizi lawama kwa sababu huenda kama sio mimi bado angekuwa hai na angefanikiwa kurudi tena kuishi na nyinyi kama alivyokuwa anatamani siku zote huku akiwa anaota na ndoto kila siku akidai kwamba amewakumbuka sana. Naomba unisamehe sana" maneno hayo yalikuwa yanamtoa machozi mke wa James, mwanamke ambaye alikubali kumpenda mwanaume ambaye alimdanganya hata kazi yake, mwanaume ambaye yeye alikubali kumsubiri kwa miaka yote ambayo alikuwa ametoweka lakini taarifa ya mwisho ilikuja kwamba alikuwa amefariki na hakuwepo tena duniani, kwake yalikuwa zaidi ya maumivu.
"How?" aliuliza akiwa anajifuta machozi na kujikaza ila uso ulikuwa unamsaliti pakubwa sana.
"Kwenye maisha mafupi ambayo tumefahamiana mimi na yeye, tumekuwa zaidi ya ndugu, amekuwa kama kaka kwangu na ni binadamu ambaye pekee aliamini kwamba kupitia mimi nchi hii inaweza kujitoa kwenye udhalimu mkubwa sana ambao unafanyika na viongozi ambao wameamua kujigeuzia nchi hii na kuifanya kuwa yao lakini yeye aliamua kujitoa sadaka na kuiacha familia yake kwa ajili ya kulipambania taifa hili liwe salama. Ameuawa leo na watu ambao walikuwa wanayataka maisha yangu ili niache kila ambacho nilikuwa nakifanya. Kiufupi naweza kusema kwamba amekufa akiwa anaipambania familia yangu kuiokoa kutoka kwa wale watu"
"Naanzia wapi kumwambia mwanangu hizi taarifa? miaka yote hii huwa anauliza baba yake alipo na nilimuahidi kwamba angeweza kurudi lakini inarudi taarifa ya kifo chake. Nitamwambia nini mwanangu mimi?"
"Siku zote maisha huwa yanatupa namna mbaya ya kukumbana na uhalisia unao umiza sana, hatia itaishi kwenye moyo wangu kwa kushindwa kuwalinda watu wangu wa karibu lakini maisha haya haya yananipa funzo kuhusu wanadamu. Maisha yamechagua kuniumiza mimi na watu wangu wa karibu, maisha yamenichagulia njia mbaya sana ambayo natakiwa kukumbana nayo hata bila kupenda wala kutaka na maisha yananitaka mimi niwe hivyo. Maisha yananipa tafsiri mbaya sana kuhusu hatima nzima ya maisha yangu, natamani niseme neno lakini najikuta najichukia sana mimi mwenyewe. Kuna kosa kubwa sana niliwahi kulifanya huko nyuma kwa sababu ya mapenzi ndiyo sababu kubwa ya haya yote kuendelea kutokea kwani kama sio hivyo hili jambo lingeisha mapema sana. Nimempoteza kila ambaye alikuwa upande wangu na nilicho bakiwa nacho ni familia tu ambayo nayo ipo mikononi mwa hao watu, mimi sina cha kukifanya kumrudisha mumeo lakini nakuahidi kwamba watu ambao wamehusika na hili muda kama huu kesho zitavuma habari kila pembe ya dunia kwamba wamekufa vibaya sana"
78 inafika mwisho.
I respect thatUzi mapya contribution will be done for you our boss
Hutaki iishe mkuu?Hii hadithi naona kama yatamatika karibuni 🤔
Siku za weekend na sikukuu wanazitumia kama muda wa kuandika simulizi maana hata wao wana majukumu siku zote za kazi kama sisi.Nimegundua humu jf watunzi hawapendi kuleta mzigo siku za mapumziko (weekends na sikukuu). Hupenda kuleta mzigo kipindi cha hekaheka (jumatatu hadi ijumaa)
CC
FEBIANI BABUYA
singanojr
Upo sawa mkuu KWA HiloSiku za weekend na sikukuu wanazitumia kama muda wa kuandika simulizi maana hata wao wana majukumu siku zote za kazi kama sisi.