Simulizi ya kipelelezi: Jiji la kamari (gambling city)

Simulizi ya kipelelezi: Jiji la kamari (gambling city)

Good evening fellas. Nimepotea kama siku mbili nikiwa kupigania tumbo ila kama kawaida nilisema nikipotea nafidia hivyo leo nitaweka episodes tano.

NB
Acheni mambo yenu nunueni simulizi, mnatukata maini waandishi kuendelea kuandika [emoji28]
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 74
"Sawa bosi" alijibu kiufupi kwa sababu hakutaka kumkera kiongozi wake lakini hata yeye ilionekana kwamba ni taarifa ambayo ilimshtua sana isivyo kawaida kuhusu kifo cha kijana huyo ambaye alitegemea kwamba muda sio mrefu angeungana naye kufanya kazi kwa pamoja. Mwanaume huyo ambaye alikuwa anatisha sana baada ya kuikata simu hiyo ya bosi wake aliitafuta namba ya kijana wake mmoja ambaye alikuwa anadili sana na mitandao na hapo ndipo kosa kubwa ambalo James na Max walilifanya lilijidhihirisha wazi.
"Mick uko wapi?"
"Nipo kambini tulipo fikia bosi"
"Unakumbuka kuhusu lile tukio la mke wa Max kupokelewa uwanja wa ndege?"
"Ndiyo mkuu mpaka sasa bado video tunazo na picha"
"Unaweza kuzipata zile platenumber za yale magari?"
"Ndiyo gari moja ya katikati inaonyesha platenumber ambazo ni binafsi hivyo inawezekana"
"Nahitaji uitraki gari hiyo haraka sana na kujua kwamba iko wapi, dakika mbili uwe umeifanya hiyo kazi na unirudie hewani haraka sana" mwanaume aliikata simu hiyo akiwa anarudi ndani na kwenda kuvaa, hata mwnaamke wake alimshangaa sana maana alirudi akiwa amebadilika hata sura yake ilikuwa inajieleza. Mwanaume huyo hakutaka hata kuaga kwa mwanamke huyo alianza kuondoka lakini alisimama baada ya kusikia swali kutoka kwa mrembo huyo.
"Kuna kitu huwa unanificha kuhusu kazi yako?" ni swali ambalo lilimfanya amwangalie sana mwanamke huyo bila kummaliza.
"Ni bora endelea tu kuhisi hivyo hivyo ila kama utafanikiwa kuujua ukweli basi kamwe hautajisamehe kwenye maisha yako" ni kauli yenye utata mkubwa sana ambayo alimwachia mwanamke huyo. Kauli ambayo angechelewa sana kuweza kuelewa na siku ambayo angeielewa basi huenda ingemuumiza sana kwa sababu mwanaume huyo kutamka hivyo alimaanisha kwamba kama siku mwanamke huyo akaja kujua kwamba huyo ndiye mwanaume ambaye amemzalisha mama yake na yeye mwenyewe basi hataisamehe nafsi yake.
Kosa la ile platenumber ya gari ndilo liliwapa wanaume hao mwelekeo kwamba ni wapi ambapo nyumba ilipokuwa gari hiyo ilipokuwepo. Zilikuwa ni dakika chache sana kuweza kulikamilisha zoezi hiyo huku yeye akitumia location ya mahali ambapo lilikuwepo jumba hilo na vijana wake nao wakiwa wanaelekea eneo hilo hilo kuweza kuwapata watu wao ambao walikuwa wamewafuata hapo.
James aliruka kwenye gari ikiwa bado kwenye mwendo ambapo ilienda kujikita kwenye ukuta na kusimama yenyewe huku mwanaume akiwa anawahi getini ambapo alikuta geti liko vizuri kama vile walivyokuwa wameliacha mwanzo. Mwanaume aligonga geti hilo na kwa ndani alisikia hatua zikija lakini hakuwa na uhakika sana na usalama wa eneo hilo hivyo alilifungua geti hilo kwa kutumia fingerprint zake na baada ya kufunguka alikuwa anaangaliana uso kwa uso na mlinzi mmoja ambaye alishangaa sana kumuona kiongozi wao akiwa kwenye hofu kubwa sana.
"Mkuu kuna usalama huko utokako?"
"Hakuan usalama sana, hakuna mtu amekuja kuichukua familia hapa saivi?"
"Hapana, mke wa bosi ni mtoto wote wamelala" James alihema kwa nguvu sana huku akianza kutembea kuelekea ndani ya jumba hilo na kumtaka mlinzi huyo alock mlango na kuhakikisha wanalinda kona zote za jumba hilo mpaka pale ambapo watakuwa wameondoka.
"Hili eneo sio salama tena tunatakiwa kuondoka wakati huu na bosi ametaka iwe hivyo kwahiyo tunaipeleka familia mahali salama kuanzia muda huu"
"Sawa kiongozi" mwanaume huyo alijibu bila kuuliza wakati huo James aliingia ndani ya jumba hilo kwenda kumchukua mama na mtoto lakini mlinzi ambaye alibaki nje alihisi kama alisikia tairi za gari zikifunga breki kali sana eneo hilo hivyo aliwaita wenzake haraka sana na kuwapa maelekezo huku asilimia nyingi wakijua ni bosi wao amerudi japo waliamua kuchukua tahadhari. Wakiwa wamejipanga hapo na kugawana kona za kusimama kuhakikisha ulinzi wa hilo jumba, umeme ulikatika ghafla sana na haikuwahi kutokea ndani ya jumba hilo umeme ukakata.
Ilikuwa ni ishara mbaya sana na utambulisho kwamba ndani ya jumba hilo walikuwa wanapokea wageni. Plate number za gari zilikuwa zinawaponza kirahisi sana, James baada ya kuona hali hiyo alikimbia haraka ndani na kwenda kumuamsha mke wa kiongozi wake pamoja na binti yake Naima ambao alihitaji wajiandae haraka sana aweze kuondoka nao ndani ya hilo eneo haraka sana na wakati huo alituma meseji kwa Max kwamba tumevamiwa.
Walinzi ambao walikuwa wapo nje alikuwa anadondoka chini mmoja mmoja wakiwa wanauawa na watu ambao hawakuwa wakiwaona kutokana na kiza ambacho kilikuwepo humo ndani na baada ya dakika kadhaa tu kazi ilikuwa imeisha na umeme ukawa umerudi kama kawaida. Wakati ambao umeme unarudi James alikuwa amewashika mikono mke na mtoto wa kiongozi wake akiwa anahitaji kutokea mlango wa nyuma na kuweza kupotelea huko lakini kwa bahati mbaya sana wakati anafungua tu huo mlango na kutokezea upande wa pli wa nyuma hiyo ambako kulikuwa na geti lingine la shaba, alishangaa kivuli kikija kwa kasi sana kutoka juu ya ukuta mrefu wa geti hilo. Licha ya kuwepo kwa nyaya za umeme lakini mtu ambaye alikuwa anakuja hapo, alidunda kwenye mti mrefu ambao ulipandwa pembezoni huku akitua chini mithili ya paka.
James alikuwa na bahati mbaya sana, mwanaume ambaye alikuwa amemtembelea hapo alikuwa ni Ted mwenyewe, mwanaume huyo wa kazi alikuwa amefika ndani ya eneo la tukio na kuifanya kazi hiyo kwenda kuwa ngumu sana. James alitoa bastola yake lakini mwanaume huyo alitikisa kichwa kumuonyesha ishara ya kukataa hilo jambo kwani alikuwa na mtoto kwenye mkono wake na kama angefanya ujinga wowote ule basi alikuwa anampoteza mama na mtoto wake ndiyo maana mwanaume huyo alimzuia kutumia silaha ya moto.
"Kuna wanaume watano ambao ndani ya dakika moja watakuwa wamefika huku tuliko na nina imani mpaka hivi tunavyo ongea wanaweza kuwa wameua walinzi wote humu ndani hivyo usifanye kosa kubwa la kutaka kuachia hiyo risasi ambayo itafanya wote mfe. Una nafasi ya kuondoka na hawa watu wako lakini mpaka uhakikishe kwamba umenipeleka chini kwanza, kama ukifanikiwa kunidondosha hata mara moja tu na sio kunipiga mimi nawaacha muende na huyo mtu nitamtafuta kwa namna nyingine"
"What does he want?" Naima, binti wa pekee wa Max aliuliza akiwa anamshangaa mwanaume huyo alivyokuwa anatisha na kuongea kwa kujiamini sana, binti huyo hakuwa anaelewa kiswahili vizuri lakini kumuona mtu wa namna hiyo kwake ilimfanya akose kabisa amani na kuwa na hofu sana kwenye moyo wake. Ted alitabasamu na kumsogelea binti huyo mdogo kisha akamshika shavuni.
"This will be over soon daughter, don't worry" alitabasamu kinafiki mwanaume huyo na kuchomoa kisu kikali sana na kumfanya Naima kupiga kelele ya kilio maana alihisi mtu huyo anataka kumkata ni yeye lakini Ted alimpa ishara Ariana aweze kusogea pembeni na mwanae maana hiyo ilikuwa ni michezo ya kiume, mtoto alitakiwa kufunikwa macho asione kilichokuwa kinaenda kutokea hapo maana huenda kingeacha kumbukumbu mbaya sana na za kutisha sana kwenye kichwa chake kwa maisha yake yote.
Ilikuwa ni fair fight ambayo wote hawakutakiwa kabisa kutumia silaha za moto kwa ajili ya mtoto. James alikuwa anamjua sana mwanaume huyo, alikuwa anajua hawezi kupambana naye kwa lolote lile kwa sababu hata kiongozi wake tu Bilali ambaye walikuwa wanamuogopa sana kwenye tasnia ya mapigano alikuwa akimuogopa vilivyo mwanaume huyo na namna alivyokuwa mkatili hivyo kitu pekee ambacho yeye alikuwa anakifanya hapo ilikuwa ni kupoteza muda ili kama inawezekana Max aweze kurudi mapema na aliomba iwe hivyo maana kama mwanaume huyo angefika hapo mapema basi hakuna mtu hata mmoja ambaye angefanikiwa kuigusa familia yake.

74 inafika mwisho.
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 75
Alihesabu hatua tano kurudi nyuma ambapo mwaname huyo alikuwa anamsogelea tu bila hofu, alichomoa visu vyake viwili kiunoni James na kuirusha saa yake ambayo ilikuwa na viwembe pembeni kwa nguvu lakini ilipasuliwa na bisu lililokuwa mkononi mwa Ted. Alisogea kwa nguvu na kurusha ngumi ambayo ilichanganywa na kisu, ilimkosa Ted kwenye shavu lake na ngumi hiyo ikazungushwa na kumpata kwenye taya lakini wakati huo huo akiwa anapambana na kukizamisha kisu kwenye shingo ya Ted, alipokea ngumi ya kifua ambayo ilimpeleka mpaka ukutani, ilikuwa ni ngumi nzito sana yenye kilo za kutosha na hakuwa na namna ya kuweza kushindana nayo.
James alijivuta kwa nguvu kuelekea pale alipokuwepo Tedy, alirusha ngumi nyingi sana za kasi akiwa anazichanganya na visu kujaribu bahati yake kama kuna ambayo ingepenya basi kwake ingekuwa ni nafuu kubwa sana lakini hakuna ambayo ilifanikiwa. Alijipinda kwa sarakasi ya mbele akiwa amelenga kwenye paji la uso la Ted lakini alirudishwa kwa buti kali ambalo lilimpasua vibaya sana sehemu yake ya jicho na kumfanya kuyumba yumba sana na kurudi nyuma.
Akiwa anasimama aliona kisu kinakuja upande wake tena kikiwa kimelenga kwenye koromeo, alikuwa amechelewa kukikwepa hivyo akakidaka kwa mkono wake ambapo kilimchana vibaya sana. Wakati anakaa sawa na kukiachia kisu hicho mkono ukiwa na maumivu makali sana, alikoswa na kiwiko ambacho kingeivunja taya yake ni kama bahati kwake aliinama haraka sana ila wakati anasimama alipigwa na viganja vikali sana kwenye masikio yake ambayo yaliacha kusikia na kuanza kumuuama sana.
Mwanaume alibaki anagugumia kwa maumivu makali sana akiachia kisua chake na kushika masikio hayo ambayo yalimzalishia maumivu makali sana ya kichwa na wakati anakiachia kisu hicho kilitua kwenye mikono ya Tedy ambapo alikitumia kumchana chana vibaya sana James kwenye kifua chake mpaka akadondoka chini akiwa anahemeana kwa taabu mno. Tedy alimsogelea pale chini na kuchuchumaa wakati huo wanaume ambao walikuwa upande wa mbele walikuwa wamefika hapo.
"Wewe bado ni dhaifu sana na najiuliza ulifanikiwa vipi kuwa komando na wenzako ambao hamuwezi hata kunivunja mfupa wangu mmoja, natamani nimpate mtu ambaye nitasimama naye ulingoni nami nijivunie kupigana. Nina zaidi ya miaka kumi na mitano sijwahi kupigana na mtu yeyote bali huwa napiga na kuua watu kwa sababu wote ambao nakutana nao ni dhaifu. Najua matumaini yako yapo kwa huyo mtu wako, nami namsubiri kwa hamu sana nione ni kwa namna gani aliweza kupona kutoka kwenye kaburi kwa msaada wako wa kipuuzi" Mwanaume alikuwa anajikubali sana, James alikuwa mnyonge kwa sababu alicho kuwa anaambiwa kilikuwa ni cha kweli, hakuwa na uwezo wa kupambana na mwanaume huyo ambaye alikuwa na uwezo wa juu sana ukimfananisha na yeye.
"Uta…kufa vibaya sa..." James alikuwa anaongea kwa taabu sana maana alikuwa anatoa damu kila sehemu, kauli yake ilikatishwa na Ted.
"Nilifanya kosa sana kukuacha hai kipindi kile kwa sababu ulijiona kama umekuwa mwokozi wa taifa tayari ila leo huna hata uwezo wa kujisaidia mwenyewe halafu unanitisha mimi kwamba nitakufa, sasa mimi na wewe wa kufa nani? naondoka na hii familia kisha nimsubiri huyo ambaye ndiye kabeba matumaini yenu nyie. Nitamuua vibaya sana kuliko nilivyowahi kumuua binadamu yeyote yule na kama tukija kukutana kwenye maisha mengine basi hakikisha unaikumbuka hii sura na kukimbilia sehemu ambayo unahisi kwamba itakuwa salama" Tedy alitamka akiwa amemkazia macho James na wakati huo alikizamisha visu vyote viwili kwenye moyo wa James na kuanza kuvinyonga taratibu hali ambayo ilimfanya mwanaume huyo kufa kwa maumivu makali sana hatimaye aliweza kutulia.
Mke wa Max alikuwa anashuhudia ukatili huo akiwa amemfumba mwanae macho ili asuione hali hiyo, alikuwa anatetemeka sana mwanamke huyo maana alicho kishuhudia hapo haukuwa ubinadamu wa kawaida bali ulikuwa ni unyama wa kutisha sana. Wanaume hao waliichukua familia hiyo na kupotea nayo hilo eneo huku wakiamini kwamba huo ulikuwa ni mwanzo wa mwisho kwani dakika yoyote kuanzia wakati huo walikuwa wanaenda kumpata Max kwenye mikono yao.

Maeneo ya Masaki nyumbani kwa Dax, Max aliwashtukiza wanaume hao baada ya kuwauliza kama walikuwa wamefika hilo eneo kwa ajili yake.
"Nilijua ni mtu wa maana sana kumbe ndo wewe hapa?" aliuliza mwanaume mmoja akiwa anaitoa bastola kwenye kiuno chake tena akiwa na hasira sana lakini alizuiwa na mwenzake.
"Huyu anahitajika akiwa hai, ukitumia bastola haina mwenyewe hiyo unaweza ukapiga sehemu mbaya akafa ikawa kesi nyingine kwa wakubwa"
"Si anajifanya alipona kwa risasi sita kwenye mwili wake, nilitaka kumuonyesha ni kwa namna gani risasi zinapaswa kutumika na kwa namna gani risasi inaweza kuyachukua maisha ya mtu" alijibu kwa hasira sana huku akiwa anairudisah bastola yake kiunoni, hakuona kama ni sawa wao kuteswa au kusumbuliwa na kijana kama huyo wakati muda huo walitakiwa kuwa na mambo mengi sana ya mhimu kuweza kuyafanya.
"Sijajua uliko kulia na ulilelewa na nani ila unaonekana kuwa moja kati ya watu wapumbavu sana ambao nimewahi kuwaona kweye maisha yangu. Huo mdomo wako kama umeshindwa kuutumia vizuri basi leo nitakufundisha namna ya kuufunga unapokutana na watu ambao hauwajui. Si unataka kujua niliponaje nikiwa na risasi sita kwenye mwili wangu? Unataka kujua nilifanikiwaje kuzikwa na nikarudi nikiwa hai? basi una dakika nne tu za kuweza kuyapata majibu ya maswali yako na kama ukimaliza hizo dakika niamini mimi utakuwa na uwezo wa kuweza kuniua au kuondoka na mimi na kama zikikushinda basi ujue kabisa kwamba kila mmoja wenu atakufa kifo kibaya sana" mwanaume aliongea akiwa anaitoa shilingi moja ya zamani sana ambayo aliwahi kuitumia kwenye ukumbi wa Alexios Arena baada ya kukutana na Siza.
Shilingi hiyo ilidondokea kwenye sakafu ya pembeni na wakati inaana kuzunguka tu, Max alirusha kisu chake ambacho mwaaume ambaye alikuwa karibu yake alikikwepa kikamkita aliyekuwa nyuma kwenye mbavu lakini huyo ambaye alikuwa mbele yake akutaniswa na shoka lililokuwa linashuka kwenye paji lake la uso. Alifanikiwa kulikwepa shoka hilo ila kwa bahati mbaya sana wakati anafanikiwa kulikepa alipigwa na buti moja kali sana ambalo liliuvunja mguu wake vibaya mno na wakati anashuka chini, alipitishiwa shoka kwenye koromeo lake likakita hapo. Mwanaume alilichomoa kwa nguvu na kupiga buti kali sana kwenye kichwa cha mwanaume huyo ambaye alikufa kama bado yupo, alidondokea kwenye bwana la maji ya kuogelea habari yake ikiwa imeisha muda mrefu sana.
Wenzake ni kama bado walikuwa wameduwaa lakini ndio ulikuwa ukweli kwamba alikufa huku mmoja akiwa anauguza maumivu makali ya kwenye mbavu. Wawili ambao walikuwa wapo sawa, walijiviringisha mithili ya nyoka ambapo mmoja alilala kwa chini akirusha miguu kwa nguvu na mwingine ambaye alikuwa juu alizunguka kwa kasi na kuyakita mabuti mawili kwenye kifua cha Max ambayo yalimuingia hasa na kumtupa mbali sana lakini wakati anarushwa na mateke hayo aliliachia shoka lake ambalo lilikita kwenye paji la yule mwanaume ambaye alikuwa amemkita na mabuti hayo likawa limezama kwenye paji hilo la uso.
Mwenzake alishtuka na kugeuka haraka sana pale chini, alimuona mwenzake akiwa ananesa nesa mpaka ikafika hatua akawa amtulia tuli akiwa amekufa tayari. Alinyanyuka kwa hasira sana na kumtaka mwenzake ambaye alikuwa anaugulia kisu cha mbavu kusimama ili wapambane kwa pamoja, mwanaume huyo alianza kuendeshwa na mihemko ya hasira na sio uhalisia wa eneo ambalo alikuwepo hali iliyomfanya kumfuata Max pale chini alipokuwepo kwa nguvu sana na kumkita na buti la tumbo ambalo lilimburuza kiasi.
Mwanaume huyo alijigeuza na buti kali mithili ya mtu ambaye anataka kulala chini ambalo Max alilikwepa kwa kujigeuza kwa mkono mmoja na kusimama wima na buti hilo lilipasua sakafu ambayo ilikuwepo hapo. Mwanaume huyo alitisha kama anakuja kwa kasi lakini alisita bila kujua kwamba alikuwa anajiingiza kwenye mtego mwenyewe kwani kusita kwake kulimfanya adui yake awe na muda wa kumsogelea kwa kasi kuliko ambavyo alifikiri yeye.
Alipigwa ngumi kumi za haraka haraka kwenye kwapa zake hali ambayo limpelekea kulegea sana. Ngumi kali ilitua kwenye uso wake, pua ilipasuka vibaya sana lakini yeye mwenyewe pia alijikaza na kujibetua kwa teke lake maana mikono haikuwa ikifanya kazi kutokana na kulainishwa na ngumi kali ambazo zilipita hapo muda sio mrefu. Teke lilitua kwenye mbavu za max na kumsogeza nyuma kidogo lakini mwanaume huyo aliona kama anapoteza muda kuendelea kukaa hapo hivyo wakati komando huyo akiwa anamsogelea kwa nguvu ili kumuongezea mateke mengine ambayo alikuwa ana imani kwamba yangemdhoofisha mtu huyo Max alirusha ngumi kuelekea kwenye teke moja ambapo moja alifanikiwa kulipangua na ngumi moja.
Ngumi hiyo ilikuwa nzito sana kiasi kwamba baada ya kukutanishwa na teke hilo ilisababisha mguu wa komando huyo kuvunjika na kukosa balansi. Alikuwa anashuka chini lakini mwanaume alimuwahi na kumdaka ambapo alichomoa bastola kwenye kiuno chake na kumpiga risasi nne usoni akiwa anaangaliana naye karibu yaani mtu huyo ahakikishe kwamba anajiona jinsi anavyokufa. Damu nyingi sana zilimdondokea Max usoni lakini hakuwa akijali lolote alimuua kikatili sana mwanaume ambaye alikuwa ana majigambo ya kutosha.
Alikuwa amebakia mmoja ambaye hali yake haikuwa nzuri sana kutokana na kupigwa kisu kibaya cha mbavu akiwa ameishika bastola yake amemuelekezea Max. Mwanaume hakuwa na hofu aliiangalia shilingi yake ambayo ilianza kudondoka chini na kutulia mwanaume mmoja akiwa bado anaishi. Komando huyo licha ya kuwa na nafsi ya kuweza kufanya chochote kile aliishusha bastola yake na kumpa Max ishara ya kwenda.
"Kwanini hautaki kurusha risasi?" Max alimuuliza mwanaume huyo
"Nilijua tu kwamba hii ni kesi ambayo imetengenezwa na wakubwa kwa ajili ya maslahi yao tu ila nimegundua kwamba hauna hatia yoyote ile hivyo unaweza kwenda na kuhakikisha unaimaliza hii kazi na kama utapata nafasi japo ni ngumu sana basi hakikisha unawaua wote"
"Nchi itakukumbuka kwa hili kamanda na huenda kuna siku nyingine tunaweza kuonana kwenye maisha mengine hata kama sio haya. Humo ndani kuna mtoto mdogo ambaye anaishi bado kwa sababu hana hatia yoyote ile, nitakushukuru sana kama ukimchukua na kumlea kama mwanao ila hakikisha tu asije kuijua historia ya maisha yake maana inatisha sana inaweza kuja kuzua mambo mengine kwa baadae" Max aliongea kama kufurahishwa na maamuzi ya komando huyo hivyo akaona anaweza kuwa mtu sahihi wa kumlea binti wa Dax kuliko kuwapigia simu polisi ambao wangefanya mambo kuwa mengi sana.
"Good luck" wanaume walipeana saluti za heshima lakini wakati anatoka hapo Max ndio muda ambao ujumbe uliingia kwenye simu yake na kumtaka awahi nyumbani kwani kulikuwa na uvamizi. Mwanaume aliingia kwenye gari ya kijeshi ambayo walikuja nayo makomando eneo hilo ili kuweza kuwahi nyumbani kwake maana simu ambayo ilitumika kumpatia ujumbe haikuwa ikipatikana na hata mkewe hakumpata, hivyo hivyo hata kwa walinzi wote hakuna ambaye alikuwa anampata hewani jambo ambalo lilimfanya kuwa mtu mwenye wasiwasi mkubwa sana.
Max alikuwa na wasiwasi sana juu ya usalama wa familia yake, alikuwa na hofu mno kwa sababu hicho ndichi kitu cha pekee ambacho alibakiwa nacho kwenye maisha yake. Mwanaume alikuwa anatokwa na jasho sana kwenye mwili wake na wakati huo alikuwa kwenye mwendo mkali sana. Alichukua muda mchache sana mpaka kufika nyumbani kwake lakini baada ya kufika hapo alishangaa kuona gari ambayo aliondoka nayo James iliwa imekita kwenye ukuta, hiyo ilimshtua sana na baada ya kufika getini, geti lilikuwa wazi kabisa.

75 inafika mwisho.
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 76
Aliingia akiwa anakimbia na shoka lake mkononi ila kwa bahati mbaya sana walinzo wote walikuwa wamechinjwa vibaya mno. Hakusimama bali alipitiliza mpaka ndani akiwa na presha sana huku akiwa anaita jina la mwanae kwa nguvu sana lakini ndani kulikuwa kimya mno hali iliyozidi kuufanya moyo wake upatwe na ubaridi usio elezeka. Aliingia mpaka chumbani lakini bado palikuwa kimya sana hapakuwa na mtu yeyote yule eneo hilo hivyo aliingia mpaka kwenye chumba chake cha siri ambacho kilikuwa nyuma ya kabati la nguo na huko kulikuwa na skrini za cctv kamera.
Aliangalia matukio yote namna yalivyotokea na kumfanya ajisikie vibaya sana kwa sababu James aliuawa kikatili sana na alitamani kwamba ni bora muda ungerudi nyuma asiende Masaki kwanza bali wangerudi wote na James huenda hayo yote yasingeweza kutokea. Kinyonge sana alisogea taratibu mpaka nyuma ya jengo hilo sehemu ambapo ulikuwepo mwili wa mwanaume huyo wa kazi. Alisogea na kuketi pembezoni mwa huo mwili na shoka lake akiliweka kando yake.
"Nisamehe sana ndugu yangu, naendelea kuyafanya makosa yale yale ambayo yanapelekea nazidi kuwapoteza watu wangu wa karibu ambao ndiyo kama familia kwangu. Wewe ni miongoni mwa binadamu wachache sana ambao wana uzalendo ulioshamiri kwenye nafsi zao. Dunia itatambua mchango wako mkubwa ambao umeufanya, jina lako litaandikwa kwenye vitabu vya mashujaa na nakuahidi nitaitunza na kuilinda familia yako kwa maisha yangu yote. Hii kazi nitaimaliza kwa ajili yako, i'm sorry brother" mwanaume aliongea kwa uchungu sana akiwa anayafumba macho ya James ambayo bado yalikuwa wazi kisha mwanaume huyo akachukua shoka lake na kuzunguka upande wa mbele mwa jengo hilo kuangalia utaratibu wa namna ya kuisafisha na kuizika miili ya mashujaa hao.
Lakini baada ya kufika huko, tairi za gari zilikuwa zinasimama kwa kasi sana nje ya jumba hilo, kulionekana kuwepo kwa ugeni mwingine mkubwa sana. Mwanaume alihema kwa nguvu sana na kwenda kukaa kwenye ngazi za kuingilia ndani ya jumba hilo kuwasubiri hao ambao walipageuza kwake kama kwao. Walionekana wanaume ambao walikuwa ndani ya suti za bei ghali pamoja na miwani wakiwa wameongoza mbele na katikati yao alikuwa anaonekana mwanamke ambaye alikuwa amefunikwa kwa koti la gharama kubwa mno la manyoya.
Mkurugenzi mpya wa shirika la kijasusi la nchi ya Tanzania Chuki Steward ndiye ambaye alikuwa amefika nyumbani kwa Max akiwa na ulinzi mkali mno. Mwanamke huyo alisogea hatua kadhaa mpaka alipokaribia ile sehemu ambayo Max alikuwa amekaa, alisimama hapo na kuwataka walinzi wake kusogea pembeni.
"Unalipwa shingapi kuyafanya haya?" ilikuwa sauti nzito ya Max akiwa bado ameinamia chini huku shoka lake likiwa limetapakaa damu.
"Nipo hapa kwa ajili ya kuhitaji msaada wako Donald"
"Unajua kabla yako kwenye hiyo nafasi aliwahi kuwepo mtu ambaye mimi nilimheshimu sana kwa sababu yeye ndiye alinitengeneza mimi kuwa hivi, lakini unajua nini kilitokea? Ni kwamba yeye aliishia kufia kwenye mikono yangu mimi na mimi nikaishia kaburini lakini baadae nikafanikiwa kuja kuishi tena. Naona unataka kurudia kosa lile lile au unahisi Denis Kijazo atakulinda wewe kwa sasa?" mwanaume aliuliza akiwa anasimama na kuanza kuzisogeza hatua zake hilo eneo kwenye mkono wake akiwa amelikamata shoka lake kwa nguvu sana hali ambayo iliwafanya walinzi wa mkurugenzi kusimama mbele yake na kuzitoa bastola zao lakini mwanamke huyo aliwapa ishara wasogee pembeni.
"Donald naomba uniskilize, naelewa mambo ambayo umeyapitia kwenye maisha yako yanatisha sana kwa binadamu wa kawaida kuweza kuyavumilia. Najua umefanyiwa mambo mengi sana mabaya ambayo yanakufanya usiweze kumwamini mtu yeyote tena lakini nakuhakikishia kwamba hata mimi kuwa kwenye hii nafasi sikuwahi kujua kwamba nimewekwa ili kuja kutumika na watu fulani hapo baadae ila nimekuja kuligundua hilo nikiwa nimechelewa sana baada ya muda wa kuanza kutumika kufika. Mimi sitaki kuwa miongoni mwa viongozi ambao wameandika historia mbaya ya kuangamia kwa taifa hili bali nataka kuwa mfano wa viongozi ambao yale ambayo wameyafanya yatalifanya taifa hili liendelee kuwepo miaka na miaka hivyo nimekuja hapa nikihitaji kuungana na wewe tuweze kuifanya hii kazi ya kuwaondoa hawa watu kwa pamoja" mwanaume huyo alimsogelea mwanamke huyo ambaye alikuwa kiongozi mkubwa sana kiwa anamwangalia usoni.
Chuki hakuwa na wasiwasi hata kidogo kwa sababu hakuja kwa ubaya hapo ndiyo maana alijiamini hata kuwasogeza walinzi wake pembeni ambao kihalisia ni kwamba walikuwa wamekakaa kwa kujipanga na silaha zao na walikuwa tayari kufanya mashambulizi kama Max angefanya ujinga wowote ule kwa kiongozi wao.
"Niliwahi kufanya kosa kubwa sana la kuwaamini watu miaka kadhaa ambayo imepita na baadae ikaja kunigharimu sana sasa kwanini unahisi napaswa kukuamini wewe kwa sasa?" swali lake lilimpa kumbukumbu za mbali sana kipindi ambacho aliwahi kumuamini Brandina lakini baadae yakaja kutokea matatizo mazito sana.
Chuki hakuongea lolote baada swali la mwanaume huyo bali alitoa ishara tu kwa wanaume wengi ambao walionekana kuwa nje. Wanaume hao waliingia na wanaume watatu wakiwa wamefungwa pingu mikono yao ikiwa nyuma, wanaume hao walikuwa ndani ya kombati za jeshi.
“Unawafahamu hawa Donald?" swali lilikuwa rahisi sana kwani alikuwa anajua kwamba watu hao walikuwa miongoni mwa wale makomando saba. Max aliitikia kwa kichwa chake kukubali jambo hilo. Baada ya kukubali mwanamke huyo alichukua bastola kwa mlinzi wake na kuwapiga risasi wanaume wote watatu hapo hapo.
"Hawa tumewakamata njiani wakiwa wanaelekea kuupeleka huu mwili kwa kiongozi wao lakini huu mwili naenda kumpekea raisi Ikulu mimi mwenyewe akaone matunda ya yale mambo ambayo yeye ameshindwa kuyalinda kwa nafasi yake. Max mimi nimejitoa sadaka juu ya hili jambo hata kama nitapoteza maisha ila nataka tushirikiane hii kazi tuimalize haraka sana iwezekanavyo kuanzia muda huu na……." akiwa anaendelea kuongea simu ya Max ilianza kuita kwenye mfuko wake, waliangaliana na mwanamke huyo kisha mwanaume akaipokea kwa tahadhari sana.
"Mwanaume usiyetaka kufa, hongera sana kwa kupata nafasi nyingine ya kuweza kuishi kama mzimu. Nataka uje unionyeshe hicho ulicho nacho kama kweli wewe ni mwanaume"
"Familia yangu iko wapi?"
"Mhhhhh huwa sipendi mtu kunikripia wakati naongea kistaarabu, hilo ni jambo ambalo huwa linanitia hasira sana na ndani ya muda mfupi naweza kubadili maamuzi yangu"
"Kama utaigusa familia yangu kwa namna yoyote ile, niamini mimi nitakufanyia jambo baya ambalo hakuna binadamu aliyapata kuishi akafanikiwa kulishuhudia kwa macho yake"
"Nikiiua muda huu utanifanya nini labda bwana mdogo? Majivuno huwa yanawafanya watu wengi sana kuingia kwenye majuto baadae. Nisikilize kwa umakini kesho usiku hakikisha unafika Arusha Ngarenaro sehemu ambayo inajulikana kama Jengo la 7, hakikisha unakuja mwenyewe kama unahitaji kuiona familia yako kwa mara nyingine. Zingatia maelezo niliyokupa, kuhusu muda utajua mwenyewe ni saa ngapi unafika ila kama ukichelewa basi utavikuta vichwa vya watu unao wapenda vimetundikwa barabaranani na mkeo ni mrembo sana nadhani atanifaa mno kama ukienda kinyume na maelekezo yangu" Ted aliongea maneni ya dharau sana na kuikata simu hiyo akimuacha Max kwenye hasira kali sana ila hakuwa na namna maana mtu huyo alikuwa na familia yake tayari na kama angefanya jambo la kijinga basi alikuwa moja kwa moja anaharibu kazi hivyo alitakiwa kufanya kama vile alivyokuwa ameambiwa.
"Familia yangu inasafirishwa kuelekea Arusha"
"Na anakuhitaji lini?"
"Kesho"
"Safi, hiyo kesho inabidi tuitumie kumaliza mambo yote na kuhakikisha tunaisafisha nchi"
"Ni familia yangu ile mbona unaongea kiwepesi sana"
"Najua kwamba ile ni familia ila kwa muda ambao nimekaa hapa sio kwamba mimi ni fala, kuna taarifa nyingi sana za mhimu ninazo. Nimefanikiwa kuipata kambi ya siri ya Denis Kijazo ambayo ipo huko Morogoro na niliwapenyeza baadhi ya mashushushu huko wamefanikiwa kutega mabomu kuzunguka hilo eneo hivyo wanasubiria amri yangu tu kuweza kuidondosha ila nimesita kwa sababu mle ndani nimegundua kwamba kuna baadhi ya watu ambao hawana hatia akiwepo gavana wa benki kuu wa zamani"
"Una hizi taarifa?"
"Mimi ni mkurugenzi wa shirika la kijasusi la nchi unahisi kuna taarifa nikiitaka naikosa? jibu ni hapana. Mara ya kwanza nilikuwa naishi kama mzimu kwa sababu sikuwa najua kilichokuwa kinaendelea nyuma ya pazia hivyo walikuwa wananichezea kama toi wanavyo jisikia wao lakini baada ya kuligundua hilo nikaamua kuchimba taarifa zote ambazo zilikuwa nyuma ya mgongo wangu na ndipo nilipo anza kuyajua haya yote na ndiyo maana hata hawa makomando nimefanikiwa kuwapata kiwepesi sana"
"Kwahiyo nini kinafuata hapa?"
"Hawa walinzi wako ambao wamefia hapa tutaichukua hii miili na kuihifadhi hospitali na baada ya haya kuisha watazikwa kwa heshima ambayo wanastahili. Wakati haya yanaendelea mimi naenda kuiteka Ikulu halafu wewe utafanya panapo bakia ikiwa ni kuifuata familia yako huko Arusha na kuja kummaliza Denis Kijazo kwa mkono wako mwenyewe maana nina imani kwamba mna mambo yenu binafsi ambayo mnatakiwa kuyakamilisha wenyewe"

76 inafika mwisho.
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 77
"Whaaat? Unataka kuiteka Ikulu?"
"Yes, sijakurupuka kuhusu hili. Kuna watu ambao nimewashawishi pale pale Ikulu baada ya kuwahakikishia kwamba raisi anaenda kufa na kama wakichagua upande wake basi akifa wataishi maisha magumu sana lakini pia nimewaahidi kiasi kikubwa sana cha pesa kazi hii ikiisha kitu ambacho mimi sina ila nitajua cha kufanya tukifika huko"
"Kuhusu pesa usijali zipo za kutosha, lakini hili jambo una uhakika nalo?"
"Mpaka nafanya maamuzi magumu sana namna hii basi ujue nina uhakika na kile ambacho nakifanya hata kama nitayatoa maisha yangu juu ya hili basi sitajutia kabisa kwa sababu nitakuwa nimekufa nikiwapigania wananchi wangu"
"Na Morogoro?"
"Kule ni mpaka kesho usiku, ikiwa imeshindikana kuwaokoa wale watu basi tunapaswa kuiteketeza ile sehemu kwa sababu inatengeneza vitu vingi sana haramu yakiwepo madawa ya kulevya"
"Mimi naondoka na kama Mungu akipenda basi tutaonana tena" mwanaume aliaga kwa njia ya kawaida sana mpaka wote walibaki wanamshangaa.
"Unaenda wapi?"
"Kulipigania taifa langu" mwanaume alikuwa anakaribia getini akiwa anaongea maneno hayo
"Donald" aligeuka baada ya kuitwa na mwanamke huyo.
"Tafadhani naomba urudi ukiwa mzima wa afya" alitabasamu tu baada ya kusikia maneno hayo ya faraja kisha akaingia ndani ya gari ya jeshi na kuondoka nayo akiwaacha watu wa shirika la kijasusi hao wakiwa nyumbani kwake na kwa wakati huo walikuwa wameungana rasmi kuweza kumaliza kazi ambayo ilikuwa imebakia kwenye mikono yao ambapo Max alitakiwa kwenda kuikomboa familia yake kwenye kambi ya kutegemewa ya Denis Kijazo lakini pia ilikuwa na watu hatari mno ambao walikuwa wakiishi huko.
Huku naye mkurugenzi wa shirika la kijasusi la nchi ya Tanzania Chuki Steward akiwa anahitaji kwenda kuiteka Ikulu pamoja na raisi lakini alikuwa anataka kuiteketeza kambi nyingine ndogo ya Denis Kijazoa ambayo ilikuwa huko Morogoro lakini alitaka kusubiri mpaka kesho yake na kama mateka ambao walikuwa ndani isingewezekana kuwaokoa basi kambi hiyo ilikuwa inateketezwa na mabomu ambayo alidai kwamba vijana wake walikuwa wameyasambaza sehemu hiyo.

Wakati mambo yote hayo yanaendelea Denis Kijazo alisafiri usiku ambao alipata taarifa kwamba Dax ameuawa kikatili sana mpaka Morogoro. Mzee huyo hakuonyesha kuwa na amani sana moyoni mwake na alikuwa na wasiwasi mno kwa yale yote ambayo yalikuwa yanatokea kwa wakati huo. Safari yake kwenda huko ilikuwa ni kuonana na gavana wa zamani wa benki kuu ambaye pia alikuwa kama mshauri wake huku akihitajika kutoa ushauri kwa lazima maana ndiyo ilikuwa njia yake ya pekee kabisa kuweza kuiweka familia yake kwenye hali ya usalama.
Baada ya kufika sehemu ambayo ilikuwa na kambi hiyo alisimama nje na kuangalia namna ukijani ulivyokuwa unavutia kutoka hapo alipokuwepo. Misitu ilikuwa imetulia sana huku kwenye sehemu hiyo wakiwepo wanaume ambao walikuwa wanahakikisha ulinzi wa kile kilichokuwa kinaendelea ndani ya jengo ambalo lilikuwa chini ya sehemu hiyo.
Baada ya kutumia muda kidogo akiwa anayaangalia mazingira ya eneo hilo, aliingia moja kwa moja ndani ambapo shughuli za utengenezaji unga na uandaaji wa viungo vya wanadamu ulikuwa unaendelea ndani ya jumba hilo bila kusahau wanyama ambao walikuwa wanauawa na viungo vyao kuandaliwa kwa ajili ya biashara kwenda kwenye masoko makubwa duniani ilikuwa inaendelea kufanyika bila tatizo. Yeye ndiye alikuwa bosi na mwanzilishi wa kila kilichokuwa kinaendelea humo ndani hivyo wakati anapita alikuwa anaangalia kila hatua kwa umakini mkubwa sana na hatimaye alifika sehemu ambayo alikuwa anatarajia kufika.
Kwenye chumba kimoja alikuwa amekaa mzee aliyedhoofu sana kwa hali, mwili wake ulisadiki kwa jinsi alivyokuwa na maisha magumu na hali mbaya sana kwenye chumba hicho ambacho alikuwepo. Alikuwa ameketi kwenye kitanda chake huku amejikumbata na macho kayafumba lakini ghafla aliyafumbua kwa shida sana huku akionekana kama analazimisha konekana kwamba kila kitu ndani ya hilo eneo kilikuwa sawa tu.
"Ni miaka mingi sana, sikumbuki tupo mwaka upi na ni miaka mingapi imepita ila naweza kusema muda mrefu sana umepita bila ya wewe kuja hapa, bila shaka naweza kusema kwamba maisha yalikuwa yanaenda kama ulivyokuwa unataka wewe, leo kimekukuta nini mpaka umekuja mnyonge sana namna hiyo?" alikuwa ni profesa Laurent Mande ambaye alikuwa gavana wa zamani wa benki kuu akiongea kwa sauti iliyo dhoofu sana.
"Yeah upo sahihi kabisa, ni miaka kumi na miwili sasa tangu mara ya mwisho niweze kufika hapa. Naweza kusema ushauri wako ulinisaidia sana ndiyo maana sikuweza kufika tena kwa sababu kila kitu kilikuwa kinaenda kwenye mipango yangu. Mipango ambayo nimefanikiwa kuitengeneza kwa gaharama kubwa sana na bado sipo tayari kuona inapotea kwa sababu ya tamaa za mtu fulani au vikwazo vya mtu fulani ila huwa sipendi kuona kuna binadamu anaingia kwenye njia zangu.
"Kwahiyo kipi kimekuleta? maana najua huwezi hata kunijulia hali kujua kwamba naendeleaje"
"Hiyo siyo kazi yangu kwa sababu uliyataka mwenyewe kuwepo hapa, umekonda sana ndugu yangu sijajua kama unakula sawa sawa ila mtu akikuona namna ulivyo hawezi kukukumbuka kabisa kwamba wewe ndiye ulikuwa mwanaume haswa enzi zako ukiwa na kitambi na kubadilisha magari kama nguo ya ndani leo hii hata tu uwezo wa kunyoa ndevu zako ambazo zimejaa usoni hauna"
"Mimi ni mtu wa kufa tu hivyo sijali sana kuhusu hilo, nambie nini kimekuleta hapa Kijazo maana unaongea kwa kutia huruma sana leo tofauti kabisa na ninavyokujua kwamba wewe ni mtu wa majivuno sana hasa mambo yanapokuwa yanaenda vile unavyotaka wewe"
"Yule bwana mdogo amerudi tena"
"Yupi?"
"Mhhhhh kweli unazeeka vibaya sana lakini nadhani sio kosa lako maana kipindi kile tulimzungumzia Teo na sio yule kijana hivyo unaweza ukawa haumfahamu kweli. Wakati Teo anakufa kuna kijana ambaye alikuwa anamlinda na ndiye ambaye alikuwa anamtegemea sana kwa kipindi kile lakini baada ya kumuua Teo hata kijana yule alipigwa risasi nyingi sana na kwenda kuzikwa lakini jambo la kusikitisha sana baada ya hii miaka kumi na miwili amerudi akiwa mzima wa afya" profesa alikohoa kwa nguvu sana baada ya kusikiliza maneno hayo hali yake ikiwa inamsaliti kabisa.
"Inawezekana vipi mtu azikwe halafu apone?"
"Inaonekana kwamba hakuwa pekeyake, wakati tunashangilia ushindi ule kuna mwenzake mmoja alikuwa hai na wakati anafukiwa alikuwa pale hivyo baada ya kazi ile kuisha alienda na kumfukua mtu wake kisha akatoweka nchini na hivi sasa amerudi na kutaka kulipa kwa kila ambacho kilitokea kwa miaka hiyo kumi na miwili iliyopita"
"Kwa upande wako mbona hilo ni tatizo dogo sana, sijajua kwanini leo unaonekana kuwa na presha sana kiasi hicho" Profesa aliuliza kwa mshangao sana maana hakuona kama kiongozi uyo alikuwa anatakiwa kuwa kwenye hali kama hiyo ambayo kwake linakuwa ni jambo dogo sana hilo.
"Unacho ongea upo sahihi huenda ni kwa sababu nilikuwa sijui nini maana ya hofu kwenye maisha yangu. Nimeishi maisha yangu karibia yote watu wakiniogopa sana ila sikuwahi kuwaogopa wanadamu kwa namna kama hii ambayo mimi ninayo sasa nadhani inaweza kuwa kuna jambo la hatari sana linakuja kwangu. Kila nikikaa nikitaka kuichukulia hii hali kwa ukawaida bado moyo unagoma kabisa, najikuta naanza hadi kuota ndoto mbaya sana za kutisha"
"Kuna kitu gani anacho mpaka unaonekana kumhofia mwanaume ambaye wewe mwenyewe unamuita bwana mdogo?"
"Ana siri zangu zote kwenye mkono wake"
"Kwenye maandishi au kichwani?"
"Zipo kwenye maandishi na zina mihuri kabisa kutoka chanzo kinacho aminika"
"Siamini kama na wewe leo uliacha jambo baya kama hilo lije upande wako"
"Ulikuwa sahihi kuniambia kwamba sio kila mtu anakuwa anafurahishwa na namna unavyokuwa unayafanya mambo fulani lakini kuna muda pia kila unacho kifanya kinaweza kukuletea maadui wengi sana sehemu yoyote ile ambayo unakuwepo na mimi nililisahau sana hilo ila kwa sasa naanza kuamini. Sikuwahi kabisa kuamini kwamba kuna siku vyombo vya usalama vitanipekua mtu kama mimi lakini kuna miongoni mwao ambao walifanya hii kazi bila hata kuogopa na ndio hao ambao wananifanya leo naishi kwa wasiwasi sana kwa sababu kama mtu huyo akiamua kuusambaza ushahidi huo basi dunia nzima itanijua mimi jinsi nilivyo, ulimwengu utanitambua namna nilivyo mshenzi nje ya hili tabasamu langu la uongo na hapo ndipo ambapo pananipa hofu kubwa sana" Denis Kijazo alikuwa anaongea kwa utulivu sana wala usingeamini kwamba aliyekuwa anaongea hapo kweli alikuwa ni yeye mwenyewe ila hakukuwa na namna nyingine kwa sababu ni kweli alikuwa yeye mwenyewe.
"Denis, unajua hata mimi kipindi nakua wakati naishi kwenye maisha ya milo miwili na sio mitatu kama ilivyokuwa kwa wenzetu, nilikuwa na njaa sana ya mafanikio, nilikuwa nina kiu mno ya kuwa miongoni mwa watanzania ambao watakuwa wanaishi maisha bora sana ambayo kila mtu anayaota. Hayo yalinifanya nijitume sana kwenye kila nilicho kifanya, njia yangu ya pekee ya kunifikisha hiyo ndoto zilikuwa mbili, kwanza ilikuwa ni kupitia kujuana na watu au elimu. Kwa bahati mbaya sikuwa najuana na watu ambao wangenifikisha mimi huko hivyo elimu ndilo lilikuwa chaguo langu lililobakia. Nilisoma kama kichaa, nilijituma na kutaka kuwa bora zaidi ya mwanafunzi yeyote yule kitu ambacho nilikifanikisha kwa asilimia miamoja mpaka nikaja kuishia kuwa profesa na gavana wa benki kuu ambapo nilikuja kuzishika sana pesa kama nilivyotaka, nilicheza na pesa sana mpaka ikafika kipindi nikazichoka mwenyewe nikabaki naziangalia tu sina la kufanya maana nilifanya yote ambayo nilikuwa nayaota na sikuwa na cha kufanya tena hapo nikaona kuna umuhimu wa kuwa na familia" mzee huyo alikohoa tena na kuendelea.

77 inafika mwisho.
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 78
"Niliwahi kufanya hayo yote kwa sababu kabla ya kuwa na maisha mazuri kwenye akili yangu niliwahi kuhisi kwamba pesa ndiyo kila kitu kwenye haya maisha, niliwahi kuamini kwamba watu wenye pesa ndio watu ambao wanaishia maisha mazuri kuliko mtu yeyote yule hapa duniani lakini nilikuja kugundua kwamba nilikuwa na mawazo ya kipumbavu sana baada ya kuwa na hizo pesa ambazo nilitaka kuwa nazo na tangu siku hiyo nilijue hilo niliacha kabisa kuhangaika na pesa na hata zile pesa nyingi ambazo nilikuwa nataka niwe nazipata kila siku sikuona umuhimu wake na ndipo nilikuja hata kukukatalia kuweza kuanza kutakatisha pesa za watu. Unajua ni kipi kilinibadilisha Denis?" mzee huyo alitulia tena na kumwangalia Denis Kijazo kwa macho yaliyo choka sana kisha akaendelea;
"Familia, familia ndicho kitu bora zaidi kwenye haya maisha ya mwanadamu. Anayekwambia kwamba pesa inaleta furaha au inanunua furaha basi huyo ni mtu muongo sana au atakuwa hajui nini maana ya neno furaha. Furaha ni nyakati tu ambazo zinakuja na kupotea haijalishi una pesa na hauna, unaweza kuwa na furaha muda huu lakini dakika tano baadae ukawa na huzuni mpaka ukataka kujiua bila kujalisha kama una pesa au hauna kama wewe hapa sasa hivi. Una mabilioni ya pesa lakini hauna raha, si unaamini pesa inakupa furaha sasa kwanini unatia huruma na kuwa mnyonge namna hiyo? Pesa haileti furaha bali inasaidia sana kwenye kutatua matatizo mengi ambayo yanaleta mawazo kichwani na hapo ndipo ambapo watu huwa wanachanganya na furaha. Pesa unapaswa kuwa nayo kwa sababu ina msaada mkubwa sana na zaidi ya asilimia sabini ya maisha ya mwanadamu kutimiza mahitaji yake kunamtaka kwanza atumie pesa hilo hakuna anayebisha ila pesa sio chanzo cha furaha"
"Ukiacha familia nimejifunza kwamba amani ni bora kuliko kuwa na huu utajiri ambao watu wengi wanakuwa wanaulilia kwa sababu kuna wakati ili kuupata huo utajiri kunakulazimu kufanya mambo ya ajabu na ya kutisha sana ambayo yanakuja kukuletea mwisho mbaya ambao hata wewe haukuwahi kabisa kuufikiria kwenye maisha yako na mambo haya hayajawahi kuwa na mwisho mzuri hata siku moja, unaweza ukaishia pabaya na pesa ambazo ulikuwa unazipigia kelele zisikusaidie lolote lile" mzee huyo alitema mate chini kuuweka mdomo wake sawa akiwa anamwangalia Denis Kijazo ambaye alikuwa mbele yake anamsikiliza.
"Umenipa maelezo mengi sana ambayo yamekaa kama unanipa wosia, unamanisha nini?"
"Una chaguo moja tu Denis, ni labda mtu huyo umuue haraka au kama sio hivyo basi wewe ndiye unakwenda kufa na kuteketea vibaya sana"
"Unahisi bwana mdogo kama yule anaweza kuniua?"
"Swali lako linapaswa kuwa kwanini amerudi na kuruhusu wewe ujue kwamba amerudi? kwa sababu alikuwa ana uwezo wa kupotea moja kwa moja maana ulijua ameshakufa hivyo kama amerudi na akataka kujua, maana yake ni kwamba anajua ataanziwa wapi kudili na wewe na atakuja kumalizia wapi kitu ambacho kinakuweka kwenye hatari kubwa sana"
"Hilo nalijua ndiyo maana nimeamua kubeba familia yake na kwenda kuihifadhi mahali ambapo atakuja yeye mwenyewe na huko nadhani napaswa kumuua moja kwa moja japo nilikuwa nina mpango wa kumhifadhi ateseke kwa miaka mingi sana"
"Hivi Denis wewe umewahi kujiuliza kwamba ingekuwaje kama kuna mtu angekuja kuiteka familia yako?"
"Hakuna mtu ambaye anaweza kuja kufanya hilo"
"Wapo ila huenda huwa wanatanguliza utu kwanza kwa sababu wanafamilia wengine wanakuwa hawahusiki kabisa hivyo inaweza kuwa ni kuwaonea tu kuwaingiza kwenye hayo mambo kitu ambacho kinaweza kuwa hatari kubwa sana kama watu ambao unatishia familia zao siku wakiamua kuijia yako"
"Ni kama unanitisha sio?"
"Sipo hapa kukutisha ila nakuona kabisa ukiwa na mwisho mbaya sana. Chaguo ni lako Denis muue mapema au uishie kwenye futi sita kama ulivyo wapeleka wengi na kama unaweza kuvumilia aibu basi kajisalimishe mwenyewe hiyo inaweza kuwa njia ya kujiweka hai tena ili ufungwe tu na usiuawe" Denis Kijazo alicheka sana baada ya mzee huyo kutamka hayo maneno ya kusema kwamba akajisalimishe, alicheka sana huku akiwa anaondoka kisha akasimama baada ya kufika kwenye mlango wa chumba hicho.
"Panapo majaliwa nitakuletea kichwa chake ukae nacho kwa wiki nzima humu ndani, nimejua kwenye ushauri wako ni kipi nikichukue na kipi nisikichukue. Kwaheri profesa" alitabasamu na kutoweka humo ndani.

Max safari yake ilienda kuishia nyumbani kwa James, komando ambaye alipoteza maisha akiwa analipambania taifa lake. Baada ya kufika sehemu hiyo aligonga geti kwa nguvu sana kaisi kwamba mlinzi alifungua kwa hasira sana akiwa na silaha mkononi lakini aliguswa shingoni akatulia na kulazwa pembeni. Mwanaume alitembea akiwa anaangalia mandhari ya eneo hilo na kumsifu sana James licha ya kuishi mbali lakini alihakikisha kwamba familia hiyo inaishi maisha mazuri sana.
Aligonga mlango wa nyumba kubwa na kusogea pembeni ambapo alisikia kwa ndani hatua za mtu zikija mlangoni. Mlango ulifunguliwa na aliyefungua alikuwa ni mwanamke ambaye umri wake alikuwa anaonekana sio chini ya miaka thelathini na mitano mpaka arobaini. Mwanamke huyo baada ya kumuona mtu ambaye hakuwa akimfahamu alishtuka sana na kuangalia getini kwake ambako alishangaa kuona mlinzi yupo chini, alipiga kelele na kutaka kukimbia lakini mwanaume alimdaka na kumuwekea alama ya kidole kwenye mdomo wake kumtaka atulie.
"Mlinzi hajafa, nimemzimisha tu na usipige kelele utamshtua mwanao. Sijaja hapa kwa ubaya na kama ningekuja kufanya hilo basi nigeshakuua muda mrefu tangu unatoka hapa"
"Wewe ni nani?"
"James unamfahamu?"
"Ni mume wangu"
"Mimi ndiye yule mwanaume ambaye aliamua kuishi mbali na familia yake ili aweze kunisaidia"
"Unamaanisha wewe ndiye yule ambaye ulipandishwa kwenye ndege siku ile usiku miaka kumi na mbili iliyopita?"
"Ndiye mimi mwenyewe na niseme tu kwamba asante sana kwa msaada wako mkubwa. Kila siku James amekuwa akiwaongelea sana wewe na mwanae na ni mtu ambaye anawapenda sana isivyo kawaida"
"Mume wangu yuko wapi?"
"Unaniruhusu niingie ndani nikae?" mwanamke huyo hakuwa na namna zaidi ya kumkaribisha ndani mwanaume akaketi kwenye sofa la bei ghali sana.
"Bila shaka huyo ndiye mtoto wenu" Max aliongea akiwa anaiangalia picha kubwa ambayo ilikuwa ukutani.
"Uko sahihi kabisa lakini bado haujanijibu swali langu"
"Mumeo amepoteza maisha usiku wa leo"
"Whaaaaaat?"
"Nasitahili sana kubeba hizi lawama kwa sababu huenda kama sio mimi bado angekuwa hai na angefanikiwa kurudi tena kuishi na nyinyi kama alivyokuwa anatamani siku zote huku akiwa anaota na ndoto kila siku akidai kwamba amewakumbuka sana. Naomba unisamehe sana" maneno hayo yalikuwa yanamtoa machozi mke wa James, mwanamke ambaye alikubali kumpenda mwanaume ambaye alimdanganya hata kazi yake, mwanaume ambaye yeye alikubali kumsubiri kwa miaka yote ambayo alikuwa ametoweka lakini taarifa ya mwisho ilikuja kwamba alikuwa amefariki na hakuwepo tena duniani, kwake yalikuwa zaidi ya maumivu.
"How?" aliuliza akiwa anajifuta machozi na kujikaza ila uso ulikuwa unamsaliti pakubwa sana.
"Kwenye maisha mafupi ambayo tumefahamiana mimi na yeye, tumekuwa zaidi ya ndugu, amekuwa kama kaka kwangu na ni binadamu ambaye pekee aliamini kwamba kupitia mimi nchi hii inaweza kujitoa kwenye udhalimu mkubwa sana ambao unafanyika na viongozi ambao wameamua kujigeuzia nchi hii na kuifanya kuwa yao lakini yeye aliamua kujitoa sadaka na kuiacha familia yake kwa ajili ya kulipambania taifa hili liwe salama. Ameuawa leo na watu ambao walikuwa wanayataka maisha yangu ili niache kila ambacho nilikuwa nakifanya. Kiufupi naweza kusema kwamba amekufa akiwa anaipambania familia yangu kuiokoa kutoka kwa wale watu"
"Naanzia wapi kumwambia mwanangu hizi taarifa? miaka yote hii huwa anauliza baba yake alipo na nilimuahidi kwamba angeweza kurudi lakini inarudi taarifa ya kifo chake. Nitamwambia nini mwanangu mimi?"
"Siku zote maisha huwa yanatupa namna mbaya ya kukumbana na uhalisia unao umiza sana, hatia itaishi kwenye moyo wangu kwa kushindwa kuwalinda watu wangu wa karibu lakini maisha haya haya yananipa funzo kuhusu wanadamu. Maisha yamechagua kuniumiza mimi na watu wangu wa karibu, maisha yamenichagulia njia mbaya sana ambayo natakiwa kukumbana nayo hata bila kupenda wala kutaka na maisha yananitaka mimi niwe hivyo. Maisha yananipa tafsiri mbaya sana kuhusu hatima nzima ya maisha yangu, natamani niseme neno lakini najikuta najichukia sana mimi mwenyewe. Kuna kosa kubwa sana niliwahi kulifanya huko nyuma kwa sababu ya mapenzi ndiyo sababu kubwa ya haya yote kuendelea kutokea kwani kama sio hivyo hili jambo lingeisha mapema sana. Nimempoteza kila ambaye alikuwa upande wangu na nilicho bakiwa nacho ni familia tu ambayo nayo ipo mikononi mwa hao watu, mimi sina cha kukifanya kumrudisha mumeo lakini nakuahidi kwamba watu ambao wamehusika na hili muda kama huu kesho zitavuma habari kila pembe ya dunia kwamba wamekufa vibaya sana"

78 inafika mwisho.
 
Good evening fellas. Nimepotea kama siku mbili nikiwa kupigania tumbo ila kama kawaida nilisema nikipotea nafidia hivyo leo nitaweka episodes tano.

NB
Acheni mambo yenu nunueni simulizi, mnatukata maini waandishi kuendelea kuandika [emoji28]
Uzi mapya contribution will be done for you our boss
 
Nouma
 
Hii hadithi naona kama yatamatika karibuni 🤔
 
Nimegundua humu jf watunzi hawapendi kuleta mzigo siku za mapumziko (weekends na sikukuu). Hupenda kuleta mzigo kipindi cha hekaheka (jumatatu hadi ijumaa)
CC

FEBIANI BABUYA
singanojr
 
Nimegundua humu jf watunzi hawapendi kuleta mzigo siku za mapumziko (weekends na sikukuu). Hupenda kuleta mzigo kipindi cha hekaheka (jumatatu hadi ijumaa)
CC

FEBIANI BABUYA
singanojr
Siku za weekend na sikukuu wanazitumia kama muda wa kuandika simulizi maana hata wao wana majukumu siku zote za kazi kama sisi.
 
Back
Top Bottom