Simulizi ya kipelelezi: Jiji la kamari (gambling city)

Simulizi ya kipelelezi: Jiji la kamari (gambling city)

HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 30
Ilichukua mwezi mmoja tu wanaume hao wakafanikiwa kurudi na majibu. Baada ya mheshimiwa raisi kupata majibu yote alichukizwa sana na jambo hilo kwa sababu wale watu ambao walikuwa wanajulikana kama magaidi, ni kweli walikuwa wao lakini jambo hilo walikuwa wamelifanikisha kwa msaada mkubwa sana wa baadhi ya viongozi wakubwa ndani ya nchi ya Tanzania ambao walifanya hivyo kwa maslahi ya kulipwa pesa nyingi sana na nyuma ya watu hao yalikuwepo mataifa ya Kenya na Uganda.

Kupitia hilo jambo raisi alikata kabisa mahusiano ya kidiplomasia dhidi ya mataifa hayo mawili kimya kimya lakini wale wote ambao walikuwa wamehusika walikamatwa na kuweza kunyongwa hadharani kila mtu akiwa anaona. Miongoni mwa watu ambao walikuwepo kwenye huo usaliti alikuwa ni waziri mkuu wa taifa la Tanzania wa wakati huo Benard Mango.

Jambo hilo lilimpa taa nyekundu raisi huyo kwa kujua na kuamini kwamba nchi yake haikuwa salama kutoka nje lakini kutoka ndani ya nchi pia hivyo akaamua kulirasimisha shirika hilo ambapo walianza kuchukuliwa vijana wenye uwezo mkubwa na kwenda kupewa mafunzo kwa siri sana ndani ya nchi kubwa duniani ili kuhakikisha taifa linakuwa salama kwa wakati wote. Hakuna kiongozi ambaye alikuwa anateuliwa au kupewa nafasi kubwa bila kufanyiwa uchunguzi wa kina kuhakikisha kama alikuwa msafi au alikuwa mchafu kama wenzake tu wa mwanzo na huo ndio ukawa mwanzo rasmi wa kulitengeneza shirika hilo la kijasusi la WTIS ambalo kila kulivyo itwa leo lilikuwa linashika mizizi na kuendelea kuwa imara sana mpaka baadae wananchi walianza kupata habari juu ya shirika hilo na mataifa mengine yalianza kuliogopa sana taifa la Tanzania huku Kenya na Uganda wakiwa wanaomba sana msamaha kwa kile ambacho kilitokea ili waweze kuimarisha mahusiano yao maana walikuwa karibu na walikuwa wanatakiwa kusaidiana kwa kila jambo. Raisi wa Tanzania aliwaambia watu hao kama walikuwa wanahitaji uhusiano huo basi walitakiwa kulipa mali nyingi sana kama malipo ya unyama ambao walifanya na kama wangegoma kufanya hivyo alitishia kuwafanyia kitu kibaya sana lakini pia angewapeleka umoja wa mataifa ili wakalipe kwa ukatili wao.

Hawakuwa na naman zaidi ya kuweza kufanya hivyo ambapo mataifa hayo yalirudisha mahusiano yao kama ilivyokuwa mwanzo kwa makubaliano ya kutoweza kuingiliana kiutendaji. Shirika hilo liliendelea kukua kwa kasi sana kutokana na usimamizi mzuri wa raisi na ukaribu wake mkubwa na swahiba wake ambaye ndiye alikuwa mkurugenzi wa shirika hilo pia hara mkuu wa majeshi ambapo ilisaidia kuwepo kwa ushirikiano mkubwa sana kati ya shirika hilo na jeshi la nchi.

Mambo yalikuwa mazuri sana mpaka ilipopita miaka thelathini tangu raisi huyo awe raisi, aliweza kujiudhulu na kumteua mkurugenzi wa shirika hilo kuwa raisi wa nchi kwani alikuwa akimuamini sana mtu huyo na aliamini kwamba angeweza kuliongoza taifa kwa weledi kwa sababu mifumo ya ulinzi alikuwa anaijua vizuri sana hivyo alimuamini kwamba angefanikiwa kuliimarisha sana shirika hilo. Kiongozi huyo ambaye alikuwa raisi mwenyewe lakini pia alikuwa mkurugenzi wa shirika hilo mwenyewe, alitengeneza shirika la kijasusi la kutisha sana ambalo lilikuwa linayafanya mataifa mengine kuiogopa sana Tanzania. Shirika hilo lilikuwa linatisha kila sehemu kiasi kwamba hata wananchi walikuwa wanaogopa sana kulitaja hadharani maana hawakuwa wakijua kwa undani hasa kwamba shirika hilo lilikuwa linajihusisha na nini zaidi ya kuamini kwamba kazi yake kubwa ilikuwa ni kufanya mauaji ya kutisha.

Miaka kumi baadae ndipo shirika hilo lilipoanza kupoteza ladha yake baada ya mtu huyo kuweza kutoka madarakani huku aliyekuwa raisi wa kwanza wa Tanzania akipoteza maisha kwa matatizo ya moyo. Kutoka kwake kwenye hiyo nafasi kuliwapa watu wengine kuliongoza, watu ambao walikuwa wanadaiwa walikuwa wanayatetea zaidi maslahi yao kuliko maslahi ya nchi na mwanaume huyo alipo jaribu kuwaingilia walimuua kwani waliamini yeye ndiye ambaye alikuwa analiharibu shirika hilo.

Ilipokuwa inaanza miaka ya 1990 uliandaliwa mpango wa kuweza kuwatafuta vijana ambao wangekuja kuwa majasusi wakubwa sana kwa maslahi ya taifa hapo baadae ili kuweza kulirudisha shirika hilo kwenye ubora wake kama ilivyokuwa mwanzo, walikuwa wanachukuliwa vijana wenye uwezo mkubwa kutoka sehemu mbalimbali nchini hususani mavyuoni, jeshini, mtaani na hata kwenye taasisi zingine kubwa za kiserikali na zisizo za kiserikali. Huo ndio ulikuwa mwanzo wa kukipata kizazi cha sasa cha mashushushu na majasusi ambao ndio walikuwa wanaliongoza taifa wakiwa nyuma ya mkurugenzi Philipo Tibaigana.

Hiyo ni historia fupi la shirika la kijasusi la nchi ya Tanzania ambayo raisi Teodensia Mpanzi alikuwa anaipitia baada ya kumuagiza mkurugenzi aweze kumpatia. Aliisoma kwa umakini mno lakini hakuwa na uhakika kama hizo zilikuwa ni taarifa zote licha ya kusoma ufupisho wake maana maelezo mengi yalikuwa kwenye kutabu ambacho kilikuwa pembeni yake. Alikuwa anahisi kwamba huenda kuna taarifa zilikuwa zinakosekana na hakuona sababu ya msingi ya kiongozi yule ambaye alisaidia kwa kiasi kikubwa kuweza kuliimarisha shirika hilo kuweza kuuawa, hata hivyo alifurahi sana kuweza kuisoma japo kwa uchache historia ya shirika hilo ambalo ilikuwa ni taasisi nyeti sana ya serikali.

Akiwa anayatafakari ambayo alikuwa ameyasoma, simu yake binafsi ilikuwa inaita na wakati huo alikuwa ndani ya chumba chake cha kulala. Aliiangalia simu hiyo kwa umakini sana na kuogopa kuipokea maana hizo namba binafsi mara nyingi alikuwa anapigiwa na Francis Mboye pale ambapo alikuwa anataka kuwasiliana naye kwa siri au kumpa maagizo ya mhimu lakini mzee huyo alikuwa amekufa sasa ni nani mwingine ambaye alikuwa anamtafuta huyo? aliiacha simu hiyo ikaita mpaka ikajikata yenyewe. Haikuchukua hata sekunde simu hiyo ikaanza kuita tena, kwa wasiwasi aliinyanyua akajikaza na kuipokea.

“Mheshimiwa heshima yako!” ilisikika sauti nzito sana kutoka upande wa pili
“Nani wewe unaongea?”

“Mkuu sidhani kama inatakiwa tutambulishane kwa simu maana huwa siziamini sana simu hata kama zikiwa na ulinzi mkubwa sana kiasi gani”

“Unahitaji nini?”
“Nataka kukutana na wewe”

“Umewahi kuona raisi anakutana kutana na watu ambao hawajulikani?”
“Hata mimi sitaki kufanya haya ila ni kwa heshima tu ya mzee ndiyo maana sina namna zaidi ya kufanya hivi”

“unamaanisha nini?”
“Nadhani unamkumbuka Francis Mboye?”
“Ndiyo”

“Hakuna mtu ambaye alikwambia kwamba unatakiwa kukutana naye baada ya yeye kufa?”
“Unataka kuniambia wewe ndiye Bilali?”

“Mheshimiwa usipende sana kutumia majina halisi kwenye simu ni hatari sana kwa sababu mpaka sasa upo kwenye hatari kubwa sana ya kuuawa hivyo haitakuwa vyema kama nitakukumbusha kwa mara nyingine”

“Nakupata wapi?”
“Unadhani ni sahihi kukutana muda huu?”

“Ndiyo, nilikuwa naisubiri sana simu yako kwa sababu muda unavyozidi kwenda ndivyo mambo yanavyozidi kuharibika zaidi kwahiyo unaweza ukanielekeza kwamba ni wapi ambako naweza kukupata na mimi nikaja huko”
“Umewaza kuhusu usalama wako?”

“Ndiyo, nakuja na mlinzi wangu mmoja ambaye ni miongoni mwa wachache sana ambao mimi nawaamini”
“Kuwa makini sana na hao watu ambao unawaamini”
“Usijali, nambie nakukuta wapi?”

“Njoo ndani ya kituo cha mwendokasi hapa posta ya zamani”
“Si walinzi watakuona hapo?”
“Mpaka nakwambia uje hapa ni kwamba nina uhakika na usalama wa eneo hilo kwa ajili ya maisha yako”

“Nipe nusu saa nakuja” raisi aliikata simu yake akiwa na tumaini jingine jipya kwenye nafsi yake kwa sababu huyo ni mtu ambaye aliachiwa na Francis Mboye na aliamini kwamba akimpata na akawa upande wake basi alikuwa na nafasi kubwa sana ya kupiga hatua kubwa sana kwenye huo mpango ambao alikuwa anaushughulikia. Simu yake aliipiga kwa Brandina ambaye siku hiyo alikuwa amepewa majukumu hapo Ikulu hivyo hakuondoka na ndiyo sababu raisi alisema kwamba anaenda na mtu ambaye alikuwa anamuamini sana.

Alimpa taarifa Brandina kwamba waondoke hapo Ikulu kwa siri sana huku Brandina akidai kwa walinzi kwamba alikuwa amepewa kazi ya kufanya na mhehsimiwa raisi na kwa sababu alikuwa ndiye mlinzi mkuu wa mheshimiwa hakukuwa na mtu wa kumuuliza maswali mengi lakini hakuna ambaye alijua kwamba kwenye hiyo gari ambayo alitoka nayo alikuwa amembeba mheshimiwa raisi wa nchi ya Tanzania.

Ndani ya muda mfupi tu walikuwa wamefika ndani ya eneo hilo kwa sababu hapakuwa mbali sana na Ikulu ilipokuwepo. Milango ya kuingilia sehemu hiyo ilikuwa wazi kabisa kama kawaida, alimtaka Brandina kubaki nje ya kituo hicho cha mwendokasi japo mwanamke huyo alisisitiza sana kwenda naye maana ilikuwa hatari sana kiongozi kama huyo kuwa mwenyewe hususani kwenye mazingira yasiyo rasmi lakini raisi huyo alisisitiza kwamba alikuwa na uhakika na kile ambacho alikuwa anakifanya hata mwanamke huyo hakutakiwa kuwa na wasiwasi kabisa.

Aliingia taratibu ndani ya kituo hicho ambapo ndani kulikuwa na taa ambazo zilikuwa zinawaka mwanga hafifu kiasi kwamba kama mtu angekuwa mbali na eneo hilo asingeweza kumtambua mtu ambaye alikuwa ndani ya kituo hicho. Teo baada ya kufika ndani, kwa mbali ulipokuwa upo mlango wa kutokea upande wa pili alikuwa amesimama mwanaume mmoja akiwa ndani ya suti huku akiwa amempa mgongo.

30 inafika mwisho.

Tchao
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 31
Alitembea taratibu kuelekea alipokuwa mwanaume huyo ambaye hakuonekana kuwa na wasiwasi juu ya ujio wa mgeni wake ambaye alikuwa tayari amefika. Raisi baada ya kufika karibu kabisa na alipokuwa amesimama mwanaume huyo aliuliza swali.
“Wewe ndiye Bilali?”

“Yes” mwanaume huyo alijibu huku akiwa anageuka alipokuwepo raisi huyo. Raisi alicho kiona mbele yake alihisi anaota, alihisi hakuwa yeye bali ilikuwa ni ndoto yake tu, raisi huyo alijikuta anaanza kutetemeka na ilibakia kidogo tu aweze kudondoka chini lakini mwanaume huyo alimkimbilia na kumdaka kisha akamsimamisha vizuri lakini hata hivyo raisi hakuwa na nguvu za kuendelea kusimama bali aliketi kwenye moja ya benchi ambazo walikuwa wanazitumia abiria ndani ya kituo hicho.

“Piusi?”
“Yeah, ndiye mimi Piusi”
“Hapana hili jambo sio kweli”
“Kama hauwezi kuamini kile ambacho unaambiwa basi yaamini sana macho yako”

“Ulikufa wewe”
“Uliambiwa hivyo lakini sidhani kama ulifanikiwa hata kuuona mwili wangu”
“How?”

“Dunia inatisha sana mheshimiwa ndiyo maana watu ambao wanaishi vizuri ni wale ambao wameamua nao kuwa watu wa kutisha hivyo kila kitu kwao wanakiona kama kitu cha kawaida sana. Mimi sijawahi kufa na wala hakutokea mtu miaka yote ambayo nimeishi kutaka kuniua kwa sababu hakuna mtu hata mmoja ambaye alikuwa ananifahamu huko nje”
“Inamaanisha kuja kwangu ulikuwa umetumwa kwa ajili ya kazi?”

“Ndiyo maana nipo hapa”
“Hahahaha hahahaha, hapana kwahiyo ulikuja kucheza na hisia zangu halafu ukamsingizia Denis Kijazo kwamba amekuua? Nini hasa lilikuwa lengo lako?”

“Ni kwa sababu ya kazi. Ni miaka kumi sasa imepita wewe ukiwa unajua kwamba nimekufa na ulisha nisahau kabisa, hiyo inatupa funzo kwamba duniani hatutakiwi kuishi kwa kuwafurahisha watu kwani ni suala la muda mfupi sana kukusahau na kukufuta kwenye kumbukumbu zao za maisha”

“Hivi uliwahi hata kunipenda labda?”
“Yeah niliwahi kukupenda lakini kwa bahati mbaya sana kazi yangu inanitaka kuwa na moyo wa chuma, sitakiwi kabisa kumpenda mtu kiasi kwamba nikasahau kazi. Nilikupenda japo nilikuja kwako kwa kazi maalumu kwa sababu ulikuwa ni mwanamke pekee ambaye uliweza kuzielewa hisia zangu mapema sana hivyo ukazibeba kwa ukumbwa ule ambao hakuna mwanamke aliwahi kunifanyia kabla”

“Unategemea baada ya hili mimi naweza kukuamini tena? Unafikiri kwamba mimi naweza nikafanya na wewe kazi tena? Ni miaka kumi umenidanganya Bilali, miaka kumi najua mwanaume ambaye nilikuwa nampenda sana alikuwa amekufa halafu kumbe upo hai na mzima wa afya kabisa?”

“Kama ungekuwa kwenye nafasi yangu, nadhani ungeelewa kwamba ni kwa namna gani maisha yetu sisi tunaishi kwa kubahatisha kama ndege ambapo unakuwa haujui kwamba kesho yako unaweza ukaamka ukiwa hai au umekufa maana ndege muda wote naye huwa anawindwa na manati, bila kujua adui yake yuko wapi na manati yake muda wowote anaweza kujikuta anauawa. Hayo ndiyo maisha yangu mimi, maisha ya kutolala usingizi kuhakikisha taifa linakuwa salama lakini nimezoea sasa licha ya kujitoa kwa kila kitu kwa ajili ya haya bado muda wote huwa napokea lawama na matusi huku wananchi wengine wakiwa wanadai uwepo wetu ni upotezaji wa kodi zao tu”

“Wewe ni nani Bilali?”
“Kama ulifanikiwa kumjua bosi wangu unashindwa vipi kujua mimi ni nani?”
“Yule alikuwa bosi wako, nataka kujua kwamba wewe ni nani?”
“Komando”
“Whaaaat?”

“Yes, mimi ndiye kiongozi wa kundi hatari ambalo uliambiwa linaitwa DRAGON BOYS, tupo watatu tu lakini ni zaidi ya jeshi zima la makamanda mlio nao huko”

“Hapana bado sikuamini” mwanaume hakuongea sana, alivua koti la suti na shati yake na mwili ambao ulikuwa umegawanyika kwa mazoeazi makali, ulikuwa unaonekana vyema sana. Aliunyanyua mkono wake wa kulia akisogea alipokuwepo raisi huyo ni kweli kama alivyokuwa amepewa maagizo na Francis Mboye kwamba kama atakuwa na wasiwasi na kijana huyo basi amwangalie chini ya kwapa ataiona alama ya Dragon na kweli aliiona alama hiyo kwa usahihi sana.

“Wenzako wako wapi?”
“Nipo nao hapa hapa” mheshimiwa aliangaza lakini hakuona kitu, mwanaume alinyoosha kidole chake mkono wa kulia nje, alionekana mwanaume mmoja ambaye alikuwa kwenye mavazi machafu akiwa amelalia makopo kana kwamba hakuwa na makazi na maisha yake yalikuwa ya kutegemea kuokota makopo. Lakini pia alinyoosha mkono wake wa kushoto karibu na ulipokuwa ukuta wa kutenganisha barabara iliyokuwa inaenda Feri na bahari na hapo alimuona mwanaume mwingine akiwa amelala kwa kujibanza kwenye ukuta huo na bila kuwa makini ilikuwa ni ngumu sana kuona kama kuna mtu hapo.

“Una lipi la kuniambia Bilali?”
“Tuna mambo mengi sana ya kuzungumza mimi na wewe ila kwa leo sio muda wake”
“Unamaanisha?”
“Leo nilitaka tukutane kwanza kwa sababu nilijua utapata mshtuko mkubwa sana kuniona mimi hivyo tutatafuta siku nzuri ya kuweza kuongea ila hakikisha unaongea na kijana wako nakutana naye”

“Max?”
“Ndiye huyo, huyu ndiye ambaye tunamtegemea zaidi kwenye hii kazi, sisi wote mimi, wewe na wenzangu tuna asilimia nyinyi sana za kufa lakini huyu bwana mdogo inabidi tuhakikishe anakuwa hai”

“Kwanini unaamini kwamba tutakufa?”
“Kwa sababu ipo hivyo mheshimiwa”
“Mtakutanaje?”

“Mpe maagizo ya kesho kwenda Kariakoo usiku kwenye kazi yoyote ile mimi nitakuwa kule hivyo nitakutana naye”
“Unahisi atakujua?”

“Watu wa aina yetu huwa kuna namna ya kutambulishana hivyo usijali kuhusu hilo. Katulie kisha ukiwa sawa mimi na wewe tutaongea vizuri ila kaa mbali na mkurugenzi wa usalama wa taifa kabla haujachelewa” mwanaume aliongea na kuanza kuondoka kama masihara ndani ya eneo hilo
.
“Bilali” aligeuka baada ya kuitwa
“Unanipenda?” alitikisa kichwa masikitiko sana.
“Bado sijui” alijibu na kuishia upande wa pili kisha umeme ukakata ndani ya eneo hilo, Brandina alikimbilia ndani kumuwahi mheshimiwa raisi maana umeme kukatika ghafla ilikuwa ni ishara mbaya sana lakini alimkuta kiongozi huyo akiwa salama kabisa ameketi kwenye benchi. Baada ya dakika mbili umeme ulirudi eneo lote kukiwa hakuna kitu wala mtu yeyote yule.

“Mheshimiwa una uhakika kuna usalama hili eneo”
“Ndiyo Brandina ni kwa sababu ya usingizi tu, turudi nikalale maana nimechoka sana” hakukuwa na cha kusubiri ilibidi tena warudi Ikulu haraka na kwa siri kubwa mno mheshimiwa akiwa na mawazo mengi sana kwenye kichwa chake maana alikuwa anahisi kama yaliyotokea kule yalikuwa ndoto na haikuwa kweli ila hakuwa na uwezo wa kubadili ukweli kuwa uongo hivyo alitakiwa kuwa mpole tu.

Brandina muda wote ambao alikuwa pale alijitahidi sana kuweza kufuatilia kujua ni kipi ambacho kilitokea na kupata jibu kwamba raisi alikuwa anakutana na nani lakini hakuna alicho ambulia maana alihisi kama aliona raisi anaongea na mtu ila hakujua ni nani na umeme ulipo katika baada ya kwenda pale hakukuta mtu yeyote hivyo akawa amepigwa za uso.

NGARENARO, ARUSHA
Wilaya ya Arusha mjini, inapopatikana Ngarenaro ya chini, eneo ambalo walikuwa wanaishi wanaume wahuni sana na makundi ya wahuni wa mitaani. Ni eneo ambalo wale watoto wa mama halikuwa likiwafaa kwa ajili ya kuishi kutokana na asili ya maisha ambayo yalikuwa huko, walikuwa wanaishi wanaume ambao kwao kulalamika ilikuwa dhambi kubwa sana, kila mtu aliamini kwamba maisha yake lilikuwa ni jukumu lake hivyo hata kuishi wao ndio walikuwa wanatakiwa kujua namna gani wanaweza kuishi na kuyamudu maisha yao kimpango wao wenyewe.

Ilikuwa ni kama sehemu tofauti kabisa ndani ya nchi kwani walikuwa wanajiongoza wenyewe na hata maisha ambayo walikuwa wanayaishi yalikuwa ni tofauti sana na watu wengine. Ndani ya sehemu hiyo pia kulikuwa na viwanda vya siri sana ambavyo vilikuwa vinajihusisha na uandaaji wa pombe kali za kiharamu na za asili ambazo kwa mtu ambaye alikuwa ni mgeni nazo kama angefanikiwa kuzinywa basi maisha yake yangekuwa kwenye mstari wa hatari sana na kama angecheza vibaya basi alikuwa anapoteza maisha yake.

Eneo hilo licha ya kuwa na wahuni sana kila mtaa lakini miaka kadhaa ambayo ilikuwa imepita walipata uvamizi mkali sana, uvamizi wa watu ambao hawakujulikana kwamba walitokea wapi, uvamizi ambao waliingia watu ambao hawakuwa wahuni bali wao walikuwa ni wauaji wa kutisha sana. Wakati wanaume hao wanaingia kulikuwa kuna tetesi za chini chini kwamba ndani ya eneo hilo kwenye moja ya kiwanda cha pombe kali kulikuwa na makazi ya watu ambao hawakuwa wanajulikana kwamba walitokea wapi.

31 inafika mwisho.

Tchao
 
Njoo na 2000 yako tu umalizie mpaka mwishi 88.

0621567672 (WhatsApp).... HALO-PESA

0745982347....M-PESA

0714581046...TIGO-PESA

FEBIANI BABUYA zote.
 
Very attractive
 
Once again tunakutana kwenye mchezo bora huu hapa. Tukapate kumsoma secret agent mmoja ambaye alikuwa assigned kuwa mlinzi wa raisi.

Lakini baadae anagundua kwamba mfumo hauko sawa na yeye ndiye alikuwa amechaguliwa na watu wasio julikana kwa ajili ya kuufuta huo mfumo. Anakuja kushtuka wakati yeye mwenyewe yupo ndani ya mfumo tayari hivyo anakuwa hana namna zaidi ya kudili na watu ambao hakuwa akiwajua na nyuma yao kulikuwa na mambo mazito sana.

Max (jina la kazi) huku jina lake halisi akijulikana kama DONALD DANIEL (DONNY) code no 001. Anaanza kuyafunua yale ambayo alipewa kazi kuyafanya ndipo anagundua kwamba kuna mlima mzito sana wa kuupanda lakini wakati anaanza kuyajua hayo mazito anakutana na jambo baya sana.

Ananasa kwenye HONEY TRAP na kuunguza mchezo mzima hali ambayo inamfanya kuishia kwenye umauti huku akishuhudia raisi ambaye ndiye alitakiwa kumlinda na raisi huyo ndiye alimpa kazi ya kuufuta huo mfumo akiwa anauawa ndani ya ofisi yake.

Muuaji anamuua raisi huku 001 akiwa ma risasi 6 mwilini hana cha kufanya hivyo yeye ndiye anauziwa kesi kwa kuhusika na mauaji ya raisi wa nchi, rasmi anavishwa taji la ugaidi huku ikionekana kwamba ameuliwa akiwa kahusika na mauaji ya raisi wake tena akiwa ndiye mlinzi mkuu wa raisi huyo.

Mwanaume huyo baada ya raisi kufa naye akiwa ana risasi sita kwenye mwili wake, anabebwa na kwenda kuzikwa akiwa bado hai hajakata roho.

001 anafukiwa na kushindiliwa ndani ya shimo la futi sita porini huku mvua ikiwa inausindikiza umauti wake na jina lake linafutwa kwenye idadi ya watu ambao waliwahi kuishi.

Lakini jambo la kutisha zaidi ni kwamba mwanaume huyo ambaye dunia iliamini kwamba alipatwa na umauti na ilithibitishwa kwamba ni gaidi ambaye aliuawa baada ya kumuua raisi akitaka kushambulia na watu wengine, alikuja kuonekana akiwa hai baada ya miaka kumi na mbili kupita.

Sasa alikufaje halafu akaja kuonekana tena akiwa hai miaka kumi na miwili baadae? Baada ya yeye kuonekana ni kipi kilitokea kwa watu wake ambao alifeli kuwafuta na mfumo wao kwa ujumla? Binafsi majibu yote nimekuandalia ndani ya hili andiko bora sana.

Ni muda wako ndio utakufanya uyapate majibu sahihi kwenye moja kati ya simulizi bora sana ya mapigano ya hali ya juu na ya kutisha muda mwingine bila kusahau stori iliyo pangiliwa unono kabisa.

Kwenye kalamu nimesimama mwenyewe Febiani Babuya wengine wapenda kuniita Bux the storyteller.

Here we go [emoji116]View attachment 2891932
Good
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 32
Ndani ya kiwanda hicho hakuna raia hata mmoja ambaye alikuwa anaruhusiwa kucheza karibu au kusogelea kwenye kiwanda hicho ambacho muda wote ungeona pako kimya sana na kama geti kufunguliwa basi ungeona linafunguliwa wakati gari zinatoka humo ndani kwenda kusambaza pombe na wakati mwingine ungeona gari za kifahari sana zinaingia hapo lakini hakuna ambaye aliwahi kujua kwamba kwenye hilo eneo ni nini kilitokea na ni kipi kilikuwa kinaendelea.

Kabla ya ujio wa watu hao hilo eneo lilikuwa linamilikiwa na mwanamke mmoja ambaye alikuwa anajulikana kama mama tengeru, Tengeru likiwa ni jina la mwanae ambaye aliuawa baada ya kukamatwa akiwa anavunja kwenye moja ya duka la mtu tajiri sana. Lakini tangu watu hao wamefika ndani ya hilo eneo mama huyo na familia yake hawakuwahi kuonekana tena huku wengine wakiwa wanadai kwamba mama huyo aliuawa na watu hao wakajenga upya ndani ya eneo hilo japo yalikuwa ni maneno ya vilingeni tu ambayo hakuna mtu hata mmoja alikuwa anaweza kuyathibitisha.

JENGO LA 7
Ndilo lilikuwa jina maarufu sana la kiwanda hicho, kiwanda ambacho kilikuwa kinajulikana na wahuni karibia wote kwa sababu walikuwa wanaipenda sana pombe ambayo ilikuwa inatengenezwa hapo lakini hawakuwahi kumjua mmiliki wa hilo eneo wala kujua watu ambao walikuwa wanatengeneza hiyo pombe yenyewe na kwa sababu waliwahi kupigwa marufuku mara kadhaa baada ya kuhitaji kujaribu kukiripoti kiwanda hicho kwa kudai kwamba inawezekana watu hao waliwahi kumuua aliyekuwa mmiliki wa hilo eneo lakini kila ambaye alijaribu kufanya hivyo alikuwa anauawa hali ambayo iliwafanya watu wa eneo hilo kuamua kuishi maisha yao ya kawaida tu kuliko kujiingiza kwenye hiyo hatari kubwa.

Majira ya usiku vijana kumi ambao walikuwa wamejipanga vya kutosha wakiwa na silaha kwenye mikono yao walijua kabisa kwamba ndani ya hilo eneo lazima kulikuwa na mali za kutosha hivyo hawakuwa tayari kabisa kuendelea kuhangaika mtaani wakati wanajua kwamba kuna watu ambao walikuwa na mali nyingi kabisa tena wakiwa ndani ya eneo ambao wao walikuwa wana uwezo wa kufika kwa muda mfupi tu hivyo wakawa wamedhamiria kujichukulia maamuzi mkononi kuweze kusogelea hilo eneo.

Walinyata mpaka kwenye kuta za kiwanda hicho na kudandia juu kwa kubebana mpaka pale ambapo wote waliingia ndani ya jengo hilo. Baada ya kuingia walikutana na korido ndefu ambapo hakukuwa na mlango wala kiashiria cha dirisha la kuingilia ndani ya majumba na magodauni ambayo yalikuwa ndani hivyo hali hiyo ikawafanya kuifuata tu hiyo korido mpaka kule ambako ingewapeleka muda huo. Walikuja kutokezea kwenye uwanja ambao kama wangefanikiwa kuuvuka moja kwa moja walikuwa wanaingia ndani, ila kila mmoja wao alishtuka sana baada ya kuona lango liko wazi, halafu kukiwa kimya vile vile.

Walianza kujishauri kwamba nani aanze kuingia lakini mwanaume mmoja alijikaza na kuweza kusogeza kichwa chake kutaka kuingia kwenye hilo lango ambalo ndani yake kulikuwa na kiza kinene sana lakini baada tu ya kuingiza kichwa chake ndani alirudi nyuma akiwa anayumba yumba tena bila hata kupiga kelele. Wenzake walimshangaa ila alipogeuka kila mtu alijikuta anapiga makekele kwa hofu kubwa sana maana mtu huyo alikuwa amepigwa shoka la kwenye paji la uso na habari yake ilikuwa imeishia hapo.

Wanaume hao tisa ambao walikuwa wamebakia ni kama walichanganyikiwa kila mtu akiwa anapiga makelele kwa hofu kubwa kiasi kwamba wakaanza kukimbia na kurudi kule ambako walikuwa wametokea ila kwa bahati mbaya sana pale kwenye korido ambapo walipita mara ya kwanza vizuri walikutana na geti la chuma likiwa limejifunga hali ambayo iliwafanya kuanza kutetemeka na kuamua kurusha risasi hovyo hovyo bila mpango.

Umeme ulizimika kila sehemu ghafla sana vikawa vinasikika vilio tu pekee ndani ya eneo hilo na umeme uliporudi mwanaume mmoja alishangaa kujikuta yupo pekeyake na wenzake wote walikuwa wameuawa kwa kukatwa katwa na shoka vibaya sana. Aligeuka kila upande akiwa analia na kutoa sauti ya kuachwa hai lakini hakuwa hata anamuona huyo mtu ambaye yeye alikuwa akimuomba msamaha.

“Nani amewatuma hapa?” ilikuwa ni sauti nzito sana ya mtu ambaye alikuwa nyuma yake na kwa mahesabu yake ni kwamba huyo mtu alikuwa juu ya ukuta maana hakukuwa na namna kwamba mtu huyo alitokea tu nyuma yake bila sababu ya msingi.

“Wewe na,, nani?” aliulizwa swali lakini naye alijikuta anauliza huku mwili wake ukiwa unamsaliti na hata silaha ambayo alikuwa nayo kwenye mkono wake ilikuwa inamsaliti kwa namna alivyokuwa anatetemka.

“Umevamia kwenye makazi ya watu na bado unataka kuwajua hao watu ni akina nani?” mwanaume huyo alikuwa akimsogelea huku akiwa analizungusha shoka lake kwa nguvu sana mkononi.

“Nitakupiga risasi kaa mbali na mimi” alifoka na kurudi nyuma lakini hakuwa na kwakwenda maana geti lilikuwa limefungwa, wakati anataka kukaa vizuri aliukanyaga mwili wa mwenzake ambaye alikatwa vibaya mno kwenye shingo, hali ambayo ilimfanya kupiga makelele sana na kudondoka chini, alitaka kunyanyuka ghafla ila kwa bahati mbaya sana adui yake ni kama alimpania mno kwani mkono wake ulipitishiwa shoka na kwenda chini. Alilia kama mtoto mdogo huku akiwa anagala gala chini.

“Wewe ni nani?” lilikuwa ni swali lingine kutoka kwa mwanaume ambaye mwilini mwake alikuwa na mavazia ya kibanditi mithili ya mtu ambaye alikuwa anaishi milimani.
“Sisi ni vijana tu wa mtaani tulikuja hapa kupata mali”

“Umefanya kosa kubwa sana kuwepo hapa bwana mdogo ungebakia tu huko huko ukauza hata ugoro” alitamka na kupitisha shoka lake kwenye shingo ya mwanaume huyo kisha akasikia hatua za mtu zikiwa zinakuja nyuma yake japo hatua za mtu huyo zilikuwa za kunyata sana ila alizisikia vizuri kabisa.
“Kennedy”
“Yes, bosi”

“Hakikisha unalisafisha hili eneo ndani ya muda mfupi sitaki kuona hii mizoga”
“Roger that, sir!” mwanaume ambaye alitoa hiyo kauli alikuwa ndani ya buti zito la kutisha sana, aligeuka na kuelekea alikokuwa ametokea.

Mwanaume huyo alinyoosha moja kwa moja mpaka ndani ya godauni kubwa ambalo lilijengwa mithili ya nyumba ya kuishi maana kuna upande ulikuwa umegawanywa vizuri sana na kutengenezwa kama nyumba ya familia. Aliingia humo ndani na kupanda lifti yake kuelekea chini, sekunde chache sana alishuka huko chini, huko ilikuwa ni kama dunia nyingine ambako watu walikuwa wanaishi, kulikuwa na wanaume wa kutosha ambao walikuwa wanaendana nae alivyokuwa.

Baada ya kufika huko alifuatwa na mwanaume mmoja ambaye alikuwa na vest tu kwenye mwili wake,
“Bosi kiongozi mkuu alikuwa anapiga simu wakati umetoka nje hivyo nadhani unaweza ukamcheki maana kutakuwa na dharura ambayo imefanya mpaka akakutafuta saivi”

“Ok ngoja nimtafute lazima kutakuwa na jambo la mhimu sana” mwanaume huyo alitembea mpaka ndani ya ofisi yake na kuipiga simu hiyo ambayo aliambiwa kwamba ilikuwa imemtafuta muda sio mrefu sana.
“Ted”
“Naam bosi heshima yako”

“Nataka uje na vijana watano Dar es salaam haraka sana”
“Saivi bosi?”
“Hapana, keshokutwa usiku mnatakiwa kuwepo huku, nadhani umesikia kila ambacho kinaendelea”
“Ndiyo bosi najua kila kitu”

“Sasa kuna kazi ambayo unatakiwa kuja kuikamilisha huku haraka sana kabla sijapata matatizo makubwa, kesho kuna mtu nakutana naye atanipa majibu ya ninachohitaji kukifanya kisha baada ya hapo utamalizia panapo bakia”

“Nimekuelewa kiongozi, na hawa mwanasayansi na mwandishi niwafanye nini?”
“Hao waache kwanza kwa sababu watakuwa na umuhimu kwa hapo baadae”
“Sawa bosi” simu hiyo ilikatwa baada ya maelezo hayo kuisha. Mwanaume huyo alihema kwa nguvu na kutoka ndani ya chumba hicho akaelekea kwenye chumba kingine ambacho kulikuwa na mwanaume mmoja ambaye alikuwa anaishi ndani ya chumba hicho huku kwenye kabati lake kukiwa na vitabu vingi sana.

“Heshima yako mr Dawson” alimasalimia mwanaume ambaye umri wake ulikuwa umeenda huku akiwa anaiwasha sigara yake mkononi na kukaa kwenye kiti huku buti lake akiliweka juu ya meza.
“Kuna siku nitakuja kutoka nikiwa hai humu ndani?” mwanaume huyo aliuliza akiwa amekata sana tamaa ya maisha.

“Hahaha hahaa hahaahaha, unatakiwa kumshukuru Mungu mpaka sasa familia yako ni nzima, unaanza kuuliza habari ya wewe kutoka humu ndani? Mimi nimechoka sana kukuhifadhi nilitaka kukuua leo una bahati tu bosi anadai kwamba bado ana kazi na wewe ndiyo maana unaendelea kuwa hai”

32 inafika mwisho

Tchao
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 33
“Hivi haujawahi kuyawazia maisha ya watu ambao wanateseka huko nje?”
“Hilo sio jukumu langu kuwajali wao, hakuna anayejali kuhusu maisha ya mtu mwingine kila mtu anatakiwa kuipambania hali yake na ndivyo maisha yapo hivyo”

“Fikiria kwa umakini sana kijana wangu”
“Kuna kitu ambacho nadhani bado haukielewi ndugu mwandishi”

“Una maanisha nini?”
“Mimi nililitumikia sana hili taifa kwa moyo sana lakini unajua kilicho nikuta?”

“Nilikuwa nafanya kazi kwa bidii sana kuilinda amani ya nchi hii lakini hakuna jambo la maana ambalo niliwahi kulipata, niliwahi kujitoa kwa kila namna lakini malipo yake ilikuwa ni kusimangwa kila sehemu na bado unanikumbusha mimi cha kukifanya? Sikuwahi kuwa na maisha mazuri hata siku moja, mimi na wenzangu baada ya kuonekana kwamba hatuna umuhimu tena hawa hawa wananchi ambao unadai kwamba wanateseka huko nje ndio ambao waliihimiza serikali sisi tukafukuzwa jeshini na kusingiziwa kesi ya kutaka kuisaliti nchi unajua ilikuwaje?”

“Pale ndipo nilijua kwamba kuwapigania watu wapumbavu kama hawa ni kupoteza muda, mimi na wenzangu tulienda milimani huko na kuanza kuishi maisha ya kibanditi huku tukiwa tunajifua na kuvamia sehemu mbali mbali kupora mali na silaha tukiwa tunawaza kuja kuipindua nchi hii lakini mitazamo yetu ilibadilika baada ya kukutana na bosi, huyu ndiye ambaye alitubadilishia maisha, huyu alitupa heshima ambayo sisi tunastahili na huyu ndiye ambaye ametupa sisi maisha. Kwa sasa naweza kwenda sehemu yoyote ile duniani, naweza kuishi sehemu yoyote ile kwa sababu nina pesa bado unawaza kwamba nitakumbuka tena kuwapigania hao wananchi wako ambao mpaka sasa hata hawawezi kuuliza wala kukumbuka kwamba nilizikwa wapi?”

“Mimi nimekuwa kiumbe cha hatari sana na siwezi kurudi nyuma hata dunia ikisogea nyuma, nina roho ngumu sana ndugu yangu na usije ukarudia tena kutaka mazoea na mimi kwa mara nyingine. Nakumbuka mimi mwenyewe nilikuja kukuonya kwamba usije ukatoa kile kitabu kabisa kwa sababu utajiletea matatizo makubwa sana kwenye maisha yako lakini ulikuwa mbishi haukutaka kusikia, mara ya pili nikamuua mtoto wako mmoja kama onyo lakini ukauvaa ujasiri mpaka ukaamua kukitoa rasmi kile kitabu “MAITI INAYO ONGEA” kile ni kitabu ambacho kilikuwa kinaenda kumharibia bosi sana na mipango yake yote kama kingefanikiwa kuwafikia watu wengi zaidi lakini unajua ni kipi kilitokea?”

“Kila ambaye alikipokea kile kitabu sisi tulimuua usiku ule ule, tuliipata orodha ya watu ambao walikuwa wamekilipia kile kitabu hivyo wote walikufa na kitu ambacho haukukijua ni kwamba vyombo vya habari ambavyo ulijaribu kuvifuata ili kukisambaza kile kitabu vilikuwa chini yetu kasoro mwandishi wa habari mmoja tu ambaye alifanikiwa kukimbia ila aliiponza familia yake” mwanaume huyo aliongea akiwa anasikitika sana huku anaiwasha sigara yake ambayo ilikuwa imezima.

“Niliiteka familia yake na kumtumia video nikiwa nambaka mkewe, nilimwambia kama asipokuja na ushahidi aliokuwa nao basi ningembaka na binti yake ambaye alikuwa na miaka kumi na mitano tu kwa sababu alikuwa ni mrembo sana. Nilimpongeza sana kwa kuwa jasiri kuisaidia familia yake hivyo alikuja mwenyewe kama nilivyokuwa nimemwelekeza lakini nisingeweza kumuacha kwa sababu tayari alikuwa anajua hivyo nilimuua na mkewe nikabaki na binti yake ambaye nadhani hauna haja ya kuuliza kwamba alibaki kwa sababu ya kazi gani” aliongea huku akiwa anazunguka mle ndani na kucheka sana kwa sauti kubwa huku akiwa anamnyooshea Dawson vidole ambayo vilikuwa na sigara.

“Kuna jambo moja bwana Dawson ambalo hauna haja ya kumlaumu mtu ila kujilaumu mwenyewe na huenda ni kitu ambacho ni ngumu sana wewe kukiamini kwa sasa ila inakulazimu uamini kwa sababu ndio ukweli”

“Wewe shetani” mzee huyo aliongea mpaka kigugumizi kikamshika huku akiwa anatokwa na machozi kwenye uso wake maana alijua hapo moja kwa moja ni familia yake ilikuwa inahusishwa.

“Pole sana kwa hili ila pia ni jambo ambalo litakuhuzunisha sana. Yule mwanamke ambaye wewe uliyatoa maisha yako kwa ajili yake, yule mwanamke ambaye kwa historia yako uliwahi kuapa kwamba unampenda sana kanisani na hata ungekufa kwa ajili yake ana mimba yangu kwa sasa”
“Whaaaaaat?” mzee huyo aliuliza akiwa ameyatoa macho yake

“Yeah mzee na sio kwamba nilimbaka hapana bali huwa ananivulia nguo zake yeye mwenyewe kwa mapenzi yake na ananipa stori zako kwamba ulikuwa mchovu sana kitandani kiasi kwamba ulikuwa huwezi kabisa kumfikisha kule ambako alikuwa anakutaka kwahiyo ananipenda sana mimi maana ile sehemu ambayo ipo katikati ya miguu yake mimi naitendea haki sana” alikuwa anaongea maneno ya kuumiza sana kiasi kwamba mzee huyo alimsogelea na kumkwida shingoni lakini mwanaume huyo alimpiga na kibao kikali sana mzee huyo mpaka sikio lake likaanza kutoa damu.

Aliitoa simu yake mfukoni na kumrushia mzee huyo, kwenye simu hiyo alikuwa anaonekana yeye akiwa uchi akiwa anafanya mapenzi na mkewe wa ndoa, mwanamke ambaye yeye aliamua kujitoa sadaka ili aishi na mwanamke huyo alikuwa anatoa ushirikiano na kuelezea ni namna gani alivyokuwa anampenda sana mwanaume huyo wa kazi ambaye alijulikana kama Ted. Video hiyo haikuwa na utofauti kabisa na video ya ngono lakini pia mzee huyo akiwa analia na kuivunja simu hiyo kwa nguvu, mwanaume huyo alitabasamu na kumsogelea tena.

“Bora hiyo unaweza kuivumilia mzee wangu lakini hili litakua ni gumu sana kwako kuvumilia” aliongea na kumpatia simu nyingine, simu ya pili ambayo ilikuwa na video pia. Aliifungua video hiyo na kuiangalia huku macho yake yakizidi kuwa mekundu kama nyanya ambazo zilikuwa zimesagwa kwenye brenda. Kwenye video hiyo alikuwa anaonekana mwanaume huyo huyo Ted akiwa na mwanae ambaye alimuacha akiwa anasoma chuo akiwa naye kitandani tena akiwa uchi kabisa bila nguo yoyote ile wakifanya na kuyafurahia mapenzi kwa fujo sana.

Aliibamiza tena simu hiyo na kuanza kupiga makelele kwa uchungu sana, ukatili ambao mwanaume huyo alikuwa anamfanyia ulikuwa umezidi mipaka, hakuona kama alikuwa anastahili kuweza kutendewa unyama wa namna hiyo maana alichokuwa anakifanya kilikuwa sahihi na alikuwa anakifanya kwa ajili ya kuweza kulilinda taifa lake ambalo alikuwa analipenda sana.

“Habari mbaya zaidi ni kwamba hao wote wawili yaani mkeo na mwanao wote wana mimba zangu kwa sasa. Unataka kujua kwamba ni kwa namna gani naonekana nikiwa nafanya nao mapenzi wote na kila mmoja anafurahi?” aliuliza akiwa anaivuta sigara yake bila wasiwasi huku akiwa anamdhihaki mzee huyo kisha akaendelea

“Kwanza nawaridhisha kitandani lakini mwanao hajui kwamba mimi ndiye ambaye nipo nyuma ya haya mambo, yeye nilimtongoza vizuri tu hivyo anajua kwamba mimi ni mumewe mtarajiwa ila mkeo ananijua vizuri sana na anajua kila kitu ila akaamua kunichagua mimi hapa kwa sababu hauna hata uwezo wa kujilinda mwenyewe hivyo anaamini kwamba hauwezi kumlinda hata yeye pia. Hawa wote hawajuani kama mimi nafanya nao mapenzi wote na nataka siku ambayo watakuja kujua iwe tayari wana watoto wangu sasa sijui kama utawaua au utawaacha hai kama utafanikiwa kuwaona kwa macho yako? Hilo ni juu yako” alimsogelea na kumpulizia moshi kwenye uso wake.

“Siku nyingine kama utapata nafasi unatakiwa kuyafanya masikio yako yasikie vizuri na ufanye maamuzi ambayo ni sahihi. Keshokutwa narudi tena Dar es salaam hivyo naenda kukutana nao na kufanya nao mapenzi tena hivyo usijali kila kitu utakiona maana lazima nitachukua video za kutosha tu” mwanaume huyo aliongea huku akiwa anazimia sigara yake kwenye shavu la mzee huyo na kucheka kicheko cha dharau sana huku akiwa anaondoka.

Mzee huyo alibaki analia mwenyewe ndani ya chumba hicho huku akiwa amejikunyata. Alitamani hata kujiua lakini hakuwa tayari kufanya hivyo kwa sababu kuwa hai kwake ndiko kuliifanya familia yake iendelee kuwa hai, hata kama mkewe alikuwa ameamua kumsaliti na kumkataa mbele ya watu hao bado aliamini kwamba alikuwa na watoto ambao walikuwa wanaihitaji imani yake ili kuendelea kuishi maana hawakuwa na hatia yoyote ile.

Jina lake alikuwa anaitwa Dawson Nduka. Alikuwa ni mwandishi maarufu sana wa vitabu ndani ya nchi ya Tanzania ambaye alijipatia umaarufu mkubwa sana kwa kutowaogopa viongozi wakubwa wa serikali huku akiwa anawafichua maovu yao na kuwajulisha wananchi kwamba ni kipi ambacho walikuwa wanatakiwa kukifanya ili nchi yao iweze kusonga mbele ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kumvutia kila mtu duniani kupitia vitabu vyake.

Kuandika kwake vitabu kulimpeleka kwenye sehemu mbaya sana baada ya kulipata file la mwanasiasa mkubwa sana kwa wakati huo Denis Kijazo. Aliandika mpango wa hatari wa mwanaume huyo wa kuhitaji kulitawala taifa kwa zaidi ya miaka miamoja. Habari hiyo ingekuwa ni mbaya sana kama umma ungejua ukweli na ndilo lilikuwa lengo lake kubwa kwamba wananchi wajue ili kama walikuwa wana uwezo basi waweze kulizuia jambo hilo kwa kufanya mapinduzi ya kumuondoa kiongozi huyo kwa lazima madarakani, lakini harakati zake hizo zilipelekea baadhi ya watu kupoteza maisha yao kwa kila ambaye aliipata nakala kabla hazijasambaa kwa watu wengi lakini pia aliiponza familia ya mwandishi wa habari ambaye aliuawa yeye na familia yake yote huku yeye mwenyewe akiwa ameishia kwenye mikono ya watu hao na kuwa mtumwa wao ambapoo walikuwa wanamtumia kuandaa nakala za hatari sana ambazo zilitumika kutekelezea mambo yao ya kisiasa.

“MAITI INAYO ONGEA” ndilo lilikuwa jina la kitabu chake hicho ambacho aliwaahidi wananchi kwa muda mrefu sana ila kwa bahati mbaya sana hawakupata bahati ya kuweza kuipata nakala hiyo maana mhusika alipotea ghafla sana kwenye macho yao. Jina la kitabu lilikuwa na maana ya mtu ambaye alikuwa anapigwa vita asiweze kupaza sauti lakini hata bila uwepo wa kitu cha kumfanya apaze sauti bado yeye alikuwa na uwezo wa kupaza sauti. Hapo alijiweka yeye kama yeye kumaanisha kwamba licha ya vyombo vya habari karibia vyote kugoma kumpa msaada yeye kama mwandishi ambaye alikuwa amewekewa vikwazo bado alikuwa anawasemea wananchi lakini matokeao yake aliishia sehemu mbaya sana.

Jengo la saba ilikuwa ni mali ya Denis Kijazo, hiyo ilikuwa ni ngome yake kubwa sana ambayo alikuwa anaitegemea zaidi kwenye kila kitu ambacho alikuwa anaifanya ila ilikuwa ni ngome yake ya siri Sana ambayo ni watu wa kuhesabika sana walikuwa wanajua kwamba mwanaume huyo alikuwa anaimiliki. Ndani ya ngome hiyo walikuwa wanatunzwa wanaume hatari sana ambao walikuwa wanaongozwa na Ted na hao ndio wanaume ambao alikuwa anawatumia sana kuweza kuyakamilisha mambo yake kwa siri kisha watu hao wangetoweka na kwenda kujificha huko.

Baada ya kuona kwamba mambo yalikuwa yameanza kwenda vibaya alimuita kijana wake ambaye alikuwa anamuamini sana kwa ajili ya kwenda kutekeleza kila ambacho yeye aliona kwamba ni sawa kukifanya kwa wakati huo ili raisi huyo auawe kama ilivyokuwa imepangwa. Ted baada ya kutoka ndani ya chumba cha mwandishi wa vitabu alijisogeza mpaka kwenye maabara kubwa sana ambayo huko ndani ilikuwa na wanasayansi wengi sana huku wengine wakiwa wanatengeneza madawa ya kulevya sambamba na warembo wengi sana ambao walikuwa uchi ndio walikuwa wanapakia madawa hayo kwenye mifuko lakini wengine walikuwa wanatengeneza sumu kali sana ambayo hata matumizi yake hayakuwa yakijulikana kwamba ilikuwa inatumika kwenye nini.

33 inafika mwisho

Tchao
 
HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+

Episode 34
“Kazi imefikia wapi?”
“Sumu tayari ipo ya kutosha na ishapakiwa tayari”
“Inafanya kazi kama tulivyo kubaliana?”
“Ndiyo kiongozi” mwanasayansi mkuu alikuwa anajibu kwa hofu sana.
“Unajua kabisa kama ukiniletea uhuni ni kitu gani nitakifanya kwa familia yako”
“Ndiyo ndiyo naelewa ndiyo maana nipo makini sana na kazi”
“Huwa siwezi kumuamini mtu kwa maneno tu”
“Unamaanisha nini?”
“Tunatakiwa kupata mtu wa kuweza kuijaribu”
“Unataka niwaue watu ambao hawana hatia kwa sumu?”

“Kwani wewe unahisi hiyo sumu inatumika kwenye nini? Na hao watu ambao hawana hatia kwahiyo familia yako ina hatia?”

“Nitafanya hivyo” mwanasayansi huyo aliongea kinyonge sana huku akimimina chai na kuweka tone moja tu la sumu ambayo ilikuwa kwenye kichupa kidogo kwnye mikono yake kisha akamuita mwanasayansi mmoja na kumpa ile chai ambapo mwanaume huyo alikuwa na wasiwasi sana lakini aliambiwa anywe.

Hakuwa na namna zaidi ya kufanya hivyo, baada ya kuinywa chai hiyo alianza kutetemeka, damu ikaanza kumtoka puani na masikioni na hakuchukua hata muda akaanza kukakamaa na kuakuka kabisa.
“Safi sana, wateja wetu wa nje wanaihitaji haraka sana. Ni sumu ambayo inauzwa bei ghali mno kwahiyo nina imani kwamba itatupatia mabilioni ya fedha, kazi nzuri dokta” alimpiga piga mgongoni na kutoka humo ndani dokta akiwa anakaa chini na kusikitika sana maana mambo ambayo yalikuwa yanaendelea yalikuwa yamevuka kwenye ubinadamu wa kawaida.

Wakati watu wanalalamika kwa baridi kali ambayo ilikuwa inaendelea ndani ya jiji la Dar es salaam kwa sababu ya hali ya mvua ambayo ilikuwepo, ilikuwa ni tofauti kabisa kwa watu wawili, watu ambao miili yao ilikuwa sehemu ya kuwapa burudani ambayo huenda watu wengi sana walikuwa wameikosa kabisa kwenye maisha yao. Max na Brandina walikuwa wanavinyoosha viungo vyao kitandani huku kila mmoja wao akiwa anamsifia mwenzake kwa namna alivyokuwa anajua kukitumia kiungo chake kuweza kumnyooshea mwenzake viungo vyake.

Mapenzi yao yalikuwa ya muda mfupi sana lakini walijikuta wanaanza kuaminiana kiasi kwamba mara nyingi walianza kulala pamoja na kazini wangewahi pamoja kisha wangeachana pamoja kwa sababu ilikuwa ni hatari sana kama wangejulikana kwamba walikuwa wamezama kwenye mapenzi kutokana na asili ya kazi yao hawakuwa wanatakiwa kabisa kuingia kwenye mapenzi kwa namna yoyote ile hata kwa bahati mbaya tu.

Mwanaume baada ya kutoka kitandani akiwa uchi, alikaa kwenye sofa ambalo lilikuwa karibu na kitanda huku akiwa anamwangalia mrembo Brandina naye akiwa uchi kabisa kwenye mwili wake. Alikuwa anamkadiria mrembo huyo anashindwa kummaliza, licha ya kwamba alikuwa ameanza kumzoea sana na kumpenda kwenye moyo wake lakini alikuwa na wasiwasi naye kwani alikuwa amekuja kwa kasi sana na kazi yake haikumruhusu yeye kuweza kumwamini mtu yeyote yule na kwa namna yoyote ile.

“Unataka nini kwangu?” ndilo swali ambalo alimuuliza mwanamke huyo akiwa amemkazia macho. Mrembo huyo licha ya kushtuka sana kutokana na aina ya swali ambalo alikuwa ameulizwa ila hakutaka kuonyesha mshtuko huo kwani ungethibitisha kwamba alikuwa na jambo lake. Alijizoa zoa na kusogea kwenye kile kiti ambacho Max alikuwa ameketi, alimkalia na kuanza kumnyongea kiuno chake mithili ya feni iliyokuwa inaongezeka kasi sana mwisho wakajikuta wamezama tena kwa penzi zito sana.

“Mimi nahitaji msaada wako Max” lilikuwa ni jibu lake baada ya kumaliza shughuli nzito ambayo iliwaweka kitandani kwa muda huo.
“Msaada upi?”

“Unajua nimepewa nafasi kubwa sana ya kumlinda raisi wa nchi nikiwa kama mlinzi wake mkuu”
“Brandina hayo siyo mambo ya kuongelea hapa saivi ni hatari sana, achana kabisa na hayo mambo”
“Nadhani wewe umeniuliza kwamba ni kwanini nimekuja kweye maisha yako”
“Sasa suala la raisi linatokea wapi?”

“Ndiyo sehemu hasa ambayo nahitaji msaada wako Max kwani nipo hatarini sana kuuawa”
“Whaaaat?”
“Ndiyo”

“Nani anataka kukuua?”
“Unamwamini mkurugenzi wa shirika letu”
“Brandina, what are you talking about?”

“Niligoma kufanya kazi yake Max, sijajua nyuma yake kuna nani na nani ila yule ni mtu hatari sana”
“Umeyajuaje haya?”
“Kwa sababu alitaka mimi nimuue raisi”
“Whaaaaat?”

“Yeah Max, niliogopa sana na ukizingatia sina mtu hata mmoja upande wangu nimebaki na wasiwasi sana”
“Ilikuaje?”
“Alinipa maagizo tu kwamba natakiwa kumuua mheshimiwa raisi bila kuacha ushahidi”
“Na wewe ukamjibu nini?” Max aliuliza akiwa anazunguka humo ndani na kushika kichwa, alikuwa hajui kama kwenye huo mchezo hata mrembo huyo alikuwa ameingizwa, hilo kwake lilikuwa ni jambo la hatari sana.

“Nilimwambia siwezi kuifanya hiyo kazi, siwezi kumsaliti raisi wa nchi yangu wala kulisaliti taifa langu kwa namna yoyote, ila aliniambia kwamba kama nikishindwa kufanya hivyo mimi ndiye natakiwa kufa. Naomba msaada wako Max” mwanamke huyo aliongea akiwa analia na kukaa chini akiwa bado uchi kabisa. Max alimsogelea na kumkumbatia kwa hisia sana, ilimuuma sana mrembo huyo kuingizwa kwenye michezo mibaya na ni wakati ambao alijihakikishia kwamba kweli mkurugenzi huyo alikuwa msaliti kama ambavyo raisi alimtahadharisha.
“Natakiwa kuongea na raisi hili jambo”
“Hapana Max usifanye hilo kosa”
“Kwanini?”

“Kwa sababu raisi atapaniki na mchezo wote unaweza ukaharibika, mimi nimekushirikisha wewe kwa sababu nimeona ndiye mtu pekee ambaye naweza kumwamini”
“Unahitaji nini?”

“Nataka unisaidie hawa watu na huu umoja wao tuweze kuupoteza na kuupoteza inatakiwa tufanye kazi bila wao kuwa na taarifa kwamba sisi tunawatafuta”
“Siwezi kukaa kimya nitakuweka kwenye hatari kubwa sana B”

“Hatuna namna Max naomba tu kujua kama unaweza kuwa na mimi kwenye hii safari maana kama tukiwaacha hawa watu wananchi wa taifa hili watateseka sana”
“Kwani kuna mengine unayajua zaidi ya haya?”
“Ndiyo”
“Unaweza kuniambia?”

“Baada ya kufuatilia kwa umakini sana nimekuja kugundua kwamba kumbe raisi mstaafu ni miongoni mwa watu ambao wapo nyuma ya haya mambo yote ambayo yanatokea na huenda ndiye yupo nyuma ya mkurugenzi”
“Una muda gani tangu umeyajua haya?”
“Siku tano sasa. Max mbona hata haushtuki kwamba unayajua haya?” Max alihema kwa nguvu sana na kuchungulia nje hakuona mtu yeyote yule.
“Yeah”
“Whaaaat?”

“Najua kila kitu Brandina”
“Niambie kwamba unanitania sio?”
“Hapana, sina utani na wewe”
“Why unajua na haufanyi jambo lolote?”

“Brandina haya mambo ni magumu sana kuliko unavyo fikiria wewe, ni watu wazito sana ambao unashauri kuingia nao kwenye vita na tangu ulipo amua kupambana nao basi maisha yako yapo hatarini sana”
“Kipi kinaendelea Max?”
“Naweza kukuamini B?”

34 naweka nukta hapa.

Hatariii upo vizuri kiongoz unatuburudisha na kutufundisha piah naamini unaitendea haki kazi ya Fasihi andishi. Mungu akujalie uendelee kutuletea vitu vizuri zaidi na ufike mbali kama malengo yako yalivyo.
 
Shukrani sana mkuu. Asante kwa kuendelea kuwa nami 🤝
 
Back
Top Bottom