Mnachihanguuu
JF-Expert Member
- Feb 10, 2023
- 4,385
- 6,443
Hatari sana
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Very attractiveHADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
Episode 31
Alitembea taratibu kuelekea alipokuwa mwanaume huyo ambaye hakuonekana kuwa na wasiwasi juu ya ujio wa mgeni wake ambaye alikuwa tayari amefika. Raisi baada ya kufika karibu kabisa na alipokuwa amesimama mwanaume huyo aliuliza swali.
“Wewe ndiye Bilali?”
“Yes” mwanaume huyo alijibu huku akiwa anageuka alipokuwepo raisi huyo. Raisi alicho kiona mbele yake alihisi anaota, alihisi hakuwa yeye bali ilikuwa ni ndoto yake tu, raisi huyo alijikuta anaanza kutetemeka na ilibakia kidogo tu aweze kudondoka chini lakini mwanaume huyo alimkimbilia na kumdaka kisha akamsimamisha vizuri lakini hata hivyo raisi hakuwa na nguvu za kuendelea kusimama bali aliketi kwenye moja ya benchi ambazo walikuwa wanazitumia abiria ndani ya kituo hicho.
“Piusi?”
“Yeah, ndiye mimi Piusi”
“Hapana hili jambo sio kweli”
“Kama hauwezi kuamini kile ambacho unaambiwa basi yaamini sana macho yako”
“Ulikufa wewe”
“Uliambiwa hivyo lakini sidhani kama ulifanikiwa hata kuuona mwili wangu”
“How?”
“Dunia inatisha sana mheshimiwa ndiyo maana watu ambao wanaishi vizuri ni wale ambao wameamua nao kuwa watu wa kutisha hivyo kila kitu kwao wanakiona kama kitu cha kawaida sana. Mimi sijawahi kufa na wala hakutokea mtu miaka yote ambayo nimeishi kutaka kuniua kwa sababu hakuna mtu hata mmoja ambaye alikuwa ananifahamu huko nje”
“Inamaanisha kuja kwangu ulikuwa umetumwa kwa ajili ya kazi?”
“Ndiyo maana nipo hapa”
“Hahahaha hahahaha, hapana kwahiyo ulikuja kucheza na hisia zangu halafu ukamsingizia Denis Kijazo kwamba amekuua? Nini hasa lilikuwa lengo lako?”
“Ni kwa sababu ya kazi. Ni miaka kumi sasa imepita wewe ukiwa unajua kwamba nimekufa na ulisha nisahau kabisa, hiyo inatupa funzo kwamba duniani hatutakiwi kuishi kwa kuwafurahisha watu kwani ni suala la muda mfupi sana kukusahau na kukufuta kwenye kumbukumbu zao za maisha”
“Hivi uliwahi hata kunipenda labda?”
“Yeah niliwahi kukupenda lakini kwa bahati mbaya sana kazi yangu inanitaka kuwa na moyo wa chuma, sitakiwi kabisa kumpenda mtu kiasi kwamba nikasahau kazi. Nilikupenda japo nilikuja kwako kwa kazi maalumu kwa sababu ulikuwa ni mwanamke pekee ambaye uliweza kuzielewa hisia zangu mapema sana hivyo ukazibeba kwa ukumbwa ule ambao hakuna mwanamke aliwahi kunifanyia kabla”
“Unategemea baada ya hili mimi naweza kukuamini tena? Unafikiri kwamba mimi naweza nikafanya na wewe kazi tena? Ni miaka kumi umenidanganya Bilali, miaka kumi najua mwanaume ambaye nilikuwa nampenda sana alikuwa amekufa halafu kumbe upo hai na mzima wa afya kabisa?”
“Kama ungekuwa kwenye nafasi yangu, nadhani ungeelewa kwamba ni kwa namna gani maisha yetu sisi tunaishi kwa kubahatisha kama ndege ambapo unakuwa haujui kwamba kesho yako unaweza ukaamka ukiwa hai au umekufa maana ndege muda wote naye huwa anawindwa na manati, bila kujua adui yake yuko wapi na manati yake muda wowote anaweza kujikuta anauawa. Hayo ndiyo maisha yangu mimi, maisha ya kutolala usingizi kuhakikisha taifa linakuwa salama lakini nimezoea sasa licha ya kujitoa kwa kila kitu kwa ajili ya haya bado muda wote huwa napokea lawama na matusi huku wananchi wengine wakiwa wanadai uwepo wetu ni upotezaji wa kodi zao tu”
“Wewe ni nani Bilali?”
“Kama ulifanikiwa kumjua bosi wangu unashindwa vipi kujua mimi ni nani?”
“Yule alikuwa bosi wako, nataka kujua kwamba wewe ni nani?”
“Komando”
“Whaaaat?”
“Yes, mimi ndiye kiongozi wa kundi hatari ambalo uliambiwa linaitwa DRAGON BOYS, tupo watatu tu lakini ni zaidi ya jeshi zima la makamanda mlio nao huko”
“Hapana bado sikuamini” mwanaume hakuongea sana, alivua koti la suti na shati yake na mwili ambao ulikuwa umegawanyika kwa mazoeazi makali, ulikuwa unaonekana vyema sana. Aliunyanyua mkono wake wa kulia akisogea alipokuwepo raisi huyo ni kweli kama alivyokuwa amepewa maagizo na Francis Mboye kwamba kama atakuwa na wasiwasi na kijana huyo basi amwangalie chini ya kwapa ataiona alama ya Dragon na kweli aliiona alama hiyo kwa usahihi sana.
“Wenzako wako wapi?”
“Nipo nao hapa hapa” mheshimiwa aliangaza lakini hakuona kitu, mwanaume alinyoosha kidole chake mkono wa kulia nje, alionekana mwanaume mmoja ambaye alikuwa kwenye mavazi machafu akiwa amelalia makopo kana kwamba hakuwa na makazi na maisha yake yalikuwa ya kutegemea kuokota makopo. Lakini pia alinyoosha mkono wake wa kushoto karibu na ulipokuwa ukuta wa kutenganisha barabara iliyokuwa inaenda Feri na bahari na hapo alimuona mwanaume mwingine akiwa amelala kwa kujibanza kwenye ukuta huo na bila kuwa makini ilikuwa ni ngumu sana kuona kama kuna mtu hapo.
“Una lipi la kuniambia Bilali?”
“Tuna mambo mengi sana ya kuzungumza mimi na wewe ila kwa leo sio muda wake”
“Unamaanisha?”
“Leo nilitaka tukutane kwanza kwa sababu nilijua utapata mshtuko mkubwa sana kuniona mimi hivyo tutatafuta siku nzuri ya kuweza kuongea ila hakikisha unaongea na kijana wako nakutana naye”
“Max?”
“Ndiye huyo, huyu ndiye ambaye tunamtegemea zaidi kwenye hii kazi, sisi wote mimi, wewe na wenzangu tuna asilimia nyinyi sana za kufa lakini huyu bwana mdogo inabidi tuhakikishe anakuwa hai”
“Kwanini unaamini kwamba tutakufa?”
“Kwa sababu ipo hivyo mheshimiwa”
“Mtakutanaje?”
“Mpe maagizo ya kesho kwenda Kariakoo usiku kwenye kazi yoyote ile mimi nitakuwa kule hivyo nitakutana naye”
“Unahisi atakujua?”
“Watu wa aina yetu huwa kuna namna ya kutambulishana hivyo usijali kuhusu hilo. Katulie kisha ukiwa sawa mimi na wewe tutaongea vizuri ila kaa mbali na mkurugenzi wa usalama wa taifa kabla haujachelewa” mwanaume aliongea na kuanza kuondoka kama masihara ndani ya eneo hilo
.
“Bilali” aligeuka baada ya kuitwa
“Unanipenda?” alitikisa kichwa masikitiko sana.
“Bado sijui” alijibu na kuishia upande wa pili kisha umeme ukakata ndani ya eneo hilo, Brandina alikimbilia ndani kumuwahi mheshimiwa raisi maana umeme kukatika ghafla ilikuwa ni ishara mbaya sana lakini alimkuta kiongozi huyo akiwa salama kabisa ameketi kwenye benchi. Baada ya dakika mbili umeme ulirudi eneo lote kukiwa hakuna kitu wala mtu yeyote yule.
“Mheshimiwa una uhakika kuna usalama hili eneo”
“Ndiyo Brandina ni kwa sababu ya usingizi tu, turudi nikalale maana nimechoka sana” hakukuwa na cha kusubiri ilibidi tena warudi Ikulu haraka na kwa siri kubwa mno mheshimiwa akiwa na mawazo mengi sana kwenye kichwa chake maana alikuwa anahisi kama yaliyotokea kule yalikuwa ndoto na haikuwa kweli ila hakuwa na uwezo wa kubadili ukweli kuwa uongo hivyo alitakiwa kuwa mpole tu.
Brandina muda wote ambao alikuwa pale alijitahidi sana kuweza kufuatilia kujua ni kipi ambacho kilitokea na kupata jibu kwamba raisi alikuwa anakutana na nani lakini hakuna alicho ambulia maana alihisi kama aliona raisi anaongea na mtu ila hakujua ni nani na umeme ulipo katika baada ya kwenda pale hakukuta mtu yeyote hivyo akawa amepigwa za uso.
NGARENARO, ARUSHA
Wilaya ya Arusha mjini, inapopatikana Ngarenaro ya chini, eneo ambalo walikuwa wanaishi wanaume wahuni sana na makundi ya wahuni wa mitaani. Ni eneo ambalo wale watoto wa mama halikuwa likiwafaa kwa ajili ya kuishi kutokana na asili ya maisha ambayo yalikuwa huko, walikuwa wanaishi wanaume ambao kwao kulalamika ilikuwa dhambi kubwa sana, kila mtu aliamini kwamba maisha yake lilikuwa ni jukumu lake hivyo hata kuishi wao ndio walikuwa wanatakiwa kujua namna gani wanaweza kuishi na kuyamudu maisha yao kimpango wao wenyewe.
Ilikuwa ni kama sehemu tofauti kabisa ndani ya nchi kwani walikuwa wanajiongoza wenyewe na hata maisha ambayo walikuwa wanayaishi yalikuwa ni tofauti sana na watu wengine. Ndani ya sehemu hiyo pia kulikuwa na viwanda vya siri sana ambavyo vilikuwa vinajihusisha na uandaaji wa pombe kali za kiharamu na za asili ambazo kwa mtu ambaye alikuwa ni mgeni nazo kama angefanikiwa kuzinywa basi maisha yake yangekuwa kwenye mstari wa hatari sana na kama angecheza vibaya basi alikuwa anapoteza maisha yake.
Eneo hilo licha ya kuwa na wahuni sana kila mtaa lakini miaka kadhaa ambayo ilikuwa imepita walipata uvamizi mkali sana, uvamizi wa watu ambao hawakujulikana kwamba walitokea wapi, uvamizi ambao waliingia watu ambao hawakuwa wahuni bali wao walikuwa ni wauaji wa kutisha sana. Wakati wanaume hao wanaingia kulikuwa kuna tetesi za chini chini kwamba ndani ya eneo hilo kwenye moja ya kiwanda cha pombe kali kulikuwa na makazi ya watu ambao hawakuwa wanajulikana kwamba walitokea wapi.
31 inafika mwisho.
Tchao
GoodOnce again tunakutana kwenye mchezo bora huu hapa. Tukapate kumsoma secret agent mmoja ambaye alikuwa assigned kuwa mlinzi wa raisi.
Lakini baadae anagundua kwamba mfumo hauko sawa na yeye ndiye alikuwa amechaguliwa na watu wasio julikana kwa ajili ya kuufuta huo mfumo. Anakuja kushtuka wakati yeye mwenyewe yupo ndani ya mfumo tayari hivyo anakuwa hana namna zaidi ya kudili na watu ambao hakuwa akiwajua na nyuma yao kulikuwa na mambo mazito sana.
Max (jina la kazi) huku jina lake halisi akijulikana kama DONALD DANIEL (DONNY) code no 001. Anaanza kuyafunua yale ambayo alipewa kazi kuyafanya ndipo anagundua kwamba kuna mlima mzito sana wa kuupanda lakini wakati anaanza kuyajua hayo mazito anakutana na jambo baya sana.
Ananasa kwenye HONEY TRAP na kuunguza mchezo mzima hali ambayo inamfanya kuishia kwenye umauti huku akishuhudia raisi ambaye ndiye alitakiwa kumlinda na raisi huyo ndiye alimpa kazi ya kuufuta huo mfumo akiwa anauawa ndani ya ofisi yake.
Muuaji anamuua raisi huku 001 akiwa ma risasi 6 mwilini hana cha kufanya hivyo yeye ndiye anauziwa kesi kwa kuhusika na mauaji ya raisi wa nchi, rasmi anavishwa taji la ugaidi huku ikionekana kwamba ameuliwa akiwa kahusika na mauaji ya raisi wake tena akiwa ndiye mlinzi mkuu wa raisi huyo.
Mwanaume huyo baada ya raisi kufa naye akiwa ana risasi sita kwenye mwili wake, anabebwa na kwenda kuzikwa akiwa bado hai hajakata roho.
001 anafukiwa na kushindiliwa ndani ya shimo la futi sita porini huku mvua ikiwa inausindikiza umauti wake na jina lake linafutwa kwenye idadi ya watu ambao waliwahi kuishi.
Lakini jambo la kutisha zaidi ni kwamba mwanaume huyo ambaye dunia iliamini kwamba alipatwa na umauti na ilithibitishwa kwamba ni gaidi ambaye aliuawa baada ya kumuua raisi akitaka kushambulia na watu wengine, alikuja kuonekana akiwa hai baada ya miaka kumi na mbili kupita.
Sasa alikufaje halafu akaja kuonekana tena akiwa hai miaka kumi na miwili baadae? Baada ya yeye kuonekana ni kipi kilitokea kwa watu wake ambao alifeli kuwafuta na mfumo wao kwa ujumla? Binafsi majibu yote nimekuandalia ndani ya hili andiko bora sana.
Ni muda wako ndio utakufanya uyapate majibu sahihi kwenye moja kati ya simulizi bora sana ya mapigano ya hali ya juu na ya kutisha muda mwingine bila kusahau stori iliyo pangiliwa unono kabisa.
Kwenye kalamu nimesimama mwenyewe Febiani Babuya wengine wapenda kuniita Bux the storyteller.
Here we go [emoji116]View attachment 2891932
Hatariii upo vizuri kiongoz unatuburudisha na kutufundisha piah naamini unaitendea haki kazi ya Fasihi andishi. Mungu akujalie uendelee kutuletea vitu vizuri zaidi na ufike mbali kama malengo yako yalivyo.HADITHI: JIJI LA KAMARI (GAMBLING CITY)
MTUNZI: FEBIANI BABUYA
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
WHATSAPP: 0621567672
AGE: 18+
Episode 34
“Kazi imefikia wapi?”
“Sumu tayari ipo ya kutosha na ishapakiwa tayari”
“Inafanya kazi kama tulivyo kubaliana?”
“Ndiyo kiongozi” mwanasayansi mkuu alikuwa anajibu kwa hofu sana.
“Unajua kabisa kama ukiniletea uhuni ni kitu gani nitakifanya kwa familia yako”
“Ndiyo ndiyo naelewa ndiyo maana nipo makini sana na kazi”
“Huwa siwezi kumuamini mtu kwa maneno tu”
“Unamaanisha nini?”
“Tunatakiwa kupata mtu wa kuweza kuijaribu”
“Unataka niwaue watu ambao hawana hatia kwa sumu?”
“Kwani wewe unahisi hiyo sumu inatumika kwenye nini? Na hao watu ambao hawana hatia kwahiyo familia yako ina hatia?”
“Nitafanya hivyo” mwanasayansi huyo aliongea kinyonge sana huku akimimina chai na kuweka tone moja tu la sumu ambayo ilikuwa kwenye kichupa kidogo kwnye mikono yake kisha akamuita mwanasayansi mmoja na kumpa ile chai ambapo mwanaume huyo alikuwa na wasiwasi sana lakini aliambiwa anywe.
Hakuwa na namna zaidi ya kufanya hivyo, baada ya kuinywa chai hiyo alianza kutetemeka, damu ikaanza kumtoka puani na masikioni na hakuchukua hata muda akaanza kukakamaa na kuakuka kabisa.
“Safi sana, wateja wetu wa nje wanaihitaji haraka sana. Ni sumu ambayo inauzwa bei ghali mno kwahiyo nina imani kwamba itatupatia mabilioni ya fedha, kazi nzuri dokta” alimpiga piga mgongoni na kutoka humo ndani dokta akiwa anakaa chini na kusikitika sana maana mambo ambayo yalikuwa yanaendelea yalikuwa yamevuka kwenye ubinadamu wa kawaida.
Wakati watu wanalalamika kwa baridi kali ambayo ilikuwa inaendelea ndani ya jiji la Dar es salaam kwa sababu ya hali ya mvua ambayo ilikuwepo, ilikuwa ni tofauti kabisa kwa watu wawili, watu ambao miili yao ilikuwa sehemu ya kuwapa burudani ambayo huenda watu wengi sana walikuwa wameikosa kabisa kwenye maisha yao. Max na Brandina walikuwa wanavinyoosha viungo vyao kitandani huku kila mmoja wao akiwa anamsifia mwenzake kwa namna alivyokuwa anajua kukitumia kiungo chake kuweza kumnyooshea mwenzake viungo vyake.
Mapenzi yao yalikuwa ya muda mfupi sana lakini walijikuta wanaanza kuaminiana kiasi kwamba mara nyingi walianza kulala pamoja na kazini wangewahi pamoja kisha wangeachana pamoja kwa sababu ilikuwa ni hatari sana kama wangejulikana kwamba walikuwa wamezama kwenye mapenzi kutokana na asili ya kazi yao hawakuwa wanatakiwa kabisa kuingia kwenye mapenzi kwa namna yoyote ile hata kwa bahati mbaya tu.
Mwanaume baada ya kutoka kitandani akiwa uchi, alikaa kwenye sofa ambalo lilikuwa karibu na kitanda huku akiwa anamwangalia mrembo Brandina naye akiwa uchi kabisa kwenye mwili wake. Alikuwa anamkadiria mrembo huyo anashindwa kummaliza, licha ya kwamba alikuwa ameanza kumzoea sana na kumpenda kwenye moyo wake lakini alikuwa na wasiwasi naye kwani alikuwa amekuja kwa kasi sana na kazi yake haikumruhusu yeye kuweza kumwamini mtu yeyote yule na kwa namna yoyote ile.
“Unataka nini kwangu?” ndilo swali ambalo alimuuliza mwanamke huyo akiwa amemkazia macho. Mrembo huyo licha ya kushtuka sana kutokana na aina ya swali ambalo alikuwa ameulizwa ila hakutaka kuonyesha mshtuko huo kwani ungethibitisha kwamba alikuwa na jambo lake. Alijizoa zoa na kusogea kwenye kile kiti ambacho Max alikuwa ameketi, alimkalia na kuanza kumnyongea kiuno chake mithili ya feni iliyokuwa inaongezeka kasi sana mwisho wakajikuta wamezama tena kwa penzi zito sana.
“Mimi nahitaji msaada wako Max” lilikuwa ni jibu lake baada ya kumaliza shughuli nzito ambayo iliwaweka kitandani kwa muda huo.
“Msaada upi?”
“Unajua nimepewa nafasi kubwa sana ya kumlinda raisi wa nchi nikiwa kama mlinzi wake mkuu”
“Brandina hayo siyo mambo ya kuongelea hapa saivi ni hatari sana, achana kabisa na hayo mambo”
“Nadhani wewe umeniuliza kwamba ni kwanini nimekuja kweye maisha yako”
“Sasa suala la raisi linatokea wapi?”
“Ndiyo sehemu hasa ambayo nahitaji msaada wako Max kwani nipo hatarini sana kuuawa”
“Whaaaat?”
“Ndiyo”
“Nani anataka kukuua?”
“Unamwamini mkurugenzi wa shirika letu”
“Brandina, what are you talking about?”
“Niligoma kufanya kazi yake Max, sijajua nyuma yake kuna nani na nani ila yule ni mtu hatari sana”
“Umeyajuaje haya?”
“Kwa sababu alitaka mimi nimuue raisi”
“Whaaaaat?”
“Yeah Max, niliogopa sana na ukizingatia sina mtu hata mmoja upande wangu nimebaki na wasiwasi sana”
“Ilikuaje?”
“Alinipa maagizo tu kwamba natakiwa kumuua mheshimiwa raisi bila kuacha ushahidi”
“Na wewe ukamjibu nini?” Max aliuliza akiwa anazunguka humo ndani na kushika kichwa, alikuwa hajui kama kwenye huo mchezo hata mrembo huyo alikuwa ameingizwa, hilo kwake lilikuwa ni jambo la hatari sana.
“Nilimwambia siwezi kuifanya hiyo kazi, siwezi kumsaliti raisi wa nchi yangu wala kulisaliti taifa langu kwa namna yoyote, ila aliniambia kwamba kama nikishindwa kufanya hivyo mimi ndiye natakiwa kufa. Naomba msaada wako Max” mwanamke huyo aliongea akiwa analia na kukaa chini akiwa bado uchi kabisa. Max alimsogelea na kumkumbatia kwa hisia sana, ilimuuma sana mrembo huyo kuingizwa kwenye michezo mibaya na ni wakati ambao alijihakikishia kwamba kweli mkurugenzi huyo alikuwa msaliti kama ambavyo raisi alimtahadharisha.
“Natakiwa kuongea na raisi hili jambo”
“Hapana Max usifanye hilo kosa”
“Kwanini?”
“Kwa sababu raisi atapaniki na mchezo wote unaweza ukaharibika, mimi nimekushirikisha wewe kwa sababu nimeona ndiye mtu pekee ambaye naweza kumwamini”
“Unahitaji nini?”
“Nataka unisaidie hawa watu na huu umoja wao tuweze kuupoteza na kuupoteza inatakiwa tufanye kazi bila wao kuwa na taarifa kwamba sisi tunawatafuta”
“Siwezi kukaa kimya nitakuweka kwenye hatari kubwa sana B”
“Hatuna namna Max naomba tu kujua kama unaweza kuwa na mimi kwenye hii safari maana kama tukiwaacha hawa watu wananchi wa taifa hili watateseka sana”
“Kwani kuna mengine unayajua zaidi ya haya?”
“Ndiyo”
“Unaweza kuniambia?”
“Baada ya kufuatilia kwa umakini sana nimekuja kugundua kwamba kumbe raisi mstaafu ni miongoni mwa watu ambao wapo nyuma ya haya mambo yote ambayo yanatokea na huenda ndiye yupo nyuma ya mkurugenzi”
“Una muda gani tangu umeyajua haya?”
“Siku tano sasa. Max mbona hata haushtuki kwamba unayajua haya?” Max alihema kwa nguvu sana na kuchungulia nje hakuona mtu yeyote yule.
“Yeah”
“Whaaaat?”
“Najua kila kitu Brandina”
“Niambie kwamba unanitania sio?”
“Hapana, sina utani na wewe”
“Why unajua na haufanyi jambo lolote?”
“Brandina haya mambo ni magumu sana kuliko unavyo fikiria wewe, ni watu wazito sana ambao unashauri kuingia nao kwenye vita na tangu ulipo amua kupambana nao basi maisha yako yapo hatarini sana”
“Kipi kinaendelea Max?”
“Naweza kukuamini B?”
34 naweka nukta hapa.
Tchao
Shukrani sana mkuu. Asante kwa kuendelea kuwa nami 🤝Hatariii upo vizuri kiongoz unatuburudisha na kutufundisha piah naamini unaitendea haki kazi ya Fasihi andishi. Mungu akujalie uendelee kutuletea vitu vizuri zaidi na ufike mbali kama malengo yako yalivyo.
Pole sana mkuu 😅Mzigo ni mkali sema ni mfupi kinoma