STELLA POINT.
Nilivyofika Gilmans nilipata some sort ya relief.. Na kwa mimi nafikiria Gilmans was the hardest part. Watu wengi huwa wanaishia hapo anakosa nguvu ya kuendelea mbele. Wote katika group yetu tulipumzika then tukaanza safari ya kuelekea Stelle.
Njiani kulikua na barafu saana.. The wind is blowing hatari.. tulikua tunatembea juu ya barafu.. Problem nyingine ni kwamba tulikua hatuwezi kuonana kutokana na ukungu..Mtu yuko hatua tatu mbele ila huwezi kumuona kwasababu kuna ukungu wa kufa mtu. To be honest ilikua inatisha..
Shida inakuja kuwa hewa inakua ndogo saana. Nikaanza kuona hali tete kabla hatujafika...baada ya Masaa kadhaa tukafika Stella... Pale Kibaoni tukapiga picha haraka ili tuendelee mbele.
Sim yangu haikuweza kuwaka.. We only took group photos
UHURU PEAK.
Baada ya pale tukaanza kuitafuta Uhuru..Ambayo ni kama 30mints.. hizi dakika kuzitamka hapa unaona chache ila ukiwa kule juu ni kama mwaka...Yaani hali ya hewa ilikua mbaya saana. Nilikua nime sha give up nimechoka na nilikua sijielewi yaani natembea tu.. Sielewi kitu. Niliambiwa nilipata Hallucination..
Kuna baba mmoja mwanzoni niliwaambia kuwa yeye kapanda mara 18 ila alisema katika kipindi choote alichopanda hakuwahi kukutana na hali tuliyokutana nayo sisi kule juu. Storm inayopiga ni ya hatari..... Upepo unapiga mnakimbilia katika jiwe kubwa ili atleast upepo upungue kidogo ndio tuendelee mbele. Jamani nilikua kama naiona jehanam. It was life and death experience kule juu. Upepo ukivuma ukija hivi uso wote unafunikwa na barafu... Nilikuja kuambiwa baadae kuwa storm tuliyokutana nayo huko juu haijawahi kutokea for decades
Tukaanza kupotezana hapo.. Guide mkuu akasisitiza hali ni mbaya turudi tusiendelee mbele..kiongozi wetu anasema haiwezekani.. Mimi nilikua sielewi kitu siwezi kuongea nawatizama tu.... hata haya mengine nilikuja kuhadithiwa Yeye alikua anasisitiza hakuna mtu anarudi.... Yaani hapo hadi ulitokea ugomvi kati yetu na guide mkuu anaetuongoza. Storm ni ya hatari inapuliza mpaka unasikia jiwe kubwa linatikisika hapo nawaza hili jiwe si linaweza kubiringita hapa then litudondokee ndio iwe bye bye
I reached Uhuru Peak.. kufika summit was one of the best experiences of my life. The summit view was absolutely stunning and I don’t think any words could really give a justice... Unapaswa ushuhudie mwenyewe mtu asikuhadithie. Yaani nilisahau hata ile dhoruba tuliyokutana nayo...
Niliona mazoezi na jitihada zangu zimezaa matunda mwisho wa siku, I felt a sense of achievement kwa kutimiza kile ambacho nilijiwekea kwamba i want to STAND ON THE ROOF OF AFRICA. Nakumbuka nililia saana.... Nikiwa summit na pia wakati wa kurudi ni machozi ya furaha na relief. Mind you sisi hatukuchuka hata dakika pale juu tuligeuza muda ule ule kutokana na hali ya hewa.
Group yetu wote hatukufanikiwa kukigusa kibao wala kupiga picha katika kile kibao.. Hii ni kutokana na barafu nyingi. Wote tulikubaliana as long as tumefika Peak hiyo inatosha... It was sad thing kutokupiga picha pale lakini pia ukifikiri ulikotoka na pale tulipofika unaona IT was okay
Nikipokea certificate yangu
Ukumbusho wa cheti.
Next post ya mwisho nitamalizia kushuka.