Simulizi ya Safari yangu ya kupanda Mlima Kilimanjaro

Watch "Climbing Kilimanjaro: Tips & Tricks" on YouTube

Nafikiri hiyo itatusaidia tunapofanya maandalizi.
Ila imesheheni na ni ndefu. 1 hour.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante sana Heaven on Earth kwa simulizi yako nzuri inayohamasisha.

Nimeishi moshi kwa karibu miaka 5 hivi, sikuwahi kuhamasika kuhusu kupanda mlima kama ilivyotokea kwa simulizi yako. Zaidi ilikua tukipata videm basi marangu falls.

Moshi nilikua na marafiki maporters, madereva na mpaka jamaa mwenye ubia na kampuni ya tours. Sikuwahi kuhamasika kama leo hadi nimeshinda YouTube kusakanya details. Very fun.

Nilichogundua wenyeji wengi wa maeneo husika huambukizwa kimazingira na kujiona na wao ni sehemu ya wamiliki au wafanyakazi au wenyeji wa eneo. Hivyo wao hawahusiki zaidi ya wanaopaswa kwenda huko ni wageni nje ya moshi (something kama washamba au wakuja)

Hii ni sawa na mtu wa mtwara kumkuta anahangaika kutafuta korosho au mwanza mtu anachanganyikiwa na sangara.

Nafikiri mamlaka husika zinatakiwa zibadirishe namna ya kutangaza utalii hapa ndani. Iwe kwa video na story zaidi kwenye mikusanyiko ya watu ili watamani kama ulivyotutamanisha.

Asante sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kilimanjaro hiking ni more than experience. Nilipanda August 2018 na tukalala kilimanjaro crater. Nikiwa mlimani niliulizwa utapanda tena nikajibu never. Kwa sasa natamani kupanda tena na tena ingawa kucha zangu za vidole gumba vya miguu ziling'oka kwasababu ya mlima

Natamani kila mtu apande Kilimanjaro

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Another exciting video kwa wale ambao hatujafika. Muone "breakfast" na "kissing stone" kama wadau walivyosimulia

Watch "What is it really like to climb Kilimanjaro? (Lemosho route) - Follow Alice" on YouTube

Enjoy!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kung'oka kucha tena?? Arghhhhh.......

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kucha za vidole vya miguu ziling'ookaje? ulikuwa umevaa kandambili au? manake kabla ya kupanda mlima Kilimanjaro ni lazima ufanye preparation ya vitu vifuatavyo:
1.Viatu vigumu (Boots) lakini viwe vyepesi ili kukusaidia kutembea bila kuchoka.
2.Soksi pair 4 ndefu safi na nzito.
3.Mycotta powder.
4 Gloves safi zenye sufi ndani.
5.Jacket au pullover zito.
6.Boshori lile kofia la sweta linalofunika kichwa na kuacha sehemu ya macho tu.
7.Miwani nyeusi kupunguza mng'ao wa theluji.
7.Climbing stick
8.Kibuyu au chupa ya maji.
9.Back pack kwa ajili ya kuhifadhi vitu vidogo vidogo kama glucose,biscuits,juice n.k.
Hayo ndio mahitajio ya msingi unayotakiwa kuconsider kabla ya kuanza safari ya kupanda mlima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Í love you Heaven on Earth. Mmmmmwaaaa 😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘😘
 
Nimefuatilia post zote pamoja na michango yote inayofikia 500.

Nimekuwa na hamu sana ya kuupanda huo mlima na nimefurahi mno kuona ushuhuda huu. Heaven on Earth Mwenyezi Mungu akubariki sana kwa ushuhuda huu.

Mipango yangu ni mwakani lazima nipande panapo uzima.

BTW, you are a good story teller. Nikikamilisha maandalizi ya kimwili (physical) ntahitaji ushauri wako pamoja na kiwatengu kuhusu tour guides na mambo yanayohusiana na hayo.

Cheers.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HIV sio ugonjwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…